Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104745 articles
Browse latest View live

Breaking News..Kabwe Zitto Kununua Timu Kubwa ya Mpira Nchini....

$
0
0
MBUNGE wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT), ametangaza azma ya kuinunua timu ya soka ya JKT Kanembwa inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.

Akizungumza , mbunge huyo alisema kuwa tayari ameshaanza mazungumzo na uongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mkoani Kigoma kuona kama upo uwezekano wa kuinunua timu hiyo.

Alisema kuwa mpango wa kuinunua timu hiyo unakuja katika kutekeleza azma ya kuwa na timu ambayo itacheza Ligi Kuu Tanzania Bara na kurudisha hadhi ya michezo ya mkoa Kigoma kwenye soka.zitto-kabwe-facebook-frontKabwe alisema kuwa iwapo uwezekano wa kuinunua timu hiyo utafanikiwa mpango utafanywa kuunda kampuni ambayo itakuwa ikisimamia uendeshaji wa timu hiyo kama ilivyo kwa timu ya Azam.

Alisema ni jambo la aibu kuona mkoa wa Kigoma hauna timu hata moja katika Ligi Kuu wakati sehemu kubwa ya wachezaji wanaochezea timu zinazoshiriki ligi hiyo wanatoka Kigoma.

Pamoja na azma hiyo alisema kuwa kama itashindikana kwa timu hiyo kununuliwa kutokana na taratibu za jeshi atatafuta timu nyingine ambayo ataisimamia na kuiwezesha kufanya vizuri ili iweze kucheza Ligi Kuu.

Katika kauli yake Kabwe ametanabaisha kuwa pamoja na mpango wa kuwa na timu ya mpira wa miguu, mpango wake ni kuhakikisha wachezaji wakongwe waliowahi kuchezea timu za madaraja ya juu na timu ya Taifa wakiwemo Juma Kaseja na wengine wanarudi mkoani humo ili kusimamia timu za mkoa huo na kuzifanya ziweze kucheza mashindano ya ligi mbalimbali nchini kwa mafanikio.

Kauli hiyo ya Zitto inakuja siku moja baada ya kuutangazia umma mazungumzo ya awali kati yake na Mkurugenzi wa timu ya Azam FC, Abubakar Bakhresa kuhusu kuanzisha shule ya kuendeleza vipaji Kigoma.


Mwanamke Akiwa na Tabia Hizi, Kwangu ni First Disqualification

$
0
0
1) Mwanamke anavuta shisha au sigara: unamkuta most of the time yupo kwenye vile vijiwe vyao vya kuvuta halafu wahuni kibao wamejaa mule, sometime hata drugs wanachanganya mule kwenye kile kibobo chao. Aisee dada zangu mnaotumia halafu wengine mnapost mpaka mtandaoni kama vile mnakula chakula mimi nimesha wa disqualify.

2) Mwanamke anapenda kupiga picha angali zaidi ya 90% ya body yake ipo wazi halafu anapost kwenye mtandao wa kijamii huyo hafai. Nimesema 90% ipo wazi ina maana 10% iliyofichwa na nguo ni hapo katikati na hapa juu sehemu nyingine zote wazi. Hapo utanisamee dada.

3) Kuna wengine unakuta wamejaliwa ila wakitembea utasema wanacheza 'full kujitingisha' mimi nikiona hivo ni first disqualification.

4) Tabia ya kujiachia sanaaa kwenye maeneo ya starehe kama club, beach na sehemu kama hizo za entartainment. Kuna ile kujiachia kawaida hiyo inaruhusiwa ila kuna ile unakuta demu every time anakuwa anazungumzia hayo maeneo zaidi ya kuzungumzia mambo yenye faida, huyo hafai. Unakuta girl most of the time ata kwenye picha zake yeye ni mtu wa ku relax tu na sun glass kubwaa halafu amelala kwenye kale ka kitanda cha beach.

5) Mwanamke mwenye marafiki wengi, unakuta girl ana marafiki kama 10 wa karibu. Labda kama ni mwanafunzi ila kama yupo uraiani mi naona kama ni tatizo. Naona kama itakuwa rais sana kumshawishi na kumbadilisha tabia. Kwa hiyo nikiona hivo ni 1st disqualification.

6) Mwanamke mbishi,

Hivi Hapa Vyama Vitano Vitakavyoshiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar...

$
0
0
VYAMA vitano vya siasa vitashiriki katika uchaguzi wa marudio wa Zanzibar, utakaofanyika Machi 20 mwaka huu, uliotangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC). Vyama hivyo ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), ADC, CCK, TLP na SAU.

Hatua hiyo inatokana na vyama vitatu vya siasa Zanzibar vya CCK, SAU na TLP, kutangaza kuwa wagombea wake, watashiriki katika uchaguzi huo wa Machi 20. Taarifa ya viongozi wa vyama vya CCK, SAU na TLP, iliyosomwa kwa pamoja katika Ukumbi wa Culture eneo la Mji Mkongwe mjini hapa jana, ilisema wagombea wa vyama hivyo vitatu, watashiriki uchaguzi huo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana, ulifutwa baada ya kujitokeza kwa kasoro mbalimbali, zilizoonesha wazi kwamba hauwezi tena kuwa huru na haki. Wagombea wa vyama hivyo vya siasa, waliotangaza kushiriki katika uchaguzi huo ni Ali Khatib kutoka CCK, Issa Mohamed Zonga kutoka SAU na Hafidh Hassan Simai kutoka TLP.

Mgombea wa CCK, Ali Khatib Ali alisema kwamba tayari wamejipanga vizuri kwa ajili ya uchaguzi huo na kuwataka wanachama na wafuasi wake na wananchi, kuitumia fursa hiyo ya kidemokrasia kuchagua viongozi watakaoongoza nchi. “Tangazo la Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) limetutaka kurudia uchaguzi kwa sababu ule wa awali umefutwa kwa hivyo hatuna sababu ya kususia uchaguzi huo na tunachofanya kwa sasa ni kuwataka wanachama wetu na wafuasi kujitayarisha kwa uchaguzi wa marudio,” alisema Ali.

Jumapili iliyopita, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein alisema chama hicho kipo tayari kwa uchaguzi wa marudio Machi 20 kwa lengo la kuhakikisha kinashika dola. Akihutubia mamia ya wanachama wao katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui wakati wa kuzindua maadhimisho ya miaka 39 ya CCM, Dk Shein alisema maamuzi ya kurudiwa kwa Uchaguzi Mkuu, yamefanywa na ZEC ambayo ndiyo chombo halali kwa mujibu wa Katiba cha kushughulikia masuala yote ya uchaguzi nchini.

Aliwataka wanachama na wafuasi wao kujipanga vizuri na kushiriki uchaguzi huo kikamilifu, kwani kwa mujibu wa Katiba ya CCM ni kushinda chaguzi zote zinazofanyika nchini ili kushika dola na kuwatumikia wananchi. “Hayo ndiyo maamuzi ya chama chetu tuliyokubaliana kushiriki Uchaguzi Mkuu wa marudio baada ya kufutwa kwa ule wa Oktoba 25 mwaka jana kwa hivyo wanachama na wafuasi jitayarisheni kushiriki kikamilifu kwa ajili ya kushika dola,” alisema Dk Shein.


Breaking News..EWURA Yatangaza Kushuka Kwa Bei ya Mafuta

$
0
0
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA) yatangaza kushuka kwa bei ya mafuta, bei ya dizeli imeshuka kutoka Sh. 1,747 hadi Sh 1,600, petroli imefikia Shilingi 1,842.

Kupungua kwa bei ya mafuta kwenye soko la ndani kwa kiasi kikubwa kumetokana na kushuka kwa bei ya nishati hiyo katika soko la dunia na pia kushuka kwa gharama za usafarishaji na bidhaa za mafuta hayo kuja nchini

Wabunge Wageuza Bungeni Uwanja wa Mipasho..Misemo Yatawala...

$
0
0
Ukumbi wa Bunge juzi uligeuka uwanja wa malumbano na mipasho huku misemo ikichukua nafasi kubwa kutoka kwa wabunge wa chama tawala CCM na upinzani.

Malumbano hayo yalizuka baada ya Bunge kukaa na kujadili Mwelekeo wa Mpango wa Taifa, lakini ghafla wabunge walianza kurushiana maneno wakituhumiana kuwa majipu yanayotakiwa kutumbuliwa.

Katika kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti, Mary Mwanjelwa, malumbano yalianza kwa Mbunge wa Viti Maalumu, Jesca Kishoa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe jambo lililoamsha mjadala mzito.

Kishoa alianza kumtaja Dk Mwakyembe kuwa ni jipu linalohitaji kutumbuliwa na Rais na kuwa nafasi aliyonayo hakustahili.

Kishoa alitaja sababu ya kumwita Dk Mwakyembe si msafi kwamba alitumia zaidi ya Sh238 bilioni kwa ajili ya kununulia mabehewa ambayo yalithibitika kuwa ni mabovu.

Kitendo hicho kiliamsha hasira za Dk Mwakyembe na kusimama kisha kukana Serikali kutumia kiasi hicho huku akisisitiza ikithibitika kuwa ni kweli yuko tayari kujiuzulu wadhifa huo.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Jenista Mhagama alisimama mara kadhaa kutaka Kishoa afute kauli lakini upinzani ulimtetea mbunge huyo.

Hata hivyo, Mwanjelwa aliwataka kuendelea na mjadala ili akaangalie kwanza kumbukumbu za Bunge kuhusu maneno yaliyotamkwa na baadhi ya wabunge.

Mwigizaji Ray Kawa Mkongo Mpaka Leo Anaishi Kwao- Nay wa Mitego

$
0
0
Msanii wa muziki wa bongo fleva Nay wa mitego ameweka wazi baadhi ya mistari ambayo ipo kwenye moja ya wimbo wake ambao ana wasiwasi kuuachia kwa mashabiki kutokana na vitu alivyozungumza.

Kwenye wimbo huo ambao anadai anaogopa akiuachia watanzania watamchukia kwa mambo aliyozungumza kwenye wimbo huo alioupa jina la ‘Shika adabu yako’.

Katika wimbo huo Nay wa Mitego ametaja majina ya watu maarufu na kuwapa maneno yake kutokana na kile ambacho yeye anakifahamu na kukiamini.

Moja ya jambo alilozungumzia kwenye wimbo huo ni kuhusu tasnia ya movie na kusema imekufa wamebaki kuuza sura na wote wanataka kuimba kama Shilole na Snura.

Pia ameonekana kumchana Ray kwa kusema kuwa mpaka sasa anaishi kwao na pesa anazopata kuuza movie ananunua mkorogo.

“Mungu hakunyimi vyote lazima atakupa chako, demu ana sura mbaya lakini na bonge la tako. Bongo Movie imekufa wamebaki kuuza sura, wote wanataka Kuimba Kama Shilole Snura. Ray Kigo kawa Mkongo mpaka leo anaishi kwao, hela za kuuza Movie zote ananunua mkorogo, haitoki hii nimeirecord tu yakusiliza na wanangu maskani maana mtanichukia kwa niliyozungumza humu” Alisema Nay wa Mitego.

Wanawake wa Haya makabila Kitandani ni Wabovu Sana

$
0
0
Hiyoooooooooooooo ndo habari kwani kuna baadhi ya makabila ukiwa una mgegeda hata hatingishiki yeye ni kutulia kama gogo tu wala hawezi hata kukukuruka kwanza wachaga, wapare, waha, wasukuma, wangoni, wakikuyu, wakurya, waluguru, wagogo, wamasai na mengine kibao yani ni shida hadi wanafanya papuchi zao kua za baridi sana jaman badilikeni, haya toeni uzoefu wenu na ninyi

Mwigizaji Batuli Afunguka Kuhusu Kuzulimiwa na Ray Kwenye Movies Mpya ya Bosi Mfupi..Warushiana Maneno Insta

$
0
0
Waigizaji Batuli na Ray ni kama wana bifu la chini chini baada ya kurushiana maneno Instagram
Picha ilianza pale Lemutuz alivyoshare Tangazo la Movie yao mpya iitwayo tajiri mfupi kwenye page yake ya Instagram ambapo Mwigizaji Batuli Aliandika kwenye picha hiyo maneno yafuatayo


Sakata La Mauaji Ya Diwani Wa CUF Lachukua Sura Mpya

$
0
0
Mauaji ya kikatili ya Diwani wa Kata ya Kimwani, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Sylvester Muliga (CUF), yameanza kuibua mambo mazito huku ikielezwa kuwa Ijumaa alikuwa awasilishe hoja kwenye Baraza la Madiwani kuhusu masuala ya ardhi.

Muliga ambaye alifia Hospitali ya Kagondo alikopelekwa kwa matibabu baada ya kukatwa mapanga Jumapili usiku, imeelezwa kuwa katika kikao hicho ilikuwa aombe kuundwa kwa kamati ya kuchunguza uhalali wa maeneo makubwa ya ardhi yanayomilikiwa na watu wachache.

Kwa mujibu wa mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Mazingira ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kasharunga, Khalid Swalehe, hoja hiyo ilikuwa iwasilishwe na Muliga na ilikuwa inaungwa mkono na madiwani wa kata zote zilizo na migogoro ya ardhi.

Baada ya taarifa za kufariki dunia kwa diwani huyo, wananchi walivamia nyumba nane za watuhumiwa wanaodaiwa kutekeleza mauaji hayo na kuziteketeza kwa moto.

Pia, walichoma moto mashine mbili za kusaga na kuharibu gari la mmoja wa wagombea wa udiwani katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Kyota, Daudi Kiruma, wananchi wamehusisha mauaji hayo na mambo ya siasa.

“Kinachoonekana hapa baadhi ya watu wanataka kupotosha ajenda ili wahusika wa mauaji wapate nafasi ya kutoroka,” alisema Kiruma.

Hata hivyo, Kiruma alisema hana uhakika kama mtuhumiwa anayedaiwa alikuwa mgombea amekamatwa, kwa sababu haonekani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi, jana alisema wanamshikilia mtuhumiwa mwingine ambaye anafanya idadi ya walikomatwa kuhusiana na mauaji hayo kufikia watatu mpaka sasa.

Kamanda Ollomi aliwataka wananchi wasijadili mauaji hayo kwa hisia za kisiasa bali waviachie vyombo vya dola vifanye kazi yake.

Mwigizaji Ray Ajibu Tuhuma za Kumzulumu Batuli..Adai Issue ya Batuli ipo Kimkataba zaidi

$
0
0
Raythegreatest 
KATIKA MAISHA YANGU HUWA SIYUMBISHWI WALA SITIKISIKI KWENYE MISIMAMO YANGU NA SIKU ZOTE UKITAKA KUWA MTETEZI MZURI LAZIMA UWEZE KUSIKILIZA PANDE ZOTE MBILI ZA SHILINGI. NINA MIAKA 15 KWENYE TASNIA HII YA FILAMU UKUWAHI KUSIKIA NENO LINALOITWA DHURUMA KUTOKA KWANGU ILA WASWAHILI WANASEMA USILOLIJUA NI SAWA NA USIKU WA GIZA. NASEMA HIVI NIKIKUPA WALAU UTENGENEZE NUSU FILAMU TU NADHANI HAYA MATUSI YOTE MNAYOTUKANA MNGEGEUKA UPANDE WA PILI WA SHILINGI. JINSI WATU WANAVYOSHINDWA KUESHIMU KAZI ZA WATU COZ WAO WANA NJIA NYINGI ZA KUPATA KIPATO AMBAZO HIZO NJIA SISI HATUWEZI ZIFANYA LAZIMA TUFANYE KAZI ILI MKONO UENDE KINYWANI. MTU YOYOTE ANAYECHEZEA MAISHA YAKO MUOGOPE KAMA UKOMA. ISHU YA BATULI IKO KIMKATABA ZAIDI YA YEYE KAMA UPANDE MMOJAWAPO WA KUTEKELEZA MKATABA ANAJUA ILO. UPANDE MMOJA WA MKATABA UNAPOSHINDWA KUTEKELEZA WAJIBU WAKE NJIA ZA KUPITA ZIKO WAZI NA ZINAJULIKANA....INAPOFIKIA MTU BADALA YA KUFUATA NJIA SAHIHI NA AKAAMUA KULETA MJADALA KWENYE SOCIAL MEDIA HAPO KUNA ULAKINI AU AMEAMUA KUJIPA UPOFU WA SHERIA YA MIKATABA NINGEPENDA MUHUSIKA AJIKUMBUSHE ILO NA AFUATE NJIA SAHIHI. KUTUMIA SOCIAL MEDIA HAZITAMSAIDIA ZAIDI YA KULIKUZA JAMBO KWA WATU WASIOJUA UNDANI WAKE.

Nay wa Mitego Mahakamani Baada ya kuwaponda Bongo Movie?..U Heard (+Audio)

$
0
0
Febr 03 2016 nakukutanisha na Soudy Brown kwenye U heard ya Clouds fm ambapo leo anazungumzia ishu ya Mbongo Fleva Nay wa Mitego kufuatia mistari yake kwenye baadhi ya nyimbo kuwadiss Wasanii wa Bongo Movie na sasa wanataka kumpeleka Mahakamani.

Full stori ipo kwenye hii sauti hapa chini;

Breaking News...Zitto Kabwe Atangaza Kusameheana na Freeman Mbowe...

$
0
0
Zitto Kabwe Akipeana Mikono na Mbowe
Kupitia ukurasa wake wa Facebook muda mchache uliopita, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ameweka picha yake na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na kuandika hivi; "Mimi binafsi siwezi kuwa mfungwa wa magomvi yetu ya miaka ya nyuma. Nilishasamehe walionikosea…Mbowe siku zote amekuwa Kiongozi wangu na siwezi kubeza nafasi yake katika kujenga demokrasia nchini. Tulipishana. Tulikoseana. Tusameheane"

Tulia utafakari, halafu tupe maoni yako

Tigo Yawapa Wateja wake Huduma ya WhatsApp bure

$
0
0
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez akizungumza na waandishi wa habari na wageni waalikwa  mbalimbali wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika jana  Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam 
 Wafanyakazi wa Tigo na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakifurahia jambo  wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam
 Hapa kila mgeni mualikwa akiwa busy na simu yake kwenye uzinduzi huo.
 Ni kama wanasema 'tumependeza sana ngoja tujipige picha'  wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam

.
Wageni waaalikwa wakiwa katika maski za  " Emojis " wakifurahia jambo kwenye uzinduzi   huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam
 Hapa ni furaha tupu kwa wanahabari.
 Washereheshaji katika uzinduzi huo,Mc  Taji Liundi na Mc Abby wakitoa maelezo jinsi gani wateja wa Tigo watakavyofurahia huduma ya whatsapp bure 
 Burudani ikiendelea kutoka kwa wasanii wa kikundi maalum cha maonesho ya jukwaa  wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini  Dar es salaam.
 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez  (katikati), akiwa na viongozi wenzake kutoka tigo katika maski za "Emojis " wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam
  Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez  (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na washereheshaji MC Taji Liundi na MC Abby  wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam

 Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kushoto )  Meneja wa gharama  wa Tigo Jakhangic Tulaganov  na Meneja masoko Olivier prentout wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency 
Bloggers wakiwa katika picha ya pamoja na msanii Lucas  Muhuvile 'Joti'  wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency



Dar es Salaam, Februari 2, 2016- Kampuni ya Tigo Tanzania ambayo inaongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali imetangaza huduma ya bure ya WhatsApp kwa watumiaji wa huduma hiyo  ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni ya simu  kutoa ofa ya bure  ya mtandao huo wa jamii  nchini.


 Akitangaza upatikanaji bure wa huduma hiyo kwa vyombo vya habarijijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema kuwa wateja wote wa Tigo  wanaotumia  vifurushi vya intaneti  vya kampuni hiyo kwa wiki na mwezi  watapata huduma ya WhatsApp bure. Tigo ina wateja zaidi ya milioni 10.


Huduma ya WhatsApp ambayo ni maarufu kwenye kutuma ujumbe  kwa njia ya simu, ina watumiaji zaidi ya milioni nane nchini Tanzania  na  duniani  inatumiwa na watu wapatao milioni 900. WhatsApp inawezesha watumiaji  kubadilishana habari, ujumbe, video na miito ya sauti.


“Kuanzia sasa na kuendelea wateja wote wa Tigo wanaonunua vifurushi vyetu vya wiki au mwezi  watakuwa na fursa ya kufurahia  WhatsApp BURE. Hili linawezekana kama mteja ana smartphone. Huduma ya bure ya WhatsApp kwa wateja wetu inaonesha  jinsi tulivyojikita katika kuboresha mabadiliko kwenye  maisha ya kidijitali  na hivyo kuongoza kwenye kutoa teknolojia ya hali ya juu pamoja na ubunifu”, alisema Gutierrez.


Kwa Mujibu wa Gutierrez, ili kufurahia huduma hii, jambo analohitaji mteja wa Tigo ni kuwa na  kifurushi cha intaneti  cha wiki au mwezi  ambacho anaweza kukipata kupitia *148*00# àTigo-Tigo Xtreme/MiniKabangà Wiki au Mwezi + WHATSAPP YA BURE. Huduma hii inapatikana kwa wanaomiliki simu  za aina ya Blackberry, Android na Nokia Symbian60.



WhatsApp ni huduma dada na huduma huduma Facebook ambayo iliingia makubaliano na Tigo mwaka 2014 na kuwapa fursa wateja wa Tigo huduma ya Facebook bure na kwa lugha ya Kiswahili kupitia simu zao.

LHRC Wamtaka Mwenyekiti wa ZEC Kujiuzulu Mara Moja......Chama cha CCK Chamvua Uanachama Katibu Wake Aliyetangaza Kushiriki Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar

$
0
0
Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kimemtaka Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Jecha Salum Jecha ajiuzulu wadhifa huo kutokana na hatua aliyochukuwa ya kufuta uchaguzi na kutangaza tarehe ya kurudiwa bila kufuata sheria hivyo kumemuondolea sifa ya kusimamia na kuongoza tume hiyo.

Tamko hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Bi Imelda Urrio ambapo amesema ukosefu wa taarifa sahihi na rasimi za michakato ya maridhiano toka kufutwa kwa uchaguzi kunaondoa imani ya wananchi juu ya viongozi wao, tume na mchakato mzima wa chaguzi za kidemokrasia Zanzibar.

Amesema kuwa kufutwa na kutangazwa upya kwa uchaguzi wa Zanzibar kunakiuka katiba,sheria,na kanuni za uchaguzi na pia misingi ya demokrasia ya utawala wa  sheria nchini.

Amesema kuwa katiba ya Zanzibar na sheria za uchaguzi hazijampa mamlaka mwenyekiti na hata tume yote kufuta uchaguzi na hivyo kilichotokea Zanzibar kimeaacha watanzania wakiwa hawaelewi ni sheria na katiba ipi imetumika kufuta uchaguzi huo.

Bi Imelda ameongeza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 123 cha sheria ya uchaguzi Zanzibar mtu akishachaguliwa uchaguzi wake hautohojiwa isipokuwa kwa kupeleka shauri mahakamani,hivyo kwa msingi huo LHRC wanaona kwamba hakuna kifungu chochote cha sheria kinachoipa tume ya uchaguzi au mwenyekiti wake mamlaka ya kufuta uchaguzi na kuamuru marudio isipokuwa kwa amri ya mahakama.

Wakati huohuo chama cha kijamii CCK kimemsimamisha kazi na uanachama naibu katibu mkuu wake wa Zanzibar Ali Khatib Ali ambaye pia alikuwa mgombea urais wa Zanzibar kwenye uchaguzi uliotangazwa kufutwa na ZEC Oktoba 2015.

Mwenyekiti wa CCK Costantine Achitanda amesema chama kimefikia maamuzi hayo ili kupisha uchunguzi dhidi yake kufuatia uamuzi wake binafsi wa kutangazia umma kuwa CCK itashiriki uchaguzi wa marudio huko Zanzibar kinyume na taratibu za chama.

Viongozi wa Dini Wazidi Kutofautiana Kuhusu Sakata La Zanzibar.......Sheikh Ponda Issa Ponda Apinga Uchaguzi Kurudiwa Zanzibar

$
0
0
Mgogoro kuhusu kurudiwa kwa uchaguzi viswani Zanzibar unazidi kupasua nchi, sasa viongozi wa Dini ya Kiislam wametofautiana.

Ikiwa ni siku moja baada ya Alhad Mussa Salum ambaye ni Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam kuunga mkono Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar (ZEC) kutangaza tarehe ya uchaguzi visiwani humo, Jumuiya ya Taasisi za Kiislam Tanzania imepinga.

Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu nchini katika mkutano wake na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam amesema, kuruhusu kurudiwa kwa uchaguzi visiwani humo ni kupandikiza mbegu za chuki kwa wananchi.

Sheikh Ponda amesema kuwa uchaguzi uliofanyika Oktoba mwaka jana haukuwa na mashaka kwa kuwa, waangalizi wa nje pia walithibitisha hilo.

“Ripoti za waangalizi wa ndani na nje zilithibitisha kuwa uchaguzi haukuwa na dosari. Kuna sababu gani ya kurudia uchaguzi,” amehoji Sheikh Ponda.

Wakati Sheikh Ponda akihoji sababu za ZEC kutaka kurudiwa kwa uchaguzi huo, Sheikh Alhad aliipongeza tume hiyo na kuongeza “tunaiomba ZEC kusimamia kazi hii kwa haki, uadilifu na umakini mkubwa…”

Sheikh Alhad jana alisema kuwa Baraza la Waislam Tanzania (BAKWATA) linaunga mkono uamuzi wa ZEC kurudia uamuzi huku akikitaka Chama cha Wananchi (CUF) ambacho kimesusia uchaguzi huo, kushiriki.

CUF kwenye mkutano wake wa Baraza Kuu uliofanyika tarehe 27 na 28 Januari mwaka huu kilieleza kususia uchaguzi huo uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi mwaka huu na kudai kuwa, hakuna sababu yoyote kwa chama hicho kushiriki. ZEC ilifuta uchaguzi huo tarehe 28 Oktoba mwaka jana.

Hata hivyo, Sheikh Ponda amesema kuwa, ZEC haikuwa na sababu ya kufuta uchaguzi  kwa kuwa, baada ya tume hiyo kutangaza matokeo, haina mamlaka ya kufuta.

Pamoja na kupinga kurudiwa kwa uchaguzi, Sheikh Ponda Sheikh Alhad amepata wapi kauli ya Kiongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), Sheikh Farid Hadi Ahmed kuwa anaunga mkutano marudio ya uchaguzi Zanzibar.

Sheikh Alhad kwenye mkutano wake jana alisema “Hata kiongozi wa Uamsho, Sheikh Farid Ahmad pia anaunga mkono suala la kufanyika uchaguzi wa marudio kwa mujibu wa barua yake aliyonitumia mimi .”

Sheikh Ponda ameeleza kwamba, Sheikh Farid hawezi kutoa kauli hiyo na kwamba kama Sheikh Alhad anayo barua hiyo, aitoe hadharani.

“Sio jambo rahisi kuamini kwamba Sheikh Farid anaweza kutoa kauli hiyo, sio jambo rahisi kabisa na kama ni kweli basi atoe ushahidi wake,” ameeleza Sheikh Ponda.

Pia Sheikh Ponda ameonesha kushangazwa na ZEC kuhalalisha matokeo ya Rais wa Muungano wa Tanzania sambamba na Wabunge wa Bunge la Muungano.

Shekh Ponda amesema kuwa uchaguzi wa Zanzibar na matokeo yake bado ni halali “Sisi kama Tasisi ya Waislamu tunapinga kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar.”

Amesema kuwa, taasisi hiyo imeunga mkono hatua za mwanzo zilizochukuliwa na CUF pia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kunusuru hali ya kisiasa visiwani humo na kutaka majadiliano yaendelee.

Shekh Ponda amemshauri Rais John Magufuli kutimiza ahadi yake aliyoitoa bungeni ya kushughulikia mzozo huo kwa kushirikiana na Maalim Seif Shariff Hamad na Dk. Ali Mohammed Shein.

Amesema kuwa, Rais Magufuli hajatoa tamko lolote na kwamba hajaeleza amefikia wapi katika kutatua mzozo huu.

Sheikh Ponda amesema kuwa kuna viashiria vya kuvunjika kwa amani visiwani humo kutokana na watu kuporwa haki zao na kwamba watakapoamua kuitafuata kutazuka vurugu.

Mbowe Akiri Kumkosea Zitto.....Amuangukia!

$
0
0
Mh Mbowe
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwenyekiti wa CHADEMA, mhe Mbowe, amemuangukia Zitto na kueleza namna ambavyo yeye na chama chake wamemkosea Zitto wakati huo Zitto akiwa mwanachama na kiongozi wa CHADEMA.

Mbowe ameyasema hayo katika mahojiano na gazeti la Mwananchi na kueleza yafuatayo:

“Hatujawahi kama kambi ya upinzani kumtenga Zitto kwenye kila jambo, yapo mambo tunaweza kulazimika kutengeneza ushirikiano na wabunge hata wa CCM ili kufanya jambo fulani kutekelezeka.

“Kushirikiana na Zitto si jambo la ajabu kama ambavyo umeona tukilifanya. Yapo majeraha mengi ambayo tumeyapitia pande zote (CHADEMA na Zitto) ambayo huwezi kuyatibu kwa siku moja. Yapo ambayo yatapona kulingana na muda. Unaweza kumfanyia mtu kitu kibaya, lakini baadaye ukatambua kuwa umekosea. Chochote katika siasa kinawezekana,” alisema Mbowe.

Zitto alifukuzwa Chadema na kujiunga na ACT Wazalendo Machi 21, 2015 chama ambacho hakina ushirikiano na vyama vinavyounda Ukawa lakini katika siku za karibuni ameonekana kuwa karibu na umoja huo wa wananchi, ikiwa ni pamoja na kushirikiana kuibua hoja mbalimbali katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.
Source: Mwananchi

Jaji Warioba: Kurudia Uchaguzi Zanzibar ni Hatari

$
0
0
Jaji warioba
Akihojiwa na ITV Jaji warioba amesema kurudia Uchaguzi Zanzibar ni hatari na inaweza kupelekea umwagaji wa damu.
Jaji warioba amesema ni vema atafutwe msuluhishi wa katikati na pande zote zirudi mezani.

MyTake: Kama Kada wa CCM amemkataa Jecha, Bado kuna watu wanajitoa ufahamu,muda utawadia..Asiyesikia la mkuu huvujika guu

By Kibo10/JF

Mwigizaji Batuli Amjibu Ray Kigosi...Amtaka Apige Picha Mkataba Unaosema Alipwe Baada ya Mwaka Mmoja Auweke Mtandaoni

$
0
0

Bifu inayoendelea Kati ya Ray na Batuli yazidi Kupamba moto, Batuli amjibu Ray Kama Ifuatavyo;

Haki Ya Mtu Haizami
Swali: Movie Yako Nimecheza Mwaka Juzi Wiki Moja Kabla Ya Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani, Makubaliano Yetu Ya Kazi Kimkataba Ni Siku 10 Tu Lkn Ulienda Kinyume Na Matokeo Yake Nilifanya Kazi Yako Mwezi Mzima Wa Ramadhan Je Ulikuwa Sawa!?
Swali: Pamoja Na Usumbufu Wako Wote Nilifanya Kazi Sikufanya!? Kumbuka Nilikuwa Kwenye Swaumu

Swali: Toka Mwaka Juzi Mpaka Mwaka Jana Ni Mm Ndie Niliekuwa Nafuatilia Malipo Yng Ofisini Sio Chini Ya 20 Times Na Umekuwa Ukinikimbia Matokeo Yake Nikachoka Kuja, Simu Zng Umekuwa Ukizipokea Unapotaka Na Sms Unanijibu Unavyotaka Je Mkataba Wetu Ulisema Hivyo!?

Swali : Naimani Ww Una Mkataba Upo Ofisini Kwako Upige Picha Tuone Kama Upo Unavyodai, Binafsi Kila Mtu Anajua Nyumba Yng Iliteketea Moto Hivyo Sina Kitu Na Ndio Maana Umekuwa Ukinitendea Unyama Huu Je Kuna Anaeweza Kukaa Kimya Zaidi Ya Mwaka Mmoja Na Hatimae Unaona Kazi Inatoka Wakati Hujalipwa!?

Swali : Ni Movie Ngapi Nilizofanya Kwenye Kampuni Yako Chini Ya Johari!? Ni Zaidi Ya 3 Je Nililalamika!? Kwanini Hii Ambayo Johari Hakuwepo Nikaingia Mkataba Na Ww Iweje Nilalamike!?
Dhulma Itakufikisha Pabaya Sana, Tambua Nilifanya Kazi Yako Ktk Mazingira Magumu, Nilikuwa Kwenye Swaumu Baba Nilifuturu Mabarabarani Chipsi Na Vingine Visivyo Rasmi Yote Ni Ktk Kutimiza Kazi Yako,

Nionyeshe Mkataba Unaosema Nilipwe Baada Ya Mwaka 1 Na Kuendelea Hakika Umeonyesha Ulivyo Na Roho Ya Dhulma Sijawahi Kulalamika Popote Kuhusu Unachonifanyia Kwa Sbb Nilijua Ipo Siku Utanilipa Changu Matokeo Yake Umeona Ujivishe Ujemedari Lakini Haitokisaidia Chochote, Kama Haki Yng Basi Itanifuata Hata Nikiwa Kaburini....Be Blessed....Allah Bariq

Nay wa Mitego Aweka Wakili Kuwakabili Bongo Movie Mahakamani

$
0
0
Hivi juzi kati kupitia akaunti yake ya Instagram,Nay Wa Mitego alipost mashairi yenye ‘utata’ ya ngoma yake mpya yakiwalenga wasanii wa Bongo Movie,baadhi ya wasanii hawakupendezwa na mashairi hayo:

Nay aliandika mshairi haya;

“Mungu akunyimi vyote lazima atakupa chako, Demu anasura mbayaa lakini ana Bonge la Tako.
BongoMovie Imekufa wamebaki kuuza Sura, Wote wanataka Kuimba Kama Shilole Snura.
 Ray Kigo kawa Mkongo Mpaka Leo anaishi kwao, hela za kuuza Movie zote ananunua Mkorogo😎.
Kuna Nivar super Marioo ana Gari la Milioni Kumi ajawai ata miliki Getto, anaishi kwa Mademu wakiachana Gari ndio Geto.
Kuna Wasanii Mapunga walio ponzwa na tamaa… #ShikaAdabuYako...
Haitoki hii nimeirecord tu yakusiliza na wanangu maskaniiiii....maana mtanichukia kwa niliyozungumza umuuu..

Kajala akafunguka;

’Nyie mnacheka mnaona sifa huyo anatukana anafanya nini… wakati sisi tunauwezo wa Bongo Movie wote kumshtaki hawezi kututukana hivyo yeye ni nani? Mnakaa mnadhalilishwa mnafurahi,’’ Kajala.

Nay akasema tena;

‘’Nimesikia kuwa Bongo Movie wana mpango wa kunipeleka mahakamani nimeongea na wakili wangu kaniambia tutashinda kesi…halafu Kajala namuheshimu sana kama mama yangu…Nimemsikia alichosema nasubiria wanipeleke mahakamani…,’’

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Februari 4, Ikiwemo ya Msekwa Kusema CCM imepoteza Sifa za Asili

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Februari 4, Ikiwemo ya Msekwa Kusema CCM imepoteza Sifa za Asili

Viewing all 104745 articles
Browse latest View live




Latest Images