Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Harmonize: Nilimuuliza Diamond ni Mwanamke Gani Ameachana nae Lakini Anashindwa Kumsahau

0
0

Msanii wa muziki kutoka ‘label’ ya WCB, Harmonize amesema wazo la wimbo wake mpya ‘Bado’ aliyomshirikisha Diamond, lilikuja baada ya kumuuliza Diamond ni mwanamke gani

ambaye ameachana nae lakini bado anashindwa kumsahau.

Akizungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds TV Ijumaa hii, Harmonize amesema baada ya kupata wazo kutoka kwa Diamond ndipo akaanza kuandika wimbo.

“Idea ilikuja kuna siku tulikuwa kwenye gari nikamuuliza (Diamond) kuna mwanamke gari ulimpenda sana hadi leo unashindwa kumsahau, akaniambia hakuna masihara kwenye mahusiano, mimi ndio nikapata idea,” alisema Harmonize.

Aliongeza, “Nikaona kama ni Diamond sio Diamond peke yake ambaye amekutwa na mambo hayo kwenye mahusiano, hata mimi mwenyewe yameshanikuta. Kwa hiyo nikaanza kuandika,

nilivyoandika mistari yangu, nikampa producer akanipa beat nikachagua. Baada ya hapo kwa sababu Diamond alikuwa Nigeria alivyorudi siku nipo nae kwenye gari nikaiplay akaikubali akasema na mimi nitaingiza verse ya pili,”

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Aamuru Kukamatwa Papo hapo Walimu 8 Kwa Kujihusisha na Mapenzi na Wanafunzi

0
0

Walimu wanane wa Shule ya Sekondari Mihama, Kata ya Kitangili, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, wamesimamishwa kazi, watano kati yao wakishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kufanya mapenzi na wanafunzi.


Pia, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo aliyetembelea shule hiyo jana, amevunja bodi ya shule hiyo baada ya kubainika kutofanya kikao hata kimoja tangu ilipoteuliwa Aprili 24, 2013.


Pamoja na Mkuu wa Shule, Joseph Malifedha, walimu wengine waliotiwa mbaroni jana ni Rodrick Uroki, Denis Sanga, Edmund Boaz, Steven Samuel.


Walimu watatu waliokuwa wakifundisha shuleni hapo, lakini wakahamishwa na hivi sasa wanasakwa na polisi kwa tuhuma hizo ni Joseph Lamongi na Joeza Mzava waliohamia Sekondari ya Sangabuye pamoja na Abdallah Mtelwe aliyehamia Tanga.


Malifedha anadaiwa kuwachangisha fedha wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha tatu kwa ajili ya picha za kuweka kwenye vitambulisho (passport size).


Akitangaza uamuzi huo, Mulongo alisema tume maalumu ya uchunguzi iliyoundwa Januari 27, kuchunguza tuhuma dhidi ya walimu hao kujihusisha na mapenzi na wanafunzi imebaini ukweli baada ya kuwahoji wanafunzi kadhaa.


“Ni fedheha na haivumiliki kuona walimu wakifanya mapenzi na wanafunzi wao. OCD wakamate walimu wote na uanze uchunguzi mara moja na kukusanya ushahidi utakaowezesha wahusika kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake,” aliagiza Mulongo.


Amri hiyo ilitekelezwa mara moja kwa walimu hao kuwekwa chini ya ulinzi.


Mulongo pia alimwagiza Katibu wa Idara ya Utumishi wa Walimu Mkoa wa Mwanza, Genzi Sahani kuwaandikia barua za onyo walimu wa kike shuleni hapo kwa kushindwa kulinda na kutetea masilahi ya wanafunzi wa kike waliokuwa wakidhulumiwa kingono na walimu wenzao kiasi cha baadhi yao kuathirika kisaikolojia.


Pia, alimwagiza Ofisa Elimu Mkoa wa Mwanza, Khamisi Maulid kuangalia uwezekano wa kuwahamishia shule nyingine wanafunzi waliodhulumiwa kingono na walimu wao ili kuwaepusha na matatizo ya kisaikolojia.


Maulidi alisema wanafunzi walioathirika zaidi ni wale wa kidato cha nne.


Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mkoa wa Mwanza, Said Mselem alisema kitendo hicho kimeifedhehesha taaluma ya ualimu na kuahidi kuwa ofisi yake itatanua wigo wa uchunguzi hadi kwenye shule nyingine. 

TRA Yamkalia Kooni Anna Tibaijuka..Yamtaka Alipe Sh Mil 500 Kutoka Katika Mgao wa Fedha za Escrow Alizotafuna..

0
0

TRA imemtaka Profesa Tibaijuka kulipa zaidi ya Sh. milioni 500 kutoka katika mgawo wa Sh. 1.62 bilioni zinazohusishwa na fedha zilizochotwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow

Amepinga madai hayo na kukata rufaa kupinga TRA kumtaka alipe kiasi hicho cha kodi, adai hajawahi kupokea fedha hizo kutoka kwa James Rugemalira.

Inadaiwa kuwa Profesa Tibaijuka, ambaye aliondolewa katika wadhifa wake wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutokana na sakata hilo, aliwekewa fedha hizo kwenye akaunti yake na James Rugemalira, Mkurugenzi wa VIP Engineering & Marketing Limited iliyokuwa kati ya wanahisa wa IPTL.

Kutokana na mgawo huo, Desemba 31, 2015, TRA ilimtaka alipe kodi hiyo, baada ya kushindwa kufanya marejesho kutokana na mgawo huo.

Baada ya Ndoa Mke wa Dr Slaa Afunguka....'Haikuwa Rahisi Kufunga Ndoa na Dk Slaa Tumepitia Mengi'

0
0
Baada ya kuenea taarifa za Dk Willibrod Slaa kufunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi, Josephine Mushumbusi, mwanamke huyo ameibuka na kuthibitisha huku akisema haikuwa kazi rahisi kufanikisha jambo hilo.

Dk Slaa na Mushumbusi walifunga pingu za maisha Februari 26 katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Merciful Redeemer, Canada na mwanamke huyo amelieleza gazeti hili kuwa, mchakato wa kufungwa kwa ndoa hiyo uliwachukua muda mrefu na kupitia vikwazo vingi.

Wanandoa hao waliondoka nchini kwenda Marekani Septemba mwaka jana, siku chache baada ya katibu mkuu huyo wa zamani wa Chadema kujiuzulu uongozi na kujivua uanachama wa chama hicho na kuachana na siasa za vyama. Baadaye walihamia Canada wanakoishi hadi sasa.

Akizungumzia ndoa yao, Mushumbusi alisema ilikuwa ngumu kufungwa, lakini walipambana na kutimiza taratibu zote na kuifanikisha.

“Tunampa Mungu sifa na utukufu, haikuwa rahisi. Tumefuata taratibu zote na kufunga ndoa takatifu kanisani kama tulivyotamani,” alisema.

Ndoa hiyo ilifanikiwa baada ya kukwama hapa nchini Julai 21, 2012 kutokana na pingamizi la mke wa zamani wa Dk Slaa, Rose Kamili na mgogoro ulitokana na aliyekuwa mume wa Mushumbuzi, Aminiel Mahimbo.

Mushumbusi alisema iliwachukua muda mrefu kukubaliwa kufunga ndoa kutokana na taratibu za Canada ambazo ziliwataka wapate mafunzo kwanza, wathibitishwe kuwa hawakufunga ndoa kabla na kuwasilisha tangazo maalumu la kustaafu upadri wa Dk Slaa.

Alisema Canada siyo rahisi kufunga ndoa bila kibali cha Serikali na kukipata ni mchakato mrefu.

“Tumevumilia na kukamilisha yote hayo, siyo kama nyumbani ambako ni rahisi kufanyika, watu wanawaza sherehe huko Tanzania lakini huku unaumiza kichwa kupata vibali vya kanisa na Serikali,” alisema.

Ndoa ya Mushumbusi na Dk Slaa ilisimamiwa na wanandoa raia wa Canada aliowataja kwa jina mojamoja la Rosemary na Emmanuel na mashuhuda kadhaa kutoka Tanzania ambao hakutaka kuwataja.

Awali, kulikuwa na taarifa kuwa wawili hao hawakufunga ndoa katika Kanisa Katoliki kutokana na kushindwa kutimiza kanuni na taratibu, lakini Mushumbusi alisema ndoa hiyo imefungwa kanisani na kupata baraka zote. Akizungumzia maisha ya huko Mushumbusi alisema kwa sasa Dk Slaa anasoma na baada ya kumaliza masomo hayo watarejea nyumbani.

Azungumzia uchaguzi

Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana, Mushumbusi alisema alifurahia Rais John Magufuli kushinda kwa kuwa anayajua madhara ya Ukawa kushinda chini ya Edward Lowassa.

“Si unaona Ukawa wanalalamika majipu kutumbuliwa, niliyajua madhara kama hayo ndiyo maana nimeshukuru Magufuli kushinda,” alisema.     

Utumbuaji Majipu:Inashangaza Mpaka Sasa Alietumia Document Fake Kuzuia Uchaguzi wa Meya Dar Hajasimamishwa Kazi

0
0
Inashangaza sana hii serikali ambayo tunaambiwa imedhamiria kurejesha nidhamu ya watumishi wa umma mpaka sasa haijamsimamisha kazi mtumishi alietumia document isiyostahili(fake) ya Mahakama kuzuia uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar-es-salaam ili nae apishe uchunguzi kama wengine.

Wacha tusubiri lakini nimekumbuka msemo wa Kiswahili usemao: "njia ya muongo ni fupi."

Picha: Lulu Michael Ndani ya Nollywood (Nigeria) Tuzo za Africa Viewers Choice Awards

0
0
Muigizaji mwenye mvuto wa aina yake bongo, elizabeth michael , maarufu kama lulu, ametua nchini Nigeria kwenye sherehe za ugawaji tuzo za Africa viewers choice awards(AMVA 2016) zinazofanyika nchini humo march 5(leo), ambapo msanii huyo amebahatika kuwa nominated kwenye tuzo hizo kubwa Africa, ambapo filamu yake ya MAPENZI YA MUNGU imechaguliwa kwenye category ya best film of East Africa.

Ukiachilia mbali lulu, wasanii wengine waliopo kwenye caregory hyo ni msanii mkongwe wa filamu nchini, Richie mtambalike ambapo filamu yake ya KITENDAWILI inashindanishwa na baadhi ya filamu katika kipengele cha filamu bora kutoka afrika mashariki.

Tunawatakia kila la kheri wasanii hao katika mchakato mzima, hili waendelee kutuwakilisha zaidi kimataifa

Mfanyabiashara Arusha Aibuka na Kukana Kuhusika na Ujambazi Uliotokea Mbagala...Adai ni Uzushi Toka Kwa Wabaya Wake

0
0
Mfanyabiashara wa mjini Arusha aliyetangazwa kupitia mitandao ya kijamii akihusishwa na ujambazi uliotokea Mbagala jijini Dar es Salaam, ameibuka na kukana taarifa hizo na kusema zilisambazwa na washindani wake.

Tukio la majambazi kupora na kuua katika benki ya Access tawi la Mbagala lilitokea Februari 26, mwaka huu na watu kadhaa wanaendelea kushikiliwa na polisi.

Mfanyabiashara huyo, Ashaeri Mollel aliliambia gazeti la Nipashe kuwa baada ya tukio hilo, washindani wake ambao hata hivyo hakuwataja, waliisambaza picha yake kwenye mitandao ya kijamii wakimhusisha na tukio hilo, hali iliyomsababishia usumbufu kwa familia na marafiki zake.

“Nimekuwa nikipigiwa simu na watu mbalimbali wakiniulizia imekuwaje nikahusika kwenye tukio hilo, sasa inakuwa usumbufu mkubwa na wapo walioathirika kisaikolojia kutokana na uzushi huo,” alisema.

Hata hivyo, Mollel alisema katika siku za karibuni alitofautiana na mfanyabiashara mwenzake (jina tunalo) wakati wakiuziana gari, hali iliyosababisha polisi kuingilia kati na kuwapeleka kituo cha polisi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mollel, wakiwa kwenye gari la polisi baadhi ya watu waliwapiga picha zilizosambazwa kwenye mitandao hiyo zikiwa na maelezo potofu kuwa alihusika na tukio la uporaji kwenye benki.

“Ukweli ni kwamba baada ya kufikishana polisi, kila mmoja wetu alitoa maelezo na tukaachiwa huru, lakini cha kushangaza wenzangu wakachukua picha zile na kunizushia kwamba nilihusika kwenye ujambazi wa Mbagala, inasikitisha ,” alisema.

Mollel ameshawasilisha malalamiko yake Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na kutakiwa kuwasilisha maelezo ya awali polisi ili hatua zichukuliwe dhidi ya wahusika.

Baada ya uchaguzi wa Meya Dar kuahirishwa Chadema Watoa Tamko Leo...'Hatutasusia Uchaguzi Mpaka Kieleweke'

0
0

Uchaguzi wa Meya Dar es salaam unazidi kuchukua headline kila siku. Ikiwa jana tu Baadhi ya Wabunge na Madiwani wa Ukawa walitinga ofisi ya Halmashauri  ya jiji kutaka kujua tarehe ipi uchaguzi utafanyika lakini hawakupata majibu hayo. Leo March 5 2016Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA‘ Taifa, Freeman Mbowembele ya Waandishi wa habari ameyazungumza haya….

’Hatutaomba tena kumpata Meya wa jiji la Dar es salaam, tutadai kumpata Meya, Serikali wasifikiri watapanga wao tarehe ya kumchagua Meya, wamekuwa na utaratibu wa kutaka tarehe ya kumchagua Meya kwa kutushtukizia masaa 24 kabla, kanuni inadai siku saba, tutataka tarehe ya kuchagua na siku hiyo atachaguliwa Meya asipochaguliwa Meya siku hiyo tusilaumiane’:-Freeman Mbowe

Aidha Mbowe ametoa msimamo wa  chama alipoulizwa kama watasusia uchaguzi, haya ni majibu yake…

’hatuwezi kususia uchaguzi wa Meya kwa sababu ni haki yetu kuongoza jiji kwa sababu ni maamuzi ya wananchi kwa hiyo hatuwezi kususa maamuzi ya wananchi’:-Freeman Mbowe

Ndoa ya Rayuu Chali Baada ya Wiki Moja Tu..Kisa Skendo Chafu za Magazetu

0
0

Baada ya kutamba kuwa tayari amepata mume wa maisha, mambo yameharibika msanii wa filamu Rayuu, kwani sasa hatoki nje wale hapokei simu za shoga zake.

Wiki moja iliyopita msanii huyo aliiteka mitandao ya kijamii hasa instagram, kwa picha zake za harusi huku akiwa na bwana ake ambaye sasa si bwana tena.

Chanzo kikubwa cha kuvunjika kwa ndoa hiyo inadaiwa kuwa mwanaume ambaye alimuoa ni mume wa mtu, ambaye tayari mke wake ana ujauzito wa miezi mitatu, lakini pia inadaiwa kuwa ni kutokana na matukio kadhaa ya msanii huyo.

Rayuu alitafutwa ili kujibu tuhuma za kuachika, alijibu yote ni matokeo na kuachika kwake isiwe sababu ya yeye kusemwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Sina muda wa kuzungumzia mambo hayo kwani nilipofunga ndoa sikusema, sitaki nasema sitaki, maana watu wanaona ni jambo la kuzungumzwa mbona wapo wanaoolewa kifahari na wanaachika,” alisema kwa ukali kisha akakata simu.

Mrembo Tunda Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Tetesi Kuwa Wameachana na Yound D

0
0

Mrembo ambaye amewahi kung’arisha vichupa kadhaa vya mastaa Bongo maarufu kama Tunda amekuwa akitajwa kutoka kimapenzi na rapa kijana maarufu kama Young D au Paka Rapper.

Hivi karibuni kuna uvumi ulizuka kuwa wawili hao wameacha baada ya mrembo huyo kufuta baadhi ya picha alizowahi kupiga na Young Dee huku kati ya zaidi ya picha 480 zilizopo kwenye ukurasa wake wa Instagram amebakiza picha moja tu ya rapa huyo.

Vilevile katika ukurasa wa Young Dee kati ya picha 125 alizowahi kupiga na mrembo huyo wa vichupa ameiacha picha moja tu, jambo ambalo limeibua maswali mengi kwa wapenzi wa burudani wanao wafuatilia mastaa hao.

Kupitia kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio mrembo huyo wa vichupa amefungukia suala hilo na kueleza  kuwa yeye na Young Dee wapo sawa ingawa kuna baadhi ya maneno yake yaliashiria kuwepo jambo analolificha.

Alipoulizwa kama yeye na Young Dee ni wapenzi alijibu.”ndiyo Mimi na Young Dee tulikuwa wapenzi”, huku kitendo hicho cha mastaa hao kufuta picha limekuwa ni jambo ambalo linawatokea mastaa wengi pindi kunapotokea tofauti kati yao.

Full Time ya Azam FC Vs Yanga ipo Hapa, Juma Abdul Afanya Maajabu Ajifunga na Kukomboa Goli....

0
0
Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea leo katika uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, vilabu vya Azam FC na Dar Es Salaam Young Africans, vilishuka dimbani kucheza mchezo wao wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania bara.

Takwimu zinatajwa kuwa Yanga na Azam FC kabla ya mchezo wa leo wamekutana jumla ya michezo 15 kila timu ikiwa imeshinda mara tano na kutoka sare mara tano. Katika mchezo wa leo March 4 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam Yanga na Azam FC zimemaliza mchezo huo kwa sare ya goli 2-2.

Azam FC ndio walikuwa wa kwanza kupata goli la uongozi dakika ya 11, baada ya beki wa Yanga Juma Abdul kujifunga na baadae kusawazisha goli hilo dakika ya 28, Yanga waliongeza kasi baada ya kusawazisha na dakika ya 41 Donald Ngoma akapachika goli la pili.

Kwa upande wa Azam FC wao walisawazisha goli lao dakika ya 70, kupitia kwa nahodha wao John Bocco ambaye ndio mchezaji anayeongoza kwa magoli ya kuifunga Yanga wakutanapo dhidi ya Azam FC, kwani hilo lilikuwa goli la nane kwa Bocco kuifunga Yanga.

Mtanzania Single Mtambalike, Ashinda Tuzo ya Filamu Bora Ya Kiswahili, Afrika!.

0
0
Star wa Bongo Movie wa Kitanzania, Single Mtanzania, Single Mtambalike, "Richie Rich", meshinda tuzo ya filamu bora ya Kiswahili katika tuzo za filamu za Afrika huko Nigeria usiku huu.

Richie ameshinda kupitia filamu yake ya Kitendawili aliyocheza na Mona Lisa na kutengenezwa na kampuni ya Proin, ameshinda katika kipengele cha ‘Best Indigenous Language Movie/TV Series/ Swahili.’

Kwenye tuzo hizo, waigizaji Elizabeth ‘Lulu’ Michael, Single ‘Richie’ Mtambalike na Yvonne ‘Monalisa’ Cherry wanawania Tuzo.

Lulu alitajwa kuwania tuzo hizo kwenye kipengele cha Best Movie – East Africa kupitia filamu yake ya Mapenzi ya Mungu pamoja na Monalisa kupitia Daddy’s Wedding.

JF pia ipo ukumbini hapo ikiwakilishwa na mwana jf Le Mutuz, hope soon ataripoti.

Mwanamuziki wa Tanzania, Ali Kiba atatumbuiza katika tuzo hizo.

Tuzo hizo kubwa za filamu Afrika, zitaoneshwa live kupitia channel ya Africa Magic na Maisha Magic East kwenye DSTV.

My Take.
Sisi wengine huwa hatuangalii bongo movies kwa sababu ya mambo ya hovyo hovyo na ujinga ujinga mwingi, lakini kitendo cha movi za kibongo kuanza kushinda tuzo za kimataifa, labda kutaturudishia attention yetu kurudi kutazama Bongo Movies, tangu alipofariki Kanumba, kwa wengine wetu, alikufa na Bongo Movie, landa sasa Kanumba kapata mrithi, hivyo kupandisha tena chati ya bongo movies!.

Hongera Richie Rich!.

Pasco

Pendeza na Kessy Products..Pata Dawa za Asili Zisizo na Madhara Wala Kemikali Yoyote

0
0

PENDEZA NA KESSY PRODUCT.
PATA DAWA ZA ASILI ZISIZO NA MADHARA WALA KEMIKALI YOYOTE,
NA MATOKEO KUANZIA WEEK (2) ADI (4) NAKUENDELEA

1) KUTOA MVI SUGU 70,000/
2) REFUSHA NYWELE NA KUZUIA KUKATIKA 50,000/
3) TENGENEZA SHEP HIPS NA MAKALIO KWA
@ KUPAKA 50,000/
@ DAW YAMAJI 80,000/
@ VIDONGE 100,000
4) PUNGUZA TUMBO NA NYAMA UZEMBE KWA
@ KUPAKA 55,000/
@ KUNYWAA 80,000/
@ MKANDA WENYE DAW 80,000/
@ BELT 150,000/
5)PUNGUZA MWILI MZIMA PAMOJA NA KILO 80,000/
6) ONGEZA UNENE WA MWILI MZIMA NA HAMU YAKULA 80,000/
7) PUNGUZA MAZIWA NA KUYASIMAMISHA 50,000/
8) ONGEZA MAZIWA SAIZ UNAYOTAKA 50,000/
9) ONGEZA NGUVU ZA KIUME KWA DAW
@ JELI YAKUPA 50,000/
@ VIDONGE 70,000/
10) ONGEZA MAUMBILE YA KIUME KWA
@ JELI YAKUPKA 100,000
@ MASHINE YA HUNDSOME UP 170,000/
11) KUWA MWEUPE MWILI MZIMA NA KUWA SOFTI 70,000/
12) TOA CHUNUS,MADOA,MAKOV 45,000/
13) RUDISHA USICHANA (BIKRA) 60,000/
14) TOA MICHIRIZI (STERCH MARKS) 50,000/
15) ONDOA NGIRI ZAAINA YOYOTE 60,000/
16) TUNDISHA NYWELE ZILIZO ISHA (KIPARA) 150,000/
17) TOA MICHUBUKO KWENYE MAPAJA NA SEHEM ZA SIR 60,000/
18) RUDISHA HAMU LA TENDO NA KUFANYA BILA KUCHOKA 60,000/
19) TOA NDEVU KWA WANAWAKE 80,000/

NA HUDUMA NYINGI USISITE KUSEMA PIGA SIMU,
TUNAPATIKANA DAR,K-KOO,POSTA NA SINZA.
KWAMIKOWANI UDUMA ITAKUFIKA KWANJIA YA MABASI BILA TATIZO.
CHAKUFANYA PG CIM 0719955528 0756259180 0785371237

PIA UTALETEWA POPOTE ULIPO

Lulu Michael Naye Aitoa Kimaso Maso Tanzania....Ashinda Movie Bora Afrika Mashariki...

0
0
Please join me to Salute another Tanzanian hero hapa Lagos Super Star Lulu Michael  kwa kushinda  tuzo ya filamu bora Afrika Mashariki (Best Movie – East Africa) kupitia Mapenzi. Muigizaji huyo alijikuta akilia kwa furaha wakati akishukuru kushinda tuzo hiyo.at 
"2016 AFRICA MAGIC VIEWERS CHOICE AWARDS" ....SALUTE SISTER NA MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

Baba Levo: Wanaosema Shilole Kachuja ni Kina Nani?

0
0
Baba Levo ambaye hivi sasa ni mheshimiwa Diwani Kata ya Mwanga Kigoma kwa tiketi ya ACT Wazalendo amefunguka na kusema kuwa wanaosema Shilole amechuja ni kina nani hao? Baba Levo alijiuliza hilo na kuzua utata kwani baadhi ya watu walianza kuhisi kwamba watu hao ni wapenzi kutokana na ukaribu wao pindi Baba Levo anapokuwa Dar es Salaam.

Kufuatia kuzua utata kipindi cha eNEWS cha EATV kilimtafuta Baba Levo ili kutatua utata juu ya suala hilo na kutaka kufahamu kama kweli Baba Levo anatoka na Shilole, lakini Baba Levo alikana kutoka kimapenzi na Shilole na kudai kwamba Shilole anatakiwa kutoka na wahanagwa wenzake lakini sio yeye, na kudai wao ni marafiki tu wa karibu.

“Shilole hawezi kuwa na mtu kama mimi, unajua mimi ni kiongozi saizi hivyo huyo Shishi anatakiwa kutoka na wahanagwa wenzake sio mimi nikija Dar es Salaam nakaa kwangu, na kuhusu mimi kuchukua gari la Shilole na kuweka bond hizo ni stori tu kwani natambua kuna watu ambao wanataka kunichafua, lakini hawajui mimi ni mchafu kwani nilishachafuliwa sana kwenye siasa lakini wale walionichafua walishindwa wao na mimi nikashinda na kuwa Mh. Diwani.” Alisema Baba Levo


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya March 6, Ikiwemo ya January Mtegoni Kashfa ya Ufisadi

0
0
SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya March 6

Zitto Kabwe Aibuka...Amtaka Rais John Magufuli Kutegua Agizo Hili la Jakaya Kikwete Alilotoa Akiwa Rais

0
0
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe anatafuta nafasi ya kukutana na Rais John Magufuli kumuomba atengue agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuzuia ujenzi wa makazi katika Mlima wa Mlole Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Rais Kikwete alitoa agizo hilo mwaka 2006 kama moja ya hatua za kudhibiti mmomonyoko wa ardhi na kujaa mchanga kwa bandari ya Kigoma.Zitto KabweAkizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Kigoma Cinema mjini Kigoma, Mbunge huyo alisema ameamua kuchukua hatua hiyo kwa kuamini kwamba taarifa alizopewa Rais Kikwete zilizosababisha kutoa agizo hilo hazikuwa sahihi.

Zitto alisema Rais Kikwete alipewa taarifa potofu kwamba mmomonyoko wa udongo kutoka katika eneo hilo ndiyo unaosababisha kujaza mchanga na kupunguza kina katika bandari ya Kigoma.

Mbunge huyo wa Kigoma Mjini alisema kuwa tafiti zilizofanyika na taarifa zilizopo zinaonesha kuwa kupanuliwa kwa Mto Lukuga kunafanya maji kutoka kwa wingi na kuingia bahari ya Atlantiki ndiko kulikochangia kupunguza kina cha maji katika maeneo mbalimbali ya mwambao wa Ziwa Tanganyika.

Kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa mwaka 2008 inaonyesha kuwa kiasi cha Sh bilioni tano kilikuwa kikihitajika kwa ajili ya kuwalipa fidia wakazi hao, fedha ambazo uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji imesema haiwezi kuzilipa hivyo kutaka mamlaka za serikali kuona namna ya kutafuta fedha hizo na kugharamia kuwalipa watu hao.

Wakizungumzia kauli ya Zitto, baadhi ya wakazi wa eneo la Mlole ambao wameathirika kwa kiasi kikubwa na agizo hilo la Rais Kikwete, walisema kuwa wameanza kupata matumaini ya kuona thamani ya nyumba zao kwani tangu kutolewa kwa agizo hilo nyumba zao zimekuwa hazina thamani mahali popote.

Mwamvita Makamba Ajibu Tuhuma za Mange Kimambi Adai January Makamba Hahusiki na Kashfa Zinazosambazwa Mitandaoni..Msikilize Hapa

0
0
January hausiki na kashfa zinazosambazwa mitandaoni.

Hao ni matapeli na wameamua kumtumia tapeli mwenzao huyo anayejiita wa kitaliano.

Mahusiano yangu, masuala yangu binafsi hayapaswi kuhusianishwa na kaka yangu January. Mimi nina maisha yangu na yeye ana maisha yake binafsi, mimi nina kazi zangu na yeye ana kazi zake.

Puuzeni upuuzi huo unaosambazwa kwa sababu ni wa kupika.

Kuniuliza Leading Questions halafu kunirekodi ili unilishe maneno ni upuuzi wa kupuuzwa.

Mwamvita Makamba SIKILIZA HAPA:

Bongo Movie Watisha Nigeria Tasnia ya Filamu.....

0
0
Usiku wa March 5 2016 nyota ya Tanzania iliweza kushine vilivyo kunako tasnia ya uigizaji baada ya waigizaji wa Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Single Mtambalike ‘Rich Richie’ kunyakua Tuzo za (MVCA) zilizofanyika jijini Lagos nchini Nigeria. Tuzo hizo pia ziliweza kuhudhuriwa na mastaa wengi tu wa kibongo.

Usiku wa March 5 2016 nyota ya Tanzania iliweza kushine vilivyo kunako tasnia ya uigizaji baada ya waigizaji wa Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Single Mtambalike ‘Rich Richie’ kunyakua Tuzo za (MVCA) zilizofanyika jijini Lagos nchini Nigeria. Tuzo hizo pia ziliweza kuhudhuriwa na mastaa wengi tu wa kibongo

Waziri January Makamba Ajibu Tuhuma za Ufisadi Dhidi yake Zilizowekwa na Mange Kwenye Mtandao..Msikilize Hapa

0
0
Baada ya Mange Kimambi Kulianzisha Mtandaoni Kuwa January Makamba na Dada yake Wamehusika katika ufisadi na utapeli kwa mtaliano waliomuahidi kumtafutia deal la bandari Bagamayo... Msikilize hapa:
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images