Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Amteua Hebert Mrango kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TBC

$
0
0
 
MKUTANO WA MHE. NAPE MOSSES NNAUYE, WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO NA WAANDISHI WA HABARI
 

TAREHE 20/02/2016
-------------
Dondoo Alizozungumza Waziri Nape Nnauye;
Napenda kuwafahamisha kuwa kufuatia Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kumaliza Muda wake, uundwaji wa Bodi Mpya umekamilika. 

Ni vyema kuwafahamisha kuwa katika utaratibu wa kisheria wa kuunda Bodi ya TBC mwenye Mamlaka ya kisheria ya Kumteua Mwenyekiti wa Bodi ni Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania.
 
Napenda kutumia fursa hii kumshukuru sana aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TBC iliyomaliza muda wake, Prof. Mwajabu Possi na wajumbe wake wote kwa kazi waliyoifanya kwa muda wote wa uhai wa bodi hiyo. 

Ninaamini Bodi Mpya itaendeleza yale mazuri yote yaliyofanyika na Baodi iliyopita na kubuni mambo mengine mapya ili kuongeza tija kwa Shirika.
 
Baada ya kutoa maelezo haya ya awali, sasa nichukue fursa hii kuwajulisha yafuatayo;
1.   Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemteua Mhe. Balozi Herbert E. Mrango (pichani) kuwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya TBC. Uteuzi huu unaanza tarehe 19/02/2016 kwa kipindi cha miaka Mitatu.
 
Balozi Mrango kielimu ana shahada ya Uzamili katika uendelezaji wa Mifumo (MSc – Systems Development) aliyoisomea Chuo Kikuu cha Dublin Nchini Uingereza. Aidha amehitimu Shahada ya kwanza ya Takwimu za Kiuchumi katika Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, Tanzania.
 
Balozi Mrango alishashika nyadhifa mbalimbali, zikiwemo kuwa Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara  ya Miundombinu Kuanzia Februari, 2011 hadi September, 2013.
 
Nachukua fursa hii kumpongeza Mhe. Balozi Mrango kwa kuaminiwa na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kushika wadhifa huu muhimu. 

Aidha nimhakikishie Mwenyekiti huyu Mpya wa TBC kwamba kwa kuwa Shirika la TBC liko chini ya Wizara yangu, tutampa ushirikiano wa kutosha ili kuendelea kuleta mabadiliko chanya katika shirika letu la Utangazaji.

2.Kwa mujibu wa Sheria iliyounda TBC, baada ya Mhe. Rais kumteua Mwenyekiti wa Bodi, Waziri mwenye dhamana na shughuli za utangazaji,  anateua Wajumbe sita wa Bodi. 

Katika uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Shirika la Umma, Ofisi ya Msajili wa Hazina ilishatupatia vigezo vya utaalamu wa wajumbe wakati wa uteuzi.

Hivyo basi, mimi Nape Moses Nnauye, nikiwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, kwa kuzingatia vigezo vilivyobainishwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kwa kufuata taratibu zingine za kufanya uteuzi, nimewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya TBC;

(i) Bw. William Steven Kallaghe; Mtaalamu wa Uchumi.  (M.A – Economics; Head of Public Policy: NBC Bank  Tanzania ).

(ii)Bw. Mustapha Kambona Ismail; Mtaalamu wa Sheria. (LLB - UDSM; Associate Director, Litigation & Investment – Bank of Tanzania; Advocate of the High Court of Tanzania).

(iii) Bi. Elimbora Abia Muro; Mtaalamu wa Uhasibu. (CPA, MBA: Senior Internal Auditor, Tanzania Investment Centre).

(iv) Bw. Mick Lutechura Kiliba; Mtaalamu wa Rasilimali watu. (MBA – Public Service Mgt; Director of Management: President’s Office – Public Service Management).

(v) Dkt. Ayub Rioba; Mtaalamu wa Sekta ya Utangazaji na Utangazaji.  (PhD – Mass Communication; Associate Dean: School of Journalism, University of Dar Es Salaam) na

6. Bw. Assah Andrew Mwambene; Mtaalamu wa Sekta ya Habari. ( MSc – Media Research and Analysis; Director of Information: Ministry of Information, Culture, Arts and Sports).

Uteuzi wa wajumbe hawa ni kuanzia tarehe 19/02/2016 kwa muda wa miaka mitatu.

3. Nimalizie kwa kuwapongeza tena wote waliopata uteuzi huu. Tuna matumaini makubwa toka kwao kwa ajili ya kuboresha ufanisi wa TBC katika tasnia ya Utangazaji katika ulimwengu wa Teknolojia inayobadilika kwa kasi kubwa duniani.

Ni imani yangu kwamba Bodi hii mpya italeta msukumo mpya katika utendaji wa Shirika ili hata watumishi wanaofanya kazi katika shirika hili waendelee kujivunia kuwa ndani ya TBC lakini pia Umma wa Watanzania wajivunie viwango vya utendaji wa Shirika hili.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Februari 21, Ikiwemo ya Mbowe Kuwataja Kikwete na Mkama Kama Majibu Makuu

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Februari 21, Ikiwemo ya Mbowe Kuwataja Kikwete na Mkama Kama Majibu Makuu 

Wadaiwa Sugu Bodi ya Mikopo Kitanzini......CAG Apewa Jukumu La Kuwasaka Popote Walipo,Kutoajiriwa Sio Kigezo Cha Kukwepa Deni

$
0
0
BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imetoa onyo kwa wadaiwa sugu ambao hawajajitokeza kuanza kulipa madeni yao, kwamba hatua mbalimbali dhidi yao zinatafuata kokote waliko.

Miongoni mwa hatua hizo, bodi hiyo imetaja kuwa ni kuwatoza wadaiwa hao sugu riba ya asilimia kumi katika deni lao na kutumia taarifa zao kuwazuia kufanya safari za nje ya nchi.

Taarifa ya hivi karibuni ya bodi hiyo , imeeleza kuwa wadaiwa hao wa tangu mwaka wa masomo wa 1994/95, wataanza kusakwa kupitia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambaye anawajibika kukagua mali zote za Serikali.

Mbali na CAG, ambaye ana mkono mrefu wa kuwasaka katika ofisi zote za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma, Serikali za Mitaa na katika miradi ambayo Serikali ina ubia na sekta binafsi, pia kampuni binafsi za ukaguzi wa hesabu, zenye mkono mrefu katika sekta binafsi, zitatumika kuwasaka katika kampuni binafsi na asasi za kiraia.

“Jukumu la CAG na kampuni zingine binafsi za ukaguzi wa mahesabu, ni kulazimisha waajiri kuwasilisha taarifa za wafanyakazi wao ambao ni wahitimu wa elimu ya juu na makato ya mkopo waliopewa,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imefanya marejeo ya Sheria ya Bodi namba 9 ya 2004 na marekebisho yake, inayomtaka kila mwajiri kutoa maelezo kwa maandishi kwa bodi, kuhusu mwajiriwa ambaye ni mnufaika wa mkopo huo, ndani ya siku 28 tangu mdaiwa alipoajiriwa.

Hatua
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mdaiwa yeyote wa bodi hiyo atakayeshindwa kulipa deni lake bila sababu za msingi, kwanza atakuwa akikabiliwa na kesi ya madai chini ya kifungu cha 6 C na H cha Sheria ya Bodi ya Mikopo namba 9 ya mwaka 2004.

Mbali na kukabiliwa na kesi hiyo, pia mkopo wake kwa namna unavyochelewa kuanza kulipwa, utakuwa ukijilimbikizia riba ya asilimia 10.

Taarifa hiyo ya bodi imeeleza kuwa mdaiwa huyo taarifa zake zitapelekwa katika taasisi za kumbukumbu ya mikopo zilizo chini ya Benki Kuu (BoT), ambazo zitazuia wadaiwa hao kupata mikopo katika mabenki na asasi zote za fedha.

Mdaiwa huyo pia atazuiwa kupata udhamini wa Serikali katika muendelezo wa masomo yake, lakini pia atazuiwa kujiunga na chuo chochote cha elimu ya juu ndani na nje ya nchi.

Aidha kwa mujibu wa taarifa hiyo, taarifa zao pia zitawasilishwa katika Idara ya Uhamiaji iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na katika ofisi zote za kibalozi, ili wakose kibali cha kusafiri nje ya nchi.

Hasara nyingine watakayokabiliwa nayo wadaiwa hao, ni Tozo ya Kulinda Thamani ya Mkopo (VRF) ya asilimia sita kila mwaka, itakayotozwa kwa kila mkopo, ili wadaiwa watakapoanza kulipa mkopo waliochukua, walipe kwa thamani ya sasa.

Tozo hiyo imelenga kuepuka athari ya mfumuko wa bei tangu mdaiwa aliponufaika, lakini pia kuwezesha urejeshwaji wa deni, uwe na thamani ya kumhudumia mwanafunzi mwingine mwenye mahitaji kwa sasa na baadaye.

Ambao hawajaajiriwa
Taarifa hiyo pia imeonya wadaiwa wanaodhani kuwa kutokuajiriwa ni sababu ya kutolipa mkopo huo, kwamba mkopo huo unatakiwa kulipwa baada ya kumalizika kwa mwaka mmoja tangu mdaiwa alipofanikiwa kuhitimu masomo yake, au mwaka mmoja tangu mhusika alipokatisha masomo yake kwa sababu yoyote.

Aidha, taarifa hiyo imeelekeza watakaojitokeza, kama wameajiriwa, asilimia nane ya mshahara wao wa kila mwezi, itatakiwa kukatwa na kuwasilishwa kwenye Bodi ili kulipa deni husika.

Lakini pia Bodi hiyo imetengeneza utaratibu kwa ambao hawajaajiriwa, kwamba wanaweza kulipa kiasi cha chini cha Sh laki moja kila mwezi katika akaunti za Bodi zilizopo Benki ya Posta yenye namba CCA0240000032; Benki ya NMB namba 2011100205 na Benki ya CRDB namba 01J1028467503.

Deni lenyewe
Kwa mujibu wa Ripoti ya CAG, hadi Juni 2014, bodi hiyo ilikuwa imewakopesha wanafunzi Sh trilioni 1.8 kuanzia mwaka wa masomo 1994/95 na kati ya fedha hizo, Sh bilioni 51 zilitolewa na iliyokuwa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia.

Taarifa hiyo ya HESLB imetolewa siku chache kabla ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako  kusitisha ajira ya Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, George Nyatega kwa tuhuma za udhaifu katika fedha za mikopo zaidi ya Sh bilioni 3.2.

Wema Sepetu na Idriss Wamtetea Lulu Michael Wadai Ahusiki Katika Mambo yao na Wala Hakufumaniwa

$
0
0
Baada ya Lulu Michael Kuhusishwa kwenye ugomvi wa Wema na Idris ...Wema na Idriss Wamechukizwa na Kitendo hicho na kuandika yafuatayo:

From @wemasepetu - Leave Her out of This... Please....!!!! @elizabethmichaelofficial Lala kwa Amani baby... Nimesema mimi... People dont know mwanzo wa vitu ila wanaongea as if wanayajua... Mi ntaendelea kukaa kimya ila muacheni huyu mtoto please...

Idriss naye Akaongezea Haya :


From @idrissultan - Acheni hizo lakini msiwe hivyo mimi na Wema we have our issues to solve na nina kiburi na yeye ana kiburi but sio ushindani nani anajua zaidi. So mnapojaribu kuingiza watoto wa watu kama @elizabethmichaelofficial my pure sister and friend ninudhalilishaji huu. Siku haya yameisha mtajiangalia kwenye vioo muone aibu kwa haya mambo tunayochochea. I believe mmepitiwa tu na hii sio nia yenu basi Mwenyezi Mungu awe nanyi katika yote mtakayosema na kutenda
Read more at http://websta.me//n/wemareplies#qFIMW6LUOuGVQDY1.99

Rafiki Yangu Ameniomba Nilale na Mume Wake Nipate Mimba Niwazalie Mtoto.....

$
0
0

Nina rafiki yangu lakini tunaishi nchi tofauti tunakutana mara 3-5 kwa mwaka hua mie nikienda nchi anayoishi anakuja kunitembelea na yeye akija ninakoishi anafikia kwangu.Yeye hajabahatika kupata mtoto mwaka wa 5 sasa tangu ameolewa, jana wakati tuna kula akaniomba tuonge kitu muhimu baada ya chakula, nikamwambia inshallah tutaongea.

Basi baada ya chakula na mambo mengine nikaenda kuwalaza watoto nikaenda chumbani kwake haya nimekuja tuongee, basi akanambia kama unavyojua sina mtoto na nimejaribu dawa zote unazozijua za kizungu na miti shamba sijafanikiwa kupata ujauzito sasa tumeshauriyana na mume wangu nikamwambia changua rafiki yangu yoyote mimi nitaongea nae ili atupatie mtoto.

Mie macho niliyatoa nakutetemeka juu, nikamwambia sijafahamu unamaanisha nini ukisema rafiki yako akupe mtoto je unataka nikupe mwanangu ule au vipi? Kasema NO nataka ulale na mumewangu nilimshangaa lakini sikutaka ahisi vibaya ilibidi nijikaze nikamwambia na ilikuwaje nikawa mie?

Kasema ndani ya moyo wangu nili wish mume wangu akuchague wewe na aliposema bora wewe ndio nikafurahi zaidi.Waungwana nilimpa maneno mengi yakumpa moyo lakini naomba nisema kua sijakubaliana na ombi lake na nimemwambia anisamehe sitoweza kufanya hicho kitu ila nitamsaidia kwa hali na mali.

Nitamuulizia kwa watu kama kuna tiba lakini kwa mimi siwezi na mumewe pia niliongea nae nikamwambia wanisamehe sitoweza, je nimekosea kuwakatalia?
Sijapenda lakini sina choice naipenda Family yangu sana na hata hili jambo silifikishi kwa Mr.

By Nimpendenani/JF...

Chama cha ACT Wazalendo Chamvua Uanachama Ofisa Mipango Na Aliyekuwa Mgombea Urais Zanzibar Kwa Kuhudhuria Vikao Vya ZEC

$
0
0
Chama cha ACT Wazalendo kimemsimamisha uanachama Ofisa Mipango wake, Ali Makame Issa kwa madai ya kukiuka maadili ya chama hicho.

Hata hivyo, Issa alisema jana kuwa hajapokea taarifa yoyote kutoka katika chama hicho.

Hatua hiyo dhidi ya kiongozi huyo mwandamizi ndani ya ACT, imekuja baada ya chama hicho kudai kuwa alishirikiana na aliyekuwa mgombea wa urais wa Zanzibar, Khamis Iddi Lila kuwahujumu.

Awali, Lila alisimamishwa uanachama kwa madai ya kutoa misimamo ya kushiriki uchaguzi wa marudio uliotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha.

Barua ya ACT, iliyosainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Juma Said Sanani imesema: “Kamati maalumu ya Zanzibar imekusimamisha rasmi uanachama kwa mujibu wa katiba ya ACT Ibara ya 11 (2) kuanzia leo Februari 19, 2016, kwa ukiukwaji mkubwa wa katiba Ibara ya 7 (3)(5)(9) Ibara ya 10 (2)(c) (d), Ibara ya 22 (1) (2) (4).”

Barua hiyo inabainisha kuwa mwanachama huyo amekiuka kanuni na maadili pamoja na kukidhalilisha chama.

“Huku ni kukiingiza chama katika mgogoro kwa kuandika barua ya kushiriki uchaguzi wa marudio na kuhudhuria katika kikao cha Tume ya Uchaguzi Februari 17 ukijua kuwa chama kimeshapeleka barua Febuari 9 ya kutoshiriki uchaguzi,” inaeleza.

Vyama vilivyowachukulia hatua viongozi wake kwa madai ya kukiuka kanuni ni Sauti ya Umma (SAU), kilichomfukuza aliyekuwa mgombea wake wa urais wa Zanzibar, Issa Mohamed Zonga, huku Alliance for Democratic Changes (ADC) kikimfukuza aliyekuwa mlezi wake, Hamad Rashid Mohamed

Kutoka Uganda..Huyu Ndio Aliyetangazwa Rasmi na Tume ya Uchaguzi Kuwa Mshindi wa Urais

$
0
0
Uganda ilikua kwenye uchaguzi mkuu wa kumchagua Rais na Wabunge juzi ambapo matokeo ya awali yalianza kutolewa kuanzia jana lakini leo matokeo kamili yametolewa na Yoweri Museveni ambaye amekuwepo kwenye kiti cha Urais toka mwaka 1986 ametangazwa mshindi huku mpinzani wake mkuu ambaye ni Kizza Besigye akikataa matokeo hayo aliyoyaita ya wizi wa kura.

Kituo cha TV cha NBS kimeripoti kwamba huduma za Taxi mitaani, mitandao ya kijamii na huduma za benki za simu za mkononi zimerejea baada ya serikali kuamuru juzi kila kitu kizimwe kuanzia Facebook, Twitter, Whatsapp.

Rais Museveni baadae alihojiwa na kusema mitandao ya kijamii ilizimwa kwa muda mfupi tu na watu hawakutakiwa kuwa na hofu sababu ilifanywa ili kuzuia upotoshaji wa taarifa tu ambao umekua ukifanywa mara kwa mara.

Ugomvi wa Wema Sepetu na Idris..Lulu Michael Ahusishwa..Adaiwa Kufumaniwa na Idriss..Mpambe wa Wema Afunguka...

$
0
0
Aliyekuwa Shabiki wa Wema Sepetu namba moja huko instagram na kiongozi wa Team Wema Amemwaga mchele kwenye kuku wengi baada ya kufunguka kuhusika kwa Lulu Michael kwenye ugomvi wa Wema Sepetu na Idriss mpaka kufikia kupigana kibuti...

Soma Alichoandika Instagram


"wemareplies @Regrann from @matikibokoyao - @idrissultan toka hizi mambo zote zimetokea umeona natia neno kwanza ni hivi sina team ila I still love @wemasepetu no matter what ila jua wewe ndio umempa @wemasepetu stress ndio hata hizo pic unazosema sijui insta mcongo nothing is going on baba ww sema unachokifanya sio vzr mmekoseana why msimalize mambo yenu huko private @wemasepetu na ww usijibu kitu maana saivi zigo limesha kuangukia mbaya ww kama usemavyo damu Ya kunguni kama mati hapa ila ulichokosea kupiga pic na mcongo hata kama ulikuwa unamrusha roho iddy umekosea tayari umesha onekana mbaya lakini behind ukweli ni kwamba ilikuwa hasira na stress la fumanizi kati Ya @elizabethmichaelofficial na @idrissultan tena fumanizi la asubuhi asubuhi mtu anatoka chumbani na kataulo ila daaah inauma sanaa kikubwa iddy maizeni mambo zenu huko private acheni utoto sema lulu nae kibokokabisaaaaa nyakunyaku  nichambeni lakini habari ndio hiyo "Matikibokoyao


Dinna Marios:Nilipoteza Kipindi cha "Leo Tena" Baada ya Kwenda Kujifungua

$
0
0
Nilipompata Zion kama mzazi yoyote ilikuwa ni furaha sanaa alileta furaha maishani mwangu na mwanzo mpya katika maisha yangu.

Katikati maisha yangu yoote nilikuwa muoga sanaa kupata mtoto sikuwa najua nitaanzia wapi kumlea.Zile story za wakinamama waliotangulia kuwa kuzaa kunauma zilikuwa zinanipa stress saana.

Lakini Nilimuomba Mungu nikifikisha miaka 30 Mungu anijaalie mtoto katika mahusiano yanayoeleweka.Zion hakuwa bahati mbaya siku ambayo baba yake alisema anatamani tupate mtoto Mungu aliweka tiki matamanio hayo wiki iliyofuata nilishika ujauzito.
Nikiwa natimiza miaka 30 nilikuwa na mimba kubwa ya Zion na nikamzaa nikiwa na miaka 30 nikaamini ni mpango wa Mungu.

Nilipopoteza leo tena nilihuzunika sana nikaanza kukufuru Mungu.Kwamba kwa miaka 8 mfululizo nimekilea kipindi leo nimeenda kujifungua narudi nakuta nafasi hiyo haipo kwa nini?kwa nini kuzaa kubadilishe tena ghafla?nakumbuka siku hiyo hata kunyonyesha sikuweza kabisa kabisa
Lakini nikamuomba Mungu anipe muongozo anataka kunipeleka wapi?Kwa sababu ya Zion niliweza kuja na product ya mafuta ya nazi dina marios coconut baby oil.
Alipotimiza mwaka mmoja picha za birthday yake ndio zilileta wazo la kuanzisha magazine ya parenting/malezi .Later nikajoin @efm_93.7 radio nakuanza kipindi kipya cha UHONDO.

Nilianza upya na MTOTO wangu Zion ndio inspiration ya mwanzo wangu mpya.Baada ya mwaka mmoja kupita wa kulipika wazo jana nikafanikiwa kutambulisha magazine ya MTOTO kwa ndugu,jamaa na marafiki waliokuja katika birthday party ya Zion.

Na magazine cover story toleo la kwanza yupo Zion na mimi mama yake kukusimulia mengi maana yeye ndio inspiration ya hiyo magazine.

Lolote tunalomuomba Mungu atatupa lakini sio kwa picha ile tunayoitaka ni kwa namna apendavyo yeye na anavyoona inakufaaa.

Usikose nakala ya MTOTO magazine kuanzia wiki ijayo kusoma mengi yahusuyo malezi ya watoto wetu . Litauzwa Tsh 5,000 tu!

Nay Wa Mitego anusurika kutekwa,Je kisa ni wimbo wa Shika adabu yako?

$
0
0
Msanii wa Nay wa Mitego ambaye kwa sasa yupo kwenye seke seke baada ya kuachia wimbo wake wa shika adabu yako ambao amewa diss watu wengi maarufu, siku kadhaa zilizopita alinusurika kutekwa na watu wasiojulikana.

Nay amekiambia kituo kimoja cha redio kuwa kuna siku alikuwa anatoka studio akaona gari limekuja kupaki nyuma ya gari lake,alipoanza kutoka gari hilo likaanza kumfuatilia kwa nyuma kila ndipo hapo alipoanza kutia mashaka.

Nay amesema kuwa alipata mashaka zaidi baada ya kuona kuwa gari hilo linazidi kumfuata hata baada ya kujaribu kubadilisha uelekeo aliokua kuwa akienda ndipo alipoamua kuwapigia marafiki zake ili waje kumsaidia.

Nay anasema baada ya kuzunguka sana ili kuwakwepa watu hao mwishowe alifanikiwa kufika manzese usiku sana kwa masela wake na kukuta amepishana nao kwa vile walikwenda kumfuata,akibidi awapige warudi haraka na ndipo hapo ilikuwa ponea yake.

Nay amesema anahisi vugu vugu la wimbo wake wa shika adabu yako linaweza likwa ndio chanzo na pia amesema anafanya mipango ya kujilinda zaidi.

Shilole Amkana Nedy Music, Asema Sio Mpenzi wake...Agoma Kumzungumzia Demu Mpya wa Nuh

$
0
0
Mwanadada anayetamba kwenye muziki wa bongo fleva na bongo muvi,Shilole amekana kutoka kimapenzi na msanii anayechipukia kwenye bongo fleva,Nedy Music.

Akihojiwa na redio moja Shilole amesema kuwa msanii huyo ni mshikaji wake tu hakuna kinachoendelea baina yao na kukanusha kuwa msanii huyo anaishi nyumbani kwake.

“Nedy music ni mshikaji wangu..anakaa kwake mimi nakaa kwangu.Mimi ni mwanamke mtafutaji kwa hiyo mambo ya mapenzi siyaweki saana,nafocus kwenye kazi” alifunguka Shilole.

Alipoulizwa kuwa inasemekana mpenzi wake wa zamani Nuh Mziwanda ameopoa demu mkali kuliko yeye,Shilole alikataa kata kata kuzungumzia hilo na kusema hana muda wa kumwongelea mtu.

Ray 'Nilishawahi Kumuokoa Nay wa Mitego Asipigwe Lakini Nashangaa Kanigeuka'

$
0
0

STAA wa Bongo Movie, Vincent Kigosi ‘Ray’ kwa mara nyingine ameendelea kuteka ‘headlines’ baada ya kuibuka na kudai kuwa alishawahi kumuokoa staa wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego asipigwe.


Akizungumza asubuhi hii katika kipindi cha Leo Tena kinachorusha na Clouds FM, Ray alisema kuwa alipokuwa katika shoo ya Fiesta Mwanza, Nay alivamiwa na kundi la wasanii wa Bongo Movie na kutaka kupigwa.

“Nilifanikiwa kumzuia kwasababu wasanii walikuwa wengi wakiongozwa na Wema Sepetu sasa nashangaa mwenzangu Nay ananisakama natumia pesa zote za mauzo ya filamu namalizia kwenye mkorogo,” alisema Nay.

Mrembo Huddah Monroe Ajitangaza Kuwa Kwa Sasa Yeye ni Tajiri..Hanywi Tena Uji wa Chumvi

$
0
0
Mwanamitindo maarufu nchini Kenya, Huddah Monroe, amejitapa na utajiri alionao kwa sasa na kusema kwamba uji wa chumvi aliwahi kunywa mara moja katika kumbukumbu za maisha yake.

Mrembo huyo mwenye mbwembwe nyingi, amedai kwa sasa yeye ni tajiri tofauti na miaka ya nyuma ambayo aliwahi kunywa uji wa mahindi uliowekwa chumvi.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, mrembo huyo aliweka picha huku akionyesha vitu vyake vya thamani, ikiwemo gari lake aina ya Range Rover SUV na nyumba yake mpya.

“Katika maisha hakuna kukata tamaa, ninaamini juhudi zangu zimenifikisha hapa kwa sasa, nina vitu vingi vya thamani kwa sasa na nishasahau maisha yale ya uji wa chumvi.

“Kwa sasa siwezi tena kunywa uji wa mahindi wenye chumvi, niangalie kwa sasa nakula soseji, mikate na vitu vingine,” alieleza Huddah.

Ameandika Hivi:


Huddahthebosschick 
Posting this sausages for a short story of not giving up or losing hope in life . When I was a kid , we never had Sausages , bread or sugar . We used to see them in newspapers passing by the roadside Coz POVERTY was real! .... But look at me now ? I'm eating sausages and I don't do sugar anymore despite the fact that I never had it when I was a kid. It's funny but We used to drink maize floor porridge (UJI) with salt in it LOL! And it tasted GOOD as Fuck! I Don't know about y'alls upbringing but that's how we used to roll. I have now done sugar , bread and sausages . Things I never dreamt off. Things I never thought I'd ever have 🙄 . Now look at that picture above! That's the real definition of MAKING IT in LIFE! NEVER LOSE HOPE BOSSES. YOU DUNNO WHAT TOMORROW MIGHT BRING! Whatever you want to have in life , you will have . Gods timing 🏾 .
P.S - I dunno what the hype was about sugar though , it's not good for your health . In fact honey is cheaper than Sugar here in Kenya . Use that . A lot of people who had sugar when I was kid have sugar issues now . See life ?

‘I am Behind Her A 100%’ Avril’s Fiancé Trashes Break Up Rumors with This Act

$
0
0
Avril’s break up with her South Africa boyfriend was started by a picture taken out of context .A picture of Dillish Mathews chilling with longtime friend Muga on Valentine’s Day while Avril performed in Kakamega.

The picture kick-started a rumor that Dillish had snatched Muga from Avril and the two were now going steady, a rumor that is now out of control as demonstrated by the hashtag#poleAvril trending on Twitter.

After being silent for a while, the two have come out to prove that they are still together .And what better way to show ‘togetherness’ like supporting your spouse.

Floyd Mayweather Flaunts His Cash in a Private Jet

$
0
0
American retired professional box Floyd Mayweather shared a photo of himself flaunting Thousands of Dollars in a Private Jet. What's the Exchange rate again? Lol


Muziki Unalipa Zaidi ya Filamu-Snura

$
0
0
Mwanamuziki na muigizaji Snura Mushi amesema muziki unamlipa zaidi ndio maana hafikirii kwa kipindi hiki kuwaahidi mashabiki wake ujio wowote wa filamu. “Muziki unalipa kwa kuwa kila kitu kinamhusu msanii na meneja wake, lakini filamu ina mambo mengi kiasi cha kumfanya msanii kuwa na mambo mengi”.

Mwanamuziki na muigizaji Snura Mushi amesema muziki unamlipa zaidi ndio maana hafikirii kwa kipindi hiki kuwaahidi mashabiki wake ujio wowote wa filamu. “Muziki unalipa kwa kuwa kila kitu kinamhusu msanii na meneja wake, lakini filamu ina mambo mengi kiasi cha kumfanya msanii kuwa na mambo mengi”

Kosa Hili Hulifanya Wakina Dada Wengi Wakiwa Faragha na Wenza Wao

$
0
0
Niende moja kwa moja kwenye mada. Tunajua akina dada wengi hutilia maanani suala la kupendezesha nywele zao.

Hakuna ubaya wa hilo ila tatizo huja pale wanapokuwa ndani ya sita kwa sita wengi wao hu pay attention sana kwenye nywele zao zisivurugike wakati wa game kiasi ya kwamba mwenzio kuona hauko na yeye bali unajali nywele.

Hii ikizidi hupunguza stimu ya wanaume. Akina dada jaribu kuchunguza hili ninalowaeleza utakuta wanaume wengi hawalipendi.

Kama ulipendezesha nywele basi huu ndo wakati wake. Jiachie hata kama zikivurugika utapewa hela utengeneze tena ili mradi uweze kuonyesha presence ya mawazo yako kwa mwenza wako.

Kundi la Wanamgambo wa Kiislam ISIS Lamkata Kichwa Kijana Baada ya Kumkuta Akisikiliza Nyimbo zenye Mahadhi ya Marekani

$
0
0
KUNDI la wapiganaji la ISIS limemuua kwa kumkata kichwa kijana mmoja baada ya kumkuta akisikiliza muziki wa Pop unaoimbwa na wasanii wa Marekani akiwa kwenye baa ya baba yake.

Kijana huyo, Ayham Hussein (15) alikamatwa mjini Mosul, Iraq baada ya wapiganaji waliokuwa kwenye doria kumsikia akisikiliza muziki huo.

Mauaji hayo yalifanyika nje ya msikiti baada ya Hussein kutiwa hatiani na mwili wake umekabidhiwa kwa wazazi wake kwa taratibu za mazishi.

Mbali na kuuawa Hussein, vijana wengine wawili nao wameuawa kwa kupigwa risasi nje ya msikiti kwa kutohudhuria Swala ya Ijumaa.

ISIS walipiga marufuku miziki ya nchi za magharibi kupigwa kwenye maeneo yao huku sababu kuu ikitajwa kuwa miziki hiyo ni chanzo cha vitendo viovu, majaribu pamoja na kumfanya mtu kushindwa kujifunza Koran hivyo kumsahau Mungu.

ZEC: Hakuna Chama wala Mgombea aliyejitoa kwenye Uchaguzi wa marudio Machi 20

$
0
0
Wakati baadhi ya vyama vya siasa vimetangaza kujitoa uchaguzi wa marudio Zanzibar, tume ya uchaguzi -ZEC- imetoa msimamao wake na kusema wagombea wote ni halali na watagombea nafasi zao kwa vile hakuna hata chama kimoja kilichofuata sheria na kanuni za uchaguzi.

Msimaamo huo wa tume umetolewa na mwenyekiti wa tume hiyo ya uchaguzi ya Zanzibar Jecha Salum Jecha katika taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo amesema kuna utaratibu wakujitoa na kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi hakuna chama kilichofuata kanuni ikiwa ni pamoja na wadhamini wawagombea kutangaza kuondoa udhamini wao, hivyo wagombea wote wa urais, uwakilshi na udiwani wote bado ni halali.

Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi vyama amabvyo vimethibitisha kushiriki ni pamoja na CCM, TADEA, ADC, CCK, AFP, SAU, TLP, huku CUF, NRA, CHAUMA, DP, Jahazi asilia na ACT Wazalendo ambao mgombea wake Khamis Lilla ametangaza kugombea huku chama chake kikimufukuza uanachama.

Meya ya Kinondoni Amtaka DC Paul Makonda Kuacha Utapeli wa Kuingilia Kazi Ambazo si zake

$
0
0
MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amemuonya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kuacha tabia ya kuingilia majukumu ya Halmashauri, badala yake afanye kazi zinazomuhusu.

Pia alisema uingiliaji huo ni utapeli uliomsababisha Rais John Magufuli kuagiza kila waziri akatwe Sh. milioni moja katika mshahara wake, pamoja na yeye mwenyewe, Waziri Mkuu Kassim Majalaliwa na Makamu wa rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa madarasa na shule mpya katika Jiji la Dar es Salaam.

Rais Magufuli alifikia uamuzi huo alipokuwa akizungumza na Taifa kupitia mkutano wake na Wazee wa Dar es Salaam, baada ya kuelezwa matatizo ya ongezeko la wanafunzi wa darasa la kwanza katika mkoa huo, lililotokana na utekelezaji wa ahadi ya elimu bure.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meya Jacob (Chadema) alisema ameradhimika kumuonya DC Makonda kutokana na tabia ya kutafuta sifa ili aonekane mchapakazi, hali ya kuwa ana dandia kazi zisizomuhusu.

Alisema hakuna sheria inayomruhusu Makonda kushirikiana kikazi na Halmashauri hadi awasilishe barua ya maombi kwa Mkurugenzi ama Meya kama anahitaji kufanya jambo lolote.
Majukumu

Jacob alisema ma-DC nchini wana majukumu muhimu matatu tu, ikiwemo Uenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Uenyekiti wa Kamati za Mashirikiano pamoja na kuwa Kiunganishi wa Serikali ya Mtaa na Serikali Kuuu.

Kuhusu wenye uwezo wa kuzungumzia maswala ya Halmashauri, Jacob alisema ni watu watatu wenye mamlaka ambao ni Mkurugenzi, Meya na Afisa Habari lakini si DC kwa kuwa haimuhusu.
“Kitu kilichosababisha nieleze haya na kutoa ufafanuzi huu ni kutokana na kitendo alichokifanya Makonda hivi karibuni kuueleza umma kwamba Halmshauri ya Kinondoni imepokea USD 300 kutoka Benki ya Dunia (WB) kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara hali ya kuwa hakupaswa kulizungumzia kwani lipo nje ya uwezo wake,

Ilikuwa bado ni taarifa ya siri lakini akaidukua na kukurupuka kuitangaza, jambo ambalo limesbabisha mtafaruku mkubwa kutoka kwa wajumbe wa Baraza la Madiwani wakihoji kwanini taarifa hizo zitolewe bila ya kamati kupitisha,’alisema.

Jacob alisema kutokana na hatua hiyo, wanamtaka Makonda kutoingilia majukumu yasiyokuwa yake;
“DC hana uwezo wa kupanga bajeti wala kutoa fidia ama kuzungumzia kitu chochote kinachosu Halmshauri hadi aombe ruhusa, pia hakuna mahusiano yoyote baina ya DC huyo na Halmashauri,”alisema

Pia alisema walimvumilia DC kutokana na vitendo vyake lakini kwa sasa wamefikia mwisho na wanamuonya kuacha tabia za udukuzi.

Utapeli
Kuhusu utapeli huo wa Makonda kwa Rais Magufuli alisema kuwa Halmashauri hiyo haina shida ya msaada wowote kutoka kwenye mshahara wa rais.
Alisema halmshauri hiyo inakusanya takribani sh.bilioni 46 kwa mwaka, huku ikipata kiasi cha sh.bilioni 78 ikijumuiha na mishahara ya watumishi, ambapo kwa mwaka inapata sh.bilioni 152.
“Hatukupenda rais atangaze kukata mshahara wake kwa kuwa hatuna shida nao, kama ingekuwa uwezo wetu tungeamuandikia barua asikate bali uende kusaidia Halmashauri ya Ilala na Temeke lakisi sio kwetu,”alisema.
Alieleza kuwa hatua hiyo inatokana na halmashauri hiyo kuwa na pato kubwa isipokuwa lilikwamishwa na uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), uliopita kwa kufanta ubadhirifu wa fedha.

“Mathalani kuna kigogo wa CCM alikuwa anafanya kufuru kwenye ulipaji kodi wa mabango madogo, ambapo tukikusanya kodi zote za mabango kama inavyotakiwa tunapata zaidi y ash.bilioni 10 kwa mwaka,
Ni aibu kuona DC anahangaika na maombi ya msaada kama omba omba hali ya kuwa Halmashauri ina uwezo mkubwa, alitakiwa aje kutuomba ili tumsaidie lakini sio kukimbilia udukuzi ili aonekane anafanyakazi kubwa,”alisema.

Hofu
Jacob alisema kutokana na udukuzi wa Makonda kuhusu taarifa za utekelezaji wa mradi huo, kwa sasa wajumbe wa Kamati ya Fedha wana hofu dhidi ya Baraza la Madiwani kwa kuwa taarifa zimevuja kabla ya kukaliwa kwa vikao halalali.

Alisema kwa mujibu wa Kanuni za Halmashauri namba 8 ya mwaka 1982 hairuhusiwi mtu yoyote akiwemo Meya na Mkurugenzi kuzungumzia suala la vikao vya halmashauri nje ya vikao, lakini Makonda amediriki kufanya hivyo.

 “Siku zote Mgema akisifiwa Pombe huitia maji, ndio haya anayoyafanya Makonda baada ya kusifiwa na rais kila kazi anajiona anaweza kuifanya ili apate sifa wakati anashindwa kujua baadhi ya vitu si jukumu lake wala havimuhusu,’alisema.

Alisema taarifa za mradi huo (DMDP) zilizosambazwa na Makonda hazikupangwa kwa Kinondoni pekee bali ni mradi uliolilenga jiji la Dar es Salaam, kuwa kama miji mingine mikubwa Duniani ikiwemo Paris Ufaransa, ambapo kuzungumziwa tangu mwaka 2014.
Pia alisema Manispaa imeingiwa na mtanziko kwani Kamati ya Baraza limeanza kuhoji uhalali wa Makonda kuhusu udukuzi huo, hivyo kuna uwezekano wa kupingwa kwa matumizi ya fedha hizo kwenye vikao vya baraza.

“Pia ameibua hofu kwa wananchi wa Bonde la Mto Ng’ombe kwamba watavunjiwa nyumba, hali ya kuwa halmashauri ilishaweka utaratibu wa kuwalipa fidia wananchi hao takribani sh.bilioni 1.7, huku waliokuwa pembezoni mwa barabara zitakazopitiwa na mradi huo watalipwa sh. bilioni 14,”alisema.
Shule

Kuhusu ujenzi wa Shule za Sekondari ambapo Makonda alitangaza arambee ya uchangiaji Saruji, Jacob alisema anachofanya Makonda ni uongo kwa kuwa sio mjumbe wa Baraza la Madiwani kwani hakupaswa kulizungumzia.

“Tangu apokee mifuko ya Saruji hadi sasa hakuna hata mmoja uliopelekwa kwenye shule, anacofanya ni utapeli tu inatakiwa tujiulize kaipeleka wapi labda iwe kwenye ofisi za CCM,”ALISEMA.

Pia alisema Makonda hana uwezo wa kumfukuza hata mfanyakazi wa kufagia katika ofisi za Halmashauri, wala kubanga bajerti ya sh.5000 au kumuwajibisha mtu yoyote kwa kuwa sio ujukumu lake kiutawala wala kisheria.
Hatua

Jacob alibainisha kuwa kutokana na kumuonya mara kadhaa DC huyo endapo akiendelea kufanya udukuzi basi watawaondoa Maafisa tarafa kwenye vikao vya Baraza la Madiwani ambao wamekuwa viunganishi wake,

“Kwa kuwa mihimili hii ni tofauti siwezi kumpigia simu Makonda kumuuliza kwanini amezungumzia hayo bali anatakiwa anitafute baada ya kusikia nimeongea haya,’alisema.
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images