Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Ahudhuria Ibada Ya Ijumaa Kuu Leo Jijini Dar Es Salaam

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akijiandaa kuubusu Msalaba wakati wa Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa April 25, 2016

Kauli ya Makonda inavyoweza kutumika kama fursa kwa vijana wa Dar

$
0
0
Mkoa wa Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji yanayoongoza kwa uchafu Tanzania.

Siku chache zilizopita Rais Magufuli alifanya uteuzi wa wakuu wapya wa Mikoa, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda aliteuliwa kuwa mkuu mpya wa mkoa wa Dar es Salaam.

Baada ya uteuzi huo na kuapishwa ikulu, Makonda alifanya mkutano kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere ambao uliwajumuisha wenyeviti wote wa mkoa wa Dar es Salaam na wadau wengine wa maendeleo.

Agenda ya uchafu ndiyo ilishika nafasi kubwa kwenye mkutano huo. Mh Makonda aliwataka wenyeviti wote wa mkoa wa Dar es Salaam kuanza usafi kwenye mitaa yao, pia aliahidi kutoa zawadi ya gari lenye thamani ya shilingi milioni 20, na zawadi ya pikipiki kwa wajumbe wake ambao mitaa yao itaonekana ni misafi.

‘Kidole kimoja hakivunji chawa’, ushirikiano pekee na umoja ndiyo unaweza kufanikisha hili kutimia. Vijana wengi wapo mitaani wanalalamika hakuna ajira, lakini kwa hili inaweza ikawa neema na fursa pekee ya ajira kwao.

Vijana wanaweza kuunda vikundi vyao kwa ajili ya kufanya usafi kwenye mitaa yao na kuweka unlizi kwa pamoja, siamini kuwa kama kutakuwa na mwenye muda kila siku wa kufanya usafi na kumsimamia mwenzake kwenye hili.

Viongozi wa serikali za mitaa na wananchi wao wanaweza kupanga kuchangishana fedha fulani ili kuwapatia vijana hao ambao watakuwa wanafanya usafi na ulinzi kwenye mitaa yao. Hakuna kiongozi anayeweza kukutafutia kazi, ila anakutengenezea misingi ya kuweza kujiajiri mwenyewe kama hili lililotokea sasa.

Tazama Hapa Video ya Wimbo Mpya wa Mwanamuziki Yemi Alade Unaitwa Ferrari

$
0
0

Baada ya kufanya vizuri katika Hit single ya ‘Na Gode’ Staa kutoka Nigeria Yemi Alade ametualika tena kuutazama mdundo wake mpya ‘Ferrari’  leo March 25 2016, ukishaitazama pia usiache kutoa comment yako umeionaje.

Kiongozi wa Kundi la Wapiganaji la Islamic State IS Auwawa Syria na Wamerekani...

$
0
0
Kiongozi wa pili kwa ukubwa katika itifaki ya kundi la wapiganaji la Islamic State ameuawa katika oparesheni iliotekelezwa na Marekani nchini Syria mwezi huu, vyombo vya habari vya Marekani vimesema.

Maafisa wa ulinzi wameliambia shirika la habari la NBC kwamba Abdul Rahman Mustafa al- Qaduli,raia wa Iraq anayejulikana kama Hajji Iman aliuwawa katika uvamizi mwezi huu.

Waziri wa maswala ya ulinzi nchini Marekani Ash Carter alitarajiwa kuthibitisha kifo cha mwana jihad huyo na kutoa maelezo ya uvamizi huo.

Marekani ilikuwa imetoa zawadi ya dola milioni saba kwa mtu yeyote ambaye angetoa habari za Qaduli.

Qaduli alizaliwa mwaka 1957 ama 1959 kaskazini mwa mji wa Iraq wa Mosul ambao ulidhibitiwa na IS tangu mwaka 2014.

Alijiunga na al-Qaeda nchini Iraq mwaka 2004 chini ya uongozi wa marehemu Abu Musab al-Zarqawi akihudumu kama naibu wake na kiongozi wa eneo la Mosul kulingana na Marekani.

Baada ya kuachiliwa kutoka kwa jela za Iraq mapema mwaka 2012,alijiunga na vikosi vya IS nchini Syria.

Maoni: Hofu yangu Kuhusu Label ya Wasafi, Diamond, Harmonize na Raymond ni Kama ‘Mtu Mmoja’

$
0
0
Makala imeandikwa na Wynjones Kinye (Mhadhiri chuo kikuu cha SAUT)

Naappreciate sana juhudi za Diamond katika kuunyanyua muziki wa Tanzania kwa kuibua vipaji vipya kama Harmonize, Raymond na watakaofuata kama wapo.

Ni dhahiri kuwa kwa hili la kusimamia vijana wawili tu kiasi kikubwa cha fedha kimetumika na kinaendelea kutumika hasa ukizingatia kuwa Diamond tayari ni mtu sensitive kwenye quality ya product, na tunajua kuwa quality ni gharama kubwa siku hizi kama sio siku zote.

Diamond amethubutu kuwekeza, kibiashara tunategemea return katika kila unachofanya ‘kibiashara’ hivyo ni muhimu sana kufikiria vitu vingi vya kuifanikisha biashara ukiachana na mtaji. Hata kama una mtaji mkubwa na fedha za ziada kuuendeleza mradi bado failure iko pale kama hutotazama vitu vingine kwa kina.

Licha ya nguvu nyingi anayoweka Diamond kwenye muziki wa vijana wake ‘publicity na video nzuri’ bado mimi nina hofu ya kufanikiwa kwake kuwafikisha vijana wake hawa chini ya label yake. Nilivumilia kulisema hili baada ya kumsikiliza Harmonize, ila sasa nimeshindwa kukaa nalo baada ya kumsikia Raymond.

Naadmit kuwa hawa vijana Raymond na Harmonize wana vipaji vikubwa, wana sauti nzuri sana na ni waandishi vizuri lakini wanakosa kitu cha kuwafanya kuwa brand. Yupo mwandishi mmoja anaitwa Angela Cross alisema…

“Your brand is the foundation of your relationship with your audience – so be mindful of who your audience is (and no, it’s not “everyone”), what they want, and how you can connect with and serve them.”

Najua brand ni neno pana na kila mtu anaweza kulitetea kivyake kutokana na mapenzi na uelewa kwenye suala husika, vyovyote iwavyo niseme Diamond, Raymond, na Harmonize ni “MTU MMOJA.” Yaani ukitoa sauti zao (ambazo pia sasa zinaelekea kufanana) vingine vyote ninafanana zaidi.

Hapa nazungumzia uandishi wao, mawazo yao katika nyimbo, mtindo wa nyimbo zao, uandishi wao, na strategies za kibiashara ambazo naweza sema ni zile zile ambazo ameziexperience Diamond. Sasa kwanini tusifikirie brand kama ‘MUHURI’ ambao utakutambulisha kwa audience kama zilivyo documents zenye huo muhuri maofisini?

Haya, dalili zinaonyesha kuwa Richard Mavoko ataingia kwenye Label ya Wasafi. Ikitokea basi ni kheri lakini ni wazi pia kuwa kutaongeza ‘mlundiko’ wa mfanano katika muziki kwani hata mtu asiyefuatilia sana anafahamu kuwa Richard kwa matoleo kadhaa amekuwa akifanana sana kiuimbaji na Diamond, hata uachiaji wa nyimbo zao ulikuwa ukifuatana. Mbona yanaweza kuepukika haya? Tazama Harmonize anavyojaribu kuwa na attitude ya kwako.

Najua Diamond uko karibu sana na vijana wako, naamini wako huru kuzungumza nawe, uhuru huu sasa naona usifike kwenye muziki unaofanya, naona vitu viwili hapa na sina uhakika kipi ni kipi, kwamba vijana ni mashabiki wa muziki wako hivyo wanajikuta wanafanya unachofanya ama wewe ni bosi wa vijana na unawaambia nini cha kufanya ili ikurahisishie wewe kuwafanikishia ndoto zao.

Sijawahi kumsikia Raymond kabla, nilipata shauku kubwa kumsikia baada ya kujua kuwa yuko chini ya Wasafi, lakini shauku kubwa zaidi niliipata baada ya kusikia kuwa ni mtumiaji wa guitar katika uimbaji. Nilipata mawazo kadhaa ya picha juu ya huyu jamaa atakavyokuwa anaimba, niliamini angekuwa tofauti na Harmonize, niliamini angekuja na nyimbo tofauti na tulizozizoea siku hizi na niseme tu kuwa nilikuwa so disappointed.

Wimbi hili halipo kwa Wasafi tu,. naona balaa hili kutokea kwa Mkubwa na Wanawe. Angalia uimbaji wa Yamoto Band na wale wadogo zao, balaa linaendelea baada ya kumsikia mshindi wa BSS ‘Kayumba’ ambaye pia ni zao la Fella na sasa yupo chini ya usimamizi unaomhusisha Fella na washirika wake. Kayumba naye kaja na muziki uleule unaofanywa na wenzake wanaomzunguka.

Diamond!! Kama umeamua kusimamia wasanii nakushauri kuwaza ‘utofauti’, utofauti na upya ni must katika soko la muziki duniani kote especially sasa hivi, ni dhambi kubwa kibiashara kuwa ‘COMMON.’ Uimbaji na uandishi vya wasanii wako hakikisha vinatofautiana na vya kwako. Kama umemudu kuajiri mwalimu wa ‘kizungu’ kwa ajili ya crew yako basi hautoshindwa kuajiri mtaalamu wa kuwatengeneza tofauti vijana wako kwa kila kitu, hii kazi usiifanye wewe tafadhali.

Kwanini usitushangaze kwa kuja na vijana wenye muziki wa kitofauti na uufanyao wewe? Kuna ugumu gani kututengenezea kichwa kingine cha RnB kikatoa changamoto kwa wakina Ben Pol na Jux?

Kwanini usiufikirie muziki wa Grace Matata na Damian Soul pia? Vipi kuhusu muziki mzuri uliofanywa na Mandojo na Domokaya na kushindwa kuvuka mipaka? Huoni kuwa hivi vinavyotokea vinafanya tuchoke muziki (kitu ambacho ni makosa makubwa), hatupaswi kuuchoka muziki, fanyeni tusiuchoke muziki.

Nia yako ni nzuri sana Diamond na uzuri ni kuwa unaimudu kabisa nia hiyo (kitu ambacho ni muhimu sana), lakini kwanini sasa ugharamike isivyostahiki kwa kutumia nguvu tele kisa tu hujaweka mawazo yako/yenu nje ya vitu visivyohusisha fedha? Hofu yangu iko hapo zaidi, matumizi makubwa ya pesa isivyostahiki.

Mutfi Wa Tanzania Amuombea Dua Mkuu Wa Mkoa Wa Dar Es Salaam, Paul Makonda

$
0
0
MUFTI wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubery amemuombea dua, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Rais Dk. John Magufuli ili waweze kulitumikia vema taifa na kuliletea maendeleo.

Zubery alimfanyia dua hiyo Makonda Dar es Salaam leo asubuhi alipofika nyumbani kwake kujitambulisha na kumjulia hali pamoja na kumueleza mambo kadhaa ya maendeleo yaliyofanyika.

"Tunakuomba mola wetu kuwapa moyo wa imani na uzalendo na kuwaepusha na mabaya yote  Mkuu wetu wa Mkoa Paul Makonda, Rais wetu Magufuli pamoja na viongozi wote ili waliongoze taifa letu kwa amani" alisema Mufti Zubery" wakati akiomba dua hiyo.

Makonda akizungumza na Mufti Zubery nyumbani kwake Mikocheni alimwambia kuwa kuna mambo kadhaa ameyafanya kwa kushirikiana na watendaji wenzake kwa kukutana na waendesha boda boda ili kuwawezesha kupata mkopo utakaowasaidia kupata vitendelea kazi zao kama kupata kofia ngumu mbili za kuvaa dereva na abiria wake ili kuwasaidia katika shughuli zao za kusafirisha abiria.

Makonda alitaja mambo mengine kuwa ni suala zima la kupambana na uhalifu ambao bado unaonesha kupamba moto hasa ujambazi wa kutumia silaha za moto.

Alitaja mambo mengine kuwa ni mkutano alioufanya hivi karibuni wa kukutana na wenyeviti wa mitaa na maofisa watendaji ili kuzungumzia suala la utunzaji wa mazingira na mambo mengine ambapo alisema ameandaa mpango wa kumzawadia mwenyekiti atakayefanya vizuri kwenye mtaa wake.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum alisema jambo alilofanya Makonda la kumtembea Mufti ni jambo zuri na kuwa kumuona mufti ni sawa kama amewaona waislam wote nchini.

Alisema wanamuombea Makonda mungu amzidishie wepesi katika kazi zake kwani ni viongozi wachache wanaopata madaraka ambao uwakumbuka viongozi wa dini kama alivyofanya Makonda.

Katika hatua nyingine Makonda alifanya ukaguzi wa barabara kadhaa za Manispaa ya Kinondoni ambazo hivi karibuni aliagiza zifanyiwe marekebisho ikiwa ni pamoja na kuchimba mifereji baada ya kuharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Mfahamu Mtanzania Anayecheza Soka Uingereza Aliyekuja Kuitumikia Taifa Stars (+Video)

$
0
0
Adi Yussuf ni mtanzania anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya daraja la pili Uingereza kwenye klabu ya Mansfield Town. Adi pia amekulia katika klabu ya Leicester City ila kwa sasa yupo Tanzania kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Chad wa kuwania kufuzu michuano AFCON 2017 Gabon.

“Ni kweli mwanzo ilikuwa ngumu kwa klabu yangu ya Mansfield Town kuniruhusu nije Tanzania kwa sababu ilikuwa tunahitaji kupandisha timu, ila sasa wameniruhusu nije kuchezea timu yangu ya taifa” >>> Adi Yussuf

Zaidi angalia exclusive interview yake aliyofanya na Amhed Ally mwandishi wa Star Tv

Je Linah Sanga Amewahi Kutoa Rushwa ya Ngono? Majibu yako Hapa

$
0
0
Kipindi cha Enews kinachorushwa na East Africa Television kilitaka kufahamu kama kuna ukweli wasanii hao wa kike huhonga ngono ili wafanyiwe kazi nzuri kwenye hizo kampuni kubwa, Linah Sanga ambaye hata yeye amefanikiwa kufanya videos na waongozaji wakubwa wa video barani Afrika akiwepo Godfather alikuwa na haya ya kusema.
"Sijui kama ipo hivyo sababu mimi kama msanii wa kike sijawahi kufanya kitu kama hicho, kwa hiyo sidhani kama hicho kitu ni cha kweli kwa sababu ukifuatilia kwa wasanii wakubwa wa kike ambao tumeweza kufanya kazi na madirectors wakubwa kama God Father na wengine ni mimi, Vanessa, labda na Aika kwa sasa hivi ambao tayari tumeshatoa kazi zetu, kwa hiyo sidhani kama hicho kitu ni kweli kwa sababu tunafanya kazi na kazi zinalipa ndiyo maana tunaweza kufanya kazi na watayarishaji wakubwa kama hivyo". Alisema Linah Sanga.

Fatma Karume: Dk. Shein Siyo Rais Zanzibar

$
0
0
MJUKUU wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, amepinga hatua ya kumtangaza Dk. Alli Mohammed Shein, kuwa rais Visiwani, anaandika Pendo Omary.

Fatma Amani Abeid Karume, mtoto wa kwanza wa rais mstaafu, Amani Abeid Karume amesema, “Dk. Shein, siyo kiongozi halali wa Zanzibar. Amewekwa madarakani na jeshi na kinyume na Katiba na taratibu za nchi.”

Amesema, “Rais aliyewekwa madarakani na vyombo vya dola, siyo rais wa wananchi. Rais anayewekwa madarakani kwa nguvu za kijeshi na vitisho, hawezi kuwa rais wa wananchi. Anakuwa rais wa majeshi.”

Akiongea kwa sauti ya uchungu na MwanaHALISI Online, Jumatano wiki hii, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, Fatma amesema, “Chama Cha Mapinduzi, kisijidanganye. Zanzibar siyo shwari. Kinachotengenezwa sasa, siyo utawala. Ni muendelezo wa chuki, visasi na uhasama.”

Amesema, “CCM ya Tanganyika, ndiyo inayoiharibu Zanzibar. Wanalazimisha viongozi wasiokubalika na wananchi Visiwani kutawala kwa manufaa yao binafsi.”
Soma mahojiano kamili na mwanasheria huyo mashuhuri nchini, katika gazeti la MwanaHALISI Jumatatu wiki ijayo.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya March 26

$
0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya March 26

Mkuu wa Mkoa Anne Kilango Malecela Atema Cheche...Awakomalia Watumishe Hewa wa Serikali...

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela ametoa siku sita kwa Wakurugenzi wa Halmashauri tatu za Ushetu, Msalala na Kahama zilizopo wilayani Kahama kuhakikisha wanawakilisha kwake majina ya watumishi hewa ifikapo Jumatano ijayo.

Mkuu huyo wa Mkoa aliyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa halmashuri zote tatu za Wilaya ya Kahama muda mfupi baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja ya kukagua shughuli za maendeleo wilayani Kahama, ikiwa ni sambamba na kuwapa pole waathirika wa mvua kubwa ya mawe katika kijiji na Kata ya Mwakata.

Mvua hiyo ya mwanzoni mwa Machi mwaka jana ilisababisha maafa makubwa, ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 38 na kujeruhi wengine zaidi ya 80.

Kilango alisema lundo la watumishi hewa katika halmashauri hizo halikubaliki, hivyo ni wajibu wa wakurugenzi kuhakikisha kuwa majina yao yanawakilishwa ofisi ya mkuu wa mkoa sambamba na maelezo ya kumbukumbu zao za ajira, wanavyolipwa na kiasi wanacholipwa.

“Hata wakurugenzi wakiwaficha, tayari orodha yao ninayo mezani…naomba mniletee majina,” alisema mkuu huyo wa mkoa aliyeanza kazi hivi karibuni baada ya kuteuliwa na Rais John Magufuli.

Katika Awamu iliyopita ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete, Anne Kilango alikuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Pia aliwataka viongozi wa halmashauri hizo kuhakikisha wanaongeza kasi ya kukusanya mapato, ikiwa ni sambamba na kuongeza weledi ili mapato hayo yasipotee.

“Maendeleo ya Kahama yanatuhusu wote. Sipendi kumsimamisha mtu kazi kwa tuhuma za ubadhirifu, lakini ikibidi kufanya hivyo nitafanya kulingana na kasi ya uongozi wa Serikali ya Awamu Tano chini ya uongozi wa Rais John Magufuli,” alisema.

Askari Aporwa Bunduki Aina ya SMG na Majambazi

$
0
0
Watu saba wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na silaha mbalimbali za jadi, wamempora bunduki aina ya SMG askari polisi PC Shadrack.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, David Mnyambuga alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 2.36 usiku katika ofisi za Kampuni ya Simu za Mkononi ya Halotel, eneo la Medeli.

“Majambazi wapatao saba wakiwa na mapanga na nondo walifika katika ofisi hizo baada ya kutoboa ukuta na kumjeruhi askari kwa mapanga na nondo na kupora silaha aina ya SMG,” alisema.

Kamanda huyo alisema polisi walifanya msako mkali usiku huo na kufanikiwa kuipata silaha hiyo eneo la Mbuyuni.

“Mtu mmoja amekamatwa kuhusiana na tukio hilo na anaendelea kuhojiwa,” alisema.

Basi la Princess Muro Laacha Njia na Kuingia Kwenye Kituo cha Mabasi ya Mwendo Kasi

$
0
0
Basi la kampuni ya Princess Muro lapata ajali baada ya kupoteza mwelekeo na kuingia kituo cha Magari ya Mwendo kasi Kimara jijini Dar es Salaam.Endelea kufuatilia taarifa zetu tutakujuza kwa kina taarifa hii.

Mtanzania Aliyefungwa Gerezani China, Ampigia Simu Millard Ayo Akiwa Ndani ya Gereza..(+Audio)

$
0
0
Mtanzania aliyefungwa gerezani China, ampigia simu Millard Ayo akiwa ndani ya gereza na kuelezea namna alivyokamatwa kwa ishu za dawa za kulevya, maisha wanayoishi gerezani na Idadi ya Watanzania waliofungwa huko.

Katika exclusive interview Mtanzania huyu anasema ‘Ilikuwa mambo ya madawa, mimi nilikuwa nimetoka Dubai kuja China, jamaa wakaingia katika hoteli na wakatukamata, jumla tulikuwa watu nane‘

‘Ujue nchi hii mambo ya madawa wanapiga vita mno, kesi ya madawa zina adhabu ya miaka mingi kuliko kesi nyingine yoyote, kama mimi nimepewa miaka kumi na miezi sita‘

‘Mimi nimefungwa nikiwa na miaka kama 26, nilianza kufanya biashara ya dawa za kulevya nikiwa na miaka kama 18, hawa jamaa wa China ni wabaguzi sana, hivyo unatakiwa uwe kauzu ili kuendana nao sawa‘

Full stori nimekusogezea hapa chini…


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Adai Yeye Ndo Mwanzilishi wa Wazo la Kuhakiki Silaha Kabla ya Paul Makonda wa Dar

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda amesema kazi ya kuhakiki silaha iliyoanza kwa wakazi wa Dar es Salaam, ilishaanza mkoani mwake takribani miezi miwili iliyopita na kwamba ndiyo maana matukio ya kihalifu kwa Arusha yamepungua.

Ntibenda alisema hayo jana katika kikao cha Baraza la Ushauri la Mkoa wa Arusha na kusema yeye ndiye mwanzilishi wa wazo la kilichoazishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hivi karibuni.

Alisema wakati wakisubiri kuapishwa katika viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam aliwaeleza wakuu wa mikoa jinsi alivyofanikiwa kudhibiti uhalifu kwa kuwataka wakazi wa Jiji na mkoa wa Arusha kuhakiki silaha zao.

‘’Kazi inayofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ni wazo langu kwani sisi Arusha si mnaona uhalifu umepungua kwa asilimia kubwa sana? Hiyo ni kwa sababu wengi wana silaha, lakini si mali zao,’’ alisema.

Akizungumzia ulinzi, Ntibenda alisema hiyo inatokana na jitihada za kamati ya ulinzi na usalama kuthibiti kwa kiasi kikubwa uhalifu na matukio yasiyokuwa na amani na sasa Jiji la Arusha liko katika hali ya utulivu wa hali ya juu.

Alisema katika kipindi cha Januari mwaka jana hadi Desemba mwaka jana, jumla ya magunia 270 ya bangi yenye uzito wa kilo 2,500 na ekari 25 za mashamba ya bangi yaliteketezwa kwa kuchomwa moto.

Mkuu huyo alisema operesheni hiyo ilifanyika katika vijiji vya Imbibya, Ngarelaoni, Kisimiri Juu na Oldonyosambu na watuhumiwa 180 walikamatwa na kesi 160 zilifikishwa mahakamani.

Akizungumzia zuio la kutocheza `Pool’ saa za kazi, Ntibenda alisema wakuu wa wilaya na wakurugenzi ni lazima washiriki kikamilifu kupiga vita mchezo huo kuchezwa wakati wa kazi kwani ni jukumu la kila mmoja hapa na sio la mtu mmoja mmoja.

Mashabiki Wakerwa na Kauli Hii ya Zari, Wadai Amewakejeli Maskini

$
0
0
Labda ukweli unauma.. Kwamba wengi tunatamani sana maisha mazuri anayoishi Diamond na mchumba wake, Zari the Bosslady. Wapo wanaoishia kutamani na kumuomba Mungu nao waje kuwa na maisha hayo, wengine hushukuru na hufurahi tu kwa kile walichonacho ama tumeseme wameridhika na kidogo wanachopata.

Lakini wapo ambao hushindwa kujizuia kupata wivu na kuwachukia tu watu wenye mafanikio – wa kuitwa haters. Hayo ni majaribu makubwa waliyonayo mastaa duniani. Lakini sio mara zote huvumilia matusi na kejeli wanazozipata kwenye mitandao ya kijamii.

Wakati Zari akiendelea kula raha Ulaya na mchumba wake Diamond, ameendelea kutupiwa vijembe na watu kuwa hawajali tena wanae watatu aliowaacha Afrika Kusini, kwamba kila siku kiguu na njia na Diamond. Hilo limemkera, na ameamua kulijibu.

Staa huyo amepost picha hiyo juu na tafsiri yake kwa maneno hayo ni:

Watoto wangu wameniuliza, kwanini kila mtu amechukia? Nimewaambia tuna vitu ambavyo hawana. Wakati mnachukua, mimi naenda mall, kumwaga fedha. Naweza, huwezi

Lakini pia aliweka caption isemayo: Baadhi yenu hamtaelewa hili lakini ni sawa. Ninawajibika kwa ninachoandika, na sio unavyokielewa.


Hilo limeonakana kuwakera wengi, wakiwemo mashabiki wake. Baadhi waliongea mambo mazito kiasi cha kumfanya awajibu pia.


Well, good news ni kubwa ex wake, Ivan, amewachukua wanae na kuwapeleka kwenye kisiwa cha maraha cha Ibiza kula pizaa! So waswahili wanasema hiyo ni ngoma drooo… Pesa inaongea!!

Watu Wawili Wauawa Na Majambazi Jijini Mwanza. Wengine Saba Wajeruhiwa.

$
0
0
Watu wawili wameuawa Jijini Mwanza kwa kupigwa risasi na Majambazi, huku Wengine saba wakijeruhiwa katika tukio la uvamizi wa duka lililokuwa likitoa huduma mbalimbali za kifedha.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Justus Kamugisha, amesema kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa mbili usiku katika eneo la Bugarika Sokoni, baada ya watu watatu wanaosadikika kuwa ni majambazi waliokuwa na bunduki aina ya SMG kuvamia katika duka la mfanyabiashara na mkazi wa eneo hilo aitwae Daniel Marwa (30).

Kamanda Kamugisha amewataja waliouawa kuwa ni Julius Wankaba (30) ambae ni dereva bodaboda, pamoja na mfanyabiashara mmoja mwenye duka katika eneo hilo aliefahamika kwa jina la Mama Yuni (35).

Amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Magesa Mungari (38), Simioni Charles (26) ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando huku wengine wakiwa ni Mwita Ryoba (30), Frank Willium (19), Saumu Said (20), Masumbuko Kanduru (38) pamoja na Emmanuel Francis ambao wanapata matibabu katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure.

Baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo, akiwemo mmiliki wa duka lililovamiwa, wanasema majambazi hao walipofika eneo la tukio walianza kufyatua risasi ovyo ili kuwatawanya wananchi waliokuwa wamekusanyika katika eneo hilo wakiangalia taarifa ya habari na wengine wakinywa kahawa,  na hivyo kusababisha wananchi kutawanyika jambo lililosababisha vifo na majeruhi hao.

Katika tukio hilo, Majambazi hao walifanikiwa kupora fedha taslimu kiasi cha Shilingi Milioni Mbili, Vocha za simu za mitandao mbalimbali zinazokadiliwa kuwa za shilingi Laki Nane pamoja na simu sita za wateja.

Kamanda Kamugisha amesema Jeshi la polisi Mkoani Mwanza limeanzisha msako mkali ili kuwakamata waliohusika na tukio hilo, huku likiahidi zawadi ya fedha kiasi cha shilingi Milioni Moja kwa yeyote atakaesaidia kufanikiwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linaendelea kumsaka mtu aliehusika na wizi wa mtoto mwenye umri wa siku moja katika Hospitali ya Wilaya ya Magu, ambapo tukio hilo limetokea Machi 23 mwaka huu, majira ya saa nane mchana baada ya mtu mmoja asiefahamika mwenye jinsia ya kike, kufika katika wodi ya wazazi na kumuiba mtoto huyo wakati mama yake amelala.

Aidha katika katika kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, Jeshi hilo limepiga marufuku watoto kwenda kuogelea katika fukweni (Beach) pamoja na uwepo wa disko toto Jijini Mwanza.

Maalim Seif Sharif Hamadi Arejea Zanzibar Baada ya Kukaa Mapumzikoni Serena Hoteli Kwa Siku 17

$
0
0
Siku chache baada ya Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein kuapishwa baada ya kushinda uchaguzi wa marudio uliosusiwa na baadhi ya vyama vya upinzani, Katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amerejea Zanzibar.

Maalim Seif ambaye alikuwa mapumzikoni katika hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar es Salaam kwa takribani siku 17, jana alirejea Zanzibar kuendelea na mapumziko yake.

Maalim Seif alilazwa katika Hospitali ya Hindu Mandal ya jijini Dar es Salaam,mara baada ya kuruhusiwa March 8 mwaka huu alishauriwa na Daktari wake kupata mapumziko ya muda mrefu.

Kurejea kwa Maalim Seif visiwani humo kunazidisha shauku na kiu ya baadhi ya Wazanzibar kutaka kusikia atakachokisema kiongozi huyo wa upinzani mwenye ushawishi mkubwa kwenye jamii.

Maalim Seif aliugua wakati Wazanzibar wakiwa katika maandalizi ya kurudia uchaguzi mkuu uliofanyika March 20, mwaka huu baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25  mwaka  jana na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar( ZEC), Jecha Salim Jecha kwa madai kuwa uligubikwa na dosari nyingi.

Gharama za Hotelini
Taarifa zilizoripotiwa kwenye vyombo vya habari siku chache zilizopita zilidai kuwa kila siku aliyokaa kwenye hoteli hiyo, Maalim Seif alikuwa akitumia wastani wa Sh. 6,162,500.

Kutokana  na  takwimu hizo, hadi kufikia jana, Maalim Seif atakuwa ametumia kiasi kisichopungua sh. Milioni 92.4

Chumba alichokuwa akilala Maalim Seif katika Hoteli hiyo yenye hadhi ya nyota tano kinalipiwa dola za Marekani 2,500 kwa usiku mmoja.

Maalim Seif alikuwa akiishi hotelini hapo na wasaidizi wake watano, ambao wote gharama zao zinalipwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)

Kasi ya Magufuli Yabaini Watumishi Hewa 515 Katika Mikoa Mitatu Mpaka Sasa....

$
0
0
Siku 15 zilizotolewa na Rais Magufuli kwa Wakuu Wapya wa Mikoa kuhakikisha wanawabainisha na kuwaondoa wafanyakazi hewa zimeanza kutoa picha kuhusu tatizo la wafanyakazi hewa nchini.

Mpaka sasa imebainika kuna wafanyakazi 515 katika mikoa mitatu ambayo ni Kigoma (169), Dodoma (144) na Singida (202).

Taswira hii inaonyesha jinsi ambavyo tatizo la wafanyakazi hewa linaweza kuwa ni kubwa zaidi ya ilivyofikiriwa hasa ikichukuliwa limekuwepo kwa muda mrefu huku mamilioni ya pesa za walipa kodi yakienda kwenye mifuko ya wajanja wachache.

Inakadiriwa serikali ina wafanyakazi zaidi 500,000 na inalipa mishahara takriban Sh. bilioni 549 kwa mwezi, ambayo kati ya fedha hizo kuna malipo ya wafanyakazi hewa.

Katika repoti yake ya mwaka 2013/14, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alibainisha kuna zaidi ya Sh141.4bn zimelipwa kwa wafanyakazi hewa katika mwaka wa fedha.

Dudubaya Afunguka...Watu Mfano wa Chid Benz Hawatakiwi Kusaidiwa Kabisa...Kifo Anakitaka Mwenyewe

$
0
0
Baada ya rapa Chidi Benz kuomba msaada ili asaidiwe kuirudisha afya yake ambayo imethorofika kutokana na matumizi ya Madawa ya kulevyana na baadae kusaidiwa na Babu Tale kwa kupelekwa rehab. Wadau mbalimbali pamoja na wasanii wenzake walimpongeza Babutale lakini Dudu Baya amedai hakupenda rapa huyo asaidiwe.
Dudu

Akizungumza na Bongo5 Jumamosi hii, Dudu amedai rapa huyo hakuwa tayari kusaidiwa ndio maana baada ya kusaidiwa anataka kujipangia baadhi ya mambo.

“Watu mfano wa Chidi Benz hawatakiwi kusaidiwa, niwakuachwa wafe na wazikwe. Kwanza ni waongo, ukikutana nao utasikia naumwa au nimefiwa, utampa msaada, mwisho wa siku anaenda kujidunga. Misaada kama hii inatufanya majina yetu kuwekwa kataka orodha ya wauaji (killers),” alisema Dudu.

Aliongeza, “Babutale na wenzake walipomfisha Chidi Benz rehab kwanza alianza kuweka masharti yake kituoni, mara hawezi kushauriwa na mtu ambaye hajawahi kutumia sumu hiyo (unga). Hapo ndipo nilipogundua amebebwa kinguvu bila yeye kuwa tayari kupona. Ni sawa na mgonjwa apelekwe hospitali then aanze kutoa masharti yake, eti hiki kitanda sikitaki. Wewe dokta huwezi kunitibu kwa sababu hujawahi kuumwa ugonjwa ninaoumwa, mgonjwa kama huyo si nachotaka ni kifo?. Hata wakati yesu amekuja kutukomboa na dhambi, aliponya wagonjwa waliokuwa tayari kupona, hata leo umpeleke ndugu yako kanisani au msikitini akaombewe aache ulevi au umalaya, kama hana dhamira ndani ya moyo wake ya kuacha, hakiwezi tokea chochote,”

Pia Dudu amesema wasanii wengi wanasikia kila siku kuhusu madhara ya Madawa ya kulevya lakini wanapuuzia.

“Chidi Benz si mtoto mdogo, ameshuhudia wasanii na watu wa kawaida wengi tukiwapoteza kwa sababu ya Madawa ya kulevya lakini wanapuumzia, wanarudia kubwia tena. iweje leo yeye ajiingize kataka ulimwengu huo? hakika kifo anakitaka mwenyewe na si kurubuniwa. Uzuri wa Tanzania hatuna umasikini wa ardhi, watu kama hawa hawana faida kwa taifa, niwakuacha wafe na wazikwe. Na kama inawezekana Mh Rais Magufuli angetoa amri mateja wakifa wazikwe na jiji. Kwa sababu sioni ndugu yeyote wa Chidi yuko bize na rapper huyo. Kwanini nyingi mumpaparikie au ndio mnauchukungu kuliko ndugu zake?. Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu,” alisema Dudu.
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images