Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Ester Bulaya Atamba 'Nitaendelea Kumgaragaza Wasira Ubunge wangu si Wakuchakachua'

$
0
0

Mbunge wa Bunda Mjini, mkoani Mara, Esther Bulaya (Chadema), ametamba kuwa ataendelea kumshinda mpinzani wake kisiasa, Stephen Wasira (CCM), kwa madai kwamba alipata ubunge huo kihalali.

Bulaya alisema hayo jana ikiwa ni siku moja tangu kutupwa kwa rufaa ya wanachama wa CCM waliokuwa wakipinga ushindi wa mbunge huyo alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 dhidi ya Wassira na wagombea wa vyama vingine.

Mbunge huyo aliiambia Nipashe kwa njia ya simu kutoka jimboni kwake kuwa, alimshinda Wasira kwa wananchi, akamshinda kisheria, lakini hakuridhika akakata rufaa na ameendelea kumshinda.

"Kama ana mpango wa kukata rufaa nyingine aende akate tu, lakini akumbuke kuwa nitaendelea kumshinda tu kwa sababu ubunge wangu sio wa kuchakachua bali nimeupata kutokana na kura za wananchi wa Bunda Mjini," alisema Bulaya na kuongeza:

"Siku zote nimekuwa nikisema kuwa waliofungua kesi sio wanachama wa CCM bali ni Wasira mwenyewe, ndio maana akawa mkali kupigwa picha na waandishi ili Watanzania waendelee kudhani kwamba hayumo katika kesi hiyo," alisema.

Alisema wakati umefika sasa mwana siasa huyo mkongwe kupumzika na kula mafao yake, kwa kile alichosema ametumikia taifa kwa muda mrefu na sasa ni zamu ya wengine kumpokea kijiti ili kuanzia pale alipoachia.

"Pamoja na hayo ninamkumbusha kuwa siku zote mahakama husimamia haki ndio maana ameshindwa mara mbili katika kesi hii, hivyo hana budi kupumzika," alisema.

Januari 25 mwaka huu, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilitupilia mbali kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na wapigakura Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagira kupinga ubunge wa Bulaya.

Bulaya alihama CCM na kujiunga na Chadema katikati ya mwaka jana na kuteuliwa na Chadema kuwania ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini na kufanikiwa kumbwaga mkongwe huyo kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.

Njama za CCM Uchaguzi Ujao wa Meya Dar

$
0
0

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewataka wananchi kutohofia vitisho vilivyopangwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salam unaotarajiwa kufanyika kesho,

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Saalam Salim Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Chadema amesema, zipo tetezi kwamba CCM wamepanga kufanya fujo katika uchaguzi huo ili kupora ushindi wa Chadema.

Amesema, licha ya wajumbe wa vyama vinavounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kuwa wengi kuliko wa CCM, bado serikali kwa kushirikiana na CCM wamepania kukamata wajumbe wa UKAWA ili kupunguza idadi ya wapiga kura.

Nakwamba, kutokana na kikao kilichokaliwa wiki iliyopita kikiwajumuisha wajumbe wanasiasa kutoka vyama vyote vya upinzani (UKAWA) kiliazimia, washiriki watakao shiriki kumchagua meya ni wale tu waliowachagua mameya wa Manispaa, hivyo wajumbe toka Zanzibar hawataruhusiwa kupiga kura.

“Jumla ya wajumbe ni 161 kwa jiji zima la Dar es Salaam ambapo, kwa upande wa Kinondoni kuna wajumbe 58 ambapo CCM wapo 20 na ukawa 38, Temeke jumla ya wajumbe 49, CCM wapo 31 na ukawa 18 na Ilala jumla ya wajumbe 54 huku CCM wakiwa 23 ukawa 31. Ni dhairi kuwa tumewashinda ila hawataki kukubali na kuachia madaraka,” amesema Mwalimu.

Pia amesema, CCM wanampango wa kuvunja la Dar es Salaam kwa kisingizio kuwa madiwani na wabunge wameshindwa kupiga kura, kwa hivyo wanampango wa kuunda Tume ya Jiji itakayokuw chini yao.

“Nitoe wito kwa wananchi, watakaohudhuria uchaguzi wa kesho wawe makini, kwani kunampango wa CCM kuwaleta maaskari wengi wenye silaha ili kuwatishia wananchi wenye haki ya kushiriki.”

Nay wa Mitego Adai Muziki wa Sasa ni ‘Ujanja Ujanja’ Sio Uwezo

$
0
0

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego amesema muziki wa sasa hivi ukileta ufundi na kujifanya unaweza sana kuchana na kuandika hautafika popote.


Nay wa Mitego amedai ili kwenda kibiashara msanii unatakiwa kubadilika ili kwenda sambamba na mahitaji ya soko.

“Muziki wa kipindi cha nyuma ulikuwa wa serious sana, ulikuwa unahitaji uumize sana kichwa ili ufanye kitu kizuri japo ulikuwa hauna hela, lakini muziki wa sasa hivi ni muziki wa ujanja ujanja mwingi, ukiwa na akili nyingi, ukiwa mjanja basi unamake mkwanja. Kwa hiyo naweza nikasema muziki wa sasa hivi una hela sana kuliko wa zamani lakini ili uzipate unatakiwa kuwa mjanja, unaweza ukawa unachana sana, unaandika sana lakini ukatoka bila,” alisema Nay.

Aliongeza, “Muziki wa sasa hivi ukidumu kwa muda mrefu ni miezi mitatu, lakini nyimbo nyingi za zamani zitaendelea kuwepo kwa sababu wasanii wake walikuwa hawana ujanja ujanja, wanaandika kweli na wanazingatia kila kitu katika uandishi,” alisema Nay.

Wabogojo Afichua Sira Adai Jela Imempenda Jack Cliff Amezidi Kuwa Mrembo

$
0
0

Mkali wa mchezo wa sarakasi Bongo, Athumani Ford ‘Wabogojo’ anayefanya kazi za sanaa nchini China, amefunguka mambo kadhaa ya mwanamitindo Jacqueline Cliff ambaye amefungwa nchini humo kwa kosa la kukamatwa na madawa ya kulevya.

Wabogojo ambaye amekuja Bongo kwa ajili ya mapumziko mafupi, alisema kuwa mrembo huyo anaendelea vizuri sana gerezani na ni mtu ambaye ameshazoea hali ya huko na amekubaliana na ukweli halisi na amezidi kuwa mrembo tofauti na watu wanavyodhani.

“Kitu kizuri sana ni kwamba Jack yuko vizuri sana, amezidi kuwa mrembo maana wengi wanajua mtu ukienda jela ni kuchakaa tu lakini siyo kwa Jack kwa sababu ameshakubaliana na yalitokea, ananawiri,” alisema Wabogojo.

Msanii huyo aliendelea kusema kuwa, kwenda kwake gerezani mara kwa mara, kunamfanya mrembo huyo kujisikia vizuri sana na kujiona kama yuko nyumbani na mara nyingi hapati muda wa kuwaza mambo ya huzuni kutokana na kifungo hicho.

“Hakuna kitu anachofarijika Jack kama akiniona pale, anapata faraja ya ajabu sana na mimi nitakuwa nafanya hivyo mpaka muda wangu wa kuishi nchini humo uishe kwa sababu hata mimi najiona fahari kutenda hivyo,” alisema Wabogojo.

Katika barua yake ya hivi karibuni aliyowaandikia Watanzania akieleza hisia zake na maisha yake kwa ujumla, Jack aliwashukuru watu wanaomtembelea gerezani akiwemo Wabogojo.

Chanzo:GPL

Mawaziri Wote Waliopewa Hadi Leo Jioni Kujaza Na Kurejesha Tamko La Mali Na Madeni, Hati Ya Uadilifu Wametekeleza Agizo La Rais Katika Muda Muafaka

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema agizo lilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli la kuwataka mawaziri ambao hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni wakamilishe kabla ya saa 12 leo jioni limetekelezwa.

Waziri Mkuu amepokea barua kutoka kwa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji (Mst.) Salome Kaganda ikithibitisha kuwa mawaziri na naibu mawaziri wote wametekeleza agizo hilo.

“Hadi kufikia saa 9.30 leo alasiri (Ijumaa, Februari 26, 2016) mawaziri wote walikuwa wamekamilisha fomu zao za kuzikabidhi katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,” alisema Waziri Mkuu.

Rais Magufuli leo asubuhi alitoa maelekezo kwamba Mawaziri ambao hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni ifikapo leo Ijumaa tarehe 26 Februari, 2016 saa 12.00 jioni wawe wamejaza na kurejesha Fomu ya Tamko la Rasilimali na Madeni katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Dar es Salaam. Waziri ambaye atashindwa kutekeleza agizo hili atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi yake.

Mawaziri waliotakiwa kurejesha fomu za tamko la rasilimali pamoja na hati ya ahadi ya uadilifu kuwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga na Waziri wa Nchi (OMR – Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba. 

Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga ambaye alitakiwa kurejesha hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako ambaye alitakiwa kutoa tamko la rasilmali na madeni.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi (OMR – Mazingira), Mhe. Luhaga Mpina alitakiwa kurejesha fomu za tamko la rasilmali na madeni pamoja na hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,11410 DAR ES SALAAM.
IJUMAA, FEBRUARI 26, 2016

Orodha Ya Majina ya Wanafunzi wa St. Joseph Kampasi ya Songea Waliohamishiwa Vyuo Vingine Baada ya TCU Kukifuta Chuo Hicho

$
0
0
The Tanzania Commission for Universities (TCU) wishes to inform the general public and particularly students, who were undertaking their studies at St Joseph University College of Agricultural Sciences and Technology (SJCAST) and St Joseph University College of Information Technology (SJCIT) in Songea, that we have transferred the respective students to other universities. 

These students are required to report to the receiving institutions upon the opening of the second semester.

The dates for opening of the second semester for each receiving institution will soon be communicated through TCU website and websites of respective institutions.
Meanwhile, TCU hereby releases the list of names of the transferred students, which contains receiving institutions and the programmes they have been transferred to.
TCU would also like to inform respective students including those with Diplomas that there are names of some students, which are yet to be posted as we are continuing with the verification of their data. 

These names shall be posted as soon as the verification exercise is completed.
For further information or clarification please contact the Tanzania Commission for Universities through the following numbers;

Landline: +255 (0) 222 772 657 
Hotlines : +255 (0) 683 921 928
                +255 (0) 675 077 673

Mrembo Kajala Afunguka..Adai Usichana Wake Umepotea Aamua Kuyapa Mambo ya Mjini Kisogo

$
0
0
Staa wa Filamu Bongo, Kajala Masanja amesema kuwa mambo ya kimjini kama wafanyavyo mastaa wengine kwa sasa ameyapa mgongo kwa madai kuwa anaona anaelekea kuzeeka.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Kajala alisema kila anapojiangalia anaona kabisa alivyokuwa zamani sivyo alivyo sasa hivyo ana kila sababu ya kubadilika.

“Kiukweli najiona kabisa naelekea kuzeeka, ule usichana unapotea hivyo ni vyema sasa mambo mengine ya kimjini nikayapa kisogo. Kwenda klabu usiku nimepunguza na kuna siku nitaacha kabisa, nguo za ajabuajabu najifikiria mara mbilimbili,” alisema Kajala.

Rais Magufuli Atumbua Mapapa Wauza ‘Unga’..Adai Haiwezekani Wauza Unga Wakawa na Nguvu zaidi ya Serekali

$
0
0
Kasi ya Rais John Magufuli ya kutumbua majipu sasa imeanza kuvunja mtandao wa dawa za kulevya (unga) nchini, uchunguzi wa JAMHURI umebaini.

Rais Magufuli ametoa maelekezo mahsusi kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga akielekeza kuwa anataka kuiona Tanzania isiyokuwa na wauzaji na watumiaji ‘unga’.

Rais amenukuliwa akisema haiwezekani wauza unga wakawa na nguvu kuliko Serikali.

Tayari maofisi wa Serikali wameanza kulifanyia kazi agizo hilo kimyakimya na kwa kasi ya aina yake, ambako sasa wanakwenda nyumba hadi nyumba wakihoji wafanyabiashara wenye ukwasi usioelezeka na katika kufanya hivyo wamekutana na ‘maajabu’.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi imeanzisha operesheni ya kukamata wafanyabiashara wote wanaohusishwa na dawa za kulevya jijini Dar es Salaam.

Katika operesheni hiyo, tayari polisi wamekamata ‘mapapa’ wawili wanaoelezwa kuwa miongoni mwa ‘mapapa’ wa biashara hiyo haramu nchini. Mapapa hao wanashikiliwa Kituo cha Polisi Oysterbay, Kinondoni.

Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni umeanza msako mkali wa kimyakimya kwa wafanyabiashara hao; operesheni inayoelezwa kuwa inahusisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Idara ya Usalama wa Taifa na kitengo maalum kutoka Ikulu.

JAMHURI limethibitishiwa kuwa Hemed Horohoro na Lwitiko Samson Adam, ni kati ya mapapa waliokuwa wakisakwa kwa udi na uvumba na sasa wametiwa nguvuni.

Lwikito ambaye anaelezwa kuwa na makazi nchini Afrika Kusini, alikamatwa nyumbani kwake Magomeni jijini Dar es Salaam. ‘Papa’ huyo, amekutwa kwenye ‘nyumba ya ajabu’.

“Huwezi kuamini. Lwitiko aliishi maisha ya peponi. Ukiiona nyumba yake pale Magomeni, nje si nyumba ya maana, lakini ukiingia ndani utashangaa. Nyumba imejengwa chini ya ardhi (underground). Huko kuna maisha ya peponi.

“Kule chini ya ardhi ana bwawa kubwa la kuogelea huko huko, baa na magari yote ya kifahari yapatayo manane tuliyakuta huko chini ya ardhi, tulistaajabu,” anasema mmoja wa watu waliofanya kazi ya kumkamata.

Magari yaliyokuwa huko chini ya ardhi mengine yana thamani ya hadi Sh milioni 500. JAMHURI limefanikiwa kupiga picha sehemu ya magari hayo katika Kituo cha Polisi Oysterbay, ambayo yamo BMW X6, Lexus, Lumma CLR RS, Cooper na mengine ya kifahari.

Wakati Lwitiko akikamatwa na baadhi ya mali zake, Hemed alikamatwa na gari moja ambalo nalo pia linashikiliwa katika kituo hicho.

Watuhumiwa hao waliokamatwa wanatajwa kuwa wamekuwa wanauza dawa aina ya heroine kutoka Pakistan; cocaine kutoka Brazil, huku wakiishi maisha ya kifahari nchini Tanzania na Afrika Kusini.

Katika kinachohofiwa kuwa taarifa zimevuja ukamataji ulipoanza wiki iliyopita, kundi kubwa la wafanyabiashara waliolengwa lilikimbia nchi.

“Wengi wamekwenda Kenya na Afrika Kusini. Weengine wameikimbia Dar es Salaam, taarifa za kiintelijensia zinaonyesha wako mikoani, lakini kwa vyovyote vile chini ya Rais [John] Magufuli wanapoteza muda. Watakamatwa tu,” amesema mtoa habari wetu.

Kamanda wa Polisi Kanda ya Kinondoni, ACP Christopher Fuime, anasema ukamataji huo ni endelevu, lakini hakutaka kuingia kwa undani zaidi akisema wananchi wasubiri kuona ‘wazungu wa unga’ wote wanapotea mtaani.

Anasema kuwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya si watu wadogo, bali wana uwezo na wanamiliki mtandao mkubwa, hivyo kukabiliana nao kunahitaji “muda na usiri mkubwa”.

Alipoulizwa ni lini wanatarajia kuwafikisha mahakamani ‘mapapa wawili’ waliokamatwa, amesema hawezi kuzungumzia hilo kwani upelelezi bado unaendelea na kwamba unahusisha taasisi nyingi, hivyo ni vigumu kubainisha hilo.

Hata hivyo, amekiri kukamatwa kwa Horohoro na Lwitiko na anasema: “Hapa tunafuatilia mambo mengi. Tunavyopeleleza kesi za dawa za kulevya tunaangalia umiliki wa mali, utakatishaji wa fedha, na mambo mengine mengi. Ila kwa sasa tumeamua ingawa wengine wanakimbia baada ya kubonyezwa, lakini hiyo siyo tatizo,” anasema Kamanda Fuime.

Katika eneo la kutakatisha fedha za dawa za kulevya, uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya wanamiliki mabasi yanayofanya kazi ya daladala jijini Dar es Salaam na mengine yanakwenda mikoani.

“Mabasi haya mengi yanatoka Mbagala kwenda Posta, yameandikwa jina la moja ya taasisi kubwa za uzalishaji mafuta duniani, na pembeni yameandikwa majina yao kwa kuongeza herufi mbili mwishoni tu zisomekazo ‘so’. Huyu anaingiza hadi kilo 500 ze heroine kutoka Pakistan, na fedha anazopata anazitakatisha kwa kuonyesha anafanya biashara ya daladala na mabasi ya mikoani,” amesema mtoa habari wetu.

“Wiki iliyopita, Wapakistani sita wameingiza kilo 500 za heroine, wakahifadhi robo Segerea jijini Dar es Salaam, nyingine zimehifadhiwa Pemba, nyingine Zanzibar na nyingine zipo kwenye boti majini hazijaingia nchini,” kiliongeza chanzo chetu.

Ukiacha magari, wanaouza dawa za kulevya wanajenga majengo makubwa katika miji ya Dar es salaam, Zanzibar, Arusha, Mwanza, Tanga na Mbeya, kisha wanatumia majengo hayo kudanganya umma kuwa fedha zao zinatokana na kodi ya pango.

Kamanda Fuime, alipoulizwa mkakati wa kupambana na wauzaji waliotajwa kuikimbia nchi, amesema kuzungumzia hilo ni sawa na kuanika mipango ya polisi; jambo ambalo si sahihi.

Miezi miwili iliyopita polisi nchini walifanya uhamisho kwa askari wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni na Tanga kuvunja mtandao wa uhalifu, hususan dawa za kulevya ndani ya Jeshi hilo.

Asilimia kubwa ya ‘mapapa’ wa biashara hiyo haramu wapo jijini Dar es Salaam, hasa maeneo ya Kinondoni, Magomeni na Mbezi Beach.

Waziri Kitwanga ameshakabidhiwa orodha ya polisi wanaojihusisha na biashara hiyo haramu ambako majina hayo aliyakabidhi kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Inspekta Jenerali Ernest Mangu.

Baada ya IGP Mangu kukabidhiwa majina hayo, aliwataka askari wa Oysterbay kumkabidhi orodha ya majina ya wauza ‘unga’ haraka.

Mpango huo ulienda sambamba na kuwapangua baadhi ya polisi walioonekana kushindwa kuukabili mtandao wa wauza ‘unga’.

Maofisa waliohamishwa ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) wa Kinondoni Camillius Wambura, aliyepelekwa Manyara na Mkuu wa Utawala Kinondoni, pamoja na baadhi ya askari wa kitengo cha upelelezi na wengine kutoka idara mbalimbali.

Kuhamishwa kwao kulitokana na kushindwa kwao kudhibiti mtandao wa dawa za kulevya nchini, kiasi cha kuifanya Tanzania kuwekwa kwenye orodha ya nchi zinazojihusisha na biashara hiyo kwa kiwango cha juu.

Awali, kabla ya matukio hayo, Tanzania ilikuwa ikitumiwa kama njia ya kupitishia dawa za kulevya kwenda Afrika Kusini, Ulaya na Amerika, lakini kadri siku zinavyokwenda inakuwa soko la dawa hizo.

Kinachotokea vijana wengi mitaani wanaoitwa mateja, ndiyo wenye kufanya kazi ya kuiba na kupora vitu vya watu mbalimbali. Fedha wanazopata wanazitumia kununua ‘kete za dawa’ na kuzitumia.

Kundi hili limeongezeka, na inaelezwa kuwa wafanyabiashara vijana wa kundi la kati wengi sasa wanatumia dawa za kulevya na hilo ndilo linachangia magari mengi kuwekewa ‘tinted’, kwa nia ya kuficha maovu.

Serikali ya Awamu ya Nne, iliamua kupambana na dawa za kulevya kwa kubadili sheria na ikaelekeza kuanzishwa kwa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, lakini hadi leo chombo hicho hakijaundwa.

Ukiacha kutoundwa kwa chombo hicho, wafadhili walikuwa wakitoa fedha za kununulia dawa ya methodine kwa ajili ya vijana walioathirika na dawa za kulevya, lakini maofisa waliopo katika Tume ya Dawa za Kulevya wakaishia kuzifuja na hivyo mradi ukafutwa.

Matumaini makubwa ya Watanzania sasa yapo mikononi mwa Rais Magufuli, kwani inaelezwa kuwa yeye hana ushirika na wafanyabiashara ambao baadhi yao wanafanya biashara ya dawa za kulevya.

“Tunachosema, Rais sasa achunguze wanaomiliki mabasi, majumba makubwa na biashara zisizoelezeka mitaji yake ilipatikanaje, kisha kuanzia hapo atajua kina nani wanafanya biashara haramu na kina nani wanatumia biashara kutakatisha fedha za dawa za kulevya,” ameshauri mtoa habari wetu.

Gazeti la JAMHURI limekuwa miongoni mwa vyombo vya habari vilivyo mstari wa mbele kwenye mapambano dhidi ya dawa za kulevya. Mwezi uliopita lilichapisha orodha ya wauza unga 560 wanaofanya biashara hiyo nchini, na ambao wengi wao wapo mikononi mwa dola kwa sasa.

Hata hivyo, kumekuwapo madai kuwa wanaokamatwa wengi ni wachuuzi wa chini na wa kati, lakini wahusika wakuu wanaogharimia biashara hiyo, wakiwamo viongozi serikalini na katika vyombo vya dola, wakiwa hawajakamatwa.

Kauli Mbili za Zitto Kuhusu Mali na Madeni ya Viongozi..Amtaka Rais Aamuru Ziwekwe Kwenye Mtandao Kila Mtu Aone

$
0
0

Zitto Amefunguka Haya kwenye ukurasa wake wa Facebook:

"Rais Magufuli aagize Mali na Madeni ya Viongozi yawekwe wazi kweny tovuti ya Tume ya Maadili ya Viongozi ( sheria irekebishwe kuzuia watu wanaoona matamko kuziweka wazi, bila uwazi ni vigumu kupambana na rushwa)"
"Taarifa kwamba kuna Mawaziri ambao hawakujaza fomu za Maadili au kuficha mali zao katika tangazo la Mali na Madeni ni jaribio kubwa kwa Rais Magufuli kuhusu dhamira yake ya kupambana dhidi ya Ufisadi. Sheria ya Maadili ya sasa, licha ya udhaifu wake, ikitekelezwa ( enforced) ni silaha bora ya kuweka misingi ya Maadili katika Uongozi wa Umma" Zitto Kabwe

Mange Kimambi Alivalia Njuga Swala la Shutuma za Diva Loveness Kung'ang'ani Pesa za Kilema Zilizochangwa na Wadau..Adai lazima Haki Itendeke

$
0
0
Mange Kimambi Alivalia Njuga Swala la Shutuma za Diva Loveness Kung'ang'ani Pesa za Kilema Zilizochangwa na Wadau..Adai lazima Haki Itendeke...

Soma Hapa:


From @mangekimambi_ - Ni mwezi Sasa Toka @divathebawse atume hii message kwa Mama Husna. Ofcourse Kesho yake huyo Msaidizi wake Maya hakutuma hata senti. Mama wa watu kuanza kudai pesa zake ndo kaonekana hana respect! . .
It's 2016 let's use social media Kwa mambo ya Maana zaidi ya umbea..... Ni wanyonge wengi wanafanyiwa Hivi Na hizi foundation.

Diva mwenyewe Hana hata mshipa wa aibu Sidhani hata Kama ana mpango wa kutoa Hizo pesa........ Ndo kwanza anajisexisha insta hana hata time.... Roho ngumuuuuu Mpaka! But tusikate tamaaaa lazma Huyu tumfanye mfano. Kuna Mtu kajitolea kumsaidia Huyu mama kufatilia hii kesi kisheria, , dhumuni sio tu hiyo laki 7 tu Ila dhumuni Ni kukomesha uonevu huu....

First of all mnaojua process za kushtaki foundation pls whatsapp me. + 1 424 333 2650. As in Naomba kujua process nzima ya kufatilia hii kesi Mpaka Huyu mama apate pesa zake.......as in waanzie wapi na Kitengo kipi serikalini Chenye mamlaka ya hizi foundation ambapo malalamiko kama haya yanapelekwa????? Pia ni (wizara) Waziri gani anahusika na issue hii ? Je yupo insta?

Ni Ndoto Maalim Seif Kuwa Rais wa Zanzibar

$
0
0
Mkurugenzi wa zamani wa Idara ya Usalama , Dr. Hassy Kitine ameweka wazi kuwa ni ndoto kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kuiongoza Zanzibar.

"Watu wengi wanashabikia mgogoro wa Zanzibar bila kujua kiini chake, ili uzungumzie vizuri Zanzibar na harakati zake za kisiasa ni lazima uifahamu historia yake. Wenzetu wamepata uhuru wao kwa kumwaga damu, tofauti na sisi huku, ambako Mwalimu Nyerere alitumia meza ya mazungumzo kusaka uhuru, kwa wenzetu siyo" anasema Dr. Kitine.

"Bahati mbaya sana zipo siri zunazowagusa baadhi ya wataka urais wa sasa moja kwa moja, ambazo zinauhusiano mkubwa na Mapinduzi ya Zanzibar" Anaendelea kutanabahisha.

" Historia ya Zanzibar inawahusisha Waarabu(mabwana) na waswahili(watwana), hali hii iliendelea hadi pale Abeid Karume alipochukua uongozi wa visiwa hivyo na kuruhusu waswahili kuoana na waarabu ili kuondoa tofauti za kibwana na kitwana. Wapo watu wa ndni na nje ya nchi wanatamani mfumo wa kitwana na kibwana urudi visiwani humo na ndiyo maana wanahangaika huku na kule kutafuta uongozi, jambo ambalo haliwezekani kwa sababu nchi hiyo haikukomholewa kwa makaratasi" Dr. Kitine aliendelea kisema alipohojiwa na Rais nguvu ya Hoja.
"Hivi hamjiulizi ni kwanini Unguja hakuna shida, badala yake Pemba ndio kuonekane kugumu. Kuna historia nzito inayohusu usultani hapo Katikati, ambayo wengo hamuijui na hata wanaoijua jawapendi kuizungumzia" alisema.

"KITENDO CHA KUFUTA HISTORIA YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR HAKIKUBALIKI NA HAKUNA MTU MAKINI ATAKAYEKUBALI KUFANYA HIVYO" Dr. Kitine alimazia.

Dogo Janja Kumshitaki Msichana Aliyemrekodi Kwenye Mazungumzo yao Wakati Amkimtongoza

$
0
0
Msanii wa bongo fleva ambaye ameachia wimbo wake mpya wa My Life,dogo Janja amesema kuwa tayari ameshakuchukua RB polisi kwa ajili ya msichana aliyerekodi mazungumzo yao ya siri na kuyavujisha mtandaoni.

Dogo Janja aliyasema hayo kwenye moja ya mahojiano yake wakati anaachia wimbo wake mpya na kueleza ni jinsi gani msichana huyo alivyompa wakati mgumu.

“baada ya kusikia ile voice note akili yangu ili stuck,zikawa zinaingia simu nyingi hasa za nyumbani wakinilaumu,nikajaribu kumcheki yule msichana akani block mpaka sasa kani block ila nina RB yake” alifunguka dogo janja.

Breaking News: Huyu Ndio Rais Mpya wa Shirikisho la Soka Duniani Fifa...

$
0
0
Raia wa Switzerland Gianni Infantino amechukua mahala pake Sepp Blatter kama rais wa shirikisho la soka duniani Fifa.

Katibu huyo mkuu wa Fifa alipata kura 115 katika raundi ya pili ikiwa ni kura 27 zaidi ya mpinzani wake wa karibu Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa.

Mwanamfalme Ali bin al-Hussein alikuwa wa tatu akiwa na kura nne huku Jerome Champagne akishindwa kupata hata kura moja.

Tokyo Sexwale alijiondoa kabla ya kura kuanza kupigwa mjini Zurich.


Raundi ya kwanza ya upigaji kura ilishindwa kum’baini mshindi wa moja kwa moja.

Wingi wowote wa kura[zaidi ya aslimia 50] katika raundi ya pili ya uchaguzi huo ulikuwa unaweza kumwezesha mgombea kutangazwa mshindi katika raundi ya pili.

Infantino ni wakili mwenye umri wa miaka 45 kutoka eneo la Brig jimbo la Valais nchini Switzerland ,ikiwa ni eneo lililopo chini ya maili sita kutoka nyumbani kwa Blatter.

Blatter ambaye aliliongoza shirikisho hilo tangu mwaka 1998 alijiondoa mwaka uliopita kabla ya kupigwa marufuku katika shughuli zozote za kandanda kwa kipindi cha miaka sita.


Baada ya kutangazwa mshindi, Infantino aliwaambia wajumbe waliopiga kura kwamba hakuweza kujielezea kutokana na hisia alizokuwa nazo.

Lakini aliwaambia wajumbe kwamba ”kwa pamoja wataweza kuirudisha sura ya Fifa na heshima ya Fifa”.

Sijui Kama Wema Sepetu Alishawahi Kuwa na Mimba -Mirror

$
0
0
Msanii wa muziki wa bongo fleva Mirror, anayefanya kazi chini ya Wema Sepetu amesema hajui kama Wema alishawahi kuwa na mimba ila na yeye anasikia kwa watu na kwenye mitandao.

Msanii huyo ambaye anatamba na wimbo wake mpya Naogopa ambao ameimba na Baraka Da Prince ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha ENews kinachorushwa na EATV.
Mirror amesema hafahamu chochote kuhusiana na jambo hilo na wiki 2 zilizopita nilikuwa naye ofisini lakini sikuona kama kuna tatizo lolote yupo ana furaha na anaendelea na kazi zake kama kawaida .

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Idriss Sultan alinukuliwa akisema watoto wake mapacha ambao walikuwa wapatikane kupitia Wema haikuwa bahati,kuwaona.

Majambazi Dar es Salaam Yavamia Benki Ya Access....Yaua Mlinzi na Kupora Pesa, Polisi Wapambana Nayo na Kuyaua

$
0
0
Majambazi  ambao  idadi  yao  haikufahamika  wakiwa  na  mabomu  na  bunduki  za  kisasa  jana  walivamia  Benki  ya  Access  tawi  la Mbagala  ambako  walipora  viroba vya   fedha, kuua  mlinzi  na  baadae wanne  kati  yao  waliuawa  na  jeshi  la  polisi.

Watu  walioshuhudia  tukio  hilo  walisema  baada  ya  majambazi  hao  kufika  katika  benki  hiyo  kwa  bodaboda  nne  majira  ya saa  nane  mchana,yalimuua  mlinzi  wa  benki  hiyo, kusha  kubomoa  kwa  risasi  mlango  wa  vioo  na  kuingia  ndani  na  kuzua taharuki  kubwa

Mashuhuda  hao  walisema, katika  tukio  hilo  lililodumu  kwa  karibu saa  moja,mmoja  wa  majambazi  hao  aliyekuwa  amevaa  kininja,alikuwa barabarani  akiamuru  magari  kupita  haraka  huku  akifyatua  risasi  hovyo.

Ilielezwa  kuwa, jambazi  huyo  aliyeonekana  kuwa  na  uzoefu  wa  matumizi  ya  bunduki  alikuwa  akifyatua  risasi  kwa  kutumia  mkono  mmoja  na  ndiye  aliyewajeruhi  baadhi  ya  wapita  njia.

Hivyo,wakati  uporaji  ukiendelea  na  jambazi  huyo  akiimarisha  ulinzi  barabarani  baadae  hakukuwa  na  magari  wala  pikipiki  zilizokuwa  zikipita.

Mfanyabiashara  wa  duka  la  vifaa  vya  ujenzi  jirani  na  benki  hiyo,Ramadhani Tairo  alisema  baada  ya  jambazi  huyo  kuliona  gari  la  polisi  likielekea  eneo  la  tukio,alifyatua  risasi  na kulipiga  kabla  halijafika.Gari  hilo  lilipoteza  mwelekeo  na  kutumbukia  mtaroni.

Tairo  alisema  mbali  na  jambazi  huyo  kulipiga  risasi  gari  la polisi  pia  alilirushia  bomu  la  mkono,lakini  liliangukia  barabarani  bila  kuripuka.Polisi  walifanikiwa  kulilipua  bomu  hilo  baadae  likiwa  halijasababisha  madhara  kwa wananchi  waliofika  kushuhudia  tukio  hilo.

Mkazi  mwingine  wa  eneo  hilo,Rebecca  Maliva  alisema  majambazi  walioingia  ndani  ya  benki  hiyo  walioneka  wakitoka  na  viroba  vitatu vya  fedha  ambavyo  walivipakata kwenye  pikipiki  na  kuondoka  kwa  kasi  kuelekea  Mkuranga kupitia  barabara  ya  Kilwa.

Rebecca  alisema  polisi  zaidi  walifika  kwenye  eneo  hilo  wengine  wakiwa  kwenye  pikipiki  na  kuanza  kuwafukuza  majambazi  hao  ambapo  walipofika  eneo  la  shule  ya  St. Marry's,walitupa  kiroba  kimoja  cha  fedha  ambacho  wananchi  waliokuwa    jirani  waligombania  na  kuchukua  fedha  zilizokuwemo  na   kisha  kila  mmoja  kukimbia  na  burungutu  la  noti.

Baada  ya  nusu  saa  wakati  umati  ukiwa  bado  upo  kwenye  benki  hiyo,magari  ya  polisi  yalipita  katika eneo  hilo  yakitokea  eneo  la  Mkuranga  yakiwa  yamebeba  miili  ya  majambazi  yaliyouawa.

Magari  hayo  yalikuwa  yakisindikizwa  na  vijana  wa  bodaboda  waliokuwa  wakishangilia  kazi  iliyofanywa  na  polisi.

Kamanda  wa  polisi  kanda  maalum ya  Dar es Salaam, Simon Sirro  alizungumzia  kwa  ufupi  tukio  hilo n kwamba  majambazi  manne  yaliuawa  na  kukamata  silaha  tatu,lakini  hakutaka  kuingia  kwa  ndani  akisema  atatoa  taarifa  zaidi  leo

Msanii Rich Movoko Amkana Mrembo Gigy Money 'Sikumbuki Hata Kukutana na Gigy Money Wala Kutoka Nae Kimapenzi Sinaga Upumbavu Huo'

$
0
0
 Gigy Money na Rich Mavoko....
Msanii Rich Mavoko amekanusha taarifa za kuwahi kuwa na mahusiano na video queen Gigy Money, ambaye alisema alishawahi kuwa naye akiwa kidato cha pili.

Akiongea na East Africa Radio Mavoko amesema taarifa hizo si za kweli, na hakumbuki hata kuwahi kukutana naye mrembo huyo, achilia mbali kuwa na mahusiano naye.
“Mi sijawahi kutoka naye, hata siku moja sijawahi, sina urafiki naye na wala sijawahi kuongea naye, sijui kama alishawahi kukutana na mimi, sijaweka kichwani kama nishawahi kukutana nae sikumbuki.

Mavoko ameendelea kusema "Sijawahi kuwa na skendo za kipumbavu, mi ni mtu ambaye sijawahi kuwa na upumbavu kama huo, kwanza mi mwenyewe nashangaa unajua kila kitu, sijawahi kutoka naye sijui mwenyewe anafikiria nini, siwezi kujua, siwezi kutambua, sijawahi kuelewa nini kilichompelekea hivyo”, alisema Richi Mavoko.

Hivi Karibuni video queen huyo alisema alishawahi kuwa na mahusiano na msanii huyo wakati yupo kidato cha pili, kitu ambacho ni kinyume na sheria za nchi na hakifai kwa mtu ambaye ni kioo cha jamii.

CUF Kuandamana Kupinga Marudio Ya Uchaguzi Zanzibar..Wadai Hali ya Zanzibar si Shwari Watu Wanaishi Kwa Hofu..

$
0
0
CHAMA cha Wananchi (CUF) Bukoba kimejiandaa kufanya maandamano ya amani keshokutwa, kwa ajili ya kupinga kufanyika upya uchaguzi wa Zanzibar unaotarajiwa kuwa Machi mwaka huu.

Kimeiomba pia serikali ya awamu ya tano, kuchukua uamuzi wa kumtambua Maalim Seif Sharif Hamad kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi wa urais Zanzibar na kuwa hakiko tayari kurudia uchaguzi huo tena.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya msimamo wa chama hicho, Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho Saverina Mwijage, alisisitiza kuwa kamwe chama hicho hakitakuwa tayari kurudia uchaguzi huo uliotangazwa na Tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kuwa utafanyika Machi 20,kwa kile kinachodaiwa ni kufutwa uchaguzi wa Oktoba 25,mwaka jana.

“Tumedhamiria kuandamana ili kumfikishia ujumbe wetu Rais John Magufuli kupitia kwa Mkuu wa mkoa wa Kagera, John Mongella lengo letu hasa ni kupinga uchaguzi wa Zanzibar. Hali ya Zanzibar kwa sasa haiko shwari, watu wanatishiwa maisha yao, wanaishi kwa hofu juu ya maisha,” alisisitiza.

Mwijage ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CUF Taifa, alisema chama hicho kinatambua uchaguzi ulishakwisha na tume hiyo ilishatoa vyeti kwa walioshinda, kwa mantiki hiyo CUF inamtambua Maalim Seif kuwa alishinda katika uchaguzi huo.

Alisema maandamano hayo yanatarajiwa kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri na baadaye utakuwepo mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mashujaa Mayunga ulioko mjini Bukoba ili kuutangazia umma juu ya msimamo wa chama hicho na baada ya hapo watazunguka katika wilaya za Muleba, Missenyi na Karagwe.

Staa wa muziki Mzungu Kichaa Awadiss Wema Sepetu na Idris Sultan

$
0
0
Mzungu Kichaa
Staa wa muziki Mzungu Kichaa, amevunja ukimya kuligusia suala ambalo pengine linawaumiza wasanii wengi, ikionekana kuwa ni 'diss' pia kwa staa Wema Sepetu na mwenzake Idriss Sultan, kupitia suala lao la ujauzito kunasa na kutoka.

Akiongea kwa hisia nzito, Mzungu Kichaa ambaye ana project kubwa ya video ambayo watu hawaifahamu kama wanavyofahamu mimba ya Wema, msanii huyo anayejinadi kuwa ni mbishi, ameelezea kusikitishwa kwake kwa mastaa hao ambao wanatumia muda wao mwingi kuleta atensheni kwa mashabiki badala kufanya shughuli zao binafsi za kila siku.
Idriss na Wema Sepetu

Mzungu Kichaa pia amekanusha suala la video yake kukosa kiki kutokana na kumhusisha Dir Adam Juma ndani yake, na kuifanyia hapa hapa nchini akisema kuwa Dir Adam ana kila sababu ya kupewa hashima yake kutokana na ubora wa kazi zake na si maelezo mengine yaliyopotofu.

Tazama Video Mpya ya Wimbo wa Nay wa Mitego Ulioleta Utata Mpaka Kufungiwa na Basata-Shika Adabu Yako

$
0
0
Msanii Nay wa Mitego baada ya nyimbo yake kukatazwa kuchezwa katika vituo mbalimbali vya radio na Basata ameachia video ya wimbo huo unaitwa “Shika Adabu Yako”, Video imeongozwa na Nicklass, angalia hapa alafu toa maoni yako.

Kama Ulikuwa Unafikiri Mr Nice Kafulia Basi Umechemsha..Adai Bado ana Hela Alizovuna Kipindi cha Nyuma Katika Muziki Wake

$
0
0
Msanii mkongwe na mwanzilishi ya style ya TAKEU, Mr Nice amefunguka kwa kusema kuwa bado yupo vizuri kiuchumi tofauti na watu wanavyodhani kwamba amefilisika.


Akizungumza na Bongo5 Alhamisi hii, Mr Nice amesema kwa kuthibitisha hilo amejenga nyumba mpya kubwa nyumbani kwao ndani ya miezi mitatu.

“Watu hawajui kwamba walinipa pesa nyingi sana mpaka leo bado nazitumia, nyie mnaona kama zimeisha hazijaishi, hapa sasa hivi nawazima kidomo domo wale waliosema nimefilisika, sasa hivi najenga nyumba nyingine kijijini kwangu Moshi na ndani ya miezi mitatu nyumba kubwa imekamilika,” alisema Mr Nice.

Aliongeza, “Watu ambao umefilisika watafikiria kujenga sasa hivi?, hamuwaoni wasanii wenye stress za maisha, kwa hiyo hili ni jibu kwa wale waliyokuwa wanaongea sana,”
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images