Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Mpoto Asimulia Alivyonusurika Kipondo Kutoka kwa Wabongo wa UK

$
0
0
Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto ameeleza jinsi alivyochezewa faulo na waandaji wa onesho lake nchini Uingereza kwa kuanza kutambulisha onesho lake jukwaani kwa kucheza wimbo wa Taifa wa Kenya.

Akizungumza katika kipindi cha Papaso cha TBC FM Jumatano hii, Mrisho Mpoto alisema hali hiyo iliwafanya watanzania waliohudhuria onesho hilo kumvamia nyuma ya jukwaa na kutaka kujua kwanini alifanya hivyo.

“Mimi nakumbuka niliwahi kuchaguliwa na Kenya ili kujumuika na wasanii wengine wa Uganda na Kenya kufanya onesho la Global Shakespeare,” alisema Mpoto.

“Kuna mwandishi duniani anaitwa William Spears aliteua vitabu vyake 42 vitafsiriwe katika lugha mbalimbali duniani kikiwemo Kiswahili. Vile vitabu baada ya kutafsiriwa akasema vikachezwe kwa lugha zao. Kwahiyo ile kazi walipewa Wakenya, Kenya walivyopata ile tenda wakasema tufanye ‘East African Project’ au mradi wa Afrika Mashariki.

Niliambiwa kwamba tunafanya project ya Afrika Mashariki na nikaoneshwa barua ya kwamba wale ‘Global Shakespeare’ kutoka London wamerecommend kwamba katika kazi hii mtu anayeitwa Mrisho Mpoto asikose. Kwahiyo wale waliniomba mimi nikafanye ile project kama mhusika mkuu ambae ni full staff. Kwahiyo mimi nikaingia mkataba na kampuni ya Kenya theater kama mwakilishi kutoka Tanzania, pia wawakilishi wengine kutoka katika mataifa ya Afrika alisaini mkataba na wote tukafanya mazoezi kwa miezi mitatu nchini Kenya,” alisema.

Aliendelea, “Tulipokuwa London kwenye show yetu ya kwanza ambayo ilihudhuriwa na watu wa mataifa mbalimbali pamoja na watanzania, sisi tukiwa back stage tukiwa tunajiandaa kwa ajili ya kuingia jukwaani kuanza kuigiza kitabu, mimi ni mhusika mkuu ambaye naingia baada ya onesho kuanza. Kwahiyo wale watu waliotangulia kabla ya kuanza mchezo lazima utaimbwa wimbo wa taifa. Kwahiyo katika kuimba wimbo wa taifa, uliimbwa wimbo wa taifa la Kenya na asilimia 90% ya watu walikuwa Wakenya. Kwahiyo baada ya wimbo wa taifa mchezo unatakiwa kuanza, kwahiyo nichague mawili, nisiingie jukwaani au niingie jukwaani kwa sababu ya mkataba halafu nije nihoji kwanini walinifanyia hivyo?@

“Kwahiyo baada ya mchezo watanzania wanaoishi Uingereza wakaja back stage, wakawa wakali wakanikunja na kutaka kunipiga. Lakini bahati nzuri polisi wakaja wakazuia, watu wakawa wamekasirika sana kwanini naimba wimbo wa Kenya wakati mimi ni Mtanzania? Lakini nashukuru Mungu niliongea mpaka kwenye BBC pia tukaenda ukabozi wa Tanzania, nikawaambia hapana mimi nilichezewa faulo, sikuwa na nia hiyo.”

Polisi Yasusia Maiti ya Polisi Aliyeuawa Akifanya Ujambazi...Yaidai Amelidhalilisha Jeshi

$
0
0
Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi limesusa kusafirisha mwili wa askari polisi, Konstebo Nobart Chacha (25) ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi kifuani wakati akifanya ujambazi.

Kwa mujibu wa habari zilipatikana, jukumu la kusafirisha mwili wa marehermu huyo limechukuliwa na marafiki wa chama cha watu wanaotoka mkoani Mara wambao wanaishi Mkoa wa Katavi.

Mmoja wa wajumbe katika chama hicho, Julius Marwa alisema kuwa wamelazimika kusafirisha mwili wa marehemu baada ya polisi kukataa kusafirisha na kushiriki mazishi kwa madai kuwa kitendo alichofanya askari huyo tayari amejifukuzisha kazi.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, alisema kwa taratibu za kijeshi mwili wake haustahili kupewa heshima yoyote, ikiwa pamoja na kusafirishwa kwa kuwa tayari amejifukuzisha kazi kwa aibu na fedheha kubwa.

Askari Polisi huyo wa kituo cha polisi wilaya ya Mpanda, aliuawa juzi usiku akiwa katika harakati za kufanya ujambazi nyumbani kwa mfanyabiashara wa madini, Daniel John katika kijiji cha Ibindi  kilichopo Kata ya Machimboni, Wilayani Mlele.

Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Machimboni, Raphael Kalinga, askari huyo akiwa na kundi la wenzake ambao idadi yao hakufahamika mara moja, walifika kijijini hapo kwa lengo la kumvamia na kumpora kwa kutumia silaha mfanya biashara huyo wa Madini ya dhahabu na mashine za kusaga.

Inadaiwa kuwa majambazi hao walivunja mlango kuingia ndani ya nyumba hiyo yakimwamuru mfanyabiashara huyo kukaa kimya, lakini hakutii agizo hilo ambapo alichukua bunduki yake na kufyatua risasi ambayo ilimpiga askari huyo kifuani na mgongoni na kufa hapo hapo.

Source; Muugwana Blog

Namshukuru Mungu kwa Mara ya Kwanza Nimepata ‘Comments’ Nzuri-Faiza Ally

$
0
0
Staa wa Bongo Movies na mkali wa ‘baby mama drama’ , Faiza Ally amemshukuru Mugu baada ya mashabiki wengi kumuandikia comment nzuri mtandaoni kwa posti yake akiwa amevalia ‘kidenti’ akiwa kwenye studio za EATV usiku wa jana tofauti na posti zake za nyuma.

Nachukua nafasi hii kumshukuru M.Mungu mwingi wa rehma kwa kuwa naona kwa mara ya kwanza katika comment zaidi ya mia 300 zote ni nzuri kasoro 3 kwa mimi ni kitu kikubwa maana kwenye maisha yangu mara nyingi nimekua mtu wa kujajiwa na kutukanwa kwa sababu tu nimechagua kuwa tofauti…

All in all inaonyesha jinsi gani watu ni rahisi kukujaji na inachukua muda kukuelewa na sasa naona baazi ya watu wanaanza kunielewa na asante wote mnao chukua muda kunisoma na zaidi wale wanao niambia….ninacho waahidi wale walio nikubali wala hawajapotea kabisa na kuna faida nyingi kupitia maisha yangu – na katika kipindi changu kuna mengi ya kujifunza kupitia maisha yangu …. Kitakua kipindi kizuri chenye uhalisia na kitakacho kufanya ujisikie uhuru kwenye maisha yako…

Na kukubali hali yako na kufurahia maisha kwa uwezo wako na zaidi vitu muhimu kuzingatia katika maisha yako ikiwemo kufanya vitu vinavyo kupa furaha bila kujali watu … Maana walio wengi hata ukimuuliza anapenda nini hajui…na pia kuna vitu muhimu vya kuzingatia kuliko kuishi kwa ajili ya macho ya watu… Na bila kusahau huwezi kukubalika kwa watu na si lazima maana tumeumbwa tofauti na uwezo wetu wa kutambua haufanani kiufupi ni kuishi huru bila kumzuru mtu wala kuvunja sheria za nchi na kufanya yalio muhimu tu….NAWAPENDA WOTE

Hivi Ndivyo Edward Lowassa Anavyoishi Kama Rais nje ya Ikulu...

$
0
0
Edward Lowassa
Licha ya kutotangazwa mshindi wa urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana, aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, amekuwa na ratiba zinazofanana kwa kiasi fulani na Rais John Magufuli, imefahamika.

Kwa mujibu wa matangazo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Lowassa aliyekuwa akichuana kwa karibu na Magufuli katika muda wote wa kampeni za miezi miwili zilizoanza Agosti 21, 2015, alishika nafasi ya pili baada ya kupata asilimia 39.97 ya kura zote halali zilizopigwa.

Magufuli aliibuka mshindi baada ya kupata asilimia 58.46 ya kura hizo na aliapishwa Novemba 5, 2015 kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tangu wakati huo ameendelea kusimamia mabadiliko kadhaa katika serikali yake ya awamu ya tano.

Hata hivyo, Nipashe imebaini kuwa licha ya Lowassa kutotangazwa mshindi na kuingia Ikulu, mgombea huyo wa urais wa mwaka jana amekuwa na mwenendo wa matukio yanayofanana kwa kiasi kikubwa na ya kiongozi dola.

Lowassa alipinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu akidai alipokwa ushindi na NEC kwavile takwimu zake zinaonyesha alipata asilimia 60 ya kura zote halali.

Katika uchunguzi wake huo uliohusisha baadhi tu ya matukio, Nipasahe imebaini kuwa Lowassa ameendelea kufanya hafla na matukio makubwa kama Rais licha ya kuwa kwake nje ya Ikulu.

“Bungeni kuna mawaziri kivuli… na sasa Lowassa ni kama Rais Kivuli kwa sababu baadhi ya matukio huhusika akiwa kama kiongozi mmoja mkubwa katika nchi,“ mmjoja wa wachambuzi aliiambia Nipashe kwa sharti la kutotajwa jina.

Kadhalika, katika uchunguzi wake, Nipashe imebaini kuwa baadhi ya matukio yanayomfanya Lowassa aishi kama rais nje ya ikulu ni kukutana kwake na wafanyabiashara, kualikwa kama mgeni rasmi na kukutana na Balozi wa Japan.

Pia amewafunda mameya na wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wanachi (Ukawa), mwamvuli wa kisiasa ambao Chadema ni mwanachama wake, kwa kuwapa onyo kuwa wasipotimiza ndoto za wananchi watachukuliwa hatua. Mambo hayo, yamefanywa pia kwa nyakati tofauti na Rais John Magufuli.

ATETA NA MAALIM SEIF
Novemba 13, mwaka jana Lowassa alikutana na aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad na kujadiliana naye juu ya mkwamo wa kisiasa wa Zanzibar miongoni mwa masuala mbalimbali.

Lowassa alifanya hivyo baada ya Maalim Seif, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, kumtembelea kwenye ofisi zake binafsi zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Kadhalika, Januari 24 Lowassa alikutana na Maalim Seif kwa mara nyingine tena mjini Dodoma na kujadili masuala ya Zanzibar, kabla wote kwa pamoja hawajakutana na wabunge wa Ukawa kutoka Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi.

Rais Magufuli aliwahi pia kukutana na Maalim Seif, Ikulu jijini Dar es Salaam na kujadiliana naye masuala kadhaa kuhusiana na hatma ya Zanzibar baada ya kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa visiwa hivyo. Kikao hicho cha Rais Magufuli na Malim Seif kilifanyika Desemba 21, mwaka jana.

AMTEMBELEA SUMAYE MUHIMBILI
Januari 11 , Rais Magufuli alifanya ziara ya kwenda kumjulia hali Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Siku mbili baadaye, yaani Januari 13, Lowassa alifanya hivyo pia, akienda kumtembelea Sumaye ambaye walikuwa naye bega kwa bega katika uchaguzi mkuu uliopita baada ya kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kutua Chadema kama alivyofanya Lowassa.

APOKEWA KWA KISHINDO NA WAKAZI DAKAWA
Januari 24 Lowassa aliyekuwa njiani kuelekea Dodoma, alikutana kwa muda na wananchi waliomsimamisha barabarani katika eneo la Dakawa mkoani Morogoro.

Lowassa alizungumza kwa muda na wananchi hao na kushangiliwa kwa nguvu kabla ya kuendelea na safari yake.
Lowassa alifanya hivyo ikiwa ni siku mbili tu zimepita (Januari 21, 2016) tangu Rais Magufuli apokewe pia kwa kishindo na wakazi wa Arusha wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.

Mamia ya wananchi walijitokeza kumsikiliza Rais Magufuli aliyekuwa amevalia magwanda ya kijeshi.    

AFUNDA MAMEYA UKAWA DAR
Januari 18, Lowassa alikutana na mameya wanaotoka Ukawa wa Manispaa za Ilala na Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuzungumza nao masuala kadhaa kabla ya kuwaonya kuwa watatimuliwa iwapo hawatatimiza lengo la kuwatumikia wananchi kwa namna inayotarajiwa, ikiwamo kuinua mapato, kuboresha usafi, kukomesha ubadhirifu kwenye manispaa zao na pia kushughulikia kero ya foleni jijini humo.

Tukio linalofanana na hilo limefanywa mara kadhaa na Rais Magufuli, ikiwamo Novemba 7, mwaka jana wakati alipokutana na makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu ambao aliwapa maelekezo ya kazi huku akiwaonya kuwa atakayeshindwa kwenda na kasi katika kushughulikia kero za wananchi hataachwa.

AKUTANA NA BALOZI WA JAPAN
Januari 18, Lowassa alikutana na Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida wakati wa kusaini mikataba ya miradi mitatu yenye thamani ya Dola 204,300 kwa ajili kusaidia Shule ya Kingolwira, Morogoro, Shule ya Muyuni na Kituo cha Afya cha Lutheran kilichopo Arusha.

Rais Magufuli, kwa nafasi yake, ameshakutana pia na mabalozi kadhaa ikiwamo Novemba 30, mwaka jana wakati alipokutana na mabalozi wa China na Korea.

AKUTANA NA WAFANYABIASHARA
Januari 14, Lowassa alitembelewa ofisini kwake, Mikocheni na wafanyabiashara kadhaa wa Kariakoo jijini Dar es Salaam na kuzungumzia nao masuala mbalimbali.

Tukio kama hilo limewahi pia kufanywa na Rais Magufuli Desemba 3, mwaka jana wakati wa mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara, alipokutana Ikulu na wafanyabiashara wakubwa na kubadilishana nao mawazo.

WASEMAVYO ZAIDI WACHAMBUZI SIASA
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, akizungumza na Nipashe, alisema Lowassa ni mwanasiasa mahiri, aliyebobea na anayejua anachokifanya.
Alisema anajitajidi asisahaulike kwenye ramani ya siasa na nyoyo za Watanzania.

"Kwa sasa hana nafasi ndani ya Chadema zaidi ya kutambulika aliyekuwa mgombea urais ambayo siyo nafasi rasmi ilishaisha wakati wauchaguzi mkuu, haendi bungeni, haudhurii vikao vya madiwani labda aalikwe Monduli, atajulikanaje anachofanya ndiyo maana atafuta fursa na nafasi ili aendelee kuwepo ndani ya mioyo ya watanzania," alisema.

Aidha, aliishauri Chadema kuangalia namna ya kumpa wadhifa ndani ya chama hicho ili awe na shughuli za kila siku za kichama na kwamba kama ana nia ya kuimarisha upinzani nchini kwa kutumia nafasi hiyo, atafanya mambo mengi.

Alisema baada ya chama hicho kumpoteza aliyekuwa Katibu Mkuu, Dk. Willbriad Slaa, sasa wanahitaji mtu mwenye mbinu na mikakati kama Lowassa awepo ndani ya uongozi na kufanya shughuli za kila siku.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa, alisema Lowassa ni mwanasiasa wa upinzani na hivyo ana hiari ya kuendelea na shughuli za siasa za kuimarisha chama chake na nyinginezo, hivyo haoni kama kuna tatizo juu ya kile anachokifanya hasa kwa kutambua vilevile kuwa ni waziri mkuu mstaafu.

“Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu, Lowassa amekuwa kimya hajafanya chochote kikubwa ukilinganisha na wanasiasa wa nchi jirani kama Kenya (Raila Odinga).

Amekuwa akifanya mikutano ya hadhara na shughuli nyinginezo," alibainisha na kuongeza:
"Anachofanya Lowassa ni siasa za kawaida. Lazima akutane na wapiga kura na makundi mbalimbali ikiwa kuiwashukuru wapigakura.”

Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwesiga Baregu, alisema anachofanya Lowassa ni kwa sababu anatambua nafasi yake katika jamii kuwa ana wafuasi wake na wa Ukawa ambao wanamhitaji hivyo ni lazima akutane nao.

“Ni mapema sana kwa sababu mwezi Oktoba mwaka jana, uchaguzi umemalizika hadi sasa tupo kwenye kipindi cha mpito. Kulikuwa na nia ya Ukawa kushukuru wapigakura lakini wamewekewa vikwazo… siyo Rais kivuli,” alisema Baregu.

“Kila mtu ana haki ya kukutana na yeyote au kundi lolote alimradi hajavunja sheria wala kwenda kinyume cha Katiba.”

Mwili wa Mtanzania Uliozuiliwa India Mpaka Walipe Deni Kuwasili Leo

$
0
0
Hatimaye mwili wa Mtanzania Abel Machanga aliyefia nchini India akipata matibabu unatarajiwa kuwasili leo baada ya kuzuiwa kwa takribani siku 28 kutokana na deni la matibabu.
Mwili huo umeruhusiwa baada ya familia ya Machanga kulipa deni la shilingi milioni 35 lililokuwa likidaiwa kama gharama za matibabu.

Abel alikutwa na mauti Desemba 31, 2015 akiwa kwenye matibabu nchini humo, mbaya zaidi, maiti yake ilizuiliwa kutolewa mochwari mpaka familia ilipe deni la shilingi milioni 35.
Abel alianza kuugua Novemba 2014 akiwa denti wa Chuo cha Biashara Dar (CBE). Alivimba macho, yakatokeza nje, akapoteza uwezo wa kuona huku pia akipumua kwa shida.

Alitibiwa Hospitali ya Macho CCBRT, Dar ikashindikana, akapelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, hali ilizidi kuwa mbaya. Novemba 24, 2015, ndugu wakampeleka India ambapo mauti yalimkuta.

Ajali Mbaya Dar Yachukua Uhai wa Kijana Kelvin Kaloosh

$
0
0
Ajali hii imetokea jijini Dar, karibu na Ubalozi wa Kenya usiku wa kuamkia leo.

Pole sana wafiwa na wote walioguswa na msiba huu Hasa wasanii na watu maarufu hapa mjini

Binafsi nimesikitika Sana ;

Mwendokasi unaua...
Usinywe pombe na kuendesha...
Usiendeshe huku ukituma sms...
Usiendeshe ukipapasa mwanamke mapaja...


RIP Kelvin Kaloosh

Msipoteze Muda Wenu Kutarajia Bifu Kati ya Zitto na UKAWA Bungeni

$
0
0
Zitto Kabwe
Madhumuni makuu ya chama chochote cha siasa ni kushika Dola. CCM imeshika Dola hivyo kazi kuu sasa ya chama cha upinzani ni kujiuza kwa wananchi ili ukifika mwaka 2020 kiweze kushika Dola.

Baada ya uchaguzi, platform kubwa kwa chama cha upinzani kwa ajili ya kujiuza ili kijiwekee mazingira ya kuwa na nafasi ya kushika Dola katika kipindi kijacho ni Bungeni na kazi pekee itakachokiwezesha chama cha upinzani kufanikiwa kwenye hili ni kuikosoa Serikali pamoja na kuiwajibisha pale ambapo inastahili kuwajibika.

Hivyo ni wazi kwamba vyama vyote vya upinzani vina mkakati mmoja nao ni kujenga hoja dhidi ya Serikali iliyoundwa na chama Dola ili kufikia malengo yake.

Hivyo ni wazi kwamba Bungeni ni mahali ambapo vyama vya upinzani havina jinsi bali kuunga mkono hoja zinazotolewa dhidi ya Serikali ama na wana CCM au wapinzani nje ya chama chao ambazo zina mashiko na kwa sababu hii si jambo la ajabu kwa vyama vya upinzani kulazimika kuungana mkono katika hoja zenye mashiko dhidi ya Serikali kama tunavyoshuhudia sasa hivi.

Ingawaje Zitto yuko peke yake kutoka chama cha upinzani cha ACT Wazalendo ukilinganisha na UKAWA ambao wako wengi kupitia tiketi za CHADEMA na CUF, bado Zitto ana kipaji kizuri tu cha kujenga hoja dhidi ya Serikali, hoja ambazo kila mpinzani lazima ataziunga mkono kama kweli anataka kufikia malengo yake ya kwenda Ikulu na kuepuka kudharauliwa na wapiga kura.

Vilevile Zitto itabidi aunge mkono hoja zinazowasilishwa na wapinzani wenzake ambazo zina tija katika kupaisha uhai na matarajio ya chama cha upinzani kuelekea Ikulu dhidi ya Serikali iliyowekwa madarakani na chama Dola kama kweli ana nia ya kukitayarisha chama chake kuwa na nafasi ya kushika Dola hapo 2020.

Hivyo tutarajie ushirikiano kati ya Zitto na UKAWA kuimarika bungeni kwa kipindi hiki cha miaka mitano na ninachokiona ni kwamba uchaguzi wa 2020 utakuwa na muungano wa wapinzani ambao unaweza kuwa na jina lingine badala ya UKAWA kama marekebisho yanayohitajika ya katiba yakifanyika kabla ya uchaguzi ujao lakini kwa vyovyote vile, iwe UKAWA ya sasa hivi au muungano mwingine bado ACT itakuwa chama ambacho kitakuwa na karata ya kuupa muungano wowote ule utakaobuniwa nguvu na matarajio makubwa ya kwenda Ikulu ifikapo 2020 kama Zitto ataendelea na kazi yake ya kuibana Serikali kama kawaida yake na kama Mwenyezi Mungu atampa busara ya kuendelea na harakati zake za kisiasa pamoja na afya njema na uhai mpaka wakati huo..

By Shafi_Abeid

Nimekoma Kumchunguza Mpenzi Wangu..Haya Ndio Yaliyonikuta..

$
0
0
Naombeni ushauri wadau,

Karibu wiki sasa nime hack Facebook, Whatsapp ya mpenzi. Awali sikutaka presha ya kujiumiza roho hivyo sikutaka kumfuatilia.

Juzi kati nikajaribu mautundu yangu.. Yesuuuu na Maria. Anachat na wanaume huyo! Sina amani, moyo unaenda mbio kila saa. Najuta kufanya hivyo maana amani yote imepotea.

Nisaidieni wadau nifanyeje maana nampenda kiama.

Rais Magufuli Akosolewa Kwa Kutohudhuria Mkutano wa Umoja wa Afrika, Ikulu yajibu

$
0
0
John Magufuli
Baadhi ya wanasiasa na wachambuzi wa mambo ya kisiasa wamemkosoa Rais John Magufuli kwa kutohudhuria mikutano ya Kimataifa ukiwemo mkutano wa Umoja wa Afrika (AU), uliofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia hivi karibuni wakidai kuwa ulikuwa muhimu sana kidiplomasia.

Wameeleza kuwa mkutano huo wa AU uliofanyika siku mbili nchini Ethiopia ulikuwa muhimu sana kwa kuzingatia utamaduni wa mikutano hiyo kuwakaribisha viongozi wapya wa nchi wanachama.

“Kama Mkuu wa nchi, Rais Magufuli alipaswa kuhudhuria mkutano huo ili akutane na viongozi wenzake na kubadilishana nao mawazo. Nadhani hayuko sahihi kwenye hili,” Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholas Mgaya aliliambia gazeti la The Citizen.

“Kwa namna hii, Tanzania inapoteza mengi, taswira yetu inafifia kwenye ngazi za kimataifa. Kiongozi wetu anapaswa kuona umuhimu wa kuhudhuria kwenye vikao kama hivyo vya kimataifa vya ngazi za juu,” aliongeza Mgaya.

Naye mhadhiri Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Ruco) ambaye ni mtaalam wa masuala ya kisiasa, Profesa Gaudence Mpangala aliunga mkono na kueleza kuwa mkutano huo ulikuwa na umuhimu sana kwa Rais Magufuli kuhudhuria akiwa na ujumbe wa viongozi wachache.

“Kama Rais Magufuli amepanga kupunguza gharama, angeenda na watumishi wachache. Lakini mkutano huo ulikuwa muhimu sana kwake na Taifa,” alisema Profesa Mpangala.

Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu, Gerson Msigwa alieleza kuwa Rais Magufu  alimtuma Makamo wa Rais, Bi. Samia Suluhu kuiwakilisha nchi kwa kuwa alikuwa na majukumu mengine nchini. Kwahiyo nchi iliwakilishwa vyema kwenye mkutano huo.

“Kama Rais hakuhudhuria ina maana alikuwa na majukumu mengine. Lakini aliwakilishwa na Makamo wa Rais. Kwahiyo kila kinachohusu Tanzania kitafanyiwa kazi ipasavyo,” Msigwa aliliambia gazeti la The Citizen.

Aidha alisema kuwa bado kuna mikutano mingi ya Umoja wa Afrika mbeleni ambayo Rais Magufuli atahudhuria.

Waziri Mkuu Majaliwa na Edward Lowassa Wakutana Uso Kwa Uso

$
0
0
Lowassa na Waziri Mkuu Majaliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Askofu Frederick Shoo kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.

Alshabab Wavamia KENYA Eneo la Mpeketoni....Idadi ya Waliorepotiwa Kuuawa Hii Hapa

$
0
0
Watu wanne wameripotiwa kuuawa katika eneo la Bondeni Mpeketoni katika jimbo la Lamu.
Waliotekeleza shambulizi hilo wanadaiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Al Shabab ambao walikuwa wamevalia magwanda ya kijeshi.

Walioshuhudia shambulizi hilo wanasema kuwa wapiganaji wao waliwaruhusu waislamu kuondoka huku wale waliokuwa wakristo wakishambuliwa kwa visu na wengine kwa risasi .
Wenyeji wanasema kuwa shambulizi hilo lilitokea mwendo wa saa kumi alfajiri.
Watu wengi waliachwa wakiuguza majeraha.

Nyumba kadha za wenyeji ambao sio waislamu zilichomwa moto.
Operesheni ya uokozi inayoendeshwa na maafisa wa usalama inaendelea katika eneo lililoko karibu na msitu wa Boni ambako inadaiwa wavamizi hao walitorokea.

Hii si mara ya kwanza kwa eneo hilo la Mpeketoni kushambuliwa na wanamgambo wa Al Shabab.
Mwaka 2014 wanamgambo wa Al shabab walishambulia mji wa Mpeketoni na kuua zaidi ta watu 60.
Washukiwa wakuu wa shambulizi hilo la kwanza Mpeketoni walifikishwa mahakamani majuzi na kusomewa mashtaka dhidi yao.

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Kundi la Mziki la Navy Kenzo Kutoa Wimbo na Video Mpya-Kamati

$
0
0
THE INDUSTRY MUSIC LABEL

TAARIFA KWA UMMA

KUNDI LA MZIKI LA NAVY KENZO LATOA WIMBO/VIDEO MPYA-KAMATIA

Baada ya kutamba Mwaka Jana Africa nzima na wimbo unaoitwa ‘Game’, Kundi la Navy Kenzo limeanza mwaka vizuri baada ya kutoa wimbo mpya pamoja na video yake unaitwa “Kamatia” , Wimbo huo umeshaanza kuwa gumzo sehemu mbali mbali na kuonyeshwa kwenye TV za kimataifa siku mbili tu baada ya kutoka, Uzinduzi wa Wimbo Huo ulifanyika Kiaina yake kwa Staili ya 'Flash Mob' Kwenye Club ya Rhapsody kwa kuwasuprise waliokuwa ndani ya Club hiyo.

Kundi la Navy Kenzo linaloundwa na Aika na Nahreel mpaka sasa wameshatoa nyimbo kadhaa zilizotamba sana kama Moyoni, Bokodo, Visa na nyingine nyingi.
Navy Kenzo wameamua kutoa Wimbo pamoja na Video yake moja kwa moja kutokana na ushindani uliopo kwa sasa kwenye Music wa Bongo Flava, Video imefanyika nchini South Africa na Muongozaji wa Video wa kimataifa anayeitwa Justin Campos.

Kamatia ni wimbo ambao unaongelea kuhusu wapenzi wawili waliomua kushikana hasa kwenye mapenzi , Midundo ya nyimbo hiyo ina mahadhi ya Dancehall na vionjo vya kipekee kutoka kwa Producer bora Tanzania Nahreel.

Nahreel Ambaye ni mmoja wa Kundi la Navy Kenzo ni Producer wa Muziki bora Mwenye tuzo ya Kilimanjaro Music, Ametengeneza nyimbo mbali mbali zilitamba Kama Nana ya Diamond Ft Flavor,  Joh Makini Ft Aka Don’t Bother and Vanessa Mdee’s Nobody but me, Never ever na Hawajui, pia ndio mpishi wa Nyimbo ya Navykenzo ‘Game’


Bonyeza Link ifuatayo Kudownload Wimbo huo ;DOWNLOAD AUDIO
au Angalia Video Hapa;VIDEO

Imetolewa na
The Industry
Email;bookings@navykenzo.com

Jinsi Rubani Rodgers Gower Alivyouawa Na Majangili

$
0
0
Siku moja baada ya kifo cha rubani Rodgers Gower (37) aliyekuwa anaendesha helikopta inayomilikiwa na Mwiba Holdings, baadhi vyombo vya habari vya kimataifa vimeripoti kuwa huenda bunduki iliyomuua ni ile iliyokuwa inatumika kuulia tembo.

Miongoni mwa vyombo hivyo ni magazeti ya Uingereza ya Daily Mail, The Guardian, The Sun, The Telegram, The Independent, Shirika la Habari la Ufaransa AFP na Shirika la Utangazaji la Marekani CNN.

Mbali na vyombo hivyo, jana asubuhi mwili huo ulifanyiwa uchunguzi ambao ulionyesha matundu manne ya risasi, moja kwenye mguu, mawili begani na jingine kwenye paji la uso ambako risasi iliingilia kichwani na haikuwa imetoka.

Chanzo cha habari katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, ulikopelekwa mwili huo kilisema walipewa maagizo kuhakikisha hauondolewi hadi risasi iliyopo kichwani imeondolewa.

“Unajua huyu aliyefariki ni Mzungu, hata kama amefanyiwa postmoterm hapa anaweza kufanyiwa nyingine Aga Khan, Dar es Salaam na akifikishwa kwao Uingereza anafanyiwa tena, ndivyo walivyo wenzetu,” alisema.

Ijumaa iliyopita, Gower aliuawa kwa risasi wakati akiendesha helikopta hiyo kwenye doria dhidi ya majangili katika Pori la Akiba la Maswa, mkoani Simiyu akiwa pamoja na raia wa Afrika Kusini, Nicky Bester ambaye alinusurika kifo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alisema Serikali inaendelea na uchunguzi ili kuwabaini majangili waliohusika.

Alivyouawa
Daily Mail lilisema jana kuwa inawezekana hata bunduki iliyomuua Gower ni ile waliyokuwa wanatumia majangili hao kuua tembo. Lilieleza kuwa wakati Gower akiwa katika doria, aliona mabaki ya tembo wawili chini.

Gazeti hilo lilimnukuu Pra tik Patel, mmoja wa marafiki wa karibu marehemu, akisema wakati anaendelea na doria aliona tembo mwingine ambaye hakuwa ameuawa muda mrefu.

“Baada ya kuona hivyo, akataka ageuze ili wakamwangalie yule tembo, huku akijaribu kuona kama kuna majangili, ndipo mwanamume mmoja alitokea akiwa na bunduki na kupiga kwenye uvungu wa helikopta,” alisema Patel ambaye pia ni mfanyakazi mwenzake.

“Ile risasi ilitoboa uvungu wa helikopta na kupenya ndani, ikampiga rubani kwenye mguu na sehemu ya bega na uso kisha kutoboa paa la helikopta na kutoka nje … kutokana na uzito wa silaha iliyotumika kumuua, pengine ndiyo ileile ambayo majangili walitumia kuua tembo.”

Hata hivyo, gazeti la The Telegram, lilieleza kuwa bunduki iliyotumika kumuua Gower ni AK47.

“Alipokuwa anamkaribia tembo mmoja aliyeuawa, ndipo akapigwa risasi na kufariki kabla ya timu ya waokoaji kufika katika eneo hilo,” ilisema sehemu ya habari hiyo.

Mwanzilishi wa Mfuko wa Hifadhi wa Friedkin (FCF) aliyetoa taarifa kwa vyombo vya habari, Dan Friedkin ambaye aliwahi kufanya kazi na Gower alisema ni jambo la kusikitisha kuona rubani huyo, aliyekuwa katika operesheni ya kusaidia Tanzania kupambana na majangili ameuawa na haohao majangili.

The Guardian liliripoti kuwa jukumu kubwa la marehemu ambaye pia alikuwa mhasibu kitaaluma, lilikuwa kusafirisha watalii kwenye kambi mbalimbali za hifadhi.

Gower ambaye pia alihitimu masomo ya urubani wa helikopta mwaka 2004 London, Uingereza amekuwa akifanya doria kwa kushirikiana na wahifadhi kwa ajili ya kupambana na majangili kwenye hifadhi.

Akizungumzia mipango ya mazishi, Patel alisema jana kuwa suala hilo bado linajadiliwa na familia ya marehemu.

Hata hivyo, taarifa nyingine zilieleza kuwa mwili huo unatarajiwa kusafirishwa kwenda Uingereza kwa mazishi.

Chanzo cha kuaminika katika Mount Meru kilisema muda mfupi baada ya mwili huo kufikishwa, wakala wa kusafirisha miili ya raia wa kigeni alifika na kuzungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Mwiba Holdings, iliyokuwa inamiliki helikopta hiyo.

Zari Hassan Ahofia Kuishi Bongo..Tumbua Tumbua ya Majibu ya Magufuli Yamtisha

$
0
0

Ubuyu! Tumbuatumbua ya majipu ya Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ inadaiwa kumtisha mwandani wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kuja kuishi Bongo ikidaiwa kisa ni utajiri mkubwa alionao wenye shaka juu ya malipo ya ushuru na mapato.

Habari kutoka kwenye chanzo cha ndani cha familia ya Diamond, zimeeleza kuwa Zari alikuwa na mpango wa kuhamishia miradi na makazi yake rasmi Dar mwanzoni mwa mwaka 2016 lakini ndoto hiyo inaonekana kuyeyuka.

Chanzo hicho kilieleza kuwa, familia ya Diamond imekuwa ikimshinikiza jamaa huyo amshawishi Zari kuwekeza Bongo lakini kwa sasa mpango huo umefutika kwani mwanadada huyo anaogopa kutumbuliwa majipu.

“Unajua Zari anafuatilia kila kitu kinachoendelea nchini. Kwa hiyo usidhani hajui mambo ya TRA (Mamlaka ya Mapato) yalivyochachamaa.

“Unajua anasema akihamia Bongo itabidi aingize nchini yale magari yake ya kifahari anayotembelea akiwa Sauz (Afrika Kusini) au Uganda lakini anahofia tumbua majipu ya Magufuli.
“Wewe fikiria kama lile Range (Rover) la Wema (Sepetu) limekamatwa na TRA, itashindikana nini kukamata Hummer au Lamborghini ya Zari?

“Nafikiri ishu ni utajiri wake. Nilishasoma kwenye vyombo vya habari vya Uganda kuwa utajiri wake wa ghafla umekuwa ukiibua sana maswali na yeye huwa hapendi kuzungumzia vyanzo vya utajiri wake,” kilinyetisha chanzo chetu.

Baada ya kumwagiwa ubuyu huo, mwanahabari wetu alithibitisha kuwa kweli Zari hayupo Bongo yupo Sauz hivyo alimsaka Diamond ambaye alikuwa na haya ya kusema: “Zari ana miradi mingi, muda wa kuwekeza Bongo ukifika atakuja kufanya hivyo.

uhusu mheshimiwa (Magufuli) mimi nampongeza kwa kutumbua majipu kwa sababu tulikuwa tunahitaji kiongozi kama yeye,” alisema Diamond na kuongeza kuwa mpango wa Zari wa kuja kuishi Dar upo palepale.

Askofu Ampasulia Majaliwa jipu la Polisi Kuingia Bungeni..Adai si Haki Bunge Kulindwa na Jeshi

$
0
0
Mkuu mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk Fredrick Shoo jana, mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alielezea kushangazwa kwake na kile alichokiita “jeshi kuingizwa ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri mjini Dodoma”.

Alisema hayo mjini hapa alipokuwa akitoa hotuba yake ya kwanza mara baada ya kuingizwa kazini kushika wadhifa huo atakaoutumikia kwa miaka minne.

Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, anachukua nafasi ya Askofu Dk Alex Malasusa ambaye amemaliza muda wake wa uongozi.

Hafla hiyo ambayo Majaliwa alikuwa mgeni rasmi, ilihudhuriwa pia na mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye na maaskofu zaidi ya 28.

Akizungumza kwa hisia, Askofu Dk Shoo alionekana kuguswa na mambo matano yaliyojitokeza katika Taifa.

Polisi bungeni

Alieleza kutoridhishwa kwake na mwenendo wa Bunge, akisisitiza kuwa ni lazima mihimili mitatu ya dola ijiendeshe kwa uhuru.

“Iachiwe ifanye kazi yake kwa uhuru na kila mhimili utunze heshima hiyo. Tunasikitishwa sana na hali inayoendelea katika Bunge letu na nashukuru nimewaona baadhi ya wabunge humu,” alisema.

Wabunge waliokuwapo ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Mbunge wa Moshi Mjini, Jaffar Michael, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema Anthony Komu wa Moshi Vijijini, James Mbatia wa Vunjo na Lazaro Nyalandu wa Singida Kaskazini.

“Hili ni lenu na Spika wenu (akiwageukia wabunge). Bunge ndiyo nyumba ya demokrasia kama kweli Tanzania tunataka kujenga jamii ya kweli ya inayoheshimu misingi ya kidemokrasia. Sisi tunatarajia kuona na kusikia hoja zikijadiliwa kwa uwazi na katika hali ya kistaarabu. Kwa kuchezeachezea heshima hii ya Bunge sasa tunaona juzijuzi tu jeshi linaingia bungeni. Nyumba ya demokrasia haiingizwi majeshi. Kwa hiyo wabunge tunzeni heshima yenu,” alisema na waumini wa kanisa hilo kumshangilia.

Utumbuaji majipu

Askofu huyo wa Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, alimpongeza Rais John Magufuli, Waziri Mkuu, Majaliwa na timu yao kwa namna walivyoanza vizuri katika utawala wa awamu ya tano.

“Rais ameshaweka wazi kwa wananchi nia yake ya kufufua uchumi na kupambana na ufisadi. Katika muda mfupi huu wa uongozi wake, mmekwishakuanza (Waziri Mkuu) kutumbua majipu makubwa ya ufisadi,” alisema na kuongeza:

“Tunamwomba sana Rais na timu yake aendelee kutumbua majipu hayo kwa ujasiri mkubwa na miji ya majipu hayo ioshwe na kukamuliwa ili yasirudie.”

Hata hivyo, alitahadharisha kuwa utumbuaji huo unatakiwa ufanyike kwa hekima na misingi ya uwazi, ili wasio na nia njema wasitumie kuwakomoa wasio na hatia.

“Yale majipu ambayo ni hasa, hayo yasiachwe kutumbuliwa na msiwe na hofu yoyote kutoka kwa watu watakaowapinga, najua kuna watu wanajipanga kuwapinga, msiwe na hofu yoyote,” alisema Askofu Shoo.


Mkwamo Zanzibar

Akizungumzia mkwamo wa kisiasa visiwani baada ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kufuta uchaguzi na kutangaza tarehe ya kuurudia, Askofu Shoo alisema yanayoendelea huko yanalitia doa Taifa.

“Tunamuomba pia Mungu awape hekima na ujasiri wa kushughulikia suala la Zanzibar ili maridhiano na haki itendeke na nchi yetu iendelee kuwa na utulivu na amani. Mambo yanayoendelea kule Zanzibar yasipodhibitiwa vizuri yataweza kutia doa Awamu ya Tano ya uongozi.”


Katiba mpya

Kuhusu mchakato wa Katiba Mpya, Askofu Shoo alisema hayo ndiyo matarajio makubwa ya Watanzania ambao wanataka kuona Serikali ya Awamu ya Tano ikiwatimizia ndoto hiyo.

“Tunazidi kumuomba Mungu. Matarajio ya Watanzania ni uwapo wa Katiba Mpya inayoheshimu matakwa ya wengi na inayosisitiza utawala wa sheria na haki za kibinadamu,” alisema na kuongeza:

“Ninashauri mchakato wa Katiba Mpya ufikiriwe kwa upya na utumike kama njia ya kuganga madhaifu na majeraha yaliyotokea au ambayo yapo katika awamu zote zilizotangulia.”



Ada elekezi

Akizungumzia ada elekezi kwa shule za binafsi, Askofu Shoo alitaka suala hilo litizamwe upya tena kwa kuwashirikisha wadau wa elimu nchini.

“Nina imani Serikali ikiboresha shule zake hakutakuwa na haja ya kuweka ada elekezi. Tunachohitaji katika ubora wa elimu ni kuanzisha mamlaka inayojitegemea ya ithibati na udhibiti. Kuwa na mamlaka hiyo na ikijitegemea naamini kutaleta mafanikio katika ubora wa elimu.”



Waziri Mkuu

Akihutubia kwa niaba ya Rais, Majaliwa alisema wabunge wanapaswa kuwa kioo cha jamii.

“Ulipozungumzia hili ulizungumzia Bunge na mimi nashukuru umelieleza hilo la wabunge wenzangu. Jambo hilo ni letu, tutahakikisha suala la demokrasia linaimarishwa ndani ya Bunge,” alisema.

“Lakini pia nataka nieleze Bunge ni eneo ambalo linaweza kuijenga jamii hii mpya. Wabunge ni kioo, ni watu wa kuigwa. Hivyo ni vyema tukalitumia Bunge kwa lugha sahihi na tabia nzuri. Tutaendelea kusimamia lugha nzuri ndani ya Bunge ili wanaoona waweze kuiga. Niwahakikishie Watanzania tutaendelea kuzungumza na wabunge ili bungeni pawe mahali panapojenga tabia njema,” alisema.

Kuhusu Katiba Mpya, alisema hoja ya Askofu Shoo ifanyiwe kazi na akadokeza kuwa amekuwa akizungumza na wabunge juu ya suala hilo.

“Suala la ada elekezi kwa shule binafsi litazungumzwa na wadau wote ili kutoa mwelekeo sahihi. Nataka nikuahidi Baba Askofu, tutaziboresha shule zote za umma ili ziweze kutoa elimu bora,” alisema.

Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi, Issac Aman alisema kama kuna jipu linalopaswa kutumbuliwa, basi ni la Watanzania kukosa moyo wa uzalendo.

Askofu huyo alisema ufisadi na ubinafsi unaofanywa na baadhi ya Watanzania ni matokeo ya kukosekana kwa uzalendo na uadilifu.


Alichoandika Zitto Kabwe Kuhusu Majangili Kutungua Helkopta ya Tanapa...Ashangazwa na Kilichotokea

$
0
0
Alichoandika Zitto Kabwe Kuhusu Majangili Kutungua Helkopta ya Tanapa...Ashangazwa na Kilichotokea

Ommy Dimpoz Amtupia Dongo Kistaili Idriss Sultan Kuhusu Kupata Hela za Big Brother na Kuja Kuzitumbua na Wema Sepetu

$
0
0
Mwanamuziki Ommy Dimpoz Amemrushia Dongo la Kiana rafiki yake Idriss Sultan Mshindi wa Shindano la Bigbrother 2014 Kwa Kuandika Haya Kwenye Ukurasa wake wa Instagram;

"Hii picha ni Pale Team Wemasepetu watakapogundua kumbe Idris Sultan hana Kizazi..Happy Birthday Milionea mwenye kampuni mbili zilizoajiri watu 7  Umekaza sana mwana kutoka kupiga picha, Kukaa ndani kama mwali Miezi 3 halafu ukapewa Hela ambazo umeamua unazitumbua na Miss wetu Kila la lakheri mwana nakuombea zikiisha tuachie Miss wetu sawa?mtoto tutamlea wenyewe  (UZURI WA IDRIS HANUNAGI MTOTO WA WATU" Ommy Dimpoz

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Azidi Kung'aa Kimataifa..Apewa Kazi Nyingine na Umoja wa Mataifa Africa

$
0
0
Jakaya Kikwete
Rais mstaafu wa awamu ya nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete Jumapili ya January 31 Umoja wa mataifa wa Afrika wametangaza kumpatia majukumu mapya. Dk Jakaya Kikwete January 31 ameteuliwa kuwa mjumbe wa amani wa Libya.

Dk Kikwete ameteuliwa kuchukua nafasi hiyo ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na Mr Dileita Mohamed Dileita wa Djibouti ambaye alikuwa mjumbe wa nafasi hiyo toka mwaka 2014. Kikwete ameteuliwa kuwa msuluhishi wa kutafuta amani Libya ambapo toka auwawe aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Muammar Gaddafi mwaka 2011, hali bado sio nzuri.

Nisha Afunguka 'Niliogopa Kula Chips Kuku Pesa zisije zikaisha, Nilikuwa Nikishindia Mihogo'

$
0
0
Msanii wa filamu na mjasiriamali, Salma Jabu aka Nisha amesema mafanikio aliyopata yametokana na kujinyima ambapo amedai ilifikia hatua alikuwa akishinda kwa kula mihogo huku akiogopa kula chipsi pesa zisije zikaisha.

Muigizaji huyo ambaye mpaka sasa ana filamu nane ambazo amezitoa kupitia kampuni yake ‘Nisha’s Film Production’, alikiambia kipindi cha Uhondo cha EFM kuwa alipitia changamoto nyingi mpaka kupata mafanikio aliyonayo sasa.

“Mimi nilianza na shilingi 50,000 tu pesa yangu ya kwanza ya filamu kulipwa, niliiweka na sikutumia hata shilingi kumi,” alisema Nisha.

“Mimi nilikuwa hata chakula saa nyingine nasema siwezi kula chipsi na kuku, hii acha hata ninunue muhogo mmoja halafu nyingine niweke akiba, ubahili wangu umesaidia. Leo nina biashara, kampuni ya filamu ya mamilioni na nimeajiri watu,” alieleza.

UKAWA Wapata Pigo Jingine Bungeni...Kamati Iliyoibua Sakata la Escrow Yakabidhiwa Kwa Wabunge wa CCM

$
0
0
Bungeni
Wabunge wa upinzani, wakiwamo wanaootoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wamepata pigo la aina yake baada ya jukumu mojawapo muhimu la kamati wanayopaswa kuiongoza kuondolewa kwao, imefahamika.

Kamati hiyo ni ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (PAC) ambayo imehamishiwa kwenye kamati mpya inayoongozwa na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Majukumu hayo muhimu yaliyohamishwa PAC ni yale yanayohusiana na hesabu za mashirika ya umma.

Majukumu hayo sasa yamehamishiwa kwenye kamati mpya ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), chini ya uenyekiti wa Mbunge wa Jimbo la Sumve (CCM), Richard Ndasa, huku makamu mwenyekiti akiwa Lolesia Bukwimba (Busanda-CCM).

Naibu Katibu wa Bunge anayeshughulikia masuala ya Bunge, John Joel, amethibitisha  juu ya kuwapo kwa mabadiliko hayo, akisema kwamba ni kweli PIC imepewa jukumu la kusimamia hesabu za mashirika ya umma kutokana na kanuni za Bunge, toleo la Januari 2016.

Alisema uamuzi wa kupeleka jukumu hilo PIC, umetokana na pendekezo la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kutokana na PAC iliyopita kushindwa kutimiza majukumu yake iliyopewa.

Katika mabunge yaliyotangulia, hesabu za mashirika ya umma zilikuwa zikisimamiwa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia (Chadema), Zitto Kabwe. Hivi sasa, Zitto ni Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT-Wazalendo.

Kamati hiyo pia iliwahi kuongozwa na aliyekuwa Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa mara zote PAC ndiyo iliyokuwa mstari wa mbele katika kuibua ‘madudu’ mbalimbali yanayohusiana na rushwa na ufisadi bungeni na kuilazimu serikali kubadili mawaziri wake mara kadhaa.

Baadhi ya mambo yaliyowahi kuibuliwa na PAC ni pamoja na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow ambayo ripoti yake ilisababisha mawaziri wawili wa serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete na maofisa wengine kadhaa wa juu kuachia ngazi.

Taarifa ya PAC kuhusiana na ripoti ya CAG mwaka 2012 pia ilisababisha vigogo kadhaa, wakiwamo mawaziri, kung’olewa.

Zitto Atoa ufafanuzi
Aliyekuwa Mwenyekiti wa PAC kwenye Bunge la 10, Zitto, amesema si kweli kwamba kuna jukumu walilopewa na kushindwa kulitimiza.

 “Kwa kweli tulitimiza majukumu yetu yote. Na ili tufanye kazi yetu kwa ufanisi, tuliigawa kamati, eneo moja likawa chini ya Makamu Mwenyekiti (Deo Filikunjombe) na moja chini yangu. Deo mashirika na mimi serikali.

"Hata hivyo, kazi ilikuwa kubwa na muhimu kugawa PAC kuwa na PIAC na PAC. Isipokuwa, PIC ya sasa haina mamlaka ya kushughulikia hesabu za mashirika ya umma kwa mujibu wa kanuni. Kamati za mahesabu ni mbili tu, PAC na LAAC,” alisema Zitto.

Aliongeza kuwa iwapo Bunge linataka PIC ishughulike na hesabu za mashirika ya umma, itabidi iitwe Public Investments Account Committee (PIAC) na itabidi iongozwe na mbunge wa upinzani na siyo wa CCM.

“Kanuni za Bunge za sasa hazielekezi PIC kushughulikia taarifa ya CAG kuhusu mahesabu ya mashirika ya umma. Pia kanuni haziipi PAC mamlaka hayo pia. Kikanuni, hivi sasa mahesabu ya mashirika ya umma hayana kamati,” alisema Zitto
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images