Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live

GARI Lateketea Kwa Moto Pamoja na Dereva Akiwa Ndani.. Share Habari Hii Imfikie Mwenye Gari

0
0
KUNA GARI IMEPATA AJALI MAENEO YA MBEZI BEACH AFRICANA GARI NO T598BEL TOYOTA LANDCRUISER DEREVA KAUNGUA HAJAFAHAMIKA HATA KWA SURA,SAMBAZA UJUMBE HUU GROUP TOFAUTI ILI WENYE NDUGU WAMFAHAMU,GARI LIPO POLISI KAWE.

Matokeo ya Mechi ya Yanga na Kagera Sugar Iliyochezwa leo Jioni Haya Hapa

0
0
Michezo ya viporo ya Ligi Kuu soka Tanzania bara imepigwa leo kwa vilabu vya Azam FC na Yanga kucheza michezo yao ambayo awali ilikuwa imehairishwa kutokana na kuingiliana na michezo yao ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, lakini na michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa Yanga.

Yanga walikuwa uwanja wa Taifa Dar Es Salaam kucheza dhidi ya Kagera Sugar ambao awali walianza kucheza kwa kasi na kufanikiwa kupachika goli la uongozi dakika ya 9 kupitia kwa Mbaraka Yusuph, dakika 16 baadae Donald Ngoma akaisawazishia Yanga na kwenda mapumziko kwa sare ya 1-1.

Wakati Kagera Sugar wakitafakari namna ya kupambana  kipindi cha pili na kuifunga Yanga, Amissi Tambwe aliongeza goli la pili dakika ya 18 baada kipindi cha pili kuanza na Haji Mwinyi akahitimisha ushindi wa Yanga wa 3-1 dakika ya 88 kwa kufunga goli la tatu.

Timu 4 za Daraja La Kwanza Zashushwa Daraja kwa Upangaji Matokeo

0
0
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya Makamu Mwenyekiti Wakili, Jerome Msemwa leo imetoa maamuzi ya shauri la upangaji wa matokeo wa kundi C kwa Ligi Daraja la Kwanza

Akisoma hukumu hiyo baada ya kumaliza kuwahoji viongozi wa vilabu na wenyeviti wa vya vyama vya mpira wa miguu vya mikoa jana, Wakili Msemwa amesema adhabu hizo zimetolewa kwa kufuata Kanuni za Nidhamu za TFF, na nafasi ya kukata rufaa kwa wahusika juu ya maaamuzi hayo ziko wazi.

Klabu za Geita Gold (Geita), JKT Oljoro (Arusha) na Polisi Tabora (Tabora) zimekutwa na hatia ya upangaji wa matokeo na kupewa adhabu ya kushushwa daraja mpaka ligi daraja la pili (SDL) msimu ujao.

Upande wa klabu ya JKT Kanembwa FC ya mkoani Kigoma, imeshushwa daraja mpaka kwenye ngazi ya ligi ya mkoa (RCL), baada ya kushika nafasi ya mwisho katika msimamo wa kundi lake, Kundi C.

Kamati ya Nidhamu imewafungia maisha kutojihusisha na mpira wa miguu mwamuzi wa mchezo kati ya JKT Kanembwa FC v Geita Gold, Saleh Mang’ola na kamisaa wa mchezo huo Moshi Juma baada ya kukutwa na hatia ya upagaji matokeo.

Aidha kamati pia imemkuta na hatia kocha msaidizi wa klabu ya Geita Gold, Choke Abeid na kumfungia maisha kutojihusisha na mpira wa miguu

Magolikipa Mohamed Mohamed wa JKT Kanembwa na Dennis Richard wa Geita Gold wamefungiwa miaka 10 kutojihusisha na mpira wa miguu sambamba na kulipa faini ya shilingi milioni kumi (10,000,000) kila mmoja.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Geita (GEREFA), Salum Kurunge, Mwenyekiti wa klabu ya Geita Gold, Cosntantine Moladi na Katibu wa klabu ya JKT Kanembwa Basil Matei wameachiwa huru na Kamati ya Nidhamu baada ya kutokutwa na hatia katika shauri hilo.

Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Tabora, Yusuph Kitumbo, Katibu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Tabora, Fateh Remtullah, Mwenyekiti wa klabu ya JKT Oljoro, Amos Mwita na kocha msaidizi wa Polisi Tabora, Bernad Fabian wamefungiwa maisha kutojihusisha na mpira wa miguu.

Mwamuzi wa mchezo kati ya Polisi Tabora v JKT Oljoro, Masoud Mkelemi na mwamuzi wa akiba, Fedian Machunde wamefungiwa kwa muda wa miaka kumi kutojihusisha na mpira wa miguu, na kutozwa faini ya shilingi milioni (10,000,000) kumi kila mmoja.

Katibu wa klabu ya Polisi Tabora, Alex Kataya, Katibu wa klabu ya JKT Oljoro, Hussein Nalinja, mtunza vifaa wa klabu ya Polisi Tabora, Boniface Komba, na Meneja wa timu ya Polisi Tabora, Mrisho Seleman, wameachiwa huru na Kamati ya Nidhamu ya baada ya kutokutwa na hatia.

Kutokana na maamuzi hayo ya Kamati ya Nidhamu ya TFF, Kamati husika zitakaa kupitia Kanuni na kutangaza timu itakayopanda Ligi Kuu (VPL) msimu ujao na timu zitakazopanda Ligi Daraja la Kwanza (StarTimes) msimu ujao.

HALIMA MDEE Amshukia Rais John Magufuli...Amtaka Ataje Marupu rupu na Posho Anazopata Tujue Jumla ya Mshahara wake

0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee amemuomba Rais John Magufuli kuweka wazi posho na marupurupu anayoyapata ili Watanzania wajue kiasi halisi anachokipata mbali na mshahara wake.

Mdee ambaye ni mbunge wa Kawe, alitoa ombi hilo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Sokoni, Jimbo la Mtama mkoani Lindi, uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa jimbo hilo.

Kauli hiyo ya Mdee imekuja siku moja baada ya Rais Magufuli kutaja mshahara wake kuwa ni Sh9.5 milioni kwa mwezi.

Juzi Rais anasema eti mshahara wake Sh9.5 milioni, sasa atutajie posho za kila siku ili kila Mtanzania ajue kiasi ambacho anakipata,” alisema Mdee.

Mdee aliongeza kuwa wabunge wanalipwa mshahara wa Sh3 milioni, lakini kuna posho mbalimbali kutokana na kuhudumia wananchi.

Sisi wabunge mshahara wetu katika hati ya mshahara unasomeka Sh3 milioni, lakini posho na pesa ya mambo ya utendaji ya mbunge inafika Sh10 milioni, Rais atuambie na yeye posho zake ni kiasi gani,” alisema Mdee.

Mbunge wa Jimbo la Ndanda katika Wilaya ya Masasi, Cecil Mwambe alidai katika mkutano huo kuwa wananchi wa Mtama wamekosa mwakilishi wa kuwasemea matatizo yao, hasa ya upande wa kilimo cha korosho kutokana na mbunge wao, Nape Nnauye kukosa uwezo wa kusimama bungeni kuisema Serikali.

Mtama mmekosa mwakilishi, hapa kuna tatizo la korosho na mbunge aliyepo anashindwa kulisemea, hivyo mtabaki hivyo hivyo bila kutatua tatizo lenu kwa kipindi cha miaka mitano,” alidai Mwambe.

ZIMWI la Escrow Lazidi Kumwandama Mbunge Anna Tibaijuka Atakiwa Kulipa Kodi ya Shilingi Milioni 586...Mwenyewe Atoa Kauli Hii

0
0
Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka amesema yupo tayari kulipa kodi ya mapato ya Sh586 milioni iwapo Mahakama itaamuru hivyo.

Kodi hiyo inatokana na Sh1.617 bilioni alizopewa  na mfanyabiashara maarufu nchini, James Rugemalira  ambazo zilidaiwa kuchotwa katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Profesa Tibaijuka aliyasema hayo jana baada ya taarifa kwamba Bodi ya Rufani ya Kodi Tanzania (TRAB), imeagiza utekelezaji wa suala hilo ili kutimiza matakwa ya sheria kuhusu mapato nchini.

“Ni kweli ninadaiwa kodi ya Sh586 milioni, ila nimeenda mahakamani kutaka ufafanuzi kama ni halali kufanya hivyo kwa fedha zilizotokana na mchango,” alisema Profesa Tibaijuka na kuongeza “Nilipewa fedha kwa ajili ya shule lakini nadaiwa kama ni kipato binafsi, hivyo nataka Mahakama iseme, ikikubali nitalipa bila shida yoyote.”

Mbunge huyo alifafanua kuwa, anatambua kulipa kodi ni suala la kila mwananchi na anachotaka ni ufafanuzi wa uhusiano uliopo kati ya mapato na kodi.

Alisema lengo ni kutaka kujua iwapo mchango ni sehemu ya fedha zinazostahili kutozwa kodi, bila kujali zimepokelewa zikiwa taslimu au kupitia kwenye akaunti benki.

“Nipo msibani hivi sasa. Watu wanakuja kunipa pole, wengine wanatoka Dar na wasioweza wanatuma michango yao na hapa ndipo nisipoelewa dhana ya kodi kwenye michango. Hii nayo inastahili kuingizwa kwenye mkumbo huo?” alihoji.

Msemaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo alithibitisha kutolewa kwa hukumu hiyo kwenye pingamizi la makadirio aliloliweka mbunge huyo na kueleza kuwa bado anaweza akatafuta haki kwenye mamlaka za juu kama hajaridhika.

“Shauri lake liliamriwa Machi 29 na akatakiwa kulipa kiwango hicho alichokadiriwa,” alisema.

Mbunge huyo wa Muleba Kusini, alitakiwa kulipa fedha hizo baada ya TRAB kutupilia mbali rufaa yake ya kupinga kulipa zaidi ya Sh500 milioni.

Profesa Tibaijuka, Waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alikata rufaa hiyo baada ya TRA kumtaka alipe kodi ya mapato Sh586,364,625 kutokana na fedha alizopokea kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited, Rugemalira.

Profesa Tibaijuka ambaye alipokea fedha hizo kupitia akaunti yake iliyopo Benki ya Mkombozi, zilisababisha kuvuliwa uwaziri na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.

Alisema fedha hizo hazikuwa zake binafsi bali zilitolewa msaada kwa Taasisi ya Joha Trust.

Hata hivyo, TRA kupitia kwa Wakili wake, Noah Tito ilisema Tibaijuka anawajibika kulipa kodi hiyo kwani fedha hizo ziliingia katika akaunti yake binafsi.

Mabenki sasa kupata Taarifa za wadaiwa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)

0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) mwishoni mwa wiki imesaini mkataba na Kampuni ya CreditInfo Tanzania Ltd utakaowezesha taarifa za wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu kufikishwa katika Kitengo Uratibu za Taarifa za Mikopo (Credit Reference Bureau) kilichopo katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kampuni ya CreditInfo Ltd ina leseni iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.

Hivyo basi, mnufaika wa mikopo ya elimu ya juu ambaye ataomba mkopo kutoka kwenye taasisi yoyote ya kifedha hapa nchini, taasisi hiyo itakuwa na uwezo wa kuhakiki kama mwombaji huyo ni munufaika wa mkopo wa elimu ya juu na ikiwa ana nidhamu ya kurejesha mikopo.

Kwa mujibu wa mkataba huo, HESLB itawasilisha orodha ya wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu kwa kampuni ya CreditInfo ambayo itahakikisha taarifa za wakopaji zinapatikana kwa taasisi zote za kifedha, yakiwemo mabenki, ili taasisi hizo zijiridhishe kabla ya kutoa mikopo mipya kwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu.

“HESLB ina furaha kufanya kazi na CreditInfo kama mdau mpya. Tunawasihi wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu waanze kulipa madeni yao ili wawe na hadhi ya kukopesheka na taasisi za kifedha,” alisema kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Jerry Sabi wakati wa hafla fupi ya kutia saini mkataba huo katika ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa CreditInfo Tanzania Ltd Bw. Davith Kahwa amesema lengo la kampuni yake ni kuhakikisha fursa za ukopaji zinazongezeka na wakopaji wanakuwa na nidhamu kwa mikopo waliyopata.

“Wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu ambao wamekuwa wakilipa watapata fursa ya kipekee ya kujadiliana na taasisi za kifedha kuhusu viwango vya riba kwa sababu ya nidhamu wanayoionyesha kwa mikopo yao,” alisema Bw. Kahwa katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Meneja wa CreditInfo Tanzania Bw. Van Reynders.

”Tumedhamiria kuiunga mkono HESLB katika kutekeleza majukumu yake hususan yale ya ukusanyaji mikopo iliyoiva,” aliongeza Mtendaji Mkuu huyo wa CreditInfo Tanzania Ltd.

HESLB ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi Julai 2005 ili kutoa mikopo kwa watanzania wahitaji na pia kukusanya mikopo iliyoiva ambayo imekuwa ikitolewa na Serikali tangu mwaka 1994.

Hadi sasa, zaidi ya Tshs 2.1 trilioni zimetolewa kwa watanzania na, kati ya hizo, Tshs 258 bilioni zimeiva na hivyo kutakiwa kukusanywa kutoka kwa wanufaika.

Kiasi kilichobaki kinajumuisha fedha walizopewa wanafunzi ambao bado wanaendelea na masomo na ambao muda wa kuanza kuwadai (miezi 12 baada ya kumaliza masomo) haujafika.

CreditInfo Tanzania Ltd ni sehemu ya Kampuni ya Kimataifa inayofanya kazi kwenye nchi zaidi ya 20 duniai na inayojishughulisha na usimamizi wa taarifa za mikopo. Ilisajiliwa na Benki Kuu ya Tanzania mwaka 2013.

Mgao wa Fedha za Mbwana Samatta Kuuzwa Genk Zaanza Kuleta Zengwe Klabu ya Simba...

0
0
TP Mazembe imemuuza Mbwana Samatta kwa KRC Genk ya Ubelgiji ikadaka fedha zake, jambo la kushangaza hadi leo Simba haijalipwa sehemu ya fedha hizo kwa mujibu wa mkataba.
Simba ilipomuuza Samatta kwa TP Mazembe ya DR Congo, moja ya masharti ya mkataba ni kulipwa asilimia 20 ya kila anapouzwa lakini hadi sasa klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi haijapokea fedha za Genk.

Ili kujiridhisha kabla ya kuchukua hatua zaidi, Simba ilifanya uchunguzi ikiwemo kuwasiliana na Genk na kuhakikishiwa kuwa, tayari waliilipa TP Mazembe fedha zote za usajili.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ameliambia Championi Jumamosi kuwa, walibaini mchezo huo baada ya kuwasiliana na Genk na sasa watalifikisha suala hilo kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

“Kila tukiwasiliana na Mazembe wanasema fedha ya Genk haijaingia kwao, tumewaandikia barua na nakala kwenda Fifa na TFF (Shirikisho la Soka Tanzania), mambo yakizidi tutaenda rasmi Fifa,” alisema Hans Poppe.

Taarifa zinasema Samatta aliuzwa kwa euro 800,000 hivyo Simba inastahili kupata euro 160,000 ambazo ni sawa na Sh milioni 388.

Chanzo:GPL

SHAMSA FORD 'Nilinusurika Kuaribika Ubongo na Kumpoteza Mtoto Tumboni Kutokana na Kipigo Kutoka Kwa Baba Mtoto Wangu'

0
0
Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford amefunguka kuwa amekutana na kipigo cha mara kwa mara kipindi anaishi na baba mtoto wake Dickson Matok ‘Dick’ kiasi ambacho alikuwa akikaribia kupata athari kwenye ubongo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Shamsa alisema kuwa amenusurika kumpoteza mtoto wake akiwa tumboni kutokana na mitama aliyokuwa akipigwa na mpenzi wake huyo lakini kwa sababu alikuwa anampenda alikuwa habanduki.

“Jamani napinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake wenzangu kwani ilibaki kidogo niharibike ubongo kwa kipigo cha mwanaume huku nikiamini napendwa kumbe ni ujinga mtupu,” alisema Shamsa.

Wema Sepetu Auvunjavunja Moyo wa Idris Sultan Kwa Video hii Akibusiana na Mwanaume Mwingine

0
0
Mapenzi yanaumiza, kama hujawahi kuumia huyajui.

Na kama unahitaji ushahidi kutoka kwa mtu ajuaye maumivu yake kwanini usimuulize Idris Sultan? Ni kwasababu mshindi huyo wa Big Brother Africa 2014 anauguza jeraha la moyo baada ya mwanamke ampendaye – Wema Sepetu kumchoma kwa mkuki wenye moto moyoni mwake.


Wakati akiwa safarini jijini Nairobi, alishangazwa na video inayomuonesha mpenzi wake akimbusu mwanaume mwingine. Video hiyo imekuwa viral mtandaoni. Story zinaeleza kuwa pamoja na jamaa huyo kuwa ‘chakula’, bado ni mwanaume tu na video hiyo imemuumiza mtoto wa Sultan.

Idris amepost picha hiyo juu kwenye Instagram na kuandika:

“I have learnt to consider all my failures as lessons learnt the hard way. As i focus on work kesho Jumapili i will land in Nairobi at 7:20 asubuhi.”

Bado Wema hajasema chochote.

CHADEMA Yazidi Kuvunjika Mwanza..Aliyekuwa Mwenyekiti Chadema Mkoa wa Mwanza Ajivua Uanachama

0
0
Aliyekuwa Mweyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mwanza, Adrian Tizeba ametangaza kujivua uanchama na kuachana na siasa.

Tizeba aliyesimamishwa uongozi na Baraza la Uongozi la Chadema tangu Mei 4, mwaka jana, alisema hatajiunga na chama chochote cha siasa.

Kwa uamuzi huo, Tizeba amepoteza nyadhifa zake zote ikiwamo ya uenyekiti wa Baraza la uongozi la mkoa na ujumbe wa Baraza la Uongozi Kanda ya Ziwa.

Mei 5, mwaka jana, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, wakati huo, Dk Willibrod Slaa, alimuandikia barua Tizeba yenye Kumb Na C/HO/ADM/KK/08 ,kumsimamisha uongozi wa chama hicho.

Akizungumzia uamuzi wa kiongozi huyo kujivua uanachama na kuachana na siasa, Mratibu wa Chadema Kanda ya Ziwa, Renatus Bujiku alisema chama hicho kimepokea kwa mshtuko taarifa hizo kwa sababu bado suala lake lilikuwa linashughulikiwa.

“Utaratibu wa chama ulikuwa unaendelea kushughulikia suala lake, nadhani kachukua uamuzi wa haraka,” alisema Bujiku.

Kaya 40 Zakosa Makazi baada ya nyumba zao kubomolewa na Mafuriko ya Mvua

0
0
Mvua  kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia juzi imeleta athari kubwa katika Kijiji cha Chenene Kata ya Haneti Tarafa ya Itiso, Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na kukosesha makazi zaidi ya kaya 40.

Akizungumza jana, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Farida Mgomi alisema nyumba nyingi zilizobomoka ni zile zilizojengwa kwa matofali ya udongo. Mgomi alisema athari hiyo inaweza kuongezeka kutokana na nyumba kujaa maji na zinaposhindwa kuhimili hudondoka.

“Nyumba nyingi zilijaa maji, kwa hiyo hata chakula, magodoro, nguo vyote vimeharibika,” alisema.

Mgomi alisema tathmini ya awali tayari imefanyika. Na hakuna mtu aliyefariki dunia kufuatia maafa hayo.

“Waathirika wote ambao nyumba zao zimeanguka tayari wamepata sehemu za kujihifadhi kwa msaada mkubwa majirani na kutoka viongozi wa Serikali ngazi ya Kijiji, Kata, Tarafa na Wilaya,” alisema mkuu wa wilaya.

Alisema Kamati ya Maafa ya Wilaya tayari imechukua na inaendelea kuchukua hatua za haraka,kuona namna ya kusaidia familia zilizoathiriwa na maafa hayo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Pia alisema hata baadhi ya mashamba (mazao) yamesombwa na maji.

“Baadhi ya wananchi wamepoteza mali zao hifadhi za chakula katika kaya zao, mabati, vyombo vya ndani na mali nyingine za namna hiyo,” alisema.

Naye Ofisa Tarafa wa Itiso, Remidius Emmanuel alisema mvua hiyo imeacha kaya zikiwa hazina makazi.

“Kaya zaidi ya 40 zimeathirika, nyumba nyingi zilizodondoka ni zile zilizojengwa kwa matofali ya udongo,” alisema Emmanuel na kuongeza kuwa nyumba nyingi zilibomoka kutokana na kujaa maji kutoka milimani. 

Pia ujenzi wa barabara ya Kondoa hadi Babati umeonesha kuathiri miundombinu kwani madaraja yaliyojengwa ni madogo yanashindwa kuhimili wingi wa maji kutoka milimani 

“Katika eneo la Chenene ujenzi wa barabara unaonekana kuleta athari kwa makazi ya wananchi kwani madaraja ni madogo, maji yanapofika kwenye barabara yanakosa mwelekeo na kurudi kwenye makazi ya watu hali hiyo ikapelekea nyumba kubomoka,” alisema Ofisa Tarafa huyo.

“Nimetembelea maeneo yote yaliyokumbwa na maafa hayo. Nimekutana na kuzungumza na waathirika wote,” aliongeza.

Jide: Sijampiga Kijembe Gardner G Habash Kwenye Wimbo Wangu Mpya...

0
0
MKONGWE wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au Jide, amefunguka kuwa katika wimbo wake mpya wa Ndindindi, hajampiga kijembe  aliyekuwa mumewe, Mtangazaji Gardner G. Habash kama wengi wanavyodhani.

Akizungumza na mwanahabari wetu, Jide alisema wimbo huo ulitungwa na watu wake tofauti na yeye kuukamilisha hivyo kwa kuwa umebeba ujumbe mzito ni rahisi mtu kuhisi amemuimba mtu fulani kumbe yeye aliimba kwa ajili ya mashabiki wake wote.


“Sijampiga kijembe huyo wanayemsema (Gardner). Mimi nimetumia utunzi wangu kuwakilisha yale yanayotokea katika jamii mbalimbali sasa kama mtu anaona umemgusa fulani atakuwa amejiongeza tu lakini mimi sikumaanisha mtu mmoja bali  ujumbe kwa mashabiki wangu wote,” alisema Jide.

Kwenye wimbo huo kuna sehemu Jide kaimba; “Niliwezaje kutoa vyote ili hali wewe ulininyima vyote” ambapo iliaminika amemzungumzia Gardner.

Mange Kimambi Ajitokeza na Kufafanua Kwanini Aliamua Kubadilika na Kuwafanyia Kampeni CCM Wakati wa Uchaguzi Instagram

0
0
Mange Kimambi Amefunguka Sababu ya yeye kubadili Gia angani na kuanza kuipigia kampeni CCM kwenye uchaguzi uliyopita ambao magufuli alishinda na kuwa rais

Ameandika Haya Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram:

Mangekimambi_ Waliokuwa wananijua Kabla ya kampeni za Uchaguzi 2015 wanajua nilikuwa nawakosoa CCM daily Tena Kwa Maneno makali mpaka watu walishangaa nilipatwa Na nini kuwafanyia CCM kampeni insta.
Kilichonipata first and foremost ni upinzani kubeba uchafu wooote uliokuwa CCM. Ni upinzani kukosa credibility kuliko hata CCM. Nikakaa nikafikiria 2 things who would I rather support Lowassa or Magu. Secondly, I knew for a fact kumsupport Lowassa ni kujichafua bure Na kupoteza muda because he can't win. Yani Hata 90% ya kura zingekuwa zake still asingeshindaaaaaa, just like ZnZ. Yani nilikuwa nawashangaaaaa wale waliokuwa wanajitoa CCM Kwa mbwembwe Thinking they are going to win. Like it's impossible for anyone to win against CCM under current conditions. Hata malaika ashuke leo awe mgombea wa upinzani still CCM watashinda tu.

Nilicho realize Ni kwamba watanzania wengi wanajua umuhimu wa katiba kubadilishwa Ila pia hawajui just how much! I think Hata upinzani Na wabunge wake bado hawajua just how much!

Hii katiba Ndo hirizi ya CCM. Zindiko la CCM Ni hii katiba. CCM hawatokaaa kung'oka bila hii katiba kubadilika. Never ever! Upinzani watapoteza Sauti Na nguvu zao bungeni kufichua masiri mazito sijui nini but mwisho wa siku Katiba itampa ushindi CCM. Hii katiba Ni stronger than kura za wananchi. .

Seriously nilikuwa nacheka watu wanasema wanaenda kulinda kura sijui kulala vituoni. Hata mlinde kura Kwa bunduki. Mtapotezwa tu, Znz si hao kura zililindwa Ila katiba ikamaliza fitna ..

People are fighting the wrong war, sijui Mafisadi, sijui kujenga vyama vipya vya siasa, all that means shit as long as katiba iko vile vile. 

For as long as Katiba iko intact na CCM inakaa madarakani. Jinsi ya kuibadilisha hiyo katiba ndo challenge iko Hapo. 

Wewe jiulize kuna nchi gani duniani chama tawala kilitoka madarakani bila kuwepo uwezekano wa elections Kuwa contested in court?? Hakuna!

Kusema ukweli baada ya hii issue ya juzi ya Nape kuwakataza TV binafsi kurusha matangazo live from bungeni eti wawe wanakopy kile wanachorusha wao CCM wamenichefuaaaaaaaa Kwa Kweli. Tanzania kwanza then ndo mambo ya chama"Mange Kimambi

Kamati Yahoji Serikali ilichofanya Dhidi ya Vigogo wa Unga wa Jakaya Kikwete

0
0
Kamati ya Bunge ya Masuala Ukimwi na Dawa za Kulevya, imeitaka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kueleza hatua ambazo imekwishazichukua baada ya Rais mstaafu wa Jakaya Kikwete, kutangaza hadharani kuwa ana orodha ya majina ya wafanyabiashara wakubwa wa mihadarati.

Ilionya kuwa kuchelewa kuchukuliwa hatua za kisheria dhidi yao, kumeongeza idadi ya watumia dawa hizo magerezani huku Watanzania zaidi ya 160 wakifungwa nchini China baada ya kukamatwa wakisafirisha dawa hizo.

Mjumbe wa kamati hiyo, Grace Tendega, (Viti Maalum Chadema), alimtaka Waziri wa wizara hiyo, Charles Kitwanga, kutoa maelezo ya hatua za kisheria zilizokwishachukuliwa baada ya JK kueleza taarifa hizo.

 “Rais Kikwete alitangaza hadharani kwamba tayari amekabidhiwa orodha ya majina ya wauza unga, Jeshi la Polisi limechukua hatua gani kushughulikia suala hili,? Vijana wetu wanaotumia mihadarati wanaongezeka na wengi wanaishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU),” alisema Tendega.

Mjumbe mwingine wa kamati hiyo Elibariki Kingu , Singida Magharibi (CCM), alihoji namna Jeshi la Polisi linavyoimarisha ulinzi katika mipaka, kudhibiti bandari bubu hususan iliyopo Mbweni jijini Dar es Salaam, kwani inaongoza kwa kupitisha magendo na dawa hizo.

Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo, John Kadutu, alisema matumizi ya dawa za kulevya yameongezeka migodini akihoji uhakika na usalama wa watoa taarifa kuhusu dawa hizo, kwani wengi wao wamekuwa hawafichiwi siri.

Akijibu hoja hizo, Kitwanga alisema hajawahi kuiona orodha ya majina ya wauza dawa za kulevya, ambayo alikabidhiwa Rais mstaafu Kikwete na badala yake wizara imeendelea kufuatilia mfumo na mtandao wa mihadarati kwa kushirikiana na idara nyingina za serikali ikwamo ya Uhamiaji na Jeshi la Magereza.

Serikali ya awamu ya tano ina dhamira ya kupambana na dawa hizo ndiyo maana kwa Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali tayari amegundua sampuli 294 za dawa za kulevya kwa kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu, wakati mwaka jana mzima zilipatikana sampli 282 pekee,” alisema Kitwanga.

Naye Kamishna Jenerali wa Magereza, John Minja , alisema kuwa, matumizi ya mihadarati kwa wafungwa yameongezeka magerezani, kutokana na askari wasio waaminifu, watu wanowatembelea kuwapelekea dawa hizo kwa njia mbalimbali.

Tunatumia teknolojia ya kizamani kukagua wafungwa waliotoka nje ya gereza kutoka kwenye shughuli nje, wanakaguliwa lakini wanazificha dawa katika maeneo nyeti ya mwili ambayo haki za binadamu zinakataza kuwashika, pia ndugu zao wanawekea katika maji, mkate au sabuni na kusababisha kukithiri kwa dawa gerezani,” alisema Minja.

Aliwaambia wajumbe kuwa kucheleweshwa kwa kesi kunawafanya watuhumiwa wa dawa za kulevya kukaa kwa muda mrefu gerezani, jambo linalo hatarisha usalama wa magereza na nchi kwani watu hao wanamtandao mkubwa kimataifa.

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu, alisema mchakato mrefu wa kuthibitisha wanaotuhumiwa kuuza dawa za kulevya, unatokana na upepelezi kuchukua muda mrefu kwani jeshi hilo linashirikiana na idara za serikali akiwamo Mkemia Mkuu , kisha kesi kupelekwa kwa mwendesha Mashtaka (DPP) hatimaye mahakamani.

Naibu Spika Dk. Tulia Akson Atumia Mil 20/- Kumshukuru Mungu

0
0

Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Akson ametoa Sh. milioni 20 na zawadi mbalimbali kwa jamii wilayani Rungwe mkoani Mbeya, ikiwemo shule ya walemavu wa mtindio wa ubongo na albino kama shukrani kwa Mungu.

Kitendo hicho cha kutoa zawadi ya zaidi ya Sh. milioni 20 kilipongezwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Zainab Mbusi, ambaye alisema amefarajika kuona mbunge huyo amefika wilayani humo na kusaidia shughuli za kijamii hasa katika shule, Kanisa na vikundi vya wajasilia mali.

Alisema katika Shule ya Msingi Mabonde alikosoma, Dk. Tulia alitoa Sh. milioni 5 kwa ajili ya ukarabati wa majengo na katika Shule ya Sekondari ya Loleza ya wasichana Mbeya alikosoma pia, alitoa Sh. milioni 5.

Mkuu wa Wilaya huyo alisema Naibu Spika alisaidia pia walemavu wa mtindio wa ubongo na albino Sh. milioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa uzio kwenye jengo lao.

Mbusi alisema amepewa kazi ya kuhakikisha anasimamia fedha hizo ili zitumike kama zilivyokusudiwa na kuwataka wadau wengine kuiga mfano wa Dk. Tulia kwa kukumbuka kwao na kusaidia shughuli hizo na kupunguza changamoto zilizopo.

Katika hatua nyingine, DC huyo aliahidi kuitisha harambee kwa wadau kwa ajili ya kutafuta fedha zitakazotumika kununua madawati ili kupunguza upungufu wa madawati wilayani humo ambapo katika halmashauri ya Rungwe pekee yanahitajika 8,000.

Alisema katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa, ametafuta wadau ambapo Shirika la Kimarekani la Africa Bridge limetoa madawati 2,000 huku wadau wengine akiwemo mfanyabiashara anayemiliki mabasi, Yona Sonelo wameahidi kuchangia.

Aliwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha zoezi hilo linakamilika ili kuondoa tatizo la madawati linalopelekea wanafunzi kukaa chini na kuwa nyuma kulinganisha na wilaya za mikoa ya kaskazini ambazo zimepiga hatua katika sekata ya elimu.


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya April 4, Ikiwemo ya NSSF Kumulikwa Kwa Ufisadi Mkubwa

0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya April 4, Ikiwemo ya NSSF Kumulikwa Kwa Ufisadi Mkubwa

Tendwa: Utendaji wa John Pombe Magufuli Amerudisha Heshima na Matumaini Dhidi ya Serikali

0
0
Msajili wa zamani wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa amesema utendaji kazi wa Rais John Magufuli umerejesha heshima na matumaini yaliyopotea kwa wananchi dhidi ya Serikali.

Akizungumza katika mahojiano maalumu hivi karibuni, Tendwa ambaye kitaaluma ni mwanasheria alisema: “Mambo anayoyafanya Rais Magufuli tangu aingie madarakani yanakubalika na wananchi anaowaongoza pamoja na nje ya mipaka ya Tanzania.”

Alisema ushahidi wa kukubalika kwa Magufuli nje ya Tanzania ni kuwapo kwa mijadala isiyokoma katika mitandano ya kijamii, ikionyesha kumuunga mkono na kukubaliana na mtindo wake wa kufanya kazi.

Ndiyo maana unasikia huko nchi jirani wakizungumza kuwa nao wakimpata Magufuli wao watafurahi...hii ni hatua nzuri, maana anakubalika na anaungwa mkono na idadi kubwa ya watu kutoka sehemu mbalimbali,” alisema.

Alisema uchapaji kazi wake ndiyo uliosababisha Serikali ya Uganda kuingia makubaliano ya ujenzi wa bomba la mafuta, yanayochimbwa Uganda na kuletwa Tanzania kwa ajili ya kusafirishwa nje.

“Hata kuhusu makubaliano ya ujenzi wa bomba la mafuta kati ya Uganda na Tanzania, kama mnakumbuka awali Uganda walitutenga wakaona Kenya ndiyo wanastahili, lakini sasa wamerudi, hii ina maana wanaona kuna matumaini makubwa kutokana na utawala wa awamu ya tano kufanya kazi inayotakiwa hasa,” alisema.

Alisema hata wapinzani wanakubaliana na kasi ya utendaji wake wa kazi, kiasi cha kukiri kuwa Rais Magufuli anatekeleza yale matakwa ya wananchi ambayo ndiyo misimamo yao.

“Jamani wakati wa kufanya kazi kwa mazoea umekwisha, na hivyo ndivyo ambavyo sisi wengine tulilelewa na kufundishwa tangu zamani. Hapa katikati ilikuwa unaweza kumtuma mtu kitu, lakini kisifanyike kwa wakati, bila kupewa sababu zinazoeleweka…hizi ni zama zingine kabisa,” alisema.

Aliyataja baadhi ya mambo mazuri yanayofanywa na Rais Magufulu kuwa ni kukemea ufisadi na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma huku akisema  yalikuwa yakisimamiwa na Baba wa Taifa (Mwalimu Nyerere) wakati wa utawala wake.

“Moja ya hotuba za mwalimu alisema, wajibu wa Serikali ni kukusanya kodi, na ndicho anachokifanya Rais, na huu ndiyo mwelekeo wa kisiasa na kiuchumi tunaouzungumzia sasa,” alisema na kuongeza kuwa kwa sasa watu wanalipa kodi jambo litakalosaidia kuinua uchumi na kuliletea taifa maendeleo.

Alisema hali hii ikiendelea hivyo, taifa litatulia na wananchi watafanya kazi na kuachana na ile hali ya kuandamana na kudai madai mbalimbali, kwa kuwa tayari Serikali iliyopo inaonekana kuwapatia kile wanachokitaka.

Wananchi wanachotaka ni maendeleo yao, na hilo linaonekana wazi, dosari zilizopo ndizo zilizosababisha watu waandamane na wawe na malalamiko yasiyokoma, haya yanaelekea kupatiwa ufumbuzi,” alisema Tendwa.

Rais na demokrasia

Mbali na sifa ya kuchapa kazi na kujenga uchumi wa nchi, Tendwa alimtaja Rais Magufuli kama kiongozi anayeheshimu utawala wa sheria na kusimamia demokrasia.

Alisema kitendo cha kukemea ucheleweshaji wa upatikanaji wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam ni ishara kuwa ni muumini mzuri wa haki na demokrasia.

Hivi karibuni, Rais Magufuli aliagiza kufanyika uchaguzi wa Meya wa Dar es Salaam  baada ya kuwapo kwa ‘figisufigisu’ za kumpata.

Kufanyika uchaguzi huo kuliwezesha kumuweka madarakani Diwani wa Kata ya Vijibweni, Kigamboni, Wilaya ya Temeke, Charles Isaya wa Chadema. Isaya alichaguliwa kushika wadhifa huo baada ya kupata kura 84 huku aliyekuwa mgombea wa CCM, Yenga Omari, akipata kura 67.

Tendwa alisema: “Kitendo cha kukemea ucheleweshaji wa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na kuwaeleza wazi CCM kukubali kushindwa, ile ni demokrasia, na mmeona, Jiji lina Serikali sasa, na Serikali yenyewe ni ya chama cha upinzani.”

Alivitaka vyama vya siasa visidorore na badala yake viendelee kufanya kazi yao ya kuisimamia Serikali, ambao ndiyo wajibu wao kwa mujibu wa sheria.

Akizungumzia staili ya Rais Magufuli ya kutumbua majipu, alisema ni vizuri watendaji wa Serikali wanapoyatumbua hayo majipu, wazingatie sheria na taratibu na vile vile wasiwaonee watu.

Lakini taratibu za sheria pia zifuatwe yaani wanaotumbuliwa wapate nafasi ya kusikilizwa, watu wapewe muda unaotosha ili wajieleze, siyo kumwambia mtu nataka mpaka leo saa saba uwe umeniletea majibu… hii siyo sahihi, inapaswa mtuhumiwa apewe muda na nafasi ya kutosha ili ajieleze kwa sababu ni haki yake ya msingi kusikilizwa, hii ndiyo sehemu ya uchunguzi,” alisema.

Bomoa bomoa

Akizungumzia uamuzi wa Serikali wa kubomoa nyumba za wananchi zilizojengwa katika maeneo hatarishi na zile za waliovamia maeneo ya wazi, alisema kazi hiyo ilikuwa na umuhimu wake kwa usalama wao wenyewe.

Alisema bomoabomoa ilikuwapo tangu enzi za Makamba (Yusuph) akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na Serikali iliwataka waliojenga mabondeni wabomoe, lakini wakakaidi huku wakijua ni hatari kwa usalama wao na watoto wao.

“Serikali iko sahihi, yale ni maeneo hatarishi, huwezi kuruhusu mtu akaishi katika maeneo hatarishi hata kidogo, kwahiyo Serikali imechukua majukumu yake ambayo ilipaswa kuyatekeleza miaka mingi iliyopita”

Alisema kutokana na umuhimu wa suala lenyewe, ndiyo maana mashirika yanayotetea haki za binadamu hayakusema lolote kuhusiana na suala hilo.

Maalim Seif Kumwaga Cheche na Kutangaza Msimamo wa Chama cha CUF Zanzibar leo

0
0
Wakati joto la kuundwa Baraza la Mawaziri Zanzibar likiwa linaendelea kupanda bila ya Chama cha Wananchi (CUF) kuwamo katika serikali, Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, leo anatarajiwa kutoa mwelekeo wa kisiasa wa chama chake baada ya kususia uchaguzi mkuu wa marudio visiwani humu.

Msimamo huo wa CUF kuhusu mwelekeo wa Chama baada ya kugomea uchaguzi mkuu, unakuja baada ya kukamilika vikao vizito vya chama hicho kikiwamo cha Kamati Tendaji na Baraza Kuu la Uongozi vilivyofanyika Shangani Mjini Zanzibar.

Akizungumza toka mjini Zanzibar jana, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF, Omar Ali Shehe, alisema kuwa tamko la chama hicho litatolewa na Katibu Mkuu wa CUF baada ya kukamilika kwa vikao muhimu vya chama hicho.

Alisema vikao hivyo vimefanyika kwa siku nne vikitanguliwa na vikao vya siku mbili vya Kamati Tendaji vilivyofanyika chini ya Mwenyekiti wake, Maalim Seif.

Vikao vimekamilika salama na ajenda kubwa tulikuwa tunajadili hali ya kisiasa ya Zanzibar baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa marudio kinyume cha Katiba na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar,” alisema Shehe.

Hata hivyo, alisema maazimio ya kikao hicho yatatangazwa na Maalim Seif ili wanachama na wananchi kwa jumla, wafahamu msimamo wa chama hicho.

Alisema mwelekeo wa CUF kisiasa utaendelea kubakia kupigania haki ya wananchi iliyoporwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec), Jecha Salim Jecha, baada ya kufuta matokeo kinyume cha Katiba na Sheria Oktoba 28, mwaka jana.

Aidha, alisema Kikao cha Baraza Kuu kilikuwa cha kwanza kufanyika tangu kilipopitisha azimio la chama la kususia uchaguzi mkuu wa marudio uliyofanyika Machi, mwaka huu.

Msimamo wa Baraza Kuu la CUF umesababisha chama hicho kupoteza viti vyote vya Uwakilishi katika Majimbo 54 na Wadi 111 za madiwani katika Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na kupoteza nafasi ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

Hata hivyo, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, alisema kuwa anaamini Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, atatumia hekima na busara kwa kutumia nafasi zake 10 za Kikatiba kuwateua viongozi wa vyama vingine kuwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa madhumuni ya kuendeleza Serikali Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK).

Hata hivyo, nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar iliyokuwa ikishikiliwa na Maalim Seif, imekwama kufanyika uteuzi wake baada ya vyama vilivyoshiriki uchaguzi wa marudio, kushindwa kufikia masharti ya Katiba ikiwamo kupata asilimia 10 ya matokeo ya kura za Rais au viti vya majimbo katika Baraza.

Azimio la CUF linasubiriwa kwa hamu kubwa na wananchi wa Zanzibar kama dira ya mwelekeo wa hali ya kisiasa ya Zanzibar baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa marudio wakati Rais Dk. Shein akiendelea kukamilisha kupanga safu za uongozi wa serikali yake.

Uhuru Kenyatta Ashupalia Ujenzi wa Bomba la Mafuta Toka Uganda hadi Tanzania.....Aenda Ufaransa kukutana na viongozi wa Total Ili Kuwaomba Lipite Kenya

0
0
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya  aliondoka  nchini mwake jana asubuhi kwenda Ufaransa na Ujerumani kwa ziara ya  kazi ambayo pamoja na mambo mengine itahusisha suala la ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda.

Kenya hivi karibuni  imeingia katika mvutano na Uganda,  ikiitaka jirani yake huyo kurudisha mpango wa kulipitisha bomba hilo la mafuta nchini humo (Kenya) badala ya Tanzania.

Suala hilo ni sehemu ya ajenda ya  biashara, ushirikiano na maendeleo ambayo ni moja ya malengo ya ziara ya Rais Kenyatta.................

Kituo cha kwanza cha ziara ya Rais Kenyatta kitakuwa Paris,   Ufaransa, kuanzia leo Aprili 4 hadi 6 kabla ya kuelekea Berlin, Ujerumani atakakokaa hadi Aprili 8, mwaka huu.

Itakuwa ni mara ya kwanza katika  miaka 17 kwa Rais wa Kenya kuitembelea Ujerumani.

Mara ya mwisho, ziara ya aina hiyo ilifanywa na Rais Daniel arap Moi mwaka 1999 huku Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, akiitembelea Kenya mwaka 2011.

Ziara nchini Ufaransa kwa mujibu wa Ikulu ya Kenya, imeandaliwa na wizara ya mambo ya nje kwa mwaliko wa Rais François Hollande.

Ziara ya Ufaransa inatarajia kuipa Kenya fursa ya kuzungumzia suala la ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda, ikilenga kuiomba serikali ya nchi hiyo kutia mkono wake  kufanikisha azma yake ya ujenzi wa bomba hilo. Kenye inahesabu imeporwa na Tanzania mradi huo.

Kampuni ya Total ya Ufaransa ni mwanahisa mkubwa wa uwekezaji wa mafuta  Uganda na inaaminika ndiyo iko nyuma ya uamuzi wa hivi karibuni wa Uganda kuachana na mpango wa ujenzi wa bomba hilo kutoka njia ya Hoima- Lokichar- Lamu  ya  Kenya na badala yake kulijenga hadi katika bandari ya Tanga,   Tanzania.

Tofauti na washirika wengine wa uwekezaji huo kutoka Uingereza na China, Total mara kwa mara imekuwa ikisisitiza ujenzi wa bomba hilo kupitia njia ya Kusini nchini Tanzania kwa kile inachosema unafuu na usalama kulinganisha na Kenya.

Tayari mmoja wa viongozi wake waandamizi amemtembelea Rais John Magufuli Ikulu,  Dar es Salaam na kumhakikishia dhamira ya kampuni hiyo pamoja na kupatikana  kwa fedha za ujenzi huo.

Kampuni hiyo pia imetoa tamko jingine hivi karibuni wakati wa mkutano wa wadau wa nishati Afrika Mashariki uliofanyika Dar es Salaam, ikisema inajua jitihada zinazofanywa na Kenya kutaka bomba hilo lijengwe nchini humo, lakini msimamo wake wa kujengwa Tanzania uko pale pale.

Kwa mujibu wa taarifa za Ikulu, Ufaransa iko katika nafasi ya sita kama mmoja wa wawekezaji wakubwa   Kenya.

Uwekezaji huo unaanzia sekta ya uchukuzi, ufamasia, magari na sekta ya huduma zikiwamo SDV-Transami, AGS, Frasers Schneider, Peugeot, Renault, Michelin na Proparco.

Wawekezaji wengine ni   Total Kenya, Bamburi Cement, Alcatel, na kampuni ya mawasiliano ya Ufaransa Telecom yenye ubia na Telkom Kenya na Orange Mobile.

Kwa mujibu wa mpango wa ziara nzima, Rais Kenyatta akiwa Ujerumani atakuwa na  mkutano na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.

Miongoni mwa masuala ya kujadiliwa nchini humo ni pamoja na biashara, uwekezaji na ushirikiano katika usalama, utamaduni na elimu, utalii, amani katika kanda na migogoro ya Sudan Kusini na Burundi.

Muimbaji Huyu wa Tanzania Aigiza Kwenye Msimu Mpya wa Tamthilia ya Empire

0
0
Tamthilia ya Empire iliyojikusanyia mashabiki wengi duniani, Jumatano iliyopita ilirejea tena katika msimu wake wa tatu.


Katika msimu huo, muimbaji wa Tanzania aishiye Marekani, Koku Gonza ameshiriki. Koku anaonekana kwenye scene moja akimfundisha Hakeem kucheza piano.


Mfahamu zaidi kwa historia yake hapo chini.

Koku Gonza, the daughter of a Tanzanian folk singer, has shared the stage with an eclectic range of her influences. She has opened for Saul Williams, Roy Ayers, Anthony David, Yahzarah, Eric Roberson to name a few. As an Indie artist, Koku Gonza composed,arranged and performed all vocals, as well as played the guitar on all of her albums. Her song, L.O.V.E. serves as the lead single from her studio album Radiozophrenic released in 2011. L.O.V.E. debuted on BET International, Channel O, and other media outlets that feature breakout artists. In July 2012, Koku Gonza completed her first music tour in France. She performed in 11 cities in Southern France, and received rave reviews from various French media outlets like Soul Bag Magazine and +D’Afrique.


Koku Gonza’s music has been compared to the late legends Bob Marley and Mama Africa-Miriam Makeba as contemporary artists like Sade, Corrine Rae Bailey and Lianne La Havas. Koku Gonza’s music is parallel to the translation of her Kihaya name, which means lovely. She applies love, soul and passion into the ingredients of her genre-defiant pallet in new project Love Culture. Recently she released her latest single and music video for her song Clearest Sky. Clearest Sky is from her self-produced album Love Culture. Love Culture features international jazz bassist and composer Lonnie Plaxico and other great musicians on her self-produced indie project.
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live




Latest Images