Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104694 articles
Browse latest View live

Msichana Mtanzania Anayesoma India Amepigwa, Kuvuliwa Nguo na Kisha Kulazimishwa Kutembea Akiwa uchi

$
0
0
Mtanzania anayesoma India amepigwa, kuvuliwa nguo na kisha kulazimishwa kutembea akiwa uchi na kundi la watu nchini humo.

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 21 (jina linahifadhiwa) anayesoma shahada ya biashara, mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Acharya, Bangalore, alifanyiwa ukatili huo akiwa na Watanzania wengine wanne.

Gazeti la Deccan Chronical la Bangalore, liliripoti kuwa tukio hilo lilitokea Januari 31, baada ya mwanafunzi raia wa Sudan, Ismail Mohammed kugonga gari la raia mmoja wa India, mkazi wa Hesaraghatta aliyekuwa na mkewe na kusababisha kifo cha mama huyo.

Nusu saa baadaye, Watanzania watano akiwamo aliyevuliwa nguo, walifika katika eneo hilo wakiwa kwenye gari ndipo kundi la watu hao lilipoanza kumshambulia binti huyo, kisha kumvua nguo na kumlazimisha atembee uchi.

Baada ya kuchoma gari lililosababisha ajali hiyo, kundi hilo pia liliteketeza gari alilokuwamo Mtanzania huyo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Mindi Kasiga alisema Balozi wa Tanzania nchini humo, John Kijazi ameshakutana na wanafunzi hao na ameshazungumza na Serikali ya India kuhusu tukio hilo.

Gazeti la Deccan Chronical liliripoti kuwa licha ya polisi waliokuwapo eneo hilo hawakuchukua hatua yoyote hata pale msamaria mwema aliyejitokeza kumsitiri msichana huyo kwa fulana yake ambaye pia alipigwa huku fulana hiyo ikichanwa.

Mshauri wa masuala ya sheria kwa wanafunzi kutoka Afrika wanaosoma Bangalore, Bosco Kaweesi alinukuliwa na gazeti la The Chronical akisema hata dereva wa gari alilokuwa  Mtanzania huyo, Micah Pundugu alipigwa na kujeruhiwa vibaya.

 Alisema hata pale msichana huyo alipojaribu kupanda basi ili kujinusuru na zahama hiyo, abiria walimshusha.

Nay wa Mitego Asababisha Ugomvi Mkubwa Bongo Flava na Bongo Movies...

$
0
0

Nay wa Mitego 
Kimenuka! Harufu ya damu inanukia ndani ya tasnia za Bongo Movie na Bongo Fleva, Mbongo Fleva Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amewachana vibaya mastaa wa filamu ambao nao wameshindwa kuvumilia, wameibuka na kujibu mapigo.

Nay ndiye aliyeanzisha chokochoko za ugomvi huo baada ya kuposti picha yake katika Mtandao wa Instagram na kusindikiza na ujumbe uliokuwa na mlengo wa kuwaponda mastaa wa Bongo Movie, mwishoni mwa wiki iliyopita:

“…Bongo Movie imekufa, wamebaki kuuza sura, wote wanataka kuimba kama Shilole na Snura, Ray Kigo kawa Mkongo mpaka leo anaishi kwao, hela za kuuza muvi zote ananunua mkorogo, kuna Nivar Super marioo, ana gari la milioni kumi, hajawahi miliki hata geto…”

Baada ya kuweka ujumbe huo ambao ulionesha wasanii wa filamu hawana maendeleo, wasanii mbalimbali wa Bongo Movie waliibuka mtandaoni humo na kusema kuwa Nay amechokoza.Wasanii wengine walimjibu kwa matusi huku baadhi yao wakiahidi kumburuza mahakamani.
Kajala Masanja hakuwa nyuma, alifunguka:

“Hivi huyu kwa nini tusimshtaki? Amezidi anajifanya kuponda Bongo Movie wakati hukuhuku ndiyo anafuata wanawake. Anatudhalilisha tumchukulie hatua.”

Jitihada za kuwapata Ray (Vincent Kigosi) na Nivar ili wazungumzie ishu hiyo hazikuzaa matunda baada ya simu zao kuiita bila kupokelewa.

Kwa upande wake Nay alipoulizwa na mwanahabari wetu sababu ya kufanya hivyo, alisema hajutii kuandika maneno hayo kwani yapo kwenye wimbo wake mpya uitwao Shika Adabu Yako ambao ameelezea vitu anavyoamini ni vya kweli.

Mwenendo wa Bunge wa Kurushiana Vijembe na Meneno ya Kejeli Wamchefua Mwanasheria Mkuu..Atoa Onyo

$
0
0
Mwanasheria  Mkuu wa Serikali, George Masaju amewataka wabunge kusimamia utekelezaji wa sheria wanazotunga na si kuhamasisha uvunjaji wa sheria za nchi.

Alitoa kauli hiyo jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji (CUF).

Mbunge huyo alihoji kwa nini serikali haiwachukulii hatua watu wanaofanya uhalifu Zanzibar na kama wameshindwa, wananchi wawaadhibu wahalifu hao kwa kuwapiga mawe.

Pia Mbunge huyo alitaka Waziri wa Mambo ya Ndani atamke kama wameshindwa kudhibiti uhalifu huo, wananchi washughulikie wahalifu hao kwa kuwapiga mawe na magari yao.

Akijibu swali hilo mwanasheria mkuu wa serikali, alisema hoja ya Mbunge huyo sio sahihi na kusisitiza, “Waziri hawezi kutamka watu wavunje sheria, wabunge wanatunga sheria wanatakiwa kusimamia utekelezaji wake”.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angelah Kairuki alisema kuhusiana na hoja kuwa vyombo vya dola vinakiuka haki za binadamu, endapo mbunge huyo ana malalamiko awasilishe kwenye tume ya haki za binadamu ili yapate kushughulikiwa.

Mbunge wa Rombo, Joseph Selesini (Chadema) katika swali la nyongeza alihoji kwa kuwa matukio ya wananchi kuchukua sheria mkononi yanasababishwa na mambo mawili, ikiwemo polisi kwenda kwenye tukio wakiwa wamechelewa na wahalifu wanapokamatwa baada ya muda wanaachiwa.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni alisema Jeshi la polisi linajitahidi kufanya kazi, idadi ya polisi haitoshelezi kutokana na polisi mmoja kuhudumia watu 300 hadi 350.

“Wakati mwingine inatokea baadhi ya polisi wana mapungufu na wamekuwa wakichukuliwa hatua za kisheria na wale wanaotenda makosa ya jinai sheria imekuwa ikifuata mkondo wake,” alisema.

Upendeleo wa Ajira Watoto wa Vigogo: Mahakama Yawaachia Huru Watoto wa Vigogo BOT Waliokutwa na Vyeti Feki

$
0
0
Bank kuu ya Tanzania
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewaachia huru watoto wanane wa vigogo waliokuwa wameshitakiwa wakidaiwa kupatiwa ajira katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kutumia vyeti vya kughushi, baada ya kutowakuta na hatia.

Walioachiwa huru ni Justina Mungai, Christina Ntemi, Siamini Kombakono, Janeth Mahenge, Beatha Massawe, Jacqueline Juma, Philimina Mtagurwa na Amina Mwinchumu.

Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema, aliwaachia huru washitakiwa hao jana, alipokuwa akisoma hukumu ya kesi hiyo iliyochukua takribani miaka minane.

“Mahakama hii imewaona washitakiwa hawana hatia na kuwaachia huru kutokana na upande wa jamhuri kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao pasi na kuacha shaka yoyote,” alisema.

Alisema wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, upande wa jamhuri ulileta mashahidi sita na vielelezo kadhaa na baada ya washitakiwa kuonekana wana kesi ya kujibu walijitetea wenyewe na kuleta vielelezo.

Alisema ni jukumu la upande wa jamhuri kuthibitisha mashitaka pasi na kuacha shaka yoyote na kwamba sio jukumu la mshitakiwa kuthibitisha kosa hilo.

Hakimu huyo alisema wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo, upande wa jamhuri uliwasilisha nakala za vyeti na kwamba ulishindwa kuwasilisha vyeti halisi kuonesha kipi halali na kipi cha kughushi.

Hakimu huyo alisema pia baada ya kufunga ushahidi pande zote ziliomba kuwasilisha hoja za kisheria iwapo zinaona washitakiwa wana hatia ama la, lakini hadi mahakama inatoa hukumu hakuna upande hata mmoja uliofanya hivyo.

Alisema upande wa jamhuri haukuleta shahidi aliyetengeneza vyeti hivyo badala yake walileta nakala tu za vyeti, hivyo upande wa jamhuri umeshindwa kuthibitisha mashitaka pasi na kuacha shaka yoyote.

Alisema upande wa jamhuri kama walikuwa na nia ya kuthibitisha kesi wangemleta mtaalamu wa maandishi ambaye angethibitisha iwapo vyeti hivyo vilikuwa vya kughushi ama la badala yake imebaki hisia tu.

Hakimu huyo alisema mahakama hiyo imesikiliza ushahidi wa kuhisi, kwa upande wa jamhuri kushindwa kuthibitisha mashitaka, hivyo imewaona washitakiwa hawana hatia na kuwaachia huru.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, washitakiwa hao walikuwa wakidaiwa kughushi vyeti vya kuhitimu kidato cha nne na kutoa hati za uongo kwa mwajiri wao ambaye ni BoT.

Ali Kiba Azinduka..Kuzindua Wimbo wake Mpya Unaoitwa Lupela Slipway leo

$
0
0
Ali Kiba
Video ya wimbo mpya wa Alikiba, Lupela itazinduliwa rasmi Alhamis hii kwenye hoteli ya Slipway jijini Dar es Salaam.

Tayari kadi za mialiko zimeanza kutolewa. Video pamoja na uzinduzi huo vimesimamiwa na Wild Aid ambayo Kiba ni mmoja wa mabalozi wake.

Video ya wimbo huo ilifanyika jijini Los Angeles, Marekani mwaka jana.

Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea Afunguka Mazito Kuhusu Suala la Uchaguzi Zanzibar..'Nchi yetu itafika Pabaya'

$
0
0


Kubenea ameyasema hayo alipokuwa akichangia hoja ya mpango wa maendeleo bungeni kwenye kikao cha 7 bunge la 11, na kusema kuwa suala la Zanzibar lisipochukuliwa hatua makini, litaipeleka nchi pabaya.

“Uchaguzi wa Zanzibar utatuletea matatizo makubwa kitaifa tusipokuwa makini, hakuna namna yoyote katika bunge hili ya kutozungumzia suala la Zanzibar, iwapo matatizo ya Zanzibar yasipotatuliwa kwa makini, mpango huu hautatekelezeka”, alisema Saed Kubenea.
Pia Saed Kubenea amesema watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini na mashirika m
balimbali ya kijamii yanaliona suala hilo, lakini wao kama wabunge hakuna ambaye amethubutu kuliongelea.

“Tunakaa kaa tu humu ndani, wakati maaskofu wanasema Zanzibar kuna tatizo, mashekhe wanaliona tatizo, tukajifanya hakuna matatizo, nchi yetu itafika pabaya na mpango wa maendeleo hautatekelezeka”, alisema Saed Kubenea

Mume Amcharanga Mke Wake Kwa Panga Sehemu Mbali Mbali Kisa Sh 5,000 ya Matumizi

$
0
0
Mkazi wa kijiji cha Buhembe, mkoani mara, Martha Hussein 'Bhoke' amecharangwa na panga sehemu mbalimbali za mwili wake na mume wake kwa kutumia Sh 5,000 ya matumizi ya nyumbani kwa kumnunulia babu yake blanketi. Bhoke alishambuliwa shingoni, mikono yake yote na kumchoma kisu shingoni huku akimtaka amrudishie sh 5,000 zake ama sivyo mwisho wa maisha yake umefika.
Unadhani ni sahihi kumjeruhi mpenzi wako kwa matumizi mabaya ya hela?

Maalim Seif Sharif Hamad Amshushia Tuhuma Nzito Jakaya Kikwete..Adai Yeye Ndio Amevuruga Uchaguzi wa Zanzibar

$
0
0
Katibu Mkuu wa (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ametoa madai mazito kuwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar mwaka jana yalipinduliwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha, baada ya kupata baraka za Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.

Alisema, saa chache kabla ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kutangaza kufuta uchaguzi huo, kituo kikuu cha kutangazia matokeo kilichokuweko Hoteli ya Bwawani kilizingirwa na vikosi vya jeshi na polisi na kwamba kitendo hicho kuwa ni “Mapinduzi ya Kikatiba”.

“Aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wakati ule alikuwa Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete na ndiye aliyepeleka vikosi vile baada ya kuona chama chake kimeelekea kushindwa kwa upande wa Zanzibar,” alisema Maalim Seif na kuongeza;
“Dkt. Shein wala Balozi Seif (Seif Ali Idd) hawamiliki jeshi wala polisi, vile ni vikosi vya Dk. Kikwete wakati ule na hawezi kukwepa lawama ya kuingilia uchaguzi wa Zanzibar.”

Maalim Seif pia amewashutumu baadhi ya viongozi wakiwemo wa dini wanaojaribu kupotosha ukweli na kuunga mkono uamuzi batili wa kurejewa uchaguzi uliotangazwa na ZEC.

Unaichukuliaje kauli hii ya Maalim Seif?

Azam FC yachukua kombe la Michuano Maalum Zambia

$
0
0
Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imetwaa ubingwa wa michuano maalumu iliyomalizika jijini Ndola Zambia baada ya kutoa suluhu dhidi ya Zanaco FC ndani ya Uwanja wa Levy Mwanawasa.

Sare hiyo imeifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi tano sawa na washindi wa pili Zanaco, lakini imewazidi washindi wa pili hao wa Ligi Kuu Zambia, kwa wastani wa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Azam FC kama ingekuwa makini kwenye mchezo huo huenda ingejiandikia bao la uongozi dakika ya 8 baada ya kufanya shambulizi kali langoni mwa Zanaco, lakini shuti alililopiga Kipre Tchetche nje kidogo ya eneo la 18, lilipanguliwa na kipa na kuwa na kona ambayo haikuzaa matunda.
Licha ya juhudi za Zanaco FC nao kutaka kupata bao kwa kufanya mashambulizi kadhaa, safu ya ulinzi ya Azam FC na eneo la kiungo lilikuwa makini kuondoa hatari zote.
Azam FC ilipoteza nafasi nyingine dakika ya 41 baada ya beki Shomari Kapombe kuingia vizuri kwenye eneo la 18 la Zanaco akipokea pande safi la Tchetche, lakini shuti alilopiga lilitoka sentimita chache ya lango.

Hivyo hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza kinamalizika timu zote ziliweza kutoshana nguvu kwa kutofungana, ambapo kipindi cha pili kilianza kwa Azam FC kufanya mabadiliko matatu, akitoka beki Pascal Wawa na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo Jean Mugiraneza mwenye uwezo wa kucheza nafasi zote za ulinzi uwanjani kasoro golini.

Wengine waliotoka kwa upande wa Azam FC ni nahodha John Bocco ‘Adebayor’ na kuingia Allan Wanga, pia alitoka Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na kuingia Mudathir Yahya, mabadiliko ambayo yalisaidia kuimarisha zaidi eneo la kiungo na Azam FC kumiliki sehemu kubwa ya mchezo.

Dakika ya 72 Allan Wanga alishindwa kutumia vema pasi ya Domayo baada ya kuchelewa kufunga bao akiwa anatazaman na kipa wa Zanaco kufuatia mabeki kumuwahi na kuokoa hatari hiyo, dakika mbili baadaye Azam FC ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Thetche na kuingia Ame Ally ‘Zungu’.
Kutokana na Azam FC kuhitaji sare tu au ushindi katika mchezo huo ili kuibuka mabingwa, ilibadilisha mchezo kuelekea dakika 20 za mwisho na kucheza soka la kujilinda zaidi na hadi dakika 90 zinamalizika iliweza kutimiza lengo lake hilo.

Mara baada ya mchezo huo kumalizika timu zote mbili zilipata fursa ya kupongezana pamoja na kusalimiana na waamuzi, kuashiria kutimiza sheria ya kiungwana mchezoni ya ‘Fair Play’.
Wakati Azam FC ikiwa inashiriki kwa mara ya pili michuano hiyo, kihistoria timu ya Power Dynamos ya Zambia ndio timu ya kwanza kutwaa ubingwa huo mwaka juzi kabla ya mwaka jana kuchukuliwa na TP Mazembe, ambayo ilienda kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.
Azam FC kutwaa ubingwa huo kunaifanya izidi kujiongezea mataji waliyotwaa msimu huu tokea kurejea kwa Kocha Stewart Hall, kufuatia Agosti mwaka jana kutwaa taji la michuano ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Kagame Cup).

Kikosi cha Azam FC kinatarajia kuanza safari ya kurejea Tanzania leo usiku na kitawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl Nyerere (JNIA) hapo kesho Alfajiri.

Kikosi Azam FC kilikuwa;Aishi Manula, Ramadhan Singano ‘Messi’, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Abdallah Kheri, Pascal Wawa/Mugiraneza dk45, Michael Bolou, Frank Domayo, Salum Abubakar/Mudathir dk45, Kipre Tchetche/Ame Ally dk74 na John Bocco/Allan Wanga dk45

Uchaguzi Mameya Kinondoni na Temeke sasa Kurudiwa

$
0
0
Uchaguzi wa umeya katika Manispaa za wilaya za Temeke na Kiondoni utarudiwa baada ya kugawanywa na kuzaa wilaya za Ubungo na Kigamboni.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene, alisema Rais John Magufuli ameridhia kuanzishwa kwa wilaya hizo pamoja na mkoa mpya wa Songwe.

Aidha, alisema ameridhia kuanzishwa kwa wilaya mpya ya Kibiti (Pwani), Malinyi (Morogoro) na Tanganyika (Katavi).
Alisema mchakato wa kuanzishwa kwa maeneo mapya ya utawala ulihitimishwa kwa kutolewa na tangazo la serikali kwa GN 69 ya Januari 29, mwaka huu, ya kuanzisha kwa mkoa wa Songwe na GN namba 68 ya kuanzishwa kwa wilaya za Songwe, Kibiti, Ubungo, Kigamboni, Malinyi na Tanganyika.

Simbachawene alisema Mkoa wa Songwe umeanzishwa kwa mujibu wa sheria, hivyo hivyo kwa wilaya za Songwe, Kibiti, Ubungo, Kigamboni, Malinyi na Tanganyika.
Kuhusu uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, alisema utarudiwa Februari 8, mwaka huu.
Alisema baada ya kugawanywa kwa wilaya hizo ni dhairi kuwa, baadhi ya madiwani itabidi wakae kwenye halmashauri zao ambazo zinaanzishwa.

Alisema hivi karibuni atateua wakurugenzi wa halmashauri hizo na baadhi ya watendaji muhimu.
Simbachawene alisema amewaagiza wakuu wa mikoa wote ambao katika mikoa yao imeanzishwa wilaya mpya kufanya maandalizi muhimu ili kuwezesha mikoa na wilaya hizo kuanza rasmi.
Katika agizo hilo, ameweka mkazo uwekezwe kwenye upatikanaji wa majengo ya ofisi na huduma muhimu ili kuweka mazingira ya shughuli za kiutawala kuanza kufanyika katika maeneo hayo ya kiutawala.

Nuhu Mziwanda Afikwa na Maji Shingoni...Ampigia Shilole Magoti

$
0
0
STAA wa Wimbo wa Msondo Ngoma, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, anasemekana amemwangukia kwa mara nyingine aliyekuwa mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kwa kumtaka warudiane. 

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Mbongo Fleva huyo amekuwa katika
wakati mgumu tangu alipoachana na Shilole hivyo kulazimika kumpigia simu na kumwandikia ujumbe wa maneno akimuomba amsamehe na warejeshe penzi lao kama ilivyokuwa zamani.
 “Ndugu yangu nikikwambia kuwa, Nuh maji yamemfika shingoni basi huna haja ya kuuliza mara mbili namna yalivyomfika kwani, juzikati nilikuwa naongea na Shilole akalalamika kwamba, jamaa huyo ameanza tabia ya kumpigiapigia simu akimwomba warudiane jambo ambalo Shilole analitolea nje,” kilisema chanzo hicho.
 Baada ya kupenyezewa ubuyu huo, paparazi wetu  alimtafuta Shilole kwa nia njema ya kutaka kujua ukweli wa madai hayo ambapo alisema ishu hiyo ipo ila hawezi kuanika wazi. “Suala la Nuh kwa sasa sitaki kuendelea kuongea kwani nitakuwa nampigia debe mtu na kazi hiyo niliifanya sana. Unachotakiwa kujua kutoka kwangu ni kwamba mimi naendelea kupigania maisha tu ili niweze kusonga mbele na hapa nipo kipesa zaidi hivyo sina tena muda wa kuendelea kumpa nafasi bwana wa aina yeyote kwani hapo nyuma maisha yangu yalirudi nyuma hatua nyingi sana,” alisema Shilole.

Pius Msekwa Asema CCM imepoteza Sifa Ya Kuwa Chama Cha Wanyonge

$
0
0
Wakati kesho CCM ikiadhimisha miaka 39 tangu kuzaliwa kwake, kada mkongwe na muasisi wa chama hicho, Pius Msekwa amechambua uwezo na udhaifu wake, akibainisha kuwa kimepoteza sifa ya asili ya kuwa chama cha wanyonge.

Msekwa amesema   kuwa matukio mbalimbali yanayokikumba chama hicho, ikiwamo migogoro baina ya viongozi wake, makundi na tuhuma za ufisadi, yameathiri taswira yake kwa jamii.
Msekwa  ambaye ni katibu mkuu wa kwanza wa Tanu na makamu mwenyekiti mstaafu (Bara), alibainisha kuwa CCM imepoteza sifa yake ya asili ya kuwa chama kinachojali wanyonge na kubebeshwa mzigo wa kuitwa “chama cha matajiri”.

“Migogoro miongoni mwa viongozi, hususan baina ya makundi yanayozozana au kuhasimiana ndani ya chama na tuhuma za ufisadi, imechangia kuifanya CCM ibebeshwe mzigo wa kuonekana kuwa ni chama kinachokumbatia mafisadi,” alisema.

Aliongeza kuwa CCM pia imeathiriwa na kujipenyeza kwa kasi kubwa kwa wafanyabiashara wasio waadilifu katika baadhi ya vikao vyake vya uamuzi.
Hata hivyo, Msekwa alisema ujio wa Rais John Magufuli umeleta matumaini mapya miongoni mwa wananchi juu ya taswira ya chama hicho.

“Nafarijika kwamba uongozi mpya wa Rais anayetokana na CCM, Dk John Magufuli umeleta matumaini hayo mapya miongoni mwa wananchi walio wengi,” alisema.

Alieleza kuwa CCM kupitia viongozi wake, haina budi kuonyesha kwamba inaweza kuleta mabadiliko yenye tija na yenye kuleta matumaini mapya miongoni mwa wananchi walio wengi.
Alisema ukongwe wa chama hicho kwa maana ya kuwa kimekuwapo na kimekuwa madarakani mfululizo tangu nchi ilipopata uhuru wake mwaka 1961, una faida na hasara zake.

“Faida ni kwamba kwa sababu ya uzoefu wake huo wa miaka mingi, kina (CCM) fursa kubwa ya kuendesha shughuli zake vizuri na kuendelea kupata ushindi katika chaguzi zijazo,”alisema.

Alibainisha pia kuwa kitendo cha CCM kuwapo madarakani muda mrefu kinaweza kusababisha hatari inayotokana na hulka ya binadamu.
Alifafanua kuwa wakati mwingine watu wanaweza kutaka mabadiliko tu ya uongozi wa nchi hata kama chama kilichopo madarakani kinafanya vizuri kiasi gani.

“Hatari iliyopo ni watu wanaweza kuchoka tu kuendelea kuwa chini ya uongozi wa chama kilekile na hatari hiyo inakuwa kubwa zaidi pale matendo ya viongozi wake yatakapokuwa mabaya kiasi cha kuwaudhi watu,”alisema. 

Msekwa alisema katika kipindi hicho cha uhai wa CCM, maadili ya viongozi yameporomoka kwa kiwango kikubwa.
Alitaja sababu za kuporomoka kwa maadili kuwa ni pamoja na kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini na ushindani mkali wa kuwania kushika dola uliojikita katika mfumo huo.
Alisema hali hiyo pia inatokana na hatua ya kusitishwa kwa mafunzo ya viongozi, makada na watendaji wa chama hicho yaliyokuwa yakitolewa kwenye vyuo mbalimbali.

“Hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na kusitishwa kwa ruzuku iliyokuwa inatolewa na Serikali kwa chama kwa ajili ya kuendesha mafunzo hayo, katika vyuo vya chama vya Kivukoni na vyuo vyake sita vya kanda vilivyokuwa mikoa mbalimbali,”alisema.

Alisema kutokuwapo kwa msaada wa mafunzo ya maadili na uadilifu kwa viongozi, pia kulichangia kuporomosha maadili ndani ya chama.

“Hapo ilibidi kila kiongozi alazimike kutumia akili zake tu katika shughuli zake za uongozi. Kama wasemavyo Waswahili; akili ni nywele, kila mtu ana zake,” alisema.
Alieleza pia kuwa ushindani katika mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini, umesababisha kukithiri rushwa katika uchaguzi.
Alisema hili hujitokeza wakati wa kura za maoni ndani ya CCM ambako baadhi ya makada wake wameanza tabia ya kuwashawishi wapigakura kwa rushwa ili wachaguliwe katika nafasi wanazozitafuta.

Alisema yapo mambo muhimu ya kuzingatia, wakati wa kutafakari chama hicho kilikotoka na kwamba katika kipindi chote hicho kimekuwa kikipata ushindi unaopanda na kushuka katika chaguzi zote zilizofanyika chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa. 

Mbunge Jesca Kishoa Ambaye ni Mke wa Kafulila Atimuliwa nje ya Ukumbi wa Bunge

$
0
0
Mbunge wa Viti maalum Chadema Jesca Kishoa ametolewa nje ya ukumbi wa bunge na kutakiwa kutohudhuria vikao viwili vya bunge linaloendelea mjini Dodoma.

Hayo yamejiri katika mkutano wa 7 wa bunge la 11 linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma ambapo Mwenyekiti wa kikao cha leo Andrew Chenge amelikumbusha bunge kuhusiana na kauli aliyoitoa mbunge huyo tarehe 01/02/2016.

Mbunge huyo alisema kwamba Waziri Harrison Mwakyembe alihusika kununua mabehewa feki 274 jambo ambalo lilizua mjadala mkali na bunge kumtaka mbunge huyo atoe ushahidi ndani ya siku 3.

Mwenyekiti Andrew chenge amesema kuwa mbunge huyo alitakiwa kwa mujibu wa kanuni za bunge kanuni ya 63(6) atoe ushahidi kwa ofisi ya bunge na ndani ya siku zote ofisi ya bunge haijapata ushahidi huo.

Kutokana na Mbunge huyo ambaye pia ni mke wa aliyekuwa mbunge wa Kigoma kusini David Kafulila NCCR Mageuzi kushindwa kutekeleza maamuzi ya bunge mwenyekiti wa bunge amemtaka kufuta kauli yake na mbunge huyo akakaidi ndipo Mwenyekiti akamuamuru atoke nje mara moja na kutohudhuria vikao vya bunge kwa siku zilizobakia 2.

January Makamba 'Wapinzani Mnaolaumu Kazi ya Rais Magufuli Mngepewa Nafasi ni Kipi Mngefanya zaidi ya Hiki?'

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba amefunguka na kusema kuwa wao kama Chama cha Mapinduzi ndiyo wenye dola na wao ndiyo wanaongoza serikali hivyo amewataka baadhi ya wabunge wa upinzani kuwa na lugha nzuri dhidi ya serikali ili waweze kupata ushiriakiano mzuri na viongozi hao pamoja na serikali hiyo pindi watakapo hitaji msaada wowote kutoka serikalini.

January Makamba amesema hayo bungeni na kudai amefadhaishwa na michango ya wabunge wa upinzani ambao walikuwa wakitumia lugha za kuudhi dhidi ya Rais pamoja na viongozi wa serikali.
"Najua kazi ya upinzani ni kulaumu hivi nyinyi wapinzani kwa kazi anayofanya Rais Magufuli leo mngepewa nafasi wapinzani ni kipi ambacho mngefanya zaidi ya hiki? Alihoji January Makamba

Lakini katika hatua nyingine amesema aina ya uchangiaji nyingine ya wabunge bungeni ni kama walikuwa wakiwatisha watanzania juu ya sakata la Zanzibar na alimaliza kwa kusema kuwa utatuzi wa suala la Zanzibar haupatikani barabarani, haupatikani bungeni bali unapatikana katika Katiba na sheria za Zanzibar pekee na si kitu kingine.

Serikali Yazungumzia Tukio la Mwanafunzi wa Kitanzania Kudhalilishwa Kwa Kuvuliwa Mguo Mbele za Watu India

$
0
0
Serikali imesema kuwa inaendelea kufatilia ili kuchukua hatia zaidi juu ya matukio yalitokea nchini India katika chuo cha Acharya Bangalore, ikiwemo la mwanafunzi wa Kike kudhalilishwa kwa kuvuliwa nguo.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Agustino Maige

Akitoa tamko la Serikali leo Bunge Mjini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Agustino Maige amesema tayari serikali imeshapeleka dokezi la kidiplomasia kwa serikali ya india ili kuonyesha kukasirishwa na kitendo hicho.

Balozi Maige ameongeza kuwa tayari wameitaka serikali ya India kuchukua hatua za kipolisi kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na kupeleka ulinzi wa kutosha katika maeneo wanaoishi wanafunzi hususani wa kitanzania ambapo leo kumeri kwa mtu anaesadikiwa kuwa mtanzania kufariki katika mazingira ya kutatanisha.

Kwa upande wa baadhi ya wabunge wameiomba serikali kuwa na tamko rasmi la kuonyesha kuchukizwa na ubaguzi kwa watanzania pindi waendapo kuishi nje ya Tanzania.

Tukio hilo limekuja baada ya Gazeti la Deccan Chronical la Bangalore kuripoti kuwa tukio hilo limetokea baada ya mwanafunzi raia wa Sudan, Ismail Mohammed kugonga gari la raia mmoja wa india mkazi wa Hessaraghata aliekuwa na Mkewe na kusababisha kifo cha mama huyo.

Wakati huo huo Wanaume wanne wanaotuhumiwa kuhusika katika kumshambulia na kumvua nguo mwanafunzi wa kike kutoka Tanzania wamekamatwa, shirika la habari la AP limeripoti.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa India Sushma Swaraj, aliandika kwenye Twitter kwamba amesikitishwa sana na “kisa hicho cha aibu” kilichotokea Jumapili eneo la Bangalore.

Sikiliza Hapa Wimbo Mpya wa Ali Kiba Unaitwa Lupela

$
0
0

Sikiliza Hapa Wimbo Mpya wa Ali Kiba Unaitwa Lupela

Picha: Diamond Asaini Dili Nono na Vodacom, Zari Amsindikiza Kusaini

$
0
0
Diamond Platnumz amesaini dili nono na kampuni ya Vodacom.


Kutoka Kushoto: Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Ian Ferrao, Diamond, Zari, Babutale na mmoja wa maafisa wa juu wa kampuni hiyo

Hitmaker huyo alisindikizwa na mchumba wake Zari the Bosslady kwenye tukio hilo lililofanyika leo jijini Dar es Salaam. Haijulikani ni mkataba wa muda gani na atalipwa shilingi ngapi lakini vyanzo vimesema Diamond amevuta mkwanja mrefu.
“Closed the deal with Vodacom…watch this space! @ianferrao,” aliandika meneja wake, Babutale.
Kwa kuanza Diamond atahusika kwenye promotion mpya ya kampuni hiyo iitwayo Ongea Deilee.

AUDIO: Msikilze Hapa Rais John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa Maadhimisho ya siku ya Sheria nchini.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Mahakimu na Majaji wa Mahakama ya Tanzania kufanya kazi kwa kuzingatia weledi wa taaluma ya Sheria katika kushughulikia mashauri  yanayopelekwa Mahakamani.

Aidha amewataka Majaji na Mahakimu kutoa hukumu za mashauri  yanayowasilishwa Mahakamani kwa haraka ili kuwasidia wananchi wanaotafuta haki.

Akizungumza na mamia ya wageni kutoka ndani na nje ya nchi waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya sheria, Dkt. Magufuli amewataka Majaji na Mahakimu hao kutanguliza Uzalendo na maslahi ya taifa mbele pindi wanapotoa maamuzi ya mashauri yaliyoko Mahakamani.

 Mhe. Rais amemtaka Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  kuchukua hatua kwa watendaji wa Mahakama wanaokiuka maadili kwa kufanya vitendo vinavyochafua taswira ya Mahakama mbele ya macho ya jamii.

Aidha, Katika hotuba yake Mhe. Rais amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuijengea uwezo wa kifedha Mahakama ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Bofya  Hapa  Kumsikiliza  Rais  Magufuli  akihutubia

Edward Lowassa Aunga Mkono Maamuzi Ya CUF Kutoshiriki Uchaguzi Zanzibar

$
0
0
Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananch UKAWA, Mh. Edwrad Lowassa amesema ni vema serikali ikahakikisha inapata suluhu ya mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio machi 20 mwaka huu.

Mh. Edward Lowassa amesema hayo ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam wakati wa kikao chake na wazee kutoka chama cha Chadema ambapo amesema  anaunga mkono uongozi wa CUF kutokushiriki uchaguzi huo huku akisisitiza endapo serikali ikishindwa kumaliza mgogoro huo kabla ya mach 20 huenda hali ya kisiasa Zanzibar ikabadilika.

Aidha amewahakikishia wazee hao kuwa yeye na uongozi mzima wa UKAWA wako imara katika kuhakikisha wanatetea maslahi ya watanaznia ambapo pia amemshukuru waziri mkuu kwa kuruhusu mikutano suala ambalo linawapa fursa ya kujipanga ili kuwashukuru watanzania waliojitokeza kupiga kura mapema 25.

Kwa mujibu wa risala ya wazee hao iliyosomwa na mzee Enec Ngombare,wamempongeza Mh. Lowassa kwa  uvumilivu wake baada ya uchaguzi ambapo pia wamemhakikishia kuwa wako pamoja nae katika safari ya kuelekea mwaka 2020.

Katika mkutano huo ambao uliohudhuliwa na kada wa siku nyingi Kingune Ngombare Mwiru, Mh Lowassa amewataka wazanzibar na watanzania kwa ujumla kuwa watulivu na kuhakikisha wanadumisha amani ya nchi hasa katika kipindi hiki ambacho viongozi wanaendelea na juhudi za kutafuta suluhu ya kisiasa visiwani Zanzibar.

Njia Kumi na Moja za Kumfanya Mpenzi Wako Asitoke nje na Michepuko

$
0
0

1. TAMBUA THAMANI YAKE

Unapokuwa Umeapa Kuwa Utampenda Mwenzako Hadi Kifo Kitakapowatenganisha, Uwe
Umefanya Hivyo Kwenye Nyumba Ya Ibada Au Kwingine, Lazima Ufahamu Jinsi Ya Kutambua
Juhudi Za Mpenzi Au Mwenzi Wako, Ili Kuepukana Na Uwezekano Wa Mwenzi Wako Kukuona
Kama Vile Unamchukulia Kawaida Na Hujali Jitihada Zake. Mtu Anapodhani Mwenzake
Hajali Jitihada Zake Ni Rahisi Kushawishika Kutoka Na Kwenda Kwa Mtu Atakayeitambua
Thamani Yake.

Ili Kuondoa Uwezekano Wa Mwenzako Kudhani Humjali Wala Kuthamini Juhudi Zake, Mara
Kwa Mara Jiulize Unaweza Kumfanyia Nini Ili Kumwonesha Kuwa Unamtambua. Jambo
Lenyewe La Kumfanyia Linaweza Kuwa Rahisi Tu, Mathalani Kumtumia Ujumbe Mfupi Kwa
Ajili Tu Ya Kumwambia Kuwa Yuko Mawazoni Mwako. Iwapo Utajenga Mazingira Ya
Kuitambua Thamani Ya Mwenzako Mara Kwa Mara Haitakuwa Rahisi Kwa Mwenzako Huyo
Kufikiria Kuchepuka.

2. JENGA UKARIBU NAYE

Mara Nyingi Jamii Huwachukulia Wanaume Kama Watumwa Wa Ashiki Zao, Lakini Matukio
Mengi Ya Kukosekana Kwa Uaminifu Hutokana Zaidi Na Mahusiano Ya Kikaribu Baina Ya
Mwanamke Na Mwanamume Na Si Tamaa Ya Mwili Ya Mwanamume. Iwapo Wanawake Wote
Wataufahamu Ukweli Huu, Watajua Jinsi Ya Kujenga Ukaribu Na Wanaume Zao Ili
Kuwaondolea Uwezekano Wa Kutekwa Na Wanawake Wengine.

Ni Kweli Kuwa Wapo Wanaume Wasioweza Kujenga Mshikamano Wa Kihisia Katika Suala La
Mapenzi, Lakini Huku Bado Wakiendelea Kuvutika Kimwili. Jambo Kubwa Ambalo Mwanamke
Anaweza Kulifanya Na Kumwepusha Mwanamume Kutoka Ni Kuhakikisha Ndiye Mtu Wake Wa
Karibu, Huku Mara Kwa Mara Akiwa Ndiye Mwanzilishi Wa Wazo La Kufanya Mapenzi.

3. MSIKILIZE VEMA MWENZAKO

Wanawake/Wasichana Huwa Na Mazoea Ya Kusemezana Na Marafiki Zao Mambo Mengi Ikiwa Ni
Pamoja Na Siri. Hata Hivyo, Wanaume Huogopa Kuwashirikisha Wenzao Mambo Binafsi Ya
Ndani. Ili Uweze Kuishi Vema Na Mwanamume, Lazima Ujue Jinsi Ya Kumhakikishia
Mwanamume Kuendelea Kuwa Mwanamume Hata Unapomweleza Mambo Yaamshayo Mihemko.

Kwako Wewe Mwanamke, Iwapo Utahisi Kuwa Mwanamume Wako Anataka Kuwa Wazi Katika
Mambo Fulani Binafsi Lakini Anahisi Tu Kuwa Atapoteza Uanaume Wake Kwa Kueleza Mambo
Yake, Mwekee Mazingira Ya Kumhakikishia Kuwa Ataendelea Kuwa Mwanamume. Msikilize Na
Usimlaumu, Muulize Maswali Yanayohitaji Majibu Chanya. Utashangaa Jinsi
Utakavyoboresha Ukaribu Wako Na Mwanamume Huyu Hivyo Kupunguza Uwezekano Wa
Kukusaliti.

4. MWACHE AWE NA MARAFIKI

Jambo Jingine Ambalo Linaweza Kumpunguzia Mwanamume Uwezekano Wa Kufanya Mapenzi Nje
Ya Uhusiano Ni Kumhakikishia Urafiki Na Wanaume Wenzake. Kwa Vyovyote Vile, Lazima
Mwanamume Wako Utakuwa Ulimkuta Na Marafiki. Usimzuie Kuendelea Kuwa Nao.

Unapomuunga Mkono Mwanamume Katika Kampani Yake Na Wanaume Wenzake Utakuwa
Umemwongezea Mwanamume Huyu Fursa Ya Kuendeleza Ukaribu Na Watu Wake, Hivyo
Kupunguza Fursa Ya Kujipenyeza Kwa Wanawake Wengine Katika Maisha Yake. Ukimbanabana
Halafu Na Wewe Ukashindwa Kuwa Rafiki Kwake, Akimpata Mwanamke Aliye Tayari
Atashikamana Naye.

5. TEKELEZA MALENGO NAYE

Hata Kama Uhusiano Wako Na Mpenzi Wako Umedumu Tangu Mlipokuwa Vijana Wadogo Chuoni,
Bado Haitoshi Kujihakikishia Kuwa Mmeshakua Pamoja. Ili Kuweza Kuepukana Na
Uwezekano Wa Mwenzako Kukusaliti, Lazima Nyote Msaidiane Katika Kutekeleza Mambo
Muhimu. Huku Ndiko Kukua Pamoja.

Njia Rahisi Zaidi Ya Kukua Pamoja Na Mpenzi Wako Au Mwenzi Wako Wa Maisha Ni Kuweka
Malengo Na Kuyatekeleza Kwa Pamoja. Mfano, Kama Mmeishi Katika Nyumba Ile Ile Kwa
Miaka Kadhaa Na Mazingira Yamewachosha (Pengine Nyumba Yenyewe Ni Ya Kupanga),
Pendekeza Kuhamia Sehemu Nyingine — Unaweza Kukuta Hata Mwenzako Kumbe Ana Hisia
Kama Hizo. Iwapo Utazigusa Hisia Zake Kwa Pendekezo Lako, Mpenzi Wako Atajihisi
Kuonekana Wa Tofauti Machoni Pako. Na Kwa Kuwa Baadhi Ya Watu Wanaotoka Nje Ya Ndoa
Huenda Kutafuta Utofauti, Utakuwa Umemzuia.

6. JITAHIDI KUMWELEWA

Mojawapo Ya Vishawishi Vikuu Vya Mwanamume Kujiingiza Katika Mapenzi Ni Kumpata Mtu
Ambaye Atamwelewa. Kama Huna Sifa Hii, Ni Rahisi Kwa Mwanamume Wako Kutoka Kwa Ajili
Ya Kuitafuta Kwingine.

Ili Kumzuia Mwanamume Kutoka, Onesha Jitihada Za Kutaka Kumwelewa Na Kufahamu
Matakwa Yake Ili Uweze Kuyatimiza. Katika Hili Usiogope Kumuuliza Maswali Magumu,
Mathalani Waweza Kumuuliza “Unajisikiaje Kuhusiana Na Uhusiano Wetu?” Au “Ni Kitu
Gani Ulichokuwa Unakitaka Katika Uhusiano/Ndoa Ambacho Hujakipata Mpaka Sasa?” Namna
Hii Utakuwa Umeonesha Jitihada Za Kutaka Kumfahamu Na Kumridhisha.

7. SISITIZA ZAIDI MATENDO

Wanawake Wana Utamaduni Wa Kupenda Kuyazungumza Mambo Yao, Ikiwa Ni Pamoja Na
Matatizo. Hili Ni Jambo Jema, Isipokuwa Tu Kinachotakiwa Ni Kuweka Uwiano Kati Ya
Maneno Na Matendo.

Mwanamke Hapaswi Kujiondoa Katika Hulka Yake Asilia Ya Kupenda Kusema Ili Aweze
Kudumisha Uhusiano Wake Na Mwanamume, Lakini Mara Kwa Mara Ni Vema Badala Ya Kusema
Tu Ukafanya Shughuli Kama Mbadala Wa Kusema. Badala Ya Kusema Sana, Unaweza
Kumshirikisha Mwanamume Katika Shughuli Fulani Ambayo Nyote Mnaipenda, Jambo Ambalo
Litaonesha Umoja Wenu, Huku Kila Mmoja Akipata Jibu Kwa Nini Alichagua Kuishi Na
Mwenzake.

Mathalani, Badala Ya Kuzungumzia Jinsi Usivyojisikia Vema Kwa Namna Msivyopata Muda
Mwingi Wa Kuwa Pamoja Na Kuzungumza, Tumia Fursa Hiyo Kuzungumza Kile Ambacho
Umekuwa Ukitaka Kuzungumza Na Mpenzi Wako, Maana Sasa Yupo. Badala Ya Kuzungumzia
Jinsi Unavyopenda Kujifunza Mapishi Fulani, Chukua Hatua Ya Kwenda Kujifunza, Na
Ikibidi Uende Na Mwenzako. Namna Hii Utaonekana Zaidi Kama Mtu Ambaye Unatenda
Maneno Yako, Si Kuzungumza Tu. Kwa Jinsi Hii Mpenzi Wako Atavutika Kwako Zaidi.

8. USIMWONDOLEE UJINSIA WAKE

Watu Wengi Katika Makuzi Yao Huwa Na Dhana Kuhusiana Na Jinsi Mwanamume Au Mwanamke
Anavyopaswa Kuwa. Kwa Mwanamume, Wengi Huamini Kuwa Atakuwa Mtendaji Kuliko Msemaji,
Asiyetawaliwa Na Mihemko, Mtawala, Jasiri, Hodari Na Kadhalika. Lakini Katika
Kipindi Cha Takriban Miongo Mitano Iliyopita, Hadhi Na Hulka Za Wanaume Na Wanawake
Zimebadilika. Isipokuwa, Bado Wanaume Halisi Wameendelea Kuwa Wanaume, Kama Ambavyo
Wanawake Halisi Wameendelea Kuwa Wanawake.

Iwapo Utakuwa Na Mazoea Ya Kumlazimisha Mwanamume Wako Kufanya Mambo Ambayo Si Ya
Kianaume, Au Ambayo Hayadhanii Kuwa Ya Kianaume, Mwanamume Huyu Anaweza Kulazimika
Kwenda Kumtafuta Mwanamke Ambaye Anampa Fursa Ya Kuendelea Kuwa Mwanamume.

Ili Kuondoa Uwezekano Wa Mwanamume Kutafuta Mahala Ambapo Uanaume Wake Utatambuliwa,
Jaribu Kufikiria Mambo Ambayo Humfanya Mwanamume Kujihisi Kuwa Mwanamume Kweli.
Namna Hiyo Utaongeza Mapenzi Yake Kwako.

9. PUNGUZA TAHADHARI

Mojawapo Ya Mambo Ambayo Huzuia Mahusiano Kufikia Ukamilifu Wake Ni Watu Kuishi Kwa
Tahadhari Wakiogopa Kuingia Katika Maeneo Ambayo Yanaweza Kuondoa Furaha Yao,
Pengine Kwa Mmoja Wa Wenza Hao Kukwazika. Ni Kweli Kuna Umuhimu Wa Kuepuka Kumkwaza
Mwenzako, Lakini Mnapoishi Kwa Tahadhari Kubwa Ni Vigumu Kufikia Ukamilifu Wa
Uhusiano Wenu Na Ni Rahisi Kwa Mwenza Kutoka Kwa Ajili Ya Kupata Uhuru Na Amani
Zaidi.

Ili Kuepusha Balaa, Jiulize Ni Wapi Wewe Na Mwenzako Hamkubaliani. Ukishayapata
Mambo Ambayo Hamkubaliani, Jaribu Kuweka Uwiano Na Kumpa Uhuru Mwenzako Katika
Kuyafanya Hayo. Namna Hii Utaongeza Ukamilifu Katika Uhusiano Wenu Na Hisia Za
Kubanwa Zitaondoka.

10. JISHUGHULISHE AKUKOSE

Wanawake Hupenda Zaidi Vitu Ambavyo Ni Haba Au Hupatikana Kwa Nadra. Katika Uhusiano
Wa Kimapenzi Mwanamke Hatakwambia Kuwa Anataka Uondoke Ili Aweze Kupata Fursa Ya
Kukumisi Na Kutamani Kukuona, Lakini Ukweli Ni Kwamba Ukipatikana Kwa Nadra
Utaongeza Mvuto Wako Kwake, Ilimradi Tu Uwe Na Sababu Ya Kupatikana Kwa Nadra.

Lazima Ujue Jinsi Ya Kumfanya Mpenzi Wako Akuhitaji. Jishughulishe Na Uchakarike,
Kwani Kwa Kufanya Hivyo Utaongeza Kipato Chako Na Kumwongezea Usalama Na Uhakika
Mpenzi Wako, Lakini Pia Utampa Mpenzi Wako Fursa Ya Kukumisi Na Kupunguza Uwezekano
Wa Kukusaliti.

11. MWEKE HURU AWE NA MUDA WAKE

Mwache awe na muda wake binafsi. Huwezi Kumzuia Mpenzi Wako Kutoka Na Wanaume/Wanawake Wengine Kwa Kuwa Na Wivu Na Kumfuatiliafuatilia. Lakini Kwa Kuzingatia Mambo Haya Yaliyobainishwa Hapa, Utakuwa
Umeondoa Sababu Nyingi Za Mpenzi Wako Kufikiria Kuwa Na Uhusiano Na Mtu Wa Nje.
Viewing all 104694 articles
Browse latest View live




Latest Images