Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

Jamani Madawa ya Kulevya si Mazuri..Tazama Jinsi Mwanamuziki CHID BENZ Alivyo Sasa....

$
0
0
 Muonekano wa Mwanamuziki Chidy Benzi Akiwa katika kituo cha Runinga cha Clouds TV....Video hii imesambaa mitandaoni ikionyesha jinsi mwili wa Mwanamuziki huyo ulivyodhoofika kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya kitu ambacho yeye mwenyewe alikuwa akipinga kuwa hatumiii...

Angalia Video Hapa:


A video posted by UDAKUSPECIALLY.COM (@udaku_special) on

Kigogo wa Madawa ya Kulevya Atiwa Mbaroni Dar.......Traffic Dar Wakusanya Milioni 577 za Makosa Barabarani ndani Ya Siku 12 Tu.

$
0
0
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo moja, akiwamo anayedaiwa kuwa kigogo wa biashara ya dawa hizo nchini.

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, juzi saa 1.15 usiku katika maeneo ya Mbezi Beach, walimkamata mtuhumiwa wa kwanza akiwa na gari baada ya kumpekua alikutwa na dawa hizo za kulevya.

Alisema walipomhoji zaidi, alidai kuwa dawa hizo siyo zake, bali za tajiri yake anayeishi Mikocheni jijini hapa ambaye wali panga kukutana naye maeneo ya Mbezi Beach kwa ajili ya kukabidhiana.

Alisema upelelezi unaendelea na utakapokamilika, watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

Kukamatwa kwa kigogo huyo na msaidizi wake ni mafanikio ya jeshi hilo ambalo hivi karibuni lilimkamata kigogo mwingine muuza ‘unga’ jijini hapa hivi karibuni.

Wakati huohuo,Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kupitia kitengo chake cha usalama Barabarani limekamata magari mbalimbali kwa makosa ya usalama barabarani

Jumla ya Tshs. 577,831,000 zimekusanywa ikiwa ni tozo kwa makosa hayo kwa mida wa siku 12, kuanzia 07/03/2016 hadi tarehe 18/03.2016.

Kamanda Sirro amewataka madereva kuwa makini na waangalifu pindi wawapo barabarani ili kuepuka adhabu zitolewazo ili vipato hivyo viwasaidie katika maisha yao ya kila siku.

Maandalizi ya Uchaguzi Visiwani Pemba Yakamilika....Wananchi Watakiwa Kujitokeza Kwa Wingi Kesho Kupiga Kura

$
0
0
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imesema maandalizi ya uchaguzi visiwani Pemba yamekamilika na kuwataka wananchi kujitokeza kesho kupiga kura na kuachana na dhana kuwa kutakuwa na vurugu.

Mwandishi wetu alishuhudia malori saba ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) yakipakia vifaa vya uchaguzi katika ofisi ya ZEC Pemba katika tukio lililowafanya baadhi ya wananchi kuacha shughuli zao wakishangaa na wengine wakisema; “sasa shughuli imeanza”.

Ofisa Mdhamini wa ZEC Pemba, Ali Mohammed Dadi alisema wameshapokea karatasi na masanduku ya kupigia kura na fomu mbalimbali.

Alisema karatasi za uchaguzi wa wawakilishi na madiwani zilianza kusambazwa jana na walitarajia kupokea za urais jana jioni na kuzisambaza leo.

Jana, magari 15 ya polisi aina ya Land Rover yakiwa na askari 10 wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kila moja, zilionekana zikirandaranda katika mitaa ya Pemba.

“Sisi tunachotaka ni amani tu hao askari waje tu watulinde hakuna mfanya vurugu hapa. Hata wakizagaa mtaani kwetu heri tu ili mradi wasituzuie kufanya shughuli zetu, “alisema Ramadhani Hamisi Omar, mkazi wa Chakechake.

Diamond Platinumz Kubeba Familia Yake Nzima Kwenda Ulaya... Amenigusa Kwelikweli

$
0
0
Katika pita pita zangu mitandaoni nimeona clip ya video ya diamond akiwa na familia yake Ujerumani Alipoenda Kufanya Show, nilichopenda ni namna kijana anavyojitahidi kuwa karibu na mama yake, kutoka katika sakafu ya moyo wangu nimefurahishwa, nimeguswa sana na upendo huu wa kijana mwenzangu kwa mama yake! Mungu ambariki sana

Baada ya Mtangazaji Zamaradi Kuweka Wazi Penzi lake Kwa Ruge...Mange Kimambi Atoa Neno

$
0
0
Mtangazaji Zamaradi Siku tatu zilizopita aliamua kutoa ya moyoni na kuweka wazi uhusiano wake wa kimapenzi na boss wake Ruge Baada ya kupost picha hiyo hapo juu na kuandika maneno haya"You are mine, Am yours and Thats enough..MY LOVE!!" 

Picha hiyo mpaka sasa kwenye ukurasa wa Zamaradi ina Comments zaidi ya 2200 kutoka kwa watu mbali mbali....
Blogger Maarufu Mange Kimambi naye Ametoa ya moyoni kuhusu uhusiano huo na kuandika yafuatayo:


Mangekimambi_
"I love Zama so much, she is so sweet but inabidi tuwe wakweli. Kwa ustaa wake angekuwa Marekani angesimangwa na wanawake kama alivyosimangwa Karrueche Mpaka sasa kajua kujidhamini na hajarudi kwa Chris Brown. .
nilimuona Karueche kwenye show ya Iyanhla akasema, 'I know he loves me', Iyanhla akaamuliza What makes you think he loves u? Mwanaume Kila siku anakukosea heshima tena bila uwoga Mara akuache arudi Kwa Rihanna, Mpaka kazaa Na mwanamke mwingine wakati ukiwa nae still unasema he loves you? What's your definition of love? Karrueche alikaa kimya akakoka cha kujibu Na manager wake akaja kukatisha interview. My point is, we as women need to respect ourselves , we need to hold men accountable for the way they treat us.Wanaume wa Tanzania wako hivyo sababu yetu Sisi wanawake, tumeyakubali haya maisha.
Especially Mtu akiwa kioo cha jamii kama Zamaradi, kuna wasichana wadogo wana muadmire nao wataona kumbe it's okay to be disrespected.We need to teach young girls self respect and self worth
Ila simjudge sana Zama maana mwanaume kama anakusaidia financially it's another issue, hata Mimi labda ningejituliza hapo kama mtu ananipa kila kitu ila no need to publicize it, kaa kimya!Maana to publicize means you are telling other women it's okay to LOVE a man who treats you so horribly wakati It's not okay. I mean ni choice yake yeye na tuheshimu maamuzi yake Ila nachosema ni kwamba wanawake ambao ni kioo cha jamii Kama Zama they have a responsibility to empower other women and to preach equality.Wanaume wa Tanzania hawatokaa kubadilika kama sisi wanawake tutaendelea kuwa hivi.Kama kaamua kuishi haya Maisha ni haki yake but being PROUD of it mpaka kuposti insta is STUPID!I mean seriously, mimba zake zote 2 mbili wanawake Wengine wanazaa pia, just few months apart. Mwaka jana kwenye birthday ya bosi wakajikuta wanawake karibia 5 wameweka Post insta za happy birthday my love na za keki mwanaume anafanya kuzunguka nyumba kula besdei keki na wenyewe wanaposti insta .Ilikuwa kituko walichekwa mpaka wakafuta. Nilidhani pale ndo Zama angejifunza to keep this private"Mange

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda Atangaza Zawadi ya Milioni 1 Kwa Askari Polisi Atakayepambana na Jambazi na Kulishinda

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amekutana na Kamanda wa Polisi kanda maalum Simon Sirro pamoja na Askari Polisi kwa lengo la kujionea mwenendo wa jeshi hilo ambapo wamekubaliana kutoa zawadi ya milioni moja kila baada ya miezi mitatu kwa kila Askari Polisi aliyepambana na majambazi.

"Askari wetu wanafanya kazi katika mzangira magumu na wanachangamoto kubwa. Nmeona nitengeneze mfumo wa kuwapa motisha, kwahiyo nimeongea na Kamanda Sirro nimemuambia kuwa kila askari atakayeonekana amefanya vizuri mimi kama mkuu wa mkoa nitakuwa na zawadi ya milioni moja kwake kama motisha.

"Kuna watu wengi wana silaha halali na  wengine wanamiliki isivyo halali, kwahiyo tumekubaliana kuanzia leo hadi tarehe 1 aprili 2016 tunawaomba wana Dar es salaam wote waende kwenye ofisi za polisi kutoa taarifa za uhalali wa silaha zao.

"Tunataka kujihakikishia tunazo silaha ngapi katika mkoa wetu maana kuna wengine wanazitumia kinyume cha taratibu.

"Sasa olewako tukukute unamiliki silaha, tunahitaji kuliona jiji letu la Dar es salaam linaongoza kwa amani, hatutaki kuona majambazi wakipora kwenye mabenki wala kuwapora watu kwa silaha." Amesema RC Paul Makonda

I Am No Longer Psquare’s Manager – Jude Okoye Fires Back In New Tweet

$
0
0
The elder brother of singing duo, P-Square , Jude Okoye, has clarified that he’s no longer the group’s manager. Read his tweet below:

CHID BENZ 'Watanzania Wenzangu Siko Sawa Nahitaji Msaada Wenu'

$
0
0

Akiongea kwa uchungu kwenye kipindi cha Da Weekend Chat Show cha Clouds TV jana, Chidi ambaye mwili wake umepungua kwa kiasi kikubwa, amesema bado uwezo kimuziki anao lakini wale aliowaita wadau walioushikilia muziki wamemtupa.

Amesema wakati wa kilele chake, alikuwa akifanya show kila siku katika wiki, lakini kwa sasa mambo yamebadilika kabisa. “Matatizo yangu na stress zangu ambazo niko nazo zinanisababishia mwili wangu unapungua kwasababu siko okay, siko poa, siko sawa yaani,” alisema.

Chidi amedai kuwa kuna watu wanaamini kuwa kama akiwa juu, wasanii wengi wa hip hop watakuwa na wakati mgumu. “Hawa Joh Makini sijui, nani wanakuwa hawapo. Sasa hakuna mdau anayeweza kukubali akina Joh Makini wasikuwepo awepo Chidi Benz peke yake,” alisema.

Katika hatua nyingine Chidi alisema pamoja na afya yake kuzorota, hivi karibuni alipiga show kwa masaa mawili hadi mama yake akalia. "Mama yangu akaniambia mwanangu unafanya show two hours, show kali watu wanapenda unachokifanya lakini sioni mwamko wa watu kutokea kukusaidia, kwahiyo tufanye mpango watu wakusaidie' na mimi namuambia nataka watu wanisaidie, natamani kusaidiwa, natamani kupata mafanikio anayopata Diamond," alisisitiza.

Breaking News: Rais Magufuli ateua wakurugenzi wakuu wapya NSSF, TBC na RAHCO

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa watendaji wakuu wa Taasisi tatu za serikali kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo.


KWANZA, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Godius Kahyarara kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).


Uteuzi huu umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya NSSF namba 28 ya Mwaka 1997, Kifungu cha 42, kinachoeleza kuwa Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua Mkurugenzi Mkuu wa NSSF.


Prof. Kahyarara anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ramadhan Dau, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.


PILI, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Ayub Rioba Chacha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).


Dkt. Rioba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Clement Mshana ambaye amestaafu.


TATU, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Mussa Iddi Mgwatu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO).


Dkt. Mgwatu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Benhadard Tito, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.


Uteuzi wa watendaji wote watatu umeanza mara moja


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.

Dar es salaam.

19 Machi, 2016.

NEC yakigomea chama cha CUF ....Yasema Haitumbui Kujitoa Kwa Mgombea Ubunge Wa Chama Hicho

$
0
0

Tume  ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),imesema haitambui  kujitoa kwa Chama cha Wananchi (CUF),katika uchaguzi wa Mbunge  Jimbo la Kijitoupele hapa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika kesho Jumapili licha ya kuwa  Tume imepokea barua rasmi toka kwa uongozi wa Chama hicho.


Mkurugenzi wa uchaguzi wa Tume ya Taifa Bw Kailima Ramadhani amesema Tume imefikia maamuzi hayo kutokana na ukweli kuwa barua hiyo ya CUF imechelewa huku maandalizi ya uchaguzi huo yakiwa yamekamilika na ni Wananchi tu kwa sasa Wanasubiriwa kwenda kupiga kura.


Aidha Bw Kailima ameeleza kuwa,kwa kuwa karatasi za kupigia kura zilishachapishwa na kuwasili hapa nchini tayari kwa uchaguzi huo,zitaendelea kuwa na picha za Wagombea wa CUF hata kama wamejitoa katika uchaguzi huo.


Awali,wajumbe wa Tume ya Taifa ya uchaguzi  wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji mstaafu Hamid Mahamood Hamid walitembelea katika vituo mbalimbali  vya kupigia kura katika Jimbo la Kijitoupele ili kujiridhisha na maandalizi ya uchaguzi huo kabla ya uchaguzi kufanyika jumapili.


Tume ilibaini kuwepo kwa baadhi ya kasoro ndogondogo katika baadhi ya vituo vya kupigia kura ikiwa ni pamoja na kubanduliwa kwa karatasi zenye majina ya wapiga kura,mfano katika kituo cha Skuli ya sekondari Kinuni.


Jimbo la Kijitoupele lina jumla ya Wapiga kura wapatao 17,274 na vituo vipatavyo 53 vitatumiwa na wapiga kura ili kumchagua mbunge wa Jimbo la Kijitoupele siku ya Jumapili.


Sambamba na Uchaguzi wa ubunge katika Jimbo la Kijitoupele, marudio ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar Oktoba 25,2015 ambayo matokeo yake yalifutwa uatafanyika Jumapili hiyo pia.


Uchaguzi katika jimbo la Kijitoupele uliahirishwa mwaka jana kutokana na hitilafu ndogondogo zilizojitokeza katika karatasi za kupigia kura,kabla ya kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25,2015.

Mwanamuziki Shaa Achukizwa Vibaya na Bifu ya Ali Kiba na Diamond Platnumz...Adai Inamuweka Katika Wakati Mgumu Sana

$
0
0
Shaa amekiri kuwa hakuna beef asiyoipenda kama ya Diamond na Alikiba.
Amesema inawaweka wasanii wengine pia katika wakati mgumu.
“Ni sababu Alikiba ni msanii ambaye nampenda hatari, halafu Diamond ni msanii ambaye namkubali hatari,” amesema Shaa.
“Kwahiyo mnaniweka kwenye wakati mgumu hata mimi mwenyewe shabiki wote wawili nawapenda, wote wawili nawakubali lakini mmevuruga issue to a point ambayo siyo. Yaani Alikiba ni njano, halafu Diamond ni kijani, halafu nyie mmevuruga mechi yaani mimi sipendi kabisa kusema ukweli,” ameongeza.
“It’s allowed kupenda wasanii wote at the same time lakini watu wa media unfortunately ndiyo mnatuweka kwenye wakati mgumu.”

Paul Amuomba Peter Msamaha, Ambembeleza Wairudishe P-Square

$
0
0
Paul ameamua kujishusha na kumuomba msamaha kaka yake Peter Okoye.

Pacha huyo wa kundi la P-Square lililovunjika ameandika maelezo marefu kwenye Instagram kuelezea hali halisi ilivyo:

Mnachotaka ni P-Square, ninachotaka ni familia, upendo na kujali. Mitandao ya kijamii ni mzizi mpya wa maovu. Kuna familia kabla ya Psquare na siku zote kutakuwepo familia baada PSquare. Jude alikuwa chambo na mhanga tu. Mtu ambaye amekuwa akituweka pamoja kwa miaka yote hii. Ukweli ni kwamba Peter na Paul wana matatizo.

Kwa mara ya kwanza nimeamua kufanya kitu nje ya Psquare, na huo ndio mfano hapa. Nimekuwa nikimuunga mkono kaka yangu kwa asilimia 100 kuanzia kwenye endorsement zake peke yake hadi kwenye Dance with Peter ambazo zingine bado zipo kwenye Instagram yangu.

Na sasa nina maswali matatu:

1.Kwanini haya mambo yanatokea muda mfupi baada ya kutoa single ya Muno chini ya Rudeboy Records?

2. Ni vipi baada ya Jude kuacha kuisimamia Psquare kwa zaidi ya mwezi sasa, matatizo bado yanaendelea?

3. Kwanini (Peter) ana haraka hivyo ya kuwa msanii anayejitegemea?

Inahuzunisha sana, na inavunja moyo sana, natamani mambo haya yasingefahamika hadharani. Na sasa mashabiki wetu wamegawanyika, tafadhali msiunge mkono ujinga wa teamPaul sihitaji hayo. Tafadhali mjizuie sababu ni uovu. Na kwa mapromota, kumuunga mkono Peter akitumbuiza nyimbo za PSquare peke yake jukwaani, mnatuua na kutuharibu sisi zaidi.

Mpendwa kaka yangU nakuomba, hata kama humtaki tena Jude na hauitaki psquare, milele utakuwa kaka yangu. Lakini natamani sisi watatu tungeendelea kuwa pamoja sababu ni kitu cha furaha. Watu wanatupenda sana si sababu tu ya muziki wetu mzuri, lakini kuwaona ndugu wakiwa pamoja, kuwa mfano mzuri kwa familia zingine na kwa watoto wetu. Tafadhali, jishushe, samehe na sahau, bado tunaweza kubadilisha hili jambo. Kama nilisema chochote au kufanya chochote nilichokuumiza, nisamehe. Na kwa mashabiki wetu wote wa ukweli, tafadhali tuombeeni. Mungu awabariki wote

Chanzo:Bongo5

Idris Aeleza Matumizi ya Milioni 500 za Big Brother Baada ya Kuambiwa Amefilisika

$
0
0
Mshindi wa Big Brother Africa 2014, Idris Sultan aeleza jinsi alivyozitumia milioni 500 za Big Brother baada ya watu kwenye mitandao ya kijamii kudai amefilisika.

Akizungumza katika kipindi cha Friday Night Live cha East Africa Television Ijumaa hii, Idris alisema pesa yote aliyoshinda imeishia kwenye miradi mbalimbali.

“Pesa yote milioni 500 niliyoipata kwenye Big Brother Africa imeisha!!. Imeisha kwa sababu ya investment, nimeinvest sana,” alisema Idris.

Mwishoni mwa mwaka jana, Idris alitangaza ujio wa vipindi vyake viwili vya TV ambavyo vitarushwa kupitia vituo vya runinga vya Vuzu, Afrika Kusini na BET Africa pia aliwahi kuweka wazi kuwa anamiliki kampuni ya matangazo.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Jeshi la Polisi Nchini Lapewa Siku 2 Kumtafuta na Kumpata Mwandishi wa Habari Kutoka Zanzibar, Anayedaiwa Kutekwa

$
0
0
Baraza la habari nchini Tanzania MCT kwa kushirikiana na taasisi nyingine nne zimetoa siku mbili kuanzia leo kwa jeshi la polisi nchini kuhakikisha linafanya uchunguzi na kufanikiwa kumpata mwandishi wa habari Bi. Salma Said anayedaiwa kutekwa.

Wakitoa tamko la pamoja, Katibu Mtendaji wa MCT Bw. Kajubi Mukajanga, Mkurugenzi wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu THRDC Bw. Onesmo Olengurumwa pamoja na mwenyekiti wa jukwaa la wahariri TEF Bw. Theophil Makunga wamesema kitendo hicho kinakwenda kinyume na misingi ya haki za binadamu.

Viongozi hao wamesema kuwa Licha ya kitendo hicho pia kuminya uhuru wa wanahabari na haki ya kupata habari, lakini pia kinajenga hofu kubwa miongoni mwa wanahabari na jamii kwa ujumla.
Aidha vyombo hivyo vimetaka vyombo vya usalama kuhakikisha vitisho vyote dhidi ya wanahabari na watetezi wa haki za binadamu visiwani Zanzibar vinakomeshwa na kuwaacha wawe huru kufanya kazi zao katika kipindi cha uchaguzi wa marudio.

Hivi karibuni Bi. Salma amekuwa akitoa taarifa mbalimbali za hali ya kisiasa visiwani Zanzibar kupitia Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani na mitandao ya kijamii ambapo alisema kuwa kuandika kwake habari hizo alikuwa akipata vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana na hapo jana katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ilisemekana mwandishi huyo alitekwa na watu wasiojulikana.

Idris Afunguka, Aeleza Kinachoendelea Kuhusu Mahusiano yake na Wema Sepetu..

$
0
0
Mshindi wa BBA, Idris Sultan amesema penzi lake mwigizaji Wema Sepetu lipo palepale na mwanadada huyo hana mtu mwingine wa Kikongo kama ilivyodhaniwa hivi karibuni.

Idriss amefunguka yote hayo katika mahojiano na kipindi cha 'Friday Night Live' kinachorushwa na EATV kila siku ya Ijumaa.

Akijibu swali la mtangazaji Sam Misago kuhusu mahusiano yake na Wema Sepetu kwa sasa kwamba inasemekana hawapo sawa Idris amesema
 ''Mimi na Wema Sepetu ni Mwaa bado tupo zizuri kabisa''
Alipoulizwa kama ni kweli anampenda Wema au anatafuta 'kiki' amasema ingekuwa anatafuta umaarufu wa namna hiyo basi angeamka asubuhi na kuandika asubuhi 'kiki day'

Kuhusu watoto ambao alisema walipotea kabla hawajazaliwa Idris amesema awamejifunza kitu kutotoa taarifa kabla ya ujauzito haujafika hata miezi 3 hadi 5.

Aidha kuhusu saa yake aliyoionyesha kwenye mitandao ya kijamii ambayo watu wanadhani ni feki Idriss ametamba kuwa saa yake ni 'original' na alipewa zawadi na mfalme mmoja barani Afrika.


Yaliyonifikia Hii Leo Kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar

$
0
0
Ni takribani masaa kadhaa yamebaki ili wananchi wa Zanzibar wafanye maamuzi ya kumchagua Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani.

Leo March 19 2016 Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ‘ZEC’ imetoa taarifa kuhusiana na Uchaguzi huo. Taarifa hiyo imetaja waangalizi wa Kimataifa ambao ni kutoka Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Umoja wa Tume za Uchaguzi za Nchi za Kusini mwa Afrika ‘ECF-SADC’, Commoro na Ubalozi wa Zambia ambao tayari wamewasili Zanzibar.

Aidha kupitia taarifa hiyo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar imewaomba wananchi wote kuzingatia ipasavyo maelekezo ambayo yametolewa na yatakayotolewa na Tume katika vituo vya kupigia kura.

Taarifa hiyo pia imesisitiza kuhusiana na upokeaji wa matokeo kwamba wagombea na wafuasi wa wagombea na vyama vyao kuwa tayari kwa matokeo ya ama kushinda au kushindwa. Na pale ambapo mgombea hakuridhika na matokeo ni vyema akatumia njia au taratibu za kisheria katika kutoa malalamiko yake.

Diamond Platnumz Afungukia Mimba Nyingine ya Zari

$
0
0
STAA wa Bongo Fleva asiyechuja kwa takriban miaka 7 mfululizo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameeleza mikakati yake kuwa ana mpango wa kumpa mimba nyingine malkia wake wa nguvu, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Risasi Jumamosi linakuhabarisha.

Diamond ambaye tayari amejaaliwa mtoto mmoja (Tiffah) na mrembo huyo raia wa Uganda, amefunguka jambo hilo hivi karibuni alipokuwa akifanya mahojiano mafupi na mwanahabari wetu kuhusu mikakati yake ya kimaisha.

Alisema anamshukuru Mungu Zari kukubali kumzalia Tiffah tofauti na warembo wengine aliowahi kutembea nao lakini kwa kuwa yeye anapenda watoto, ameanza ‘kuchakarika’ ili Tiffah apate mdogo wake na si huyo tu, hata na mwingine kadiri Mungu atakavyombariki.

“Mimi napenda watoto. Bahati nzuri Mungu pia amenipa mwenzangu ambaye naye anapenda watoto. Hivyo si vibaya nikifikiria mtoto mwingine na mwingine yani kadiri Mungu atakavyonijalia.

“Yote hayo nitayafanya kwa utaratibu maana si unajua tena shughuli zangu za muziki nazo zinanibana, bado nahitajika nilee familia hivyo nitajipanga vizuri nina imani hakuna kitakachoharibika,” alisema Diamond.

Kabla ya kukutana na Zari, kwa nyakati tofauti Diamond aliwahi kubanjuka penzini na warembo kama Penniel Mungwila ‘Penny’, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Wema Sepetu ‘Madam’ pasipo kupata mtoto ambapo staa huyo wa Wimbo wa Utanipenda akisema warembo hao hawakuwa tayari kumzalia kwa kile alichodai kuwa walizidiwa na nguvu ya ujana.

Chanzo: GPL

Yanga Yajipeleka Kwa Waarabu' Klabu Bingwa Afrika

$
0
0
Unaweza kusema kitendo cha wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika timu ya Yanga ni kama wamejipeleka kwa waarabu kutokana na mchezo unaofuata kuwa ni kati yao na mshindi kati ya Al Ahly ya Misri ama Libolo ya Angola.

Mfungaji pekee wa bao la Yanga hii leo Donald Ngoma akishangilia bao lake.
Timu ya soka ya Yanga hii leo pamoja na kulazimishwa sare imefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika kufuatia kuitoa APR ya Rwanda kwa jumla ya mabao 3-2.

Yanga SC ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Taifa Jijini Dar es Salaam hii leo imelazimishwa sare ya bao 1-1 na timu ya jeshi la Rwanda katika mchezo wa marudiano ikiwa ni wiki moja imepita tangu timu hiyo ifanikiwe kuifunga timu hiyo ya jeshi la Rwanda nyumbani kwao Kigali katika dimba la Amahoro kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza.

Kwa matokeo hayo Yanga sasa watamenyana na mshindi wa jumla kati ya Al Ahly ya Misri na Recreativo de Libolo ya Angola katika hatua inayofuta ambapo kwa matokeo ya awali ya suluhu ya 0-0 ya ugenini huko Angola baina ya wababe hao yanatoa nafasi kwa Wamisri kuibuka kidedea na kuwakabili Yanga.

Katika mchezo wa leo, APR ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 4 kupitia kwa Fiston Nkinzingabo aliyefumua shuti kali akimalizia pasi ya Jean Claude Iranzi.
Yanga walifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 28 kupitia kwa mshambuliaji wake, Donald Dombo Ngoma aliyefumua shuti la kitaalamu baada ya pasi nzuri ya kiungo Mzimbabwe mwenzake, Thabani Scara Kamusoko.

Kwa ujumla mchezo wa leo, Yanga walicheza kwa kujihami zaidi wakionekana dhahiri kutaka kuulinda ushindi wao wa ugenini.
Laiti kama wageni APR ingeongeza juhudi kidogo ingeweza kuwatia simanzi mashabiki wa nyumbani – lakini huenda bahati haikuwa yao kwa siku ya leo baada ya kupoteza nafasi nyingi za wazi kufuatia juhudi za washambuliaji wao kuishia kwa kukosa umakini wa umaliziaji baada ya kushindwa kutumia makosa mengi ambayo yalikuwa yakifanywa na walinzi wa Yanga.

Paul Makonda Aweka Wazi Mikakati yake ya Kuubadilisha Mkoa wa Dar es Salaam, Ataka Wenye Nyumba zilizochakaa Wazipake Rangi

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amezindua kampeni ya kufanya jiji la Dar es salaam kuonekana safi ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko pamoja na kufanya jiji kuwa kivutio kwa wageni.

Makonda amefanya uzinduzi huo leo alipokuwa akizungumza na watendaji wa halmashauri zote za Dar es salaam katika kuwakumbusha namna ambavyo amejipanga katika kutatua kero za wananchi na kuwataka watendaji hao kuendana na kasi yake.

Kampeni hiyo ambayo inakwenda kwa jina la 'Naona Aibu' ina lenga kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakuwa safi kuanzia kwenye mazingira ya majumbani hadi kwenye barabara zote za jiji.
''Hatuwezi kuwa wasafi wa mioyo kama tunaishi kwenye mazingira machafu kila mtu aseme naona aibu, ukipanda kwenye daladala ukiona uchafu sema naona aibu, ukiwa mtaani kwako sema naona aibu''. Amesisitiza Makonda katika hotuba yake ambayo imedumu kwa zaidi ya saa 3.

katika kuhakikisha kampeni hiyo inafanikiwa, ametangaza kuanzisha shindano kwa kila mtaa, ambapo mitaa yote ya jiji la Dar es salaam itashindanishwa kwa usafi, na mtaa utakaoibuka mshindi utapata zawadi ikiwa ni pamoja na kitita cha shilingi milioni 5 kwa wajumbe wa mtaa huu.

Pia amewashauri wenyeviti wa serikali za mitaa kuwahamasisha wananchi wao kupaka rangi nyumba zao ili kupendezesha jiji kwa kuwa usafi ni pamoja na kuwa na nyumba zinazopendeza.
"Usafi ni pamoja na kupendezesha nyumba, waambieni watu wenu wapake rangi nyumba zao, zipendeze" Amesema mkuu huyo wa mkoa.

Aidha Mkuu huyo wa mkoa amewataka watendaji wote wa mkoa wa Dar es salaam na wanasiasa wote kutambua kwamba muda wa siasa sasa umekwisha na kilichobakia ni kufanya kazi kwa maendeleo ya wananchi.

''Wanasiasa kwenye jambo langu ukikaa mbele nitakushughulikia na wala sioni haya''- Amesema Makonda.
Hata hivyo amepiga marufuku biashara mbalimbali zinazofanyika katika maeneo ya barabara za jiji la Dar es salaam na kusisitiza kuwa biashara hizo hulikosesha taifa mapato vilevile kuweka wananchi katika hali ya hatari ya kugongwa na magari muda wowote.

TBC1 Hawana Pesa ya Kurusha Bunge ila Wana Pesa ya Kumrusha Paul Makonda

$
0
0
Jana nikiwa nyumbani naperuzi peruzi channel zetu zina nini cha mimi kuweza kuangalia, wakati napitapita nikapita na TBC, chaneli yetu ya Taifa. Nakutana na Makonda anahutubia, akili ya mwanzo nikawaza labda Rais Magufuli yuko sehemu na Makonda kaalikwa.

Baadae inapita banner kuwa ni kikao cha Makonda na watendaji wa Halmashauri, dah kinarushwa live televisheni ya taifa. Nadhani tatizo lililopo TBC ni aidha kukosa priorities au kuleta siasa lakini si rasilimali fedha au kubana matumizi kama wanavyotuaminisha.
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images