Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Sakata la Bunge Kutokuonyeshwa Laivu Lawapatanisha Zitto Kabwe na Mbowe...Wapeana Mikono na Kukaa Pamoja

$
0
0

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (kulia) akipeana mkono na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kabla ya kuanza kwa mkutano na waandishi wa habari wakipinga kitendo cha kutolewa kwa nguvu katika Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana. 

March 10 2015, Zitto Kabwe alivuliwa uanachama wa CHADEMA  kwa tuhuma za kukihujumu na kikisaliti chama hicho.

Hata hivyo, baada ya muda mfupi, Zitto alijiunga na chama cha ACT-Wazalendo na kuteuliwa kuwa kiongozi mkuu wa chama hicho huku mwenyekiti wake akiwa Anna Mghwira


Breaking News: Kimenuka Tena Bungeni..Upinzani Watoka nje Baada ya Kunyimwa Muongozi na Naibu Spika Tulia

$
0
0

Hali ya sintofahamu imeendelea ndani ya bunge baada ya wabunge wote wa Upinzani kutoka ndani ya bunge mara baada ya Wabunge kuanza kuchangia hotuba ya Rais.

Baada ya  kipindi cha Maswali na Majibu, yalifuata matangazo  na   baada ya Matangazo, wabunge wakaanza kuchangia hotuba ya Rais Magufuli .

Wakati hayo yakiendelea, wabunge kadhaa wa UKAWA akiwemo mbunge wa Ubungo(chadema), Saed Kubeneawalikuwa wakiomba muongo wa Naibu Spika ili waongee lakini hawakupewa nafasi.

Naibu Spika alikataa miongozo hiyo na kulitaka Bunge lijikite katika kujadili Hotuba ya Rais. Hali hiyo iliwakera wabunge wa upinzani  kwa madai kuwa wamezibwa midomo na hivyo wakaamua kutoka nje ya ukumbi wa bunge

Blog ya Kenya Yasambaza Uongo Kuhusu Rais Maguguli Kwenda Kenya Kwa Mara ya Kwanza

$
0
0

Kumekuwepo na habari za uongo na potofu katika mtandao wa jamii wa www.kenya-today.com kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atazuru Kenya kuhudhuria kumbukumbu ya marehemu Mhe.

Jaramongi Odinda na Fidel Odinga Jumamosi hii.
Inasikitisha kuona kwamba mwandishi wa Kenya anachukua nafasi ya Mwanhabari wa Rais wa Tanzania kwa kuwa na  ratiba ya Mhe. Rais wa Tanzania kuliko waTanzania wenyewe.

Haijulikani ni nini has nia ya mtandao huo, lakini ukweli ni kwamba ratiba hiyo ni batili na ya uongo uliotukuka. Hawa watani wetu wa jadi wana lao jambo!
Wapuuzeni. Taarifa hiyo si ya kweli.

Penzi la Aslay wa Yamoto Band na Mrembo Video Qeen Laingia Shubiri

$
0
0
Msanii wa kundi la Yamoto Band, Aslay Isihaka ametangaza kuwa yupo single.

Kabla ya hapo, Aslay aliwahi kuweka hadharani uhusiano wake na video model aitwaye Tessy Chocolate.

Hata hivyo siku za hivi karibuni muimbaji huyo aliacha kupost picha za mrembo huyo kwenye mtandao wa Instagram kiasi cha watu kuanza kuhisi kuwa mambo yameharibika.

Wiki hii aliiambia E-Newz ya East Africa Television kuwa kwa sasa hana mahusiano na binti yoyote.

Alisema kuhusiana na kinachoendelea katika upande wa mahusiano yake, hawezi kukizungumzia kwa sasa mpaka atakapoamua kuweka wazi nini kilitokea. Pia Aslay alishindwa kuzungumzia uvumi uliopo kuwa amemuacha msichana huyo baada ya kupata ujauzito.

Diamond Platnumz Kumsaini Rich Mavoko Kwenye Lebo yake WCB

$
0
0
Rich Mavoko
Staa wa Africa na Bongo flava, Diamond Platnumz ameendelea kuonyesha nia yake ya kuwasaidia wengine kukua kimuziki baada ya kufikia hatua kumsainisha Rich Mavoko kwenye lebo yake ya Wasafi.

“Rich Mavoko mara ya mwisho nilikuwa natakiwa nimsaini wasafi, Rich mavoko alitakiwa awe signed wasafi kabla ya nyimbo yake hii kutoka, ilitakiwa ikitaka awe chini ya wasafi, lakini kuna vitu vilichelewesha kwasababu kulikuwa na project namalizia kwanza,”

Diamond aliiambia Ayo Tv, “Nikamwambia, alikuwa anazungumza na uongozi wangu, kwahiyo wakamwambia kwasababu ishafika time unatakiwa utoe wimbo basi itoe tu hii nyimbo alafu then after hapo ikiwezekana kuanzia next project ndo anaweza akawa anatoa nyimbo akiwa chini ya wasafi.” Alielezea.

Hadi sasa waanii ambao wapo chini ya label hiyo ni pamoja na Harmonize na Raymond.

Kufutwa Kwa Matokeo Zanzibar: Makamba Amsafisha Jecha Bungeni

$
0
0
January Makamba
Waziri wa Mazingira na Muungano, January Makamba amesema kuwa Tangazo la Kufutwa kwa Uchaguzi wa Zanzibar lilitolewa na Tume ya Uchaguzi visiwani humo lilikuwa halali na kwa mujibu wa sheria.

Makamba amesema kwenye kikao cha tume cha tarehe 21 January cha kuamua kutangazwa kuamua kurudiwa kwa uchaguzi, akidi ilitimia na wengi walikubaliana na uamuzi ule. Kwa hiyo uamuzi ni halali kisheria na kikatiba na katiba ya Zanzibar inasema hakuna mwenye mamlaka hata mahakama ya kuhoji au kuchunguza maamuzi yanayotolewa na tume kuhusu uchaguzi.

Amesema hayo Bungeni wakati akitoa ufafanuzi Bungeni kuhusu Mkwamo wa Kisiasa unaoendelea Visiwani Zanzibar.

Mtazame Hapa;

Chadema Watoa Tamko Kuhusu TBC Kusitisha Matangazo ya Bunge Laivu..Kumshitaki Nape Kwa Wananchi

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrosia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu akitoa taarifa yake kwa wanahabari (hawapo pichani).

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kitapeleka hoja kwa wananchi juu ya hatua ya serikali ya kusikitisha matangazo ya Bunge moja kwa moja (live) kwenye Televisheni ya Taifa (TBC) kwa madai kuwa ni kulipunguzia gharama shirika hilo.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu amesema kufuatia  kauli ya Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliyotolewa jana bungeni, atapeleka hoja kwa wananchi ili kuona kitendo hicho kama kinakubalika ama la.

Alisema hayo leo katika Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na wanahabari, akisema kutorusha matanagzo hayo ‘live’ ni kumnyima mtanzania haki yake ya msingi kwa kuwa matangazo hayo yanalipiwa na  kodi za wananchi wenyewe.

Alisisitiza kuwa haiwezekani kurushwa baadhi ya vipengele, tena nyakati za usiku, muda ambao televisheni nyingi huonyesha vipindi vya burudani na wananchi wengi pia huwa wamechoka kutokana na kazi.

Aliitaka serikali kutaja kiasi cha fedha zinazotakiwa kurusha matangazo hayo ‘Live’ ili atakapopeleka hoja yake kwa wananchi, wakikubali kuchangia, wajue ni kiasi gani kitatakiwa ili hata kama TBC itakataa, wapeleke kwenye televisheni nyingine.

TFF Wakiri Kulikoroga Suala la Azam Kupewa Ruhusa Kwenda Zambia..Malinzi Aomba Radhi

$
0
0

Rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi ameviomba radhi vilabu vya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kutokana na timu ya Azam kupewa ruhusa na TFF kwenda nchini Zambia kushiriki mechi za kirafiki ambazo hazipo kwenye kalenda ya CAF, FIFA wala chama chochote cha soka kati ya Tanzania na Zambia.

Malinzi amekiri makosa yamefanyika ndani ya TFF kuiruhusu Azam lakini amejitetea kwamba wakati ruhusa hiyo inatolewa yeye hakuwepo nchini.

Malinzi pia amesema Yanga kutofanya uchaguzi mkuu wa viongozi wa klabu yao haimaanishi kwamba wako juu ya sheria na amewataka Yanga kuheshimu katiba yao pamoja na ile ya TFF.

“Naomba nivitake radhi vilabu vyote 15 vinavyoshirili ligi kuu Tanzania bara kwa kosa lililofanyika la kuwaruhusu Azam FC kwenda Zambia kucheza mechi za kirafiki, najua maamuzi yamefanyika mimi nikiwa Burundi, lakini kama kiongozi nakiri kosa kufanyika na naviomba radhi vilabu vyote”.

“Kuhusu Yanga kutofanya uchaguzi ukweli ni kwamba, Yanga hawapo juu ya sheria na wanapaswa kuheshimu katiba yao na ya TFF”.

Kuondoka kwa Azam kunasababisha mechi zinazoihusu timu hiyo kusogezwa mbele na kusababisha viporo vya mechi visivyokuwa vya lazima na kuvisababishi gharama na usumbufu vilabu ambavyo vingecheza na Azam mechi hizo.

Malinzi pia ametuma salu za rambirambi kwa familia, ndugu jamaa na marafiki wa  Epaphra Swa aliyefariki leo asubuhi kwenye hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Epaphra Swai alikuwa ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Simiyu.


Wema Sepetu: Idris Umenifanya Nijivunie Kuwa Mwanamke

$
0
0
Idriss na Wema Sepetu
Zikiwa zimepita siku kadhaa toka Idris Sultan kuweka wazi kumpa ujauzito bidada Wema Sepetu kupitia katika account yake ya Instagram Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa Idris amempa heshima na kumfanya ajivunie kuwa mwanamke.

Wema Sepetu leo kupitia ukurasa wake wa Instgram amefunguka mambo mengi na kuonyesha kufurahishwa na wala hajutii kuanzisha mahusiano na Idris Sultan, katika ujumbe wa Wema anasema wazi anampenda Idris si kwa sababu tu na yeye anampenda hapana bali ni kutokana na ukweli kwamba Idris ametengeneza historia nyingine katika maisha yake na kumfanya kuwa mtu bora na kubadili kabisa maisha yake.

Wema Sepetu alizidi kushusha shukrani kwa kijana huyo na kusema ikiwa leo ni siku yake ya kuzaliwa Idris Sultan anataka kumueleza kuwa yeye Wema Sepetu anajiona ni mtu mwenye bahati kumpata yeye kama mtu wake au mpenzi wake na kusema atamtunza na kumheshima kwa muda mrefu sana.

Zifuatazo ni baadhi ya nukuu kutoka kwa Wema Sepetu katika ujumbe wake huo ambao umekuwa ujumbe maalumu kwa mpenzi wake huyo katika siku yake ya kuzaliwa.

" Nimeandika na kufuta karibia mara mia maana kila ninachotaka kuandika najikuta naona hakifai and maybe hakitoshi.... Im busy looking for the Proper words to tell you how I truly feel but naona kama sio.... I thought deep and I jus simply decided to write this Idris I love you, not only because you are my man or because you love me too No...!!! I love you because you make me a Better person, You changed my whole life.... You Complete me" Alisema Wema

"You are the only person That has really made me feel like a woman.... Oh...! I just love you with all my heart... Now before The Clock strikes 12, Let me be The 1st to wish you a Happy Birthday My Love " Alimaliza Wema Sepetu

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa Ya Januari 29, Ikiwemo ya CUF kugomea Uchaguzi Kwa Hoja 12

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa Ya Januari 29, Ikiwemo ya CUF kugomea Uchaguzi Kwa Hoja 12

Jokate, Kiba Kumwagana, Kumbe Chanzo Mimba

$
0
0
Jokate na Ali Kiba
Wakati mastaa wenzake Bongo, Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja wakifurahia kunasa ujauzito, taarifa ambazo zimevuja zinadai kwamba, chanzo cha Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’ kumwagana na Mwanamuziki Ali Saleh Kiba ni kufuatia kuchoropoka kwa mimba ya mrembo huyo hivyo kumsononesha moyo wake, Ijumaa limenyetishiwa siri nzito.
Habari kutoka ‘redio mbao’ za mjini zilidai kwamba, wiki mbili zilizopita, Jokate na Kiba waliingia kwenye gogoro zito mara tu baada ya kuripotiwa kuchoropoka kwa ujauzito huo ikisemekana kuwa hali hiyo ilimpata kufuatia kufanya mazoezi makali ya kudensi akijiandaa na shoo.

“Unajua Kiba aliposikia mimba ya Jokate ambayo aliamini ni yake imechoropoka, alihisi anafanyiwa figisufigisu na kwamba huenda Jojo hakuwa amejiandaa kuitwa mama,” kilidai chanzo chetu kilichoomba hifadhi ya jina na kuongeza:

“Ndiyo chanzo cha ugomvi wa Jokate na Kiba licha ya zile sababu nyingine za tofauti ya dini, wazazi wa Jokate kutomtaka Kiba. Bado vikao vya kuwasuluhisha vinaendelea lakini jamaa (Kiba) anaonekana kutia ngumu.”

Hata hivyo, habari mpya zilizolifikia gazeti hili zilidai kuwa kumwagana kwa Jokate na Kiba kulipokelewa kwa kicheko na ndugu wa mrembo huyo ambao tangu awali walionekana kutounga mkono penzi la wawili hao.

Gazeti hili lilipomtafuta Kiba ili kufafanua ishu hiyo, kama kawaida simu yake iliita bila kupokelewa lakini kwa upande wake Jokate alikuwa na haya ya kusema: “Jamani naombeni mniache, sitaki kabisa kuongelea hayo mambo ya Ali Kiba.”

Hata hivyo, mwanahabari wetu alipotaka kusikia japo neno lake juu ya kuachana na Kiba na kwamba chanzo ni kuchoropoka kwa ujauzito huo, alisisitza kwamba aachwe.

Source;Global

Wema Sepetu, Najma Washea Penzi la Idris

$
0
0
Ubuyu mpya kabisa uliotua kwenye meza ya dawati hili unadai kuwa, Mshindi wa Shindano la Big Brother 2014 ambaye anatajwa kuwa ndiye ubavu wa Wema Sepetu kwa sasa, Idris Sultan, anatoka pia na msanii anayefahamika kwa jina la Najma Dattan ‘Naj’.
Najma ni msanii wa muziki aliyewahi kuwa na uhusiano na Mr Blue kabla ya kuhamia kwa Diamond miaka kadhaa iliyopita.

Kisikie chanzo
Chanzo chetu kilicho karibu na Najma kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, Idris na Najma wamekuwa wakitoka kwa muda mrefu na kwa ndugu wa binti huyo wala siyo siri.

“Unajua watu hawajui kuwa Idris yuko na Najma na mara kwa mara amekuwa akienda nyumbani kwao na hata ndugu wa Najma wanamjua.

“Kilichoibua taharuki ni juzikati Idris kudai ile mimba ya Wema ni yake, unaambiwa Najma anashangazwa na taarifa hizo,” kilidai chanzo hicho.

Wanaswa pamoja
Wakati madai hayo yakitua kwenye meza ya gazeti hili, mmoja wa mapaparazi wa Ijumaa hivi karibuni aliripoti tukio la Idris na Najma kunaswa pamoja kwenye hafla ya Clouds TV iliyofanyika pale Escape One, Mikocheni jijini Dar ambapo alisema:
“Mimi niliwaona pale Escape One, Idris alifika na kumchukua Najma na kumuingiza kwenye gari lake na kuondoka, alishuhudia Martin Kadinda, Steve Nyerere na mastaa wengine,” alisema paparazi huyo na kudai alikuwa akifuatilia ili kujua uhusiano wao.
Najma asakwa
Baada ya madai hayo kutua kwenye dawati la Ijumaa, jitihada za kumtafuta Najma kwa njia ya simu zilifanyika na alipopatikana alikiri kujuana vilivyo na Idris ila akagoma kuzungumzia uhusiano wao.
Ijumaa: Najma habari yako, unafahamiana na Idris? Je, ni mpenzi wako kwani kuna madai kuwa wewe unatoka na yeye kimapenzi na kwamba jamaa kakuzimia ile mbaya licha ya yeye kudai kampa mimba Wema, unalizungumziaje hilo?

Najma: Mh! Yaani nyie mmekosa la kuandika na udaku wenu, naomba nisiongelee lolote juu ya hilo.
Ijumaa: Tunachotaka kujua ni kama wewe na Idris ni wapenzi kweli, hilo tu.Najma: Niacheni jamani.
(Akakata simu)
Alipopigiwa tena hakupokea. Kwa upande wa Idris simu yake iliita weee, haikupokelewa, alipotumiwa sms pia hakujibu.
Ijumaa linaendelea kuwawekea mitego kwani kuna msemo wa Kiswahili usemao, mapenzi ni kikohozi, hawawezi kuficha uhusiano wao milele.

Source;Global Publishers

Askari Auawa Akituhumiwa Kufanya Ujambazi

$
0
0
Askari polisi wilayani hapa, Nobart Chacha (25) ameuawa kwa kupigwa risasi akituhumiwa kupora mali za mfanyabiashara wa madini kwa kutumia silaha za jadi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema jana kuwa askari huyo aliuawa kwa kupigwa risasi kifuani na mgongoni.

Diwani wa Kata ya Machimboni, Raphael Kalinga alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika Kijiji cha Ibindi kilichopo Kata ya Machimboni wilayani Mlele.

Alisema askari huyo akiwa na wenzake walifika kijijini hapo kwa lengo la kumpora mfanyabiashara huyo wa madini ambaye pia anamiliki mashine za kusaga nafaka.

Kalinga alisema askari huyo na watuhumiwa wengine walivunja mlango wa mbele wa nyumba ya mfanyabiashara huyo wakati amelala chumbani.

“Baadaye waliingia ndani walimwamuru mfanyabiashara huyo kukaa kimya, lakini hakutii agizo na badala yake alichukua bunduki yake aina ya Shortgun na kumpiga askari huyo kifuani na mgongoni,” alisema.

Alisema baada ya kuona askari huyo amepigwa risasi, watuhumiwa wenzake walimchukua na kwenda kumtupa kwenye kichaka kilicho umbali wa mita 200 kutoka kwenye eneo la tukio na kisha kutoweka.

Alisema wakazi wa kijiji hicho ndiyo waliomtambua askari huyo baada ya kufuatilia michirizi ya damu na kuukuta mwili wake wake ukiwa kichakani na kutoa taarifa polisi. Alisema polisi walifika kwenye eneo hilo baada ya muda mfupi na kumtambua askari huyo.

Idriss Sultan Asimulia A to Z Jinsi Alivyompa Mimba Wema Sepetu.....

$
0
0
WEMA ALIMWAMBIA IDRIS KUWA ANATAKA KUSAFISHA KIZAZI...IDRIS AKASEMA SUBIRI KWANZA TUJARIBU TUONE KWA HIYO AKAMWAMBIA SIKU YA KUFANYA HILO TENDO ASILE KITU CHOCHOTE KUANZIA SAA TANO NA MIDA YA JIONI WAWEZE KUFANYA KITU HICHO..BAADA YA KUFANYA HICHO KITU  KESHO YAKE WEMA AKAANZA KUTEST MKOJO NA VIPIMO VYAKE KUONA KAMA AMENASA MARA VIPIMO VIKAONESHA KAMA AMENASA.BAADA YA KUONA HIVYO AKAPAGWA NA AKAONA NI BORA AENDE KWA DAKTARI WAKE ILI APATE UHAKIKA ZAIDI.
DAKTARI NAYE AKATHIBITISHA KWAMBA NI KWELI AMEPATA MIMBA.MTANDAO HUU WA UDAKU UNAWAPA HONGERA SANA WEMA SEPETU NA IDRIS

Chadema Wadai wako Tayari Kuchangisha Fedha Kuilipa TBC irushe Bunge Lote 'Live'

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kuwa kiko tayari kuzunguka nchi nzima kuchangisha fedha kwa ajili ya kulilipa Shirika la Habari Nchini (TBC) gharama za kurusha moja kwa moja matangazo ya vikao vyote vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema – Zanzibar, ambaye pia ni Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, Salum Mwalimu ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari akipinga sababu zilizotolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuhusu uamuzi wa TBC kutorusha ‘Live’ vikao vyote vyote Bunge bali kurusha ‘Live’ baadhi ya sehemu ya vikao hivyo.

Nape alieleza kuwa serikali imechukua uamuzi huo kwa lengo la kubana matumizi kwa kuwa TBC imekuwa ikitumia shilingi bilioni 4.2 kwa ajili ya kurusha moja kwa moja matangazo ya vikao vya Bunge.

“Watafute namna gani ya kuweza ku-mobilize fedha ili ilipwe TBC au Taifa litafute Channel nyingine za kuweza kurusha matangazo hayo. Na Chadema tuko tayari kusaidia hilo. Tuko tayari kuhamasisha Watanzania mwenye shilingi moja, shilingi mbili au tatu atoe tuilipe TBC ili Bunge lirushwe moja kwa moja,” alisema Mwalimu.

Katika hatua nyingine, Mwalimu alionesha kutokubaliana na hesabu za shilingi bilioni 4.2 zilizotajwa na Waziri Nape kuwa gharama za kurusha matangazo ya Bunge ‘Live’ kwa TBC.
“Mimi nimekuwa mwandishi wa habari na nimefanya kazi kwenye TV. Kila nikichambua  shilingi 4.2 bilion kwa ajili ya kurusha Bunge katika muda ambao sio ‘prime’… yaani kila nikipitia rate zote za Televisheni, sioni hiyo 4.2 bilioni zinapatikanaje,” aliongeza.

Wabunge wa upinzani leo pia walitoka nje ya Bunge hilo kushinikiza serikali kubadili tangazo lake kuhusu TBC na vikao vya bunge.

Wema Sepetu Aelezea Kwa Kina Beef yake na Zari, ‘Sio Nasib Wala sio Mwanamke Wake, Wote Waniache’ (Audio)

$
0
0
Wema Sepetu amefunguka kwa mapana kuhusiana na ugomvi wake na Zari the Bosslady ulioshuhudia warembo hao wakibadilishana michambo kwenye Instagram.


Miss Tanzania huyo wa zamani alikuwa akihojiwa kwenye Ijumaa hii kwenye kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM. Alikuwa ameongozana na mpenzi wake, Idris Sultan.

Mimi nilivyoamua kuwa out of Diamond’s life niliamua hivyo and I am out of Diamond’s life. I don’t know why watu wanajaribisha sana kunibring back to his life wakati I have already like moved on,” alisema Wema.

“I accepted my break up with Diamond from the beginning and I never wanted anything to do with him, nilivyoamua kwamba this is is going to be it nikaamua. Mimi na Diamond tumeachana 2014 and I was the one who actually decided that it’s going to be over. Lakini wakati Diamond ameshamove on ameshakutana na girlfriend wake, mama wa mtoto wake mimi sikuwahi kujihusisha katika mambo yao. Lakini I think the girl (Zari) anakuwa kama ana kitu na mimi. I have been quite for a very long time, first year nimekaa kimya, second year nimekaa kimya, it’s like kama vile anataka kunichokonoa,” alifafanua.

Wema alisema kuwa kuna wakati Zari alikuwa anatembelea ukurasa wake wa Instagram na kulike baadhi ya post zake lakini aliamua kumblock ili kuepusha shari.

“Nilivyomblock nikaona sasa anaendelea,ataongea atamtag Esma sasa nikitagiwa mimi nakuta kwenye ‘photos of you.’ Anasema ndipo alipogundua kuwa Zari amemwandikia maneno makali yaliyomuumiza kiasi cha kuamua kuuvunja ukimya wake.

“So I said what I have to say, kwasababu najua at that point nimwambie tu kitu ambacho kitamkera, sijui kuhusu mtoto wao that’s their life na sitaki kujihusisha. So nikafanya hivyo ili naye kumkera kwasababu lengo si ni kukerana.”

Wema anasema baada ya kumjibu hivyo Zari, mpenzi wake Idris alimgombeza sana kwakuwa hakufurahia. Hata hivyo amesema watu wake wa karibu walimjaza kuwa amekuwa akimvumilia Zari kwa miaka mingi sasa na kwamba ifike wakati naye ajibu mashambulizi.

“So I was like ‘okay let me do it’ so I did lakini sio kwamba nimetaka kufanya ni kitu ambacho this is not me.” Muigizaji huyo alisema ndio maana aliamua kuandika post kwake kuwa amefunzwa kutogombana na ‘watu wazima.’

Kwa upande wake Idris alisema hakupenda kitendo hicho na hapendi kuona kikitokea tena.

"Mimi sipendi, mimi na Diamond hatuna tatizo, he has been a brother to me for a long time. Naamini kwamba yeye na Wema haya mambo ni ya nyuma na yalishatokea na hakuna tatizo. Sio kwamba wewe ukishaondoka ndio umefunga basi marafiki zako wote, Diamond anajuana na watu wangapi? Kama watu wote anaojuana nao ikitokea mmoja amependana na ex wake basi nilishatoka na kaka yangu basi ndio imetoka,” alisema Idris.

Wema alimalizia kwa kuwataka Diamond na Zari waachane na maisha yake. Mrembo huyo na mpenzi wake Idris wanatarajia kupata mtoto katikati ya mwaka huu.

Sikiliza sauti yake hapo chini.

Source;Bongo5

Chadema Waungana na ACT -Wazalendo........Wadai Serikali ya Magufuli ni ya kidikteta

$
0
0
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekosa imani na serikali ya awamu ya tano kwa kuwa na matendo ya kidikteta na kwenda kinyume na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kwa kuminya uhuru wa wananchi wa kupata habari.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam, na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari ambapo amesema kuwa serikali imekuwa ikijinadi kwa kauli mbiu ya hapa kazi huku ikiwa mstari wa mbele kwa kuwanyima haki ya msingi wananchi ya kupata habari.

Amesema kuwa matendo hayo ni pamoja na kuzuia Shirikia la Utangazaji la Tanzania(TBC), kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mikutano ya bunge inayoendelea ,kufutwa kwa Gazeti la Mawio pasi na sababu za msingi,kuzuia vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara, na kuunda kamati dhaifu bungeni.

Amesema kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Mnauye ametoa sababu zisizokuwa za msingi ambapo alidai kuwa serikali inaepuka gharama za kurusha matangazo hayo moja kwa moja na baadala yake kurekodi vikao hivyo vya bunge kwa  kurushwa saa nne usiku.

Amesema inaonekana Waziri huyo hajafanya utafiti na kwamba ikiwa  tatizo lipo kwenye gharama alizotaja chadema ipo tayari kuchangia gharama hizo kwa kuanzisha harambee maalumu pamoja kuwataka chama cha wamiliki wa vyombo vya Habari (Moat) na Baraza la Vyombo vya Habari (MCT) kulisimamia suala hilo.

“Nape ataje gharama hizo tutachangishana ......mwenye mia moja mia mbili ili wananchi wajue mambo muhimu yanayoendela kwa wakilishi wake”,amesema Mwalimu.

Amesema Nape alikuwa anayumba kwa kuwa na ndimi mbili kwa kuongeza sababu nyingine ya kuzuia kurusha kwa matangazo hayo ni kuwa muda huo ni wa kazi na kwamba watu watakuwa hawafanyi kazi kutokana na kuangalia bunge.

Amesema kuwa hoja ya watu kutofanya kazi haina mashiko kutokana na watu huwa wanafanya kazi ilhali bunge linaendelea ambapo kama kuna hoja muhimu watu huzisikia bila kuathiri shuguli zao lakini kuna wengine muda huo sio wa kazi kwao.

Amesema kuwa serikali imekusudia kuminya uhuru wa habari kutokana na matukio yaliyofuatana ya kushugulikia vyombo vya habari.

Amesema kuwa serikali imezuia mikutano ya siasa ambapo Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa na Nape Mnauye walitoa kauli hizo walipokuwa Mkoani Lindi na baadaye Jeshi la Polisi kuweka mkazo wa suala hilo.

Amesema suala hilo hawawezi kulikubali kutokana na chama kuwa na mikutano yao kila baada ya muda na kwamba muda wa kuratibu mikutano hiyo watafanya vikao vyao.

Amesema serikali imeunda kamati dhaifu bungeni  kwa nia ya kudhoofisha shughuli za utendaji bungeni na maendeleo ya nchi kwa kuwaweka wabunge wageni kwenye kamati muhimu ilhali hawana uwezo kuzisimamia ambapo kamati ambazo hazina umuhimu kupangiwa watu wenye uwezo.

Ubalozi India Tanzania Waingilia Maiti ya Mtanzania Kuzuiwa India

$
0
0
Ubalozi wa India nchini umeingilia kati sakata la kuzuiwa mwili wa Mtanzania, Abel Machanga aliyekwenda kutibiwa nchini India kabla ya kufariki dunia.
Mwili wa Machanga umezuiwa katika Hospitali ya Colombia Asia iliyopo kwenye mji wa Bangarole, hadi deni la dola 16,396 sawa na Sh 35 milioni litakapolipwa. Ufuatiliaji huo umekuja ikiwa ni siku moja baada ya gazeti hili kuchapisha habari kuhusiana na kuzuiliwa kwa mwili huo kwa siku 27 katika hospitali hiyo. Hivi sasa zinafikia siku 30.

Abel alifariki dunia Desemba 31 mwaka jana baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe wa kichwa aliogundulika kuwa nao baada ya kufanyiwa uchunguzi . Julai mwaka jana, gazeti hili lilichapisha habari ya maradhi ya kijana Abel hatua iliyosaidia kupatikana kwa dola 7,700 fedha zilizohitajika kwa ajili ya matibabu yake India.

Kwa mujibu wa mmoja wa maofisa wa ubalozi, aliliambia gazeti hili kuwa taarifa hiyo imemfikia, Balozi Sandeep Arya ambaye ametaka kujua ilipo hospitali hiyo.

Balozi ameguswa na hiyo taarifa na kama inavyoonekana inaharibu picha ya India hivyo anataka kuifuatilia hiyo hospitali ingawa sijui ni kwa namna gani atalishughulikia suala hilo,” alisema

Ofisa huyo alieleza kuwa hospitali za Colombia Asia ziko nyingi nchini India hivyo inamlazimu balozi kupata anuani kamili ya eneo ambalo Abel alipatiwa matibabu na hatimaye kuaga dunia.

Katika hatua nyingine baba wa Abel, Revocatus Machange amesema mpaka sasa amepata takribani dola 16,000 ambazo ameshazituma nchini India.

“Namshukuru Mungu wasamaria wema wamesikia kilio changu nimeshatuma kiasi kikubwa cha pesa ninachosubiri kwa sasa mwili wake utolewe hospitali”

Kuhusu gharama za usafirishaji Machanga alisema anasubiri mwili wa Abel utolewe hospitali kisha masuala ya usafirishaji yatafuata baada ya kupimwa na kujua itagharimu kiasi gani.

Kambi Rasmi Ya Upinzani Yagoma Kusoma Hotuba Yao Bungu Lasitishwa

$
0
0
Bunge
Kwa mara nyingine bunge limesitisha shughuli zake baada ya kambi rasmi ya upinzani bungeni kugoma kusoma hotuba yao ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano.

Hali hiyo imejitokeza baada ya Mh Zitto kuomba mwongozo na kusema "Serekali imefanya makosa kwa kuwasilisha mpango huo kwa mwaka mmoja mmoja jambo ambalo ni kinyume na kanuni na katiba yetu
Wakati Zitto anaomba mwongozo, alimwomba mwenyekiti wasitishe shughuli mpaka marekebisho yakafanyike. Lakini Chenge alikataa, Cha kushangaza baada ya upinzani kugoma kuwasilisha Hotuba yao ghafla alisitisha.

Nimejiulizaa alichomkatalia Zitto ni nini na alichokuja kukifanya ni nini?

Hii Kolabo Ya Zitto Na Lissu Ni Hatari Tupu! Yamtoa Jasho Chenge

$
0
0
Kwa mara ya kwanza namwona nimemshuhudia Mwanasheria msomi kutoka Harvard Bw Andrew Chenge akibabaika baada ya kukumbana na kibano kikali cha hoja nzito kutoka kwa Zitto Kabwe na Tundu Lissu kuhusu kukiukwa kwa kanuni za bunge juu ya hoja iliyowasilishwa na wizara ya fedha na mipango.Hoja ya Zitto imepelekea kikao cha bunge kuahirishwa mpaka jioni.Hongera Zitto na Lissu,endeleeni kumfunda Bw Chenge kuhusu sheria na kanuni za binge mpaka aelewe.CCM walidhani watawadhibiti wabunge wa upinzani kupitia Chenge,imekula
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live




Latest Images