Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

U.S. President Barack Obama Do not Recognise Mr. Museveni As The Elected President of Uganda

0
0
The elections were not free and fair! They were characterised by police brutality and vote rigging. Although Mr. Museveni did all that, Ugandans overwhelmingly voted for Dr. Kiiza Besigye, But the Electoral Commission declared results that were completely different from those got at the polling stations! Therefore, we request that before Mr. Museveni is recognised as Uganda's elected president; All the votes should be recounted by an independent commission to get the actual results!


Talaka ya Jide Mazito Yaibuka!

0
0

Siku chache baada ya staa mwanadada mkongwe wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ kupewa talaka mahakamani na mumewe Gardner G. Habash ‘Captain’ mazito yameibuka baada ya kubainika uwepo wa hati nyingine ya talaka aliyoitoa Gardner kwa mwanamke mwingine, Risasi limeinasa.


Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa mbali ya Jide anayetarajia kuibuka na kishindo kikubwa cha mabadiliko ya muziki wake hivi karibuni, Gardner alimpa talaka mahakamani mkewe wa awali aliyefahamika kwa jina la Idda Pius Mkunja, mwaka 2003.

“Mwenzangu Gardner anaonekana ndiyo kamchezo kake kumalizia ndoa mahakamani, ukiachana na Jide nimeona hati ya talaka nyingine aliyoitoa kwa Idda ambaye alimuona mwaka 1997,” kilisema chanzo hicho huku kikimpenyezea hati hiyo ya talaka (tazama pichani) mwanahabari wetu.

Kama hiyo haitoshi, chanzo hicho kiliweka wazi kuwa Gardner na Jide walishindwana miaka michache tu baada ya kufunga ndoa lakini waliendelea kuishi kwa imani kwamba wanaweza kuelewana lakini haikuwezekana.

“Hii ishu si ya miaka miwili iliyopita kama wengi wanavyojua. Ndoa ilikuwa na figisu muda mrefu sana, walishashindwana sema walifanya siri tu,” kilisema chanzo.

Baada ya kupewa hati hiyo, mwanahabari wetu alimtafuta Gardner ili aweze kuzungumzia suala hilo, simu yake iliita bila kupokelewa.

Chanzo: GPL

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya Februari 22, Ikiwemo ya Jecha Kumgombea Maalim Seif

0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya Februari 22

Wema Sepetu Asema Ataendelea Kukaa Kimya,ila Muacheni Lulu.

0
0
Mastaa ambao wamekuwa wakichonganishwa kwa muda wanazidi kukataa kuonyesha tofauti zozote kati yao, Wema Sepetu amewaponda wanaomsogeza movie staa Lulu kwenye mambo ya mahusiano ya Wema Sepetu.

Haya maneno ya Wema kuhusu issue hii “Leave Her out of This… Please….!!!! @elizabethmichaelofficial Lala kwa Amani baby… Nimesema mimi… People dont know mwanzo wa vitu ila wanaongea as if wanayajua… Mi ntaendelea kukaa kimya ila muacheni huyu mtoto please…“

Taarifa ya Msajili Wa Vyama Vya Siasa Kukanusha Habari Iliyoandikwa Na Gazeti La Tanzania Daima Kuhusu Vyama Kutopewa Ruzuku

0
0
Taarifa ya Msajili Wa Vyama Vya Siasa Kukanusha Habari Iliyoandikwa Na Gazeti La Tanzania Daima Kuhusu Vyama Kutopewa Ruzuku

Kwanini Shaffih Dauda Anasema Abdi Banda wa Simba Alistahili Kadi Nyekundu?

0
0
Jumamosi February 20, 2016 umechezwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya Yanga vs Simba (Dar es Salaam derby) na kuishuhudia Yanga ikipata ushindi wa pilli wa goli 2-0 dhidi ya Simba kwa mara ya pili kwenye msimu huu.

Mengi yamezungumzwa baada ya mchezo huo lakini huu ni mtazamo wangu baada ya kuufatilia mchezo ho kwa umakini mkubwa .

Kabla ya Abdi Banda kuoneshwa kadi nyekundu na kuiacha Simba ikiwa pungufu kwa mchezaji mmoja hali ya mchezo ilikuwaje?

Kabla ya kadi nyekundu kutolewa kwa Abdi Banda, game ilikuwa ime-balance na Simba walikuwa wameitawala Yanga kwenye eneo la midfield lakini baada ya kadi nyekundu ya Banda, ikailazimu Simba kumshusha Majabvi kwenye nafasi ya ulinzi wa kati. Katika eneo la kiungo wakabaki Ndemla, Kazimoto na Mkude Yanga wakawa wengi kwenye eneo la katikati.

Kadi nyekundu iliwaathiri kwa kiasi gani wachezaji wa Simba?

Namna ambavyo wachezaji wa Simba walivyochukulia tukio la kutolewa kwa Abdi Banda iliwashusha morali. Wachezaji wakaona tayari wapo pungufu kwenye mechi kubwa dhidi ya Yanga halafu kadi imetoka mapema ikawavunja ari. Lakini kama wachezaji wangeandaliwa kisaikolojia kabla ya mechi kwamba wanaenda kwenye mechi kubwa, tukio la kadi nyekundu linaweza kutokea wakati wowote, tukio kama hilo likitokea wanachezaje ingeweza kuwasaidia.

Je Banda alistahili kadi nyekundu?

Kadi ya kwanza ya njano aliyooneshwa Banda ukiangalia unaweza kudhani alikuwa ni mtu wa mwisho na kujiuliza kwanini hakupewa straight red card. Kwasababu watu wengi wanavyoelewa ni kwamba ukicheza rafu ukiwa mtu wa mwisho unapata red card. Lakini haiko hivyo, kadi ya njano alistahili. Na nimsifu mwamuzi kwa maamuzi aliyofanya kwa kadi ya kwanza. Kwasababu hata kama Ngoma angefanikiwa kumpita Banda tayari kulikuwa na Juuko ambaye angeweza kuokoa mpira kutoka kwa Ngoma. Kadi ya njano ya kwanza ilikuwa sahihi kabisa.

Kadi ya njano ya pili Banda alistaili bila kujalisha alishapewa kadi ya njano awali. Kwasababu sheria inasemaje? Kama alifanya makosa inabidi aadhibiwe kulingana na makosa yake bila kujali kama tayari anakadi au hana.

Nini kilitakiwa kifanyike baada ya kadi nyekundu ya Banda?

Nilifikiri kocha na benchi lake la ufundi watafanya mabadiliko ya mapema kwa kumtoa striker mmoja na kumuingiza beki moja au kiungo lakini kwenye benchi lao hakukuwa na beki. Lakini ili kuweza kumudu ushindani kwenye eneo la katikati wangemtoa Kiiza au Ajib. Lakini kwa mtazamo wangu wangemchomoa Kiiza halafu waongeze kiungo kwa ajili ya kuongeza ushindani kwenye eneo la katikati.

Wakati huo wanamuongezea majukumu Ajib ya kukimbia na kupambana kwenye eneo la mbele kwasababu aina ya uchezaji wa Ajib angemudu kucheza akiwa mshambuliaji pekee.

Bila shaka yoyote kadi nyekundu aliyopewa Banda mapema iliwaathiri Simba kwa kiasi kikubwa kwa dakika zilizokuwa zimesalia kwenye mchezo.

Angalia video hapa chini uone namna Shaffih Dauda na Ally Mayay ‘Tembele’ walivyo dadavua kuhusu kadi nyekundu aliyooneshwa Abdi Banda.

Diva Loveness Adai Ujumbe wa Kutafuta Mwanaume Aliouandika Kwenye Page yake Alimaanisha..."Hamna Hacker wala Hucker , Hellow It's Me"

0
0
Leo Mchana Diva Loveness wa Clouds aliacha mashabiki wake kwenye sintofahamu baada ya kupost picha akiwa nusu utupu na kusema kuwa anatafuta mwanaume baada ya kukaa muda mrefu single.....baadhi ya mashabiki wake waliingiwa na woga wakidhani account yake imekuwa hacked lakini jioni hii Diva amewahakikishia hakuna cha hacker wala nini....

Divathebawse :
Hamner Hacker wala Hucker , Hellow It's Me ... Diva Ndio Naandika ... Cha ajabu nini? Simu yangu Ninayo Mkonon nimelala kitandani , So this is Me...Siku Hazilingan, kila mtu atafsiri atakavyo , i don care , This is Just life , we live , we gon die anyways .. tunakuwa dissapointed .. sometimes , Yaan mie mwenyewe ndio nafanya hivi and sitak kiki wala nini kick ninazo kibao .... Mpaka zanishinda ati, naandika kwa akili yangu yanatoka Moyoni Mwangu , wala sio ya kushikiwa, Nina Maumivu yangu Moyoni Lakini nina akili zangu timamu, this is My life this is My Page , My life My rules , I can do anything i want with My life, ....niacheni" Divathebawse :

Ali Kiba Adai Yeye Hashindani na Mtu yoyote Katika Game la Bongo Fleva..

0
0
Staa wa bongo fleva Ali Kiba amekiri kuwa ushindani uliopo sasa kwenye muziki wa bongo fleva umemfanya arekebishe vitu kadhaa kwenye muziki wake hii ni pamoja na kufanya video zenye viwango zaidi.

Licha ya kauli yake hiyo Ali Kiba ameweka wazi kuwa ushindani haupo kabisa kwenye akili yake,yaani yeye hashindani na mtu yeyote yule.

“ushindani umenifanya nifanye marekebisho kwa mfano videos na support..Ushindani upo,ni kitu cha kawaida ila haupo akilini..naamini sishindani na mtu” alifunguka Kiba alipoulizwa anaonaje hali ya ushindani kwenye muziki wa bongo fleva.

Mikoa Inayoongoza Kwa Uvivu Tanzania

0
0
Pamoja na serikali kuweka bidii ktk kuwaletea maendeleo wananchi lakini moja ya kikwazo ni tabia ya uvivu ya wananchi.

Serikali inatakiwa kujenga miundo mbinu na wananchi kupitia miundo mbinu hiyo wajiletee maendeleo.

Insemekana mikoa ifuatayo inaongoza kwa uvivu.

1. Dodoma
2. Mtwara
3. Lindi
4. Pwani
5.Tabora
6. Tanga
7. Dar es Salaam
8. Morogoro

Hii mikoa serikali inatakiwa iwekeze kwenye elimu na kazi

Unaweza ongeza mikoa mingine unayo ifahamu.

** wageni wameshikilia maendeleo

Wachimbaji 800 Waweka Kambi Geita Gold Mine Wakisubiri Kugawiwa Mawe ya Dhahabu

0
0
Tamko lililotolewa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wachimbaji wadogo watapewa mabaki ya mawe ya dhahabu maarufu magwangala kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) limesababisha wakazi wa Mtaa wa Nyakabale kufurika mgodini hapo kusubiri ahadi hiyo.

Vijana hao zaidi ya 800 walisema kuwa wamekusanyika kwa kuwa Serikali ilitangaza kutoa magwangala Februari 28.

Akizungumza na umati wa vijana hao Kaimu Ofisa Madini wa Mkoa wa Geita, Fabian Mshai aliwataka vijana hao kuwa watulivu na kutii sheria za nchi kipindi hiki ambacho tume iliyoundwa kufuatilia suala la magwangala, imepeleka maoni kwa katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kujua utaratibu utakaotumika.

Mshai alisema lazima taratibu zifuatwe ili kuepuka kuhatarisha uhai wa wananchi kwa kugombana wakati wakinyang’anyana mawe.

Alisema pia wanaweza kuharibu mazingira kwa kuwa kuna kemikali kali zinazotumika wakati wa uchanjuaji wa dhahabu.

Alisema kitendo kinachofanywa na wachimbaji wadogo walioamua kuanza kuingia katika maeneo ya mgodi na kuchukua mawe ni kukiuka sheria za madini na kuhatarisha maisha yao.

Diwani wa Mgusu, Pastory Ruhusa aliwataka wachimbaji wadogo kuwa watulivu na kuiomba Serikali kuharakisha taratibu za kutoa magwangala kwa kuwa kuna ongezeko kubwa la wananchi kutokana na ahadi waliyopewa.

Alisema, juzi vijana hao walifunga barabara baada ya kuitwa wakimbizi na kusababisha wananchi kushindwa kusafiri kwenda nje ya kijiji na kusababisha usumbufu kwa wagonjwa na wananchi.


Mbunge Hawa Ghasia Aibuka Kidedea Kesi ya Kupingwa Matokeo ya Ubunge.

0
0
Waziri wa zamani wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Hawa Ghasia, ameshinda kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa dhidi yake na wanachama wawili wa Chama cha Wananchi (CUF) katika Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, kupinga kuchaguliwa kwake kuwa Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini.

Ushindi huo unatokana na uamuzi uliotolewa na Jaji Fauz Twaib, baada ya kutupilia mbali maombi ya kupunguziwa gharama za kesi yaliyowasilishwa mahakamani hapo na wanachama hao kutoka chama cha upinzani, Alli Mohamed Lipemba na Bora Abdallah Mkonda.

Jaji Twaib alikubaliana na pingamizi la awali lililowasilishwa na wakili wa Ghasia, Samson Mbamba, ambaye aliiambia mahakama kuwa maombi ya kupunguziwa gharama yalikuwa yamewasilishwa nje ya muda unaotakiwa kisheria.

Mbamba alieleza kuwa kwa mujibu wa Sharie ya Uchaguzi, mwombaji anapaswa kuwasilisha maombi ya kupunguziwa gharama ndani ya siku 14 tangu shauri la kupinga matokeo linapofunguliwa mahakamani. 

Kwa mujibu wa kumbukumbu za mahakama, waombaji walifungua kesi ya uchaguzi Novemba 25, 2015, ambapo siku 14 ziliishia Desemba 9, 2015, ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuwasilisha  maombi ya kupunguziwa gharama. 
Lakini waombaji waliwasilisha maombi yao Desemba 10, 2015.

Kufuatia uamuzi huo wa mahakama, kesi ya uchaguzi nayo imekufa na hivyo kumfanya Mbunge huyo mteule aliyechaguliwa kwa tiketi ya Chama Cha Mapindzi (CCM) kwa kura 24,258 kuendelea kushikila jimbo hilo.

Mpinzani wake kutoka CUF aliambulia kura 22,615 katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015.

Wanachama hao wa CUF walidai kuwa matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi yalighubikwa na dosari nyingi ambazo zilijitokeza tangu wakati wa kampeni, siku ya uchaguzi na mchakato mzima wa ujumlishaji na hivyo kufanya shughuli nzima kuwa batili.

Walidai kuwa jumla ya kura zilizotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi kumfanya Ghasia mshindi hazikulingana na zile zilizokuwa zimebandikwa kwenye vituo katika jimbo zima.

Kwa mujibu wa wanachama hao, mgombea kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alijitoa kwenye kinyang’anyiro hicho na alitoa taarifa kwa Msimamizi wa Uchaguzi kuhusu kujitoa kwake.

Lakini cha kushangaza Msimamizi wa Uchaguzi katika jimbo hilo hakuondoa jina la mgombea wa Chadema katika orodha ya wagombea na katika uchaguzi huo alipata kura 793.

Kutokana na dosari hizo na nyinginezo, ziliwafanya wanachama hao wawili wa CUF kukimbilia mahakamani kupinga matokeo hayo ya uchaguzi dhidi ya Ghasia na walalamikiwa wengine wawili, akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Wabunge wa Upinzani Waingia na Mabomu ya Machozi Bungeni...Wavaa Gas Mask na Kuyalipua...

0
0
Hili ni bunge la Kosovo, nchi iliyojipatia uhuru mwaka 2008 baada ya Yugoslavia kusambaratika. Bunge la Kosovo ni bunge linaloongoza kwa vituko barani Ulaya.

Kwa muda mrefu kumekuwa na mvutano mkali bungeni kati ya Serikali na wabunge wa upinzani. Hoja kuu ya upinzani ni Serikali itoe ufafanuzi kwanini nchi yao ya Kosovo imekithiri kwa rushwa, ubadhirifu, ukosefu wa ajira na umasikini.

Tarehe 19 Februari mwaka huu bila kutarajiwa wabunge wa upinzani waliamua kuingia bungeni huku wakiwa wamejihami kwa kuvaa vifaa vya kuzuia gesi (gas mask) na kuanza kuwarushia wabunge wa chama tawala mabomu ya machozi.

Huu Ndio Uamuzi wa Tip Top Kuhusu Dogo Janja Baada ya Kulalamika Kuwa Wanambania

0
0
Baada ya kuvuja kwa sauti ya Dogo Janja akilalamika (kwa demu) kuhusu uongozi wake wa Tip Top connection kumbania, Madee ametoa uamuzi walioamua kuuchukua.

Madee alianza kwa kusema kuwa hakuwa na taarifa yoyote juu ya malalamiko yoyote ya Dogo Janja kubaniwa mpaka alipokutana nayo kwenye audio hiyo iliyosambaa mitandaoni, na kuongeza kuwa siku moja kabla ya audio hiyo kuvuja alikuwa na Dogo Janja wakimalizia video ya wimbo wake mpya na hakujua kama kuna tatizo lolote.

Hii ndio kauli ya Madee kuhusu uamuzi wa Tip Top juu ya Janjaro;

“Mimi nabaki kwenye maamuzi ambayo tumeshaongea na Tale, kwamba hatuwezi kutoa maamuzi ambayo wao wanadhania yatakuwa ni ya kumkandamiza moja kwa moja Dogo Janja, kwa sababu sawa, mwanaume kama mwanaume unapoamua kutongoza unatumia mbinu zako nyingine nyingi tu, yeye ndio ile mbinu ambayo aliona anaweza.” alisema Madee.

“Lakini kama kazi zake sisi tumezifanya na tumeshafanya kila kitu video tayari kwahiyo sidhani kama kweli yale maneno yametoka moja kwa moja kwenye moyo wake kina Madee wananibania wakati tayari kazi zake zimeshafanywa na ratiba yake imeshafanywa, nachoamini mimi ni kwamba alikuwa anataka kumuwin tu Yule mwanamke, lakini kikubwa ambacho amehaaribui ni matusi pamoja na kutoa siri ambazo yeye anaona ni sawa kuzisema.” Alieleza Madee.

Licha ya Janjaro kufanya hayo, Madee amesema kuwa hawatasitisha kutoa kazi zake ambazo tayari zilikuwa kwenye ratiba ya kutoka.

“Ratiba lazima ziendelee kwasababu tayari tumeshapata hasara tumeshatoa hela za kufanya audio , video ratiba itaendelea lakini lazima Dogo Janja atakuwa chini ya adhabu.” alisema Mdee


Nuh Mziwanda – Shilole Kanifanya Nishindwe Kununua Hata Feni Amwomba Radhi Mama yake...Kwa lipi?

0
0
Msanii wa bongo fleva Nuh Mziwanda amefunguka na kusema kuwa mpenzi wake wa zamani Shilole alikuwa hataki yeye amiliki kitu chochote kwa kuhofia kwamba anaweza kumkimbia iwapo atafanikiwa.

Msanii huyo pia amemwomba radhi mama yake na ndugu zake ambao kila siku walikuwa wanamsihi ajipange lakini yeye alikuwa anawachukulia poa na kusema amejifunza mengi.

Nuh alifunguka hayo wakati akilelezea kitu gani kilimfanya asijipange vizuri kimaisha.Msanii huyo alifunguka na kusema
“Ni kweli nilikuwa naishi kwa mwanamke wangu na alikuwa hataki ninunue hata feni..wazazi wangu walikuwa wakiniimiza kujipanga,leo nimeyaona.Namwomba msahamaha mama yangu,ndugu zangu marafiki zangu walikuwa wakinipa ushauri mimi nikawa naona nimepata kumbe nimepatikana” alifunguka Nuh na kusema kwa sasa maisha yake yamekuwa mazuri hata mashabiki zake wanamkubali zaidi.

Lulu Michael Azushiwa Kifo....Asema "Kufa, Nitakufa SIKATAI Lakini Mpaka Nimalize Miaka Niliyoandaliwa"

0
0
Kwenye ukurasa wake wa instagram Lulu ameandika maneno hayo huku akionyeshwa kuchukizwa na kitendo hicho cha kuzushiwa kifo, na kujisifia kuwa ana jina maarufu.

"Nasikia Nimekufa, wewe uliye Post hii Kama wewe utakuwepo tutaonana tena 2017 Inshaallah, halafu jifunze na kuandika Elizabeth vizuri kwanza (Niki report live kutoka heaven), this shows how jina langu lina KiKi, nishasema mniache jamani, kufa ntakufa sikatai lakini mpaka nimalize miaka iliyoandikwa kwenye biblia", aliandika Lulu.

Maneno hayo ya Lulu yameibua hisia za watu na kumjia juu mtu aliyepost taarifa hiyo kwenye mitandao, huku wakimtaka Lulu kutopigizana nao kelele kwani yeye ni kioo cha jamii hivyo ni kawaida kwa kuzushiwa taarifa za uongo.


ACT-Wazalendo Watoa Msimamo wao Baada ya Jecha Kusema Hakuna Chama Kilichojitoa Uchaguzi Zanzibar...

0
0

ACT-Wazalendo
TAARIFA KWA UMMA:
Tumekuwa tukipokea simu za waandishi mbali mbali baada ya kauli ya jana ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC),Jecha Salum Jecha kuwa hakuna chama kilichojitoa katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika machi 20 mwaka huu
Msimamo wa ACT-Wazalendo ni kuwa hatutashiriki Uchaguzi huo kama ilivyoazimiwa katika kikao cha kamati kuu cha february 14 mwaka huu
Hatushiriki kwa kuwa tunaamini kuwa hakuna sababu ya kufanyika uchaguzi mwingine nje ya ule uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana
Taarifa hii ya kutoshiriki uchaguzi wa machi 20 mwaka huu imewasilishwa katika ofisi ya ZEC Zanzibar february 9 mwaka huu baada ya wao kututaka tuthibitishe kwa maandishi kama tutashiriki au la
Hivyo kauli ya Jecha kuwa hakuna chama kilichofuata utaratibu ni muendelezo mwingine wa kutaka kuhalalisha haramu kuwa halali kama walivyofanya katika kufuta uchaguzi wa Oktoba 25
Kwa kuthibitisha dhamira yetu hii ya kutoshiriki hivi karibuni kamati Maalum ya uongozi Zanzibar ilimsimamisha uanachama ndugu Khamis Idi Lila,aliyedhaminiwa na chama kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar katika uchaguzi uliofutwa kwa "Zengwe" hivyo hatuna mwanachama anayewania nafasi hiyo
Jecha amezungumzia Sheria ya Uchaguzi na wajibu wa mgombea aliyedhaminiwa na chama kuthibitisha ushiriki wake,huku akiacha kwa makusudi kuainisha udhamini huo ni katika uchaguzi gani
ACT-Wazalendo haijamdhamini mwanachama wake yeyote kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa Machi 20 na hili lilipewa msisitizo katika kikao cha kamati kuu iliyofanyika february 14 na taarifa kutolewa kwa umma siku iliyofuata
Tunaomba wananchi wapuuze ulazimishaji huu wa ZEC kwa kutaka kuionesha dunia kuwa vyama vimeshiriki uchaguzi huo haramu
ACT wazalendo katika kikao chake cha kamati kuu iliazimia kuwa haitakuwa muhuri wa kuwasafisha wabakaji wa Demokrasia kwa kushiriki uchaguzi wa Machi 20
Abdallah Khamis
Afisa Habari
ACT Wazalendo 

Kesi Ya Kafulila Yahirishwa Mpaka March 9, 2016 Baada Ya Mawakili Wa Serikali Kutofika Mahakamani Leo

0
0
KESI No. 2 ya mwaka 2015 ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Kigoma kusini iliyofunguliwa na mlalamikaji  David Kafulila dhidi ya mbunge Hasna Mwilima,Msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria mkuu wa serikali imeahirishwa leo na mahakama kuu kanda ya Tabora mpaka  marchi 9, mwaka huu itakapoanza kusikilizwa tena.

Kesi hiyo ambayo ilikuwa  ianze mapema leo katika mahakama ya hakimu mkazi Kigoma,  Mbele ya Jaji Dr Wambari ambae pia ni Mkuu wa chuo cha sheria lushoto mkoani Tanga, imeahirishwa kwasababu mshatakiwa Hasna pamoja na wakili wake Kennedy Fungamtama pamoja na mawikili wa serikali kushindwa kufika mahakamani hapo, kwa madai ya kuchelewa kupata wito wa mahakama hiyo, huku mlalamikaji David Kafulila akifika na wakili wake Prof Safari.

Katika mazingira hayo Jaji Wambari aliagiza mawasiliano yafanyike kwa pande hizo ili kujua ni lini kwa hakika mawakili hao wataweza kushiriki katika kesi hiyo.

Kutokufika kwa mlalamikiwa  na mawakili wake na wale wa upande wa serikali ilipelekea zoezi la kusikiliza kesi hiyo kusimama kwa saa mbili kutoka saa tano asubuhi  mpaka saa saba mchana na baada ya hapo hakimu mfawidhi wa Mkoa wa Kigoma kwa niaba ya Jaji silivesta Kahinda alisema  kuwa kesi itaendelea march 9 mwaka huu na kwamba kwakuwa tarehe hiyo imependekezwa na mawakili na pande zote mbili.

Akiongea na mtandao huu mlalamikaji wa kesi hiyo David Kafulila alisema kuwa anakubaliana na uamuzi wa mahakama hivyo aliwataka wananchi wawe na subiri hadi hiyi tarehe 9 march mwaka huu.

Bodi ya Wakurugenzi wa Magazeti ya Serikali,(TSN) Yamsimamisha Kazi Mhariri Mtendaji

0
0
BODI ya wakurugenzi wa magazeti ya Serikali,(TSN) imemsimashisha kazi Mhariri Mtendaji wa magazeti hayo Bw Gabrieli Nderumaki kupisha uchunguzi kutokana na utendaji usioridhisha ndani ya kampuni hiyo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw Prof Moses Warioba amesema hatua za kumsimamisha kazi Mhariri Mtendaji huyo umetokana na kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambapo nafasi yake itachukuliwa na Naibu Mhariri Bi Tumma Abdalah.

“Kumekuwa na mambo mengi yanayofanyika bila kufuata utaratibu ndani ya kampuni hii ikiwemo wafanyakazi kutoelewana na menejimenti katika kulipwa stahili zao, pamoja na wafanyakazi kupewa majukumu ambayo hawana uwezo wa kuyatekeleza”.Alisema Prof Warioba.

Aidha Prof Warioba ametengua uteuzi wa Bw Felix Mushi aliyekuwa Meneja mauzo na masoko katika kiwanda cha uzalishaji kwa kukosa sifa na utendaji mbovu uliopelekea kampuni kushuka katika uzalishaji.

Hatua hiyo ya kuwawajibisha watendaji hao imetokana na Ziara ya Mhe. Nape Nnauye Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika Kampuni hiyo ambapo pia hakuridhiswa na utendaji mbovu uliopelekea wafanyakazi 21 kuacha kazi.

“Nataka Bodi itafakari juu ya malalamiko yaliopo kwa wafanyakazi na wachukue hatua kabla mimi sijakutana na wafanyakazi hao wiki ijayo ili kujua mapungufu yako wapi.”Alisema Mhe Nape.

Hata hivyo Bodi hiyo ya wakurugenzi inaendelea kutafuta namna ya kuboresha utendaji ndani ya kampuni ili iendane na kasi iliyopo katika uzalisahaji wa magazeti kwa kiwango kikubwa.

Ray Kusaka Ubalozi Kwenye Makampuni ya Maji..Baada ya Ishu yake ya Kunywa Maji Ku Kiki

0
0

Baada ya kauli ya msanii wa bongo muvi Ray kigosi kuwa gumzo kila kona msanii huyo amesema amepata wazo la kufanya biasahra kupitia kiki hiyo.

Ray amesema amepata mawazo kutoka kwa watu wengi na yeye yuko kwenye mpango wa kuzungumza na makampuni yanayouza maji ili aweze kuyatangaza au anaweza kutengeneza documentary inayoelezea umuhimu wa kunywa maji na kuomba air time kwenye vituo vya televisheni

“Nimepata mawazo kutoka kwa watu wengi,ulaya ingekuwa ni kitu kikubwa lazima makampuni yangenifuata niwafanyie matangazo lakini kwetu Afrika bado..naweza kwenda kampuni yoyote kuomba sponsorship nikapata au kutengeneza documentary ya umuhimu wa maji nikapeleka kwenye TV nikapata pesa” alifunguka Ray ambapo wiki iliyopita alisema anakunywa sana maji ndio mana anakuwa mweupe kufanya kauli hiyo kuwa gumzo kwenye mitandao.

Kikosi cha Polisi cha Wanamaji Kimekamata Shehena ya Mizigo Isiyolipiwa Kodi Bandarini DSM

0
0

Kikosi cha Polisi cha wanamaji kimekamata jahazi likiwa linatokea bandari ya Zanzibar kwenda bandari ya Dar es Salaam likiwa limesheheni bidhaa mbalimbali zikiwemo spika za redio na friji wakati jahazi hilo liliondoka bandari ya Zazibar kibali chake kikionyesha kuwa limebeba mafuta ya marashi.

Ripota wetu alifika makao makuu ya kikosi hicho na kukuta jahazi hilo linaloitwa Najat likiwa limejaa vifaa hivyo huku polisi na wafanyakazi wa jahazi hilo wakisaidia kushushwa kwa vifaa hivyo ambapo kamanda wa kikosi hicho Semboje Kanga amesema nyaraka za mzigo haziendani na kilichobebwa

Katika hatua nyingine wenye mzigo huo wamejitokeza na kusema kuwa wananyaraka zote muhimu na wanashindwa kuelewa kwa nini polisi wanasema shehena hiyo wanamashaka nayo.

 

Naye mliki wa chombo hicho kilichokamatwa Bw Iddy Hadibu amesema kilichotokea ni kwamba wakati wanakuja bandari ya Dar es Salaam baharini wakakuta chombo kingine kimelemewa na mzigo na ndio wakawasaidia ili wasipate shida na hapo ndipo walipojikuta wanaingia katika dhahama hiyo.
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images