Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Afichua Vietnam ilivyopaa Kiuchumi Kwa Mbegu za Tanzania..

$
0
0
Rais Dk. John Magufuli amefichua siri kwamba mbegu za mpunga, korosho na samaki kutoka Tanzania ndivyo vilivyoipaisha Vietnam Kiuchumi.

Amesema mbegu hizo zilizochukuliwa miaka ya 1970, zimeifanya nchi hiyo kuwa kinara katika uzalishaji wa mazao hayo pamoja na ufugaji wa samaki.

Kutokana na maendeleo hayo, Rais Magufuli amewataka Watanzania kuiga Vietnam katika uzalishaji wa mpunga, korosho na ufugaji wa samaki, ili kuchangia uchumi wa nchi na pato la taifa.

Rais Dk. Magufuli aliyasema hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam alipofanya mazungumzo na Rais wa Vietnam, Truong Tan Sang, ambaye yuko nchini kwa ziara ya kikazi.

Alisema Watanzania wanatakiwa kuiga Vietnam yenye watu wanaokadiriwa kuwa milioni 91, ambao wamepiga hatua kubwa ya uzalishaji, hata uchumi wao umekua kwa asilimia 50.

Rais Magufuli aliongeza kuwa Vietnam imefanikiwa kupunguza umasikini kwa asilimia 50 na sasa imetoka katika uchumi wa chini hadi uchumi wa kati.

Alisema nchi hiyo ilichukua mbegu za korosho na mpunga nchini pamoja na samaki katika Ziwa Victoria na kuwapeleka kwao, lakini kwa sasa ni vinara wa uzalishaji wa mazao hayo, huku Tanzania ikiwa haijapiga hatua yoyote.

Alisema Tanzania ina mifugo milioni 22 na ni nchi ya pili kuwa na idadi kubwa ya mifugo Afrika, ya kwanza ikiwa Ethiopia lakini Tanzania haizalishi bidhaa ya ngozi kwa wingi.

Rais Magufuli alisema hiyo ni changamoto kubwa kwa Tanzania kuhakikisha inapiga hatua na kwamba ujio wa Rais Tan Sang utasaidia kuweka uhusiano karibu katika kibiashara, uwekezaji, mawasiliano na kilimo.

“Vietnam wanazalisha mpunga mara tatu kwa mwaka, lakini sisi tunazalisha mara moja. Walikuja kuchukua mbegu ya samaki wa maji baridi miaka ya nyuma, lakini sasa wanaongoza kwa ufugaji duniani,” alisema Dk. Magufuli.

Alisema wafanyabiashara wasione taabu kujifunza kwa Vietnam kwa kuwa imeobobea katika kilimo kwa sasa, japokuwa walijifunza kutoka Tanzania.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli alisema biashara yenye thamani ya dola za Marekani milioni 300 (Sh. bilioni 640) imefanyika kati ya Tanzania na Vietnam.

Kutokana na mafanikio hayo, serikali za nchi hizo zimekubaliana kuongeza biashara hiyo hadi kufikia dola bilioni moja (zaidi ya Sh. trilioni mbili).

Naye Rais Tan Sang alisema Tanzania ni moja ya nchi za mwanzo zilizokuwa na uhusiano wa kisiasa wa karibu na Vietnam miaka ya 1960.

Alisema Tanzania ni nchi iliyopiga hatua katika uchumi barani Afrika, hivyo watashirikiana katika biashara, uwekezaji, mawasiliano na kilimo.

Wakati huo huo, Rais Tan Sang alitembelea  ofisi ndogo za CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam  na kupokewa na Mwenyekiti wake, Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

“TANU ndiyo ilikuwa inaisaidia Vietnam katika kudai uhuru, tena nakumbuka vijana wa TANU wakiongozwa na Benjamini Mkapa (Rais mstaafu) walichangisha pesa kwa ajili ya kukisaidia chama hicho,” alisema Kikwete.

Kikwete alisema uhusiano wa Tanzania na Vietnam ulianza zamani wakati TANU na Chama cha Kikomonisti cha Vietnam viliposhirikiana katika mapambano ya kudai uhuru.

Vijana ni Wakati wa Kuwa Original

$
0
0
Inasemkana kwamba, “ni bora kushindwa katika kuwa Original kuliko kufanikiwa kwa kuiga.” Kwa bidhaa ya kondomu halisi na kongwe za kitanzania, Salama kondomu imeibuka na msemo wa “Kuwa Original” kwa ajili ya vijana. Kuwahamasisha kukubaliana na kusherehekea uhalisia wao!


Sasa, unaweza kusema “ni rahisi kutamka kuliko kutenda” ukizingatia jinsi vijana walivyo leo hii katika jamii. Kila mtu anataka kuwa mtu fulani na kila mmoja anataka mafanikio. Lakini siku zote kuna matumaini kwa wale ambao wanajitahidi/wanaopambana kuwa wajasiri na tofauti. Na kwa hilo akilini, Salama kondomu wamechukua hatua ya kuwatafuta vijana wajasiri na Original watakaosimulia hadithi zao.

Kuna wasanii wengi vijana siku hizi. Wengine hupenda kushuka mistari vyumbani mwao, baadhi katika studio gizani chini kwa chini Ubungo, bila kitu chochote bali midundo. Pia kuna baadhi yao wanapendelea kuwa katika mkumbo wa wapenzi na marafiki kuwasikiliza wakishuka misatari kama Faraji Junior, kijana wa Kitanzania akiwa ni rapa na mtunzi ambaye ni sehemu ya kundi hilo.


Pengine umeona baadhi ya hawa vijana wakiteleza na viatu vyenye matairi karibu na stendi ya mabasi ya Morocco BRT, wakifanya makeke na kuruka kwa kila mtindo. Miongoni mwao, jina lake ni Walter Mzengi, ambaye ametokea kuwa mwanzilishi na “skateboarder” wa “Tanzania Skate Society. Uhalisi wa kijana huyu Mtanzania umechochewa na ujuzi wake.

Skater 2

Umewahi kukutana na kijana mwandishi na shupavu akiwa umri wa miaka 22?! Basi kukutana na Zuhura ambaye ni kijana mshairi wa Kitanzania, mwenye kipaji cha hadithi simulizi na kueleza hisia zake kupitia sanaa ya mashairi na kunena maneno. Maneno yake yanaweza kukupa hisia kali na pia yakakupa uwazi na furaha.

Umewahi kuona kitu kawaida kilichotengenezwa kisanaa na ubunifu wa hali ya juu? Kukutana na Yvette Nkhoma, kijana wa Kitanzania mwenye kipaji cha kutengeneza urembo akitumia malighafi za kawaida. Kipaji chake kinaendeshwa na imani yake kwamba kila mwanamke ana uzuri katika dosari yake.


Umewahi kusikia ya sanaa ya ngoma ya kisasa? Kukutana na Alawi kijana wa Kitanzania ambaye ni dansa wa ngoma za kisasa mwenye uwezo wa kukonga nyoyo za umati kwa umahiri wa kipekee. Juhudi za kijana huyu zinaweza kufanana na zile za Michael Jackson katika Billie Jean na ujasiri kama Duma.



Chukua ujumbe huu; kuchukua nafasi, ishi maisha kwa uhuru lakini yenye afya, na daima kubaliana na uhalisi wako kuwa ndio njia ya furaha na mafanikio. Dumisha kaulimbiu, #KuwaOriginal #ChaguaOriginal

Alichosema Meneja wa Diamond Kuhusu Kufanya Kolabo na Kanye West Hiki Hapa

$
0
0
Siku chache baada ya msanii Diamond platnumz kupost picha kwenye instagram akiwa na kanye West ambaye ni rapper mashuhuri ulimwenguni watu wengi wamekuwa wakihisi pengine kuna kolabo inaweza kutokea hasa baada ya kusemekana wasanii hao walibadilishana namba.

akihojiwa na redio moja mmnoja wa mameneja wa Diamond,Sallam amesema kuwa huwezi kufanya kolabo na msanii kama kanye West kisa umekutana naye tu kwani kuna protokali nyingi zinabidi zifuatwe mpaka kukamilisha hilo na kuongeza kuwa kwa CV ya Diamond nafasi inaweza kupatikana.

“Unajua wenzetu hawafanyi kolabo kwa sababu umekutana naye,lazima utengeneze kuwa wewe ni nani,ukifanya naye kolabo itamsaidia nini yeye,nashukuru kwa upande wetu tuna Cv nyingi kwa hiyo nadhani itatusaidia kwa upande mwingine” alifunguka Sallam.

Jibu la Mrembo Naj Kuhusiana na Kutoka Kimapenzi na Baraka da Prince...Amkana na Kusema Haya

$
0
0
Msanii bongo fleva Naj amevunja ukimya na kusema kuwa yeye hana mahusiano yoyote ya kimapenzi na msanii Baraka da Prince.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuenea habari kuwa anatoka kimpenzi na msanii huyo na kusisitiza kuwa Baraka ni rafiki yake wa karibu na hakuna zaidi.

“Mimi baraka ni mchizi wangu wa karibu sana hakuna mapenzi kati yetu,ila siwezi kubadilisha mawazo ya watu kwa sababu wameshafikiria wanavyojua wao” alisema Naj na kuongeza toka aanze urafiki na baraka wana kama mwezi.

Wapiga Kura Bunda Mjini Wanaomtetea Wasira Dhidi ya Ester Bulaya Wakumbana na Pingamizi Jingine Mahakamani

$
0
0

Wapiga kura wa Bunda Mjini waliowasilisha maombi ya kuruhusiwa kukata rufaa nje ya muda, kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Ester Bulaya dhidi ya Steven Wasira, wamekumbana na kigingi kingine cha pingamizi.


Maombi hayo namba 25 ya mwaka 2016 yaliwasilishwa na wapiga kura Magambo Masato na wenzake watatu, wakiiomba mahakama hiyo iwaruhusu kukata rufaa nje ya muda baada ya kutupiliwa mbali na mahakama kuu.


Pingamizi hilo liliwasilishwa jana na wakili wa wajibu maombi wa pili na wa tatu, Paschal Malulu akiiomba mahakama kutupilia mbali maombi hayo kwa kuwa kiapo kilichoambatanishwa ni batili kwa kuwa aliyeapa ni tofauti na aliyethibitisha.


“Haya makosa yaliyofanyika ni makubwa mno, kiasi cha kutokurekebishika, kwa sababu kiapo kimethibitishwa na wakili Constatine Mutalemwa huku aliyeapa ni wakili James Kahangwa,” alidai Malulu.


Alidai kiapo hicho kimekosa nguvu kisheria kwa mujibu wa sheria Na. 19 (1) (2), ni lazima kiwe na mambo ambayo mtu anaweza kuyathibitisha au kuyasimamia, hivyo hii sheria imekiukwa, kwa lugha nyingine kiapo kimekosa uthibitisho.


Malulu alidai kuwa kuna sheria inayosimamia kiapo wala siyo Katiba kwa ujumla wake, kama alivyoitaja Mutalemwa.


Jaji anayesikiliza shauri hilo, Rose Ebrahim aliahirisha shauri hilo hadi Machi 14, mwaka huu atakapolitolea maamuzi pingamizi hilo.

Mbunge wa Ubongo Saed Kubenea Akamatwa na Jeshi la Polisi Leo Asubuhi

$
0
0
MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea amekamatwa na Jeshi la Polisi leo asubuhi wakati akiwa katika Mahakama ya Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, anaandika Faki Sosi.

Kubenea amekamatwa na polisi akituhumiwa kushiriki kumpiga Terresia Mmbando, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mmbando alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliofanyika wiki mbili zilizopita na baadaye kuahirishwa hatua ambayo iliibua malumbano.

Katika mtandao wa mawasiliano wa mwanahalisi, Kubenea ameandika “leo nikiwa mahakamani Kisutu nimekamatwa na polisi. Natuhumiwa kumpiga Katibu Tawala, nipo polisi kati.”

Kubenea ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers alikwenda leo mahakamani kuendelea na kesi yake inayohusu kumtukana Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Kesi hiyo ilifunguliwa tarehe 15 Desemba mwaka jana baada ya wawili hao kukutana kwenye Kiwanda cha Nguo cha TOOKU kilichopo Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Katika tuhuma za kupiga Mmbando, waliokamatwa katika hatua ya kwanza ni Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Mwita Waitara, Mbunge wa Ukonga na madiwani wawili ambao kwa sasa wapo nje kwa dhamana.

Baada ya kupata dhamana Mdee alisema “Watake wasitake wataachia, hapa ni Ukawa tu. Yote haya yana mwisho lakini wajue kuwa namba ‘zinatufeva’ na si vinginevyo.”

Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar s Salaam ndio chanzo cha kukamatwa kwa Kubenea na wengine waliotangulia ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimekuwa vikisigana.

Ukawa wanalalamika kuminywa na Halmashauri ya Jiji kwa madai ya kushirikiana na CCM. Ukawa wameeleza kuwa zinafanyika hujuma ili CCM ishinde Umeya wa Jiji.

Jumla ya wajumbe wa mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji ni 161. Kwa upande wa Kinondoni kuna wajumbe 58 ambapo CCM wapo 20 na ukawa 38.

Temeke jumla ya wajumbe 49, CCM wapo 31 na ukawa 18 na Ilala jumla ya wajumbe 54 huku CCM wakiwa 23 ukawa 31.

Mwanamuziki Diamond Platnumz Aonyesha Ulimwengu Pesa Aliyozovuna Kwenye Show Dubai.....

$
0
0

Diamond ameamua kuwaonesha mashabiki wake madolari aliyoyachuma Dubai wiki hii. Ni mengi!!Staa huyo amepost burungutu sita
zilizoshiba za dola mia mia zikiwa juu ya gitaa.

Sasa ni Rasmi..Rich Mavoko Asaini Katika Label ya ‘ WCB ‘ ya Diamond

$
0
0
Mmoja kati ya member wa ‘label’ ya WCB, Harmonize amethibitisha kuwa Rich Mavoko ni mmoja kati ya wasanii wa label hiyo.

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Jumatano hii, Harmonize alisema label ya WCB ina wasanii watatu yeye mwenyewe , Raymond aliyekuwa Tip Top Connection pamoja na Rich Mavoko.

“Unajua mwanzo zilikuwa ni tetesi lakini naweza kusema ‘its official’ sasa Rich Mavoko yupo chini ya WCB,” alisema Harmonize

Aliongoza, “Kusema kuwa Rich Mavoko amenyoosha mikono kwa Diamond si vizuri kwani watu wanaweza kupata picha tofauti maana si unajua watu wanaweza kupokea jambo kwa maana na ikaleta picha mbaya wakati ni jambo la kawaida,”



Je Lulu Michael na Mama Kanumba Wanaugomvi? Lulu Adai 'Ningemkuta Mama Kanumba Uwanja wa Ndege Nisingemfukuza'

$
0
0
Msanii wa filamu Tanzania, Elizabeth Michael alimaarufu kama 'Lulu' amefunguka na kusema kuwa yeye hafahamu sababu zilizofanya mama mzazi wa Kanumba asitokee kwenye mapokezi yake baada ya kushinda tuzo nchini Nigeria.

Mtangazaji wa kipindi cha eNEWS alihoji ni sababu zipi zimepelekea Mama Kanumba kushindwa kutokea kwenye mapokezi yake ili hali Mama huyo alishiriki kwenye movie hiyo ambayo imempa ushindi Lulu Michael, ndipo hapo Lulu alipodai yeye hatambui sababu na kusema yeye alikuwa Nigeria na watu wote Tanzania walipata taarifa kupitia vyombo vya habari na ndio maana waliweza fika uwanja wa ndege kumpokea hivyo alidai hata kama angemkuta Mama Kanumba hapo ( Uwanja wa ndege) asingeweza kumfukuza.

Kauli hii ya Lulu Michael ni wazi inaonyesha huenda labda hawako sawa na mama mzazi wa Kanumba.

Katika hatua nyingine Baba Mzazi wa msanii huyo alifunguka ya moyoni na kusema kwamba yeye toka awali hakupenda mwanae ajihusishe na masuala ya filamu yeye alitaka mwanae asome shule, lakini anadai kutokana na mafanikio ambayo mwanae ameyapata anaamini kuwa kweli alikuwa amepangiwa kufanikiwa kupitia filamu

Tazama Show Nzima ya Navy Kenzo Walivyoipeleka Kamatia Chini Mjini Dodoma..Mtwara Week End Hii Kaeni Tayari

$
0
0
Kamatia Chini Lights Up Tour ya kundi la muziki wa bongofleva Navy Kenzo iliangukia Dodoma weekend iliyopita ambapo Aika na Nahreel pia walipata time ya kumleta Jux kwenye stage kwa muda mfupi… hii video hapa chini itakuonyesha zaidi…

Source:Millard Ayo

Mwalimu Adaiwa Kumtia na Kumtoa Mimba Mwanafunzi.....

$
0
0
Mwalimu mmoja wa Shule Sekondari Nyugwa wilayani hapa Mkoa wa Geita anadaiwa kutoroka katika kituo chake cha kazi kwa tuhuma za kumpa mimba mwanafunzi wake wa kidato cha tatu.

Inadaiwa baada ya mwanafunzi huyo (jina linahifadhiwa) kubainika kuwa na ujauzito, mwalimu huyo aliamua kushirikiana na baadhi ya watumishi wa Kituo cha Afya cha Kharumwa kutoa. Inadaiwa Machi 3, ndiyo mimba hiyo ilitolewa kwa ushirikiano wa daktari na muuguzi waliokuwa zamu.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa shule hiyo, Henrick Jembe alidai Februari 18, mwanafunzi huyo aliomba ruhusa kwenda hospitali akidai anaumwa.

“Ingawa sikuwapo shuleni siku hiyo, lakini kumbukumbu zinaonyesha mwanafunzi huyu alipewa ruhusu baada ya kukamilisha utaratibu ikiwamo kuandikiwa daftari la kumuwezesha kupatiwa matibabu,” alidai mkuu huyo wa shule na kuongeza:

“Alisindikizwa na wanafunzi wenzake wawili, mmoja wa kiume na mwingine wa kike.”

Alidai waliporejea shuleni, mwanafunzi huyo alisema baada ya vipimo alikutwa na vimelea vya malaria, hivyo akaruhusiwa aende nyumbani kupumzika.

“Lakini baada ya siku mbili nilipokea wito kutoka polisi nikitakiwa kufika na mwalimu anayetuhumiwa ambaye siku hiyo alikuwa na kazi ya kushughulikia chakula cha wanafunzi, ikabidi niende mwenyewe na kukuta maelezo kuwa mwanafunzi wangu ana ujauzito na anayetuhumiwa ni huyo mwalimu,” alidai Jembe na kuongeza:

“Nadhani alipopata taarifa kuwa anatuhuma hizo aliamua kukimbia na mpaka sasa hajulikani alipo.”

Katibu Mkuu Idara ya Utumishi wa Walimu wilayani hapa, Aron Andrew alisema baada ya kumhoji mwanafunzi huyo alibaini kuwa alianza uhusiano wa mapenzi na mwalimu wake tangu mwaka jana.

“Alisema baada ya kutolewa mimba, mwalimu wake alimsafirisha hadi jijini Mwanza kwa mtu aliyemtambulisha kwake kuwa ni dada wa mtuhumiwa ili ajiuguze huku akiendelea kunywa dawa alizoandikiwa hospitali,”alisema

Hata hivyo, alisema hawawezi kuchukua hatua yoyote dhidi ya mwalimu huyo kwa sasa kwa sababu wanasubiri taarifa kutoka kwa mwajili wa mwalimu huyo ambaye ni mkurugenzi.

Alisema mwajiri huyo akitoa taarifa hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi mwalimu huyo kwa kuwa amekiuka sheria na kanuni za utumishi wa umma.

Kaimu Mkurugenziwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Venance Ngeleuya alisema ofisi yake pia haijapokea taarifa za tuhuma hizo na kusisitiza watafuatilia.

Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Dk Lutale Josephat alisema ofisi yake itachukuwa hatua kama itathibitika kuwa baadhi ya watumishi wa kituo cha afya cha Kharumwa walishiriki kumtoa mimba mwanafunzi huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Ibrahimu Marwa alisema amewaagiza polisi wilayani hapa kumsaka na kumtia mbaroni mwalimu huyo ili afikishwe mahakamani kujibu mashtaka ya tuhuma zinazomkabili.    


Atupwa Jela Miaka 7 kwa Kumkata Mkewe Sehemu za Siri Ili Apate Mali

$
0
0
Mkazi wa Kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora, Mashaka Maziku (60) amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa kosa la kumkata sehemu za siri mkewe kwa imani za kishirikina ili apate mali.

Hakimu Joctan Rushwela alisema jana kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora imeridhishwa na ushahidi uliotolewa upande wa mashtaka.

Hakimu Rushwela alisema anamhukumu mshtakiwa huyo kwenda jela ili iwe fundisho kwa wengine wanaokuwa na tamaa ya kujipatia mali kwa njia za kishirikina.

Awali wakili wa Serikali, Idd Mgeni alidai kuwa mshtakiwa huyo na mganga wa jadi, walitenda kosa hilo kati ya Oktoba 29 na Novemba 2, 2014 katika eneo la Kazaroho Kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora.

Wakati wa tukio hilo, ilidaiwa kuwa Maziku aliambiwa na mganga huyo ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Kahele Paul kwamba akipeleka sehemu za siri za mkewe atapata Sh5milioni.

Alidai baada ya kupewa ushauri huo, alimchukua mkewe na kwenda kumnywesha pombe ili aweze kutimiza ukatili huo.

Alidai baada ya kunywa pombe nyingi, alichukua kisu na kumkata sehemu za siri mkewe na kuzihifadhi kwenye mfuko wa suruali yake na kutoweka.

Alidai kwa mujibu wa mashahidi wanne, mwanamke huyo alikuwa akipiga kelele kutokana na maumivu makali aliyopata huku akivuja damu nyingi.

Menaja wa Diamond Akosoa Kauli ya Harmonize Kuhusu Rich Mavoko Kusign Mkataba wa Kuwa Chini ya Diamond...Asema Haya

$
0
0
Rich Mavoko bado hajasaini na Wasafi Records, kwa mujibu wa meneja wa Diamond, Sallam.

Awali msanii wa WCB, Harmonize alidai kwenye interview kuwa hitmaker huyo wa Roho Yangu ameshainguka saini na kujiunga kwenye himaya hiyo.

Sallam amelazimika kuweka mambo sawa kupitia Twitter.
Hajakuwa signed Ila Harmonize ameona kuwa Rich alikuwa na mazungumzo na Viongozi akajua ni tayari.

Watu Watano Wafa Kwa Kufunikwa na Kifusi Wakati Wakijaribu Kuchimba Mawe Waliyodhania ni Dhahabu

$
0
0
Watu watano wamepoteza  maisha na wengine watatu kujeruhiwa vibaya kwa kuvunjika viungo vyao baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba mawe yanayodhaniwa kuwa ni dhahabu.

Tukio hilo limetokea jana saa 9:00 Alasiri, katika kata ya  Mgusu Wilayani Geita  ambapo watu  hao waliangukiwa na ukuta wa udongo waliokuwa wakiuchimba.

Wakizunguza na channel Ten iliyofika katika kata hiyo baadhi ya wachimbaji waliokutwa katika eneo hilo wakaeleza hali ilivyokuwa.

Pamoja na tukio hilo la kusikitisha wachimbaji hao wakatoa kilio chao kwa Serikali kuhusu maeneo ya kuchimba yaliyo salama ikiwa ni pamoja na kuwapa zana za kuchimbia na uokoaji.

Katibu tawala ya wilaya ya Geita Gaspar Kanyaiita aliyetembelea eneo hilo ameagiza Ofisi ya Madini kuwakamata wachimbaji wote wanaokiuka kanuni huku kaimu Afisa Madini Mkoa wa Geita akisema eneo hilo limefungwa tangu jana mpaka itapotangazwa utaratibu mwingine.

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe Keshawasili Jijini Mwanza Kwa Ajili ya Kikao cha Kumpata Mrithi wa Dr. Slaa

$
0
0
Mwenyekiti wa chama cha Demokrsaia na Maendeleo (CHADEMA) akiwasili uwanja wa ndege jijini Mwanza.kwaajili ya mkutano wa  baraza kuu CHADEMA  ambao utamtangaza  Katibu  mkuu wa chama hicho kuchukua mikoba ya Dr. Slaa

Rais Magufuli Afanya Ziara Ya Kustukiza Benki Kuu (BOT) Jijini Dar Es Salaam Leo..Atoa Maagizo Haya...

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara Benki Kuu ya Tanzania (BOT), ambapo pamoja na mambo mengine ameiagiza Benki hiyo kusitisha mara moja ulipaji wa malimbikizo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara Benki Kuu ya Tanzania (BOT), ambapo pamoja na mambo mengine ameiagiza Benki hiyo kusitisha mara moja ulipaji wa malimbikizo ya malipo ambayo tayari yalishaidhinishwa (Ex-Checker) na badala yake yarejeshwe Wizara ya fedha na Mipango kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki.

Rais Magufuli wakati Benki Kuu ya Tanzania ilikuwa katika mchakato wa kufanya malipo ya shilingi Bilioni 925.6, ambazo Wizara ya Fedha ilitoa idhini ya kufanyika malipo.

Akizungumza na watendaji wakuu wa Benki Kuu ya Tanzania waliojumuisha Gavana, Naibu Magavana, Wakurugenzi na Mameneja, Rais Magufuli ametaka Wizara ya Fedha ifanye upya uhakiki wa malipo hayo, ili kubaini kama walengwa walioidhinishwa kulipwa wanastahili kulipwa ama vinginevyo.

Aidha, Dkt. Magufuli ameagiza Kitengo cha madeni ya nje ambacho awali kilikuwa chini ya Benki Kuu na baadaye kikahamishiwa Wizara ya Fedha, kirejeshwe Benki Kuu mara moja ili kuimarisha udhibiti wa ukopaji na ulipaji wa madeni.

Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Beno Ndulu kupitia upya orodha ya wafanyakazi wa Benki hiyo, na kuwaondoa mara moja wale wote ambao hawana ulazima wa kuwa wafanyakazi katika benki hiyo.

Rich Mavoko Akana Kusign Mkataba wa Kuwa Chini ya Diamond..Atoa Ufafanuzi Hapa nini Kinaendelea Kwa Sasa

$
0
0
Baada ya msanii wa muziki kutoka ‘label’ ya WCB, Harmonize kudai Rich Mavoko tayari ni member wa label hiyo, Rich Mavoko aibuka na kuzungumzia swala hiyo.

Rich amedai bado yeye ni msanii huru.

“Hizi stori nimezisikia kama Harmonize alivyosema, hii issue imetokea kwa sababu aliniona na Salam (Meneja na Diamond) na tulikuwa tunaongea issue nyingine, atakuwa hajaelewa nini kinaendelea na siwezi kumlaumu sana. Lakini sijui kusema nipo official hapana bado, kama ikiwa official kwanini niwafiche?, haya ni maisha ya mtu na hii ni biashara,” alisema Rich Mavoko.

Aliongeza, “Tunapokuja kwenye swala kama hili ni lazima niangalie kama kuna faida ua hasara. Kwa hiyo kitu kikubwa ndio hicho Harmonize aliniona na Salam na simlaumu kwa sababu hajui chochote, kama itakuwa official lazima nitasema kila mtu ajue,”

Pia Mavoko ameeleza nini kinamchelewesha kusaini kwenye label hiyo.

“Hili swala tatizo linazungumza sana mitaani, lakini mimi binafsi nisema vitu vitakapo kuwa tayari mimi nitaweka wazi na kama ikishindikana pia nitasema, lakini kwa sasa kuna mambo yanaendelea,” alisema Rich.

VIDEO: Rais Magufuli Akionyesha Majina ya Wafanyakazi Hewa wa Bank Kuu Tanzania

$
0
0
Rais Magufuli akiwaonyesha wakuu wa BOT majina ya wafanyakati hewa ambao uongozi umekili kufanya makosa na kuahidi watarekebisha mara moja kwa kuyaondoa kwenye vitabu vya BOT.

Rais amewaamuru wayaondoe mara moja ili pesa zitumike kulipa wafanyakazi wanaostahili kulipa kama wafanyakazi wa BOT.

Rais amesitikishwa na uzembe na pia wizi unaofanyika BOT kwa njia za udanganyifu.


Angalizo:
Kama na Bank of Tanzania inaweza kufanya madudu kama haya, sina budi kukubaliana na maneno ya Rais Magufuli wakati akiongea na wananchi wa Arusha aliposema,


‘’Tanzania hii, ilikuwa shamba la bibi, watu walikuwa wanafanya ya ovyo. Ninaposema ya ovyo ni ya ovyo kweli, mimi nipo serikalini, lakini nimekuwa waziri kwa miaka 20, ninayajua. Ninaposema ya ovyo, ndugu zangu naomba mniamini.
“Mambo ya mateso kwa wananchi hayana chama. Ukikosa madawa hospitalini hata ukiwa Chadema utakosa tu, hata ukiwa CCM unaimba kila siku CCM oyeee, utakosa tu madawa. Kwa hiyo hatua tunazotaka kuzichukua ni kwa wananchi wote bila kujali itikadi zao.
“Tumefika katika wakati huu, ni lazima patokee mmoja wa kuyafanya. Na ndiyo maana siku zote nimekuwa nikiwaeleza. Ndugu zangu mimi nimeamua kuwa sadaka ya Watanzania. Kazi hii ni ngumu, ni ya ajabu. Kila mmoja anajitahidi haya tunayoyafanya tusiyafanye, lakini nawashukurui mnaendelea kuniombea. Ndiyo maana niko hapa. Endeleeni kutuombea lengo letu ni la kuwasaidia ninyi. Ni lazima tufanye’’.

Nay wa Mitego Afunguka Sababu za Kutowataja Diamond na Ali Kiba Kwenye Ngoma Zake

$
0
0
‘’Sikutaka kulizungumzia hili lakini nilijua watu watajaji,hata kwenye ‘comments’ watu wengi wanasema kwanini sijamuimba rafiki yangu Diamond na ana skendo nyingi’’ Alisema Nay Wa Mitego.

‘’Unajua sitaki kufanya kitu ambacho kila mtu tayari anacho kichwani mwake ili ni jawabu tosha kwa watu ambao wanajaji hilo kila mtu angekuwa anategemea ningemdisi Ali Kiba au Diamond sikutaka na kama ningeamua kuwazungumzia hawa watu mimi nazungumzia vitu ambacho kila mtu angekuwa nacho kwenye kichwa chake kama aliwahi kukifikiria lakini hawezi kuhisi kama kuna mtu kukizungumzia ina maana kila mtu alikuwa akitegemea anataka kuona nimemzungumzia Diamond au Ali Kiba’’Aliongeza Nay Wa Mitego.
’Sijafanya hivyo kwa makusudi tu ijapokuwa kuna vitu vya kuzungumza juu yao lakini kulikuwa hakuna umuhimu sana kuna watu walikuwa na vitu muhimu sana ndio maana hii imeenda kiasi hicho’’Alimaliza Nay

Mwanamuziki Diamond na Mtoto wake Tiffah Wapima DNA Sauzi

$
0
0
Hii ni EXCLUSIVE stori! Kufuatia kelele kibao kutoka kwa wadau mbalimbali kwamba mtoto wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, yaani Latifah ‘Tiffah’ aliyemzaa na Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ si wa nyota huyo, hatimaye, jamaa ameamua kupima vinasaba ‘DNA’ (DeoxyriboNucleic Acid).

ISHU ILIKUWA AFRIKA KUSINI
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, Diamond aliamua kutekeleza mpango huo nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ ambako aliamini hakuna ‘macho mengi’ ya watu, hususan mapaparazi.

SIKIA HII
“Jamani mimi nataka niwape stori ambayo ni ya uhakika. Hivi mnajua kwamba Diamond aliamua kwenda Sauzi kupima DNA yake na mtoto wake Tiffah?
“Kutokana na manenomaneno ya watu, ilifika mahali alichoka, akawa njia panda. Hivyo ili kuondoa figisufigisu, akamwambia Zari waende wakampime DNA mtoto na yeye. Ni kabla hajaenda Marekani.”

MAJIBU HAYA HAPA
Chanzo hicho kikasema: “Majibu ya DNA yamesema, Nasibu Abdul ni biological father (baba wa damu) wa mtoto Tiffah. Ilibidi jamaa amwage chozi maana alifikiria mengi, watu wamesema sana kuhusu yeye na Tiffah, kwamba si mwanaye, mara ni mtoto wa Ivan (Ssemwanga, mtalaka wa Zari), mara ni mtoto wa pedeshee mmoja wa Bongo. Yaani mengimengi yalisemwa.”

Chanzo: GPL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images