Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Amuapisha Mkuu Wa Mkoa Mpya Wa Songwe Mhe. Chiku Gallawa Ikulu Dar Es Salaam

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Luteni Mstaafu Chiku Gallawa kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016

Jinsi Bifu la Diamond na Alikiba Linavyowanufaisha Wasanii wa Nje

$
0
0
Ni ukweli kuwa Diamond na Alikiba ni wasanii ambao hawapatani kwa muda mrefu.
Kutokana na ugomvi wao uliopo umepelekea mpaka mashabiki wao kuanzisha team, team hizi zinakuwa zinamsupport msanii wao na kumpinga mpinzani wao.

Diamond aliwahi kuhojiwa kwenye kipindi cha Sporah Show alisema, “Kuna wimbo wa Alikiba ‘Singel Boy’ nilimuomba Alikiba kuingiza sauti tulipokuwa studio alikataa na kusema kuwa nataka mteremko.”

Alikiba aliwahi kusema, “Kwenye wimbo wa ‘Lala Salama’ niliingiza sauti yangu lakini nilishangaa kuona sauti yangu imefutwa kwenye wimbo huo, kibaya zaidi ametumia melody yangu niliyorekodia mwanzo.”

Hakuna mwenye uhakika wa hili kuwa nani ni mkweli na nani anatudanganya. Ugomvi wao unazidi kuwa mkubwa kila siku, sasa hivi umeenda mbali zaidi mpaka msanii atakayekuwa karibu na mmoja kati ya hawa wawili wenye ugomvi mwingine anakuwa anachukia.

Ukiwa karibu na msanii mmoja unakosa support ya upande wa pili, hata kama umeingia kwenye mashindano hutaweza kupigiwa kura na mashabiki wa team nyingine. Hili linarudisha nyuma muziki wetu Angalia kilichotokea kwa Ommy Dimpoz hutataka kuangalia tena nyuma, unakumbuka Wema Sepetu mwanzo alikuwa team gani na sasa yuko wapi? Vipi Jokate kilichomtokea kwenye pande zote mbili kwa sasa unadhani atakuwa wapi tena?

Angalia support wanayopeana Wanigeria kwenye tuzo na muziki wao, hawaonyeshi tofauti zao japo wapo wengi hawapatani. Kwanini tugombee fito wakati tunajenga nyumba moja? Ni ukweli usihitaji ushahidi, Diamond akiingia kwenye tuzo zozote mashabiki wa Alikiba hawampigii kura wanaona ni bora kumpigia kura msanii wa nje ili Diamond akose hiyo tuzo.

Hilo pia lipo kwa upande wa pili kama Alikiba akiingia kwenye mashabiki wa Diamond hawampigii kura. Hata kama Wizkid ana ugomvi na Davido mashabiki wao hawawezi kumpigia kura Diamond au Alikiba ili ashinde tuzo.

Kuna haja wa kuweka tofauti pembeni na kuhakikisha muziki wetu unafika mbali zaidi, ‘Kidole kimoja hakivunji chawa’, unajisikiaje tunaposhiriki kwenye tuzo za nje kwenye category moja unawaona wapo wasanii wanne kutoka Nigeria na mmoja tu ndiyo wa Tanzania.

Utajisikiaje siku ukiona Jay Z akapenda kufanya kazi na msanii wa Tanzania? Kwa hili lililopo sasa hivi kufika huko ni mbali sana, kila team inafanya msanii mwingine asifanikiwa. ‘Adui muombee njaa’, kwetu imekuwa tofauti tunaombeana wenyewe hiyo njaa.

Dogo Janja: Shule Sio Kitu cha Kufanya Kwa kuiga, Siitaki Tena (Video)

$
0
0

“Msomi Nick wa Pili, mimi niliachaga Makongo,” anasema Dogo Janja kwenye wimbo wake mpya, My Life.

Na sasa rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa hawezi tena kurudi shule.

“Siku zote linapokuja suala la elimu, sio kitu cha kufanya kwaajili ya kuiga na pia unatakiwa ufuate kichwa chako kinaenda vipi. Sometimes watu wanaweza wakawa wanakuforce sana ‘soma, soma’ lakini wewe mwenyewe unakuwa unaangalia future yangu mimi haipo kwenye kusoma,” amesema.
“Au hata nikipelekwa kusoma, siwezi nikafanya vizuri, kwahiyo ni bora ukomboe hela za watu wanaotaka kukusaidia kukupeleka shule,” ameongeza.
“Kama kuna kitu cha kusomea nitasoma, lakini sio ile elimu ya kuvaa masare, kukimbia pale getini pale Makongo, kutembea na mguu, Mwenge to Makongo, hapana siwezi.

Machangudoa Wanne Kati ya Kumi Wanaojiuza Wanamaambukizi ya Virusi vya Ukimwi.....

$
0
0
Utafiti uliofanywa na Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na upimaji wa virusi vya Ukimwi la MATUMAINI, unaonyesha kuwa kati ya wanawake kumi wanaofanya biashara ya ngono wanaopima wanne kati yao wanakutwa na virusi vya Ukimwi.

Akizungumza na East Africa Radio Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Bw. Onesmo Mwihava amesema wamekuwa wakifanya zoezi la upimaji katika maeneo ya majumba ya starehe, baa na katika baadhi ya madanguro yasiyo rasmi na kuwa licha ya kuwepo kwa jitihada za serikali katika kutokomeza biashara ya ngono lakini wengi wa wanaojiuza wanakutwa wameathirika ama kuwa na magonjwa ya zinaa.

Aidha, Bw. Mwihava amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakijihadhari na suala la kupata mimba na kuacha kuchukua tahadhari kuwa katika kupata maambukizi pamoja na magonjwa ya zinaa ambapo katika utafiti wao, kati ya watu kumi waliojitokeza kupima kati yao sita huwa na magonjwa ya zinaa.

Ameongeza kuwa mojawapo ya waathirika wakubwa wa ugonjwa wa ukimwi pamoja na magonjwa ya zinaa ni vijana kutokana na kutochukua tahadhari kwa kufanya ngono zembe na kuwa hali hiyo mara nyingi hutokana na kiwango cha fedha alizotoa kwaajili ya huduma hiyo.

Mwihava amezitaka taasisi na serikali kulivalia njuga suala la kutokomeza biashara ya ngono pamoja na kutoa elimu kwa vijana na wanaojihusisha na vitendo hivyo haswa baada ya kukamatwa kwakuwa kwa sasa wanawake hao wengi wameanzisha mbinu mpya kwa kukaa katika baa na majumba ya starehe na kutoka na wateja.

Babu Tale Atangaza Vita na Baghdad...Kisa Kizima Hichi Hapa

$
0
0
Msanii Baghdad ambaye kwa sasa anafanya project yake ya Old is old ya kurudia nyimbo za wasanii wa bongo fleva, amefunguka kuhusu bifu yake na meneja wa wasanii Babu tale.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Arica Radio, Baghdad amesema chanzo cha ugomvi huo ni kipande cha video kilichotengenezwa na director wake ili akipost kwenye mitandao ya kijamii kutengeneza promo, na yeye kukipost kwenye group la wasanii, ndipo Babu Tale akaja juu.

“Mi nilichofanya nilichukua ile clip nikaituma kwenye group la wasanii wa Tanzania, baada ya kukituma kule baada ya dk 15 nikaona Tale kapost katuma maneno makali sana, ole wake msanii atakayepost hii ntatuma 'team zangu' wamtukane, ole wenu sasa ndo nataka niwaonyeshe utandale, halafu we Baghdad usinichukulie poa, mi nikakomenti kwa muuliza 'Babu tale every thing you know wakati narekodi', tukaongea kwenye simu nikawa namwambia na nakuchana kwenye wimbo, and he was ok”, alisema Baghdad.

Lakini pia Baghdad alielezea kitendo cha yeye kutolewa kwenye group hilo la wasanii wa Tanzania, na kuleza hisia zake huku akihoji kama group hilo ni la wasanii wote au ni la babu Tale na wasanii wake?
“Nilishangaa baada ya kuona amenitoa kwenye group baada ya kuona ile clip ya video, sasa.

alivyonitoa mi nilikuwa najiuliza maswali mengi, lile group la wasanii lililoanzishwa ni group la Babu Tale featuring wasanii au la wasanii kama wasanii, kwa sababu kama mi nimewachana wasanii its ok ningeweza kupata adhabu hiyo”, alisema Baghdad.

Tazama Video Jinsi Raila Odinga Alivyoanguka Jukwaani Wakati Akihutubia Wananchi Siku ya Pasaka....

$
0
0
Cord leader Raila Odinga is reportedly nursing injuries after he was injured during a recent trip to Mombasa County.

Odinga was addressing his supporters when a dais he was speaking on collapsed and leaders fell to the ground.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya March 29

$
0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya March 29

Wafuasi Zaidi ya 600 wa UKAWA Wakiongozwa na Freeman Mbowe Wafanya Tukio Kubwa Nyumbani Kwa Lowassa

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe, amewashauri Watanzania wasife moyo kwa matokeo mabaya ya uchaguzi yaliyopinduliwa; na kwamba matokeo hayo yawe chachu ya kufanya  vizuri zaidi katika uchaguzi ujao.

Amesema uchaguzi si tukio, bali mchakato; na kwamba kama kuna watu wamekufa moyo kwa sababu ya kilichofanywa na serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupindua matokeo, hasa ya urais,  watafakari upya na wajipange kwa kazi kubwa inayokuja, kwani mafanikio ya kisiasa hayapimwi kwa tukio moja la uchaguzi na matokeo yake. Alisema matokeo hayo yanapswa kuwatia hasira na kuwahamasisha waendelee kupambana,

Mbowe aliyasema hayo Masaki, nyumbani kwa Edward Lowassa, Waziri Mkuu wa Zamani ambaye pia alikuwa Mgombea Urais wa Chadema aliyeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwenye hafla ya kumshukuru Mungu iliyoandaliwa na familia hiyo. Ukawa unaundwa na Chadema, Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD.

“Hatukushinda serikali kuu kama tulivyokusudia na kupenda iwe kwa sababu ambazo si wakati wake kuzisema sasa, lakini ni vema tukumbuke kwamba mapambano tunayofanya, kama kuna yeyote miongoni mwetu anafanya kwa ajili yake binafsi, ana wajibu wa kujitafakari upya,” amesema Mbowe.

Aliongeza kwamba, kazi ya mapambano wanayofanya viongozi sasa ina manufaa kwa kizazi kijacho, na kama wanaoifanya sasa wakafanikiwa kuonja matunda ya kazi ya mikono yao basi ni jambo la kumshukuru Mungu.

“Kazi anayofanya Lowassa (Baba Kadeti) si lazima aone matunda yake leo, huenda mtoto wake ataonja na asipoonja Kadeti basi wajukuu wataonja matunda hayo na kutambua mchango mzuri wa babu yao kwa kazi kubwa ya maana anayofanya sasa,” amesema.

Aliwahimiza Watanzania zaidi ya 600 waliokuwepo kwenye halfa hiyo kuwa wale walio wafuasi wa vyama vya siasa hata wasio na vyama wana wajibu wa kuendelea kwa nguvu zote na kazi ya kupambana ambayo Lowassa amejiunga nayo, kwani wakati wa uchaguzi watu wengi walipigana kumsaidia sio kwa ajili ya familia yake ila walifanya vile kwa sababu ya nchi hii, huku Lowassa akiwa kiongozi na mpeperusha bendera.

Mbowe alitumia fursa hiyo kuwataka watanzania waendelee kumwombea neema, ujasiri na afya njema Lowassa kwani taifa bado linamhitaji kuliko pengine anavyohitajika na familia yake.

Aidha, Mbowe alimsifu pia Regina, mke wa Lowassa, kwa ujasiri wake na familia nzima kwa uamuzi mzuri na ujasiri aliochukua katika kuhakikisha Watanzania wanatafuta haki na ujasiri kwa kukata minyororo ya watesi.

“Mama ulikuwa mwoga kwenye kampeni katika hatua za awali, lakini baadaye ulipata ujasiri kama mgombea mwenyewe. Asante sana kwa kuondoa woga; asante kwa kuongoza familia, na sasa tuendelee na mapambano.” alihimiza Mbowe

Kabla ya Mbowe kusimama, neno la kuwashukuru watu waliofika nyumbani lilitolewa na Regina akasema familia, hasa Lowassa mwenyewe, ilikuwa inasubiri kwa hamu siku ya kumshukuru Mungu na Watanzania kwa mazuri mengi aliyowatendea.

Hafla hiyo ya shukrani ilianzia kwa ibada katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front, Dar es Salaam. Lilichagizwa na nyimbo kadhaa za shukrani zilizopendekezwa na Lowassa mwenyewe, na kuimbwa na washiriki wote, wakiwamo wa madhehebu mengine ya dini.

Miongoni mwa washiriki wa hafla hiyo ni baadhi ya wanachama wapya wa  UKAWA waliojiengua CCM mwaka jana, wakiwamo Hamisi Mgeja, Mgana Msindai, Lawrence Masha, John Guninita, na wengine.

Ilihudhuriwa pia na wanasiasa, viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali, vijana na wazee, matajiri na watu wa kawaida kutoka sehemu mbalimbali.

“Tumepata mengi mazuri, tunaweza kusafiri kwenda Monduli na kurudi si sababu tuna magari mazuri kuliko wengine; tunaweza kusafiri kwa ndege na tukarudi salama, lakini hata wakati mwingine unasikia mtu anakupigia simu kukusalimu au kukuandikia ujumbe mzuri wa faraja, haya yote  ni sababu ya Mungu na tukaona leo tufike Kanisani kusema Mungu asante kwa mema yote uliyotujalia,” alisema Regina akiwa amejawa tabasamu muda wote, huku akishangiliwa.

Wajukuu wa Lowassa walijumuika kumwimbia babu yao wimbo kutoka miongoni mwa tenzi za Injili zilizoandaliwa kwa ajili hiyo, huku wakiongozwa na mpiga kinanda.

Baada ya wajukuu, Masha alitumbuiza washiriki kwa wimbo wa Kiingereza “Amazing Grace,” akatuzwa kiasi cha Tsh. 50,000 ambacho, hata hivyo, alikigawa kwa wajukuu wa Lowassa


Vigogo Wawili Maliasili Waliotoa Vibali vya Kusafirisha Tumbili Watiwa Mbaroni

$
0
0
Kikosi kazi maalumu cha kuchunguza makosa makubwa ya kihalifu kimewatia mbaroni vigogo wawili wa Wizara ya Maliasili na Utalii, wakihusishwa na utoaji wa kibali cha kusafirisha tumbili 61 kwenda nchini Albania.

Maofisa hao ni Mkurugenzi wa Idara ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Dk Charles Mulokozi na ofisa mfawidhi wa kituo cha uwindaji wa kitalii, utalii wa picha na Sites cha jijini Arusha, Nyangabo Musika.

Kikosi hicho kinaundwa na wachunguzi kutoka Polisi, Idara ya Uhamiaji, Usalama wa Taifa, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kikosi cha kupambana na ujangili nchini na Takukuru.

Wakati Dk Mulokozi anakamatwa, tayari alikuwa amesimamishwa kazi kwa agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe kwa kutoa kibali wakati Serikali ilishazuia.

Vyanzo mbalimbali vimesema jana kuwa Dk Mulokozi alikamatwa mwishoni mwa wiki na jana alisafirishwa chini ya ulinzi kwenda kituo cha polisi cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia).

“Hivi tunavyozungumza, Dk Mulokozi yuko njiani anapelekwa Kia chini ya ulinzi mkali wa polisi.Nyangabo yeye tayari yuko mikononi mwa vyombo vya ulinzi na usalama pale Kia,” kilidokeza chanzo chetu cha uhakika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alipoulizwa jana hakukanusha wala kukiri kuwa na taarifa za kukamatwa vigogo hao, lakini alisema atakuwa na mamlaka ya kuliongelea wakiingia mkoani kwake.

“Bado sijapewa hizo taarifa, lakini hata kama ningezijua nisingeweza kuzungumzia tukio la kukamatwa kwao lililofanyika mkoa mwingine. Nikikabidhiwa ndiyo naweza kusema chochote,” alisema Kamanda huyo. 

Hata hivyo, Waziri Maghembe alithibitisha kukamatwa kwa vigogo hao, akisema katika tukio hilo yeyote aliyetia mkono wake lazima akamatwe na kushitakiwa.

“Ni kweli Dk Mulokozi amekamatwa na siyo yeye tu kuna ofisa mwingine pale ofisi yetu ya Arusha naye tumemkamata. Hatuna mchezo katika suala hili,” alisisitiza.

Profesa Maghembe alitumia fursa hiyo kusisitiza kuwa raia wa Uholanzi waliokamatwa na polisi hawakuwa na vibali halali vya kufanya biashara ya kusafirisha wanyama hai kwenda nje ya nchi kama baadhi ya watu wanavyodai.

“Hawa Waholanzi walikuwa na tourist visa (waliingia kama watalii). Halafu Watanzania waelewe mtu hawezi kupata kibali cha kusafirisha mnyama hai kabla ya kumkamata, kuhesabiwa, akakaguliwa na kupata vibali stahiki,” alisisitiza.

Raia hao wa kigeni ambao ni ndugu wa familia moja, Artem Alik Vardanyian (52) ni mkurugenzi wa mgahawa huko Uholanzi na Eduard Alik Vardanyian (44), meneja wa hoteli huko huko Uholanzi.

Hata hivyo, vyanzo vingine vimedai  kuwa pamoja na kuwapo kwa vibali hivyo, lakini hapakuwapo na “release order” inayotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kama sheria inavyoelekeza.

Chanzo hicho kilidai wanyama hao walikuwa wasafirishwe kwa kutumia ndege ya mizigo ya kukodi ambayo ilitokea Afrika Kusini na ilikuwa iwapeleke wanyama hao Albania kupitia Nairobi nchini Kenya na Nigeria.

“Hao marubani wa hiyo ndege waliitwa pale Polisi (Kia), wakaandikisha maelezo yao kuwa walikuja kuchukua wanyama hao na wakaambiwa wao waondoke tu hakuna mnyama anaondoka,” alidokeza ofisa mmoja katika uwanja wa Kia.

Dk Shein amteua Balozi Seif Ali Idd Kuwa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar

$
0
0
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein amemteua Balozi Seif Ali Idd kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa visiwa hivyo.

Kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 39 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Dk Shein amemteua Balozi Idd ambaye alikuwa na wadhifa huo hata kipindi kilichopita.

Uteuzi wa Balozi Idd aliyezaliwa Februari 23, mwaka 1942, ulianza jana ikiwa ni siku nne tangu kuapishwa kwa Shein kuwa Rais wa Zanzibar.

Balozi Idd anakuwa mtu wa pili kuteuliwa na Dk Shein baada ya kuteuliwa kwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said mwishoni mwa wiki.

Dk Shein sasa atakuwa na wakati mgumu wa ama kumteua au kutomteua Makamu wa Kwanza wa Rais ili kukidhi matakwa ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwani hakuna chama cha upinzani kilichokidhi vigezo vya kushirikishwa katika kuunda Serikali.

Rais Magufuli Akabidhiwa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

$
0
0
Rais John Magufuli, ambaye amejipa kazi ya “kutumbua majipu”, sasa anaweza kufanya kazi yake vizuri zaidi baada ya kukabidhiwa ripoti tano na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambazo anaweza kuzitumia kama kitendea kazi.

Tangu aingie Ikulu, Rais Magufuli na Serikali yake amekuwa akifanya kazi ya kuibua uozo kwenye taasisi za Serikali, kusimamisha na kutengua uteuzi wa watumishi wa umma wanaojihusisha na ufisadi na wakati fulani amekuwa akiitaja ripoti iliyopita ya CAG kuwa ndiyo iliyoanika uozo anaofanyia kazi.

Jana, “mtumbua majipu” huyo alikabidhiwa ripoti ya kwanza ya CAG tangu aapishwe kuwa Rais Novemba 5 mwaka jana na sasa ana kitendea kazi rasmi cha kufanyia kazi.

CAG Mussa Assad alimkabidhi Rais Magufuli taarifa ya ukaguzi wa hesabu za Serikali ikiwa ni kwa mujibu wa Katiba inayomtaka akabidhi ripoti hizo kwa Rais kabla ya mwisho wa mwezi Machi.

Taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, kaimu mkurugenzi wa mawasiliano – Ikulu, Rais Magufuli, ambaye aliwaomba wabunge kumpa ushirikiano katika kutekeleza kazi za wananchi wakati akizindua Bunge Novemba 20, atazikabidhi ripoti hizo kwenye chombo hicho ndani ya siku saba za mwanzo za Mkutano wa Tatu wa Bunge la Kumi na Moja utakaofanyika mjini Dodoma kuanzia Aprili 19.

“Rais Magufuli amempongeza CAG na timu yake kwa kuandaa taarifa hiyo na ametoa wito kwa chombo hicho kuendelea kufanya kazi kwa uhuru na ufanisi. Ameahidi kuwa serikali itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha kazi zake,” inasema taarifa hiyo. 

Kutana na Bilionea Mtanzania Anaetaka Kuanzisha Benki yake… Anawazia Kuinunua BARCLAYS Tanzania!

$
0
0
Inabidi ujue Tanzania inao watu wenye pesa zao na wanayo malengo au mipango mikubwa zaidi ya kibiashara ambayo kama ikienda inavyotakiwa wanaweza kuifanya nchi hii kutajwa zaidi kuwa na matajiri miongoni mwa nchi zenye Mabilionea Afrika.

Kituo cha Television cha Marekani CNN kilimuhoji Mtanzania huyu na kikaweka kichwa cha habari ‘kutana na Bilionea mwenye umri mdogo Afrika‘ ni Mohammed Dewji ambaye ameajiri watu karibu elfu ishirini na nane kutokana na viwanda na biashara zake.

Mbunge huyu wa zamani wa Singida mjini amesema ‘nimekua nikitaka kununua Benki kwa miaka minne mitano iliyopita, sasa hivi nimeamua nataka kuanzisha Benki yangu kabisa japokuwa hii ishu ya Benki ya Barclays Afrika kuuzwa imekuja na nashawishika japo sijajua kama wanataka mnunuzi atakaeichukua Afrika nzima‘

‘Nimeshawishika kuinunua Barclays upande wa Afrika Mashariki na ninayo pesa tayari, sijajua wanaiuzaje lakini sina mpango wa kuichukua Barclays yote kwa Afrika, ningependa kuinunua upande wa Afrika Mashariki kwenye nchi za Kenya, Uganda, Tanzania yaani kwenye nchi nne au tano hivi’ – Mo
Dewji

March 24 2016 Mohammed Dewji aliandikwa na CNN kwamba anataka kuingia kwenye soko la ushindani Afrika na kushindana na Coca cola kupitia kinywaji chake cha Mo Cola na namnukuu akisema ‘tunashindana na Red Bull kupitia Mo Energy Drink’

Siri ya Utoroshaji wa Wanyama na Wadudu Hai Kutoka Tanzania Kwenda Nje ya Nchi Imebainika.

$
0
0
Siri ya utoroshaji wa wanyama na wadudu hai kutoka Tanzania kwenda nje ya nchi imebainika. Wamekuwa wakitumika katika nchi mbalimbali kwenye utafiti, mapambo na kitoweo.

Uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu, umebaini matumizi hayo na kuwa wanyama wanaotakiwa kwa wingi ni mijusi ya bluu, kenge na tumbili wanaopelekwa katika nchi za Ulaya kupitia viwanja viwili vya ndege hapa nchini.

Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Herman Keraryo alisema mbali na wanyama hao, wengine wanaopelekwa nje ni jamii ya nyani, wadudu na ndege.

Alisema hakuna nchi ambayo imejitambulisha kipeke kununua wanyama hao, bali imekuwa ni biashara kati ya mzawa na mnunuzi.

Alipoulizwa kuhusu uhalali wa biashara hiyo, Keraryo alisema mfanyabiashara lazima awe na leseni inayotambuliwa na Serikali; “... na siyo kila ndege anasafirishwa au nyani, kuna aina ya ndege wasioruhusiwa ila kwa kutozingatia sheria, baadhi ya watu wanaivunja.” Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Tanapa, Gerald Bigurube alisema wanyama kama kobe na kakakuona nao wamekuwa wakisafirishwa zaidi kwenda Vietinam na China kwa matumizi ya chakula na dawa.

Alisema matumizi mengine ya wanyama hao wanaopelekwa Marekani na Ulaya yamekuwa ni kwa ajili ya shughuli za mapambo.

“Wanyama hai na wadudu kwa kifupi wana soko pana sana duniani na matumizi yake ni kama hayo lakini inakuwa vigumu kujua moja kwa moja wanapelekwa nchi gani,” alisema.

Bigurube alisema wanyama wengine wamekuwa wakipelekwa kwenye maeneo ya mafunzo ili watu wengine duniani wajifunze historia yao. Imeelezwa kuwa mijusi ya bluu ambayo inapatikana Tanzania pekee ndiyo inayotafutwa zaidi na kila mmoja umekuwa ukiuzwa kwa Euro 5,000 (Sh12.2 milioni.)

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali ndani ya Idara ya Wanyamapori, wimbi la ukamataji na utoroshaji wa mijusi hiyo na tumbili linatokana na kuhitajika katika nchi mbalimbali kwa ajili ya utafiti.

“Kitu kinachoibwa zaidi sasa hivi nchini ni hao tumbili kwa sababu wanatumika sana huko nje kwa ajili ya utafiti wa kitabibu,” kilidokeza chanzo chetu na kuongeza: “Hata unavyoona, faru wanauawa ni kwamba wenzetu huko nchi za Asia wanaamini unga wake unasaidia kuongeza nguvu za kiume.”

Matumizi hayo yamebainika siku chache baada ya vyombo vya dola kuwashikilia raia wawili wa Uholanzi kwa kosa la kusafirisha tumbili 61 ambao walikuwa wapelekwe Albania kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia).

Habari zilizopatikana juzi zilidai kwamba mmoja wa maofisa wanyamapori alipewa bakshishi ya Dola 3,000 za Marekani, sawa na Sh6.4 milioni za Tanzania katika ‘dili’ hiyo ya tumbili 61.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alikiri kuwa tumbili na mijusi hao wa bluu ndiyo wanaowindwa zaidi kwa sasa; “... na huyo Williams Blue Lizard ni mjusi anayepatikana Kimboza na Ruvu. Ndiyo maeneo pekee duniani. Huyo mjusi anakaa juu ya miti kwa hiyo wanachofanya ni kukata mti na kuuangusha ndipo wanawakamata na kuwaweka kwenye mabegi. Wanafanya uharibifu mkubwa.”

Profesa Maghembe alisema mijusi hao huuzwa kati ya Euro 5,000 hadi 6,000 kila mmoja katika nchi za Ulaya.

Kuhusu tumbili, Profesa Maghembe alisema mpango ulikuwa ni kukamata tumbili 441 kwa awamu lakini kikwazo kikubwa kilikuwa ni upatikanaji wa kibali cha kuwasafirisha kwenda nje.

Alipoulizwa kwa nini raia hao wa Uholanzi wamekamatwa wakati walikuwa na kibali, alisema kibali hicho kilitolewa katika mazingira ya rushwa.

“Ni kweli walikuwa na kibali lakini kilitolewaje wakati nilishazuia na waraka ukatolewa? Lakini ujue hawakuwa na kibali pia cha kuwakamata hao wanyama,” alisema.

“Hili jambo lina njama kubwa na ndiyo maana tumeamua lichunguzwe na kile kikosi kazi cha kitaifa ambacho huchunguza makosa makubwa ya kihalifu,” alisisitiza.

EDWARD Lowassa Afunguka: Niacheni Kwanza Jamani...

$
0
0
Ikiwa ni miezi minane tangu Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kuhamia CCM na kutua Chadema, jana alitoa sadaka yake ya kumshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyomtendea na anayoendelea kumtendea. 

Hata hivyo, wakati Watanzania wengi wakisubiri kauli ya Lowassa aliyegombea urais 2015, kwa tiketi cha Chadema chini ya mwavuli wa Ukawa, kuhusu uchaguzi wa Zanzibar, akiwa katika Kanisa Kuu la Kilutheri la Azania Front jijini Dar es Salaam jana alisema: "Niacheni kwanza".

Lowassa ambaye alishiriki ibada hiyo maalum  ya kutoa sadaka ya shukrani yake na familia, alipoulizwa juu ya maoni yake kuhusiana na uchaguzi huo, alisema “Tungeje kidogo kitakachoendelea huko. Niache kwanza nitaongea.”

Aidha, aliwapongeza viongozi wa dini kwa kuhuribi amani nchini na kwamba ndiyo tunu pekee inayotakiwa kulindwa kwa kiasi kikubwa.

“Nawatakia sherehe njema wabarikiwe katika sherehe hii ya Pasaka, tuendelee kuhubiri amani ndiyo tuzo pekee tuliyonayo. 

Nawashukuru viongozi wa dini kufanya wajibu wao, ni wajibu wetu nasi kufanya wajibu wetu kwa hayo tuliyohubiriwa,” alisema.

Juzi wakati wa ibada ya Pasaka katika kanisa hilo, kulikuwa na tetesi za Lowassa kuwapo na wangekutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza na Rais Dk. John Magufuli, ambaye alisali kanisani hapo kwa kushtukiza.

Katika ibada hiyo iliyoongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk. Alex Malasusa, aliwatangazia waumini kuwa Lowassa na familia yake watatoa sadaka maalum ya shukrani kwa Mungu kutokana na mambo mbalimbali aliyowatendea na anayoendelea kuwatendea.

Kama Lowassa angeshiriki ibada ya juzi, ingekuwa ni mara ya kwanza kwa wawili hao ambao walikuwa wagombea wanaochuana kwa karibu zaidi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kukutana na kukaa katika eneo moja.

Katika uchaguzi huo Okotoba 25, mwaka jana, Dk. Magufuli aliibuka mshindi kwa zaidi ya kura milioni nane dhidi ya Lowassa aliyepata kura zaidi ya milioni sita.

Hata hivyo, Lowasaa amekuwa akipinga matokeo hayo akidai kuwa alishinda uchaguzi huo kwa zaidi ya asilimia 64.

Duru za kisiasa zinaeleza kuwa Lowassa angeweza kugusia hali ya kisiasa Zanzibar na hasa uchaguzi wa marudio uliofanyika bila wapinzani wakuu wa CCM, ambao ni CUF sambamba na utendaji kazi wa Serikali ya Magufuli, lakini alikwepa.

Pia Lowassa ni msharika wa Azania Front, lakini katika ibada iliyohudhuriwa na Rais hakuwapo.

Akitoa salamu za Pasaka, Rais aliwaomba Watanzania kumuombea kwa kuwa kazi ya uongozi aliyonayo siyo ndogo na kuacha kubaguana kwa vyama, dini na makabila ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii kuiwezesha Tanzania kupiga hatua kubwa kimaendeleo.

Katika ibada ya jana, Lowassa aliambatana na familia yake, watoto na wakwe zake akiwamo Sioi Sumari, huku viongozi wa Ukawa wakiwakilishwa na James Mbatia, ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa NCCR-Magaeuzi.

Wengine waliohudhuria ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, Meya wa Ilala, Charles Kuyeko na Meya wa Kinondoni, Jacob Boniface, aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrance Masha na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji.
Watu maarufu waliohudhuria ibada hiyo ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Malecela, Balozi Emmanuel Ole Naiko na Askofu wa Dayosisi ya Morogoro, Jacob Ole Mameo.

Katika ibada hiyo, ilitarajiwa kuwa Lowassa angezungumza, lakini Askofu Malasusa alimkaribisha Askofu Mameo kuzungumza kwa niaba ya wageni wote ambaye alimpongeza kiongozi huyo kwa kuwa mtoaji.

“Nimekuja kumsindikiza kaka yangu Lowassa kutoa sadaka yake ya shukurani ya pekee maana ni jambo la busara na hekima kumtolea Mungu, nilimkaribisha wakati natoa shukrani yangu ya pekee Ubungo kanisani, nakumbuka maneno aliyoniambia,” alisema na kuongeza:

“Baba Askofu Mameo umekuwa mfano wa viongozi wa juu wa Kanisa wanaokumbuka kutoa shukrani kanisani maana Wakristo raia tumezoea kutoa na ninyi (viongozi wa kanisa) hamtoi, nami nasema ni bahati ya pekee kuwa na watu wacha Mungu wanaokumbuka kumrudishia Mungu shukrani zao kwa mambo aliyowatendea.Tunapoona watu wa aina hiyo, ni lazima tuwaunge mkono na Mungu ndivyo anavyotaka, tunafanyiwa mambo mengi sana na Mungu.”

“Namshukuru sana kaka yangu Lowassa anamtolea Mungu mara kwa mara na anatendewa mambo mengi na Mungu na ndiyo maana hadi sasa yupo na Mungu, anapenda watu wanaotoa shukrani. Katika vitabu vya Ijinili, Yesu aliwaponya watu 10, mmoja ndiye alirudi kushukuru, sote tuna sababu ya kumshukuru Mungu kwani tunatendewa mengi sana,” alisisitiza.

“Lowassa tutaendelea kukuunga mkono, umetendewa mambo mengi sana, kutoa  siyo jambo la kuiga ni la moyoni na kama siyo la kuiga utaendelea kulitenda kila mara siyo kwa kuambiwa,” alisisitiza.

SAFARI YA LOWASSA MILIMA NA MABONDE 
Machi 20, mwaka 2014, CCM ilitangaza kuwafungia kwa miezi 17 makada wake sita waliodaiwa kuanza kampeni za urais kabla ya muda ulioruhusiwa na chama na walifunguliwa Mei 22, mwaka jana.

Chama hicho kilisema kitafanya tathmini kama walikiuka kanuni za adhabu hiyo na iwapo ingebainika wangechukuliwa hatua zaidi.

Baada ya kufunguliwa na kabla ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake (wakati huo) kupeperusha bendera ya chama hicho, makundi mbalimbali yalikwenda nyumbani kwake mjini Dodoma kumshawishi kuchukua fomu ya urais na ilipoelezwa kuwa makundi hayo yaliandaliwa naye, alisema hawezi kuzuia mafuriko kwa mikono.

Lowassa alikutana na wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali nchini Mei 27, mwaka jana na kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ikiwamo kueleza safari ya matumani.

Lowassa akiwa ameambatana na makada mbalimbali wa chama hicho katika Uwanja wa Shekhe Amri Abeid jijini Arusha Mei 30, mwaka jana na kutangaza kuanza safari ya matumaini ambayo itatimiza ndoto za Watanzania kupata elimu bure, majisafi na salama na maendeleo kwa ujumla, kisha kutangaza rasmi nia ya kuwania urais kwa tiketi ya CCM wakati huo.

Mafuriko ya Lowassa yaliteka jiji hilo na kuvunja rekodi ya mikutano iliyowahi kufanyika nchini huku kukiwa na viongozi maarufu kama kada wa zamani Kingunge Ngombale-Mwiru, wenyeviti wa CCM wa mikoa mbalimbali na waliowahi kuwa mawaziri na watumishi serikalini.

Lowassa alichukua fomu katika makao makuu ya CCM mjini Dodoma Juni 4, mwaka jana na kutembeza kuomba wadhamini kwenye mikoa yote nchini huku kukiwa na mafuriko ya watu na alirejesha Julai mosi, mwaka jana.

Hata hivyo, safari ya matumaini ya kiongozi huyo kwa CCM iliishia Julai 10, mwaka jana, baada ya kikao cha Kamati Kuu (CC) kukata jina lake na kupitisha jina la Dk. Magufuli, jambo lililozua taharuki na maandamano ya wafuasi wake katika mji wa Dodoma na viunga vyake kiasi cha polisi kuingilia kati kuwatawanya.

Julai 27, mwaka jana, Lowassa alijiunga rasmi Chadema na kukabidhiwa kadi ya uanachama wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho na baadaye alitangaza kupeperusha bendera ya Ukawa katika uchaguzi huo.

Baada ya kuhama, makada wengine akiwamo Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, walimfuata na alichukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chadema kuwania nafasi hiyo.

Agosti 10, mwaka jana, Lowassa alichukua fomu ya kuwania urais katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).

Nec ilipuliza kipenga cha kampeni Agosti 22, mwaka jana, Lowassa alifanya kampeni kwa gari na helkopta katika maeneo mbalimbali nchini, huku kukiwa na vita kali ikiwamo ya kueleza udhaifu wa afya yake na kutuhumiwa kwenye majukwaa ya kisiasa ya wapinzani wake wa karibu.

Oktoba 29, mwaka jana, Nec ilimtangaza Dk. Magufuli mshindi wa nafasi ya urais kwa kura 8,882,935 sawa na asilimia 58.46 dhidi ya Lowassa aliyepata kura 6,072,848 sawa na asilimia 39.97.

Baada ya matokeo hayo, Lowassa alikuwa kimya na licha ya kushawishiwa na makundi ya vijana kutoa tamko kali, hakufanya hivyo na kuwataka kuwa watulivu.

Kutokana na hali hiyo, Desemba 19, mwaka jana, Lowassa alitunukiwa tuzo ya amani na taasisi za kidini 1,200.

Video ya Nicki Minaj akitupa simu ya mkononi ya mlinzi wake,sababu iko hapa

$
0
0
Wanasema unapolipwa kiasi flani cha pesa ili uweke ulizi juu ya mtu wakati anafanya jambo flani, ni muhimu utekeleze wajibu wako sababu huwezi jua usalama gani anahitaji mtu huyo mpaka kukupa wewe kazi.

Je alichofanya Nicki Minaj ni sawa, wengi wanasema ndio sababu mlinzi huyu hakuwa anafanya kazi yake, je angepanda mtu kwenye jukwa na kumthuru Minaj.


Kama Romeo na Juliet: Diamond na Zari Ndani ya Mahaba Mazito Sweden

$
0
0
Watukufanya utamani kupenda ukapendwa – maake kunakupenda usipendwe na badala yake ikawa tu karaha, mapenzi usiyafurahie tena. Lakini kwa Zari the Bosslady na Diamond Platnumz ni mahaba mazito kama ya Romeo and Juliet kwenye visa vya William Shakespeare. Wenyewe wanajiita Mr and Mrs Smith aka Brad Pitt na Angelina Jolie.

Mapenzi yao (ambayo walau yanadhihirika kwa picha zao za Instagram), yanaweza kuwapa wivu uliochanganyikana na hasira maex wao. Jioneee mwenyewe picha zao wakiwa backstage kabla ya hitmaker huyo wa ‘Make Me Sing’ hajapanda stejini huko Stockholm, Sweden.


Ray C Akana Kurudia Madawa ya Kulevya...Apanga Kuvishitaki Vyombo vya Habari

$
0
0

Msanii Ray C amevijia juu vyombo vya habari vinavyoandika taarifa za uongo juu yake, kuwa amerudia kutumia madawa ya kulevya, na kuahidi safari hii atavifikisha mahakamani.


Katika ukurasa wake wa instagrama Ray C ameandika ujumbe mrefu kuhusu vyombo vya habari vinavyomchafua, na kwamba wana mpango wa kukwamisha harakati zake za kupambana na madawa ya kulevya.


“Hujuma hizi najua mnazifanya ili niishie njiani katika harakati za kupambana na dawa za kulevya nchini, Mimi na taasis yangu nitaendelea kusonga mbele na hakika sitakwamishwa na nyumbu kama hawa kwanza mwonekano wa picha uko wazi mimi sina nywele fupi kiasi hicho Ray C wa sasa si yule wa kipindi na enzi hizo now I'm not catalysts of drugs, hata hivyo tayari nimewasiliana na mwanasheria wangu ili niweze kuwawajibisha hawa nyumbu” aliandika Ray C.


Pia Ray c amesema kwa sasa yuko kwenye maandalizi ya mwisho kuandaa nyimbo yake, japokuwa bado yuko kwenye dozi ya methadone, inayotibu uathirika wa madawa ya kulevya.


“Mimi Niko katika maandalizi yangu ya mwisho ya kuaanda nyimbo yangu japo bado niko katika dose ya methadone”,aliandika Ray c.

Ajali za Mabasi zaendelea Kutumaliza...Hii Hapa Ajali Nyingine Iliyochukua Uhai wa Watu

$
0
0

Watu sita wamekufa na wengine zaidi ya 38 kujeruhiwa na kulazwa Hospitali ya Rufani Mkoa wa Iringa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Mwanza kwenda Iringa kupinduka mlima Ipogolo Manispaa ya Iringa.


Mganga Mkuu Mkoa wa Iringa, Dk Robert Salim alisema waliokufa ni sita, wawili kati yao walifia hospitalini wakati wakipatiwa matibabu. 


Dk Salim alisema waliokufa ni wanaume wanne na wanawake wawili na kwamba, maiti waliotambuliwa ni wawili, Makka Msigwa na Venant Mhagama.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Peter Kakamba alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 3.30 usiku baada ya basi la Lupondije aina ya Scania lililokuwa likitoka Mwanza kwenda Iringa kumshinda dereva na kupinduka.


Alisema majeruhi 38 walifikishwa hospitalini hapo, 11 walitibiwa na kuruhusiwa na wengine 27 wamelazwa kwa matibabu.


Kakamba alisema wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo.


Mmoja wa abiria walionusurika katika ajali hiyo, James John alisema walipofika Iringa, dereva waalikataa kuwashusha abiria waliokuwa wakiishia mjini ili awapeleke waliokuwa wakienda Mbeya kwenye basi jingine eneo la Ipogolo.


John alisema kutokana na uamuzi huo abiria waliotakiwa kushuka Kituo cha Kihesa na Kituo Kikuu cha Mabasi Iringa walipitiliza, lakini hawakufika Ipogolo wakapata ajali eneo la mlimani.


Dereva huyo, Castory Mwalusako (35) alisema basi hilo lilimshinda wakati akishuka mlima kutokana na kupoteza upepo kwenye breki na kulikwepa gari dogo lililokuwa mbele yake na kupoteza mwelekeo kisha kupinduka. 

Wema Sepetu Atoboa Siri...Aliyekuwa Mume wa Zari Anamtongoza na Ahadi ya Kumuoa

$
0
0
Supastaa wa Bongo, Wema Sepetu ‘madam’ ameanika siri zilizojificha nyuma ya pazia kati yake na aliyekuwa mume wa mwanamuziki nyota wa Uganda, Zarina Hassan ‘Zari’, Ivan Semwanga, kuwa anataka kumuoa.

Katika mazungumzo yake exclusive na mwanahabari wetu juzi jijini Dar, Wema alianza kwa kuweka bayana kwamba, mawasiliano yake na Ivan yalianzia nchini Afrika Kusini wakati alipokwenda kikazi, Februari, mwaka huu.

“Nilikwenda na Ommy Dimpoz (Faraj Nyembo). Tulikuwa na project yake lakini tulipokuwa kule, Ivan na marafiki zake walisikia kuwa mimi nipo, wakatuomba sana kupitia kwa wenyeji wetu kuwa wanataka kutuona na kutoka nao out pamoja.”

“Mimi nilikuwa bize sana na kazi zangu, awali niliwaambia kuwa hatutaweza lakini baadaye walitubahatisha klabu, wakaomba kukaa na sisi, mwishoni ilibidi tuwakubalie lakini kwa masharti ya kuwa wasije wakatuzushia lolote.

“Tulikubali, wakaja, tukakaa nao meza moja, tukabadilishana mawasiliano kama marafiki. Lakini baadaye tukaona wanaongezeka, sikupenda vurugu ya watu wengi, mimi na Ommy tukaamua kuondoka zetu,” alisema Wema.

Akizidi kumwaga siri zake na mwanaume huyo, Wema alisema baada ya yeye kumaliza project yake nchini humo, alirejea Bongo na ndipo Ivan alipozidisha ufundi wa kumuomba urafiki wa kimapenzi huku akimuahidi mambo mengi ya muhimu.

Msikie Wema: “Baada ya hapo tulikuwa tunawasiliana na Ivan, lakini kadiri siku zilivyokuwa zikisonga mbele, nikaona mwenzangu anaanza kunitongoza, tena akawa anaendelea kila siku licha ya mimi kutomkubalia.”


Aliyekuwa mume wa mwanamuziki nyota wa Uganda, Zarina Hassan ‘Zari’, Ivan Semwanga.

Wema alizidi kutiririka kuwa, hadi sasa (mapema wiki hii), Ivan hajakata tamaa, amekuwa akiendelea kumtongoza na kumuahidi ahadi mbalimbali.

Endapo atamkubalia na kuwa baby wake, basi atampa nyumba ya kifahari na magari ya kisasa (awe kama Zari).

Wema anakiri mwenyewe: “Alianza kuniahidi maisha mazuri, nyumba, magari na hata kunioa lakini kimsingi sijamkubalia kwani sijamwamini kama ana mapenzi ya dhati. Nahisi kuna kitu nyuma yake kinamsukuma kufanya hivyo.”

Kwa mujibu wa chanzo makini, kuna uwezekano mkubwa Wema akaingia kwenye himaya ya Ivan kutokana na ushawishi wake mkubwa anaoufanya kwa madam huyo, hivyo akawa tajiri mkubwa.

“Wema kwa sasa hatakiwi kuichezea bahati kwani Ivan ni mtu anayejiheshimu. Ana biashara zake kubwakubwa, hivyo suala la fedha za maisha hazimpigi chenga,” kilisema chanzo hicho.
Akizungumzia suala hilo, rafiki wa karibu wa Wema ambaye hakupenda jina lake liandikwe , alisema licha ya Wema kutokubali ombi la Ivan lakini anaamini siku si nyingi atakubali na atakuwa vizuri kiuchumi kuliko alivyo sasa.

“Jamaa yupo serious na ndoa, Wema atakubali tu na ndoa itafungwa. Mtoto wa kike sasa atakuwa si wa magari ya kawaida, full kubadilisha, atakuwa mtamu kama mcharo,” alisema rafiki huyo.

Rafiki huyo aliendelea kusema kuwa, Wema ana wasiwasi kwamba, mapenzi ya Ivan kwake ni kwa ajili ya kulipa kisasi kwa sababu ya Diamond (aliyekuwa mpenzi wa Wema) sasa yuko na Zari (aliyekuwa mke wa Ivan).

“Kwa hiyo Wema ana wasiwasi kwamba, siku akimkubalia tu Ivan akapiga naye ngwara, biashara itakuwa imeishia hapo kwani nia ya kisasi ya mwanaume huyo itakuwa imekamilika,” alisema rafiki huyo.

Mwanamume Aliyeteka Ndege ya Misri Akamatwa....Mapenzi Ndio Chanzo cha Yeye Kuiteka Ndege

$
0
0
Mwanamume aliyeteka nyara ndege ya shirika la Misri la EgyptAir na kuishurutisha kutua Cyprus amekamatwa, wizara ya mashauri ya kigeni ya Cyprus imetangaza.

Mwanamume huyo alidai kwamba alikuwa na mkanda wa kujilipua na kumwamuru rubani wa ndege hiyo kuielekeza Cyprus au Uturuki.

Ndege hiyo, iliyokuwa safarini kutoka Alexandria hadi mjini Cairo, mwishowe ilitua uwanja wa Larnaca nchini Cyprus.

Abiria karibu wote walikuwa wamefanikiwa kuondoka kutoka kwenye ndege hiyo.

Ripoti zinasema kuwa mtekaji wa ndege ya EgyptAir anataka kuongea na mkewe walietengana naye anayeishi Cyprus ambaye kwa sasa anadaiwa kuelekea katika uwanja huo wa ndege.
EgyptAir: Mtekaji ataka kumuona ''mkewe''

Rais wa Cyprus Nicos Anastasiades amewaambia waandishi wa habari kwamba tukio hilo la utekaji nyara halikuwa la kigaidi.

Akijibu maswali ya waandishi iwapo mtekaji huyo alishinikizwa na mapenzi, alicheka na kusema, ''kila mara kuna mwanamke anayehusishwa''.

Shirika la habari la Cyprus CYBC linasema kuwa mtekaji huyo huenda alikuwa na malengo yake ya kibinafsi, mtekaji huyo alikuwa na mkewe waliyetengana nchini Cyprus.

Walioshuhudia wanasema kuwa mtekaji huyo alirusha barua katika uwanja huo wa ndege ilioandikwa Kiarabu akiomba ipelekwe kwa mwanamke huyo.
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images