Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104428 articles
Browse latest View live

Shamsa: Mkongo wa Wolper,Wema Amenitongoza

0
0
STAA wa filamu Bongo, Shamsa Ford juzikati alimwaga ‘ubuyu’ hadharani kwa kusema kwamba, yule jamaa Mkongo ambaye amekuwa akidaiwa kutoka na Wema Sepetu, Jacqueline Wolper amemtongoza.

Akizungumza na kona ya Bongo Movies Shamsa alisema, hivi karibuni alienda saluni na kukutana na ujumbe wa Mkongo wa Wema, Wolper ukimuhitaji kimapenzi jambo ambalo lilimuudhi sana.

“Hii si mara ya kwanza kunitongoza kwani nakumbuka kuna siku mtu aliniomba namba ya simu na baadaye nikapigiwa na huyo Mkongo akinihitaji hotelini kuongea mambo ya filamu nikamwambia amtafute meneja wangu akakataa na kung’ang’ania niende mimi nikakataa,” alisema Shamsa.

Chanzo: GPL

Vodacom, Tigo, Airtel, Smart na Zantel Zapigwa Faini ya Mamilioni ya Pesa Na TCRA Kwa Kutoa Huduma Mbovu za Mawasiliano

0
0
Kufuatia malalamiko kuhusu huduma duni za mitandao ya simu nchini, Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imezitoza faini kampuni kwa kushindwa kuwajibika katika huduma zao.

Kampuni za simu zilizopigwa faini kutokana na kutoa huduma mbovu ni pamoja na Airtel, Smart, Tigo, Vodacom na Zantel. Pamoja na hivyo, zimetakiwa kuboresha huduma zake ndani ya miezi sita.

TCRA imefanya tathimini juu ya ubora wa huduma za mawasiliano ikiwemo sauti na data zinazotolewa na kampuni hizo ambapo imebainika kutowatendea haki watumiaji wake.

“TCRA inazipiga faini kampuni hizi zinazoanzia milioni 12.5 mpaka milioni 27.5 na inazitaka kuboresha huduma zao, miezi sita tangu siku ya kutolewa kwa tangazo hili,” imeeleza sehemu ya taarifa ya TCRA kwa vyombo vya habari.

Usumbufu unaotajwa na TCRA ambao unafanywa na mitandao hiyo ni pamoja na kudai namba haipatikani ilihali ipo hewani, kudai namba inatumika ilihali sivyo, kukata salio la mteja pasipo ridhaa yake na kukatika kwa mawasiliano mara kwa mara.

Kampuni ya Vodacom ndiyo iliyopigwa faini kubwa zaidi (milioni 27.5) huku Kampuni ya Smart ikipigwa faini ndogo zaidi (milioni 12.5), faini hizo zimetozwa kulingana na ukubwa wa makosa ambayo kampuni husika imekuwa ikiyafanya katika utoaji wa huduma zake.

Kampuni ya Airtel imepigwa faini ya Sh. 22.5 milioni, Zantel Sh. 25 milioni na Tigo Sh. 25 milioni. TCRA imezitaka kampuni hizo kulipa faini hizo haraka iwezekanavyo na kuboresha huduma zao kabla ya mamlaka hiyo kuchukua hatua kali zaidi.

Kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta Sura ya 306 mamlaka hiyo hapa nchini inayo mamlaka ya kutoa adhabu kwa kampuni yoyote inayokiuka masharti ya leseni ya utoaji huduma.

Mkubwa Fella Akanusha Wasanii Wake Kujihusisha na Biashara ya Madawa ya Kulevya

0
0
Meneja wa Kundi la TMK Wanaume Family na Yamoto Band, Mkubwa Fella amekanusha madai ya

Akiongeza na Sporah Show ya Clouds TV Jumamosi hii, Fella aliulizwa kwamba kuna taarifa zina sambaa kuwa wasanii wake pamoja na yeye mwenyewe anajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.

“Hakuna madawa ya kulevya wala nini,” alisema Fella.

Aliongeza, “Mimi mwenyewe nakituo changu cha kuwasaidia walio athirika na madawa ya kulevya. Teja wowote akitaka kuja kupona ni bure, sasa kama mimi ni muuzaji tena kwanini niwatibu, si napoteza wateja,”

Huyu Ndiye Wema Sepetu Tunayempenda

0
0
Wema Sepetu ni mwanamke maarufu si Tanzania tu bali Afrika Mashariki na ana mashabiki wengi zaidi – #TeamWema. Tangu awe Miss Tanzania mwaka 2006, mrembo huyu ameendelea kuwa kwenye headlines bila kupunguza.

Umaarufu wake ulichangiwa zaidi na mahusiano yake ya kimapenzi na watu maarufu kuanzia TID, Mr Blue, marehemu Steven Kanumba, Diamond na hivi karibuni, mshindi wa BBA 2014, Idris Sultan. Lakini niseme kuwa uhusiano wake na Diamond ndiyo uliomulikwa zaidi kuliko mwingine wowote.

Ni katika uhusiano wao, jina la Diamond lilivuma zaidi hasa kwakuwa kipindi wanaanza, Wema alikuwa tayari kwenye kilele cha umaarufu, na hitmaker huyo alikuwa ameanza kuikwea ngazi.

Kwa kipindi chote hicho, Wema amekuwa ni brand kubwa. Wema ni mgodi unaotembea. Hii ni kwasababu hakuna staa mwingine wa kike Afrika Mashariki mwenye kundi kubwa zaidi la mashabiki nyuma yake. Ni kundi kubwa ambalo lipo tayari kumtetea na kumpigania katika nyakati zote, mbaya au nzuri.

Kundi hili limeendelea kuwa aminifu kwake hata pale anapoanzisha uhusiano na mtu mwingine. Lilikuwa nyuma yake kipindi yupo na Diamond na hadi walipoachana. Limeendelea kumfuata kipindi ameanzisha uhusiano na Idris kiasi cha kuifanya couple hiyo itengeneze headlines nyingi ndani ya muda mfupi.

Kwahiyo kwa namna yoyote ile, Wema ni brand inayoweza kuingiza fedha nyingi. Japo alitakiwa kuwa mbali sana kutokana na ushawishi alionao, nafurahi kuona kwamba tayari ameigundua thamani yake na kuanza kuitumia. Napenda kumuona Wema huyu wa sasa ambaye akili yake imefocus zaidi kibiashara na kupush brand yake ya lipstick, Kiss by Wema Sepetu.

Napenda ninavyoona anavyotumia nguvu kuisambaza na kutafuta mawakala nchi nzima. Ninachofurahia zaidi ni kuona kuwa anaisambaza hadi Kenya ambako kuna mashabiki wake wengi sana. Lipstick zake zipo katika rangi mbalimbali na kwa muonekano wa picha ninazoziona, zinaonekana ziko poa.

Cha msingi sana mashabiki wake wa kike na hata wanawake wengine tu wanaopenda urembo, wamuunge mkono kwa kununua bidhaa za mzawa. Ni kwa kufanya hivyo ndivyo tunavyoweza kutengeneza mastaa ambao hawaiishi kuwa na majina tu, bali pia wanakuwa na uwezo kifedha. Naamini huu ni mwanzo wa Wema kuliwekea thamani jina lake na kutengeneza bidhaa nyingi zaidi sababu wateja wapo.

Leo ameanza na lipstick, kesho anaweza kuja na perfume, lotion, mafuta na bidhaa zingine kibao. Cha msingi napenda kuona akiendelea na mzuka huu wa kupush brand yake yeye mwenyewe kwa nguvu zote. Ni hivi ndivyo wanavyofanya mastaa wa nje kama akina Diddy kupromote bidhaa zao.

Kwa kufanya hivi na kwa jitihada zake, haitachukua muda mrefu kampuni kubwa kuonesha interest ya kuwekeza mabilioni ya shilingi kwenye brand yake. Huyu ndiye Wema tunayempenda, na sio yule wa drama ambaye mwisho wa siku tumejikuta tukimpa jina The Drama Queen.

Source:Bongo 5

Rais Magufuli akutana na kufanya Mazungumzo na Rais Kenyatta na Rais Kagame

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, kando ya Mkutano Mkuu wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Mkoani Arusha, ambapo viongozi hao wamekubaliana kuimarisha mahusiano hususani katika masuala ya kiuchumi.

Baadhi ya maeneo waliyokubaliana kutilia mkazo katika mahusiano hayo, ni pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo inayounganisha nchi mbili ikiwemo ujenzi wa miundombinu, kukuza biashara na kuzalisha ajira kupitia viwanda.

Rais Uhuru Kenyatta amesema amefurahishwa sana kuona Rais Magufuli yupo tayari kuhakikisha nchi ya Kenya na Tanzania zinakuwa karibu, na miradi ya maendeleo inaharakishwa.

"Kwa sababu nia yetu sisi ni kuona maendeleo ambayo yatagusa mwananchi wa kawaida, tumalize umasikini, uchumi ukue, na hivyo hatuwezi kufanya tukiwa tumetengana" Amesisitiza Rais Kenyatta.

Kwa upande wake Rais John Pombe Magufuli, amesema Tanzania na Kenya zina kila sababu ya kuimarisha mahusiano ya kibiashara hasa katika ujenzi wa viwanda utakaozalisha ajira kwa kuwa watu wake ni wamoja.

"Wazee wetu Mzee Kenyatta na Mzee Nyerere walijenga mazingira mazuri ya kuwa na nchi hizi mbili wakati wakipigania uhuru, sasa sisi vijana wao ni wakati wetu kwenda mbele kwa ajili ya maendeleo"amebainisha Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli amebainisha kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinajenga mahusiano na ushirikiano zinalenga kupata manufaa hayo ya kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wake.

Ameutaja mradi mmojawapo kuwa ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Tanzania kwenda nchini Kenya kupitia Namanga, na akaongeza kuwa Tanzania itakapoongeza uzalishaji wa umeme na kuanza kuvuna gesi, itaiuzia pia Kenya, halikadhalika Kenya nayo itauza bidhaa zake Tanzania.

Kabla ya kukutana na Rais Kenyatta, Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame, ambapo viongozi hao wamekubaliana kuzidisha mahusiano kati ya Tanzania na Rwanda ambapo Rais Magufuli amemhakikishia kuwa serikali yake itakamilisha ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani "Standard Gauge" ili kurahisha usafirishaji wa bidhaa na watu.

Rais Kagame amempongeza Rais Magufuli kwa uongozi wake bora uliolenga kuimarisha uchumi, ikiwemo kuimarisha bandari ya Dar es salaam ambayo Rwanda inaitegemea na ujenzi wa Reli ya Kati ambayo pia ni tegemeo kubwa kwa uchumi wa Rwanda.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiano, IKULU
Arusha- 02 Machi, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.

==

January:Edward Lowassa Aliisaidia Sana CCM 2015 Kushinda Urais

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, January Makamba amesema uamuzi wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuondoka CCM, ulikuwa moja ya sababu ya chama hicho tawala kushinda urais katika Uchaguzi Mkuu wa  mwaka jana.

Makamba pia amemshauri Lowassa kuachana na harakati za kuwania urais kwa kuwa ni muda mrefu tangu alipogombea kwa mara ya kwanza mwaka 1995 na kuishia kwenye uteuzi ndani ya CCM.

“Kuondoka kwa Lowassa kwenda upinzani ndiyo kulirahisisha sisi (CCM) kushinda uchaguzi kwa sababu kuliwaondolea wapinzani hoja mbili muhimu ambazo ni ufisadi na mabadiliko,” alisema Makamba, ambaye alikuwa msemaji wa kampeni za CCM kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita, wakati wa mahojiano na Mwananchi ofisini kwake Jumapili.

Lowassa, ambaye alikuwa waziri mkuu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne kabla ya kujiuzulu mwaka 2008 baada ya kuibuka kashfa ya Richmond, alijiengua CCM Julai 28, mwaka jana ikiwa ni siku chache baada ya jina lake kuchujwa pamoja na wagombea wengine 33 wa urais kwa tiketi ya CCM.

“Niliwekewa mizengwe kuhakikisha jina langu halifiki Kamati Kuu na Halmashauri Kuu,” alisema Lowassa wakati akitangaza kujiengua CCM na baadaye akajitetea kuwa kuhusishwa kwake kwenye sakala la Richmond kulitokana na kupokea maagizo kutoka juu.

Akiwa Chadema, Lowassa alipitishwa kugombea urais na akaungwa mkono na vyama vingine vitatu vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), hali iliyomfanya aweke rekodi ya upinzani tangu kurejeshwa kwa vyama vingi baada ya kuzoa asilimia 39.97 za kura akizidiwa na John Magufuli wa CCM, ambaye alipata asilimia 58.4.

Katika mazungumzo na Mwananchi, Makamba alikiri CCM kupata ushindani mkubwa kutoka vyama vya upinzani katika uchaguzi huo uliokuwa na msisimko, lakini akasema kuhama kwa Lowassa kuliwapa nguvu zaidi.

“Kuhusu Lowassa kujiunga na upinzani kwamba ndio kuliwapa nguvu (Ukawa), hapana. Suala hili kwangu nalitazama tofauti,”  alisema Makamba.

“Mnapomchukua mtu (Lowassa) ambaye miaka 10 iliyopita mmekuwa ndiyo mnashika picha yake kwamba ni kielelezo cha rushwa na ufisadi ndani ya nchi na CCM, halafu mnamchukua, mnaenda naye kwenye kampeni maana yake ile hoja (ya ufisadi) mmeamua kuiachia.”

Makamba pia alisema Lowassa amekuwa sehemu ya mfumo wa utawala na uongozi wa nchi kwa miaka 40, hivyo hawezi kuwa kinara wa mabadiliko.

Alisema kitendo cha Chadema kuhubiri mabadiliko huku mgombea akiwa Lowassa, maana yake ni kwamba wameamua kuiacha hoja hiyo.

“Kwa tathmini yangu na utafiti tulioufanya, hizo hoja mbili ambazo siku zote zilikuwa silaha za upinzani, wameamua kuziachia na matokeo yake ilikuwa rahisi kwetu (CCM) kupata ushindi,” alisema.

Alipoulizwa atamwabia Lowassa nini siku wakikutaka, Makamba alisema: “Kwanza, nimemsikia akisema atagombea tena mwaka 2020, nitamwambia mambo mawili;  hii habari kuwa aliibiwa kura aachane nayo maana si kweli, pia inampunguzia heshima maana uchaguzi umeisha na wananchi wameridhika lakini wewe peke yako unabaki kualalamika.”

Pili, alisema hoja ya pili itakuwa ni kumshauri asigombee urais mwaka 2020 kwa kuwa CCM watamshinda na atakuwa ametumia miaka 25 kuwania nafasi hiyo bila mafanikio.

“Alianza kuutaka urais mwaka 1995 ni  kipindi kirefu na mle bungeni tutakuwa na wabunge ambao kabla hawajazaliwa, Lowassa alikuwa anagombea. Nadhani nchi hii watu wana vipaji, waachiwe nafasi watoe mchango wao kwenye kujenga demokrasia ya nchi yetu. Kifupi apumzike,” alisema Makamba.

Katika uchaguzi wa mwaka 1995, Lowassa aliondolewa mapema kwenye mbio za urais kwa tiketi ya CCM na mwaka 2005 hakuchukua fomu, badala yake akawa nguzo kuu ya kampeni za rafiki yake, Jakaya Kikwete ambaye aliibuka kidedea CCM na baadaye kushinda urais. Baada ya uchaguzi, Kikwete alimteua Lowassa kuwa Waziri Mkuu.

Akizungumza na wazee wa Chadema jimbo la Ubungo hivi karibuni, Lowassa aliwataka kutokata tamaa na kujipanga kimkakati kujiandaa na kuimarisha chama kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2020 na kuahidi kugombea tena.

Nguvu ya upinzani

Makamba pia alisema alitegemea nguvu ya upinzani kuongezeka kadri muda unavyokwenda kwa sababu baada ya zaidi ya miaka 23 tangu kurejeshwa kwa mfumo wa siasa za ushindani, upinzani usingeendelea kubakia uleule.

Alisema hivi sasa mwamko wa Watanzania katika kusikiliza mawazo na fikra tofauti umeongezeka na kwamba CCM imepewa  changamoto kutokana na mabadiliko ya mfumo katika jamii, uhuru wa habari, wa kuamua na kujieleza.

“Yaliyotokea ni matokeo ya mafaniko ya maendeleo ya demokrasia katika nchi yetu miaka 10 iliyopita,” alisema.

Alisema hali hiyo imewafanya wananchi kutoogopa kujitokeza na kuunga mkono waziwazi upinzani, akivituhumu baadhi ya vyombo vya habari kujipambanua msimamo wake kwa wagombea wa upinzani.

Wanaomponda Rais Magufuli

Kwa nyakati tofauti viongozi wa Chadema, wakiongozowa na mwenyekiti wao Freeman Mbowe wamenukuliwa wakisema kuwa mambo yanayofanywa na Rais Magufuli ni mawazo ya wapinzani na yapo katika ilani ya uchaguzi ya Chadema, lakini Makamba amepinga akisema wanamsifia Rais ‘kwa mamna yake’.

“Nadhani wanajaribu kudandia treni inayokwenda vizuri. Pengine ndiyo namna nzuri ya kiungwana ya kumsifia mtu kwa sababu wamekosa ujasiri wa kusema anafanya kazi nzuri,” alisema Makamba.

“Ilani yetu ukiisoma ina vipaumbele vikubwa vinne; cha kwanza ni kupinga rushwa, uzembe na ubadhilifu wa mali ya umma. Hatua zinazochukuliwa sasa ni ahadi tulizotoa katika ilani. Pili, wakati wa kampeni Rais Magufuli aliahidi haya anayofanya. Tulitegemea atayafanya kwa sababu aliyasema katika kampeni.”

Alisema CCM ilimteua Magufuli kwa sababu ilijua inateua aina ya kiongozi atakayesaidia kutokana na kujulikana kwa utendaji wake.

“Hiyo ilani ya Chadema sisi hatuijui na hata mgombea wao alikuwa anaongea dakika tatu, sasa kwa muda huo ataongea jambo gani la kuigwa,” alisema Makamba huku akieleza mambo mengine mawili yaliyokuwepo kwenye ilani ya CCM kuwa ni ajira na umasikini.


Ukivunja sheria, uhusiano mzuri utakosa - BASATA

0
0
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha east Africa Radio, Afisa habari wa BASATA Artides Kwizela, amesema wao kama chombo cha serikali kazi yao ni kuratibu kazi za wasanii, na iwapo zimeenda kinyume lazima litaingilia kati, kwani uhusiano mzuri hauwezi kukaa kimya pale mambo yanapokwenda kinyume.

"Linapokuwa limetokea suala fulani BASATA inaiunuka inasema no, ni kwa sababu kunakuwa kuna mambo fulani hajaenda sawa, na sisi kazi yetu kama BASATA ni kuratibu sekta ya sanaa, ni kuhakikisha kila kitu kwenye sekta ya sanaa kinakwenda kwa utaratibu, kwa hiyo kunyoosheana kidole au BASATA kusimama na kusema no, ni kwasabau kunakuwa kuna taratibu fulani hazijafuatwa, kwa hiyo kitu ambacho ni cha msingi uhusiano wowote ule hauwi uhusiano unaelekeza kwenye kuvunja sheria", alisema Bwn. kwizela.

Pamoja na hayo BASATA imesema wasanii wanatakiwa kutumia ubunifu zaidi katika kufikisha ujumbe wao, na sio kwa kutaja majina na kutumia lugha chafu, ili kufikisha ujumbe wao kwa hadhira.

"Sanaa ni ufundi ni ubunifu, na katika vitu ambavyo ni vya wazi ambavyo msanii lazima avizingatie ni matumizi tu ya lugha ya picha ya kawaida lakini linafikisha ujumbe, sio lazima ufikie hatua ya kutaja majina ya watu na kuwatukana watu ndio ufikishe ule ujumbe mzuri", alisema Bwn. Kwizela.

Edward Lowassa Bado Una Nafasi Kubwa Kwangu -Shamsa Ford

0
0
Msanii wa filamu nchini na aliyekuwa akitoka kimapenzi na msanii Nay wa Mitego amefunguka na kusema kuwa bado aliyekuwa mgombea wa urais nchini mwaka jana.

kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo yupo moyoni mwake.
Kupitia Account yake ya Instgram Shamsa Ford alipost picha ya Mh Edward Lowassa na kusema ni kumbukumbu yake lakini siku zote atakuwa na nafasi moyoni mwake.

"My FIRST TBT...YOU will always have a space in my heart dady...✌✌" Aliandika Shamsa Ford
Kipindi cha kampeni za uchaguzi Shamsa Ford alikuwa ni kati ya wasanii ambao walionyesha wazi kumpa support Mgombea wa urais kwa tiketi ya CHADEMA na aliyekuwa akiungwa mkono na UKAWA, Mh Edward Lowassa.

Lakini kutokana na post hiyo wapo baadhi ya mashabiki ambao walionyesha kutopenda ujumbe wake huo huku wengine wakimuunga mkono kwa kusema kuwa Edward Lowassa alistahili kuwa kiongozi wa juu wa nchi, kama ambayo Comment zinavyosema hapo chini.
"Miaka elfu moja haitatokea awe Rais labda awe Rais wako wewe Shamsa na Nay mibangi wako" Peterteddy31

"Huyo hatumtaki sasa hivi hapa ni kutumbua mijipu tu mabadiliko peleka Monduli maana tulichotaka tunakiona kwa Magufuli wewe huna jipya" Alisema Saidi_geleta
"Huyo ndio Mr president wangu hata wanune ukweli wanaujuaaa u winn" Alisema mc_nyemolicious
"Hapo nakupendaga sana Shamsa Ford, ni vizuri kuamini unachoamini ni sawa, na ni mbaya kumdhihaki mtu anachoamim" Alisema frankatilio

Pendeza na Kessy Products..Pata Dawa za Asili Zisizo na Madhara Wala Kemikali Yoyote

0
0

PENDEZA NA KESSY PRODUCT.
PATA DAWA ZA ASILI ZISIZO NA MADHARA WALA KEMIKALI YOYOTE,
NA MATOKEO KUANZIA WEEK (2) ADI (4) NAKUENDELEA

1) KUTOA MVI SUGU 70,000/
2) REFUSHA NYWELE NA KUZUIA KUKATIKA 50,000/
3) TENGENEZA SHEP HIPS NA MAKALIO KWA
@ KUPAKA 50,000/
@ DAW YAMAJI 80,000/
@ VIDONGE 100,000
4) PUNGUZA TUMBO NA NYAMA UZEMBE KWA
@ KUPAKA 55,000/
@ KUNYWAA 80,000/
@ MKANDA WENYE DAW 80,000/
@ BELT 150,000/
5)PUNGUZA MWILI MZIMA PAMOJA NA KILO 80,000/
6) ONGEZA UNENE WA MWILI MZIMA NA HAMU YAKULA 80,000/
7) PUNGUZA MAZIWA NA KUYASIMAMISHA 50,000/
8) ONGEZA MAZIWA SAIZ UNAYOTAKA 50,000/
9) ONGEZA NGUVU ZA KIUME KWA DAW
@ JELI YAKUPA 50,000/
@ VIDONGE 70,000/
10) ONGEZA MAUMBILE YA KIUME KWA
@ JELI YAKUPKA 100,000
@ MASHINE YA HUNDSOME UP 170,000/
11) KUWA MWEUPE MWILI MZIMA NA KUWA SOFTI 70,000/
12) TOA CHUNUS,MADOA,MAKOV 45,000/
13) RUDISHA USICHANA (BIKRA) 60,000/
14) TOA MICHIRIZI (STERCH MARKS) 50,000/
15) ONDOA NGIRI ZAAINA YOYOTE 60,000/
16) TUNDISHA NYWELE ZILIZO ISHA (KIPARA) 150,000/
17) TOA MICHUBUKO KWENYE MAPAJA NA SEHEM ZA SIR 60,000/
18) RUDISHA HAMU LA TENDO NA KUFANYA BILA KUCHOKA 60,000/
19) TOA NDEVU KWA WANAWAKE 80,000/

NA HUDUMA NYINGI USISITE KUSEMA PIGA SIMU,
TUNAPATIKANA DAR,K-KOO,POSTA NA SINZA.
KWAMIKOWANI UDUMA ITAKUFIKA KWANJIA YA MABASI BILA TATIZO.
CHAKUFANYA PG CIM 0719955528 0756259180 0785371237

PIA UTALETEWA POPOTE ULIPO

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya March 3, Ikiwemo ya Magufuli Kuhamisha Utumbuaji Majibu EAC

0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya March 3, Ikiwemo ya Magufuli Kuhamisha Utumbuaji Majibu EAC

Hatimaye Dr Slaa Afunga Ndoa na Josephine Mushumbusi Ughaibuni

0
0
Hatimaye aliyekuwa Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Josephine Mushumbusi.

Wawili hao walifunga ndoa nchini Canada jana katika kanisa  moja, lakini  habari zinaeleza si kanisa Katoliki ambalo Dr Slaa aliwahi kuwa Padri kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita.

Ndoa hiyo imetimiza ndoto za muda mrefu  za Dr Slaa ambaye mwaka 2010 aliyekuwa mume wa Mushumbusi alikimbilia mahakamani  akidai bado anamtambua Josephine  kuwa ni mke wake wake halali.

Mume huyo alidai Dr Slaa alimpora mke wake, hivyo akaitaka mahakama  impatie haki  yake. Hata hivyo kesi hiyo haikupewa mashiko makubwa.

Misukosuko ya wawili hao iliendelea ambapo mwaka 2012 aliyekuwa  mke wake, Rose Kamili alifungua kesi kupinga ndoa hiyo huku akitaka alipwe milioni 50.

Dr Slaa na Mushumbusi wanaishi kwa takribani miaka sita sasa na waliwahi kuanza maandalizi ya kufunga ndoa wakiwa hapa nchini lakini wakashindwa kutokana na mapingamizi hayo

Mbunge wa Kinondoni (CUF) Maulid Mtulia Apinga Mpango wa DC Makonda Kuwaruhusu Walimu Wasafiri Bure Kwenye Daladala

0
0
Mbunge wa Kinondoni, (CUF), Maulid Mtulia amepinga mpango wa walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam kusafiri bure kwenye daladala akisema utawashushia heshima.

Badala yake, alitaka Manispaa ya Kinondoni iweke utaratibu wa kuwaongezea walimu fedha za usafiri kwenye mishahara yao ili wajilipie wenyewe.

Kauli ya mbunge huyo imekuja baada ya Mkuu wa Wilaya ya hiyo, Paul Makonda kutangaza kuwa walimu wa shule za Serikali za Dar es Salaam watasafiri bila kulipa nauli kwenye daladala.

Katika mpango huo ambao umepangwa kuanza Jumatatu ijayo unaozigusa pia manispaa za Temeke na Ilala, walimu watapatiwa vitambulisho maalumu vyenye saini ya Makonda.

Akizungumza katika mahojiano maalumu juzi, Mtulia alisema licha ya kuwa wazo lililenga kuwasaidia walimu, lakini litawasababishia dhihaka.

Alisema kinachopaswa kufanyika ni kutafuta suluhisho la kudumu la kero zinazowakabili walimu ambazo zinachangia kushuka kwa kiwango cha elimu nchini.

“Itafika hatua kondakta atamsimamisha mwalimu kwenye kiti kama ilivyo kwa wanafunzi kwa sababu tu halipi nauli… Wazo hili ni zuri lakini lilipaswa kuboreshwa kama kweli nia ni kumsaidia mwalimu,” alisema.

Alisema ikiwa kweli nia ni kuwasaidia walimu, basi halmashauri zina wajibu wa kuhesabu siku za kazi na kiasi ambacho mwalimu atalipia nauli ili fedha hizo ziongezwe kwenye mshahara wake.

Alisema njia hiyo itakuwa ya heshima zaidi kuliko walimu kusafiri bure kwa kutumia vitambulisho kama walivyo wanafunzi wao.

Hata hivyo, alisema ipo haja kwa viongozi wa manispaa hiyo kukaa meza moja na walimu ili kujua changamoto zinazohitaji suluhu ya haraka, akisema huenda nauli ikawa si ya msingi kwao.

Rais John Magufuli Awaaibisha Wale Waliokuwa Wanasema Hajui Kuongea Kiingereza

0
0
Unapozungumza jina la Dr John Pombe Magufuli ni jina lilopata umaarufu sana duniani kote kuanzia mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kwa sasa Dr. Magufuli (CCM) ndio Rais wa Tanzania awamu ya tano , Magufuli ni raisi mwenye busara, mvuto kwa jamii, weredi, jasiri,mwenye huruma na wanyonge,mzungumzaji mzuri(good speaker) na mtu mwenye uwezo mkubwa wa akili (IQ and EQ).

Katika kipindi cha kampeni mwaka jana kulitokea uzushi uliosambazwa na wapinzani juu ya mgombea wa CCM hususani UKAWA kwamba mgombea wa CCM Dr. Magufuli hajui kuongea Kingereza. Uzushi huu ulienezwa kwa kasi na kufanya baadhi ya watu kuamini kuwa ni kweli, lakini kumbe sio kweli ilikuwa ni kutaka kumchafua kisiasa. Rais Magufuli aliposhinda uchaguzi na kuwa rais alianza kuwadhihirishia kuwa anajua kuongea kingereza pale alipokuwa anakutana na wageni mbalimbali Ikulu na kuzungumza nao kwa lugha ya kingereza na wapinzani hao kukaa kimya kwa aibu.

Katika mkutano wa 17 wa EAC Raisi Magufuli akiwa mwenyekiti wa mkutano huo AMEWAAIBISHA KABISA WAPINZANI WAKE KWA KUONGOZA MKUTANO WOTE KWA LUGHA YA KINGEREZA na kuzungumza kingereza fasaha kabisa kwa ujasili na ubora wake ule ule kama akiwa anazungumza lugha adhimu ya Kiswahili. Pia haikuishia hapo Rais Magufuli akawadhihirishia wana EAC kuwa yeye ni bora katika lugha kwa kuzungumza lugha zote za EAC kuanzia KIGANDA, KINYARUANDA, KURUNDI, KIJALUO, na kushangiliwa kwa makofi makubwa na wajumbe wa mkutano huo kwa uwezo wake huo wa kuzungumza lugha mbalimbali kwa ubora ikiwemo pia KINGEREZA NA KISWAHILI kwa ubora wa hali ya juu.

Sasa ujinga wa kusema Magufuli hajui kingereza utakuwa ni unyumbu kwani lazima ujiulize, je, leo Magufuli kashikiwa mdomo sio yeye aliyekuwa anazungumza? Je, alivyoongea watu walikuwa hawamsikii au?? Je, anavyokuwa Ikulu na wageni nyie Nyumbu ndio mnakuwa mnamsemea?? Je , PhD yake ninyi nyumbu ndio mliomsaidia kusoma ?? Ukitaka kujua wewe ni Nyumbu sema tena Magufuli hajui ongea kingereza wakati EAC wote wamejionea wenyewe Jembe JPM akiunguruma Ngurudoto na kutumbua majipu ya EAC kwa kutumia kingereza, kwa kweli ukisema tena Magufuli hajui kingereza utakuwa nyumbu tu , maana utakuwa huna akili bali wewe una yako mengine au wewe ndio hujui kingereza.

Kweli Magufuli ni GIFTED LEADER tulienaye Tanzania , Tumuunge mkono na kumuombea kwa Mungu amlinde azidi kututumikia watanzania wote kwa ubora na weredi, leo kadhihirisha kuwa viongozi bora Afrika wataendelea kutoka Tanzania. HONGERA MAGUFULI KUONGOZA VIZURI MKUTANO EAC NA KUCHAGULIWA TENA KUONGOZA EAC KWA MWAKA MMOJA ZAIDI.

Majibu ya Baraka da Prince Baada ya Kudaiwa Kumtelekeza Mwanae

0
0
Msanii wa bongo Fleva,Baraka da Prince baada ya kudaiwa kumzalisha binti na kumtekeleza mtoto wake(stori hipo hapa) amekana na shtuma hizo na kusema kuwa yeye hawezi kufanya kitendo cha laana kama hicho.

Aidha Baraka amekiri kuwa na mtoto na anajivunia kiasi kwamba hawezi kukaa bila kutuma matumizi ya mtoto kama inavyodaiwa.Baraka ameweka wazi kuwa mama yake na ndugu zake wanaweza kuwa shahidi ni jinsi gani anamuhudumia mtoto huyo na ana mihamala ya simu inayoonyesha pesa alizotuma kwa mama mtoto wake.

Baraka amesema kuwa hana uhakika kama aliyetoa taarifa hizo ni mama wa mtoto wake kwani kwa anavyomjua sio mtu wa kuongea sana na amejaribu kumpiga simu hakupokea.

Pia Baraka kama mama wa mtoto wake ameamua kufanya hivyo itakuwa ni hila zake tu za kumchafua kwa kuwa labda walishaachana na anaona kuwa yuko na mtu mwingine na yeye ni staa na kuongeza kuwa zaidi ya kuzaa mtoto hawana mahusiano yoyote.

Baraka ameweka wazi pia hii ndiyo taarifa namba moja iliwahi kum dissapoint na kumuumiza kwa kuwa yeye anajua anajua ni jini gani anampenda mwanae halafu watu wanasema vingine.

Pia Baraka da Prince ameeleza kuwa aliwahi kumuona mtoto huyo alipokwenda Iringa kwenye show kwani hakuwa amewahi kumwona toka amezaliwa akaona ni vyema kumwona.

Rais John Magufuli Awashukia Umoja wa Afrika Mashariki Kuhusu Gharama za Mikutano ndani ya Hotel ya Ngurudoto Badala ya AICC

0
0
Wakati Rais Magufuli anatoa hotuba ya kufunga mkutano wa Afrika mashariki, uliofanyika ndani ya ukumbi wa Ngurdoto, alitema cheche zake na kuwapa picha halisi watu wa afrika mashariki, kuhusiana na ubanaji wa matumizi.

Rais anashangaa kwanini mikutano ya afrika ya mashariki ifanyike kwenye hoteli ya Ngurdoto wakati kuna ukumbi wa AICC ambao hauna gharama kama zinazotozwa na hoteli ya hadhi ya Ngurdoto. Rais Kenyatta aliinamisha kichwa huku akicheka, wajumbe wote kwenye ukumbi wakauelewa ujumbe wa ubanaji wa matumizi.

Lakini ni Ngurdoto hii hii ambayo wakati awamu ya nne inaanza kazi, ilihodhi semina elekezi, ambayo ilitumia fedha nyingi. Sina uhakika, nadhani kwamba mmiliki wa hii hoteli atakuwa ni mmoja wa vigogo wa nchi hii, hivyo tenda za uhakika kama vile semina elekezi na mikutano ya east africa, huwa ni kipindi cha neema.

Sekretarieti ya east african community imekumbushwa kuwa watu wa ukanda huu ni masikini, hivyo wasipende anasa za ajabu ajabu. Ni ujumbe mzuri, ila mmiliki wa hoteli ya Ngurdoto atauchukia sana uongozi mpya wa Rais Magufuli ndani ya jumuia ya afrika ya mashariki, katangaziwa njaa tangu mapema kabisa.

Zuio la Uchaguzi Meya wa Dar Lageuka Kaa la Moto..... Aliyelisoma asema Hakujua kama ni Halali au Feki

0
0
Baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kulikana zuio llilotumika kuahirisha uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, suala hilo limekuwa sawa na kaa la moto na hakuna mtu anayetaka kulishika.

Jana Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando, ambaye alikuwa mwenyekiti wa uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Jumamosi iliyopita,  jana alisema hajui lilikotoka zuio hilo kwa  kuwa alipewa tu na wanasheria wa jiji ili alisome kama lilivyo.

“Baada ya kufika eneo la tukio (kwenye ukumbi wa Karimjee), nilikabidhiwa zuio hilo nilisome. Suala la kujua kama limeisha muda wake au la naomba uwasiliane na mwanasheria wa jiji au mwanasheria wa mkoa, wao ndio walikuwa nalo na hata nilivyopoteza vitu vyangu vingine, hilo (zuio) wao wanalo,” alisema Mmbando.

Baada ya kutimiza wajibu wake, kama alivyotakiwa na wanasheria hao, alisema ndipo zilipozuka vurugu na yeye kupoteza nyaraka zake ikiwa pamoja na ajenda na miongozo ya kikao hicho.

Kwa upande wake, Mwanasheria wa Jiji la Dar es Salaam, Jackline Mosha, alisema hakupitia tamko hilo kabla ya kumpa aliyekuwa mwenyekiti wa uchaguzi huo na kwamba alilikuta kwenye ukumbi huo bila kujua limetoka wapi.

Alisema walijua kuna zuio hilo baada ya kufika katika viwanja vya Karimjee siku hiyo ya uchaguzi.

“Zuio lilitoka Februari 5, sisi tulijua siku ya tukio, tulimkabidhi mwenyekiti Mmbando alisome, hatukufahamu kama limeisha muda wake.

“Hatukupata muda wa kulipitia na kujiridhisha kwa sababu haikuwa siku ya kazi kwa mahakama. Hata hivyo zuio hili hatukupewa mapema, wangetupa mapema tungejiridhisha na yote hayo tungeyajua kabla ya siku ile,” alisema.

Kuhusu madai kuwa walitumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya hivyo, alisema wao ni wanasheria na kwamba wanafanya kazi kitaalamu.

Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene, amesema kuwa tayari ameagiza apelekewe taarifa rasmi na Theresia Mmbando, ili kubaini ukweli kuhusu zuio hilo kama lilikuwa la kweli au la.

Waziri Simbachawene alitoa kauli hiyo juzi na kusisitiza kuwa kwa wakati huo hakuwa na taarifa zinazothibitisha  zuio la kuahirishwa kwa uchaguzi huo lililosomwa na Mmbando kama ni la kweli au la.

“Kwa sasa kama wizara hatuna cha kusema kuhusiana na tukio zima lililitokea siku ile. Kama mnavyojua Katibu Tawala alipigwa anaumwa, yeye ndiye aliyesoma zuio hilo hivyo tunasubiri apone atuandalie taarifa kamili,” alisema na kuongeza:

“Kama Waziri sijapokea taarifa zozote zinazosema zuio hilo lilikuwa halali au la. Tusubiri kwanza atuandikie hiyo taarifa yake ili tufanye ulinganisho ndipo wizara itapata cha kusema,” alisema.

Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika kwanza Desemba, mwaka jana, ukapangwa kufanyika Januari 23, mwaka huu lakini na baadaye kupangwa kuwa Februari 8.

Februari 8, mwaka huu, madiwani baada ya kufika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya uchaguzi, walikabidhiwa barua ambazo hazikueleza sababu za kuahirishwa kwake bali utafanyika utakapopangwa tena na ndipo ulipopangwa kufanyika Jumamosi iliyopita.

Jumatatu wiki hii, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Warialwande Lema, alikanusha taarifa kwamba   mahakama hiyo imetoa zuio la uchaguzi huo.

“Mahakama ilitoa amri ya zuio la muda Februari 5, mwaka huu la kuzuia uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 8 na ilipanga kusikiliza maombi hayo Februari 15 lakini walalamikaji hawakufika mahakamani,” alisema na kuongeza:

“Mahakama ilipanga tena maombi hayo kusikilizwa Februari 23, mwaka huu, lakini pia walalamikaji hawakutokea mahakamani.”

Walalamikaji katika shauri hilo walikuwa Susan Massawe na Saad Khimji, dhidi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam.

Akiendelea kufafanua, Hakimu Lema alisema baada ya walalamikaji kushindwa kufika, mahakama iliondoa maombi ya zuio yaliyokuwa yamewasilishwa  mbele yake na walalamikaji pamoja na zuio lililokuwa limetolewa awali.

“Aliyesema mahakama imetoa zuio ni uongo kwa kuwa walitumia amri ambayo ilipitwa na wakati. Sijui chochote kuhusu zuio la Februari 27, mwaka huu,” alisema Hakimu Lema.

Kwa upande wake, Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi Cyprian Mkeha, alisema baada ya maombi hayo kuondolewa mahakamani, hajapokea maombi mengine kuhusu kuzuia uchaguzi huo.

Hivi Ndivyo Ezekiel Wenje Alivyovuka Kikwazo Cha Mabula Kesi ya Uchaguzi Mwanza

0
0
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, jana ilitupilia mbali kwa gharama pingamizi lililowekwa na upande wa wakili wa mjibu maombi wa kwanza, Stanslaus Mabula, katika kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo la Nyamagana.

Kwa kutupwa pingamizi hilo lililowekwa na Mabula, mbunge wa sasa wa  wa jimbo hilo, kesi hiyo itaanza kusikilizwa Jumatatu ijayo.

Jaji Kakusulo Sambo wa Mahakama Kuu Kanda Mwanza, alikubali kuahirisha shauri hilo baada ya kuridhika na sababu zilizotolewa na pande zote mbili, zikiomba kesi hiyo isikilizwe Machi 7, mwaka huu.

Upande wa mleta maombi ukiongozwa na wakili Elias Hezron, akisaidiana na Geofrey Kalaka, uliomba kuahirishwa kwa kesi hiyo baada ya wakili mwenzao mwandamizi, Deya Outa, kuugua. Waliomba muda wa kuandaa maombi mengine baada ya yale ya awali kutupiliwa mbali kwa gharama kutokana na kunukuliwa vibaya kwa vifungu vya sheria na kuiongoza vibaya mahakama.

Upande wa mjibu maombi namba moja (Mabula) aliyewakilishwa na wakili Constantine Mutalemwa akisaidiana na Faustine Malongo, waliiomba mahakama kuahirishwa kesi hiyo kutokana na kukubali sababu zilizotolewa na upande wa waleta maombi pamoja na wakili huyo (Mutalemwa) kusafiri kwenda jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kesi iliyoko katika Mahakama ya Rufani, hivyo kusababisha kutokuwapo jijini Mwanza.

Awali, Jaji Sambo alikubaliana na pingamizi lililowasilishwa mahakamani hapo na Wakili Mwandamizi wa Serikali Ajuaye Bilishanga, kuiomba mahakama kutupilia mbali maombi namba 8 ya mwaka 2016 kwa kuwa yalifunguliwa chini ya kifungu ambacho hakipo (kifungu cha 14 (1) sura ya 189 ambacho kilitakiwa kinukuliwe kifungu cha 89) hivyo kuiongoza vibaya mahakama, hivyo pingamizi la upande wa jamhuri lina mashiko na mahakama kukubaliana nalo na kulitupilia mbali kwa gharama.

Vilevile, ombi la upande wa mleta maombi la kutaka mahakama hiyo itoe ruhusa ya kupeleka maswali mawili kwa wajibu maombi wa kwanza na wa pili ambao wana nyaraka za fomu namba 21 (B) zilizotumika kwenye uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana, yamekataliwa na mahakama haitotoa kibali cha maombi hayo. badala yake hatua ya utoaji kibali Itafanyika wakati kesi ya msingi imeshaanza kusikilizwa.

Shauri hilo lilikuwa likiendelea huku umati mkubwa wa wafuasi wa Wenje wakiwa wanasubiri nje ya mahakama. Baada ya uamuzi ya Jaji, umati huo ulilipuka kwa nderemo na vifijo na kushangilia huku wakiimba Wenje, Wenje na kulisukuma gari lake.

Jaji Sambo amezitahadharisha pande zote katika kesi hiyo kujiandaa na uhakika uwapo mahakamani hapo kwa ajili ya usikilizwaji wa awali wa shauri hilo ambalo amekusudia kulipeleka haraka ili kufikia uamuzi mapema, kabla ya kuanza vikao vya Bunge Juni, mwaka huu.

Wenje alifungua kesi hiyo dhidi ya Mabula, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Nyamagana, Kitia Sylvester na Mwanansheria Mkuu wa Serikali.

Wassira Amvaa January Makamba...... Asema Huenda Yeye ndo Alibebwa Tano Bora ya Urais CCM

0
0
MWANASIASA mkongwe aliyekuwa waziri katika Serikali ya awamu nne, Stephen Wasira, amemshangaa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, January Makamba aliposema kuwa uwajibikaji katika utawala wa awamu ya nne ulikuwa ni wa kuleana.

Kauli ya Wasira imekuja siku moja baada ya gazeti la Mwananchi kumnukuu Makamba akisema uwajibikaji katika Serikali ya awamu hiyo haukuwa wa kuridhisha kwasababu kulikuwa na utamaduni wa kuoneana haya, kujuana na kusitiriana.

Akizungumza  katika mahojiano maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake Mbezi jijini Dar es Salaam jana, Wasira alieleza kushangazwa na kauli hiyo ya Makamba akisema yawezekana aliyelelewa ni yeye.

“Labda alilelewa yeye…kama rafiki yangu Makamba anasema kulikuwa na kuleana, mimi kwa upande wangu sikulelewa nilifanya kazi na nikatimiza wajibu wangu kama nilivyopewa na Rais.

“Sasa kama aliona kulikuwa kuna kuleana mimi sijui yeye ndiye anajua maana mimi sikulelewa. Kama unafanya makosa halafu unaachwa huondolewi hapo ni kuleana.

“Na yeye inawezekana alilelewa maana kuna watu wanasema kuingia kwake tano bora ya urais alipendelewa labda huko ndio kulelewa ndio maana akasema hivyo,”alisema Wasira.

Wasira ambaye aliongoza kamati iliyoandaa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015, alisema kasi ya utumbuaji majipu aliyoanza nayo Rais Dk. John Magufuli ipo katika ilani ya chama hicho tawala na kwamba walipanga hivyo.

Mwanasiasa huyo ambaye alikuwa waziri katika kipindi chote cha miaka 10 ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete, alisema si kweli kama ambavyo baadhi ya watu wanasema kwamba Serikali ya awamu ya nne haikufanya kitu, bali ilikuwa ikitumbua majipu kwa mtindo wa kimya kimya.

Alisema kila awamu inayoingia madarakani inakuwa na mtindo wake wa kufanya kazi na kwamba ni vigumu kulinganisha na awamu nyingine.

“Kila kiongozi ana ‘style’ yake, huwezi kulinganisha wakati wa Magufuli na Nyerere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete hawa ni watu ‘individuals’ kila mtu ana mtazamo wake wa kuongoza na kila mtu ana ilani kwa wakati wake.

“ Wengine mara wanasema hatukuwa na Serikali awamu iliyopita wakidai kwamba haikufanya kitu, si kweli kabisa, Serikali ilikuwepo, lakini ili concentrate (kujielekeza) kwenye nini…lazima tufanye tathimini. Kila Serikali ina mazuri na mabaya.

“Ukitaka kufanya tathimini unawezaje kusema Jakaya Kikwete hakufanya kitu? Wakati alijenga shule nyingi za kata, barabara zilizojengwa wakati Magufuli akiwa waziri wa ujenzi hazikuwa zake bali ni mpango wa Serikali ya awamu ya Kikwete.

“Hakuna Serikali iliyo perfect (kamilika)na huku inaongozwa na wanadamu. Kila Serikali ina style yake na awamu ya nne ilikuwa ya kimya kimya kama nilivyoeleza. Ilifanya vizuri, mengine haijafanya sana na mengine haikufanya kabisa.

“Ukifanya uchunguzi Serikali zote utakuta kuna mazuri na mabaya. Mwalimu Nyerere alikuwa anaipenda Tanzania na Watanzania kutoka moyoni mwake na alikuwa tayari kufanya kazi bila kulipwa na wakati anastaafu akasema chukueni mambo mazuri tuliyofanya, mabaya acheni…hapo aliona kabisa Serikali haikuweza kutimiza yote,”alisema Wasira.

Kutokana na hilo, Wasira alisema popote duniani hakuna Serikali ambayo inaweza ikafanya kila kitu kwasababu hakuna binadamu aliye malaika.

“Hakuna Serikali itakayofanya kila kitu hata Magufuli ataacha mengine na mwingine atayakuta. Hakuna Serikali inayoongozwa na malaika bali inaongozwa na wanadamu. Kuendesha nchi si jambo dogo kwasababu ina mambo mengi.

“Matatizo ya bandari yalikuwepo na si kwamba yameisha. Mfano hivi sasa wamebadili jina la rushwa kuwa posho…kwa hiyo hivi sasa wamegeuza rushwa kuwa posho.

“Kwa kasi hii sasa wafanyakazi watarudi nyuma na kufanya kazi kwa nidhamu zaidi, lakini vichwa maji nao watatumia ‘style’ nyingine tu kama hiyo ya kugeuza rushwa kuwa posho,”alisema Wasira.

Wasira ambaye alikuwa miongoni mwa wanachama wa CCM waliojitokeza kutaka kuteuliwa na chama hicho kuwania urais, akizungumzia uteuzi huo alisema hakukuwa na namna kwasababu waliojitokeza walikuwa wengi.

“Walikuwepo watu 38 waliochukua fomu na kurudisha, wakateuliwa watano si kwamba walikata majina bali waliteua. Kanuni ya CCM ndiyo inasema hivyo sasa hivi hata nikisema haki haikutendeka itasaidia nini wakati uchaguzi ulishapita?

“Kanuni ya chama haisemi lazima waitwe ndio wahojiwe bali Kamati Kuu inajadili jina moja moja… kwa kuwa mimi sikuwepo ndani ya kikao hicho sijui kama nilijadiliwa… sielewi.

“Lakini nilisikitika kama binadamu na sikufanya chochote zaidi ya kusikitika maana ndio utaratibu wa chama inawataka watano,”alisema mwanasiasa huyo.

Akizugumzia kuhusu hali ya kisiasa visiwani Zanzibar, Wasira alikishauri Chama cha Wananchi (CUF) kikubali kushiriki uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20, mwaka huu kwasababu wapiga kura ni wale wale.

Alisema amani ya Zanzibar ipo mikononi mwa Wazanzibari kwa kushiriki uchaguzi huo.

“Ili kuwe na amani Zazinzibar CUF waende kwenye uchaguzi kwasababu wapiga kura ni walewale, kama wanajua walishinda hofu yao nini?…hata wakirudia watashinda.

“Ushauri wangu kwa Wazanzibari wasaidie katika kuleta amani, wapige kura…wanaoipigia CUF au CCM na vyama vingine wafanye hivyo halafu kura zihesabiwe mshindi atangazwe kwa sababu hakuna namna kwa vile Mwenyekiti wa ZEC alisema uchaguzi uliopita ulikuwa na kasoro,”alisema.

Wasira ambaye alikuwa Mbunge wa Bunda kwa muda mrefu, akielezea kuhusu namna alivyoshindwa na upinzani katika uchaguzi wa mwaka jana katika jimbo hilo, alisema uchaguzi huo haukuwa wa huru na haki.

“Uchaguzi ule uligubikwa na corruption (rushwa), ulikuwa na kasoro nyingi sana…hakukuwa na uchaguzi pale, lakini kwa kuwa bado suala hili liko mahakamani tuliache kwanza,”alisema.

Credit:Mtanzania

Belle 9: Mimi Sina Tatizo na Diamond, ni Baada ya Watu Kuhack Akaunti yake na Kumtukana Diamond

0
0
Watu wasiyo julikana wamehack akaunti ya facebook ya msanii Belle 9 na kuweka post yenye picha ya msanii Diamond na kuandika maneno yanayoashiria matusi ya nguoni.
Belle99

Akizungumza na Bongo5 Alhamisi hii, Belle 9 amesema yeye anajulikana sio msanii wa kufanya vitu kama hivyo.

“Mimi sina tatizo na msanii wala sina upande wowote,” alisema Belle 9.
“Hili ni tatizo kama matatizo mengine, ni geni kwangu kwa sababu halijawai tokea lakini kwa wasanii wengine yalishatokea. Kwa hiyo naweza sema bado watu wangu wanaendelea kurekebisha tatizo na kuirudisha akaunti yangu. Mimi naimani kuwa watu wameelewa kwa sio mimi kwa sababu mimi sio mtu wa mambo hayo,” aliongeza Belle.

Ali Kiba Asema Atahakikisha Anafanya Kazi na Master Jay na P – Funk

0
0
Staa wa muziki Ali kiba amedai anatamani kufanya kazi na producers wa Kitambo kwenye sanaa Tanzania, Master Jay wa MJ Records pamoja na P Funk Majani wa Bongo records.
Ali Kiba

Akizungumza katika kipindi cha The playlist cha Times Fm, Kiba amesema hakuwahi kufanya nao kazi ndio maana ana hamu nao sana.

“Kiukweli Master Jay na P funk natamani sana kupiga nao kazi, na naahidi kuwatafuta na kufanya nao kazi, kwa hiyo fans wangu wategemee kazi nzuri ntakazofanya nao” alisema.

Katika ‘line’ nyingine King kiba amedai, anamkumbuka sana pia producer aliyetengeneza kazi zake kadhaa, KGT kwa sababu alikuwa ni zaidi ya mwalimu wa muziki kwake.
Viewing all 104428 articles
Browse latest View live




Latest Images