Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

Ukweli Mchungu: Mwanamke ni Miguu na Makalio Sura Hata Mbuzi Anayo.

0
0
Tunaweza tukasema tu ilimradi tuoneka lakini huo ndio Ukweli. Mwanamke ni miguu na makalio ndivyo vinavyomfanya awe na mvuto popote pale. Angalia tu Mwanamke mwenye sura nzuri na yule mwenye makalio waongozane ni nani atakayetizamwa sana au kupigiwa miluzi. Na hii ndio iliyowapelekea wanawake wengi ambao ni vimbau mbau kutafuta hata makalio ya kichina ilimradi tu waonekane.

Sakata la Zari na Makalio Bandia Lashika Kasi Mtandaoni

0
0
Achana na habari zote zinazotikisa kwa sasa,habari ya Zari a.k.a Boss lady kuweka makalio ya bandia imeshika kasi.

Kama mtakumbuka majuzi hapo Zari alihudhuria hafla ya tangazo la Vodacom ambalo yeye na mwenzi wake Diamond wameingia mkataba wa kulitangaza bibie Zari alipigilia kigauni matata chekundu.

Hafla hiyo imezua minong'ono mingi kuhusu Zari wengi wakidai ni mzee kuliko anavyopost picha zake yeye mwenyewe (too much editing) maana wadau waliokuwa pale walimpiga picha original ambazo zimezua kizaazaa.

Achana na hilo la sura balaa kubwa lipo kwenye shape aliyoonekana nayo Zari kwenye hafla hiyo kuwa tofauti na ile tuliyoizoea hadi wadau kuhoji je bibie Zari nae ni mdau wa kigodoro? (kuvaa nguo za ndani zilizotuna kuboresha muonekano wa shape)

Maneno pembeni, hapa kuna picha za Zari kabla akiwa na shape tuliyoizoea na shape 'TATA'.


Mbuzi Na Kondoo 200 Wakatwakatwa Mapanga Wakituhumiwa Kuvamia Shamba La Mkulima Huko Mvomero Morogoro

0
0
Zaidi ya Mbuzi na kondoo 200 huko Dihinda mvomero Mkoani Morogoro wamekatwa katwa na walinzi wa jadi kutoka Gairo wanaojulikana kwa jina la Mwanu '

Taarifa zinadai kuwa mifugo hiyo ilikula nusu ekari ya mazao ya mkulima mmoja kijijini hapo na taarifa zikawafikia walinzi hao ambao walifika na kukatakata mifugo hiyo mali ya mama mmoja mjane mfugaji wa jamii ya kimasai

Lakini Inadaiwa kuwa mifugo ya mama huyo haikuhusika kula mazao hayo bali ni mifugo ya mfugaji mwingine.

Waziri mwenye dhamana kupitia wizara ya mifugo na kilimo hivi sasa ameelekea eneo la tukio .

CHADEMA yampigia magoti Dk. Slaa. Wamtaka Arejee Kwenye Ukatibu Mkuu, Mwenyewe 'Awatolea nje'

0
0
Kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, zimesambaa taarifa za CHADEMA kumuomba Dr Slaa kurejea chamani na kwenye nafasi yake ya Ukatibu Mkuu. Tafsiri ya ombi hilo la CHADEMA kwa Dr Slaa ni kwamba hawajapata mtu wa kuvaa viatu vya Dr Slaa ambavyo hakuna mwenye uwezo wa kuvivaa. Hapa maneno ya Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Tundu Lissu kuwa viatu vya Dr Slaa ni vikubwa na kwamba hakuna mwenye uwezo wa kuvivaa ndani ya CHADEMA yanapodhihiri.
Taarifa za chini chini zinasema kuwa Dr Slaa amekataa wito huo wa CHADEMA 

Diamond Kuonyesha Uwezo Wake Mbele ya Kiba..Kuachia Video Nyingine Wiki Hii Kuifunika Lupela

0
0
Haya sasa Chibu dangote! Diamond katika ukurasa wake wa twitter amesema kuwa wiki hii anaachia video mpya ya kwake na kutaka watu kukaa mkao wa kula

Sijajua Diamond ana Maana Gani akati kiba kaachia video nae mda mfupi tuu

Ngoja tusubiri

Update: Waziri Mwigulu Nchemba Amefika Eneo la Mapigano ya Wakulima na Wafugaji na Kuamuru Mambo Haya

0
0
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mwigulu Nchemba ametembelea Kijiji cha Kigurukwa mjini Morogoro kulikotokea mapigano ya Wakulima na Wafugaji yaliyosababisha kuuawa kwa mbuzi takribani 200.

Waziri Mwigulu ameagiza Kamati ya Ulinzi ya Mkoa kuhakikisha wote waliohusika katika tukio hilo wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Pia ameagiza kutekelezwa haraka hukumu ya mahakama iliyotolewa mwaka 2005 iliyoagiza kuwekwa kwa mipaka kati ya eneo la wafugaji na wakulima

"Wema Sepetu Una Mimba Kweli au Unatafuta Kiki"- Nay wa Mitego

0
0
Nay Ameachia Wimbo Mpya na kusema kuwa aliyoyazungumza humo ni mambo ambayo yapo na huenda tunayajua au tumesha yasikia mitaani.
Katika moja ya mistari yake amemzungumzia Rais John Pombe Magufuli na kusema kuwa kama watu watamzingua avunje mpaka Ikulu

"Mliopanga kunishtaki mkanishtaki hata kwa Magu na bado nitawapa fact, si wamekuchagua wenyewe Magufuli waonyeshe maujuzi vunja mpaka Ikulu wakikuletea upuuzi, sifanyi bifu mimi na watoto wa juzi" Asema Nay

Miongoni mwa vijembe vinavyopatikana kwenye wimbo huo ni;

Msanii Ray kujifanya Mkongo kwa kununulia mkorogo fedha zinazotokana na mauzo ya movie zake na kuishi kwao hadi sasa, Bongo Movie imekufa kufikia hatua wasanii wa kike wa filamu kutaka kuimba km snura na shilole, Niva kuishi kwa mademu na huku akimiliki gari ya M10 wakati hana getto, wanafunzi wa chuo kuishi maisha ya anasa na kupoteza dhana ya usomi. Wadada wengi wa mjini na kutovaa chup**, biashara?

Hakuishia hapo, alihamia kwa BASATA, kwa kuwashangaa wanavyoshindwa kufanya kazi yao kwa weledi na kuishia kuwafungia wasanii nyimbo bila kujua ugumu wanaopitia..

Pia, akaendelea na wadananda kwa kumtaja Shetta kuwa anaringishia gari ya kifahari aliyohongwa na Chief Kiumbe kwa kujitapa 'My new ride', Ommy Dimpoz kuhusishwa na Ushoga kitaani, DJ Choka kuwa bize na bata bila kujali familia huku hana hata godoro la kulalia.

Katika wimbo huo Nay wa Mitego hajamuacha Wema Sepetu na alikuwa na haya kusema juu yake " Wema Sepetu una mimba kweli kweli au unatafuta kiki za msimu, miezi tisa si mingi isije ikakugharimu, na anamshauri aangalie umri unaenda asiendekeze kiki kwani mwishowe ataitafuta Kiki hadi kwa FID Q. "

Hata hivyo baada ya Nay wa Mitego kuachia wimbo huo amesema maneno haya "Hii sio Vita japo inaweza kua vita. Ni muziki mzuri na mtamu sana wenye maneno flani ya wazi tu ata wewe unayajua.! #ShikaAdabuYako nitaenda likizo kidogo baada ya hii Ngoma kuanza kuchezwa." Aliandika Nay wa Mitego

Nafasi za Kazi Tanzanite One Mining Limited na National Lottery of Tanzania, Apply Here


Bunduki iliyotungua Helkopta na Kuua Mzungu yapatikana Simiyu.

0
0
Bunduki hiyo aina ya Riffle Na 7209460 CAR Na 63229, imepatikana mara baada ya jeshi la polisi kufanikiwa kuwakamata watu 9 wanaotuhumiwa kuhusika na tukio hilo.

Kamanda Lazaro Mambosasa amesema kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na jeshi hilo kushirikiana na wananchi, pamoja na uongozi wa TANAPA.

Aidha waliokamatwa wamekiri kuhusika na tukio hilo, huku akieleza kuwa msako mkubwa ulifanywa na jeshi hilo mara baada ya tukio kutokea chini ya mkuu wa upelelezi mkoa Jonathan Shana.

Mwimbaji Criss Wamarya Amkimbia Baba Yake Baada Ya Kuugua

0
0
Yasemekana kuwa baba wa Criss Wamarya alianza Kuugua tangu mwaka jana, ambapo alifikishwa hospitali ya Mzinga Mjini Morogoro kwa matibabu zaidi.

Inavyo semekana Criss Amemkimbia na kumtelekeza Baba yake mazazi ambae amepata stock ya upande moja wa kulia inavyosemekana mwanzo alikuwepo lakin gafla akunekana akiwa pamoja na familya hiyo kumuuguza mzee yake.

Kwa sasa amepelekwa mtwara kutibiwa uko na familya inamlaum Criss kwa kutomjali mzazi wake na ikiwa yeye ndio mtoto wakiume kati ya dada zake nne.
Ata hivyo Criss wamarya ajaenda ata Mtwara kwenda kumuuguza baba yake na hali hiyo inaleta maswali mengi kwa familia yake.

Ila wengi wao wakipita mitaani wanasikia nyimbo zake kwakuona Criss wamarya ajali jambo linalo msibu baba yake ambaye sasa yupo kitandani na hapo hapo akiwaameachia wimbo mpya unaoitwa Pepea ambao amemshirikisha Madee na kuacha kumuuguza baba yake mzee.

Raia wa Kigeni Waushika Uchumi wa Tanzania......Ni 10% Tu Ya Watanzania Wanaomiliki Uchumi wa Nchi, Serikali Yatangaza Mkakati Kuokoa Jahazi

0
0
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amesema serikali ya awamu ya tano inafanya kila juhudi kuhakikisha uchumi wake unamilikiwa na wananchi, nia ikiwa ni kuifanya nchi kuwa na uchumi wa kati.

Majaliwa aliyasema hayo jana, wakati akizindua mpango wa uwezeshaji wananchi kiuchumi, ambao pamoja na mambo mengine utatoka na mapendekezo ya nini cha kufanya kufikia malengo yake.

Kwa mujibu wa waziri mkuu, ili kufikia malengo ya mkakati huo, wadau wote hawana budi kuunganisha nguvu pamoja kuanzia ngazi ya juu hadi chini.

“Taarifa zilizopo zinaonyesha ni asilimia 10 tu ya Watanzania ndio wanaomiliki uchumi wa nchi na sera hiyo ndiyo inatoa mwongozo wa jumla unaohakikisha kwamba wananchi wanapata fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo zitawawezesha kujenga na kufaidika na uchumi wa mchi yao,” alisema.

Aidha alizitaja mojawapo ya nyenzo muhimu katika kufanikisha suala hilo ni pamoja na uhakika wa masoko, riba nafuu kwa wajasiriamali, pamoja na ushirikishwaji wa viongozi wote.

“Napenda mkimaliza mkutano wenu mnipatie mapendekezo ya kile mlichokubaliana hapa, kwani nimekuwa na utaratibu kila nikifanya ziara zangu mikoani lazima nizungumze na wananchi na huwa nawaeleza haya masuala ya mipango ya serikali katika kuwawezesha,” alisema waziri mkuu.

Awali akimkaribisha waziri mkuu, Waziri wa Nchi Ofi si ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Uwezeshaji, Ulemavu Vijana na Wazee, Jenister Mhagama, alisema kuwa kuwawezesha wananchi ni hatua muhimu katika maendeleo ya taifa.

Katika kufanikisha azma hiyo, Waziri Jenister alisema tayari serikali imefanikiwa kutenga maeneo maalumu ya uwekezaji, ambapo vijana na wananchi kwa ujumla watapewa kipaumbele zaidi.

“Mikoa 20 tayari imeshatenga maeneo na sasa wanaweka miundombinu ambayo nia yake ni kuwasaidia wananchi kuweza kumiliki uchumi wao,” alisema.

Hatahivyo mojawapo ya changamoto inayokabili utekelezaji wa sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ni ukosefu wa ajira na umasikini, ambavyo vinalikabili kundi hili muhimu.

Imeelezwa kuwa maeneo ambayo yanatajwa kama sehemu muhimu zenye kuwezesha kupatikana kwa matokeo ya haraka ni sekta ya utalii, ujenzi, usafirishaji, kilimo, madini, misitu na viwanda.

Baada ya Kukamatwa na Kitengo cha Madawa ya Kulevya, Kigogo Dar Kortini

0
0
Yule mfanyabiashara mkubwa jijini Dar es Salaam mwenye hadhi ya kigogo, Daudi Yakubu Adam ‘Daudi Kanyau’ (46) ambaye jana gazeti dada na hili, Uwazi liliandika habari yake akilidai gazeti hilo Sh. Milioni 500 kwa madai lilimchafua, ameburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar Jumatano iliyopita akituhumiwa kwa mambo mawili.

kanyau (2)
MASHITAKA YAKE YAKO HIVI
Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Thomas Simba, Kanyau ambaye ni mkazi wa Salasala, Dar alisomewa mashitaka ya kujipatia mali zinazodhaniwa kuibwa au kupatikana kwa njia isiyo halali.
Kanyau aliambiwa mahakamani hapo kuwa, makosa hayo yapo kinyume cha sheria namba 16, kifungu cha 312 (1) (b) ya mwaka 2002.

“Kesi hii namba 17/ 2016 naiahirisha hadi Februari 17, mwaka huu na mtuhimwa utaendelea kuwa nje kwa dhamana, “ alisema Hakimu Simba.

kanyau (3)
AWAPIGA MKWARA WAANDISHI
Wakati anatoka mahakamani, mtuhumiwa huyo alikuwa akiwazuia waandishi wa gazeti hili kumfotoa. Hata hivyo, juhudi zake hazikuzaa matunda.


KABLA YA KIZIMBANI
Kanyau alipandishwa kizimbani baada ya kushikiliwa kwa siku 7 na Polisi wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Makao Makuu, Kurasini jijini Dar es Salaam na habari za kukamatwa kwake kuandikwa na gazeti dada na hili, Uwazi la Januari 19, mwaka huu.

kanyau (1)Gazeti la Uwazi liliripoti kukamatwa kwake.
KANYAU ACHARUKA
Mara baada ya habari hiyo kuandikwa gazetini, Kanyau kupitia kwa mawakili wa Kampuni ya Brocard Attorneys ya jijini Dar, wiki iliyopita, waliliandikia barua Gazeti la Uwazi akilidai fidia ya Shilingi 500,000,000 kwa madai kuwa, habari ile ilikuwa ni ya uongo kwani mteja wao hajawahi kutuhumiwa, kukamatwa na polisi wala kufikishwa mahakamani.


KAMANDA WA KIKOSI CHA KUZUIA MADAWA YA KULEVYA
Baada ya Uwazi kupata barua hiyo kutoka kwa watu ambao Kanyau anawaamini ni wanasheria, Februari 2, mwaka huu, waandishi wetu walikwenda Makao Makuu ya Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania na kuonana na mkuu wa kitengo hicho, DCP Robert Boaz (mrithi wa Geofrey Nzowa) ambaye alithibitisha kikosi chake kumkamata Kanyau.

“Siyo tu kwamba tumemkamata, tayari tumeshamfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.”
Akanyanyua simu yake ya mkononi, akaongea na upande wa pili kuulizia kuhusu kesi hiyo kisha akakakata na kuendelea kusema:

“Haya! Kumbe kesi yake itatajwa tena kesho Jumatano (Februari 3, mwaka huu).”
Kamanda Boaz alisema kikosi chake kinapomkamata mtu na kumhoji, humpeleleza mambo mengi na wakipata uthibitisho humpeleka mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake.


WAZIRI KITWANGA AKAZIA MADAI
Katika kudhihirisha kuwa, kweli Kanyau alishikiliwa na ‘polisi wa kuzuia unga’, hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumzia hali ya madawa ya kulevya nchini, aliliambia Gazeti la Raia Mwema jinsi kikosi cha kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya kilivyomkamata Daudi Kanyau kwa madai ya ‘unga’.


NUKUU YA WAZIRI KITWANGA KUHUSU ‘UNGA’
“Nimeagiza wakuu wa upelelezi kote nchini waunde timu za kupambana na madawa ya kulevya maana tumekamata mengi sana na hiyo si nguvu ya soda, labda mimi nifukuzwe hapa (uwaziri).

“Nimeagiza watendaji wa polisi na uhamiaji na idara nyingine wanipatie taarifa Ijumaa ya kila wiki. Ninafahamu mtandao wote, ndiyo maana nilisema sihitaji orodha bali nahitaji kufanya kazi ili watu wanaofanya hizi biashara wafikishwe mahakamani.
“Mfano ni namna kikosi changu (dhidi ya madawa ya kulevya) kilivyomtia nguvuni Daud Kanyau, anayedaiwa kujihusisha na biashara hizo.“Wewe mtu kama Kanyau alikuwa anakamatika? Ninachohitaji ni ulinzi. Kuwa ‘protected’. Mungu akihitaji ufe leo utakufa saa hiyohiyo lakini akihitaji kukutumia kwa ajili ya watu wake atakutumia, hata kwenye vitabu vitakatifu imeandikwa,” mwisho wa nukuu ya Waziri Kitwanga na gazeti hilo la Februari 3, mwaka huu.

MASWALI KWA KANYAU
Kama kweli Kanyau hakukamatwa kama mawikili wake walivyosema, Waziri Kitwanga alikuwa akimzungumzia Kanyau gani?!Kama kweli hajatuhumiwa chochote, kule mahabusu ya Polisi Ufundi iliyopo Kilwa Road kwenye kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya, alikaa kwa siku saba kwa sababu gani?!


KUTOKA MEZANI KWA MHARIRI
Tunapenda kuwaambia wasomaji wetu kwamba, habari ambazo zimekuwa zikiandikwa na Magazeti Pendwa ya Global Publishers (Risasi Jumatano, Amani, Ijumaa, Risasi Jumamosi, Ijumaa Wikienda, Uwazi pamoja na ya michezo, Championi), ni za uhakika na ukweli mtupu zikiwa zimefanyiwa uchunguzi wa kutosha.


Source:Global Publishers

Usharobaro Wamtokea Puani Stan Bakora

0
0
Usharobaro umemtokea puani komediani wa Bongo, Stanley Yusuph ‘Stan Bakora’ baada ya kudondoka na kuumia mguu wa kulia wakati akifanya mazoezi ya kutumia Cyboard (Saibodi).

Ishu nzima ilitokea wiki iliyopita katika moja ya duka la nguo lililopo Kinondoni, Dar baada ya kupiga mwereka wa kufa mtu na kujikuta akianguka kama mkungu wa ndizi kutoka juu ya mgomba kisha kuumia mguu.

“Hicho kidude, kwangu ni kigeni ndiyo nilikuwa nakijaribisha nione inakuwaje ndipo nilipoanguka kama mara mbili hivi na kuumia mguu wa kulia, kiukweli kimenitoa ushamba,” alisema Stan Bakola.

Chanzo:GPL

Mramba Afunguka Kuhusu Maisha Ya Gerezani.....Aishauri Serikali Kuwatumia Wafungwa Wenye Utaalumu Badala Ya Kuwarundika Gerezani

0
0
Aliyekuwa  Waziri wa Fedha katika Serikali ya awamu ya tatu, Basil Mramba, ameishauri Serikali kuhakikisha inawatumia wafungwa kutumikia jamii badala ya kuwarundika magerezani.

Amesema pamoja na hayo, maisha ya gerezani si salama na si njia pekee ya kumrekebisha mhalifu aliyehukumiwa na mahakama.

Kutokana na hali hiyo, alisema kuna haja kwa Serikali kuanza kutumia sheria namba 6 ya huduma kwa jamii kuwaangalia wafungwa wenye taaluma kutumika adhabu zao katika fani au taasisi za umma ili kupunguza gharama kuwahudumia watu ambao wanaweza kuisaidia jamii.

Mramba alitoa kauli hiyo jana, wakati yeye na mwenzake aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona, walipomaliza kufanya usafi katika Hospitali ya Sinza Palestina, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kutumikia adhabu ya kifungo chao cha nje baada ya wiki iliyopita Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuridhia kuwa wanastahili kutumikia jamii kwa kipindi cha miezi sita hadi Novemba 5.

Alisema imekuwa ni kawaida jamii kuwa na mtazamo kwamba mtu yeyote anayekutwa na hatia lazima atapelekwa jela ajirekebishe na kuacha tabia aliyonayo jambo ambalo si sahihi.

“Jamii inaamini jela ni sehemu salama na mtu akishikwa na hatia kwa kosa lolote, mahala sahihi ni jela tu, kule anakutana na watu wa kila aina, wenye makosa tofauti, hali ambayo inamfanya ajifunze mambo mengine mapya.

“Unakuta mtu amefanya uhalifu wa kuiba kitu, anafungwa na kupelekwa gerezani, anakutana na majambazi sugu wanaompa mbinu zaidi, sasa akitoka jela anakuja akiwa ameiva, anarudia kwenye matukio akiwa amekamilika,” alisema Mramba.

Alisema kuwapeleka wafungwa katika huduma za kijamii kutasaidia kupunguza gharama kwa Serikali na msongamano ndani ya magereza.

Akizungumzia suala la kuwatumia wafungwa ambao ni wanataaluma, Mramba alisema sheria hiyo ikitumika vizuri italisaidia taifa kwani wapo baadhi ya wafungwa wana taaluma ya udaktari, ualimu, ufundi na uhasibu, ambao wanaweza kutumika katika fani zao kwenye taasisi za umma.

“Kuna maeneo mengine yana uhaba wa wataalamu ambao wengine wapo magerezani wanahudumiwa na Serikali kuanzia chakula, malazi na hata afya zao, hivyo wakiwatumia hao itakuwa faida kwa taifa kwa kuwa watafanya kazi bila malipo,” alisema Mramba.

Alisema suala la kuwatumia wafungwa katika huduma za kijamii si geni kwa nchi zilizoendelea ambako kwa kiasi kikubwa wamesaidia kuinua uchumi wa nchi zao.

Kwa siku ya jana, Mramba na Yona walianza kufanya usafi saa 2 asubuhi kwa kufagia nyuma ya jengo la wazazi katika hospitali hiyo.

Naye Ofisa Huduma za Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Deogratius Shirima, alisema gharama zinazotumika kuwahudumia wafungwa magerezani ni kubwa, hivyo ni vyema wale wanaoguswa na sheria ya huduma za jamii namba 6 ya mwaka 2002 kutumikia kifungo cha nje.

“Sheria hii ni vyema ikatumika kwa wale inaowagusa kwani itapunguza gharama za kuwahudumia magerezani, na pia adhabu wanayopata wafungwa wa nje ni wazi jamii ambayo ndiyo iliyokosewa inaona utekelezaji wake kwa uwazi,” alisema Shirima.

Alisema mataifa mengine ikiwamo nchi ya Kenya wanatumia sheria hiyo ambapo nusu ya wafungwa nchini humo wapo katika huduma za jamii.

Februari 6, mwaka huu mawaziri hao walibadilishiwa adhabu ya jela na kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha nje mwishoni mwa wiki iliyopita na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kukamilika kwa mchakato wa kufikia hatua hiyo.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkeha, alisema sheria ya huduma kwa jamii namba 6 kifungu namba 3(1) ya mwaka 2002 inasema mtu yeyote anayetiwa hatiani kwa kosa ambalo adhabu yake ni miaka mitatu kushuka chini mahakama inaweza kumpa adhabu ya kutumikia jamii.

Mramba na Yona, ambao baada ya rufaa walibakiwa na adhabu ya miaka miwili, walitiwa hatiani kwa kutumia madaraka vibaya ambapo walitakiwa kumaliza kifungo Novemba mwaka huu.

Hata hivyo, hakimu huyo alisema magereza walifikisha barua mahakamani hapo Desemba 5, mwaka jana yenye kumbukumbu namba 151/DAR/3/11/223, wakipendekeza kifungo cha nje kwa mawaziri hao.

Hakimu Mkeha alisema baada ya kupokea barua hiyo, mahakama iliamuru watu wa huduma za jamii kuchunguza kama wanastahili kupewa adhabu hiyo na kwamba walifanya hivyo na kurudisha ripoti kwamba wanastahili.

Alivitaja vigezo vya kupewa adhabu hiyo kuwa ni umri ambapo Mramba na Yona wana miaka 75.

Kamari yamtoa Roho Mtanzania uko Nairobi, Kenya

0
0
Kijana mwenye umri wa miaka 28 mwenyeji wa wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro ameuawa katika jiji la Nairobi Kenya baada ya kuwaua watu wawili kwenye Casino.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kijana huyo alikuwa amepoteza dola 300 za kimarekani baada ya kucheza kamari.

Baada ya hapo alijaribu kumsihi mwenye Casino arudishe pesa yake kwa kuweka simu yake rehani ndipo akaambiwa simu haikuwa na uwezo wa fedha hiyo ndipo akamchoma kisu mmiliki huyo na mlinzi wake katika mtaa wa Eastleigh.

Aidha baada ya kufanya tukio hilo umati wa watu ulimshambulia kwa kipigo na kusababisha kifo chake.

Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo kijana huyo alikuwa dereva bodaboda na inasemekana aliuza pikipiki yake na kucheza kamari katika Casino hiyo.
Chanzo BBC

Shilole 'Ukinitaka Mimi Bila Milioni 20 Hunipati'

0
0
Amepanda dau? Msanii wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kuwa bila mtu kuwa na kiasi cha Sh. Milioni 20 mkononi, hawezi kucheza filamu yake kwa kuwa kwa sasa anaona kama ni kumpotezea muda.

Akipiga na Ijumaa Wikienda, Shilole au Shishi Baby alifunguka kuwa soko la filamu Bongo, linashuka na pia wasanii wanatumia muda mwingi lakini wanapata malipo kidogo tofauti na nguvu pamoja na muda waliotumia.

“Kama mtu akinitaka kwa sasa ili nicheze filamu yake awe na milioni 20 ndiyo nifanye maana ni kitu ambacho kinachukua muda sana halafu malipo yake ni kidogo,” alisema Shilole.

Chanzo:GPL

Ommy Dimpoz Amuonyesha Mpenzi wake Hadharani na Kumchana Nay wa Mitego Baada ya Nay Kumuhusisha na Ushoga Kwenye Nyimbo yake

0
0
Barua kutoka kwa @ommydimpoz kwenda kwa Nay wa mitego baada ya Nay wa Mitego kumuhusisha na Ushoga katika nyimbo yake mpya...

"Barua ya wazi kwa Neema wa Mitego kwanza pole kwa Malezi ya Watoto ambao mama zao wamekukimbia, hakuna Mwanamke ambae anaweza kuishi na mwanaume mwenye tabia za kike kama zako  inatakiwa ujiulize una tatizo gani maana km umaarufu mavi unao,nyumba unayo,magari unayo na hivyo ndo vitu dada zetu wanapenda lakini kwanini wanakukimbia pili kila nikiwaangalia watoto naona kabisa hamjafanana kuna umuhimu wa DNA Da Neema trust me. Hiyo video nimekuwekea hapo juu ni kukuonyesha kuwa mimi na wewe Ligi zetu hazifanani  vitu navyokula mimi wewe utaishia kuviona kwenye TV maana kuvipata mpaka uwe Unapanda sana Ndege sasa mimi najaza passport ya Tatu wakati wewe hata kurasa 4 za passport yako ya kwanza hujamaliza  Sasa wewe ushazoea wanawake zako wa jumuiya basi unataka kila mtu apost demu wake haya sasa Chuma hiko kimetoka ulaya kuja kufuata dodoki nimekujibu ili nikusaidie promo ya nyimbo yako Atleast upige na Vishoo baba  Sema nakuomba usirushe ngumi tu maana nakujua Mzee wa Kupanic Maana katika hao mabebi mama wako kuna mmoja nilishapitaga nae Uliza vizuri atakwambia kama jogoo anawika au vipi Ukitaka kudownload wimbo wa @naytrueboy #ShikaAdabuYako nenda kwenye bio ya Da Neema"Ommy Dimpoz

Profesa Muhongo: Sijawahi Kupokea Rushwa wala 10% Ya Mwekezaji

0
0
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amesema hajawahi kupokea rushwa kwa mtu yeyote wala asilimia 10 ya wawekezaji wa miradi mbalimbali ya umeme nchini.

Aidha, ametaka kuachwa kuingizwa kwa masuala ya siasa kwenye umeme, kwani umeme ni suala linalohitaji utaalamu zaidi na si maneno.

Alitoa kauli hizo juzi wakati akizungumza na wazalishaji wa umeme kwenye mkutano uliofanyika Mtera.

“Mimi hakuna mtu yeyote dunia nzima aliyewahi kunipa rushwa, nia yangu ni kuhakikisha taifa linapata umeme ikiwa ni pamoja na kuongeza wawekezaji, sihitaji hela ya mtu,” alisema Profesa Muhongo.

Pia alisema baadhi ya mitandao ya kijamii, imekuwa ikiripoti kuwa amewaita wazalishaji hao ili wamlipe asilimia 10 ; na kusema jambo hilo si la kweli hata kidogo.

“Kwenye masuala mengine ya mtandao ambayo hayana ukweli wowote muwe mnajitetea,” alisema Profesa Muhongo. “Acheni kuingiza masuala ya siasa kwenye umeme,” alionya.

Diamond Platnumz Afunguka Kuhusu Wimbo wake Mpya Anaeutoa Ijumaa Hii...Soma Hapa Alichosema

0
0

AFRICA!!!! i know you been waiting for this...and it's ready for You!... TANZANIA + SOUTH AFRICA = HIT..this Friday!

( kwanza kabisa ningependa kumshkuru Mwenyez Mungu kwa kuweza katusaidia kufanikisha ndoto zetu za Bongo falvour kuweza kuingia na kupata nafasi nzuri West africa... kama nilivyoahidi na kuzungumza mwanzo kuwa mwaka huu Moja ya Mission zangu ni kuhakikisha pia Muziki wetu unapata nafasi nzuri South Africa na America... tafadhali usiache kunisupport ili kwa pamoja tuufikishe mziki wetu Kileleni...) #MakeMeSing @akaworldwide X @DiamondPlatnumz Drops on Friday!

Picha ya Mwigulu Nchemba na Mwanae yazua Mjadala Mitandaoni

0
0
Picha ya Waziri wa Kilimo na Mifugo na Mbunge wa Iramba Mashariki imezua "hisia" tofauti na mijadala mitandaoni.Picha hiyo inamuonyesha Mh.Mwigulu akiwa na mwanae wa kiume,na "Caption" ya picha inayosomeka elimuniufunguo. Kikubwa kilichozua mjadala ni nembo katika fulana ya mtoto yenye maandishi ya FEZA SCHOOL.

Maswali na mijadala ya wengi ni kuwa,itakuwaje na moyo wa kuimarisha elimu ktk shule za umma kama sehemu ya mawaziri ambao ni watekelezaji wa sera ya Elimubure na Uboreshwaji wa elimu katika shule za umma wanakimbiza watoto wao katika shule binafsi? Kwanini Mawaziri ambao ni sehemu ya utekelezaji wa sera wanaoamini katika elimu bora katika shule za umma wao hawawapeleki watoto wao huko?

Picha hii imezua mijadala tofautitofauti na wapo wanoona Mh.Mwigulu yupo sahihi kupeleka watoto shule binafsi sababu ukweli ni kuwa shule za serikali elimu yao ni duni na isiyo na ushindani.

Hivyo mawaziri kuwapeleka watoto shule binafsi na zenye ubora kama FEZA SCHOOL ni kuwaepusha na elimu duni inayotolewa na serikali
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images