Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Tuzo Ya Lulu Michael Yamliza Mama Kanumba

$
0
0
Tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Filamu Afrika Mashariki, iliyotwaliwa na Mbongo,
chozi mama wa aliyekuwa nyota wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa, tambaa na Risasi Mchanganyiko liujaze moyo wako.

Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na mama Kanumba, muda mchache baada ya Lulu kutangazwa na waandaaji wa tuzo ambao ni African Magic Viewers Choice ‘AVCA’ kwamba yeye ni mshindi, aliwasiliana na mama yake mzazi, Lucresia Karugila, ambaye naye alimtwangia simu mama Kanumba ili kumfahamisha ushindi huo ambapo mama huyo alitoa chozi.

WEWE SIKIA HII
“Sasa sijajua, yule mama alilia kwa sababu ya furaha au vipi! Maana si unajua siku za karibuni hawakuwa vizuri? Lakini inawezekana akalia kwa chuki kweli?,” kilihoji chanzo hicho.

NJIA PANDA
Pamoja na maneno yote, bado chanzo hicho kilishindwa kuweka wazi kilio cha mama Kanumba kilitokana na nini lakini kilisema kuwa, mwanamke huyo, baada ya kupokea salamu hizo, alionekana kuwaza mbali sana huku akitanabaisha kuwa, amemkumbuka mwanaye Kanumba ambapo alimtaja kama mara tatu hivi lakini pia alikumbuka ukaribu wake na Lulu.

WAMEPATANA SASA?
Chanzo kikazidi kuanika kwamba, mbali na kumjulisha mama Kanumba kuhusu ushindi wa tuzo kwa binti yake, pia aliitumia simu hiyo kumtaka mama Kanumba washirikiane kuandaa sherehe ya kumpongeza Lulu, inadaiwa mama Kanumba alikubali kwa herufi kubwa hali inayoonesha kumalizika kwa bifu.

RISASI LAWASAKA WOTE
Baada ya ubuyu huo, gazeti hili lilichacharika kuwatafuta wawili hao ili kujua nini kilijiri juu ya taarifa hiyo ya Lulu kutwaa tuzo ambayo huenda itamfunulia ukurasa mpya katika tasnia hiyo, aliyoianza kuitumia akiwa bado mdogo kiumri.
mama_kanumbaMama Kanumba, Flora Mtegoa.

MAMA LULU HUYU HAPA
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko juzi, mama Lulu alisema alipopata taarifa za ushindi wa mtoto wake kupitia Filamu ya Mapenzi ya Mungu ‘alichizika’ kwa furaha kutokana na binti huyo kuanza kazi hiyo ya kuigiza kwa muda mrefu lakini kipindi hiki Mungu amemuona na kumshika mkono.
“Yaani nilipopata taarifa za ushindi wa mtoto wangu nilichizika kabisa kwa furaha, maana mwanangu kasota sana jamani! Mungu amemuona na mimi nazidi kumwombea, ” alisema mama Lulu.

KUHUSU KUMPIGIA SIMU MAMA KANUMBA
Kuhusu madai kwamba alimwendea hewani mama Kanumba kumhabarisha, mama Lulu alisema:
“Huwezi amini, sijazungumza na mama Kanumba kwa kipindi kirefu sana kutokana na matatizo ya hapa na pale kama binadamu, lakini niliweka bifu pembeni na kumpigia simu kumuuliza kuhusu kumpongeza mtoto wetu kwa sababu filamu hiyo aliyoshinda, naye (mama Kanumba) alishiriki kucheza, tena vizuri.”

MAMA KANUMBA SASA
Baada ya kumwacha kando mama Lulu, Risasi Mchanganyiko likamvutia ‘waya’ mama Kanumba ambapo alikiri kupigiwa simu na mwanamke mwenzake huyo japokuwa hakuwa ameelewa vizuri kuhusu tuzo hiyo. Hata hivyo, alisema anamshukuru Mungu kwa Lulu kunyakua tuzo hiyo.
“Mimi sijaelewa vizuri kuhusu tuzo yenyewe, lakini mama Lulu aliponipigia na kunipa taarifa nimefurahi na nimemshukuru Mungu kwa hilo kwa sababu ushindi huo ni wetu sote Watanzania,”alisema mama Kanumba.

KUHUSU KUTOA CHOZI
Risasi Mchanganyiko lilipoanza kumuuliza kuhusu kutoa chozi kwa taarifa hiyo, mama Kanumba aliashiria kuitoa simu yake kwenye sikio hivyo kutosikia tena na alipopigiwa tena, hakuwa akipokea.

MAWAKILI WASHINDANA SAFARI YA LULU NIGERIA
Wakati huohuo kumekuwa na mzozo wa kisheria kati ya wanasheria wawili nchini, Ado Novemba na wakili wa Lulu ambaye aliomba jina lake kupigwa ‘tintedi’, ishu ikiwa ni ile kesi inayomkabili Lulu ya kudaiwa kumuua Kanumba bila kukusudia.
Ado amesema kuwa, Lulu ana zuio la kutosafiri nje ya Dar es Salaam kutoka Makahama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambako kesi itasikilizwa. Akahoji amewezaje kufika Nigeria mbali kote huko.

KAMA NI RUHUSA
Ado aliendelea kusema kuwa, mtu mwenye kesi kama ya Lulu akipewa zuio, anaweza kusafiri kwa kibali cha mahakama kama itajiridhisha.
“Lakini ili mahakama ijiridhishe inatakiwa sababu za msingi sana kama kwenda kutibiwa nje ya nchi. Kinyume cha hapo hakuna kibali,” alisema Ado.

WAKILI WA LULU
Naye wakili huyo wa Lulu alisema: “Hawezi kusafiri bila kuomba ruhusa kutoka mahakamani. Halafu mtu anaposema mpaka mahakama ijiridhishe hilo ni suala la hakimu husika. Kwani kujiridhisha ni nini?! Lulu alikwenda kufanya jambo la Watanzania wote, si lake binafsi.”

Picha: Raisi Magufuli Amtembelea Maalim Seif katika Hoteli ya Serena kwa ajili ya kumjuilia hali yake.

$
0
0

Rais Magufuli akisalimiana naKatibu mkuu waCUF Maalim Seif Sharif Hamad   ndani  ya  Serena  Hoteli  alipoenda  kumjulia  hali  leo march 9

Habari Mbaya Kwa Wapaka Poda...Poda Zadaiwa Kusababisha Kansa

$
0
0

Kuna ne.no moja tu linaloweza kusemwa kwa sasa, kuwa tumekwisha, baada ya kubainika kuwa poda iliyotumika kwa miaka mingi nchini, ambayo ni maarufu kama Johnson’s Baby Powder inadaiwa kusababisha kansa ya kizazi inayoleta maafa ikiwemo vifo, Risasi Mchanganyiko lina taarifa kamili.

Taarifa zilizopatikana kupitia mitandao ya internet, zinadai kwamba kampuni inayotengeneza poda hiyo ya Johnson and Johnson ya Marekani, Februari 25, mwaka huu ilihukumiwa kulipa faini ya kiasi cha dola milioni 72 (sawa na shilingi bilioni 144) katika Mahakama ya Missouri kama fidia kwa mwanamke mmoja aliyefariki dunia kwa kansa ya kizazi iliyotokana na matumizi ya vipodozi hivyo.

Familia ya mwanamke huyo, Jacqueline Fox ilitakiwa kulipwa kiasi hicho cha fedha baada ya mahakama kuridhika kuwa ugonjwa na kifo chake kilitokana na matumizi ya vipodozi hivyo kwa zaidi ya miaka 35, akitumia poda pamoja na losheni ya bidhaa hiyo.

Kampuni hiyo ya Johnson & Johnson ilikabiliwa na tuhuma kwamba kwa miongo mingi, kwa lengo la kufanya biashara zaidi, haikuwaonya wateja wake kuwa miongoni mwa viungo vinavyotengeneza bidhaa hiyo, vinasababisha kansa. Zaidi ya kesi 1000 zimefunguliwa huko Missouri na 200 New Jersey, zote zikiilalamikia bidhaa hiyo.

Mwamuzi wa Kike Jonesia wa Tanzania Achakuguliwa Kuchezesha Kombe la Dunia

$
0
0
Mwamuzi wa kike wa Kimataifa wa Tanzania mwenye beji ya FIFA, Jonesia Rukyaa ameteuliwa kuungana na waamuzi kutoka nchini Kenya kuchezesha mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake wenye umri chini ya miaka 17 (WWC-Q 17) mwishoni mwa mwezi huu.

Jonesia Rukyaa atakua mwamuzi wa akiba katika mchezo huo kati ya Misri dhidi ya Cameroon utakaochezwa jijini Cairo wikiendi ya tarehe 25,26,27 Machi, 2016.

Mwamuzi wa kati katika mchezo huo atakua ni Carolyne Wanjala (Kenya), akisaidiwa na Carolyne Kiles (Kenya), Mary Njoroge (Kenya), huku kamisaa wa mchezo huo akiwa ni Leah Annette Dabanga kutoka nchi ya Afrika ya Kati.

Baada ya Maneno Mengi Kusemwa Kuhusu Mr NICE Leo Ameachia Video Mpya..Itazame Hapa...Je Itamtoa Tena?

$
0
0
Msanii mkonge wa muziki, Mr Nice ameachia video yake mpya ya wimbo ‘Kioo’. Video imeandaliwa na director Jeef Mlapon
Itazame Hapa Alafu Utoe Maoni yako

Kigogo wa Serikali Amnasa Mkewe Nyumba ya Kulala Wageni Gesti....

$
0
0
Mke wa kigogo mmoja wa serikali Mkoa wa Morogoro ambaye ni mwenyeji wa Wilaya ya Iringa, Kijiji cha Mlangali, Sakina Kisukari, amenaswa akiwa katika nyumba ya kulala wageni (gesti) akiwa na mfanyabiashara ambaye inadaiwa ni mchepuko wake.

Tukio hilo la aina yake lilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo eneo la Mshindo, Iringa baada ya kufyatuka mtego uliowekwa na mume wa mwanamke huyo kwa kushirikiana na gazeti hili kabla ya kuwashirikisha polisi ili kuepusha damu kumwagika.

Mtego huo uliwekwa kwa zaidi ya wiki mbili ili kufuatilia nyendo za mwanamke huyo ambaye aliondoka mkoani Morogoro anakoishi na familia yake kikazi na kuelekea Iringa kwa madai ya kwenda kuwasalimia ndugu zake.

Hata hivyo, baada ya bosi huyo wa serikali (jina lake limehifadhiwa kwa heshima ya kazi yake) kujaribu kupeleleza ili kujua kama kweli mkewe huyo yupo nyumbani kwa wazazi au kwa ndugu zake Iringa, aligundua hakuwepo hivyo kuanza msako wa kimyakimya kabla ya kutoa taarifa polisi kuhusu kupotelewa na mke.

Katika upelelezi wake, aligundua kuwa mke wake yupo na mchepuko katika nyumba ya kulala wageni ambayo mfanyabiashara huyo alikuwa amepanga kwa zaidi ya wiki mbili sasa akiwa na mkewe ndipo alipokwenda kumfumania akiwa chumbani.

Akisimulia mkasa mzima, kigogo huyo alisema kuwa alilazimika kufika mjini Iringa baada ya watu ambao aliwapa kazi ya kumsaka mkewe kurejesha taarifa Ijumaa jioni kuwa mkewe huyo alikuwepo katika nyumba hiyo ya kulala wageni.

“Nilifunga safari usiku na kuingia Iringa mjini saa 8 usiku, kabla ya kwenda eneo la tukio, nimekuja na cheti changu cha ndoa (nakala tunayo) tuliyofunga mwaka 2003 kama ushahidi wa ndoa yetu na nyumbani nimeacha watoto wetu watatu,” alisema.

Gazeti hili pamoja na polisi lilishuhudia kigogo huyo akimfumania mkewe baada ya kuomba wanausalama kushuhudia ili kuepusha machafuko kati ya mwenye mke na mgoni huyo ambaye alilipongeza jeshi la polisi kwa kufika kwani alisema uhai wake ungekuwa mashakani.

Akizungumza eneo la tukio akiwa chumbani, aliyefumaniwa aliyejitaja kwa jina mmoja la Hemed, alisema: “Ni kweli nimekuwa na mwanamke huyu kwa wiki mbili katika nyumba hii ya kulala wageni lakini alinidanganya kuwa hajaolewa ila ana watoto.”

Naye mwanamke huyo baada ya kuona watu wakiwa na mumewe, awali alimkana mume wake na kueleza kuwa ni shemeji yake lakini alipobanwa alikiri kuwa ni mumewe.

“Mimi kweli huyo ni mume wangu wa ndoa nilikuwa najitetea ili asinipige lakini naomba kusamehewa, ni shetani tu amenipitia kuchepuka,” alisema mwanamke huyo huku akifuta machozi.
Mumewe alimtaka mkewe amrudishie pesa zake zaidi ya Sh. milioni mbili pamoja na kitambulisho cha kazi na simu aliyoondoka nayo ili amwache aendelee na mfanyabiashara huyo.

Chanzo:GPL

Rais Wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang Akaribishwa Ikulu, Jijini Dar Leo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili kushoto) akimkaribisha mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam.

Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kulia) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye koti la drafti) mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam. Kulia niRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa tatu kulia) akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (wa tatu kushoto) mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam. Wa pili kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili kulia) pamoja na mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakipanda jukwaani kwa ajili ya kuimbiwa nyimbo za Taifa kabla ya kukagua gwaride 9 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) pamoja na mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakiwa katika jukwaa kwa ajili ya kuimbiwa nyimbo za Taifa kabla ya kukagua gwaride 9 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (mwenye tai nyekundu) akikagua gwaride la heshima katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016.
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh akipokea zawadi ya ua toka kwa mtoto mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 akiwa amefuatana na mmewe kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam.
  Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kushoto) pamoja na mkewe mama Mai Thi Hanh wakiwasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbalikati ya Tanzania na Vietnam.(Picha Zote Na Benedict Liwenga-MAELEZO)

Mjadala wa Katibu mkuu mpya CHADEMA Kuziba Nafasi Aliyoacha Dr Slaa Wateka Nchi...

$
0
0
Ni ukweli uliodhahiri kwamba kwa sasa mjadala ulioteka kila kona ya nchi ni jina la Katibu mkuu mpya CHADEMA.

Kwa mujibu wa Katiba ya chama Mwenyekiti ndiye mwenye mamlaka ya kupendekeza jina la Katibu mkuu na hatimaye kupigiwa kura na Baraza Kuu.

Jumamosi ya wiki hii nchi inatarajiwa kutikisika kwa tukio linalosubiriwa na mamilioni ya wafuasi wa Chadema kote nchini ambapo kutokea jijini Mwanza moshi mweupe utaonekana pale Freeman Mbowe atakapoibua jina la Katibu Mkuu.

Shauku ni kubwa kutokana na ukweli kwamba Chadema ndicho chama kikuu cha upinzani nchini kikiwa na mashabiki kila kona ya nchi.

Pia sababu nyingine ni kutokana na mazingira aliyoacha Katibu mkuu wa zamani Wilbroad Slaa ya kususia uongozi baada ya kukosa fursa ya kugombea Urais.Ususiaji ambao unadaiwa ulisababishwa na mkewe Josephine Mushumbusi.

Pia chama hicho kinajaza nafasi hiyo huku kikiwa na hazina kubwa ya wanachama maarufu wakiwemo mawaziri wakuu wawili wastaafu Edward Lowassa na Fredrick Sumaye.

Yote kwa yote Freeman Mbowe ndiye anatarajiwa kutegua kitendawili hiki huku wafuasi wake wakimpa jina la utani..' mzee wa kubadili gear angani..''

Tusuburi tuone...

TRA Yakusanya Trilioni 1.04 Mwezi Februari Ambayo ni Sawa na Asilimia 101% Ya Lengo La Ukusanyaji Mapato

$
0
0
Katika Kipindi cha miezi nane  kuanzia  Julai 2015 hadi Februari mwaka huu, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imekusanya jumla ya Sh  Trilioni 8.5  ikilinganishwa na lengo la kukusanya Sh trilioni 8.6 ambayo ni sawa na asilimia 99 ya makusanyo yote.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Alphayo Kidata wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu  mwenendo wa ukusanyaji wa mapato, matumizi ya mashine za EFDs, kusitisha kwa bei elekezi na usajili wa vyombo vya moto.

Amesema lengo la Mamkala hiyo ni kukusanya Trilioni 12.3 hadi ifikapo Juni mwaka huu na kwamba asilimia moja iliyobakia katika kukamilisha asilimia 100 ya ukusanyaji wa mapato kati ya Julai mwaka jana  hadi Juni mwaka huu,  itakamilika ndani ya miezi nne iliyosalia ambayo itaisha Juni mwaka huu.

Amesema pia kwa mwezi Februai pekee, Mamlaka hiyo imefanikiwa kukusanya mapato ya kiasi cha Sh Trilioni 1.04 kwa upande wa Tanzania  Bara na Zanziba ambayo kiasi hicho ni sawa na asilimia 101.18 ya lengo la ukusanyaji ambayo ilikuwa ni Sh  Trilioni  1.028 kwa mwezi.

Amesema kuongezeka kwa mapato haya kunatokana na kudhibiti kwa mianya ya ukwepaji wa kodi na kuweka mazingira rafiki kwa mlipa kodi, kurekebishwa kwa misamaha ya kodi ambayo ilikuwa inachangia upotevu wa mapato, kuongezeka kwa watumiaji wa mashine za EFDs pamoja kudhibiti eneo la forodha ambalo lilikuwa linasababisha upotevu wa mapato ya TRA.

Maeneo yaliyochangia kuongezeka kwa mapato hayo:        
“Maeneo ambayo yamechangia kuongezeka wa mapato haya ni kuimarishwa kwa bandari yetu kwa kuziba mianya ya ukwepaji kodi , kurekebishwa kwa misamaha ya kodi ambayo hapo awali ilikuwa inachangia upotevu wa ukusanyaji wa mapato, kuongezeka kwa matumizi ya utumiaji wa mashine za EFDs kwa wafanyabiashara, Mamlaka kuwatengenezea mazingira mazuri kwa walipa kodi, kudhibitiwa kwa eneo la forodha ambapo wajanja wachache walikuwa wanatumia mwanya huu kuikosesha serikali mapato” amesema Kidata.

Kwa mwezi Januari walikusanya Trilioni 1.079:
Katika  kipindi cha Januari pekee, Mmalaka hiyo ilikusanya  kiasi cha  Trilioni 1.079 kwa Tanzania bara na visiwani ambapo kiasi hicho ni sawa na asilimia 102 ya lengo la Sh Trilioni 1.059 kwa mwezi.

“Makusanyo  haya ya Januari yametokana na ari  na uthubutu ambao TRA imejiwekea katika kusimamia na kuhakikisha inaendelea kuziba mianya ya ukwepaji kodi na kuweka mazingira rafiki kwa mlipakodi  kwa kulipa kwa wakati na urahisi kwa kutumia mifumo mbalimbali iliyopo”ameongeza.

Faini ya mashine za EFDs kwa Wafanyabaishara:
Kidata amesema katika kipindi cha mwezi Februari pekee, Mamlaka hiyo imefanikiwa kukusanya  faini ya Sh 800milioni kwa watu wa jiji la Dar es Salaam ambapo walikiuka na kufanya makosa katika utumiaji wa  mashine za EFDs.

“Kuanzia mwezi Machi mwaka huu kila mtu anayetakiwa kutumia mashine za EFDs atumie  vinginevyo hatua kali za kisheria zitafuatwa”amesema Kidata.

Amesema utaratibu wa matumizi ya EFDs ulifanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza iliwahusisha  wafanyabiashara ambao wamesajiliwa kutoa VAT na awamu ya pili ilihusisha  wafanyabaishara ambao hawakusajiliwa na Vat ambao mauzo yao kwa mwaka ni zaidi ya Sh 14milioni.

Serikali kugawa bure mashine za EFDs:
Kwa upande wake Kamishna wa Kodi za Ndani kutoka TRA, Yusuph Salum alisema  serikali imeagiza Mamlaka ya Mapato nchini kutoa bure mashine za EFDs kwa wafanyabiashara  wadogo ambao uwezo wa kununua mashine hizo unaweza kuathiri mitaji yao ya biashara.

“Kwa sasa tuko katika hatua za mwisho kukamilisha manunuzi wa mashine za uniti 5700 na kwamba wafanyabiashara wakubwa hawatahusika na mgao wa mashine hizi za bure bali wao wataendelea na utaratibu wa zamani wa kujirejeshea gharama za mashine kupitia ritani za mwezi” amesema Salum.

Amesema pamoja na kuwepo kwa sheria inayomtaka mfanyabiashara kununua , kutumia mashine, kutoa risiti na kulipa kodi, TRA imebaini wafanyabiashara waliowengi hawana mashine hizo za kutolea risiti pindi wanapofaya  mauzona hivyo kuikosesha serikali.

Usajili wa magari:
Kidata alisema TRA, imefanya ukaguzi na kubaini kuwepo kwa magari ambayo yaliingizwa nchini na kusajiliwa bila kufuata taratibu za forodha hivyo kuyafanya yamilikiwe bila kulipiwa kodi stahiki na kwamba kuna jumla ya magari 9000 ambayo yanaingia nchini na kutolewa.

“Wamiliki wa magari wote  tayari  tumeshawataarifu  kufika TRA kufanyiwa uhakiki ili kuyalipia kodi stahiki lakini pia kumekuwa na matumizi mabaya ya misamaha iliyotolewa hasa kwa upande wa magari, hivyo utaratibu wa misamaha uliwekwa kwa ajili ya kuwapa nafuu wawekezaji ili wahusika wamekuwa wakiitumia vibaya kwani magari yameingizwa mengi kuliko mahitaji na kupelekea serikali kukosa mapato” amesema

Amesema sheria za kodi zinatoa misamaha mbalimbali kupitia utaratibu wa Kituo cha Uwekezaji cha Taifa(TIC) na mashirika yasiyo ya kiserikali na kwmaba nia na madhumuni ya misamaha hiyo ni kuvutia uwekezaji na kutoa unafuu wa huduma kwa jamii.

Kufutwa kwa bei elekezi:
Katika hatua nyingine,  Mamlaka hiyo imefuta bei elekezi katika  mchakato wa uthaminishaji wa bidhaa bandarini kwa sababu  ni kinyume cha sheria ya Jumuiay ya Afrika Mashariki na kwamba TRA itaendesha shughuli za kiforodha kulingana na sheria husika.

“Tumeona bei elekezi haisaidi kwa sababu uingizaji wa bidhaa unatawaliwa na sheria ya Afrika Mashariki ambapo na sisi Tanzania ni wanachama, hivyo Mamlaka itadhibiti ukaguzi na uthaminishaji halisi ili kila mfanyabaishara alipe ushuru na kodi kulingana na thamani ya bidhaa husika, hata hivyo uthaminishaji mizigo kwa wafanyabiashara umepelekea wengine kulipa kodi kubwa kuliko thamani ya bidhaa husika” amesema.

Nina Kazi nzuri.. Gari...Nyumba, Pesa...Lakini Sipati Mke

$
0
0
Mmh nimekuwa mchangiaji mzuri sana wa threads za wengine ila leo limenigusa so nimeamua tu na mimi nianzishe kathread kangu lol. Excuse my gazeti

For a while nimekuwa nikisikia na kuona wakaka wengi, especially wale ambao wanataka kuoa wakilalamika "nina gari, nina nyumba, kazi nzuri, hela etc. But sipati mke wa kuoa". Jana tu I was talking to a certain brod na yeye akaniambia the same thing. Yani hiyo statement huwa inanipa a series of unanswered questions. Najua hiyo type na humu ndani wapo kibao. Siwatukani ila najiuliza tu, hivi mnavyowazaga hivyo huwa mnakuwa kwenye akili zenu timamu au? Tangu lini gari likaoa mke, unataka mke au unataka dereva/abiria? Una nyumba..so what, are you looking for a tenant, a house keeper or what? Aliyewaambia kwamba kuwa na gari, kazi na nyumba ndo kigezo tosha cha kuoa ni nani? Hivi hukai hukajiuliza mbona nina hivyo vyote but huu ni mwaka wa 3, 4, 5 natafuta "mke" na Sijapata? Kuna tatizo gani? Ungekuwa umekaa kwa kina ukajiuliza hivyo basi naamini akili yako ingekuwa imefunguka hata kidogo.

Apart from nyumba, kazi, gari.. what else can you offer?. Kama hivyo ndo vingekuwa the only vigezo, basi kila mwenye navyo angekuwa ameoa warembo wa kutosha sana tu. Hivyo mnavyoviona ndo vigezo tosha, baadhi yetu tunaviona kama "bonus" tu kwa mwanaume anayejitambua. Mnatiana tu ujinga humu, Tafuta pesa, utang'oa mademu wa kila aina, nachokagaaa mimi mmh. Of coz utang'oa mademu wasiojitambua, sio wenye akili zao timamu unless una extra things to offer. Kila mtu anapenda pesa/gari, lakini sio kila mtu anashobokea pesa/gari. Hivi seriously unampata msichana eti kwa sababu una gari, hivi hii century kuna watu still wanashoboka na magari, unless wana matatizo. Gari ambalo unapewa lift mara moja kwa wiki/ mwezi siku zingine zote unashika bomba, ndo limfanye mtu avue tei tei? Hivi ukiwa na mwenye gari na wewe unakuwa unaown hiyo gari au ownership yake ni sexually transfered? Wewe utakayemla huyo girl na huyo girl wote mna matatizo tena makubwa tu. Tafuta hela zako, jitambue then utapata wanawake wanaojitambua. Wanaume malimbukeni wa hela hatuwataki. Kuna watu hata watokee kwenye Forbes na WB waseme watafinance harusi yenu, hukubali kuolewa naye ng'oooo maana hajitambui. Mtu hana cha maana anachoongea ila kujibrag tu, nina hiki, nina kile mweee yani hapo mwenyewe anaona kashamaliza mchezo. So disgusting, ndo maturity ya mtu anayetaka kuoa huyo pyeee. Huna cha maana cha kukudefine apart from gari na nyumba mmmh. Usipendwe na mtu, basi ushajistukia "au kisa nina gari" mwee jamaniii. Siku ukimiliki jet si ndo hata humu Ukipewa like utahisi "ashasikia nina jet, ananishobokea" hahahah

Afu nyie average joes ndo mnasumbua kweli. Mtu akifanikiwa tu kidogo anajikuta Bakhresa na yeye, hivyo vigezo sasa "huyu demu sio wa hadhi yangu". Wewe hadhi yako ni ipi haswa?. It reaches a stage mnatuita watoto wa watu "scrapers" hivi una uwezo wa kuumba hata kidole wewe? If you can afford someone expensive please just go for her, sie wenye sura na shape za wajomba zetu tuacheni kwa heshima tu. Have you ever asked yourselves watu wenye hela za uhakika, mawaziri, the high profile Men wake zao wakoje? Unakuta ni mabinti wa kawaida tu wengi, but wana class. Hata kama ukikuta binti ni famous, beautiful ana status etc, lazima "ANAJITAMBUA" kwanza. Ila nyie ndugu zangu sasa ukiwa na hela tu kinachokuja ni "a very beautiful girl" washkaji wakukomeeee. please kabla beauty haijaja pima anajitambuaje. Uzuri, hela, status ni "BONUS" jamani. Angalia ni Vitu gani mtu anavyo vya kusustain ndoa yenu. (Sijasema muoe wanawake mvutoless, sio sifa na hata hao mvutoless sometimes wanapretend kuwa decent ili kujiongezea marks. Beauty + brain+ character). Mnajikuta mnajenga mahusiano yanayobase kwenye hela za mawazo, kesho na kesho kutwa umetetereka kidogo mke kakukimbia utamlaumu? She was there for money, hela imeisha afanye nini sasa. Oooh nina gari, sawa utaoa "dereva/abiria " na sio "mke mwema". Kesho ukiwa huna gari usishangae dereva/abiria wako akikutoroka. Abaki kufanyaje kwa mfano, acha akatafute gari lingine

Embu leo hii, ufahamu wako utanuke kidogo. Jiulize unataka mahusiano Yenye misingi ipi, na hiyo misingi yako itakupelekea kuwa na ndoa ya aina gani. Una kitu gani cha kuoffer mahusiano yako ili yawe sustainable (things that are looking for long term sustainability) apart from vigezo "bonus". Jitafute wewe binafsi, jijenge vizuri then jikabidhi kwa Mungu akuongoze kwenye huo mchakato. Usichague kwa macho ya kibinadamu na akili tu za kawaida. Muombe Mungu akupe macho ya rohoni, utaona hadi na attributes zisizoonekana kwa macho ya kawaida. Hela ni za muhimu sana lakini sio kitu pekee kwenye mahusiano. I pray wote mnaotafuta wake mpate wake wema eeh, mtuletee testimonies nzuri nzuri jamani
Anyway zilikuwa tu ni akili zangu za wakati huu, I'm still entitled to my opinions. Additions + Polite criticisms are warmly welcome, I don't invite insults abegooooo

HAPPY WOMEN'S DAY

By Heaven Sent

Tazama Picha za WEMA SEPETU Alivyopamba Mapokezi ya Lulu Michael Jana Kutoka Airport.....

$
0
0
 Kwa Mara ya Kwanza toka habari za ujauzito wa Wema kutoka Jana Amejitokeza hadharani kumpokea rafiki yake Lulu Michael Alipowasili kutoka Nigeria akiwa na tuzo mkononi..Wema Alipendeza Sana na kuonekana mwenye furaha muda wote wa msafara......


Ukitaka Kupata Msongo wa Mawazo Mpaka ufe oa Hawa Wafuatao

$
0
0
1. Mama mwenye mtoto/watoto aliyeachika akiwa kwenye ndoa

2. Mwanamke aliyeachika ndani ya ndoa

3. Mwanamke yupo karibu mitandao yote ya kijamii, hakuna habari ya kimbea yeye anapitwa (Tena siku hizi WhatsApp wanawake hasa akina dada wana magroup, hadi migegedo ya saizi mbalimbali wanatumiana)

4. Mdada aliyeenda umri halafu anaishi gheto ( Hawa mara nyingi wamekubuhu, hadi wanaume wakwere wanawakwepa, wadada hawa hujifanya social, wana msururu wa marafiki wa kiume, mara nyingi hit and run kwao ni kawaida)

5. Mdada unayemtongoza siku moja, ya pili au ya tatu ukimwita kwako, anajileta. Kumbuka wewe sio wa kwanza kumtongoza, wewe labda ni wa hamsini.

Dunia Inahitaji Kiongozi Namna ya Donald Trump....Hakuna Kuremba Wala Kupakana Mafuta Kwa Mgongo wa Chupa..Hapa Kazi Tuuuu

$
0
0
Kama kuna kupindi amerika na Dunia vinahitaji kiongozi wa namna ya Trump ni sasa, Licha ya kashfa nyingi anazotoa kwa Afrika na nchi nyingine kama Mexico na China ila Dunia ya sasa inamuhitaji sana, Hasa Tanzania kwa kuwa tumepata kiongozi mwenye hulka ya kazi ambayo ni legacy ya Trump mwenyewe basi itakuwa kolabo bora zaidi kama wamarekani watampa Trump urais.

Dunia ya sasa haihitaji Rais wa marekani mnafiki anayepaka nchi nyingine mafuta kwa mgongo wa chupa ili ale nao kama kipofu, Tunahitaji kiongozi wa Marekani aliye straight foward na asiyeogopa nchi yoyote akitaka kufanya biashara.

Moja ya jambo kubwa linalomchukiza Trump ni swala la marekani kujifanya kiranja wa dunia kila jambo lazima aingilie, yeye amesema kufanya hivyo ndio kunaifanya marekani irudishwe nyuma na nchi kama china.

So kama wamarekani watampa uyu jamaa nchi basi dunia itakuwa huru zaid kwenye biashara na nadhani kwa hari ya kazi ya Magufuli Tanzania tutapiga hatua kubwa . . .

Mbunge Ala Kichapo Cha Maana Toka Kwa Mkewe Siku ya Wanawake Duniani...

$
0
0
Mwanasiasa mkongwe Moses Wetang’ula Senator wa kaunti ya Bungoma, ambaye pia ni Waziri wa zamani wa mambo ya nje na Waziri wa zamani wa Biashara nchini Kenya. Jumapili ya tar.6 March (siku mbili kabla ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani) alipewa kipigo kikali na mke wake An Wacheke Ngugi hali iliyopelekea kukimbizwa hospitali kwa matibabu kabla hajaenda kuripoti Polisi ambapo alikuta mkewe ameshamtangulia kuripoti. Yani mke alimpiga mume kisha akawahi Polisi kusema amepigwa.

Hali hiyo ilipelekea kutengenezwa kwa picha hii na wapinzani wake kisiasa (photoshop) wakionesha alivyoathiriwa na kipigo cha mkewe. Licha ya kuwa picha hii ni photoshop lakini ni kweli kuwa Wetangula alipigwa na mkewe na kupatiwa matibabu ktk hospitali ya Bungoma.

Gazeti la Daily Nation la nchini Kenya limeripoti kuwa hii si mara ya kwanza kutokea mafarakano na kupigana kati ya Wetangula na mkewe Ann. Licha Ann kutoa kipigo hicho kwa mumewe lakini na yeye amekimbilia Polisi kumshtaki Wetangula. Kesi hii ni ya pili baada ya ile aliyofungua February 18 akidai kupigwa tena na mumewe.

Ann Wacheke Ngugi ni mfuasi wa muungano wa vyama vya siasa vya Jubilee Alliance vinavyoongoza serikali chini ya Rais Uhuru Kenyatta, licha ya kuwa mumewe ni kiongozi wa chama cha upinzani cha CORD. Tofauti ya kisiasa ya wenzi hao wawili inasemekana kuwa chanzo cha mfarakano ndani ya ndoa yao.

Kumekuwa na desturi kwa wanasiasa wengi nchini Kenya kupokea kipigo au kufanyiwa unyanyasaji wa kijinsia na wake zao. Rais Kibaki na Arap Moi ni miongoni mwa viongozi wa juu wa nchi hiyo waliodaiwa kupigwa na wake zao. Wetangula pia ametangaza nia ya kugombea Urais mwakani. Ikiwa atapitishwa na chama chake na kushinda bila shaka ataendeleza list ya Marais wa Kenya kupigwa na wake zao. Je ingekua wewe ndo Wetangula ungefanyaje??

Rekodi Yangu Kamwe Haitavunjwa – Mr. Nice

$
0
0
Mr. Nice ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio na kusema kuwa kwa sasa kazi anazofanya ni kwa ajili tu ya mashabiki wake, ili asiwapoteze lakini hahitaji hata promo.

“Ninachojaribu kukifanya hapa ni kwamba naendelea kuwa mwanamuziki kwa sababu sasa hivi sitafuti promo ya aina yoyote, the only thing I need is respect and money, ni heshima na pesa tu ndio natafuta, , kwa hiyo naendelea kutoa nyimbo nzuri ili niendelee kuwa na mashabiki wangu nisiwapoteze,”, alisema Mr. Nice.

Pamoja na hayo Mr. Nice amesema haitaji kazi zake za sasa zifanye vizuri, kwani hataki kuvunja rekodi aliyoiweka kwenye muziki, kutokana na kazi zake za kwanza.

“Mimi ninachoombea Mungu katika kazi ninazotoa sasa hivi zisibeat rekodi zangu ambazo nimeweka, sababu zitaniharibia rekodi, sitaki kujenga rekodi mpya, rekodi iliyokuwepo ipo kwa sababu haitakaa ivunjwe na hata mwenyewe sitaki kuivunja lakini sio kwa ajili ya kubreak records zangu, rekodi zangu zipo na zitaendelea kuwepo”, alisema Mr. Nice.

Maongezi Ya Rais Magufuli na Rais Truong Wa Vietnam Baada Ya Kukutana IKULU Yako Hapa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam Mheshimiwa Truong Tan Sang ambaye amewasili hapa nchini jana jioni tarehe 08 Machi, 2016 kwa ziara ya kiserikali ya siku nne, amepokelewa rasmi na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Katika lango kuu lililopo Mashariki mwa Ikulu, Rais Truong Tan Sang amekagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima yake na amepigiwa mizinga 21 iliyokwenda sambamba na nyimbo za mataifa yote mawili.

Pamoja na mapokezi hayo, Marais hao wawili wamefanya mazungumzo ya faragha ambayo yamehudhuriwa pia na makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, na baadaye kufuatiwa na mazungumzo rasmi kati ya Rais Magufuli na ujumbe wake na Rais Truong na Ujumbe wake.

Katika Mazungumzo hayo, Rais Magufuli ameahidi kuuendeleza na kuuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Vietnam ambao ulijengwa na waasisi wa mataifa haya mawili Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Ho Chi Minh, hata kabla ya Uhuru, huku akitilia mkazo juu ya ushirikiano katika maendeleo ya kiuchumi.

Rais Magufuli amemweleza Rais Truong Tan Sang kuwa katika miaka mitano ijayo, Tanzania imedhamiria kujikita katika uanzishwaji wa viwanda vingi, na hivyo ametaka mahusiano kati ya Tanzania na Vietnam yajielekeze katika kuendeleza Kilimo na ufugaji na hivyo kuiwezesha nchi kuwa na uhakika wa chakula na pia kupata ziada itakayouzwa nchi.

"Tunatambua jinsi Vietnam ilivyopiga hatua kubwa katika uvuvi, uzalishaji wa kahawa na uzalishaji wa mpunga. Uzalishaji katika maeneo hayo umeiwezesha kuwa nchi inayoongoza duniani, na sisi Tanzania tunataka kujifunza kutoka kwenu" Amesisitiza Rais Magufuli.

Kufuatia hali hiyo, Rais Magufuli amemuomba Rais Truong Tan Sang, kuwa uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizi mbili ujikite katika kuendeleza kilimo hususani kutumia zana bora za kilimo badala ya jembe la mkono, Kilimo cha umwagiliaji badala ya kutegemea mvua, kuzingatia mbinu bora za ugani, kukabiliana na wadudu waharibifu wa mazao na kupata masoko ya mazao.

Kwa upande wake Rais wa Vietnam Mheshimiwa Truong Tan Sang amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuiongoza awamu ya Tano na amemhakikishia kuwa Vietnam itaendelea kushirikiana na Tanzania, huku ikitambua mchango mkubwa uliotolewa na watu wa Tanzania walioiunga mkono juhudi za kuiunganisha nchi hiyo na kuwa Jamhuri ya Kisoshalisti mwaka 1968.

Amesema kwa kuzingatia mazingira bora ya Tanzania yenye amani na utulivu, Vietnam imedhamiria kuwa Tanzania iwe kituo chake cha kuzifikia nchi nyingine za Afrika Mashariki na sehemu nyingine za Afrika.

Rais Truong Tan Sang ameomba mahusiano ya Tanzania na Vietnam, sasa yajielekeze katika kuongeza Biashara, huku akieleza kuwa biashara ya Dola za Marekani milioni takribani milioni 300 haitoshi, na hivyo amependekeza wafanyabiashara wa Tanzania kuunganishwa na wenzao wa Vietnam ili mauzo ya bidhaa kutoka pande zote mbili yaongezeke hadi kufikia dola za Marekani bilioni 1 ifikapo mwaka 2020.

Ameongeza kuwa Vietnam ipo tayari kutiliana saini mikataba mbalimbali ya ushirikiano katika biashara, Viwanda na Kilimo, na ametoa mwaliko kwa wakulima wa Tanzania kwenda kujifunza nchini Vietnam.

Mara baada ya Mazungumzo hayo, Marais wote wawili wamezungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari ambapo wote wawili wamesisitiza kuwa, nchi zao zipo tayari kukuza zaidi mahusiano na ushirikiano kwa faida ya wananchi wake.

Gerson Msigwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam-09 Machi, 2016.

Kiingereza Kibovu cha Rais Magufuli Chaibua Jipu la Miaka 55

$
0
0
KATI ya mambo mawili yaliyofanywa na Rais John Magufuli wiki iliyopita, moja lilinifurahisha; jingine lilinisikitisha. Nitaanza na lililonifurahisha, anaandika Ansbert Ngurumo.

Rais Magufuli, akiwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, alitumia Kiswahili kuhutubia marais wenzake na washiriki wengine, katika ukumbi wa hoteli ya Ngurdoto, mkoani Arusha.

Alinifurahisha jinsi alivyotumia fursa hiyo kusisitiza masuala nyeti ambayo, ama angependa yasimamiwe au yalimkera na aliagiza yasahihishwe.

Rais alisisitiza mambo kadhaa. Kwanza, alizungumzia haja ya nchi wanachama kuvumiliana, kwani kila moja ina matatizo yake.

Pili, alisisitiza umuhimu wa sekretarieti kubana matumizi. Akasema wanatumikia nchi maskini, kwa ajili ya wananchi maskini; hivyo wanapaswa kufanya kazi wakijielekeza kuokoa fedha ili kuelekeza nguvu katika huduma.

Alitoa mfano wa gharama za ukumbi waliotumia kwa ajili ya mkutano huo, katika Hoteli ya Ngurdoto, akisema hesabu zinaonesha kila mshiriki amelipiwa dola 45.
Akasema kama mkutano huo ungefanyikia katika Ukumbi wa Mikutano wa Kituo cha Kimataifa cha Arusha (AICC), kila mjumbe angelipiwa dola 30.

Akatoa mfano kwamba dola 15 ambazo zingeokolewa zingeweza kusaidia ununuzi wa madawati au kuchangia gharama za usuluhishi wa mgogoro wa Burundi.
Mambo haya yatakuwa yamemjengea Rais Magufuli taswira chanya mbele ya wenzake na jamii ya kimataifa.

Hata wananchi wake waweza kuwa walijisikia vizuri kwamba rais wao amethubutu kukumbusha wenzake masuala muhimu waliyopuuza kwa muda mrefu.
Na amefanya hivyo mapema kabisa mwa kipindi cha uenyekiti wake. Ameweka mweleleko mpya unaosisitiza utumishi badala ya utawala.

Hata hivyo, licha ya uzuri wa hoja zake, kuna moja ambalo lilionekana kukera wengi, wakiwamo wasaidizi wake wa karibu.

Nilibahatika kuzungumza na baadhi ya wasaidizi wake. Wengine walisema kwa uwazi; wengine wakakwepa kuzungumza kwa uwazi.

Baadhi ya wasaidizi wa rais, viongozi wa serikali, na wananchi wasomi makini, wameonekana kuchukizwa na jinsi Rais Magufuli alivyotupia maneno ya Kiingereza, hapa na pale katika hotuba yake.
Zipo sababu za mtu kuonekana amechukia. Mambo mazuri niliyozungumzia hapo juu yangeweza kusisitizwa vizuri tu kwa Kiswahili bila kuchomeka Kiingereza.

Au kama mzungumzaji aliamua kuchomeka Kiingereza, basi alipaswa achomeke Kiingereza sanifu.
Yafuatayo ni baadhi ya maneno ya Kiingereza aliyochomeka Rais Magufuli, ambayo hayakupendeza wasikilizaji. Ninaweka hapa mifano mitatu:

“…We are supposed to look each other as one family.”
“Kila siku they come with a special proposals. And that proposals is always positive proposals. Not negative proposals…”
Count on me. I don’t know to whom interest…”
Hotuba ya Rais Magufuli imeibua maneno mengi kutoka kwa watani wake wa kijamii na wa kisiasa.
Nimesikia mmoja akisema, “…sasa naelewa kwanini rais hakuhudhuria hafla ya mabalozi aliyoandaa mwenyewe Ikulu mwezi uliopita.”

Mwingine akisema, “…kumbe ndiyo maana mgombea urais wa UKAWA alipoambiwa mdahalo akasema angeshiriki kama ungeandaliwa kwa Kiingereza.”

Mwingine akidiriki kulinganisha Kiingereza cha Jacob Zuma, Rais wa Afrika Kusini, (ambaye hakukwea madarasa na kutafuna karatasi za vitabu vingi); na kile cha Dk. Magufuli, mwenye shahada ya tatu – ya uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mzazi mmoja jijini Dar es Salaam amesema Kiingereza cha Magufuli kimesababisha ugomvi kati yake na mtoto wake.

Mzazi huyo hakufurahishwa na kitendo cha mtoto wake cha kuchambua makosa ya kisarufi katika “Kiingereza cha rais.”

Hoja yangu ni ipi? Rais kujua au kutojua Kiingereza? Hapana! CCM ina kigezo cha mgombea urais kuwa angalau na digrii moja. Hicho ndicho walitumia “kumzuia” Augustine Mrema.
Sasa huyu mwenye shahada anatarajiwa walau ajue vema lugha mbili kuu, kikiwemo Kiingereza. Tuangalie hoja zifuatazo:

Kwanza, kwa kuwa rais amejifunza lugha hiyo na atakuwa ameitumia kujifunzia masomo mengine hadi kupata digrii ya uzamivu, anapaswa – siyo tu kuielewa bali hata kuiheshimu – na kuitumia inavyopasa.

Pili, rais hakuwa na sababu ya kutumia maneno ya Kiingereza. Kama alikuwa ameamua kuchanganya Kiswahili na Kiingereza, angetumia Kiingereza sanifu.

Tatu, rais kukosea maneno ya kawaida na kuzungumza Kiingereza “ndivyo-sivyo,” amekuwa mfano mbaya kwa watoto wanaojifunza lugha hiyo, huku wakigombezwa na walimu wao kwa makosa ambayo hata rais anafanya.

Nne, washauri wa rais wamwandalie hotuba. Katika mazingira haya ndipo uzuri wa hotuba zilizoandikwa unapoonekana. Angeweza kusema maneno haya kwa kuyasoma. Yawezekana hata Kiingereza kingenyoshwa, kama angetaka kiwemo.

Tano, kwamba mwalimu wa zamani wa kemia katika shule ya sekondari, ambaye sasa ni msomi wa ngazi ya shahada ya uzamivu katika kemia, anapokosea vitu vidogo lakini muhimu kama hivi, hatoi mfano mzuri kwa watoto wetu ambao wanagombezwa na walimu na wazazi kila wanapokosea Kiingereza kama alivyofanya.

Sita, rais ajenge utamaduni wa kusikiliza washauri wake Ikulu – kama alikuwa hajajenga tabia hiyo. Ni kwa njia hiyo aweza kuepuka makosa ya aina inayojadiliwa. Akubali kusoma hotuba alizoandika au alizoandikiwa na washauri wake.

Saba, ujengwe utaratibu wa kudumu kwa viongozi wetu kuenzi Kiswahili na kukitumia katika mikutano ya kitaifa na kimataifa, ndani na nje ya nchi. Kiswahili kimeshakua. Kama Tanzania tunajiita kitovu cha Kiswahili, tuoneshe kwa vitendo kwamba tunaweza kuipa dunia lugha ya kazi.
Nakumbuka miaka kadhaa iliyopita, katika mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika, wakati Benjamin Mkapa akiwa rais, alihutubia viongozi wenzake kwa Kiingereza sanifu.

Ilipofika zamu ya Joachim Chissano, aliyekuwa rais wa Msumbiji, akahutubia kwa Kiswahili mwanzo hadi mwisho. Tulimsema Rais Mkapa kwamba alikuwa amenyang’anywa fursa adhimu ya kumiliki Kiswahili na kuonyesha kuwa Tanzania ndiyo kisima cha Kiswahili.

Tangu mwaka 2005, Kiswahili ni moja ya lugha rasmi za Umoja wa Afrika, kikiwa lugha pekee yenye asili ya bara hili.

Tunatambua kuwa viongozi wetu wengi wanajua Kiswahili kuliko Kiingereza.
Ni vema basi watumie lugha yao kuliko lugha ya kigeni inayowapa shida katika kuwasiliana na wenzao.
Mwaka 2007 nilialikwa kutoa mhadhara katika Kongamano la Highway Africa, lifanyikalo kila mwaka katika Chuo Kikuu cha Rhodes, Grahamstown, Afrika Kusini. Mada yangu ilihusu jinsi ya kublogu kwa Kiswahili.

Katika utafiti wangu, niligundua kuwa Kiswahili kimekua kuliko wengi wetu wanavyofahamu. Niliwaeleza wasikilizaji kutoka nchi zote za Afrika kwamba Kiswahili ni moja ya lugha zinazokua kwa kasi duniani.

Katika Afrika pekee kilikuwa na wazungumzaji zaidi ya milioni 100. Katika Afrika Kusini mwa Sahara, Kiswahili ni lugha inayozungumzwa kuliko lugha nyingine zote.

Katika maeneo kadhaa ya Afrika, Kiswahili kinatumika Tanzania, Kenya, Uganda, Somalia, Kongo (DRC), Burundi, Rwanda, Msumbiji, Zambia, Malawi, Sudan, Comoro na Malagasy.
Vyuo vikuu zaidi ya 100 duniani vina programu ya kufundisha Kiswahili. Vituo kadhaa vya redio vya nchi mbalimbali duniani vina idhaa ya Kiswahili.

Mifano michache ni BBC, Uingereza; Radio Deutsche Welle, Ujerumani; Nippon Hoso Kyokai (NHK), Japan; Voice of America (VoA), Marekani; Radio China, China; Radio Cairo, Misri; Radio Moscow International, Urusi; Radio Sudan, Sudan; Channel Africa ya Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini (SABC), Radio France International (RFI), Ufaransa; na Radio India, India.
Nilipokuwa Uingereza, moja ya kazi nilizofanya ili kuongeza kipato ni kuwa mfasili wa kazi za Kiswahili kwenda Kiingereza kwa ajili ya kampuni kadhaa zilizokuwa na mikataba na vyuo kadhaa vya Marekani katika kukuza Kiswahili.

Kilichonisikitisha ni kwamba katika mradi huu, tulikuwa wafasili zaidi ya 20 wa Kiswahili kutoka nchi mbalimbali; lakini mimi ndiye pekee niliyekuwa Mtanzania. Wengine walitoka Kenya, Afrika Kusini, Canada na Congo.

Wanaosafiri kwa ndege za KQ – Shirika la Ndege le Kenya – wamekuwa wanasikia Kiswahili chenye lafudhi na msamiati wa Kenya kwenye matangazo yao. Hata kwenye mitandao, Kiswahili ambacho kinaonekana kurasimishwa ni cha Kenya, si cha Tanzania.

Sisi tumetumia nguvu nyingi kung’ang’ania Kiingereza, ambacho watu wetu hawawezi kuzungumza vizuri kwa kuwa hawakupata msingi mzuri wa kufunzwa lugha hiyo; ingawa imetumika kama lugha ya kufundishia masomo mengine tangu sekondari hadi chuo kikuu.

Ndiyo, Kiswahili ni lugha ya taifa tangu 1961. Watanzania wengi wanazungumza Kiswahili. Vyombo vyetu vya habari vingi, vinaandika au kurusha taarifa za habari na matangazo kwa Kiswahili.

Tuna BAKITA, Baraza la Kiswahili la Taifa. Tuna TUKI, Taasisi ya Ukuzaji wa Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambayo nasikia imekua na kujitanua zaidi.
Tuna miradi mingi ya kukuza Kiswahili. Lakini tumejifanya wanyonge wa kuenzi Kiswahili. Wakenya sasa wanaelekea kupora lugha yetu. Tusipostuka, kuna wakati tutajikuta tunakwenda Kenya kujifunza Kiswahili.

Natambua kuwa mjadala juu ya lugha ya kufundishia katika shule zetu haujaisha. Wapo wanaotaka Kiingereza kiendelee kutumika kufundishia watoto wetu. Wengine wanasema Kiswahili kitumike.
Hoja hiyo itajadiliwa siku nyingine. Lakini lililo wazi ni kwamba, lolote tutakaloamua halitakuwa na uzito, halitatekelezeka, iwapo litakosa msukumo wa kisiasa.

Kwa sasa, hatuna mwingine wa kubeba jukumu hili, bali Rais Magufuli. Alibebe kwa kuazimia na kuonyesha kwa vitendo kuwa popote atakapokuwa, atahutubia kwa Kiswahili ili kukidhi matakwa haya na kuepusha adha niliyotaja hapo awali.

Hatua hii itasaidia kuongeza ajira. Watahitajika wafasili. Yeye azungumze, wengine watafsiri, dunia isikilize.

Kwetu, au kwa yeyote anayejua lugha hiyo, Kiswahili ni hazina. Ni soko la ajira. Ni mtaji. Lakini hakijaweza kutumika kiuchumi kuboresha maisha ya wananchi kwa sababu viongozi wanakipuuza.
Inasikitisha zaidi kwamba marais wetu wameshindwa kukuza Kiswahili katika ngazi ya kimataifa.
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alikuwa mwandishi na mzungumzaji mahiri wa Kiswahili na Kiingereza. Lakini alitumia Kiingereza kila alipohutubia jamii ya kimataifa.
Marais Ali Hassan Mwinyi, na Benjamin Mkapa nao walifuata nyayo za Mwalimu Nyerere. Walihutubia kwa kusoma hotuba walizoandika au walizoandikiwa na wasaidizi wao – kwa Kiingereza sanifu.

Mara moja tu, Rais Jakaya Kikwete, alianza kwa kuhutubia mkutano wa Umoja wa Afrika kwa Kiswahili. Baadaye naye alitawaliwa na Kiingereza.

Hata hivyo, tofauti ya marais hao wanne na Rais Magufuli ni uwezo wao wa kumudu lugha hiyo. Hili ndilo limesababisha mitandao ya kijamii kujadili sana “Kiingereza kibovu cha Magufuli” na kusahau maudhui ya hotuba yake.

Na huu ndio msukumo wa ushauri wangu kwa Rais Magufuli. Atutangulie katika mradi mpya wa kukuza na kueneza Kiswahili duniani.

Kwa kutekeleza mradi huu, Rais Magufuli atakuwa ametumbua jipu lililoshindikana kwa miaka 55. Asishindwe.

Uchambuzi huu umechapishwa kwa mara ya kwanza katika gazeti la MwanaHALISI toleo Na. 329 la Jumatatu, Machi 7, 2016.

Rais wa Zanzibar Dr. Shein Amtembelea na Kumjulia hali Maalim Seif Jijini Dar es Salaam

$
0
0
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiambatana na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala bora Mheshimiwa Dkt. Mwinyihaji Makame, amemtembelea kumjulia hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Maalim Seif Shariff Hamad ambaye yuko hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mapumziko baada ya kutolewa hospitali.

Amesema afya yake inazidi kuimarika siku hadi siku. Dkt. Shein alifika hotelini hapo jana  saa mbili usiku. (Picha na Salmin Said, OMKR)

Donald Trump ni Zaidi ya Mgombea Urais wa Marekani Msema Ovyo

$
0
0
Mtia nia ya urais wa Marekani kupitia tiketi ya Chama cha Republican, Donald Trump ameelezewa kuwa tishio kwa wapanga sera za Marekani wajulikanao kama “the stablishment.”

Marekani kuna genge la watu mashuhuri wa aina mbalimbali wanaoshika hatamu za Taifa hilo kubwa duniani wajumuisha wanachama wa vyama vikuu viwili vya nchi hiyo Democrats na Republican.

Genge hilo lenye azma ya kuitawala dunia kupitia kile kiitwacho mfumo mpya wa ulimwengu au ‘New World Order’, huendeshwa na genge jingine dogo lijulikana kama “The Globalists.”

Watu hawa hujumuisha wamiliki wa mabenki makubwa, wamiliki wa viwanda vikubwa vikiwamo vile vya silaha, kampuni kubwa, wanasiasa na wamiliki na waandamizi wa vyombo vya habari.

Genge hilo limeunda mashirika maalum kutekeleza ajenda yao ya kuitawala dunia chini ya serikali moja, sarafu moja, jeshi moja na mfumo mmoja wa siasa.

Mashirika hayo ni pamoja na The Council on Foreign Relations (CFR) lililoundwa mwaka 1920. Tangu CFR iundwe, hakuna rais hata mmoja wa Marekani ambaye ametoka nje ya shirika hili.

Shirika jingine ni lile liitwalo The Bilderberg Group au kifupi Bilderberg. Hili ni jukwaa maalumu la kuandaa wanasiasa watarajiwa kuongoza nchi mbalimbali za Ulaya na Marekani.

Trialateral Commison ni shirika jingine la kistratejia zaidi ambalo huhakikisha kuwa nchi za Ulaya, Marekani na Japan zinaoanisha mambo yao ili kuendelea kutawala dunia.

Watu wa ndani na wa nje

Watu wote wanaoshiriki siasa za Marekani wamegawika katika makundi mawili makuu- moja linaitwa Insiders yaani watu wa ndani ya mfumo nilioeleza na jingine Outsiders yaani watu walio nje ya mfumo hupo.

Kati ya wagombea wote wanaowania urais wa Marekani, ni Donald Trump ndiye anayeonekana kuwa mtu kutoka nje ya mfumo nilioueleza hapo juu kwa sababu yeye hayupo CFR, Bilderberg wala Trilateral.

Kwa siasa za Marekani, Donald Trump ni mtu wa nje hivyo hata kama ni mwanachama wa Chama cha Republican na anashinda katika kinyang’anyiro cha kuwania kuteuliwa mgombea urais wa chama cha Republican bado haaminiki na washika dau wakuu wa chama hicho.

Kwa jinsi mfumo wa siasa za Marekani ulivyo, mtu anayestahiki kubeba jukumu la kuwa mgombea urais iwe ni kwa Chama cha Republican au Democrats lazima utokane na mfumo niliouelezea hapo juu.

Sababu ni kwamba mtu anayetokana na mfumo huo anajua malengo ya muda mrefu ya genge linalotawala Marekani hivyo akiwa rais hatokwenda kinyume na matakwa ya genge hilo.

Mtu kama Donald Trump, bilionea wa majumba ya kamari (casinos) na wa majumba ya kupanga (real estate) nchini Marekani, kwa kuwa ni mtu wa nje ya mfumo hivyo haaminiki kuliongoza taifa hilo kwani akifanikiwa kuwa rais atafanya uamuzi ambao utaliathiri genge hilo.

Ni kweli Trump anatishia masilahi ya wakubwa?

Kwa mujibu wa jarida maarufu Marekani la Wall Street Journal na vyombo vingine vya habari nchini humo, kauli za Donald Trump zinaelezewa kuwatia hofu matajiri wa Marekani kwamba akishinda urais atafanya mageuzi ya sera mbalimbali zilizokuwa zinawanufaisha wao.

Miongoni mwa kauli hizo ni ile ya kupinga mikataba ya kibishara inayofuta kodi ya ushuru kwa bidhaa zinazoingia nchini Marekani, mikataba ambayo inawanufaisha wafanyabiashara wakubwa na wenye viwanda.

Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, chini ya kichwa cha habari “As Stock Market Plunges, Donald Trump Takes a Worldview”, Trump anaelezewa kuwanyima usingizi wafanyabiashara na wenye viwanda wanaonufaika na mikataba hiyo.

Katika makala hiyo gazeti hilo liliandika “Mr. Trump has said that bad trade deals with China and Mexico are to blame for a sluggish American economy and weak job creation.

Kwamba Trump amesema mikataba mibaya ya kibiashara na China na Mexico ndiyo sababu ya kuzorota uchumi wa Marekani na uzalishaji dhaifu wa fursa za ajira.

Ameahidi kufanya mikataba bora na nchi nyingine kulinda wafanyakazi wa Marekani na ametishia kupandisha kodi kwa bidhaa kutoka nje zinazoingizwa Marekani ili kuinua uzalishaji wa ndani.

Mikataba inayotajwa kuwanufaisha matajiri wakubwa na kuwanyima ajira na kipato Wamarekani wengi ni kama ule wa mapatano ya biashara huru nchi za Amerika Kaskazini au North America Free Trade Agreement (Nafta) uliotiwa saini enzi za Rais Bill Clinton wa Democrats.

Kwa mujibu wa wachunguzi wa habari za kibiashara na uchumi, miaka kumi ya Nafta Wamarekani 766,000 wamekosa kazi kwa sababu wamiliki wa viwanda wamefungua viwanda vyao katika nchi za Canada na Mexico badala ya Marekani.

Hillary Clinton anawania urais kupitia tiketi ya chama cha Democrats. Hillary anajulikana kama mtu wa ndani hivyo hata akichaguliwa atalinda masilahi ya wakubwa wa Marekani kama mume wake alivyofanya.

Mikataba mingine ambayo Trump anatishia kuivunja ni pamoja na makubaliano ya jumla kuhusu kodi na biashara yaani General Agreement on Tarrifs and Trade (GATT) wa mwaka 1947 ambao lengo lake ni kupunguza kodi za bidhaa kutoka nje na kukuza biashara duniani.

Ingawa GATT ilikuja kuzaa Shirika la Biashara la Kimataifa (WTO) mwaka 1994 baada ya mazunguko ya Urugway au Urugway Round Agreements, masharti ya GATT bado hufanya kazi chini ya muundo wa WTO.

Mkataba mwingine ambao Trump ametishia kuufutilia mbali ni ule wa Makubaliano ya kibiashara huru kati ya Marekani na mataifa ya Amerika ya Kusini au Central America Free Trade Agreement (CAFTA) uliowekwa saini wakati wa rais Bush mdogo (Bush Jr.) wa Republican mwaka 2005.

Vyama vya wafanyakazi vya Marekani yaani Trade Unions vinapinga mikataba yote hii ambayo inahamisha ajira kutoka Marekani kwenda mataifa ya nje kama vile Amerika ya Kati na Asia.

Hoja yao ni kwamba mikataba hiyo inatoa mwanya kwa wamiliki wa viwanda wa Marekani kuhamishia viwanda vyao huko kufuatia gharama ndogo za uzalishaji katika nhci hizo.

Bidhaa mbalimbali zinazouzwa Marekani hivi sasa hutengenezwa nje ya nchi hiyo na kwa kuwa kuna mikataba hiyo bidhaa hizo hatimaye huingizwa bila ushuru au kwa ushuru mdogo. Matokeo yake uchumi wa Marekani unaathirika.

Kauli za Trump kupandisha kodi za bidhaa kutoka nje na hata kufuta mikataba ya biashara huru kimsingi ni tangazo la vita baina yake na genge linalotawala dunia yaani Globalists.

By Idd Hamis

Picha: Mapokezi ya Lulu Michael Tanzania yawashtua Afrika Magharibi

$
0
0
Mapokezi ya Elizabeth ‘Lulu’ Michael wiki hii yameishtua Afrika Magharibi.

Lulu alishinda tuzo ya filamu bora ya Afrika Mashariki kwenye tuzo za Africa Magic Viewers Choice, AMVCA 2016 zilizotolewa Jumamosi nchini Nigeria. Muigizaji huyo alipokelewa kishujaa na mashabiki alipowasili Jumanne hii akitokea Lagos.

Mapokezi hayo yametuma ujumbe Nigeria ambako website maarufu za huko zimempa mashavu.

Blog namba moja wa burudani nchini humo, The Net, umeandika habari yenye kichwa kisemacho: Tanzanian actress gets heroic welcome after ‘winning big’ at AMVCA.

Blog nyingine iliyoandika ni The Nigerian Bulletin.

Kwa muda mrefu Tanzania kwa nchi za magharibi mwa Afrika imekuwa ikijulikana kwa muziki wa Bongo Flava zaidi na hivyo ni kitu cha kutia moyo kuona wasanii wa filamu wanaanza kupata majina huko pia.

Hiyo inamaanisha kuwa ushindi wa Lulu unaweza kumsaidia kujitanua zaidi nje ya Tanzania na huenda kuanza kufanya filamu na wasanii wa huko. Lulu ana kila sifa ya kuwa msanii wa kimataifa.

Nampongeza kwa mara nyingine kwa ushindi huo

Bongo5
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images