Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live

Mapya yaibuka juu ya NEY WA MITEGO adaiwa kujichubua na kuchonga nyusi

$
0
0

Hali imezidi kuwa mbaya baada ya Masnii maarufu Ney wa Mitego kutoa nyimbo yake Mpya ya "SHIKA ADABU YAKO" Ambayo imepelekea nyimbo hiyo kuzua maneno ya kila aina juu ya mashahiri yake yalio wagusa baadhi ya wasanii hapa nchini..


Hata hivyo hali sio nzuri kwenye mitandao ya kijamii baada ya mashabiki wakila pande kutukanana na kutoleana maneno machafu. 


Baadhi ya mashabiki wa Team zilizo chambwa katika wimbo huo wamekuja na madai haya mapya juu ya Ney wa Mitego..

Hii Ndio Sababu Kwanini Mwanamuziki Jux Hapendi Kumuongelea Mpenzi Wake wa Zamani Jack Cliff Aliyoko Jela China

$
0
0

Msanii mahiri wa miondoko ya R&B amekuwa hapendi kuzungumzia suala la mpenzi wake wa zamani Jack Patrick ambaye anatumikia kifungo akiwa jela huko Macau, Hong Kong nchini China kwa tuhuma za kugundulika na madawa ya kulevya katika mwili wake.

Jux amekuwa akiulizwa mara kadhaa na waandishi wa habari kuhusu suala hilo lakini amekuwa hataki kulizungumzia suala hilo lakini kupitia kipindi cha XXL kinachorushwa na Clouds Fm Radio amefungukia suala hilo na kusema kuwa hapendi kulizungumzia suala hilo ili asije akaonekana anapatia umaarufu au kiki kupitia yaliyo msibu mpenzi wake.


Jux ameongeza kuwa siyo vizuri kulizungumzia suala hilo kwani atandugu zake Jack hawapendi, hivyo anapenda kuulizwa zaidi kuhusu kazi zake anazo zifanya, huku akisisitiza kuwa kwa sasa ana mpenzi ambaye anampenda kwa dhati na ikitokea x-wake akaachiwa itabidi akubaliane na atakayo yakuta.

Sababu ya Mimba Kuharibika, Dalili na Matibabu yake Unapoona Dalili

$
0
0

Mimba kuharibika au kutoka ni hali ya mimba yenye wiki 28 au chini ya hapo kuharibika au kutoka. Hali hujulikana kama miscarriage au spontaneous abortion kwa kiingereza. Mtoto aliye tumboni katika umri huu hataweza kuishi nje ya tumbo la mama. Katika nchi zilizoendelea huchukuliwa mimba iliyo chini ya kipindi cha wiki 24.

Zaidi ya asilimia 80 ya mimba huharibika katika miezi 3 ya kwanza ya ujauzito. Baada ya miezi hii kupita, uwezekano wa mimba kuharibika hupungua.

Dalili Za Mimba Kuharibika
Karibu asilimia 50 ya mimba zote huharibika hata kabla ya mwanamke kujua kama ni mjamzito, hasa ikisababishwa na matatizo katika vinasaba vya mtoto (congenital chromosomal abnormalities). Kwa mimba zilizoanza kukua dalili za mimba kutoka huwa ni

Kutokwa Damu Kwenye Uke. Damu inaweza kutoka kama matone kwenye nguo za ndani na baadae damu nyingi, au damu nyingi kama ya hedhi.Maumivu ya Tumbo. Mara nyingi hutokea chini ya kitovu. Yanaweza kuwa makali sana.Kutoa tishu, mabonge ya damu na mabaki ya kiini tete.Homa. Unaweza kupata homa kama mji wa uzazi ukipata maambukizi wakti mimba inaharibika.
Sababu Za Mimba Kuharibika
Kuna sababu nyingi zinazosababisha mimba kuharibika zikiwemo;


Matatizo ya maumbile ya mtoto tumboni (genetic abnormalities)Maambukizi ya magonjwa wakati ujauzitoVivimbe vya tumbo la uzazi (uterine fibroids)Kovu kwenye tumbo la uzazi kutokana na kusafisha mimbaShingo ya uzazi kulegeaUgonjwa wa kisukariUgonjwa wa tezi ya shingo (hyperthyroidism)Uchunguzi na Vipimo

Pale unapopata dalili hizi, wahi kituo cha afya haraka. Hii itasaidia kuokoa maisha yamtoto ikiwezekana na yako!

Mtaalamu wa afya atakufanyia uchunguzi wa tumbo na via vya uzazi ikijumuisha kutazama tumbo, uke na shingo ya uzazi kama imefunga au la.

Vipimo ambavyo vinaweza kufanyika ni;

Kipimo cha mkojo cha ujauzito (Urinary Pregnancy Test)Ultrasound ya Tumbo. Huonesha sehemu mimba ilipopandikizwa, hali ya mtoto tumboni na maumbile yake.Vipimo vya damu kupima wingi wa damu huweza kufanyika pia.


Matibabu

Baada ya uchunguzi na vipimo, matibabu hutolewa kutokana na hali ya mimba ilivyo. Mimba inaweza kuwa;


Imeharibika na kutoka (complete abortion)Imeharibika lakini bado ipo kwenye mji wa uzazi (incomplete abortion)Kama mimba imeharibika na kutoka, basi utapewa dawa za kutumia ili kuzuia maambukizi ya vijidudu vya bakteria (antibiotics) na za kuongeza damu hasa kama ulitokwa na damu nyingi.


Kama mimba imeharibika lakini bado haijatoka yote, basi mji wa uzazi utahitaji kusafiswa. Kuna njia mbili ambazo hutumika kusafisha mji wa uzazi nazo ni;

Kuusafisha kwa kuvuta (Manual Vacuum Aspiration)
Njia hii hutumika pale ambapo mimba ina chini ya wiki 12. Kifaa maalumu huingizwa kwenye mji wa mimba na kuvuta uchafu mpaka utakapoisha. Huleta maumivu makali, hivyo unaweza ukapewa dawa ya ganzi au kuzuia maumivu.


Kusafisha mfuko wa uzazi kwa kuuwangua (Dilatation and Curretage)
Njia hii hutumika kama mimba ni kubwa zaidi ya wiki 12. Shingo ya uzazi hutanuliwa na kisha curreter huingizwa ambayo hukwangua mji wa uzazi kuondoa masalia ya mimba au mimba iliyobaki. Njia hii husababisha maumivu makali, utapewa dawa ya usingizi, ganzi au kuondoa maumivu wakati zoezi hili linafanyika.

Baada kusafiswa utapewa dawa za kuzuia maambukizi ya bakteria na dawa za kuongeza damu ikibidi.

Baada Ya Mimba Kutoka
Baada ya mimba kutoka hakikisha unatumia dawa za kuua bakteria (antibiotics) kwa siku 5 mpaka 7.

Zingatia yafuatayo:

Unaweza ukaendelea kupata maumivu kwa siku kadhaa, lakini yatakuwa yanapungua polepole.Damu inaweza ikaendelea kutoka kidogo kwa muda wa wiki mojaUnaweza kuanza kufanya mapenzi baada ya damu kuacha kabisa, kama wiki 2 toka mimba kutoka.


Rudi haraka hospitali ikiwa;
Maumivu ya tumbo kuongezeka kadri siku zinavyoendaDamu nyingi inatoka ukeniUnapata homa



Kupata Ujauzito Tena
Kumbuka unaweza kupata ujauzito wiki 2 baada ya mimba kutoka. Tunashauri kusubiri kwa muda usiopungua miezi 3 kabla ya kupata mimba tena, ili kuruhusu viungo vipone vizuri na kuwa tayari kutunga mimba nyingine.

Wakati huu chagua njia salama ya kuzuia mimba utakayotumia na mwenzi wako. Shauriana na mtaalamu wa afya ili ujue aina ya njia unazoweza kutumia.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Februari 18, Ikiwemo Mnyukano wa Waziri, RC na DC

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Februari 18

Kasi Ya Rais Magufuli Yawagonganisha Waziri Wa Afya na Mkuu wa Wilaya Temeke

$
0
0
Siku mbili baada ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kusema Wilaya ya Temeke inaongoza mkoani Dar es Salaam kwa kuwa na wagonjwa sita wa kipindupindu, Mkuu wa wilaya hiyo (DC), Sophia Mjema amesema hadi jana hakukuwa na mgonjwa hata mmoja.

Baada ya DC huyo kukanusha, jana wizara hiyo ilitoa taarifa ikisisitiza kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na ugonjwa huo.

Kipindupindu ni moja ya vigezo vinne vilivyowekwa na Rais John Magufuli kupima utendaji kazi wa wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kabla ya kufanya uteuzi mpya.

Jumatatu iliyopita akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Waziri Ummy alitoa takwimu za ugonjwa huo na kuitaja Temeke kuwa kinara lakini juzi, Mjema alisema kulikuwa na wagonjwa ambao hawakuwa wamethibitika kama wanaugua kipindupindu.

Jana, Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Temeke, Joyce Msumba alisema juzi kulikuwa na mgonjwa mmoja wa kipindupindu lakini aliruhusiwa baada ya kupona.

“Kwa hiyo leo (jana) Manispaa ya Temeke haina hata mgonjwa mmoja na kambi ni nyeupe haina mtu,” alisema.

Alisema manispaa hiyo inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kanuni za afya ili kujikinga na ugonjwa huo baada ya kufanikiwa kuutokomeza.

“Hatutapumzika tutaendelea kuwakumbusha wananchi kutunza mazingira yao kuwa safi kwa sababu kipindupindu ni hatari,” alisema.

Wakati ofisa hiyo akisema hayo, Waziri Ummy alitoa taarifa akisema Mkoa wa Dar es Salaam kwa siku 10 zilizopita kuanzia Februari 7 hadi 16 kulikuwa na wagonjwa 16; Temeke 12 na Ilala wanne.

Alisema wizara yake ndiyo yenye dhamana ya kusimamia huduma za afya kwa jamii, hivyo wagonjwa hao walikidhi vigezo vya ainisho sanifu na kupata matibabu katika kambi ya kipindupindu kwa wagonjwa wa Temeke na Hospitali ya Amana kwa wagonjwa wa Ilala hivyo kulazimu kutolewa taarifa kwa mujibu wa mwongozo.

Mgogoro wa Kifamilia Walimaliza Kundi la Music la P-Square..Watupiana Madongo Mitandaoni....

$
0
0
Baada ya Peter Okoye kuandika mfululizo wa tweets kueleza kuwa biashara ya familia ni ngumu, kaka yake na pacha wake Paul Okoye ametumia Instagram kueleza kusikitishwa na kitendo hicho.


Awali Peter alidai kuwa wamesimama kufanya kazi na kaka yao, Jude Okoye anayeamini amegeuka kuwa kikwazo kwao. Akipost picha aliyoikata kumuondoa Peter na kubaki na kaka yake Jude, Paul ameandika:

This is where I belong and this is where I stand…….you do music in the studio, not on social media, you have family issues, you discuss that in close doors, not on social media ….. Family is family, blood is blood …. If you don’t do family business, then who am I to you?

Peter hakukaa kimya, amejibu kwa kuandika:

And cutting me off from a picture and replacing me with a studio set says it all my bro. All because you want to sound matured And letting the pple insult and Laff at me. Peter Okoye the social media rant. I wish you well in all you do my bro. God bless our hustle . #voice4thevoiceless.”

Hii si mara ya kwanza kundi hili la Nigeria limeingia kwenye migogoro ya familia. Mwaka na kitu uliopita, Paul na ndugu wengine walidaiwa kutokuwa na maelewano mazuri na mke wa Peter

Barack Obama Asema Donald Trump Hawezi Kuwa Rais wa Marekani

$
0
0
Rais wa Marekani Barack Obama amesema anaamini mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump hatakuwa rais wa Marekani.

Rais Obama ameyasema hayo wakati wa mkutano mkuu wa kiuchumi wa nchi za kusini mashariki mwa Asia unaofanyika katika jimbo la California.

''Ninaendelea kuamini kwamba Bw Trump hatakuwa rais. Na sababu ni kwamba nina imani sana na Wamarekani,” amesema Bw Obama.

Kiongozi huyo amebainisha kuwa Wamarekani hawatampigia kura Bwn Trump kwa kuwa wanajua kazi ya urais ni kazi kubwa si kazi ya kuongea na kuonekana kwenye vyombo vya habari tuu.

Kwa upande wake Bwn Trump amemjibu Rais Obana na kusema kuwa hakuna mtu aliyeharibu nchi kama kipindi chake.

Mwanasiasa huyo anamchukia sana Obama na miaka ya nyuma alizoea kumtaka atoe stakabadhi za kuthibitisha kwamba alizaliwa Marekani.

Chanzo BBC

Mpenzi Mpya wa Nuh Mziwanda Huyu Hapa, Anaishi Oman Amekuja Tanzania Kuanza Rasmi Penzi na Nuhu

$
0
0
Msanii wa bongo fleva Nuh mziwanda ameamua kuweka uhusiano wake mpya hadharani.Kupitia akaunti yake ya instagram Nuh amekuwa akimpost mara kwa mara mrembo anayetumia jina la @_erah_erah_ kwenye mtandao huo

Kupitia mahojiano yake na radio moja Nuh alikiri kuwa huyo ndiye baby number one wake kwa sasa na anaishi Oman na amekuja Tanzania kwa muda tu.

“Ni mpenzi wangu ila aishi hapa amekuja kutembea kwa sababu tulianza ku date tangu yupo nje kwa hiyo amekuja sa hivi tumeanza mapenzi yetu rasmi..yeye anaishi Oman” alifunguka Nuh na kusema kwa sasa hataki kuzungumza mengi anaangalia upepo kwanza.

Dogo Janja Aikana Sauti yake Akimtongoza Msichana na Kuwaponda Tip Top...Madee Amtetea Asema Utoto Unamsumbua...

$
0
0
Rapper Dogo Janja ambaye kwa sasa yuko chini ya uongozi wa Tip Top  ameikana sauti iliyosambaa mitandaoni inayodaiwa kuwa ni yake akiwa anamtongoza msichana na kusikika akiu diss uongozi wa Tip Top kuwa unambania(soma hapa)

Dogo Janja alipoulizwa na kituo kimoja cha redio kuhusiana na sauti hiyo alikataa na kusema hajui chochote kuhusiana na swala hilo mpaka afuatilie.

Hata hivyo Madee alipoulizwa kuhusiana na sauti hiyo akasema ameisikia lakini ameigundua ni mambo ya kitoto ya dogo Janja pengine aonekane ana sauti kwa huyo binti aliyekuwa anamtongoza.

“Nimesikiliza nimeona mambo ya kitototo ndo maana hata sijataka kuhangaika nayo sana,nilichogundua ni kwamba alitaka kujionyesha anaweza kuongea kwa sauti yoyote kwa mwanamke lakini kama Tip Top tutakaa tutajua nini cha kumwambia” alifunguka Madee na kuweka wazi kuwa ngoma mpya ya dogo Janja itatoka mwisho wa mwezi huu.

Team Kiba Acheni Majungu, Msapotini Kiba..Lupela Imepitwa Hata na Shika Adabu yako ya Nay wa Mitego

$
0
0
Kama ulikua hujui nakujuza nyimbo ya Shika adabu yako ya @naytrueboy imeikimbiza vibaya kwa kudownlodiwa mkito nyimbo ,mpka sasa ina zaid ya downloads 12,000 + wakat Lupela ya @officialalikiba ina 7,000 + tu!!! ingawaje lupela ilianza kutoka kabla yanyimbo ya Nay. Eti mashabiki ni halali kumfananisha Kiba na Diamond kwa mwendo huu wa kukalishwa na mzee wa Shika Adabu yako ney wa Mitego!!! Mashabiki msiishie kucomment insta muwe mnadownload pia nyimbo za wasanii wenu,hii ni aibu kabisaa kwani team kiba mnatukana kuliko kumsapoti mtu wenu kiba,wenzenu team Diamond, wanatukana na wana msupport mtu wao.. !! Nacho washauri tukaneno sana na msapotini kuliko kumtia aibu namna hii, Oneni sasa Ney anamzid taratibuuuu...

By Msaga sumu (Jamii Forums)

‘Jogoo wa Ommy Dimpoz’ Anawika,Ex Wake Athibitisha...Asema Nay wa Mitego Anatafuta Kiki.

$
0
0
Baada ya diss ya Nay wa Mitego kuwa “jogoo wa Ommy Dimpoz hawiki” yaani jamaa “hapigi mechi”,mpenzi wa zamani wa Ommy Dimpoz amejitokeza hadharani na kukanusha tuhuma hizo ambazo Nay wa Mitego alimminia Ommy Dimpoz kupitia wimbo wake wa Shika adabu yako.

Mwanadada huyo ambaye picha yake akiwa na Ommy Dimpoz ilizagaa huku wakiwa wamevalia sare za shule ameweka wazi kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Ommy dimpoz na kuthibitisha kuwa Dimpoz alikuwa “akipiga mechi” kama kawa.

“Ni mzima kabisa,i don’t know huyu Nay anatafuta tu kiki..” alifunguka mrembo huyo ambaye kwa sasa anasema yuko kwenye mahusiano mengine.

Afukuzwa CCM Kwa Kumfanyia Kampeni Edward Lowassa

$
0
0
Halmashauri ya CCM Mkoa wa Geita imemvua ujumbe wa Mkutano Mkuu, Peter Mwininga baada ya kudaiwa kukiuka maadili ya Umoja wa Vijana (UVCCM).

Licha ya kukiuka maadili ya umoja huo, Mwininga anadaiwa kukisaliti chama hicho wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita kwa kuwatukana viongozi wa ngazi za juu kwa njia ya mtandao.

Akizungumza baada ya kikao hicho juzi, Katibu wa Siasa na Uenezi CCM mkoani hapa, Said Kalidushi alisema baada ya wajumbe wa halmashauri kuu kupokea malalamiko na mapendekezo kutoka UVCCM, waliamua kumvua nafasi ya ujumbe huo kutokana na kupungukiwa na sifa.

Kalidushi alisema wakati wa kampeni Mwininga alikihujumu chama chao na kumfanyia kampeni mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, huku akijua wazi kuwa ni kosa.

Katibu wa UVCCM mkoani hapa, Mashaka Mshola alisema kitendo cha Mwininga kuvuliwa nafasi aliyokuwa nayo kinatokana na usaliti na huo ni mwanzo wa chama hicho kuwafukuza wasaliti.

Nay wa Mitego Ampa Pole Wema Sepetu Kwa Kupoteza Ujauzito Kama ilikuwa ni Mimba Kweli....

$
0
0
Msanii wa muziki wa Hip Hop Nay wa Mitego amesema hakupenda ujauzito wa Wema Sepetu uharibike kama baadhi ya mashabiki wa Wema Sepetu wanavyodai katika mitandao ya kijamii.
nay new2

Rapa huyo kupitia wimbo wake “Shika Adabu Yako’ alimchana Wema ‘una mimba kweli, au ndio kiki za msimu?. Miezi tisa sio mingi, isije ikakugharimu” kauli ambayo ilitafsiriwa vibaya na mashabiki wa Wema.

Akizungumza katika kipindi cha Ubaoni cha EFM Jumatano hii, Nay alisema yeye hawezi mwombea mabaya Wema kwa kuwa anapenda sana watoto.

“Sijapenda ujauzito wa Wema uharibike kwani napenda watoto. Kama ilikuwa mimba kweli nampa pole sana dada yangu ila kama ilikuwa kiki imefika mwisho Kwani nilichoongea kwenye wimbo ilikuwa ni swali Je? Una mimba kweli au drama.,”alisema Nay.

Idris Amkingia Kifua Wema Sepetu, ni Baada ya Kuambiwa Anamharibu..Otoa Onyo Kali

$
0
0

Ukitaka kukosana na Idris Sultan, mtukane kipenzi chake, Wema Sepetu.

Mshindi huyo wa shindano la Big Brother Africa mwaka 2014 aligeuka mbogo baada ya shabiki mmoja kudai kuwa Wema anampoteza.

Soma mwenyewe:

Matokeo Kidato Cha Nne: Shule 10 Bora Kitaifa na Shule 10 za Mwisho Kitaifa Ziko Hapa......Aliyeongoza Kitaifa Ni Msichana

$
0
0
Baraza la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2015 yanayoonesha kiwango cha ufaulu kushuka kwa asilimia 0.80.

Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde amesema kuwa jumla watahiniwa 272,947 sawa na 67.53% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2015 wamefaulu tofauti na mwaka 2014 ambapo ufaulu ulikuwa 68.33%.

Msonde amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, waliofaulu ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 11,125 (64.84) na wavulana wakiwa 124,871 (71.09).

Amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, ufaulu umeshuka kwa asilimia 1.85 ikilinganishwa na mwaka 2014.

Aidha kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, Dkt Msonde amesema watahiniwa 31,951 sawa na asilimia 64.80 wamefaulu ikilinganishwa na watahiniwa 29,162 (61.12) waliofaulu mwaka 2014.

Kwa upade wa ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule, Msonde amesema waliopata daraja la kwanza ni 9,816 sawa na asilimia 2.77, daraja la pili ni 31,986 sawa na asilimia 9.01, daraja la tatu ni 48,127 sawa na asilimia 13.56.

Aidha waliopata daraja la nne ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 na waliopata daraja la sifuri (waliofeli) ni 113,489 sawa na asilimia 32.09.

Watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa kati ya daraja la kwanza hadi la tatu ni 94,941 sawa na asilimia 24.73 wavulana wakiwa 56,603 sawa na 29.99 na wasichana 38,338 sawa na asilimia 19.63.

Amesema kwa upande wa ufaulu wa masomo kwa watahiniwa wa shule, ufaulu wa juu kabisa ni wa somo la Kiswahili ambapo asilimia 77.63 wamefaulu huku ufaulu wa chini kabisa ukiwa ni wa somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 16.76 wamefaulu.

Baraza hilo limezuia matokeo ya watahiniwa 121 kutokana na sababu za kiafya na watahiniwa hao wataruhusiwa kufanya mitihani ambayo hawakuifanya katika mtihani wa kidato cha nne, mwaka 2016.

Aidha baraza hilo limefuta matokeo ya watahiniwa 87 waliobainika kufanya udanganyifu katika mtihani ambapo kati yao 25 ni wa kujitengemea na 52 ni watahiniwa wa shule wakati 10 ni wa mtihani wa maarifa (QT)

Amezitaja shule 10 zenye watahiniwa zaidi ya 40 zilizofanya vizuri zaidi kuwa ni Kaizerege ya mkoani Kagera, Alliance Girls ya Mwanza, St. Francis Girls ya Mbeya, Canossa ya Dar es salaam, Marian Boys ya Pwani, Alliance Rock Army ya Mwanza, Feza Girls Dar es salaam, Feza Boys ya Dar es salaam na Uru Seminary ya Kilimanjaro.

Shule 10 zilizofanya vibaya zaidi kwa watainiwa zaidi ya 40 ni pamoja na Pande ya mkoani Lindi, Igawa ya Morogoro, Korona ya Arusha, Sofi ya Morogoro, Kurui ya mkoani Pwani, Patema ya Tanga, Saviak ya Dar es salaam, Gubali ya Dodoma, Kichangani ya Morogoro na Malinyi ya Morogoro.

Kwa upande wa watahiniwa, Dkt Msonde amesema kati ya watahiniwa 10 waliofanya vizuri zaidi, wanne na wasichana na sita ni wavulana.

Mwanafunzi aliyeongoza ni msichana Butogwa Charles Shija wa Canossa, akifuatiwa na msichana mwingine Congcong Wang wa Feza Girls na wa tatu ni mvulana Innocent Lawrence wa Feza Boys.

Wengine ni Dominick Marco Aidano wa Msolwa, Sang'udi E Sang'udi wa Ilboru, Asteria Herbert Chilambo waCanossa, Belinda Jackson Magere wa Canossa, Humfrey Martine Kimanya wa Msolwa, Bright B Mwang'onda wa Marian Boys na wa 10 ni Erick R Mwang'ingo wa Marian Boys.

Matokeo hayo yamepangwa katika mfumo wa madaraja (Division) badala ya ule wa wasatani wa alama (GPA) kama ambavyo iliagizwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi hivi karibuni

Picha: Ray Baada ya Kudai Siri ya weupe wake ni Kunywa Maji, Watu Mbali Mbali Waanza Kampeni...

$
0
0
Baada ya Ray Kigosi kuweka wazi kuwa anakunywa sana maji ndio maana anakuwa mweupe, Godzilla pamoja na mashabiki mbalimbali katika mitandao ya kijamii wamenza kufanya zoezi hilo kwa kuwahamasisha watu kunywa maji ili na wao wapate upako huo.

Hivi karibuni Ray Kigosi kupitia kipindi cha Enewz cha East Africa Television alidai kuwa weupe wake una sababishwa na kunywa maji ya kutosha pamoja na kufanya mazoezi.

Idris Sultan Ajipoza kwa Lulu Michael..Amebambwa Kiwanjani

$
0
0
Siku chache baada ya taarifa za kutoka kwa mimba ya mwandani wake, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, Mshindi wa Shindano la Big Brother Africa ‘Hotshot’ 2014, Idris Sultan amebambwa kiwanja akijipoza machungu na staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Amani limenasa tukio.

Tukio hilo lililopigwa chabo na paparazi wetu lilijiri wikiendi iliyopita ndani ya Ukumbi wa Sky-Night Life uliopo Masaki jijini Dar ambapo wawili hao walikuwa wakijiachia wakati wa shoo ya Love Posion iliyokuwa imeandaliwa mahususi kwa msanii wa Bongo Fleva, Abednego Damian ‘Belle 9’ katika kukamilisha shamrashamra za Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day).

Wakiwa ndani ya ‘kiota’ hicho wakila bata, wawili hao walibambwa uso kwa uso na kamera yetu ambapo mwanzo walijifanya hawafahamiani huku Idris akisimama kando ya sehemu aliyokuwepo Lulu na ndugu zake.
Mambo yalianza kubadilika baada ya Belle 9 kupanda jukwaani ambapo Idris ambaye inasemekana alilia kama mtoto baada ya kusikia mimba ya Wema imetoka, alishuhudiwa akimsogelea Lulu aliyekuwa meza moja na mwigizaji Rose Peter ‘Muna’ na Mtangazaji wa CloudsTV, Casto Dickson.

Baada ya kumsogelea, Idris alimsalimia Muna kisha akamkumbatia Lulu kwa takriban dakika mbili na kuanzia hapo ndipo mambo yakawa ‘shatashata’ huku wakipiga stori ndipo kamera yetu ikawageukia na kuanza ‘kuwafotoa’ hatua kwa hatua.

Akiwa ameketi ‘veri klozi’ na Lulu, Idris alionekana kuwa mwenye tabasamu ‘baab’kubwa’ ambapo wakati wote vilisikika vicheko, ikiwemo kunong’onezana mara kadhaa, jambo lililosababisha baadhi ya wadau kuhojiana kama Idris amehamishia majeshi kwa Lulu au la.

“Ebwana eeh, ujue mimi kama sijaelewa uwepo wa Lulu na Idris hasa kinachonifanya kushangaa ni namna ambavyo wawili hawa wanaongea tena kwa kunon-g’onezana wakati kama maongezi yao yasingekuwa na tatizo si wangeongea tu kama walivyokuwa wakisalimiana kwa sauti na wenzao wakawa wanasikia?” alihoji mmoja wa wadau hao.
Baadaye Idris alionekana akijipenyeza kuondoka ukumbini hapo ambapo dakika chache Lulu naye alimfuata akiwa na wenzake.

Hata hivyo, kila mmoja alipoulizwa kulikoni kama kuna kinachoendelea kati yao, hawakutoa ushirikiano huku nyumbani kwa Wema, Ununio, Tegeta jijini Dar, kukidaiwa kuwa kama kuna msiba kufuatia tukio la kutoka kwa mimba ambalo bado ni gumzo.

Chanzo:GPL

Wema Sepetu Alitamani Ajifungua Mtoto wa Kiume

$
0
0
Usiku wa kuamkia leo, Idris Sultan ameandika waraka mrefu kuhusiana na ujauzito wa mpenzi wake, Wema Sepetu ambao kwa post ile amemaanisha haupo tena (umetoka), lakini siku chache zilizopita wakati akiwa na mimba alitamani sana ajifungue mtoto wa kiume kwa kuwa kwenye familia yao wamezaliwa wote wanawake.

”Yaani huwezi amini kabla sijashika mimba nilikuwa na majina mengi sana ya watoto, lakini sasa hivi ninayo nimejikuta majina yote yamepotea labda mtoto wangu akifikisha miezi saba nitaanza kugoogle nipate jina lenye maana nzuri kwa mtoto wangu wa kiume, “Wema Sepetu.

” Unajua sisi katika familia yetu upande wa mama tumezaliwa watoto wote wa kike, mama yangu amekuwa akitamani sana mtoto wa kiume, kwahiyo nikipata mtoto wa kiume nitafurahi zaidi, “Wema.

Cloudsfm.com

‘Don’t Kill Innocent Babies in Your Own Fake Movie’ Zari Hassan Pounces At Wema Sepetu Following Her Miscarriage

$
0
0

Zari Hassan seems to be taking the phrase ‘all is fair in love and war’ too far in her latest attack on Wema Sepetu.

Zari savagely mocks Wema Sepetu by asking whether she still wants Tiffah’s DNA test after her ‘miscarriage’. Before accusing Wema of killing innocent babies in her fake movie, suggesting that Wema Sepetu had faked her pregnancy.

She then goes on to accuse Wema of being on another level of craziness by writing ‘Gaarl! You are something else.’ Before going on to add ‘No throwing shade, just stating facts.’



KANUSHO: Mwenyekiti wa CHADEMA, Freman Mbowe Kuchukua 'Zabuni Zote' Hai

$
0
0
Kuna taarifa zisizokuwa na chembe ya ukweli ambazo zimezushwa na kusambazwa mitandaoni, ikiwa na pamoja na jukwaa hili zikijaribu kumhusisha Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe kuwa amechukua zabuni zote katika Wilaya ya Hai.

Wanaosambaza uongo huo, wamesema kuwa Mwenyekiti Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, amefanya hivyo kwa ubabe.

Ni vyema tukaweka ukweli kuhusu uzushi huo ambao umeanza kuwasumbua wanachama, wapenzi, mashabiki na wapenda mabadiliko kwa ujumla, kuwa Mwenyekiti Mbowe hana zabuni yoyote katika Wilaya ya Hai wala hajawahi na hana zabuni katika wilaya yoyote nyingine katika maisha yake yote ya uongozi na utumishi anaowajibika kwa umma.

Halmashauri ya Wilaya ya Hai kama yalivyo maeneo mengine ya halmashauri, manispaa na majiji ambayo yako chini ya uongozi wa Chadema na UKAWA kwa ujumla inajiandaa kuwa mojawapo ya maeneo ya kupigiwa mfano kwa mabadiliko yatakayofanyika kutokana na kusimamia uwajibikaji utakaotanguliza uadilifu mbele wenye dira ya maendeleo kwa ajili ya wananchi.

Hai ni halmashauri ambayo tayari imeweka rekodi kadhaa, kwanza inaongozwa na CHADEMA kwa 'full majority' kwa maana ya madiwani wanaounda baraza ambalo liko chini ya Mwenyekiti wa Halmashauri mwanamke ikiwa ni mara ya kwanza.

Makene
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live




Latest Images