Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live

Ulisikia Habari ya Serikali ya Eritrea Kutoa Amri Kwa Wanaume Kuoa Wake Wawili..!...Mapya Yaibuka

0
0
Habari ya mzaha kwamba wanaume wa taifa la Eritrea wameagizwa kuoa wake wawili, ambayo imesambaa barani Afrika imewaudhi maafisa wa taifa hilo.

''Hata mwendawazimu katika mji mkuu wa Asmara atajua kwamba habari hii sio ya kweli'',afisa mmoja wa ubalozi wa Eritrea Kenya ameiambia BBC.
Habari hiyo ilichapishwa katika mtandao wa kitengo cha gazeti la The Standard la Kenya cha Crazy Monday.

Baadhi ya watu wametoa maoni yao katika mtandao wa Twitter kwamba wako tayari kusafiri hadi Eritrea ili kutafuta wanawake wa kuoa.

''Jarida la Crazy Monday ambalo huchapishwa na gazeti la Standard hujulikana sana kwa stori zake za udaku, likiwa ni mpango wa kutaka kuwavutia vijana," anasema Mathias Muindi wa BBC Media Monitoring.

Lakini hilo halijazuia taarifa hiyo kuripotiwa katika mataifa ya Nigeria hadi Afrika Kusini huku wengine wakisema kuwa ni ukweli.

Habari hiyo inasema kwamba ili kuhakikisha kuwa kuna wanaume walio wachache nchini humo wanaokidhi mahitaji ya wanawake walio wengi, kufuatia vita kati ya taifa hilo na Ethiopia mwaka 1998-2000, kila mwanamume lazima aowe wake wawili la sivyo afungwe jela.
Lakini afisa wa ubalozi wa Eritrea aliyezungumza na BBC amesema idadi ya wanawake na wanaume inakaribiana.

Waziri wa habari nchini Eritrea Yemane Gebremeskel alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter akisema kwamba habari hiyo ni ya uvumi, sio ya kweli na inakera.

Serikali Yatoa Tamka Kuhusu Kuruhusiwa TV Binafsi Kurusha Matangazo ya Bunge Laivu

0
0
Wakati Bunge likieleza kuwa haliwezi kuzuia vituo vya televisheni nchini kuonyesha moja kwa moja matangazo ya shughuli za vikao vya Bunge, Serikali imetoa sababu tatu za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kupunguza matangazo hayo ya shughuli za chombo hicho chenye mamlaka ya kutunga sheria.

Uamuzi wa Serikali kuhusu TBC ulizua sintofahamu bungeni na kusababisha polisi kutumika kuwatoa katika Ukumbi wa Bunge, wabunge wa upinzani waliokuwa wakishinikiza kusitishwa kwa mjadala wa hotuba ya Rais John Magufuli, badala yake lijadiliwe suala hilo la shirika hilo.

Naibu Katibu wa Bunge, John Joel alisema jana kuwa hakuna televisheni yenye mkataba na Bunge kurusha moja kwa moja matangazo hayo, zote zinazorusha zinatumia gharama zao wenyewe.

Baada ya TBC kupunguza matangazo ya moja kwa moja ya shughuli za Bunge, televisheni zilizobaki ambazo zinarusha moja kwa moja matangazo hayo, ni Star TV kupitia chaneli yake ya Star Bunge pamoja na Azam TV.

 “Sisi hatuna mkataba nao, wao wanarusha kwa gharama zao na Bunge haliwezi kuwazuia, labda waulizwe wenyewe kama wataendelea kurusha matangazo hayo ama laa,” alisema Joel huku akisisitiza kuwa hakuna zuio lolote.

Juzi jioni Waziri wa Habari, Nape Nnauye alizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma na kueleza sababu tatu za kupunguzwa kwa matangazo hayo.

Nape aliitaja sababu ya kwanza kuwa ni kupunguza gharama za uendeshaji, “Kwa mwaka TBC ilikuwa inatumia Sh4.2 bilioni kurusha moja kwa moja matangazo haya. Fedha hizi hazilipwi na Bunge wala Serikali, zinatokana na matangazo madogo ya TBC, sasa pia hesabu tangu 2005 mpaka sasa zimetumika kiasi gasi.”

Alisema sababu nyingine ya kupunguza kurushwa kwa Bunge ni kutaka wafanyakazi wa Serikali kufanya kazi kikamilifu, kwa madai kuwa wengi badala ya kufanya kazi walikuwa wakifuatilia vipindi hivyo.

Alisema utafiti uliofanywa na Serikali umebaini kuwa waendesha bodaboda, mamalishe, wamachinga, wakulima, wafugaji na watu wenye shughuli nyingi wanashindwa kufuatilia vipindi vya Bunge asubuhi na mchana kutokana na kubanwa na shughuli zao.

Desperate Single Women, Acheni Complication

0
0
Desperate Single Women
Watajwa hapo juu ni wanawake ambao hawana waume/mahusiano ya kudumu.
Wanaomba wapate japo mwanaume atakaweza kumsitiri, wengi wao ni wale ambao umri wa kugombaniwa na wanaume umepita kundi hili ndio wateja wazuri wa waganga wa kienyeji kwaajiri ya kusafisha nyota na kununua MGAGANE, ili aweze kuwanasa wanaume.

Tatizo lililopo ni baadhi yao wako very complecated, anaweka sifa na vigezo utafikiri ametoka kufanya NECTA Mwaka jana. Wadada, ukiwa kwenye fainali usisumbue bidders (watarajiwa) kuwa mnyenyekevu shukuru kwa yeyote anayekujia mradi anaakili timamu na anaweza kujitegemea na imani zenu ziwe sawa achana na kutafuta HB mda umeshakuacha!

Karibu tujumuike

Onyo, nothing personal here so don't come crushing to attack an innocent messenger like me.

Download Udaku Special Blog Android Application Katika Smart Phone Yako Kupata Habari za Udaku na Siasa Kwa Urahisi

0
0

Good News! Sasa Blog yako ya Udaku Special Ipo Google Play Store.

Download Udaku Special Blog Android Application CLICK HERE From Play Store

Au Bonyeza hii picha hapa chini

Stori Kuhusu Mbwana Samatta Mara Baada ya Kutua Ubelgiji Kwenye Club ya Genk

0
0

Mbwana Samatta, amewasili nchini Ubelgiji tayari kujiunga rasmi na Klabu ya KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.

Samatta aliondoka nchini juzi saa 6:00 usiku kuelekea Ubelgiji ili kukamilisha taratibu za kujiunga na klabu hiyo mpya ya Genk, baada ya bosi wa TP Mazembe, Moise Katumbi, kukubali kumuuza.

Meneja wa mshambuliaji huyo, Jamal Kisongo, alisema amewasiliana na Samatta na kumweleza kwamba amefika salama na ameanza kufuata taratibu zote ili aweze kufanya kazi nchini humo.

Alisema mara baada ya kuwasili, alitakiwa kufuatilia kibali cha kazi ambacho kitamruhusu kufanya kazi katika klabu hiyo mpya na muda wowote ataanza mazoezi.

“Kuhusu Hati ya Uhamisho wa Kimataifa) (ITC), Katumbi (Moise) amemhakikishia kuituma kwa klabu hiyo, kwani kabla ya kuondoka juzi aliongea naye na kumpa baraka zote za maisha mapya katika Klabu ya Genk,” alisema.

Kisongo alisema kwa kuwa bosi huyo wa TP Mazembe ameridhia kumuuza Samatta kwa Genk, siku chache zijazo anatarajia kwenda nchini Ubelgiji kwa ajili ya kusaini mkataba ambao atafaidika nao ikiwa mshambuliaji huyo atauzwa kwa klabu nyingine.

Samatta ambaye alitwaa tuzo ya kuwa Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, alikubali kujiunga na timu ya KRC Genk na kugomea ofa zilizotolewa na klabu za Nantes na Olympique Marseille za Ufaransa.

Aika na Nahreal; Muziki Kama Kawa, Mapenzi Kama Dawa

0
0

 Miongoni mwa wasanii wanao-ipeperusha vyema bendera ya Bongo kwa sasa ni Aika na Nahreal wanaounda Kundi la Navy Kenzo ambao pia ni ‘couple’ waliodumu kwenye uhusiano wa mapenzi kwa muda wa miaka 8, tangu waanzishe uhusiano huo mwaka 2008 walipokutana wakiwa masomoni India.
Ni ukweli usiofichika mafanikio ya wasanii hawa yanakua kwa kasi kutoka ‘uyoga’ kuelekea kuwa ‘mbuyu’, haya chini ni mambo ambayo huenda ulikuwa huyafahamu kuhusu wao.

Maisha yao binafsi
Aika na Nahreal wanakula na kupakua pamoja, akizungumzia juu ya maisha yao, Nahreal anasema imewalazimu kupanga saa za kufanya kazi pamoja na kutenga muda mwingine wa mapumziko ambao huutumia kama familia kuimarisha uhusiano wao na kutengeneza mustakabali wa maisha yao ya baadaye.

Kuhusu kazi
Wanapiga mzigo chini ya Kundi la Navy Kenzo na lebo ya The Industry inayobebwa na jina la studio wanayoimiliki, wote wakiwa mameneja mbele ya timu ya watu nane.

Kama kundi, tangu wameguke kutoka Pah One wamefanya nyimbo nyingi zikiwemo Hold Me Back, Cheza Kizembe (Waliurekodia Uganda), We Do Work, Bokodo, Aiyola, Visa na Game.

Japo hawajafanikiwa kupata tuzo lakini wameorodheshwa kwenye tuzo nyingi ikiwemo ya Top Naija Music Awards ya Nigeria pia wamewahi ‘kupafomu’ kwenye tamasha kubwa la muziki lililowashirikisha wasanii wa Kiafrika lakini wanaofanya vyema kimataifa. Tamasha hilo lilibebwa na jina la African Music Concert na lilifanyikia Afrika Kusini.

Changamoto
Nahreal anasema mwanzoni wakati wanaingia kwenye gemu changamoto kubwa ilikuwa pesa na sehemu ya kurekodia. Lakini baada ya kupata studio na muziki wao kueleweka kiasi cha kupata shoo nyingi, changamoto zote hizo zimekimbia.

Hawajawahi kutengana
Hivyo ndivyo ukweli ulivyo. Aika na Nahreal wanasema tangu waanze muziki hawajawahi kufanya kazi kila mtu kivyake, mara zote studio wako pamoja, majukwaani na kila kona wanakopiga mzigo kwenye kazi yao hiyo ya muziki.

“Unaweza kufikiri ni masihara lakini ukweli ni kwamba miaka yote sisi tumekuwa tukifuatana kama kumbikumbi linapokuja suala la kazi na hatujawahi kutengana hata siku moja,” anamaliza Nahreal.

Breaking News: Mbwana Samatta Atia Saini Kuichezea Genk..Atavaa Jezi Namba....

0
0

He signed 4.5 years deal Leo Genk hapa Belgium..Atakuwa akivaa jezi namba 77 ..Hongera Mbwana Samatha

Zitto Kabwe: "Serikali Imekurupuka, Kuongoza Nchi Sio Kutumbua Majipu Tu"

0
0

Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amefunguka na kuonesha masikitiko yake kwa kitendo cha serikali kushindwa kuleta Bungeni mpango wake wa maendeleo wa miaka mitano.

Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook ameweka wazi jambo ambalo serikali inapaswa kufanya baada ya uchaguzi na kusema ni kuwasilisha mpango wa maendeleo wa miaka mitano.

"Shughuli ya kwanza ya serikali baada ya uchaguzi ni kuwasilisha mpango wa maendeleo wa miaka mitano ( kutafsiri ilani yake kwenda kwenye mpango wa utekelezaji) . Bunge linapaswa kujadili na kuidhinisha Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 na kisha Mpango wa mwaka mmoja kuanza kutekeleza Mpango huo wa miaka 5. Kwa mujibu wa Katiba ya JMT Ibara ya 63(3)(c), Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 hutungiwa sheria kwa ajili ya utekelezaji." Alisema Zitto Kabwe

"Leo Serikali ya Rais John Magufuli ilipangiwa kuwasilisha Mpango huo wa Maendeleo wa miaka 5. Imeshindwa. Imeleta mwelekeo wa Mpango. Haikuleta sheria na Kamati ya Bajeti Imeleta maelezo yake kuhusu Mpango wa Maendeleo wa mwaka mmoja ilhali hakuna Mpango wa Miaka 5. 

"Mwenyekiti Chenge alitaka wabunge wajadili kwa mujibu wa kanuni ya 94 ambayo kimsingi ni Kanuni inayohusu Mpango wa mwaka mmoja. Serikali imejichanganya. Uongozi wa Bunge umechanganyikiwa." Aliongeza Zitto Kabwe

Zitto Kabwe alimaliza kwa kusema kuwa ni aibu kubwa kwa serikali inayojinasibu kwa kauli ya "Hapa kazi tu"

"Bunge linapaswa kuagiza Serikali ikalete Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 ili uidhinishwe na utungiwe Sheria kabla ya kuanza kujadili mipango ya mwaka mmoja mmoja.

"Ni aibu kubwa kwa Serikali ya ‪#‎HapaKaziTu‬ kushindwa kuleta Bungeni Mpango wake wa Maendeleo wa miaka 5 na hata ule wa mwaka wake wa kwanza. Itapangaje bajeti zake? Itatekeleza vipi ilani yake? Kuongoza nchi sio kutumbua majipu tu, ni kuendesha nchi." Alimaliza Zitto Kabwe.


Hivi Ndivyo Gari Jipya la Wema Sepetu Aina ya Range Lilivyokamatwa na Maafisa wa TRA..

0
0
Mama kijacho Wema Abraham Sepetu ‘Madam’ kwa mara nyingine ametengeneza kichwa cha habari, safari hii amewekwa chini ya ulinzi wa polisi kwa kosa la kuendesha gari aina ya Range Rover Evogue bila kuwa na vibali, Risasi Jumamosi lina ‘full’ stori.
Tukio hilo lililodumu kwa takriban saa tatu lilijiri Jumanne iliyopita maeneo ya Aficana, Mbezi Beach jijini Dar wakati mrembo huyo alipokuwa ‘kiguu na njia’ kwenda kwenye bethidei ya rafiki yake aliyefahamika kwa jina la Kibadude.

Gari lake likikaguliwa na maofisa wa TRA

NI LILE ALILODAI KUJIZAWADIA
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichokuwepo eneo la tukio, gari hilo alilokamatwa nalo Madam ni lile alilojizawadia kwa mbwembwe nyingi mwishoni mwa mwaka jana katika siku yake ya kuzaliwa ambalo lina thamani ya shilingi milioni 200 za Kibongo.
“Nimepiga picha. Wamemtaiti hapa Mbezi Africana, naona maofisa wa TRA wanamhoji. Lina tatizo katika uhalali wa kuingia nchini. Hapa sasa naona wanaomhenyesha ile mbaya. Si kawaida.”

AMWAGA CHOZI
“Sasa namuona Madam machozi yanamtoka yenyewe… anahaha, mara aende huku mara kule. Nahisi so litakuwa limemkalia vibaya maana kila simu anayopiga hapati msaada,” kilinyetisha chanzo hicho.
index2Ukaguzi ukiendelea

TRA WABAINI FIGISUFIGISU
Gazeti hili lilizungumza na ofisa mmoja wa TRA ambaye alikuwepo kwenye tukio hilo aliyeomba hifadhi ya jina kwa kuwa si msemaji wa mamlaka hiyo aliweka wazi kuwa, walibaini figisufigisu katika gari hilo.


“Hili gari ni moja kati ya magari ambayo yanaingia nchini kutokea nchi ya Msumbiji. Hata namba zake za usajili zinaonesha hivyo. Sasa huwa yanakatiwa vibali vya miezi mitatu au kulipiwa ushuru na kununuliwa. Liliingia nchini tangu mwaka jana.

“Tumekuta halina vibali maana vibali vya miezi mitatu vimeisha, tumemuuliza atoe nyaraka za gari, anasema zipo nyumbani, tukamwambia twende huko nyumbani ukazitoe, akabadili lugha, akasema anazo Steve (Nyerere). Inaonekana hili gari lina matatizo makubwa ya ushuru,” alisema ofisa huyo.

FIGISU NYINGINE
Kumbukumbu zinaonesha gari hilohilo la Wema ambalo alisema amejinunulia kwa fedha zake, ndilo alilodaiwa kununuliwa na mbunge machachari wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye aliwahi pia kutajwa kuwa ndiye baba kijacho wake kabla ya Idris Sultan kuibuka na kujinadi kuwa ndiye ‘mmiliki’ halali wa tumbo hilo.

KIGOGO SERIKALINI AMUOKOA
Paparazi wetu alimtafuta mtu wa karibu kabisa na Wema ambaye alieleza kuwa, Madam baada ya kuhaha kwa muda mrefu eneo hilo huku akiwa chini ya ulinzi wa polisi wenye bunduki, alipata wazo la kumpigia kigogo mmoja serikalini (jina tunalo) ambaye alimpa msaada kwa masharti.
“Alimpigia simu… (anataja jina la kigogo), akamweleza matatizo yaliyomkuta, naye akazungumza na maofisa wa TRA, wakakubaliana kwa masharti kwamba asilitumie gari hilo ndani ya wiki moja mpaka apeleke vibali vya gari hilo,” alisema mtu huyo wa karibu na Wema.

HUENDA LIKATAIFISHWA KAMA LA WOLPER
Kwa mujibu wa taratibu na sheria za TRA, endapo Wema atashindwa kutoa nyaraka muhimu za gari hilo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na  kutaifishwa kwa gari hilo kama ilivyomtokea mwigizaji Jacqueline Wolper ambaye mwaka 2014, gari lake aina ya BMW X6 lilikamatwa na kutaifishwa kwa kushindwa kulipia ushuru na kukosa vibali halali.

WEMA ASAKWA
Baada ya kupewa taarifa hizo, gazeti hili lilimtafuta Wema kwenye simu yake ya mkononi lakini muda wote iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu.

MENEJA WA WEMA ANENA
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, meneja wa msanii huyo, Martin Kadinda alisema yeye alisikia kwa watu kuhusu taarifa za Madam kukamatwa na gari hilo lakini alipomuuliza alimwambia si kweli, ni uzushi tu na hata gari hilo lipo nyumbani aende kuliona jambo ambalo alilifanya na kweli akajionea gari hilo.

“Ni uzushi tu. Nimeongea na Madam, akanihakikishia kwamba hamna kitu kama hicho. Nikaenda kulitazama gari, nikalikuta nyumbani kwake Ununio, shwari kabisa,” alisema Martin.
Gazeti ndugu na hili, Amani, toleo la Alhamisi iliyopita, ukurasa wa nyuma kulikuwa na habari yenye kichwa; Range la Wema layeyuka. Msingi wa habari hiyo ni taarifa kuwa, Wema haonekani akiwa na gari hilo licha ya kujinadi kuwa ni lake. Amekuwa akitumia kigari kidogo ‘ki-kirikuu’ kuendea kwenye shughuli zake.

Ilidaiwa kuwa, Wema alilipeleka gereji au yadi ya kuuzia magari, gari hilo hali iliyowafanya mapaparazi wa OFM kulisaka bila mafanikio huku ikielezwa kuwa, gari hilo si lake bali huwa anapepewa kwa muda kujiachia nalo.

Source;Global Publishers

LHRC Yaitaka Serikali Kuheshimu Haki ya Watanzania Kupata Taarifa, Yalaani Wabunge Kudhalilishwa na Mbwa wa Polisi

0
0
Serikali imetakiwa kuheshimu haki ya kikatiba ya kuwapa wananchi habari na taarifa muhimu zinazowahusu bila ya kujali gharama za taarifa hizo kwa kuwa ni jukumu lake kufanya hivyo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na kituo cha sheria na haki za binadamu kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi wake Bi. Imelda Urio na kuongeza kuwa kusitishwa baadhi ya matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge kwa kisingizio cha gharama ni kitendo cha makusudi kwa kuwanyima wananchi taarifa muhimu toka kwa wawakilishi wao ambao ni wabunge.

Bi Imelda Urio ameongeza kuwa muhimili wa bunge na viongozi wake lazima wafanye kazi kiueledi na kuzuia mianya ya kuingiliwa na mihimili mingine hususani serikali.

Aidha LHRC imelaani vikali kitengo cha kuzalilishwa kwa wabunge kwa kutolewa bungeni na mbwa wa jeshi la polisi,

Kwa upande wa kaimu mkurugenzi wa utetezi na maboresho Bi. Anna Henga yeye amesema kuwa haki yoyote haina gharama na ni jukumu la serikali kulipia gharama hizo za matangazo ya bunge.

Mume Wangu Hanitoshelezi, Kimwili na Kimahitaji......

0
0
Mume wangu ana tatizo la kuwahi kumwaga. Yaani dakika 2 tu ameshamaliza na kuniacha nikiwa nateseka huku nikiwa nina hamu. Tatizo hili limekuwa linanisababishia maumivu ya tumbo na kiukweli nikiwa naye sikuwahi kufika kileleni na kwa kuwa alinioa nikiwa bikira sikuweza kugundua mapema tatizo ni la nani.

Muda mwingi nilikuwa najichukia na kuwaza huenda mimi ndio nina tatizo na yeye mwenyewe wakati nikilalamika alikuwa ananiambia kuwa mimi ndio nina tatizo kwanini kila siku sifiki kileleni; mara nilikuwa siko tayari basi tu ilimradi nionekane tatizo liko kwangu.

Basi siku moja niliamua kujaribu nje, lol sitasahau ilikuwa ndio siku yangu ya kwanza kujua raha ya mapenzi. Sasa toka wakati huo nimekuwa simpendi kabisa mume wangu na nina mpango niachane naye kwani mbali na kutokuwa mzuri kitandani pia hatoi huduma kwa familia, kiufupi ni mvivu kila idara.

Naombeni ushauri wenu nifanyeje ili niweze kuachana naye coz siwezi kuishi na mume ambaye anamaliza haja zake tu (mbinafsi).

By Fiona

Sikuwahi Kumpenda Kanye West, Wiz Khalifa Ndiye Aliushika Moyo Wangu – Amber Rose

0
0
Amber Rose amesema hakuwahi kumpenda Kanye West wala ex wake wengine.

“Real love? Was with my husband [Khalifa],” Rose, aliimbia podcast ya Guys We F–ked ya Krystyna Hutchinson na Corinne Fisher.

“My soon-to-be ex-husband. Absolutely, for sure. When you really find love, you just know. So you look back at your past relationships and go, ‘Eh, I didn’t love those fools.'”

Rose alisema aliwahi kuwatamkia ex wake wengine ‘Nakupenda’ lakini hakujua upendo wa kweli hadi alipokutana na Khalifa. “He was the love of my life,” aliongeza kuhusu Wiz aliyezaa naye mtoto mmoja. “He was the only man I’ve ever loved.”

Rose na Khalifa walivunja ndoa yao miezi 14 baadaye September 2014, na ni wazazi wa mtoto wa kiume aitwaye, Sebastian, 2. Kabla ya Khalifa, Rose alikuwa na uhusiano na Kanye, kuanzia 2008 hadi 2010.

Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye Aiangukia Serikali Kuomba Msaada Baada ya Wananchi Kuvamia Shamba Lake La Ekari 33

0
0
WAZIRI Mkuu Mstaafu Mhe. Fredrick Sumaye, ameiangukia serikali na kuomba msaada baada ya wananchi kuchukua sheria mkononi na kuvamia eneo lake la ekari 33 lililopo Mabwepande katika Manispaa ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Serikali imemuahikikishia Mhe. Sumaye kuwa haina mpango wa kumkandamiza mtu mnyonge wala tajiri hivyo itahakikiha inatoa haki kwa kila mmoja baada ya wiki mbili kwa kua imesikiliza pande zote mbili katika mgogoro huo.
 
Akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya wananchi wa kitongoji  cha Kimondo mtaa wa mji mpya Kata ya Mabwepande na Mhe. Sumaye  Dar es Salaam jana asubuhi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda alisema ili kumaliza mgogoro huo ambao Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye ameiomba serikali kuingilia kati ni lazima busara kutumika.
 
Alizitaka pande hizo mbili kuiachia serikali kwa wiki mbili ili kutafuta njia bora ya kumaliza tatizo hilo huku wananchi wakitakiwa kuacha kuendelea na ujenzi na kugawiana maeneo katika shamba hilo.
 
“Serikali ya Rais Magufuli ni sikivu na ndio maana ilikuwa tayari kumsikiliza Waziri Mkuu wetu Mstaafu Sumaye na kusikiliza wananchi. ili kutenda haki tunatambua migogoro ya ardhi ilivyokuwa na athari kwa jamii hatuna mpango wa kumkandamiza tajiri wala mnyonge,”alisema.
 
Alisema katika eneo hilo anajua jinsi wananchi walivyotumia nguvu katika kuwekeza ujenzi na rasilimali zao lakini kwa sasa wasitishe shughuli hizo na kuendelea kugawana maeneo na Sumaye pia kuacha uwekezaji ili kutafuta suluhu.
 
"Zipo njia nyingi tutazitumia kumaliza mgogoro huu ikiwemo kufuata sheria kwa kuangalia iwapo mzee wetu alikiuka taratibu za kumiliki ardhi kama ilivyodaiwa na wananchi ili tujue hatua za kuchukua,”alisema.
 
Alisema pia wanaweza kukaa na Sumaye na kuzungumza naye ili kukubali hasara kwa kutoa eneo kidogo na kuwapatia wananchi  hao ambao hawana makazi au Manispaa kutafuta eneo mbadala na kuwauzia kwa bei nafuu.
 
Alizitaka pande hizo mbili kutambua umuhimu wa kulinda amani katika mgogoro huo kwa changamoto zilizopo kutatuliwa bila kutumia nguvu.
 
Makonda pia aliagiza serikali ya kijiji kufanya utambuzi wa wananchi hao wenye makazi katika shamba la Sumaye.
 
Awali katika mkutano huo Mhe. Sumaye alimueleza Mhe. Makonda jinsi serikali ilivyo na kazi ngumu ya kushughulikia migogoro ya ardhi na kuomba kutumia busara zake kumpatia eneo hilo analomiliki kihalali.
 
“Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya kama nilivyokueleza awali serikali yetu inakazi ngumu sana hasa kutokana na viongozi wa chini kutokuwa wasikivu na wakweli .Eneo hili namiliki kihalali ,nina nyaraka zote na ninalipia kila mwaka na nilikuwa katika mpango wa kutafuta wafadhili ili kuliendeleza kwa kujenga Chuo Kikuu,”alisema.
 
Alisema  yeye na familia yake waliuziwa eneo hilo toka mwaka 1997 na anaamini serikali itatenda haki.
 
 Diwani wa kata hiyo Suzan Masawe alisema anauthibitisho kuwa eneo hilo lilikuwa pori na Sumaye alilitelekeza kwa muda mrefu na kusababisha uhalifu ikiwemo wanawake kubakwa,mali za wizi kufichwa na uhalifu mbalimbali.
 
Alisema kutokana na hatua hiyo   walimtafuta Sumaye lakini hakuwa na ushirikiano kwakuwa hata alipofanya uwekezaji kwa kuchimba kisima cha maji alikataa kuwapa wananchi .
 
Suzan alisema kutokana na hasira za wananchi hao kwa kukosa huduma za kijamii kwa muda mrefu ikiwemo eneo hilo kutokuwa na shule,Zahanati wala kituo cha polisi waliamua kuvamia na kujigawia maeneo. 
 
Mmoja wa wananchi hao Athuman Mnubi alikiri kweli hawana umiliki halali wa eneo hilo na katika hatua ya kutafuta makazi walivamia msitu huo uliotelekezwa na Sumaye.
 
Alisema wanaamini kutokana na ahadi ya serikali ya Rais Magufuli katika kupora maeneo yaliyotelekezwa  na wawekezaji watasaidiwa.
 
WAKATI huo huo Makonda alisimamisha na kukamata baadhi ya malori ya kokoto na mchanga, wafanyakazi na Mwekezaji wa kigeni kutoka India  Sules Waljan wanaochimba mchanga,kokoto na kifusi katika eneo la Mabwepande.
 
Hatua hiyo imekuja baada ya kuona uharibifu mkubwa wa mazingira na alipowahoji wafanyakazi na Mwekezaji huyo kama wanavibali walisema hawana.
 
Makonda amewafikisha watuhumiwa hao kituo cha polisi cha Wazo Hill ili kutoa maelezo ya kina na kusema kuwa serikali inatumia gharama kubwa kwa uhalibifu huo wa mazingira ambao pia unafanywa katika vyanzo vya maji na matengenezo ya madaraja yanayoharibiwa ni makubwa.
Hapa Sumaye na viongozi wengine wakitafakari jambo.
DC Makonda akihutubia katika mkutano huo. Kulia ni Diwani wa Kata ya Mabwepande, Suzan Masawe.
Mheshimiwa Sumaye (kushoto), akiongoza kuonesha mpaka wa shamba lake.
Mhe. Sumaye akielezea uhalali wake wa kumiliki eneo hilo.

Mbunge Chadema Achaniwa Suti Mbili na Polisi

0
0
DODOMA: KALI ya mwaka. Mbunge wa Jimbo la Kilombero, Peter Lijuakali wa Chadema, amechaniwa suti mbili katika matukio mawili tofauti na Jeshi la Polisi ndani ya wiki moja, Risasi Jumamosi linakutaarifu.

Katika tukio la kwanza, mbunge huyo alitolewa nje kwa nguvu kutoka Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, baada ya kukaidi agizo la mwenyekiti wa kikao, Yahaya Nania la kumtaka asishiriki katika zoezi la kuapishwa kwa madiwani wateule na kumchagua mwenyekiti na makamu wa halmashauri hiyo kwa kili kilichodaiwa kuwa hakuwa mjumbe halali wa baraza hilo.

Katika purukushani hizo, zilizotokea Januari 24 mwaka huu, ambazo yeye aligoma kutoka akidai ni mwakilishi halali wa wananchi wa jimbo lake, mbunge huyo alichaniwa suti yake katika vuta nikuvute ya polisi.

Katika tukio la pili, Januari 27, mwaka huu, lililosababisha suti yake nyingine kuchanwa na polisi, Lijualikali alikuwa mmoja wa wabunge wa upinzani waliotolewa nje kwa nguvu, baada ya kukaidi amri wa Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge ya kukaa chini na kutulia.

Wabunge hao walichukuliwa hatua hiyo baada ya kupinga kujadiliwa kwa hotuba ya rais, aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa Bunge Novemba mwaka jana, wakitaka kwanza kupata ufafanuzi wa serikali kwa kitendo chake cha kulizuia Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kurusha vipindi vyote vya vikao vya Bunge moja kwa moja (live).

Kana kwamba haitoshi, wabunge wa upinzani kwa mara nyingine walitoka nje ya Bunge katika kikao chake cha asubuhi, Alhamisi iliyopita baada ya Naibu Spika, Tulia Akson kukataa kusikiliza mwongozo uliokuwa ukiombwa na wapinzani, baada ya Naibu huyo kuzuia kujibiwa kwa swali la mmoja wao kuhusu elimu ya bure.

Zitto Kabwe Atoa Mpya 'Serikali Isipojipanga Upya Itaendelea Kuaibika'

0
0

Kauli za Zitto Kabwe Asubuhi ya leo Facebook;

"Serikali ijue kuna Bunge. Bunge lina wabunge makini na wenye mapenzi ya dhati kwa Taifa letu. Serikali isipojipanga upya itaendelea kuaibika"

"Bunge limeiamuru Serikali kuleta Mpango wa Maendeleo. Shughuli ya kwanza ya Serikali Bungeni imeondolewa kwa hoja kutoka Upinzani. Serikali ya Awamu ya 5 imeanza na mguu mbaya. Wajue Bunge lipo. Hatuburuzwi"

Mbwana Samatta Aeleza ni Kwanini Ameamua Kuichagua Jezi Namba 77 Kwenye Timu yake Mpya

0
0
Mbwana Samatta Akionyesha Jezi yake Mpya
Baada ya mchezaji wa Timu ya taifa ya Tanzania ya mpira wa miguu “Taifa stars” na mchezaji wa kimataifa Mbwana Ally Samatta kusaini mkataba wa miaka minne na klabu yake mpya GENK FC ya nchini Ubelgiji wa kuichezea soka klabu hiyo, alitambulishwa kwa waana habari kama ishara ya utambulisho rasmi wa Samatta klabuni hapo.

Katika utambulisho huo Samatta alikabidhiwa Jezi nambari 77, wakati katika klabu yake ya zamani ya TP Mazembe jezi yake ilikuwa nambari 9 mgongoni, jambo ambalo Mbwana Samatta alilazimika kulitolea ufafanuzi baada ya kutafutwa kwa njia ya simu kwenye kipindi cha Sports Bar ya Clouds TV, ambapo mbwana samata alijibu kuwa yeye anapenda jezi 7 lakini kwakuwa jezi hizo katika klabu nyingi huwa zimesha chukuliwa aliamua kuomba jezi nambari 77 kwakuwa aliamini ni mara chache watu kuitumia.

Samatta aliongeza kuwa hata wakati alipokuwa akiichezea TP Mazembe alikuwa akiushawishi uongozi umpatie jezi nambari 7, alkini haikuwa raihisi kwa kuwa ilikuwa na mtu tayari, na hivyo katika klabu yake mpya ya GENK FC hakuona sababu ya kuomba tena jezi hiyo badala yake aliamua kuomba jezi nambari 77 kwakuwa bado ana mapenzi na namba 7.

Kipya Kinachoendelea Kuhusu Kuanzishwa Kwa Mahakama ya Mafisadi Tanzania

0
0
SERIKALI imewahakikishia Watanzania kuwa mchakato wa kuanzishwa kwa Mahakama Maalumu ya mafisadi na wezi, umefikia hatua nzuri. Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe alisema hayo juzi bungeni mjini hapa, wakati akichangia Hotuba ya Rais ya Ufunguzi wa Bunge.

Akizungumzia mchakato wa kuanzishwa kwa mahakama hiyo maalumu, Mwakyembe alisema unakwenda vizuri na utakapokamilika Watanzania watafahamishwa. “Kiongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, akitoa tamko lazima litekelezwe.mwakyembe (1)

Kama tunakumbuka Rais, kwa nyakati tofauti kipindi cha kampeni, aliahidi kuanzisha Mahakama Maalumu ya Mafisadi na Wezi,” alisema Mwakyembe. Akiizungumzia hotuba ya Rais, Mwakyembe alisema ikiachwa hotuba ya Mwalimu Nyerere, ya Magufuli pia ni bora na iligusa mioyo ya Watanzania wenye nia njema na Taifa.

“Wakati rais anatoa hotuba yake iliyokuwa na aya 160, alipigiwa makofi na vigelegele mara 137, ni zaidi ya asilimia 86, ya Dk Martin Luther ambaye ni Mmarekani mweusi,” alisema na kuongeza kuwa hatua hiyo, imewaweka pabaya wapinzani waliokuwa wanapinga kila kitu.

Dk Mwakyembe alisema tatizo ni kwamba kwa hotuba hiyo, yeyote akijaribu kuipinga, wananchi watamuona wa hovyo. Aliendelea kusema; “Wamejaribu (upinzani) kutoka kwenye mjadala, kwa hoja tu ya TBC (Shirika la Utangazaji Tanzania), ili wasiwepo kwenye mjadala, kwani wakiwepo lazima wataisifia tu.”

Kocha wa Manchestet United Afunguka Kwa Uchungu 'Sipo Tayari Kujiuzuli'

0
0

Meneja wa klabu ya Manchester Louis van Gaal amesema kwasasa hana mipango ya kujiuzulu kutoka katika wadhifa wake na kushutumu sana habari ambazo zimekuwa zikienea kwenye vyombo vya habari.

United hadi sasa wameshinda mechi tatu pekee kati ya mechi 13 walizocheza karibuni ligini na katika shindano la kombe.

Van Gaal na wachezaji wake walizomewa na mashabiki baada ya kufungwa 1-0 na Southampton Jumamosi katika mechi ya Ligi ya Premia jambo hilo lililofufua tena uvumi kuhusu hatima yake.

“Ni mara ya tatu kwangu kufutwa (kwenye vyombo vya habari) na bado niko hapa,” amesema Van Gaal. United wamo katika nafasi ya tano ligini, alama 10 nyuma ya viongozi Leicester City zikiwa zimesalia mechi 15.

Manchester United watakuwa ugenini dhidi ya Derby County katika raundi ya nne ya Kombe la FA Ijumaa.

Tazama Hapa Video Nzima ya Wema Sepetu na Idriss Walivyohojiwa na Diva Clouds FM

0
0
Idriss na Wema Sepetu
Couple ya ‘Wedris’ ilipata nafasi ya kuhojiwa exclusive na mtangazaji wa Clouds Fm, Diva kwenye kipindi cha Ala Za Roho usiku wa Alhamisi (Jan 28), ambapo kila mmoja alifunguka mambo mengi kuhusu toka walipokutana na kuanza kupendana, kuhusu wema alivyogundua kuwa ameshika ujauzito wa Idris na mambo mengine.

Kama hukupata bahati ya kusikiliza tazama hapa sehemu ya mahojiano hayo walipokuwa studio za Clouds Fm.

Nchi 12 Za Ulaya na Marekani Zalaani Tume Ya Uchaguzi Zanzibar Kutangaza Tarehe Ya Marudio Ya Uchaguzi Wakati Mazungumzo Yakiendelea

0
0
Mabalozi wa nchi zinazounda Umoja wa Ulaya (EU) wameeleza kusikitishwa na kitendo cha Tume ya Uchaguzi (ZEC) kutangaza tarehe ya marudui ya Uchaguzi wakati mazungumzo ya kutatua mgogoro yakiendelea na kumtaka Rais John Magufuli kutumia nafasi yake ya uongozi kutatua mtanziko wa kisiasa visiwani Zanzibar.

Taarifa ya pamoja iliyotumwa kwa vyombo vya habari na mabalozi hao jana, pia inamtaka Rais Magufuli kuendeleza wito wake wa kuzitaka pande zote zitafute suluhu kwa amani.

Tamko hilo limetolewa siku saba baada ya mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha kutangaza kuwa uchaguzi wa rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani utarudiwa Jumapili ya Machi 20, lakini siku tano baadaye CUF ilitoa tamko la kutoshiriki uchaguzi huo wa marudio.

Kutokana na sakata hilo, mabalozi hao wamelaani kitendo hicho wakisema kurudia uchaguzi kwa kigezo kuwa utaratibu ulikiuka, kinawatia wasiwasi kwa kuwa tume hiyo haikutoa ushahidi wa ukiukwaji huo.

Mabalozi hao wamesema katika tamko lao kuwa ZEC imerudia kauli yake ya kuwa uchaguzi ulikiuka taratibu licha ya waangalizi kutoka EU, Jumuiya za Afrika Mashariki, Sadc Marekani na Jumuiya ya Madola kufanya tathmini na kujiridhisha kuwa ulikuwa huru na haki.

“Tunasikitika kuwa ZEC imetangaza tena kuwa uchaguzi utarudiwa Zanzibar, wakati mazungumzo baina ya pande mbili yanaendelea. Kwa manufaa ya Watanzania wote, tunasisitiza kuwa hali ya kisiasa ya visiwani humo ni bora ikatatuliwa kwa pande mbili kukubaliana,” inasema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliyotumwa kwa ushirikiano wa mabalozi wa Uholanzi, Norway, Hispania, Italia, Ujerumani, Finland, Ufaransa, Sweden, Uswisi, Uingereza, Ireland na Marekani inasisitiza kuwa kitendo cha upande mmoja kuamua kurudia uchaguzi, kinaweza kuzidisha hofu na taharuki miongoni mwa Wazanzibari.

“Tunawaomba Wazanzibari kuwa watulivu na wavumilivu nyakati hizi na tunazitaka pande zote mbili na washirika wao kuendelea kufanya kazi pamoja ili wapate suluhisho la amani,” ilisema taarifa hiyo.

Pia inasema ili uchaguzi uwe wa kuaminika, mchakato wake hauna budi kuziwakilisha pande zote na kuwa huru na wa haki.

Hata hivyo, mabalozi hao wamesema kulingana na mazingira ya Zanzibar kwa sasa, itakuwa vigumu kwa waangalizi wa kimataifa kutegemewa kushiriki kwa namna yoyote katika uchaguzi huo.


Dar es Salaam, 29 January, 2016STATEMENT ON ANNOUNCEMENT OF ELECTION RE-RUN IN ZANZIBARThe High Commissioners and...
Posted by U.S. Embassy Tanzania on Friday, January 29, 2016
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live




Latest Images