Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Watupwa Jela Miaka 60 Kwa Kukutwa Ngozi za Chui na Chatu

$
0
0
Mahakama ya Mkoa wa Manyara imewahukumu watu watatu kifungo cha miaka 60 jela kwa kosa la kukutwa na nyara za Serikali, ikiwamo ngozi ya chui na nyoka aina ya chatu.

Washtakiwa hao ni Mathayo Mchono, Bura Massay, wakazi wa Gembaku wilayani Mbulu na Bryson Jacob wa Bashey wilayani Karatu.

Hakimu Bernad Nganga amesema leo kuwa mahakama hiyo imetoa hukumu hiyo baada ya ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka kuwatia hatiani washtakiwa hao.

Hakimu Nganga amesema kila mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka 20 gerezani.

Awali, waendesha mashtaka, Linus Bugaba na wakili wa Serikali, Timotheo Mmari waliiomba mahakama itoe adhabu kali iwe fundisho kwa wengine.

Ilidaiwa kuwa washtakiwa hao walikamatwa Novemba 30, 2014 eneo la Kilima Punda wilayani Mbulu wakiwa na ngozi ya chui yenye thamani ya Sh6.3 milioni na ya chatu ya Sh648,000.    


Wenje Apasua Kichwa Mawakili wa Serikali Kesi ya Kupinga Matokeo Mwanza...

$
0
0
Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi katika jimbo la Nyamagana, jana iliahirishwa kwa mara nyingine, baada ya kutokea mvutano wa kisheria baina ya mawakili wa mlalamikaji, Hezekiah Wenje na wale wa mlalamikiwa, Stanslaus Mabula na wa serikali.

Hali hiyo ilitokea baada ya mawakili wa serikali wakiongozwa na Vincent Tangoh na wale wa Mabula, kupinga mahakama kupokea fomu namba 21B, ambacho kinaonyesha idadi ya kura katika vituo 693.

Wenje alitoa kielelezo hicho kama ushahidi, baada ya kumaliza kutoa ushahidi alipokuwa akihojiwa na wakili wake, Elias Hezron, hatua iliyozusha ubishaji wa kisheria kwa takriban saa mbili huku mawakili wa mlalamikiwa wakivikataa.

Ubishani huo wa kisheria, ulitokana na jopo la mawakili wa serikali,  liliongozwa Wakili Tangoh pamoja na mawakili wa Mabula, Constantine Mutalemwa na Faustine Malongo, kugoma kupokea vielelezo hivyo kwa madai kuwa kisheria shahidi hatakiwi kuviwasilisha mahakamani hapo.

Hali hiyo ilisababisha, mawakili wa Wenje, Daya Outa na Hezron, kusimama kidete kutetea sababu za mteja wao kuwasilisha ushaidi wa fomu hizo No. 21B mahakamani.

Kutokana na ubishani mkubwa wa kisheria, Jaji Kasukulo Sambo,  aliamuru kesi hiyo iahirishwe hadi Jumanne ijayo, atakapotoa uamuzi iwapo shahidi huyo aendelee kutoa ushahidi wake mahakamani au la.

Awali, Jaji Sambo, alianza kutoa uamuzi ya pingamizi dogo la kupinga aya ya vipengele vilivyokuwamo kwenye utetezi wa Wenje, huku akikubaliana na wakili Tangoh, kuondoa aya tatu zilizokuwamo kwenye ushahidi huo lakini akipinga kuondoa aya zingine tatu zilizopingwa na Mutalemwa.

Wakati hayo yakiendelea, Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Mwanza, jana kililituliza jiji la Mwanza kwa muda, baada ya  kusambaratisha makundi ya wafuasi na wanachama wa Chadema, waliokusanyika kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.

FFU hao, waliotanda katika mitaa mbalimbali ya jiji la Mwanza, walikuwa na lengo la kutibua vikundi vya wafuasi hao waliokuwa wamesimama makundi makundi.

Hata hivyo, FFU hao ambao mara nyingi hutumia mabomu ya kutoa machozi, jana waliamua kutumia fimbo na virungu, licha ya gari la maji ya kuwasha (washawasha) kurandaranda mitaani.

Ulinzi huo mkali uliowekwa mitaani, pia ulionekana katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, baada ya watu waliotakiwa kuingia mahakamani hapo kuulizwa maswali na askari.

Rais Magufuli Anasa Wauza Madawa ya Kulevya 3,000 Kimyakimya.....

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, amesema ikiwa ni miezi mitatu tu tangu aingie ofisini baada ya kuteuliwa Desemba 10, mwaka jana na kuapishwa siku mbili baadaye, mpaka sasa tayari watu 3,000 wamekamatwa kwa tuhuma za kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.

Kauli hiyo ya Waziri Kitwanga inakuja ikiwa ni siku chache tangu Ofisi ya Hazina inayoshughulikia udhibiti wa mali za nje ya Marekani (Ofac), kutangaza kushikilia mali za raia wa Tanzania, Ali Khatib Haji Hassan maarufu kama ‘Shkuba’, zilizo nchi mbalimbali, kutokana na kumtuhumu kuwa ndiye msambazaji mkubwa wa dawa hizo kutoka Afghanistan kwenda barani Asia, Marekani na eneo kubwa la Afrika.

Wakati Marekani ambayo pia imepeleka suala hilo kwenye Bunge la Congress tangu ilipotoa taarifa hiyo, Bodi ya Kimataifa ya Kudhibiti Dawa za Kulevya (International Narcotic Control Board – ICBC), nayo ilitoa ripoti ya mwaka 2015 iliyolenga Afrika na Tanzania, ikionyesha kuwa Tanzania ni kichochoro cha kupitisha dawa za kulevya zinazosambazwa karibu nusu ya dunia.

Akizungumza na Nipashe katika mahojiano maalum, Kitwanga alisema:

“Kama utakumbuka mara tu nilivyoteuliwa, nilisema suala la dawa za kulevya tutapambana nalo na siogopi kufa, nilisema na narudia tena siogopi kufa, hili ni suala la kufa au kopona.

“Hatutakubali tena Tanzania iingize dawa za kuleva au iwe njia ya kupitishia kwenda sehemu nyingine, au hata kama soko, kikubwa tunachokifanya sasa ni kujenga mifumo itakayozuia kabisa dawa kuingia nchini kwetu na zile zilizopo zitafutwe na zikamatwe, ndiyo sababu tunasema tumekamata watu wengi sana kwa muda mfupi sana ili kuhakikisha dawa za kulevya hazipitishwi hapa Tanzania.”

Alipoulizwa idadi ya watu waliokamatwa, Kitwanga alisema: “Kwa muda niliokaa hapa, zaidi ya watu 3,000 wamekamatwa, kuna wakubwa sana, wakubwa wa kati, wale wanaopokea tumewakamata zaidi ya 20, wanaosambaza tumekamata zaidi ya 100 na wale wanaouza kidogo kidogo ndiyo wengi zaidi." na kuongeza:

“Lakini bado tunaendelea na sasa hivi siyo suala tu la kwamba tukukamate na dawa za kulevya, tunakwenda mbali zaidi kwamba ukitajwa au tukikuhisi, tuone na utuhakikishie kwamba wewe kweli siyo muuza dawa za kulevya.

“Kuhisiwa tu ni kwamba lazima tufanye uchunguzi wetu utuhakikishie kuwa wewe siyo muuza dawa za kulevya.”

Akizungumzia mkanganyiko wa kauli aliyonukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa ana orodha ya majina ya wauza dawa za kulevya, Kitwanga alisema alinukuliwa vibaya.

“Watu walininukuu vibaya, ile ya kwamba nayajua (majina ya wauza dawa), huwezi ukawajua wote, hata ukijua, utajua kidogo tu, kinachotakiwa ni kuweka mfumo wa kufumua kila kitu, na huo ndiyo tumeuweka na tunaendelea kuuimarisha,” alisema na kuongeza:

“Nilisema jamani mimi sijapewa orodha, na siijui orodha, mimi ninachotaka kutengeneza ni kujenga mfumo utakaohakikisha kwamba dawa za kulevya haziingii na zilizopo ndani zinakamatwa na wahusika wote wanakamatwa wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.”

Alipoulizwa kama alipoingia ofisini alikuta orodha ya  wauza dawa za kulevya na majangili ambayo kiongozi mmoja wa serikali ya awamu ya nne alisema anayo, Kitwanga alisema yeye haangalii orodha, kazi yake ni kuwasaka wauza dawa hizo tu.

“Mimi nadhani sikumbuki sana, lakini nakwambia sasa hivi, sisi siyo suala la orodha, sisi ni suala la kuwasaka, kuwakamata na tutaendelea na hii siyo ya siku moja, siyo ya siku mbili ni endelevu, niwapo wizarani mimi, nisiwapo wizarani, kwa sababu tunajenga mfumo,” alifafanua Kitwanga.

Alisema kazi yake ni kujenga mfumo utakaohakikisha dawa za kulevya haziingia nchini na kwamba mfumo uliokuwapo awali ulikuwa dhaifu kidogo.

Mwanamuziki Diamond Platnumz Akanusha Kumpima Tiffah DNA....Adai Kupima DNA ni Kutojiamini

$
0
0
Mkali wa muziki wa Bongo fleva hapa nchini, Nasib Abdul aka Diamond Platnumz, amekanusha tetesi zakwenda kumpima mtoto wake Latiffah 'Tiffah' vinasaba 'DNA' ili kupata uthibitisho wa kuwa ni mwanawe au sio mwanae.

Diamond amezungumza hayo baada ya kufanyiwa mahojiano na eNewz kuhusiana na tetesi hizo ambapo alikanusha suala hilo, Diamond Anasema kumpima mtoto wako DNA ni kutojiamini na yeye hawezi kufanya hivyo, Diamond anasema alianza kumjua Tiffah akiwa tumboni.

Pia Diamond ameweka wazi kuwa picha inayomuonyesha akilia ni ya show yake ya Dar Live.

UVCCM Wapinga Balozi Juma Mwapachu Kurejea CCM.....Wataka Waliompokea Watimuliwe

$
0
0
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi wilayani Hai (UVCCM),Arnold Swai amepinga ya kurejea ndani ya chama hicho kwa mwanadiplomasia na mwanasiasa mkongwe nchini, Balozi Juma Mwapachu.

Balozi Mwapachu, juzi alitangaza kurejea CCM kwa madai ya kuridhishwa na utendaji wa Rais Magufuli.

Akizungumza na wanahabari jana mkoani hapa,Swai alisema kuwa chama hakipaswi kumpokea mwanasiasa huyo kwa madai kuwa ni msaliti huku akienda mbele zaidi na kutaka waliompokea wachukuliwe hatua za kinidhamu kwa mujibu wa kanuni za chama.

"Ni lazima tujiulize, hivi mwanadiplomasia huyo angekuwa tayari kurejea CCM kama mgombea urais wa UKAWA, Edward Lowassa angeshinda urais?" alihoji na kuongeza:

"Hatuwezi kumpokea msaliti  kama  huyu, wakati chama kilipokuwa kwenye mapambano aliondoka tena kwa kejeli, leo chama chetu kimesimama imara chini ya mwenyekiti wetu Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ndio anarudi na wimbo uleule kwamba chama kimemlea, haikubaliki."

Alisema wakati wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,baadhi ya makada maarufu wa CCM walikisaliti chama huku wakitoa kauli za kejeli na kusababisha mpasuko ndani ya chama ambao majeraha yake hayajapona.

Mwenyekiti huyo alieleza kukerwa na kauli  ya Balozi Mwapachu kwamba chama ndo kimemlea na kwamba hayo si maradhi ya kumuua mtu bali yanatibika, lakini dhambi ya usaliti haitibiki

"Nguvu kubwa iliyotumiwa na CCM kuwanadi wagombea wake ilisababishwa na wasaliti kama hawa,nawaomba viongozi wa ngazi za juu kutofumbia macho jambo hili kwani ni hatari kwa ustawi wa chama chetu." Alisema

Balozi Mwapachu alirejea CCM juzi na kupokelwa na mwenyekiti wa CCM kata ya Mikocheni jijini Dar es Salaam, Athuman Mareenda, ambaye alimkabidhi tena kadi ya uanachama wa chama hicho.

Mashauzi Yanapoteza Wasanii Wengi-Diamond Platnumz

$
0
0
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Diamond Platnumz amedai kuwa mafanikio yake kimuziki na kuzidi kuendelea kufanya vizuri ni kutokana na ukweli kwamba yeye si mtu wa starehe na wala si mtu wa mashauzi kutaka kufanya vitu ili kuwaonesha watu, bali yeye amekuwa akitunza pesa anazofanya na kufanya mambo ya msingi ndiyo maana labda anazidi kufanikiwa kimaisha pamoja na sanaa.

"Unajua wasanii wengi wanapoteza na kushuka kimuziki sababu ya starehe pamoja na mashauzi, unakuta mtu amepata mafanikio kidogo anaanza mashauzi na kufanya starehe zisizo na tija, ndiyo maana mimi huwezi kuniona kwenye starehe hata wasanii wa WCB ni hivyo hivyo" alisema Diamond Platnumz.

Katika hatua nyingine Diamond Platnumz amemwelezea msanii Shettah na kusema ni mfano mzuri kwani Shettah na yeye wanazijua pesa hivyo ni wabahili sana wanaweza kutoka kufanya show na ukiwapiga kizinga cha pesa watakwambia kuwa hawana pesa.

'Mimi namkubali sana Shettah kwani jamaa ni bahili sana anaweza kutoka kufanya show na akakwambia sina pesa, hata gari yake aliyonunua juzi amenunua kwa pesa zake sababu anakusanya pesa zake na kufanyia vitu vya msingi, saizi Shettah anajenga nyumba yake na hiyo yote sababu si mtu wa mashauzi na wala si mtu wa starehe"Alisema Diamond Platnumz

Serikali Kutoa Mil.50 kwa Kata Zote Maskini Nchini

$
0
0
Mkurugenzi Dawati la Wazee Tume ya Utumishi na Utawala Bora nchini Tanzania Bw. Joshua Tarimo amesema Serikali imeahidi kutoa shilingi milion 50 kwa Kata zote nchini lengo likiwa ni kupunguza umaskini hasa kwa wazee wasiojiweza kujikimu katika kupata mahitaji yao ya kila siku.
Bw.a Tarimo ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na wazee kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa lengo lakuwasikiliza mikakati yao na mipango ambayo wanataka itekelezwe na kusimamiwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dk. John Magufuli.

Serikali imeahidi kutoa shilingi Milion 50 kwa Kata zote nchini lengo likiwa ni kupunguza umaskini hasa kwa wazee.
Mkurugenzi Dawati la Wazee Tume ya Utumishi na Utawala Bora nchini Tanzania Bw. Joshua Tarimo amesema Serikali imeahidi kutoa shilingi milion 50 kwa Kata zote nchini lengo likiwa ni kupunguza umaskini hasa kwa wazee wasiojiweza kujikimu katika kupata mahitaji yao ya kila siku.
Bw.a Tarimo ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na wazee kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa lengo lakuwasikiliza mikakati yao na mipango ambayo wanataka itekelezwe na kusimamiwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dk. John Magufuli.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Shirika la Saidia Wazee Tanzania SAWATA Bi. Clotilda Kokupima amesema bado wazee nchini wanakabiliwa na wanachangamoto kubwa sana ya kukosa haki zao kwa kutokuwepo kwa Sheria na Sera maalum ambazo zitalinda na kusimamia haki za wazee nchini na pia kuitaka Serikali itoe elimu ya ziada kwa jamii kuhusu imani potofu walizonazo juu ya wazee nchini.

Bi. Kokupima amesema katika tafiti walizofanya wamegundua kila siku Tanzania wanakufa wazee 283 kwa sababu ya kukosa huduma muhimu za kibinadamu hivyo Serikali inapaswa kuanza kuwatambua wazee nchini na kuwahudumia.

Mwanamke Aliyeoa Wanaume Wawili Afariki Dunia

$
0
0
MKAZI wa Kijiji cha Ikondamoyo, Wilaya ya Mlele mkoani Katavi, Veronica Salehe (54), aliyeoa wanaume wawili kwa kipindi cha miaka tisa amefariki dunia.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ikondamoyo, John Maganga, alisema Veronica alifariki dunia wiki iliyopita mkoani Tabora alikokuwa amekwenda  kupatiwa matibabu kwa kaka yake.

Maganga alisema kuwa ndoa hiyo iliwezeshwa na mume mkubwa ambaye alikubali kuishi na mume mdogo.

Alisema kuwa Veronica ndiye aliyewaoa wanaume wote wawili na kuishi nao kwa miaka tisa, na kwamba ndiye aliyekuwa na amri kuu katika nyumba yao.

Aliwataja wanaume hao kuwa ni Paulo Sabuni (62) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (47).

Maganga alisema Veronica na mume wake mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita wakitokea Kijiji cha Usumbwa, mpakani mwa Chunya na Tabora.

“Baada ya kufika kijijini hapa, walianza kujishughulisha na shughuli za kilimo na biashara ya kuuza pombe za kienyeji aina ya komoni,” alisema Maganga.

Katika uhai wake, Veronica alibahatika kupata watoto wanne, kati yao wawili wa kike.

Maganga alisema mtoto mdogo wa kiume, ni wa mume mdogo ambaye ana miaka tisa, anayesoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Ikondamoyo, na watoto wengine watatu ni wa mume mkubwa.

Kuhusu maisha ya Veronica ya kuishi na wanaume wawili, Maganga alisema haikuwa siri kijijini hapo kwa sababu walizoeleka kwa wanakijiji.

Alisema mume mdogo alikuwa anaishi kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake, lakini alikuwa akishinda kwa mume mkubwa ambako kulijulikana zaidi kwa jina la ‘nyumba kubwa’.

“Mambo ya kula, kunywa na mengine, mama   alikuwa akiwapangia zamu kama afanyavyo mume mwenye wake wengi,” alisema Maganga na kuongeza kuwa wanaume hao walikuwa wanaridhika na kufurahia maisha.

Alisema siku mama akichoka kupika, mume mdogo alikuwa akiingia jikoni na kuwaandalia chakula watoto na mume mkubwa maji ya kuoga.

Wakati wa mazishi, wanaume wote walishiriki shughuli zote, jambo ambalo limeacha maswali mengi kwa jamii.

Akizungumzia msiba huo, mume mkubwa alisema kuwa amepata pigo kubwa kwa sababu alikuwa anasaidiwa mno na marehemu Veronica kutokana na biashara zake za pombe za kienyeji ambazo zilisaidia kuendesha maisha ya kila siku.

“Veronica aliugua muda wa miezi miwili, nilikuwa namplekea Kituo cha Afya Urwila kupata matibabu, lakini Mungu kampenda zaidi,” alisema.

Watoto wa Mastaa wa Bongo Wanaotabiriwa Kuja Kuwa Mastaa Kama Wazazi Wao Hawa Hapa

$
0
0
Kila mtoto anapozaliwa huanza kumuangalia mzazi wake kama ni role model wake, lakini baadaye wengi huanza kubadili mawazo yao.


Mastaa wa Bongo wameanza kuwatengenezea mazingira watoto wao ya kutembelea nyota za wazazi wao ili watengeneze hela kuanzia sasa mpaka hapo baadaye.

Hawa ni baadhi ya watoto wa mastaa wanaotabiriwa kuja kuwa mastaa baadaye, wengine wanaweza wakawa na majina makubwa kuliko ya wazazi wao.

Latifa Nasibu (Tiffah)

Mpaka sasa ana umri wa miezi saba na siku kadhaa, Tiffah amekuwa ni staa pia ana followers kibao kwenye akaunti yake ya Instagram. Kutokana na umaarufu aliokuwa nao baba yake, Diamond na mama yake Zari, Tiffah ameshapata dili kadhaa ambazo zinamuingizia pesa kwa sasa huku akiwa bado hajui nini kinachoendelea.

Tiffah ni balozi wa Msasani Mall & Pugu Mall, pia ni balozi wa NMB Junior Account hii ni akili pekee iliyotumiwa na Diamond Platnumz na Zari ambayo inaweza ikamfanya Tiffah akatumia fursa hiyo kuja kuingiza hela nyingi hapo baadaye na akawa maarufu zaidi duniani.

Kendrick Mabeste

Mabeste na Lisa wanajivunia kuwa na mtoto kama Kendrick, akiwa anakaribia umri wa miaka mitatu, Kendrick ameshaanza kuwa maarufu na kuingiza mkwanja wake binafsi kwa kufanya baadhi ya matangazo.

Pia Kendrick amewahi kuwa mshindi kwenye shindano la Tabasamu akiwa ni mtoto mwenye kupendeza kwenye picha (Photogenic). Nje ya kufanya matangazo watu wameanza kumtabiria Kendrick kuja kuwa rapper kama baba yake (Mabeste).

Tanzanite Hamisi

Madini ya Tanzanite yana patikana Tanzania pekee, japo nchi ya India ndiyo inaonekana ni ya kwanza kwenye kuuza madini hayo. H Baba na Flora Mvungi hawakukosea kumuita mtoto wa jina la Tanzanite, ni mmoja kati ya watoto wa mastaa wenye mvuto na wenye muonekano mzuri.

Tanzanite yupo chini ya menejimenti ya Lisa Karl Fickenscher, ambaye anamsimamia Kendrick pia. Koffie Olomide aliwahi kumweka Tanzanite kwenye Instagram yake baada ya kushinda shindano ambalo Koffie alilitoa mtu ajirekodi akiimba wimbo wa Ekotite na kuahidi atakaye shinda angewekwa kwenye Instagram yake.

Pia alipata mualiko wa kushiriki mashindano ya U miss kwa watoto ambayo yalifanyika nchini Rwanda. H. Baba aliwahi kusema “kuwa kuna matangazo mengi ambayo Tanzanite anatakiwa kuyafanya kwa sasa.”

Jenista Mhagama: Kuweni na Subira Bosi Mpya wa NSSF Mamlaka za Juu Zitakuja na Jibu...

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Walemavu), Jenista Mhagama amewataka wananchi kuvuta subira kuhusu uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa sababu mamlaka za juu zitamteua wakati mwafaka ukifika.

“Niliteua kaimu mkurugenzi wa NSSF, uteuzi ukatenguliwa kwa sababu baadhi ya taratibu zilikuwa hazijakamilika, the business is over (biashara imekwisha), tusubiri mamlaka za juu zitafanya uteuzi, mna haraka ya nini?” alihoji Mhagama.

Alipoulizwa nani anayesimamia uendeshaji wa shirika hilo kwa sasa, Mhagama alisema: “Jamani, nimeshasema tusubiri mamlaka za juu, sina cha kuongeza.”

Waziri Mhagama alimteua Dk Carina Wangwe kukaimu nafasi hiyo lakini uteuzi huo, ulidumu kwa saa tano na kutenguliwa.

Nafasi hiyo ipo wazi tangu Februari 15, baada ya Rais John Magufuli kumteua aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhani Dau kuwa balozi.

Ripoti NSSF yatia shaka

Awali, Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ilisema ripoti ya utendaji ya NSSF iliyofikishwa mbele yake haina viwango kama ambavyo mfuko huo unavyoonekana mbele ya jamii.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mohamed Omar Mchengerwa alisema taarifa zilizomo kwenye ripoti hiyo hazionyeshi miradi inayoendelezwa na mfuko huo.

“Tumeipokea na kuijadili kwa sababu ya kuheshimu kazi zinazofanywa na mfuko na uwapo wa Waziri Mhagama, vinginevyo tungewatoa nje mkaifanyie marekebisho,” alisema.

Hata hiyo, Mchengerwa aliagiza watendaji wa shirika hilo kupeleka ripoti yenye taarifa kamili ifikapo Machi 31. “Tunataka tukiisoma taarifa tunaijua vizuri NSSF, miradi yake yote na thamani yake, nyie mnatuletea taarifa fupi ambayo haina majibu ya maswali tunayoyataka,” alisema.

Katika taarifa hiyo, mfuko huo unalalamikia wanachama wengi kujitoa mara wanapomaliza mikataba na waajiri wao na kuhitaji mafao kabla ya umri wa kustaafu.

NSSF inasema kumekuwa na ongezeko kubwa la mfuko kulipa mafao wanachama wa aina hiyo na kwamba, miaka michache ijayo kutakuwa na wastaafu wengi ambao hawana mafao ya uzeeni hivyo kuwapo wazee wengi wasio na kipato.

Akifafanua hilo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori alisema kuna haja ya Serikali kurudisha sheria ya kuzuia wanachama kujitoa kabla ya kufikisha umri wa kustaafu.

Magori alisema wazee wengi ambao hawana mafao ya uzeeni wanakufa haraka, kuliko wanaolipwa mafao kila mwezi.

“Kuna takwimu zinaonyesha ukubwa wa tatizo hilo, Serikali inatakiwa kurudisha sheria na kuzuia wanachama kujitoa kwenye mifuko kwani wao wenyewe ndiyo watakaoumia uzeeni,” alisema.

Naye Waziri Mhagama aliwaagiza watendaji wa mfuko huo kutayarisha ripoti ambayo itakusanya miradi yote inayoendelezwa. 

Ukimya wa Reginal Mengi Serikali ya Rais Magufuli Wazua Maswali....Je Kaikubali ama Anaogopa....?

$
0
0
Mwenyekiti wa makampuni ya IPP huwa mwepesi sana kutoa duku duku ya msitakabali wa nchi, nakumbuka enzi zile za mzee wa msoga alikuwa akimukosoa kila siku kwa utendeji wa serikali ile, lakini inakaribia miezi minne mkereketwa huyu wa wanyonge amekaa kimya kiasi kwamba wafuatiliaji wa maswala ya siasa tumeingiwa na hofu ama Mengi anaogopa serikali hii au ameikubali serikali hii.

Watanzania tulizoea ukosoaji wake, yote aliyekuwa anamkosoa msoga sasa yanaonekana dhahiri, rais aliyepita kwa kweli bado watanzania hatujawa ilikuwepo kwa ajili ya nani, maana hii ni noma, wizi kila kona, ufisadi kila kona, ukwepaji kodi kila kona, mzee amekaa tu, sijui huko msoga anajikia vipi maana kashfa moja baada ya nyingine, mpaka naona aibu. nchi ilipotea khaa.

*****SEMA MAWAZO YAKO, MENGI KUKAA KIMYA, ANAOGOPA AU AMEKUBULI SERIKALI HII?

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda Atangaza Zawadi ya Milioni 1 Kwa Askari Polisi Atakayepambana na Jambazi na Kulishinda

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amekutana na Kamanda wa Polisi kanda maalum Simon Sirro pamoja na Askari Polisi kwa lengo la kujionea mwenendo wa jeshi hilo ambapo wamekubaliana kutoa zawadi ya milioni moja kila baada ya miezi mitatu kwa kila Askari Polisi aliyepambana na majambazi.

"Askari wetu wanafanya kazi katika mzangira magumu na wanachangamoto kubwa. Nmeona nitengeneze mfumo wa kuwapa motisha, kwahiyo nimeongea na Kamanda Sirro nimemuambia kuwa kila askari atakayeonekana amefanya vizuri mimi kama mkuu wa mkoa nitakuwa na zawadi ya milioni moja kwake kama motisha.

"Kuna watu wengi wana silaha halali na  wengine wanamiliki isivyo halali, kwahiyo tumekubaliana kuanzia leo hadi tarehe 1 aprili 2016 tunawaomba wana Dar es salaam wote waende kwenye ofisi za polisi kutoa taarifa za uhalali wa silaha zao.

"Tunataka kujihakikishia tunazo silaha ngapi katika mkoa wetu maana kuna wengine wanazitumia kinyume cha taratibu.

"Sasa olewako tukukute unamiliki silaha, tunahitaji kuliona jiji letu la Dar es salaam linaongoza kwa amani, hatutaki kuona majambazi wakipora kwenye mabenki wala kuwapora watu kwa silaha." Amesema RC Paul Makonda

Uchaguzi Zanzibar: Chama cha CUF kimewataka wanachama na wananchi wote kukaa ndani siku ya upigaji kura katika Uchaguzi wa Marudio

$
0
0
Siku ya Jumapili, tarehe 20 Machi 2016, Zanzibar itashuhudia, kwa mara nyingine tena, ubakwaji wa demokrasia kwa kufanyika kile kinachoitwa Uchaguzi wa Marudio’ kufuatia tamko binafsi la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, alilolitoa tarehe 28/10/2015 kwamba ameufuta Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25/10/2015 na matokeo yake yote.

Tangazo hilo la Jecha Salim Jecha, lililo kinyume na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11 ya 1984 na linalopingana na Katiba ya Zanzibar, lilikuja baada ya waangalizi wote wa Uchaguzi wa ndani na wa kimataifa ikiwa ni pamoja na Umoja wa Ulaya (EU), Jumuiya ya Madola (The Common Wealth), Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na Waangalizi wa Marekani na Uingereza, kutoa taarifa zao na kueleza kuridhishwa na mwenendo wa Uchaguzi huo na kwamba ulikuwa huru na wa haki kwa sababu ulifuata taratibu za kisheria na ulifanyika kwa amani.

Aidha, baada ya kukamilika kwa hatua ya upigaji kura, wadau na washiriki wa ndani wa uchaguzi huo akiwemo, yeye mwenyewe, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Dk. Ali Mohamed Shein, mgombea wa Urais wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na wagombea kutoka vyama vyengine walikiri kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.

Ghafla, kutokana na shindikizo kubwa kutoka kwa viongozi wa Chama chake, ambacho aliwahi kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge kupitia chama hicho na kuanguka katika hatua ya kura za maoni, Mwenyekiti wa Tume alitangaza kuufuta Uchaguzi huo kwa kutumia hoja na maelezo yaliyotolewa na CCM baada ya kubaini imeshindwa kwenye nafasi ya Urais wa Zanzibar.

Tokea kutolewa kwa tangazo hilo kumekuwepo na juhudi mbalimbali ndani na nje ya nchi za kutafuta suluhisho kutokana na mgogoro ulioibuliwa kwa makusudi kwa lengo la kukinusuru Chama Cha Mapinduzi CCM kuondokana na aibu ya kushindwa katika Uchaguzi Mkuu wa 25 Oktoba 2015.

Miongoni mwa juhudi za ndani ni pamoja na Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kukutana na viongozi mbalimbali akiwemo mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dr. Ali Mohamed Shein, Marais wastaafu wa Zanzibar, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli na Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete ili kufanya mazungumzo na kuiepusha nchi kutokana na migogoro na mifarakano ya baada ya uchaguzi. Viongozi wa dini mbalimbali nao pia walichukua dhamana na dhima ya kuhakikisha kuwa mgogoro wa Zanzibar unapatiwa ufumbuzi kwa lengo la kuibakisha Zanzibar katika hali ya umoja na masikilizano miongoni mwa wananchi wake.

Kwa upande wa juhudi za nje, jumuiya ya kimataifa imesikika mara kadhaa ikitoa matamko na kuchukua hatua mbalimbali kuitaka Tume ya Uchaguzi kukamilisha kazi ya uhakiki na majumuisho ya matokeo ya uchaguzi na kumtangaza mshindi.

Jumuiya hiyo pia iliushauri uongozi wa vyama vya CCM na CUF kukaa pamoja kuzungumza jinsi ya uundwaji na uendeshaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar kama yalivyo matakwa ya Katiba ya Zanzibar na kuhakikisha kuwa demokrasia, haki za binadamu na amani vinaenziwa, kulindwa na kutunzwa.

Kwa makusudi na kwa lengo maalum, hatua zote hizo zimepuuzwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na Serikali zote mbili, na hatimaye Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar alitangaza kufanyika kwa kile kinachoitwa Uchaguzi wa Marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi 2016.

Kupuuzwa huko kwa juhudi za ndani na nje, kunakochochewa na baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM na Serikali zote mbili, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi) lililokutana katika kikao cha dharura tarehe 07 Novemba, 2015, mjini Zanzibar kuzungumzia hali ya kisiasa hapa nchini kufuatia Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 lilifikia maamuzi ya kuitaka Tume ya Uchaguzi, pamoja na mambo mengine, irudi kukamilisha hatua zilizobaki za uhakiki na majumuisho ya matokeo ya Uchaguzi.

Kimsingi, Baraza Kuu lilisisitiza halitakubaliana, kwa namna yoyote ile, na hatua ya kufanya Uchaguzi wa marudio kwa kuzingatia kukosekana kwa uhalali wa kisheria katika ufutwaji wa matokeo ya Uchaguzi na kwamba uchaguzi ulishafanyika na kazi ya kuhesabu kura kumalizika.

Tokea kutolewa kwa tamko la kufutwa kwa Uchaguzi, kutangazwa kwa Uchaguzi wa marudio, na kutolewa kwa Azimio la Baraza Kuu la Uongozi la CUF, Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejikuta katika taharuki na wasiwasi mkubwa na kupelekea khofu isiyomithilika kuhusiana na hali ya kisiasa na kiusalama ya Zanzibar.

Kwa mfano, kumeripotiwa matukio mengi ya uvunjwaji wa haki za binadamu ambapo raia wasio na hatia wanapigwa na kujeruhiwa vibaya, nyumba na makaazi ya watu kuvunjwa na kuchomwa moto, maeneo ya vyama vya siasa, kama vile barza za CUF, yamehujumiwa kwa kuchomwa moto na ofisi zake kuvunjwa na kuibiwa mali zote kabla ya kuwashwa moto na kuteketea kabisa.

Kwa mfano, siku ya Jumatatu, tarehe 15, Machi 2016, makundi ya askari wakiwa na silaha za moto walivamia ofisi ya Chama Cha Wananchi CUF iliyopo katika eneo la Mpendae na kuvunja na kuiba vifaa mbalimbali vya ofisi hiyo zikiwemo kompyuta, printers na photocopy machines.

Katika tukio hilo, maharamia hao walivunja eneo linalotumika kuhifadhia vifaa vya muziki na kuiba vifaa vyote vya BRASS BAND ya CUF.

Mengi ya matukio haya yamefanywa na kikundi kidogo cha askari wa vikosi vya SMZ, ambacho hutumia magari yenye namba za usajili za SMZ na silaha za moto na kujifunika nyuso zao kwa staili ya ninja kilichoandaliwa maalum kwa ajili ya kuwahujumu raia, wakisaidiwa na vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sambamba na hujuma hizi kumeibuka mtindo wa kuwatisha raia kwa kuwavamia kuwapiga na kuwabambikizia kesi kwa lengo la kuwashikilia katika vituo vya Polisi, kinyume na utaratibu wa kisheria, na kuwadhalilisha kwa kuwapiga na kuwatolea maneno ya vitisho na matusi.

Katika uvamizi uliofanywa katika ofisi ya CUF ya Mpendae, zaidi ya vijana 30 walikamatwa na jeshi la Polisi, lililoshiriki katika uhalifu huo kwa lengo la kuwapatia ulinzi maharamia waliopewa kazi ya kuhujumu ofisi hiyo, na kuwarundika katika vituo vya Polisi na kuwanyima dhamana.

Mkakati wa kuwatisha raia ulielekezwa pia kwa viongozi wa CUF. Tarehe 16 Machi 2016, Jeshi la Polisi lilivamia nyumbani kwake na kumkamata Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma, Mheshimiwa Hamad Masoud na kumuweka ndani na kumnyima dhamana.

Tukio hili la kukamatwa Mheshimiwa Hamad Masoud linafuatia kuwekwa ndani na kunyimwa dhamana kwa aliyekuwa mjumbe wa Timu ya Kampeni inayojulikana kama Timu ya Ushindi ya Chama Cha Wananchi (CUF) ndugu Mohamed Ahmed Sultan Al-Mugheir (Eddy Riyami) tarehe 16, Februari 2016 na kuitwa Polisi Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui tarehe 3 Machi, 2016 kwa kuwataka wanachi wajilinde kutokana na kushamiri kwa vitendo vya hujuma dhidi ya wafuasi wa vyama vya upinzani vinavyofanywa na makundi tuliyoyataja.

Vilevile, jana tarehe 17 Machi, 2016 aliyekuwa Mjumbe katika Timu ya Ushindi ya CUF na Mgombea Uwakilishi wa jimbo la Chukwani, Mheshimiwa Mansour Yussuf Himid, aliitwa na Jeshi la Polisi kwa madhumuni ya kuhojiwa.

Sambamba na haya, kumekuwepo na juhudi kubwa zinazoongozwa na Mamlaka mbalimbali ikiwemo Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuvishurutisha vyama vya siasa, hasa vile vilivyotangaza waziwazi kugomea Uchaguzi wa marudio, kushiriki katika uchaguzi huo kwa lengo la kuhalalisha mkakati ulioandaliwa wa kulazimisha ushindi wa CCM ambao waliukosa katika uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba, 2015.

Kwa mfano, tarehe 25 Januari, 2016, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar iliwasilisha Makao Makuu ya CUF barua yenye kumbukumbu TUZ/78/16/2015/2016/Vol.I/2 kwa lengo la kutoa taarifa kuhusu uchaguzi wa marudio.

Kutokana na barua hii, CUF, kupitia Naibu Katibu Mkuu, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui, iliiandikia Tume barua yenye kumbukumbu namba CUF/HQ/AKM/ZEC/037/016/055 ya tarehe 05/02/2016 kujibu barua ya Tume ya tarehe 4 August, 2015 yenye kumbukumbu TUZ/78/2015/2016/VOL.VI/68 na barua ya kukumbushia barua yake ya tarehe 17, August, 2015 yenye kumbukumbu CUF/HQ/AKM/ZEC/037/015/032.

Kwa barua yake ya tarehe 5 Februari, 2016 CUF iliitaarifu Tume ya Uchaguzi juu ya maazimio ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kutoshiriki katika Uchaguzi ambao umetangazwa kufanyika tarehe 20/03/2016 kwa sababu kufutwa kwa uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba, 2015 ni batili na kwa hivyo marudio ya uchaguzi wa tarehe 20 Machi 2016 ni batili pia, na ni kinyume na Katiba ya Zanzibar na Sheria ya Uchaguzi ya 1984.

Aidha, kwa barua hiyo, CUF iliitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar, kutokana na Azimio la Baraza Kuu la Uongozi, kuondoa majina ya wagombea wake wote, akiwemo Maalim Seif Sharif Hamad, katika orodha ya wagombea wa Uchaguzi huo na vile vile yasiingizwe katika karatasi za kura kwa uchaguzi wa marudio.

Zaidi, tarehe 8 Februari, 2016 Naibu Katibu Mkuu wa CUF aliwasilisha barua, kwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, iliyokuwa na lengo la kuelezea msimamo wa CUF kuhusiana na kufutwa isivyo halali kwa uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba 2015 na kuitishwa kwa kile kinachoitwa uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi, 2016.

Kwa barua hiyo pia, CUF ilibainisha mapungufu ya kisheria na ukiukwaji wa Katiba ya Zanzibar katika tangazo la kufutwa kwa uchaguzi na kwa hivyo kutothibitisha mgombea yoyote katika ngazi zote za uchaguzi wa zanzibar kama ilivyotakiwa kufanya na Tume ya Uchaguzi.

CUF iliikumbusha Tume na kusisitiza juu ya uamuzi wake wa kuitaka tume kuhakikisha haitumii jina, alama, wala picha ya mgombea yoyote kupitia CUF katika karatasi za kura.

Hata baada ya rundo la barua hizi za CUF, zenye lugha rahisi na maelezo yanayojitosheleza, kwa Tume ya Uchaguzi kukataa kushiriki katika batili iliyopachikwa jina la uchaguzi wa marudio, tarehe 29 Februari 2016, Tume ya Uchaguzi, kwa mara nyingine tena, iliiandikia CUF barua yenye kumbukumbu namba TUZ/78/16/015/016/VOL. I/200 kuitaka CUF kuwasilisha majina ya mawakala wake katika uchaguzi ambao kimsingi walishautolea msimamo.

CUF kwa upande wake ilimwandikia Mkurugenzi wa uchaguzi barua yenye kumbukumbu CUF/HQ/AKM/ZEC/037/016/056 ya tarehe 03 Machi 2016 kukumbushia msimamo wake wa kutoshiriki Uchaguzi huo na kwamba kutokana na uchaguzi huo kukosa uhalali kisheria na kikatiba, haioni haja ya kuwasilisha majina ya waangalizi kwa uchaguzi huo.

Kwa mara nyingine tena, tarehe 8 Machi 2016, Tume iliiandikia CUF barua yenye kumbukumbu TUZ/78/16/2015/2016/VOL.II/6 kutoa taarifa kuhusu kuwasili kwa karatasi za kupigia kura kwa ajili ya Uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi 2016 na kuitaka CUF kutuma majina mawili ya watakaoshiriki katika mapokezi ya karatasi hizo.

Bila ya shaka, Tume imo katika mpango wa kuilazimisha na kuishurutisha CUF, hata kama haitaki, kushiriki katika uchaguzi huo kama inavyothibika katika hatua mbalimbali za Tume hiyo ikiwa ni pamoja na kuchapicha majina, nembo na picha za wagombea wa CUF katika karatasi za kura kwa ajili ya uchaguzi wa marudio hata baada ya CUF kukataa kushiriki katika uchaguzi huo

Tukiwa tunakaribia siku ya Uchaguzi wa marudio, CUF imebaini njama kadhaa mpya zinazoratibiwa na baadhi ya viongozi wa CCM na kutekelezwa na baadhi ya watendaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.

Miongoni mwa mbinu hizo ni pamoja na kutoa vitisho kwa wafanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na askari wa vikosi vya Idara Maalum ya Zanzibar na askari wa majeshi yaliyo chini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Polisi na Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopo Zanzibar, ya kuhakikisha wanajitokeza kwa lazima katika uchaguzi wa marudio na kuipigia kura CCM.

Pia, kumekuwepo na mpango wa kuandaliwa kwa mawakala ‘feki’. Katika hili Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inashirikiana kwa karibu na kwa kiasi kikubwa na baadhi ya watendaji wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wakiwemo viongozi wa vikosi vya idara maalum, kuandaa watu, ambao wengi wao ni askari wa vikosi hivyo, watakaopewa vitambulisho vinavyowaonesha kuwa ni mawakala wa CUF, na kutumia majina ya mawakala wa CUF wa 25 Oktoba 2015, na kusambazwa katika maeneo yote ya Uchaguzi nchi nzima.

Lengo la mpango huu ni kutaka kuwahadaa wanachi kuwa CUF ilishiriki Uchaguzi kwa kuwa ilitoa mawakala walioshiriki katika Uchaguzi.

Pia, mpango huu unalenga katika kuzusha hali ya kutofautiana miongoni mwa uongozi wa CUF na wanachama wa kawaida ili ionekane uongozi wa juu wa CUF umewasaliti wananchi katika dakika za mwisho kuelekea uchaguzi wa marudio.

Kwa upande mwengine, CCM yenyewe imekuwa inaongoza mkakati maalum wa kuwatafuta baadhi ya waliokuwa mawakala wa CUF katika uchaguzi wa terehe 25 Oktoba 2015, na kuwapa fedha nyingi ili wakubali kuwa mawakala wa CUF katika uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi 2016.

Ili kuhakikisha lengo la kuwatumia mawakala hao kufanikisha mchezo wao mchafu waliouanza mara tu baada ya kufutwa kwa uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba, 2015, CCM imekuwa ikiwazaini mawakala hao wa CUF kwa ahadi mbalimbali za fedha na vitu vya thamani.
 
Kutokana na hayo yote tuliyoyaeleza kwa kina, CUF-Chama Cha Wananchi:

• Kinatoa wito kwa wananchi wote kufuata kwa umakini na ukamilifu maelekezo na kauli za viongozi wazalendo, wanaoitakia mema nchi hii kwa kuchukua juhudi kubwa kuinusuru na mifarakano ya aina zote, kususia kile kinachoitwa uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili, tarehe 20 Machi, 2016 kwa kukaa majumbani mwao kwa utulivu na kujiepusha na mikusanyiko isiyo ya lazima ili kujikinga na dhamira na matendo maovu ya kiharamia yaliyopangwa na kikundi cha wahuni wachache wa kisiasa dhidi ya raia wasio na hatia.

• Kinawafahamisha na kuwatanabahisha wafuasi wake na wananchi wengine wote walioamua kuchagua mabadiliko ya kiuongozi katika nchi yetu katika uchaguzi uliopita kwamba haijawasilisha jina hata moja la mtu yoyote kama mapendekezo yake kwa ajili ya mawakla watakaotumika katika uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi, 2016 kwa hivyo haitokuwa na wakala hata mmoja kwa ngazi yoyote katika uchaguzi wa tarehe 20 Machi, 2016. Ni muhimu kwa wanachi kuachana na propaganda zilizopitwa na wakati zinazoenezwa na CCM kuhusu mikakati ya CUF kuelekea 20 Machi, 2016.
• Mbali na kutoshiriki uchaguzi wa marudio unaosimamiwa na ZEC, pia CUF inawataka wanachama, wafuasi wake na wananchi wote kutoshiriki katika uchaguzi wa marudio katika Jimbo la Kijitoupele unaosimamiwa na Tume ya Tiafa ya Uchaguzi (NEC). CUF inawataka wananchi kususia uchaguzi huo kwa sababu kwa Zanzibar ni ZEC ndio hufanya kazi kama wakala wa NEC, hivyo hakuna haki itakayotendeka katika uchaguzi huo.

• Kinawataka wananchi wote kufahamu kuwa suala la kushiriki uchaguzi ni suala la mtu binafsi na hakuna mtu au mamlaka yoyote yenye uwezo wa kulazimisha watu kushiriki katika suala hilo. Chama kinawataka wananchi kuwa watulivu na kuondoa khofu kutokana na idadi kubwa ya askari wa JWTZ na Polisi wanaoranda randa mitaani wakiwa na silaha nzito. CUF inawaomba wananchi kubaki na msimamo wao wa kutoshiriki uchaguzi.

• Kinawasihi wale wote waliotishwa kwa kunyang’anywa vitambulisho vyao vya Mzanzibari na vitambulisho vya kupigia kura, kutotishika na hatua zinazochukuliwa sasa na watendaji waandamizi wa SMZ na mawakala wao kwa kukataa dhulma na kutumiliwa nguvu katika mambo yaliyo chini ya khiari zao. Pia, CUF inawasihi wananchi hao kuonesha msimamo wao katika kulinda na kutetea haki zao za kikatiba na kuonesha mapenzi yao kwa nchi yao kwa kukataa ukiukwaji wa Katiba na uvunjwaji wa Sheria za nchi yetu kwa kushiriki katika ukandamizaji na uvizwaji wa demokrasia nchini.

• Kinawakumbusha askari wa vikosi vyote, walio na uchungu na mapenzi mema na nchi yetu, kukataa kutumiwa na wanasiasa walioweka mbele maslahi yao binafsi na kuusahau umma wa wananchi wanyonge wa nchi hii.

 Ni vyema kwa askari hawa kutambua kuwa wao ni sehemu ya jamii yetu na kwamba shida na maisha magumu tuliyonayo yanawahusu na kuwakumba kama raia wengine wote. Kukataa kwao kuwa ngazi ya viongozi wanaotafuta hadhi na heshima kwa kupitia migongo ya wengine kutawatoa wao katika idhilali ya kutumika kila nyakati za uchaguzi zinapowadia na kutelekezwa hadi kipindi kama hicho baada ya miaka mitano ambapo hutafutwa na kupewa tena ahadi kemkem zisizotekelezwa.

• Kinamnasihi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli kutambua kuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), lililo chini ya amri yake kama Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, linaendesha vitisho kwa wananchi kutokana na kuonekana kwa wingi wakiwa na silaha nzito katika maeneo ya wananchi.

CUF inamtaka Mheshimiwa Magufuli kuondosha majeshi yake yanayoshirikiana na Polisi na vikosi vya SMZ kuendesha unyanyasaji na udhalilishaji wa raia wasio na hatia.

CUF-Chama cha Wananchi kinawataka wanachama, wafuasi wake na wananchi wote waliochagua mabadiliko ya uongozi wa kisiasa katika nchi yetu na kuonesha msimamo wao wa kuikataa CCM kupitia sanduku la kura tarehe 25 Oktoba, 2015 kutovunjika moyo na siasa uchwara zinazoendeshwa na CCM kwa lengo la kuwatoa katika mstari wa kupigania ushindi wetu mkubwa tulioupata.

Tunawahakikishia kuwa subra zao na jitihada kubwa inayochukuliwa na Viongozi wa Chama Chetu vitachochea kufikiwa kwa malengo yetu na maamuzi yao ya kuchagua mabadiliko yatazingatiwa na kuheshimiwa.

NASSOR AHMED MAZRUI
NAIBU KATIBU MKUU-CUF ZANZIBAR

Juma Jux Asema Hataki Maswali ya Vanessa na Jack...

$
0
0
Jux ameweka wazi hisia zake hizo baada ya kufanyiwa mahojiano na eNewz ambapo alisema kuwa yeye pia ni mwanamuziki kama ilivyo kwa Vanessa Mdee na kusema kuwa imejengeka kuwa kila interview anayoifanya ni lazima watu wamuulize kuhusu uhusiano wake na Vanessa na kwasasa imeibuka ya kumuuliza juu ya Jack Cliff.

Jux alishawahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na ‘video vixen’ Jack Cliff ambaye anashikiliwa nchini China kwa kukutwa na madawa ya kulevya na kwasasa staa huyo anajihusisha na mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki mwenzake Vanessa Mdee.

Jux anasema kuwa kuna mambo mengi sana ya kuzungumza kwenye interview ambayo yatakuza muziki wake mbali ya kuzungumza mambo ambayo yatakuwa hayasaidii mahusiano yake wala muziki wake.

Hii Imekaaje Kwa Kijana Wetu Diamond platnumz...Atua Ujerumani na Timu Kubwa Kutoka Tanzania..

$
0
0
Katika kile kinacho itwa From Tandale to world tour,Diamond leo ametua Ujerumani kwaajili ya kukinukishaaa!

Lakini kilicho nishangaza ni kundi kubwa la watu alio nao,Sina kinyongo nao sababu wote nilio waona wanaumuhimu wake kwa huko aliko enda lakini najiuliza malipo ya show yake Moja yatakuwa yanamlipa sana hadi anweza kufanya hivi

Nimeona yupo na Mama ake its gud kwa shida walizo pitia na mama ake sasa niwakati wao wakula mema ya dunia amefanya kitu kizuri sana,Mwingine nimemuona Mke wake na mwanae nayo haina tatizo ni kizuri kwa mapenzi alio nayo kwa mke wake na mwanae,Nimemuona Rommy Jons naye hana shida ndo official Dj apart from kuwa na undugu na Diamond,

Nimeona Babu tale na Sallaam wote ni Mamanager wake its gud nayo,Nimewaona Madancer wake wanne yaah nao ni muhimu ukizingatia kuwa wanapiga sana kazi,nimeona Maphotographer wake akiwemo Kifesi ya nimuhimu kwa picha na Video kwa mashabiki

Sasa swali langu ni kuwa hivi hizi show Diamond zinamlipa sana hadi kufikia kuwa na watu wengi hivyo ambao anawagharamia kuanzia ticket za ndege Go and return ambapo kwenda nauli inaweza kuwa zaidi ya 2M kwa kichwa kimoja,atawagharamia malazi na chakula,Kuna wanao tegemea kulipwa hapo kama madancer,Dj,na Maphotographer,bado kuna zile bata ndogo ndogo na watakaa si chini ya Siku mbili!

Inaonekana Diamond hizi show Zina mlipa sana kwa hili la leo alilo tuonesha ni salamu tosha kwa Wasanii wengine kuwa Mziki unalipa na waache kulemba kwenye Game,kumbuka apo atagharamia mavazi ya kwenye show daaaa Diamond tunyooosheee

Zaidi ya watu kumi kweli Diamond kiboko Tunyooshe

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya March 19, Ikiwemo ya Vick Kamata Afunga Ndoa

$
0
0
SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya March 19, Ikiwemo ya Vick Kamata Afunga Ndoa

Zanzibar: Mwandishi wa Habari wa Radio Deutsche Welle(DW-Swahili), Salma Said Akamatwa na Haijulikani Alipo......Hapa Kuna Mahojiano Akiwa Kusikojulikana

$
0
0
Mwandishi wa Habari wa Radio Deutsche Welle(DW-Swahili), Salma Said jana alikamatwa na watu wasiojulikana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Unguja, alipokuwa akisafiri kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia afya yake.

Akizungumzia tukio hilo jana, mume wa Salma, Ali Salim Khamis ambaye pia ni Mbunge wa Mwanakwerekwe (CUF), alisema alipata ujumbe wa maandishi kutoka kwa mkewe kwamba amekamatwa.

Khamis alisema alipokwenda uwanja wa ndege aliambiwa na mkuu wa polisi wa uwanjani hapo kwamba hana taarifa za tukio hilo jibu ambalo alilipata pia kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Mjini Magharibi.

Alisema aliamua kwenda kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa ambako pia aliambiwa hawana taarifa za kukamatwa kwa Salma. “Hadi sasa sijui mke wangu yuko wapi bado naendelea kumtafuta.”

Khamis alisema Salma alikuwa tayari amepitia taratibu zote na alikuwa akisubiri kuingia ndani ya ndege ambayo haikutajwa, lakini alisema ndege hiyo iliyokuwa iondoke saa 8.05 mchana ilizuiwa na watu hao wanaodaiwa kuwa ni askari hadi saa tisa kasoro, walipoiruhusu lakini ikidaiwa kuwa waliondoka na Salma kwenda kusikojulikana.

==> Hapo chini kuna  Mahojiano ya DW na Salma Said akiwa sehemu ambayo haijulikani

Chadema Yawafuata CCM Mahakamani....Yapinga Agizo la Jiji La Dar Kuwazuia Wananchi Kuingia Kwenye Ukumbi wa Uchaguzi wa Meya

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema hakikubaliani na agizo la serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Jiji la kuwataka wanaotakiwa kuhudhuria kwenye kikao cha uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es salaam wawe ni wajumbe pekee watakaopiga kura.

Chama hicho kimekataa agizo hilo na badala yake kinataka wananchi wote wa jiji la Dar es salaam wahudhurie katika kikao hicho.

Msimamo huo wa Chadema unapingana na barua ya wito wa mkutano wa uchaguzi huo iliyoandikwa Machi 15, 2016 na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sarah Yohana, iliyosema kuwa watakaoruhusiwa kuingia katika viwanja hivyo ni wajumbe pekee ambao ni wapigakura.

Akizungumza na wanahabari jana jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Mwita Waitara alisema sheria na kanuni zinaruhusu wananchi kushiriki kikao hicho cha wazi, hivyo Yohana hana mamlaka ya kuwazuia.

“Sisi tunafuata sheria na kanuni, barua ya mkurugenzi inaeleza kinyume cha utaratibu,” alisema.

Alisema kufuatia hali hiyo, Ukawa umemwandikia barua Mkurugenzi huyo ya kutokubaliana na matakwa yake ya kuzuia wafuasi wa vyama kuingia ukumbini wakati wa uchaguzi kwani ni uvunjifu wa sheria na kwamba hawatakubali, bali watawapigania na kuhakikisha wananchi wanaingia ukumbini.

Katika hatua nyingine, Waitara alisema CCM kwa sasa  inawaandaa wanachama feki wa CCM wakiongozwa na wakili Elias Nawela kufungua kesi ya madai huku wakitaka wajumbe 9 toka Zanzibar na 11 kutoka mikoa mingine kushiriki uchaguzi wa meya.

Alisema, ili kukabiliana nao, wameamua kuwafuata hukuhuko mahakamani  ambapo tayari wameshatuma maombi ya  kujiunga na kesi hiyo  namba 39  ya  mwaka 2016 huku wakiwa na mawakili wao ambapo inatarajiwa kusomwa Machi 21 mwaka huu katika Mahakama ya Kisutu.

Akina Masogange, Jack Wolper na Wengine....Huyu Mkongo Mwami Radjabu Sio...Anawachanganya.....

$
0
0
KUNA mshkaji anaitwa Mwami Radjabu, wadau wanamtaja kama kijana mwenye uraia wa nchi jirani ya Kongo (DRC), kwamba ni mfanyabiashara mwenye ukwasi wa kutosha. Kutokana na mkwanja wa kutosha alionao, ana ukaribu na akina dada wengi wa Kibongo, hasa hawa wenye majina katika tasnia ya filamu, wenyewe tukiwajua zaidi kama Bongo Muvi.

Leo utasikia akitajwa kama Mkongo wa Wolper au wa Masogange, kesho yake watasema ameporwa na Hamisa Mabeto, mara utasikia sasa anajirusha na Husna Maulid na ghafla watasema hivi sasa anatesa na Wema Sepetu.

Na hawa madada wote wanaotajwa, ni mastaa wetu wanaofanya vizuri katika filamu na uanamitindo. Wamecheza sinema nyingi na kwa hakika, wanao mashabiki wa kutosha kote nchini. Kuna msemo unaosema, katika msafara wa mamba na kenge wamo. Usitegemee kuwakuta mastaa wa fani fulani katika kijiwe cha peke yao.

Kilakiwanja, wanakuwepo wote, Bongo Fleva, filamu, dansi, mitindo, soka na aina nyingine zote za michezo na burudani. Kwa maana hiyo, wakati msichana mmoja anapokuwa katika ukumbi f’lani wa burudani na mtu wake, mastaa wenzake nao wanakuwepo maeneo hayo, wakifanya yao.

Hivyo inakuwa rahisi kwa mfano, mwanaume asiyejulikana anayetembea na staa, kuwafahamu mastaa wengine, kama ambavyo mastaa nao wanavyoweza kumjua ‘shemeji’ yao asiye maarufu. Hiyo inamaanisha kesho akiibuka katika ‘kiwanja’ kingine cha starehe, hata kama hakuwa na mtu wake wa jana, ataweza kukutana na shemeji zake na kuendelea na makamuzi kama kawa.

Ni hapo ndipo tabu inapotokea. Labda ni kinywaji, labda ni ofa za maisha mazuri, labda ni mapenzi, lakini kinachotokea kinakera kukisikia, kwamba mwishowa mchezo, akina dada hawa wanageukana na kujikuta wote wakiunga ‘cheni’ kwa mtu mmoja. Lakini kinachosikitisha zaidi ni kusutana kunakotokea baada ya mambo yao kufahamika.

Ooh huyu ananichukulia bwana’angu, ananifuatafuata au anikome na kadhalika. Hili siyo jambo linalopendeza kulisikia kutoka kwa watu ambao jamii inawachukulia kama kioo.
Katika zamam hizi, hivi kweli watu bado wanachukuliana mabwana? Licha ya magonjwa, lakini pia haifurahishi kuona watu tunaoamini kuwa mastaa wakipanga foleni kwa mtu, eti tu kwa sababu ana pesa.

Hii inaonesha huenda hawana njia nyingine ya kujipatia kipato zaidi ya kutegemea waleti za wanaume. Kama hivi ndivyo, niwashauri dada zangu kuachana na staili hiyo ya maisha, kwa sababu licha ya kujidhalilisha wao wenyewe, lakini pia inaleta picha mbaya kwa mashabiki na wadau wengine wanaoweza kuwazuia watoto wao kujiingiza katika fani za umaarufu, wakihofia na wao wataishi kwa kutegemea wanaume! Dada zangu kuweni makini na Mwami aliyeamua kuwadilisha kama nguo.

Tanzania yenye Neema: Madini ya Almasi Yagunduliwa Mkoa wa Singida

$
0
0
Madini ya Almasi yamegunduliwa katika mkoa wa Singida.Hayo yamesema na kamishna wa madini. Hata hivyo uchimbaji wa madini hayo mkoani hapo hayajaanza kuchimbwa.

Chanzo: Magazeti asubuhi

Rai yangu ni kwamba iwekwe mikakati thabiti kuhakikisha madini hayo yanakuwa msaada kwa watanzania sana sana mkoa wa Singida ambao ni mkoa masikini Tanzania.

Sitegemei kuona wanasiasa wanaanza kujimilikisha vitalu ili kunufaisha mitumbo yao na familia zao.
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live




Latest Images