Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Marekani Yasitisha Msaada wa Mabilioni ya Pesa Kwa Tanzania...Watoa Sababu Hizi Hapa

$
0
0
Shirika la ufadhili la serikali ya Marekani limesitisha msaada wake kwa serikali ya Tanzania likilalamikia matukio kuhusu uchaguzi wa Zanzibar na kutekelezwa kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao.

Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) imesema Tanzania haijatimiza viwango vinavyohitajika ili kunufaika na ufadhili kutoka kwa shirika hilo, na hivyo basi haitapokea msaada wa awamu ya pili ambao ulikuwa wa jumla ya Dola 472.8 milioni ambazo ni sawa na shilingi trilioni moja za Tanzania.

Kupitia taarifa, bodi hiyo imesema: "Serikali ya Tanzania haijachukua hatua za kuhakikisha kuheshimiwa kwa uhuru wa kujieleza na uhuru wa kujumuika katika utekelezwaji wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao.”

Bodi hiyo aidha imesema Tanzania iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar ambao "haukushirikisha wote na wala haukuakisi maoni ya wote, licha ya malalamiko kutoka kwa serikali ya Marekani na jamii ya kimataifa.”

Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Ali Mohammed Shein alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo uliosusiwa na chama kikuu cha upinzani, Chama cha Wananchi (CUF).

MCC imesema kwamba huwa inatilia mkazo sana demokrasia na kujitolea kwa nchi kufanikisha uchaguzi huru na wa haki.

"Uchaguzi uliofanyika Zanzibar na kutekelezwa nwa Sheria ya Uhalifu wa Mitandao vinaenda kinyume na hili,” imesema.

Tanzania ilipokea Dola 698 milioni katika awamu ya kwanza.

Pesa za MCC hutumiwa kufadhili miradi ya maji, barabara na nishati.

Uchambuzi wa Humphrey Polepole Kuhusu Marekani Kusitisha Msaada wa Mabilioni ya Pesa na Shughuli zake Tanzania

$
0
0
Nianze na nukuu hizi mbili kuntu za Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere- Mwenyezi Mungu amrehemu.


“Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country”. June 1991 in Rio De Janeiro, Brazil

"Demokrasia sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuagiza. Demokrasia lazima ikue na kuendelezwa kulingana na nchi husika". Juni 1991 Rio De Janeiro, Brazil (Tafsiri ni yangu)

“No nation has the right to make decisions for another nation; no people for another people”. From ‘A Peaceful New Year’ speech, Tanzania, January 1968

"Hakuna Taifa lina haki ya kufanya maamuzi juu ya Taifa lingine; wala watu juu ya watu wengine ". Hotuba ya Amani ya Mwaka Mpya, Tanzania, Januari 1968 (Tafsiri ni yangu)

Hili la Marekani na uamuzi wa MCC ni jambo la mpito na haliwezi kuua mahusiano yetu na Marekani. Tanzania na Marekani zinashirikiana kwa mambo mengi na MCC ni sehemu tu tena ni eneo jipya la ushirikiano.

Uamuzi huu ni jaribio kwa uhuru wa Taifa letu. Hakuna namna nyingine ila kushinda hili kama tulivyoshinda mengine huko nyuma. Kwa wale ambao wameuona umri watakumbuka namna tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi 1964 pale walipotaka kuwa na kauli hasi dhidi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi baada ya kutaka kuingilia Uhuru wa Mataifa Mawili huru yaliyoamua kuungana na kuunda Nchi Mpya ambayo leo tunajivunia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1965 Tulivunja uhusiano na Uingereza kufuatia na kitendo cha wazungu wachache kujitangazia Uhuru (Unilateral Declaration of Independence) kule Rhodesia na uingereza kukaa kimya na kushindwa kuchukua hatua stahiki.

Tulivunja Uhusiano na Uingereza kuieleza Dunia kwamba Uhuru wa nchi za Afrika ni kipaumbele muhimu kwa Tanzania. Jambo tunalopaswa kufahamu ni kuwa MCC 2 toka mwanzo imekuwa ni mtihani dhidi ya uhuru wetu.

Napenda ieleweke kwamba kipindi hiki kilichotokea sio kuvunjika kwa uhusiano wetu na Marekani bali taasisi ya MCC ndio imesitisha msaada wao kwetu, lakini mahusiano yetu na marekani bado yako pale pale, na si Marekani au Tanzania inayoweza kuugharimu uhusiano wetu.

MCC 1 ilikuwa ni chambo cha kutuvuta na tulipewa bila masharti tena hela nyingi dola milioni 698 na ni fedha tulizopewa moja kwa moja na kupewa uhuru wa kuamua tuzitumieje.

Tanzania ilitakiwa kuainisha maeneo kisha wao wanatoa hela. Ndio maana miradi kama ile barabara ambazo hazikuwa zikipata ufadhili kwa kuwa hazikuonekana ni za kiuchumi na miradi ya maji ya Morogoro na kwingineko iliingizwa humu na kupata ufadhili.

MCC 2 sio hivyo. Kwenye MCC 2 walengwa wakubwa ni sekta binafsi ya Marekani, hapa kuna mtego hapa, hapa ni biashara hapa.

Mchakato wa MCC 2 ulipoanzishwa, wafanyabiashara kwa kushirikiana na Maseneta wakaanzisha hoja kuwa kwanini Marekani inatoa fedha kwa ufadhili katika nchi ambazo China ndio wenye kufaidika na fedha hizo?

Wakaleta hoja ya kuwa Serikali ya Marekani ifanye jitihada ya kuweka fedha kwa kusaidia Sekta Binafsi ya Marekani kupenya Afrika.

Ukaitishwa mkutano wa US-Africa Summit na agenda kubwa ikawa Power Africa. Katika Power Africa, Marekani ikalichagua eneo la Nishati (si uzalishaji viwanda) kwa kutambua kuwa ndio eneo pekee wanaloweza kushindana na wachina.

Wakasema wataelekeza fedha huko kuisaidia Afrika kutatua tatizo la nishati ambalo ndio pembejeo ya viwanda. Wakaweka sharti kuwa fedha hizo na miradi hiyo itatekelezwa na Sekta Binafsi ya Marekani.

Ndio sababu wengi wenu mtakumbuka hata Rais Obama alitangazia dhamira ile pale Ubungo kwenye Mitambo ya Symbion Power na sio kwamba alipenda kwenda kutembea Ubungo.

Kuanzia hapo kumekuwepo na shinikizo kubwa sana na masharti magumu na yenye kuhamahama (shifting goal post) kutaka kuibaka sekta ya nishati nchini ikiwemo mageuzi ya TANESCO.

Zikaainishwa hatua kadhaa,ambazo utekelezaji wake baadhi ni kisheria na kisera na hivyo haziwezi kwenda kwa deadline walizotaka.

Kila bodi ikikutana wanaibua hiki na kile lakini wakisema hela watatoa. Hela hizi zikawa zimeshikiliwa kama chambo ukisogelea zinasogea, ni sawa na ule mchoro wa Mpanda Punde aliyeshika fimbo yenye majani na akiielekeza mbele ya punda, kwamba punda ataendelea kuyafuata majani akidhani atayafikia kumbe ndio anaupiga mwendo.

Hatimaye wakasema wanasubiri uchaguzi mkuu jambo ambalo halihusiani na madai ya mwanzoni. Baada ya uchaguzi wakaibuka na suala la Zanzibar.

Hivyo, uamuzi wao wa leo ni uamuzi uliotarajiwa. Pia ni uamuzi wenye madhara kwa sekta binafsi ya Marekani pia ambayo ndio ilikuwa itekeleze miradi hiyo.

Kama Taifa ni muhimu kulinda utu na uhuru wetu. Ndio msingi wa sera yetu ya nje toka mwanzo na hata sasa. Tumetofautiana na Marekani katika hili tutapatana katika mengine. Ndio uhai wa maisha ya diplomasia.

Wao nao wanayo hadhira ya wapiga kura wao wanayojaribu kuituliza huko nchini kwao kwa uamuzi huu. Tunapaswa kuheshimu uamuzi wao kama ambavyo wanapaswa kuuheshimu wetu.

Hatimaye baadae tutapatana. Marekani inaihitaji Tanzania zaidi na Tanzania inaihitaji Marekani. Marekani inahitaji MCC 2 zaidi hali kadhalika Tanzania inahitaji MCC 2.

Mahusiano ya Tanzania na Marekani hayakuanza na hayataisha na MCC. MCC imeyakuta na itayaacha.

Kama marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo, basi Marekani isingekuwa inatoa zaidi ya Dola Bilioni 3 kila mwaka kwa Egypt iliyo chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa Egypt na Israel na isingetoa kiasi cha dola bilioni 6 kwa Israel kila mwaka kwa yale wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina.

Huu ni wakati ambao Taifa linawaita Wazalendo wake. Wazalendo wasimame na kusema 'Nchi yangu KWANZA, iwe Sahihi au Imekosea" na Makuwadi watashangilia na kusema "si mnaona sasa kiko wapi?".

Huu ni wakati wa kujifunga mikanda na kulinda heshima yetu kama Taifa letu. Tuna vyanzo vya mapato vingi sana ambavyo hatujaanza kukusanya mapato, tuwe wabunifu na tusibweteke na kutegemea mapato yataongezeka maradufu kwa vyanzo vile vile.

Niseme kwa uchache, sababu walizotoa MCC, na ieleweke aliyetoa tamko ni MCC, heri lingetoka tamko hili Wizara ya Mambo ya Nje au Ikulu ya Marekani, moja ni Zanzibar na pili ni Sheria ya Makosa ya Mitandao (Cyber crimes Act).

Sasa hebu tujadili kidogo, hivi kule Zanzibar tulitaka kitokee nini pale ambapo wanasiasa walikuwa hawataki kujadiliana?

Tume ile ile ya Uchaguzi ambayo bado ilikuwa na uhalali wa kikatiba na kisheria kuuitisha, kuufuta na kuuitisha tena uchaguzi ikachukua nafasi yake.

Wanasiasa wasio makini wakaishia kuhamishia malumbano mitandaoni badala ya kuitafuta suluhu ya kisiasa na pale siasa iliposhindikana basi wangeitafuta suluhu katika mahakama za Zanzibar.

Mezani wakashindwa, mahakamani hawakwenda. Tume ikachukua uongozi, uchaguzi ukaitishwa Wananchi wakapiga kura na sasa huko Zanzibar kuna serikali na baraza la wawakilishi.

Hata mimi sifurahii sana njia waliyoichukua Zanzibar lakini ilibidi siasa za madaraka zisite ili tuanze kufanya siasa za maendeleo. Je wamarekani walitaka muujiza gani utokee huko.?

Kuhusu Sheria ya Mitandao, hata mimi siipendi, si twende mahakamani, bunge litaanza vikao muda si mrefu je wabunge si wapeleke hoja ya kuifanyia marekebisho sheria hii.

Sasa Marekani (MCC) inapoweka shinikizo kwa suala la Sheria ambayo ni jambo la ndani na linaloweza kujadilika, sijaelewa.

Mbona sie hatujapiga kelele Yule jamaa yao Trump alipotutusi waafrika na kusema sisi stahili yetu ni kuwekwa tena chini ya ukoloni (hapa nimechomekea tu).

INDHARI

Ni aibu kwa viongozi wa kisiasa kufurahia jambo hili, ni ishara ya ukuwadi wa kisiasa na ambao uko tayari kukumbatia mahusiano yanayotweza Uhuru wetu. It is now high time kufanya siasa safi za maendeleo (politics of development) na sio kujikita katika katika siasa za madaraka (Politics of Power).
*************

Imeandikwa  na: Humphrey Polepole.
Mwandishi, Ndg. Humphrey Polepole amenufaika na uelewa wa watu wenye uzoefu wa mahusiano ya Tanzania na nchi za Nje. Aidha, ni mnufaikaji (alumni) wa programu ya uongozi chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Taarifa ya ACT-Wazalendo:Uamuzi Wa Bodi Ya Wakurugenzi Ya MCC Wa Kusitisha Mahusiano Na Tanzania Yatawaumiza Wananchi Wa Vijijini

$
0
0
TAARIFA KWA UMMA
UAMUZI WA BODI YA WAKURUGENZI YA MCC WA KUSITISHA MAHUSIANO NA TANZANIA YATAWAUMIZA WANANCHI WA VIJIJINI

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimeupokea kwa masikitiko makubwa uamuzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa wa MCC wa kusisitisha mahusiano na Tanzania.

MCC ni Shirika la misaada la Marekani lilianzishwa na Bunge la Nchi hiyo mwaka 2004 kwa lengo la kusaidia miradi ya maendeleo katika nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa haraka wa uchumi.

Tangu kuanzishwa kwake, shirika hili limesaidia miradi mingi ya maendeleo nchini ikiwemo ujenzi wa barabarani na usambazaji wa umeme vijijini kwa sasa miradi ya aina hiyo inaendelea sehemu mbali mbali hapa nchini na miongoni mwao ni pamoja na mradi wa REA,miradi ya barabara kama ile ya Tnduma Sumbawanga pamoja na Tanga katika barabara ya Horohoro.

Pamoja na vigezo vingine, kigezo mama kwa nchi kufuzu kupata misaada ya MCC ni kwa nchi husika kuzingatia misingi kidemokrasia ikiwemo kufanya uchaguzi ulio huru na haki.

Jana tarehe 28 Machi 2016 Shirika la MCC lilitangaza kusitisha mahusiano na Tanzania kutokana na serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM),kubariki kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika tarehe 25 Oktoba 205 na kubariki kurudiwa kwa uchaguzi huo tarehe 20 Machi 2016 katika mazingira ambayo hayakuzingatia misingi ya demokrasia ya vyama vingi na kuvunja matunda ya mwafaka wa kisiasa na kikatiba uliojengwa kwa gharama kubwa visiwani humo.

Chama cha ACT-Wazalendo kinapigania nchi yetu kujitegemea kiuchumi kama msingi wa kujenga utu na uhuru endelevu wa kisiasa na kijamii. Hata hivyo tunatambua kwamba katika kipindi hiki nchi yetu inahitaji mahusiano mema na Jumuiya ya Kimataifa na wadau mbalimbali wa maendeleo duniani, likiwemo shirika la MCC, katika kuendeleza miradi ya maendeleo. Shirika la MCC limekuwa mdau mkubwa katika miradi ya barabara na kusambaza umeme vijini.

Uamuzi huu wa Bodi ya Wakurugenzi wa MCC utawaumiza na kukwaza juhudi za wananchi wa vijijini katika kujikwamua na umaskini.

Tunasikitika kwamba ubabe wa Serikali ya CCM na woga wake wa kushindana kidemokrasia umesababisha nchi yetu ikose pesa za MCC ambazo zingesukuma mbele juhudi za kupambana na umaskini.

Tunatoa wito tena kwa Serikali ya chama cha Mapinduzi kuacha ubabe na kufifisha juhudi za miaka ishirini za ujenzi wa demokrasia hapa nchini. Tunatoa wito maalumu kwa wadau wote wa siasa visiwani Zanzibar kurudi mezani na kutatua mgogoro wa kisiasa kwa njia za kistaraabu na katika hali ambayo itarudisha heshima ya nchi yetu katika kukuza demokrasia nchini.

Imetolewa na

Theopister Kumwenda
Makamu Mwenyekiti, Kamati ya Katiba, Sheria na Mambo ya Nje
29/03/2016

Rais Magufuli Awataka Watanzania Waepuke Misaada ya Masharti Toka kwa Wazungu.....Pia ameahidi Kuwapunguzia Kodi Wafanyakazi Hadi Asilimia 10 au 9

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefika nyumbani kwake katika kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais, ambapo akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Chato, ametoa wito kwa kila mtanzania kuchapa kazi kwa juhudi ili nchi iondokane na utegemezi wa misaada ya wafadhili ambayo huambatana na masharti.

Dkt. Magufuli amesema jukumu kubwa lililo mbele ya watanzania kwa sasa, ni kushikamana na kujisimamia katika maendeleo ili kila mmoja ahakikishe anaongeza uzalishaji na utendaji kazi mahali pake pa kazi.

"Kwa hiyo ni lazima tujisimamie sisi wenyewe, na tukijisimama sisi wenyewe kwa kila mmoja kuwajibika mahali alipo, kama ni mfanyakazi afanye kazi kwelikweli, kama ni mkulima afanye ukulima wake kwelikweli, kama ni mfanyabiashara afanye biashara kwelikweli, kama ni mfugaji afuge kwelikweli, kama ni mvuvi avue kwelikweli, Tanzania hii tutavuka" Amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amesema serikali yake imeamua kuchukua hatua kudhibiti nidhamu serikalini, kwa kuhakikisha inawachukulia hatua watumishi wa umma wanaolisababishia taifa upotevu mkubwa wa fedha, na ameahidi kuwa hatua hizo maarufu kwa jina la "Kutumbua Majipu" zitaendelea kuchukuliwa hadi tatizo hilo likomeshwe.

Dkt. Magufuli pia amekumbusha viongozi wote wakiwemo Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala na Wakurugenzi, kutekeleza wajibu wao ipasavyo na ameweka bayana kuwa mahali popote ambapo hapatakuwa na ufanisi, kiongozi husika atakuwa amedhihirisha kuwa hatoshi kuendelea na wadhifa aliopewa.

Rais Magufuli amewapongeza walimu kote nchini kwa kufanya kazi nzuri ya kufundisha, licha ya changamoto ya ongezeko kubwa la wanafunzi waliojiunga darasa la kwanza mwaka huu, lakini ametaka Wazazi na kamati za shule kushirikiana na walimu kuwasimamia wanafunzi ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.

"Niziombe kamati za shule zote Tanzania nzima, kama haziwezi kusimamia nidhamu ya wanafunzi shuleni, zile kamati za shule zijiuzulu. Lakini pia kama wewe ni Mwalimu Mkuu, shule yako kila siku inatoa divisheni ziro nyingi kila mwaka, sioni sababu ya wewe kuendelea kuwa Mwalimu Mkuu" Alisisitiza Dkt. Magufuli.

Kuhusu tatizo la wafanyakazi hewa, Rais Magufuli amesema uhakiki mdogo uliofanywa hivi karibuni, umebaini wafanyakazi hewa 1,680 waliokuwa wakilipwa shilingi bilioni 1 na milioni 800, na kwamba ni matarajio kuwa uhakiki unaofanywa nchi nzima utaisaidia serikali kubaini wafanyakazi hewa wengi zaidi na kunusuru fedha nyingi zaidi za watanzania.

Ametolea mfano wa mfanyakazi mmoja wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) ambaye alikuwa akilipwa mishahara ya watu 17, na kueleza kuwa mfanyakazi huyo atafikishwa mahakamani.

Pia Rais Magufuli amesema serikali yake imejiandaa kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kupunguza kodi kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 10 au 9 kuanzia bajeti ijayo, lakini amesema kwa wale wanaolipwa mishahara mikubwa ambayo inafikia hadi shilingi milioni 40, itapunguzwa na kuweka kima cha juu cha mshahara usiozidi shilingi milioni 15.

Juma Nature Adai Mshindani Wake Kwenye Muziki kwa Sasa ni Diamond

$
0
0
Msanii mkongwe wa muziki, Juma Nature amedai msanii pekee ambaye anaweza akashindana naye kwa sasa ni Diamond.
nature

Akizungumza na tovuti ya Times Fm, Juma Nature ameomba wadau kuandaa tamasha ili washindanishwe.

“Watu wanamtukuza sawa lakini watuweke stage moja tuone nani atakamua, unajua tuseme ukweli bongo flava sasa mimi na Diamond ndio wapinzani pekee,” alisema Juma Nature.

Aliongeza, “Watu waandae pambano, na mpunga pia uwepo nioneshe na mimi nguvu yangu ilivyo mtaani,”

Nature amesema anaamini muziki wake aliyokuwa anafanya zamani una nguvu kubwa kuliko huu wa wasanii wa sasa.

Uongozi wa Bagamoyo Sober House Wazungumzia Maendeleo ya Chidi Benz

$
0
0
Ikiwa ni wiki moja toka Chidi Benz achukuliwe na meneja wa Diamond, Babutale pamoja Kalapina na kupelekwa Life and Hope Rehabilitation Organization iliyopo Bagamoyo kwa ajili ya kusaidiwa kuacha matumizi ya Madawa ya kulevya, uongozi wa Sober hiyo umeeleza maendeleo ya rapa huyo.
Babu Tale, Chidi Benz na Kalapina

Akizungumza katika kipindi 360 cha Clouds TV Jumanne hii, Mkurugenzi wa Life and Hope Rehabilitation Organization, Bwana Al-Karim Banji amesema Chidi Benz amekuwa msikivu na afya yake imeanza kurudi.

“Chidi Benz anaendelea vizuri sana, tena nimeshangaa amepata hamu ya kula kitu ambacho ni tofauti kwa waathirika wengine,” alisema Bwana Banji.

“Mimi mwenyewe nilikaa na Chidi Benz nikaongea nae na alinisikiliza sana, nilimwambia maneno mengi ya busara, alinisikiliza na akaniambia mimi niko tayari kubadilika. Kwa hiyo Chidi Benz anaendelea vizuri na ana kula vizuri yaani yupo very positive,” aliongeza.

Banji alisema ndani ya miezi miwili mpaka mitatu Chidi Benz anaweza kukaa sawa kabisa kwa kuwa anapitia semina mbalimbali za kumjenga kiakili.

Pia Banji amewataka watanzania kuacha kumsema vibaya kwa ile ni hatua ya maisha ambayo binadamu yeyote anaweza kuipitia.

Watu Wanne Watiwa Mbaroni Kwa Tuhuma za Kutumia Jina la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kutapeli

$
0
0
Watu wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na tuhuma za kujipatia fedha kwa kutumia jina la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Washtakiwa hao walifikishwa katika mahakama hiyo jana kujibu mashtaka 12 yanayowakabili, likiwamo la kughushi barua na kuziwasilisha katika vituo vya mafuta wakirubuni watumiwe kiasi cha fedha ili waweze kupata punguzo la kodi.

Washtakiwa hao ni mwanafunzi, Issa Mohamed Awadhi (27)
maarufu kama Charles Robert au Mwamunyange, mkazi wa Ilala, ambaye hakuwapo mahakamani hapo kutokana na kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya kuugua.

Wengine ni Hamisi Tembo(37) mkazi wa Ilala, mtengeneza mihuri, Nicolaus Obado(32), mkazi wa Mbagala Kuu na Wakati Mungi (51) mfanyabiashara na mkazi wa Yombo Makangarawe.

Washtakiwa walikana mashtaka na upande wa mashtaka ulidai upelelezi haujakamilika na kukosa dhamana. Kesi itaendelea Aprili 11

Wafanyakazi watatu TANESCO Watiwa Mbaroni Kufuatia Kifo cha Mfanyakazi Mwenzao Aliyenaswa na Umeme Juu ya Nguzo

$
0
0
Wafanyakazi watatu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoani Morogoro, wanashikiliwa na Polisi wakihojiwa kutokana na kifo cha mfanyakazi mwenzao, Deo Elias (30), mkazi wa Mazimbu, Manispaa ya Morogoro kwa kunaswa na umeme juu ya nguzo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 5.30 asubuhi maeneo ya Mafiga, wakati Elias akiwa na wafanyakazi wenzake katika eneo la kazi.

Kamanda Matei alisema Elias alipokuwa na wenzake katika eneo hilo wakirekebisha umeme, alinaswa na kufa papo hapo.

Meneja wa Tanesco Mkoa wa Morogoro, Mhandisi John Bandiye akizungumzia tukio hilo ofisini kwake jana, alisema Elias alikuwa katika kazi za kawaida kama fundi na tukio hilo limetokea kwa bahati mbaya.

Mhandisi Bandiye alisema mfanyakazi huyo alikuwa akirekebisha njia ya umeme ya Ngazengwa iliyopo eneo la Mafiga na ilikuwa imezimwa, lakini cha kushangazwa ilikuwa na umeme uliosababisha kifo chake.

“Kwa sasa shirika lina wafanyakzi wa muda wanaosaidiana na mafundi wakuu na hupatiwa mafunzo na wanatambulika, tofauti na maneno yaliyozagaa mitaani kuwa marehemu hakuwa mfanyakazi,” alisema.

Alisema mwili wake umesafirishwa kwenda kwao mkoani Mbeya kwa ajili ya maziko.

Chato Yatangaza Kiama cha Mapato

$
0
0
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita, Batholomeo Manunga amewataka madiwani kuwafichua watendaji wa vijiji wanaoshirikiana na mawakala kuhujumu mapato.

Akizungumza wakati wa kufungua kikao cha baraza la madiwani, Manunga amesema baadhi ya watendaji wa vijiji na kata wanahujumu mapato kwa kula njama na wazabuni.

“Hatutaendelea kuvumilia hali hii, na ni jukumu letu sote kukabiliana na wote wanaohujumu mapato ya halmashauri kwa sababu bila kuongezeka hatutaweza kuwahudumia wananchi waliotuamini na kutuchagua,” amesema Manunga.

Bila kutaja majina wala kata husika, mwenyekiti huyo alisema tayari halmashauri imegundua mtandao wa wanaohujumu mapato ambao wataanza kushughulikiwa baada ya uchunguzi kukamilika.

Amesema watu hao wamekuwa wakiihujumu halmashauri hiyo na kuifanya ishindwe kutekeleza majukumu iliyojipangia kutokana na fedha nyingi kuishia mifukoni mwao.

Manunga aliwasihi madiwani kuacha kuwaonea aibu wezi wa mali za umma ili kuisaidia halmashauri hiyo kupiga hatua kubwa ya maendeleo.

Diwani wa Kata ya Bwina, Sospeter Nyamang’ondi ameishauri halmashauri hiyo kuwachuja mawakala wasiotimiza wajibu na wanaoshirikiana na watendaji kuhujumu mapato.

Amesema iwapo mapato yatasimamiwa vizuri, halmashauri hiyo inaweza kukusanya zaidi ya Sh2 milioni kutoka kwenye mialo.

Diwani huyo amesema mapato mengi yamekuwa yakiishia mikononi mwa watu wachache kutokana na kutokuwapo kwa mikakati mathubuti ya kuwadhibiti.

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Athanas Ngambakubi ameahidi kuweka mikakati kuongeza mapato na kubaini vyanzo vipya.

Amewaomba madiwani kushirikiana na watendaji wa halmashauri kubaini vyanzo vipya vya mapato, ukusanyaji na udhibiti wa mapato na usimamizi wa mapato ili kuiwezesha kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mkurugenzi huyo amesema bila ushirikiano kutoka kwa viongozi na wananchi itakuwa vigumu kufikia malengo.     

Akina Dada Msipende Kuwadharau Vijana Mnaofanya nao Kazi Maofisini...

$
0
0
Akina dada nipende kuwashauri kitu kimoja.

Msipende kuwadharau vijana mnaofanyanao kazi ofisi moja na kuwaona wa thamani kubwa watu msiowajua hasa wa kwenye mitandao mkidhani kuwa hao ndio wana maisha bora.

Ukweli ni kwamba akina dada wengi wanatabia ya kuwadharau vijana wanaoishinao wakiamini kwamba watawapata watu wenye sifa wanazozihitaji toka kwenye mitandao ya kijamii.

Matokeo yake kwa sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wasiokuwa na baba au kwa jina maarufu kama watoto wa love connect, wakishazalishwa huko walikokimbilia na kuachwa ndio wanawaona wa thamani kubwa hawa waliowaacha mtaani.

Ushauri kwa wadada acheni tamaa rizikeni na vijana mnao ishi nao kwenye mazingira yenu kwani wengi wao ni watu wenye nia nzuri kwenu.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya March 30, Ikiwemo Kigogo wa TRA anayelipwa Mishahara 17

$
0
0

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya March 30

Mwimbaji Rose Mhando Ashtakiwa Kwa Waziri Nape Juu ya Utapeli Anaofanya.....

$
0
0
Msanii wa nyimbo za injili nchini, Rose Mhando, ameshtakiwa kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye, kwa kitendo cha utapeli na kushindwa kutekeleza mkataba wa kuhudhuria na kutumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka lililofanyika jijini Mwanza licha ya kulipwa gharama zote alizotaka.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions inayoongozwa na Alex Msama, ambayo ina mkataba naye imekuwa ikiuza na kuandaa matamasha ya msanii huyo pamoja na tamasha la Pasaka la kila mwaka, alimweleza Waziri Nnauye, mbele ya halaiki ya wananchi alipokuwa mgeni rasmi wa sherehe za tamasha hilo lililofanyika kwa mara ya kwanza jijini Mwanza na mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Msama alieleza kusikitishwa na kitendo cha Rose Mhando kuingia mitini ilihali akiwa ameingia mkataba na kulipwa gharama zote pamoja na nauli alizodai kabla ya kuanza safari kufika Geita, Mwanza na Kahama kujiunga na wasanii wenzake kwa ajili ya kutumbuiza katika tamasha hilo.

“Mheshimiwa Waziri, Rose Mhando naye amekuwa ni jipu kwa kuwa amefanya utapeli kwa kukubali kulipwa gharama zake zote lakini ameshindwa kuhudhuria na kutumbuiza kama wenzake wakina Solomon Mkubwa, Bonny Mwaitege, Upendo Nkone na wengine uliowashuhudia hapa.

“Hii ni mara ya tatu amekuwa akifanya hivi na mara kwa mara nimekuwa nikimsamehe,” alisema bila kutaja kiasi alichomlipa katika mkataba waliokubaliana ili aweze kufanya onyesho hilo.

Msama pia akatumia fursa hiyo kuwaomba radhi wananchi waliofika katika Uwanja wa CCM Kirumba kwa kutegemea mwimbaji huyo angekuwepo na kutumbuiza na wenzake lakini kilichotokea ni aibu na utapeli wa msanii huyo mkubwa wa nyimbo za injili aliyejizolea umaarufu ndani na nje ya nchi.

“Kuanzia leo mtu yeyote asije akaingizwa mjini na Rose Mhando kwa kuingia naye makubaliano akidhani yupo chini ya Kampuni ya Msama Promotions, kwa kitendo alichoendelea kukifanya naomba kutangaza rasmi kuvunja mkataba wa kufanya kazi na msanii huyo ili kulinda hadhi na heshima ya Kampuni yangu,” alisisitiza Msama.

Msama aliomba wananchi waendelee kuipa sapoti kampuni yake kwa kuwa imekuwa ikirejesha mapato ya viingilio na sadaka katika tamasha hilo kwa jamii hasa kwa watu wasiojiweza, makundi maalumu pamoja na kuendeleza vipaji vya wasanii chipukizi wa nyimbo za injili nchini kote.

Hata hivyo, wadau mbalimbali waliokuwepo katika uzinduzi huo walisikitishwa na kutokutokea kwa mwanamuziki huyo huku wengine wakimlalamikia kuwa na tabia hizo kwa muda mrefu na kufanya bila woga na hofu yoyote.

Mwanamuziki huyo aliwahi kuripotiwa kutuhumiwa kufanya udanganyifu kwa kupokea zaidi ya Sh milioni 3 na kisha kushindwa kufanya onyesho katika tamasha la nyimbo za injili lililoandaliwa mkoani Njombe mwaka jana.

Mkurugenzi wa Kampuni ya The Comfort Gospel Promotions, Seth Sedekia, ndiye alimfungulia kesi hiyo  katika kituo kikuu cha polisi Njombe na akapewa RB namba: NJ/RB/1793/2015.

Kushindwa kutokea kwa mwanamuziki huyo siku hiyo ya Jumapili iliyopita, kuliwafanya mashabiki waliokuwa wamelipa kiingilio cha shilingi 5,000 kila mmoja kuzusha vurugu kubwa kwa mwandaaji huyo wakidai wametapeliwa huku wengine wakionyesha kuchukizwa na kitendo cha mwanamuziki huyo kushindwa kutokea kufanya onyesho hilo.

Mwandaaji wa onyesho hilo, Sedekia alisema amefikia hatua ya kufungua kesi kituo cha polisi kufuatia kumlipa fedha zote shilingi milioni tatu Mhando ambazo alisaini mkataba naye akiwa mjini Dodoma kwa ajili ya kufanya onyesho mjini Njombe. Katika onyesho hilo, Mhando alitarajiwa kushirikiana na msanii wa nyimbo za injili, Happy Kamili kutoka jijini Mbeya ambaye alifika katika tamasha hilo akishirikiana na wasanii wengine kutoka mjini Njombe.

Ofisa Habari wa Kamanda wa Polisi mkoani Njombe, Franco Malimba, alipoulizwa juu ya kuwepo kwa taarifa hizo katika kituo cha polisi, alikiri kuwepo lakini alisema hawezi kulizungumzia kwa sababu halijafika ngazi za juu.

Mwanamke Mbaroni kwa Kukutwa na Meno ya Tembo Morogoro....

$
0
0
Jeshi la polisi mkoani Morogoro linamshikilia mwanamke mmoja Magreth Mosha mkazi wa Kibaha mkoani Pwani kwa tuhuma ya kupatikana na vipande saba vya meno ya tembo.

Jeshi hilo pia linamshikilia Bw. Hamis Balewa mkazi wa kijiji cha Mbasa wilayani Malinyi kwa kukutwa na nyama ya sheshe kilo ishirini zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja.

Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Morogoro SACP Urich Matei amesema watu hao walikamatwa katika matukio mawili tofauti ambapo tukio la kwanza limetokea katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo katika manispaa ya Morogoro ambapo akiwa na vipande saba vya meno ya tembo.

Katika hatua nyingine watu watano wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo katika matukio tofauti wakiwemo watumishi watatu wa shirika la ugavi wa umeme Tanzania (TANESCO) mkoani humo baada ya mfanyakazi mwenzao Deo Elias kufariki dunia baada ya kunaswa na umeme wakati akiwa kazini .

Akizungumzia matukio hayo kamanda wa polisi Urich Matei amesema katika tukio la kwanza watu wawili wakazi wa jijini Dar-es-salaam bw. Arisha Shaaban na Bi Zainabu Athuman wanashikiliwa kwa kukutwa na debe sita za bangi huku wafanyakazi watatu wa shirika la TANESCO Bw Ramadhani Yusuf, Bi Elizabeth Kihimbo na Bw Jonas Sajinga wakishikiliwa kuhusiana na kifo cha mtumishi mwenzao.

Watuhumiwa wote wanaohusika na matukio hayo wanatarajia kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili mara baada ya upelelezi wa jeshi hilo kukamilika.

Waliompiga Daktari Mkoani Mtwara Wakamatwa Wakijiandaa Kutoroka Kwenda Nje ya Nchi

$
0
0

Kufuatia tukio la ndugu wa mgonjwa  kumpiga Daktari Mkoani Mtwara, tayari jeshi la Polisi Mkoani humo linawashikilia watu kadhaa kwa kitendo hicho cha kumpiga Daktari wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara,Henry Mwaibambe (Pichani) amesema hadi sasa watu 2 wanaotuhumiwa kumpiga daktari hospitali ya Mkoa wamekamatwa usiku wa kuamkia jana wakitoroka nchini huku wengine 3 wakiendelea kusakwa.


Awali wauguzi na Madaktari wa Hospitali hiyo waligoma kufanya kazi hadi hapo watakapohakikishiwa usalama wao ndipo wafanye kazi


Jana, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu aliweza kufika Hospitalini hapo na kusuluhisha mgogoro huo huku akiomba Jeshi la Polisi kuongeza usalama kwa watumishi hao wa Afya.

Binti Mrembo Ajinyonga Kwa Kamba Hadi Kufa..Aacha Ujumbe Mzito..Usome Hapa

$
0
0

Binti mmoja anayejulikana kwa jina la Jesca ambaye ni mfanyakazi wa Longido Mountain Lodge amekutwa amejinyonga katika hotel ya Longido Mountain Lodge akiacha ujumbe kuwa kifo chake kisihusishwe na mtu yeyote amejinyonga kwa ridhaa yake mwenyew akiacha ujumbe wa majina ya watu anao wadai walipe madeni yake kabla ya kusafirishwa kwao pamoja na namba za Mama yake mzazi.

Mkoa wa Mwanza Waongoza Kuwa na Watumishi Hewa Wengi Serekalini Ukifuatiwa na Mkoa wa Arusha...Habari Nzima Ipo Hapa

$
0
0
Mkoa wa Mwanza waongoza kuwa na watumishi hewa 334 ukifuatiwa na Mkoa wa Arusha kwa kuwa na watumishi hewa 270 ikiwa nchi nzima na watumishi hewa 2,702.

Hata hivyo Shinyanga na Songwe ni mikoa isiyo kuwa na watumishi hewa. Sababu kubwa iliyoiwezesha smShinyanga kutokua na watumishi ni matokei ya mikakati ya mkoa hu kupeleka majina ya watu wanaostahili kulipwa mishahara kila mwezi.

Akizungumza na Wakuu wa Mikoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene aliwataka wakuu wa mikoa wafanye kazi ikiwemo ubunifu wa miradi ya kuongeza mapato.

Tanzania yapokea Msaada wa Shilingi Bilioni 116.4 kutoka Japan.

$
0
0
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini hati mbili za makubaliano na Serikali ya Japan itakayoiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati hizo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile alisema mkataba wa kwanza utasaidia katika kukamilisha bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17.

Dkt. Likwelile alisema kuwa msaada huo unalenga kuweka mazingira rafiki ya kwa wafanyabiashara, kuboresha masoko na kuwezesha mazingira ya ushindani katika utengenezaji wa ajira nchini.

Mkataba wa pili  unahusu masuala ya kiufundi  yatakayotumika katika kufanya marekebisho ya mkataba uliosainiwa  Octoba 20, 1966, kwa kuzingatia sheria nyingi zimebadilika, kusainiwa kwa hati hiyo ya makubaliano itasaidia kutabadilisha baadhi ya vifungu vyenye jina Tanzania na kuweka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kujumuisha pande zote mbili za Muungano katika kutekeleza miradi ya maendeleo nchini.

Aidha, makubaliano hayo yatasaidia kubadilisha baadhi ya vipengele vya mkataba uliopita ikiwemo kipengele cha usambazaji wa madawa ili kuweza kukidhi mahitaji ya sasa ya wataalamu kutoka nchini Japan kuweza kuja kufanya kazi za kujitolea hapa nchini Tanzania.

Katibu Mkuu Dkt. Likwelile ameishukuru Serikali ya Japan na kusisitiza kuwa fedha hizo zitatumika kama ilivyopangwa ili kuweza kuwa na tija na kuwaletea maendeleo Watanzania.

Naye Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japan ina imani kuwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili utasaidia kukuza maendeleo ya uchumi na kijamii.

Balozi Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japani inaunga mkono juhudi za Serikali inayo ongozwa na Rais Dkt. John Magufuli katika masuala ya viwanda na mazingira mazuri yanayovutia wawekezaji  kuwekeza nchini Tanzania.

Adha Balozi Yoshida amesema kuwa Japan itaendelea kuwaleta vijana wanaojitolea katika sekta ya uchumii na ya kijamii jambo limekuwa likitekelezwa tangu mwaka 1969 ambapo hadi sasa idadi ya vijana hao wa kujitolea imefikia zaidi ya 1500.

Ishu ya Madawa ya Kulevya, Mrembo Tunda Amkingia Kifua Young D...Asema Haya

$
0
0
MUUZA nyago kwenye video za Bongo Fleva, Tunda Sebastian amejikuta akimkingia kifua mwandani wake, David Genzi ‘Young D’ kutokana na kuhusishwa na matumizi ya madawa ya kulevya na kudai maneno hayo ni uzushi mtupu.

Akibonga na Showbiz alisema kuwa, anawashangaa watu ambao kila kukicha wamekuwa wakimsakama kipendacho roho wake huyo kuwa ni mtumiaji mzuri wa unga, wakati yeye ndiyo anayemjua vizuri.


“Watu wanapenda sana kuzusha yasiyofaa, sasa kama mimi ndiyo mpenzi wake na sijawahi kumuona kabisa akitumia unga wala kumuhisi hivyo iweje watu wasiomfahamu kiundani wamkomalie hilo suala, hakuna kitu kama hicho, jinsi watu wanavyomfikiria ni tofauti na alivyo,” alisema.

Chanzo: GPL

Diamond: Sina Tatizo na Msanii yoyote Hata Ukija Ofisini Kwangu Utakuta Nimebandika Picha ya Alikiba na Mr.blue

$
0
0
Diamond amesema hataki kuulizwa tena kama ana bifu na msanii mwingine, amedai hana tatizo na msanii yoyote na ndio maana hata ukienda ofisini kwake utakuta ameweka picha za wasanii wote  hata ambao amekuwa akihusishwa kuwa na bifu nao.

“Ukija ofisini kwangu me nna kuna picha ya blue nimembandika, kuna picha ya Juma Nature, kuna picha ya Ali , kuna picha ya Prof, Jay, kuna picha ya Ray C, kuna picha ya Q chief, TID, AY, wasanii wote wakubwa ambao anajua walianza katika huu muziki, wana mchango katika huu muziki wote me nimewaweka” Diamond Alisema

 “Ofisini kwangu tu ukiingia tu reception, ukiingia tu kunasehemu nimeweka picha za wasanii wote , siwezi kuweka wote kwasababu  zisingetosha lakini kuna baadhi ya wasanii nimeweka kwasababu najua wanamchango kwenye soko la muziki wa Tanzania.” Diamond alielezea

Diamond pia amesema kuwa yeye ndio huwa anahushishwa na bifu na wasanii wengine lakini yeye hana tatizo na mtu

Mwimbaji Vanessa Mdee Amfungukia Laivu Jack Patrick Aliyoko Jela....

$
0
0
Baada ya kumkwapua Juma Mussa Mpolopoto ‘Jux’ aliyekuwa mpenzi wa modo Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Cliff’ kisha modo huyo kufungwa kwa msala wa madawa ya kulevya nchini China, mtoto mzuri wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘V-Money’ ameibuka na kumzungumzia ‘mtalaka’ huyo wa Jux.

V-Money alimfungukia modo huyo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akifanya mahojiano maalum (exclusive) na Global TV Online ambapo pamoja na mambo mengine ya kimuziki, staa huyo anayetamba na Wimbo wa Niroge, alitumia dakika kadhaa kufafanua tuhuma zinazoelekezwa kwake kuhusiana na Jack.

Awali, wanahabari wa Global TV walianza kumuuliza kama alikuwa akimfahamu Jack tangu alipokuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Jux ambapo Vanessa alijibu kuwa alikuwa hamfahamu.

“Jack nilikuwa sifahamiani naye. Nilikua namjua tu ni msichana anayefanya music video na nilikuwa naona kazi zake za umodo,” alisema Vanessa kwa kujiamini.

Alipoulizwa anazungumziaje kama endapo Jack atakuwa anaumia kule gerezani anaposika amekwapuliwa bwana wake (Jux) na pengine haoni kama anamuongezea machungu, Vanessa alifunguka:
“Kwanza kabisa sijamchukulia bwana wake. Namuombea atoke mapema. Ninachoweza kusema, namuombea atoke jela mapema. Matatizo anayoyapata kule ni makubwa kuliko haya ambayo anafikiria.

“I don’t think she even think about me at all (sifikirii kama ananifikiria mimi kabisa). Nadhani anawafikiria familia yake na hali ambayo amefungiwa pale. Sidhani kama hata ananiwaza.”
Jack alikamatwa Desemba 19, 2013 akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guandong Kusini mwa China.

Chanzo:GPL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images