Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live

Waziri wa Ardhi, William Lukuvi Akataa Rushwa ya Bilioni 5

0
0

Waziri wa  Ardhi, William Lukuvi amesema rushwa imekithiri kwenye sekta ya ardhi kiasi kwamba wafanyabiashara wawili walimuahidi rushwa ya Sh5 bilioni afanikishe mpango wao wa kuiuzia Serikali ardhi kwenye eneo linalotakiwa kujengwa mji wa kisasa wa Kigamboni.


Mji huo kabambe wa Kigamboni unajumuisha kata za Kigamboni, Tungi, Vijibweni, Mjimwema, Kibada, Somangila na eneo lote lina ukubwa wa takribani ekari 6,000.


Awali mradi huo ulitarajiwa kugharimu Sh13 trilioni ambazo zingetolewa na Serikali, lakini ikaamua kushirikisha sekta binafsi ili zishiriki kuujenga na Serikali ishughulikie uwezeshaji wa awali.


Lukuvi, ambaye alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu kwa takriban miaka mitano kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Ardhi mapema mwaka jana na kubakizwa wizara hiyo na Rais John Magufuli, alitoa siri hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.


Mbunge huyo wa miaka mingi wa Isimani mkoani Iringa alisema amegundua kuna mtandao mkubwa wa rushwa unaoanzia ngazi ya halmashauri mpaka wizarani ambao unahusisha maofisa wa Serikali na viongozi wa wizara.


Waziri Lukuvi alisema mtandao huo ni hatari na unaweza kusababisha mtu ashindwe kufanya kazi ya wananchi iwapo ataendekeza rushwa.


“Hapa (Wizara ya Ardhi) fedha ipo,”alisema Lukuvi ambaye amekuwa mbunge wa Isimani tangu mwaka 1995.


“Kama ukiwa na tamaa huwezi fanya kazi uliyotumwa. Kuna wakati walikuja wafanyabiashara wawili wakubwa na kutaka wanipe Sh5 bilioni ili nikubali kupitisha mradi wao wa mabilioni ya shilingi na walitangaza kwa marafiki zangu kuwa wangenipa fedha, lakini hapa hawawezi” alisema Lukuvi.


“Wakati naingia tu wizara hii, nilikuta harakati za kukamilisha mradi wa Kigamboni ukiwa katika hatua za mwisho na kila kitu kilikuwa kimekamilika. Lakini nilipopitia vizuri, nilikataa kuwalipa wafanyabiashara hao. Cha ajabu hazikupita siku mbili wafanyabiashara hao walipata taarifa wakaja mbio kutaka kuniona.”


Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, wafanyabiashara hao walitaka walipwe kiasi cha Sh141 milioni kwa kila ekari wakati wao walinunua ardhi kutoka kwa wananchi kwa Sh5 milioni kwa ekari, jambo ambalo alisema lilishapitishwa awali.


“Niligundua pale kuna udanganyifu na wizi mkubwa. Haiwezekani mwekezaji anunue kutoka kwa wananchi ekari moja kwa Sh5 milioni, kisha Serikali tumlipe Sh141 milioni kwa ekari kwa kuvuka pantoni tu. Ni wizi mkubwa. Kama kweli Serikali ina fedha hizo kwa nini tusimlipe mwananchi moja kwa moja?” alihoji.


Waziri Lukuvi alisema endapo njama hizo zingefanikiwa, Serikali ingetumia zaidi ya Sh84 bilioni kuwalipa wawekezaji hao hewa kwa kuwa mmoja anamiliki takribani ekari 200 na mwingine 400.


“Niliwaambia Serikali haiwezi kuwalipa fedha hizo na badala yake waende kuiendeleza ardhi wenyewe kulingana na mradi unavyotaka. Walitaka kutajirika kwa ujanja ujanja,” alisema Lukuvi.


“Eti walidai wamekopa benki kwa ajili ya mradi huo. Haiingii akilini mtu utumie Sh5 milioni, halafu uje uvune mabilioni ya fedha kwa kuvuka pantoni tu.”


Hata hivyo, Lukuvi alikataa kutaja majina ya wafanyabiashara hao.


Akiongea na gazeti moja la kila wiki mwaka 2013, Profesa Anna Tibaijuka, waziri aliyemtangulia Lukuvi kwenye wizara hiyo, alisema tayari kampuni mbili za Miworld kutoka Dubai na China Hope (China) zilishasaini mkataba wa maridhiano na Serikali wa kujenga nyumba takriban 20,900 kwenye eneo hilo.


Miworld ilisaini mkataba wa kujenga nyumba 5,000 wakati China Hope ilitaka kujenga nyumba 15,900 kwenye eneo hilo la mradi wa mji mpya.


Profesa Tibaijuka aliliambia gazeti hilo wakati huo kuwa wananchi wangefidiwa kwa bei za soko kwa mujibu wa sheria, akisema ekari moja ingefidiwa Sh141 milioni kwa ajili ya kumuwezesha kulipia gharama ya nyumba mpya mbadala.


Akizungumzia migogoro ya ardhi, Waziri Lukuvi alisema amegundua mingi inasababishwa na maofisa na viongozi wa wizara hiyo wasio waaminifu, lakini pia wawekezaji wenye tamaa ya kumiliki kiasi kikubwa cha ardhi hata kama hawana shughuli nayo.


“Nimegundua kuna watu hapa wanataka kumiliki ardhi kila sehemu. (Mtu huyo) Atafanya kila njia ashirikiane na watumishi wasio waaminifu ili wampatie eneo hata kama limeshauzwa,” aliongeza.


Lukuvi alisema wengi wao ni wafanyabiashara wenye asili ya Kiarabu na Asia ambao kwa muda aliokaa wizarani hapo amegundua wamehodhi  mashamba katika miradi yote ya viwanja au mashamba iwe ya halmashauri au wizara.


“Wanasiasa na viongozi wa Serikali wanaohodhi maeneo wapo, lakini siyo wengi ukilinganisha na hawa wafanyabiashara wengi wenye tamaa ambao wakishapata ardhi wanatumia kukopa mabilioni ya fedha ndani na nje ya nchi kisha wanawekeza katika miradi yao mingine ikiwamo kujenga majumba katika nchi za Dubai na Ulaya na kuyatelekeza maeneo hayo kuwa mapori hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi wasio na maeneo."


Akizungumzia matarajio yake, Waziri Lukuvi alisema endapo Rais John Magufuli ataendelea kumuweka katika wizara hiyo anatamani amalize migogoro yote baina ya wananchi katika kipindi cha miaka mitano

Chanzo:  Mwananchi

Wafanyakazi 597 wa NIDA wafutwa kazi. Waliofutwa wadai hawakulipwa mshahara kwa miezi 3

0
0

"NIDA chini ya malengo yake ilitarajia kuzalisha vitambulisho 24,000 kwa siku kukiwa na wafanyakazi 802 wenyemkataba wa kudumu na 597 mikataba ya muda,tumekuwa tukizalisha chini ya 10% kwa siku tuko jumla 1399 ukigawanya tu kwa sisi wote ukweli kunawengine wanabaki bila uzalishaji.haiwezeka"Alifafanua Dr.Kipilimba Mkurugezi wa NIDA



Updates:
Vijana waliofutwa kazi NIDA watakutana Victoria jengo la BMTL.

Wanadai kwamba wamefukuzwa kazi kabla ya mikataba yao kuisha na pia hawajalipwa mishahara kwa miezi 3, Watakuwa Makumbusho leo saa nne asubuhi, wanataka kukutana na kuongea na Waandishi wa Habari.

Donald Trump Afananishwa na Madikteta Wakubwa Waliowahi Kutingisha Dunia

0
0

Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto amesema lugha anayotumia mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump ndiyo iliyotumiwa na madikteta Adolf Hitler na Benito Mussolini.

Amesema hayo kwenye mahojiano na gazeti la Excelsior ambayo yamechapishwa kwenye gazeti hilo Jumatatu.

Kiongozi huyo amesema matamshi ya Trump yameathiri uhusiano kati ya Mexico na Marekani, kwa mujibu wa shirika la habari la AP.
Alipoulizwa kuhusu Trump, Pena Nieto alisema mambo ambayo mgombea huyo amekuwa akiyafanya na kuyapendekeza “yamewahi kusababisha maafa makubwa katika historia.”

“Hivyo ndiyo Mussolini alijitokeza na ndivyo Hitler alivyojitokeza,” amesema Pena Nieto.

Bw Pena Nieto alikuwa hajazungumza moja kwa moja kumhusu Bw Trump ambaye ameahidi kujenga ua kati ya Mexico na Marekani ili kuzuia wahamiaji kutoka nchi hiyo wasiingie Marekani.

Bw Trump alisema wahamiaji hao huingiza mihadarati na uhalifu Marekani na kwamba ni “wabakaji”.

Mfanyabiashara huyo kutoka New York amekuwa akiongoza kwenye kura za maoni kati ya wale wanaowania kueperusha bendera ya chama cha Republican kwenye uchaguzi mkuu Novemba na viongozi wa sasa na wa zamani wa Mexico wameanza kueleza wasiwasi wao.

Marais wa zamani Vicente Fox na Felipe Calderon pia wamemtaja Hitler wakimzungumzia Trump.

Bw Pena Nieto amesema kamwe Mexico haitafadhili mpango wa kujenga ukuta mpakani kama alivyopendekeza Bw Trump.

Lakini ameeleza matumaini kwamba wapiga kura watamkataa Bw Trump.

Je Diamond Platnumz Alikutana na Huddah Monroe Alivyokuwa Las Vegas Hivi Karibuni? Picha Yazua Utata

0
0
Nchini Kenya limeibuka swali la je Diamond Platnumz alikutana na Huddah Monroe alivyokuwa Las Vegas hivi karibuni?

Swali hili limeibuka baada ya picha inayoonyesha gari aliyopanga Diamond likiwa kwenye picha aliyopiga Huddah Monroe ambaye alikuwa Sin City kwenye tamasha kubwa huko Las Vegas Hotel & Casino.

Diamond Platnumz na Huddah Monroe walipoz kwenye gari moja ambayo imeonekana kuwa na Rim zilizofanana.

Stephen Wasira Amng’ang’ania Ester Bulaya......Wapiga Kura Wanne Wanaompigania Wawasilisha Upya Ombi la Kukata Rufaa

0
0
Wapigakura wanne wa Jimbo la Bunda Mjini mkoani Mara, wamekamilisha taratibu za kimahakama na kuwasilisha upya maombi ya kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kutokana na maombi yao ya awali kutupiliwa mbali Februari 24, mwaka huu.

Maombi hayo yamewasilishwa na wapigakura Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagila dhidi ya Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya, kuiomba mahakama hiyo kuwapa kibali cha kukata rufaa katika mahakama hiyo.

Wapigakura hao ambao wamekuwa wakimpigania aliyekuwa Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika na mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Bunda Mjini, Stephen Wasira, waliwasilisha maombi ya kufungua shauri katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ili itoe ufafanuzi kuhusu haki ya mpigakura ya kuhoji matokeo pamoja na vigezo vinavyotakiwa ili aweze kuhoji matokeo ya uchaguzi.

Maombi yao ya awali yalitupiliwa mbali na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Sirilius Matupa kutokana na kuwasilishwa sura 141 ya sheria ya rufaa na kueleza kuwa yalikuwa yamewasilishwa chini ya kifungu cha 15 (a) (b) badala ya kifungu 15 (c) ambacho ndiyo sahihi kwa ajili ya maombi hayo na kuwaeleza wanaweza kurekebisha na kuyawasilisha upya.

Januari 25, mwaka huu Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mohamed Gwae, aliitupilia mbali kesi namba moja ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Jimbo la Bunda Mjini iliyofunguliwa na wapigakura hao dhidi ya Bulaya.

Wakati huo huo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Sumbawanga, Kakusulo Sambo anayesikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi Jimbo la Nyamagana, amekutana na mawakili wa pande zote na kuweka mikakati ya namna ya kuiendesha.

Jaji Sambo amekutana jana na mleta maombi (Ezekiel Wenje), mjibu maombi wa kwanza (Stanslaus Mabula) pamoja na mawakili wanaowawakilisha kuweka mikakati ya uendeshwaji wa kesi hiyo ikiwa ni pamoja na kubainisha sehemu zinazobishaniwa.

Akizungumzia hatua hiyo, Wakili Deya Outa anayemwakilisha Wenje, alisema katika kikao hicho wamebainisha sehemu zinazobishaniwa na pande zote katika kesi hiyo pamoja na mashahidi watakaotakiwa kufika mahakamani kutoa ushahidi.

Mwanafunzi wa Kidato cha Pili Ampachika Mwalimu Mimba....

0
0
WAKATI ikiwa imezoeleka kuwa baadhi ya walimu wa kiume huwarubuni wanafunzi wao wa kike na hata kuwaharibia kabisa ndoto zao za kielimu kutokana na kuwapa ujauzito, hali imekuwa tofauti mkoani Rukwa ambako mwanafunzi wa Kidato cha Pili anadaiwa kumzalisha mwalimu wake.

Mwanafunzi huyo aliyemzalisha mwalimu wake ana umri wa miaka 17, wakati mwalimu huyo anayefundisha katika Shule ya Sekondari ya Umma ya Nkasi, iliyopo mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi, Rukwa, ana umri wa miaka 25.

Tukio hilo linalotajwa kuwa la kwanza kutokea wilayani hapa, limekuwa gumzo kubwa kwa wakazi wa Nkasi na wilaya jirani.Hata hivyo, kwa wanafunzi, wamekuwa wakimpongeza mwenzao kwa kujaliwa kupata mtoto katika umri wake huo mdogo, huku mzazi mwenzake akiwa na uhakika wa maisha kutokana na kuwa ni mtumishi serikalini.

Imeelezwa kuwa licha ya tukio hilo, mwalimu huyo aliyezaa na mwanafunzi wake bado anaendelea na masomo shuleni hapo, huku `mzazi’ huyo wa kiume akifundishwa na mzazi mwenzake.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini Namanyere hivi karibuni.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Nkasi mjini Namanyere ambayo ni ya mchanganyiko ya umma, Amiamie Nanga alisema mwalimu huyo alianza kazi shuleni hapo ikiwa ni mara yake ya kwanza kufundisha baada ya kuhitimu mafunzo ya ualimu chuoni.

Picha: Mapokezi ya Lulu Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam (JNIA)

0
0
 Picha za mapokezi za Mshindi wa Tuzo ya AMVCA2016 kipengele cha Movie bora ya Afrika Mashariki elizabeth michael ‘Lulu’ wakati akiwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam (JNIA) akitokea Nigeria.


Mzee Yusufu: Wake Zangu Marufuku Kutumia Instagram

0
0
WAKATI wanawake duniani kote leo wakiadhimisha siku ya wanawake duniani, wake wa mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yusufu, Leila Rashid na Chiku wamekatazwa kutumia tena mtandao wa Instagram.

Wanawake hao wamekatazwa kutumia mtandao huo na endapo watatumia kwa siri mume wao huyo amewaeleza kwamba ndiyo itakuwa talaka yao.

Mzee Yusufu amechukua uamuzi huo baada ya hivi karibuni kuzuka kwa majibizano ya wake zake hao kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Whatsap na Instagram.

Akizungumza kwenye mahojiano na kipindi cha taarabu kinachorushwa na Redio Clouds, Mzee Yusufu, alisema mtandao huo ndio chanzo kikubwa cha kukuza mgogoro huo.

“Nimewatoa wake zangu wote kwenye mtandao huu ambao ndio nimeona umekuza sana mgogoro huu na mimi pia nipo njiani kutoka katika akaunti hiyo ili ibaki kwa ajili ya kazi tu na endapo nitagundua yeyote ana simu ya siri ambayo anaitumia kuingia kwenye mtandao huo ndiyo itakuwa talaka yake.

“Hivi tunavyozungumza wake zangu wote hawana akaunti za Instagram, zinazoendelea kusambaza maneno ni majina feki na ndiyo nimeshaamua hivyo,” alisema.

Mtanzania

Maalim Seif Sharif Hamad azungumzia hali ya afya yake leo

0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya Hindu Mandal Jijini Dar es Salaam kuelezea maendeleo ya afya yake. 

Amesema anaendelea vyema baada ya jana kuugua ghafla na kulazwa katika hospitali hiyo. 

Amewashukuru wananchi ndani na nje ya nchi kwa kuonesha mapenzi na ushirikiano makubwa. 

Anatarajiwa kutoka hospitalini hapo leo jioni

Kuvunjika Ndoa ya Rayuu, Mashehe Waingilia Kati

0
0
Baada ya uvumi kuwa staa wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ ameachika kwenye ndoa yake ambayo imedumu kwa siku nne tu huku chanzo kikiwa ni familia ya mwanaume, hatimaye mashehe wameamua kuingilia kati kuinusuru ndoa hiyo.

Februari 26, mwaka huu, Rayuu alifunga ndoa na mwanaume mwenye asili ya Kiarabu, Ahmedi Said lakini siku ya nne baadaye ulienea ‘ubuyu’ mitandaoni kuwa alitwangwa talaka tatu kwa sababu ya skendo.

Kutokana na sekeseke hilo lililoacha historia ya kipekee, mashehe mbalimbali walidaiwa kuingilia kati na kuilaumu familia ya mwanaume huyo kuwa ilienda kinyume na matakwa ya Kiislam.

Kwa upande wake, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar, Alhad Mussa aliliambia gazeti hili kuwa ni jambo la ajabu kufanywa na Waislam kwani katika dini ya Kiislam, sababu iliyoainishwa kwenye talaka hiyo haina uzito wa kumfanya aachike kwa sababu walipaswa kubaini hayo kabla ya ndoa hivyo kuitaka familia hiyo kuweka mambo sawa haraka.

Rayuu yeye alisema kuwa alisikitishwa na mwanaume huyo ambaye alimwambia kuwa familia ndiyo iliyoamua iwe hivyo.

Chanzo: GPL

Diamond Platnumz Huwa Hali Chakula Anachopika House Girl Wake..Kisa? Harmonize Afunguka Hapa

0
0
Msanii wa bongo Fleva Harmonize amefichua siri kuwa bosi wake msanii Diamond Platnumz huwa anakula chakula ambacho mke wake Zari amepika wakati akiwa nyumbani.

Harmonize amefunguka kuwa shemeji yake,Zari huwa hapendi chakula anachokula Diamond kipikwe na msaidizi wa kazi za ndani,huwa anapika yeye mwenyewe.

“Yani Zari ni shemeji bora kwangu, kwanza chakula cha Diamond hakipikwi na yeyote zaidi yake, so akimuwekea na mimi huwa nakula pia sababu Diamond nae hapendi kula peke yake” alifunguka msanii huyo anayetamba na wimbo wake wa Bado.

SAED Kubenea Amkana Paul Makonda Mahakamani....

0
0
SAED Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo pia Mkurugenzi wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers amekana kumtusi Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, anaandika Faki Sosi.

Kubenea amekana kumtukana Makonda leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Slaam wakati akitoa ushahidi wa kesi inayomkabili kufanya hivyo iliyofunguliwatarehe 15 Desemba mwaka jana.

Kwenye kesi hiyo, Kubenea alifungiliwa madai matatu ambayo ni lugha ya matusi, kumwita Makonda mpumbavu, mjinga pamoja na cheo cha kupewa.

Katika kesi hiyo iliyopo mbele ya Hakimu Thomas Simba ambayo Kubenea alionekana kuwa na kesi ya kujibu, imeanza kusikilizwa leo baada ya mbunge huyo kuanza kutoa ushahidi wake.

Kubenea ndiye shahidi namba moja kwenye kesi hiyo ambapo ameieleza mahakama kwamba, katika vuta nikuvute iliyotokea tarehe 14 Desemba mwaka jana kwenye Kiwanda cha nguo cha TOOKU kilichopo Ubungo, jijini Dar es Salaam hakumtukana Makonda na kwamba, hatua ya kumkatalia kuzungumza na wananchi si kitendo cha kiungwana.
Kesi hiyo inaendelea kusakilizwa.

Viongozi hao wawili Desemba mwaka jana waligombana kwenye kiwanda hicho ambapo Kubenea alikamatwa na polisi kwenye eneo hilo kwa amri Makonda .

Tukio lililohusisha kukamatwa kwa Kubenea lilikuwa ni mgomo wa wafanyakazi zaidi ya 1800 wa kiwanda hicho ambao walimpigia mbunge wao aende kutatua mgogoro huo ambapo Kubenea alifika katika eneo hilo saa 6 mchana na kukutana na wafanyakazi kusikiliza kero zao za muda mrefu.
Kisha aliamua kuondoka na viongozi wa wafanyakazi hao na kufanya kikao na menejimenti ya kiwanda hicho kuanzia saa 7 hadi saa 9.

Ilipofika saa 10:30 Makonda alifika na kupata taarifa kwa muafaka uliofikiwa kati ya Kubenea, menejimenti na viongozi wa wafanyakazi.

Alitoa amri wafanyakazi wakusanyike, akaawaambia kesho atafika huko na Waziri wa Viwanda na Biashara, Waziri wa Kazi na Ajira, na Waziri wa Afya Wanawake, Jinsia na Watoto.
Baada ya kutoa maagizo hayo, Makonda alimzuia Kubenea kuhutubia na kuaga wananchi aliokuwa nao tangu mchana, kutokana na hali hiyo (Kubenea) alisema ni vema aseme neno, ndipo mvutano ulipoanza.

Makonda alimuru mkutano ufungwe lakini wafanyakazi hawakutawanyika eneo hilo, alipoona hivyo aliamrisha Polisi wamkamate Kubenea ambapo sintofahamu iliongezeka.

Ajali Mbaya Yatokea Asubuhi ya leo..Daladala Lagongana na Lori la Kubebea Ng'ombe Eneo la Tabata Matumbi

0
0
AJALI DAR: Daladala (DCM) lagongana na Lori la kubebea Ng'ombe eneo la Tabata Matumbi na kusababisha vifo na majeruhi (idadi bado). Barabara za kutoka na kwenda Buguruni zimefungwa

Nisha Afunguka Asema Hajawahi Kuwa Mpenzi wa Baraka da Prince Wala Rafiki.

0
0
Msanii wa bongo movie,Nisha amefunguka na kusema kuwa hajawahi kuwa kwenye mahusiano yoyote na msanii wa bongo fleva Baraka da Prince kama ambavyo imewahi kuvumishwa.

Nisha amesema hajawahi kuwa hata na urafiki na msanii huyo,huwa anamfahamu kama msanii tu.

“kwanza hatuna mahusiano yoyote yawe ya kimapenzi au kirafiki,namfahamu kama msanii tu ambaye namfahamu tu” alifunguka mwigizaji huyo.

Peter wa P Square Atoa Wimbo Wake Kama Solo Artist ‘Look Into My Eyes’ iko Hapa

0
0
Member wa kundi la P-Square, Peter Okoye ameanza kufanya kazi kama solo artist na ametoa wimbo wake wa kwanza Look Into My Eyes.

Wimbo umetoka chini ya jina la Peter Okoye, na ni wimbo wa R&B na taarifa zinazidi kusamba kuhusu kutoelewana kwa wasanii hawa wawili Peter na Paul wa P Square.

Isikilize hapa chini Peter Okoye (P-Square) – Look Into My Eyes

Harmonize Asema Haya Kuhusiana Beef ya Diamond na Ali Kiba....Amesemaje?

0
0
Msanii wa bongo fleva,Harmonize ambaye yuko chini ya lebel ya wasafi inayomilikiwa na Diamond amefunguka na kusema yeye hajui kama kuna ugomvi wowote kati ya bosi wake na Ali Kiba kwani hajawai kusikia akimzungumzia vibaya msanii huyo.

Harmonize pia ameenda mbali na kusema kuwa yuko tayari kufanya kazi na Ali Kiba kama itatokea kwani ni moja kati ya msanii mkali.

“Mimi sijui kama kuna beef,sijawahi kumsikia Diamond akimwongelea msanii yeyote tofauti..Diamond ni kati ya watu wanao support muziki wa Tanzania,ukiona kolabo nyingi za wasanii wa Tanzania na nje Diamond ana Mchango wake” na kuendele kusema kuwa yuko tayari kufanya kazi na Kiba “Ali Kiba ni msanii mzuri,kwa hiyo kolabo ikiwa na tija nitafanya naye“.

Rihama Ally na Flora Mvungi Wasikitishwa na Kitendo cha Baadhi ya Wana Bongo Movies Kukataa Kwenda Kumpokea na Kumpongeza Lulu Michael

0
0
Flora Mvungi Jana Amewashukia Baadhi ya Bongo Movies wenzake kwa kuendesha kampeni ya chini chini wasiende kumpokea lulu Michael na Kumpongeza Airport Mara baada ya Kurudi na Tuzo toka Nigeria.....

From @florahmvungi - IMENIUMA KUKOSA KUKUPOKEA MANA SIKO DAR ,,KWANZA HONGERA SANA SANA..@elizabethmichaelofficial SANA..HII TUZO C YAKO PEKE YAKO NI YA TANZANIA UMETUWAKILISHA VYEMA KABISA NA UMEFUNGUA NJIA KIUKWELI ASIYEKUBALI ATAKUWA NA TATIZO ILA KUNA KITU KIMETUUMA SANA NAJUA WAPO WANAONA NA WATAJIFUNZA KITU KWA MTAZAMO WETU HATA KAMA HAUKO KWENYE CHAMA FULANI HAIKUPASWA KUWA HIVI,,SHERIA ZINAVUNJWA NGAZI ZA JUU ITAKUWA KWENYE VYAMA VYA SANAA..ETI WANADIRIKI KUSEMA HATUWEZIKWENDA KWAKUWA C MWANACHAMA WETU JAMANI HEBU TUWE NA FIKRA PANA BASI HATA KAMA ILA ALICHOKIFANYA LULU HESHIMA ALIYOTULETEA TANZANIA HATA WEWE INAKUHUSU KWAKUWA LEO HII HATA WEWE ITAKUWA RAHISI KUFIKA HATUA NYINGINE KUPITIAHUYO UNAYEMUITA SIO MWANACHAMA WAKO..SIJAPENDA NA MY DADA @riyamaally AMELIA KWA UCHUNGU NDO KABISA HADI TUMELEFT GROUP LAO..IT'S NOT FAIR..NIMEGUNDUA KWELI HATUPENDANI HALAFU WAZIWAZI DAH ILA WENYE ROHO MBAYA HAWAFANIKIWAGI ASILANI..@elizabethmichaelofficial keep up your good work darling haya mengine ni changamoto tu za maisha...@elizabethmichaelofficial
UJUMBE UTAKAA NUSU SAA HAPA BASII

UPDATES:Ajali Mbaya Iliyohusisha Daladala na Malori Mawili Yaua Watu 4 na Kujeruhi 25 Jijini Dar es Salaam

0
0
Ajali Mbaya imetokea leo asubuhi eneo la Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam ikihusisha malori mawili  na daladala iliyo kuwa ikitokea Gongo la Mboto kuelekea Ubungo 

Kwa mujibu wa mganga mkuu Hospitali  ya  Amana, Dr Stanley Binagi, watu wanne wamefariki dunia huku 25  wakijeruhiwa.

Inaelezwa kuwa, Chanzo cha ajali hiyo, ni Lori lililobeba Mchanga ambalo liliikuwa kwenye mwendo kasi, kwenda kuligonga Daladala hilo kwa nyuma, hali iliyopelekea Daladala hilo kukosa mwelekeo na kwenda kugongana na Lori lingine lililokuwa limepakia Ng'ombe waliokuwa wakipelekwa Pugu Mnadani.



==

Mawaziri Watano Kikaangoni...Siku 87 Tangu Rais John Magufuli Awaapishe

0
0
Siku 87 tangu Rais John Magufuli awaapishe, mawaziri watano  wa Baraza la Mawaziri la Serikali ya Awamu ya Tano wako kwenye msukosuko kutokana na kutajwa, kuhusishwa ama kufanya uamuzi wenye dalili za majipu.

Mawaziri hao, George Simbachawene, Profesa Sospeter Muhongo, Jenister Mhagama, Harison Mwakyembe na January Makamba wamekuwa wakihusishwa na kufanya uamuzi bila ya kufuata kanuni, kufanya mipango ya kuwezesha mgeni kupata zabuni za ujenzi, kufanya uteuzi kinyume na taratibu na kustua watendaji wajiandae kukabiliana na ziara za kustukiza za viongozi wakuu wa Serikali.

Rais John Magufuli, ambaye amekuwa akiwawajibisha watendaji wa umma tangu aapishwe Novemba 5, 2015, alishasema kuwa hataonea aibu yeyote atakayeonekana kutokwenda na kasi yake, msimamo unaowaweka mawaziri hao kwenye hali ngumu wakati huu ambao tuhuma dhidi yao zinashamiri.

Hadi sasa, Serikali haijatoa tamko kuhusu tuhuma zilizoibuliwa dhidi yao, wakati Rais amekuwa hatabiriki katika uamuzi wake na hali hiyo aliizidisha Jumapili alipomuondoa Ombeni Sefue siku 67 baada ya kumteua tena kuendelea na nafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi.

 Simbachawene, ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) amekuwa akitajwa kwenye sakata la ununuzi wa mafuta ya mwezi Septemba, Oktoba na Novemba mwaka 2015 bila ya kushindanisha zabuni na hivyo kusababisha aliyepewa kazi hiyo kupandisha bei kwa Sh40 bilioni.

Mbunge huyo wa Mpwapwa, ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati huo, alijitetea kuwa alichukua uamuzi huo kutokana na wasiwasi wa usalama baada ya Uchaguzi Mkuu na sheria inamruhusu kufanya hivyo.

Hata hivyo, Ewura ilisema wakati Waziri Simbachawene anafikia uamuzi huo tayari kulikuwa na zabuni mezani na walitoa ushauri wao.

Ewura ilisema ununuzi huo umesababisha bei ya mafuta kutoshuka kwa kadiri inavyotakiwa na hivyo kuwafanya Watanzania wasinufaike na kuporomoka kwa bei ya nishati hiyo duniani.

Profesa Muhongo anatajwa kuhusika katika sakata la uwashwaji wa mita ya kupimia mafuta kwenye Bandari ya Dar es Salaam siku moja kabla Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutembelea eneo hilo.

Mita hizo zilikuwa zimezimwa kwa takriban miaka mitano kwa madai kuwa ilikuwa ikipunja wafanyabiashara, lakini iliwashwa kabla ya ziara hiyo baada ya Profesa Muhongo kudaiwa kumtaka bosi wa Wakala wa Vipimo, Magdalena Chuwa kuziwasha siku moja kabla ya ziara ya Majaliwa.

“Mita imeanza kufanya kazi jana kutokana na maagizo yaliyotolewa ngazi za juu, nilitumiwa meseji (ujumbe mfupi) kutoka kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo.Aliagiza ianze kazi ndani ya saa 24,” alisema Chuwa alipoulizwa na Majaliwa kuhusu kuwaka kwa mita hizo.

Kwa nyakati tofauti, Profesa Muhongo amelitolea ufafanuzi suala hilo akisema kuwa mita hizo zinamilikiwa na wakala wa vipimo ambao uko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.

Waziri mwingine, Mhagama ambaye anaongoza Wizara ya Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, alifanya uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk Carina Wangwe, lakini saa tano baadaye alilazimika kutengua “kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya taratibu”.

Nafasi ya bosi huyo NSSF imezingirwa na mbigiri na hadi sasa haijapata mrithi wala kaimu wake. Dk Wangwe, ambaye ni Mkurugenzi wa Tehama wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Hifadhi ya Jamii (SSRA), aliteuliwa kushika nafasi hiyo Machi 3 saa 11:15 jioni na kutenguliwa siku hiyo hiyo saa 4:15 usiku.

Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alitolea ufafanuzi suala hilo kwamba uteuzi huo ulikosewa na Dk Wangwe aliteuliwa kuwa mwangalizi tu, siyo kaimu mkurugenzi mkuu.

“Kiswahili cha neno caretaker (mwangalizi) kilikosewa na kuandikwa kaimu mkurugenzi mkuu na hiyo imetokea wakati ambao taratibu za kupata kaimu hazijakamilika.Kutokana na mkanganyiko huo, waziri aliamua kutengua tu,” alisema Balozi Sefue.

Sakata jingine linamuhusisha January, ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais.

Waziri huyo kijana anatajwa kwenye tuhuma zinazomuhusisha dada yake, Mwamvita za mipango ya kumtafutia zabuni raia wa Italia, Vincenzo Cozzolino kwa kutumia nafasi za kisiasa. Zabuni niyo ni ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, ambao umesimamishwa kwa muda kutafuta fedha.

Tuhuma hizo zimetanda kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya jamii, ingawa wawili hao wamekanusha kuhusika lakini wanakiri kuwapo kwa uhusiano baina ya Mwamvita na Cozzolino uliohusisha kupeana fedha.

January alisema kuwa raia huyo wa Italia alikuwa na urafiki na dada yake, lakini anashangazwa na kitendo cha kutajwa jina lake katika suala hilo.

Cozzolino amenukuliwa katika vyombo vya habari akikanusha January kuhusika katika suala hilo, huku katika mitandao ya kijamii kukiwa na taarifa zinazoonyesha mawasiliano kati ya Mwamvita na raia huyo wa Italia.

Chanzo cha taarifa hizo ni sauti za mazungumzo baina ya Cozzolino na Mwamvita zilizorekodiwa kupitia akaunti ya Instagram ya mmoja wa watu wanaomfahamu Mwamvita, kisha kusambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

January pia yumo kwenye sakata la mawaziri watano walioshindwa kujaza fomu za mali wanazomiliki lililobainika Februari 25, mwaka huu.

Kwa upande wake  Dr Mwakyembe,anatuhumiwa akiwa Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, wizara yake iliingiza mabehewa feki 25  na kuisababishia serikali hasara ya mamilioni ya pesa. Sakata hilo la mabehewa  limewafikisha baadhi ya watumishi mahakamani

Mzee Yusuf, Watulize Wake zako! Wanachofanya Mitandaoni ni Aibu Kwako

0
0
KWAKO Big Boss wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf, habari za siku? Uko poa? Pole na majukumu ya kila siku.

Wajionaje na hali? Familia yako kwa ujumla haijambo? Ukitaka kujua afya yangu, mimi ni mzima wa afya. Namshukuru Mungu. Napata haki yangu kupitia taaluma yangu na maisha yanazidi kuyoyoma.

Madhumuni ya kukuandikia barua hii ni kutaka kukueleza kwamba sikufurahishwa sana na mgogoro ulioendeshwa na wake zako ambao kimsingi niliamini ulikuwa unaweza kuepukika kabla ya kuwafaidisha watu.

Wiki iliyopita haikuwa nzuri sana kwako. Kwa kuwa Watanzania wanakuheshimu, wanakuamini naamini hawakufurahishwa na malumbano yaliyoibuliwa na wake zako. Naamini hata wewe hayakukufurahisha. Ndoa yako imejadiliwa sana mitandaoni.

Mmewapa sana nafasi watu kuzungumza vitu ambavyo havikuwa na sababu ya kuzungumzwa.
Kutukanana, kushutumiana mambo mazitomazito halikuwa jambo jema. Ilileta picha mbaya kwa mashabiki wako na wale wa Jahazi. Kama baba, ulipaswa kulidhibiti kabla halijatoka nje.
Nasema hivyo kwa sababu vitu ambavyo walianza kuvizungumza vilikuwa ni vya kujidhalilisha wao wenyewe na wewe pia.

Kwa kuwa wote ni wake zako, ulikuwa na nafasi ya kuwakanya wasitoe siri za ndani. Kuwaambia wote wasizungumze na vyombo vya habari maana kufanya hivyo kulilifanya sakata hilo kuzidi kuwa kubwa.

Badala yake ugomvi ulikuwa mkubwa. Watangazaji nao wakadandia sakata hilo. Kila mmoja akawa na upande wake, mwisho wa siku ilikuwa ni fedheha kwa familia yako.
Sakata hilo limewafanya hata ambao hawakuwa na wazo la kujadili maisha yenu binafsi, kuanza kufanya hivyo. Nakushauri kama bado hujaamua, amua sasa. Kaa nao chini na kubaini kiini cha ugomvi. Kujua nani alianza na nini ufanye ili uweze kumaliza tofauti.
Wanawake ni mama zetu, lakini tunafahamu mara nyingi huwa ni rahisi kukuza ugomvi mdogo na kuufanya uwe mkubwa. Pengine chanzo kilikuwa ni kidogo, waeleze ukweli kwamba hawapaswi kuyatoa nje mambo yao.

Waeleze kwamba madhara ya hivyo ni kujidhalilisha na kuwafanya waonekane hawajafundishwa na wazazi wao. Waeleze kwamba wewe ni nani, una heshima gani katika jamii, hivyo waishi kulingana na heshima yako. Waache mambo yale ya ‘kiswahili’.

Ikiwa unaona unazungumza kama mume na bado mmoja wao au wote wanakuwa hawakuelewi, ni vyema kuchukua hatua kali zaidi. Heshima yako umeijenga kwa muda mrefu, ni vyema kushirikisha hata wazazi kusaidia kutatua mgogoro huo.

Simama kama mwanaume. Kuwa mkali pale inapobidi kufanya hivyo maana wakati mwingine wapo baadhi ya wanawake wanaojaribu kutikisa kiberiti ili waone ndani kina nini. Ukiwa mkali, utamuona amenywea.

Nakuamini maana ni muda mrefu uliweza kudhibiti mikwaruzano ya kifamilia kutoka nje. Naamini katika hili imepenya bahati mbaya. Unajua wapi imepenyea, basi jitahidi kudhibiti isitokee tena siku za usoni.

Ni matumaini yangu utasimama kama mwanaume na mgogoro huo utaisha na hata siku nyingine hatutasikia mambo binafsi yanatoka katika vyombo vya habari.
Mimi nduguyo;
Erick Evarist
Global Publishers
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live




Latest Images