Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Mrembo wa UDSM Aliyedaiwa kuwa Msukule Uliokutwa Kwenye Shimo la Mfanyabiashara Dar Anena kwa Uchungu

$
0
0
Picha zinazomuonesha mwanamke aliyekutwa kwenye shimo la mfanyabiashara mmoja jijini Dar es Salaam akiwa katika hali ya kutisha zimetumiwa kufanya upotoshaji kwa kumzushia msichana mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Picha iliyounganishwa ikionesha taswira ya msichana huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakidai kuwa hapo ni kabla zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na watu wasio na nia njema na kusababisha usumbufu kwa mrembo huyo.

Msichana huyo ambaye anatumia jina la Ms.Adelaide kwenye Instagram amekanusha vikali taarifa hizo huku akieleza kwa uchungu jinsi ambavyo ameathiriwa na uzushi huo.

“NAJUA WENGI MTAKUA MMEKUTANA NA HIZI HABARI..SIJAJUA NANI ALIEANZISHA HII MADA NA SIJUI IMEANZIA KWA NANI.
 "MIMI NI MZIMA NA SIO MSUKULE JAMANI NINA WAZAZI WOTE WAWILI WAPO HAI NA WAMEUMIZWA SANA NA HIKI KITENDO, MY FAMILY MEMBERS WAMEUMIA MNOOO KUPITA KIASI
"LICHA YA HIYO MIMI BADO NI MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU, WANAFUNZI WENZANGU WENYE MAPENZI NA MIMI WANAUMIA SANA PIA WANAPOONA MAMBO KAMA HAYA. 
"PLEASE ACHENI KUENDELEZA HIZI HABARI ZA UONGO, TUSIPELEKANE MPAKA TCRA SASA MAANA TUTAKUA TUNAPOTEZEANA MUDA,” aliandika Instagram.

January Makamba Awafuta Kazi Vigogo Watatu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira

$
0
0
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUIMARISHA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA BARAZA LA TAIFA LA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA-NEMC

Katika kikao kilichoitishwa na Mhe. January Makamba (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira tarehe 24 January 2016, kuhusu kuimarisha utendaji ndani ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC maamuzi yaliyofikiwa ni kama ifuatavyo:

1. Kuhusu suala la kiwanda cha kusindika minofu ya punda mkoani Dodoma, imegundulika kulikuwa na ukiukwaji mkubwa, wa makusudi na wa wazi wa miiko ya kazi kwa watumishi wa NEMC walioshughulika na kiwanda hicho. Hivyo, Mhe. Makamba ameagiza watumishi wa NEMC wafuatao wasimamishwe kazi mara moja:

a.  Dkt. Eladius Makene -Afisa Mazingira Mwandamizi,
b. Wakili Heche Suguta Manchare - Mwanasheria Daraja la II
c. Mhandisi Boniface Benedict Kyaruzi, Afisa Mazingira.Hatua nyingine za kinidhamu na kisheria zitafuatia

2. Vilevile, imebainika kwamba usimamizi wa watumishi wa NEMC siyo makini na thabiti na kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa Baraza.

Hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Mhandisi Bonaventura Baya apewe barua ya onyo kali  na la mwisho kwa udhaifu katika usimamizi wa watumishi wa Baraza.

3. NEMC kama chombo muhimu nchini kilichopewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira inatarajiwa kazi zake zifanyike kwa ufanisi wa kiwango cha juu kulingana na majukumu yaliyoko kwenye Sheria.

Hivyo, kwa mapungufu yanayojitokeza Mhe. Makamba, ndani ya wiki moja ataunda jopo la wataalamu wasiozidi watano ili kutathmini utendaji wa NEMC na changamoto mbali mbali katika usimamizi wa hifadhi ya mazingira na kuishauri Serikali ipasavyo.

4. Ili kuimarisha ufanisi na udhibiti wa utendaji wa NEMC, ndani ya wiki moja litatolewa Tangazo litakalokuwa na mambo yafuatayo:

Anwani ya barua pepe (email), Nukushi (fax), Namba ya simu, Namba ya Whatsapp ili mtu yeyote mwenye malalamiko au aliyewahi kuombwa rushwa chochote na watumishi wa NEMC ambacho ni kinyume na maadili ya kazi yao atoe taarifa mara moja ili uchunguzi ufanyike na hatua zichukuliwe.

5. Kutokana na mapungufu yanayojitokeza katika utekelezaji wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira, ndani ya wiki moja, NEMC ipitie upya orodha ya wataalamu na taasisi elekezi zilizosajiliwa na kufuta wataalamu na taasisi zote ambazo zimekuwa zikikiuka maadili ya kazi zao likiwemo suala la kuwasilisha taarifa zilizo chini ya viwango, kuchelewesha kazi za wateja wao na kutowasiliana na wateja wao kuhusu hatua za utekelezaji wa maombi yao.

6. Ndani ya wiki tatu uitishwe mkutano wa dharura wa Bodi ya NEMC kujadili na kufanya maamuzi juu ya changamoto za utendaji katika Baraza.

IMETOLEWA NA
IDARA YA MAZINGIRA,
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
TAREHE 24.01.2016

Haya Ndio Matokeo ya Mechi Aliyohaidi Madee Kuchoma Gari yake Moto Kama Arsenal itafungwa

$
0
0
Jumapili ya January 24 Ligi Kuu Uingereza iliendelea kwa michezo miwili kupigwa, mchezo wa kwanza kuchezwa ulikuwa mchezo kati ya Everton dhidi ya Swansea City mchezo ambao ulimalizika kwa Swansea kuibuka na ushindi wa goli 2-1 licha ya kuwa katika uwanja wa ugenini.

Mchezo wa pili ulikuwa ndio mchezo ulioteka hisia za watu wengi zaidi wa jiji la London, kwani ulikuwa unazikutanisha timu za jiji moja Arsenal dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Emirates, hisia za mchezo huo hazikuishia Ulaya pekee, Tanzania msanii wa Bongo Fleva Madee Ali alitangaza kuwa kama endapo Chelsea itaifunga Arsenal basi atachoma moja kati ya magari yake moto,

Kwa bahati mbaya licha ya kuwaArsenal walikuwa na mwenendo mzuri katika Ligi msimu zaidi ya Chelsea, walikubali kipigo cha goli 1-0 kutoka Chelsea wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani. Goli la Chelsea lilifungwa na Diego Costa dakika ya 23, goli hilo lilipelekea Madee kutopatikana hewani. Kwa matokeo hayo Chelsea wanatimiza point 28 na kuwa nafasi ya 13, wakati Arsenal wameshuka hadi nafasi ya tatu wakiwa na point 44.

TRA Yadai Kukamata Simu 2,744 Katika Ghala la StarTimes zilizoingia Nchini Kwa Magumashi

$
0
0
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imedai kukamata maboksi 294 yenye simu 2,744, na vifaa mbalimbali vya simu katika ghala la Kampuni ya StarTimes.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bodi ya StarTimes, Clement Mshana alisema yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa wiki na hajapokea taarifa yoyote kutoka TRA kuhusu kukamatwa kwa mizigo hiyo.

“Nimesikia kwenye gazeti lenu sijui chochote,” alisema.

Juzi, mamlaka hiyo ilikamata maboksi hayo ambayo thamani yake haijajulikana baada ya kutilia shaka nyaraka za mizigo hiyo iliyoingizwa nchini ikiwa haionyeshi ni ya nani.

Pia, TRA ilitilia shaka mizigo hiyo ilikotoka na kuwa na taarifa zenye utata kuhusu idadi ya mizigo hiyo. Mkurugenzi wa Huduma ya Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA), Richard Kayombo alisema walipokea taarifa za utata wa mizigo iliyodaiwa kuingizwa na kampuni hiyo jambo lililowalazimu kwenda kuikamata kwa ajili ya uchunguzi.

“Tulikamata maboksi yaliyokuwa na simu na vifaa mbalimbali kama vile betri, chaji za simu, powerbank na kava za simu,” alisema Kayombo.

Alisema baada ya kuikamata waligundua kulikuwa na udanganyifu wa idadi ya maboksi yaliyokuwa kwenye nyaraka, kwani zilisomeka kuwa kuna maboksi 211, lakini katika uchunguzi walikuta 294.

Alisema mizigo hiyo ilikuwa haionyeshi ni ya nani na kama imelipiwa kodi, hivyo bado iko mikononi mwao hadi pale watakapojiridhisha na uchunguzi.

“Boksi hizo ziko chini ya TRA, bado tunaendelea na uchunguzi ili kujiridhisha na kujua mizigo hiyo ni ya thamani kiasi gani, imelipiwa kodi na kufuata taratibu zote za usafirishaji au la,” alisema.

Alisema endapo watabaini kuwa mizigo hiyo haijalipiwa kodi hatua za kisheri a zitachukuliwa kwa wahusika.

Ajali Nyingine leo..Basi la Adventure Lagongana na Noah..Idadi ya Waliofariki iko Hapa

$
0
0

Ajali hii iliyotokea maeneo ya Chamwino, Dodoma ikilihusisha basi la Adventure na gari binafsi aina ya Noah inadaiwa kuchukua uhai wa watu watatu.

Tuwaombee marehemu wapumzishwe mahala pema

Huyu Dereva Tax Atanivunjia Ndoa Yangu, Nifanyeje?

$
0
0
Nimekuja kwenu nahitaji ushauri, ni urgent.

Hapo katikati niligundua kuwa Mr wangu ana kimada, tukasumbuana na kugombana sana juu ya hilo, ingawa sikumshika live ila ni wazi kwamba alikua nae, mbali na hilo pia ni mlevi kupindukia.

Nilipoona suala hilo linaendelea nikaona isiwe tabu, nikatafuta suluhisho.

Na mimi nikatafuta mtu pembeni aniliwaze, kuna dereva tax huwa tunamtumia sana kwa shughuli za kifamilia,
Nikaamua kumzawadia penzi huyo jamaa, sio kwamba nilimuanza mimi, bali alikua akinisumbua siku nyingi, hivyo nikaona nimkubali.

Katika mara zote nilizokutana nae (6) niligundua kwamba hajiwezi kabisa, nikaona this relationship is not worth it, nikampiga chini, pia mtu mwenyewe hana hata Chumba cha kulala, Mara zote anaazima Chumba kwa mwenzie, ingawa ukimuona kwa nje ubrazamen alionao huwezi amini, ni type ya wale wanaume wenye kuongea sana na mbwembwe nyingi lakini hamna lolote.

Nikakata mawasiliano nae na kumwambia asinitafute tena, akaanza kunililia nisimwache, anapiga simu muda wote kunibembeleza, kila akiniona hata na watu wengine Mtaani, labda Dukani n.k atakimbia haraka kuja na kuomba tuongee pembeni hadi kero.

Hivi karibuni nimepata mtu mwingine mahali nakoabudu, he is so caring, ni mtu mwenye Upendo sana, hanywi pombe na ananipenda kwa dhati, he is god fearing and above all his performance is much better than my husband and the tax driver's.

Juzi kumetokea shida kubwa baada ya Mr kushika sms ya yule tax driver akiendelea kunibembeleza, Nikalazimika kusema kuwa jamaa ndio ananifuatilia, ananitaka kimapenzi, akasema kama ni kweli na ili aniamini Basi tufanye fumanizi la kutengeneza, kwamba nikubaliane na yule kijana wa tax kwenda nae guest na yeye aje atufumanie na kundi la mabaunsa wamwoe wote.

Nikikataa mpango huo basi atajua nilishatembea nae, na mimi najua yule tax driver kwa vyovyote vile atauvaa huo mtego, namuonea huruma sitaki apate aibu hiyo wakati tulishaachana nae.

Nipo njia panda naombeni ushauri nifanyeje?

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya Januari 25, Ikiwemo Vita ya Madaraka ya Bunge yakolea

$
0
0


Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya Januari 25, Ikiwemo Vita ya Madaraka ya Bunge yakolea

Rais Kikwete Apata Shavu Jingine la Kimataifa..Achaguliwa Kwenye Jopo La Wenyeviti Wa Ushauri Ngazi Ya Juu Ya Afya Ya Mama Na Mtoto Duniani

$
0
0
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea kwa furaha uteuzi uliofanywa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Ban Ki-Moon wa kumteua Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais  Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa mmoja wa wenyeviti wa jopo la ushauri la ngazi ya juu kuhusu Afya ya Mama na Mtoto (Every Woman, Every Child) Duniani.

Kwa niaba ya Serikali, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kwa niaba yangu binafsi napenda kuchukua fursa hii kumpongeza kwa dhati Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa uteuzi huu.

Wakati wa uongozi wa Serikali yake ya awamu ya nne, Mhe. Dkt Jakaya Kikwete amekuwa mstari wa mbele kitaifa na kimataifa katika kusimamia na kutetea huduma bora za afya ya mama na mtoto.

Mwaka 2005, mara baada ya kuingia madarakani Mhe. Dkt Jakaya Kikwete aliagiza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuandaa Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi (MMAM) akiwa na nia ya kusogeza huduma za afya karibu na wananchi, hususan huduma ya afya ya uzazi na mtoto. Kutokana na jitihada zake hizo, vituo vya kutolea huduma za afya vya umma viliongezeka kutoka 5,172 mwaka 2005 hadi 7,247 mwaka 2015.

Mwaka 2007, Mhe Dkt. Jakaya Kikwete aliungana na Waziri Mkuu wa Norway Mhe. Jens  Stoltenberg na viongozi wengine  wa kimataifa kuanzisha Mtandao wa Viongozi wa Dunia wa kutoa msaada wa kisiasa katika ngazi ya juu kabisa na kufanya uragibishaji  (advocacy) kwa ajili ya malengo ya milenia namba 4 na 5 yanayohusu kupunguza vifo vya watoto na wanawake wajawazito. (Network of Global Leaders Advocating for MDG4 and 5).

Mwaka 2008, Mhe Dkt. Jakaya Kikwete alizindua Mpango Mkakati wa Taifa wa Kuongeza Kasi ya Kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vya watoto wachanga (Road Map to Accelerate Reduction of Maternal Newborn and Child Health 2008-2015).

Mwaka 2014 alizindua Mpango Mkakati ulioboreshwa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vya watoto (Sharpened One Maternal Newborn and Child Health Plan 2014-2015).

Sambamba na uzinduzi wa mpango mkakati huo, pia alizindua kadi maalum ya kutathmini utekelezaji katika afua za kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vya watoto.

Kadi hii aliikabidhi kwa Wakuu wa Mikoa wote nchini na kuwaagiza wasimamie kwa karibu na kuwa atafuatilia utekelezaji wake.

Mwaka 2010, Dkt. Jakaya Kikwete aliungana na Mhe. Ban Ki-moon wakati anatangaza nia ya kuwa na mpango mkakati wa kimataifa wa afya ya wanawake na watoto “UN Secretary General’s Strategy for Women’s and Children’s Health 2010-15”.

Baada ya mkakati huu kukamilika Desemba  2010, Mhe. Dkt. Kikwete aliteuliwa na Mhe. Ban Ki-Moon kuwa Mwenyekiti Mwenza wa Tume ya Taarifa na Uwajibikaji kwa ajili ya Afya ya Wanawake na Watoto “UN Commission on Information and Accountability for Women’s and Children’s Health”.

Kazi hii aliifanya kwa umahiri na weledi mkubwa kwa kushirikiana na Mwenyekiti mwenza aliyekuwa Waziri Mkuu wa Canada, Mhe. Stephen Harper.

Tume hiyo iliwasilisha ripoti yake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwezi Septemba, 2011.  Ripoti hii iliwezesha nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuchukuwa jitihada mbalimbali za haraka na za makusudi za kuboresha afya ya mama na mtoto katika nchi zao.

Baada ya hapo, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete aliendelea kuwa mtetezi wa afya ya akina mama na watoto, chanjo, kudhibiti malaria na UKIMWI ndani na nje ya Tanzania.

Katika kipindi cha uongozi wake, nchi yetu imepata mafanikio makubwa katika kutimiza malengo ya milenia hususani lengo namba 4 linalolenga kupunguza vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano, ambapo vifo vimepungua kutoka 112 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2005 hadi 81 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2010.

Aidha, mwaka 2013 ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu vifo vya watoto ilionyesha kuwa Tanzania imefikia vifo 54 kwa kila vizazi hai 1,000 na hivyo kufikia lengo la Milenia namba 4 hata kabla ya mwaka 2015.

Vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi vimepungua kutoka 578 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2005 hadi 454 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka  2010.  Na kutokana na ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2014 tumefikia vifo 410 kwa kila vizazi hai 100,000.

Afya ya mama na mtoto ni kipaumbele kwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto itaendeleza juhudi hizi na kuhakikisha tunapiga hatua kufikia Malengo Endelevu ya Kimataifa (Sustainable Development Goals 2030).

Tumedhamiria kuwapa uhakika kina mama wa Tanzania wa kutopoteza maisha yao wanapotekeleza haki yao ya msingi ya uzazi. Tutahakikisha tunapunguza au kumaliza kabisa tatizo la vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga. Chini ya Kauli Mbiu ya ‘Hapa Kazi tu” ni dhahiri kuwa hili linawezekana.

Pia, tunaahidi kumpa ushirikiano Mhe. Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete katika jukumu hilo alilopewa ambalo ni heshima kubwa kwa Taifa letu. Tunamtakia kila la kheri katika utekelezaji wa majukumu yake.

Imetolewa na:
Ummy A. Mwalimu (Mb.)
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dodoma
24 Januari  2016.

Rais John Magufuli Arejesha Ikulu Kuwa Mahala Patakatifu

$
0
0
John Magufuli
Mwaka mmoja uliopita ungeweza kuamini kuwa Mtanzania aliyetwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani hatoitwa Ikulu na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kupongezwa?

Jibu la swali hilo ni hapana; hasa ukizingatia kuwa wapo wanamichezo na wasanii waliotwaa tuzo ndogo zaidi lakini wakaalikwa katika ofisi kuu hiyo ya nchi kwa ajili ya kukutana na Rais.

Mwaka mmoja baadaye, Rais wa Tano John Magufuli amejikita katika kushughulikia matatizo halisi ya Watanzania na kufunga milango kwa wageni wasio na shughuli muhimu kwenda Ikulu, gazeti hili limebaini.

Ikulu pia imekomesha tabia iliyokuwa imezoeleka ya wageni kujazana kila siku sehemu ya mapokezi kwa ajili ya kwenda kuomba misaada mbalimbali kwa Rais, kama ilivyokuwa imezoeleka kwenye serikali iliyopita.

Gazeti hili lilifanikiwa kufika Ikulu sehemu ya mapokezi na kukuta viti vikiwa vitupu tofauti na awamu iliyopita ambapo mapokezi ya Ikulu ilikuwa ikitaka kufanana na eneo la shughuli hiyo katika hospitali yoyote ya mkoa nchini.

Viti vilijaa hadi kufikia hatua ya wageni hao kukaa kwa kupokezana.

Wakati leo ametimiza siku ya 80 tangu alipoapishwa Novemba 5, mwaka jana, Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wachache muhimu, hali inayoashiria kuwa Ikulu sasa ni mahala patakatifu, kama ambavyo Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere alipata kuusia katika moja ya hotuba zake za kukumbukwa, ya Mei Mosi 1995 jijini Mbeya.

Miongoni mwa viongozi ambao Rais Magufuli amekutana nao Ikulu tangu aingie madarakani ni Sheikh Mkuu, Aboubakar Zuberi, Rais wa awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Kikwete.

Rais Magufuli pia alikutana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Idd kuzungumzia hali ya mkwamo wa kisiasa inayoendelea visiwani humo.

Wengine aliokutana nao kwa mazungumzo Ikulu hivi karibuni ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Mpya, Jaji Joseph Warioba, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Abdalah Bulembo, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Musa Jumma Assad na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.

Kutoalikwa Ikulu kwa Samatta ndiko kumedhihirisha kwamba sasa milango ya kwenda kumuona Rais haiko wazi sana kama ilivyokuwa kwenye awamu hiyo ya nne.

Rais Magufuli pia amepokea hati za mabalozi mbali mbali wanaoiwakilisha nchi zao ambao walifika Ikulu kwa ajili ya kujitambulisha.

Januari 7, Samatta alinyakua tuzo hiyo ya pili kwa ubora kwa wachezaji wa Afrika, baada ya Mchezaji Bora wa Afrika ambayo ilikwenda kwa Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon.
Tuzo hizo hutolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Kama Samatta angetwaa tuzo hiyo mwaka mmoja uliopita kwa mfano, isingekuwa rahisi kupita wiki moja bila Mbwana Sammatta kualikwa na Rais Ikulu.

Rais mstaafu Kikwete, ambaye ni mwenyekiti wa CCM,  ameshakutana na Samatta kwenye Ofisi Ndogo za chama hicho, Lumumba jijini.

Baada ya ushindi wake, Samatta alipokewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Wasanii, Nape Nnauye, ambaye alimpa gari lake atumie kwa muda pia.

Miongoni mwa wageni waalikwa wa mara kwa mara wa Kikwete Ikulu ni pamoja na mwanamuziki maarufu wa zamani Ray C ambaye Desemba 10, 2012 alikwenda kumshukuru kwa kumsaidia tiba ya matumizi ya madawa ya kulevya.

Habari ambazo Nipashe inazo, Ray C bado anaendelea kupata tiba ya kuacha dawa za kulevya katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Diamond Platnumz amewahi kualikwa mara kadhaa Ikulu, hata pale alipotwaa tuzo ndogo ambazo zilikabidhiwa kwenye hata klabu za usiku nje ya nchi.

Timu ya Azam imewahi kualikwa Ikulu baada ya kutwaa kwa mara ya kwanza Kombe la Kagame la Afrika Mashariki na Kati, taji ambalo Simba na Yanga zimelichukua jumla ya mara 11 katika historia.

Wachambuzi wa mambo walisema hali hiyo inadhihirisha kwamba Rais Magufuli amejikita katika kushughulikia matatizo ya msingi ya nchi, hasa vita dhidi ya ufisadi wa rasilimali za taifa, upatikaji wa huduma za jamii na uimarishaji wa miundombinu.

Dalili kwamba Ikulu sasa ni mahali patakatifu ilianza kujidhihirisha wakati wa kuapishwa kwa Baraza la Mawaziri mwishoni mwa mwaka jana.

Mawaziri hao waliapishwa bila mbwe mbwe wala shamra shamra kama ilivyozoeleka kwenye awamu ya nne, wahusika wakifika Ikulu bila kuambatana na utitiri wa ndugu na jamaa ambao chini ya Kikwete waliwalaki kwa maua na mashada baada ya kuapishwa.

Kwenye awamu ya nne, baadhi ya wateule walikuwa wakienda kuapishwa Ikulu na wake au waume zao, watoto, ndugu, majirani na jamaa zao na kupata fursa ya kupiga picha na Rais mara baada ya zoezi la kuapishwa.

Utaratibu huo umefutika baada ya Rais Magufuli kuonekana kujikita kwenye masuala ya msingi kama kupanga safu ya uongozi wake kwa kuwafuta kazi watendaji ambao anaona hawawezi kwenda na kasi yake.

Aidha, punde baada ya kuingia Ikulu Novemba 5, mwaka jana Rais Magufuli alifuta kitengo cha mapokezi ya wageni kwenye lango kuu la Ikulu na kuagiza watendaji wa serikali katika ngazi zote kutatua kero za wananchi mahala walipo ili kuwapunguzia usumbufu.

Kitengo cha Lishe kilichokuwepo Ikulu wakati wa serikali ya awamu ya nne kilivunjwa na watendaji wake kurudishwa kwenye Wizara mama walizotoka.

Membe Tena: Serikali isicheze na Wafanyabiashara

$
0
0
Benard Membe
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali iliyopita, Benard Membe amempongeza Rais John Magufuli kwa kasi aliyoanza nayo katika vita dhidi ya ufisadi na kudhibiti mianya ya wakwepa kodi, lakini akamshauri kuwa mwangalifu katika kushughulikia wafanyabiashara.

Membe alisema hayo katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika mapema wiki hii kuhusu, mambo mbalimbali yanayoendelea tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani.

Mwanadiplomasia huyo alisema hatua ambazo Rais Magufuli amekuwa akichukua kuwabana wakwepa kodi ni za msingi, lakini lazima alifanye kwa uangalifu mkubwa ili asiwafukuze wawekezaji ambao kimsingi ndiyo wabia wa maendeleo ya taifa.

“Wafanyabiashara ni watu wa ‘kuwahandle’ vizuri na kwa uangalifu mkubwa kwa sababu wao ndiyo gurudumu la maendeleo ya nchi yoyote duniani,” alisema Membe.

“Tunapozungumzia ajira, tunazungumzia wafanyabiashara ambao ndiyo wawekezaji. Sasa ombi langu ni kwamba Serikali isicheze nao.”

Akitumia ishara ya mkono wake wa kulia, Membe alisema: “(Mfanyabiashara) Ni kama ndege ambaye ili uendelee kuwa naye, ni lazima umshikilie hivi, lakini ukiachia vidole ataruka na kwenda kutaga mahali kwingine.”

Vyuo Vikuu CCM Wamshukia Benard Membe Kwa Kumkosoa Rais Magufuli

$
0
0
SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ndugu waandishi wa habari, nimewaita hapa kuelezea masikitiko makubwa kutokana na kauli za hivi karibuni za aliyekuwa waziri wa mambo ya nje ndugu Bernard Membe. Akifanya mahojiano na kunukuliwa na gazeti la Mwananchi la tarehe 22 na 23 Januari, 2016 , ndugu Membe amekaririwa akitoa kauli zenye maudhui ya kubeza juhudi za mh. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli na kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar. Kauli hizi zilijikita katika maeneo makubwa manne kama ifuatavyo:-
membe
1. Ndugu Membe amebeza juhudi za Rais Dr. John Magufuli za kupunguza ukubwa wa serikali, na kwamba hatua yake ya kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri haijasaidia chochote kwa taifa. Na kwamba ni sawa na kupunguza idadi ya mifuko huku idadi ya mayai ikiwa ni ile ile.

2. Ndugu Membe amekosoa na kubeza hatua ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr. Magufuli ya kupunguza safari za nje zisizo za lazima na tija kwa taifa, na kwamba safari hizo zilikua na neema kubwa kwa watanzania.

3. Ndugu Membe amepinga kufutwa kwa matokeo yote ya uchaguzi visiwani Zanzibar na kudai kwamba dunia nzima inatushangaa kwa uamuzi huo.

4. Ndugu Membe amekosoa mazungumzo ya kutafuta maridhiano baina ya Chama cha CUF na CCM visiwani Zanzibar huku akidai kuwa ni makosa kuwaachia Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein na Maalim Seif Shariff Hamad kufanya mazungumzo peke yao.

Tumesikitishwa sana na kauli hizo na vijana wasomi tumeamua kumjibu kama ifuatavyo:-

KUPUNGUZA UKUBWA WA SERIKALI

Rais Dr. John Magufuli amechukua juhudi za kupunguza ukubwa wa serikali kwa kuanza na baraza la mawaziri. Idadi ya mawaziri imepungua kutoka mawaziri 60 wakati wa serikali ya awamu ya nne hadi mawaziri 34 tu katika serikali ya awamu ya tano. Punguzo hili ni idadi ya mawaziri 26.

Gharama za kawaida za kumuhudumia waziri zilizopungua:

a. Kila waziri na naibu wake hupewa gari aina ya GX V8 ambalo thamani yake inakadiriwa milioni 400. Gari hili linahitaji mafuta na gharama ya kulitunza. Hivyo magari 26 yamepungua ambayo gharama yake ya manunuzi na matunzo ni mabilioni ya pesa.

b. Nyumba ya kuishi. Mawaziri wote wanapewa nyumba na serikali. Nyumba hizo zinalipiwa umeme na maji

c. Wasaidizi wa mawaziri. Kila waziri anapewa katibu wake, hivyo serikali imepunguza nafasi 26 za makatibu kwa kupunguza mawaziri 26. Hawa wanalipwa mishahara na posho.

d. Madereva. Kila waziri ana dereva wa serikali anayelipwa mshahara na posho awapo nje ya kituo cha kazi. Hivyo serikali imepunguza mishahara na posho za watu 26.

e. Kila waziri anapewa ulinzi nyumbani kwake wa askari wawili wa jeshi la polisi masaa 24. Hivyo kwa kupunguza mawaziri 26, tumepunguza askari 52 ambao sasa watakwenda kuongeza ulinzi wa raia na mali za wananchi wengine.

f. Kila waziri anatengewa mafungu ya fedha kwa ajili ya mawasiliano, safari zake za kikazi, ziara za mikoani, vikao na majukumu mengine ya kazi ambayo ni mamilioni ya shilingi kila mwezi. Kwa kupunguza mawaziri 26 Rais ameokoa mamilioni ya shilingi kila mwezi.

g. Gharama za kuwahudumia mawaziri 26 wakiwa bungeni Dodoma pia zimepungua.

WIZARA ZILIZOUNGANISHWA

Katika muundo wa baraza la mawaziri la Dr. John Pombe Magufuli alilolitangaza , ziko wizara 5 ambazozimeunganishwa pamoja. Wizara hizi ni

a. Kilimo, Mifugo na Uvuvi (wizara 3 zimeunganishwa, sasa zina waziri 1)-Mh. Mwigulu Nchemba

b. Wizara ya mambo ya nje, kikanda na kimataifa (wizara mbili zimeunganishwa, sasa zina waziri 1)- Mh. Augustine Mahiga

c. Wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji (wizara 2 zimeunganishwa,sasa zina waziri 1)- Mh. Charles Mwijage

d. Wizara ya elimu, sayansi, teknolojia na ufundi (wizara 2 zimeunganishwa, sasa zina waziri 1)- Mh. Joyce Ndalichako

e. Wizara ya ujenzi, mawasiliano na chukuzi (wizara 3 zimeunganishwa, sasa zina waziri 1) –Mh. Makame Mbarawa

Katika hali hiyo, ni dhahiri idadi ya mawaziri imepungua na hivyo gharama ya kuwahudumia pia imepungua. Kutoka hadharani na kusema hakuna kilichopungua ni upotoshaji mkubwa ambao mtu mwenye uelewa wa kawaida kabisa anaweza kuubaini.

IDADI YA MAKATIBU WAKUU

Makatibu wakuu na manaibu waliohudumu wizara wakati wa serikaliya awamu ya nne walikua jumla ni 54. Mh. Rais Dr. Magufuli ameteua makatibu wakuu 29 na manaibu 21. Hivyo hapa pia idadi imepungua na kufanya gharama kupungua pia.

WATANZANIA WANAMSHANGAA MEMBE

Kitendo cha ndugu Bernard Membe kudai kuwa kupungua huku kwa ukubwa wa baraza la mawaziri hakujasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali, ni jambo la ajabu ambalo watanzania wote wanalishangaa na kuliona kuwa ni uongo na upotoshaji mkubwa. Upotoshaji huu unastahili kupuuzwa na kila mpenda mabadiliko ya kweli.

Baada ya Mh. Raisi kuteua baraza lake la mawaziri mwezi desemba, mwanazuoni profesa Samuel Wangwe alikaririwa na gazetila Habari Leo la tarehe 11 Desemba, 2016 akisifu Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli kupunguza idadi ya mawaziri. Profesa Wangwe alisema mawaziri ni watu wa kusimamia sera, na watendaji wakubwa ni makatibu wakuu. Aidha, wanaharakati na wadau mbalimbali wote walipongeza kupunguzwa huko kwa baraza la mawaziri wakisema taifa limepunguza mzigo. Lakini ajabu, ndugu Bernard Membe hajaliona hilo. Inasikitisha sana.

Wakati mwingine inatufanya tujiulize, ndugu Membe ambaye alikua miongoni mwa wana CCM waliowania kuteuliwa na Chama kugombea Urais wa Tanzania, na baadae kushindwa kwa kura ndani ya Halmashauri Kuu ya CCM taifa, amesema maneno haya kwa malengo au makusudio yapi? Waswahili wanasema, aliyepata kapata. Tunamtaka ndugu Membe ajiunge na watanzania kukubali kuwa Dr. Magufuli ndiye Rais wa nchi yetu aliyechaguliwa na wananchi. Hivyo amuache atimize wajibu wake kwa taifa.

KUPUNGUZA SAFARI ZA NJE

Katika hatua nyingine ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima serikalini, Raisi ameagiza kufutwa kwa safari zote zisizo za tija kwa nchi, na kwamba safari zote zitatolewa kwa kibali maalum cha Raisi.

Kwa mujibu wa hotuba ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli bungeni mjini Dodoma, safari za nje za miaka miwili pekee (2013-2015) ndugu Membe akiwa waziri wa mambo ya nje, shilingi bilioni 356.324 zilitumika kwa safari za nje huku tiketi za ndege peke yake zikigharimu bilioni 183.160. Taasisi zilizoongoza kwa matumizi hayo ni pamoja na wizara ya mambo ya nje aliyokuwa anaihudumia ndugu Membe. Tunajiuliza, ni trilioni ngapi zilitumika kwa safari za nje katika kipindi chote cha miaka 8 ambacho ndugu Membe alikuwa waziri? Je, huu haukua mzigo kwa taifa? Ndugu Membe anazungumziaje matumizi haya mabovu ambayo yalifanyika yeye akiwa na dhamana ya wizara hiyo?

Watanzania wote tunafahamu na kukubali kuwa safari hizi zilikua mzigo mkubwa kwa taifa, na tunaunga mkono juhudi za kupunguza na kudhibiti safari zisizo za lazima.

BERNARD MEMBE SI MKWELI

Ndugu waandishi, ili kudhihirisha kuwa ndugu Bernard Membe si mkweli kwa anayoyasema kuhusu safari za nje, na kwamba kauli zake kuhusu jambo hili zinakinzana, baada ya hotuba ya Rais Dr. John Magufuli bungeni mjini Dodoma, bwana Membe alinukuliwa akimpongeza mh Rais kwa uamuzi wake wa kupunguza safari za nje kwani kwa maneno yake alisema walikua wanapishana angani kama vile nyumbani kunawaka moto.

Ni Bernard Membe huyuhuyu ambaye leo anatafuna maneno yake bila aibu na kutueleza kuwa safari zile zilikua na neema kwa taifa.

KUHUSU KUTOKUA NA BALOZI KATIKA NCHI ZOTE

Katika kuhalalisha safari za nje zisizo za lazima, ndugu Membe alieleza kuwa Tanzania ina mabalozi 36 tu katika nchi 194 ambazo tunapaswa kuwa na mabalozi.

Tunapenda kumfahamisha ndugu Membe kuwa kutokuwa na balozi katika nchi zote sio kigezo cha kutumia mabilioni ya pesa kwa ajili ya safari zisizo na tija kwa taifa. Kutokana na kuwa uchumi wetu bado unakua, na haustahamili gharama za kuweka mabalozi katika nchi zote, wako mabalozi wetu nje ya nchi ambao wanawakilisha nchi zaidi ya moja zilizoko katika ukanda mmoja. Mfano, balozi Ombeni Sefue aliwahi kuwa balozi wetu Marekani akiwakilisha pia CUBA. Aidha, uamuzi wa nchi kufungua ubalozi katika nchi nyingine hutegemea vigezo mbalimbali kama faida za kiuchumi, kisiasa, kiusalama na kidiplomasia.

RAIS HAJAKATAA KUSAFIRI NJE YA NCHI

Ndugu Membe anapotosha ukweli anaposema Tanzania sio kisiwa na kwamba Raisi na waziri wake wa mambo ya nje lazima wasafiri nje ya nchi watake wasitake.

Tunapenda kumfahamisha ndugu Membe kuwa, mh. Raisi Dr. John Magufuli hajatoa kauli kuwa yeye au wasaidizi wake hawatosafiri nje ya nchi katika safari za muhimu na zenye tija. Isipokuwa, muongozo wa mh. Rais kuhusu safari za nje unalenga kupunguza safari zile ambazo hazina ulazima na tija kwa taifa.

KUHUSU MGOGORO WA UCHAGUZI WA ZANZIBAR

Katika maelezo aliyonukuliwa na gazeti la Mwananchi, ndugu Membe alieleza kupinga kufutwa kwa matokeo yote ya uchaguzi wa Zanzibar yakiwemo ya wawakilishi, na kwamba jambo hili limeihuzunisha dunia.

Kauli hii ya ndugu Membe inatushangaza na kutusikitisha sana. Kwanza tunajiuliza, Je, ikiwa sehemu kubwa ya uchaguzi iligubikwa na udanganyifu na ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi kinyume na sheria za uchaguzi wa Zanzibar, ni kwanini ndugu Membe ashangae uchaguzi wote kufutwa na tume ya uchaguzi ZEC?

Tunamtaka ndugu Membe atueleze, ni dunia ipi hiyo inayotushangaa?

Ni kwanini dunia hiyo anayoitetea ndugu Membe haijashangaa kumuona maalim Seif Shariff Hamad akijitangaza kuwa mshindi kinyume cha sheria za uchaguzi?

Ndugu Membe anapaswa kushangaa, ni kwanini hadi leo hii maalim Seif Shariff Hamad hajakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya kujitangaza kuwa mshindi kinyume cha sheria.

KUHUSU VIKAO VYA MARIDHIANO

Kuhusu vikao vya maridhiano vilivyokua vinaendelea, ndugu Membe amekosoa kitendo cha Raisi wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na maalim Seif Shariff hamad kuachwa wakazungumza wenyewe wawili.

Kwanza tunasikitika kuwa ndugu Membe huenda ama hajui kinachoendelea Zanzibar au ameamua kupotosha umma kwa makusudi. Hii ni kwasababu mazungumzo yaliyokua yakiendelea Zanzibar, hayakuwahusisha Dr. Shein na maalim Seif Shariff peke yao. Bali yalishirikisha marais wastaafu wa Zanzibar, Raisi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar na makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar.

Pili, katika muafaka wa kisiasa wa Zanzibar wa mwaka 2009/2010 uliopelekea kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, kwa kiasi kikubwa ni maalim Seif Shariff hamad na Rais wa Zanzibar wa wakati huo mh. Amani Abeid Karume pekee walioshiriki mazungumzo.

RAI KWA NDUGU MEMBE

Mosi, tunapenda kumkumbusha ndugu Bernard Membe kuwa yeye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa amewahi kuwa mjumbe wa kamati kuu ya CCM. Hivyo anajua utaratibu wa Chama na anayo nafasi ya kuyasema mawazo yake juu ya uendeshaji wa serikali ndani ya vikao halali vya chama. Aidha, ndugu Membe kwa nafasi yake kama mjumbe wa NEC na waziri wa zamaniwa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, anayo nafasi ya kutoa ushauri na maoni yake moja kwa moja kwa Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh. Dr. John Magufuli, Mwenyekiti wa CCM taifa Dr. Jakaya Kikwete au kwa Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana.

Kutotumia fursa hizo kutoa maoni yake ni kujishushia heshima mbele ya jamii.

Pili, tunamkumbusha ndugu Membe kuwa yeye sasa ni mstaafu aliyeitumikia nchi yake kwa muda mrefu na nafasi mbalimbali. Ni vema sasa akatoa fursa kwa viongozi wengine walioko madarakani kutimiza wajibu wao wa kuwatumikia watanzania. Muda wake umekwisha na sasa ni busara akakaa kimya na kuchunga maneno yake.

Raisi mstaafu wa awamu ya tatu mh. Benjamin William Mkapa aliwahi kusema (nanukuu):-

“Siku moja mtoto mdogo aliwahi kuniuliza. Nani ni bingwa wa kuendesha shughuli za serikali? Nikatafakati sana swali lile, kisha baada ya muda nikamjibu…Ni mwanasiasa aliyestaafu kisha akachunga ulimi wake…”

MWISHO

Tunamshauri ndugu Membe kuuchukua ushauri huu wa Raisi mstaafu Benjamin Mkapa, utamsaidia. Aidha tunamtaka afahamu kwamba watanzania wana imani kubwa na juhudi zinazofanywa na serikali katika kupunguza matumizi, kuziba mianya ya rushwa, ukwepaji kodi na ubadhirifu wa mali za umma. Wakati huu si wa kupika majungu, fitina wala ubabaishaji. Ni wakati wa kuungana pamoja kama taifa na kuchapa kazi tu.

Asanteni.

Imetolewa na ndugu

ALLY S. HAPI

KATIBU WA IDARA,

ELIMU, UTAFITI NA UONGOZI,

SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU TANZANIA

Zari Hassan wa Diamond Awachana Wabongo Wasioelewa Lugha ya Kizungu....Is English The Problem !

$
0
0

Zari wa Diamond Awachokonoa Tena Watanzania...Andika Maneno yafuatayo kwenye picha;


Baadhi ya Comments za Wabongo baada ya post hiyo ya Zari Hizi Hapa chini;

angiielly 
Uande hukoo kama hatujui English si arid kwao wanakoangea English stupid kabisaaa..... Nashangaa mijitu inamsupport huyu mkimbizi kwel kuna mijitu bado mikolon

angeljohn__
Hihihi tatizo Nyerere dah tungekuwa tunamwaga ung'eng'e na cc

doro_cute3 
Awache kupotezea story za DNA, we want to see or else take tiffa to katunzi

ma_fusa_de_beauty 
@zarithebosslady wew n nyoko boss wng sio kwa kauli io panic at your own risk haha salute

kisuramie
Chezea lugha ilokuja kwa majahazi@olivermakundi wifi kaamua now dayz c kwa kutushushua huku

catyfranco19
 thanx to those kwonz english en not kiswakinge 4h


Sakata la Katibu wa Yanga Kuondoka Yanga..Manji Afunguka Mazito

$
0
0
TAARIFA KWA WANAYANGA KUPITIA VYOMBO YA HABARI
1. Baada ya kuupitia uamuzi wa Kamati ya Nidhamu kuamua sababu kuvunja mkataba kati ya klabu Yanga na mchezaji Haruna Niyonzima, nilihisi kulikuwa kuna kasoro hasa kwa mchezaji anayelipwa mshahara wa Sh milioni 6 anaweza vipi kupuuzia maisha yake na kuanzisha mgogoro usiokuwa na tija kwa maisha ya kipato. (angalia kiambatanisho 1)

Niliamua uchunguzi wa ndani ufanyike katika suala hilo zima na mwisho, Jonas Tiboroha alibainika kuwa hakuwasilisha ushahidi ya mawasiliano sahihi kwa Kamati ya Nidhamu kuhusiana na Haruna Niyonzima, hali iliyosababisha kamati kuchukua uamuzi ambao haukuwa sahihi kwa sababu;
Kulifanyika mambo ambayo hayakuwa sahihi, mfano barua za Niyonzima kutoka kwa Shirikisho la Soka la Rwanda (Ferwafa) ambazo zilitumwa kwa TFF na kupokelewa kama ambavyo Azam FC walipokea ya mchezaji wao kupitia kwa Afisa Mtendaji Mkuu wao. Lakini barua ya Niyonzima kuja Yanga, ilionekana haikupokelewa kama ilivyokuwa kwa barua yake ya utetezi na ile ya kuomba radhi alizoandika, nazo zilipokelewa lakini hazikuwasilishwa kwenye kamati ya nidhanmu na hili, mhusika ni Tiboroha.

kiachana na kamati kufanya uamuzi usio sahihi, hili pia limemjengea mchezaji chuki kubwa kwa wanachama na mashabiki. (angalia kiambatanisho 2 & kiambatanisho 3)

Kamati ya Utendaji (EXCOM), bada ya kupitia kwa kina iliona uamuzi ilichukua haukuwa haukuwa ya haki kutokana na kupotoshwa na Tiboroha tena aliendelea kuipotosha kamati kwa makusudi kutokana na kuficha nyaraka hizo ili Niyonzima afukuzwe. Tulifikia maamuzi Tiboroha alikuwa na ajenda yake binafsi.

Hii kama ilikuwa haijagunduliwa mapema, ilikuwa na hatari ya kusababisha upotevu kifedha za Yanga kulingana na kanuni za TFF/FIFA na ukilichimba suala hili kwa undani, kwa kufuata weledi. Kamwe hauwezi kusema yalikuwa ni makosa ya kibinadamu badala yake ni chuki ya kibinadamu ambayo haistahili kufanywa na kiongozi wa Klabu kubwa yenye heshima kama Yanga.

Zaidi, Katika hali nyingine, uamuzi wa Kamati ya Nidhamu uliandikwa na Gazeti la Uhuru na mwisho wa uchunguzi ulidhibitisha mtoa habari hizo alikuwa ni Tiboroha, akilenga kutaka kuuchafua uongozi wa Klabu, mchezaji mwenyewe dhidi ya jamii na kuusukuma uongozi kufanya uamuzi usio sahihi kwa faida zake yeye binafsi na si klabu.

1. 2. Aidha, EXCOM ilifanya uchunguzi wa ziada na kugundua vitendo, Tiboroha hakuweza kufikia malengo aliyekuwa ameyawekewa na EXCOM kwa kuwa zaidi alionekana kutaka kujiendeleza binafsi, kusikika peke yake na kujulikana mwenyewe kama “Mungu Mtu”, jambo ambalo lilichochea kelele ndani ya klabu kama vile yeye ni malaika:

∞ Angalia kiambatanisho (3), eti Mwenyekiti wa Matawi (nafasi ambayo haitambuliki kwenye katiba ya Yanga), amekuwa akiniagiza kubadili nafasi za waajiriwa, mfano ile ya (Tiboroha) ni lazima abaki kwa sababu mchango wake ni mkubwa na bila yeye hatuwezi kushinda au kufanya vizuri. Ukisoma barua yake utafikiri Tiboroha alikuwa akifanya kazi zake bure wakati anajua alikuwa ni mwajiriwa wa Klabu, tena kazi zake nyingi alikuwa akizifanya kwa kufuata “maagizo” anayopewa kama mwajiriwa.
Tayari kupinga kuondolewa kwake kumeanza kuripotiwa kwenye vyombo vya habari kama shinikizo la chinichini kupitia Msumi, huenda anafikiri kufanya hivyo inanitisha ili nibadili mambo kwa matakwa ya wasioelewa mamlaka ya Katiba. Naendelea kukumbusha Tiboroha alikuwa mwajiriwa anayelipwa mshahara (angalia kiambatanisho 4) huku mimi kama Mwenyekiti au Wajumbe wa EXCOM tumekuwa tukijitolea na kutolipwa hata posho.

∞ Ajabu Kichekesho zaidi, kila kizuri kilichokuwa kikifanyika, vyombo vya habari viliripoti kuwa ni kazi nzuri ya Tiboroha, lakini wakasahau kila zuri, yeye alikuwa ni mtekelezaji tu baada ya kuagizwa kutoka kwangu mimi mwenyekiti au baada ya ushauri wa kamati ya utendaji na baada ya hapo, yeye alipewa kibali cha kutekeleza jambo husika. Kila zuri lilikuwa lake, mabaya yakiwemo yale ya kuisaidia TFF kuiangamiza shingo ya Yanga, aliyeficha kapuni.

∞ Kuna taarifa kwenye vyombo vya habari ambazo zilithibitisha wazi kuwa Tiboroha alipania kujijenga binafsi kama Katibu Mkuu Bora zaidi kuwahi kutokea Yanga; hoja potofu kwa sababu wakati akiwa Katibu, hata mwalimu wa Klabu alifanikiwa kupatikana kwa ubingwa moja tu. Lakini akasahau kabla yake, Yanga ilishachukua ubingwa mara 24. Tena, propaganda ya kuwa yeye ndiye aliyeisaidia Klabu kusajili wachezaji wa kiwango cha juu zaidi huku akijua wazi kwamba wachezaji hao walikuwa ni pendekezo la Kocha Mkuu, huu ni uputofu wa hali ya juu kabisa.

¥ Ndani ya miezi yake 12 ya uongozi amechangia kushuka kwa kasi kubwa kwa mapato ya klabu huku matumizi ya klabu yakipanda mara nne zaidi kutoka Sh milioni 500 kwa mwaka hadi sasa takriban Sh bilioni 2. Kabla hajaja klabuni, tulikuwa tumekaribia kujikomboa na kuanza kujitegemea. Hii pia ni kwa yeye kukubaliana na ujinga wa kuitetea TFF ambayo mikataba yake, kwa kiasi kikubwa imeporomosha mapato yetu na kutuweka katika wakati mgumu kabisa, ajabu Tiboroha alikuwa upande huo.

3. Masuala ya kupotosha ya Tiboroha si mapya:
a. a. Wakati FIFA ilipoialika Yanga kwenye semina ya mafunzo iliyofanyika nchini Ghana, Tiboroha alijichagua mwenyewe asafiri kwa niaba ya Klabu bila kuitaarifa EXCOM, halafu akachukua “Cheti cha ugonjwa” na kukiwasilisha kwa mwajiri wake Yanga ili apate nafasi ya kusafiri kwenda nchini Ghana. Kujichagua yeye mwenyewe, ilikuwa ni kutofuata weledi.
a. b. Daktari (jina linahifadhiwa) aliajiriwa kwa ajili ya mechi dhidi ya MGAMBO likiwa ni pendekezo la Tiboroha, lakini baadaye Kamati ya Mashindano (baada ya kuwa imesababisha tatizo ndani ya Klabu), iligundua daktari huyo alikuwa ni mwanachama tena mwenye kadi wa Simba, akaondolewa’ pia.

a. c. Ngoma alipewa taarifa na Tiboroha kwamba anatakiwa kwenda kufanya majaribio na klabu moja nchini Uturuki. Tiboroha alifanya hivyo akijua Ngoma alikuwa anakwenda kushiriki michuano ya MAPINDUZI Cup, mbaya zaidi hakuwa amewasiliana na EXCOM kuhusiana na hilo kabla kumfahamisha mchezaji na kumpa taarifa hiyo. Baadaye kocha Kocha Mkuu, alilalamika kwamba kufanya vile ilikuwa ni kuondoa morali ya mchezaji katika michuano hiyo ya MAPINDUZI CUP na baada ya hapo, angekuwa akiwaza kuhusiana na Uturuki tu. Mwisho, kocha alisema, Ngoma alicheza chini ya kiwango katika michuano hiyo, akiamini Yanga inamzuia kusonga mbele kimaisha.
a. d. BDF ya Botswana ilianzima US$ 5,000/- ambazo hadi sasa hazijarejeshwa: EXCOM iligundua taarifa kuhusiana na deni hili, imekuwa ikifichwa na hakuna maelezo mrejesho kuhusiana hilo kutoka kwa Tiboroha ambaye amekuwa na ukaribu na wahusika kutoka Botswana.

a. e. Kuna mtu aliajiriwa kama Katibu Muktasi (PS) pamoja na mtu mwingine pia, lakini haikuidhinisha wala mwanasheria wa Yanga, hakutaarifiwa kuhusiana na hilo lilifanyika bila ridhaa ya EXCOM, badala yake alilifanya kwa kuwa anaona yeye ni mtu maarufu sana!

a. f. Hakufuata ushauri aliopewa na wataalamu wa TRA, hali iliyosababisha akaunti za Yanga kufungwa, hivyo mimi kulazimika kuanza kutoa fedha zangu za mfukoni katika uendeshaji wa Klabu kwa kipindi chote na wakati huo wachezaji walikuwa wakidai mishahara na tuko katikati ya msimu.
a. g. Alikuwa akitetea maslahi ya TFF na sio Yanga na kukubali kila TFF ilichokipendekeza. Mtu mwenye akili anaweza kufanya hivyo utadhani alikuwa mwajiriwa wa TFF na si Yanga? Hii inaonyesha hakuwa akifanya kazi kwa maslahi ya Yanga kama ilivyotakiwa, angalia katika masuala dhidi ya TFF, ukijumuisha.

a. h. Lile la kushindwa kumpigania msemaji Msemaji wa Klabu, Jerry Murro asifungiwe na TFF, huku akimchimba huku akijua alikuwa akipitia taarifa zote kabla ya Jerry kuzitoa. Alikuwa na roho mbaya kwa kuwa Jerry alipata umaarufu zaidi kwa wanachama kutokana na kuipigania klabu.
4. 4. Ukiangalia hayo juu, ni kati ya machache ambayo nimeona ninaweza kuyaanika kwenye vyombo vya habari, lakini yako mengi ambayo ni nyeti na haitakuwa sahihi kuyaanika kwenye vyombo vya habari kwa maslahi ya klabu. Yanga ilianza kung’amua mambo yanayomhusu Tiboroha muda sasa, alipoona mengi yamegundulika. Januari 14, 2016 aliandika barua kuomba radhi kwangu, akikiri kufanya makosa na kusema alikuwa akiyajutia. (angalia kiambatanisho 6)

4. 5. Sisi, hatukukubaliana na kutoa msamaha kutokana na hofu ya unafiki wake, na nilitoa ushauri; kwamba vizuri akachukua hatua ya kujiuzulu mara moja na huenda ingekuwa vizuri aeleze ana matatizo ya kifamilia pia kiafya, lengo lilikuwa ni kumpa nafasi ya kuachana na Yanga kwa amani pia kuilinda familia maisha yake huko mbeleni. Lakini nilimtaka ahakikishe zile fedha tunazowadai BDF kutoka Botswana, mara moja zinawasilishwa Klabuni na baada ya hapo, rasmi atakuwa amejiondoa.
4. 6. Tiboroha alikubaliana na hilo na kuandika barua ya kujiuzulu alioiwasilisha Januari 22, 2016 (angalia kiambatanisho 7)

4. 7. Pamoja na kumshauri ili ajiuzulu kwa heshima, lakini alionekana kuanza kutengeneza “Presha ya wanachama” kama vile mtu aliyeonewa. Kuna mkutano wa ujanjaujanja uliitishwa makao makuu ya Klabu, Tiboroha akiwa mshiriki mkuu nyuma ya pazia, hii ilikuwa ni Januari 23, 2016. Lengo ni kutengeneza hali ya hofu kwa Wanachama, jambo ambalo si sahihi. (angalia kiambatanisho 8)
7. Kwa yote hayo hapo juu:

a. a. Kamati ya Utendaji (EXCOM) inapenda kutoa taarifa kuwa imevunja mkataba wa Tiboroha kama Katibu Mkuu wa Yanga.

a. b. Klabu inatangaza, mara moja kuwa:
i. i. Baraka Deudeit atashikilia nafasi hiyo ya Katibu Mkuu wa klabu.
ii. ii. Omar Kaya atachukua majukumu yanayohusiana na wanachama wa klabu. Pia atahakikisha anasimamia mikutano yote ya matawi, kusaidia maandalizi ya uchaguzi ujao pamoja na masuala ya wanachama wapya.

iii. iii. Jerry Muro ataendelea kubaki katika nafasi ya msemaji wa klabu,
iv. iv. Faidhal Mike ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha cha Klabu, akisaidiwa na Justina ambaye amepandishwa cheo na kuwa mhasibu mkuu msaidizi,
v. v. Klabu ipo katika kipindi cha kuboresha kitengo cha masoko cha klabu na hivi karibuni itatangazwa lakini kabla ya hivyo, Omar atashikilia kwa muda kitengo hicho.
vi. vi. Mwanasheria Frank Chacha kama mkuu wa kitengo cha Sheria Klabuni, yeye tunamuacha aendelee na mambo yake na masuala yote ya kisheria, klabu itayafanya kutumia wanasheria, nje ya klabu.

8. 8. Kuhusiana na uchaguzi na maneno ya kinafiki ya nungunungu ya chinichini kuwa eti ninaogopa uchaguzi; huku wakiwa hawajui kuwa katika maisha yangu sijawahi kushindwa uchaguzi: Ukweli mimi ndiyo nimekuwa nikusukuma kuitishwa kwa uchaguzi uitishwe ili nistaafu kupitia nafasi yangu ya uenyekiti. Nilimwaandika Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, kuitisha uchaguzi mara moja, akishindwa basi itabidi niivunje Kamati ya Uchaguzi na kuunda nyingine. (angalia kiambatanisho 9)
8. 9. Kutokana na kuuguliwa na baba yake mzazi, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi alishindwa kutekeleza hilo na akaamua kujiuzulu. (angalia kiambatanisho 10)

8. 10. Ikiwa ni sehemu ya majukumu yangu, kwa ushauri wa EXCOM niliomba kwao majina mapya ya Kamati ya Uchaguzi ili mchakato ufanyike (angalia kiambatanisho 11)
Hitimisho, nimegundua potofu ya kufikiri Tiboroha ni Katibu Mkuu wa kuchaguliwa, badala yake ni mwajiriwa wa kawaida ambaye aliingia mkataba kwa maslahi ya mapato yake. Tena kosa kumchukulia kama mtu ambaye amekuwa akitoa fedha zake za mfukoni kwa ajili ya kuendesha Klabu, mtu ambaye mimi nilipendekeza aajiriwe kama nililivyopendekeza kwa Mwalusako, Njovu, Mwesigwa, Maximo na wengine na nina mamlaka ya kuamua hatma ya mwajiriwa kulinda heshima na maslahi ya Klabu.

Kwa sababu mimi nimewekea dhamira ya uchaguzi ufanyike kwa haraka, huu unaweza ukawa wakati mwafaka wa wanachama kumpa Tiboroha imani ya kura zao ili awanie nafasi Mwenyekiti wa Klabu na wanipe uhuru wangu wa kuendelea na mambo yangu mengine, ambayo yapo karibu na moyo wangu kama vile kusaidi mandeleo ya Mbagala Kuu.

Katika maisha yangu, sijawahi kutanguliza au kupigania cheo, ndani ya Yanga maendeleo yanaonekana lakini wapo watu ndani ya Yanga wanaona mandeleo ipo kwake. Basi tuache demokrasia itawale; lakini na mimi nitatangaza kugombea tena nafasi hiyo, ingawa sidhani kama nitamaliza kipindi chote cha uongozi iwapo nitashinda kwa kuwa kutoka awali nilieleza Yanga kuwa yenye mafanikio ni katika Ligi ya Mabingwa Afrika lakini hilo halitawezekana bila ya Klabu kumiliki uwanja wake binafsi pale Jangwani.
Daima Mbele, Nyuma Mwiko
_____________
YUSUF MANJI

Membe: Sitanyamaza,Ni Haki yangu Kikatiba..Nijibuni Kwa Hoja na si Kuniziba Mdomo

$
0
0
Benard Membe
Aliyekuwa waziri wa mashauri ya nje,Ndg.Membe amewajibu wanaotaka akae kimya kuwa hawezi kunyamaza na anatumia haki yake kikatiba bila kuvunja sheria.

Membe amewataka wajibu kwa hoja badala ya kumziba mdogo.

Membe ameongeza kuwa baadhi ya wana CCM wamekuwa wanafiki wa kutupwa na hawataki Magufuli akosolewe.

Atakuwa mstari wa mbele kutoa maoni huru kwa mambo yanayoendelea bila kuvunja sheria.

Amesisitiza kuwa rais Kikwete atakumbukwa sana kwa kuwapa watu uhuru wa kutoa maoni yao

Hatimaye Idriss Sultan Azibitisha Kuwa Wema Sepetu Ana Ujauzito Wake..Amwita Wife

$
0
0
Leo Asubuhi Idriss Sultan Ameweka Wazi uhusiano wake na Wema Sepetu na Kuwa wanategemea Kupata Mtoto kupitia Meneno haya hapa chini;

"Me and You are not the ordinary. I sleep,eat, talk and wake up to only thinking about you. As much as utadhani kuwa you are blessed to have me no no i am blessed to have you. At 1st it was weird me kuangalia ndani ya kabati langu kuona nguo zako na viatu au ukiwa unaongea na mimi unaniambia vitu kama "Hivi baby unahisi akiwa wa kiume utafanyaje maana naona umekazana na wa kike" au ukiingia jikoni kwangu and take over my house with good food. The way you look at other women wakinisogelea, how you always know when i need a kiss or a tight hug. The way you force me kuangalia Disney channel, how you wake up early these days to make me breakfast. I might bring you the most beautiful rose flower in the world and it will never look even half as beautiful as you are. When you're jealous unasonya sonya, when am jealous i smile. I would move mountains and planets just to make you happy. I will protect you, love you, spoil you, fight with you, cook with you, watch movies together, drive at night for no reason, sit with you and just stare at the stars.
You're more than i ever asked for, you're my everything "My Wife" 

Uamuzi wa Kufuta Uchaguzi Zanzibar Wazidi Kukosolewa..Mwanasiasa Mwingine Mkongwe Atoa ya Moyoni

$
0
0

Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, ameshangazwa na uamuzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kufuta uchaguzi visiwani humo.

Amesema jumuiya za kimataifa zilishtushwa na uamuzi huo, amesema kinachotakiwa hivi sasa ni haki itendeke kwa kila kila upande kukaa na kutafuta suluhisho la kudumu. “Tanzania haijazoea migogoro ya siasa jambo ambalo si jema katika sura ya kimataifa,” alisema.

Mwanadiplomasia huyo wa kimataifa ametoa kauli hiyo,baada ya Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, kutangaza kufuta matokeo ya uchaguzi huo Oktoba 28, mwaka jana.  Alisema hatua ya kufutwa uchaguzi  wa Zanzibar ni jambo lililowashangaza  wengi kwa kuwa uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu, huku waangalizi wa ndani na nje wakiusifia katika ripoti zao. “Ni hatua ambayo imewashangaza wengi…imeibua sintofahamu kubwa katika nchi yetu kwa sababu uchaguzi uliopita Tanzania ilipata sifa,baada ya uchaguzi kufanyika kwa amani na utulivu. Lakini kitendo cha kufutwa kumewashangaza wengi na bado suala hili halieleweki. “Pia hili jambo sidhani kama ni la mtu mmoja…sidhani kama ni la Jecha peke yake. Huu si mustakabali mzuri kabisa, Zanzibar ni nchi ndogo, lakini ina historia kubwa kisiasa hivyo juhudi za pamoja zifanyike kutatua mgogoro huu kwa matakwa ya Watanzania kwa ujumla.

Sakata la IPTL na ESCROW Laibuka Upya..Watetea Rasilimali Wamtaka Rais Magufuli Amkamate Seth wa IPTL

$
0
0

JUMUIA ya Wanazuoni Watetezi wa Rasilimali nchini (JUWARA), imewataka wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania linalotarajia kuanza rasmi vikao vyake vya kujadili hotuba ya Rais aliyoitoa wakati wa kulizindua bunge hilo hapo kesho, 
kumuomba na kumkumbusha Rais DK. John Pombe Magufuli kutoa agizo la kukamatwa mara moja kwa mfanyabiashara Harbinder Sing Sethi ambaye ni mmiliki wa kampuni ya IPTL/PAP inayoendesha mtambo wa kufua umeme wa dharura uliopo tegeta Salasala kama sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge lililopita .

Wanazuoni hao wamesema kuna kila sababu ya wabunge wa bunge hili la 11 kusimama imara ili kutetea rasilimali za taifa letu zinazoonekana kutafunwa na wajanja wachache wanaotumia visingizio dhaifu vya sheria na uwekezaji kwa kumtaka Rais John Magufuli aharakishe utekelezwaji wa maazimio hayo ya Bunge hasa azimio namba moja lililoitaka serikali kumchukulia hatua kali na kumkamata mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Herbinder Sing Seth kwa makosa ya kulisababishia taifa hasara ya zaidi ya bilioni 320 kutokana na wizi uliofanyika katika akaunti ya TEGETA ESCROW.

Pia, jumuia hiyo imesema ina imani kubwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo huku ikimtaka awe mwangalifu na asiwe mtetezi wa IPTL safari hii kwa kuwa maamuzi ya bunge yalikuwa sahihi dhidi ya kampuni hiyo, ambayo imeisababishia hasara kubwa serikali kutokana na vitendo vyake vilivyofanya.

Wakizungumza na JAMVI LA HABARI, Mwenyekiti na Katibu wa Jumuia hiyo, Omary Kisambu na Mahmud Salibaba kila mmoja,wameonyesha kusikitishwa na kitendo cha serikali kumkumbatia mfanyabiashara huyo, anayelalamikiwa na watanzania wengi kwa kulitia hasara taifa kutokana na vitendo vyake alivyovifanya kwenye sakata nzima la akaunti ya Tegeta Escrow.

"Tunashangaa mpaka sasa mapendekezo na maazimio muhimu ya Bunge kuhusu TEGETA ESCROW hayajatekelezwa na badala yake wameishia kuwatoa kafala kina William Ngeleja na Anna Tibaijuka, hii haitakiwi kuachwa ipite hivi hivi, lazima kama vijana wasomi tusimame kidete kupigania taifa letu na rasilimali zake"alisema Mwenyekiti huyo.

Naye, Katibu wa Elimu na Mawasiliano wa Jumuia hiyo, Mahmud Salibaba amelinukuu azimio namba moja na kushangaa kuona serikali imekubali kutekeleza azimio namba nane wakaliacha azimio namba moja ambalo linahitaji utekelezaji tu.

Mahmud aliongeza kuwa azimio namba moja linasema

"Bwana Harbinder Singh Seth na wengine,Bunge linaazimia kwamba, TAKUKURU, Jeshi la Polisi na Vyombo vingine husika vya Ulinzi na Usalama, vichukue hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, dhidi ya watu wote waliotajwa na Taarifa Maalumu ya Kamati, kuhusika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na Miamala ya Akaunti ya Escrow, na watu wengine watakaogundulika kufuatia uchunguzi mbalimbali unaoendelea kuhusika katika vitendo vya jinai". Aliinukuu.

Katibu huyo, alisema "Hatuna wasiwasi na Prof. muhongo, Tunaamini ana mapenzi mema na utayari wa kulitumikia taifa katika sekta hii, lakini kwenye hili tunamtaka aweke mbele maslahi ya Taifa na kamwe asigeuke kuwa mtetezi wa IPTL wala Sethi".

Wanazuoni hao wameendelea kuonyesha matumaini yao kwa Bunge hili huku wakiamini kwamba kama ilivyo kawaida ya mabunge yaliyotangulia, panapotokea masuala ya kitaifa yenye maslahi mapana kwa nchi basi wabunge wav yama vyote huungana na kuweka tofauti zao pembeni na kulisimamia taifa liokoe rasilimali zake.

IPTL/PAP YAMZUIA ZITTO KABWE KUZUNGUMZIA.

Wakati hayo yakiendelea, kampuni hiyo inayolalamikiwa kuingizia hasara ya mabilioni serikali na kupelekea kuwajibishwa kwa watumishi kadhaa wa umma, imejitokeza na kuwataka wabunge waache kulizungumzia suala hilo kwa kuwa bado lipo mahakamani.

Katika taarifa iliyosambazwa kama tangazo iliyosainiwa na Katibu na Mshauri mkuu wa sheria wa Kampuni hiyo, Joseph Makandege, imemtaka Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto kutokuendelea kulizungumzia suala hilo na kwamba aache mpango wake wa kutaka kulifufua upya suala hilo hasa bungeni kwa kuwa tayari kampuni hiyo imeshamshitaki katika kesi ya madai iliyopo mahakama kuu na kwamba haitakuwa busara kwa mbunge huyo kulizungumzia suala hilo ambalo yeye binafsi ana maslahi nalo.

Kadhalika taarifa hiyo inasema kwamba tayari serikali imejibu kupitia hotuba ya Rais mstaafu Jakaya kikwete pindi alipokuwa madarakani kuwa haipo tayari kumkamata Sethi wala kutaifisha mitambo hiyo kwa kuwa itasababisha kuanzishwa kwa mahusiano mabovu na wawekezaji, hivyo Makandege amesisitiza kwamba ni vema mbunge huyo na mbunge mwingine yoyote aachane na mpango wa kuliibua suala hilo bungeni. 

‘’kwa uelewa wetu mdogo kuhusu maswala haya, kauli ya Rais huwa ndio kauli ya mwisho na ni sawa na hukumu, na tayari Rais (Rais Mstaafu Kikwete) alishasema kuwa suala hilo haliwezekani ‘’. Ilisisitiza taarifa hiyo ya Makandege.

‘’katika hali ya kiubinaadamu, si vema kwenda bungeni kushusha lawana na tuhuma kuwatuhumu watu na ama kampuni ambazo zenyewe haziwezi kuingia bungeni kujitetea’’. Ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

‘’Hata mheshimiwa Zitto alifanya makosa kujihusisha na suala la IPTL/PAP wakati akijua kuwa ameshtakiwa mahakamani na kwamba moja kwa moja anakuwa na mgogoro wa kimaslahi, japo hajatamka mahala popote kuwa ana mgogoro wa kimaslahi na sakata husika’’. Iliongeza sehemu ya taarifa hiyo

ZITTO KABWE AWAJIBU .

Naye mbunge wa Kigoma mjini ACT – WAZALENDO ambaye wakati wa mjadala wa sakata hilo la ESCROW alikuwa mwenyekiti wa kamati ya Bunge inayosimamia hesabu za serikali, amejibu taarifa hiyo kwa kusema ni ya uongo inayoambatana na uoga wa kuwajibishwa na bunge baada ya kugundua maovu yao na kwamba IPTL /PAP hawana mamlaka ya kisheria kumzuia mbunge kujadili swala lolote ndani ya bunge akiwa anatimiza wajibu wake wa kikatiba.

‘’Sikuwa na soma ripoti yangu wala kuwasilisha maoni yangu, nilikuwa nawasilisha ripoti ya kamati ya kudumu ya bunge kwa hiyo si sahihi kulihusisha swala lile na mambo binafsi’’inasema taarifa ya Zitto Kabwe

‘’Mpaka wakati nawasilisha taarifa ya kamati bungeni, sikuwa nimewahi kupokea hicho wanachosema ni shitaka lao kwangu, kwa kuwa tumesoma ripoti mwezi November mwaka 2014 na nimeletewa shitaka lao mwezi mei mwaka 2015, kwa hiyo sikuwa na mgogoro wowote wa kimaslahi kama wanavyotaka kuuaminisha umma’’. Iliongeza taarifa ya mbunge huyo.

Zitto aliongeza zaidi kwa kusema kwamba mpaka sasa hajapokea taarifa ya kimahakama ikimzuia kutokujadili hoja inayohusiana na yeye kujadili jambo linahusiana na IPTL/PAP na badala yake amepokea taarifa ya kesi ya madai ya fedha na hivyo haki zake za kutumia katiba kujadili maswala ya kitaifa ndani ya bunge zipo pale pale na kwamba ataendelea kuwawakilisha watanzania kwa kusimamia rasilimali za taifa.

Sakata la IPTL na akaunti ya ESCROW lilibua hisia mbali mbali wakati wa mjadala wake uliodumu kwa zaidi ya miezi saba mwaka juzi na kuhitimishwa mapema January mwaka jana baada ya Waziri Muhongo kujiuzulu

Credit: Jamvi La Habari

Zari Hassan wa Diamond Aukacha Ukristo ! Atoa Tamko la Kuifuata Dini ya Baby Wake

$
0
0

BAADA ya sintofahamu nyingi kuibuka katika mitandao ya kijamii kuhusiana na picha za mpenzi wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zari the boss Lady, kusambazwa katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha akibatizwa mtoni, mwenyewe ameibuka na kuweka sawa sintofahamu hizo.

Akizungumza na mtangazaji, Millard Ayo kupitia kipindi cha Top Twenty, Zari alikubali kuwa picha hizo ni kweli zinaonyesha tukio la kweli la kubatizwa kwake lakini ilikuwa mwaka 2013 huku akishangazwa na usambazaji wa picha hizo kwa mwaka huu wa 2016.

“Nikweli nilibatizwa na kuwa Mkristu ilikuwa mwaka 2013, lakini sasa nina maisha mengine nimefuata dini ya mpenzi wangu, Diamond, nashangaa kwa nini picha hizo za mwaka huo ziwe stori leo wakati ni muda mrefu na sasa nina maisha yangu mengine,” alisisitiza Zari.

Aliongeza kwamba, licha ya kuwa na maisha yake mapya anaendelea na mambo yake mengine kwa kuwa yupo na maisha mapya hivyo anafuata dini ya mpenzi wake huyo ambaye ni maarufu na nyota katika muziki wa Bongo Fleva nchini huku akiwa na idadi kubwa ya tuzo zinazotokana na umahiri wa muziki wake.

Mtanzania

Penzi Moto Moto la Nisha na Baraka de Prince..Nisha Atia Neno

$
0
0

Staa wa Bongo Muvi, Salma Jabu ‘Nisha’ ambaye kwa sasa yupo kwenye malavidavi na Mwanamuziki Baraka Andrew ‘Barakah Da Prince’, amefunguka kuwa hajali ni wangapi wanampenda jamaa huyo kikubwa analala naye na kuamka naye.

Akizungumza na mwandishi wetu, Nisha alisema kuwa kwa kawaida tamaa kwa wanaume ni jambo la kawaida lakini kwa upande wake anaangalia ni jinsi gani mwanaume huyo anavyompenda na kumjali huku akilala na kuamka naye.

Chanzo: Global Publishers

Marudio ya Uchaguzi Zanzibar Yaivuruga CUF

$
0
0

Uchaguzi wa marudio wa Zanzibar ambao umepangwa kufanyika Machi 20, mwaka huu, umesababisha Chama cha wananchi (CUF) kushindwa kufanya maadhimisho ya kuwakumbuka wenzao waliofariki dunia mwaka 2001.

Maadhimisho hayo hufanyika Januari 27 ya kila mwaka yakishirikisha viongozi wakuu wa chama hicho pamoja na wafuasi wake.

Akizungumza na Nipashe jana, Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho Taifa, Abdul Kambaya, alisema uongozi wa CUF taifa hautafanya maadhimisho hayo kwa kuwa siku hiyo Kamati Ttendaji itakuwa inafanya kikao cha kujadili tarehe ya marudio ya uchaguzi ambayo ilitangazwa hivi karibuni na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec).

Kambaya alisema siku hiyo kamati itakutana kuandaa ajenda kuhusiana na kutangazwa kwa tarehe hiyo ya uchaguzi ambazo zitapelekwa katika Baraza Kuu la chama.

“Ni vijana tu ndiyo watafanya maadhimisho hayo kwa upande wa Zanzibar na ndiyo ambao watafanya maandamano ya kukumbuka mauaji hayo.”

Maandamano hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka kama kumbukumbu ya kuomboleza vifo vya wafuasi wa chama hicho waliouawa Januari 27, mwaka 2001 wakati wa maandamano ya kupinga matokeo ya urais visiwani humo.

Viewing all 104709 articles
Browse latest View live


Latest Images