Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live

Waziri Muhongo Amjia Juu Zitto Kabwe, ni Kuhusu Kampuni ya IPTL

0
0
SIKU chache kupita baada ya Mbunge wa Kigoma mjini,Zitto Kabwe kusema tangu utawala wa Rais John Magufuli kuingia madarakani,Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imeitia hasara serikali ya Bilioni 36 kwa kile anachodai Kampuni hiyo inaitapeli serikali kwenye Malipo ya Capacty Charge,

Naye Waziri wa Nisharti na Madini,Sospeter Muhongo ameibuka na kusema Mbunge huyo anatumiwa kuisakama kampuni ya IPTL kwa maslahi yake kisiasa,

Waziri Muhongo ameitoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam,wakati alipokuwa anazungumza na mwandishi wa Fullhabari.blogs mara baaada ya kumalizika mkutano na waandishi wa habari aliokuwa anazungumzia ugunduzi mpya wa Gesi asilia,

Ambapo Waziri Muhongo ni kama amemshangaa mbunge huyo kwa kitendo chake achodai ni kushikilia hoja ya IPTL kila siku badala ya kutamaza mikataba yote ya Makampuni ya umeme ambayo inauzia umeme Tanesco ambayo amekili ni mibovu,

“Yaani huyu mtu anaugomvi tu na hii kampuni na anaitumia kwa ajili ya kujijenga kisiasa,maana kila siku yeye na IPTL tu,kama hoja ni mikataba ni mbovu,ni makampuni yote yanayoiuzia shirika la umeme Tanesco mikataba mingi inakasoro nyingi,lakini nashangaa huyu Zitto ayasema haya kila siku na IPTL,mbona mengine hasemi”amesema Waziri Muhongo,

Waziri Muhongo ameongeza kuwa “na nyinyi wanahabri tumieni elimu yenu kuelimisha umma,tuache kuingia kwenye mitego ya wanasiasa wa aina hii,tusema ukweli juu ya mkataba wa IPTL na Tanesco”

Kauli ya Waziri Muhongo inakuja ikiwa Mbunge huyo ambaye ni Kiongozi wa mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo kuandika kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo aliandika kuwa kitendo cha Rais Magufuli kushindwa kuchukua hatua juu ya malipo ya IPTL ambayo yanalipwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kila mwezi yamepelekea sasa hivi kufikia jumla ya bilioni 36 kupotea,

"Tshs bilioni 8 kila mwezi TANESCO bado wanalipa IPTL. Rais haijampendeza kumaliza ufisadi huu. IPTL nadhani ni Jipu la Mgongoni (kwa kutumia maneno ya Hidaya wa Richard Mabala ). Raisq, kwa kutochukua kwake hatua, ameshaliingizia taifa hasara ya tshs 36 bilioni toka aingie madarakani" aliandika Zitto Kabwe.

Aidha,Zitto Kabwe aliongeza kusema kuwa Wakati Rais Magufuli anatimiza siku 100 toka kutangazwa kama Rais Zitto Kabwe alitoa tathimini yake na kugusia sakata la Escrow pamoja na kampuni ya IPTL na kusema kuwa pesa ambazo wamelipwa IPTL/PAP kwa siku 100 tu zingeweza kununua CT Scan kwa hospitali zote za mikoa nchini,

"Mkataba wa IPTL bado unaendelea kunyonya Nchi na Serikali inatazama tshs 8 bilioni zinalipwa Kwa matapeli wa IPTL na PAP kila mwezi.

"Katika siku 100 tangu Rais Magufuli aingie madarakani, jumla ya tshs 30 bilioni zimeshalipwa Kwa IPTL/PAP ambazo zingeweza kununua CT scan Kwa hospitali zote za mikoa nchini.

Msanii wa Uganda Kuhamia Tanzania ili Kusajiliwa WCB Ya Diamond Platnumz

0
0
Msanii wa Uganda anayefanya muziki wa rnb ‘Aziz Azion’ ameripotiwa kuhamia Tanzania ili kufanya wimbo na Diamond Platnumz na kujiunga na lebel ya Diamond Platnumz ya Wasafi records.

Mshkaji wa karibu wa Aziz amesema kama jamaa aki saini na Wasafi itabidi ahamie Tanzania.

Madam Wema Sepetu, Tusamehe tu Watanzania

0
0
Naandika uzi huu kwa niaba ya Watanzania, kumhusu Madam Wema Sepetu, mlimbwende wa zamani wa Tanzania, akishinda Taji hilo mwaka 2006 mbele ya Jokate Mwegelo, mjasiriamali, msanii wa filamu, muziki na mwanaharakati na Lisa Jensen, aliyekuja kuwa Redds Miss World Tanzania mwaka 2012.

Kwa muda mrefu Madam amekuwa kwenye vichwa vya habari kwa wema na kwa ubaya, kama lilivyo jina lake, Wema Sepetu a.k.a Mama Ubaya, lakini ubaya ukionekana kuzidi wema wake machoni pa kundi la 'Watanzania Wastaarabu'.

Wema, kama washindi wengine wa taji hilo la Umiss, amelitendea haki kwa kufanya kazi zinazotakiwa, na walau kuka nalo vema hadi alipolikabidhi kwa mrithi wake, Richa Adhia mwaka 2007.

Wema Abraham Sepetu akiwa na Diamond Platinumz, msanii wa kimataifa wa Tanzania, enzi za mapenzi yao, kwenye Tuzo za MTV Afrika.​

Licha ya ushindi huo, madam amekuwa na 'kismati', kama wenyewe wanavyodai. Wachumba aliokuwa anatembea nao walipata mafanikio makubwa kwenye kazi zao, iwe muziki, uzalishaji au uigizaji wa filamu na pengine hata biashara zisizohusisha sanaa.

Ukikaa na Waridi utanukia, bila shaka mada amekuwa waridi kwa watu wengi, akiwaangazia nyota na kuwatangaza kimataifa. Madam akiwa upande wako, nani aliye juu yako? Kwa hili tuna deni kwake...

Madam amemsaidia sana msanii Diamond Platinumz, licha ya kuwa pumziko lake kwa miaka kadhaa, alimfundisha mambo mengi ya msingi ikiwemo lugha ya Kiingereza, nyenzo muhimu kwenye utandawazi.

Madam alimtoa Diamond kutoka uselebriti kunuka na kumfanya kuwa wa kisasa, msanii wa kimataifa. Popote tunapomsifia Chibu, tujue tuna deni kwa Madam Wema Sepetu.


Licha ya umaarufu wa magazeti na Blogu, madam ana juhudi binafsi za kimaisha, uzinduzi wa Kampuni ya Endeless Fame (inayomsimamia msanii Mirror), brand yake ya ' Kiss Lipstick' na maajabu mengine kibao.

Madam ni msanii, NDIO, mmoja wa wasanii wakubwa kabisa wa Bongo Movie... Tunapoona mafanikio yoyote kwenye tasnia, madam ana mchango wake mkubwa sana, kwa kweli anatudai.

Madam amewahi kushiriki kwenye Siasa ngazi ya kitaifa, kwa kugombea Ubunge Viti Maalum ndani ya Chama cha Mapinduzi. Licha ya kuwepo kwa dalili za ushindi wake kuchakachuliwa, alionesha uungwana wa hali ya juu kwa kukubali matokeo na kushiriki kikamilifu kwenye kampeni za Uchaguzi 2015.



Madam ni Celeb pekee kuwahi kuwa na Timu yake, timu inayojitambulisha kama #TeamMadam na ikijumuisha watu wakubwa na maarufu; Kajala, Petit Man, Aunt Ezekiel, DJ Rommie Jones (DJ wa Diamond Platinumz) na wengine wengi... Huu ni umaarufu wa Kiwango cha Kimataifa.


Licha ya kupumzika kidogo shughuli za filamu, bado hayuko nyuma kuwaunga mkono wasanii wenzake. Juzi alienda na gari lake kumpokea Elizabeth Michael Lulu, huu ni upendo uliopitiliza.

Madam ni mshiriki mzuri wa matukio ya kijamii na kindugu. Anahudhuria misiba, sherehe na matukio mengine kwa ukamilifu.Hata uhusiano wake na washabiki wake sio wa kunata wala kujidai, kama wadada wengine maarufu.

Sijasahau alivyojitolea kumtoa jela Kajala Masanja, wakati ambao wasanii wengine maarufu walipomsusa. Huu ni wema usio na kipimo...

Licha ya utu wake huu, madam amesakamwa na magazeti, blogu, mitandao na watanzania kwa ujumla. Wakimtusi, wakimkejeli, wakitengeneza picha za uongo, wakimuita malaya na wakati huo wakinufaika na kuuza habari zake.

Licha ya ubaya huu tuliomlipa, bado Wema ameendelea kuwa mzalendo, na mtu anayejitolea kwa taifa, kwa wasanii wenzake na jamii kwa ujumla. Kwa ambao wamewahi kuroll na Mama Lao, watakubaliana na mimi kuwa hayuko namna ambavyo watu wanamchukulia.

Kwa kweli wema wa Madam ungekuwa unaandikwa, vitabu vya dunia hii visingetosha kuuelezea wote.

Natoa wito kwa sisi kama taifa, kutafakari ubaya huu tuliomvika madame, na tumuombe radhi kwa ujumla wetu... Ikiwezekana tumjengee na mnara wa kumbukumbu.

By Mbilimbi Mbovu

Breaking News: Balozi Juma Mwapachu Atangaza Kurudi CCM, Adai Alilewa Mahaba ya Lowassa na Ahadi ya Kuwa Waziri wa Mambo ya Nje

0
0

HOTUBA YA BALOZI JUMA MWAPACHU KUTANGAZA KUREJEA CCM​


MIKOCHENI 16/03/2016​


Ndugu zangu,

Mtakumbuka kwamba mnamo tarehe 13 Oktoba 2015, nilitangaza kuihama CCM na kurejesha kadi yangu ya uanachama kwenye ofisi ya CCM Kata ya Mikocheni. Nilitoa maelezo kwanini niliamua kujiondoa CCM (maelezo hayo pia niliyabandika katika ukurasa wangu wa facebook). Nilieleza kwamba CCM imepoteza mwelekeo kwa kuamua kumnyima haki ya kugombea mcha mungu Edward Lowassa. Nikasema Edward Lowassa ndiye chaguo la wana-CCM na ndiye chaguo la Watanzania. Nikasema nitakuwa mnafiki nikiendelea kubaki CCM huku naamini Edward Lowasa anafaa kuwa Rais kuliko John Pombe Magufuli.

Baada ya miezi miwili ya uongozi wa Magufuli nataka niseme nilikosea sana. Nililewa mahaba ya Lowassa, nililewa ahadi ya Lowassa kunipa uwaziri wa mambo ya Nje. Niliamini mafuriko ya Lowassa ambayo yakanifanya niamini kabisa anachukua nchi. Tulikubaliana na wenzangu kwamba wiki mbili za mwisho tuihame CCM kwa wimbi kubwa ili kuitikisa na kuitoa madarakani. Lakini baadhi wakaogopa na hadi sasa wengine wamebaki CCM na wana vyeo.

Leo natangaza kurudi CCM kwa sababu nimeona kazi nzuri ya Magufuli. Nimefanya kosa kubwa katika siasa ambalo nawasihi vijana kwenye siasa wasifanye. Nilihama kwa kwa sababu ya mtu (Lowassa). Nimerudi kwa sababu ya mtu (Magufuli). Nataka niwaahidi kwamba CCM ikiweka mtu hovyo baada ya Magufuli, sitahama. Usemi wa CCM kwamba Chama Kwanza, Mtu Baadaye sasa ndio nauona maana yake. Niliwalaumu CCM kwa kumuacha Lowassa lakini sikujua kwamba CCM ina uwezo wa miujiza wa kuibua jembe bora linaloitwa Magufuli.

Naomba mnisamehe kwa kulifanya jambo langu la kujitoa CCM na kurudi CCM kuwa jambo la kitaifa ukizingatia kwamba sikuwa na nafasi yoyote ya uongozi wa CCM wakati nahama na pia sijawahi kuwa hata Mjumbe wa NEC ya CCM na nilikuwa nje ya ulingo wa siasa za CCM kwa miaka 20. Niliamua kulifanya jambo kubwa ili kumsaidia Lowassa. Na sasa nimeamua kulifanya jambo kubwa ili Magufuli ajue sasa niko naye kwasababu sitaki shughuli zangu na za washirika wangu zikwamishwe na Serikali kwa sababu tu huko nyuma niliamua kumsaidia swahiba wangu.

Naomba radhi kwa familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa kuitumia kisiasa siku aliyokufa (tar 14 Octoba) na kutumia msiba wake kutoa kauli za kisiasa zidi ya chama chake alichokiunda na ambacho hadi anakufa alikuwa mwanachama.

Wananchi wote tumuombee Magufuli na tumsaidie kwani tumepata Nyerere mpya.

Mungu Ibariki Tanzania
mungu Ibariki Afrika

Balozi Juma Mwapachu

Jeshi La Ulinzi La Wananchi Wa Tanzania Lakanusha Kupeleka Wanajeshi Visiwani Zanzibar.

0
0
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kwa Umma juu ya uvumi ulioenea katika mitandao ya kijamii kuwa, limepeleka Wanajeshi wengi visiwani Zanzibar kwa ajili ya kudhibiti Usalama wakati wa kipindi hiki cha uchaguzi marudio unaotarajia kufanyika tarehe 20 Machi, 2016

Habari hizo siyo za kweli na zina lengo la kupotosha Umma. Kimsingi JWTZ linao Wanajeshi visiwani Zanzibar wakati wote kwa majukumu yake ya msingi ya Ulinzi wa nchi yetu.

Hivyo hakuna Mwanajeshi yeyote aliyeongezwa zaidi ya wale waliopo visiwani humo tangu awali. Taarifa hizo zipuuzwe,zisipewe nafasi yoyote ya kujenga hofu kwa Wananchi.

JWTZ linapenda kwa mara nyingine tena kuwahakikishia Wananchi kuwa wasiwe na wasiwasi wowote kuhusu ulinzi na usalama wa nchi yetu, kwani wakati wote Jeshi lao lipo imara kuwalinda.

Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638.

Hiki Ndicho Kanye West Alivutiwa kwa Mwanamuziki Diamond Platnumz Hadi Kuomba Kupiga Picha Nae

0
0
Muziki wa Bongo Fleva umeanza kulipa, tunaweza tukawa nchi ya tatu Afrika baada ya Nigeria, Afrika Kusini.

Hivi karibuni picha kibao zilisambaa mitandaoni baada ya msanii, Diamond Platnumz kupost picha akiwa na staa wa Hip Hop kutoka nchini Marekani, Kanye West. Diamond amesema ‘Kanye West alivutiwa na viatu vyangu ambavyo nilikuwa nimevivaa.’

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Diamond alisema,
 “Nilipokuwa airport pale Los Angeles tunasubiri kuchukua mabegi yetu, nilisikia mtu akisema ninaweza kupiga picha viatu vyako? Kwakuwa alikuwa ameinama sikuweza kumtambua lakini alipoinuka nikashangaa kumuona ni brother Kanye West. Nilimuomba tupige picha kwanza halafu vingine vitaendelea.”

“Tumuombe Mungu mambo yaendelee vizuri kama tulivyopanga, kuna kitu kizuri kinaweza kikatokea kati yetu,” aliongeza Diamond.

Kamwe Sitafuti Kiki Nirudi Kwenye Chat ya Music....Nina Biashara Zangu Zinazoniingizia Pesa Nyingi - Dudu Baya

0
0
Msanii Dudu baya amesema kwamba katika maisha yake hawezi kutafuta kiki ya kurudia kwenye game, kwani ana biashara yake inayomuingizia pesa nyingi zaidi.

Dudu Baya ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye stori 3 za Planet Bongo inayorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa ana biashara na kampuni, na hivi karibuni anafikiria kuleta wasanii wakubwa kutoka nje.

"Nikifungua bar ni mambas, kwa sasa nina kampuni ya Mambas Entertainment, nimeanza kazi muda mrefu naweza kuongea na msanii tukaenda Musoma tunapiga show, na may dream nitakuwa nawaleta hata wasanii kutoka nje, lakini sasa hivi toka 2013 niko kanda ya ziwa, na ndio maana hata show zangu sitegemei nipigiwe show na promota", alisema Dudu Baya.

Pamoja na hayo Dudu Baya amesema shughuli za ujenzi na biashara ya mbao, ndio inayomfanya asisikike kwenye muziki kwa sasa.

"Mi nimesomea archteck uchoraji wa majengo na ujenzi, natoa mbao Kasulu, ukiona sisikiki kwenye muziki ujue hiyo ndio business im doing", alisema Dudu Baya.

Kama Wewe ni Msichana na Unamzidi Ruby Kuimba Njoo WASAFI Records - Babu Tale

0
0
Meneja wa lebel ya WCB Babu Tale ametoa fursa kwa wasanii wa kike wenye vipaji kuonyesha vipaji vyao, na hatimaye kuweza kupata fursa ya kuwa chini ya uongozi wao wa WCB.

Babu Tale ametoa fursa hiyo alipokuwa akiongea ndani ya Planet Bongo ya East Africa Radio, alipoenda kumtambulisha msanii mpya amabye atakuwa chini ya uongozi huo Raymond TipTop, na kusema kuwa wasani wa kike ni wachche hivyo wana fursa kubwa ya kufanya vizuri iwapo watajituma.

Tuna Plan kuwapata wasanii wa kike lakini wenye vipaji vya ukweli, asikwambie mtu industry yetu ina wanawake wachache, tungepata wananwake wanne hata watano', alisema Babu Tale
Pia babu Tale alisema anatamani sana msanii Ruby angekuwa kwenye management yake, kwani ana uwezo mkubwa lakini kwa bahati mbaya ytayari yuko chini ya management nyingine ya THT.
Kwangu mimi ingekuwa Ruby hayuko chini ya THT, au hana management tungemchukua, lakini nasema hivi, kama anakuja mwanamke, awe na level ya kufanana na Ruby au kumshinda Ruby", alisema Babu Tale

Pamoja na hayo nae Diamond Platnums amesema ameweka wazi vigezo ambavyo msanii huyo wa kike avifikie ili aweze kuwa chini ya uongozi huo, pamoja na kujituma tofauti na walivyozoea kuwa hawawezi.

Aweze kuandika mashairi, aandike nyimbo zake mwenyewe unajua kuna kitu kimoja, wanawake washajiwekea kuwa wao hawawezi, sio kweli hawataki kufocus na kujaribu", alisema Diamond.

Magufuli "Mtaalam Atakayekodi Mitambo Kuzalisha Umeme Badala ya Kununua Mitambo Hatufai Tanzania"

0
0
Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli leo ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi namba mbili, uliopo katika wilaya ya Ilala Mkoani Dar es salaam.

Mradi huo utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawatts 240 za umeme.
Mradi huo ambao utazalisha umeme kwa kutumia gesi asilia inayosafirishwa kwa bomba kutoka Mtwara, unatarajiwa kuanza kuzalisha umeme katika kipindi cha kuanzia miezi 21 hadi 28 utakapokamilika kabisa.

Kuanza kwa ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme huo, kunafuatia juhudi zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano ya kufanikisha upatikanaji wa shilingi bilioni 120, ikiwa ni asilimia 15 ya fedha zilizopaswa kutolewa na Tanzania na fedha nyingine shilingi Bilioni 292 zimetolewa na Japan.
Mradi huu umetanguliwa na mradi wa Kinyerezi namba moja ambao una uwezo wa kuzalisha megawatts 150 za umeme, na mitambo yake tayari imeanza uzalishaji wa megawatts 105 zilizoingizwa katika gridi ya Taifa.

Pamoja na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa Kinyerezi namba mbili, Rais Magufuli amekagua mitambo ya kuzalisha umeme ya mradi wa Kinyerezi namba moja, ambapo Mkuu wa Kituo cha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) cha Kinyerezi Mhandisi John Mageni, ametoa maelezo kuwa shirika hilo lina mpango wa kupanua uzalishaji wa umeme katika mradi huo kutoka megawatts 150 hadi kufikia megawatta 335, kwa kuongeza mitambo ya kufua umeme kwa teknolojia inayojumuisha matumizi ya gesi asilia na mvuke uzalishwao na mitambo hiyo.

Baada ya ya kupokea maelezo hayo, Rais Magufuli ameridhia kuwa serikali yake itatoa dola za kimarekani milioni 20, kwa ajili ya kufanikisha upanuzi wa mradi huo na ameagiza kuwa wataalamu wa TANESCO washirikiane na mkandalasi kuhakikisha upanuzi huo unafanyika haraka iwezekanavyo, badala ya muda wa miezi 12 uliopangwa.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa mradi huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO, kuanza kuachana na mitambo ya kukodi kwa ajili ya kuzalisha umeme, na badala yake nchi ijenge mitambo yake yenyewe ili kuondokana na gharama kubwa za nishati hiyo muhimu.

"Waziri, ukiona mtaalamu anakuletea mapendekezo ya kutaka kukodi mitambo ya kuzalisha umeme, badala ya kuleta mapendekezo ya kununua mitambo yetu wenyewe ujue mtaalamu huyo hafai, mtoe" Amesisitiza Rais Magufuli.

Ameongeza kuwa tafiti zimethibitisha kuwa hadi sasa Tanzania ina zaidi ya futi za ujazo Trilioni 57 za gesi asilia, ambayo itazalisha umeme wa kutosheleza mahitaji ya ndani, na umeme mwingine kuuzwa nje ya nchi ikiwemo Kenya ambayo tayari imeomba kuuziwa umeme kutoka Tanzania.
Aidha, Rais Magufuli ametoa onyo kwa TANESCO kuwa hatarajii kusikia bwawa la maji la Mtera limeishiwa maji, kwa kuwa katika msimu huu wa mvua maeneo ya Iringa yalikuwa na mvua nyingi ambazo zimesababisha hadi mafuriko mafurukio.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo amesema tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, juhudi zilizofanyika zimefanikisha kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka megawatts 800 hadi kufikia megawatts 1,000 kiasi ambacho ni pungufu kwa megawatts 20 tu, ikilinganishwa na mahitaji ya megawatts 1020 za sasa.

Ameongeza kuwa pamoja na kuweka jiwe la msingi la mradi wa Kinyerezi namba mbili, hivi karibuni serikali inatarajia kujenga miradi mingine ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia, ikiwemo Kinyerezi namba tatu utakaozalisha megawatts 600, Kinyerezi namba nne utakaozalisha megawatts 300, na mingine itakayojengwa Lindi na Mtwara.

Prof. Muhongo amebainisha kuwa mpaka sasa gesi asilia inazalisha kati ya asilimia 50 na 60 ya umeme wote hapa nchini, Maji yanazalisha asilimia 30 hadi 40, na umeme unaozalishwa kwa mafuta hauvuki asilimia 10.

Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Balozi wa Japani hapa nchini Mheshimiwa Masaharu Yoshida, Wabunge wa kamati ya Nishati na Madini, wafadhili wakiwemo Benki ya Dunia, Benki ya Afrika na Shirika misaada la Japan (JICA.

Utata wa Filamu ya Lulu Michael Iliyoshinda Tuzo Nigeria..Wizara Yatoa Tamko Hili Hapa....

0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kumekuwa na minongono mingi kutoka kwa baadhi ya wananchi kuhusu Filamu ya Mapenzi ya Mungu ya msanii Elizabeth Michael (Lulu) iliyoshinda tuzo ya Filamu bora Afrika Mashariki mapema mwezi huu huko Lagos Nchini Nigeria katika tuzo za African Magic Views Choice Award (AMVCA).

Ili filamu ikamilike inahusisha watu mbalimbali wanaoshirikishwa kukamilisha filamu kuanzia mtoa wazo ambaye wazo hilo huwekwa katika mswada na mtaalamu jambo ambalo haliondoshi umiliki wa filamu.

Tunapenda kuufahamisha umma kuwa mmiliki halali wa Filamu ya Mapenzi ya Mungu ni Msanii Elizabeth Michael (Lulu) na ndiye aliyepata tuzo kwani ana haki zote za kupata tuzo hiyo kama mmiliki halali wa filamu hiyo.

Filamu ya Mapenzi ya Mungu imetengenezwa chini ya kampuni ya Proin Promotion na imesajiliwa kwa namba ya usajili CO831190.

IMETOLEWA NA
WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Rais Magufuli na Mke Wake Wamekifagilia Kipindi cha 360 cha Clouds FM..Wapiga Simu Laivu Wakiwa Hewani Nakusema Haya

0
0
Leo asubuhi Mkuu wa Nchi Rais John Pombe Magufuli amepiga simu kwa kusuprise kwenye kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV huku kikiwa hewani na Kuwaambia kuwa yeye na mkewe ni washabiki wakubwa sana wa kipindi hicho..amesema yeye na mkewe kila asubuhi huwa waangalia na kufurahishwa sana na watangazaji hao....Mkewe naye aliongea na kusema huwa anacheka sana kwa vituko vya watangazaji hao wakati wakichambua habari mbali mbali ....

Sasa ni rai kwa waandishi kufanya kazi mkijua rais wa nchi anafatilia utendaji wenu wa kazi wa kutuhabarisha wananchi na huwenda mambo mengine anayajua kupitia vipindi vyenu.

Hongera wana Clouds 360.....

Watu 42 Watiwa Mbaroni Zanzibar Wakituhumiwa Kulipua Nyumba ya Kamishna wa Polisi

0
0
Jeshi la Polisi Zanzibar linawashikilia watu 42 wakituhumiwa kuhusika na mlipuko uliotokea juzi usiku katika nyumba ya Kamishna wa Polisi, Hamdan Omar Makame.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya polisi Ziwani, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam alisema hadi jana mchana watu 42 walikuwa ndani kwa ajili ya kuhojiwa na jeshi hilo.

Alisema uchunguzi unaendelea na bado watu wengine wanatafutwa kuhusiana na tukio hilo.

“Bado tunaendelea na uchunguzi wa jambo hili na tukishakamilisha tutatoa taarifa rasmi,” alisema Kamanda Mkadam.

Tanzania: Tupo Kwenye top 10 ya Nchi Zisizo na Furaha Duniani

0
0
Denmark imechukua nafasi ya Switzerland kama nchi yenye furaha zaidi duniani kwa mujibu wa ripoti iliyotoka Jumatano hii.

Ripoti hiyo imeandaliwa na ‘Sustainable Development Solutions Network and the Earth Institute’ katika chuo kikuu cha Columbia.

Ilionesha kuwa Syria, Afghanistan na nchi zingine 8 zilizopo chini ya jangwa la Sahara ndizo sehemu zisizo na furaha zaidi. Nchi hizo ni pamoja na Madagascar, Tanzania, Liberia, Guinea, Rwanda, Benin, Togo na Burundi.

Nchi 10 za juu zenye furaha zaidi ni Denmark, Switzerland, Iceland, Norway, Finland, Canada, Uholanzi, New Zealand, Australia na Sweden.

Nchi tano duniani, Bhutan, Ecuador, Scotland, UAE na Venezuela zimeteua mawaziri watakaoshughulikia ukuzaji wa furaha.

Tanzania tuna matatizo gani? Kuna umuhimu wa Magufuli kuanzisha wizara kama hiyo pia?

Jina la Msanii wa P Square Analotumia Kama Solo Artist ‘Mr P’ Limepondwa na Kukataliwa na Mashabiki wa Muziki Nigeria

0
0
Jina la msanii wa P Square analotumia kama solo artist ‘Mr P’ limepondwa na kukataliwa na mashabiki wa muziki Nigeria na wengi wametoa majina kadha anayoweza kutumia kama solo artist.

Majina haya ni

Mr Pedro>Ikimaanisha Peter kwa lugha ya Spanish au kilatino

Pitrus Mushica

P-Money> Ni vizuri jina la msanii lihusishwa na pesa kama bosi wa Kcee E-Money.

P-Love> sababu ya uimbaji wake anafaa sana kuwa na jina kama hili.

Young P>Hapa sina la kusema.

UKAWA Yaanza Kupasuka Mdogo Mdogo..Baada ya Mwapachu Kurudi CCM Wengine zaidi Kurudi

0
0
Ukawa yaanza kupasuka katika hali ya kushangaza wanachama wengi wachadema waobesha hali ya kuikubali CCM, hii ni dalili tosha kabisa ya kifo cha Ukawa. Week iliyoopita wanachama zaidi ya mia hamsini walikihama Chadema na kurudi ccm, Leo tena mwapachu aliyeihama ccm kwa mbwebwe na kwenda ukawa arudi kwa mwenyewe ccm, na tetesi zinaonesha kesho pia SAA NNE mgeja na wenzake baadhi wanachama wa Chadema tegemeo watajiunga ccm ili kuudhihirishia umma wa Tanzania kuwa sasa CCM ya Mwalimu imerudi. Hali hii imemfanya mbowe kuchanganyikiwa na sasa anatapatapa hajui afanyeje kuuzuia upepo wa magufuli unaowavuta wengi CCM. POLE SANA NYUMBU HALI TETE KIBANDA KINATEKETEA

Mtoto wa Will Smith Jaden Smith Aendelea Kusimangwa Kwa Kuvaa Nguo za Kike.....

0
0
BAADA ya kushambuliwa sana kwenye mitandao ya kijamii kutokana na aina ya mavazi yake, msanii wa muziki na filamu, Jaden Smith, amesema ataendelea kuvaa nguo yoyote atakayoona inampendeza.

Msanii huyo anashambuliwa kutokana na kuvaa nguo za kike, lakini aliwajibu wanaomkashifu kwa nguo hizo kwa madai kwamba anaendelea kuvaa nguo hizo kutokana na mwili wake ulivyo.

“Akili yangu inanituma kuvaa nguo zitakazonipendeza mwilini na kunikaa, hivyo siwezi kuwasikiliza watu wanachotaka juu ya mavazi yangu.

“Hakuna nguo zilizoandikwa kuwa ni za kiume ama za kike, hivyo unaweza kuvaa kama itakuwa inakupendeza, haya ni maisha yangu hakuna wa kuniingilia,” aliandikwa Jaden kwenye akaunti yake ya twitter.

Henry Kilewo Afunguka 'Balozi Juma Mwapachu Alipoondoka Hakujiunga na Chama Chochote Cha Upinzani...Umedharaulika Sana Balozi'

0
0
Balozi Juma Mwapachu alipoondoka ccm hakujiunga na chama chochote cha upinzani.
Alibaki NEUTRAL.

Kwa akili yake finyu alidhani viongozi wa chadema watamfuata ili kumwomba ajiunge na chama chetu.

Baada ya kuona hakuna chama kinachomuhitaji,akaamua arudi alikotokea unless otherwise njaa ingemuua na family yake.

Alidhani labda watu wanaoondoka ccm na kutangaza kuisupport chadema wanapewa hela na uongozi wa Chadema kumbe laa.

Huku wamejaa Makamanda tupu hakuna mtu anayeipigia serikali goti kuomba kuishi...bali ni wajibu wa serikali kutekeleza wajibu wake kwa Wananchi...Pole sana huku ni Ukamanda wala hakuna wakukufata ujiunge na Chama...Daaah umedharaulika san Balozi....

Rais Magufuli Akerwa Na Mikataba Mibovu Ya Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL....Aeleza Kilichomfanya Amrudishe Profesa Muhongo Wizara ya Nishati

0
0
Rais John Magufuli jana aliitaja kampuni ya kuzalisha umeme ya IPTL wakati akizungumzia matatizo yanayosababishwa na kununua umeme unaozalishwa na mitambo ya kukodi na kupiga marufuku mikataba hiyo.

Rais pia alipuuzia shutuma zinazorushwa dhidi ya Profesa Sospeter Muhongo, ambaye alijiuzulu wadhifa wa Waziri wa Nishati na Madini kutokana na sakata la IPTL, akisema “wakati mwingine vitu vizuri hupigwa vita” na hivyo amemrejesha mbunge huyo wa Musoma Vijijini kwenye wizara hiyo kwa sababu ya uchapakazi na si siasa.

 Tangu aingie madarakani, Rais Magufuli amekuwa akifichua kashfa za ufisadi ambazo hazikuwahi kujadiliwa vikali katika utawala uliopita, lakini jana alitoa mfano wa IPTL kama moja ya mikataba iliyoisababishia Serikali matatizo.

Kashfa zilizoikumba sekta hiyo ni pamoja na mkataba wa uzalishaji umeme na kampuni ya Richmond Development iliyodhihirika baadaye kuwa haikuwa na uwezo, uchotwaji wa zaidi ya Sh300 bilioni kutoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyohusisha IPTL, mikataba ya ununuzi umeme kwa bei kubwa kutoka kampuni binafsi na ununuzi wa umeme kutoka mitambo ya kukodi.

“Ni matumani yangu kuwa sitasikia tena mnaleta mapendekezo kwamba tunataka kuongeza mkataba huu au tunataka kukodi mtambo huu.Suala la kukodi likalegee, lizimie na life kabisa huko,” alisema Rais Magufuli wakati akizindua ujenzi wa kituo cha umeme cha mradi wa Kinyerezi ll utakaokuwa ukizalisha megawati 280 kwa mwaka jijini Dar es Salaam jana.

“Hayo mawazo yafe, sasa tuwe na mawazo ya kujenga mitambo yetu. Cha kuazima ni kibaya. Hivi sasa vya kukodi na vya kuazima achaneni navyo. Nendeni na mawazo ya kujenga mitambo yetu.

“Tumechoka kuchezewa. Kuna miradi hapa ya hovyo kweli. Kila siku inazaa matatizo. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri (Muhongo) lisimamie hilo. " Alisema Rais Magufuli

Alisema Profesa Muhongo akipata ushauri kutoka kwa wataalamu wake kuhusu miradi ya kukodi mitambo, atambue kuwa hawafai. “Ujue huyo si mtaalamu mzuri, ikiwezekana mtoe. Wataalamu wako wakuletee mawazo ya kujenga mitambo yetu,” alisema.

Rais Magufuli alisema ni lazima ufike wakati Tanzania iwe na umeme wa uhakika tena wa kujitegemea.

 “Si umeme kwa kukodisha- kodisha. Umeme ni wa kutumia watu. Na ndiyo maana kumekuwa na matatizo mengi. Mara IPTL mara nini. Ni kwa sababu tulizoea umeme wa kukodisha kwa wafanyabiashara,” alisema.

Kampuni ya IPTL iliingia kwenye mgogoro na Serikali baada ya kudaiwa kuwa inaitoza Tanesco tozo kubwa gharama za uwekezaji kuliko makubaliano ya mkataba.

Wakati wa kashfa ya escrow, zaidi ya Sh300 bilioni zilizokuwa zimewekwa kwenye akaunti hiyo kusubiri kumalizika kwa mgogoro wa kimkataba baina ya IPTL na Tanesco zilichotwa na kuonekana zikiingia kwenye akaunti za mawaziri, majaji, wabunge na watumishi waandamizi wa Serikali, jambo lililolifanya Bunge limlazimishe Profesa Muhongo awajibike kwa kushindwa kusimamia fedha za Serikali.

 Profesa Muhongo alijiuzulu, lakini akateuliwa na Rais Magufuli kurudi kwenye nafasi hiyo na jana mkuu huyo wa nchi hakusita kummwagia sifa.

 “Wizara ya Nishati mmenifurahisha sana. Tuachane na mitambo ya kukodi. Tumechoka kufanya biashara na wawekezaji wa ajabu ajabu. Halafu tunalipia capacity charges za ajabu na umeme unakuwa juu. Tunawapa shida Watanzania wa maisha ya chini,” alisema Magufuli.

“Nendeni kwa kasi ya hapa kazi tu. Na ndiyo maana niliamua kumrudisha Profesa Muhongo hapo. Wakati mwingine vitu vizuri vinapigwa vita. Sichagui mwanasiasa. Mimi nataka mtu mchapa kazi. Maendeleo hayana chama.”

Akizungumzia ujenzi wa kituo cha Kinyerezi ll utakaogharimu dola 344 za Marekani (sawa na Sh688 bilioni), Rais alisema amefarijika kuona ndani ya muda wake mfupi akiwa madarakani amealikwa kuweka jiwe la msingi kwenye mradi huo.

 Alisema Serikali ya Japan ilitoa dola 292 milioni za Marekani na Tanzania ilitakiwa kutoa dola 52 milioni za Marekani sawa na asilimia 15, lakini ikashindikana na kutakiwa wasubiri.

“Baada ya makusanyo kuimarika tulipoingia madarakani mwezi Novemba na Desemba mwaka jana, tulitoa maelekezo na hizo dola 52 milioni sawa Sh110 bilioni za Tanzania na zikapatikana ndiyo maana leo tupo hapa kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi huu kuanza,” alisema.

 “Hivi sasa tuna uwezo wa kuzalisha megawati 1,200 hadi 1,500 za umeme kwa mwaka. Sasa tumefikia 1026. Hiyo ina maana kuwa kila Mtanzania kwa sasa anatumia wastani wa wati 30 kwa mwaka,” alisema.

Pia alisema amefurahi kupata taarifa kuwa mradi ya Kinyerezi l utaongezewa uwezo wa uzalishaji kutoka megawati 150 hadi 335.

“Nimeambiwa mkandarasi anataka dola 20 milioni za Marekani (sawa na Sh 40 bilioni). Sasa kama tuliweza kutoa hela kwa ajili ya Kinyerezi II, hatuwezi kushindwa kuongeza kwa ajili ya Kinyerezi l. Hiyo hela tutatafuta hata mwezi huu tutampa,” alisema.

Jokate Mwegelo Afunguka "Nangoja Edward Lowassa Kurudi chamani CCM Kama Mwenzake..."

0
0
Kupitia account yake ya twitter Jokate ameandika ujumbe mfupi na kusema anasubiri EL kurudi chamani "Waiting on EL kurudi chamani".

Ujumbe huu wa Jokate umekuja masaa machache baada ya Balozi Mwapachu kutangaza kurudi rasmi leo katika chama chake hicho cha CCM na jambo hili limepokelewa tofauti na baadhi ya mashabiki wa ukurasa wa facebook wa East Africa Radio, wapo wanaompongeza na wapo wanaombeza.

"Huyo CCM mwogopeni kama ukoma, tatizo lake anahangaika kutafuta madaraka, anasaliti huku na huku ndio wanaosababisha uhasama katika nch,inatakiwa achukiwe kila mahali" aliandika Daud Mwakyeja.

Na upande wake Emmanuel Mwakyusa alikuwa na haya ya kusema "Duuuuu angekuwa baba yangu ningemwambia kitu kwa vile sio nampotezea, msomi mzima kubadili msimamo miezi miwili ni aibu hana uzalendo wala thamani ya uelewa tuwakatae kina Mwapachu hawana msaada 'Edo' inaonekana thabiti hajarudi nyumba kuliko Mwapachu".

Kiongozi wa CUF Aliyetangaza Kuwa Wafuasi wa Chama Hicho Wamekimbilia Porini Akamatwa na Polisi

0
0

Ikiwa ni siku tatu tangu Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa Chama cha Wananchi (CUF), Hamad Masoud Hamad, atangaze kuwa baadhi ya wananchi wa Zanzibar wanakimbilia porini kuhofia usalama wao, ametiwa mbaroni.


Kukamatwa kwa Masoud sasa kunafanya idadi ya viongozi wa chama hicho waliotiwa mbaroni na kuhojiwa polisi kufikia wanne tangu kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka jana.


Viongozi wengine waliohojiwa na Polisi na kuachiwa kwa dhamana ni Naibu Katibu Mkuu, Nassor Ahmed Mazrui, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Omar Alin Shehe na mshauri wa mikakati wa chama hicho, Eddy Riyami.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkadam Khamis Mkadam, jana alithibitisha kukamatwa kwa Masoud, ambaye ni Waziri wa zamani wa Miundombinu na Mawasiliano katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa.


Alisema kiongozi huyo alikamatwa na kitengo cha upelelezi nyumbani kwake mtaa wa Mbweni mjini Zanzibar jana.


Alisema kwa sasa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Mwembe Madema ili kusadia uchunguzi juu ya taarifa alizotoa katika mkutano wake na waandishi wa habari na kuzungumzia hali ya amani ya Zanzibar na wananchi wake.


“Tunamshikilia kwa uchunguzi, kuna mambo ya msingi tunaona yanahitaji kufanyiwa uchunguzi na yeye kusadia polisi uchunguzi wake,” alisema Mkadam.


Kufuatia kukamatwa huko kwa Masoud, CUF imelaani kitendo hicho na kusema kuwa kamata kamata hiyo inawalenga viongozi wa chama hicho na wanachama wake pekee.


Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Mazrui alisema matukio yote ya uvunjifu wa amani yaliyotokea visiwani hapa, yamekuwa yakihusishwa  na CUF na Jeshi la Polisi huwakamata viongozi wa chama hicho pekee.


“Tunasema huu ni uonevu wa hali ya juu, maana viongozi na wafuasi wa CUF pekee ndio wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi, hii yote inatokana na uchaguzi wa marudio, hivyo  kutoshiriki kwetu kwa uchaguzi isiwe sababu ya kuadhibiwa,” alisema.


Aidha, alisema suala la kushiriki au kutoshiriki katika uchaguzi ni hiari ya mtu, hivyo kwa wale ambao hawatashiriki uchaguzi huo, wasiadhibiwe wala wasidhalilishwe na wale ambao wametangaza kushiriki waende wakapige kura.


Kwa upande wa mke wa Masoud, Rahma Issa, alisema askari kazu wasiopungua sita wakiwa na silaha za moto mbili walifika nyumbani jana saa moja asubuhi na kudai wanamhitaji mumewe.


Alisema baada ya kubisha hodi, kijana wake mmoja alifungua mlango na kisha askari watatu waliingia ndani mmoja akiwa na silaha ya moto kifuani.


“Baada ya kuamshwa na kutoka chumbani walimwambia yupo chini ya ulinzi anahitajika kituo cha polisi,” alisema Rahma.


Hata hivyo, alisema baada ya kumkamata, hawakumwambia sababu ya kukamatwa kwake, lakini baada ya kuwauliza wanampekeka kituo gani walimwabia Kituo cha Polisi Mwembe Madema, Zanzibar.


Naye Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF, Omar Ali Shehe, alisema vitendo vya kukamatwa viongozi wa CUF ni mwendeleo wa Serikali ya CCM kuwanyanyasa viongozi na wanachama wake chama hivyo visiwani hapa.


Alisema vitendo vnavyoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi vinakwenda kinyume cha misingi ya demokrasia na haki za binadamu.


Shehe alisema matunda ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya kujenga amani na umoja wa kitaifa yameanza kuvurugwa tangu kuingia mgogoro wa uchaguzi mkuu.
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live




Latest Images