Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

Kama Kweli Ray Anatumia Mkorogo Basi Yuko Hatarini Kupata Magonjwa Haya Kumi

$
0
0
Lile sakata la nyota wa sinema Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ kudai kwamba, siku hizi amekuwa mweupe pee kwa sababu ya kunywa sana maji na kufanya mazoezi, limechukua sura mpya kufuatia daktari mmoja jijini Dar kusema mwongozo huo ni upotoshaji mkubwa, Amani linakupa zaidi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi, daktari wa kituo cha kutoa huduma za afya kilichopo Kimara jijini Dar, Godfrey Chale alisema binadamu kunywa maji kwa wingi, hata kiasi cha pipa kwa siku moja, hakusababishi kuwa mweupe.

“Mtu akinywa maji kwa wingi na kufanya mazoezi anapata faida ya kuifanya ngozi yake kuwa nyororo zaidi. Na wengi wanaofanya hivyo ni wale wanaopoteza hali ya kuzeeka. “Lakini weupe siku zote unatokana na kujichubua. Ila sasa, madhara ya kujichubua ni mengi. Wanaojichubua wanakuwa katika hatari ya kupata magonjwa kama kumi hivi.

“Kwanza wanaweza kupata kansa ya ngozi, chunusi kwa wingi, uvimbe kwenye ngozi, ngozi kuwa nyembamba, kuongezeka kwa hamu ya kula na uzito, kutokwa na mabakamabaka mwilini, kupata pumu na kuzaa watoto wenye kasoro.

“Lakini pia wanaweza kupata magonjwa ya akili, kuharibika kwa maini, kuharibika kwa mishipa ya fahamu na figo kwa sababu ya wingi wa mercury (zebaki) inayokuwa kwenye vipodozi. Pia wanaweza kupata tatizo la kupungua kwa uzito wa mifupa hivyo kuwa katika hatari ya mifupa hiyo kuvunjika. Madhara haya huonekana mara moja lakini pia yanaweza kujitokeza kadiri mtu anavyoendelea kujichubua.

Juzi Amani lilimsaka Ray kwa njia ya simu yake ya kiganjani na kumpa salamu hizo ambapo alisema: “Huyo dokta amesema tu, lakini sidhani kama anafahamu. Mimi weupe wangu unatokana na kunywa maji kwa wingi na mazoezi.

“Halafu pia isitoshe, katika ukoo wetu hakuna mtu mweusi. Kwa hiyo mimi kuwa mweupe ni jambo la lazima,” alisema Ray ambaye mpaka sasa hajawahi kubadili kauli yake ya kunywa maji ndiko kumemfanya awe mweupe sana.

Chanzo: GPL

Zitto Kabwe Afunguka...Ataka Jimbo la Kigoma Ujiji Liwe Mfano wa Kuigwa Tanzania

$
0
0
Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema mafanikio yatakayopatikana katika Halmashauri ya Kigoma Ujiji inayoongozwa na chama hicho, yatawapa picha Watanzania kuwa wanaweza kuongoza nchi.

Akizungumza katika mikutano ya hadhara iliyofanyika Kigoma jana, Zitto alisema wamepanga kufanya makubwa katika halmashauri hiyo.

“Watu wa Kigoma wameonyesha mapenzi makubwa kwetu. Ninawashukuru sana kwa niaba ya chama chetu. Ninyi ndiyo mmetoa mbunge pekee kutoka ACT-Wazalendo na ninyi pia ndiyo mmefanya tuwe chama tawala hapa Kigoma Mjini. Naomba, kwa niaba ya ACT, niahidi kuwa Kigoma itakuwa mfano,” alisema Zitto.

Alisema wanatamani wananchi wa Kigoma Mjini wawe wa kwanza nchini kupata huduma bora za afya bure kupitia mpango maalumu wa Hifadhi ya Jamii utakaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB).

Kupitia mpango huo, takribani wananchi wote 256,000 wa Kigoma Mjini watapata huduma za afya bure kwa kuchangia kiasi kidogo cha fedha.

Kuhusu mradi mkubwa wa ujenzi wa barabara za mawe utakaofadhiliwa na Serikali ya Ubelgiji, alisema una lengo la kushirikisha vijana wa Kigoma.

Zitto ambaye alichaguliwa kuwa mbunge wa Kigoma Mjini Oktoba 25 mwaka jana, yuko katika ziara ya wiki mbili katika kata zote za jimbo hilo kuwashukuru wananchi kwa kuchagua chama hicho.

Katika ziara hiyo, anafuatana na Meya wa Manispaa hiyo, Hussein Juma na madiwani walioshinda katika uchaguzi huo uliovishirikisha vyama vingi vya siasa nchini.    


Necta Yapata Mwarobaini wa Udanganyifu Katika Udahili wa Wanafunzi Kwenye vyuo Ambayo Havijasajiliwa

$
0
0
Udanganyifu katika udahili wa wanafunzi kwenye vyuo ambayo havijasajiliwa kuanza kudhibitiwa, baada ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte) kuzindua mfumo wa udahili wa pamoja (CAS) kwa mwaka wa masomo 2016/17.

Hayo yameelezwa leo na Kaimu Katibu Mtendaji wa Nacte, Dk Adolf Rutayuga na kusema mfumo huo utaanza kutumika kesho saa 6.00 mchana.

Dk Rutayuga amesema mfumo huo utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya astashahada, stashahada na shahada ya kwanza kwa kozi zote zinazotolewa na vyuo vikuu na taasisi zote za elimu nchini, tofauti na ilivyokuwa awali.

Amebainisha kuwa Serikali imeamua maombi yote ya udahili kwa ajili ya mafunzo ya ngazi hizo yafanywe kupitia mfumo huo.

Kaimu Katibu huyo alisema mfumo huo wa i utafanyika kwa utaratibu unaotambulika.

“Mfumo huu utatumika kudhibiti udanganyifu katika udahili na kugundua baadhi ya waombaji wanaotumia vyeti vya bandia,” amesema.

Amesema mfumo huo utaiwezesha Serikali kuwa na takwimu sahihi za waombaji kwa ajili ya kufanikisha mipango ya elimu nchini na waombaji kujiunga na mafunzo kwenye taasisi zinazotambuliwa na Serikali peke yake.

Vilevile, Dk Rutayuga amesema mfumo wa CAS utawapunguzia waombaji gharama za kuomba udahili katika vyuo mbalimbali, kuondoa uwezekano wa mtu mmoja kudahiliwa zaidi ya mara moja, hivyo kuwanyima wenzake nafasi.

Ofisa Mafunzo ya Kompyuta wa Necta, Daud Mabena amesema waombaji wanatakiwa kutembelea tovuti ya baraza ambayo ni www.nacte.go.tz na kufuata maelekezo ya udahili.

Gharama ya kutuma maombi kwa kozi moja ni Sh20,000 na zaidi ya moja Sh30,000.    


Je Unajua Faida za Mmea wa Aloe vera...Soma Hapa Kuzijua na Uanze Leo Kuutumia..

$
0
0
1. Huondoa uvimbe katika jicho
Weka kiasi kidogo cha majimaji ya mu-aloe vera freshi kisha kuamka asubuhi, acha kwa dakika kadhaa kisha jisafishe. Uvimbe lazima ukimbie. Pia unaweza kuloweka pamba katika majimaji ya mualoe vera na kisha jisafishe katika jicho lenye uvimbe.

2. Huzuia na kuondoa michirizi ya tumbo itokanayo na ujauzito
Anza kwa kupakaa majimaji ya mualoevera juu ya tumbo lako na ufanye kama masaji hivi taratibu juu ya tumbo mara 2 kwa siku katika kipindi chote cha ujauzito na baada ya kujifungua kwa miezi michache mpaka michirizi ipotee yote.

3. Hutibu bawasiri
Ile ile sifa moja iliyonayo ya kutibu uvimbe ambayo inaweza pia kutibu malengelenge na uvimbeuchungu kwenye mwako wa mwili, ndiyo hiyo hiyo pia husaidia kutibu au kupunguza maumivu ya bawasiri. Chana tawi la aloe vera freshi na upate jeli yake, kisha pakaa eneo linalosumbuliwa na bawasiri mara mbili mpaka tatu kwa siku kwa wiki kadhaa hasa kama bawasiri imejitokeza sehemu ya nje hadi hapo uvimbe huo utakapopotea.

4. Ni tiba kwa matatizo ya tumbo
Kama utainywa, hutibu vidonda vya tumbo na kiungulia, na kwa ujumla ni kuwa husafisha mfumo wote wa mmeng’enyo wa chakula. Chukua jeli ya aloe vera nusu kikombe (ml 125) changanya na maji ya kawaida nusu kikombe tena kupata ujazo wa  robo lita, changanya vizuri mchanganyiko huu na unywe kutwa mara 2 kwa siku 3 hadi wiki 1 kujitibu matatizo ya tumbo kama kuum, kuondoa sumu, kuunguruma, kuhara na hata kutibu malaria.

Madhara ambayo yameripotiwa kutokana na kunywa aloe vera ikiwa freshi ndani ya tumbo ni pamoja na kuharisha na matatizo kwenye figo.

5. Huziimarisha kucha dhaifu
Kwa taratibu pakaa majimaji ya aloe vera juu ya kucha zako sehemu zote juu na chini kila siku na uzitazame baada ya siku kadhaa uone zitakavyokuwa zimerudisha ule uzuri na ugumu wake wa mwanzo.

6. Huondoa Makeup
Kwa usalama kabisa huondoa makeup kwenye jicho na ni nzuri kwa ngozi laini inayozunguka jicho lako.

7. Husafisha ngozi na kuondoa alama zitokanazo na kuungua na jua
Chunusi, ukurutu na kuungua kwa ngozi kutokana na jua vyote hivi vinatibika kirahisi kwa kutumia aloe-vera. Pakaa mara 2 hadi 3 kwa siku katika ngozi mpaka uone umepona kabisa. Mu-aloe vera pia una sifa ya kupoza kama ilivyo menthol ambayo unaufanya Mu-aloe vera kuwa dawa ya asili nzuri zaidi katika kutibu alama zitokanazo na kuungua na jua.

8. Ni jeli ya asili ya kunyolea na baada ya kunyoa
Aloe Vera ni dawa ya asili katika kutibu michubuko asante kwa vimeng’enya vyake ambavyo huwa na kiasi kingi cha maji ambayo ni mhimu kuzuia kukauka kwa ngozi. Wakati unanyoa ndevu pakaa jeli ya aloe vera na hata baada ya kunyoa pakaa kama after shave jel kuzuia na kuponya michubuko itokanayo na kunyoa.

9. Huondoa makunyanzi na mikunjo ya ngozi
Ngozi hupenda sana Vitamini C na E ambazo zote zinapatikana katika aloe vera na kusaidia kuboresha unene wa ngozi na kuiacha katika hali ya umajimaji. Ikiwa utachanganya jeli ya aloe-vera na mafuta ya asili ya nazi utapata krimu nzuri ya kuongezea viinilishe, mafuta mhimu na unyevunyevu katika ngozi.

Jeli ya Aloe Vera hupenyeza katika ngozi kwa haraka mara nne zaidi ya maji ya kawaida na sifa yake ya kulainisha ngozi husaidia ngozi kubaki na unyevunyevu muda wote.

10. Hutibu homa na mafua
Jeli ya Aloe Vera huongeza kinga ya mwili. Mu-aloe-vera una viinilishe vingi sana mhimu kwa afya ya binadamu. Ina Vitamini A, B, C, na E. Mmea huu una orodha ndefu ya madini mhimu kwa mwili na vimeng’enya vingine mhimu.

11. Vitamini B12 kwa wale wasiotumia nyama (Vegans)
Matumizi makuu ya aloe vera kimatibabu ni kusaidia na kuboresha uundwaji wa bakteria wazuri. Kwa kuongezea aloe vera huwa na jumla ya madini ambayo bakteria huyahitaji katika kutengeneza Vitamini B12.

12. Huongeza nguvu mwilini
Matumizi mengine ya kitabibu ya mmea wa mu aloe vera au mshubiri kwa kiswahili chake hasa, ni kuongeza usawa wa nguvu mwilini. Hii ni kutokana na uwepo wa vitamin b 14 na viinilishe vingine ambavyo husaidia kubadili asilimia kubwa ya chakula katika tumbo lako na kuunda nguvu.

13. Huondoa mba kichwani
Changanya jeli ya asili ya aloe vera na shampoo yako, dakika chache kabla ya kwenda kulala pakaa vizuri mchanganyiko huo kwenye nywele zako na uache zikauke kidogo na usafishe nywele zako asubuhi.

14. Huondoa maumivu wakati wa hedhi
Changanya jeli ya Aloe vera na pilipili manga ya unga kidooogo, meza kijiko cha chakula kimoja mara tatu kwa siku kila siku hadi maumivu yatakapoacha.

15. Hulainisha nywele
Jeli ya Aloe vera ni nzuri katika kutibu tatizo la nywele kujisokota na ni mbadala mzuri kwa bidhaa nyingi za madukani zenye gharama kwa ajili ya nywele.

16. Ni dawa ya asili ya kusafishia mdomo
Changanya jeli ya aloe-vera ml 100, vijiko 3 vya chai vya baking soda, maji ml 100 na kijiko 1 kidogo cha juisi ya limao. Changanya vizuri vyote kwa pamoja na utumie kama dawa yako ya asili ya kusafishia mdomo.

17. Hutibu matatizo katika mmeng’enyo wa chakula
Juisi ya Aloe vera ni nzuri sana katika kurekebisha matatizo katika mmeng’enyo wa chakula, hurekebisha kuvurugika kwa tumbo na kiungulia. Itumie kama ilivyoelezewa kwenye kutibu matatizo ya tumbo hapo juu namba 4.

18. Hushusha lehemu (Cholesterol)
Tafiti zimeonyesha kuwa kunywa juisi ya aloe vera kwa kipindi kirefu kunaweza kushusha kiwango cha lehemu mwilini. Itumie kama ilivyoelezewa kwenye kutibu matatizo ya tumbo hapo juu namba 4.

19. Hutibu chunusi
Aloe Vera huondoa chunusi kwa kuziondoa seli zilizokufa katika ngozi na hivyo kuvifungua vishimo katika ngozi na kuondoa mafuta yaliyoganda katika hivyo vishimo. Pakaa jeli ya aloe vera moja kwa moja katika eneo lililoathirika na chunusi. Pia makovu yaliyoachwa kutokana na chunusi yanaweza kuondolewa kwa kupakaa jeli ya aloe vera pekee.

20. Hutibu ukurutu na upele
Ukurutu ambao ni matokeo ya juu ya tetekuwanga kwa kawaida hutokea kwa watu wazima wenye kinga ya mwili pungufu. Aloe Vera inaweza kutumika kutibu tetekuwanga zinazosababishwa na kirusi aina ya herpes virus. Kwa kupakaa jeli ya aloe vera moja kwa moja kwenye sehemu zilizowazi hutanua mishipa ya damu jambo linalosaidia kutibu vidonda.

21. Huzuia ngozi kuunguzwa na jua (Sunscreen)
Kupakaa jeli ya Aloe Vera katika mwili hulinda ngozi dhidi ya miale yote ya jua kutua moja kwa moja kwenye ngozi na hivyo kukufanya usizeeke mapema, pia ni dawa nzuri kwa ngozi inayofubaa.

22. Hulainisha sehemu kavu za siri
Aloe Vera hufanya kazi kama kilainishi bora kabisa cha asili katika maeneo ya siri kwa jinsia zote mbili na kutoa unyevunyevu wa asili.

23. Hutibu vidonda katika mdomo
Mu Aloe vera unazo vitamini na asidi amino ambazo husaidia kuzitengeneza upya tishu zilizoharibika. Tafiti zimeonyesha kuwa watu wanaosumbuliwa na vidonda mdomoni waliotumia jeli ya aloe vera walifanikiwa kutibu karibu asilimia 50 haraka zaidi kuliko wale ambao hawakutumia jeli ya aloe vera.

24. Hutibu maambukizi katika uke
Unaweza kutibu maambukizi katika uke kwa kupakaa jeli ya aloe vera kwa nje na kwa kuinywa jeli kupata faida yake ya kutibu fangasi. Mililita 120 mpaka 200 za jeli ya aloe vera kila siku zinaweza kusaidia kutibu maambukizi na fangasi katika mwili na ikiwa utaendelea kuinywa kwa muda mrefu kunaweza kuzuia maambukizi zaidi kutokujirudia baadaye.

25. Husaidia wawindaji
Wawindaji wa wanyama katika barani Afrika mara kwa mara hupakaa jeli ya aloe vera katika miili ili kupunguza kutokwa jasho na kuondoa harufu yao ya asili katika mwili isisikike na wanyama.

26. Suluhisho kwa watafuna kucha
Burashi kucha za mtoto anayependa kutafuna kucha na jeli ya aloe vera, ile radha ya uchungu katika aloe vera kutamfanya aache kuzitafuna kucha zake.

27. Hutumika katika kupunguza uzito
Watafiti wameweza kugundua kuwa kunywa juisi ya aloe vera husaidia kupunguza sukari kwenye damu jambo mhimu kwa wale wenye kisukari cha aina ya pili. Wanasayansi wanaamini kuwa kuweka kiwango cha sukari chini hupunguza uzito.

28. Hutibu upungufu wa damu (Anemia)
Kunywa jeli ya aloe vera kunasaidia uzalishaji zaidi wa seli nyekundu za damu katika mwili wako na hivyo kutibu tatizo la kupungua kwa damu.

29. Huondoa maumivu ya mishipa
Kutokana na sifa yake ya kutibu uvimbe, unaweza kutibu uvimbechungu (inflammation) katika maungio yanayopelekea maumivu katika mishipa kwa kupakaa jeli ya aloe vera katika eneo unalosikia maumivu.

30. Hutibu maumivu katika sikio
Matone kadhaa ya aloe vera yakinyunyizwa sikioni yanaweza kuleta nafuu kubwa kama unapatwa na maumivu katika masikio. Hii ni nzuri pia kwa masikio yanayotoa usaha na maumivu mengine katika masikio.

BREAKING: Waziri Jenister Mhagama Kafanya Maamuzi NSSF Usiku Huu...Atengua Uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NSSF

$
0
0
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenister Mhagama ametengua uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dkt. Carina Wangwe uliotangazwa leo Dar es salaam.

Taarifa iliyotolewa usiku huu imeeleza kuwa uteuzi huo umetenguliwa kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya taratibu, uteuzi mpya kwa mujibu wa mamlaka na sheria utakapofanyika taarifa zitatolewa kwa wananchi

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa Ya March 4, Ikiwemo ya Rais Magufuli Kuhujumiwa

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa Ya March 4, Ikiwemo ya Rais Magufuli Kuhujumiwa

Madaktari 2 na Wauguzi 4 Wasimamishwa kazi Jijini Mwanza Kwa Kukataa Kumzalisha Mjamzito Ambaye Alijifungua Mapacha Wawili Chooni Wakafariki

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Baraka Konisaga, amemwamuru Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Adam Mgoyi kuwasimamisha kazi madaktari wawili na wauguzi wanne katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana iliyopo Kata ya Butimba kwa kushindwa kumuhudumia mama mjamzito aliyefikishwa hospitalini hapo na kusababisha kujifungua watoto mapacha na baadaye kufariki.

Hatua hiyo imesababishwa na tukio la mgonjwa Suzana John (27) mkazi wa Kata ya Mkolani kufikishwa na ndugu zake katika Hospitali hiyo, aliyekuwa mjamzito na kupokelewa na Dk Norin Magesa na Muuguzi, Janet Foya waliokuwa zamu ya usiku siku ya Machi Mosi, mwaka huu majira ya saa 4:00 usiku na kushindwa kumuhudumia zaidi ya kutoa lugha isiyoridhisha, pamoja na uzembe.

Akielezea tukio hilo, mwanamke huyo ( Suzan John ) alidai kuwa alianza kusikia uchungu na kuomba msaada kutoka kwa madaktari na wahudumu wa afya waliokuwa hospitalini hapo bila mafanikio.

“Nilifika nikiwa hoi, nikawaambia muda wangu tayari  lakini hawakunisaidia zaidi ya kunitolea maneno machafu.

"Wakati muda ukizidi  kwenda huku nikiwa sipewi huduma yoyote, nilihisi kubanwa haja ndogo hivyo nikaamua kwenda chooni .

Kule chooni mambo yakabadilika ghafla, mtoto wa kwanza akawa keshaanza kutoka.Bahati nzuri mle chooni kulikuwa na beseni

"Nililichukua lile beseni kwa ajili ya kuwaweka watoto huku niwakaita manesi.Manesi hao walikuja wakanichungulia halafu wakarudi. Akaja Nesi mmoja mwanafunzi, akakata kitovu akawaweka kwenye nguo, wakawa wamefariki,” Bi. Suzan alieleza kwa uchungu huku akilia.

Baada  ya mapacha hao kufariki, ndugu wa mwanamke huyo pamoja na wagonjwa wengine walioshuhudia mkasa huo walipandwa na hasira huku wakitaka kuwapiga wauguzi hao.

Taarifa za vurugu hizo zilimfikia DC Konisaga ambaye alifika hospitalini hapo  na kukutana kwa dharula na Mkurugenzi wa Jiji, Adamu Mgoyi, baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Nyamagana, Kaimu Mganga Mkuu Mkoa, Uongozi wa Hospitali na baadhi ya ndugu wa mgonjwa Suzana John aliyejifungua watoto mapach.

Katika kikao hicho cha dharura, walipokea maelezo ya pande mbili, kutoka kwa wauguzi na familia ya mgonjwa Suzana, na kupitia taarifa zilizokuwa zimeandikwa na Madaktari wawili waliomuona mgonjwa huyo, ndipo DC Konisaga akamuagiza Mkurugenzi Mgoyi na Kaimu Mganga Mkuu kuwasimamisha kazi madaktari wawili na wauguzi wanne ili kupisha uchunguzi wa kitaalamu juu ya tukio hilo.

Konisaga aliwataja wanaotakiwa kusimamishwa kazi kuwa ni Dk Magesa na muuguzi Foya waliompokea mgonjwa wakiwa zamu ya usiku wa Machi Mosi, mwaka huu na kushindwa kumpatia huduma zaidi ya kumtolea lugha chafu na uzembe huku wakishindwa kutoa maelezo wakati wa kukabidhi majukumu kwa madaktari na wauguzi walioingia zamu ya asubuhi ya Machi 2, mwaka huu.

DC Konisaga pia alieleza kuwa pamoja na kuingia kwa madaktari na wauguzi wa zamu ya asubuhi ya Machi 2, bado hawakumjali na kumhudumia mgonjwa huyo huku baadhi wakitoa lugha zisizo za faraja kwa ndugu wa mgonjwa.

Hata alipozidiwa na kupewa taarifa na ndugu wa mgonjwa huyo, hawakufika na mara kadhaa walikuwa wakifika na kutoka bila kumudumia pamoja na kumsikiliza akilalamika.

Aliwataja wengine wanaotakiwa kusimamishwa kazi mara moja ni Dk Emiliana Mvungi, wauguzi ni Maria Mkankule, Suzana Sindano na Bibiana Moshi ambao walikuwa zamu na kutomhudumia mgonjwa ambaye alijifungua katika mazingira hatarishi akiwa Hospitalini hapo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo amemwagiza Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk Rweyendela Onesmo ambaye ni Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya Sekou -Toure kupewa maelezo ya kina kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Nangi William na Mganga Mkuu wa Jiji, Dk John Andrew juu ya kushindwa kuchukua hatua pamoja na kupewa taarifa hizo.

Mulongo pia amemuagiza Dk Onesmo kuunda tume ya uchunguzi itakayoshughulikia suala la tukio hilo na kisha kukamilisha kazi hiyo kwa siku moja na kumpatia taarifa ili hatua kali za maadili ya utumishi wa umma zichukue mkondo wake ili pia kuwezesha kusaidia jinsi ya kuboresha utendaji wa kitaalamu na kitabibu katika hospitali hiyo ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kutokuwa na huduma nzuri kwa wagonjwa.

Hivi Ndivyo Alivyopongezwa Mchezaji Mbwana Samatta Baada ya Kuipatia Timu yake Bao la Ushindi.....

$
0
0
WALSH (WA PILI KULIA) AKIWA NA SAMATTA PAMOJA NA WACHEZAJI WENGINE WA GENK WAKISHANGILIA USHINDI WAO DHIDI YA CLUB BRUGGE.

Beki kisiki wa KRC Genk, Sandy Walsh amempongeza Mbwana Samatta kwa bao lake la kwanza akiwa na kikosi hicho.

Walsh ametupia picha wakiwa na wachezaji wengine pamoja na Samatta katika mtandao wa kijamii wa Facebook akimpongeza Samatta baada ya kufunga bao la tatu katika mechi dhidi ya Club Brugge ikiwa ni dakika chache tu baada ya kuingia. Katika mechi hiyo, Genk iliibuka na ushindi wa mabao 3-2.
Mtanzania huyo amejiunga na Genk akitokea mabingwa wa Afrika, TP Mazembe ya DR Congo ambayo kwa kiasi kikubwa aliisaidia kubeba ubingwa huo.

Aliyekuwa Meya wa Ilemela, Henry Matata Afikishwa Mahakamani Kwa Matumizi Mabaya ya Madaraka

$
0
0
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Mwanza, imemfikisha mahakamani aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ilemela, Henry Matata (63) na wenzake wawili wakikabiliwa na mashitaka ya kutumia vibaya madaraka.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo waliofikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Nyamagana ni aliyekuwa Mhandisi wa Manispaa ya Ilemela, Justine Lukaza (42) na mfanyabiashara Hemedi Hamad (54).

Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Mwema Mella, alidai mbele ya hakimu Greyson Sumaye kwamba kati ya Juni mosi na Julai 31, mwaka 2014, washitakiwa hao walitumia vibaya madaraka kwa kutoa zabuni ya kutoza ushuru katika Kituo cha Mabasi cha Buzuruga kinyume cha utaratibu.

Alifafanua kuwa makosa waliofanya ni kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mamba 11/2007 na pia walikiuka sheria ya manunuzi ya umma namba 7/2011

Wakati kesi hiyo inafikishwa mahakamani jana, mshitakiwa Lukaza hakuwepo, hatua iliyomfanya Mwendesha Mashitaka kuomba mahakama hati ya kumkamata.

Hakimu aliridhia ombi hilo na kesi hiyo ilioahirishwa hadi Machi 29 mwaka huu. Washitakiwa wawili waliokuwepo mahakamani walikana mashitaka hayo na wako nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Kigogo wa Chadema Amtosa Lowassa Arejea Cuf Kimya Kimya...Wafurukutwa Wadai ni Mamluki

$
0
0
Kigogo wa Chadema Amtosa Lowassa  Arejea Cuf Kimya Kimya...Wafurukutwa Wadai ni Mamluki

Paul Makonda Amkataa Hakimu Anayesikiliza Kesi ya Kuwakashfu Makada Wenzake wa CCM.....Kubenea Naye Akutwa na Kesi Ya Kujibu Sakala la Kumtusi Makonda

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda jana alitinga mahakamani na kumkataa hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi iliyofunguliwa dhidi yake na makada wawili wa zamani wa CCM wanaodai aliwakashifu.

Kesi dhidi ya Makonda, ambayo awali ilikuwa inasikilizwa na Hakimu Hellen Liwa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilishafikia hatua ya utetezi na Makonda alitakiwa kuanza kujitetea jana, baada ya mahakama hiyo kumuona kuwa ana kesi ya kujibu.

Hata hivyo, jana Makonda ambaye alifika mahakamani kwa mara ya kwanza tangu kesi hiyo ilipofunguliwa, alishikilia msimamo wa kutokuwa na imani na hakimu huyo na hivyo kuomba apangiwe hakimu mwingine.

Makonda alifikia msimamo huo kutokana na maneno aliyoelezwa na wakili wake, ambayo kwa mtazamo yalionyesha kuwa hakimu atakuwa anawapendelea wadai na hivyo asingemtendea haki.

Kutokana na madai ya Makonda, Hakimu Liwa amejitoa kwenye kesi hiyo na amepanga ianze kusikiliza upande wa mashtaka Machi 23.

Kesi dhidi ya Kubenea
Wakati Makonda akimkataa hakimu, mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya Chadema, Saed Kubenea ameonekana ana kesi ya kujibu katika kesi inayomkabili ya tuhuma za kumtukana mkuu huyo wa wilaya.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu anayesikiliza kesi hiyo, ikiwa ni siku chache baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wake.

Akitoa uamuzi huo jana, Hakimu Simba alisema kuwa baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka uliotolewa na mashahidi watatu, aliridhika kuwa mshtakiwa ana kesi ya kujibu.

Baada ya uamuzi huo wakili wa Kubenea, Peter Kibatala aliieleza mahakama kuwa mteja wake atajitetea kwa kiapo na kwamba watakuwa na mashahidi wanne na wanakusudia kuwaita wote mahakamani siku ya kujitetea.

Hakimu Simba alipanga mshtakiwa huyo aanze kujitetea Machi 7, mwaka huu.

Kubenea, ambaye alipandishwa kizimbani, mahakamani hapo Desemba 15, mwaka jana, anadaiwa kumtolea DC huyo lugha ya matusi Desemba 14 mwaka jana wakati wakiwa kiwanda cha Tooku Garments kilichoko Mabibo External, Kinondoni, jambo ambalo lingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Anadaiwa kuwa siku hiyo alimuita Makonda kuwa ni “kibaka, mpumbavu na mjinga” na kwamba cheo chenyewe cha ukuu wa wilaya ni cha kupewa.

Wakati wa ushahidi wake, Makonda aliieleza mahakama kuwa alitumia nafasi yake ya ukuu wa wilaya kwenda kiwandani kwa lengo la kuzungumza na wafanyakazi waliokuwa wamegoma.

Mashahidi wengine wa upande wa mashtaka walikuwa ni maofisa wa polisi waliokuwapo eneo la tukio siku hiyo.

Alisema alipomaliza kuzungumza na wafanyakazi hao na kufunga kikao hicho, wakati anageuka alishangaa kumsikia mshtakiwa akimtukana.

Roma Afungukia Uhusiano Wake na Dada’ke Ali Kiba Baada ya Kukutwa Katika Pozi Tata..

$
0
0
SIKU chache baada ya kuzagaa picha zikimhusisha staa wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ na dada wa staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba, Zabibu Kiba, Roma ameibuka na kutolea ufafanuzi kuwa hawana uhusiano wa kimapenzi kama watu wanavyodhani na kwamba ni mshkaji tu.
Akichonga na Showbiz Xtra, Roma anayebamba na Ngoma ya Mtoto wa Kigogo alisema kuwa picha hizo alipiga kipindi cha nyuma ambapo walikuwa wote studio.
“Sina uhusiano wa kimapenzi naye, Zabibu ni mshkaji wangu tu, siku hiyo alikuja akanikuta niko studio ndiyo nikapiga naye,” alisema Roma anayetarajiwa kufunga ndoa baada ya Pasaka na mpenzi wake wa siku nyingi, Nancy.

Simulizi ya Maisha ya AY: Ataja Sifa za Mwanamke Amtakaye

$
0
0
WIKI iliyopita tuliishia pale nilipoeleza kuwa pamoja na mafanikio niliyonayo ila sijafanikiwa kupata mtoto wala wa kusingiziwa na hii ni kutokana na maamuzi yangu binafsi na kama nikifanikiwa  basi nitahitaji mke wangu anizalie watoto wawili ili niweze kuwapa kile wanachokihitaji na kustahili kupewa na baba au familia bora na pia kutokumchosha mke wangu.
Songa nami…

“Siku zote maisha ni kuchagua na kupanga, kama ikitokea nikahitaji kuongeza watoto zaidi ya wawili basi itakuwa hivyo ila mpango wangu ni wawili tu wananitosha ili mke wangu aendelee kuwa kwenye ubora wake na siyo kumchosha.

“Kwa upande wa mwanamke ninayempenda na kuhitaji awe mke wangu na mama wa watoto wangu ni yule tu mwenye sifa zifuatazo;

Hofu ya Mungu
“Akiwa na hofu ya Mungu, atajiheshimu, atakuwa na upendo, atakuwa na huruma kwangu, watoto na familia nzima kwa ujumla na hii itasaidia kujenga familia iliyo bora mfano wa kuigwa. Pia atajilinda na kujithamini kama mke wa mtu ingawa majaribu anaweza kuyapata kama mwanadamu mwingine ila kwa sababu ya hofu ya Mungu anaweza kuyashinda na kuyaepuka.
Aidha, atakuwa mcha Mungu kwa kwenda kwenye ibada jambo litakaloifanya familia yetu kuishi kwa kufuata taratibu za Mungu.

Mwaminifu
“Hakuna kitu kinachoumiza katika uhusiano wa mapenzi kama uaminifu kwa hiyo sihitaji kuumia, napenda kupata mwanamke ambaye atakuwa ni mwaminifu kwa kila kitu, akiwa mwaminifu ni dhahiri ni mtu ambaye anajitambua.”

‘Smart’ kichwani
“Ukiachana na ishu ya elimu, napenda mwanamke ambaye kichwani mwake ni smart, ambaye tunaweza kukaa na kushauriana na akashauri vitu, mwenye hoja au kama kuna kitu anapinga basi anapinga kwa hoja, hii itasaidia sana katika ushauri wa familia, muziki, biashara na hata maisha yetu kwa ujumla. Namaanisha mtu ambaye tunaweza kukaa na kushauriana kuhusu maendeleo ya familia yetu kwa ujumla ikiwa ni pamoja na wazazi na ndugu zetu.”

Upendo
“Upendo ni kila kitu katika maisha ya mwanadamu, Mungu anatuagiza kuwapenda ndugu, jamaa, marafiki na hata maadui zetu, sihitaji kuwapoteza ndugu, jamaa au mashabiki wangu kwa sababu ya kuwa na mwanamke asiye na upendo. Mtu asipokuwa na upendo atasababisha chuki na mifarakano ndani ya nyumba yetu jambo ambalo sipendi lije kutokea.

“Ukiachana na sifa za mwanamke ninayempenda kwangu kazi ndiyo kila kitu, niliamua kusafiri na kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya remix ya video ya wimbo wangu wa Zigo ambao nimemshirikisha Nasibu Abdul ‘Diamond’  kuna kitu kilinishangaza baada ya Wazungu kuvujisha picha za wimbo huo ambapo sisi tulitaka tufanye kama sapraizi kwa Watanzania.

“Kingine kilichonishtua ni kusikia wimbo wangu wa Zigo remix umekatazwa kuchezwa mchana mpaka usiku ambapo watoto watakuwa wamelala hii ni kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawa-siliano Tanzania, (TCRA), nashangaa kwa sababu ninaona baadhi ya video za wasanii wengine zinaendelea kuchezwa lakini sioni kama kuna hatua yoyote inachukuliwa…

Source:Global Publishers

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Nassor Ahmed Mazrui Ahojiwa na Jeshi la Polisi Zanzibar Na Kuachiwa Kwa Dhamana

$
0
0
Wakati polisi visiwani Zanzibar wakimhoji Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui jana, ulinzi uliimarishwa mjini Unguja huku askari wenye silaha na magari ya deraya wakifanya doria mitaani.

Mazrui, ambaye alifika makao makuu ya jeshi hilo saa 2:00 asubuhi akiambatana na wakili wake, ndiye aliyekuwa mkuu wa timu ya kampeni ya mgombea urais wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, katika uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, ambao chama chake kinaamini kuwa kilishinda.

Barabara zinazoelekea makao makuu ya polisi kutokea Jang’ombe, Kilimani na Bomani zilifungwa huku vikosi vya ulinzi na usalama vikiwa vimetapakaa maeneo hayo na mitaa mbalimbali mjini Unguja.

Wakazi wa Zanzibar wanaojiandaa kwa uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20, kuanzia Jumatano mchana walishuhudia askari wenye sare wakiwa katika magari maalumu ya kijeshi wakirandaranda kwenye barabara za Unguja, hususan mitaa ya Ng’ambo kupitia Mnazi Mmoja, Darajani, Amani, Chumbuni na Mtoni kuelekea Bububu.

Wakati hali ikionekana hivyo mitaani, Mazrui alikuwa ndani ya Ofisi ya Upelelezi ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Ziwani mjini Unguja ambamo alihojiwa kwa saa tatu na nusu.

Alianza kuhojiwa tangu saa 2.00 asubuhi kama alivyotakiwa na jeshi hilo kuripoti kupitia barua ya wito aliyotumiwa hivi karibuni, hadi saa 5.30

Hata baada ya kumaliza kuhojiwa, Mazrui aliyekuwa waziri wa biashara, alilazimika kubaki kituoni hapo akisubiri kukamilika kwa taratibu za dhamana. Aliruhusiwa kuondoka saa 6.40 mchana.

Pamoja na ulinzi kuimarishwa, mamia ya wananchi, hasa wapenzi, wanachama na wafuasi wa CUF, walifika makao makuu ya chama hicho yaliyoko Mtendeni ili kumpokea Mazrui akitokea polisi.

Baada ya kuachiwa kwa dhamana, Mazrui alisema alihojiwa na polisi kuhusu kauli aliyoitoa hivi karibuni alipokuwa Dunga Kiembeni, Wilaya ya Kati mkoani Kusini Unguja kwamba chama chake cha CUF kimechoshwa na vitendo vya hujuma na vya kihuni dhidi ya mali na ofisi zao.

“Naam, nimewaambia kwamba hiyo ni kauli yangu na niliyesema hayo ni mimi kuwa CUF tumechoshwa na uhuni huo,” alisisitiza Mazrui mara baada ya kuachiwa kwa dhamana ya masharti ya kuwa na wadhamini wawili na kila mmoja wao kutakiwa kuweka hapo Sh500,000.

“Wamesema nimetoa kauli za uchochezi hivyo watanishtaki mahakamani na wamenitaka niripoti polisi Jumanne na Alhamisi.” Alisema

Tungeshangilia Filamu za Bongo Kama Tulivyofanya Kwa Ray na Hadithi yake ya Maji na Weupe Wake, Tungekuwa Mbali

$
0
0
Ray alitengeneza headlines sana hivi karibuni kwa kauli yake kuwa weupe wake umetokana na kunywa maji mengi. Story ilikuwa viral na ilisambaa kwenye mitandao yote.

Watu walianza kupost picha wakinywa maji kuutafuta weupe kama wa Ray kama njia ya kumtania kwa kauli yake hiyo. Sikumbuki mara ya mwisho ni lini muigizaji huyu alikuwa gumzo kama hivi. Hadi kuna tetesi kuwa kutokana na kauli yake kusambaa kwa ukubwa usioelezeka, makampuni ya maji yanataka yampe mchongo.

Hatua hiyo ilinifanya nianze kujiuliza maswali mengi. Ni lini Ray amekuwa midomoni kwa watu kwa filamu aliyoifanya? Ni kwasababu Ray ana filamu yake mpya iitwayo Tajiri Mfupi ambayo ajabu haizungumzwi kama inavyozungumzwa kauli yake hiyo ya maji na weupe wake.

Utasema kuwa filamu za Bongo sio nzuri ama hazina viwango kama za nje lakini kumbe tunawafahamu waigizaji hawa na tunawafuatilia. Tunapenda kujua maisha yao lakini hatupendi kuangalia filamu wanazofanya.

Kwahiyo huenda wachawi wa filamu za Tanzania ambazo zinadaiwa kuanza kudoda, ni sisi wenyewe. Tunafawahamu sana wasanii hawa lakini hatutaki kuunga mkono kazi zao.

Pale wanapotoa kauli za kama za weupe kusababishwa na kunywa maji mengi tunapagawa! Vipi kama tungekuwa na mwamko kama huu wa kusambaza filamu wanazotoa akina Ray? Nadhani tungesaidia kuinyanyua tasnia hii inayopumulia mashine.

Beyonce Kavua Pete ya Ndoa Aliyovalishwa na Jay Z...IS IT OVER?

$
0
0
Beyonce na Jay-Z wanazidi kuandamwa na taarifa za kuachana na kupeana talaka. Taaarifa hizi zimepewa nguvu na kitendo cha Beyonce kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya rafiki yake Kelly Rowland aliyefikisha miaka 35.

Mtu aliyekuwepo kwenye pati hio anasema “Beyonce alivua pete yake na kuiweka juu na kusema hii ni mara ya mwisho ataonekana amevaa pete hio,marafiki walibidi wamtulize”

Jay Z ’46’ na Beyonce wamekuwa wakizungukwa na taarifa hizi kwa muda mrefu sasa.

Navy Kenzo Wanaendelea Kutengeneza Mabomu Kwaajili ya Album yao ijayo, Above in A Minute.

$
0
0

Navy Kenzo wanaendelea kutengeneza mabomu kwaajili ya album yao ijayo, Above in A Minute.likiba na Aika kwenye studio za The Industry

Wiki hii Navy Kenzo wameingia kwenye studio za The Industry kutayarisha wimbo mpya wa ushirikiano na Alikiba. Hiyo inakuwa collabo nyingine kubwa baada ya Game waliyomshirikisha Vanessa Mdee.

Katika hatua nyingine, Vanessa amesema album ya Navy Kenzo ni moto wa kuotea mbali.

Kundi hilo linaloundwa na Nahreel na Aika, linatarajia kuichia album hiyo mwaka huu. Kwa sasa linaendelea na ziara yake iliyopewa jina ‘Kamatia Chini Light Up Tour.’

Rais Magufuli Alivyodhaniwa Kabla ya Urais na Alivyo Sasa Baada ya Kupata Urais

$
0
0

Udhaifu wa Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete inaelezwa ilikuwa ni uzito katika kufanya uamuzi. Wengi tulichukia jambo hilo. Sasa tumempata John Magufuli Rais wa uamuzi wa haraka.

Ulinganifu mwingine ni jinsi watu walimvyomjadili Magufuli kabla hajawa rais na baada ya kuwa kushika wadhifa huu.

Kama ilivyo ada, enzi ya mkuu wa nchi inapoelekea ukingoni, watu hujadili wanasiasa wanaoweza kumrithi. Hivyo ndivyo ilivyokuwa wakati kipindi cha Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (1986 – 1995).

Ilikuwa hivyo pia kipindi cha Rais Mkapa (1995 – 2005) na baadaye pia katika kipindi cha Rais wa Awamu ya Nne, Kikwete (2005 – 2015).

Nakumbuka katika miaka mitano ya mwisho ya Kikwete, mijadala ilianza kuibuka katika vijiwe, ofisini na majukwaa mengine mbalimbali juu ya nani angefaa kumrithi.

Rais wetu wa sasa, Magufuli, naye alikuwa miongoni mwa waliojadiliwa, ingawa hakupewa nafasi kubwa na watu wengi.

Wengi waliomjadili Magufuli walimsifu, pia walitaja upungufu waliodhani kuwa wangemfanya asifae kushika wadhifa huo.

Licha ya sifa ya kutoa uamuzi wa haraka niliodokeza awali, sifa nyingine nzuri ambazo Magufuli alitajwa kuwa nazo ni utendaji uliotukuka katika historia ya maisha yake ya kisiasa.

Akiwa Waziri wa Ujenzi na kabla ya hapo Waziri wa Uvuvi, Magufuli alijulikana kama mpambanaji aliyesisitiza katika matokeo. Magufuli hakuvumilia makandarasi wazembe na wanaochelewesha kazi na pia alipambana na uvuvi haramu.

Kabla ya kuwa mgombea, wachambuzi pia walimtaja Magufuli kuwa ni msafi na muadilifu, ikilinganishwa na wengine ndani ya CCM na hakuwa na makundi.

Rais Magufuli amebeba sifa hizo katika utawala wake akionyesha mfano wa uchapakazi na kusimamia uadilifu kuanzia siku ya kwanza ya utawala wake na kuambukiza sifa hizo timu yake ya wasaidizi na sasa tunaona wakihangaika huku na kule kumridhisha bosi wao.

Udhaifu aliotajwa kuwa nao
Mijadala ya mrithi wa Kikwete iliibua pia udhaifu wa Magufuli, huku wengi wakisema hafai kuwa kiongozi mkuu yaani mtu wa mwisho katika kutoa uamuzi.

Waliomtathmini waliona Magufuli ni mtu wa maamuzi ya haraka, mwenye misimamo mkali (au mbishi) na wakati mwingine hutawaliwa na mihemko na kushindwa kufikiria vema kabla ya kutoa kauli.

Wakosoaji walisema akiwa mkuu wa nchi, ipo hatari kuwa angeweza kutoa kauli na maamuzi ya jazba na kuishushia heshima nafasi hiyo. Akiwa mtu wa mwisho, kama akitoa uamuzi usio sahihi, angekosekana mtu wa kuingilia kati na kurekebisha.

Wakosoaji walisema nafasi ya urais inahitaji mtu mwenye uwiano mzuri wa ukali, busara na diplomasia kwani wakati fulani katika nchi zetu sheria peke yake haitoshi kutenda haki.

Waliomtathmini Magufuli kipindi kile walisema angeweza kuwa Waziri Mkuu mzuri, lakini siyo nafasi ya urais kwa sababu kutokana na wajihi wake, alihitaji bosi wa kumdhibiti anapovuka mipaka.

Wakosoaji pia walisema Magufuli ana sifa ya utendaji kuliko uongozi. Walipozungumzia kiongozi walimaanisha mtu mwenye dira ajuaye wapi anataka kuipeleka nchi, mwenye uelewa mpana wa falsafa, itikadi na mwelekeo wa siasa za ulimwengu huu wa leo.

Kutokana na taaluma yake ya sayansi, Magufuli alifahamika kwa ubobezi wake wa vitu vya kiufundi vya Wizara za Ujenzi na kabla ya hapo Wizara ya Mifugo ikiwamo kuhifadhi takwimu mbalimbali.

Mifano iliyotolewa
Akiwa Waziri katika Wizara ya Ujenzi, Rais Magufuli aliagiza Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) kuweka alama ya ‘X’ kwenye nyumba zilizojengwa katika maeneo ya hifadhi ya barabara na kuagiza wahusika wabomoe.

Waathirika walilalamika kwa rais na kudai hawakujua ni eneo la hifadhi ya barabara na kuhoji kwa nini Serikali haikuwazuia wakati huo na kuwaacha wakijenga nyumba na kuishi miaka mingi? Kikwete akaamua kusimamisha zoezi hilo.

Mfano mwingine ni mgomo wa wenye malori ya mizigo ulioanza baada ya Magufuli kuagiza watozwe asilimia tano kwa kila lori litakalozidisha mizigo, kwa mujibu wa sheria. Mgomo huo uliendelea kwa siku kadhaa na kusababisha hasara kubwa kwa pande zote ndipo Waziri Mkuu wa wakati huo, Mizengo Pinda, akaingilia kati na kusitisha tozo hiyo.

Matukio hayo mawili yalionyesha kuwa Magufuli ni mtu wa misimamo na mtendaji anayefuata sheria hadi nukta.

Hata hivyo, wakati fulani busara za kisiasa huhitajika. Angekuwa rais, huenda Magufuli angeng’ang’ania misimamo yake mikali na kuleta zaidi madhara kisiasa na kiuchumi.

Magufuli pia alituhumiwa kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh1 trilioni katika kesi ya meli ya Wachina waliokamatwa mwaka 2009 kwa tuhuma za uvuvi haramu.

Baada ya mchakato mrefu, mahakama iliagiza Serikali kulipa watuhumiwa meli, samaki waliokuwamo na gharama za mawakili.

Meli hiyo ilikamatwa wakati Magufuli akiwa Waziri wa Uvuvi kuanzia 2008 – 2010 kabla kuhamishiwa Wizara ya Ujenzi.

Huu ulitajwa kuwa ni mfano wa maamuzi yaliyokosa umakini kutokana na jazba. Vilevile, wakosoaji wa wakati ule pia walitaja kauli tata na za kuudhi za Magufuli ikiwamo aliyoitoa kwa wakazi wa Kigamboni kuwa wapige mbizi kama hawataki kulipa nauli mpya ya kivuko!

Magufuli baada urais
Je, yale yaliyoonekana kuwa ni udhaifu wa Magufuli yamethibitika baada ya kuingia madarakani? Hili ni swali muhimu ambalo wachambuzi waliojadili siku 100 za Rais Magufuli wangetusaidia kutathmini.

Kwa mtazamo wangu, Magufuli hajabadilika, alivyokuwa ndivyo alivyo. Yaliyodhaniwa kuwa ni upungufu wake, yamethibitika katika kipindi ambacho ameiongoza nchi.

Bomoabomoa iliyositishwa na Rais mstaafu Kikwete, ilianza tena baada ya Magufuli kuingia madarakani. Kujali utu ndiyo sababu iliyomsukuma Kikwete kusimamisha kazi hiyo. Ni jambo zuri kuwa Serikali ya Rais Magufuli iligundua ugumu wa utekelezaji wa zoezi hilo na gharama zake kisiasa na kuamua kulisimamisha kiaina.

Hii inaonyesha inawezekana kupata busara akiwa kazini.
Kwa sasa mambo mengi yanaendelea nchini. ‘Majipu’ yanatumbuliwa. Nyuma ya hadithi za hayo majipu kuna heshima za watu wenye familia zao zimewekwa rehani. Serikali ikikosea kipimo kwa kutumbua uvimbe kwa kudhani ni jipu, hatari yake ni kubwa. Pia, ikitumbua majipu vibaya mgonjwa anaweza kudhurika badala ya kupona.

Hata hivyo, katika siku zijazo yafaa Rais Magufuli awe muangalifu zaidi na kuzingatia kuwa taasisi anayoingoza ni kuu, yenye heshima huku yeye akiwa mtu wa mwisho kwa uamuzi.
Siku aliyotangaza baraza lake la mawaziri, Rais Magufuli alijibu maswali ya waandishi wa habari kwa mkato na kudhihirisha upungufu wa waandishi.

Kadhalika, wakati anaongea katika siku ya kilele cha sheria duniani, Rais Magufuli aliahidi kutoa robo ya fedha ambazo mahakama ingeziokoa kutokana na kesi za waliokwepa kulipa kodi, kesi ambazo Serikali yenyewe ndiyo mdai. Wadaiwa watatendewa haki?

Vilevile, akiongea na wazee wa Dar es Salaam, Magufuli aling’aka kuwa kamwe hataingilia kati mgogoro wa Zanzibar kwa sababu anaheshimu sheria na uhuru wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na kwamba wasioridhika waende mahakamani.

Tulitegemea matamshi haya yangetolewa na Katibu Mkuu wa CCM na Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ, Balozi Seif Idd.

Kauli hii ikiwa imetoka kwa Magufuli, mtu wa mwisho katika uamuzi ya kiserikali. Yako wapi matumaini ya kupatikana suluhu Zanzibar? Ni muhimu kwa Magufuli awe muangalifu na maagizo mbalimbali anayoyatoa kuepuka kukiuka sheria, maadili ya uongozi au kusababisha madhara kutokana na matokeo yasiyotarajiwa.

Hivi karibuni, Magufuli alizuia uagizaji wa sukari ila kwa kibali maalumu, hatua ambayo inatajwa kupandisha bei ya sukari. Katika suala la dira, hivi karibuni, msomi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Profesa Kitila Mkumbo akitathmini siku 100 za Rais Magufuli alimkosoa kwa kusema bado hajaona dira ya kiongozi huyo, akitoa mifano ya sera za kiuchumi. Nakubaliana naye.

Kinachotokea sasa katika utendaji wa Rais Magufuli ni kama mzazi ambaye mwanaye yu mgonjwa anahangaika apone. Dira ya kimalezi ya mtoto huyu imesahauliwa.  

Mganga wa Jadi Akamatwa Akimtoa Mwanafunzi Mimba ya Miezi Saba....

$
0
0

MGANGA wa tiba za asili, Juma Ramadhani pamoja na mwanafunzi wa Chuo cha Utalii Masai, Saumu Mohamed (19) wanashikiliwa na Polisi mkoani Tanga kwa tuhuma za kuharibu mimba ya miezi saba.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Mihayo Msikhela aliwaambia waandishi wa habari jana, watuhumiwa hao ambao ni wakazi wa mtaa wa Sahare, walikamatwa Februari 29 mwaka huu saa 2:00 usiku katika mtaa huo ulio kata ya Mzingani.

Alisema kukamatwa kwao kumekuja baada ya wananchi kuokota maiti ya mtoto mchanga mwenye jinsia ya kike ambaye inadaiwa alikuwa ni mimba ya miezi saba.

“Siku hiyo ya tukio katika maeneo ya Sahare jijini Tanga aliokotwa mtoto wa kike ambaye ni mimba ya miezi saba. Inadaiwa mimba hiyo iliharibiwa na Saumu ambaye in mwanafunzi wa Chuo cha Utalii Masai cha mkoani hapa”.

Alisema na kuongeza: “Binti huyo kulingana na uchunguzi wetu wa awali anadaiwa kunywa dawa ya kutoa mimba kwa kutumia dawa maalumu ambayo alipewa na mganga wa kienyeji aitwaye Juma Ramadhani na ndipo ikaharibu ujauzito huo na kisha Saumu alipofanikiwa kujifungua, akaamua kutupa maiti ya mtoto huyo ambayo baadaye iliokotwa na wananchi.”

Alisema watuhumiwa wote wanashikiliwa na Polisi na watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika

Mgombea wa Urais Marekani Donald Trump Ashutumiwa Kuwa ni Tapeli...Atakiwa Kukatwa

$
0
0

Aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani Mitt Romney amekitaka chama chake kumkataa Donald Trump ,akimtaja mgombea huyo aliye kifua mbele kuwa ”tapeli”.

Bwana Romney amemshtumu Bwana Trump kwa kuwachukulia raia wa Marekani kama wajinga katika hotuba ya siri iliotolewa kwa vyombo vya habari.

Bwana Trump hatahivyo amemkejeli bwana Romney katika mtandao wa tweeter kama mgombea aliyefeli na ambaye hafai kutoa ushari wowote kuhusu uchaguzi.
Viongozi wakuu wa chama cha Reupblican wameshangazwa na vile bwana Trump anavyoelekea kushinda tiketi ya chama cha Republican kwa uchaguzi huo wa mwezi Novemba.

Inadaiwa kuwa wanachama kadhaa wa kamati ya kitaifa kuhsu usalama wa jamii waliandika barua ya wazi wakielezea maono ya bwana Trump kama yasio na msingi wala sera.

Bwana Trump amejiwasilisha kama muunganishi kufuatia ushindi wake katika majimbo saba katika ile ilipotajwa kuwa jumanne maalum na hivyobasi kuimarisha uongozi wake katika chama chake.

Romney ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa Trump anatarajiwa kutoa onyo katika hotuba yake siku ya Alhamisi,kwamba sera za bwana Trump ni tishio kwa chama cha Republican na taifa zaima kwa jumla.

Bwana Romney pia ataonya kuwa uteuzi wa Trump utarahisisha harakati za Bi Hillary Clinton kushinda urais nchini humo.
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images