Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Dk.Hamis Kigwangalla Afunguka na Kusema "Poleni CHADEMA Kwa Kumchagua Dkt. Mashinji Kuwa Katibu Mkuu"

0
0
Kupitia Account yake ya Facebook Dk Hamisi Kigwangalla anakiri wazi kuwa Dkt. Mashinji ni msomi mzuri na mwanasiasa mzuri ingawa anadai hana uhakika kama alimaliza masomo ya ubingwa.

"Ndg., Dkt. Mashinji is a friend, brother and colleague. Hakuwahi kutuokoa mimi na Dkt. Ulimboka, na hakuwahi kuongoza mgomo, sema alishiriki mgomo ulioongozwa na mimi na Dkt. Ulimboka. Kiukweli, ni mwanasiasa mzuri, msemaji, msomi mzuri (tumesoma naye MBA chuo kimoja), sina hakika kama alimaliza masomo ya Ubingwa maana alinyanyaswa na Supervisor wake, akasusa akaamua kujiiunga masomo ya MBA na sina hakika sana kuhusu 'msimamo usiotetereka'. Maana baada ya vitisho vya 2005, aliyumba sana na tulimtenga na ku-aVoiD kumualika vikao vya CC ya mgomo. Hivyo, kama kigeZo kilikuwa ni hii historia, pole kwa CHADEMA."Ameandika Dk Kigwangalla

Baada ya Kuteuliwa Kuwa Mkuu wa Mkoa ANNA Kilango Malechela Ataja Sababu Zilizofanya Magufuli Amchague

0
0

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Same Mashariki ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa mteule wa Shinyanga, Anna Kilango Malechela, amesema jitihada zake na utendaji katika kuihudumia jamii ndio sababu kuu iliyomfanya Rais Magufuli kumpa nafasi ya kuuongoza mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza kupitia Kipindi cha Sun Rise cha Times Fm, Malechela amedai hata ‘anguko’ lake katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, aliangushwa na watu wenye sababu binafsi na si kukataliwa na Wananchi.

“Mungu ni mwema, sikuwa na hili wala lile, nimekaa Bungeni miaka 15 na Mh Rais akiwa kama Mbunge, kwahiyo alikuwa anaona utendaji wangu, kupambana na kero za wananchi na jinsi nilivyo na jitihada.

“Unajua wanaosema tuna bebwa tulianguka kwenye uchaguzi, watazame kwa utandi wengine tuliangushwa, naahidi kuzikabili na kauli mbiu ya kazi tu kuitumikia Shinyanga” Alisema Mama Anna Kilango.

Zitto Kabwe Ataka Benk Ya Standard Ichunguzwe Upya Kwa Rushwa......Anakuomba Mtanzaia Uweke saini yako Kwenye Petition Hii ili Uchunguzi Ufanyike

0
0
Mbunge  wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, amesema Benki ya Standard inapaswa kuchunguzwa kwa rushwa kuhusu suala la hati fungani ya Dola za Marekani milioni 600.

Amesema kwa sasa deni la Taifa limepanda na kufikia dola bilioni 15  sawa na Sh trilioni 30, ambapo kutokana na ukubwa wa deni hilo, Tanzania hulipa huduma ya deni la Taifa takribani Sh trilioni 2.2 kila mwaka.

Alisema licha ya hali hiyo bajeti ya kuhudumia deni la Taifa ni kubwa zaidi kuliko bajeti ya wizara yoyote nchini.

Alisema kutokana na suala hilo katika madeni hayo yapo ambayo yamepatikana kwa rushwa na mengine yamechukuliwa kwa matumizi ya anasa.

“Kitaalamu madeni haya yanaitwa ‘Odious debts’. Moja ya Deni la hovyo ni la dola za Marekani milioni 600 ambalo Tanzania ilikopa kutoka Benki ya Standard ya Uingereza kupitia hati fungani.

“Taasisi ya SFO ya Uingereza inayoshughulika na rushwa kubwa imeonyesha kuwa mkopo huu ulipatikana kwa rushwa. Taasisi ya Corruption Watch ya Uingereza imeonyesha kuwa Tanzania imepata hasara ya takribani dola milioni 80 sawa na bilioni 160 kwa kuchukua mkopo huu.

“… hata hivyo uchunguzi wa SFO haukuhusisha maofisa wa juu wa Standard Benki makao makuu na hivyo kufunika kombe mwanaharamu apite.

“Iwapo uchunguzi ungegundua kuwa Standard Benki walihusika moja kwa moja na hongo hii, Tanzania ingefutiwa deni lote na kuokoa fedha nyingi sana ambazo zingewekezwa kwenye sekta za elimu, afya na maji,” alisema Zitto.

Mbunge huyo wa Kigoma Mjini, alisema wanaitaka Benki ya Standard ya Uingereza ichunguzwe upya na SFO kuhusu tuhuma za rushwa ili kupata biashara Tanzania ya hati fungani pamoja na kujua ukweli wa kile alichodai ufisadi huo.

Kutokana na hali hiyo alisema wameandaa maombi kwa kuitaka FSO ya Uingereza ifungue upya uchunguzi kwa kuzingatia ushahidi mpya kuwa mabosi wa Benki ya Standard ya Uingereza walihusika na mipango ya kutoa hongo ili kupata biashara Tanzania.

Alisema ikibainika mabosi hao walishiriki maana yake Tanzania itafutiwa deni lote kwa sababu benki hiyo itawajibika kurudisha fedha za watu kwani Hati fungani itaonekana ni batili.

Zitto  alisema hivi sasa Tanzania inaanza kulipa deni hilo kuanzia Aprili, mwaka huu na kama wasipozuia tunazuia kwa maombi haya kwa FSO.

Alisema iwapo deni hilo litalipwa juhudi za Rais Dk. John Magufuli, kupata mapato zitaathiriwa na sekta nyeti kama elimu, afya na maji zitakosa bajeti ya kutosha.

Alisema kutokana na hali hiyo aliwaomba Watanzania kote duniani kuitaka SFO ifungue uchunguzi kwa kuzingatia ushahidi mpya dhidi ya Benki ya Standard ambayo sasa inaitwa ICBC plc

Petition hii imeletwa kwenu na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi ughaibuni. 
 
Bofya hapo chini kuweka saini yako ili  kuwashawishi SFO wafanye uchunguzi upya. Tetea Tanzania yako. Uzalendo wako ndio uhai wa Tanzania yako. 

<<<BOFYA  HAPA>> 
Bofya  hapo  juu  kuweka saini yako

Nyumba ya Mzee Katwila Yamuua Bibi Yake Mwanamuziki Q Chief

0
0
Mwanamuziki wa Bongo fleva, Q Chief, yupo kwenye majonzi baada ya kumpoteza Bibi yake aliye fariki kwa mstuko wa moyo baada ya misuko suko ya madeni na kutolewa kwenye nyumba baba mzazi wa msanii huyo Mzee Shaaban Katwila.

E-newz imekutana na mmiliki wa Q S Entertainment inayomsimamia Q chief ijumaa iliyopita katika onesho la band ya QS Band pale Escape One. QS J. Mhonda na kutufahamisha makubwa yaliyomkuta Bibi yake Q chief upande wa mama aliposikia taarifa ya nyumba kuchukuliwa na mtu anayedai pesa alizomkopesha mzee Shaaban Katwila. Taarifa iliyopelekea bibi kupata presha na kuiaga dunia na mpaka kufikia siku ya Ijumaa Bibi yake na Q Chief akapumzishwa katika nyumba yake ya milele.

Mbali na yote hayo kutokea Q Chief alionesha ukakamavu na kupanda kwenye stage na kuendelea kutumbuiza siku ya ijumaa pale ESCAPE ONE.

Mwigizaji Lulu Michael Agonganisha Mabwana Wawili Nigeria...Stori Nzima Nimekuwekea Hapa

0
0
Ustaa una mambo! Pamoja na kuchukua tuzo na heshima kedekede, Ijumaa Wikienda limetonywa upande wa pili wa ‘shilingi’ ambapo inadaiwa kuwa, Mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ aligonganisha mabwana wawili katika hafla ya utoaji wa Tuzo za African Magic Viewers Choice (AMVCA) ililofanyika hivi karibuni nchini Nigeria.

WALISHINDA WABONGO WAWILI
Lulu na mwigizaji Single Mtambalike ‘Richie Richie’ walikuwa ni Watanzania pekee waliokwenda nchini Nigeria na kutunukiwa tuzo hizo ambapo Lulu alishinda kupitia Kipengele cha Filamu Bora ya Afrika Mashariki huku Richie akiibuka kifua mbele kwa ushindi wa Filamu Bora ya Kiswahili Afrika Mashariki (Kitendawili).
kiba na lulu tuzoLulu na staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba.

CHANZO CHAVUJISHA MCHAPO
Chanzo makini kilichoshuhudia tukio hilo, kilipenyeza habari kuwa, Lulu, pasipo kujua, alijikuta amegonganisha mabwana wawili, staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba na bosi mmoja wa redio yenye jina kubwa Bongo (jina tunalihifadhi kwa sasa).
“Si unajua Kiba naye alikuwa bado ana matumaini na Lulu maana wametoka mbali. Kiba alijua kwamba kwa kuwa alialikwa kutumbuiza, basi ingekuwa rahisi kuwa ‘klozi’ na Lulu baada ya kupewa taarifa kwamba Lulu naye anakwenda.
“Akaibuka mazima pasipo kujua kuna mtu mwingine ambaye ndiye anasimamia mpango mzima wa Lulu kwa sasa. Kuanzia mavazi hadi malazi, achilia mbali mazagazaga ya kila siku.
luluLulu alivcyopokelewa Tanzania.

BOSI WA REDIO FULL KUSIFIWA
“Bosi wa redio si unajua tena yeye nd’o mwenyewe? Full kujiamini. Hakuwazia kabisa kama kuna mtu mwingine anaweza kuwa na nafasi kubwa kwa Lulu kama ilivyo yeye. Si unajua tena kasimamia shoo nyingi tu hadi ya kuhamasisha watu kumpigia kura Lulu?

KIBA AAMBULIA HOTELINI
“Kiba alipata bahati ya kukutana na Lulu kwenye Hoteli ya Eko ilipofanyika hafla ya utoaji wa tuzo hizo wakapiga picha ya pamoja lakini baada ya kumalizika kwa sherehe hiyo, mtoto mzuri alikamatiwa na the big boss wa redio, wakaenda zao kulala,” kilisema chanzo hicho.

BOSI WA REDIO NI NANI?
Katika kumwaga ubuyu, chanzo hicho kilizidi kumdadavua bosi huyo wa redio ambaye ndiye aliyeshikilia ‘mpini’ siku hiyo kwani Lulu hakuweza kupata muda hata kiduchu wa kukutana na Kiba tofauti na pale ukumbini.

“Kwani unafikiri bosi mwenyewe ni nani basi, si ni (anamtaja jina) ambaye kama mnakumbuka vizuri alikuwa mchumba wa yule Video Queen wa Bongo, Hamisa Mobeto, Lulu akampora. Bosi kubwa hakumpa nafasi Lulu hata kidogo ya kutembea,” kilisema chanzo hicho.

KIBA AREJEA BONGO KIVYAKE
Vyanzo mbalimbali vya habari vilitonya kuwa, Kiba alirejea Bongo kivyake huku Lulu akiwasili jijini Dar akiwa sambamba na watu wake wa karibu akiwemo bosi huyo wa redio.

BOSI ANASEMAJE?
Baada ya ya jitihada za kumtafuta Kiba kugonga mwamba, gazeti hili lilimvutia waya bosi huyo wa redio ili kutaka kumsikia anazungumziaje kitendo cha yeye kuonekana kule huku pia mwanaume aliyetajwa kutembea na Lulu zamani (Kiba) akiwepo, bosi huyo hakutaka kuzungumzia chochote.
“No comment.”

LULU ASAKWA, KIMYA!
Gazeti hili lilifanya jitihada za kumsaka Lulu ili kuzungumzia suala hilo lakini hakupokea simu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno, bado hakujibu chochote.

SHOSTI WAKE AKIRI
Hata hivyo, rafiki mmoja wa msanii huyo aliyeomba hifadhi ya jina, alikiri Lulu kuwa na bosi huyo kama mpenzi wake wa sasa lakini akampa pole Kiba.
“Huyo bosi ndiyo mtu wake, alikuwa na haki ya kwenda na Lulu kule na kuwa na uhuru wa kila kitu lakini Kiba ni rafiki na mdau mkubwa wa sanaa alienda kufanya shoo,” alisema shosti huyo.

Chanzo:Global Publishers

Jack Cliff Kuhojiwa Gerezani Kuhusu Vigogo wa Unga Waliokuwa Wakimtuma Kabla Hajakamatwa....

0
0
Kila kona kimenuka! Ule mkakati wa Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ wa kuwasaka na kuwatumbua vigogo wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya ‘unga’ ili kumaliza mtandao huo, unadaiwa kumfikia Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ ambaye ni modo wa Kibongo na Watanzania wanaotumikia kifungo nchini China kwa kosa la kukamatwa na unga.

Habari za ndani kutoka kikosi maalum cha Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maofisa wa Uhamiaji zilidai kwamba, ukiacha nusanusa ya ndani ya Bongo, kikosi hicho kwa sasa kimeungana na kile cha Polisi wa Kimataifa (Interpol) katika kuwahoji Watanzania hao ili kuwakamata waliowatuma.
“Pamoja na kwamba wengine walishahukumiwa kama Jack Patrick anayetumikia kifungo cha miaka sita Macau (China) tangu mwaka 2013 lakini ishu hapa ni kuwataja wale waliowatuma.

Unajua waliofungwa kama akina Jack wakibanwa lazima watawataja wahusika hivyo kazi ya kuwakamata itakuwa rahisi japokuwa ushahidi unaweza kuwa mdogo.

“Ukweli ni kwamba popote alipofungwa au kushikiliwa Mbongo kwa ishu za unga lazima Interpol watamfikia kama ilivyokuwa kwa Jack.

“Sijui kama atakuwa aliwatajia aliyemtuma lakini mhusika atakuwa tumbo joto huko aliko.
“Unajua baada ya kuona ishu inazidi kuwa ya moto, baadhi ya hawa jamaa waliokuwa wanafanya kufuru ya fedha sasa hivi wamefyata. Zile mbwembwe za kumwaga fedha na kuhonga zimekwisha,” kilisema chanzo hicho kikiitaja China kuwa ni nchi yenye wafungwa wengi wa Kibongo wa unga.
Kwa mujibu wa chanzo kingine kilichomtembelea Jack gerezani katika Mji wa Macau hivi karibuni ni kweli mrembo huyo amekuwa akibanwa mara kwa mara kueleza kigogo aliyemtuma.
magufuli_aapaRais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’.

“Sasa kama aliwatajia ni siri yake na wao (Interpol) lakini suala la kuhojiwa aliyemtuma alishahojiwa sana na sasa hivi ndiyo mambo yamepamba moto baada ya Magufuli kuwatangazia vita,” kilisema chanzo hicho ambacho ni mfanyabishara za nguo kati ya Bongo na China.

Akizungumzia ishu hiyo, mkali wa sarakasi Bongo, Athumani Ford ‘Wabogojo’ anayefanyia kazi zake za sanaa nchini China ambaye huwa anakwenda kumuona Jack mara kwa mara gerezani alisema kuwa ni Wabongo wengi waliokumbana na msala huo ila mrembo huyo ndiye aliyebanwa zaidi.
Alisema kuwa hata yeye alipata taarifa kuwa Jack alibanwa zaidi kwa kuwa hakutaka kumtaja aliyemtuma mzigo huo.

Video Mpya: ‘My Life’ ya Dogo Janja Imeachiwa Tayari, Itazame Hapa

0
0
Baada ya kimya cha muda mrefu Dogo Janja kutoka Tip Top Connection 2016 aliachia hit single yake ya ‘My Life’, ngoma hiyo Dogo Janja amebadili ni tofauti na tulivyomzoea katika ngoma zake za nyuma. March 14 Dogo Janja kaachia rasmi video ya hit Single ya ‘My Life’ enjoy mtu wangu.

TAZAMA HAPA:

Kauli Ya Abbas Kandoro Baada Ya Rais Magufuli Kukata Jina Lake na Kutomchagua Kuwa Mkuu wa Mkoa

0
0
Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe  Magufuli  alitoa orodha ya wakuu wapya wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara.

Katika orodha hiyo Rais Magufuli , amewaacha wakuu kadhaa akiwamo aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bwana Abbas Kandoro.

Kipindi cha Sun Rise cha Radio Times Fm, kimefanya mahojiano na Kandoro asubuhi ya leo, ambapo amekiri kuachwa kwake na kuongeza kuwa tayari amefikia kikomo cha uongozi kwa maana umri wake haumruhusu kuendelea kutumikia nyadhifa hiyo.

“Unajua kuna watu wakituona wanajua kwamba bado tupo kwenye ujana, Ndugu mtangazaji mimi nina miaka 66 sasa hivi, tayari umri umenitupa mkono katika nafasi hii.

“Haijanishtua kwa sababu wakati tunapewa hii mikataba tuliambiwa kabisa ukomo wa mkuu wa Wilaya ni miaka 60 na Ukuu wa Mkoa ni miaka 66, hivyo nmetimiza umri wangu kisheria na napenda nimshukuru Mh Rais kwa hili” Alisema Abbas Kandoro.

Mpaka kustaafu kwake, Kandoro amehodhi nafasi ya ukuu wa Mikoa katika zaidi ya Mikoa Sita Tanzania Bara ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Singida na Mbeya.

Wafuasi wa CHADEMA Wafurika Mahakamani Kufuatilia Kesi ya Ezekiel Wenje ...Polisi Walazimika kutumia nguvu ya ziada kuimarisha ulinzi

0
0
Mamia ya wafuasi wa CHADEMA  wakiongozwa  na  Mwenyekiti  wao Freeman Mbowe leo  wamefurika mahakama  kuu  jijini  Mwanza katika kesi ya  mbunge wa zamani wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA)  anayepinga  matokeo  ya  Stanslaus Mabula (CCM). 

Polisi  wametumia  nguvu  ya  ziada  kuhakikisha  ulinzi  unaimarika  mahakamani  hapo





Ndoa ya Mwanamuziki Young D na Mrembo Tunda Inanukia...Wazazi Wameshaafikiana......

0
0
Mbongo-Fleva, David Genzi ‘Young D’ na mwandani wake ambaye ni muuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Tunda Sebastian, wameibua gumzo kwa taarifa kuwa wapo kwenye mikakati mizito ya kufunga pingu za maisha kutokana na upendo wa kweli walionao na jinsi wanavyoendana bila kujali udogo wao kiumri.

Kwa mujibu wa chanzo makini kilichopo karibu na Tunda, eti ndoa ya wawili hao kwa sasa inanukia kwani ishu hiyo hata wazazi wa pande zote mbili wameshaikubali na kilichobaki ni siku ya cherekochereko tu japokuwa watu hawaamini kama hilo linawezekana.

Baada ya kuunyaka ‘ubuyu’ huo, paparazi wetu alianza kwa kumvutia waya Young D ambaye simu yake haikuwa hewani lakini kwa upande wake Tunda alipotafutwa aliangua kicheko na kusema kuwa, siku zote watu wenye mapenzi ya kweli lazima wawe na malengo ya kuoana.

“Hakuna mwenye pingamizi kati yetu kuhusu hilo tunapendana na tunaendana ndiyo maana tukaanika uhusiano wetu, kwani tumeshatambulishana kwa wazazi, kwao najulikana na kwetu pia wanamjua, wapenzi wanaopendana kweli kifuatacho huwa ni ndoa tu,” alisema Tunda.

Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Lampongeza Rais Magufuli Kwa Kutumia Lugha Ya Kiswahili Kwenye Mikutano ya Kitaifa na Kimataifa

0
0
Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) limempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa uzalendo wake wa kuitumia lugha ya Kiswahili katika mikutano mikubwa na hafla mbalimbali za kitaifa na kimataifa.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi BAKITA, Prof. Martha Qorro ameeleza msimamo huo wa Rais Dkt.Magufuli  umewasidia Watanzania kupata taarifa moja kwa moja kutoka tukio husika.

“Uamuzi na msimamo wa Rais Magufuli wa kutumia lugha ya Kiswahili katika mikutano mikubwa ikiwemo  mkutano mkuu wa 17 wa viongozi wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umepokelewa kwa furaha kubwa na wananchi na wadau wengi wa Kiswahili ndani na nje ya Tanzania” alisema Prof.Martha.

Aliongeza kuwa kupitia msimamo huo wa Mhe. Rais Magufuli,   Baraza linaamini kwamba hatua hiyo itasaidia kukuza lugha ya Kiswahili na kutoa fursa ya ajira kwa Watanzania kupitia tafsiri na ukalimani na hivyo kuwapelekea maendeleo wananchi wote wa Afrika Mashariki.

Naye Katibu Mtendaji wa BAKITA Dkt. Seleman Sewangi ametoa wito kwa viongozi wengine wa ngazi mbalimbali za Kitaifa kufuata nyao za Mhe.Rais Magufuli kwa kuipa kipaumbele lugha ya Kiswahili ili kufikisha ujumbe kwa Watanzania walio wengi.

“Natoa wito kwa viongozi wetu wa ngazi mbalimbali za kitaifa kuitumia lugha ya Kiswahili katika mikutano mikubwa na hafla mbalimbali za kitaifa na kuachana na dhana ya kutumia lugha ya kigeni yenye lengo la kuwafurahisha wageni wachache” alisema Dkt. Sewangi.

Aidha, aliongeza kuwa katika kuhakikisha kuwa lugha ya kiswahili inatumiwa vizuri, Baraza hilo linaendelea kutekeleza mkakati wa kukamilisha kanuni zitakazopelekwa bungeni ili kumuwezesha Waziri mwenye dhamana kuwa na mamlaka ya kusimamia sheria ya lugha ya Kiswahili ya mwaka 1961 iliyorekebishwa mwaka 1985 ili kuipa nguvu ya kumshitaki mtu yeyote kwa matumizi mabaya ya lugha hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi,Taasisi ya Taaluma za Kiswahili chuo kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Ernesta Mosha ameziomba ofisi za Serikali hususani mahakama kutumia lugha ya Kiswahili kwa kuwa ni lugha inayoeleweka na Watanzania wengi ikizingatiwa kuwa sio wote wanajua kutumia lugha ya kiingereza.

Waziri Anayefaidi Posho za Magufuli Huyu Hapa...

0
0
Wakati amri ya Rais John Magufuli ya kufuta safari zote za nje ya nchi kwa watumishi wa umma ikiendelea kushika kasi, imebainika kuwa hadi sasa ni waziri mmoja tu ndiye walau amefanikiwa kwenda nje ya nchi baada ya kukidhi vigezo vilivyopo.

Uchunguzi uliofanywa na Nipashe, umebaini kuwa waziri huyo mwenye bahati ya pekee hadi sasa ni Balozi Augustino Mahiga wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Katika agizo lake alilolitoa siku chache baada ya kuingia madarakani Novemba 5, Rais Magufuli alisema ni marufuku kwa kiongozi au mtumishi yeyote wa umma kwenda nje ya nchi bila ya kupata kibali kutoka kwake au kwa Katibu Mkuu Kiongozi – Ikulu.

Taarifa zaidi zilieleza kuwa ili kiongozi au mtumishi yeyote wa umma apate kibali cha kusafiri kwenda nje ya nchi, ni lazima aeleze wazi kuwa safari hiyo anayotaka kwenda ina manufaa gani kwa taifa na kwamba, ni athari zipi zitatokea kwa taifa iwapo safari hiyo haitafanyika.

Uchunguzi umebaini kuwa tangu kutolewa kwa agizo hilo, ni Balozi Mahiga pekee ndiye aliyemudu kukidhi vigezo vya safari na hivyo kupata fursa ya kufaidi posho zianzoambatana na safari za aina hiyo ambazo Rais Magufuli anazipinga vikali kwa maelezo kuwa huligharimu taifa mabilioni ya fedha ambayo yangeweza kutumika kwa shughuli nyingine za maendeleo.

Katika hotuba yake wakati akizindua Bunge Novemba 20, 2015, Rais Magufuli alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2013/2014 na 2014/2015, taifa lilitumia zaidi ya Sh. bilioni 356.3 kwa ajili ya kugharimia safari za nje; jambo ambalo kamwe yeye hatakubali litokee kwa sababu fedha hizo zinaweza kukamilisha miradi mingi ya maendeleo ikiwamo kujenga barabara ya lami ya urefu wa kilomita 400.

“Kwakweli hali ni mbaya. Safari za Ulaya, Marekani na kwingineko nje ya nchi ndizo zilizokuwa zikitumiwa na mawaziri na vigogo wengine wa taasisi za umma kuvuna utajiri kupitia manunuzi ya tiketi na posho… hivi sasa anayenufaika ni Waziri Mahiga tu ambaye twaweza kusema ana bahati sana kwa sababu wizara yake haiwezi kukwepa safari,” chanzo kimoja kiliiambia Nipashe.

Wakati wa utawala wa awamu ya nne, mawaziri walikuwa wakisafiri mara kwa mara, katika kile ambacho aliyekuwa waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, aliwahi kukaririwa akisema kuwa ‘walikuwa wakipishana angani utafikiri nyumbani kunawaka moto’.

Chanzo kingine kiliiambia Nipashe kuwa kabla ya kuingia Ikulu kwa Magufuli, kuna mawaziri walikuwa wakivuna kati ya Sh. milioni saba na milioni tisa kwa siku kupitia malipo mbalimbali wawapo nje ya nchi lakini sasa hali iko tofauti kwani safari hizo zimebaki kuwa historia.


“Anayefaidi hapa ni Mahiga tu kwa sababu maelezo ya safari zake yako wazi, yanajitosheleza kutokana na wizara anayoiongoza… hawa mawaziri wengine mambo kwao ni magumu. Wapo waliojaribu kuomba safari wakaishia kugonga mwamba kwa sababu ya kutokidhi vigezo vya kupata kibali,” chanzo kingine kiliongeza. 

MAHIGA ANAVYOFAIDI 
Uchunguzi wa Nipashe umebaini kuwa kutokana na asili ya wizara anayoiongoza, walau Balozi Mahiga amesafiri kwenda nje ya nchi mara nyingi kuliko hata Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Magufuli mwenyewe ambaye hadi sasa hajawahi kuvuka mipaka ya Tanzania.

Safari pekee ya Majaliwa kwenda nje ya nchi ilikuwa Januari 17 wakati alipokwenda kumuwakilisha Rais Magufuli kwenye mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika GaboroNe, Botswana.

Baadhi ya safari za Balozi Mahiga ni pamoja na ile aliyokwenda Kigali, Rwanda Februari 18 wakati alipokwenda kupeleka ujumbe wa Rais Magufuli kwa Rais wa nchi hiyo, Paul Kagame na kisha akaenda Burundi kupeleka ujumbe kama huo kwa Rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunzinza.

Januari 30, Mahiga alisafiri pia na Makamu wa Rais, Samia Suluhu, kwenda Addis Ababa, Ethiopia kumuwakilisha Rais Magufuli kwenye mkutano wa 26 wa marais wa Afrika. Wakati wa Rais Kikwete, mikutano kama hiyo ilihusisha msafara wa Rais pamoja na mawaziri wasiopungua wanne, achilia mbali maafisa wengine mbalimbali.

Hata hivyo, licha ya unafuu wa safari za nje alio nao Mahiga, chanzo kimedai kuwa hata yeye (Mahiga), kwa nafasi yake, ni kama hajasafiri kitu kulinganisha na hali ilivyokuwa hapo kabla.

“Ingekuwa kipindi cha awamu ya nne, saa hizi Mahiga angesafiri mara nyingi zaidi kuliko hivi sasa ambapo safari zake hazifiki sita… ila kwa wengine hali ni mbaya zaidi kwa sababu hakuna aliyewahi kwenda nje ya Tanzania,” chanzo kiliiambia Nipashe.
BILIONI 7/- KATIKA SIKU 100

Wakati akizungumzia siku 100 za Rais Magufuli tangu aingie Ikulu, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema Sh. Bilioni 7 zimeokolewa kwa kupiga marufuku safari holela za viongozi kwenda nje ya nchi.

WAZIRI KITWANGA AKIRI KUTOSAFIRI
Alipoulizwa kuhusu safari za nje, Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga, alisema yeye ni miongoni mwa wengi ambao hadi sasa hajawahi kusafiri kwenda nje ya nchi tangu aapishwe na Rais John Magufuli kushika wadhifa huo.

Alisema ameshindwa kufanya hivyo kwa sababu hajawahi kupata mwaliko au kutumwa na Rais Magufuli, kusafiri kwenda nje ya nchi.
“Mimi sijawahi kwenda kwa sababu sina shughuli za kufanya huko na wala Rais hajawahi kunituma… sasa naendaje bila kutumwa wala kuwa na mwaliko?” Alisema Kitwanga.

MWIJAGE, MWIGULU MBIONI KUSAFIRI 
Baada ya kutokwenda nje ya nchi tangu waapishwe, hatimaye Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba wanatarajiwa kusafiri kwa mara ya kwanza baada ya Rais Magufuli kuwaruhusu juzi kwenda Vietnam kujifunza mbinu za kuinua kilimo na kujenga viwanda.

Malawi Yatekeza Tani Mbili za Pembe za Ndovu Kutoka Tanzania Zilizonaswa na Maafisa wa Usalama wa Nchi Hiyo..

0
0
Malawi imeteketeza tani 2.6 ya pembe za ndovu ambazo zilinaswa na maafisa wa usalama zikitokea nchi jirani ya Tanzania.

Meno hiyo 781 ya tembo ambayo inakisiwa kugharimu takriban dola milioni tatu ilipatikana baada ya operesheni dhidi ya ulanguzi na uwidaji haramu.

Mkurugenzi wa idara inayosimamia mbuga za wanyama pori Bright Kumchedwa, amesema kuwa hiyo ni ishara ya kwanza na dhabiti kutoka kwa Malawi kuwa haitaruhusu tena ardhi yake kutumika kulangua bidhaa za uwindaji haramu.

Hafla ya hiyo ya kihistoria ilifanyika katika eneo la Mzuzu kaskazini mwa nchi hiyo.
Kenya inatarajiwa kutekeleza hatua kama hiyo mwishoni mwa mwezi huu, Kenya imekamata takriban tani 120 ya meno ya ndovu.

EDWARD Lowassa: Rais Magufuli ni Mfano wa Viongozi wa Afrika Wasio na Maono

0
0
Edward Lowassa leo ameamua kumuelezea ukweli rais Magufuli kuwa ni miongoni mwa marais wa Afrika wasio na maono. Lowassa pia amesema kuwa Tanzania chini ya Magufuli itakosa kabisa ubunifu.

Hayo yanajiri baada ya rais John Magufuli kuzuia mambo mengi kwa lengo la kubana matumizi. Huku wataalam mbalimbali wakikwama kuwekeza kwenye taaluma baada ya kuzuiwa kupata mafunzo mbalimbali nje na ndani ya nchi.

Aidha rais Magufuli amekuwa akitoa hotuba kwa hisia kali hali inayowafanya wasaidizi wake kuingiwa na woga kwenye uthubutu.

"Magufuli ewafanya wasaidizi wake kukosa kabisa ubunifu na uthubutu wa kufanya maamuzi. Tanzania chini yake haitakuwa na jipya" amesema Lowassa.

Aidha Lowassa amesema kuwa sera ya elimu bure kwa Magufuli imekuwa "zero" baada ya kuiga.

HATIMAYE Peter wa P-Square Ajitenga na Kaka Yake na Kuanzisha Management yake

0
0
Kundi la P-Square halipo tena. Member wa kundi hilo, Peter Okoye amejitenga na kuanzisha management yake.

Hatua hiyo imekuja baada ya muimbaji huyo kutofautiana na meneja wao, Jude Okoye ambaye ni kaka yake. Jude anaendelea kuwa meneja wa pacha mwingine, Paul. Kupitia Instagram, Peter ameandika:

Work Mood. Thanks for all the love, support and concern pls continue to remain blessed as always. For bookings and enquiries, please contact my new management on 08037531340 [email] bookmrp2@gmail.com ||oyesng@yahoo.com #MrP.

Wakati huo huo Paul ambaye ameanzisha record label yake, Rudeboy Records, amepost picha ya mama yao na kuandika:

Wish you were around, now I understand what these life is without having a mother, you’ve played your part thank you very much mum, miss you.”

Utafiti: Tanzania Yabainika Kuwa Nchi ya Kwanza Isiyo Aminifu Duniani.....

0
0
Utafiti huo umebainisha kuwa uaminifu binafsi huwa mkubwa kwenye jamii zenye matatizo machache ya rushwa, ukwepaji kodi na utapeli wa kisiasa.

Wakati ambapo Austria, Uholanzi na Uingereza zimeshika nafasi ya kwanza katika nchi aminifu duniani, Tanzania na Morocco ambazo ubora wa taasisi zake ulibainika kuwa wa chini, zilifanya vibaya.


Utafiti huo ulifanywa na chuo kikuu cha Nottingham na kuhusisha nchi 159.
Walitumia taarifa zilizopo kuanzia mwaka 2003 za utapeli kisiasa, ukwepaji kodi na rushwa.

Utafiti huo ulibaini kuwa watu wanaoshi kwenye nchi zenye matukio machache ya uvunjaji sheria, walikutwa na uwezekano mdogo wa kudanganya ili kupata fedha ukilinganisha na nchi zenye matatizo ya rushwa.

Ulidai kuwa uwepo wa matukio ya uvunjaji sheria, huwafanya watu kupindisha ukweli.

The End of an Era? Peter Okoye Reveals New Stage Name and Management...

0
0

Peter Okoye seems to be going forward as a solo artist. He updated his Instagram bio adding the stage name "Mr P" and contact information of his new management.

He wrote: "Work Mood. Thanks for all the love, support and concern pls continue to remain blessed as always. For bookings and enquiries,please contact my new management on 📞08037531340. bookmrp2@gmail.com ||oyesng@yahoo.com. #MrP


WEMA SEPETU Afunguka Kuhusu Kutoka na Mkongo Man...Adai Amechoka Kutumika Kama Daraja

0
0
Wema Sepetu afunguka kuhusu tuhuma za kutoka na Mkongo Man apocalypse

"Sijawahi na sitowahi kuwa na mwanaume Mcongo wa aina yoyote ile... Sasa nashangaa watu wameona mimi ndo daraja la kuwapa umaarufu... Im Tired... Huyo apocalypse sijui kitu gani aint my man... I only know him as a friend... So please guys.... Niacheni kidogo tafadhal... Alam-siq...!!! And ontop of all dat I think u all know me by now nikiwa na mtu sijivungi kumtangaza maana huwa I live to please my heart... Mwanaume wangu nadhani anajulikana... Sasa endeleeni kumpa huyo baba attention sababu yeye nako naona kashaona ni kamchezo kakupatia followers... Na nyie mnampa airtime ya kutosha.... So anaendelea... Ananiudhi na mimi kiukweli hadi napata hasira... But nakaa tu kimya... This is too much now..."Wema Sepetu

Hii Hapa Post ya Mkongo Man Iliyomfanya WEMA Sepetu Kufunguka na Kukanusha Kutoka Kimapenzi na Mkongo Man

0
0
Mkongo Man anayejiita Apocalypse jioni ya leo alipost meseji kwenye ukurasa wake wa Instagram iliyomtaja Wema Sepetu ikionyesha kuwa kuna kitu kinaendelea kati yao kitu kilichomfanya Wema Afunguke....Soma Hapa Alichoandika Mkongo Man......

Je Mwanamuziki AY Kajiunga Wasafi ? Kama Ulikuwa Hujui Meneja wa Diamond, Sallam, Sasa ni Meneja wa AY Pia

0
0
Sallam Sharaf, meneja wa Diamond, sasa ni meneja wa AY pia.
Taarifa hiyo imetangazwa Jumatatu hii na wao wenyewe.

Alianza AY aliyeandika kwenye Instagram:

"Great Team.. My Manager @sallam_sk #Mendez & My Supa Dupa Producer @hermyb Nairobi..Much next…Dar es Salaam #strictlyBusiness.”

Naye Sallam aliandika kwenye Instagram:

"GOODBYE NAIROBI…. Thank You Again…!! And the Good news is @aytanzania he’s under my management. What a Bless to manage THE LEGEND. Don’t Listen to THEY BE INSPIRED.”

Kitu ambacho huenda wengi hawajui ni kwamba Sallam na AY ni washkaji na business partners wa muda mrefu. Wawili hao walikuwa wakifanya biashara pamoja hata kabla ya Sallam kuwa meneja wa Diamond. Huenda sasa wameona ni muhimu kuupeleka ushkaji wao kwenye level nyingine.


Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images