Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Mbunge Godbless Lema Awachana CCM Laivu....Hawawezi Kukaa Madaraka Kwa Maisha yote

$
0
0
Mbunge wa arusha mjini Godbless lema amesema leo bungeni swala la Zanzibar si la kichama,Ni swala la nchi na lisipotafutiwa ufumbuzi lina athari kwa kila mtu,

Lema ameenda mbali zaidi na kuwaambia Wabunge Wa CCM hii nchi ikiharibika hata watoto wao wataharibikiwa na hawawezi kukaa madarakani kwa maisha yao yote.

Lema amemtolea mafano mbunge Marry nagu na kumwambia akumbuke serakali iliyopita alikuwa waziri,Lakini leo naye anauliza maswali ya nyongeza.

Lema alienda mbali zaidi na kumwambia Mwenyekiti wa bunge Chenge asijione ni mdogo wake mungu kwa kukalia kiti cha spika.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa Ya Februari 5, Ikiwemo Siri ya Magufuli Kutosafiri Nje ya Nchi

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa Ya Februari 5, Ikiwemo Siri ya Magufuli Kutosafiri Nje ya Nchi

Imebainika Mashine ya CT Scan Iliyofungwa Muhimbili Hospital ni ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

$
0
0
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imekiri kwamba mashine ya CT Scan iliyofungwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ilikuwa ni ya kituo cha kisasa cha kutolea huduma za afya cha Benjamin Mkapa kilichopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Akijibu swali la nyongeza bungeni mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Khamis Kigwangalla alisema mashine hiyo iliingia nchini kwa lengo la kupelekwa katika kituo hicho lakini ikapelekwa Muhimbili kutokana na kutokamilika kwa majengo ya kufungwa mashine hiyo katika kituo hicho.

Alisema, uamuzi huo waliuchukua pia kwa sababu hela ya kununua mashine nyingine ambayo itapelekwa kufungwa katika kituo hicho ilikuwepo na kwa sasa mchakato wa ununuzi unaendelea.

Dk Kigwangalla alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM) aliyetaka jibu la Serikali kama ni kweli ilichukua mashine ya kituo hicho na kufunga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ama ilinunua.

Awali katika swali la msingi msingi, Nkamia alitaka kujua mpango wa Serikali wa kununua mashine mpya ya CT -Scan kwa ajili ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.

 Kuhusu hilo, Dk Kigwangalla alisema, Desemba mwaka jana Serikali ilipeleka mashine ya CT-Scan katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo inatumia teknolojia ya kisasa yenye X-ray tube mbili na uwezo wa kupiga picha ya 128 slice mara mbili.

Bomoa Bomoa Zaikumbu Sinza...Baa za Uwanjani Legho Zavunjwa

$
0
0
BAADHI ya baa zilizopo katika viwanja vya Legho, Ubungo jijini Dar, leo zimevunjwa kufuatia agizo la mahakama kwa kile kilichodaiwa wamiliki walivamia eneo ambalo siyo lao.
Akizungumza na mwandishi wetu, dalali wa mahakama kutoka katika kampuni ya Mem Auctioneers and General Brokers Ltd, Elieza Mbwambo, alisema mmiliki halali  wa eneo hilo ni Dar Cool Makers Limited ambaye baada ya  kuvamiwa eneo lake alifungua kesi mahakamani mwaka 1993 ambapo iliendelea mpaka ilipofikia leo.

Wavamizi wa eneo hilo ambao ni John Ondoro Chacha, Jumuiya ya Wazazi CCM na mtu mwingine mmoja baada ya kuona mmiliki halali amepeleka kesi mahakamani nao wakaenda kuweka zuio ambapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliamuru eneo hilo lirudi kwa mmliki halali ambapo wavamizi walitakiwa wabomoe vibanda walivyokuwa wamejenga walikokuwa wakifanya biashara ya baa.

“Januari 25 mwaka huu tulipewa oda na mahakama tuje kuwatoa hawa wavamizi, tuliweka tangazo kama wiki moja iliyopita lakini hawakujali hivyo leo ikawa ndiyo siku rasmi ya kuwaondoa na kama unavyoona ndiyo tunabomoa hivi.

“Mwenye kesi ya msingi ambaye ni John Ondoro Chacha alitakiwa kuwaambia wapangaji wake kwamba ameshindwa kesi lakini hakuwaambia ndiyo maana hata tangazo lilipowekwa hawakushtuka, kwa mujibu wa mahakama huyu Chacha ambaye kwa sasa ni marehemu na watoto wake ndiyo walikuwa wakipokea kodi ya kila mwezi kwa wafanyabiashara waliowapangia  wakati eneo hili siyo lao,” alisema Mbwambo.

Watu mbalimbali walionekana wakiwa wamesimama huku wakishangaa eneo hilo huku wengine wakilalamika kwamba watakuwa wanajiachia  wapi wakati walikuwa wamezoea viwanja hivyo.

Source-Global Publishers

Siri Imefichuka..Kumbe Rwanda ilitoa Mafunzo ya Kijeshi kwa Wakimbizi wa Burundi Wamwondoe Nkurunziza Madarakani

$
0
0
Ripoti ya siri ya Umoja wa Mataifa(UN): Rwanda ilitoa mafunzo ya kijeshi kwa wakimbizi wa Burundi wamwondoe Nkurunziza madarakani.

Burundi imekabiliwa na machafuko tangu mwezi Aprili 2015, wakati Rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kwamba atawania muhula wa tatu wa urais, ambao alishinda.

Akijibu madai hayo, waziri wa maswala ya kigeni nchini Rwanda Louise Mushikiwabo amesema kuwa mgogoro huo wa Burundi ni mzito na wa kujitakia miongoni mwa viongozi wa Taifa hilo na kwamba jamii ya kimataifa inafaa kuuangazia na kuwacha kutafuta sababu za kuuepuka. ''Ni Muhimu kuelewa kwamba usimamizi wa wakimbizi wa taifa jirani ni suala gumu, hivyo basi Serikali ya Rwanda imelazimika kuweka sheria kali dhidi ya wakimbizi wa Burundi''. Mushikiwabo amesema kuwa madai hayo yanatokana na hatua ya Rwanda kuwahifadhi wakimbizi wa Burundi ambao wanadaiwa kuwa wapinzani wa Serikali.

Waziri huyo ameongezea: Hatuwezi kuwarudisha wakimbizi hao hadi pale kutakapokuwa na mfumo ambao utalinda maisha yao nchini Burundi

______________________
A United Nations report has accused Rwanda of recruiting and training refugees from Burundi to oust President Pierre Nkurunziza, according to a Reuters news agency report.

Rebel fighters told the UN panel of experts who monitored sanctions on the Democratic Republic of Congo, that the training was done in a forest camp in Rwanda.

“They told the group that they had been recruited in the Mahama Refugee Camp in eastern Rwanda in May and June 2015 and were given two months of military training by instructors, who included Rwanda military personnel,” according to Reuters.

18 Burundian combatants including six children in South Kivu province, in eastern Congo told the experts they were trained in military tactics, use of assault rifles, rocket propelled grenades among others.

Rwanda Ambassador to the UN Eugene Gasana dismissed the claims.

“This further undermines the credibility of the Group of Experts, which seems to have extended its own mandate, but apparently investigating Burundi,” Ambassador Gasana told Reuters.

In December, Burundi had accused Rwanda of supporting a rebel group that was recruiting Burundi refugees in Rwanda but President Paul Kagame dismissed the claims describing it as “childish”.

Source: Reuters

Mke wa Dr Slaa Atupia Picha Mtandaoni Wakiwa na Dr Slaa Wakisoma Magazeti

$
0
0

Baada ya Kimya Kingi Mke wa Dr Slaa Josephine Mushumbusi Ameamua Kutoa Picha Kwenye Mtandao wa Facebook Akiwa na Dr Slaa na Kuandika "Tupo Tunasoma Magazeti"

Baadhi ya Komenti Toka kwa Wadau wao;

Kapalatu Salim
Mungu hamtupi mtu mwenye dhamila ya kweli hawezi shindwa hawezi kata tamaa. Maneno hayo aliniambi ZZK miaka mitatu iliyopita. So simama katika kupigania haki wazalendo tupo nyuma yako. Mungu atawalinda sana

Aaron Mwakajonga 
huyo nae ni jipu

Telesphory Masalu 
Hongereni sana kwa misimamo yenu ya dhati iliyokataa kuyumbishwa na fedha za Mafisadi.Dr Slaa will remain my role model forever.

Amani Magingi 
Bado nashindwa kukuellewa mamaa mushumbusi... hakika sikuelwwiii hivi kweli ulimtupia virago dr???? Kwelii kabisaaaa??? Yaaan bado sielewiii dr.was my role modal... lkn kwa yaliyotokea.... daaah sijui lini tz itapata ukombozi

Meshack Samweli
Mungu atawalipa hapahpa duniani kama mliwasalit watanzania mie sjui ipo sku ukwel utajulikana


Bryton Myrium Chadema
 mama ni kweli ulitumia nyumba ya dr slaa kumuombea mkopo jamaa mwingine sory kama nimekosea kuulliza

Rais Magufuli Afunguka na Kusema Yeye si Kichaa wala Dikteta ila Inafika Wakati Lazima Afanye Hivyo!!

$
0
0
RAIS Dk. John Magufuli amesema anapochukua hatua yeye si kichaa, si dikteta, si shetani wala si mnyama, ila ni mpole, lakini amefika mahali lazima afanye hivyo kwani ndani ya Serikali yanafanyika mambo ya ajabu.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam katika kilele cha Siku ya Sheria nchini, alipokuwa mgeni rasmi kwa mara ya kwanza katika uzinduzi wa Mwaka wa Mahakama tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisifu kazi kubwa inayofanywa na Idara ya Mahakama, huku akitangaza uamuzi wa gharama za kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge zaidi ya Sh bilioni nne ni bora zikawasaidia wananchi.

“Ninapochukua hatua mimi si mnyama, si dikteta, si shetani, ni mpole kweli, lakini inafika mahali lazima nifanye, yanayofanyika serikalini ni mambo ya ajabu sana, nataka kutoa sadaka yangu, inawezekana hata nikifa naweza kuwa rais wa malaika,” alisema.

Alipongeza kazi kubwa inayofanywa na mahakama huku akibaki kujiuliza kwanini katika maadhimisho ya siku yao hawarushi matangazo yao moja kwa moja kupitia luninga.

“Mnafanya kazi kubwa, nilipofika niliuliza kwanini hii siku yenu hamrushi ‘live’, nikajibiwa fedha za kurusha ‘live’ zinapelekwa kuwahudumia wananchi.

“Kipindi kimoja kurusha ‘live’ kwa wiki mbili inatumika zaidi ya Sh bilioni nne, ni vizuri kuzikata hizo fedha zinazopelekwa kurusha ‘live’ zikapelekwa katika kesi za ubunge zinazohitaji shilingi bilioni tatu kusikilizwa hadi kumalizika kwake,” alisema.

Alisema mahakama ilikuwa inapewa bajeti ya Sh bilioni 41, lakini mwaka 2015/2016 ilishuka wakatakiwa kupewa Sh bilioni 12 ambazo hadi sasa hawajapewa.

“Kiongozi lazima ufikirie wapi pa kupeleka fedha na wapi pa kunyima, watu wa mahakama mnafanya kazi ya Mungu, nawaahidi ndani ya siku tano nitakuwa nimewapa Sh bilioni 12 zote.

“Sina tatizo la masilahi ya wafanyakazi wa mahakama, katika bajeti ya mwaka huu nitawapa fedha nyingi kuliko bajeti zote zilizopita, fedha zipo,” alisema.

Mahakimu Kutumbuliwa
Rais Magufuli alisema anamwagiza Jaji Mkuu kuwachukulia hatua mahakimu 502 ambao hawakufikia malengo ya kumaliza kesi 250-260 kwa mwaka. Walimaliza kesi chini ya 100.

“Mahakimu ambao hawajafikia kumaliza kesi 260 hayo ndiyo majipu yako Jaji Mkuu, unatakiwa kuyatumbua, wewe uliniapisha hata mimi, leo unapitisha agizo mwingine anapinga.

“Unatoa siku saba sasa sijui ndiyo watamaliza kutoa hizo hukumu, nakuagiza wachukulie hatua, tusipochukua hatua hakuna kitakachofanyika.

“Walioshindwa kufikia lengo unawabakiza wa nini, wasomi wako wengi, hata ukitangaza leo watajitokeza, niruhusu mimi nitangaze, sitaki kuingilia mahakama,” alisema.

Mabilioni ya NIDA
Akizungumzia hatua yake kwa watendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), alisema ilipewa Sh bilioni 176.6, lakini vitambulisho vilivyotengenezwa havifiki hata milioni mbili na havina sahihi wakati vitambulisho vya kupigia kura fedha iliyotolewa haizidi Sh bilioni 70, lakini vina sahihi za wapigakura wote wa Tanzania ambao ni milioni 23,253,982.

“Utaona ugumu wa kuongoza, nchi inatawaliwa na madudu ya kila aina, wapo watu wanacheza na fedha wanavyotaka wakati wapo watu masikini sana, wengine wanataka bodi zao wakakae Ulaya.

“Hapo ndipo tulipofikia, wengine wanalipwa mshahara kwa mwezi Sh milioni 35, naomba mniombee kabla ya kunihukumu, toeni hukumu kwa haki kwa hawa wanaotaka kuifikisha nchi pabaya, toeni hukumu zao haraka,” alisema.

Kesi za Wakwepa kodi
Rais Magufuli alisema kuna kesi 442 za kukwepa kodi ambazo zingeamuliwa Serikali ingepata Sh trilioni moja, ambayo ingeweza kununua ndege zaidi ya sita.

Alimuomba Jaji Mkuu kuzimaliza kesi 442 na kama zikimalizika fedha hizo Sh trilioni moja ataipa Idara ya Mahakama Sh bilioni 259 na Sh bilioni 750 zilizobakia zitanunuliwa ndege sita na wafanyafakazi 250 ATCL waliopo sasa wataondolewa.

Akizungumzia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alisema kuna kesi 26 za watu waliokutwa na nyara za Serikali, ambazo zipo zaidi ya miaka mitano hazijaamuliwa kwa sababu upelelezi bado.

“Polisi wapo, DPP yupo, upelelezi unaendelea kila siku, hapo unaona tatizo lilipo, DPP upo unapeleleza nini au unatafuta rushwa?” alisema.

Alisema suala la kuanzishwa kwa mahakama ya mafisadi ya wahujumu uchumi halihitaji kwenda bungeni kufanya mabadiliko, lifanywe haraka, mahakama ianze kwani nchi inachezewa.

Pamoja na hali hiyo Rais Magufuli alikubali kupokea maombi yote yaliyotolewa na mahakama na kuyazingatia kwani lazima ayaunge mkono ikiwamo kukubali watumishi wa Idara ya Mahakama wasome na kupatiwa mikopo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

“Nimeamua nchi iende na itaenda, anayefikiria ataikwamisha atakwama yeye, nategemea zaidi mahakama katika kufanikisha hilo,” alisema.

Mke wa Dr Slaa Josephine Mushumbusi Ajibu Kuhusu Tuhuma za Kuomba Mkopo Bank Kwa Kutumia Nyumba ya Slaa

$
0
0
Mke wa Dr Slaa Amejibishana na Wadau Katika page yake ya Facebook na kujikuta akijibu tuhuma zilizozagaa jana kwenye magazeti kuwa aliomba mkopo wa sh mil 300 kwa kutumia nyumba ya Dr Slaa...

Soma Majibisha yao hapa;

Bryton Myrium Chadema 
"Mama ni kweli ulitumia nyumba ya dr slaa kumuombea mkopo jamaa mwingine sory kama nimekosea kuulliza"


Josephine Mushumbusi
"Sandra Bahati mbaya sana huwa siamini taarifa za magazeti,hivyo huwa hazipotezi mda Wangu sana. Pili hiyo ni taarifa hakuna mahala wamewasiliana na mimi.
Tusubiri,maana najua wapi pa kuwauliza taarifa hizo walizitoa wapi.
Ufupi bado mtu WA kuniumiza hajazaliwa"

Aggrey Charles
"Mama Josephine Mushumbusi kwa nafasi yako nadhani ugeiga hata zuri moja la Lowassa la UKIMYA. Kwani ni lazima ujibu kila kitu mama? Na ukijibu utajibu mangapi? Ushauri wangu kwako tulia kimya ujisomee tu huku mitandaoni siku zisogee. Mimi ni moja ya wafuasi wazuri wa Mh Dr W. SLAA ila si mama (yaani wewe) lakini heshima yenu ipo kwangu siku zote. UKIMYA wako utakuongezea kitu kuliko huku kuja kulumbana na vijana wenye njaa ya kuona kuna kitu kipya kinazaliwa katika nchi. Watu wenye njaa na kiu ya mabadiliko halisi hugombana na yeyote wanayemwona kama kikwazo. Ni Ushauri tu mama".

Josephine Mushumbusi
"Sometimes it is too much.
Nimekuawa kimya sana.
Na nafikiri ni Leo tu nimeonekana hapa.
Lowasa Hana ukimya naomba tusifananishwe"

Breaking News: Mbowe Atangaza Baraza la Mawaziri Kivuli leo Bungeni

$
0
0
Kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe ametangaza baraza lake la mawaziri kivuli leo bungeni mjini Dodoma.
Mbowe, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chadema ametaja baraza lake ambalo litakuwa na lengo la kuishinikiza serikali ya Rais Magufuli kutimiza kile alichoahidi kwa Watanzania.

Baraza hilo ni kama ifuatavyo;
1.Wizara ya Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.
Mawaziri – Jaffar Michael
Naibu Waziri – Joseph Nkundi na Ruth Mollel

2.Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
Waziri – Ali Saleh Abdalla
Naibu Waziri – Pauline Gekul

3.Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu
Waziri – Esther Bulaya
Naibu – Yusuph Makame na Maftah Abdalla

4.Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Waziri – Magdalena Sakaaya
Naibu Waziri – Emmaculate Swari

5.Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri-Inj. James Mbatia
Naibu Waziri Willy Kombucha

6.Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri – Halima Mdee
Naibu Waziri – David Silinde

7.Wizara ya Nishati na Madini
Waziri – John Mnyika
Naibu Waziri – John Heche

8.Wizara ya Katiba na Sheria
Waziri – Tundu Lissu
Naibu Waziri Abdalla Mtolela

9.Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Waziri – Peter Msigwa
Naibu Waziri – Riziki Shaghal

10.Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri – Juma Omari
Naibu Waziri Mwita Waitara

11.Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri – Godbless Lema
Naibu Waziri Masoud Abdalla

12.Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri – Wilfred Lwakatare
Naibu Waziri – Salum Mgoso

13.Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri Esther Matiko
Naibu Waziri– Cecilia Pareso

14.Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Waziri Anthony Komu
Naibu Waziri Cecil Mwambe

15.Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi
Waziri – Suzan Lyimo
Naibu Waziri Dkt. Ali Suleiman Yusuph

16.Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Waziri – Dkt. Godwin Mollel
Naibu Waziri Zubeda Sakul

17.Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo
Waziri – Joseph Mbilinyi
Naibu Waziri – Devotha Minja

18.Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Waziri – Hamidu Hassan
Naibu Waziri– Peter Lijualikali

Serikali Yafunguka Bungeni Kinachosababisha Umeme Ukatike Mara Kwa Mara Hasa Mikoani

$
0
0
Serikali  imesema tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara nchini linatokana na uchakavu na kuzidiwa kwa vituo vya kupoza umeme na miundombinu ya usafirishaji na usambazaji nishati hiyo.
Katika kukabiliana na tatizo hilo Tanesco inachukua hatua za kujenga mifumo ya njia kubwa za umeme wa msongo wa kilovoti 400 (Iringa- Dodoma-Singida-Shinyanga), gridi ya Kaskazini 
Mashariki (Dar es Salaam, Chalinze,Tanga –Arusha), ya Kaskazini Magharibi (Geita- Kagera –Katavi- Kigoma- Rukwa na Mbeya) na Makambako- Songea wa kilovoti 220.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani wakati akijibu swali la Mbunge wa Magu, Boniventure Kiswaga (CCM). 

Kiswaga alitaka kufahamu serikali imejipangaje kukabiliana na tatizo la kukatika katika kwa umeme.
Pia mbunge huyo alitaka kufahamu, Je serikali itakamilisha lini kupeleka umeme katika vijiji vya jimbo hilo ikizingatiwa mpaka sasa ni asilimia 20 tu ya vijiji ndiyo vina umeme. 

Kalemani akijibu swali hilo, alisema tatizo la kukatika kwa umeme linatokana na uchakavu na kuzidiwa kwa miundombinu ya kupoza umeme pamoja na matukio ya kulipuka kwa transfoma yanayosababishwa na radi hasa kipindi cha mvua pamoja na wizi wa mafuta ya transfoma unaofanywa na wananchi wasio waaminifu.

Alisema Tanesco inakamilisha upanuzi wa usambazaji wa umeme katika majiji makubwa ya Arusha, Dar es Salaam, na Mwanza ambapo kazi hizo zitahusisha ujenzi wa njia mpya za umeme na kupanua vituo vya kupoza umeme.

“Kukamilika kwa kituo cha kupoza umeme cha KIA mkoani Kilimanjaro kumeimarisha upatikanaji wa umeme maeneo ya Mirerani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA),” alisema Kalemani.

Pia vituo vya kupoza umeme katika jiji la Dar es Salaam vya Gongo la Mboto, Kipawa, Mbagala, na Kurasini vitaunganishwa kwa njia ya sakiti mzunguko kutoka Ubungo na Kinyerezi kuanzia Machi mwaka huu.

Idriss Sultan Una Uhakika Gani Kama Mimba ya Wema Sepetu ni Yako?

$
0
0
WAKATI Mwisho Mwampamba aliposhiriki kwa mara ya kwanza Shindano la Big Brother miaka ile ya mwanzo wa 2000, Wabongo wengi hawakuwahi kufikiri kama ni kitu ambacho kingeweza kuwasaidia vijana wetu, hata pale dau kubwa la mshindi lilipotangazwa. Wengi walitazama zaidi katika maadili, kwa sababu kulikuwa na mambo mengi ambayo kwa utamaduni wetu, hayakustahili kuoneshwa katika televisheni kama yalivyokuwa yakifanyika.

Lakini taratibu wakajikuta wanaliona shindano hilo kuwa la kawaida, lenye ‘kuburudisha’ hasa baada ya ushindi wa Richard mwaka ule wa 2007.

Leo hii, vijana wawili wa Kitanzania tayari wameweka kibindoni jumla ya dola 400,000 kutoka shindano hilo, kwani Richard alichukua dola laki moja alipotwaa ushindi na Idriss Sultan, aliyeibuka namba moja mwaka jana, kwa pesa ya madafu, ana kama milioni 500 hivi!

Sasa Idriss amekuwa kijana maarufu sana katika jamii yetu, akiwa ngazi moja ya mastaa wenzake wengine wa Bongo Fleva, Bongo Muvi na kada nyingine za ustaa, maana hapa kwetu, umaarufu ni jitihada zako tu katika kujipromoti!

Kama kijana, ninajivunia Idriss, kwa sababu ameongeza idadi ya masupastaa, lakini pia kiasi cha fedha alizopata zimechangia kuwagawia Watanzania wengine kwa namna moja au nyingine kwa vile nina uhakika, mshindi wetu huyu, ana kitu anakifanya na fedha zake, ambacho kwa vyovyote amewapa ajira wenzake, hata kama siyo ya kudumu.

Lakini nje ya ustaa, nina ushauri ninaopenda kumpatia na hasa kwa kuwa ninaamini bado ni bwana mdogo kiumri, hivyo kuna mambo ambayo hayahitaji fedha ili kuyapata, isipokuwa yanahitaji kujiongeza tu kiakili.

Yeye amethibitisha katika vyombo kadhaa vya habari kuwa hivi sasa anatoka na Wema Sepetu, ambaye naye ameutangazia umma kuwa ni mjamzito. Ni jambo la kheri kwake, hasa kwa vile kwa miaka mingi, wapinzani wake wametumia kukosa kwake mtoto kama fimbo ya kumchapia.

Ambacho hakijakaa sawa kwangu, ni kauli ya Idriss kuwa mimba ya Wema ni yake. Sibishi, lakini kuna vitu ambavyo mwanaume hatakiwi kupaza sauti, hasa unaposhiriki mapenzi na mwanamke wa aina ya Wema. Historia ya muigizaji huyu staa kimapenzi, inaonesha amekosa utulivu.

Ni kujilipua kwa kiwango cha juu, mtu kuja na kutoa kauli ya kujiamini kiasi hiki na tena mtu huyo anapokuwa kijana mdogo kama Idriss. Anayejua baba wa mtoto ni mama na kwa wasichana wa Kibongo, mtu kupewa ujauzito wala siyo suala la kuuliza.

Siku zote mwanaume anapaswa kuwa mtulivu kichwani, hasa anapozungumza mambo ambayo siku moja yanaweza kumgeuka. Sisemi kwamba amebambikwa, la hasha, ninachosema hapa ni umuhimu wa kuchukua tahadhari katika matamshi.

Na hii ni kwa sababu Wema ni rafiki yake tu, angekuwa amemuoa, yupo ndani kwake muda wote ingeweza kuwa sawa, lakini hawa dada zetu ambao wakati mwingine inapita hata wiki hujaonana naye, maneno haya ni ujasiri wa hali ya juu.

Hivi siku moja ikatokea wamekorofishana (na hili linawezekana kabisa) halafu huyu binti akaamua kumvua nguo na kumwambia mimba haikuwa yake, itakuwa aibu yake au yetu?

Maneno kama haya hutakiwi kutamka hadharani, unaiambia familia yako, jamani eeeh, ule mzigo wa Wema ni wanguu! Halafu walimwengu unawaacha wenyewe wajikanyage, wakisema ni wa kigogo wewe sawa, wakisema sijui ni ya nani wewe hewala, kwa sababu siku likisanuka, utakuwa salama mbele yao !
GPL

Mimba ya Wema Sepetu Yamtia Uchizi Mtangazaji Penny...Naye Apata Hamu

$
0
0
Mwanadada anayepiga dili la utangazaji kupitia Zouk TV ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungwilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa mimba ya shosti wake, Wema Sepetu inampa ‘uchizi’ kwa kutamani kila kukicha na yeye anase ujauzito.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Penny alisema kuwa hivi sasa karibia rafiki zake wote wana watoto kitu kinachomchanganya na kumtamanisha na yeye atundikwe kibendi.
“Unajua Wema atakapojifungua na kuna rafiki zangu wengine wana watoto nikikaa nao stori nyingi zitakuwa ni za watoto zao, mimi nitaongea nini sasa? Ndio maana nilipopata taarifa za ujauzito wake nilifurahi sana, pia amenipa mshawasha,” alisema Penny.

Sasa Udaku Special Blog Ipo Play Store..Unaweza Download Kwenye Smart Phone yako Hapa

$
0
0

Good News! Sasa Blog yako ya Udaku Special Ipo Google Play Store.

Download Udaku Special Blog Android Application CLICK HERE From Play Store

Au Bonyeza hii picha hapa chini

Edward Lowassa: Tutaingia IKULU Kwa Amani Bila Kumwaga Damu

$
0
0
Aliyekuwa Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa, akizungumza na wazee wa chama hicho, jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam jana walipomtembelea ofisini kwake amewataka wazee hao kutokata tamaa na kujipanga kimkakati kujiandaa na kuimarisha chama chao pamoja na ukawa kwa ujuml ili kujiandaana uchaguzi ujao wa 2020.

Lowassa pia ameendelea kuwataka Watanzania kuwa watulivu na kulinda amani ya nchi na kujiepusha na kila jamboambalo wanaona linamwelekeo wa uvunjifu wa amani.

Hayo aliyasema wakati alipokuwa akijadili mambo mbalimbali ya kuimarisha chama.

Aidha, aliwaomba wazee hao kutokata tamaa kwani kuna mambo mengi ya kufanya hadi kufikia malengo waliyojiwekea.

"Hali ya chama chetu na UKAWA iko vizuri, uchaguzi tulishinda, sisi tunajua, Jumuiya za Kimataifa zinajua na hata CCM wenyewe wanajua kama tulishinda, ila ubabe wao na dhuulma ndio wamefanya waliyofanya," alisema.

Lowassa alifafanua zaidi kuwa kama chama kinachojiandaa kushika dola hawakuwa tayari kuingia Ikulu kwa damu ya watazania na ndiyo maana hata vijana walipomtaka atoe kauli ya kuingia barabarani anasema, "niliwazuia."

Kauli ya Rais Imevunja Katiba; kwa Kuingilia Uhuru wa Mahakama

$
0
0
Napenda kusema wazi kabisa kua Rais wetu alishauriwa vibaya, na waliomshauri wamemweka katika kikaango na wadau wa sekta ya sheria.

Hii ni kutokana na kauli aliyoitoa jana katika maadhimisho ya siku ya sheria duniani au " Law day" pale aliposema kwamba kuna kesi zaidi ya 400 zilizopo mahakamani ambazo kama zikiendeshwa ipasavyo basi serikali inaweza kujipatia kiasi cha shilingi trilioni moja kama fidia toka wa wadaawa, ambazo ameahidi kuwapatia mahakama kiasi cha shilingi bilioni mia mbili.

Kuna mambo machache ya kuangalia hapa ;

1. Ni hakimu gani au jaji atakayekua tayari kutoa hukumu dhidi ya serikali.

2. Ni wakili gani anapoteza muda wake kwenda mahakamani wakati anajua kua mteja wake anakwenda kushindwa.

3. Vipi kuhusiana na uhuru wa mahakama kufanya kazi yake bila kuingiliwa.

4. Vipi kuhusiana na haki ya mtuhumiwa kuwa hana hatia mpaka pale mahakama itakapomtia hatiani.

5. Ina maana serikali itashinda kesi zote 400??

Napenda nikumbushe kwamba mashauri yakishafikishwa mahakamani mambo hua yanaendeshwa kwa taratibu, kanuni na sheria ambazo tayari zipo, hayaendeshwi kwa kauli za kisiasa, huko ni kuingilia uhuru wa mahakama.

Kauli ya Rais ukiitazama kwa kina utaona kwamba imevunja ibara ywa 13 (6) (a) na 107B ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , 1977, nanukuu;

Equality before the law 13.-(1) All persons are equal before the law and are entitled, without any discrimination, to protection and equality before the law.

(6) To ensure equality before the law, the state authority shall make procedures which are appropriate or which take into account the following principles, namely: (a) when the rights and duties of any person are being determined by the court or any other agency, that person shall be entitled to a fair hearing and to the right of appeal or other legal remedy against the decision of the court or of the other agency concerned;

Independence of the Judiciary 107B. In exercising the powers of dispensing justice, all courts shall have freedom and shall be required only to observe the provisions of the Constitution and those of the laws of the land.

Ukipitia ibara zote mbili, utaona kwamba kwa kauli ya Rais, majaji na mahakimu hawatakua katika hali ya uhuru wa kufanya kazi zao kwani hawatataka kwenda kinyume na maagizo ya rais ambayo yanaelekeza makusanyo ya trilioni moja.

Vile vile haki ya wadaiwa itakua imevunjwa maana mpaka sasa wanachukuliwa kua tayari ni wakosaji wakati mashauri bado hayajamalizika na mahakama kufikia maamuzi yake.

Jambo la msingi kabisa la kufanyika hapa ni kwa Rais, kuiondoa kauli ile kwani kwa kiasi kikubwa italeta usumbufu mkubwa katika mashauri yanayoendelea mahakamani.

Wanasheria wanaweza kutuhumu majaji kua wamefikia maamuzi yao kutokana kua waliahidiwa bilioni miambili na rais , kwahiyo wanafanya hivyo kutimiza malengo yao.

Kama mwananchi wa kawaida na mdau wa sheria, kwakweli kauli ile haikua sahihi. Na inahitajika uamuzi wa busara kabisa ufanyike ili hili jambo liishe vyema kwani kuna kila dalili ya maombi kupelekwa mahakamani ili mashauri yasimamishwe mpaka kauli hiyo itakapofutwa.

Nawasilisha by Stroke/Jamii Forums

‘SIMBA’ Amfanya Alikiba Ashindwe Kufanya Uzinduzi wa Lupela Mbugani

$
0
0
Jana pande za SlipWay ,Ali Kiba alizindua video yake ya Lupela lakini mipango yake ilikuwa ni kufanya uzinduzi wa video hiyo kwenye mbuga za wanyama.

‘’Nilitamani sana kwenda kufanya ndani ya mbuga ili I’make sense’ zaidi ili ‘honey’ wangu Lupela ainjoy zaidi lakini kiukweli ilikuwa ni uoga wangu tu,asije akatokea simba halafu Lupela akafia pale pale,lakini sio kitu tumefanya kitu kizuri na tumejaribu ku’create’ vitu ambavyo  watu watapenda tumecheza,tumeinjoi,kuna ‘parts’ za elephants kidogo kuonyesha kwamba najali jinsi gani kwamba mimi ni balozi nafanya kazi yangu vizuri,’’Ali Kiba

@cloudsfmtz on Instagram

Mwanafunzi Mtanzania Aliyefariki India Hajafa kwa Kupigwa ila Alifariki Baada ya Pikipiki yake Kugonga Nguzo

$
0
0
Waziri Mahiga ametoa ufafanuzi huo leo bungeni, na kuthibitisha ni kweli wanafunzi hao wamefanyiwa vitendo hivyo, ambavyo watanzania walikuwa wanavisikia bila kuwa na taarifa rasmi.

“Wananchi wa India walichoma gari lake, na punde kidogo gari lingine lilifuata likiwa na wanafunzi wanne watanzania, mmoja msichana na watatu wavulana, walilisimamisha lile gari na kuwavuta wale wanafunzi nje, na wakamchukua yule msichana na kumvua nguo na kuanza kumtembeza barabarani uchi, wale wavulana walipigwa na gari lao lilichomwa, katika gari lile kulikuwa na simu zao na documents mbali mbali nazo ziliteketea”, alisema waziri Mahiga.

Waziri Mahiga aliendelea kwa kusema kuwa baada ya hapo askari wa India walifika lakini hawakuonyesha ushirikiano wa kutosha, lakini wanafunzi hao walipelekwa hospitali na kupatiwa matibabu ya majeraha waliyokuwa nayo, lakini walilazimika kuondoka mapema kwa kuwa hawakuwa na pesa.

“Baada ya hapo ubalozi wetu wa India uliandika dokezo la kidiplomasia kwa serikali ya India, ikilaani kitendo hicho na kuitaka serikali ya india ichukue hatua za kisheria na haraka katika kupeleleza kufuatia matukio hayo, na waziri wa mambo ya nchi za nje wa India, alitoa taarifa rasmi kule New Delhi,kwanza kuomba radhi kwa Tanzania na watanzania walioko India kwa kitendo hicho kilichotokea, akaagiza serikali yake ichukue hatua za kisheria na kupeleleza na kukamata wale waliohusika, na wote sasa wamekamatwa na wamepelekwa mahakamani”, alisema Waziri Mahiga.

Pamoja na Hayo Waziri Mahiga alisema serikali India iliagiza kwamba wanafunzi wa Tanzania wapewe ulinzi maalum kule wanakoishi na kusindikizwa pale wanapokwenda masomoni au madarasani , na tatu serikali ya India ilimtaka balozi wetu afuatane na maafisa waandammizi wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya India mjini Bangalow, ili kukutana na wanafunzi wa Tanzania na wengine wa Afrika, na kuweka mahusiano mazuri kati ya wananfunzi na wenyeji katika mji huo.
Pia Waziri Mahiga alitoa taarifa rasmi juu ya kifo cha mwanafunzi mwingine Mtanzania nchini humo, na kusema mwanafunzi huyo hakufariki kwenye tukio hilo la uvamizi, bali alipata ajali ya pikipiki iliyosababisha kifo chake.

“Nilielezwa kwamba kuna mwanafunzi mmoja ambaye amefariki karibu na maeneo hayo hayo , taarifa za awali zilikuwa zinatatanisha wakadhani kifo hicho kilitokana na tukio hilo la kuvamiwa wanafunzi wetu, lakini si kweli, mwanafunzi huyo mtanzania alikuwa anaendesha piki piki bila kofia, akaenda kugonga nguzo ya taa na kufariki pale pale, ubalozi wetu unashughulikia mazishi na mwili wake utarudishwa Tanzania mapema iwezekanavyo.

Tukio hilo limeingia siku ya tatu sasa tangu kutokea kwake nchini India, ambapo kumeibuka hisia tofauti tofauti miongoni mwa watanzania, na kuwatia hofu wanafunzi wanaosoma nchini humo.

Magufuli Aanza Kutimiza Ahadi ya Kufufua Viwanda...Kiwanda Cha Matairi cha General Tyres Arusha Chatengewa Mamilioni

$
0
0
Shillingi Billioni 60 zinategemea kutumika kufufua kiwanda ya matairi cha General Tyres kilichopo Jijini Arusha ambacho kimesharudi mikononi mwa Serikali, na fedha hizo zitatumila kurekebisha mitambo ya umeme ya kiwanda hicho na kupata mitambo mipya itakayoendana na teknolojia ya utengenezaji wa matairi duniani.

Akijibu swali la Mhe. Joshua Nassari Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) lililouliza ni lini serikali itafufua kiwanda cha matairi cha General Tyres kilichopo Jijini Arusha kwani ni tegemeo kwa ajira kwa wananchi wa Jijini la Arusha,Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles John Mwijage amesema kiwanda hicho kimesharudi mikononi mwa Serikali na wako mbioni kukifufua ili kianze kufanya kazi ya kuzalisha matairi nchini.

“ Tumeanzisha viwanda nchi ili kuzalisha bidhaa na kutoa ajira kwa watanzania na sio kuwatesa wananchi kwa kukosa ajira au kuagiza bidhaa ambazo tunaweza kuzalisha hapa hapa nchini, hivyo basi Serikali kupitia Wizara yangu tutatenga fedha kwa ajili ya kufufua kiwanda hiki ili kianze kufanya kazi mara moja”

“ Sio tu tutafufua kiwanda cha General Tyres pekee bali tunafatilia viwanda vyote ambavyo vimekiuka sheria na kanuni kwa kutoviendeleza viwanda hivyo ili kuvirudisha mikononi mwa Serikali au kuwatafuta wawekezaji wengine watakaoweza kuviendesha viwanda hivyo” Alisema Mhe. Mwijage.

Aidha Mhe. Charles  John Mwijage amesema ni kweli makampuni mengi yaliyobinafsishwa hayakufanya vizuri katika uendeshaji wake ukiacha mifano ya makampuni machache yanayofanya vizuri yakiwemo Tanzania Breweries Limited (TBL),Morogoro Polyester 21st Century na Tanzania Cigarette Company Limited (TCC), hivyo Wizara yangu ikishirikiana na Msajili wa Hazina juu ya Viwanda ilifanya tathmini iliyoonesha kuwa mashirika mengi yaliyobinafsishwa hawakutekeleza mikataba ya mauziano kikamilifu.

Ameongeza kuwa lengo ni kuhakikisha makampuni yote haya yanazalisha kwa tija ili tupate bidhaa,kodi ya Serikali na ajira kwa wananchi wa Tanzania ili kutimiza adhma ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli ya kuwa na Tanzania yenye viwanda kwa maendeleo ya taifa.

Serikali kupitia Wizara yetu inaboresha mazingira ya uwekezaji hali itakayowajengea imani kwa wawekezaji na kupelekea kupanua zaidi shughuli zao za kibiashara na pia kuendeleza mpango wa Viwanda vidogo na vya kati unaoshirikisha SIDO na Halmashauri za Wilaya na Mikoa ili kuanzisha Viwanda vya Mkoa vya kuongeza thamani ya bidhaa za Kilimo,Uvuvi na ufugaji kupitia njia hii ajira nyingi zitaongezeka na kupunguza tatizo la ajira nchini.

Maalim Seif Afunguka ' Wazanzibar Wapenda Amani Ondoeni Shaka Nitatangazwa Kuiongoza Zanzibar'

$
0
0
ALIYEKUWA mgombea urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF) visiwani Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amewataka Wazanzibari na wapenda amani kuondoa shaka na kwamba, atatangazwa kuongoza visiwa hivyo. Anaandika Mwandishi Wetu.

Maalim Seif ametoa kauli kwenye viwanja vya Nngoma Hazingwa, Chake Chake Pemba akiwa na viongozi wa wilaya, majimbo na jumuiya za chama hicho ikiwa ni siku moja baada ya kufanya mkutano wa namna hiyo Unguja.

Kiongozi huyo ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF amesema kuwa, ukweli umedhihiri ndani na nje ya nchi na kwamba hakuna sababu ya kutotangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana.

Amesema, “jumuiya na waangalizi wote wa uchaguzi wa kitaifa na kimataifa wameshuhudia uchaguzi huo na kujiridhisha kuwa ulikuwa huru, haki na wa uwazi na wanaendelea kushikilia msimamo wao kutaka mshindi wa uchaguzi huo atangazwe.”
Amesisitiza kuwa CUF haitoshiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi mwaka huu kauli ambayo pia imeungwa mkono na wafuasi wa chama hicho Pemba kama ilivyokuwa Unguja.

Mapema Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui amemtaja Maalim Seif kuwa kiongozi aliyebobea kisiasa na anayejali maslahi ya Wazanzibari.
Katika hatua nyingine mawakilishi na madiwani wateule wa CUF kupanga kwenda mahakamani kutetea nafasi zao.

Wameeleza kwamba, kwa kuwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imewapa hati za ushindi baada ya kufanya uchaguzi mkuu tarehe 25 Oktoba 2015, mpaka sasa hakuna aliyejitokeza kupinga ushindi wao.

Hata hivyo, Maalim Seif amesema, viongozi hao waliochaguliwa na wananchi katika uchaguzi huo na kisha kupewa shahada zao, watakwenda mahakamani kutetea nafasi zao na kutoruhusu viongozi wengine wa ngazi hizo kuchaguliwa tena kwa vile wao wanavyo vielelezo vyote vya kuchaguliwa kwao.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi yaliyobandikwa katika vituo vya kupigia kura na kuthibitishwa na wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo, majimbo yote 18 ya uchaguzi Kisiwani Pemba yalichukuliwa na CUF, sambamba na wadi zote 32 za uchaguzi.

Afisa wa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam Akamatwa na Takururu Kwa Tuhuma za Kuomba na Kupokea Rushwa

$
0
0
 Mkuu wa TAKUKURU (M) Ilala,
S.L.P 6420, Kinondoni
Simu : (022)2861088 Nukushi 2150047
Barua pepe: rbcilala guy@pccb.go.tz
Wavuti www.pccb.go.tz

Ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Ilala imemkamata afisa wa ofisi ya uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam kwa tuhuma ya kuomba shilingi milioni 1 na kupokea Shilingi laki 5 kutoka kwa mfanyabiashara mwenye asili ya Kisomali mnamo tarehe 4 Februari, 2016.


Bw.Kiangwike Ngumba mwenye cheo cha afisa mkaguzi wa uhamiaji alikamatwa baada TAKUKURU kupokea taarifa kutoka kwa Bw.Bille Mohamed kuwa mtuhumiwa na maafisa wengine walifika katika eneo lake la biashara na kuchukua hati ya kusafiria ya ndugu yake kwa madai kuwa wanakwenda kuifanyia ukaguzi. Hata hivyo, baadaye afisa huyo alimtaka mtoa taarifa kutoa kiasi cha shilingi milioni moja kama sharti la kurejesha hati hiyo.

Uchunguzi wa tuhuma hii unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwafuatilia na kuwachunguza maafisa wengine waliohusika ili wafikishwe mahakamani. Afisa huyo na wenzake wanakabiliwa na tuhuma ya kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007.

Tunatoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kuripoti vitendo au viashiria vyovyote vya rushwa dhidi ya watumishi wasio waadilifu katika ofisi za TAKUKURU ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

IMETOLEWA NA RAPHAEL MBWAMBO- MKUU WA TAKUKURU MKOA WA ILALA 05/2/2016
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images