Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Ujauzito wa Wema Sepetu Waanza Kuonekana..Team Wema Sepetu Wafurahia

0
0

Ujauzito wa Staa na Mrembo wa Bongo Asiyeishiwa na Skendo hatimae waanza kuonekana wazi wazi kitu ambacho kimewafurahisha Team Wema Sepetu baada ya boss huyo wao kushutumiwa kuwa ni mgumba kwa muda mrefu...
Hapa ninekuwekea picha ujionee:


Serekali Yatangaza Kusitisha Matangazo ya Bunge Laivu Kuanzia Jana..Sababu Hizi Hapa

0
0

Serikali yatangaza leo Bungeni kuwa kuanzia tarehe 26 Januari 2016 TBC imesitisha kuonyesha baadhi ya matangazo ya moja kwa moja ya shughuli za Bunge, kutokana na bajeti finyu.

Baada ya tamko hilo wabunge wa upinzani walipinga na kusimama na kupelekea bunge kuhairishwa

Soma, Zaidi

Mheshimiwa spika,
Naomba kutoa kauli ya serikali kuhusu TBC kutangaza moja kwa moja vikao vya majadiliano ya bunge. Mheshimiwa spika, shirika la utangazaji Tanzania, TBC lilianza kurusha moja kwa moja matangazo ya vikao vya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 2005. Kabla ya kuanza kurusha moja kwa moja, TBC wakati huo televisheni ya taifa ilikuwa inarekodi matukio yote ya bunge na kurusha usiku katika vipindi maalumu vilivyojulikana kama bungeni leo kwa maana ya yaliyojiri ndani ya bunge kwa siku husika.

Baada ya kuanza kwa utaratibu wa kuanza kurusha matangazo moja kwa moja mwaka 2005, gharama za kufanya kazi hio zimekua zikipanda kwa kasi hadi kufikia Tshs. bilioni 4.2 kwa mwaka kwa maana ya mikutano minne ya bunge.

Shirika limekuwa likigharamia kwa sehemu kubwa matangazo hayo kwa kutumia mapato yake yanayotokana na matangazo madogo madogo ya biashara, ifahamike kuwa asilimia 75 ni vipindi vingi vinavyolenga kutoa elimu kwa umma na asilimia 25 ni burudani.

Mheshimiwa spika, kutokana na hali hii, TBC imeona ni busara kubadilisha mfumo wa utangazaji wa shughuli za bunge ili kukabiliana na kupanda kwa gharama za uendeshaji, hivyo basi, TBC imeona ni busara kuanzia mkutano huu wa bunge iwe inarusha baadhi ya matangazo ya bunge moja kwa moja yaani live ikiwa ni njia ya kubana matumizi.

Chini ya utaratibu huu, TBC itahakikisha kuwa, baadhi ya matukio ya matukio ya bunge yatarushwa moja kwa moja na mengine kurekodiwa na kuandaliwa kipindi maalum kitakachoitwa leo katika bunge. Kipindi hiki kitakua na mambo yote muhimu yaliyojiri ndani ya bunge kwa siku husika. Kipindi hichi kitakuwa kinarushwa kuanzia saa nne usiku hadi saa tano usiku.

Na mheshimiwa spika kipindi hicho kimeanza jana na tayari baadhi ya wananchi wameonyesha kuridhishwa na utaratibu huu na kuwa na kipindi maalum usiku kikishughulikia shughuli za bunge, mheshimiwa spika, uamuzi huu utapunguza gharama za uendeshaji

Hotel ya Mtoto wa Amani Karume yateketea kwa moto, Vijana wawili wahusishwa

0
0

Moto mkubwa umeteketeza hoteli ya kitalii ya Konokono Beach Resort iliyoko Michamvi mkoa wa kusini Unguja, inayomilikiwa na mtoto wa rais wa zamani wa Zanzibar, Amina Karume pamoja na wawekezaji wawili kutoka nje ya nchi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kusini Unguja, Juma Saadi amesema kuwa moto huo uliteketeza nyumba tatu na mgahawa mmoja katika hoteli hiyo, ni watu wawili waliokuwa wakichoma nyasi karibu na hotel hiyo. Aliwataja vijana hao kuwa ni Meshak Amos Elisha na Mohamed Abdallah Hassan.

Kamanda Saadi aliwataka wananchi kupuuza habari zilizoenea zinazohusisha tukio hilo na mambo ya kisiasa, husasan vyombo vya habari vya kimataifa vilivyoripoti habari hiyo.

“Wakati wa kuchoma moto ndani ya uzio huo, ulizuka upepo mkali majira ya saa tano na nusu na kusababisha nyumba moja ya makuti katika hoteli ile kushika moto na kusababisha hasara hiyo,”kamanda Saadi alifafanua.

Kikosi cha zima moto na uokoaji kilifika katika eneo hilo na kufanya kazi za kuzima moto huo.

Vurugu zaibuka, Wabunge wa Upinzani Watimuliwa Bungeni..Wapinga TBC Kukatazwa Kuonyesha Bunge live

0
0
Hali ya Sintofahamu imetawala Bungeni jioni hii kufuatia wabunge wa Upinzani kupinga TBC kusitisha kurusha live matangazo ya moja kwa moja kuanzia jana kwa kigezo cha kubana matumizi.

Kutokana na vurugu hizo, Polisi wamelazimika kuingia Bungeni na kuwatoa nje wabunge wa Upinzani kufuatia kugoma kutokana na maagizo ya Mwenyekiti wa Kikao cha Bunge, Andrew Chenge.

Chanzo cha vurugu hizo  ni  Wabunge wa Upinzani kupinga kuendelea kwa mjadala wa Bunge wakitaka kauli ya Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuhusu TBC kusitisha kurusha matangazo ya moja kwa moja toka Bungeni  ijadiliwe kwanza.

Sakata hilo liliibuka tangu asubuhi ambapo Mwenyeki wa Bunge, Andrew Chenge aliahirisha Kikao cha Bunge mara mbili huku akiitaka kamati ya uongozi kukutana  ili kutoa majibu.
Maamuzi ya kamati ya uongozi  
Baada ya Bunge kurejea jioni hii mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge ameliambia Bunge kuwa maamuzi ya kamati ya uongozi baada ya kuketi mchana wa leo ni kama ifuatavyo.

(a) Mwenyekiti wa Bunge alikuwa sahihi kutaka hoja iliyokuwa mbele ya Bunge kuhusu hotuba ya Rais iendelee.

(b) Hakuna haki yoyote ya Bunge iliyovunjwa kwa Bunge kuendelea na kazi yake baada ya hoja ya Waziri

(c) Hoja ya Bunge iliyo mbele ya Bunge ni hotuba ya Rais na kamati ya uongozi imeagiza shughuli ziendelee kama kawaida.

(d) Endapo kuna Mbunge yoyote ambaye hataridhika atumie kanuni ya 5 (4) kuomba kibali kwa katibu wa bunge ili apate nafasi maalumu.

Aidha kwa mujibu wa ratiba ya kikao cha Bunge ni kwamba Bunge litajadili hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11 Novemba 20, 2015 kwa muda wa siku 3. Baada ya kauli hii, vurugu ziliibuka Bungeni
Wabunge  wa  Upinzani walianza kupiga mayowe, ikiwemo kuimba nyimbo mbalimbali suala lililomlazimu Mwenyekiti kuwaondoa Wabunge wa Ukawa wote watoke nje ili wabunge wengine waendelee na kikao cha kujadili hotuba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Wabunge wa CCM wako Bungeni wanaendelea na kikao cha Bunge 

Serikali Yasema Mawaziri Wakuu Waliokihama Chama cha Mapinduzi (LOWASSA na SUMAYE ) Wataendelea Kulipwa Pensheni Zao Kama Kawaida

0
0
Serikali imesema leo kuwa mawaziri wakuu waliokihama Chama cha Mapinduzi (CCM) wataendelea kulipwa pensheni zao kwa mujibu wa sheria ya nchi.

Mawaziri wakuu hao; Fredrick Sumaye na Edward Lowassa walihama CCM na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema)na badaye Lowassa aligombea urais chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Akijibu maswali ya baadhi ya wabunge waliohoji endapo watu waliokuwa katika nyadhifa hizo wanaweza kuzuiwa kuchukua pensheni zao kwa kuhamia upinzani, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Utumishi wa Umma, Angellah Kairuki amesema sheria haizuii kwa kuwa kuhama chama ni haki ya kikatiba.

Akinukuu Sheria ya mwaka 1999 pamoja na ile ya mwaka 2005 ya Utumishi wa Umma, Kairuki amesema waliokuwa viongozi katika nyadhifa hizo wana haki ya kuendelea kupata stahiki hizo kisheria.

Hata hivyo ameonya kuwa, wanapaswa kuheshimu sheria ya nchi inayowazuia kutoa siri za nchi wakati wakiwa katika nyadhifa zao.

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji, amesema uchumi ukiimarika utaisaidia serikali kuwalipa wastaafu pensheni itakayokidhi mahitaji yao.

Picha Hii ya ‘Mahaba Niue’ ya Jokate na Alikiba Yawa Gumzo Mtandaoni

0
0
Penzi la Jokate Mwegelo na Alikiba linazidi kupamba moto.

Wawili hao wanaonekana kuanza kukubaliana na ukweli kuwa hawawezi tena kuyaficha mahaba yao kiasi cha kuanza kufanya photoshoot za pamoja za mradi ambao bado haujajulikana ni wa nini.

Weekend iliyopita, picha yao inayowaonesha wakiwa wamezama kwenye dimbwi la mahaba, ilisambaa mtandaoni huku Jokate akiiweka pia kwenye Instagram.

Maoni ya Wananchi: Ni Sawa Kusitisha Matangazo ya Bunge LIVE TBC?

0
0
Je,Unadhani ni haki kwa serekali kukatiza matangazo ya moja kwa moja kwa shughuli za bunge?
Tutoe maoni yetu hapa serekali itayaona na kuyafanyia kazi.
Karibuni!

Hivi Ndivyo Zitto Kabwe Alivyosimamisha Bunge Baada ya Kutoa Hoja ya Kupinga Kutokuonyesha Vipindi vya Bunge

0
0
Zitto Kabwe
ZITTO KABWE ALISIMAMISHA BUNGE.Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe amelisimamisha Bunge kuanzia Saa tano asubuhi mpaka saa kumi jioni.Baada ya kutoa Hoja ya kumpinga uamuzi wa serikali wa TBC 1 kutokuonyesha vipandi vya Bunge.Hoja ambayo ilitolewa na Waziri Nape Nnauye;ndipo Zitto Kabwe akasimama na kuitaka Serikali iondoe hoja Hiyo Kwani TBC 1 ni shirika la Umma ambalo linaendeshwa kwa kodi za Wananchi.Zitto Kabwe ameungwa mkono na 70% ya Wabunge wote.Hivyo Serikali inatakiwa ije majibu.

Mengine yaibuka Kuhusu Ranger Rover ya Wema Sepetu Baada ya Kusemekana Imekamatwa

0
0
Baada ya Martin Kadinda kusema gari ya Wema yuko nayo kihalali, hakuna deni lolote la kodi alikwepa kwenye kulipia gari hilo aina ya Range Rover aliyojipa zawadi.

Soudy Brown kayanasa mengine, amesema kulikuwa na stori kwamba kuna watu walikamata garni hiyo ikiwa haina baadhi ya nyaraka zake, mambo yakaenda baadae jamaa wakalikamata gari hilo na kuondoka nalo.. Soudy akamcheki Martin Kadinda, jibu lake ni kwamba na yeye aliisikia story ya namna hiyo lakini hakuwa anajua kinachoendelea.

Martin amesema alimtafuta Wema, akaenda nyumbani kwake na kukuta gari hilo lipo, alipomuuliza Wema kuhusu stori ya gari kukamatwa amesema Wema alimwambia hakuna sababu ya kuuliza gari wakati analiona lipo kwake halijakamatwa.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Januari 28, Ikiwemo ya Vurugu Kubwa Bungeni

Azikwa Kaburini na Kreti za Bia na Soda Kahama

0
0
Wakati serikali ikipigia kelele kukemea imani za kishirikina, wilayani Kahama bado ni kitendawili baada ya mkazi mmoja wa Kijiji cha Mwamande, Kata ya Mwanase katika Halmashauri ya Msalala kufariki na baadaye wanakijiji kumzika na mali zake zote yakiwemo makreti ya bia na soda aliyokuwa akiyatumia kwenye biashara yake ya baa.

Tukio hilo limetokea  jana katika kijiji hicho baada ya mwanakijiji huyo, Mahushi Lutaja kufariki na baadaye familia yake kupitisha maadhimio ya kumzika na mali zake zote kwa imani ya kwamba kifo chake kimetokana na kurogwa na wao kuhofia kwamba wakibaki na mali zake nao watakumbwa na mauti.

Kwa mujibu wa diwani wa Kata ya Mwanase, Samson Masanja, Lutaja baada ya kifo chake alizikwa na baisikeli moja vitanda vinne na magodolo yake pamoja na masanduku ya nguo zake zote na vitu vingine vidogovidogo alivyokuwa akivitumia

Pia Masanja alisema, Lutaja alizikwa na makreti ya bia na soda ambayo kabla ya kifo chake alikuwa akiyatumia kwenye biashara yake ya kuuza vinywaji kwenye kijiji hicho cha Mwamande ambapo  tukio hilo limehusishwa na imani za kishirikina

Wakati akiugua ndugu zake waliamini kwamba ugonjwa huo uliopelekea kifo chake ulitokana na kurogwa hivyo familia yake iliingiwa na hofu hiyo hasa kutokana na kuwepo madai ya waganga wa jadi kuamini kwamba ndugu yao alirogwa

Kampuni ya Magazeti ya Mwananchi Yatoa Kauli Kuhusu Kujihusisha na Biashara ya Kusafirisha Wahamiaji Haramu

0
0
Wahamiaji Haramu Wakiwa chini ya Ulinzi
Idadi ya Raia wa kigeni kutoka nchini Ephiopia waliokuwa wakisafirishwa na Gari la magazeti la kampuni ya Mwananchi Communication Ltd imefikia 12 baada ya wengine 4 kukamatwa Jioni wakiwa Eneo la Kibwabwa  mjini Iringa wakiwa wamefichwa porini.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Iringa Peter Kakamba amesema kuwa tayari ametuma usafiri kwenda kuwabeba Raia hao ambao wanadai walishushwa katika gari hilo aina ya Hiace ili kuvuka eneo la ukaguzi wa Magari ( check pointi)  kijiji cha Igumbilo nje kidogo ya mji wa Iringa.

Wakati huo huo Kampuni ya Mwananchi Communication Limited (MCL)  imetoa ufafanuzi kuhusiana na kuhusishwa na kadhia hiyo. Soma zaidi:

Kanumba Feki Adaiwa Kuwa Mhamiaji Haramu...Mwenyewe Ajitetea na Kusema Haya

0
0
Rammy Gallis
Mkali wa filamu Bongo, Rammy Gallis ‘Kanumba Feki’ anadaiwa kuishi nchini bila vibali maalum, jambo linalomuweka hatarini muda wowote kuweza kutimuliwa Bongo kutokana na tumbuatumbua ya Serikali ya Rais John Pombe Magufuli inayoendelea.

Kwa mujibu wa chanzo, kuna hatihati kubwa ya msanii huyo ambaye wengi wamezoea kumuita Msomalia kufungashiwa virago kwani hana uhalali wa kuendelea kuwepo nchini.

“Yaani kwa hii kasi ya Mh. Magufuli sidhani kama Rammy atasalimika, si unaona jinsi ambavyo mzee wa kutumbua majipu yupo makini kwenye uongozi wake, yule kaka ni mkimbizi yaani akae tayari kwa safari ya kurudi kwao huko,” kilisema chanzo.

Baada ya kupata madai hayo, Showbiz Xtra ilimpo-vutia waya msanii huyo ili kusikia kauli yake kufuatia madai hayo alijibu;

“Mimi ni Mtanzania halali nina vigezo vya kuwepo Bongo, mama yangu ni Msomali baba ni Muarabu kachanganya na Mbrazil.” 

Wema Sepetu Naye Afunguka Mazito Kuhusu Penzi Lake Kwa Idris Sultan..

0
0
Baada ya Idriss Kufunguka na kuweka wazi uhusiano wake na Wema Sepetu Siku kadhaa zilizopita ,usiku huu wa tarehe 27 siku moja kabla ya Birthday ya Sultan Wema Amefunguka Haya;

"Nimeandika na kufuta karibia mara mia maana kila ninachotaka kuandika najikuta naona hakifai and maybe hakitoshi.... Im busy looking for the Proper words to tell you how I truly feel but naona kama sio.... I thought deep and I jus simply decided to write this: "Idris I love you, not only because you are my man or because you love me too.... No...!!! I love you because you make me a Better person, You changed my whole life.... You Complete me.....!!! I love you because you make me feel good about myself, you make my heart skip a beat everytime I see ur name appear on my phone as u call me, you fill my tummy with butterflies everytime I see u... I love you because you can make me cry but at the same time make me laugh hysterically... I love you because you have been nothing but Da Man Ive always wanted... From your character, your personality, your IQ and your way of thinking to The way u touch me, feel me, hold me, Kiss me.... The way u look at me, The look on your face wen u know Iam not okay or maybe im nat happy.... These are some of the few things that make me Love You more everyday...." On ur birthday I want to tell you that Im the Luckiest girl to hav you as My Man and Im gon keep you for a veeeery veeeery long time( I couldve said forever but we all know forever doesnt exis...Well im nat so sure) I cant ask for more... You are Just Wonderful... Lord I thank you for this Being... Iam Forever Grateful....!!! Lord I ask you to protect my love... Keep him for as long as you can because he is dat person I do not want to lose anytime soon... I just wish nothing but Happiness for you and I babe...Happy Birthday Booboo... Happy Birthday to you Hubby....!!!You are the only person That has really made me feel like a woman.... Oh...! I just love you with all my heart... Now before The Clock strikes 12, Let me be The 1st to wish you a Happy Birthday My Love....!!!" Wema Sepetu

CUF: Tunaandaa Tamko zito, Tutaishangaza Dunia.

0
0
Baraza Kuu la Chama Cha Wananchi (CUF), leo linatarajia kutangaza uamuzi mzito kutokana na kikao cha Kamati ya Utendaji, kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam chini ya Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad.

Kikao hicho cha Kamati ya Utendaji kilifanyika kwa saa tatu kujadili suala la tarehe iliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ya kurudia uchaguzi wa Zanzibar, uliofutwa Oktoba 28, mwaka jana.

Kamati hiyo ambayo ilikuwa na ajenda moja pekee, ilijadili na  kutoa uamuzi mzito ambayo yatawasilishwa kwenye Baraza Kuu leo na kutolewa kwa umma.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji, ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini, aliiambia Nipashe kuwa, maazimio yaliyotolewa na kikao hicho kilichoanza saa nne asubuhi, yataishangaza dunia.

Alisema uchaguzi uliotangazwa na ZEC kuwa utafanyika  Machi 20, mwaka huu, ni batili kwa kuwa tayari mshindi wa uchaguzi huo anafahamika ni Maalim  Seif.

“Jukumu kubwa la kikao cha Kamati Tendaji kwa mujibu wa Katiba (ya CUF) ni kuandaa ajenda kwa ajili ya kikao cha Baraza Kuu litakaloanza kesho (leo) na baada ya hapo tutatangaza msimamo wetu juu ya uchaguzi huo,” kilieleza chanzo hicho.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa CUF, Silas Bwire, Kamati ya Utendaji ilikuwa na wajumbe 18 kutoka Tanzania Bara na  Zanzibar, ambao ni viongozi waandamizi wa chama.

Baraza kuu ambalo linatarajia kufanya kikao chake leo, litakalopokea ajenda zilizojadiliwa jana, lina wajumbe 60.

Kikao cha Baraza ambacho kitaongozwa na Mwenyekiti wake, Dk. Twaha Tasilima, kitajadili kwa kina ajenda zitakazowasilishwa pamoja na kuzitolea uamuzi.

HALI ILIVYOKUWA CUF
Nipashe jana lilifika katika ofisi hizo za makao makuu ya CUF, zilizoko Buguruni saa tano asubuhi na kukuta ulinzi ukiwa umeimarishwa wakati kikao kikiendelea.

Maofisa wa usalama wa chama hicho walionekana wakiwa nje ya geti la kuingilia katika ofisi za chama, karibu na mlango wa ukumbi wa mkutano na maeneo yote ya ofisi hizo.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, eneo ambako magari yanaegeshwa siku zote yalizuiwa kuegeshwa kwa madai ya kuimarisha ulinzi kutokana na uwepo wa Maalim Seif, ambaye alikuwa mgombea urais wa Zanzibar.

Wiki iliyopita, ZEC ilitangaza tarehe ya kurudiwa kwa uchaguzi uliofutwa Oktoba 28 mwaka jana kuwa utarudiwa Machi 20 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jecha Salum Jecha, alisema uchaguzi huo utawahusisha wagombea wa nafasi za urais, uwakilishi na udiwani na kwamba hakutakuwa na uteuzi mpya wa wagombea wala mikutano ya kampeni.

VIGOGO WAGAWANYIKA ZANZIBAR
Wakati hatima ya CUF kushiriki au kutoshiriki uchaguzi wa marudio inatarajia kufahamika leo, mgawanyiko mkubwa umeibuka miongoni mwa wajumbe wake wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa.

Katika mgawanyiko huo, wamo wanaopinga kushiriki huku wengine wakitaka chama kuangalia upya msimamo wa kususia uchaguzi huo.

Wakizungumza Nipashe kwa mashariti ya kutotajwa majina, baadhi ya wajumbe hao kutoka Pemba  walisema msimamo wa kususia uchaguzi una manufaa na hasara kubwa kwa chama na unaweza kuleta mgawanyiko kwa viongozi na wagombea katika majimbo ya uchaguzi.

Mjumbe mmoja alisema iwapo chama kitaamua kushiriki uchaguzi huo, kitakuwa kimejimaliza kisiasa pamoja na kutokuaminika tena na jumuiya ya kimataifa hasa nchiu na taasisi zilizotoa ripoti kuwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa mwaka jana ulikuwa huru na wa haki.

Aidha, alisema kitendo kilichofanywa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha,  cha kufuta matokeo baada ya kuona CCM wako katika mwelekeo mgumu wa kuanguka katika uchaguzi, utakuwa mchezo wa kudumu wakati hauna manufaa katika kuimarisha demokrasia Zanzibar.

Alisema hata wananchi wenyewe msimamo wao wanataka kuona ZEC inakamilisha uchaguzi huo uliofutwa kwa  kumtangaza mshindi wa urais katika uchaguzi huo pamoja na matokeo ya wawakilishi na  madiwani

Alisema kuwa haiwezekani uchaguzi kurudiwa na kusimamiwa na tume ambayo imepoteza imani kwa wananchi wake na kwamba uchaguzi huo umelenga kuhakikisha CCM inashinda, ndiyo maana wapinzani wanazuiwa kufanya harakati za kisiasa tangu kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi huo.

Hata hivyo, mjumbe mmoja akiwa na wezake watatu katika mazungumzo na mwandishi wa habari hii, alisema hatua ya kususia uchaguzi italeta madhara makubwa kwa maendeleo ya demokrasia na utakuwa mwanzo wa kufa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Alisema Wawakilishi wengi wametumia gharama kubwa katika majimbo yao na hatua ya kususia uchaguzi inaweza kuleta mgawanyiko mkubwa pamoja na chama kuwa katika wakati mgumu wa kujiendesha kutokana na kutegemea ruzuku na michago ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge.

Kwa mujibu wa mjumbe huyo, wagombea wengi wa uwakilishi hawakubaliani na msimamo wa kususia uchaguzi lakini wanashindwa kujitokeza na kuzungumza hadharani.

Alisema chama kilitakiwa kungalia umuhimu wa kuwa na tume huru ya kusimamia uchaguzi pamoja na jumuiya ya kimataifa kupewa nafasi ya kusimamia kwa karibu uchaguzi wa marudio badala ya kususia.

Mjumbe huyo alisema pamoja na kasoro mbalimbali zilizojitokeza katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa bado imesaidia katika kuimarisha amani na kuondoa chuki na uhasama wa kisiasa na kwamba hatua ya CUF kujiondoa katika serikali kunaweza kuleta matatizo makubwa kutokana na kuwa na uwakilishi wananchi wengi sawa na CCM.

JUSSA ANENA
Akizungumzia mgawanyiko huo, Mkurugenzi wa Mawasiliano  wa  CUF, Ismail Jussa Ladhu, alisema kutokana na ukubwa na uzito wa mgogoro wa uchaguzi, mgawanyiko ni jambo ambalo halikwepeki kwa chama kikubwa kama hicho.

Alisema uongozi wa chama uko makini katika kujadili ajenda ya mgogoro wa uchaguzi na kuwataka viongozi na wanachama pamoja na wananchi kwa ujumla kuwa na moyo wa subira wakati Baraza Kuu la Uongozi la Chama linajiandaa kutoa kauli ya mwisho juu ya hatima ya uchaguzi huo.

Jussa alisema uamuzi utakaotolewa na Baraza Kuu ndio utakuwa mwongozo kwa wagombea wote wa chama pamoja na wanachama na watu wanaokiunga mkono chama.

Alisema mchezo aliyoufanya Jecha wa kufuta matokeo ya uchaguzi kwa manufaa ya CCM, haukubaliki katika misingi ya demokrasia na utawala bora.

Mahakama Kuendelea na Kesi ya Gwajima ya Kutoa Lugha ya Matusi

0
0
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima
Mahama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imesema itaendelea kusikiliza ushahidi wa Jamhuri katika kesi inayomkabili  Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.

Gwajima anakabiliwa na tuhuma za kutoa lugha ya matusi dhidi ya  Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, kwamba ni mtoto, hana akili na mpuuzi. Anadaiwa kutoa maneno hayo.

Kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa ushahidi huo jana lakini iliahirishwa baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro, anayeendesha kesi hiyo kuwa mgonjwa.

Kimaro alitoa madai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi, Cyprian Mkeha, anayesikiliza kesi hiyo.

Wakili wa utetezi Peter Kibatala, alidai kuwa hana pingamizi na maombi ya Jamhuri.

Hakimu Mkeha alisema kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Februari 24, mwaka huu na dhamana ya mshtakiwa inaendelea.

Katika kesi ya msingi, Askofu Gwajima anadaiwa kuwa kati ya Machi 16 na 25, mwaka jana, katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam, alitoa lugha ya matusi kwamba “mimi Askofu Gwajima nasema Askofu Pengo ni mpuuzi mmoja yule, mjinga mmoja, amekula nini yule, sijui amekula nini yule mtoto hana akili yule”.

Alidai kuwa Askofu Gwajima alitoa maneno hayo ya kufadhaisha dhidi ya Kardinali Pengo na kwamba yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
CHANZO: NIPASHE

Wale Watuhumiwa Saba wa Ufisadi wa Makontena Waliotoroka Sasa Mikononi Mwa Polisi

0
0
Makontena Bandarini Dar es Salaam
Wafanyakazi saba kati ya wanane wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) waliotuhumiwa kuhusika kutorosha makontena 11,019 na magari 2,019 kutoka bandarini ambao walitoroka, wamepatikana na tayari wanaendelea kuhojiwa na polisi juu ya tuhuma hizo.

Watumishi hao ni kati ya watuhumiwa 15 wa TPA waliotangazwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kuwa wameshiriki kuondosha makontena na magari hayo kutoka katika bandari kavu saba bila kulipa ushuru wa Bandari.

Meneja Mawasiliano wa TPA, Janet Ruzangi alisema jana kuwa mfanyakazi mmoja kati ya hao wanane, hajapatikana; na anaendelea kusakwa na polisi ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
“Wote walishapatikana kasoro mtumishi mmoja, Happygod Naftali, ambaye huyu alishaacha kazi siku nyingi baada ya viongozi kuanza kufuatilia suala hilo; lakini bado polisi wanaendelea kumsaka,” alisema Ruzangi.

Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alithibitisha watuhumiwa hao, kukamatwa na kwamba bado wanaendelea kuhojiwa kuhusu tuhuma hizo.

“Ni kwamba tunaendelea na upelelezi wetu,” alisema Sirro licha ya kuwa hakutaka kutaja idadi ya wafanyakazi wa TPA ambao wamepatikana.“Kwa kweli idadi nitaitoa siku nitakapozungumza na waandishi wa habari wiki hii,” alifafanua.
Watumishi waliokuwa wanasakwa na polisi waliopatikana kwa mujibu wa Ruzangi ni Aron Lusingu, Amani Kazumari, John Mushi, Valentine Sangawe, Bonasweet Kimaina, Zainab Bwijo na Nathan Edward.

Watumishi hao wanaungana na watumishi wengine saba John Elisante, Leticia Masaro, Christina Temu, Merina Chawala, Adnan Ally, Masoud Seleman na Benadeta Sangawe waliokamatwa na kuhojiwa kuhusu sakata hilo. Watumishi hao saba, kwa mujibu wa Sirro, tayari walishapelekwa mahakamani.

“Ukiacha wale saba ambao tumeshawafikisha mahakamani, hawa wengine bado tuko nao tunaendelea kufanya upelelezi,” alieleza.

Wafanyakazi hao wanatuhumiwa kuhusika kutorosha makontena 11,884 na magari 2,019 ambayo yalitoroshwa kutoka katika Bandari Kavu (ICD) saba bila kulipiwa ushuru wa bandari na hivyo kuipotezea Serikali mapato ya Sh bilioni 48.55.

Kuhusu mawakala 280 waliopewa siku saba wawe wamewasilisha maelezo yao makao makuu ya TPA namna ya walivyohusika kulipia makontena hayo, Ruzangi alisema mamlaka yake inajipanga kutoa taarifa kamili juu ya suala hilo.

“Tunaendelea kuandaa taarifa ya kilichotokea na kilichobainika kuhusu mawakala hao, tutatoa taarifa hivi karibuni,” alisema Meneja Mawasiliano huyo.

Tangu Rais John Magufuli aingie madarakani, uongozi wake umeibua ufisadi wa kutisha ambao ulikuwa unafanywa Bandari ya Dar es Salaama kwa kuwashirikisha wafanyakazi wa TPA na mawakala pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA).

Kwa mara ya kwanza upotevu wa makontena 349 uligundulika baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutinga bandarini na kubaini makontena hayo kutolewa bandari kavu bila kulipiwa kodi.
Upotevu huo ulifanya vigogo wa TRA, akiwemo Kamishna Mkuu Rished Bade na makamishna wengine kusimamishwa kazi na kufikishwa mahakamani.

Baadaye Majaliwa alibaini upotevu wa makontena 2,431 yaliyoondolewa bandari kavu bila kulipiwa ushuru wa Bandari.
Katika sakata hilo, baadhi ya mawakala wa forodha walifungiwa kufanya biashara na TPA Sakata la mwisho ni la kupotea kwa makontena 11,019 na magari 2,019, ambayo yaliondolewa kwenye ICD saba bila kulipiwa ushuru wa bandari na kuipotezea serikali mapato ya Sh bilioni

Kilichotokea Jana Bungeni Kinatuweka Njia Panda ya Hatari Sana Wananchi....

0
0
Fujo Bungeni Jana
Kama tunaweza kuruhusu askari aingie ndani ya Bunge,amkung'ute Mbunge vibao na kumbeba mzobemzobe kumtoa nje ya ukumbi mahali ambapo alikuwa hafanyi fujo ya kuhatarisha usalama wake binafsi au wa wengine bali kutetea anachokiamini na ambacho bila shaka anaamini waliomtuma Bungeni wanakiamini pia (Fujo za malumbano ya maneno ni kawaida ya Mbunge), basi tupo njia panda ya hatari sana

Jeff Msangi

Ali Kiba: Cindelela ilipo’Hit’ Ndoto za Kuwa Mchezaji Mpira Maarufu zilikufa

0
0
Ali Kiba Uwanjani
Ali kiba tangu akiwa mdogo alikuwa na ndoto za kuwa mchezaji mpira maarufu Bongo na mpira alikuwa anauweza hasa mpaka kutaka kusajiliwa na timu moja kubwa..
Kiba amefunguka kwanini aliacha mpira;

‘’Sababu ilikuwa wimbo wangu wa Cindelela ulikuwa umehit ikabidi niachane na mpira nikaanza kupiga hela Tanzania nzima nikazunguuka,lakini kwenye mpira nilikuwa katika form,nikashindwa kuendelea nilikosa muda kabisa wa kucheza mpira,’’Kiba.

Kutorushwa Kwa Bunge Live kupo Pale Pale- Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

0
0
Waziri Mkuu Majaliwa
Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la papo kwa papo la Mbunge wa Hai ambaye pia ni msemaji wa kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe aliyetaka kujua kwanini serikali imefanya maamuzi ya kuzuia wananchi wasione matangazo ya Bunge moja kwa moja.
Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amesema kwamba uamuzi wa kutoonyeshwa kwa matangazo ya moja kwa moja uliombwa na chombo cha umma chenyewe kwamba hakina uwezo kujiendesha na uamuzi wao huo umeungwa mkono na serikali.

''Maamuzi ya chombo hiki yameungwa mkono na serikali na waziri Nape Nnauye amefanya kipindi maalum kuhusiana na jambo hilo na wananchi wameelewa vizuri na wameiunga mkono serikali kwamba matangazo yatarekodiwa na yatarushwa kama kipindi maalum usiku'' Amesema Waziri Majaliwa.

Aidha chombo cha umma kitakuwa kinarusha matangazo ya moja kwa moja kwa muda wa maswali na majibu kwa serikali na baada ya hapo matangazo yatarekodiwa na kurushwa katika kipindi kiitwacho leo katika Bunge.
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live


Latest Images