Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live

January Makamba: Bila Magufuli CCM ilikuwa Imekataliwa na Wananchi Uchaguzi 2015

0
0
Akiongea na kituo cha Taifa cha Utangazaji(TBC),Mbunge wa Bumbuli na Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano,Ndugu January Makamba,amesema katika uchaguzi wa mwaka 2015 CCM ilikuwa inaondoka madarakani kwa nguvu ya wananchi,lkn kwa uchaguzi wao wa kumchagua ndugu JPM kidogo imani ya wananchi ikarudi kwa Chama Cha Mapinduzi.

Makamba Jnr anasema CCM ilipoteza imani na kutoaminiwa na wananchi kwa kiasi kikubwa sana kiasi cha wao kuona dalili la wazi la kuanguka kwa CCM.Anasema uchaguzi wa 2015 ulikuwa ni moja ya chaguzi ngumu kuwahi kutokea na wana imani kwa utendaji huu wa JPM wananchi watarudisha imani kwa CCM na Serikali yake na kuepuka kuwaadhibu ktk sanduku la kura mwaka 2020.

Matokeo Ya Mtihani Kidato Cha Nne -2015 Yametoka....Yatazame Hapa

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa Ya Februari 19, Ikiwemo ya Magufuli Kusema kuna Majipu yanahitaji Tiba Mbadala

0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa Ya Februari 19


Dallas wa Jack Wolper Afunga Ndoa...

0
0
ALIYEKUWA mchumba wa staa wa Bongo Muvi, Jacqueline Wolper, Ramadhan Mtoro ‘Dallas’ inadaiwa kuwa hivi karibuni amefunga ndoa na mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Suleiya, Amani lina mchongo kamili.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita maeneo ya Mbezi-Ununio jijini Dar ambapo wawili hao walionekana wakiwa katika hali ya furaha muda wote huku ndoa hiyo ikifungwa bila kificho.

“Hatimaye leo yamekuwa, yaani yule jamaa (Dallas) aliyekuwa akimpatia Wolper magari ya kifahari na mipesa leo hii saa saba mchana (Jumapili) anafunga ndoa tena na mwanamke mwingine mkali kuliko hata huyo Wolper,” kilisema chanzo.

Baada ya kuunyaka ubuyu huo, Amani lilifanikiwa kutimba eneo la tukio na kushuhudia Dallas akifunga ndoa kweli na mwanamke huyo ambapo baadaye waliingia moja kwa moja kwenye gari na kutokomea.

Miaka mitatu iliyopita Dallas alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Wolper hadi kufikia hatua bi’dada huyo kubadili dini ili aolewe naye lakini mwishowe uhusiano huo uliyeyuka.

Embu Tuweke Ushabiki Pembeni, Couple Gani Kati ya Hizi Unaipenda Kutoka Moyoni?

0
0
Embu tuweke ushabiki pembeni, Couple gani kati ya hizi unaipenda kutoka moyoni?

Varangati: Mbunge Msigwa na Mkuu wa Wilaya Kasesera Nusura Ngumi Zichapwe Kavu Kavu

0
0
Kumetokea mabishano makali sana kati ya Mbunge Msigwa na DC Kasesera eneo la Iringa Mjini baada kuwa wamewatembelea wahanga wa nyumba zilizoezuliwa na mvua kubwa na kusababisha baadhi ya watu ktk Tarafa ya Nduli

Vurumai hizo zilizotokea baada ya Msigwa kukasirishwa na kitengo cha DC kutaka kumuengua ili asionekane anatoa msaada kwa watu wa jimbo lake bali DC ndio ionekane anajali wananchi.Shutuma zilienda mbali baada ya Msigwa kumueleza DC kuwa anajuwa anamhujumu na amekuwa anapanga mikakati ya siri ya kumfanyia hujuma ili aonekane hafanyi kazi jimboni kwake.

Juhudi hizo zimefanyika week iliyopita ambapo DC kwa kushirikiana na Humphley Polepole waliandaa "mdahalo" na wanafunzi wa vyu vikuu mkoani Iringa na kuanza kumsema vibaya Mbunge Msigwa,katika mdahalo huo Polepole amerekodiwa akisema Iringa awalikosea sana kumchagua Msigwa sbb alikuwa anamuunga mkono "fisadi" Lowassa

Wakati DC Kasesera alimshutumu Mb Msigwa kutokwenda Tarafa ya Pawaga kusaidia wahanga wa mafuriko na Msigwa akamjibu kuwa aanze kumwambia Lukuvi kwanini hajaenda maana Tarafa ya Pawaga ipo ndani ya Jimbo la Isimani,na hata yeye akienda sio lazima DC ajue,kama ambavyo yeye anaenda na kupiga picha na kurusha Facebook akimbeba mpiga picha ambaye haitaji msaada wa kubebwa.

Vurugu hizo ziliamuliwa na diwani na Meya wa Mji. Mwishoni Msigwa akamwambia DC awaite polisi wamuweke ndani maana katika viako vya CCM DC Kasesera amekuwa akisema lazima amuweke ndani Msigwa kumtia adabu

Angalia Video Hapa:


Hii ndoo njia sahihi ya Ku deal na hawa wasio tambua majukumu yao wakuu wa wilaya walio pewa izo nafasi kwa kuwafunga kamba za vitu watawala. Safi sana Peter Msigwa kwa kuvunja ukimya Ila ulimkosea unge maliza nabvibao.Ccm Tumainiel W Seria, elnanyaro
Posted by Sadru Samanta on Thursday, February 18, 2016

Mama Apewa Mimba na Mtoto wake wa Kumzaa..Adai Wako Katika Mapenzi Mazito na Wameamua Kuoana

0
0
Mama wa miaka 40, Betty Mbereko wa huko nchini Zimbabwe anataka aoelewe na mtoto wake wa kiume Farai Mbereko (23). Imeelezwa kuwa wawili hao wako kwenye mapenzi makali na hivyo kuamua kuupeleka uhusiano wao kwenye level nyingine ya ndoa huku tayari mama huyo akiwa na ujauzito wa miezi sita aliopewa na mwanae.

Embu tuambie, unadhani dunia inaelekea wapi?

Huyu Hapa Ndio Mwanafunzi Mchina Aliyeshika Nafasi ya Pili Matokea ya Kidato cha Nne Yaliyotoka Jana

0
0
Mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne Feza Girls 2015 , Mtanzania mwenye asili ya China, Congcong Wang,ameshika Nafasi ya pili Kitaifa ,amepata Divisheni 1.7 yenye 'B' ya Kiswahili!

Nini maoni yako?


A.Y Afunguka Kuhusu Mpango Wake wa Ndoa, Asema Bado Yupo Sana...Kwanini..?

0
0
Rapper mkongwe kwenye tasnia ya muziki nchini Tanzania, A.Y amefunguka na kusema kuwa bado hajapata msukumo wowote wa kuoa toka nafsini mwake.

Rapper huyo aliyasema hayo kwenye mahojiano yake na kituo kimoja cha Tv na kuongeza kuwa ndoa ni wito,ukimwita ataitika

“Ndoa ni wito kuna sauti huwa inakwambia kabisa huu ndio muda wako,sauti hiyo kila nikiiita nasikia mwangwi tu” alisema A.Y na kutania kuwa mpaka swahiba wake Mwana Fa aoe kwanza maana yeye ndio mkubwa

Kambi ya Upinzani bungeni Yaendelea Kumgomea Spika Ndugai

0
0
Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Tundu Lissu amesema kambi hiyo haitaongoza kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (Laac) hadi ofisi ya Spika itakapobadilisha uteuzi wa wajumbe wa kamati hizo.

Kwa mujibu wa mabunge ya Jumuiya za Madola, kamati hizo huongozwa na wapinzani, lakini tangu Spika wa Bunge, Job Ndugai afanye uteuzi wa wajumbe, kambi hiyo imesusia kushiriki uchaguzi kwa kile wanachokiita “kupangiwa wajumbe”.

Jana, Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alisema mazungumzo kati ya ofisi ya spika na kambi hiyo bado yanaendelea na kusisitiza kwamba uteuzi huo unaweza kutenguliwa au kuachwa kama ulivyo.

Katika maelezo yake, Lissu alisema licha ya kambi hiyo kuwa katika mazungumzo na ofisi ya spika, suluhisho halijapatikana na kusisitiza kuwa msimamo wao upo palepale.

“Hatujafika popote. Msimamo wetu uko palepale na hatutakubali kuchaguliwa viongozi wa hizo kamati na CCM, kama wanafikiria ni lazima iwe wanavyotaka sisi hatutakubali,” alisema.

Joel aliwahi kunukuliwa na na vyombo vya habari  akisema kuwa kama kambi hiyo itasusia uchaguzi, shughuli za kamati zitafanywa na makamu wenyeviti ambao wanatokea CCM.

“Ni bora tusiziongoze kabisa kamati hizi. Ukifuatilia utabaini kuwa katika PAC na Laac tuna wajumbe sita kila kamati kati ya wajumbe 23, wakati huohuo kamati ya Ukimwi tumepewa wajumbe 12 kati ya wote 23,” alisema Lissu.

Alisema wajumbe sita waliopo katika kamati ya Laac na PAC wameteuliwa na CCM na kama kamati hizo zinaongozwa na upinzani ni lazima wapinzani wajichagulie wajumbe wao, wakiwamo watakaochaguliwa kuwa wenyeviti. Alisema wabunge wana haki sawa, lakini hawana uwezo sawa.

Lissu ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alisema uamuzi wa spika kuwapangia wajumbe katika kamati hizo hauna nia nzuri na kwamba, huenda ni mkakati wa ofisi hiyo kuifanya Serikali iwe inapitisha mambo yasiyofaa bungeni.

Februari Mosi mwaka huu, Kambi ya Upinzani bungeni ilisusia uchaguzi wa viongozi wa kamati hizo kwa maelezo kuwa Spika Ndugai alifanya uteuzi ‘kiholela’ na kuahidi kutoshiriki mpaka pale watakapopewa idhini ya kupendekeza wenyeviti.

Jeshi la Kenya lamuua kamanda wa al-Shabab

0
0

Jeshi la Kenya KDF limethibitisha kuwa limemuua kiongozi wa al-shabab anayesimamia intelijensia ya kundi hilo Mohammed Karatey pamoja na makamanda wengine 10.

KDF limesema kuwa liliwaua wapiganaji hao katika shambulio kubwa mnmo mnamo tarehe 8 mwezi Februari.

Kulingana na taarifa iliotumwa kwa vyombo vya habari na wizara ya Ulinzi nchini Kenya,wapiganaji hao waliuawa katika kambi ya Nadaris kati ya Buale na Sukow.

 Inadaiwa kuwa Karatey alikuwa amezuru kambi hiyo kwa hafla ya kufuzu kwa takriban wapiganaji 80 wapya wa alamnyat waliokuwa katika mafunzo ya kijeshi.Inadaiwa kuwa wapiganaji 42 waliuawa huku wengine wengi wakipata majeraha.

Kitengo cha alamnyat ndicho chenye wapiganaji wa kujitolea muhanga,wataalamu wa vilipuzi na watafutaji habari hivyobasi mauji ya kamanda huyo ni pigo kubwa wa alshabab.

Peter wa P Square Aomba Radhi kwa Kuweka Mgogoro wa Kifamilia Mtandaoni?

0
0

Msanii peter ambaye anaunda kundi la P Square, ameomba radhi kwa kitendo chake alichokifanya, ingawa hajaweka bayana analenga lipi katika aliyoyafanya kwenye kundi lake abalo ni la familia, na jamii kiujumla.

Kwenye ukurasa wake wa twitter Peter ameomba msamaha huo akiandika maneno haya..... "I am not perfect i make mistakes, and it hurts people. But when I say sorry I mean it. I am so SORRY for my actions. I sincerely apologize", aliandika Peter akimaanisha kwamba (Mimi siko sahihi nafanya makosa, na inawaumiza watu, lakini ninaposema samahani namaanisha, samahani sana kwa vitendo vyangu, naomba msamaha huu kwa dhati).

Hapo jana kuliiibuka mzozo mkubwa kati ya kundi hilo ambapo Peter akitaka kaka yao Jude ambaye ndio kiongozi wao atoke kwenye kundi na kuwaacha yeye na Paul, kitendo ambacho pacha wake Paul alikijia juu na kumwambia kama ni matatizo ya familia ni ya kuzungumza nyumbani, na sio kwenye mitandao.

TCU Yafuta Vyuo Vishiriki Vya Mtakatifu Joseph.....Wanafunzi Watakiwa Kuondoka Chuoni Mara Moja, Watapangiwa Vyuo Vingine

0
0
KUFUTWA KWA KIBALI KILICHOANZISHA VYUO VIKUU VISHIRIKI VYA SAYANSI ZA KILIMO NA TEKNOLOJIA (SJUCAST) NA TEKNOLOJIA YA HABARI (SJUCIT) VYA CHUO KIKUU CHA MT. YOSEFU TANZANIA (SJUIT), KAMPASI YA SONGEA

1.  Tunapenda kuuarifu umma kwamba, Chuo Kikuu cha Mt. Yosefu Tanzania (SJUIT) ni mojawapo ya vyuo vikuu vilivyosajiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). Chuo hiki kinamilikiwa na Shirika la Kitawa la Dada wa Maria Imakulata (DMI) pamoja na washirika wao. Hapa nchini chuo hiki kilianzishwa mwaka 2003 chini ya usajili wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE). Mnamo mwaka 2011, chuo hiki kiliwasilisha maombi ya kusajiliwa na TCU. Maombi hayo yaliidhinishwa na Tume tarehe 14 Desemba, 2011. Kisha tarehe 27 Septemba, 2012 kufuatia maombi ya uongozi wa Chuo, Tume iliidhinisha kuanzishwa kwa Vyuo Vikuu Vishiriki vitatu ambavyo ni: Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi za Kilimo na Teknolojia (St. Joseph University College of Agricultural Science and Technology - SJUCAST), na Chuo Kikuu Kishiriki cha Teknolojia ya Habari (St. Joseph University College of Information Technology - SJUCIT) ambavyo vilianzishwa Songea; na Chuo Kikuu Kishiriki cha Uongozi, Uhasibu na Fedha (St. Joseph College of Management, Accounting and Finance - SJUCMAF) kilichopo Makambako, Njombe. Hivi sasa Chuo Kikuu hiki kina Kampasi nyingine Arusha, Boko na Luguruni, Dar es Salaam, huku Makao Makuu yakiwa katika Kampasi ya Luguruni.

2. Kwa mujibu wa kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Vyuo Vikuu, Sura ya 346 ya Sheria za Tanzania, Tume ina mamlaka ya kusimamia na kudhibiti ubora na usimamizi wa uendeshaji wa Vyuo Vikuu hapa nchini.

3. Kwa muda mrefu katika Vyuo Vikuu Vishiriki vya Sayansi za Kilimo na Teknolojia (SJUCAST) na Teknolojia ya Habari (SJUCIT) kumekuwapo na mlolongo wa matatizo ya ubora, uongozi, ukiukwaji wa sheria na taratibu za uendeshaji wa chuo kikuu kama zilivyobainishwa na Sheria ya Vyuo Vikuu. Jitihada za Tume ya Vyuo Vikuu kukitaka Chuo Kikuu cha Mt. Yosefu Tanzania (SJUIT) kuhakikisha hivi Vyuo Vikuu Vishiriki vinatoa elimu inayokidhi viwango vya ubora vilivyowekwa na Tume hazikupewa uzito stahiki na uongozi wa chuo. Matokeo yake wanafunzi wa SJUCAST na SJUCIT wamekuwa hawapati elimu kwa kiwango stahiki. Hivi sasa katika vyuo hivi vishiriki viwili kuna jumla ya wanafunzi 2046 wanaosoma programu za digrii zifuatazo:
a)Bachelor of Technology in Agriculture [B. Tech. in Agriculture](wanafunzi 282)
b)Bachelor of Technology in Horticulture [B. Tech. in Horticulture](wanafunzi 61)
c)Bachelor of Technology in Agricultural Engineering [B. Tech. in Agric. Eng.]
(wanafunzi 255)
d)Bachelor of Technology in Food Process Engineering [B. Tech. in FPE.]
(wanafunzi 238)
e)Bachelor of Science with Education (wanafunzi 732)
f)Bachelor of Science in Computer Science (wanafunzi 250)
g)Bachelor of Computer Science with Education and Bachelor of Science in
Education with Computer Science (wanafunzi 196)
h)Diploma in Computer Science (wanafunzi 81) 
 
4.Kutokana na yaliyobainishwa hapo awali, tunapenda kuuarifu umma kwamba, Tume imejiridhisha kuwa hivi Vyuo Vikuu Vishiriki viwili havitoi elimu ya chuo kikuu ya viwango stahiki. Kwa kuzingatia ukweli kwamba wanafunzi katika vyuo hivi vishiriki vya SJUCAST na SJUCIT ndio waathirika wakuu wa matatizo yaliyopo kwenye vyuo hivi, Tume imeamua kufuta kibali kilichoanzisha hivi vyuo vikuu vishiriki viwili yaani: St. Joseph University College of Agricultural Science and Technology (SJUCAST) na St. Joseph University College of Information Technology (SJUCIT); na kuidhinisha uhamisho wa wanafunzi wote waliokuwa wanasoma katika vyuo hivyo kwa gharama za Chuo Kikuu cha SJUIT. 
 
  Uhamisho huo pia unahusu wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wa pili wanaosoma digrii za Bachelor of Technology in Agricultural Engineering [B. Tech. in Agric. Eng.] na Bachelor of Technology in Food Process Engineering [B. Tech. in FPE.] ambao hivi sasa wanasoma katika Kampasi ya Luguruni, Dar es Salaam. 
 
5.    Kufuatia uamuzi huu, wanafunzi wote wanaosoma katika Vyuo Vikuu vishiriki vya SJUCAST na SJUCIT wanaarifiwa kuwa watahamishiwa kwenye vyuo vikuu vingine vinavyofundisha programu za masomo zinazofanana na masomo wanayosoma hivi sasa chini ya utaratibu na masharti yafuatayo:
i) Wanafunzi wote wanapaswa kuondoka chuoni mara moja baada ya kukamilisha taratibu za kukabidhi mali na vifaa vingine vya chuo kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.
ii)Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti kwenye vyuo watavyopangiwa wakati wa kufunguliwa kwa muhula (semester) wa pili. Tarehe halisi ya kuanza kwa muhula wa pili kwa kila chuo watakachopangiwa itatangazwa na kuwekwa kwenye tovuti ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania.
iii)Wanafunzi wote wanaosoma digrii ya sayansi za kilimo na uhandisi(programmes related to agricultural sciences and engineering)watahamishiwa katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).
iv)Wanafunzi wanaosoma digrii ya ualimu wa sayansi watahamishiwa katika mojawapo ya vyuo vikuu vifutavyo: Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
(SUA); Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM); na Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Mwenge (MWECAU).
v)Wanafunzi wote wanaosoma digrii na diploma ya sayansi ya kompyuta watahamishiwa katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA). vi) Wanafunzi wote wanaosoma digrii ya ualimu na sayansi ya kompyuta watahamishiwa katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha (RUCU).
vii)Orodha ya wanafunzi waliohamishwa na majina ya vyuo vikuu walivyohamishiwa itatangazwa na kuwekwa kwenye tovuti ya Tume ya Vyuo Vikuu hivi punde.
viii)Wanafunzi wote waliohamishwa ambao hawakukamilisha mitihani yao ya mwisho wa muhula wa kwanza, au hawakufanya kabisa mitihani hiyo, watatakiwa kufanya mitihani hiyo katika vyuo vikuu watavyohamishiwa kwa utaratibu maalum utakaondaliwa na chuo husika.
ix)Kila mwanafunzi anawajibika kutunza kumbukumbu zake zote muhimu za maendeleo ya kitaaluma kwa ajili ya matumizi ya baadaye, ikiwa ni pamoja na matokeo ya mitihani aliyokwishafanya.
x)Wanafunzi wote ambao ni wanufaika wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, mikopo yao itahamishiwa katika vyuo wakapokuwa wamehamishiwa.
6.Kampasi nyingine za Chuo Kikuu cha SJUIT zinaendelea na masomo kama kawaida.
7.Kwa taarifa hii, vyuo vikuu vyote nchini vinakumbushwa kufuata sheria na kuzingatia utoaji wa elimu inayokidhi viwango vya ubora vinavyokubalika kitaifa na kimataifa. Tume haitasita kuchukua hatua stahiki kwa chuo kikuu chochote kitakachobainika kutoa elimu isiyokidhi viwango vya ubora kwa kisingizio cha aina yoyote. 
 
Imetolewa na 

PROF. YUNUS D. MGAYA
Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
19 Februari 2016

Waziri Nape Nnauye Atengua Uteuzi Wa Katibu Mtendaji Baraza La Michezo Tanzania ( BMT )

0
0
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ametengua uteuzi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania Henry Lihaya baada ya kushindwa kutekeleza wajibu wake.

Mhe. Nnauye ametengua uteuzi huo katika ziara yake aliyoifanya leo mapema katika ofisi za BMT kuona miundo mbinu ya ofisi hizo na kujua changamoto walizonazo.

“Baraza likirekebishwa vyama vya michezo navyo vitakuwa mguu sawa na kuleta chachu na maendeleo katika michezo,”alisema Mhe. Nnauye.

Aliongeza kwa kusema kuwa, miaka saba ambayo Lihaya amekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza imetosha kwani hakuna mabadiliko yoyote aliyoyafanya katika sekta ya michezo tangu alipoteuliwa mwaka 2009.

Kutokana na utenguzi huo Mhe. Nnauye amemtaka Mwenyekiti wa BMT Dionis Malinzi kupendekeza jina la Katibu Mtendaji mpya wa BMT ambaye anampendekeza kwa mujibu wa sheria ya BMT kifungu cha 5(1) baada ya kupata idhini ya waziri mwenye dhamana.

Vilevile, Mhe. Nnauye amemtaka mwenyekiti kuteua Katibu Mtendaji ambaye atakuwa ni mchapa kazi na mwenye mipango ambayo itaibadilisha BMT na kuleta chachu katika michezo nchini.

Aidha, Mhe. Nnauye amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara ya habari, utamaduni sanaa na michezo kumpangia Lihaya kazi nyingine wizarani.

Hatimaye Lady Jaydee Avunja Ukimya Wake

0
0
Mkongwe wa muziki wa bongo fleva Lady Jaydee ametangaza rasmi kurudi tena kwenye muziki baada ya ukimya wa muda kidogo kwenye muziki.

Lady Jaydee ameweka wazi ujio wake mpya kwenye muziki baada ya siku 30 kuanzia leo.
Wiki kadhaa zilizopita Lady Jaydee aliwahi kuwaomba wapenzi wa muziki wake kuwa wavumilivu na kuwataka wasubiri kwani kwa kipindi hicho alikiri wazi kuwa hana kitu cha kuimba wala hakuwa na mizuka ya kuimba, kutokana na mambo yake ya hapa na pale na kuwataka wapenzi wake kwenye muziki kudumisha amani.

"Karibu tu lakini sina lolote kwa sasa, sina kabisa na sitakuwa nalo kwa kipindi kirefu sana, yaani sina, sina, sina. wapenzi huvuta subira mashabiki huhama hama. Wapenzi vuteni subira na dumisheni amani" Aliandika Lady Jaydee

Baada ya ukimya na mashabiki kuanza kuhoji juu ya ukimya wake kwenye muziki, mwanadada Lady Jaydee alikuja na kuweka wazi kuwa amekuwa kimya lakini hawezi kufanya lolote sababu hakuwa na jambo la kusema au kuimba kwa wakati huo na kuwataka tena mashabiki na wapenzi wa muziki wake kuwa wavumilivu.

"Ni kweli sijasema ,ni kweli nimekaa kimya lakini siwezi sema tu endapo sina cha kusema mnaweza kuvumilia? Kama ninavyo vumilia? Napumzika tu sina cha kufanya mvumilie nitarudi sema sina cha kusema na siko tayari kusema, nitasema nikiwa tayari kusema" Alimaliza Lady Jaydee

Lady Jaydee sasa amepata cha kusema na amepata ya kuzungumza na ndio maana ametangaza rasmi ujio wake mpya kwenye muziki wa bongo fleva, Jide amesema kuwa baada ya siku 30 kuanzia leo atasimama tena.

File la Mpenzi Mpya wa Nuhu Mziwanda Lawekwa Wazi...Mwenyewe Acharuka na Kusema Haya...

0
0
Huku Instagram Mambo ni moto..Watu washafukua file ya demu mpya wa Nuhu Mziwanda na kuliweka hazarani....Demu aja juu na kuwajibu waliofukua file....

baby_ake
 Jina kamili anaitwa Zuhura abdul Sabil ,Huyo msichana kwanza kwao rujewa mbeya mama ake alikuwa diwani wa rjw, ni mke wa mtu mumewe anaitwa naseeb huko Oman alienda kumsimamia mumewe biashara yake, Alishawah kutaka kuolewa na mwarab mmoja wa Iringa yule baba baada ya kupata story yake siku ya harus hakutokea bibie huyo akalazwa hospitali!!!! Ashatembea na abdukiba, Sam wa ukweli , beka na wasanii kibao mpka tino Wa bongo move kapiga ni mtanzania Pure kabisaaaa kazaliwa rujewa mbeya, kasoma shule inaitwa St Anna na secondary kasoma usangu sec mpaka form two na hakuendele kwao wamezaliwa watatu Kakaake anafanyaga mazingaombwe anaitwa Dr Sabil ukimsearch YouTube utampaka, sasa point YANGU ni kwamba nuh bdo unasafari ndefuuu ya kutafuta demu mwingine au ndio unalipiza kisasi kwa shishi ila mke Wa mtu sumu oooh utatolewa busha tutashangaa nuh anatembea na msuri kumbe watu washafanya vyao

Majibu ya demu wa Nuhu Mziwanda haya hapa....

Huyu Ndo Binti Aliyeongoza Kitaifa Katika Matokeo ya Mtihani wa Kidato Cha Nne

0
0
Huyu ndiye Mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza  Kitaifa katika Mtihani wa Kidato cha Nne  toka  shule  ya  Canossa Girls.Anaitwa Butogwa Charles Shija, akiwa mwenye furaha, nyumbani kwa wazazi wake Kipunguni Jijini la Dar es Salaam jana. 
 

Huyu anaitwa Congcong Wang,ameshika Nafasi ya pili Kitaifa.Amemaliza kidato cha nne Feza Girls.Ni  Mtanzania mwenye asili ya China

Chuchu Afunguka Kuhusu Weupe wa Mpenzi wake Ray

0
0
Msanii wa filamu nchini ambaye pia ni mpenzi wa Ray Kigosi amefunguka na kusema hapendi watu wanapokuwa wana msema mchumba wake Ray Kigosi kuwa amejichubua na kudai anaamua kupuuza ila huwa hapendezwi na suala hilo.

Chuchu Hans alisema hayo kupitia kipindi cha eNEWZ jana na kudai kuwa mpenzi wake huyo kwa sasa amependeza kutokana na maisha yake kubadilika kwani zamani kwake maisha yalikuwa magumu na muda mwingi alikuwa akitembea kwa miguu na kuhangaika kutoka kimuziki ndiyo maana alikuwa anaonekana vile.

"Unajua mimi huwa sipendi sana watu wanapozungumzia suala hilo ila kwa kuwa sisi ni watu maarufu inafika mahali unaamua kupotezea tu, unajua watu wanashindwa kuelewa kuwa maisha yamebadilika na saizi sanaa ina lipa ndiyo maana Ray Kigosi amebadilika na kutakata, unajua zamani maisha hakuwa na uwezo sana na alikuwa anahangaika na kutoka na muda mwingi alikuwa akitembea kwa miguu ndio maana alikuwa akionekana vile" Alisema Chuchu Hans

Kwa upande wake Ray Kigosi alikiri kuwa sasa amebadilika na kuwa mweupe na kusema siri kubwa ni yeye kunywa maji sana, kufanya scrub ndiyo maana amekuwa hivyo ila hajichubui kama ambavyo watu wanasema.

Wema Sepetu Wewe Bado Mdogo Sana Usizae - Mange Kimambi

0
0
Blogger maarufu hapa nchini Mange Kimambi ametoa ushauri ambao mwenyewe ameuita wa bure kwa mwanadada mwenye jina lake hapa mjini Wema Sepetu, na kumtaka asizae kwa kulazimishwa na maneno ya watu, bali asubiri mpaka akiolewa.


Mange ametoa ushauri huo kwenye ukurasa wake wa instagram baada ya seke seke lililomkuta mwanadada huyo la kushambuliwa na watu wakimtuhumu kuwa hana uwezo wa kuzaa, kabla na hata baada ya kuharibika kwa ujauzito aliokuwa nao siku za hivi karibuni.

Mange amedai pia Wema ni mdogo kiumri kuitwa mama, hivyo asikimbilie kuzaa kama muda bado.
"Hivi kwanini unakubali kuwa pressured na wajinga wa social media kuzaa when you are not ready? Mbali na familia yako ni mimi peke yangu ndo ninae jua umri wako Wema, Wema huna hata 26 years we mtoto, toka lini mtu mdogo hivyo akawa classified as tasa? Why unakubali kupewa pressure uzae ukiwa mdogo hivi? hata kuolewa hujaolewa??

Ameendelea kwa kumshauri .....

"Achana nao mdogo wangu, acha waongeee midomo mali yao, ubiri uolewe ndo uzae, mwishowe uje kuzaa mtoto while you are not ready au uzae na mtu huna mpango wa kuishi nae kisa tu uwakomeshe hawa wajinga wa kwenye mitandao. Utajikomesha mwenyewe, Please dont succumb to the pressure, You are way too young". Ameandika Mange kwenye ukurusa wake, maneno yaliyosindikizwa na picha ya Wema sepetu.

Pamoja na hayo Mange pia alimtaka Wema kuwa kwenye mahusiano na watu wasiojulikana kama yeye mwenyewe alivyo, kwani itamsaidia kumuongoza na kuepuka maneno ya watu pale atakapokuwa msiri wa maisha yake, na kuepuka mabalaa ya kudhalilishwa na kukashifiwa kwenye mitandao, iwapo hawatafikia mahusiano yake na Idris hayatafanikiwa.

"If not nakushauri tafuta mwanaume ambaye hayuko hata Instagram au social media ili akuongoze vizuri. Find a guy mwenye maisha tofauti kabisa na ya kwako. Mkaka flani meneja wa benki huyo ndo atakubadilisha completely but these guys wa kwenye mitandao kama wewe issue itakuwa pale pale", aliandika Mange.

Ifahamike kwamba Mange Kimambi ndiye mtu aliyevumbua kipaji cha Wema, na kumshauri kuingia kwenye mashindano ya ulimbwende ya Miss Tanzania, ambapo aliibuka mshindi na kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya urembo ya dunio (Miss World).

Shilole Ala za Uso, Atakiwa Kuacha Kubemenda Vijana Wadogo....

0
0
Msanii wa bongo fleva asiyeisha vituko Shilole au Shishi Baby, ameijiwa juu na mashabiki wake na kumtaka kuacha tabia ya kupenda wavulana wadogo, huku wakimtuhumu kuwabemenda na kujidhalilisha.

Kwenye ukurasa wake wa instagram ambapo Shilole amepost picha akiwa na mwenzi wake huyo mpya ambaye pia ni mwanamuziki Nedy Music, mashabiki hao wamemtaka Shishi kuacha mara moja kwani anawafundisha vibaya watoto wake ambao ni wakubwa.

ester_mbise : Mbona huo ni ubakaji sasa!! Kitoto kidogo sana hicho unakibemenda!!! Yaaaaan bora hata Nuh kdg japo naye alikuwa katoto!!! Daaaaaaaaah

janejoseph88.jj : acha kubeba watoto wadogo dada yangu hebu jiheshimu japo kidogo fikria kuwa na ww pia unamtoto wa kike hata kama unahela

anifamwakalobo : Jmn kumbe ndo style yako unapenda vitoto haaaa wewe mmama saiz zako huzioni mbona utamaliza kubemenda watoto wa wenzio!!! Huyo kijana ilifaa atoke na mtoto wako ww uwe mamamkwe daaa kweli hii dunia kuna watu na viatu ila wengine ni yeboyebo sasa,,, umezidi unatuzalilisha wanawake wenzio hiv unafikili wazazi wa huyo kijana watajiskiaje kwa mfano shilolekiuno???

lily_da_bae:This lil boy is being raped. This is so disgusting. Dating kids who are almost same age as your own kids. Hm!! Im sure this kid is broke n all he needs is $$$ but not true love. Look for a man if you want to be truly loved, otherwise you will date more than 100 of these kidos.

Akimaanisha....... (huyu mvulana mdogo anabakwa, hii inachukiza, kuwa na mahusiano na watoto ambao umri wao ni karibu sawa na watoto wako, hm, nina uhakika huyu mtoto amefulia na vyote anavyotaka ni dola na si mapenzi ya kweli. Tafuta mwanaume kama unataka kupendwa kweli, vinginevyo utatoka na zaidi ya 100 ya hawa watoto).

Hayo yameandikwa na mashabiki hao wakimtaka Shilole kuacha hiyo tabia ya kuwa na mahusiano na vijana wenye umri mdogo.

Hivi karibuni Shilole aliachana na mpenzi wake Nuh Mziwanda, ambaye pia alikuwa mdogo kwake kiumri.
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live




Latest Images