Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104694 articles
Browse latest View live

Soma Jinsi Diamond Alivyotaka Kugoma Kushoot Video ya Make Me Sing Baada ya Hili Kutokea..

$
0
0
Diamond si msanii anayekubali tu kirahisi kitu ambacho anahisi kinaweza kupoteza wazo lake la awali analoamini kuwa ni muhimu kufanikisha kupata zao zuri zaidi.

Hanscana amesimulia jinsi staa huyo alivyogoma kuendelea kushoot video ya wimbo wake na AKA ‘Make Me Sing’ baada ya muongozaji kutaka kurahisisha mambo:

Kipindi inashutiwa video ya make me sing by @diamondplatnumz nilijifunza vitu vingi sana ila hiki ni kimoja wapo. Tulitembea umbali kama wa km 300 hivi kwenda ku shoot zile scene Diamond anaimba kwenye white bed afu kati kati ya pori tupu. Kufika kule jamaa aliyepewa deal ya kuleta bed akageuza maelezo baada ya kuleta cheupe akaleta cheusi.

Diamond akagoma kushoot alafu zilitumika gharama nyiingi sana kuandaa production kwaajili ya hiyo scene so isiposhutiwa muda huo ile gharama yote inakuwa hasara na mbaya zaidi juwa lilikuwa linazama hata wangesema waende town wakachange ingekuwa nje ya muda na kesho yake ilikuwa tunarudi Dar kumalizia shots za video ya kama utanipenda.

So ilikuwa no way out Diamond lazima ashoot basi wakaanza kumjaza pale washoot hivo hivo tu ‘ Diamond aligoma mpaka mwisho alisema huwa siamini Plan B hata kidogo so i can’t broo. Na wote tukamuona miyeyusho but baada ya video kutoka nimeona faida ya ubishi wake siku ile.”

Watanzania Wamjia Juu Mkenya Aliyesema Olduvai Gorge Ipo Nchini Kenya Mpaka Imebidi Aombe Radhi

$
0
0
Watanzania wamemjia juu Mkenya Rosemary Odinga ambaye pia ni mtoto wa mwanasiasa mkubwa wa nchini kenya Raila Odinga, ambaye ametoa taarifa za bonde la Olduvai Gorge kuwepo nchini Kenya, na kumtaka kuomba msamaha na kusahihisha kauli yake.

Wakiendesha kampeni hiyo kwenye mitandao ya kijamii kwa kutoa maoni kwenye picha yake, kumeibua hisia kubwa baina ya jamii ya Wakenya na Watanzania, huku Watanzania wakidai Wakenya wanawachokoza.

onesmo_killenga: Na hili tutalifanya fundisho kwenu omba msamaha mapema @rosemaryodinga la sivyo tutachukua hatua kama wananchi wa nchi yetu na hamta amini tutasusia bidhaa zenu zilizopo nchini ili tuendelee kuheshimiana hubacaren: Rosemaryodinga you still remain silent? ignoring this or what??? umewakosea watanzania wote na you should apologize publicly or you will just tarnish your image.

esteriche: Dd kasema oldvai ipo kenya xa ona watanzania wanavyomfrahisha ...atafrahiii kwa kweli hizo comments watanzania katika ubora wao na masters za kutetea vya kwao yani hapa nacheka na comment tu.

call_me_kimodo: Mama hivi unajua wa tz wewe, haya matusi tutayoanza kukuporomoshea utaomba poa, omba radhi mwenyewe mwizi wa rasilimali zetu.

Baada ya mkiki huo wa kwenye mitandao kutoka kwa watanzania, wakenya hawajakaa kimya na kuamua kujibu mapigo.

kimathijr: Mnajua nyie wabongo huwa mnabonga sana.. hata kichwa zenu tunajua zimejaa maji. sijapata ona majitu majina in the continent kama nyinyi mazee.... ur such as disgrace to our east community. smh.

Baada ya malumbano hayo Rosemary aliamua kujirudi na kuomba radhi., huku akisema hakuwa nania mbaya kusema kuwa Olduvai Gorge ipo Kenya, kwani Afrika mashariki ni moja.



CCM Imefanya Uhuni na Ubabe Uchaguzi Kilombero - Godbless Lema

$
0
0
Mbunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mh Godless Lema amefunguka na kusema kitendo kilichofanyika katika uchaguzi wa Halmashauri ya Kilombero leo ni ubabe na uhuni wa CCM.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Godbless Lema amesema kitendo cha polisi kuwakamata wabunge wa Chadema na kuwaweka ndani wakati uchaguzi wa Halmashauri ukiendelea ni mbinu waliyotumia CCM ili kupunguza kura za wajumbe hao, jambo ambalo limepelekea UKAWA kushindwa ili hali wao walikuwa na wajumbe wengi zaidi ya CCM.

"Leo ilikuwa siku ya Uchaguzi Halmashauri ya Kilombero baada ya kuahirishwa mara kadhaa. UKAWA ina wajumbe 20 na CCM 19. Hii ina maana kuwa UKAWA tulikuwa na uhakika wa kushinda na kuongoza Halmashauri hiyo. Baada ya CCM kujaribu kuwahonga madiwani kadhaa na kushindwa kufanikisha lengo lao, leo wakabuni mbinu mpya ya kishetani. Wakamkamata Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali na Mbunge wa Viti Maalum Devotha Minja na kuwaweka mahabusu huku uchaguzi ukiendelea" Aliandika Godbless Lema

Kufuatia jambo hilo Mbunge huyo amesema kuwa jambo hilo ni jambo ambalo halivumiliki kwani ni ukatili, ubabe na uhuni

"Kwa kufanya hivyo wakawa wamepunguza kura 02 za UKAWA (kura ya Lijualikali na ya Devotha). So UKAWA ikabaki na madiwani 18.

Uchaguzi umefanyika CCM wameshinda kwa kura 19 na CHADEMA 18. Huu ni ubabe, uhuni na ukatili usiovumilika. We must take action. Haiwezekani tuhujumiwe kwa kiasi hiki halafu tukae kimya. Huu ni ubabe ambao hata Shetani hawezi kuufanya.

Tusipochukua hatua wataendeleza ubabe huu wa kijinga. Watafanya hivyo pia kwa Dar" Aliongeza Godbless Lema.

Harmonize Afunguka Kwanini Hajawai Kufanya Show Dar..Adai Menejimenti yake ilimkataza

$
0
0
Msanii wa bongo fleva Harmonize ambaye yuko chini ya lebel ya Wasafi inayomilikiwa na Diamond amefunguka kuhusiana na yeye kutowahi kufanya show jijini Dar es salaam na kusema ni mikakati ya menejiment yake kum brand.

Msanii huyo ambaye ameachia wimbo mpya wa Bado amesema aliahidiwa kuanza show baada ya wimbo wa pili na pia kuna uwezekano wa kuachia album.

“Msanii lazima uji brand,muziki ni biashara na kila biashara ina misimamo na mikakati yake,ukiweka mikakati mibovu huwezi kuingiza faida.Halafu pia menejimenti yangu ilinambia the way tunaku brand hatutaki ufanye show Dar es salaam kwanza mpaka ukitoa wimbo wa pili ndio utakuwa una uwezo wa ku perfom Dar es salaam na popote duniani” alifunguka Harmonize.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya March 2, Ikiwemo ya CCM Kushinda Kilombero Kwa Goli la Mkono

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya March 2, Ikiwemo ya CCM Kushinda Kilombero Kwa Goli la Mkono

Bei Mpya za Mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa Zimetangazwa....

$
0
0
March 1 2016 Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji nchini (EWURA) ilitangaza bei mpya ya bidhaa za mafuta ya Petrol, Diesel na ya mafuta ya taa katika masoko yote ya jumla na rejareja ambapo bei hizo zitaanza kutumika kuanzia tarehe 2 march 2016.

Akiongea na waandishi wa habari Dar es salaam, Mkurugenzi wa huduma za nishati na maji (EWURA), Felix Ngamlagosi amesema ‘kuanzia tarehe 2 March bei za mafuta zimebadilika ikilinganishwa na toleo lililopita la February 2016, kwa March 2016 bei ya rejareja za petroli imepungua Tsh 31 kwa lita sawa na 1.70%, Diesel imepungua Tsh 114 kwa lita sawa na 7.10% na mafuta ya taa yamepungua kwa Tsh 234 kwa lita sawa na 13.75%’

‘kwa kiasi kikubwa , kupungua huku kwa bei za mafuta kwenye soko la ndani kumetokana na kuendelea kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia‘

Polisi na UKAWA Ngoma Nzito....Naibu Katibu Mkuu CUF Nassor Ahmed Mazrui Naye Atakiwa 'Kujisalimisha' Polisi Kwa Mahojiano

$
0
0
Jeshi la Polisi limeendelea na kamatakamata ya wapinzani wa vyama vinavyounda Ukawa katika maeneo mbalimbali likieleza sababu tofauti za kijinai zinazohusishwa na masuala ya kisiasa.

Mpaka sasa wabunge wa upinzani waliokamatwa ni; Halima Mdee (Kawe), Mwita Waitara (Ukonga) na Peter Lijualikali (Kilombero), wote wa Chadema na baadhi ya madiwani wa chama hicho katika Jiji la Dar es Salaam.

Vilevile, imeelezwa kuwa Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea alikuwa anatafutwa kuunguanishwa na wenzake.

Pia, baadhi ya wanasiasa wa CUF Zanzibar wamekamatwa na kuhojiwa kwa madai ya kuwatusi viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Viongozi wa CUF waliohojiwa na polisi mpaka sasa ni Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Omar Ali Shehe na Kiongozi wa Mkakati wa Ushindi, Mohamed Sultan Mugheir ‘Eddy Riyami’ ambaye yuko nje kwa dhamana.

Mbali na viongozi hao, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui  jana  amepatiwa barua ya wito  na Polisi Zanzibar  ikielezwa kuna mambo yanamhusu.

Hii ni mara ya pili kwa Mazrui kuitwa polisi tangu kufutwa kwa uchaguzi wa Oktoba 25, huku CUF ikidai kuwa huo ni mwendelezo wa mkakati maalumu dhidi ya viongozi wa chama hicho.

Jana, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Umma wa CUF, Maalim Hamad Masoud Hamad alidai kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya kisiasa ya kutaka kumkamata kila kiongozi wa juu wa CUF kuelekea uchaguzi wa marudio.

“Kwa viongozi wa CUF hili halishangazi, nahisi ingelikuwa ni hatua ya kushangaza sana iwapo wanaoitwa kuhojiwa na polisi ni viongozi wa vyama vingine.

"Sisi upande wetu hili ni jambo la kawaida mno na watu wasishangae,” alisema.

Mazrui ambaye pia alikuwa Waziri wa Biashara na Uwekezaji, ametakiwa kuripoti Makao Makuu ya Polisi, Ofisi ya Upelelezi Ziwani mjini hapa kesho saa 2.00 asubuhi na kuonana na mkurugenzi wa makosa ya jinai Zanzibar.

Polisi Zanzibar imethibitisha kuwapo wito huo ikisema kuna mambo muhimu yanayomhusu mwanasiasa huyo.

Mwanamuziki Baraka Da Prince Adaiwa Kumzalisha Binti na Kumtelekeza Mtoto..Stori Nzima Ipo Hapa

$
0
0
Msanii wa bongo Fleva anayetamba sasa kwa kibao chake cha siwezi,Baraka da Prince amepata kashfa ya kumzalisha binti wa miaka wa 19 aishie Iringa aliyejitambulisha kwa jina la Candy kisha kumtelekeza  mtoto huyo.

Akiongea na redio moja binti huyo amedai mtoto wake na Baraka da Prince ana mwezi mmoja na nusu ambapo alimzaa kwa kwa opresheni mwezi wa Desemba mwaka Jana.baraka

Binti huyo amedai kuwa alianza mahusiano na baraka da Prince wakati alipoenda Iringa kipindi baba yake anafanya kazi huko na badaaye wakakubaliana aje Dar ambapo wakawa wanaishi wote mpaka binti alipopata ujauzito na kurudi Iringa kwenda kulea ujauzito huo.

Candy akaendelea kusema kuwa baada ya yeye kurudi Iringa hakupata matunzo yoyote kutoka Baraka da Prince hata alipojifungua.Binti anasema kila akijaribu kumtafuta Baraka kwenye simu hudai yuko bize na mara nyingine humtolea maneno ya kuudhi.

Candy amedai kuwa ana ushahidi wa picha kadhaa za Baraka da Prince na mtoto na juzi tu Baraka alivyoenda kufanya show alienda kuwaona na kutoa ahadi kibao lakini mambo yamebaki vile vile hakuna matunzo yoyote.

Nafasi za Kazi Diamond Trust Bank (DTB), Application Deadline 31st March 2016

$
0
0
DIAMOND TRUST BANK (DTB)
EMPLOYMENT OPPORTUNITY

Established 70 years ago as a finance house, Diamond Trust Bank has today grown into a leading commercial bank offering a wide spectrum of banking services. Through its affiliation in Uganda, Kenya and Burundi, DTB ha s a regional presence which none of the peer banks can boast of DTB Tanzania is consistently ranked amongst the most successful banks in the country with Profit before Tax Increasing at a CAGR of 32% over the last 6 years.

With 25 operations branches in Tanzania, DTB is now looking for capable and qualified individuals to fill following positions:-


  1.  Chief Operation Officer
  2. Head-Risk Management
  3. Deputy Head- Risk management
  4. Head-Corporate
  5. Deputy Head-Operation
  6. Manager-Sales(Head Office DSM)
  7. Manager Loan Recovery
  8. Branch Manager( DSM and Upcountry)
  9. Banking Assistant(Teller &Front Officer)


How to Apply

If you meet the above requirement email:

  • Covering letter clearly indicating the position
  • The subject of the email and application letter clearly indicating the position


The application must be sent digitally only to: recruitmentmarch@diamondtrust.co.tz before 31st March 2016

Head Office:
Diamond Trust Bank Tanzania Limited
901 Harborview Towers, Samora Avenue
P.O Box 115
DAR ES SALAAM

Tel: +255 22 2114891/2
Fax: +255 22 2124244


Source: The Guardian 1st March 2016

Hivi Ndivyo Rais Museven Alivyofurahishwa na Rais Magufuli Walipokutana Jijini Arusha...

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, amekutana na kufanya Mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mheshimiwa Yoeri Kaguta Museveni, ambapo pamoja na mambo mengine wamekubaliana kujengwa kwa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Bandari ya Tanga nchini Tanzania hadi nchini Uganda.

Rais Museveni amemtembelea Rais Magufuli katika Ikulu ndogo ya Arusha leo jioni mara baada ya kuwasili hapa nchini akitokea nchini Uganda, ambapo hapo kesho atahudhuria Mkutano Mkuu wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, utakaofanyika katika Hoteli ya Ngurudoto Jijini Arusha.

Akizungumza baada ya viongozi hao kufanya mazungumzo ya faragha, Rais Magufuli amesema wamekubaliana kutekeleza mradi huo wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Tanga hadi Uganda, kwa manufaa ya nchi zote mbili na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Amesema bomba hilo litakuwa na urefu wa kilometa 1,120 na kwamba mradi huo utazalisha ajira za watu zaidi ya 15,000.

Rais Magufuli ameongeza kuwa pamoja na kujengwa kwa bomba la mafuta, pia wamezungumzia kuongeza biashara ndani ya nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki, kujenga viwanda na kuzalisha ajira zaidi kupitia sekta mbalimbali za uzalishaji mali.

Aidha, Rais Magufuli amesema katika Mkutano huu nchi wanachama watajadili maombi ya nchi ya Sudan Kusini kupata uanachama ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Nchi Jirani ya Kenya Yashika Nafasi ya Tatu kwa Ufisadi Duniani

$
0
0
Shirikisha la Wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Kenya wameelezea hofu ya taifa kujikuta katika mapinduzi kutokana na ufisadi uliokithiri, huku walala hoi wakiendelea kutaabika ndani ya nchi yao.

Ripoti mpya ya viwango vya ufisadi inaonesha Kenya ikishikila nafasi ya tatu kote ulimwenguni, licha ya serikalib kuweka mikakati ya kukabililiana na viotendo vya rushwa na ufisadi.

Utafiti huo wa shirika la Pricehouse-Water-Coopers unaonesha Kenya ikiwa nafasi ya tatu nyuma ya Ufaransa na Afrika Kusini. Wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Kenya wameelezea hofu ya taifa kujikuta katika mapinduzi kutokana na ufisadi uliokithiri, huku walala hoi wakiendelea kutaabika ndani ya nchi yao.

Katika mahojiano na sauti ya Amerika Maur Abdalla Bwanamaka, mwenyekiti wa chama cha Uzalendo nchini Kenya, ameutaja utumiaji mbaya wa mamlaka kama unaochangia kwa kiasi kikubwa hali ilivyo

Baada ya Chama Cha Walimu Kukosoa Mpango wa ‘Daladala za Bure Kwa Walimu’ Dc Makonda Kawajibu Hapa

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda Jumapili ya February 28 2016 alitangaza kuwa Walimu wa shule za Dar es salaam wataanza kupanda daladala bure kuanzia March 7 2016 baada ya kukubaliana na wamiliki pamoja na madereva wa daladala, habari hii wengine wakaipokea vizuri wengine wakaikosoa.

Dc Makonda amehojiwa na millardayo.com na kusema ‘Najua nipo kwenye jamii ambayo inapenda kuongea sana kuliko kufanya kazi, jamii inayojua kuongelea kukwama kwa jambo hata kabla ya kuanza kufanya kazi , watu wengi wanesema tungewapa pesa ya nauli, wengine wanasema pesa hizi wangepewa wanafunzi, wanasahau kama Walimu ndio uti wa mgongo wa taifa‘

‘Huu ni mchango wa wadau, wadau ndio wanawasaidia Walimu, mimi nasimama kama daraja tu na inabidi watu wajue huu sio mpango wa serikali, ni wadau wamekubali kusaidia Walimu, watu wasichanganye mambo, Mkuu wa Wilaya hana pesa‘ – Makonda
‘Nadhani Walimu walitakiwa kwanza kushukuru wamekumbukwa, ningefurahi wangesema tumepokea nafasi ambayo jamii sasa imeanza kutambua heshima ya Walimu, kwa moyo huu ambao Wadau wameuonyesha tunaiomba sasa wizara ya elimu iendelee kuangalia kuboresha zaidi‘ DC Makonda

Kubenea Aaishiwa na Uvumilivu Kamata Kamata ya Madiwani na Wabunge wa Ukawa

$
0
0
SAED Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema) amepanga kutoa taarifa itakayowagusa viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli na Jeshi la Polisi, anaandika Faki Sosi.

Kwenye taarifa hiyo pia ataeleza taarifa za kukamatwa kwake zilizothibitishwa na Simon Siro, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Taarifa kwenye vyombo vya habari jana zilieleza kwamba, Kubenea ni miongoni mwa waliokamatwa na Jeshi la Polisi ambapo Kamanda Siro alidai kukamatwa kwake.

Taarifa kutoka ndani ya Chadema zinaeleza kuwa, anatarajia kutoa taarifa kwa umma wakati wowote kueleza kile kinachoitwa sakata la polisi, madiwani na wabunge wa Ukawa wakati wa vurugu za uchaguzi wa meya ulioghairisha Jumamosi wiki iliyopita.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa juu wa Ukawa inaeleza kuwa, Kubenea anatarajia kutoa taarifa ili kutoa ufafanuzi wa ndani kuhusu tukio hilo.

“Kubenea atatoa taarifa muda wowote kuanzia sasa, kwa kuongea moja kwa moja na waandishi wa habari, ama kutoa taarifa kwa vyombo vya habari,” amesema

Source

Kampuni ya Rifaro Yadaiwa Kufanya Kazi Tanzania Bila Kibali cha TCRA...Soma Hapa Taarifa Kwa Umma Kutoka TCRA

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
ISO 9001:2008 CERTIFIED


TAARIFA KWA UMMA

KUTUMIKA RASILIMALI NAMBA MAALUMU 15420 NA KAMPUNI YA RIFARO BILA CHETI CHA MATUMIZI YA NAMBA CHA MAMLAKA YA MAWASILIANO


1.0   UTANGULIZI

1.1. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ni taasisi ya Serikali yenye jukumu la kusimamia huduma za Sekta ya Mawasiliano na Utangazaji nchini, ikiwa ni pamoja na usimamizi wa rasilimali namba kwa mawasiliano na anwani kuhakikisha matumizi sahihi.

1.2. Katika siku za hivi karibuni, Mamlaka imeona taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu Kampuni ya RIFARO AFRICA LIMITED kuwa na leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano. Yafuatayo ni maelezo ya Mamlaka kuhusu taarifa hizo:

1.3.Mnamo tarehe 28 Julai, 2014 Mamlaka ilitoa kwa RIFARO AFRICA LIMITED Cheti cha Matumizi ya Rasilimali Masafa kwa ajili ya huduma za ziada za Mawasiliano kupitia SMS (VAS SMS CODE) namba maalumu 15420 kutumika katika kutengeneza mfumo wa Mawasiliano wa SMS kuunganisha na kupokea taarifa za mawakala wao wa kuuza na kusambaza muda wa maongezi kupitia wavuti yao (website);

1.4.Mnamo tarehe 27 Julai, 2015 Cheti hicho kilimalizika muda wake na Kampuni ya RIFARO Africa Limited haikuomba kuongeza muda wa matumizi wa rasilimali namba maalumu 15420. Kuendelea kutumia rasilimali namba hiyo bila cheti cha kuruhusu kufanya hivyo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano ni ukiukwaji wa Kanuni ya 17 (1) ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2011 - Matumizi ya Namba na Anwani za Mawasiliano - (Electronic Communication Numbering and Addressing) Regulations, 2011.

2.0   AMRI YA UTEKELEZAJI

Mnamo tarehe 24th Februari, 2016, Mamlaka ilitoa Amri ya Utekelezaji kwa kampuni ya RIFARO AFRICA LIMITED kwa mujibu wa Kifungu cha 45 cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania sura ya 172 kama ilivyorekebishwa na Kifungu cha 179 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielectroniki na Posta, na kuimauru kampuni hiyo kufika mbele ya Mamlaka ya Mawasiliano kujitetea kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria kwa kuvunja na kukiuka Kanuni namba 17 (1) ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya Mwaka 2011 - Matumizi ya Namba na Anwani za Mawasiliano kwa kutumia rasilimali namba maalumu 15420 bila Cheti cha kuruhusu matumizi yake kutoka Mamlaka ya Mawasiliano.

3.0 KUSIKILIZA SHAURI

Katika kusikiliza shauri la utetezi wa RIFARO AFRICA LIMITED:

1. Walikubali kupewa kibali cha kutumia rasilimali namba maalumu 15420 na kukubali pia kuwa matumizi yake yaliisha muda wake mwezi Julai, 2015;
2. Aidha walikubali kuwa Cheti Cha Matumizi ya Rasilimali Namba Maalumu 15420 kilipokwisha muda wake hawakuomba kuongezewa muda wa matumizi yake;
3. Hali kadhalika walikiri wameingia mkataba wa kibiashara na Kampuni ya Zanzibar Telecom Limited (ZANTEL) kwa ajili ya huduma ya Ezzy Pesa kama mtoa huduma mkubwa wa kampuni hiyo (mobile money super dealership).

4.0 MAAMUZI YA MAMLAKA

RIFARO AFRICA LIMITED imekuwa ikitumia rasilimali namba maalumu (VAS SMS CODE) 15420 bila cheti cha Mamlaka kuwaruhusu kufanya hivyo kinyume na Kanuni ya 17 ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2011 (Electronic Communication Numbering and Addressing) Regulations, 2011.

Baada ya kutafakari utetezi wa Kampuni ya RIFARO AFRICA LIMITED na matokeo ya utetezo wao, Mamlaka inatoa maamuzi kama ifuatavyo:

1. RIFARO AFRICA LIMITED kulipa kwa Mamlaka faini ya shilingi milioni 10 (TZS 10,000,000) kwa kutumia rasilimali namba maalumu 15420 bila cheti cha kuruhusu kufanya hivyo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano; na

2. RIFARO AFRICA LIMITED iache mara moja kutumia rasilimali namba maalumu 15420 kwa kuwa haina ruhusa ya kufanya hivyo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inapenda kuarifu umma kuwa RIFARO AFRICA Limited haina leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. Kampuni hii ilikuwa na Cheti cha matumizi ya rasilimali namba maalumu 15420 ambacho kiliisha muda wake tangu mwezi Julai 2015.

Dkt. Ally Y. Simba
MKURUGEZI MKUU

02/03/2016

Source:Muugwana Blog

Kigogo wa BOT Aliyepokea Rushwa ya Mamilion ya Fedha Kutoka James Rugemalira Asafishwa na Mahakama Sakata la Escrow

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeyafuta mashtaka ya kupokea rushwa ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa mfanyabiashara James Rugemalira, yaliyokuwa yakimkabili   Mkurugenzi wa Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Julius  Rutta  Angello.

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi jana alimfutia Angello mashtaka hayo yaliyokuwa yakimkabili baada ya Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Maxi Ali  kudai kuwa hawana nia ya kuendeleza mashtaka hayo.

Kesi hiyo ambayo ilikuwa imefikia hatua ya usikilizwaji wa awali, Ali alimweleza Hakimu Shaidi kuwa ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa na kwamba, wana shahidi mmoja  lakini hawana nia ya kuyaendeleza mashtaka hayo na kuomba yaondolewe kortini chini ya kifungu cha 98 (a) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Shahidi alikubaliana na Ali hivyo kumfutia mshtakiwa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.

Angello anadaiwa Februari 6, 2014 maeneo ya Benki ya Mkombozi, akiwa Mkurugenzi wa Fedha wa BoT alipokea rushwa ya Sh 161.7 milioni kupitia akaunti namba 00120102646201 kutoka kwa James Rugemalira.

Fedha hizo zinazodaiwa  zilikuwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow, alipokea kama tuzo kutokana na malipo yaliyotolewa katika akaunti hiyo kwenda Pan Africa Solutions Limited (PAP).

Mshtakiwa  huyo alikana shtaka, upelelezi ulikuwa umekamilika  na akaunti yake hiyo inayodaiwa kutumika kupokea fedha hizo ilizuiwa na mahakama kwa muda, mtu yeyote hakuruhusiwa kufanya kitu chochote kwenye akaunti hiyo. Alikuwa nje kwa dhamana.

Mshtakiwa huyo alikuwa nje kwa dhamana baada  ya kukamilisha masharti aliyopewa.

Haya Hapa Ndio Makosa ya Mwanaume Yanayosababisha Mke au Mchumba Amsaliti

$
0
0
Kuna sababu anuai zinazomfanya mwanamke amsaliti mumewe. Ni muhimu kutambua kuwa mwanamke ni kiumbe mwenye hisia kali na daima ahisi raha na amani. Baadhi ya nyakati hufanya usaliti ili kuziba pengo la upungufu unaotokea katika maisha yake. Zifuatazo ni sababu kubwa ambazo zinamfanya amsaliti mumewe:

1. KUTOMPA KIPAUMBELE NA KUTOMTHAMINI

Tunatambua kuwa mke anafanya kazi kubwa sana ambayo lau kama ingekuwa ni kampuni basi pangehitajika watu zaidi ya 10 kuzifanya. Atamtunza mume, watoto, nyumba na familia kwa ujumla.

Wakati fulani mume anaweza akampuuza na asimthamini, licha ya kujitoa kwa moyo wote kumtunza na kuihudumia familia. Hivyo, kutotoa kipaumble kwa mke ni kosa kubwa ambalo linaweza likamgharimu mume, mke akipata mtu anayempa kipaumbele na kumuonesha thamani hakika hataacha kuitumia hiyo fursa.

2. UKOSEFU WA MAHABA

Kwa asili mwanamke ana silika ya hitajio la kupendwa, mwanamke anahitaji kupendwa, mwanaume yeye ana silika ya kupenda ngono, ukimpa ngono tu basi anaridhika.

Mwanamke anahitaji kupetiwapetiwa, anahitaji kudekezwa, anahitaji aambiwe maneno yenye ladha adimu yaliyochanganywa na vionjo vya ndimu, mwanamke anataka hivyo, anataka aone kama anapendwa, anataka aone mtu anamwambia vile alivyo, alivyo maridhawa, amueleze hisia zake, ampe lugha ya kimajnun, mwanamke anamtaka Majnun. Sasa akimpata mtu wa aina hiyo, tofauti na mumewe, huwa ni balaa tupu, mnanipata hapo?

3. USALITI WA MUME

Miongoni mwa mambo ambayo huibadilisha roho ya mwanamke ni pale anapogundua kuwa mumewe kipenzi anamsaliti. Hapo mwanamke anaweza akabadilika kabisa. Wapo wanaosamehe, lakini wapo wanaolipiza kisasi.

4. KUTOJIAMINI

Mwanamke anahitaji mwanaume anayemfanya ajiamini iwapo mumewe hatekelezi jukumu hilo, akimpata mtu anayemfanya ajiamini, yanaweza kutokea mengine kabisa. Hivyo, nasaha zangu kwa kaka zangu kuyaangalia kwa makini mambo haya.

Jiji la Mwanza Lasimama...Wenje Ashinda Kesi ya Pingamizi Lililowekwa na Mabula Mahakamani

$
0
0
Aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana Ezekiah Wenje ameshinda pingamizi aliyowekewa na mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula

Kesi ya msingi itaanza kusilizwa tarehe 6|03|2016.

Jiji limesimama kwa muda watu wanashangili kwa furaha mama ntilie machinga ..wanashingilia taarifa kamili tutawaletea baadae.

Godbless Lema Afunguka Baada ya Ezekiel Wenje Kushinda Pingamizi la Mbunge Babula Kwenye Kesi ya Uchaguzi

$
0
0
Mara tu ya Taarifa kusambaa kuwa Aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana Mwanza Ezekiel Wenje ameshinda pingamizi lililowekwa na Mbunge Mabula kesi ya uchaguzi Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema Ameandika haya kwenye ukurasa wake wa Facebook:

"Hongera Ezekia Wenje kwa kushinda pingamizi lilowekwa na Mabula kwenye kesi yako ya Uchaguzi ni hatua kubwa ya kurudi bungeni na kuwatumikia wana Mwanza" Godbless Lema

Source:Ntukula Boaz 

Halima Mdee (Kawe) na Mwita Waitara (Ukonga) na Makada Wengine Watatu Wafikishwa Mahakamani Leo

$
0
0
Mbunge wa Kawe Halima Mdee na wenzake wanne  wamefikishwa mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam na kusomewa  shitaka moja la kumjeruhi katibu tawala wa mkoa wa Dar es salaam

Halima Mdee akiwa na mbunge mwenzie Mwita Waitara wa jimbo la Ukonga  pamoja na makada wengine watatu wa Chadema  wamekana shitaka hilo na wametakiwa kujidhamini wenyewe kwa kiasi cha Shilingi Milioni mbili kila mmoja.

Mahakama hiyo imewaachia kwa dhamana baada ya kuweza kujidhamini

Baraka Awaponda Wasichana Wanaomshobokea Kimapenzi..Atoa Onyo na Kusema Ameshamjua Anayewatuma Wasichana Hao

$
0
0
Kwenye ukurasa wake wa Instagram Baraka amepost picha akiwa na mwananmke lakini hakumuonyesha sura ni nani, na kusema kuwa mwanamke huyo ndiye anayemtambua na sio wengine.

"My life na uyu tu ndio namtambua, hao mnawatambua ninyi, haya ni maisha yangu,na yapo kwenye serekali yangu, ustake niishi unavyotaka, mnajaribu sana kuchafua jina langu kwa mashabiki zangu, na pia mnajarbu kushusha heshima yangu kwa wanaonieshimu ila mmechelewa sana, nachoamini shabiki wa kweli awezi nichukia kwa upumbavu au uvumi wa kijinga unaoendelea, hii ya mtoto imegoma tengenezi nyingine tena,na tambueni haya ni maisha yangu #SUPER na tumeshamjua anaewatuma kunichafua", aliandika Baraka da Prince.
Hivi karibuni Baraka alikanusha kuwa na mahusiano na msanii wa filamu za kibongo Nisher ambaye alikuwa anasema kuwa ni mpenzi wake, na kusema akuwa yeye ndio baby mama wake kwani ana ujauzito wake.
Viewing all 104694 articles
Browse latest View live




Latest Images