Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

Shilole Ametua kwa Kidume Mpya

$
0
0


Baada ya kumwagana na aliyekuwa mwandani wake, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, staa mwenye makeke wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ametua kwa kidume mpya ambaye ndiye mrithi wa Nuh ambapo wikienda iliyopita alijiachia naye ‘live’ wakiwa nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.

Akizungumza na mwanahabari wetu kwa njia ya simu wikiendi iliyopita, Shilole alifunguka kwamba hataki tena ‘stresi’ kama alizokuwa akizipata kwa mpenzi wake huyo wa zamani hivyo sasa hivi anataka maisha ya furaha na jinsi gani ya kutumia akili yake ili kutengeneza fedha.
“Acha tu sasa hivi nipunguze machungu yangu maana sihitaji tena stresi, nimepumzisha akili yangu kwa mtu sahihi kabisa ambaye nafikiri yuko karibu yangu, mambo ya Nuh tupa kule,” alisema Shilole au Shishi.

Msanii huyo alifunguka kuwa maisha yake yamebadilika kabisa na hataki kuwa na kitu cha historia ambacho kilimuumiza na kumtesa kwani anataka maisha mapya kabisa ndiyo maana ameamua kutumbua majipu ambayo yalikuwa yakimsumbua.
Kwa upande wake Nuh alipotafutwa kujua mtazamo wake baada ya Shishi kumwanika mwanaume wake mpya, jamaa huyo hakuwa na la kusema zaidi ya kumtakia Shilole kila la heri.

Source GPL

Mwanasheria Mkuu Amtaka Shein Kujiuzulu Urais

$
0
0

Mwanasheria Mkuu (AG) wa zamani Zanzibar, Othman Masoud Othman, amesema Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, anapaswa kujiuzulu kwa sasa na Jaji Mkuu kuiongoza visiwa hivyo kwa kuunda kamati maalum itakayochunguza uhalali wa kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu visiwani humo. 

 Aidha, amesema Rais Dk. John Magufuli anapaswa kuingilia kati mgogoro uliopo visiwani humo, ili kuinusuru nchi kuingia katika mgongano wa kisiasa.

 Aliyasema hayo jana wakati wa kongamano la wazi juu ya changamoto za kisheria zilizojitokeza baada ya kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana, lililoandaliwa na Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), jijini Dar es Salaam jana.

 Alisema Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu, anapaswa kuingoza Zanzibar kwa sasa na kuunda tume huru itakayochunguza uhalali wa kisheria uliosababisha kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi huo na kusababisha mvutano wa kisiasa visiwani humo.

 Alisema endapo kamati hiyo itabaini kuwa hakukuwa na uhalali wa kufutwa kwa uchaguzi huo, waliohusika kufutwa watatakiwa kufikishwa katika mikono ya sheria.

Source: Nipashe

Breaking News:Rais Magufuli Atumbua Majipu NIDA....Amsimamisha Kazi Mkurugenzi Mkuu na Maofisa Wengine Wanne Kwa Tuhuma za Ubadhirifu wa Fedha

$
0
0

1.0           Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

1.1 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ametengua uteuzi waBwana Dickson E. MAIMU, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kuanzia leo, tarehe 25 Januari, 2016.

1.2 Aidha, baada ya utenguzi huo, Bwana Dickson E. MAIMU amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, pamoja na wafuatao:

1.2.1    Bwana Joseph MAKANI, Mkurugenzi wa TEHAMA

1.2.2.   Bi Rahel MAPANDE, Afisa Ugavi Mkuu

1.2.3    Bi Sabrina NYONI, Mkurugenzi wa Sheria

1.2.4    Bwana George NTALIMA, Afisa usafirishaji

1.3  Taarifa zilizomfikia Rais zinaonesha kuwa NIDA hadi sasa imetumia Sh.179.6 bilioni. Kiasi hiki ni kikubwa na Rais angependa ufanyike uchunguzi na ukaguzi jinsi fedha hizi zilivyotumika, maana Rais amekuwa akipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na kasi ndogo ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa.

1.4 Hivyo, Rais ameelekeza Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) wafanye ukaguzi maalum wa manunuzi yote yaliyofanywa na NIDA.

1.5 Rais pia ameelekeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanye ukaguzi maalum wa hesabu za NIDA, ikiwemo ukaguzi wa “value for money” baada ya kuthibitisha idadi halisi ya vitambulisho vilivyotolewa hadi sasa.

1.6 Rais vile vile ameelekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ifanye uchunguzi kujiridhisha kama kulikuwa na vitendo vya rushwa au la.

2.0  Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa

2.1 Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Mahadhi Juma MAALIM ameteuliwa kuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Kuwait, kufuatia uamuzi wa Serikali kufungua Ofisi ya Ubalozi katika nchi hiyo rafiki.

2.2  Rais ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kianda na Kimataifa kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili ambao mikataba yao imeisha. Leo hii Mabalozi hao wanatakiwa kukabidhi kazi kwa Afisa Mkuu au Mwandamizi aliye chini yao. Mabalozi hao ni:

2.2.1    Bi Batilda Salha BURIANI, aliyeko Tokyo, Japan

2. 2.2   Dkt. James Alex MSEKELA, aliyeko Rome, Italia.

2.3 Rais amemrejesha nyumbani Balozi wa Tanzania aliyeko London, Uingereza,Bwana Peter Allan KALLAGHE. Anarejea Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa atakapopangiwa kazi nyingine.

2.4  Kwa maana hiyo, vituo vya Ubalozi vifuatavyo viko wazi:

2.4.1  London, kufuatia kurejea nchini kwaBalozi Peter A. KALLAGHE

2.4.2    Brussels, kufuatia aliyekuwaBalozi, Dkt. Deodorous KAMALAkuchaguliwa kuwa Mbunge.

2.4.3    Rome, Italia, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Dkt. James Alex MSEKELA.

2.4.4    Tokyo, Japan, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Bibi Batilda BURIANI

2.4.5    Kuala Lumpar, Malaysia, kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt. Aziz PonrayMLIMA, kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa.

2.4.6    Brasilia, Brazil, kufuatia kustaafu kwa aliyekuwa Balozi, Bwana Francis MALAMBUGI.

3.0   Tawala za Mikoa

3.1 Rais ametengua uteuzi wa Eng. Madeni Juma KIPANDE kabla hajathibitishwa kwenye cheo cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi kutokana na utendaji kazi usioridhisha.

4.0       Utumishi wa Umma

3.2  Nachukua nafasi hii kuwahimiza viongozi wote katika Utumishi wa Umma, na watumishi wote wa umma, kubadilika kwa dhati kwenye utendaji wao na uadilifu wao.

3.3 Napenda kusisitiza kuwa Rais na sisi tunaomsaidia hatuoni raha kuchukua hatua dhidi ya viongozi na watumishi wengine. Tungependa kila mtu mwenyewe ajirekebishe na kutomfikisha Rais mahali ambapo inabidi amchukulie hatua. Mambo yafuatayo ni muhimu:

4.2.1 Kila kiongozi na kila mamlaka ya nidhamu isipate kigugumizi kusimamia utendaji na maadili ya kazi.

4.2.2 Kila kiongozi na kila mamlaka ya nidhamu asipate kigugumizi kuchukua hatua za nidhamu, lakini afanye hivyo kwa kuzingatia kwa ukamilifu sheria, kanuni na taratibu katika Utumishi wa Umma.

4.2.3   Lazima uongozi na watumishi wa umma wawahudumie wananchi kwa haki, weledi, uadilifu na heshima. Kwa sababu hiyo:

a)  Kila ofisi ya Serikali iwe na dawati la kusikiliza shida za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

b) Kwenye kila Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wajenge uwezo wa kushughulikia shida za wananchi kwa ukamilifu na kwa wakati. Kwa muundo wa Serikali yetu hakuna sababu kwa mwananchi kufunga safari mpaka Ikulu Dar es Salaam kwa kuamini kuwa ni Rais tu anayeweza kumaliza matatizo yake, maana wawakilishi wa Rais wako kila pembe ya nchi yetu. Ikibidi wananchi wafike Ikulu ina maana hao wawakilishi wa Rais hawakutimiza wajibu wao.

c)  Kuanzia sasa watumishi wote wa umma wavae majina yao ili iwe rahisi kwa mwananchi kumtambua anayemhudumia na hivyo kumsifu mtumishi wa umma anayewahudumia kwa weledi, uaminifu na kwa wakati, na kumtolea taarifa yule anayefanya mambo ya hovyo.

d) Kila ofisi ya Serikali iwe na utaratibu wa kupokea maoni ya wananchi kuhusu huduma inayotolewa kwenye ofisi hizo, na kushughulikia haraka maeneo yote ambayo wananchi wataonesha kutoridhika na huduma.

                                                            

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Arusha

25 Januari, 2016

Baaada ya Home Shopping Center, UDA Nayo Yatangaza Kufilisika..Wadau Wadai ni Ujanja

$
0
0

Baada ya Home Shopping Center, sasa Robert Kisena naye atangaza UDA kufilisika. Wadau wadai ni janja ya kukwepa mkono wa sheria.

Yeye adai ni kutokana na madeni makubwa anayodaiwa ambayo yanazidi fedha zilizomo kwenye akaunti ya UDA.

ESTER Bulaya Amgaragaza Tena Wasira...Ashinda Kesi ya Uchaguzi iliyofunguliwa Kupinga Ushindi Wake

$
0
0
Ester Bulaya Ameandika Maneno haya Baada ya Ushindi wa Mahakamani;

"Nilimshinda Wasira kwa wananchi, na leo nimemshinda kisheria, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imetupilia mbali kesi ya Uchaguzi dhidi yangu, iliyofunguliwa na wapambe wa wasira. Mungu husimama na watu waliowema. Nakutumaini mungu wangu na wewe ndiye mlinzi wangu.Asante sana Wananchi wangu wa Bunda Mjini mliokwenda Mwanza kusikiliza Hukumu. Mbunge wenu nipo dodoma tayari kwa kuanza vikao vya Bunge Kesho." Ester Bulaya

Wema Sepetu na Idriss Sultan Wavujisha Picha Wakiwa Kitandani Kama zile za Watuache Tulale..Mashabiki Walalamika

$
0
0
Picha za Wema Sepetu na Idriss Wakiwa kitandani asubuhi ya leo zimesambaa katika mitandao ikiwa ni siku moja tu baada ya Idriss kuweka wazi uhusiano wao wa kimapenzi na kuwa wanakaribia kupata mtoto...

Mashabiki wa couple hiyo inayoongelewa zaidi kwa sasa wametoa maoni yako katika picha hizo, hapa nimekuwekea baadhi ya maoni;

 tamia_ismail
@zara_elia u u gat the point,l lov ths lady ila apo tu ndo anaponiudhi ...she like to expose evrythin i wsh she cn lern to keep othr things fr herself wala asingekua midomon mwa watu..anyway evry one has got a weaknes

sy_salum_y_madai 
Wewe idrus chaliloo ukija machimboni R chugga lazima tukuwekechini...maan kweli... Ustaa wa gafla unakuzingua maan wakati tumetoka mbali Manzi yako umemwacha bonge lakisu unaenda Pambana na makonkodi maan... Dah unazingua maan

 team.watafutaji 
Kila mwanaume anamtimia wema kwa manufaa yake na kujipatia umaarufu


pcolour543 
Tushazoea huyo dada na hzo picha.. Sio ajabu


 zara_elia
Ila jamani vitu vingine wema angekuwa havionyeshi sasa kila mwanaume anayekutana nae asubui jion kitandani picha haipendezi jamani..angekuwa anasubiri hadi aone uhusiano ukikomaa japo


violetmoshi
@nchinyavu Unajua Sina Team Hapa Ila Unajua ukiwa Kwenye Sanaa Ni bora uexpose kazi yako Na Maisha yako private yawe Ni Siri yako! Nampenda sana Shaa, Kiukweli natamani Wasanii wote Wafuate mienendo yake Na Ndio maana humsikii akisemwa Ovyo, Unadhani hana kasoro au scandal?! No anayo maana Na yeye Ni Binaadam lkn Kwa Kuwa Kwenye social media tunaona habari Za Shaa Na hatuoni habari Za Sarah Kaisi Wala kuzijua! Nadhan anatumia njia nzuri ya Kimaisha Na si Kama hawa wengine kutwaaaa mitandaoni na private life Zao mwishowe tuna kujua nyumbani Hadi mwilini Mpaka vinyweleo Na makovu uliyonayo!


mwacityhamis
Team @DNA mkilala mwalala na makeup mwamuona mwenzenu alivyo mzuri bila makeup akaaaa nipishe mieeeee


guga_ii 
Subiria uzimalize za bba ndo utajutraaaa


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Januari 26, Ikiwemo ya Mama Idris Kuikataa Mimba ya Wema Sepetu

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Januari 26, Ikiwemo ya Mama Idris Kuikataa Mimba ya Wema Sepetu

Membe Adai Wana CCM ni Wanafiki Hawataki Magufuli Akosolewe

$
0
0
Benard Membe
Aliyekuwa waziri wa mashauri ya nje,Ndg.Membe amewajibu wanaotaka akae kimya kuwa hawezi kunyamaza na anatumia haki yake kikatiba bila kuvunja sheria.

Membe amewataka wajibu kwa hoja badala ya kumziba mdogo.
Membe ameongeza kuwa baadhi ya wana CCM wamekuwa wanafiki wa kutupwa na hawataki Magufuli akosolewe.

Atakuwa mstari wa mbele kutoa maoni huru kwa mambo yanayoendelea bila kuvunja sheria.
Amesisitiza kuwa rais Kikwete atakumbukwa sana kwa kuwapa watu uhuru wa kutoa maoni yao

Tahadhari kwa Wazazi Wanaogiza Wasichana wa Kazi Toka Mikoani ,Ambao Unatoa Pesa na Kutumiwa Mdada wa Kazi

$
0
0
Picha ni ya Tukio jingine la mfanyakazi aiusiani na habari hii
Nimepokea huu ujumbe kutoka Arusha..Nami nimeona si vibaya na wewe ukausoma;

Onyo kwa wazazi wanaogiza wasichana wa kazi,ambao unatoa pesa unatumiwa! Jana huko Arusha ilikuwa hivi;

Mschana wa kazi alitoroka na mtoto wa miaka kumi tangu saa kumi usiku akamuacha wa miaka 5 akamwambia tunakuja,mtoto mdogo wa miaka 5 aliogopa chumbani na kuamua kwenda kugonga kwa mama yake, kuanzia saa kumi usiku dada hakujulikana alipo na mtoto wa miaka 10, mama alitangaza Redio Safina na Monchwary alienda hola! Kamanda wa polis na jeshi la polis jana walitanda mji wa Arusha na kukagua kila gari bila mafanikio, Baadae sana wakaona Tax nyeusi wakasimamisha dada kabadili mavazi na mtoto wa miaka 10 akiwa amelala tu gari ikawapelekwa kituo cha polisi kusachia dada kakutwa na kisu kipya kikali sana, anaulizwa alikuwa wanaenda wapi hajibu, kisu cha nini nilikuwa naenda kumuuwa mimi huwa nafanyaga hivyo na hii sio mara moja hii ni kazi yangu cha ajabu yule mtoto mpaka saa 6 tunapigiwa simu ajazinduka, hasemi kampa nini mtoto, mtoto amepelekwa hospitali kwa uchunguzi,wazaz wezangu watoto wetu tunawapata kwa shida sana katika kujifungua tuwe makini uzazi umekuwa mgumu sana na hao wasichana wakutumiwa katika gari mh mh!! Msichana wa kirangi anajibu mimi ndio kazi yangu nishawauwa wengi sana bila kuogopa police inatisha...

Rais Magufuli Amempongeza Jakaya Kikwete Kwa Kuteuliwa Nafasi ya Umoja wa Mataifa Kama Mshauri

$
0
0
Jakaya Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Ban Ki-moon kuunda jopo la watu mashuhuri watakaomshauri juu ya namna bora ya kuendeleza na kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu hususani katika afya ya uzazi ya Mama na mtoto.

Jopo hilo la watu mashuhuri linaongozwa na wenyeviti wenza ambao ni Rais wa Chile Mheshimiwa Michelle Bachelet na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mheshimiwa Hailemariam Desalegn, huku Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete na Rais Mstaafu wa Finland Mheshimiwa Tarja Halonen wakiteuliwa kuwa wenyeviti mbadala.

Katika Pongezi hizo Rais Magufuli amesema kuteuliwa kwa Rais Kikwete kuwa miongoni mwa jopo la kumshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kumeijengea heshima Tanzania na kumechochea matumaini ya mafanikio ya kukabiliana na changamoto za afya ya mama na mtoto hususani kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.

Rais Magufuli ameahidi kuwa serikali yake ya awamu ya tano itatoa ushirikiano katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ambayo jopo hilo litamshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ikiwemo katika kuimarisha afya ya uzazi wa mama na mtoto.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
25 Januari, 2016

Download Udaku Special Blog Android Application Katika Smart Phone Yako Kupata Habari za Udaku na Siasa Kwa Urahisi

$
0
0

Good News! Sasa Blog yako ya Udaku Special Ipo Google Play Store.

Download Udaku Special Blog Android Application CLICK HERE From Play Store

Au Search Udaku Special Blog Kwenye Play Store kisha Bonyeza Install

Usipitwe!!!

Diamond Platnumz: Baada Ya Nape Nnauye Mimi Ndo Waziri wa Habari Na Michezo Mtarajiwa

$
0
0
Diamond Platnumz amesema akiachana na muziki anataka kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuweka vitu sawa na kutoa fursa zaidi kwa vijana.

Akizungumza katika kipindi cha Papaso cha TBC FM, Diamond alisema kama akiingia kwenye siasa basi nia yake ni kuwa Waziri wa Michezo.

“Kwa sasa hivi siasa bado ila nikiingia kwenye siasa baadaye akimaliza mheshimiwa Nape nachukua mimi kile cheo cha Waziri wa Michezo,” alisema na kuongeza;

“Kile nakiweza kabisa kwa sababu mimi ukinimbia sijui kuhusu mpira, movie mimi naweza kabisa nikiwa Waziri, nikavifanya na vikawa na maendeleo.

"Ni kitu ambacho naweza siyo nasema nataka kuwa mbunge ila mimi nataka ile siku nimeacha kufanya muziki naingia kwenye siasa basi nakuwa Waziri  wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuboresha vitu”

Diamond ambaye hakuweka wazi kwamba ataingia kwenye siasa kupitia chama gani, mwaka jana katika kampeni za uchaguzi mkuu uliomuingiza rais Magufuli madarakani, alishiriki kikamilifu kwenye kampeni za CCM na kutengeneza wimbo pamoja na video.

Le Mutuz Mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu Amvaa Benard Membe..Adai Membe Ametukosea Sana Watanzania....

$
0
0
Lemutuz
Kufuatia kauli za aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa katika awamu ya nne Bernald Membe, kuonekana kupinga juhudi za Rais John Pombe Magufuli kwenye masuala mbalimbali ikiwemo suala la Safari za nje kwa viongozi wa Umma.lemutuzzzzsss

Mtoto wa aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania John Malecela, anaefahamika kwa jina la Le Mutuz Nation amefunguka ya moyoni na kueleza kuwa anachokifanya Membe sio ustarabu kwa serikali ya Magufuli kwani hajatumia ustarabu kama kiongozi na kuamua kuonesha ubinafsi.

Ameandika Kama Ifuatavyo;

LIVE STRAIGHT TALK:- Morning Guys Membe ametukosea sana WaTanzania kwa kauli zake Kali za kukemea juhudi za Mabadiliko ya Rais Magufuli ambaye ndio kwanza anakaribia kutimiza mwezi wa pili katika Madaraka infact Membe ameonyesha Tabia moja isiyokuwa nzuri sana kwetu wote binadam yaani UBINAFSI au SELFISHNESS...I mean Rais Magufuli anachokifanya ni kile alichokiahidi ambacho hata Membe mwenyewe alikiunga sana mkono kwenye kampeni za Urais na sisi wote Magufuli alisema wazi kwamba Taifa limeoza Membe alikuwa na nafasi kubwa kumkatalia then kwamba sio kweli Taifa halijaoza kwa sababu labda moja ya sababu ya Membe kujitokeza now na kauli Kali ni kujaribu kutetea record ya utawala aliokuwa mshiriki wa karibu na Rais aliyepita basi anakosea sana kwa sababu tulimkataa Lowasaa kwa kuwa alikuwa Rafiki na matajiri na waliotuambia kwamba Lowassa hafai ni pamoja na yeye mwenyewe Membe sasa Leo kweli tena Membe anasimama kushambulia kazi za Magufuli kwa niaba ya Wafanyabiashara? ....Please Membe atuombe radhi WaTanzania Millioni 50 tuliomchagua Magufuli cause sisi bado hatujalalamika kivileee kama yeye mtu Mmoja ambaye hapa anakuwa kigeu geu ni yeye Membe aliyesifia uamuzi wa Magufuli kusimamisha Safari za Nje kwa Maofisa wa Serikali akasema "Tulikuwa tunapishana Juu kwa JUU kama nyumbani kuna moto" Leo Mwezi Mmoja na Nusu later Membe tena amebadilika anasema Safari ni lazima? WHY? .....jana nilikuwa mstaarabu kidogo nilidhani Membe alipitiwa tu lakini kumsikia akizungumza tena Jana nasema HAPANA agenda aliyonayo Membe this time around sio yetu Wananchi ninaanza kuwa na wasi wasi labda Rais JK aliwapa watu wengi vyeo kwa USHAURI wa Membe ndio maana sasa anaumia kuona alikuwa anamshauri vibaya Rais like sio siri Mkurugenzi wa NIDA alikuwa ni Rafiki wa karibu sana wa Membe Jana tu imedhirika huenda amefuja karibu Tsh. 156 Billion za kodi zetu kwenye vitambulisho vya Taifa now niambie kipi cha ajabu Mkurugenzi wa Shirika la Umma amepata wapi mapesa ya ajabu mpaka kujenga MRC pale nyuma ya Shoppers Plaza Mikochen? ...I mean kuna mambo mengine wanatufanya kama Watoto WHY? Membe amezungumza kutetea Wafanyabiashara na mediocre leaders it is wrong atuombe radhi Watanzania..Lemutuz

Kampuni ya UDA Yakanusha Kufilisika..Yadai ni Njama..Ripoti Kamili ipo Hapa

$
0
0
Mabasi ya UDA
Kumekuwepo na taarifa za uwongo kwenye vyombo vya habari, hasa kijarida cha Dira ya Mtanzania, na mitandao ya kijamii kuhusu uongo kuwa kufilisika kwa Shirika la Usafiri Dar Es Salaam (UDA) Limited.

Menejimenti ya Shirika la Usafiri Dar Es Salaam inakanusha uwongo huo kuwa UDA haijafilisika na haina dalili zozote za kufilisika isipokuwa ni Shirika la namba moja nchini na Afrika Mashariki na Kati linalokuwa kwa kasi ya ajabu kimaendeleo na kibiashara.

Zifuatazo ni takwimu zinazodhihirisha ukweli huu:

UDA imeongeza idadi ya mabasi kutoka mabasi 7 makukuu na mabovu Mwaka 2012 na kufikia takribani mabasi 400 mwaka 2015 yakiwemo mabasi 255 ya kawaida na mabasi makubwa – Hercalus, mapya na ya kisasa kabisa duniani (ya BRT) 140.

Ndani ya miaka 3, kampuni ya UDA imekuwa kwa zaidi ya asilimia 5,000

Kampuni hii imeweza kufanya maandalizi yote ya kuwezesha kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART Project) kwa ufanisi mkubwa. Mbali na kununua mabasi, kampuni imeweze kununua mtambo bora na wa kisasa kabisa duniani wa kukusanya nauli na kuongezea mabasi (Intelligent Transportation System – ITS) wenye thamani kubwa kutoka Ubelgiji na Ujerumani. Vile vile kampuni imeweza kusaili na kufundisha madereva wa Kitanzania zaidi ya 300 na kuwaajiri kwa ajiri ya kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART Project)

Kampuni imejenga karakana bora na imara na kununua vitendea kazi vya kisasa kwa ajiri ya mabasi yake ya kawaida na mwendo haraka.

Kampuni imepeleka watendaji wake kwenye miradi mbalimbali ya BRT duniani ili kupata uzoefu wa kuwawezesha kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART Project) kwa ufanisi. Vile vile Kampuni imeweza kuajiri wataalam kutoka nje (expatriates) kwa ajiri kuongezea nguvu wataalam wake wa ndani.

Kwa takwimu chache hizo hapo juu, Kampuni ya UDA ni namba moja Afrika kwenye sekta ya usafirishaji wa abiria barabarani kwa idadi ya watu inaosafirisha, idadi ya mabasi na ubora wa menejimenti.

Mafanikio haya ya Kampuni ya UDA yanatokana na umahiri wa uendeshaji kutoka Simon Group chini Uongozi thabiti wa Mwenyekiti wake Ndugu Robert Simon Kisena na si vinginevyo, kama washindani wetu wavyojaribu kutuchafua kwamba kuna wanasiasa nyuma yake.

Tunawataka washindani wetu waache tabia ya fisi ya kumfuata mtu anayetembea kwa haraka wakidhani atandondosha mkono wapate kitoweo vinginevyo watakufa njaa.

Imetolewa na Uongozi wa SHIRIKA LA USAFIRI DAR ES SALAAM (UDA) LIMITED

Msikilize Idriss Sultan Akifunguka Kwa Mara ya Kwanza Kuhusu Mimba yao na Wema Sepetu..Ataja Mimba Ina Miezi Mingapi!

$
0
0
Wema na Idriss
Kumekuwa na headline nyingi zikiandikwa kuhusu mastaa wa bongo Idris Sultan na Wema Sepetu na hii ni kuhusu mapenzi yao, hapa nakukutanisha na Idris akifunguka yote makubwa usiyoyajua kuhusu mapenzi yao.

Maswali 9 ‘Msukule’ Kukutwa Nyumba ya Tajiri Chini ya Shimo la Choo

$
0
0
Hofu imeendelea kutanda maeneo ya Kibamba jijini Dar na kuacha maswali tisa kwa wananchi kuhusiana na mwanamke aliyekutwa kwenye shimo la urefu wa futi kumi, nyumbani kwa mfanyabiashara aliyejulikana kwa jina moja la Mtei.

HALI YA MWANAMKE HUYO
Mwanamke huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 27, aliwashangaza wakazi wa eneo hilo kwani ndani ya  shimo alilokutwa alionekana mchafu, aliyenyongea, akiwa hoi kwa njaa na mtupu kiasi cha kudhaniwa ni msukule (mtu aliyechukuliwa ndondocha).

SIKU YA TUKIO
Ilikuwa Jumanne ya Januari 19, mwaka huu katika shimo hilo lililojengwa na Mtei, inasemekana kuwa, shimo hilo  ni kwa ajili ya chemba ya choo lakini haijaanza kutumika kwa vile nyumba hiyo nayo haijaanza kukaliwa rasmi na familia zaidi ya kuwepo kwa mlinzi.

 Akiwa uchi shimoni.
UWAZI ENEO LA TUKIO
Kufuatia kusambaa kwa taarifa za mwanamke kukutwa shimoni kwenye nyumba ya mfanyabiashara huyo, Uwazi kama ilivyo ada yake, lilitinga eneo la tukio kwa lengo la kuchimba mawili, matatu kuhusu hali halisi.

MAJIRANI WASHANGAZWA
Baadhi ya majirani wa eneo hilo walionesha kushangazwa na tukio hilo huku wakiwa na maswali hayo tisa kuhusu mwanamke huyo ambaye walisema si mkazi wa maeneo hayo na wala hawajawahi kumuona.

 Mwanamke huyo baada ya kutolewa shimoni.

MASWALI YA MAJIRANI
Ni nani aliyemuingiza shimoni mwanamke huyo na kwa madhumuni gani? Kwani kwa jinsi shimo lilivyo, lazima aliingizwa au aliingia kwa kutumia ngazi.

Alikuwa akiishi kwa kula chakula gani kwani wakati anatolewa, muda mwingi alikuwa akilalamikia njaa.

Swali la tatu ambalo majirani walikuwa nalo, mwanamke huyo aliishi ndani ya shimo hilo kwa siku ngapi? Kwani nywele na kucha zake ziliashiria si zaidi ya mwezi mmoja. Swali kuu, aliingia/ aliingizwa lini na muda gani kati ya mchana na usiku?

Je, aliingizwa kwenye shimo hilo akiwa na nguo zake halafu aliyemwingiza/ waliyomwingiza walizipeleka wapi?

Swali la tano ambalo majirani hao walikuwa wakilijadili sana ni, je! Mwanamke huyo ni mgonjwa wa akili au ni msukule? Kama si chochote kati ya hayo mawili, kwa nini alikuwa hapigi kelele?
Sita, majirani hao waliulizana kama siku za karibuni wamewahi kusikia kwenye vyombo vya habari kuna mwanamke mwenye umri huo anatafutwa? Wote walisema hawajasikia.

Wengi walisema huenda mwanamke huyo aliingizwa kwenye shimo hilo na ‘maadui’ wa biashara wa Mtei. Lakini kama ni kweli, walikuwa na lengo gani na walimpata wapi mwanamke huyo na akiwa katika hali gani?

Katika mahojiano na majirani wakati bado akiwa ndani ya shimo amekaa, mwanamke huyo aliweza kujibu maswali karibu yote, lakini swali la anaitwa nani na ameolewa au la, yalimshinda kujibu. Ni kwa nini?

Polisi Mbezi wanasema wamekuwa wakimpigia simu Mtei, lakini hapokei. Ni kwa nini?

MFANYAKAZI WA MTEI SASA
Naye mfanyakazi anayeitunza nyumba hiyo, Richard Pascal alipozungumza na Uwazi kuhusu tukio hilo alikuwa na haya:

 “Ninachokumbuka mimi, Jumanne, wiki iliyopita, saa 3:00 asubuhi, bosi wangu Mtei alikuja. Ni kawaida yake kuja na kukagua mji wake.

 “Nikiwa naendelea na shughuli zangu, aliniita hapa nje. Nilipofika  aliniambia nichungulie ndani ya shimo. Nilifanya hivyo, nikashtuka sana kumwona mwanamke akiwa mtupu huku akinikodolea macho.
“Niliogopa kwa sababu sikutarajia kama kuna mtu anaishi shimoni bila mimi kujua wakati ndiyo nalinda hapa siku zote.”

Hali aliyokuwa nayo.

AWAITA MAJIRANI
“Niliamua kuwaita majirani. Baada ya muda mfupi watu wakawa wamejazana hapa kila mmoja akishangaa na bosi wangu akatoa taarifa Kituo Kidogo cha Polisi Kibamba ambapo askari walifika.
“Lakini na wao walipatwa na mshangao huku wakijiuliza ni vipi mwanamke huyo aliingia shimoni bila kuumia wala kuvunjika?”

POLISI WAMUHOJI
“Mwanamke huyo alipohojiwa na polisi alisema ameishi humo miaka mingi na mara nyingi alipokuwa akihojiwa alikuwa akililia chakula. Polisi waliniomba ngazi, wakaitumbukiza shimoni kisha yeye mwenyewe akapanda haraka mpaka nje.”

APELEKWA TUMBI
“Polisi walimchukua na kumpeleka Hospitali ya Tumbi (Kibaha mkoani Pwani) ambako nadhani anapatiwa matibabu.”

MLINZI APATA WASIWASI
“Mpaka sasa hivi mimi napatwa na wasiwasi. Nitamuomba bosi wangu aniongezee mtu mwingine ili tuwe wawili, kwani mimi hapa ni mgeni. Nimekuja hapa, Desemba 9, mwaka jana.”

SIKILIZA MAHOJIANO
Uwazi lilifanikiwa kunasa mahojiani kati ya mwanamke huyo akiwa ndani ya shimo amekaa na polisi huku wananchi wakiwa nje wakitaka kumuokoa.
Polisi: “We, unaitwa nani?”
Mwanamke: (kimya).
Polisi: “Unakaa wapi?”
Mwanamke: “Mbezi Makabe.”
Polisi: “Umeolewa?”
Mwanamke: (kimya).
Polisi: “Umekuja lini hapo?”
Mwanamke: “Hapa kwangu.”
Polisi: Umekuja lini?”
Mwanamke: “Mi njaa inaniuma bwana.”

UWAZI NYUMBANI ANAKOISHI MTEI
Uwazi lilifika nyumbani kwa Mtei, Kibamba ya Luguruni jijini Dar, hatua chache tu kutoka kwenye Kituo cha Mabasi Kibamba lakini hakupatikana, Uwazi liliacha namba ya simu lakini hakupiga na ilipopigwa, imekuwa ikiita bila kupokelewa.

UWAZI KITUO CHA POLISI
Siku hiyohiyo, Uwazi lilifika Kituo cha Polisi Mbezi ambapo askari mmoja ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa vile si msemaji wa jeshi hilo, alisema mpaka sasa wanamtafuta Mtei ili kumsikia kwa kina kuhusu tukio hilo kwa vile yeye ndiye aliyepiga simu polisi kutoa taarifa.
“Huyo Mtei, tunamtaka hapa. Yeye ndiye aliyetoa taarifa ya mwanamke kukutwa kwenye shimo nyumbani kwake. Lakini tulipofika hatukumkuta. Na kila tukipiga simu yake, inaita tu bila kupokelewa,” alisema afande huyo.

UWAZI HOSPITALINI TUMBI
Baada ya hapo, Uwazi lilifunga safari hadi Hospitali ya Rufaa ya Tumbi, Kibaha, Pwani ambapo halikufanikiwa kumpata msemaji, lakini muuguzi mmoja wa hospitali hiyo alikiri kupokelewa kwa mwanamke huyo.

UWAZI LAMBANA MTEI
Juzi, Uwazi lilimpigia simu Mtei na mambo yakawa hivi;
Uwazi: “Wewe ni Mtei?”
Mtei: “Eee, unasemaje?”
Uwazi: “Tunaomba ufafanuzi kuhusu yule mwanamke aliyekutwa kwenye shimo nyumbani kwako…”
Mtei: “Ooh! Siyo mimi, yule ni Mchaga mimi ni Muhaya, nipo Kagera.”
Uwazi likamrudia aliyetoa namba…
“Kwani si ulikuwa unaongea naye sasa hivi na akakwambia yeye si Mtei! Nimesikia maongezi yenu, lakini alisogea mbali. Kwa hiyo sijui zaidi.”

KAMANDA WA POLISI KINONDONI
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Christopher Fuime alipoulizwa kuhusu tukio hilo,  alikiri kulitambua na kwamba, bado wanalifanyia uchunguzi.
Yeyote anayemjua mwanamke huyo (pichani ukurasa wa mbele) apige simu namba 0715454656 au 0784 339616, chumba cha habari.

Source;Global Publishers

Nyumba ya Mchungaji Lakatware Yasababisha January Makamba Kuchukua Hatua Kali Kwa Maafisa Hawa

$
0
0
SAKATA la maofisa watatu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), waliosimamishwa kazi kwa tuhuma ya kukiuka miiko yao ya kazi, limechukua sura mpya, baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, kuagiza wafikishwe mbele ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Pamoja na hayo, Waziri huyo amemsimamisha kazi aliyekuwa mwanasheria wa baraza hilo, John Mnyele kwa matumizi mabaya ya ofisi.

Akizungumza  jana, alisema tayari amemwagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, kuwasilisha mashtaka yanayowakabili maofisa hao watatu Takukuru kwa ajili ya uchunguzi na hatua zaidi, ikiwemo kufikishwa mahakamani.

Maofisa waliosimamishwa kazi kutokana na udhaifu huo ni pamoja na Ofisa Mazingira Mwandamizi Dk Eladius Makene, Mwanasheria Daraja la II Wakili Heche Suguta Manchare ; na Ofisa Mazingira Boniface Benedict Kyaruzi. Wanatuhumiwa kukiuka miiko ya kazi yao katika kusimamia kiwanda cha kusindika minofu ya punda kilichopo mkoani Dodoma.

Pamoja na maofisa hao, pia Mwanasheria Mnyele, anayetuhumiwa kuingia mkataba na Mchungaji Getrude Rwakatare wa kuondoa kesi mahakamani kwa niaba ya NEMC bila kuijulisha ofisi, naye anachunguzwa na taasisi hiyo ya rushwa.

Mama Rwakatare kwa sasa ana kesi mahakamani dhidi ya baraza hilo ya kupinga kubomolewa kwa nyumba yake, inayodaiwa kujengwa mahali pasiporuhusiwa.

Kiwanda hicho cha minofu ya Punda cha China, kilianza kazi hiyo rasmi mwaka 2012 huko Dodoma ambapo pamoja na kuchinja, pia huuza nyama hiyo nje ya nchi, hususan China.

Kiwanda hicho kilipatiwa vibali vyote, ikiwemo cha Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA) na cha Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi cha kuchinjia.

Pia, kilikuwa na vibali vingine vya Manispaa. Hata hivyo, hakikuwa na kibali cha masuala ya mazingira kutoka NEMC.

Katika ukaguzi uliofanywa siku za nyuma na Baraza hilo, ilibainika kuwa kiwanda hicho hakina kibali hicho cha mazingira, lakini pia kilikuwa kikilalamikiwa na wananchi wanaokizunguka kutokana na kutofuata taratibu za utunzaji wa mazingira.

NEMC ilibaini kuwa kiwanda hicho, hakikuwa na mfumo wa majitaka, lakini pia kilikuwa kikichoma mabaki yanayotumika kuchinjia ndani ya kiwanda hicho na moshi wake kusambaa maeneo yanayokizunguka.

Kutokana na makosa hayo, baraza hilo lilikifungia kiwanda hicho kama adhabu na kukilipisha faini ya Sh milioni 240.

Juzi Waziri January pamoja na kuwasimamisha maofisa hao watatu kwa kukiuka miiko yao ya kazi, pia aliagiza Mkurugenzi Mkuu wa baraza hilo, Mhandisi Bonaventura Baya, apewe barua ya onyo kali na la mwisho kwa tuhuma za udhaifu katika usimamizi wa watumishi wa baraza hilo, hivyo kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa baraza hilo.

CHADEMA Wamwambia Benard Membe Asiwe Mwoga..Kama Anataka Kuikosoa Serikali Vizuri Ahamie Upinzania Kama Kina Lowassa

$
0
0
Waziri wa zamani wa Mamboya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amekaribishwa kujiunga na Chama Cga Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ikiwa ni siku chache tangu atoe maoni yake akiikosoa serikali ya Rais John Magufuli.

Mwanasiasa huyo mkongwe amekaribishwa na Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob ambaye alimshawishi kwa kutumia mifano ya wanasiasa wakongwe waliokuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliohamia Chadema na Ukawa kwa ujumla akiwemo Edward Lowassa, Frederick Sumaye na Kingunge Ngombale Mwiru.

Wiki iliyopita Membe alinukuliwa akimkosoa Dk Magufuli katika maeneo kadhaa, likiwamo la kubana matumizi, kudhibiti safari za nje na uteuzi wa Baraza la Mawaziri.

Jana, meya huyo kutoka Chadema alisema watu wanamshangaa Membe na kumshambulia siyo kwa sababu amesema mambo ya ajabu, ila yeye si mtu sahihi wa kutoa kauli hiyo.

“Watu hawashangai alichosema (Membe) kwa sababu siyo hoja ngeni, zimesemwa sana na wapinzani. Wanachoshangaa ni yeye (Membe) kusema hayo. Hafanani na hoja anazoziongea,” alisema.

Jacob ambaye alikuwa diwani katika manispaa hiyo katika Serikali ya Awamu ya Nne alisema, hoja zilizotolewa na Membe ni nzuri na kama zingetolewa na mpinzani zingeonekana zina mashiko zaidi.

"Asiwe vuguvugu, hicho ndicho kinachompa shida. Kama anataka kuja huku asiwe na wasiwasi chama changu kitampokea na hata hayo anayoyaongea yatakuwa na mantiki na watu watamsikiliza kwa sababu ni upinzani,” alisema na kuongeza;

“Avuke moja kwa moja kama walivyofanya akina Kingunge (Ngombale Mwiru), (Edward) Lowassa, na (Frederick) Sumaye kuhamia upinzani.”

Jacob alisema Sumaye na Lowassa ambao waliwahi kuwa mawaziri wakuu na Kingunge aliyekuwa kada mkongwe wa CCM, walikuwa viongozi wa ngazi za juu, lakini walihamia upande wa pili (upinzani) na sasa wanaisimamia na kuikosa Serikali kwa uhuru.

“Asiwe mwoga kwamba ataishi maisha gani, Sumaye na Lowassa wamekuwa mawaziri wakuu wakaondoka na maisha yanaendelea.”

Hata hivyo, Jacob alisema Membe hakupaswa kukosoa sera ya Rais Magufuli ya matumizi na Rais kudhibiti safari za nje, kwa sababu yeye amenufaika nayo.

“Nadhani hakuwa mtu sahihi kusema hayo, alipaswa kwanza kumtafuta mtu mwingine aseme halafu yeye afuate baadaye, lakini kuanza kusema yeye moja kwa moja wakati alikuwa ananufaika na anachopinga Rais, anaonekana anamwonea wivu na mgongano wa masilahi.

“Sasa anapoanza yeye kujibu inashangaza. Kwa sababu yeye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje, iliyokuwa inafanya matumizi makubwa halafu unakosoa unaonekana kabisa unaonyesha kuna mgongano wa masilahi,” alisema na kuongeza:

Jacob alisema kwa mpinzani kusema hivyo angeonekana anataka kumuwajibisha Rais ili hayo mambo yaangaliwe kwa kina zaidi.

Alitoa mfano wa waziri wa zamani, Dk Makongoro Mahanga na kusema alipoikosa Serikali hakushambuliwa kwa sababu alishahama kutoka CCM na sasa yupo upinzani.

“Alipozungumzia suala la matumizi ya ardhi, Serikali haikujibu ilikaa kimya kwa sababu aliyeongea ni mtu sahihi,” alisema na kuongeza.

" Kwanza alikuwa kwenye Baraza la Mawaziri na pili hivi sasa yupo kwenye upande wa kuishambulia na kuikosoa Serikali na kuiwajibisha.”

Wema Sepetu kujifungua mwezi August

$
0
0
Malkia wa filamu, Wema Sepetu anatarajia kujifungua mwezi August 2016, kwa mujibu wa mpenzi wake Idris Sultan.

Akizungumza katika kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM Jumanne hii, Idris alisema mpenzi wake huyo anatarajia kupata mtoto baada ya miezi 6 au 7 hali ambayo imetafsiriwa na wadau wa mambo kuwa huenda mwanadada huyo akawa na mimba ya miezi 3 au 2.

“Yes very soon natarajia kupata mtoto kama miezi 6 au 7 ijayo,” alisema Idris. Pia Idris alisema bado hajatambua jinsia ya mtoto anayetarajia kujifungua mpenzi wake.

“No hatujui mwenzangu anataka surprise. Mimi nataka kujua kabla kwahiyo bado hatujafikia muafaka, naogopa nisije nikawa nanunua vigauni akaja Wa kiume bure,” alisema.

Aliongeza, “Huwezi kuwazuia watu kuongea, waache waongee maana sometimes watu ni wagumu kupokea changes lakini siku zinavyoenda naamini wataelewa tu.”

Pia Idris alisema wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni

Mtanzania Akamatwa na Madawa ya Kulevya Uwanja wa Ndege South Africa

$
0
0

Mwanaume mmoja aliyekuwa anasafiri kutokea Tanzania amekamatwa na madawa ya kulevya katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo nchini Afrika Kusini.

Inadaiwa madawa hayo ya kulevya aliyokamatwa nayo, yana thamani ya Randi milioni 12

Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images