Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104706 articles
Browse latest View live

Mke wa David Kafulila Amshukia Andrew Chenge na Vinara wa Kashfa ya Tegeta Escrow..Ashangaa Kwanini Hawapo Katika List ya Takururu

$
0
0
Mke wa David Kafulila
Mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Jesca Kishoa, amehoji kwa nini Tasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru), imesema watu 36 watafikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi lakini vinara wa kashfa ya Tegeta Escrow, ikiwa ni pamoja na Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Habirnder Seth Singh, hayumo.

Kishowa ni mke wa aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye aliishupalia hoja hiyo bungeni na kuwang’oa baadhi ya vigogo wa serikali wakiwemo mawaziri.

Kafulila ndiye Mbunge wa kwanza kuifikisha kashfa hiyo kwenye Bungeni la 10 na baadaye Ofisi ya Mdhimiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ikafanya uchunguzi na kuwasilisha ripoti yake ambayo ilifikishwa Bungeni na Kamati ya Hesabu za Serikali.

Kashfa hiyo ilisababisha aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kuachia ngazi.

Watumishi wengine walioguswa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, Wenyeviti wa Kamati ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa, Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, William Ngeleja na Kamati ya Bajeti, Andrew Chenge.

Aidha, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, alikumbwa na fagio hilo.

Kwenye mkutano wa jana wa Bunge, Kishowa alitaka kupewa maelezo kwa nini mmliki huyo wa IPTL hajachukuliwa hatua na kusema hata baadhi ya maazimio ya Bunge yaliyopitishwa hayajafanyiwa kazi.

Alisema ingawa anajua Mwenyekiti aliyekuwa akiongoza kikao cha jana, Chenge, ana maslahi katika suala hilo ni vyema akatoa mwongozo wa kiti.

Akijibu mwongozo huo, Chenge alisema, limeulizwa sehemu ambapo siyo kabisa.

Kuwa wa Kwanza Kudownload Wimbo Mpya wa Navy Kenzo - Kamatia!

$
0
0
Kundi la Mziki la Navy Kenzo linalo Undwa na Nahreel na Aika Wameachia Wimbo wao mpya unaitwa Kamatia.....

Hapa nimekuwekea Sehemu ya Kudownload Wimbo Huo...

Ali Kiba Amfananisha Mwanamuziki Ruby na Mbwa..Ruby Amshukia Ali Kiba na Kufunguka Makubwa

$
0
0
Mwanamuziki Ruby amefunguka kwa uchungu kuhusu Mwanamuziki Ali Kiba Kumfananisha na Mbwa....

"Kabla ya yote naombeni sana mashabiki zangu, mniwie radhi kwa nnacho kiandikia katika ujumbe huu binafsi mimi sijapendezewa kabisa na alichokisema kaka yangu @officialalikiba kwenye kipindi cha @thesporahshow kilichorushwa kupitia @cloudstv kaka yangu alikiba mimi ni mdogo sana kwako si kwa umri wa kimuziki, sikutegemea na sijapendezwa na kauli yako yakunifananisha mimi na MBWA mimi ni binaadam na ni mdogo wako kama alivyo @zabibu92kiba sidhani kama ungeweza kumwita huyo mbwa wako zabibu au abdul, mimi sina ukaribu wowote na wewe lakini kama mtu niliyemkuta kwenye industry na uliyenitangulia kuliona jua na mpaka uliponifwata kuniambia una- appreciate kazi yangu nakuniomba nifanye nyimbo na mdogo wako @officialbdukiba na nikakubali yote hayo yalifanikiwa kutokana na love niliyokuwa nayo kwako kama kaka yangu,hujawahi hata siku moja kunitamkia kwamba unambwa wako anaitwa Ruby, kwa sababu mimi na wewe tumesha kutana nakuongea si chini ya mara moja, hujawahi kusema hilo kwangu, ila umekuwa ukiniambia tu naimba vizurii, je ulisahau nini kaka yangu hadi kushindwa kuniambia muhusika wa jina la mbwa wako mpya,mimi nimeona ni kejeli na dharau kubwa na hazisaidii katika maisha zaidi ni kujishushia heshima yako haipendezi kwa mtu kama wewe ambae pia unaangaliwa na watu wengi kama kioo cha jamii,nategemea kuona mfano mzuri kutoka kwako nikiwa kama mdogo wako lakini umenitia giza machoni @officialalikiba kakaangu kwakweli nimekwazika sana kwasababu mimi ndo kwanza naanza game naanza kazi ya kuendeleza nchi hii na afrika kwa dunia nzima kwenye upande wasanaa ambao wewe umeshaanza muda ,lakini nimestaajabu unanifananisha na mbwa ,cha ajabu zaidi hata watu wako wa karibu @rehemavisuallab @zabibu92kiba hawaitamki wala kuileta katika jamii kwa usahihi wa mbwa kweli ,Naamini Mungu hamtupi mja wake, chozi la mnyonge haliendi bure, Me namuachia Mungu" Rubby

Aliyekuwa Mchumba wa Idriss Samantha Ampa za Uso Idriss na Kudai Anatukanwa na Watu Kwenye Page yake Bila Sababu

$
0
0
Samantha Aliyekuwa mpenzi wa Idriss Kabla ya Kumwagana baada ya muda mfupi wa penzi lao amefunguka kuhusu kero na matusi anazozipata kwasababu ya Idriss kutoka kwa mashabiki

Samanthajannsen 
@idrissultan I think you and I have had this discussion a few times and you know as well as I do that I don't want you and that we better off as friends. With that being said I would like to congratulate @wemasepetu and wish you all the best , but also kindly respect me as I have , because there's no where I have ever mentioned your name or called you any other name like you called me.Now please can people respect my page and stop with unnecessary drama , I have companies am working with and when they go on my social media pages , all they see is insults and negativity, why ? We all have lives past relationships , can we focus on positivity with all this strength people are using on negativity , I think we all have better things to do on social media 

Mahakama yamfutia Kesi Mtuhumiwa wa Kupokea Fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow

$
0
0
Aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Philip Saliboko, ameachiwa huru katika shtaka la kutuhumiwa kuwa alipokea rushwa ya Sh milioni 40.4 kutoka kwa Mkurugenzi wa zamani wa Kampuni ya IPTL, James Rugemalira.

Saliboko aliachiwa jana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kumuona hana hatia.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, aliyesema mahakama imemuona mshtakiwa hana hatia kutokana na upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha shtaka dhidi yake pasi na kuacha shaka yoyote.

“Mahakama inaona upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha kesi bila ya shaka. Mshtakiwa (Saliboko) hana hatia, anaachiliwa huru na mna haki ya kukata rufani kwa upande ambao haujaridhika,” alisema Simba.

Alisema mshtakiwa huyo aliposomewa shtaka kwa mara ya kwanza alikana na kwamba wakati wa usikilizwaji upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Dennis Lekayo, ulileta mashahidi watatu ambao ni mpelelezi mkuu na maofisa wawili wa Benki ya Mkombozi iliyoko Ilala, Dar es Salaam.

Pia alisema mshtakiwa anatetewa na Wakili Jamhuri Johnson, alijitetea mwenyewe baada ya mahakama kumuona ana kesi ya kujibu.

Hakimu Simba alisema shahidi wa kwanza wa upande wa Jamhuri alikuwa Mpelelezi Mkuu, Emmanuel Koroso, aliyeeleza kuwa alikabidhiwa jalada afanye upelelezi juu ya tuhuma hizo za Saliboko Oktoba 9, mwaka juzi na Mkurugenzi wa Takukuru.

Akichambua ushahidi wake, Hakimu Simba, alisema shahidi huyo alieleza alikusanya hati mbalimbali na kuhoji watu na alijitosheleza fedha hizo ziliingizwa katika akaunti ya Saliboko na mshtakiwa huyo hakuwa na maelezo mazuri kuonyesha namna gani alipokea fedha hizo.

Alisema mashahidi wawili kutoka Mkombozi, walithibitisha Saliboko alienda kufungua akaunti kama mteja wao na fedha hizo ziliingizwa katika akaunti ya mshtakiwa huyo na alizitoa mara tatu.

Kwa upande wa utetezi wa mshtakiwa Saliboko, alikubali kufungua akaunti ya Mkombozi na kuingiziwa fedha hizo na Rugemalira aliyekuwa na makubaliano naye ya kumtafutia shamba katika mikoa ya Tanga na Dar es Salaam ili aendeleze biashara zake.

Baada ya kuchambua ushahidi huo, Hakimu Simba alisema utaratibu wa sheria ni kwamba upande wa Jamhuri ndio wenye wajibu wa kuthibitisha mashtaka pasi kuacha shaka yoyote na sio jukumu la mshtakiwa kuthibitisha kwamba hajafanya kosa.

“Katika kesi hii, hakuna ubishi kwa upande wa Jamhuri na ule wa utetezi kwamba fedha ziliingizwa katika akaunti ya Saliboko, hivyo hakukuwa na ulazima wa kuwaleta wale mashahidi wawili kutoka Benki ya Mkombozi.

“Shahidi muhimu aliyebaki ni mpelelezi mkuu ambaye alipohojiwa na wakili wa utetezi alidai hakuna siku hata moja alienda kumuuliza Rugemalira fedha ziliingia katika akaunti ya Saliboko kwa kazi gani.

"Kwa mujibu wa sheria za Takukuru, mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni wakosaji, kama kweli ilikuwa rushwa kwanini Rugemalira hakuletwa mahakamani kushtakiwa maana ni mtoaji,” alisema Hakimu Simba.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Saliboko alikuwa anadaiwa Februari 5, mwaka juzi katika Benki ya Mkombozi, iliyoko wilayani Ilala, Dar es Salaam, akiwa mkuu wa Rita alipokea Sh milioni 40.4 kupitia akaunti ya VIP Engineering ya Rugemalira ambaye alikuwa Mkurugenzi wa IPTL.

Ilidaiwa alipokea fedha hizo kutokana na kazi yake kama bosi wa Rita wakati IPTL ilikuwa mfilisi na yeye alishughulikia hilo.

Mbaba Atupwa Jela Miaka Mitatu Kwa Kunajisi Zabinti zake Wawili wa Kuwazaa

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Pwani imemuhukumu kifungo cha miaka mitatu jela, Abdallah Saidi Kundumu, mkazi wa Miembesaba wilayani Kibaha, baada ya kukutwa na hatia ya kunajisi mabinti zake wawili wa kuwazaa.

Akisoma hukumu hiyo mahakamani hapo hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Aziza Mbadjo alisema kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 2013 na 2015, hivyo kutokana na kifungu cha sheria 158, kifungu cha kwanza cha kanuni ya adhabu anapaswa kutumikia adhabu hiyo.

“Ushahidi umejitosheleza pasipo kuweka shaka, maana hii ni kesi ya Jamhuri na kabla ya kutoa hukumu tunazingatia ushahidi wa kuaminika unaojitosheleza kulingana na taratibu zinavyoagiza na nimejiridhisha, hivyo anapaswa kutumikia kosa hilo,” alisema.

Mwendesha mashitaka katika kesi hiyo Inspekta Rashird Chamwi alidai kuwa kwa mujibu wa maelezo kutoka baadhi ya majirani wamshtakiwa huyo, zilieleza kuwa amekuwa akiwafanyia vitendo hivyo mabinti zake wa umri wa miaka 15 ni mwingine miaka 11.

Alidai kuwa watoto hao baada ya kuchoshwa na vitendo hivyo vya baba yao, waliamua kumjulisha mama yao mzazi ambaye kulingana na shughuli zake za ujasirimali amekuwa akilazimika kuondoka nyumbani alfajiri, kabla watoto hawajaamka na kurejea usiku jambo ambalo limekuwa likimpa nafasi mzazi huyo wa kiume kutekeleza vitendo hivyo.

Alidai kuwa kutokana na hali hiyo majirani wa familia hiyo walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na kufanyika uchunguzi wa kina na kubaini kuwapo kwa ukatili huo, kwa kuzingatia sheria watoto hao walifanyiwa vipimo na kukutwa na athari ambazo zinasababishwa kufanyiwa vitendo hivyo.    

Mbwana Samatta Ampa Ujumbe Huu Thomas Ulimwengu Baada ya Kujiunga na Genk.

$
0
0
Ulimwengu na Samatta ni washkaji wa karibu sana ambapo walijuana kwa karibu sana kutokana na kucheza pamoja kwenye club ya TP Mazembe. Sasa hivi Mbwana Samatta amejiunga na KRC Genk na kumuacha Ulimwengu ndani ya TP Mazembe.

Baada ya kutangaza kumbwa amejiunga na club ya Genk Samatta ameonyesha furaha lakini pia huzuni wake upo anapotengana na mshkaji wake Thomas Ulimwengu.

Huu hapa ni ujumbe mrefu alioandika Samatta kwa ajili ya Thomas Ulimwengu.

“Am gonna miss you my nigga, hope to have you near me again/Nitaku miss sana rafiki yangu nina imani nitakuwa nawe karibu tena. Ulikuwa mshauri na mtia moyo sana katika vipindi vigumu ila ndio maisha yametupa “No Choice” katika hili. Stay blessed bro your my nigga forever😢😢. Kila nikicheki picha we are pamoja najiskia ku-cry but no way. Wish you do the best in TP bro!!.

Ali Kiba Aguswa na Maneno ya Ruby..Amuomba Msamaha Baada ya Kumfananisha na Mbwa...

$
0
0
Ali Kiba Ameshutumiwa na Mwanamuziki Ruby kuwa amemfananisha na Mbwa alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha Sporah Show..
Ali Kiba Amemjibu Ruby Kupitia Ukurasa wake wa Insta na kumuomba msamaha lakini post hiyo haikukaa sana kwani aliifuta baada ya muda si mrefu ila tumeipata na kukuwekea hapa chini;



Kwa Fowadi hii ya Wachezaji wa Genk? Mbwana Samatta Labda Arogwe

$
0
0
Samatta ameikuta Genk ina mastraika saba kutoka Uturuki, Jamaica, Ugiriki, Georgia na wazawa wa Ubelgiji.

KWA mwanetu Mbwana Samatta tunayemjua na kwa Genk hii aliyokwenda,  labda alogwe. Lakini hakuna kitakachomzuia kuingia kwenye kikosi cha kwanza baada ya jana Ijumaa jioni kusaini mkataba wa miaka minne ambao unaanzia 2016-2020 mwaka ambao Rais John Magufuli atakuwa anatimiza miaka mitano ya kuongoza nchi.

Samatta ameikuta Genk ina mastraika saba kutoka Uturuki, Jamaica, Ugiriki, Georgia na wazawa wa Ubelgiji.

Huyo straika wa Uturuki anaitwa Enes Unal ni mchezaji wa Manchester City ya England ambaye ameletwa Genk kwa mkopo wa misimu miwili huu ni msimu wake wa kwanza na amepachika bao moja tu katika mechi zaidi ya 10 alizocheza.

 Huyo wa Georgia ni jamaa mmoja mtata sana uwanjani anaitwa Nikolaos Karelis anatumia guu la kushoto, mpaka sasa amefunga bao moja tu.

Sasa kuna mashine zao mbili wanazoziaminia ijapokuwa kiuhalisia umri umewatupa. Mmoja anaitwa Igor Alberto Camargo ana miaka 32, huyu jamaa amefunga mabao matano tu katika mechi zote 23 alizocheza.

Ni Mbrazili aliyepewa uraia wa Ubelgiji. Hao wangapi? Staa mwingine ni kibabu pia ana miaka 34 wanamuita Thomas Buffel ni pande fulani la mtu amefunga mabao matatu. Huyo wa Jamaica anaitwa Leon Bailey ni bwana mdogo kuliko hata Samatta, yeye ana mabao matatu.

Hao mafowadi wengine wala hata usitake kuwajua utakuwa unapoteza muda wako tu. Ila kwa jinsi Samatta alivyopania lazima mtu aende benchi.Sikia sasa mastraika saba wa Genk kwa ujumla wao katika mechi zote 23 walizocheza wamefunga mabao 12. Buffel na Camargo wamefunga mabao manane kati ya hayo. Ukiangalia takwimu hizo za mabao unapata jibu la kwanini Kocha Mbelgiji, Peter Maes alimtaka Samatta kwa nguvu zote kuokoa kibarua chake. Genk ipo katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi ikiwa pointi 32, huku AA Gent wakiongoza msimamo kwa pointi 49.

Kwenye timu hiyo kuna Wakongomani wanne ambao wamezaliwa Ubelgiji wana uraia wa nchi mbalimbali. Wakongomani hao ni Derick Katuku Tshimanga ambaye ni beki wa kushoto anayetumia mguu wa kulia mwenye kilo 68 ana miaka 27.

Mwingine ni Christian Kabasele ambaye ni bonge la beki anatumia guu la kulia na kwa sasa amepachika mabao mawili kwenye ligi. Kuna Mkongo Mwingine anaitwa Neesken Kebano ni kiungo ana mabao matatu msimu huu.

Kuna Mnigeria anaitwa Onyinye Ndidi ni beki fulani mjanja mjanja mwenye bao moja. Yule Mghana Bennard Kumordzi ni beki. Wachezaji hao wameshazoea mazingira kwenye kikosi hicho na huenda wakawa msaada mkubwa kwa Mbwana Samatta ambaye jana Ijumaa alitaraji kufanyiwa vipimo vya afya pamoja na TP Mazembe kumalizana na Genk.

TP Mazembe jana ilikuwa kwenye mishemishe za kumalizana na Genk na kupokea dau lao la zaidi ya Sh.1.8 bilioni ambapo Simba wanasubiri mgao wao kutoka hapo. Klabu ya Genk  baada ya kushiriki Ligi ya Mabingwa mwaka 2012 iliwauza kipa wa sasa wa Chelsea, Thibaut Courtois na  Kevin De Bruyne ambaye pia alienda Chelsea kabla ya kutua Man City. Ilimuuza pia Christian Benteke kwa Aston Villa, sasa yuko Liverpool.


Helkopta ya TANAPA Yaangushwa na Majangili ikiwa Katika Doria

$
0
0

Watu wanaodaiwa kuwa ni majangili na wawindaji haramu wameitungua kwa risasi helkopta ya doria ya wanyamapori katika pori la akiba la maswa lililoko wilaya ya Meatu mkoani Simiyu kusini mwa hifadhi ya taifa ya Serengeti na kumuua rubani wa helkopita na kumjeruhi askari mmoja wa wanayamapori.

Kufuatia tukio hilo, waziri wa maliasili na utalii Profesa Jumanne Maghembe amefika katika eneo la tukio na kusisitiza kwamba serikali kwa kushirikiana na vyombo vyote vya dola na vyombo vya ulinzi na usalama inaanzisha mkakati mpya wa kupambana na ujangili na uwindaji haramu wa maliasili ikiwemo Tembo ambao ni rasilimali muhimu kwa taifa na kwa uhifadhi wa taifa la Tanzania.

Waziri Maghembe ambae amefika kwenye eneo hilo ilipotunguliwa helkopita hiyo katika safari iliyokuwa na msukosuko mingi ya barabara na hasa kipindi hiki cha mvua na kuikuta helkopita iliyokuwa inarushwa na kepten Roger Gower raia wa Uingereza ambae alifariki baada ya kujeruhiwa kwa risasi amesema tukio hilo limewakera wadau wote wa uhifadhi na serikali kwa ujumla na kamwe haliwezi kuachwa lipite bila hatua madhubuti kuchukuliwa huku akiwaonya baadhi ya watumishi wa serikali na askari wa wanyamapori wanaoshirikiana na wahalifu kuwa sasa kiama chao kimefika.

Nae kamanda wa upelelezi wa mkoa wa Simiyu Jonathan Shana amesema tukio hilo lilitokea jana jioni wakati helkopita hiyo ikiwa katika doria baada ya kusikika milio ya risasi ya majangili katika pori hilo ambapo Tembo watatu waliuwawa na kwamba watu watatu wanashikiliwa na polisi wakihojiwa kufuatia tukio hilo ambapo mkurugenzi mkuu shirika la hifadhi za taifa Tanzania Tanapa Allan Kijazi amesisistiza umuhimu wa wadau kuongeza nguvu katika kukabiliana na matatizo ya ujangili nchini.




Wakazi Ubungo Walalamika Kuhusu Mbunge Wao Wadai Kazi yake ni Kugombana na Kina Zitto na Makonda

$
0
0

Ndugu zangu wana JF kama kuna wabunge majipu basi mbunge wangu wa Ubungo Mh Kubenea ni jipu na linaitaji kupasuliwa.

Naamini wana Ubungo mtakubaliana na mimi kuwa kwa miaka hii mitano tumekula shoti kama sio loss.

Ubungo maji kwa wiki yanayoka mara moja wakati mwingine yanaweza yasitoke kabisa, Ubungo imejaa vibaka yani ukisahau jeans yako nje ndo nitolee, Ubungo wafanyabiashara ndogo ndogo wanapata shida, Ubungo barabara za ndani hazipitiki, Ubungo kuna kila aina ya matatizo.

Cha kushangaza tangu tumchague Kubenea sijasikia akiongelea matatizo ya Ubungo zaidi ya kupambana na Zitto , Makonda na wengine katika magazeti yake.

Mbunge huyu ata akichangia bungeni ni pumba tupu Ubungo tumezoea wabunge wenye uwezo wa kujenga hoja sio huyu Kubenea pamoja na kwamba Mnyika hakufanya makubwa sana ila afadhari yeye alikuwa ni mbunge wa kitaifa zaidi hakuna ubishi wanaubungo kwa Kubenea tumekula loss.

Source: Jamii Forums

Stori ya Mwigizaji Stallone Rambo Iliyowagusa Wengi..Kabla ya Kutoka Hakuwa na Pakulala..Isome Hapa

$
0
0

This is one of the SADDEST stories ever told in Hollywood. His name is Sylvestar Stallone. One of the BIGGEST and Most famous American Movie superstars. Back in the day, Stallone was a
struggling actor in every definition. At some point, he got so broke that he stole his wife's jewellery and sold it. Things got so bad that he even ended up homeless. Yes, he slept at the New York bus station for 3 days. Unable to pay rent or afford food. His lowest point came when he tried to sell his dog at the liquor store to any
stranger. He didn't have money to feed the dog anymore. He sold it at $25 only. He says he walked away crying.

Two weeks later,he saw a boxing match between Mohammed Ali and Chuck Wepner and that match gave him the inspiration to write the script for the famous movie,ROCKY. He wrote the script for 20 hours! He tried to sell it and got an offer for $125,000 for the script. But he had just ONE REQUEST. He wanted to STAR in
the movie. He wanted to be the MAIN ACTOR. Rocky himself. But the studio said NO. They wanted a REAL STAR.

They said he "Looked funny and talked funny". He left with his script. A few weeks later,the studio offered him $250,000 for the script. He refused. They even offered $350,000. He still refused. They wanted his movie. But NOT him. He said NO. He had to be
IN THAT MOVIE.

After a while,the studio agreed,gave him $35,000 for the script and let him star in it! The rest is history! The movie won Best Picture, Best Directing and Best Film Editing at the prestigious
Oscar Awards. He was even nominated for BEST ACTOR! The Movie ROCKY was even inducted into the American National Film Registry as one of the greatest movies ever!

And do You know the first thing he bought with the $35,000? THE DOG HE SOLD. Yes,Stallone LOVED HIS DOG SO MUCH that he stood at the liquor store for 3 days waiting for the man he sold
his dog to. And on the 3rd day,he saw the man coming with the dog. Stallone explained why he sold the dog and begged for the dog back. The man refused. Stallone offered him $100. The
man refused. He offered him $500. And the guy refused. Yes,he refused even $1000. And,Believe it or Not,Stallone had to pay $15,000 for the same,same dog he sold at $25 only! And he
finally got his dog back!

And today,the same Stallone who slept in the streets and sold his dog JUST BECAUSE he couldn't even feed it anymore,is one of the GREATEST Movie Stars who ever walked the Earth!

Being broke is BAD. Really BAD. Have You ever had a dream? A wonderful dream? But You are too broke to implement it? Too tiny to do it? Too small to accomplish it? Damn! I've been there too many times!

Life is tough. Opportunities will pass you by,just because you are a
NOBODY. People will want your products but NOT YOU. Its a tough
world. If you ain't already famous, or rich or "connected", You will find it rough.

Doors will be shut on You. People will steal your glory and crush your hopes. You will push and push. And yet NOTHING WILL HAPPEN.

And then your hopes will be crushed. You will be broke. Damn broke. You will do odd jobs for survival. You will be unable to feed yourself. And Yes, you may end up sleeping in the streets.
It happens. Yes, it does.

BUT NEVER LET THEM CRUSH THAT DREAM. Whatever happens to
You, Keep Dreaming. Even when they crush your hopes, Keep Dreaming. Even when they turn you away, Keep Dreaming.
Even when they shut you down, Keep Dreaming.

NO ONE KNOWS WHAT YOU ARE CAPABLE OF EXCEPT YOURSELF! People will judge You by HOW you look. And by WHAT You have.
But please, Fight on! Fight for Your place in history. Fight for your glory. NEVER EVER GIVE UP!

Even if it means selling all your clothes and sleeping with the dogs, ITS OKAY! But AS LONG AS YOU ARE STILL ALIVE, Your STORY IS NOT OVER. TRUST ME.

Keep Up the Fight. Keep your dreams and hope alive. Go great .

Like and share if inspired. Lovely day people!

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Januari 31, Ikiwemo ya Dr Slaa Kukimbilia Canada

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Januari 31, Ikiwemo ya Dr Slaa Kukimbilia Canada

Hii Ndio Sababu ya Rais Magufuli Kumuongezea Mwaka Mmoja Mkuu wa Majeshi Jenerali David Mwamunyange..

$
0
0
RAIS John Magufuli amemwongeza muda wa mwaka mmoja Mkuu wa  majeshi ya ulinzi nchini,Jenerali David Mwamunyange, ambaye alitakiwa kustaafu leo baada ya kutimiza umri  kwa mujibu wa katiba na sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mapema kwenye Makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyopo  Upanga jijini Dar es salaam,Jenerali Mwamunyange amesema leo alitakiwa kuungana na Brigedia wanne wa Jeshi la ulinzi nchini  pamoja na Meneja Jenerali  wawili  ambapo wote kwa  pamoja wamestaafu ndani ya Jeshi kwa mujibu wa sheria ya jeshi hilo.

“Mimi mwenyewe ilikuwa nistaafu kazi leo tarehe 30 Januari 2016,lakini Rais na Amri Jeshi mkuu ameamua kunibakiza katika utumishi jeshini kwa mwaka mmoja kuazia leo tarehe 30 januari,2016 hadi tarehe  31 Januari 2017,” amesema Jenerali Mwamunyange

Jeneral Mwamunyage amesema sababu iliyomfanya Rais Magufuli kumwongezea mda huo imetokana na Rais kutopata mtu sahihi wa kujaza nafasi hiyo aliyonayo .

Hata hivyo, Jenerali Mwamunyange amesema Rais Magufuli amemteua  Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa mnadhimu mkuu wa Jeshi la ulinzi la wananchi.

Balozi Amina Salum Ali Amuomba Seif Sharif Hamad Kufikiria Upya Uamuzi Wa Kususia Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar

$
0
0
Balozi Amina Salum Ali
Kada aliyegombea urais kwa tiketi ya CCM, Amina Salum Ali amesema mgogoro wa kisiasa Zanzibar hautakwisha hata baada ya Uchaguzi wa marudio kwa kuwa ni wa kihistoria na baadhi ya viongozi hawana nia ya dhati ya kuendeleza Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) visiwani humo.

Balozi Amina pia amesema uamuzi wa CUF kususia uchaguzi wa marudio visiwani humo utasababisha mpasuko mkubwa zaidi na kumtaka katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kufikiria upya na kubadili msimamo huo kwa faida ya Wazanzibari wote.

Zanzibar imekuwa ikikumbwa na mgogoro wa kisiasa kila inapoingia kwenye Uchaguzi Mkuu kuanzia mwaka 1995 baada ya vyama vya upinzani kuruhusiwa, na vurugu za mwaka 2005 zililazimisha CUF na CCM kuingia kwenye mazungumzo yaliyozaa SUK.

Lakini dalili za SUK kuendelea sasa zinaonekana kufifia baada ya CUF kupinga uamuzi wa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha wa kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais wa, wawakilishi na madiwani visiwani humo Oktoba 28, mwaka jana na kutangaza uchaguzi mpya Machi 20, ambao chama hicho kikuu cha upinzani kimesema hakitashiriki.

Balozi Amina anaona kuyumba kwa Serikali hiyo ya umoja wa kitaifa kunatokana na Maalim Seif kutotambua kuwa maridhiano hutokana na kupata kitu fulani na wakati huohuo kukubali kupoteza kingine.

“Mimi namshauri Seif kujua kuwa katika uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, afahamu kuwa Tanzania itajengwa na Watanzania na kwa upande wa Zanzibar, Wazanzibari wanataka maendeleo,” alisema.

“Seif analalamika wakati yuko serikalini, anakutana na mwenzake (Dk Shein) wanakula haluwa na kufurahi pamoja, lakini akitoka nje, anageuka. Tutafika wapi kwa siasa za namna hii?”

Amina alisema Zanzibar ilikuwa na bahati kumpata Dk Shein ambaye Maalim Seif angeweza kumtumia kufanya mambo anayotaka, lakini ameshindwa kugundua fursa hiyo na kuanza kujivuruga.

“Chini ya Dk Shein, Zanzibar imepata fursa nzuri ya kufikia maelewano. Shein anawawakilisha Wazanzibari wote na anajua siasa za Zanzibar ni mstahamilivu, ni mwenye busara, msomi na mpenda maendeleo,” alisema Balozi Amina na kuongeza kuwa:

“Hivyo huu ulikuwa wakati mzuri kwa Seif kushirikiana wafanye anachotaka kwa ajili ya maendeleo ya Wazanzibari.”

Alisema kitendo cha CUF kususia uchaguzi wa marudio kitaongeza mpasuko wa kisiasa badala ya kuupunguza, hivyo ni vyema Seif akaliangalia hilo vizuri na kubadili msimamo huo kwa faida ya Wazanzibari wote.

“Uchaguzi huu wa marudio ndio utakuwa kipimo cha kuonyesha nani anakubalika Zanzibar sasa Seif akisusa maana yake nini?” alihoji.

Mkoa wa Dar es Salaam Sasa Kuwa na Wilaya Tano

$
0
0
RAIS Dk. John Magufuli ameidhinisha kuwepo kwa wilaya tano katika jiji la Dar es Salaam, badala ya tatu zilizokuwepo awali, ili kuleta maendeleo ya haraka hususan katika elimu. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, alisema jana kuwa, waliwasilisha ombi la ugawaji wa wilaya za Kinondoni na Temeke kwa rais, ambapo ameshaliidhinisha.

“Hatua hii ya kuwepo kwa wilaya tano italiwezesha jiji la Dar es Salaam, kupata maendeleo ya haraka kwa kugawanywa kwa wilaya hizo, ambapo kutakuwa na usimamizi thabiti na hakutakuwa na kisingizio cha kuelemewa kwa majukumu kwa watendaji,”alisema.

Aliomba katika ugawaji wa wilaya hizo, rasilimali zilizopo na mipaka igawanywe kwa manufaa ya wananchi wa wilaya hizo. Aidha, alisema kinachosubiriwa ni ugawaji wa mipaka na kutangazwa rasmi kuongezeka wilaya mbili ya Kigamboni na Ubungo na kufikisha idadi ya wilaya tano katika jiji la Dar es Salaam.

Kutokana na kuongezeka kwa wilaya, Sadiki aliwataka watendaji wake kuwa waadilifu katika ugawaji wa mipaka na rasilimali zilizopo ili kuleta maendeleo yaliyokusudiwa.

Akizungumzia ombi la ugawaji wa wilaya za Kinondoni na Temeke, Sadiki alisema hadi kufi kia jana, ombi hilo lilishaidhinishwa na rais, hivyo Kinondoni itakuwa na wilaya mbili za Kinondoni na Ubongo huku wilaya ya Temeke ikiwa na wilaya za Temeke na Kigamboni.

Source:JPM ARIDHIA WILAYA ZA UBUNGO NA KIGAMBONI | Uhuru

Maswali Muhimu ya kujiuleza kwa yeyote anayeweza kutoa ufafanuzi:
1. Je ni kweli kuongeza wilaya kutaleta maendeleo ya haraka? Vipi kuhusu gharama za uendeshaji zitakazotokana na kuongeza watendaji na kujenga makao makuu ya wilaya?
2. Je ni kweli usimamizi thabiti hautakuwa na kisingizio?
3. Vipi kuhusu mipaka?
4. Vipi kuhusu mabaraza ya Madiwani?

Source;Uhuru

Diamond Aombwa Kufanya Kazi na Mume wa Alicia Keyz, Swizz Beatz, Kwenda Marekani Kushoot Video ya Collabo na Ne-Yo

$
0
0
Mwaka jana (2015) tulishuhudia producer na rapper Swizz Beatz wa Marekani ambaye ni mume wa muimbaji wa RnB, Alicia Keyz walidhihirisha hadharani kuwa wao ni mashabiki wa kazi za Diamond Platnumz kwa kupost video wakiwa wanasikiliza nyimbo zake (Ingia hapa).

Hiyo ilikuwa ni dalili kwamba kuna siku Swizz Beatz na Diamond wanaweza kuja kufanya kazi endapo itatokea wamekutana. Lakini kabla hata hawajakutana tayari mtayarishaji huyo ameonesha nia ya kutaka kufanya kazi na Simba.

Diamond amesema kuwa Swizz alimtafuta hivi karibuni na kumwambia inabidi wafanye kazi,

“Kuna Collabo na watu wengi sana Kwa mfano kama juzi kati nafikiri, kama siku tatu nyuma hivi Swizz alinicheki akaniambia itabidi tufanye kazi, nikamwambia sawa, na tuko tunaplan,” alisema Diamond kupitia Ayo TV.

Katika maelezo yake Diamond pia ameweka wazi kuwa anampango wa kwenda Marekani kushoot video ya collabo yake na Ne-Yo mwezi wa tatu, na alimwambia Swizz kuwa atakapokwenda kwaajili ya video hiyo ndio anafikiria wafanye kazi pia.

“Nikamwambia mimi nakuja Marekani nafikiri mwezi wa tatu kama sijakosea, au before mwezi wa tatu, kwasababu kushoot video yangu niliyofanya na Neyo, ndio tunaenda kushoot video, nikamwambia nikija ndio itakuwa time nzuri tunafanya hapo hapo”.

Katika collabo hiyo Platnumz amesema pia ana mpango wa kumuomba Alicia Keyz aimbe kiitikio kwenye collabo hiyo na Swizz.

Katika hatua nyingine, Diamond amesema kuwa ana collabo nyingine na msanii wa Marekani ambaye hata hivyo hakupenda kumtaja kwa sasa.

Source;Bongo5

Msanii wa Muziki Niki wa Pili Aikosoa Serikali Kuhusu Kuzuia Bunge Kurushwa Laivu

$
0
0
Msanii wa muziki wa bongo kutoka katika kundi la Weusi, Niki wa pili amefunguka na kusema kuwa serikali kabla ya kufanya maamuzi ya kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya bunge kurushwa kupitia Televisheni ya taifa walipaswa kwanza kuwauliza wananchi.

Niki wa Pili amesema hayo kupitia Account yake ta Twitter baada ya serikali kuweka msimamo wake kuwa wamefanya hivyo kwa lengo la kupunguza gharama za urushaji wa matangazo hayo.
Niki wa pili ameeleza kuwa sababu nyingine iliyotolewa na serikali kuwa watu wengi huwa hawapati muda wa kuangalia shughuli za bunge si za kweli kwani watu huwa wanapata muda wa kufuatilia bunge hilo.

“Sisi walipa kodi ndio tungeulizwa kwanza, je kwa hizi gharama tuoneshwe bunge au hapana…mbona makampeni pia yalikuwa gharama kubwa, Bunge huwa linaangaliwa sana, sehemu nyingi unakuta wame tune…so wangetafuta matangazo ya biashara ku cover gharama hizo” Alisema Niki wa Pili.

Jana serikali kupitia kwa waziri Nape Nnauye ilitoa taarifa ya kuzuia bunge kurushwa live kupitia Televisheni ya taifa na badala yake walisema bunge litakuwa linarekodiwa na kurushwa kwenye kipindi maalum kupitia televisheni hiyo ya taifa kuanzia saa nne usiku mpaka saa tano za usiku, na kusema kuwa kipindi cha maswali na majibu tu ndio kitakuwa kinarushwa live jambo ambalo limepokea tofauti na watu huku wengi wao wakionesha kutofurahishwa na maamuzi hayo ya serikali.

Habari Njema Kwa Timu ya KRC Genk Siku Moja Baada ya Kumsajili Mbwana Samatta....

$
0
0
Siku moja baada ya klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji imsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa anaichezea klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta, January 30 ilishuka dimbani ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani Cristal Arena kuikabili klabu ya Kortrijk.

Licha ya kuwa Samatta hakuwa kwenye kikosi, kwa sababu hakufanya mazoezi na timu, KRC Genk imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na mshambuliaji mwenye asili ya Zaire Christian Kabasele dakika ya 21, hizi ni taarifa na mapokezi mema kwa Samatta ambaye ndio kwanza ametua Ubelgiji kuanza maisha yake ya soka.

Jaji Bomani Anena...Tume ya Uchaguzi (ZEC) Imejipotezea Imani Kwa Wananchi Kwa Kufuta Uchaguzi Bila Sababu za Msingi

$
0
0
Mwanasheria Mkuu mstaafu nchini, Jaji Mark Bomani amesema kitendo cha Tume ya Uchaguzi (ZEC) kutangaza marudio ya uchaguzi wa rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani, kumepunguza imani ya wananchi kwa chombo hicho. Bomani pia amesema huenda uamuzi wa kutangaza kurudiwa kwa uchaguzi huo Machi 20, hakikuishirikisha tume hiyo na hivyo lawama zinapaswa kuelekezwa kwa mwenyekiti wake, Jecha Salim Jecha.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake jana, Bomani alisema anahisi huenda uamuzi wa kufuta uchaguzi huo na kisha kutangaza tarehe mpya, haukuishirikisha ZEC.

“Hizo dosari hazikuwekwa kinagaubaga hii inaacha maswali mengi kuliko majibu,” alisema mtaalamu huyo wa katiba. “Yeye ndiye alifuta na leo ametangaza, je hizo dosari ameshatangaza kwamba zimerekebishwa?”

Bomani alisema kwa namna uamuzi wa kufuta uchaguzi huo ulivyofanywa, inaonyesha dhahiri kuwa maofisa wengine wa ZEC hawakushiriki, hivyo si sawa kutangaza marudio ya uchaguzi huo.

“Kufuta matokeo ya uchaguzi bila ya maelezo yanayoridhisha au bila ya ushahidi kunaonyesha uamuzi huo haukutokana na tume. Ni kama uamuzi wake Jecha kwa hiyo haitoshi yeye pekee kutangaza uchaguzi unarudiwa maana haitakuwepo imani,” alisema.

Hata hivyo, alisema ili kutatua mgogoro wa Zanzibar njia pekee ni kuunda jopo la watu wachache wanaoheshimika chini ya uenyekiti wa mmoja wa majaji wakuu mstaafu nchini, ili wazingalie dosari za kufuta uchaguzi huo endapo zilikuwepo na kisha kutoa maoni au ushauri.

Kuhusu mchakato uliosimama wa kuandika Katiba mpya, Bomani alisema suala hilo ni zito na linapaswa kushughulikiwa baada ya Serikali ya Zanzibar kupatikana na si kuachwa hewani.

Alisisitiza kuwa suala hilo linapaswa lifanywe kwa umakini kwa kuwa baadhi ya mapendekezo ya Katiba mpya tayari yalishafanyiwa kazi na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba na Bunge Maalumu la Katiba (BMK).

Kuhusu serikali ya Rais John Magufuli, mwanasheria huyo alimpongeza kiongozi huyo wa nchi kwa jitihada za kupambana na rushwa na ufisadi na kumshauri arekebishe mfumo wake serikalini ili uweze kwenda na kasi yake.

Chanzo:Mwananchi
Viewing all 104706 articles
Browse latest View live




Latest Images