Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live

Siwezi kurudiana na Nay wa Mitego - Shamsa Ford

0
0
Ikiwa imepita siku moja toka Nay wa Mitego kupost picha ya Shamsha Ford kwenye mitandao yake ya kijamii ikiwa na ujumbe wa 'Happy Valentine' hususani siku ya wapendanao mwanadada Shamsha Ford amefunguka na kusema

kuwa kamwe hawezi kurudiana kimapenzi na msanii huyo wa bongo fleva ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa 'Shika Adabu yako'

Shamsha Ford amesema kuwa kwa sasa ana maisha yake na mwanaume mwingine ambaye wanaheshimiana na anampenda hivyo kitendo cha Nay kupost ujumbe wa Valentine akitumia picha yake yeye anaona ni kama msanii huyo anataka kuwakumbusha watu mambo ambayo yeye alishayasahau na mashabiki walisha sahau na kumtaka msanii huyo amuheshimu kwani kwa sasa hayupo kutafuta kiki wala scandal za kijinga.

"Naona mambo yanazidi kuvumishwa kwamba nimerudiana na Nay. Pls pls nina maisha yangu na mwanaume ambae nampenda na kumuheshimu. ..sijarudiana na nay na haiwezi kutokea kabisaaa. ..Nay una ndugu na marafiki wengi wa kuwaposti siku ya leo haikuwa muhimu uniposti mimi. nilishukuru Mungu watu walishasahau kuhusu mimi na wewe but naona umetaka kuyafufua. Sipendi scandal na si maisha yangu kutafuta kiki za kijinga. KAZI YANGU NDO INAYONITAMBULISHA. ..PLS TUESHIMIANE" alimalizia Shamsa Ford

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya Februari 16, Ikiwemo Kauli Tata za Magufuli..

0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya Februari 16, Ikiwemo Kauli Tata za Magufuli..


Waziri wa Afya Awasimamisha Wakurugenzi Wanne MSD

0
0
WAFANYAKAZI wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), wametakiwa kuanza kujisafisha huku wakiambiwa kwamba taasisi hiyo haitaepuka kutumbuliwa majipu.

Aidha, wameagizwa kuwasilisha upya taarifa za mali zao kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, zifanyiwe uhakiki wa mali; moja baada ya nyingine kubaini waliofanya udanganyifu wa umiliki wa mali zao.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki alisema hayo jana Dar es Salaam kwenye ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa viongozi wa taasisi hiyo.

Alisisitiza kuwa tayari anazo taarifa zinazohitaji baadhi ya viongozi wa taasisi hiyo kutumbuliwa majipu muda muafaka utakapowadia.

Kairuki aliagiza taasisi hiyo kufanyia tathmini kesi zake zote, ilizowahi kushindwa na kuja na majibu ya sababu za kushindwa na endapo itabainika hazikushinda kutokana na mchezo mchafu wa wachunguzi, wahusika wachukuliwe hatua haraka iwezekanavyo.

“Niliposikia mnataja majina yenu wakati wa kujitambulisha, nilikuwa nafurahi sana kwani wengi wenu nawajua na nina taarifa zenu. Haiwezekani wewe mtu mmoja watu wengi wawe wanakuongelea vibaya. Msifikiri majipu humu (Takukuru) hakuna, yapo na nawahakikishia tutayatumbua tu,” alisisitiza Waziri huyo.

Alisema iwapo yupo mtumishi hasa viongozi wa taasisi hiyo, anayejitambua kuwa ni ‘jipu’, ajisalimishe kwani akiendelea kusubiri na kutumbuliwa, mwisho wake utakuwa mbaya.

“Tukiwatumbua hali itakuwa mbaya kwani nyie mko chini ya Ofisi ya Rais, hata Rais (Dk John Magufuli) hatasita kuwachukulia hatua si tu za kinidhamu bali hata za kisheria,” alibainisha.

Alisema katika taasisi hiyo, yapo maeneo mengi yanayohitaji kutumbuliwa majipu kuanzia Uhasibu, Ukaguzi na Manunuzi zikiwemo ofisi za mikoani akitolea mfano Mkoa wa Kilimanjaro na makao makuu, Upanga, Dar es Salaam.

“Tutasafisha nawahakikishia hata ikibidi kuanza upya, ikitulazimu pia kufukuza wote ikithibitika mnakwenda kinyume na maadili yenu tutawafukuza ila hatutamwonea mtu, kwani wako watu wengi wenye sifa wanaotaka kufanya kazi,” alisisitiza Kairuki.

Alisema kuanzia sasa, ofisi hiyo itawekewa malengo ya utendaji wake na kufanyiwa tathmini hasa kwa kesi zilizoshindwa ifahamike aliyezifanya, sababu za kushindwa, iwapo imetokana na uzembe au kama upo mkono wa mtu.

Alisema imefikia wakati sasa watumishi wa taasisi hiyo wanapaswa sasa wale kiapo cha ahadi ya uadilifu na kukisaini ili watakaoshindwa wachukuliwe hatua za kinidhamu.

Taarifa za mali
Aliwataka watumishi wote wa taasisi hiyo, kurejea upya kuwasilisha taarifa za mali zao kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

 Alisema taarifa hizo zitapewa kipaumbele cha kuhakikiwa mali moja baada ya nyingine na endapo mtumishi atabainika kufanya udanganyifu wa mali anazomiliki, atachukuliwa hatua.

Alihadharisha kuwa chombo hicho cha kupambana na rushwa hakipaswi kutuhumiwa kwa rushwa. Alisema kikituhumiwa kwa sifa hiyo, ni sawa na kuigeuza Takukuru kuwa jipu badala ya vidole vya kutumbulia majipu.

Takukuru mpya
Alisema Serikali ya Awamu ya Tano, imejipanga kuhakikisha inazalisha chombo kipya cha kuzuia na kupambana na rushwa chenye maadili.

Aliwataka wanaoona hawawezi kwenda na kasi hiyo, wawasilisha barua zao za kujiuzulu kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Kamishna wa Polisi Valentino Mlowola.

Hata hivyo, alisema Serikali inatambua kuwa kazi ya upelelezi na uchunguzi ni ngumu kutokana na kukabiliwa na vishawishi vingi, jambo ambalo wanahitaji ujasiri. Alisisitiza watumishi hao kutunza heshima yao na chombo hicho.

“Faraja ya uchunguzi ni kufanikisha majalada kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) na baadaye watuhumiwa kufikishwa mahakamani. Sasa ili kufanikisha faraja hii ni vyema kufanya kazi kwa weledi na tusiwe na pupa ili mradi tupeleke kesi nyingi kwa DPP na kuziwasilisha mahakamani,” alisema Kairuki.

Aliendelea, “Nasema haya kwa sababu nafahamu bado kwenye uchunguzi hapa Takukuru kuna upungufu. Nafikiri mmemuona Mheshimiwa Rais anavyoshughulikia suala la rushwa na ufisadi, ni wajibu wenu Takukuru kufanikisha azma hii kwa kuja na matokeo ya utendaji chanya.”

Aidha, waziri huyo aliitaka taasisi hiyo kutumia weledi, sifa yaa ukachero wa kiupelelezi na kiuchunguzi kufuatilia matukio yenye shaka yanayoendelea mitaani na si kusubiri taasisi kubwa kuyavumbua.

“Nyie ndio makachero tumieni ukachero wenu kuibua ufisadi, kuna mtu mmoja amebainishwa na Rais lakini jina lake kwa umaarufu na utajiri wake linatumika kama kituo, alishajiuliza sababu na kuchunguza?” alihoji.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mlowola aliwataka wafanyakazi wa taasisi hiyo kubadilika na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Kasi ya Magufuli
Aliwataka wahakikishe wanaendana na kasi ya Dk Magufuli na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya utendaji na utumbuaji wa majipu katika maeneo yenye ubadhirifu wa fedha, rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

“Natarajia tutafanya kazi kwa weledi na si nguvu, kwa mfano taarifa zilizotolewa katika maeneo ya bandarini na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), siye ndio tulitakiwa tuziwasilishe juu (ngazi ya Rais). Naomba tusisubiri kuletewa,” alisisitiza.

Aliwataka watumishi hao kujiepusha kuwa watuhumiwa wa rushwa. “Jamani hii ni mbaya kwetu Polisi akituhumiwa ujambazi ni mbaya sana, lakini ofisa wa Takukuru akituhumiwa rushwa ni dhambi kubwa. Sisi tuwe watu wa mwisho kutuhumiwa kwa rushwa."

Aliwataka watumishi hao kuelekeza nguvu zao katika kuhakikisha wanaisaidia Serikali kwenye eneo la upotevu wa fedha kwa kufuatilia matumizi na miradi ya maendeleo na fedha zinazopelekwa kwenye halmashauri na kwenye manunuzi ya umma.

Alisema katika utekelezaji wa jukumu la kuzuia na kupambana na rushwa nchini kwa mwaka 2014/15 taasisi hiyo ilipokea malalamiko 4,675. Ilifanyia uchunguzi na kukamilisha majalada 667, kupeleka kwa DPP majalada 278, walirejeshewa majalada 172 yenye vibali vya kufungua mashtaka na kufungua kesi mpya 314 nchini kote.

Aidha alisema taasisi hiyo ilishinda kesi 132 mahakamani na washitakiwa walihukumiwa vifungo mbalimbali ikiwemo faini. Ziliokolewa Sh bilioni saba zilizokuwa ziingie kwenye mifuko ya wabadhirifu wachache.

Ndani ya siku 100 za Rais Magufuli madarakani taasisi hiyo ilipokea malalamiko 411 kutoka kwa wananchi, imefungua mafaili 146 ya uchunguzi. Imepeleka kwa DPP mafaili 103, mafaili 65 yenye kibali cha DPP yamerejeshwa kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka, jumla ya kesi 72 mpya zimefunguliwa mahakamani na imeshinda kesi 40 na kushindwa kesi 52.

“Ndani ya siku 100 tumefanikiwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa 11 akiwemo Mtendaji Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Kipallo Kisamfu,” alisisitiza.

Habari Mbaya:Rapper John Woka Afariki Dunia Baada ya Kupata Ajali ya Kulipukiwa na Gesi

0
0
Rapper anayejulikana kwa kurap kama mlevi, Michael Dennis Mhina maarufu kama John Woka, amefariki dunia alfajiri ya Jumanne hii.

Woka amefariki baada ya juzi kupata ajali ya kulipukiwa na mtungi wa gesi. Alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Hii ni taarifa iliyotolewa na mtu wa karibu na rapper huyo kuelezea ajali hiyo:

Walikuwa wanahangaika kurekebisha usafiri kwenye garage hapo Sinza, sasa katika kuhangaikia upande wa AC mtungi wa gas ukalipuka,moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani. Madaktari wanahofia imefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo.

Kwa yeyote aliyeguswa na angependa kutoa rambi rambi anaweza kuwasiliana na kaka yake kwa namba +255767007005.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

Baada ya Kimya cha Siku Kadhaa Wema Sepetu na Idriss Sultan Waja na Mpya...

0
0
Idris Sultan na mpenzi wake Wema Sepetu wanakuja na reality TV show ambayo itakuwa inazungumzia maisha yao.

Akizungumza na Bongo5 Jumamosi hii, Idris alisema ameamua kuungana na mpenzi wake Wema ili kuandaa project mbalimbali ambazo zitakuwa zinawaingizia pesa.

“Unajua mkiwa katika mahusiano halafu wote ni celebrity lazima angalau mfanye kazi mbili tatu ambazo zitawaingizia pesa,” alisema Idris.

“Zipo project nyingi lakini tunaanza na reality show. Hii ni nyingine na mpya na itakuwa inazungumzia matukio mbalimbali ya maisha yetu,” aliongeza Idris

Source:Bongo5

Tetesi za Kutimuliwa kwa Van Gaal zashika Kasi...

0
0
Kocha mkuu wa klabu ya Manchester United Louis Van Gaal huenda akatupiwa virago na nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho kabla ya mwisho wa mwezi Februari kwa mujibu wa gazeti la The Sun.

Kipigo cha 2-1 kutoka wa Sunderland Jumamosi kumewaacha mashetani wekundu na nafasi ndogo sana kumaliza nafasi ya nne msimu huu huku Ligi ya Uropa ndiyo michuano pekee wanayoweza kufuzu kwa ajili ya msimu ujao kucheza klabu bingwa barani Ulaya.

Mourinho amekuwa akitajwa sana kwenye tetesi za kibarua cha Man United licha ya nadharia zilizozuka kuwa huenda asiendane na tamaduni za klabu hiyo.

Inaaminika kuwa kwa hali hii hawawezi kutinga nne bora kabisa huku habari zinadai kuwa uongozi wa mashetani hao wekundu unaweza kusitisha mkataba wa Van Gaal na kumleta Mourinho sasa wakati wakilenga mechi dhidi ya Arsenal Februari 28

Shirika la Kimataifa la DKT Lazindua 'Fiesta Condoms' Nchini Tanzania

0
0
Mkurungezi wa shirika la DKT International Tanzania Raphael Da Silva akizungumza machache kwenye uzinduzi wa chapa mpya ya shirika hilo “Fiesta condoms” katika soko la Tanzania uliofanyika katika hoteli ya kitalii ya Ledger Plaza, Kunduchi jijini Dar es salaam.

Wanandoa mbalimbali wakishiriki kwenye michezo inayohamasiha upendo na mshikamano wakati wa maandalizi ya kusherekea siku ya wapendano ambayo iliambatana na uzinduzi rasmi wa chapa mpya za “Fiesta condoms” nchini Tanzania. Uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya kitalii ya Ledger Plaza, Kunduchi jijini Dar es Salaam.

   
Washindi wa safari ya Cape town Bw & Bi.  Mohammed wakifurahia jambo na Mkurugenzi wa shirika la DKT International nchini Tanzania Bw. Raphael Da Silva (Kulia) mara baada ya kuibuka washindi kwenye bahati nasibu iliyochezeshwa wakati wa uzinduzi rasmi wa “Fiesta condoms” nchini Tanzania uliofanyika hoteli ya kitalii ya Ledger Plaza, Kunduchi jijini Dar es salaam.

     
Meneja Masoko wa shirika la DKT International Tanzania Bw. Davis Kambi (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa bahati nasibu iliyochezeshwa na shirika hilo wakati wa uzinduzi wa “Fiesta condoms” nchini Tanzania uliofanyika katika hoteli ya kitalii ya Ledger Plaza jijini Dar es salaam. Washindi hao walijishindia safari za mapumziko kuelekea Zanzibar, Cape town na Dubai.

PRESS RELEASE
Februari 2016, Dar es Salaam Tanzania
Shirika la kimataifa la DKT, linalojihusisha na elimu ya uzazi wa mpango pamoja na vita dhidi maambukizi ya VVU na UKIMWI, hivi leo limezindua kondomu za Fiesta katika soko la Tanzania.
Kondomu za Fiesta zimekuwa sokoni kwa zaidi ya miaka 20 na zinapatikana nchi zaidi ya 40 duniani kote. Uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Ledger Plaza maeneo ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huu umekuja kipindi kifupi kabla ya sikukuu ya wapendanao duniani ya Valentine ambayo pia ni siku ya kimataifa ya uelewa wa kondomu.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo, meneja masoko wa DKT International nchini Tanzania, Bwana Davis Kambi alisema anaamini ni muda muafaka kwa chapa hii kupatikana katika soko la Tanzania.
“Huu ndo utambulisho rasmi wa chapa hii Tanzania ikiwa kama njia ya kukabiliana na mahitaji ya wateja wetu na kuvutia watumiaji wapya” alisema wakati wa uzinduzi. Pia alisema uzinduzi huo utawapa wapendanao chapa wanayoweza kuiamini na itakayoboresha maisha yao. Wakiwa wameweka mikakati ya kuipa nguvu chapa hii kwa kutumia njia za mawasiliano na ushiriki katika nyanja mbalimbali ili kumrahisishia  mtumiaji kuielewa na kuikubali chapa hii kama kitu poa kutumia.

“Kondomu za Fiesta ni mahususi kwa wapendanao ambao husaka raha na hisia kali zaidi. Fiesta ni sherehe yenye nakshi, Fiesta ni kwa ajili ya ukaribu zaidi. Fiesta ni chapa ya kisasa inayoshindana na chapa nyingine za kondomu kubwa kimataifa” alisema Kambi.

Fiesta ina zaidi ya ladha 55 tofauti na zaidi ya aina 60 lakini kwa sasa DKT International Tanzania imetambulisha aina nne tu; Fiesta Heat, Fiesta Ultra-thin, Fiesta Strawberry and Fiesta Max dotted. Aliongezea kwa kusema kuwa shirika linatazamia kuongeza aina tatu (3) zaidi kabla ya kufikia mwisho wa mwaka 2016.

Kambi alisema uzinduzi huu wa kondomu za Fiesta utatengeneza historia kwa kuunga mkono juhudi za kufikia lengo la kuzuia maambukizi ya VVU kabisa. Alisema katika kulinganisha tafiti za VVU ya mwaka 2007-08 na Malaria 2011-12 nchini Tanzania, wamebaini kuwa maambukizi ya VVU yamepungua kutoka asilimia 5.7 hadi asilimia 5.1 kati ya watu wenye miaka 15-49. Vivyo hivyo maambukizi yamepungua kwa wanawake kutoka asilimia 6.6 hadi 6.2 na kwa wanaume kutoka asilimia 4.6 hadi 3.8 na kama shirika linalopambana na VVU na UKIMWI katika dhana zote wanaendelea kuona haja ya kupunguza uenezaji wa gonjwa hili.

Aliwashauri watu wakumbuke kuwa kondomu husaidiaa kuzuia maambukizi ya VVU na hivyo ni muhimu kutumia. Aidha Kambi aliasa kuwa ni muhimu kondomu kupatikana kiurahisi na kwa bei poa ili kuvutia watumiaji wengi kitaifa.

Alielezea zaidi kwamba Fiesta zitapatikana kwa bei ya rejareja ya shilingi 1500 za Kitanzania ambayo ni kwa paketi ya kondomu tatu ambayo kiuhalisia ni bei rahisi kwa chapa ya kimataifa. Kwanzia mwezi huu zitapatikana maduka ya madawa, maduka makubwa ya rejareja, hoteli, gesti na klabu za usiku kubwa nchini kote. Alisema pia kwamba wanafanya kampeni maalum ya kuitambulisha zaidi Fiesta kwa soko la Tanzania.

Kwa maelezo zaidi:
Tovuti ya Trust: www.trustlife.co.tz
Twitter: @trustlifetz
Instagram: trustlifetz

Mwanasiasa Mkongwe, Augustine Mrema Atoa ya Moyoni Kuhusu Rais Magufuli Siku 100 za Ikulu...

0
0
Mwanasiasa Mkongwe, Augustine Mrema amemuelezea Rais John Magufuli kama kiongozi wa Tanzania anayetenda miujiza kutokana na utendaji wake ndani ya siku 100 tangu alipoingia madarakani.
Mrema ambaye alikuwa mbunge wa zamani jimbo la Vunjo na kuangushwa kwenye uchaguzi uliopita na James Mbatia (NCCR – Mageuzi), aliendelea kuutetea uamuzi wake wa kumpigia debe Dk. Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu ingawa chama chake cha TLP kilikuwa kimesimamisha mgombea urais.
“Nilijua wazi Rais Magufuli ni mtendaji ndio maana hata wananchi waliponiadhibu kwa sababu ya kumpigia debe sikuumia, najivunia chaguo langu na kiukweli anafanya miujiza ya hali ya juu,” alisema Mrema.
Mrema ambaye ni mwenyekiti wa TLP, alimuelezea Magufuli kama kiongozi mwenye uthubutu huku akiwataka watanzani kuacha unafiki na kumpa nafasi zaidi ya kufanya kazi

Breaking News: Waziri wa Elimu Amfuta Kazi Mkurugenzi wa Bodi Ya Mikopo Kwa Utendaji Mbovu

0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amemfuta  kazi  Mkurugenzi wa bodi ya mikopo na wakurugenzi wengine wa nne kutokana na utendaji mbovu katika kuendesha bodi hiyo.

IMEVUJA...Sikiliza Sauti ya Dongo Janja Akimtongoza Msichana..Afunguka Yote Mpaka Kuwaponda na TIP TOP Connections..Adai Wanamfanyia Revenge

0
0
Ikiwa zaidi ya mwaka mmoja tangu tusikie Dogo Janja kurudi Tip Top Connection bado tunasubiri ujio wake mpya akiwa na kundi lake hilo la zamani,Nimefanikiwa kupata sauti ya Dogo Janja Akimtongoza Msichana Na Kufunguka yote kuhusu Tip Top Connection Kumbania...

Majibu aliyotoa Dogo Janja ndiyo yanayobeba kitu tunachojiuliza kama ana bifutena na Tip Top Connection,unaweza kusikiliza kwa kubonyeza play hapo chini.

Sasa Udaku Special Blog Ipo Play Store..Unaweza Kuinstall Kwenye Smart Phone yako Hapa

0
0

Good News! Sasa Blog yako ya Udaku Special Ipo Google Play Store.

Download Udaku Special Blog Android Application CLICK HERE From Play Store

Au Bonyeza hii picha hapa chini

Mange Kimambi Atolea Ufafanuzi Sakata la Kumtukana Hoyce Temu Mtandaoni..Adai Hana Tatizo na Hoyce Bali Mdogo Wake Ndo Shida

0
0

Jana Hoyce Temu Alilalamika kupitia Radio kuhusu kusemwa vibaya kwenye mitandao..Leo Mange ameibuka na kutolea ufafanuzi kwanini Hoyce Temu Ameingia katika Ugomvi wake na Rachel Temu mdogo wa Hoyce.....Ameandika hivi

"Okay nimesikiliza interview ya Hoyce Temu CloudsFm. I'm glad hakunilaumu Mimi peke yangu, Ila pia ingekuwa vizuri zaidi yeye Kama dada angekuwa fair na asingenilaumu mimi hata robo! .

Sometimes Embu tuweni fair Jamani. Hivi Jamani how many times nimejaribu kuepuka ugomvi na Rachel Miwaya? How many times nimekaa kimya? Na hata huu ugomvi Ulivyo anza si nilimtusi yeye Kama yeye nilimtaja ndugu yake au Mwana familia yake??? Nani alieanza mambo ya kutukana ndugu na Watoto? na mkumbuke alinitukaniavMarehemu baba yangu na still nikikaaa kimya simkutukana ndugu yake, then ni kampa warning kuwa akiendelea kutukana ndugu zangu ntamwanika dadake Hoyce Temu still akadhani I'm just bluffing. Nyie mnaonilaumu mnataka niwe na roho Kama ya Yesu?Kama Ni kumgeuzia shavu la pili I think nilimgeuzia Mara 70. Mtu anajifabya yeye ndo mvuta bangi wa Instagram mlitaka nifanye nini? Mtu anamtukana mwanangu mlitaka mimi nimtukane Nani wakati yeye hana mtoto? Mtu kawa tukana dada zangu mlitaka nimtukanie paka wake na sio dada yake? Mtu katukana baba yangu Marehemu mlitaka nitukane ndugu zake walio hai?Mnakuwa hamko fair at all. .

Imagine nilisema this year staki mabeef na Mtu , kwanini Mtu asichukulie hii as a sign of peace instead anachukulia as a weakness na kupata bichwa. Nilisema Na ntasema tena jamani 2016 Ni Mwaka wa kutafuta pesa staki shobo na Mtu. Ila Mtu anaponichokonoa for a long time sometimes na mimi nashindwa kuvumilia.

Hoyce unajua Mimi sina shida na wewe. Tatizo mdogo wako tu, huyu ndo adui yako, Huyo ndo mwiba kwenye maisha yako. Kila Mtu ana past yake na wengi mno ndoa zao pia zina Siri kibao Ila mdogo wako matusi yake yanafanya watu tunaongea Maneno mazito. Deal with Rachel kwanza Kabla ya Mtu mwingine yoyote Yule and you will live your life in peace.
.
Ni hayo tu jamani, just because nimesema sitaki ugomvi in 2016 it doesn't mean I'm weak au namuogopa mtu yoyote Yule it means nimekuwa, it means nazeeka naingiza 36 Mwaka huu soon ntakuwa 40 years sitaki kuwa in my 40s bado Niko mitandaoni nachambana na watu, so I'm making the change. But that doesn't mean eti mtu ndo ajifanye anataka kuni bully, ukinichokonoa sana ntakumalizaaaaaa!" Mange Kimambi

Zitto Kabwe Amvaa Rais John Magufuli Posho za Wabunge na Kuendelea Kuilipa IPTL

0
0

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amemvaa, Rais John Magufuli na kuhoji mpango wake wa kubana matumizi, huku akiachia posho za wabunge kupanda maradufu na Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, ikiendelea kulipwa mabilioni YA fedha licha ya Bunge la 10 kutaka mkatanba wake na Tanesco uvunjwe.

Taarifa ya Zitto kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana ilisema kuwa, posho zinazolipwa zimependekezwa kufutwa na Mpango wa Maendeleo 2011/12 - 2015/16.

“Badala ya kuzifuta, serikali imeongeza posho za kujikimu mpaka Sh. 120,000 kwa siku kwa wabunge na bado wanalipwa posho za vikao Sh. 220,000 kwa siku,” alisema.

Zitto alisema posho ambazo zimeshalipwa tangu Rais Magufuli aingie madarakani ni sawa na kujenga barabara zote viporo za lami za kuunganisha mkoa wa Tabora (Kaliua - Urambo na Nyahua - Itigi).

Alisema pia mkataba wa IPTL unaendelea kunainyonya nchi kwa serikali kuendelea kulipa Sh. bilioni nane kila mwezi kwa kampuni hiyo na PAP.

“Katika siku 100 tangu Rais Magufuli aingie madarakani Sh. bilioni 30 zimeshalipwa kwa IPTL/PAP, ambazo zingeweza kununua mashine za CT-Scan kwa hospitali zote za mikoa nchini.

"Fedha hizi ni zaidi ya mkopo ambao serikali imechukua kutoka Benki ya Dunia ili kujenga 'flyover' ya Ubungo, jijini Dar es Salaam,” alisema Zitto.

Alisema serikali bado inatumia mashangingi na kila waziri, katibu mkuu na wakuu wa idara wanatumia magari hayo ya gharama kubwa.
Mambo mengine yaliyogusiwa na Mbunge huyo ni serikali kuendela kuagiza nje ya nchi sukari, jambo ambalo ni hatari kwa wakulima wa sukari na viwanda vyake nchini.

“Hivyo hivyo kwa sekta ya nguo bado viwanda vya ndani vinapata ushindani usio halali kutoka kwa nguo za nje zenye kuingia nchini bila kodi,” alisema Zitto.

Pia, alisema taarifa ya serikali kuhusu utoroshaji wa fedha nje bado imefichwa na haijafikishwa bungeni.

“Hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kudhibiti utoroshaji fedha na hakuna mashtaka yaliyofunguliwa kwa wahusika,” alisema Zitto.

Mbali na mambo hayo, alisema Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), bado haina mamlaka ya kukamata na kushtaki wenye makosa ya kifisadi.

 “Vile vile mfumo wa kila mwenye mali kutakiwa athibitishe kaipataje (reverse burden of proof) haujaanzishwa nchini na matokeo yake ni kuzorota kwa juhudi za kumaliza ufisadi kwa kuboresha mifumo.

Kinachoendelea ni kutumbua majipu kimkakati bila kuzuia majipu kuota tena,” alisema.

Udom Watuhumiwa Kutumwa na CCM Kufukuza Mwanafunzi

0
0

Hali ya sintofahamu imeibuka baada ya Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), kumsimamisha masomo Rais wa Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii, Victor Byemelwa, na kudaiwa kumwandikia barua Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa, kumueleza kwamba wamemaliza kazi aliyowatuma.

Uongozi wa chuo hicho umethibitisha kumsimamisha masomo mwanafunzi huyo lakini ukikanusha kuandika barua kwenda kwa Kimbisa.

Jana kwenye mitandao ya kijamii, barua inayodaiwa kuandikwa Februari 5, mwaka huu na Mshauri wa Wanafunzi wa chuo hicho, Dick Manongi, ilikuwa ikisambazwa.

Barua hiyo yenye kumbukumbu namba Udom/Dos/36, ilikuwa na kichwa cha habari: "Ukamilisho wa kazi iliyopangwa kufanyika katika koleji ya Humanities & Social Science."

Iliendelea kusema:  "Ofisi  ya Mshauri wa Wanafunzi Udom, inapenda kukujulisha komredi Adam Kimbisa (Mwenyekiti wa CCM Dodoma,) kuwa kazi mliotupatia katika kutekeleza mkakati wa kuiondoa serikali ya wanafunzi wa upande wa Humanite, imekamilika kwa kijana Victor Byemelwa (aliyekuwa Rais) kuondolewa chuoni kwa kipindi kisichojulikana.

"Napenda kukuhakikishia kuwa kwa kuwa mashtaka yametolewa na Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Mipango, Utawala na Fedha na yeye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, ni wazi kuwa kijana huyu hataweza kamwe kurudi chuoni hivi karibuni.

Tutumie sikukuu hii ya Chama kupanga mikakati ya kuweka serikali mpya tuitakayo mapema iwezekanavyo."

Akizungumzia sakata hilo, Manongi alikanusha kuandika barua hiyo na kudai kuwa imeghushiwa na tayari ameshatoa taarifa polisi katika kitengo cha ufuatiliaji makosa ya kimtandao (cybercrime) ili kutafuta aliyeighushi.

"Barua nimeiona, lakini naomba uwasiliane pia na uongozi wa chuo, mimi nisingependa kuzungumza hilo maana hilo suala nimelipeleka kwa watu wa Cyber Crime Dodoma, wao watatueleza hiyo barua imetoka wapi, binafsi sijaiandika," alisema Manongi.

Kwa upande wake, Ofisa Uhusiano Udom, Beatrice Ntenga,  alisema mwanafuniz huyo alisimamishwa kutokana na kosa la kuitisha Baraza la Shule bila kupata idhini ya Mkuu wa Chuo au Makamu Mkuu wa Chuo na kwamba amesimamishwa kwa muda usiojulikana.

Alisema mwanafunzi huyo anatakiwa kujibu mashtaka yake kwa mujibu wa taratibu za chuo na baadaye ataitwa kamati ya nidhamu.

"Barua hiyo tumeiona ikisambaa kwenye mitandao haijatolewa na Dean of Student, imeghushiwa maana muhuri na saini vinaonekana 'vimeskaniwa' na kuwekwa na hata hiyo kumbukumbu namba ya barua haipo kwa Dean ukiisogeza utagundua mapungufu mengi. Tumepeleka huko Cyber Crime wanafuatilia,"alisema Ntenga.

Alisema barua hiyo si ya kweli bali imetengezwa ili kutafuta huruma ya watu huku akithibitisha taarifa za barua hiyo zimewasilishwa polisi.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Kimbisa, alipopigiwa simu hakupokea na badala yake alitaka atumiwe ujumbe mfupi wa simu, baada ya kutumiwa ujumbe wa simu yake hakujibu.

Updates za Habari ya Kufutwa Kazi Kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo na Wenzake..Walioteuliwa Kushika Nafasi Hizo Hawa Hapa

0
0
Waziri wa Elimu Sayansi, Teknolojia na ufundi, Prof Joyce Ndalichako amesitisha mkataba wa kazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo George Nyatenga (Pichani chini).

Pia amewasimamisha kazi Wakurugezi watatu wa Bodi hiyo ambao ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Yusufu Kisare, Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo Juma Chagonja na Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo.

Prof. Ndalichako amemwagiza Mkaguzi wa ndani Mkuu wa Serikali ahakiki maelezo na Nyaraka zilizowasiliwa na Bodi ya Mikopo pamoja na kufanya ukaguzi maalum kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi sasa.

Amewateua wafuatao ku Kaimu nafasi; Kaimu Mkurugenzi Mtendaji mteule ni Bw. Jerry Sabi kutoka Mzumbe University na Kaimu Mhasibu Mkuu mteule ni Bw. Daniel Mafie kutoka NECTA

Magufuli Ataka Bandari Zilindwe Na Jeshi La Polisi Kama Ilivyokuwa Hapo Awali

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka jeshi la polisi nchini kurejesha kitengo cha ulinzi bandarini na pia eneo ambalo linafungwa mita za mafuta.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imesema Rais Magufuli ametaka jeshi la polisi nchini kurejesha ulinzi kama ilivyokuwa nyakati za nyuma kabla mamlaka ya bandari haijaamua kubandilisha mfumo wa kuweka walinzi wake.

Balozi Ombeni Sefue ameongeza kuwa katika eneo ambalo linafungwa mita za mafuta (Flowmeters), ambalo waziri mkuu alitembelea na kumsimamisha mkurugenzi wa wakala wa vipimo sasa ni lazima lilindwe na jeshi la polisi.

Linnah Afunguka Sababu za Wasanii wa Kike Kutofanya Vizuri Kwenye Game la Bongo Fleva

0
0
Kwenye upande wa game la muziki nadhani hii iko world wide kwamba watoto wa kike wako wachache sana,hata kibongo bongo pia,sasa kuhusiana na game la kibongo linah ana sababu zake ambazo anahisi ndizo zinazosababisha watoto wakike hawatusui kibongo bongo lakini.

‘’Tumekuwa hatuko ‘real’ tuna nafikiana sana maneno huyu kampelekea huyu,mara kutengenezeana stori,halafu vitu vingine zinakuwa sio vya kweli,ukiwa karibu na mtu Fulani mwingine anaona bora akakuharibie,kuna vitu vinaendelea chini ya kapeti tunafanyiana sisi wasanii vinakuwa sio poa,hiyo hali inapelekea tunakuwa hatusapotiani,ndio maana muziki wetu hauendelei,hatuna umoja,’’Linnah

Cloudsfm.com

Supastaa Hasheem Thabeet yu Wapi?

0
0
Kama watanzania wazalendo tulifurahia sana ufiko wa kilele cha mchezo wa kikapu wa mbongo mwenzetu huyu.

Ni mafanikio makubwa naweza kuyaita kwa upande wa burudani na michezo kwa hatua aliyofikia Hasheem!
Ni masikitiko yangu kwamba simuoni kwenye maHeadline ya michezo na burudani kwa ujumla!

Yu wapi huyu supastaa na afanya nini sasa aliko!?
Kwa wenye data zake wakuu, mimi nashabikia sana wabongo watuwakilishao vyema Internatianale!!

Nay wa Mitego Asema: Ommy Dimpoz Akipata Mtoto ndo Atabishana Naye

0
0
Rapa mtukutu kutoka kiwanda cha muziki Tanzania, Nay wa Mitego, amejibu shutuma za msanii mwenzie Ommy Dimpoz aliyemtaka akapime DNA ili kujiridhisha kuwa mtoto aliyenaye (Curtis) ni wake ama la.

Akizungumzia kauli hiyo, Nay amesema anaona kauli hiyo haina maana kwa kuwa mtoto ni wake na kuongeza kuwa hawezi kubishana na Ommy sababu hana mtoto hata wa kusingiziwa.
“Mimi kwenye shika adabu yako nilimchana Ommy, kiukweli tetesi zilizopo mtaani yule jamaa (Ommy) hajawahi kuonekana na demu hapa Bongo Live.

Ameishia tu mara kupost wanawake waliopo Ulaya wakimbusumbusu, kwanini hatumuoni na mademu hapa? wakati wanawake wa Kiafrika ndio wazuri zaidi na wanakila kitu? kuhusu mtoto siwezi bishana nae, angekuwa na yeye anamtoto sawa, akipata mtoto nitamjibu kuhusu DNA”

Ushahidi Mpya : Penati ya Messi na Suarez ni Feki..Sio Goli..

0
0
Moja kati ya habari kubwa weekend iliyopita ni penati ya Lionel Messi na Luis Suarez. Jana nilikupa story kwamba Neymar amelalamika kwamba ilibidi iwe penati yake na Suarez alikimbilia tu kupiga.

Sasa leo kutokana na picha mpya zilizotoka ni kwamba ile penati ilikua feki na imevunja sheria ya upigaji penati. Kitu cha kawaida kila mtu anajua ni kwamba mtu akiwa anapiga penati inatakiwa wachezaji wote wakae nje ya box la kipa had pale atakapogusa mpira.

Sasa kwenye hii picha inaonyesha kwamba Suarez alikua ameshaingia ndani ya Box wakati Messi bado hata hajapiga mpira. Kama ilivyotokea kwa Henry na Robert Pires na Messi na Suarez nao wamefanya kosa la kisheria.

Picha hii imeenda viral kwenye mtandao wa twitter na kuonyesha kwamba halikua goli halali kwa mujibu wa sheria za penati.

Viewing all 104429 articles
Browse latest View live




Latest Images