Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

Uchaguzi Zanzibar : Mgombea Urais wa CCM Dr. Shein Apiga Kura Asubuhi Hii

$
0
0
Zoezi  la upigaji kura limeanza  ambapo mgombea urais wa CCM Dkt Ali Mohammed Shein amepiga kura asubuhi hii katika kituo cha Bungi kisiwa cha Unguja.

TCRA Yazifunga Kurasa za Facebook FEKI za Mke wa Rais Janet Magufuli na Makamu wa Rais Samia Suluhu

$
0
0
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezifungia kurasa za facebook na tovuti ya www.focusvikoba.wapka.mobi baada ya kugundua kuwa zinatumia majina ya viongozi kutapeli watu.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Ally Simba aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, matapeli wanaofanya uhalifu huo wametumia majina ya Janet Magufuli, ambaye ni mke wa Rais na Samia Suluhu ambaye ni Makamu wa Rais kufanikisha utapeli wao.

Dk Simba alisema mamlaka yake imegundua kuwa wahalifu hao wa mtandao huanzisha tovuti, kurasa za facebook na blogu kwa kutumia majina ya viongozi wakuu wa nchi ili kujipatia fedha kutokana na umaarufu wa watu hao.

Alisema matapeli hao hutumia mitandao hiyo kuwadanganya wananchi kuwa kuna fursa za kupata mikopo au misaada kupitia vikundi vya kusaidiana, maarufu kwa jina la vikoba.

“Kwa mfano kuna matapeli walioanzisha ukurasa wa mtandao wa kijamii wa facebook kwa jina la mke wa Rais, Mama Janet Magufuli na kwa jina ma Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan wakilenga kujipatia kujipatia fedha,” alisema Dk Simba.

Aliongeza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 15 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015, mtu yeyote haruhusiwi kujitambulisha kwenye mitandao kwa kutumia utambulisho wa mtu mwingine.

Alisema adhabu ya kosa hilo imeainishwa kwenye kifungu cha 15(2) kinachosema anayepatikana na hatia anaweza kutozwa faini isiyopungua Sh5 milioni au mara tatu ya thamani ya kile atakachokuwa amekipata kupitia utapeli.

Aliwataka wananchi kuwa macho dhidi ya mitandao ya kijamii, tovuti na blogu ambazo zinawataka kutuma fedha au kuchangia kitu chochote ili wapewe mikopo au misaada.

Soma Habari Zilizopop Karika Magazeti Ya Leo Jumapili Ya March 20, Ikiwemo ya Jakaya Kuiponza Tanzania...

$
0
0

Soma Habari Zilizopop Karika Magazeti Ya Leo Jumapili Ya March 20, Ikiwemo ya Jakaya Kuiponza Tanzania...

Juma Nature Ataka Show ya Kushindana na Diamond Platnumz Uwanja wa Taifa....

$
0
0
Juma Nature asema yeye ndiye mwenye ubavu wa kupambana na Diamond Platnumz na wala si Ali Kiba,Kupitia Fnl Juma Nature aliniambia kuwa anaomba mpambano huo ufanyike kwenye Uwanja wa Taifa wa zamani [Shamba la bibi].

“Diamond ndiye anakalia game ya muziki nchini kwa sasa, na muziki ni furaha basi nataka kupambana naye kwenye uwanja wa Taifa na mashabiki wakitazama huku kusema nani ni mshindi, Diamond ndiye kaiteka game kuliko Alikiba na kama viongozi wapo tayari kuunga mkono na kutengeneza muziki mzuri basi waandae tamasha hilo”

Pia Nature amezungumzia kuhusu kufanya kazi na Said Fela ambapo majuma kadhaa yaliyo pita Fela alizungumzia kuhusu kufanya kazi na Juma Nature nakusema kama ikitokea ataweza kufanya naye kazi.

”Mimi sina tatizo lakini maslahi kwanza, kama kufanya naye kazi itabidi tuandikishane mkataba kwanza”.

Ommy Dimpoz Awekwa Njia Panda na Ugomvi wa Diamond na Ali Kiba..Hajui Aende wapi....

$
0
0
Msanii wa bongo fleva Ommy Dimpoz ni moja kati ya wasanii wanaoathiriwa na kuwepo kwa ile bifu kati ya Team Diamond na Team Kiba kwa kuwa wote ni washikaji zake.

Ommy amesema kuwa mashabiki wanamweka katika wakati mgumu kwani akionekana yuko na mmoja wapo anaonekana snitch kwa wengi na kusema yeye hajaegemea upande wowote bali ana focus na mambo yake.

“Yanapotokea matatizo kama haya hutakiwi ku choose side,unayaangalia yapite kwa sababu naamini yataisha,mimi najaribu ku focus kwenye mambo yangu binafsi.Ukisema uegemee upande huu utazua matatizo mengine bora niyasome kama shabiki.” alisema Ommy Dimpoz alipoulizwa kwanini urafiki wake na Diamond umepungua.

Source: Chill na Sky

Diamond Platnumz Ametoa Sababu za Wasanii Wakubwa Afrika Kupotea Kwenye Ramani ya Muziki...

$
0
0
Diamond Platnumz ametoa sababu ambazo anaimani zinasababisha wasanii wakubwa AFrika kupotea kwenye ramani ya muziki na kusema ni kuendekeza mashauzi, starehe na kutaka kujionesha.

“Unajua wasanii wengi wanapoteza na kushuka kimuziki sababu ya starehe pamoja na mashauzi. Unakuta mtu amepata mafanikio kidogo anaanza mashauzi na kufanya starehe zisizo na tija, ndiyo maana mimi huwezi kuniona kwenye starehe hata wasanii wa WCB ni hivyo hivyo”

Diamond amempa shavu Shettah kwa kusema ni mfani mzuri wa kuigwa

“Mimi namkubali sana Shettah kwani jamaa ni bahili sana anaweza kutoka kufanya show na akakwambia sina pesa, hata gari yake aliyonunua juzi amenunua kwa pesa zake sababu anakusanya pesa zake na kufanyia vitu vya msingi. Sasa hivi Shettah anajenga nyumba yake na hiyo yote sababu si mtu wa mashauzi na wala si mtu wa starehe”

Diamond alifanyiwa mahojiano wakati anamtambulisha RayMond

Mbunge Vicky Kamata Afunga Ndoa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Likwelile

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalamu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Vicky Kamata amefunga ndoa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servacius Likwelile.

Dk Likwelile amefunga ndoa hiyo baada ya mkewe wa awali kufariki dunia Mei mwaka 2014.

Kwa hatua hiyo, Dk Likwelile amemfuta machozi mbunge huyo kijana baada ya ndoa yake ya awali aliyotarajia kuifunga na Charles Pai kukwama dakika za mwisho wakati wa maandalizi yote ya msingi kukamilika.
Dk. Likwelile


Habari ambazo Tanzania Daima imezipata, zilieleza kwamba mbunge huyo ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya , alifunga ndoa hiyo Septemba mwaka jana katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Geita.

Habari zinaeleza kuwa wawili hao baada ya kufunga ndoa, hawakuwa na sherehe kubwa bali walikuwa na ‘pati mchapalo’ iliyofanyika nyumbani kwa Dk Likwelile na kuwashirikisha baadhi ya wana ndugu na marafiki wa pande zote mbili.

“Wamefunga ndoa bomani, hakukuwa na sherehe bali kulikuwa na hafla ndogo iliyofanyika nyumbani na wanafamilia wachache ndio walioshiriki,” alisema mtoa habari wetu ambaye alikuwa mmoja wa watu wachache walioshuhudia ndoa hiyo.

Alipotafutwa kwa njia ya simu kuthibitisha taarifa hizi, Kamata alikiri kufunga ndoa hiyo, lakini hakuwa tayari kuzungumza zaidi.

“Umepata wapi hizi taarifa? Ila ni kweli nimefunga ndoa, ninachojua ni kwamba Dokta Likwelile ni mume wangu halali, namshukuru Mungu kwa hilo,” alisema kwa kifupi Vick na kukata simu.

Mei 24 mwaka 2014, Vick Kamata alikwama kufunga ndoa na Charles Pai baada ya kubainika kuwapo kwa kasoro kwenye nyaraka za mwanaume.

Hali hiyo ilisababisha mbunge kuugua ghafla kutokana na mshituko alioupata na kulazimika kulazwa katika Hospitali ya Tabata Genaral iliyopo Segerea. Ndoa hiyo ilikuwa ifungwe katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza jijini Dar es Salaam na tayari kadi za mialiko zilikuwa zimesambazwa kwa watu mbalimbali wakiwamo wabunge.

Kamata ni msanii wa muziki aliyetamba na kibao chake cha “ Wanawake na Maendeleo” na pia ni mtetezi wa haki za wanawake.

Dr. Shein Afunguka: Nategemea Ushindi wa Kishindo.

$
0
0

Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar Dkt Ali Mohammed alizungumza na wanahabari baada ya kupiga kura yake katika kituo cha Bungi, Kibera kisiwani Unguja  ambapo alisema anaamini atashinda kwa kishindo na kuhusu kushindwa  alisema tusubiri matokeo ya uchaguzi ndiyo yataamua.


"Nimepata nafasi ya kupiga kura kama haki yangu ya  kimsingi na kumekuwa na utulivu mkubwa kwenye zoezi hili,hali ya ulinzi imeimarishwa. 


"Matumaini yangu ni kushinda kwa kishindo, kuhusu kushindwa ndugu muandishi tusubiri matokeo ndiyo yataamua".Alisema Dkt. Ali MohammedShein

Hamad Rashid: Nina Uhakika wa Kuwa Rais wa Zanzibar au Makamu wa Rais

$
0
0

Mgombea Urais kupitia Chama cha  ADC Mheshimiwa Hamad Rashid ametimiza haki yake ya msingi ya kupiga kura. 

Akizungumza na Waandishi mara baada ya kupiga kura katika kituo cha shule ya sekondari  Wawi Kisiwani  Pemba,  Rashid amesema  anauhakika wa kuibuka mshindi wa kiti cha Urais wa Zanzibar. 

Amesema kama hatashinda Urais,  basi atakuwa Makamu wa Rais

Sugu: CCM inatia doa nchi...Dunia Nzima Inaelewa Uchaguzi wa Marudio Zanzibar ni Batili...

$
0
0
WAKATI Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ikiendelea kusimamia uchaguzi haramu wa marudio visiwani humo, Joseph Mbilinyi, Waziri Kivuli wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo anasema, Serikali ya CCM inatia doa nchi, anaandika Faki Sosi.

Mbilinyi kwa jina maarufu Sugu amesema, Tanzania na dunia nzima inaelewa kuwa marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ni batili.

“Na kwa kuwa uchaguzi huu ni batili, watawala yaani Chama cha Mapinduzi kimeingia katika historia ya kipekee duniani kwa kuwanyima haki wananchi wake.”

anasema, matukio mbalimbali yaliyotokea na yanayotokea Zanzibar ikiwemo matumizi ya nguvu, vitisho na hata vitendo vya kikatili dhidi ya wanaosimamia haki, vinaendelea kuitia Serikali ya CCM doa si kwa taifa letu tu pekee bali pia kwa dunia nzima.

Akizungumzia kutekwa kwa Salma Said, Mwandishi wa Habari wa Kampuni ya Mwananchi (MCL) na Makilishi wa Idhaa ya Ujerumani (DW) amesema, tukio hilo limezua maswali na hofu kubwa kwa wananchi, familia yake na wadau hasa wanahabari wa ndani ya nchi na jumuyia za kimataifa.

“Ni dhahiri kuwa, kutekwa kwa Bi. Salma Said kunatokana na kazi yake ya uanahabari na ndio maana ushahidi wa awali ambao umepatikana kwa njia ya ujumbe wa sauti ukiwa na sauti inayoaminika kuwa ni yake, unaelezea wazi kutekwa kwake kunatokana na yeye kuripoti dosari zinazoendelea hasa katika uchaguzi batili wa marudio ya Zanzibar,” amesema na kuongeza;

“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inalaani kwa nguvu zote kitendo cha utekaji wa mwanahabari huyu kutokana na kazi yake. Aidha, tunaitaka Serikali kuhakikisha kuwa mama, dada, rafiki na ndugu yetu Bi Salma Said anapatikana akiwa salama.”

Amesema, wataendelea kuamini kuwa, kuchelewa kupatikana kwa Salma na ukimya wa vyombo vya Serikali na Usalama ni matokeo ya uminyaji wa demokrasia kwa wale wasiofanya kazi kwa mashinikizo ya chama tawala.

“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, itaitisha maandamano makubwa nchini ili kushinikiza upatikanaji wa haraka wa Bi Salma Said lakini pia kupaza sauti kwa ulimwengu kuwa Tanzania si mahali salama kwa wanahabari,” amesema

Hotuba Ya Kwanza Ya Ole Sendeka Kama Msemaji Wa CCM

$
0
0
Machi 15, 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akiwaapisha Wakuu wapya wa mikoa, aliagiza pamoja na mambo mengine, viongozi katika ngazi mbalimbali kuhakikisha wanasimamia nguvu kazi ya vijana katika maeneo yao ili waache kukaa kijiweni.

Agizo hilo lililenga utekelezaji wa vitendo wa matumizi bora ya rasilimali watu nchini wakiwemo vijana ambao ni nguvu kazi muhimu kwa taifa, kujengewa mazingira mazuri yatakayowawezesha kujiajiri katika shughuli za uzalishaji mali.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinampongeza kwa dhati Rais Magufuli kwa agizo lake hilo lenye lengo muhimu la kuwafanya watanzania kwa pamoja kuwajibika.

CCM inampongeza Rais Magufuli kwani kwa mara nyingine tena amedhihirisha kuwa wapiga kura walio wengi walifanya uamuzi sahihi kwa kumchagua yeye kuwa Rais wa Serikali
ya awamu ya Tano katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.

CCM kama chama anachotoka Rais Magufuli na ambacho ndicho Ilani yake inatekelezwa na serikali kwa kupindi cha 2015/2020, ina kila sababu ya kumpongeza kwa kuanza
vizuri katika uongozi wake wa miaka mitano na tunaamini kuwa katika kipindi hicho, “Tanzania Tunayoitaka” itafika mbali kimaendeleo kwenye kila ngazi.

Historia ipo wazi kuwa wakati Tanzania inapata uhuru wake mwaka 1961, Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliongoza taifa letu na kauli mbiu ya UHURU NA KAZI baadae ikabadilika kuwa Uhuru ni Kazi na sasa awamu ya Tano inaendesha shughuli zake kwa kauli mbiu ya “HapaKaziTu” ambayo kila mmoja ni shahidi kuwa hivi sasa kazi inatekelezwa kwa kasi kubwa.

Utekelezaji wa kauli mbiu ya HapaKaziTu umejidhihirisha katika kipindi kifupi cha uongozi wa Serikali hii yak awamu ya tano katika kudhibiti rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma, matumizi mabaya ya madaraka na na ukwepaji kodi, mambo ambayo matokeo yake yameshaanza kuonekana.

Matokeo hayo ni pamoja na kuongezeka kwa makusanyo ya kodi ya serikali, ambayo yameiongezea serikali uwezo wa kuwahudumia wananchi kujikwamua na umaskini kwa
ustawi wa jamii kwa ujumla.

Aidha CCM kinamuunga mkono Rais Magufuli pia kwa hatua anazozichukua yeye na serikali yake katika kurudisha nidhamu na uwajibikani katika utumishi wa umma.

Kumbukumbu zinaonyesha mpaka sasa watumishi wa umma waliochukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali kwenye utumishi wao, na wengine wakifikishwa kwenye vyombo vya sheria, wamefanyiwa hivyo kwa kufuata sheria na kuzingatia misingi ya utawala bora.

Hata hivyo wapo watu wachache wameamua kupotosha nia njema ya Mheshimiwa Rais na serikali yake kwa kuonesha kuwa haya yanayofanyika ni udikteta na uonevu.

Naomba ifahamike kuwa CCM iliiagiza serikali yake kwenye ilani yake ya uchaguzi ya 2015/2020 kuhakikisha inarudisha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma kwa hiyo kinachofanywa na Rais Magufuli na serikali yake ni utekelezaji ilani ya CCM na ndiyo mahitaji na matakwa ya watanzania walio wengi.

Watanzania walio wengi wanataka kuuona utumishi wa umma wenye nidhamu na uwajibikaji hivyo tunawaomba watanzania kuwapuuza wale wote wanaotafsiri hatua hizi kuwa ni udikteta na uvunjifu wa sheria, kwani kwa matendo yao na maneno yao wanashabikia uzembe na kutowajibika kazini jambo ambalo CCM haikubaliani nalo.

CCM inawasihi wanachama wake, wapenzi, wakereketwa, mashabiki na watanzania wote kwa ujumla kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono kwa vitendo Rais Magufuli kwa dhamira njema aliyonayo kwa taifa letu, ili hatimaye Tanzania yenye maendeleo ifanikiwe.
………………………………………………………………………

Ndugu Christopher Ole Sendeka
MSEMAJI WA CCM
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,

20/03/2016

Jionee Picha Jinsi Zari Hassan na Mama Diamond Wanavyokula Raha Ujerumani..

$
0
0
Diamond and Diamond's family are in German for Diamond's show and family vacation. See below what Tiffah and Mama Diamond wore in German..

Daktari Afunguka: Maini ya Penny yameanza Kuharibika Sababu ya Unywaji wa Pombe Kali.....

$
0
0
Habari mbaya! Majibu ya daktari yamemkatisha tamaa Mtangazaji wa Zouk TV, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ baada ya kuambiwa kuwa, kutokana na unywaji wa pombe kali kupitiliza, maini yake yameanza kuharibika na asipochukua hatua za haraka hali itazidi kuwa mbaya zaidi.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Penny, hivi karibuni mrembo huyo aliyewahi kuwa mwandani wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alikuwa hajisikii vizuri na mara nyingi alipokuwa akijaribu kula, alitapika na kuishiwa nguvu hivyo akaamua kwenda kupima kwenye Hospitali ya AAR jijini Dar.

Mpashaji huyo alidai kwamba baada ya Penny kuchukua vipimo vyote, ilibainika kwenye maini yake kuna tatizo na chanzo chake ni unywaji wa pombe kali.“Maskini Penny, sasa hivi hana raha kabisa tangu daktari amwambie ana matatizo kwenye ini, mara nyingi anakuwa mnyonge na mwenye wasiwasi sana,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kupokea taarifa hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Penny ambapo alizungumza kwa upole kuwa angeomba vitu vingine asiviweke wazi kwenye vyombo vya habari kwani ni mambo ya kidaktari zaidi.

“Kiukweli sijisikii vizuri na hata kuongea sana naona shida. Unajua vitu vya kidaktari siyo vizuri kuviweka kwenye vyombo vya habari. Kifupi sipo vizuri,” alisema Penny akionekana kutokuwa na furaha.
 GPL

Mange Kimambi Awalipua Wauza Unga Sakata la Mwanamuziki Chid Benz...Awataja Majina Laivu Bila Woga

$
0
0
Kutokana na sakata la mwanahiphop Chidi Benz, Mwanadada Mange kawacha live wauza unga huku akiwataja majina baadhi ya makada maarufu wa CCM Kinje Ngombare na Iddy Azan kama wahusika wa hii game.
Note: Magu anza na hawa waliotajwa maana kama Iddy Azan hii ni mara nyingine anatajwa...

Ameandika hivi Kwenye ukurasa wake wa Instagram:

From @mangekimambi_ - "Chi chi chi chi Chidi Benz... I respect huyu msanii sana. Ni Mtu wa kujitolea, about 4 years ago nilikuwa na event ya Watoto yatima pale Kurasini nikamuomba aje kuwafanyia show watoto, akaja kwa cost zake Na akafanya show bureeeeeeeeeeee. Sio wasanii wengi wanaokubali kufanya Hivi. So Leo nikimuona ana hali hii inanisikitisha mnoooo...
.
.
Kweli binadamu tumeumbwa tofauti Jaman. I love money mpaka huwa naziota ndotoni Ila siwezi kufanya biashara ya unga au siwezi kuwa na mume muuza unga, yes ukiwa na mume muuza unga na wewe huna tofauti na mumeo Maana unakula hiyo pesa......... As much as I love money siwezi Taka pesa ambayo inatokana na binadamu Mwenzangu kuwa Hivi. Raha yake ni nini??? Yani niendeshe gari zuri, au nivae designer stuff au nijenge mansion Kwa pesa inayotokana Na binadamu Mwenzangu kuwa Hivi jamani au mwishowe afe kabisa??? .
Anyways, biashara ya madawa ya kulevya haiwezi kufa kabisa no matter what because of the huge profits but what we can do is tunaweza kuipunguza mnooooooooooooooooooo. .
.
Kwako Mr. Sembe @nsembo2014 kwako Mrs. Sembe @8020fashions kwako @KinjeNgombaleMwiru kwako @IddiAzzan2015 kwako @Rummy_26square kwako @DaudiKanyau na wengineo wengi Hivi mna roho za vipi nyie watu? 40 zenu zitafika tu.....
.
.
Alafu hawa wauza unga naowatajaga eti wanazanigi nawaonea wivu. Niache kuwaonea wivu kina Klyn Mengi wanaokula bata la pesa halali niwaonee wivu nyie criminals??? Mnamaliza vijana wa kitanzania then mnataka kujifanya watu wa maana kwenye jamii.
.
.
Alafu I have a question hivi kwanini wauza unga wengi wa Bongo wanahamia South Africa? Kwani South Africa kuna laws za kuwalinda ama? Maana sijaelewa. So many of Tanzania's drug dealers wanahamiama huko wanakuwa wanaenda bongo kuchungulia. Mnaojua embu tuelewesheni" Mange

Watu Wasio Julikana Wasambaza Vipeperushi vya vitisho Visiwani Zanzibar

$
0
0
Siku moja kabla ya kufika siku ya uchaguzi mkuu wa marudio visiwani Zanzibar hapo kesho watu wasio julikana usiku wa kuamkia leo wameziwaekea X Nyekundu nyumba kadhaa za wakazi wa Pujini katika wilaya chake chake chake na kuwaekea kipeperushi cha onyo juu ya ushiriki wao kwenye uchaguzi huo.

Moja kati ya watu walio wekewa X hizo kwenye  nyumba yake amesema wamelala walipo amka walijikuta nyumba zao zikiwa tayari zina X na kuekewa kipeperushi hicho cha onyo.

Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa Kusini Pemba ilifika kijijini Pujini Kumvini na Kijili kujionea nyumba hizo zilizo wekewa X nyekundu ampapo mwenyekiti wakamati hiyo mkuu wa mkoa Kusini Pemba Bio Mwanajuma Majidi Abdalla amewataka watu wanao taka kwenda kupiga kura waende kupiga kura na kuzipuzia X hizo huku ulinzi ukiwa umeimarishwa.

Bimwana Juma amewataka wanaume wasiwatishe wana wake kwa kutishia talaka kwa sababu ya kwenda kupiga kura badala yake wawape uhuru wanawake kuamua pindi wakitaka kwenda kwenye uchaguzi waende pasi vitisho vya vua aina yoyote.

Nae kamanda wa polisi mkoa kusini pemba kamishimna msaidi mohamed shekhan mohamed amesema jeshi lake halitishiki na vitendo vya aina hio na kwamba watawakamata wale wote waliohisika na uwekaji wa x hizo.

Azam FC yaichapa Bidvest Wits ya South Africa 4-3...Yasonga Mbele

$
0
0
TIMU ya Azam FC leo imefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuifunga Bidvest Wits ya Afrika Kusini kwa mabao 4-3 kwenye mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar.

Mabao ya Azam FC yamepachikwa kimiani na Kipre Tchetche aliyefunga mabao matatu ‘hat trick’ na moja likapachiwa na nahodha wa timu hiyo, John Bocco.

Katika mechi ya kwanza, Bidvest ilipoteza kwa mabao 3-0 ikiwa nyumbani Johannesburg. Safari hii imepata mabao matatu lakini ikashindiliwa mengine manne. Maana yake Azam FC imevuka kwa jumla ya mabao 7-3

Mwandishi Salma Said Apatikana Baada ya Watekaji Kumuachia Huru

$
0
0
Siku tatu baada ya mwandishi wa Mwananchi na DW, Salma Said kutoweka, jana alipatikana baada ya kukutwa katika Hospitali ya Regency ya jijini Dar es Salaam  na kupelekwa kituo kikuu cha polisi kuhojiwa.

Habari zilizopatikana jana jioni na kuthibitishwa na mumewe, Ali Salim Khamis na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi, Simon Siro zilisema Salma alisajiliwa jana mchana katika hospitali hiyo.

Ali aliyekuwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, alisema kwa ufupi kuwa amepata taarifa hizo na kufika Dar es Salaam kuzifuatilia. 

Kamanda Siro alisema ni kweli Salma amepatikana na ametumwa mkuu wa upelelezi wa kanda hiyo kumfuata hospitali ampeleke kituoni kwa mahojiano. 

“ Tumefungua jalada la uchunguzi wa tukio hili juzi,” alisema Sirro na kuongeza. 

“Wapelelezi walizungumza na mume wa Salma na kuna mambo amewaeleza lakini hatuwezi kuyaweka wazi kwa sasa, hadi uchunguzi utakapokamilika, tumeipata namba ya simu aliyowasiliana nayo na mumewe akiwa huko kunakoaminika amefichwa,” alisema. 

Wakati huo huo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika tamko lake ililolitoa jana ilieleza kuwa kutekwa kwa mwanahabari huyo kumezua maswali mengi kwa wananchi, familia yake, wadau na wanahabari wa ndani ya nchi na wale wa jumuia za kimataifa.

“Kutekwa kwa Salma kunatokana na kazi yake ya uanahabari, ndiyo maana ushahidi wa awali uliopatikana kwa njia ya ujumbe wa sauti ukiwa na sauti inayoaminika kuwa ni yake, ulieleza wazi kutekwa kwake kunatokana na yeye kuripoti dosari zinazoendelea katika uchaguzi wa marudio Zanzibar,” alisema Joseph Mbilinyi, Waziri Kivuli wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo wa Kambi ya Upinzani. 

Mbilinyi ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) alidai kuwa matukio mbalimbali yanayoendelea Zanzibar yakiwamo ya matumizi ya nguvu, vitisho na hata vitendo vya kikatili dhidi ya wanaosimamia haki, vinaendelea kuitia Serikali ya CCM doa, Taifa na dunia nzima.

CCM kuweka utaratibu mpya wa kuwapokea Wanachama waliokihama Chama hicho na Kukimbilia Vyama vya Upinzani

$
0
0
Siku kadhaa baada ya mwanachama wa siku nyingi wa Chama cha Mapinduzi,balozi Juma Mwapachu, kurejea katika chama hicho baada ya kukihama wakati wa harakati za Uchaguzi mkuu wa mwaka jana, kimekiri kuwa kuna haja ya kusikiliza hisia za wanachama wake na kuangalia upya namna gani wanachama wa Chama hicho walioondoka na kwenda kujiunga na vyama vingine wanapokelewa kufutia mazingira ya siasa yalivyo sasa.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana , ametoa kauli hiyo jijini Dar Es Salaam,wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliolenga kumtambulisha Mjumbe wa Halmashauri kuu Ya Taifa ya Chama hicho Christopher Ole Sendeka, kuwa msemaji wake, kuchukua nafasi ya Nape Nauye, ambaye sasa ni waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Bwana Kinana, amekiri kuwa ni vyema sasa CCM ikae na kutengeneza namna ya watu fulani kurudi ama kutorudi kabisa katika chama hicho kwa kuwa kwa sasa utaratibu unatambua mchakato kumrejesha mwanachama bila kuangalia alitoka kwa mtindo upi.

Katibu Mkuu huyo wa CCM, ameenda mbali zaidi na kusema kuwa lazima chama hicho kiheshimu hisia za wanachama wake.

Akizungumza baada ya kutambulishwa, Ole Sendeka amesema CCM kinampongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wake na kwamba huo ndio msimamo wa Chama na kukanusha maeneo yanayoelezwa kwamba huo ni udikteta na uonevu

Idris Sultan Afunguka: Tulifanya Kosa Kubwa Sana Kutangaza Mapema Mimba ya Wema Sepetu

$
0
0
Maisha ya mastaa duniani hufuatiliwa kwa karibu sana na watu wengi. Kuna kipindi yanakuwa ni asali lakini yanapobadilika huwa ni shubiri.

Mwanzo mahusiano ya Idris Sultani na Madam Wema Sepetu, yalionekana kuvunjika lakini wenyewe wameonyesha kuwa bado wapo pamoja lakini wameamua kuyaficha kwa sasa.

Akizungumza na kipindi cha Friday Night Live (FNL), kinachoruka kupitia EATV, Idris alisema walifanya haraka kutangaza mimba ya Wema.

“Mwanzo tulifanya sana makosa kutangaza mimba ya Wema, culture yetu hairuhusu. Tulitakiwa kuweka wazi kama ingekuwa mimba imefikia miezi minne hivi na kuendelea,” alikiri.

Millen Magese: Tanzania Hainisupport Kwenye Kampeni Zangu za Endometriosis..Siwezi Poteza Muda....

$
0
0
Ukweli mchungu na kuusema ni muhimu ili wahusika wajirekebishe. Millen Magese yupo kwenye kampeni kubwa dhidi ya ugonjwa unaowatesa wanawake wengi duniani akiwemo yeye, Endometriosis ambayo kwa sasa inapewa support dunia nzima.

Na wikiendi iliyoisha alifanya matembezi nchini Afrika Kusini ya kampeni nyingine aliyoipa jina #13IsEnoughFindCure4Endo inayosisitiza umuhimu wa kupatikana kwa tiba hiyo. Lakini Miss Tanzania huyo wa zamani, amedai kuwa Tanzania imeshindwa kumuunga mkono. Anadai kuwa Watanzania wamekuwa wakisupport pale tu anaposhinda kitu.


Aliamua kuusema ukweli huo baada ya mrembo mwenzie, Miriam Odemba kumpongeza na kumshauri afanye matembezi kama hayo Tanzania pia.

Ni kweli, ni muda sahihi wa Tanzania kumuunga mkono Millen kwenye juhudi zake hizo za kutafuta tiba ya ugonjwa huo uliomfanya afanyiwe upasuaji mara 13.

Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images