Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104781 articles
Browse latest View live

TAKUKURU Yawafikisha Mahakamani Vigogo 11 wa Kampuni ya Reli (TRL)

$
0
0
Hatimaye vigogo 11 wa Kampuni ya Reli (TRL) waliosimamishwa kazi hapo awali wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakishtakiwa na makosa tisa yakiwemo matumizi mabaya ya madaraka yaliyopelekea manunuzi ya mabehewa mabovu 25 kinyume na utaratibu.

Washtakiwa hao ni pamoja na  Kipallo Aman Kisamfu  (Mtendaji Mkuu), Jasper Hurbert Kisiraga (Mkurugenzi Mkuu wa Ndani), Ngoso Joseph Ngosomwiles (Mhandisi Mkuu wa Mitambo), na Mathias Andrew Massae.

Wengine ni pamoja na Muungano Kaupunda, Paschal Mafikiri, Kedmon Mapunda, Felix Kashaigili, Lowland Simtengu, Joseph Syaizyagi, na Charles Ndege.

Akiwasomea mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Emillius Mchauru, Mwendesha mashtaka wa TAKUKURU, Maxilmillian Ari amesema washtakiwa walitenda makosa hayoa kati Januari 1, 2013 na Mei 31, 2014.

Maximillian alisema mshtakiwa wa kwanza Kipallo Kisamfu akiwa kama Mtendaji Mkuu alitumia vibaya madaraka yake kwa makusudi kwa kushindwa kuhakikisha mkataba wa tenda no. PA/113/2012-13/ME/G/OE/013 unatekelezwa kwa mujibu vigezo na masharti ya utoaji tenda na kukiuka kifungu cha 33(k) na 44(1) na (3) cha Sheria ya Manunuzi na kusababisha Kampuni ya M/S Hindustan Engineering and Industries Ltd kujinufaisha kutokana na mkataba huo.

Ilidawa pia kuwa mshtakiwa namba 6, Paschal Mafikiri akiwa kama Injinia Mkuu alitumia vibaya nafasi yake kwa kupitisha michoro na dizaini za mabehewa aina ya Ballast Hopper Bogie Wagons (BHB) iliyoandaliwa na Kampuni ya M/S Hindustan Ltd ambazo zilikuwa kinyume na vigezo na masharti ya mkataba katika tenda tajwa.

Mwendesha mashtaka wa TAKUKURU aliiambia mahakama kuwa washtakiwa wa pili na wa tatu (Jasper Kisanga na Mathias Massae), wakiwa kama Mhasibu Mkuu na Mhandisi Mkuu wa TRL, walitumia vibaya nafasi zao kwa makusudi kwa kuidhinisha malipo ya kiasi cha Dola za Marekani 1,280,593.75 kwenda Kampuni ya M/S Hindustan Ltd bila ya kuthibitisha ufanisi wa mabehewa 25 aina ya Ballast Hopper Bogie Wagons ndani ya muda wa uangalizi (warranty period), kinyume na Sheria ya Manunuzi.

Vilevile mshtakiwa wa 4, Muungano Kaupunda, akiwa kama Fundi Mkuu wa TRL alitumia vibaya nafasi yake kwa kuruhusu Kampuni ya M/S Hindustan Ltd kuanza utengenezaji wa mabehewa hayo 25 bila ya kujiridhisha kama vigezo na masharti vya utolewaji wa tenda hiyo vilifatwa kama inavyoainishwa na Sheria.

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka, washtakiwa wa 4,7,8,9 na 10 kama wajumbe wa kamati ya uthibitisho na huku wakijua wanatenda kosa walitumia vibaya nafasi zao kwa kushauri na kupendekeza Kampuni ya M/S Hindustan Ltd kushinda tenda tajwa kinyume na Sheria ya Manunuzi.

Washtakiwa wote walikana mashtaka yao na mshtakiwa 3, 4, na 11 walifanikiwa kupata dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wa kuaminika watatu watakaosaini dhamana ya Shilingi Milioni Kumi kila mmoja ikiwa ni pamoja na kuwasilisha hati zao za kusafiria mahakamani.

Washtakiwa wengine 8 walirudishwa rumande kwa kushindwa masharti ya dhamana huku wengine wakiwa hawana wadhamini kabisa hadi hapo kesi yao itakapotajwa tena Februari 25, mwaka huu.

Machi 21, 2013, TRL iliingia mkataba wa kununua mabehewa hayo aina ya Ballista Hopper Bogie (BHB) kutoka Kampuni ya M/S Hingustan Engineering and Industrial Limited ya nchini India kwa ajili ya kutumika katika uimarishaji wa njia za Reli ya Kati na yaliwasili Julai, 2014.

Hata hivyo, baada ya kuanza kazi yalilalamikiwa kuwa hayakuwa na ubora unaotakiwa na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe aliunda kamati kwa ajili ya kuchunguza tuhuma hizo na kamati hiyo ilikabidhi ripoti yake Desemba 1, 2014 na Waziri huyo kuahidi kuishughulikia bodi ya zabuni ya TRL.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya Februari 13, Ikiwemo ya TB Joshua Kuhamia Zanzibar

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya Februari 13

Utafiti: Umaarufu Wa Lowassa Waporomoka, Magufuli Apaa

$
0
0
Matokeo ya utafiti mpya uliofanywa mapema mwezi huu yanaonyesha kuwa umaarufu wa Rais John Magufuli umeongezeka kufikia asilimia 74.5, akimuacha mbali mpinzani wake wa karibu kwenye Uchaguzi Mkuu, Edward Lowassa.

Magufuli alishinda mbio za urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, akipata asilimia chache kuliko wagombea wengine kutoka CCM, lakini amejiongezea umaarufu kutokana na hatua ambazo amekuwa akichukua tangu alipoapishwa Novemba 5, 2015.

Katika uchaguzi huo, Dk Magufuli alipata kura milioni 8.8 sawa na asilimia 58.47, akifuatiwa na Lowassa aliyepata kura milioni 6.07, sawa na asilimia 39.97.

Lakini utafiti huo uliofanywa na taasisi ya Ms Infotrak Researc and Consultant na Ms Midas Touche East Africa kwa kuwahoji watu 1,200 wenye umri wa zaidi ya miaka 18 katika kanda sita na mikoa 15, unaonyesha kuwa Magufuli ameongeza umaarufu kwa takriban asilimia 20, huku Lowassa akishuka kwa asilimia 20 pia.

Katika utafiti huo, Lowassa anaonekana kushuka hadi asilimia 20.1.

Wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni Anna Mghwira aliyepata asilimia 1.1, Hashimu Rungwe (0.4), Fahmi Dovutwa (0.2), Lutalosa Yemba (0.1), Janken Kasambala (0.1) na Machmillan Lyimo aliyepata asilimia 0.0. Asilimia 3.5 ya walioulizwa swali hilo walikataa kujibu.

Vilevile, wananchi walipouliza iwapo Uchaguzi Mkuu ukifanyika leo wangemchagua nani kati ya makada waliojitokea kugombea urais mwaka jana, wengi wamemtaja Magufuli.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba wanawake wengi ndiyo wanamuunga mkono Magufuli ikilinganishwa na wanaume.

Asilimia 77.9 ya wanawake wanasema wapo tayari kumchagua tena kuwa Rais iwapo kutakuwa na uchaguzi mpya, wakati wanaume wanaosema hivyo ni asilimia 71.5 pekee.

Kinyume na ilivyo kwa Magufuli, utafiti umebaini kwamba Lowassa anapendwa zaidi na wanaume huku asilimia 22.6 wakisema wapo tayari kumchagua kuwa rais. Ni asilimia 17.4 ndiyo wametoa maoni kama hayo kwa Magufuli.

Kwa upande wa kanda; Kanda ya Zanzibar ndiyo inayoongoza kwa ‘kumkubali’ Magufuli ikiwa na asilimia 91.6, ikifuatiwa na Kanda ya Kati yenye asilimia 81.6, Kanda ya Kaskazini (77%), Kanda ya Pwani (72.7) na Kanda ya Ziwa asilimia 67.6.

Alipoulizwa kuhusu matokeo ya utafiti huo, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa George Shumbuso alisema kuongezeka kwa umaarufu wa Rais Magufuli kunatokana na utendaji wake kugusa kero za wanyonge.

Alisema Watanzania wengi hata wale waliokuwa wakiunga mkono vyama vya upinzani, wameanza kukubaliana na Magufuli kutokana na namna alivyoweza kufanya mambo makubwa na yenye umuhimu kwa Taifa ndani ya muda mfupi.

“Hakuna Rais aliyefanya mambo makubwa namna hii ndani ya siku 100 ndiyo maana wanyonge wameonekana kumkubali kwa sababu amegusa na kuonyesha wazi nia ya kumaliza changamoto zao,” alisema.

“Hata ikitokea uchaguzi ukafanyika sasa nina uhakika Magufuli atashinda kwa sababu wananchi wamebaini wazi kuwa anachokizungumza ndicho anachomaanisha. Si siasa kama ambavyo imezoeleka kwa wanasiasa wengine.”

Kauli hiyo iliungwa mkono na mwenyekiti wa Tanzania Labour Party na mbunge wa zamani wa Vunjo, Augustine Mrema aliyesema kuwa Watanzania walifanya uchaguzi sahihi kumuweka Magufuli madarakani.

Alisema katika kipindi cha siku 100 kiongozi huyo amefanya miujiza ambayo hakuna Mtanzania ambaye alifikiria kuwa ingeweza kufanyika.

Huyu Hapa Ndio Mwanamke Kutoka Tarime Aliyemkaba Jambazi Na Kumpora Bunduki Aina Ya SMG

$
0
0
Mwanamke aliyepambana na jambazi na kufanikiwa kumnyang’anya bunduki aina ya SMG, Sophia Manguye (46), amepewa zawadi ya Sh 500,000 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Tarime/Rorya, Gemini Mushy.

Mwanamke huyo ambaye aliomba Serikali kumpa silaha ili kujilinda, alisema kuwa hajaridhika na zawadi hiyo kwa kuwa kama asingemmudu jambazi huyo watu wengi wangepoteza maisha.

Hata hivyo, Mushy alimwomba Manguye kupokea kiasi hicho japokuwa ni kidogo kwa kuwa ni zawadi kutoka ofisi yake.

Tukio hilo lilitokea Februari 9, saa 2.42 usiku, baada ya watu watatu kufika dukani kwake, mmoja wao akiwa na bunduki kisha kumwamuru atoe fedha alizokuwa nazo.

Manguye alisema alichukua Sh80,000 alizokuwa nazo na kumkabidhi jambazi huyo, lakini hakuridhika na kumlazimisha aongeze kiasi kingine.

“Nilipandwa hasira nikanyanyuka wakati jambazi anainama kuangalia kwenye kiboksi cha fedha, nikamkamata kifuani na kung’ang’ania mkanda wa bunduki, akaanza kunivuta kwenda nje, nami nikamvutia ndani, lakini alifanikiwa kunitoa nje akaniangusha chini, lakini sikuachia mkanda wa bunduki,” alisema Manguye na kuongeza:

“Aliposikia wananchi wameanza kupiga yowe akaniachia na kutoa mkanda wa silaha begani, akakimbia na kuniachia bunduki. Wakati huo huo jambazi mwingine alikuwa amekamatwa kwenye duka la Zaituni Magasi, wananchi walipofika wakaanza kumshambulia, wakati huo taarifa ilikuwa tayari imetolewa Kituo cha Polisi Sirari, wakafika kumchukua,” alisema.

Hii ni mara ya pili kwa Manguya kuvamiwa na majambazi wenye silaha, ambapo mwaka 2014 alivamiwa dukani kwake na majambazi waliokuwa na bunduki, lakini alifanikiwa kumpiga kwa kigoda aliyekuwa na bunduki na alianguka chini.

Magasi alisema wakati wa tukio hilo, alikuwa amevamiwa na majambazi waliokuwa na bunduki, mapanga na nondo.

“Wakati anatoka mvunguni mdogo wangu alimkamata kwa nyuma na kummudu huku akipiga kelele, watu wakafika wakaanza kumpiga hadi akazimia, polisi walipofika wakamwokoa kwani kidogo wamuue,” alisema.

ZEC Yagoma Kuondoa Picha ya Maalim Seif Kwenye Karatasi za Kura........CUF Yasema Ipo Tayari Kwa Mazungumzo ila Sio Kurudia Uchaguzi

$
0
0
Zikiwa  zimebaki siku chache kabla ya kurudiwa kwa uchaguzi Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharrif Hamad amehoji sababu za chama tawala, CCM kuhofia CUF kuongoza visiwa hivyo.

Maalim Seif, ambaye aligombea urais wa Zanzibar katika uchaguzi wa Oktoba 25 ambao matokeo yake yalifutwa, pia amesema endapo CCM itasitisha uchaguzi huo uliopangwa kufanyika siku 36 zijazo, CUF watakuwa tayari kufanya mazungumzo lakini si kwa wakati huu ambao maandalizi ya kupiga kura yanaendelea.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, katibu huyo mkuu wa CUF aliitoa hofu CCM kuwa chama chake hakina ajenda ya kulipiza kisasi.

Matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani yalifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salum Jecha siku ambayo chombo hicho kilitakiwa kumtangaza mshindi, na mwezi uliopita alitangaza Machi 20 kuwa siku ya uchaguzi wa marudio visiwani humo.

Wakati CUF ikipinga vikali kufutwa matokeo na kutangaza tarehe mpya, Serikali imesema kuna nafasi ya kufanya mazungumzo kabla ya uchaguzi wa marudio kwa kuwa kuna muda  mrefu wa kufanya hivyo.

Jecha alitangaza uamuzi huo wakati tayari matokeo ya urais ya majimbo 31 yalishatangazwa, na ya majimbo tisa yaliyosalia yalishahakikiwa, huku washindi wa viti vya uwakilishi na udiwani wakiwa wametangazwa na kupewa vyeti vya ushindi.

Sijui kwa nini CCM wanaogopa sisi tukiongoza?” alihoji Maalim Seif kwenye mkutano huo na waandishi akiwa pamoja na aliyekuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa.

Wana wasiwasi gani, kwamba CUF ikiongoza kutatokea nini? Sisi hatuna ajenda ya kulipiza kisasi,” alisema.

Katika mkutano huo, Maalim Seif mbaye pia ni katibu mkuu wa chama hicho alisema kama CCM ina wasiwasi na idadi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), haina budi kuondoa shaka kwa kuwa idadi kwa pande zote inakaribiana.

“Hawa wanahisi hawatapata uwakilishi mkubwa, lakini mbona miaka yote tunakuwa na idadi isiyopishana ya wawakilishi?” alihoji.

Kuna Vitisho  Zanzibar 
Katika mkutano huo, Maalim Seif alisema kumekuwapo vitendo vya wananchi kupigwa na vikundi vya watu wasiojulikana.

Alidai wafanyakazi wa Serikali na taasisi zake wameamrishwa kupeleka vitambulisho vyao vya kazi na vya kura serikalini ili vikahakikiwe.

Hii si mara ya kwanza wafanyakazi wa Serikali kutakiwa kupeleka vitambulisho, sisi tunajua kuwa wanataka wawatishe kuwa watajua nani kapiga kura na nani hajapiga,” alisema na kusisitiza:

Hii ni kama kitisho cha kuwalazimisha wakapige kura, zaidi hasa hizo ni dhuluma ambazo wananchi wanafanyiwa.

Kadhalika Maalim Seif alizungumzia uwapo wa watu wanaovaa soksi usoni na kuwashambulia raia, akisema Serikali haijachukua hatua stahiki kudhibiti hali hiyo.

Alisema watu hao ambao wamepachikwa jina la mazombi, wamevamia maeneo kadhaa kama Baraza la CUF, Jang’ombe na yaleambayo yana wafuasi wa chama hicho kikuu cha upinzani visiwani humo.

Wanawapiga watu, wanawajeruhi na wanaiba mali, lakini inashangaza sana mambo haya na si Serikali wala polisi iliyochukua hatua,” alisema.

Maalim Seif alisema amezungumza na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kuhusu matukio hayo ya uharamia wanaofanyiwa wananchi, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.

Alisema CCM wanatafuta sababu ili machafuko zaidi yatokee visiwani humo wapate kisingizio.

Aliwataka wafuasi wa CUF kuvumilia hali hiyo ili nchi isiingie kwenye machafuko kama yaliyotokea mwaka 2000, wakati watu zaidi ya 20 waliuawa na wengine kukimbilia Shimoni, Mombasa nchini Kenya ambako waliishi kama wakimbizi.

 Lowassa Azungumza
Kwa upande wake, Lowassa aliwataka viongozi wa ngazi za juu wachukue   hatua kumaliza mgogoro wa Zanzibar.

“Hili tulichukulie kwa umakini sana. Viongozi wafanye vikao vya maridhiano, tunaipenda sana amani tuliyonayo,” alisema.

Lowassa alisema anashangazwa na jinsi CCM wanavyoshindwa kuheshimu makubaliano ya SUK na kukataa kukubali matokeo.

ZEC  yagoma  kuondoa  picha  ya  Maalim 
Wakati huohuo, habari zinaarifu kuwa Tume  ya  Uchaguzi  Zanzibar( ZEC)  imegoma  kuondoa  picha  za  wagombea  Urais,Udiwani  na Uwakilishi  kutoka  vyama  vilivyotangaza  kutoshiriki  uchaguzi  wa  marudio,ikiwemo  jina  na  picha  Maalim Seif Sharif Hamad.

Hilo  lilifahamika  jana mjini Unguja  baada  ya  kigogo  mmoja  wa  ZEC ambaye  hakuwa  tayari  kutaja  jina  kusema  kuwa  sheria  hazimruhusu  mgombea  yeyote  kujitoa  mwenyewe  kwa  utashi  wake  binafsi.

Kiongozi  huyo  alisema  kwa  mujibu  wa  kifungu  cha  36  cha  sheria  ya  uchaguzi  namba  11  ya  mwaka  1984,mgombea  hawezi  kujiondoa  kwa  utashi  wake  baada  ya  Tume  kukamilisha  kazi    ya  uteuzi  ambayo  ilifanyika  kabla  ya  Oktoba  25  mwaka  jana.

"Ieleweke  kwamba mgombea  urais  anaweza  kujiondoa  katika  kinyang'anyiro  kwa  kuwasilisha  taarifa  za  maandishi  yeye  mwenyewe  ofisi  za  ZEC  kabla  ya  saa 10  jioni  ya  siku  ya  uteuzi." Alisema  ofisa  huyo  akinukuu  kifungu  cha  katiba.

Alisema  uteuzi  wa  mgombea  mwingine  unaweza  kufanyika  ndani  ya  siku 21  kama  mgombea  hatafariki dunia,lakini  hakuna  ruhusa  ya  kujitoa  kabla  ya  kukamilika  kwa  uchaguzi.

Alisema  ZEC  tayari  imeviandikia  vyama  kuvitaka  vithibitishe  iwapo  wagombea  wao  wangali  hai  au  kuna  waliofariki dunia, na si kutaka  kufahamu  kama  watashiriki  uchaguzi  wa  marudio  au  la.

Mkurugenzi  wa  Mipango  na  Uchaguzi CUF  anena
Mkurugenzi  wa  Mipango  na  Uchaguzi  wa  CUF, Omar Ali Shehe  amesema  ZEC  inasuka  mkakati  wa  siri  wa  kutaka  kuzitumia  picha  na  taarifa  za  wagombea wao  kwa  lengo  la  kuidanganya  dunia  na  jumuiya  za  kimataifa  kwamba  CUF  walishiriki  uchaguzi  huo.

Shehe  amesema  CUF  kilitangaza  mapema  kabisa  kutoshiriki  uchaguzi  wa  marudio,hivyo  dunia  nzima  inaelewa  kabisa  kwamba  CUF  haishiriki  uchaguzi  huo  na  kitendo  cha  kuendelea  kuchapisha  picha  na  taarifa  za  wagombea  wao  katika  karatasi  za  wapiga  kura  si  sahihi.

Niva Amfungukia Nay wa Mitego Baada ya Kuchanwa Kwenye ‘Shika Adabu Yako’

$
0
0
Baada ya msanii Nay wa Mitego Kumchana Niva Kwenye ‘Shika Adabu Yako’ kupitia mtandao wa instagram Niva amefunguka haya;

Alianza kuwa kuandika haya;

“Jioni ya Leo ndio watu watajua. Kama natafuta Kiki kwako au wewe @naytrueboy umeamua kuipata Kiki kwangu coz ney watu wameanza kukujua 2013… mimi watu wameanza kunijua tangia elfu mbili na sita kupitia tamthili ya jumba la dhahabu kipindi hiko wewe upo manzese unatafuta kutoka.. mwenzio nikitajaga tamthili ya jumba la dhahabu uwa nawaumizaga watu wengi Sana coz uwa nawakumbusha kumbukumbu za maisha Yao ya kipindi icho wengine wenzao wamesha wazika walio kua wakiangalia nao. Sasa wewe @naytrueboy unakipi cha kuwakumbusha mashabiki zako.”

Kisha akaweka picha akweka picha hiyo hapo juu akiwa na Nay na kuandika;

“Sasa mkitazama iyo picha mtangundua ni wiki ngapi zimepita na hapo mulizeni alikua wapi na kwanani na alifata nini Tena alikua anajipima mwili wake na wangu… niliwai kusema kuwa ni mdogo wangu kwaiyo kwangu yameisha nanimemsamee coz ni mdogo wangu ila kuusu kumuigiza na yeye kupo pale pale nimesha maliza kutoka moyoni”

Mnyika Tumekupa Madiwani Wote, Watendaji Wote Lakini Barabara Hazipitiki

$
0
0
Mimi ni mkazi wa Mbezi Makabe naandika haya kwa uchungu sana jinsi barabara yetu ilivyo mbovu na hakuna mtu hata mmoja anaiangalia. Barabara ya kwenda Mbezi Makabe imekuwa mbovu mbovu. Haipitiki kabisa.

Hii barabara inayoanzia kituo cha zamani cha daladala Mbezi Mwisho kwenda Makabe-Msakuzi.wananchi wanataabika. Wanakaa zaidi ya masaa 3 barabaran kusubiri daladala. Daladala zimekimbia kutokana na ubovu wa barabara.

Magari ya watu binafsi nayo yanapata shida sana. Maji tunayonunua kwenye malori nayo yamepanda bei. Tunauziwa lita 1000 sh. 15 hadi elfu 20.Mbunge tuliempa kura nyingi na madiwani wote hatuwaoni jimboniMh. Mnyika wananchi walikuchagua wanapata shida.

Tunakuomba angalau lipitishwe greda tu. Wananchi wapo tayari kuchangia.Hali ya barabara ni Mbaya ni Mbaya ni Mbaya.Huduma za kijamii zimepanda. wananchi wamekata tamaaa.

Tafadhali Mh Mnyika, hii la barabara na Maji Makabe ni jipu. Rudi jimboni saidia wananchi.

By trplmike/Jamii Forums

Wabunge Wazidi Kuibana Serikali Sera ya Tanzania ya Viwanda...

$
0
0
Bila kujali itikadi za vyama vyao wabunge wameendelea kuishukia Serikali wakitaka ieleze kwa kina jinsi itakavyotekeleza sera ya ‘Tanzania ya Viwanda’ katika Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa Miaka Mitano, unaoanzia Juni.

Wakizungumza jana katika semina elekezi kwa wabunge iliyofanyika katika jengo la Millennium Tower jijini Dar es Salaam, wabunge hao walisema kauli ya Serikali juu ya kuanzisha viwanda nchini, haiendani na maelezo yaliyomo katika mapendekezo ya kuanda mpango huo.

Wakati wabunge wakieleza hayo, mchambuzi wa masuala ya uchumi, Profesa Honest Ngowi ambaye pia alitoa mada katika semina hiyo, alisema Serikali ni lazima ieleze sababu za viwanda vyake kufa, ianzie hapo kuvifufua ama kujenga vipya.

Katika mjadala wa mapendekezo ya Mpango wa Taifa katika mkutano wa pili wa Bunge la 11, suala la viwanda liliibuka na wabunge waliibana Serikali baada ya mpango huo kutofafanua kwa kina uanzishwaji wa viwanda nchini.

Akizungumza katika semina hiyo iliyohudhuriwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea aliitaka Serikali kuanza kueleza sababu za kuua viwanda, kabla ya kueleza mpango wa kuanzisha viwanda vipya.

“Serikali itueleze sababu za viwanda kufa, na ichambue kwa kina kama sababu hizo hazitaweza kuathiri mpango wake wa kuanzisha upya viwanda.

Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola alisema, “Suala hili la kuanzisha viwanda lipo katika ilani ya CCM, lakini ukiutizama mpango huu hamna kitu kama hicho. Hatujaona nguvu iliyowekwa katika kilimo ili twende sambamba na uanzishaji wa viwanda.”

Lugola ambaye ni makamu mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (Laac) alisema, “Watueleze watajenga viwanda gani na wapi? Vitakuwa vingapi na itatugharimu kiasi gani kuvijenga.

Haya yote hatujaelezwa wakati huu ambao tunaelekea katika bajeti ya 2016/ 17. ”

Kwa upande wake mbunge wa Igunga (CCM), Dk Dalali Kafumu alisema, “Sijui tutafanya miujiza gani kufufua viwanda! Nimeishauri Serikali kufanya utafiti kwanza sababu za kufa kwa viwanda kwa sababu huu ni mpango wa siku nyingi sana lakini utekelezaji wake umekuwa mgumu.”

Mbunge wa Bagamoyo (CCM), Dk Shukuru Kawambwa alisema, “Tukitaka kufufua viwanda lazima tujifunze kwa nchi kama China, Singapore, Ufilipino na Malaysia ambazo zilikuwa na uchumi kama wetu ila baada tu ya kuanzisha viwanda zimekua sana.”

Alisema mpango wa Taifa wa maendeleo ni mzuri na kitu pekee kilichobaki ni utekelezaji, kwa maana ya Serikali kueleza nini itafanya ili kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda.

Mbunge wa jimbo la Malindi (CUF), Ally Saleh alisema, “Utekelezaji wa mpango kama huu wa miaka mitano iliyopita ni asilimia 53 tu, sasa sijui huu wa miaka mitano ijayo utakuwaje? Serikali ifufue viwanda na si kujenga vipya. Inapaswa kutueleza itavifufuaje.”

Wabunge hao walisema hayo baada ya ofisa kutoka Tume ya Mipango, Kessy Maduka kuelezea mambo ya kuzingatia kufanikisha Mpango wa Maendeleo ya Taifa.  

Maeneo ya Wazi Yaliyovamiwa na Kujengwa Sinza Yameanza Kuwekwa X Tayari Kuvunjwa

$
0
0
Huku Sinza ni vilio na taharuki. Serikali inaweka X kwenye maeneo ya wazi ambayo watu wamejenga nyumba za makazi au Biashara kwa kuvamia bila vibali....

Unaambiwa Magufuli Kuzuia Safari za Nje Kwa Vigogo Imeokoa Mabilioni ya Pesa...

$
0
0
Badala ya sherehe za Uhuru, tumefanya usafi ili kupambana na kipindupindu, na fedha zilizookolewa zinajenga sehemu ya barabara iliyokuwa kero kubwa kwa wananchi.
Badala ya Rais na Wabunge kujipongeza kwa sherehe kubwa, fedha zilizookolewa zimetatua tatizo la vitanda kwa wagonjwa.

Badala ya sherehe za siku ya UKIMWI, fedha zimekwenda kununua dawa za kufubaisha makali ya UKIMWI.

Badala ya semina elekezi ya Mawaziri, fedha zake zitakwenda kutekeleza mradi wa kufunga vifaa vya kisasa vya kuchunguza magonjwa katika hospitali 37 kote nchini.

Badala ya safari za nje fedha zilizookolewa zitatumika kwenye miradi ya maendeleo. Zaidi ya Sh.7 bilioni ambazo zingeweza kutumika kwa safari za nje zimeokolewa katika siku 100 na zitatumika kwenye miradi hiyo ya maendeleo.

Hatua hizo, na nyingine nyingi, zimevuta hisia za watu mbalimbali kote duniani. Mnaofuatilia mitandao ya kijamii mnajua hivyo, na wapo wameonesha wazi kutamani tungewaazima Rais wetu kwa muda" Alisema Balozi Ombeni Wakati akitoa Tasmini ya Siku 100 za Rais Ikulu

Idara wa muziki ya East Africa Radio/EATV yadai Wimbo wa Nay ‘Shika Adabu Yako’ Hauna Matusi

$
0
0
Baada ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu kuufungia wimbo mpya wa Nay wa Mitego ‘Shika Adabu Yako’ na kudai kushangazwa na baadhi ya radio kuanza kuupiga wimbo huo na baadae kuwataka BASATA wafafanue kuhusu uhalali wake, Idara ya muziki wa EATV na East Africa Radio imetolewa ufafanuzi swala hilo.

Akizungumza katika kipindi cha Enewz cha East Africa Television, Mkuu wa idara ya muziki kutoka EATV na East Africa Radio, DJ Bigman ‘Kim’ amedai wimbo wa Nay ‘Shika Adabu Yako’ hauna matusi.

“Sisi kama East Africa Radio na EATV tuna utaratibu wetu, kuna kitengo kabisa cha muziki ambacho kinaitwa ‘Music Committee’. Kamati ya muziki kazi yoyote mpya inayokuja kwenye radio na TV kazi yetu ni kuiangalia na kuhariri. Tukiona kama nyimbo ina ukakasi, tunawasiliana na msanii either atuletee nyingine nzuri ambayo itakuwa kwa ajili radio au atupe ruhusa ya sisi kuhariri kwa vile ambavyo tutaona inafaa. Kwa sababu tunajua kwamba msanii anakuwa na fans wake na wale fans wanahitaji kitu kutoka kwake, kwahiyo tunaona ile nyimbo kutokwenda hewani tunamnyima haki msanii. So kwa issue kama hii sisi tumeusikiliza wimbo, tumeona ni wimbo mmoja kama ni controversial fulani lakini hajatukanwa mtu, hakuna neno lolote la kumtusi mtu, yaani ni kama comedy fulani hivi, kama rap katuni hivi imetungwa ambayo imewekwa katika mtiririko mzuri. Kwa mimi binafsi ninaweza sema hii kama imeishtua game, game kama ilikuwa imelala. Yaani zinahitaji vitu kama hivi ili watu wapate kufunguka,” alisema DJ Kim.

ALI KIBA Afunguka Kuhusu Mapenzi yake na Jokate...Adai Watu Wanafiria Tofauti

$
0
0
Alikiba na Jokate Mwegelo wamekuwa wakihusishwa kuwa wapenzi kwa miezi kadhaa sasa lakini hawajawahi kukiri hadharani.


Uhusiano wao umekuwa ukionesha kuwa upo kwa picha zao tu wanazopost kwenye mitandao ya kijamii, lakini tofauti na couples zingine wamekuwa wakiupeuka sana kuweka sentensi moja kuwa ‘sisi ni wapenzi.’

Tumezungumza na Alikiba kutaka kuujua ukweli na huenda akawa ametoa ‘hints’ ya kukusaidia kuthibitisha kama kweli uhusiano wao upo. “Watu wanafikiria tofauti, mimi na Jojo ni close friends,” amesema Alikiba.

“Tunapendana, tunashauriana, tunashare vitu vingi in a good way and she is a nice girl, she is beautiful na anastahili kuwa hata na mimi, kwanini sasa unashangaa? Lakini kama nikiamua kufanya vitu kama hivyo naweza kukuambia ‘Jojo si my girlfriend’ sishindwi lakini sasa watu wako tofauti,” ameongeza.

“Mimi siwezi kuweka personal life yangu hadharani, watu watanijua mimi kama mwanamuziki Alikiba na kuwapa vitu ambavyo wanastahili kupewa.”

Moyo wa Chuma wa Mbwana Samatta na Kilichowashinda Boban na Henry Joseph Kucheza Mpira wa Kulipwa Ulaya

$
0
0

Wahenga wana usemi wao ati ‘mvumilivu hula mbivu’ usemi huu kwa tafsiri ya kawaida kabisa humaanisha jinsi ambavyo binadamu anaweza kula matunda mazuri endapo tu atavumilia shida na jua wakati wa utafutaji wa tunda hilo.

Kwa utamaduni wetu wa Kiswahili hakuna kitu kigumu kama kuishi kwa ndugu,  mbali na nyumbani kwenu.  Ni rahisi sana kutafuta vijisababu ati unateswa na shangazi yako ama shemeji ili tu urudi ukajitanue nyumbani kwenu.

Mwaka 2013 niliposafiri kwenda Johannesburg,  Afrika Kusini kwa ajili ya mashindano ya Guinness Football Challenge niliamini kuwa hakuna kitu kigumu kama kwa Mtanzania wa kawaida kuishi umangani,  hali ya hewa (baridi kali), chakula (hakuna chipsi mayai) na mambo mengine mengi ya Kiswahili tuliyoyazoea,  kupiga soga na marafiki na mambo kama hayo,  inahitaji kujitolea sana kuishi.

Ukisoma historia ya safari ya Yaya Toure kutoka Abdjan hadi sasa anakula maisha Etihad, akihama kutoka nchi ya joto Cote d’Ivory hadi Moscow sehemu yenye baridi kali,  kubaguliwa rangi na matatizo ya lugha,  lakini alikomaa hadi sasa sio tu siye waafrika wenzake bali wazungu wanamtukuza,  kweli mvumilivu hula mbivu.

Haruna Moshi Boban alipata fursa ya kucheza ligi kuu ya nchini Sweden,  tukafurahi kwamba sasa Tanzania inaanza kupata wachezaji wa kimataifa,  lakini kilichomfanya Boban arudi Dar es Salaam,  bila shaka tumekielewa kidogo mara baada ya kusoma hapo juu,  nchi nyingi za wenzetu,  zina mazingira magumu sana kwa mtu kupata bangi na mambo mengine kama hayo,  la!  kwa gharama kubwa, ni ngumu sana kwa uswahili wetu huu.

Unakijua alichoshauriwa ndugu yangu Mrisho Ngassa asiende Sudan, na kuamua kubakia zake ligi ya Bongo?  Je, nini kilimshinda Henry Joseph Shindika hata arudi nyumbani akishindwa maisha ya Norway?  Inahitaji moyo wa chuma wa Yaya Toure, kufikia kilele.

Wiki hii nikiwa natazama mahojiano maalumu kati ya watangazaji wa Sports Bar ya Clouds Tv na mshambuliaji wa Tanzania anayekipiga Genk Ubelgiji, nilikumbwa na hisia kubwa na kumwomba Mungu wangu azidi kumtia nguvu na kumfanyia wepesi Mbwana Samatta afikie kilele cha matarajio yake.

Maisha ya Mbwana Samatta ni magumu mno kwa wachezaji ama yeyote mwenye moyo wa karatasi na mtu asiye mvumilivu.

Ingawa ni mapema bado sana,  lakini kwa Mbwana Aly Samatta,  ni ngumu sana kukubali yaishe huko umangani ili arudi kuandikwa na magazeti yetu hapa ya sports,  tumuombee.

Safari hii ya Mbwana Aly Samatta ni zaidi ya funzo kwa wanamichezo wote nchini pamoja na yeyote yule mwenye kutaka kuziishi ndoto zake.  Juhudi na uvumilivu wa Samatta utampeleka sehemu ambayo hakuna mtu yeyote amewahi kufikiria kuna siku Tanzania itakua na mwakilishi wake, kila la kheri Mbwana Ali Samatta.

By Na Simon Chimbo

WEMA SEPETU Hivi Huna Ndugu Wanaojitambua Wakakushauri? Where is Endlessfame? Drama Zina Mwisho Wake

$
0
0

Mnasemaje? Wema hakuwa na mimba? Mnamaanisha watu wazima kabisaaa mkaaminishwa na mkapost kwenye accounts zenu! jamani eeh Mimba si matangazo, mimba haijifichi msipate shida .

.
Mnajua nini? Inachekesha but inatia uchungu na huruma Sana! Mtu anawezaje ku fake maisha? Yaani nahisi ni risk na gharama Sana kufurahisha watu! Why Wema kuhangaika na hizo mambo wakati unaweza kufanya vizuri zaidi!?! Why usiwe wewe? Na mbaya zaidi wanaoyasema ni watu wa karibu, habari zafikaje kwa media? Unazipeleka wewe au Marafiki!!?? Hivi huna ndugu wanaojitambua wakakushauri???
.
Mimba kutafutwa, matangazo,
Mimba kuingia, matangazo
Mimba kujaa tumboni, matangazo,
Mimba Radio Matangazo
Mimba social networks matangazo,
Mimba kuumwa tumbo, matangazo
Mimba chumba cha operation, Matangazo
Mimba kutoka, tena mapacha, matangazo
.
Matangazo, matangazo, drama drama, scandal scandal....kweli unayaweza! Ugua pole sidhani kama uko mzima! Kuna pepo limekaa mahali inabidi litolewe ndo utajitambua kwamba maisha si matangazo maana watu wataona ukweli mwisho wa siku!! tumia jina lako vizuri kutangaza zaidi Kazi zako, where is Endlessfame? inabidi i kiki kuliko mimba!! Fanya kazi tafuta Pesa, drama zina mwisho wake, but huwa haviingiagi kwenye ubongo so ni Kazi bure!!

By Mrekebishatabia

Shamsa Ford Afunguka Kuhusu Nay wa Mitego Pamoja na Mzazi Mwenzake..Adai Hana Msaada Kwake

$
0
0
Staa wa Bongo Movie, Shamsa Ford, amesema mzazi mwenzie hasaidii huduma zozote za kibinadamu kama mahitaji kwa mtoto wao Terry.

Akifunguka mbele ya vipaza sauti vya Times Fm, Shamsa amedai Baba Terry hatoi hata ‘thumni’ kwa ajili ya matumizi ya mtoto.shamsa

“Ninapo sema mi ndo baba na mi ndo mama naomba nieleweke hivyo, Terry namlea mimi mwenyewe na ndio maana nampenda sana, baba Terry hachangii chochote, anyways ngoja ninyamaze tu” Alisema kwa hisia .

Katika hatua nyingine muigizaji huyo, ameweka wazi kuwa kwa sasa hana uhusiano wa kimapenzi na Ney wa Mitego, ila wamebaki kuwa marafiki wazuri.

Profesa Muhongo Mtegoni Tena..Meseji Aliyomtumia Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Yazua Maswali na Wingu la Shaka

$
0
0
UJUMBE mfupi wa  maneno alioutuma Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA),  Magdalena Chuwa,  akimtaka awashe  mita ya kupimia mafuta kwa sababu tu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anafanya ziara bandarini umezua maswali na kuacha wingu la shaka.

Mashine hiyo (flow meter) ambayo haijawahi kuwashwa kwa takribani miaka mitano  tangu inunuliwe kwa gharama inayozidi Sh bilioni 12, imesababisha jana Waziri Mkuu, Majaliwa awasimamishe kazi watendaji wawili wa WMA, akiwemo Chuwa na Meneja Vipimo Kitengo cha Mafuta, Bernadina Mwijarubi, ili kupisha uchunguzi wa upotevu wa mafuta bandarini kutokana na zuio la kutotumia mita hiyo kupima nishati hiyo.

Tayari ujumbe huo wa Muhongo umezua mjadala mkubwa katika maeneo mbalimbali, ikiwemo mitandao ya kijamii, wengine wakidai kuna namna na huenda Waziri huyo alikuwa anajua kinachoendelea Bandarini kuhusu wizi wa mafuta.

Wengine wamekwenda mbali na hata kujenga hisia kwamba huenda ujumbe huo usingetumwa Waziri Mkuu Majaliwa angekuta hali mbaya zaidi, huku wengine wakitaka achukuliwe hatua kama ilivyochukuliwa kwa wengine.

Juzi Chuwa alimwambia Waziri Mkuu kuwa sababu ya  kuwasha mita hiyo imetokana na kutumiwa ujumbe mfupi na Profesa Muhongo kuwa ahakikishe anawasha kifaa hicho  ndani ya saa 24.

“Mita imeanza kufanya kazi jana (Jumatano) kutokana na maagizo yaliyotolewa ngazi za juu, nilitumiwa meseji (ujumbe mfupi) kutoka kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo aliagiza ianze kazi ndani ya saa 24,” alisema Chuwa.

Baada ya  kutoa maelezo hayo, Waziri Majaliwa alimtaka Chuwa aseme kama serikalini wanafanya kazi kwa utaratibu wa ujumbe mfupi, lakini alishindwa kujibu.

Kutokana na ujumbe huo kuzua maswali, gazeti hili lilimtafuta Profesa Muhongo kwa njia ya simu ili kuweza kutolea ufafanuzi suala hilo, japo hakupokea simu lakini alipotumiwa maswali kwa njia ya ujumbe mfupi alijibu.

Maswali na majibu kati ya gazeti hili na Profesa Muhongo yalikuwa ni kama ifuatavyo;
Mwandishi: Habari Profesa Muhongo. Mimi naitwa Aziza Masoud, mwandishi wa gazeti la Mtanzania, nilikuwa naomba kujua kwa nini kitengo cha upimaji mafuta kilikuwa hakifanyi kazi, na ilikuwaje ukaandika ujumbe juzi kuwa kifanye kazi. Je, tunaweza  kupata ufafanuzi kwako kama waziri mwenye dhamana.

Profesa Muhongo: Flow meters hizo zinamilikiwa  na kusimamiwa na wakala wa vipimo (Weight & Measures) ambayo iko chini ya Wizara ya Biashara na Viwanda, waulize wakusaidie.

Swali: Asante, nimeelewa maelezo yako, lakini tulikuwa tunataka kujua kwa nini uliamuru ziwashwe, maana Mtendaji Mkuu wa WMA katika maelezo yake kwa Waziri Mkuu anadai ulimtumia ujumbe mfupi kumueleza aziwashe, tukaona kama unaweza ukawa unajua chanzo.
Profesa Muhongo: Waulize, hazipo chini yangu, mbona hutaki kwenda Wizara ya Viwanda na Biashara???????

Mwandishi: Ok, jioni njema, asante Profesa.
Profesa Muhongo: Nashukuru kwa kuelewa.
Profesa Muhongo ameingia katikati ya sakata hilo wakati ambako uteuzi wake katika Serikali ya Magufuli ukizua mjadala mkubwa kutokana na kuhusishwa na kashfa ya Escrow, wakati akiwa Waziri wa Nishati na Madini katika serikali iliyopita.

Ingawa katika serikali iliyopita  katika uchunguzi wake ilimsafisha Profesa Muhongo, hata hivyo, alivyoteuliwa katika serikali ya awamu ya tano, hatua hiyo ilipigiwa kelele na baadhi ya wanasiasa, akiwemo Mbunge wa  Singida Mashariki, Tundu Lissu pamoja na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, wakiapa suala hilo kulirejesha bungeni.

Wakati Profesa Muhongo akikwepa kuzungumzia ujumbe aliomtumia  Chuwa, taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Waziri Mkuu ilieleza kuwa uamuzi wa kumsimamisha Mtendaji huyo Mkuu wa WMA na Meneja wa  Vipimo Kitengo cha Mafuta, Mwijarubi ulifikiwa kwenye kikao cha Makatibu Wakuu kilichofanyika jana ofisini kwake, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,  Waziri Mkuu Majaliwa amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Adelhelm Meru, awaandikie barua za kuwasimamisha kazi watendaji hao kuanzia muda huo ili kupisha uchunguzi.

“Katibu Mkuu Viwanda, waandikie barua za kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi, katika kipindi hiki hawatatakiwa kusafiri kwenda popote hadi uchunguzi utakapokamilika, pia utafute mtu wa kukaimu nafasi hiyo ili kazi ziendelee,” alisema.

Alisema mbali na masharti hayo, ofisi yake pia itawaandikia barua ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Jeshi la Polisi wafuatilie suala hilo mara moja.

Alisema baada ya uchunguzi endapo itathibitika kuwa watendaji hao walihusika  na hujuma hizo, hatua rasmi zitachukuliwa na ikithibitika hawakuhusika watarudishwa kazini.

Katika taarifa hiyo pia Waziri Mkuu Majaliwa ameagiza mfumo wa upimaji mafuta kwa kutumia flow meters uendelee kutumika na ule upimaji wa kukadiria uache kutumiwa mara moja.

Katika ziara ya juzi pia alikagua flow meters za zamani zilizopo Kurasini (Kurasini Oil Jetty), kisha kutembelea na kukagua flow meters mpya ambazo zinajengwa Kigamboni.

Alisema mita hizo zimegharimu dola za Marekani milioni 6 (sawa na Sh bilioni 12.96 za sasa).
Pia Waziri Mkuu alitembelea sehemu ya kuchukulia mafuta yanayotoka bandarini (TPA Manfold) iliyoko Kigamboni na kukagua mitambo ya kusambazia mafuta kwenye matenki ya mafuta ya kampuni ya TIPER yaliyoko Kigamboni, yanayomilikiwa kwa ubia baina ya Serikali na Kampuni ya Oryx Energies.

Katika ziara hiyo ilibainika kuwa Kampuni ya TIPER imejiunganishia bomba la moja kwa moja kutoka kwenye bomba kubwa la mafuta linalotoka Bandarini, hali iliyomlazimu Waziri Mkuu kuagiza kwamba bomba hilo litolewe kwenye maungio hayo ndani ya mwezi mmoja.


  • “Jana (juzi) niliagiza kuwa bomba hilo ling’olewe, nimetoa mwezi mmoja ili kurekebisha mfumo huo, simamieni vizuri na kuhakikisha kuwa na wao pia wanarudi kwenye manfold kama ilivyo kwa wengine,” alisema Waziri Mkuu.

Rais Magufuli Asema Watu Wasishangae Paul Makonda Akipanda Cheo Kazi yake Imeoneakana

$
0
0
Magufuli akiongea na Wazee wa Dar es Salaam leo Amemsifia Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda na Kusema siku akipanda cheo watu wasinung'unike, kazi yake imeoneakana na heshima yake imeonekana

Hongera Makonda. Nyota yako imewaka. Mh Raisi kakuona... Sasa usiende kulala.

Nadhani leo Mbunge wa Ubungo (Mh Kubenea) ataugua homa...

Sitaingilia Uchaguzi wa Zanzibar - Rais John Magufuli

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema amekaa kimya kwa muda mrefu kuhusiana na suala la Zanzibar kwa sababu Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar ni huru na hawezi kuiingia kwa namna yoyote.

Rais Dkt. Magufuli ameyasema hayo leo katika ukumbi wa Diamond Jublee jijini Dar es salaa alipokuwa akilihutubia taifa kupitia mkutano ulioandaliwa na wazee wa Jiji la Dar es salaam.

''Zanzibar ina tume yao ya uchaguzi (ZEC) kama ilivyokuwa Tanzania bara tulivyo na (NEC) hivyo kama kuna ambaye hajaridhika na hali hiyo aende mahakamani mahakama ndiyo itakayotoa tafasiri'' amesema Dkt. Magufuli.

Rais ameongeza kuwa ataendelea kukaa kimya kuhusu Zanzibar ili wajiendeshe wenyewe kumaliza uchaguzi wao kama Tanzania bara tulivyomaliza uchaguzi wetu salama.

Aidha Rais amesema yeye kama Amiri Jeshi mkuu hatakubali chokochoko yoyote Zanzibar au katika eneo lolote la nchi na yeyote atakaye jaribu kuleta vurugu vyombo vya usalama vipo makini na vitahakikisha amani na usalama wa nchi unadumu siku hadi siku.

Producer Nahreel Ameingiza Pesa zaidi Mwaka 2015, Ametengeneza Hits Kali zaidi ya 16

$
0
0
Mtayarishaji wa muziki anayetamba kwa sasa,Nahreel kutokea studio ya The Industry amesema kuwa mwaka 2015 ndio umekuwa wa neema kwake kwani ndio mwaka ambao pochi lake limetuna sana kwa kutengeneza mkwanja mrefu zaidi kwenye tasnia hiyo kuliko miaka mingine yote huku akitingisha mawimbi ya redio kwa hits zaidi ya 16 kutokea mikononi mwake.

Nahreel amesema kuwa mwaka jana ameweza kupata nafasi ya kushiriki kwenye coke studio nchini kenya ambapo alikatiwa mkwanja unaovutia pia ukitoa kazi za studio ameweza kupata deals za matangazo nyingi.

“kweli,muziki unalipa na mimi kama producer umenilipa kwa njia nyingi,kwa wasanii kunilipa studio,kwa kazi nazopata off studio.Mwaka 2015 nilihusika kwenye coke studio nililipwa hela nzuri,nilipata radio adverts za makampuni tofauti..as producer nimenufaika sana mwaka 2015 kuliko miaka mingine yote" alifunguka producer huyo ambaye pia ni msanii wa navy Kenzo.

VIDEO: Waziri Muhongo Atajwa Kuvujisha Ziara ya Waziri Mkuu Kwa Meseji

$
0
0
Kumekuwepo na Watu waliokua wakitetea kwamba Waziri Muhongo hajamtumia Meseji meneja wa kurasini oil Jetty kuhusu ziara ya Waziri Mkuu.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo na Mizani, Bibi Magdalena Chuwa, amemtaja live kwamba, ametumiwa Meseji kutoka ngazi za juu, alipoulizwa na Waziri Mkuu ngazi za juu zipi zitaje, ndipo akasema alitumiwa meseji na Waziri wa nishati na madini Mh. Prof. Muhongo kwamba, akitupa maelekezo kwamba within 24hours, hizo mita zianze kufanya kazi.

Angalia Mwenyewe Video:


Viewing all 104781 articles
Browse latest View live




Latest Images