Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Hoyce Temu: Miss Tanzania Aliyejitoa Kusaidia Watanzania Kupitia Kipindi Cha Mimi na Tanzania

$
0
0
Hoyce Temu

Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akimlisha chakula Narsa Ramadhan (2) akiwa na mama yake Tatu Saleh (kushoto) wakati wa hafla ya chakula kilichondaliwa kwa watoto na wazee wanaoishi katika makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.(Imeandaliwa naModewjiblog)

Licha ya kuvaa taji la ulimbwende, Miss Tanzania 1999, Hoyce Anderson Temu amekuwa mfano wa kuigwa kwa walimbwende waliopita wa taji hilo nchini kwa kujitoa kusaidia jamii ya Tanzania kwa kutumia nafasi aliyonayo nchini.
Hoyce ambaye ni mzaliwa wa Arusha amekuwa mstari wa mbele kusaidia Watanzania ambao wanamatatizo mbalimbali kama ya kiafya na elimu ambapo amekuwa akitoa misaada na muda mwingine kutafuta wadhamini ili kusaidia jamii ambayo ameifikia kwa muda huo.
Baadhi ya mafanikio ambayo yamepatikana kupitia kipindi cha Mimi na Tanzania ni pamoja na kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya kupata matibabu akiwepo mtoto Hamisi ambaye alimsaidia kwenda kupata matibabu ya mguu wake.
Kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania kinachorushwa upitia Channel Ten kila siku ya jumapili, saa 9:30 usiku, Hoyce amefanikiwa kuandaa vipindi zaidi ya 1,000 maeneo mbalimbali nchini na katika maeneo yote ambayo ametembelea amefanikiwa kutoa msaada kulingana na mahitaji yanayohitajika.
Hoyce Temu

Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akisalimiana na mmoja wa wazee wenye ulemavu uliotokana na ugonjwa wa ukoma, Mganga Shija (66), wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.

Uamuzi wa Hoycekuwa na moyo wa aina hiyo ulikuja baada ya kutambua nafasi aliyonayo kwa jamii na kuona wingi wa matatizo waliyonayo Watanzania wenzake na hivyo kufikia uamuzi wa kuanzisha kipindi ambacho kwa sasa kina zaidi ya miaka 5 na bado ameonyesha nia ya dhati kuendeleza kipindi hicho.
Kwa kutambua huduma yake kwa jamii, Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga aliwahi kunukuliwa akimtaja Hoyce Temukama mlimbwende bora kuliko wote wakati alipotembelea kituo cha Nunge kilichopo Kigamboni, Dar Es Salaam kinachotumika kutunza wazee wasiojiweza na walemavu wasiokuwa na uwezo.
Pamoja ya kujitoa kusaidia Watanzania wenzake walio na uhitaji na kutumia muda wake mwingi katika huduma za kijamii, baadhi ya watu wasio na nia njema na Hoyce wamekuwa wakimwandika vibaya ilimradi tu kumchafulia jina katika jamii inayomzunguka.
Hoyce Temu

Mtangazaji wa kipindi cha Mimi na Tanzania, Hoyce Temu akirekodi moja ya kipindi chake cha Mimi na Tanzania na mtoto ambaye aliaga dunia kabla ya matibabu.

Kama Watanzania ambao tunapenda kuona huduma za kijamii zinaboreshwa kupitia kwa Hoyce Temuna kipindi chake cha Mimi na Tanzania tuna wajibu wa kuhakikisha tunaungana kwa pamoja kumsaidia Hoyce kama mwanamke shujaa na mwenye moyo wa huruma kuwasaidia Watanzania ili kufikia malengo ambayo ameweka kuisaidia jamii..
Muungano wa Watanzania ndiyo pekee utakaozidi kumfanya Hoycekuwa na moyo zaidi wa kusaidia Watanzania wenzake wenye uhitaji na amekuwa mtu ambaye anaonekana kuzingatia maoni ambayo anapewa na Watanzania wenye nia njema na yeye ili kuzidi kuwa mtu mwema katika jamii ya Tanzania na dunia kwa ujumla.
Hata hivyo licha ya watu wachache kumchafua amekuwa mtu ambaye hajishughulishi kuwajibu wenye nia mbaya na mipango yake kuwasaidia Watanzania na muda mwingi kuendelea kuitumia jamii na kufanya kazi kwenye kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano katika ofisi za Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini.
Pia licha ya kazi anazofanya Hoycekwa sasa anatumia muda wake mwingine kuongeza elimu yake kwa kuchukua PHD ya mambo ya Mawasiliano.

Kingunge Agoma Kuzungumzia Siku 100 za Rais John Magufuli Ikulu....

$
0
0
Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, amesema hatazungumzia lolote kuhusu utendaji wa Rais John Magufuli katika siku 100 za kwanza tangu aingie Ikulu.

Awali, mwanasiasa huyo ambaye mwishoni mwa mwaka jana alikihama chama alichokiasisi na kukitumikia kwa zaidi ya miaka 60, aliliahidi gazeti hili kuwa atazungumzia utendaji wa Rais atakapofikisha siku 100 madarakani.

Kingunge alisema mapema mwaka huu kuwa marais na viongozi mbalimbali hupimwa ndani ya siku 100, hivyo alitaka apewe muda hadi siku hizo zitakapotimia.

Lakini Kingunge alipotakiwa kutoa maoni yake jana mara baada ya Rais Magufuli kutimiza siku 100 tangu aingie Ikulu Novemba 5 mwaka jana, alikataa katakata kusema lolote na kumweleza mwandishi wa gazeti hili kuwa hakuna wa kumlazimisha kuzungumza.

“Hata kama niliahidi kuzungumza baada ya siku 100 kama unavyosema lakini hakuna mwenye uwezo wa kunilazimisha kuzungumza,” alisema Kingunge. "Sitazungumza, waulizeni wengine watasema ila mimi naomba mniache."

Kingunge ambaye alikuwa na kadi namba 8 ya CCM kabla ya kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kumpigia kampeni aliyekuwa mgombea urais wa Chadema kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Edward Lowassa, alisema ni mapema mno kumjadili Magufuli.

Wakati Kingunge akiahidi kuzungumza baada ya siku 100, Rais Magufuli alikuwa ametimiza siku ya 59 tangu aingie madarakani mwaka jana.

“Jamani ni mapema mno kumpima, msiwe na haraka nitatoa maoni yangu wakati huo ukifika kwasasa mwacheni afanye kazi zake msimwingilie ingilie,” alisema Kingunge ambaye aliwahi kushika nyadhifa nzito serikalini na kwenye CCM.

Kingunge alisisitiza kuwa hakuna haraka ya kuanza kumchokonoa Rais na badala yake aachwe atekeleze majukumu yake na tathmini atafanyiwa baada ya siku 100 akiwa Ikulu.

Oktoba 4 mwaka jana, Kingunge alitangaza rasmi kujiengua CCM, akisema alifanya hivyo kutokana na kile alichokiamini kuwa CCM haifanyi yaliyoasisiwa na kujengewa misingi bora na waasisi wake.

Wakati akitangaza uamuzi huo, alisema hakusudii kuhamia chama chochote cha siasa nchini bali atakuwa mtanzania huru lakini muda si mrefu aliungana na Ukawa kumnadi Lowassa.

Mwanasiasa huyo ambaye sehemu kubwa ya maisha yake alikuwa CCM, alisema wananchi wanataka mabadiliko na wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya chama hicho, ikiwa ni nukuu ya nasaha maarufu iliyowahi kutolewa na Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere.

Ndege ya Air Tanzania Yanusurika Kuwaka Moto Katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere

$
0
0
Msemo wa waswahili kwamba ng’ombe wa maskini hazai unaonekana kuwa kweli kwa Shirika la Ndege Nchini (ATCL), ambalo ndege yake pekee imenusurika kuwaka moto katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam juzi.

Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa wakisafiri kwenda mataifa mbalimbali ambao walizungumza na Nipashe juzi jioni, ndege hiyo ilionekana ikitoa moshi mwingi hali iliyosababisha magari ya zimamoto kufika eno hilo ili kuzima moto.

Msafiri mmoja ambaye alikuwa akipanda ndege kuelekea Nairobi, Kenya aliliambia gazeti hili kuwa waliona ndege hiyo ya ATCL ikitoa moshi mwingi hali iliyoashiria kuwa kulikuwa na hitilafu kwenye injini yake.

“Tuko hapa na tunaiona ndege inatoa moshi kweli kweli, watafuteni wahusika wawaambie tatizo nini,” alisema abiria huyo ambaye baadaye alituma picha mbalimbali za mnato na video kwa njia ya simu zikionyesha ndege hiyo ikitoa moshi mwingi.

Gazeti hili liliwasiliana na Katibu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, Ramadhani Maleta, ambaye alisema hawezi kulizungumzia suala hilo na alielekeza watafutwe wahusika wakuu ambao ni ATCL.

“Mimi siyajui hayo na wala siwezi kuwasemea wakati wenyewe wapo, watafuteni ATCL wao ndiyo wanauwezo wa kulizungumzia kwa kina suala hili, mimi kwanza siko kazini muda mrefu,” alisema Maleta.

Alipoulizwa kuhusu hitilafu ya ndege h iyo, Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, TCAA, Bestina Magutu, aliliambia gazeti hili kuwa ni vyema suala hilo wakaulizwa wahusika ambao ni ATCL kwa kuwa yeye si msamaji wa shirika hilo.

Jitihada za kumpata msemaji wa ATCL hazikuzaa matunda jana.

Akizungumza wakati wa siku ya sheria nchini, Rais John Magufuli alielezea kushangazwa kwake na kudumaa kwa ATCL hata kushindwa kumudu kuwa na ndege zake kama yalivyo mashirika mengine ya ndege Afrika na duniani.

Rais Magufuli alisema ana uwezo wa kununua hadi ndege sita mpya za kuliendesha shirika hilo lakini lazima wapatikane watumishi ambao watakuwa na uwezo wa kuliendesha na ikiwezekana "kuwafuta wafanyakazi wote walioko sasa."

Source:Nipashe

Sultan Idriss Awaomba Radhi Mashabiki Kwa Niaba ya Wema Sepetu Baada ya Wema Kukacha Kutokea Club Billz Jana

$
0
0
Usiku wa Jana Mrembo Wema Sepetu Alitakiwa Kuwepo Club Billz kujumuika na mashabiki wake lakini hakuweza tokea, Japo Club ilifurika mbaya baada ya taarifa kuwa Wema Atakuwepo...Idriss Sultan Asubuhi hii Ameandika Haya Kwenye Ukurasa wake wa Instagram

Idrissultan
 "Asanteni sana for all the major love and support mmeonyesha Billz ilikua ni  mmetisha sanaa.
I apologize kwa niaba ya wa ubavu wangu kutokufika mnilaumu mimi si mnajua tena tarehe 14 niliamka na usongo  ila anapumua bado "

Picha za Mafuriko ya Diamond Alivyopokelewa Turkana Kenya..Amrushia Dongo Ali Kiba..

$
0
0
Diamond Platinumz “Kwenye Mitaa!!!....Molah nakushkuru kwakuwa naamini hizi zote ni baraka zako.... ila tu niwakumbushe ndugu zangu kuwa "Kuku hata umlishe nini kamwe hawezi kunyonyesha!"..... NAIROBI get ready for your Platnumz!!! AMERICA | EUROPE see you soon!”


Lundenga Asikitishwa na Maneno Yanayosambazwa Mtandaoni Kuhusu Hoyce Temu...

$
0
0
Hashim Lundenga
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (pichani) amezungumza  kuhusu habari zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kumhusu Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu.
Lundenga amesema kuwa yeye kama Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania na Mtanzania wa kawaida amesikitishwa na maneno hayo na kuwa hayapendezi kusemwa kwa mtu kama Hoyce ambaye amejitoa kusaidia jamii.
Alisema kuwa anashangazwa na mtu ambaye amekuwa akiandika maneno hayo mtandaoni kwani hawakuwa na utofauti wowote na kilichokifanya ni kumuandika Hoyce ambaye hakuhusika katika ugomvi uliokuwepo baina ya mtu huyo na mdogo wake Hoyce, Rachel.
“Nimesikia habari hizo kumhusu Hoyce kwa kweli nimesikitishwa sana, sio jambo zuri ambalo amelifanya huyo aliyemuandika,” alisema Lundenga.
Hata hivyo mwenyekiti huyo aliwataka watumiaji wa mtandao kuwa na matumizi mazuri ya mtandao ili kuzidi kuifanya mitandao ya kijamii kuwa sehemu salama kwa ndugu na marafiki kuwasiliana.
Zaidi unaweza kusikiliza maneno ya Lundenga hapa chini.

Nafasi za Kazi Kama Internship At The Economic and Social Reseach Foundation (ESRF)

$
0
0
Nafasi za Kazi Kama Internship At The Economic and Social Reseach Foundation (ESRF)

More details on the documents below;-

Hatimaye Lady Jay Dee na Gadner G Habash Wapeana Talaka

$
0
0
BAADA ya mvutano wa muda mrefu, hatimaye diva wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ amepewa talaka rasmi kwenye Mahakama ya Manzese, Sinza jijini Dar.

Jide alifungua kesi ya madai ya talaka katika mahakama hiyo baada ya kutofautiana na mtangazaji maarufu Bongo, Gardner G. Habash ‘Captain’, aliyekuwa mumewe wa ndoa kabla ya kumwagana takriban miaka miwili iliyopita.


Taarifa kutoka kwa chanzo cha kuaminika, wawili hao waliooana mwaka 2005, walitinga katika viunga vya mahakama hiyo Alhamisi iliyopita kisha hukumu ya kesi hiyo kusomwa na talaka rasmi kutolewa kwa Jide na Gardner.

“Nimemuona Jide na Gardner hapa, wamekuja kusikiliza hukumu yao. Taarifa za uhakika ni kwamba tayari mahakama imevunja rasmi ndoa na kila mmoja kapewa hati yake ya talaka na sasa kila mtu yupo huru kuendelea na maisha yake,” kilisema chanzo.

Baada ya taarifa hizo kutua kwenye dawati la gazeti hili, mwanahabari wetu alimtafuta Jide ili aweze kuzungumzia hatua hiyo waliyoifikia lakini simu yake haikuwa hewani kama ilivyokuwa kwa Gardner lakini bahati nzuri mmoja wa ndugu wa mrembo huyo mkongwe wa Bongo Fleva aliyeomba hifadhi ya jina alipatikana na kufunguka:

“Ni kweli tulikuwa mahakamani. Jide ameshapewa talaka yake na kila kitu kimeenda vizuri. Gardner naye kapewa hati yake ya talaka hivyo kuanzia sasa kila mmoja yupo huru kufanya yake.”

KIMENUKA..Zari Hassan Mpenzi wa Diamond Atajwa Kuwa ni Mwanachama wa Freemanson Uganda

$
0
0
Mwandani wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ameorodheshwa kwenye listi ya watu maarufu nchini Uganda ambao ni wanachama wa jamii ya siri ya Freemason kisa kikielezwa kuwa ni utajiri alionao wenye maswali mengi.

Habari kutoka Kampala, Uganda zilizoripotiwa hivi karibuni zilieleza kwamba, mwanamama huyo ana ukaribu mkubwa na matajiri wa Nigeria ambao wanaaminika kuwa utajiri wao ulitokana na kuwa ‘memba’ wa mtandao huo mkubwa duniani.

Ilidaiwa kwamba, Zari amekuwa akifanya kufuru ya fedha zinazowashangaza wengi, kuwa kwa muziki au biashara gani anazofanya zinazomuingizia mkwanja mrefu kiasi cha kumiliki magari ya kifahari kama Lamborghini na Hummer ambayo yote ameyaandika majina yake badala ya namba za usajili.

Katika habari hiyo, wengine waliotajwa ni pamoja na aliyekuwa mumewe aliyezaa naye watoto watatu, Ivan Semwanga, wachungaji maarufu nchini humo na wanamuziki kama Joseph Mayanja ‘Jose Chameleone’ na Bebe Cool.


Zari anayemiliki hoteli ya kifahari iliyopo kwenye Mtaa wa Kagwa, Kampala nchini Uganda, anasemekana kumiliki vyuo vya urembo na maduka ya vipodozi nchini Afrika Kusini huku akijiingizia mkwanja kupitia shoo zake za Zari All White Party anazozifanya kwenye nchi za Afrika Mashariki za Uganda, Tanzania na Kenya.

Ijumaa Wikienda lilipomtafuta Zari hakupatikana badala yake aliyezungumzia ishu hiyo ni mpenzi wake, Diamond ambaye alisema kuwa mama mtoto wake ana miradi mingi na siyo kama wanawake wa mjini ambao wanabweteka badala ya kutafuta mkwanja.

Mke Wa Kafulila ( Jesca Kishoa ) Aendelea Kumkalia Kooni Mwakyembe..Ataka Naye Afikishwe Mahakani Kwa Ufisadi wa Mabehewa Mabovu

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalumu, mkoani Singida Jesca Kishoa(CHADEMA), amesema aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe na Katibu Mkuu wake, wanapaswa kufikishwa mahakamani katika sakata la mabehewa mabovu.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,  Kishoa alisema viongozi hao, pia aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha wakati huo, naye afikishwe mahakamani kwa sababu ndiye alikuwa mlipaji Mkuu wa Serikali.

Alisema ni aibu Kiti cha Spika kumfukuza mbunge bungeni akidaiwa kuzungumza uongo kabla ya kudai ripoti ya mabehewa ili kujua ukweli wa jambo hilo ni upi.

Aliongeza kuwa, Katibu Mkuu huyo alilipa fedha asilimia 100 kinyume cha sheria wakati Dkt. Mwakyembe ambaye kwa sasa ni Waziri wa Katiba na Sheria, aliruhusu mabehewa yanunuliwe.

"Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi naye awajibishwe kwa kosa hilo kama Mtendaji Mkuu wa Wizara...mabehewa hayo yalipokewa kwa mbwembwe lakini kasoro zake zinatokana na zabuni ya utengenezaji wake kutozingatia viwango.

"Kampuni ya Hindustan Engineering haikufanyiwa uchunguzi kuhusu rekodi na uwezo wake, malipo yalifanyika kwa asilimia
100 kabla ya mabehewa hayajawasili nchini," alisema.

Alisema umma unashuhudia baadhi ya vigogo wa TRL wanafikishwa mahakamani kutokana na sakata la mabehewa hayo na kusisitiza sheria ichukue mkondo wake kwa wote waliohusika si  kuwashtaki wachache wakati Mawaziri wanaachwa.

Kishoa ambaye ni Mke wa aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila (NCCR-Mageuzi), alisema hakuna mtu mwenye uhakika kwamba mabehewa mabovu ni 25 kati ya 275.

"Nani ana uhakika kwamba waliokamatwa ndio wanahusika peke yao, haiwezekani Serikali ikajichunguza yenyewe, kujishughulikia yenyewe kwa kuamua nani imtoe kafara, nani imlinde wote, wote washtakiwe kama ilivyo kwa wengine," alisema Kishoa.

Kishoa alihoji kwanini ripoti ya mabehewa inaendelea kufichwa na haifikishwi bungeni ili Bunge liweze kuisimamia Serikali jambo ambalo halitoi picha kwa Bunge la 11.

Msikilize Hoyce Temu Kwa Mara ya Kwanza Akizungumza Kuhusu Kuandikwa Vibaya Katika Mtandao wa Instagram

$
0
0
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu ametoa hisia zake kuhusu kuandikwa katika mitandao ya kijamii kupitia kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na Clouds Fm.
Unaweza kumsikiliza hapa chini wakati akizungumzia jambo hilo;

Breaking News: Vigogo Wanne MSD Wamesimamishwa Kazi Kwa Ufisadi wa Billion Moja

$
0
0
Waziri wa Afya, Ummy Mwaimu amewasimamisha kazi vigogo wanne wa bohari ya dawa (MSD) kwa tuhuma za ubadhirifu wa billion 1 na nusu ili kupisha uchunguzi dhidi yao.

Shamsa Ford Akasirika Baada ya Nay wa Mitego Kumpost na Kumtakia Happy Valentines Day...Amtaka Ajiheshimu

$
0
0
Shamsaford 
"Naona mambo yanazidi kuvumishwa kwamba nimerudiana na nay. Pls pls nina maisha yangu na mwanaume ambae nampenda na kumuheshimu. ..sijarudiana na nay na haiwezi kutokea kabisaaa. ..Nay una ndugu na marafiki wengi wa kuwaposti siku ya leo haikuwa muhimu uniposti mimi.nilishukuru Mungu watu walishasahau kuhusu mimi na ww but naona umetaka kuyafufua. Sipendi scandal na si maisha yangu kutafuta kiki za kijinga. KAZI YANGU NDO INAYONITAMBULISHA. ..PLS TUESHIMIANE" Shamsa Ford

Rapper John Woka Apata Ajali ya Kulipukiwa na Gesi, yupo ICU

$
0
0
Rapper anayejulikana kwa kurap kama mlevi, John Woka, amepata ajali ya kulipukiwa na mtungi wa gesi. Kwa sasa amelazwa kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Walikuwa wanahangaika kurekebisha usafiri kwenye garage hapo Sinza, sasa katika kuhangaikia upande wa AC mtungi wa gas ukalipuka,moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani. Madaktari wanahofia imefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo.

Mpaka hapa bado hajapata fahamu,mipango ya matibabu inaendelea. Tunasubiri kuambiwa kinachotakiwa kufanyika na mahitaji. Hospitali pale yupo kaka yake ambaye anapatikana kwa number ya Woka +255767007005 na mzee wake,kwa yoyote ambaye angependa kufika,kujua kinachoendelea au kuchangia chochote anaweza kumpigia tu moja kwa moja.

KIMENUKA...Aunty Ezekiel na Moze Iyobo Wapigana Kibuti?

$
0
0
Msanii wa filamu za Bongo Aunty Ezekiel maarufu kwa jina la mama Cookie siku hizi, ameonekana akiwa mbali na mwandani wake Moze Iyobo, na kuibua hisia kuwa huenda wawili hao wamemwagana siku ya valentine

Tukio hilo limetokea kwenye sherehe za uzinduzi wa albam ya msanii Mirror ambaye yuko chini ya mwanadada Wema Sepetu, usiku wa siku ya wapendanao (valentine) na kuwafanya watu wengi wawashangae, ndipo camera za EATV zilipowanasa baba na mama Cookie wakiwa mbali mbali, kama hawajuani.

Wakiwa ukumbini hapo Aunty Ezekiel (mama Cookie) alionekana akiwa close na Idris Sultan ambaye shemeji yake kwa shoga yake kipenzi Wema Sepetu, huku Moze Iyobo (baba Cookie ) akionekana akiwa na marafiki zake, ilihali siku hiyo ilikuwa maalum kwa wapendanao.

Zicheki picha hapa chini za tukio zima lilivyoenda.


Niva kumjibu Ney kwa kutumia Filamu...Ayaanika Maisha ya Nay wa Mitego Kabla ya Umaarufu

$
0
0
Mwigizaji wa filamu Tanzania Niva a.k.a Super Mario ameingia 'location ku shoot' filamu yake mpya inayoonesha maisha halisi aliyo pitia msanii wa Bongo Fleva Ney wa Mitego.

Hatu hiyo inakuja ikiwa ni sehem ya kujibu vijembe vya Ney alivyo vitoa kwenye wimbo wake na kuwagusa wasanii kadhaa wa movie akiwemo Niva.

Enews ilifanikiwa kumkuta msanii huyo akiwa katika kazi ya kushoot filamu hiyo ambayo inamdiss moja kwa moja Ney wa Mitego na kuonesha maisha ya Ney kabla ya kuwa Star wa Bongo fleva ili iwe funzo na kuacha kuwaimba wasanii wenzake.

Niva amesema kuwa mashabiki zake wamchukulie Ney kama mtu asiyejielewa na wakae tayari kusubiri Movie hiyo ambayo itakuwa funzo kwa Ney wa Mitego kwa tabia zake za kuwaimba wasanii.

Rais Magufuli Amteua Dr. Asha Rose Migiro Na Mathias Chikawe Kuwa Mabalozi Wapya....Dr. Kipilimba Kateuliwa Kuwa Bosi Mpya Wa NIDA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi watatu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Rais Magufuli pia amefanya uteuzi wa makamishna wanne wa Jeshi la Polisi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imewataja mabalozi walioteuliwa kuwa ni Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe na Dkt. Ramadhan Dau.

Vituo vya uwakilishi kwa mabalozi hawa vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia kukamilika.

Kwa upande wa Makamishna wa Polisi, Balozi Sefue amewataja walioteuliwa kuwa ni:

Naibu Kamishna wa Polisi Simon Nyakoro Sirro ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi, na ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam. Kamishna Sirro anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Mstaafu Suleiman Kova.

Naibu Kamishna wa Polisi Albert Nyamuhanga ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Fedha, Utawala na Lojistiki. Kamishna Nyamuhanga anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Clodwing Mathew Mtweve aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.

Naibu Kamishna wa Polisi Robert Boaz Mikomangwa ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Intelijensia.

Kamishna Mikomangwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Valentino Mlowola aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Nsato Marijani Mssanzya ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Mafunzo na Operesheni.

Kamishna Mssanzya anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Paul Moses Chagonja aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.

Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Kipilimba alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Udhibiti (Director of Risk Management) katika Benki Kuu ya Tanzania. Dkt. Kipilimba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dikson Maimu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Teuzi zote zinaanzia leo tarehe 15 Februari, 2016

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
15 Februari, 2016

Nape Nnauye Amsimamisha Kazi Mkurugenzi Wa Habari Na Matukio Pamoja Na Meneja Wa Vipindi TBC

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amewasimamisha kazi watumishi wawili wa Shirika la Utangazaji la Taifa TBC kutokana na utendaji usioridhisha.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TBC leo jijini Dar es Salaam, Waziri Nape amewataja watumishi waliosimamishwa kazi kuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Matukio Bwana Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi Bibi. Edna Rajab ambao wote kwa pamoja wasimamishwa kazi na uamuzi huo utafikishwa kwa Bodi ya TBC kwa hatua zaidi.

“Tunachukua uamuzi wa kuwasimamisha kazi watendaji hawa ili kujenga upya Idara hii muhimu katika ustawi wa TBC na habari kwa ujumla” Alisema Nape

Aidha Waziri huyo amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TBC kuwachukulia hatua watumishi wengine walio chini ya Idara hiyo kwakuwa wako chini ya mamlaka yake na kutoa mrejesho wa hatua alizochukua dhidi ya wale wote wilioonyesha utendaji mbovu.

Alisema kuwa Serikali imefikia uamuzi huo kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya muda mrefu juu ya utendaji mbovu na wakutoridhisha viongzi na baadhi ya watumishi wa Idara hiyo hiyvo hatua hizo zimechukuliwa ikiwa ni  kujenga upya na kuboresha Idara hiyo muhimu katika uendeshaji wa Shirika lolote lile la Habari na kuongeza ufanisi.

Idara ya Habari na Matukio ya TBC inaundwa na Mkurugenzi wa Idara, Meneja wa Vipindi Wahariri na Waandishi wa Habari ambapo tayari Mkurugenzi na Meneja wa Vipindi wamesimamishwa kazi leo tarehe 15 Februari 2016 na watumishi wengine watachukuliwa hatua kufuatia agizo la Mhe. Waziri wa Habari kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC alilolitoa leo wakati akitangaza kuwasimamisha kazi viongozi hao.

Wimbo wa Shika Adabu Yako Wafanya Mashabiki Wambebe Nay wa Mitego Ju Juu, Mwenyewe Ashangaa na Kusema Haya

$
0
0

Naytrueboy Ameandika Haya:

"MadLove AboutLastNight Masasi #ShikaAdabuYako ilipoanza tu Ikawa ivii 
Asanteni Watu wangu wa Kusini #ShikaAdabuYako hii Ngoma nadhani kwangu haijawaitokea. Sitaki kuamini kua mpaka Uku mikoani tayari ni Wimbo unaoimbwa na kila Na Kila mtu Kama imetoka miezi Miwili iliyotoka.!! Faraja niliyonayo haielezeki. #ShikaAdabuYako Next week Video out!!" Nay wa Mitego

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yahamisha wafanyakazi 104 Dar es Salaam

$
0
0
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imefanya mabadiliko makubwa baada ya kuwahamisha wafanyakazi 104 waliokuwa Mkoa wa Dar es Salaam na kuwapeleka mikoa mbalimbali nchini.

Mbali na wafanyakazi hao, uhamisho huo umemkumba pia mmoja wa wakurugenzi wake, Aboubakar Kunenge ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala aliyehamishiwa mkoani Rukwa.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Huduma kwa Walipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alithibitisha wafanyakazi hao 104 kuhamishwa.

“Ni kweli wafanyakazi hao wamehamishwa, lakini huu ni utaratibu wa kawaida wa kiutawala na tumekuwa tukiufanya mara kwa mara, kila baada ya muda tunawahamisha baadhi ya wafanyakazi wetu,” alisema Kayombo.

Aidha, Kayombo alithibitisha kuwa ni kweli Kunenge ni mmoja wa watumishi wa mamlaka hiyo waliohamishwa na kukiri amepelekwa Rukwa, ambako ataendelea kushughulikia masuala hayo ya utawala na rasilimali watu.

Katika uhamisho huo, wafanyakazi wanaotoka kituo cha TRA Ilala waliohamishwa ni 43 ambao wamepelekwa mikoa ya Iringa, Kigoma, Mbeya, Rukwa, Shinyanga, Ruvuma, Manyara, Tanga, Kilimanjaro, Pwani, Tabora, Morogoro, Lindi na Arusha.

Katika kituo cha Kinondoni, jumla ya wafanyakazi zaidi ya 11 wamehamishiwa katika mikoa Singida, Iringa, Rukwa, Mbeya, Ruvuma, Kagera, Mara, Tabora, Arusha na Tanga. Aidha, katika vituo vya Temeke, wafanyakazi zaidi ya 10 walihamishiwa katika mikoa ya Arusha, Morogoro, Iringa, Tabora, Mara, Kagera, Lindi, Morogoro, Kigoma na Rukwa.

Aidha, pia wamo wafanyakazi wawili kutoka Iringa waliohamishiwa Kinondoni Dar es Salaam, mmoja kutoka Iringa kwenda Ilala, Kisarawe kwenda Shinyanga na Bagamoyo kwenda Ruvuma.

Ingawa mkurugenzi huyo alikataa kuzungumzia sababu za kuhamishwa kwa mkupuo kwa watumishi hao, lakini kwa muda mrefu tangu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa afanye ziara ya kushtukiza katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) Novemba mwaka jana, kumekuwa na msukosuko pia katika TRA.

Baada ya kukuta uozo wa kashfa ya ufisadi wa makontena, Waziri Mkuu huyo aliamuru kusimamishwa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade baada ya kubaini kupitishwa kwa makontena zaidi ya 300 bandarini bila kulipa kodi na kusababishia hasara Serikali ya zaidi ya Sh bilioni 80.

Pamoja na hayo, maofisa wote wa TRA ambao walihusishwa na sakata hilo walitakiwa kutosafiri nje ya nchi na kukabidhi hati zao za kusafiria mpaka pale uchunguzi dhidi yao utakapokamilika.

Aidha, miongoni mwao tayari wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakihusishwa na uzembe uliosababisha kutoroshwa kwa makontena TPA bila ya kulipiwa ushuru.
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live


Latest Images