Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104664 articles
Browse latest View live

Polisi Dar Yakamata Magari 2 Yaliyotumika Kubeba Kompyuta Zilizoibwa Kwenye ofisi ya Aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Philip Mpango.

$
0
0
Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata magari mawili yakihusishwa na wizi katika ofisi ya kamshina mkuu wa TRA huku yakiwa na vifaa vilivyoibiwa katika ofisi hiyo vikiwa ni pamoja na komputa  na TV.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema kutokana na oparasheni kali iliyokuwa ikiendeshwa na jeshi ilifanikiwa kuwatia nguvuni watuhumiwa wanne wakiwa na vifaa vilivyoibiwa.

Ameyataja magari hayo  kuwa ni Toyota Noah yenye namba za usajili T 989 CNV  na Mitubish Pajero yenye namba za usajili T 386 CVV .Pia  walinzi wawili waliokuwa zamu kulinda siku hiyo wamekamatwa.

"Katika wizi huo vitu vilivyoibwa ni Compyuta mbili, aina ya Dell pamoja na CPU, Monitor zake na Televisheni moja aina ya Sumsung inchi 40" Alisema Sirro.
Aidha kamanda huyo wa kanda maalum ya Dar es Salaam amesema katika oparesheni hiyo pia jeshi la polisi lilifanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi milioni 150 mali ya Bw Ahmed Huwel mkazi wa Msasani.

Katika hatua nyingine kamanda Sirro ametangaza kusitishwa kwa muda kwa shughuli za ulinzi shirikishi katika vituo vya polisi kutokana na vikundi hivyo kualamikiwa na wananchi kwa kutokuwa na tija katika jamii

Maandammano ya CHADEMA Kesho Kuelekea Ikulu Yapigwa Marufuku

$
0
0
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika hapo kesho na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuelekea Ikulu jijini Dar es salaam kushinikiza kurejeshwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Naibu Kamishna wa Polisi Simon Siro amesema Chama hicho kinatakiwa kutumia mbinu nyigine ya kushinikiza kurejeshwa kwa matangazo hayo ya Televisheni ya Taifa na sio kupitia maandano.

Huyu Ndio Lady Boss wa Ukweli Sio Hao Wengine Kutwa Kucha Kutuigizia Maisha Feki Instagram

$
0
0
Anaitwa Jacqueline Ntuyabaliwe aka K-Lynn Miss Tanzania 2000 na Mwanamuziki, Mke wa Bilione Reginald Mengi........

Nimekutana na Comments Mbali mbali Instagram Baada ya Picha hii kuzagaa mitandaoni leo hii
embu na wewe jisomee baadhi ya comments kutoka Instagram;

fetttyy 
Huyo ndo boss lady Africa nzima ndo hapigi kelele wala kujionyesha onyesha anajua anazo lakini hawa visokorokwinyo wengine ngachoka miyeeee kutwa kutuigizia insta

mariebellahfonte 
Njoen mumuone boss lady Wa ukweli



 angie_jansie 
Watoto wa kigoma hatunaga makuu huwa tunasemaga papa Asante kwel wewe ni Mungu tu.....


 paulina_minango 
Kwakweli huyu ndie bosslady wengine wanatafuta kiki tu mjini anajielewa huyu dada mrs mengi#jn_mengi


hallopkingu 
@kittynswe ahaha nilijua ni mm tuu ndo namkubali huyo bosslady.. woman of class


tedysilla___ 
Nampenda mnooo uyu dda anajielewa michirz angekuwa na maisha kama ya uyu dda tungekoma


Idriss Amjibu Shabiki Kuhusu Wema Kupunguza Kwenda Club Akiwa Mama Kijacho...Idriss Adai Atakaye Mgusa Atamuua

$
0
0
Idriss Amjibu Shabiki Kuhusu Wema Sepetu Kupunguza Kwenda Club Akiwa Mama Kijacho...Idriss Adai Atakaye Mgusa Atamuua

Jisomee Hapa;

Wolper Atendwa Tena?, ‘Wakati Mwingine Unaweza Ukajiona Umempata Kumbe Umepatikana’

$
0
0
Staa wa filamu Jacqueline Wolper ameibua maswali mengi kwa mashabiki wake wa filamu katika mitandao ya kijamii baada ya kuandika ujumbe unao onyesha huenda ametendwa katika mapenzi.

Muigizaji huyo ambaye mwisho wa mwaka jana (2015) alimtambulisha mpenzi wake mpya kwa mashabiki wake baada ya kuvalishwa pete, Ijumaa hii ameweka wazi yale yanayomsibu moyoni hali iliyowafanya mashabiki wake watafsiri ametendwa.

Kupidia instagram, Wolper ameandika:

"Maisha yana mitihani migumu saana wakati mwingine unaweza kujiona umempata kumbe umepatikana. Unaweza hata kukufuru Mungu lakini kuna kale kausemi kanachosema tunajifunza kutokana namakosa me nimeanza kuzingatia misemo baada yakukua mkubwa.
Unaweza ukahsi unaishi na mjusi kumbe unaishi na nyoka mwenye sumu kali akikung’ata auponi ewwwe Mungu nipe nguvu eewe Mungu wangu nitoe upofu eewe Mungu washa taa kwenye giza nene nililopo ili nipate muangaza"

Haya ni maoni ya mashabiki wake wa instagram

kate_brown538
Ushaachwa ivo ba pete kidolen hamna kiruuu, nenda kwa mond

zai2n1804
Asante Dada @wolperstylish kwa ujumbe wako mzuri japo wengi wamehisi tofauti kutokana na maneno uloyasema hapo juu ila Mimi nimeelewa vizuri sana thanks again coz nimejifunza kitu kutokana na ujumbe wako barikiwa sana

chegya_boy_
Pole sana my mungu yupo yote mapito IPO siku mungu atakuonesha chaguo llako xo omba mungu

Jose Mourinho Anatua Man United? Safari Hii Imetajwa Hadi Tarehe Rasmi …

$
0
0
Stori za kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea ya Uingereza Jose Mourinho kujiunga na klabu ya Manchester United zinazidi kushika kasi, licha ya kuwa ni tetesi hadi sasa kuhusu Jose Mourinho kurithi nafasi ya Louis van Gaal ndani ya Man United, stori hiyo inapata nguvu baada ya stori nyingi mwishoni mwa mwaka 2015 zilizoanza kuandikwa kama tetesi zote zilitimia.

Zilianza stori za Raphael Benitez kuwa atafukuzwa Real Madrid kweli stori hiyo ikawa kweli, Jose Morinho kufukuzwa Chelsea ikawa kweli, Pep Guardiola kuwa kocha wa Man City, kweli Man City wamethibitisha, stori mpya kutoka Marca gazeti ambalo stori zake zinaaminika, limetaja tarehe rasmi ya Jose Mourinho kutua Man United.

Marca wameandika kuwa Jose Mourinho atakuwa kocha mpya wa Man United kuanzia July 1 2016, licha ya kuwa Marca wanaripotiwa kuandika stori hiyo kama tetesi, lakini inapata nguvu kutokana na stori nyingi zilizoandikwa kama tetesi msimu huu zimekuwa kweli.

Gazeti la Marca linataja kuwa kama Louis van Gaal akiendelea kufanya vibaya kabla ya msimu huu kumalizika atafukuzwa na nafasi yake kurithiwa kwa muda na Ryan Giggs ambaye ni kocha msaidizi na July 1 Jose Mourinho ndio anatajwa kuwa atakuwa kocha rasmi wa Man United.

Waasi Wa Burundi Wakimbilia Nchini Kushawishi Watanzania Wajiunge Na Vikundi Vya Waasi

$
0
0
BAADHI ya askari waasi wa Burundi, wamebainika kukimbilia nchini na kuanza kushawishi vijana wajisajili ili wajiunge na vikundi vya waasi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema hayo jana alipokuwa akifunga Mkutano wa Pili wa Bunge mjini Dodoma jana na kuwataka wakimbizi na wananchi, kushirikiana na vyombo vya usalama, kutoa taarifa za uhalifu.

“Kutokana na ujio wa wimbi kubwa la wakimbizi kutoka Burundi, kumejitokeza matukio ya uhalifu wa kutumia silaha za moto ndani na nje ya kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu.“

"Aidha, kutokana na upekuzi na ukaguzi kwa wakimbizi unaofanywa kwa pamoja na vyombo vya dola sanjari na taarifa za ki-intelijensia, imebainika kuwepo kwa askari waasi waliokimbia pamoja na raia wa kawaida, ambao wanajaribu kuwashawishi vijana kujisajili ili kujiunga na vikundi vya waasi,” alisema Majaliwa.

Pamoja na changamoto hiyo, ambapo kambi za wakimbizi zilizoko mikoa ya Kigoma, Katavi, Tabora na Tanga zinahifadhi wakimbizi wapatao 218,895 kutoka mataifa ya Burundi (156,377), Congo-DRC (62,176), Somalia (150) na mataifa mchanganyiko (192) ikiwemo Rwanda, Uganda, Sudan Kusini na Ethiopia, hali usalama katika nchi kwa ujumla ni shwari.

Akizungumzia kuimarisha maadili na utendaji serikalini, Majaliwa alisema Serikali imedhamiria kurejesha nidhamu na maadili ya watendaji wa Serikali na watumishi wa umma katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi.

“Katika kuhakikisha watumishi wa umma na Watanzania wote wanafanya kazi, Mheshimiwa Dk John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekuja na kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu.

 “Tafsiri ya falsafa hii ni kuwataka Watanzania wote katika nafasi mbalimbali walizopo, kufanya kazi kwa bidii na kujiepusha na vitendo vya uzembe, urasimu na kutenda kazi kwa mazoea,” alisema.

Alimtaka kila mwananchi, kuwa na nidhamu ya kazi na kuhakikisha anafikia malengo yaliyowekwa na kuwakumbusha watumishi wa umma kuwa, wamepewa dhamana ya kuwahudumia wananchi kwa niaba ya Serikali.

Kwa kuzingatia wajibu huo, amewataka watumishi hao kuhakikisha wanawahudumia wananchi kwa haki, weledi, uadilifu na kwa taaluma zao na kuhakikisha kuwa wanatatua kero za wananchi.

Waziri Mkuu alisema wanatambua kuwa wapo watumishi wanaotekeleza vyema majukumu yao, lakini pia wapo watumishi ambao hawazingatii maadili ya kazi zao na pia wanafanya kazi kwa uzembe.

“Serikali haitaacha kuchukua hatua za nidhamu kwa watumishi wote wasiozingatia kikamilifu sheria, kanuni na taratibu katika utumishi wa Umma.

"Aidha, kwa kuzingatia maelekezo ya Mheshimiwa Rais, viongozi na watumishi wote wa umma lazima tufanye kazi kwa kuzingatia weledi na kujiamini. Kila mtu anapaswa kujitathmini kama dhamana aliyopewa anaitendea haki,” alisema.

Kuhusu dhana ya kutumbua majipu, Majaliwa alisema Rais ametumia dhana hiyo kusimamia uwajibikaji, hasa kwa wale wenye dalili ya kukosa maadili ya utumishi wa umma.

“Tafsiri ya dhana hii ya “Kutumbua jipu” inalenga katika kuwarejesha watumishi wa umma na walioko serikalini katika mstari mzuri wa utendaji. Nitoe mwito kwa waheshimiwa wabunge wote kama tulivyo na kwa umoja wetu tumuunge mkono Mheshimiwa Rais katika vita hii kubwa ya ‘Kutumbua Majipu’.

“Tukiwa pamoja na kwa kushirikiana tutaweza kuibadilisha nchi yetu kuwa nchi ya maadili na yenye sifa ya juu katika utendaji wa utumishi wa umma,” alisema.

Kuhusu elimu, Majaliwa alisema tangu Rais Magufuli atoe maelezo ya utekelezaji wa elimu msingi bila malipo, kumekuwa na umuhimu wa kutoa elimu na ufafanuzi zaidi juu ya utekelezaji wa agizo la elimu bila malipo kwa Watanzania kuanzia darasa la awali hadi kidato cha nne katika shule za umma.

Alisema katika mpango huo, Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa mwanafunzi atasoma kuanzia darasa la awali hadi kidato cha nne bila ya wazazi na walezi kulipa ada ya shule, gharama za mitihani na michango mbalimbali.

“Hata hivyo, yapo majukumu ambayo yataendelea kutekelezwa na wazazi na walezi ambayo ni pamoja na kununua sare za shule na michezo, madaftari, kalamu na chakula kwa wanafunzi wa shule za kutwa.

“Maeneo mengine ni kulipia nauli ya kwenda na kurudi shule, na mahitaji mengine kama kununua godoro, shuka na vifaa vya usafi binafsi. Mzazi au mlezi ana wajibu wa kugharamia matibabu ya mtoto wake,” amesema.

Kuhusu elimu ya juu, amesema hadi kufikia mwishoni mwa Januari 2016, Serikali ilikuwa imetoa mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 207.9 kwa wanafunzi 122,786 wa elimu ya juu, wakiwemo wanafunzi wa mwaka wa kwanza 53,850 ambao ni asilimia 98.9 ya wanafunzi 55,254 walioomba mikopo hiyo.

Kuhusu uendeshaji wa Bunge, Majaliwa alisema uzoefu alioupata katika muda mfupi aliokaa pamoja na wabunge Dodoma, amegundua kuwa kuna wabunge mahiri waliobobea katika nyanja mbalimbali.

Alisema amebaini wapo wasomi wa ngazi zote, wazee kwa vijana ambao wana uzoefu na utaalamu mkubwa na kuongeza kuwa wakitumia utaalamu na uwezo mkubwa walionao katika kuijenga nchi, nchi itapiga hatua.

Aliwataka wabunge watangulize uzalendo katika kila jambo wafanyalo kwa manufaa ya Taifa na watu wake, ili nchi ifike mahali ambapo kwa elimu, busara na hekima na kwa kuacha ushabiki wa kisiasa, watazame mbele katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Rais Magufuli: Waliotelekeza Mashamba na Viwanda, Wavifufue Haraka Sana la Sivyo....

$
0
0
Rais Dk. John Magufuli amewataka watu wote waliotelekeza Mashamba na Viwanda walivyouziwa na serikali, kuhakikisha wanafufua mashamba na viwanda hivyo mapema iwezekanavyo, kabla serikali haijawanyang’anya na kuwagawia wanaoweza kuviendesha.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake njiani akiwa safarini kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma ambapo amesema mkoa wa Morogoro ulikuwa na viwanda vingi na mashamba mengi makubwa ambayo kama waliouziwa wangeyaendeleza, yangezalisha ajira na kuongeza uzalishaji wa bidhaa za viwandani na Mazao ya kilimo, lakini waliouziwa mashamba na viwanda hivyo wameamua kutekeleza ama kubadilisha matumizi, huku baadhi wakitumia rasilimali hizo kuombea mikopo katika mabenki jambo ambalo serikali yake haitalikubali.

Rais Magufuli pia amesimamishwa na kuwasalimu wananchi wa Wami Dakawa, Magole na Dumila ambako pamoja na kuwahakikishia kuwa atatekeleza ahadi yake ya kuwapa mashamba atakayonyang’anya kutoka kwa walioyatelekeza, amewataka kuachana na migogoro kati ya wakulima na wafugaji badala yake watatue migogoro hiyo kwa kutumia njia za kisheria.

Aidha, amewataka viongozi wote wa Mkoa hadi vitongoji kushirikiana kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji kabla haijasababisha madhara, na ameonya kuwa migogoro hiyo ikileta madhara itakuwa ni kigezo tosha kwa viongozi hao wameshindwa kutekeleza wajibu wao na wanapaswa kuachia ngazi.

Maskini Mimba ya Mwigizaji Kajala Yadaiwa Kuchoropoka..Kisa....

$
0
0
Baada ya kunasa ujauzito ambao ulisemekana ni wa kigogo mmoja serikalini, bahati haikuwa yake mwigizaji Kajala Masanja kwani mimba hiyo imechoropoka. Rafiki wa karibu na mwigizaji huyo ameliambia Risasi Jumamosi kuwa mwigizaji huyo aliugua malaria ambapo dawa alizokunywa zimemsababishia mimba hiyo ichoropoke.

“Nahisi ni madawa ya malaria aliyokunywa, huwezi amini alijisikia vibaya baada ya kumeza, ghafla akashangaa mimba imetoka,” alisema rafiki huyo wa karibu na Kajala. Ubuyu huo ulipotua kwenye dawati la Risasi Jumamosi, mwanahabari wetu alimtafuta mwigizaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja (Paula) ambapo alipopatikana alikiri kuwa mimba hiyo imetoka kwa bahati mbaya. 

“Imeniuma sana maana mwanangu alikuwa akitaka mdogo wake lakini ndiyo hivyo tena dawa zimenisababishia madhara nafikiri, mimba imetoka,” alisema Kajala.

Global Publishers

Tathimini: Naibu Spika wa Bunge Anayumbishwa na Bunge, Awe Mtulivu

$
0
0
Toka bunge la 11 limeanza nimeshuudia uongozaji wa bunge kwa spika na naibu wake pamoja na wenyeviti.

Ila kwa tathimini ya haraka niliyofanya mpaka hapa bunge lilipofikia,na kiri wazi naibu spika Tulia ndio kaonyesha kushindwa,Amejawa na hisia na gadhabu na si mvumilivu.

Yapo mambo madogo anayostahili kuyaacha kama changamoto lakini amekuwa akipaniki na kung'aka
Tuelekeapo asipojirekebisha kiti kitampwaya na bunge litakosa mwelekeo,Ni vema Mhe.Tulia ajifunze utulivu alio nao Spika na wenyeviti.

By Kibo10/JF

Johari: Nimemchuna Sana Ostaz Juma Namusoma Lakini Hakuambulia Kitu Kwangu....

$
0
0
Mkongwe kwenye sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amevunja ukimya na kuweka bayana kuwa miaka kadhaa iliyopita aliwahi kumchuna sana Mkurugenzi wa Kampuni ya Watanashati Entertainment, Ostaz Juma Namusoma alipokuwa akimhitaji awe mchumba wake.

Johari alifunguka hayo hivi karibuni baada ya mwanahabari wetu kumfungia safari hadi ofisini kwake Sinza-Mori, jijini Dar es Salaam na kumuuliza juu ya taarifa zilizokuwa kwenye makabrasha yetu kwamba mwigizaji huyo miaka kadhaa iliyopita, aliwahi kumchuna sana Ostaz Juma lakini habari hizo hazikuandikwa gazetini.

“Mh! Jamani hayo mambo ya zamani. Ujue watu wamekuwa wakinisumbua sana na ishu ya kusema mimi niliwahi kutoka kimapenzi na Ostaz Juma Namusoma jambo ambalo si kweli, Ostaz Juma aliwahi kunitongoza siku nyingi sana bado nipo Kaole na alikuwa akija mazoezini karibia kila siku ila mimi nilikuwa simtaki hata kumsikia.

“Kutokana na kuwa na mkatalia mara kibao kwa kuwa alikuwa na fedha alikuwa akinipatia fedha si unajua yule ni tajiri, ukipiga hesabu vizuri kama ningekuwa najenga basi leo hii ningekuwa hata na maghorofa mawili kupitia fedha alizokuwa akinipa, alikuwa ananipatia kila siku ya Mungu fedha na marafiki zangu pia ila mimi tu nilikuwa nikimkataa hivyo kuwafanya marafiki zangu kunishangaa ingawa na wao walinufaika.

“Ostaz Juma alikuwa na kawaida ya kunifuata kila siku mazoezi huko Kigogo na akija ananinunulia kila kitu na mara nyingine ananikodia usafiri wa kunirudisha nyumbani lakini pamoja na hivyo niliishia kutumbua fedha zake nyingi na hakuweza kunipata jambo ambalo aliendelea kunisisitizia kuwa lazima siku moja angeweza kuwa na mimi japo hakufanikisha kunipata,” alisema Johari. Ostaz Juma ambaye amekuwa akiwasaidia wanamuziki mbalimbali nchini kifedha, hakutaka kuzungumzia ishu hiyo kwa kudai ni ya zamani sana, kwa sasa ameoa na anaendesha familia yake.

Global Publishers

Ukiona Dalili Hizi Jua Kuwa Kwa 100% Mpenzi Wako/ Mke Wako Anakusaliti

$
0
0
  • Anakuchangamkia wewe mpenzi au mume wake kupita maelezo.
  • Hakuombi pesa yoyote ile.
  • Kila mara anapenda kukupigia simu na kukupa maneno matamu na ya kimahaba zaidi.
  • Hapendi uwajue ndugu zake wote au marafiki zake wote.
  • Ukiwa nae katika gari hunyamaza au hujifanya yupo busy na mambo yake au simu.
  • Anapenda sana kudadisi kujua unapokea au unapata mshahara kiasi gani huko kibaruani kwako.
  • Hupenda kumsifu sana best friend wako.
  • Mkiwa mnashiriki tendo la ndoa au mnazini huwa hakupi ushirikiano zaidi ya kukutaka uharakishe.
  • Hata upendeze vipi hawezi kukusifia.
  • Ukimpa zawadi au kumfanyia chochote kizuri huwa hakuambii asante na hujifanya yupo busy.
  • Ukiwa nae hujifanya hapendi kabisa stori za kungonoka na mara nyingine hata hukasirika.

Kazi kwako na chukua tahadhari usije ukawa unajitapa au unatamba kumbe unachoreka tu au unasaidiwa na wenzio katika kulisukuma gurudumu la mapenzi.

AL SHABAAB Is Dying! See What They Are Doing to Women Out of Desperation Just to Survive

$
0
0
It appears the intensified efforts to hunt down Al Shabaab terrorists deep into Boni Forest by the gallant Kenya Defence Forces (KDF) is taking a toll on the militants and could starve them to death.

This was revealed by a senior police officer in Lamu, who said that the Al Shabaab have resorted to doing desperate things just to survive.


According to the officer who declined to be named for obvious reasons, the Al Shabaab have been raiding some villages near the forest in Lamu and forcing women to cook for them.

He said the terrorists have run out of food supply and often come to the villages to beg for food and water just to survive.

“The militants have no place to get food and have resorted to get it from residents or attacking new areas within Lamu (that are not in ‘KDF zones’),” said the officer.

He added that some of them have even resorted to living among locals so as to camouflage and shield themselves from the ongoing KDF operation dubbed Linda Boni.

“Some of the militiamen are also believed to be living among locals or disguising as herdsmen. Locals have a lot of information about these people. If they share it with us, we shall flush the extremists from the area in a very short time,” he said.

Kenyan News

LADIES, Here’s The Secret to Happy Marriage, Thank us Later

$
0
0
1). Never raise your voice for any reason to your husband. Its a sign of disrespect.(Prov 15v1)

2). Don't expose your husband's weaknesses to your family and friends. You are each other's keeper.(Eph 5v12)

3). Never use attitudes and moods to communicate to your husband, you never know how your husband will interpret them.(Prov 15v13)


4). Never compare your husband to other men, you've no idea what their life is all about.

5). Never ill treat your husband's friends because you don't like them, the person who's supposed to get rid of them is your husband.(Prov 11v22)

6). Never forget that your husband married you, not your maid or anyone else. (Gen 2v24)

7). Never assign anyone to give attention to your husband, people may do everything else but your husband is your own responsibility.(Eph 5v33)

8. Never blame your husband if he comes back home empty handed. Rather encourage him (Deut 3v28)

9). Never be a wasting wife, your husband's sweat is too precious to be wasted.

10). Never pretend to be sick for the purpose of denying your husband sex (SS 7v12

11). Never compare your husband to your one time sex mate in bedroom.(SS 5v9)

12). Never answer for your husband in public opinion polls, let him handle what is directed to him although he may answer for you in public opinion polls.(Prov 31v23)

13). Never shout or challenge your husband in front of children(Eph 4v31)

14). Don't forget to check the smartness of your husband before he checks out.(Prov 12v4)

15). Never allow your friends to be too close to your husband.

16). Never be in a hurry in the bathroom and on the dressing table. Out there your husband is always surrounded by women who took their time on their looks.( 1 Sam 25v3)

17). Your parents or family or friends do not have the final say in your marriage. Don't waste your time looking up to them for a final word.(Luke 21v16)

18). Never base your love on monetary things. Will you still submit to him even if you earn more money than him?

19). Don't forget that husbands want attention and good listeners, never be too busy for him. (Gal 6v9)

20). If your idea worked better than his, never compare yourself to him. Its always teamwork. (Gal 6v10)

21). Don't be too judgemental to your husband.(Eph 4v29)

22). A lazy wife is a careless wife. She doesn't even know that her body needs a bath.(Prov 24v27)(Prov 20v13)

23). Does your husband like less cooked food?, try to change your cooking.(Prov 31v14)


24). Never be too demanding to your husband, enjoy every moment, resource as it comes.(Luke 11v3)

25). Make a glass of water the very first welcome to your husband and everyone entering your home. Sweetness of attitude is true beauty. (Prov 31v11)


26). Don't associate with women who have a wrong mental attitude about marriage.(Prov 22v14)

27). Your marriage is as valuable to you as the value that you give it. Recklessness is unacceptable.(Heb 13v4)

28). Fruit of the womb is a blessing from the Lord, love your children and teach them well.(Prov 22v6)

29). You are never too old to influence your home. Never reduce your care for your family for any reason. (Prov 31v28)

30). A prayerful wife is a better equipped wife, pray always for your husband and family(1 Thess 5v17)

Mwenyekiti Wa CCM, Jakaya Kikwete Aomba Wazee Wamuunge Mkono Rais Magufuli

$
0
0
MWENYEKITI  CCM, Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amewaomba wazee kote nchini, kumuunga mkono Rais John Magufuli katika uongozi wake ili kumpa moyo wa  kuwatumikia Watanzania.

Amesema kipindi ambacho Dk Magufuli ameingia madarakani hadi sasa ni muda mfupi, hivyo si vema kuanza kudodosa na kulaumu panapopwaya, badala yake Wazee na watanzania kwa jumla wazidi kumuunga mkono ili kumtia moyo wa kutekeleza  yote aliyokusudia kuyafanya kwa manufaa ya taifa.

Kikwete alitoa ombi hilo alipokuwa akizungumza katika mkutano na wazee wa Mkoa wa Singida, ambapo alisema kuwa kuongoza bila ushauri wa wazee nchi inaweza kuyumba.

“Kuongoza nchi bila wazee mambo hayaendi vizuri na  ukikosa mzee kwenye jahazi wapiga makasia vijana wanaweza kuanza kuzozana na chombo kwenda mrama, lakini wakiwepo wazee watawaongoza vizuri  na chombo/ nchi kwenda  salama”. Alisema Kikwete huku akishangiliwa na wazee.

Alisisitiza kwamba ukitaka nchi itulie kamata wazee, lakini ukiongoza nchi kwa kutumia vijana  pekee nchi inaweza kuyumba, na itafika mahali mtakosa mahali pa kushika.

Alisema kuwa hata yeye kwa mara ya kwanza .alipokwenda kuomba ubunge jimboni kwake Bagamoyo, Pwani aliunda kamati ya wazee ambayo ilimsaidia sana.

Wazee ni sehemu ya matumaini ya chama na Serikali, panapokuwepo  wazee hapaharibiki jambo.

 “Nawashukuru sana wazee endeleeni kukijenga chama na kuiunga mkono Serikali inayoongozwa sasa na Dk John Magufuli.” Alisisitiza Kikwete na kuongeza kuwa,

“Hata kwenye chama chetu tumeunda Baraza la Washauri la Wazee wasitaafu ambapo wengi walipinga. Hata hao wazee tuliowataka waunde baadhi yao walipinga, lakini mwisho walikubali kwa masharti kwamba wawe wanaitwa panapotokea jambo kubwa litakalohitaji ushauri wao.”

Alisema mmoja wa viongozi aliyekuwa msitari wa mbele kuunda baraza hilo alikuwa Rais msitaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ambaye alitoa ushauri wa kuitwa kutoa ushauri panapotokea jambo kubwa na kwamba hata wakitoa ushauri, viongozi waliopo madarakani wawe hiari kuukubali au kuukataa.

Aliwataka wazee kuendelea kuiunga mkono serikali ya sasa ambayo kwa hivi sasa imetimiza muda mfupi wa miezi mitatu ambaye ni sawa na mtoto mdogo anayekua.

Alisema kuwa Jambo kubwa ni kuwaunga mkono, kuliko kuwalaumu ama sivyo watavunjika moyo, ndani ya miaka mitano itakuwa hasara. ...."Watieni moyo ili wajiamini wahudumie vizuri zaidi ili nchi isonge mbele kimaendeleo."

Kikwete alisisitiza kuwa hata yeye akitakiwa kwenda kutoa ushauri atakwenda  na akiwa na jambo la kushauri atakwenda pia, lakini aliwaasa kuwa  si kila jambo wazee watake kwenda kutoa ushauri, itachelewesha mambo mengi.

BASATA yaitaka kamati ya Miss Tanzania imalize tofauti yake na kampuni ya Lino

$
0
0
Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA limeitaka kamati ya Miss Tanzania iliyojiuzulu mapema mwaka huu kukaa chini na waandaji wa shindano hilo, Lino Agency kumaliza tofauti zao.

Kupitia Twitter BASATA limeandika:

BASATA imeitaka kampuni ya LINO waandaaji wa Miss Tanzania kurudi mezani na kamati ya shindano kujadiliana namna bora ya kusonga mbele. Imeiagiza LINO kuandaa MoU na kamati ya shindano la Miss Tanzania ili kuchora mipaka ya kiutendaji baina yao.

Kama ya shindano la Miss Tanzania, ilitangaza kujiuzulu kwa kile mwenyekiti wa kamati ya maandilizi ya shindano hilo Juma Pinto, kudai ni kutokana na kushindwa kujua nini majukumu yao na yale ya kampuni inayoyaanda, Lino.

Alidai kuwa awali iliwekwa wazi kuwa ni kamati hiyo ndiyo itakayoratibu mashindano hayo huku Lino Agency ikibaki kuwa washauri.

Pinto alisema Lino imeendelea kufanya kazi yake lakini wao wakibaki bila kujua kinachoendelea. “Sisi tumeona tuje tuzungumze tu kwamba sisi hatupo huko,” amesema Pinto.

Naye msemaji wa kamati hiyo, Jokate Mwegelo alisema kutokana na ukubwa wa kile Miss Tanzania imefanya kwa wasichana, wasilichukulie kwa wepesi na kiubinafsi.

“Waangalie wasichana wa Tanzania wanawatoaje? Na kuwatoa ni kuhakikisha kwanza misingi ya shindano lenyewe iwe ya kueleweka. Kama misingi haieleweki ndio tunarudi kule kule,” amesema Jokate.

Aliongeza kuwa makosa yaliyojitokeza miaka iliyopita pamoja na malalamiko mengi dhidi ya shindano hilo yanapaswa kufanyiwa kazi.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Asema Rais Magufuli Hana Mamlaka Kikatiba Ya Kuingilia Mambo Ya Zanzibar

$
0
0
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju amesema Rais John Magufuli hana mamlaka ya kikatiba ya kuingilia masuala ya Zanzibar ukiwamo uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20.

Hii ni kauli ya pili kutolewa ndani ya wiki moja ikieleza hali hiyo, baada ya ile ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Luvuba aliyoitoa wiki iliyopita baada ya kufanya mazungumzo na Rais Magufuli, Ikulu, Dar es Salaam.

Akizungumza bungeni juzi, Masaju alisema: “Katiba ya Zanzibar si ya Muungano, masuala ya ulinzi na usalama ndiyo ya Muungano na ndiyo sababu ulinzi umeimarishwa visiwani humo kuhakikisha nchi hiyo inakuwa salama."

Alitoa kauli hiyo juzi jioni wakati akifafanua mambo mbalimbali yaliyozungumzwa na wabunge wakati wa mjadala wa mwongozo wa mpango wa Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha wa 2016/17 na Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka 2016/17.

Tangu kuibuka kwa mgogoro Zanzibar watu wa kada mbalimbali wamekuwa wakisema mwarobaini wa mgogoro huo kwa kutumia jitihada za ndani, ufanywe na Rais Magufuli baada ya jitihada za viongozi wa kisiasa visiwani kukwama.

Mgogoro huo, ambao umekuwa kawaida kuibuka kila baada ya Uchaguzi Mkuu, uliibuka baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salum Jecha kufuta matokeo Oktoba 28 na baadaye kuuitisha upya, kitendo ambacho CUF inakipinga.

Tangu wakati huo, Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd na marais wa zamani wa Zanzibar, Dk Salmin Amour, Ali Hassan Mwinyi na Amani Karume wamekuwa kwenye mazungumzo ambayo hayakuzaa muafaka.

“Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua uwepo wa Serikali mbili. Hizi Serikali uwepo wake ni Katiba ya Muungano na Katiba ya Zanzibar. Ukisoma Ibara ya nne ya Katiba si tu kwamba inaweka mgawanyo wa madaraka katika mihimili mitatu ya Dola, bali inaweka mgawanyo wa madaraka kati ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar.”

Ibara ya 4 ya Katiba inasema (1) Shughuli zote za Mamlaka ya nchi katika Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji, vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki na pia vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma.

(2) Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, vyombo vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki vitakuwa ni Idara ya Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Idara ya Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa ni Bunge na Baraza la Wawakilishi.

(3) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za umma katika Jamhuri ya Muungano, na kwa ajili ya mgawanyo wa madaraka juu ya shughuli hizo baina ya vyombo vilivyotajwa katika ibara hii, kutakuwa na mambo ya Muungano kama alivyoorodheshwa katika nyongeza ya Kwanza iliyoko mwishoni mwa Katiba hii, na pia kutakuwa na mambo yasiyo ya Muungano ambayo ni mambo mengine yote yasiyo ya Muungano.

(4) Kila chombo kilichotajwa katika ibara hii kitaundwa na kutekeleza majukumu yake kwa kufuata masharti mengine yaliyomo katika Katiba hii.

Masaju alisema Katiba ya Zanzibar ndio inayozaa ZEC.

“Kile ambacho baadhi ya wabunge wamekisema hapa ni kama kuitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuingilia mamlaka ya Zanzibar na tafsiri yake ni kama unataka kuleta hoja ya kujenga Serikali moja,” alisema.

Alisema kufanya hivyo ni kuvunja Katiba ya Muungano na ya Zanzibar na Serikali haiwezi kufanya hivyo

Ray Kigosi Apigilia Msumari Mwingine kwa Batuli

$
0
0

Staa wa filamu Vicent Kigosi, maarufu kama Ray ameeleza mustakabali wa filamu yake mpya inayokwenda kwa jina Tajiri Mfupi aliyomshirikisha ndani yake staa wa filamu Batuli ambaye anamtuhumu kwa kutokumlipa chake kwa ushiriki wake ndani ya kazi hiyo.

Ray amesema kuwa, filamu hiyo itatoka kama ilivyopangwa licha ya tuhuma za Batuli, akijitetea kuwa, hawezi kushindwa kumlipa mtu mmoja na kufanikisha kuikamilisha kazi hiyo waliyoifanya miaka 3 iliyopita tayari kwa kuiingiza sokoni.

Ray pia akatolea ufafanuzi hisia zilizoanza kujengeka kuwa, wametengeneza ugomvi huo na Batuli ili kuipatia kiki kazi yao, kitu ambacho amekipinga kwa nguvu.

Picha Za Maadhimisho Ya Miaka 39 Ya CCM Kitaifa Mkoani Singida

$
0
0
Msafara wa Mh. Rais John Pombe Magufuli ukiwasili kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida tayari kwa kuhudhuria sherehe hizo.
Mh.Rais Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Singida Mh. Dk. Parseko Kone
Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili uwanjani hapo katikati ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwapungia mikono wana CCM na wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akipokelewa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili kwenye maadhimisho ya miaka 39 ya CCM yanayofanyika kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mh. Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo mara baada ya kuwasili uwanjani hapo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akizungumza na Mh. Rais John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mh.Mama Samia Hassan Suluhu, Kushoto ni Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Move waliohudhuria katika maadhimisho hayo kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida.

Nafasi za Kazi NSSF na Coca Cola Kwanza LTD....Apply Here

Viewing all 104664 articles
Browse latest View live




Latest Images