Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104774 articles
Browse latest View live

Irene Uwoya Adai Anapenda Kuigiza ‘Scene’ za Mahaba

$
0
0
Staa wa filamu Irene Uwoya amesema anapenda sana kuigiza ‘scene’ za mapenzi katika filamu kwa sababu ni kitu ambacho anaweza kukifanya kwa ukamilifu zaidi.

Muigizaji huyo ambaye alionyesha uwezo mkubwa katika filamu ya Fair Decision, Pretty Girl pamoja na Oprah, amekiambia kipindi cha Uhondo cha EFM kuwa filamu ya Oprah ndio filamu ambayo ilimpa mume.

Kiukweli scene za mapenzi (mahaba) nazipenda kwa kuwa nazifanya vizuri,” alisema Irene. “Kama filamu ya Oprah ndio filamu ambayo ilisababisha nikaolewa, mume wangu alinipigia simu akaniambia nimeona movie yako ya Oprah nataka nikuoe,” alifanunua zaidi.

Lakini ni movie ambayo ilinipa wakati mgumu sana kwa familia yangu, wakiona hii movie si wataniua?. Lakini bahati nzuri baada ya baba kuiona akanipa big up na akanipa ruhusa ya kufanya movie,” aliongeza Irene.

Irene Uwoya kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja aitwaye Krish.

Bifu la Wanamuziki Diamond Platnumz na Ali Kiba Sasa ni Vita ya Kifamilia!

$
0
0
Imevuja! Harakati za kusaka mafanikio na kufika mbali kimuziki zimeibua jipya kati ya wakali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ ambapo vita yao imehama kutoka kwa mtu na mtu na sasa imekuwa ya kifamilia.

Wachunguzi wa masuala ya burudani Bongo wanadai kwamba, kila mmoja anatumia familia yake kujifanyia matangazo (promo).Kwa mujibu wa sosi aliye karibu na Kiba, kwa sasa jamaa huyo anatembelea nyota au Waswahili wanasema viatu vya Diamond kwa kufuata staili ileile anayoitumia kujifanyia promo ambayo mpaka sasa imempa mafanikio makubwa.

KISIKIE CHANZO
“Hivi Wikienda mnajua kuwa kwa sasa Ali (Kiba) ameona afuate staili ya Diamond? Kwa sababu kama ninyi ni wafuatiliaji mtagundua kuwa zamani alikuwa hana mazoea ya kuanika familia yake kama ilivyo sasa.

AANISHA STAILI HIYO
“Kwa mfano ni hii staili yake mpya ya kutoka na mama, dada yake, Zabibu na sasa anatumia hata watoto kama Diamond anavyomtumia Tiffah (Latifah Nasibu).

“Hii ni staili ambayo amekuwa akiitumia Diamond ambaye huwa anapenda kutoka na Esma (Platnumz) au Queen (Darleen) na mama yao, Sandra (Sanura Kassim) kisha anamuongezea Zari

UHUSIANO NAO WATAJWA
“Kiukweli kabla ya Diamond kuwa anafanya hivyo, zamani Kiba tulikuwa hatumuoni anaonesha uhusiano wake na mwanamke hadi ana watoto watatu kwa mama tofauti lakini hata siku moja, hakuwahi kuwaonesha mama zao kwa maana ya uhusiano alikuwa akifanya siri.

AANIKA UHUSIANO WAKE NA JOKATE
“Kuonesha kuwa anakanyaga viatu vya Dangote (Diamond), alivyoingia kwenye uhusiano na Kidoti (Jokate Mwegelo), akaanza kujiweka wazi kama Diamond huku habari zake zikitawala kwenye media (vyombo vya habari) mbalimbali ndipo akaanza kushaini,” kilisema chanzo hicho na kuweka pozi kidogo.

MAMA ADAIWA KUTOA KIAPO
Chanzo hicho kiliendelea kunyetisha kuwa, Mama Kiba amekula kiapo cha kuhakikisha anamtoa mwanaye kama ilivyo Mama Diamond na kuahidi kuwa naye kwenye kila jambo atakalokuwa akilifanya kuhakikisha anampaisha mwanaye.

Kilitambaa na mistari kuwa, Mama Kiba anajua busara za mama humuongoza mtoto hivyo kwa sasa hataki kukaa mbali hivyo atafanya kila njia kuhakikisha mwanaye anakuwa juu.

KIBA AANGUSHA PATI YA MWANAYE AMAYA
‘Ubuyu’ ulizidi kumwagwa kwamba, katika kuonesha kuwa kwa sasa ameamua, hivi karibuni Kiba alimfanyia mwanaye, Amaya bonge la pati ya ‘bethidei’ akionekana akikata keki na kuruhusu mapichapicha tofauti na zamani ambapo alifanya mambo yake kwa usiri mkubwa.

DIAMOND MBELE KWA MBELE
Chanzo kingine cha upande wa Diamond kilieleza kuwa wakati Kiba akimfukuzia jamaa huyo kwa kufuata nyayo zake, msanii huyo naye ameongeza spidi ili kuzidi kufika mbali.

“Sasa hivi vita ni ya kifamilia zaidi, yaani Diamond ndiyo anazidi kuongeza familia ya Wasafi ili kila mmoja atumie fursa ya kumtangaza afike mbali zaidi,” kilisema chanzo hicho.
diamondplatnumzMondi akiwa na mamaake.


Baada ya kunyetishiwa habari hiyo, Wikienda lilimwendea hewani Kiba ili kupata ukweli wa kile kinachoelezwa ambapo mambo yalikuwa hivi;
Wikienda: Kiba mambo vipi? Nina maswali nataka kukuuliza maana kuna shabiki wako ametunyetishia ubuyu f’lani hivi.
Kiba: Hakuna shida ongea tu.

Wikienda: Kuna madai kuwa wewe kwa sasa unafuata staili ya Diamond kwa kuamua kumuanika mama yako kila kona, unalizunguziaje hili?
Kiba: Siyo kweli. Mama yangu aliniomba aje kwenye event yangu ndiyo maana nilimkubalia.
Wikienda: Mbona inadaiwa kuwa umeona ndiyo njia ya kukupaisha kwani zamani ulikuwa huna kawaida ya kuanika uhusiano wako wakati wa Jokate umemwanika kwa sababu ya kutafuta kiki?
Kiba: Ehee, endelea..
Wikienda: Samahani hivi wewe una baba?
Kiba: Ninaye ndiyo, yupo nyumbani Kariakoo (Dar). Kwani vipi?
Wikienda: Mbona hujawahi kumuanika kwa mashabiki wako?
Kiba: Siyo kweli, alishaonekana, kuna wakati waandishi walinifuata nyumbani nikapiga naye picha na naomba niseme tu mimi kuonekana na wazazi wangu siyo lazima, inategemea na ishu, kama ishu itakuwa ni lazima wazazi waonekane, wataonekana lakini kama haina ulazima hawataonekana.

DIAMOND VIPI?
Alipotafutwa kuhusiana na ishu ya vita yao ya mafanikio kuwa sasa inahusisha familia, Diamond alifunguka:

“Kila mtu ana namna yake ya kutoboa ‘so’ siyo mbaya mtu ukitumia fursa zote zilizopo, mimi sasa hivi kuna vitu vipya kibao, hapa (Paris, Ufaransa) nimekutana na Fally (Ipupa) na Awilo (Longomba) na tayari mtoto wa Kimanyema nimeshafanya kweli,” alisema Diamond.

DIMOND NA KIBA
Diamond na Kiba wamekuwa kwenye vita kubwa ya kutafuta mafanikio ya kimuziki kwa muda mrefu ambapo wachambuzi wa burudani wanaitafsiri kuwa imechangia kuwasukuma mbele lakini imewagawa mashabiki wao.

Chanzo:GPL

Mwanafunzi wa Darasa la Tano Ajinyonga Kwa Kutumia Khanga ya Mama Yake..

$
0
0
Mshtuko! Mwanafunzi wa wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Mchikichini ‘B’ ya mjini hapa, Anosisye Gidion (12), ameacha viulizo kibao baada ya kujinyonga kwa kutumia kitenge cha mama yake, Judith Kilalu ‘Mama Kapipi’.

Tukio hilo la kuhuzunisha lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita, majira ya saa 1:00 asubuhi nyumbani kwao maeneo ya Mji Mpya mjini hapa.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Ashura na rafiki wa marehemu, Hussein walisema kuwa chanzo cha denti huyo kujinyonga kilidaiwa kuwa ni kitendo cha mama yake kumchapa na kumtishia kumpeleka polisi baada ya kuchukizwa na kitendo chake cha kurudi nyumbani saa 6:00 usiku huku akidaiwa kuonekana akiwa na kundi haramu la vibaka la Kizazi Jeuri.
Kanga Aliyotumia Kujinyongea

“Anosisye alichelewa kurudi nyumbani, ilipofika saa 4:00 usiku, mama yake aliamua kumtafuta akaambiwa alionekana akiwa na lile kundi lililokupora wewe (mwandishi wetu) maeneo ya Stendi ya Daladala ya Mji Mpya,” alisema mmoja wa mashuhuda hao huku akirekodiwa.

Kwa upande wake, mama mzazi wa denti huyo aliyeangushiwa zigo la lawama juu ya kifo cha mwanaye alisema: “Mwanangu alichelewa kurudi nyumbani usiku. Nilizunguka kumtafuta, nikaambiwa alionekana akiwa na Kizazi Jeuri hivyo nilimchapa sana na kumtisha kukicha nitampeleka polisi.

“Kulipokucha aliandaa nguo za shule, cha ajabu nimemkuta amejinyonga. Inauma sana jamani.”
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa  wa Makaburi B, Amiri Kombo aliyekuwepo eneo la tukio alithibitisha kutokea kwa tukio hilo katika mtaa wake.

Wazazi wanahofia watoto wao kujiunga na kundi hilo lililomvamia mwandishi wetu na kumpora kamera na simu ambao aliwafungulia jalada la kesi namba MOR\RB\140\2016 hivyo wanasakwa na polisi.

Mzee Yusuph Aamua Kufunguka Kuhusu Wake Zake...Adai Wanamuumiza Kichwa Sana Kiasi cha Kumvuruga Akili

$
0
0
Mkurugenzi wa Kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yussuf amesema hakuna kitu kinamuumiza kichwa kama kutoelewana kwa wake zake wawili.
mzee2

Akizungumza katika kipindi cha Sporah Show cha Clouds TV, Mzee Yussuf amesema anapitia wakati mgumu sana kuwamiliki wake wawili anaowapenda wakati wao hawapendani.

“Kusema kweli napata wakati mgumu kuwahandle, yanii linanivuruga sana hili swala,” alisema Mzee Yussuf. “Ndio maana natamani hata kesho waelewane. Sometime ni raha wakiwa hawaelewani kwa maana hata kama nimeenda pahali labda nimezunguka hakuna anayelinda” alifafanua zaidi.

“Lakini hii ni chugu sana, hili kwangu ni tatizo, natakamani leo au kesho waelewane. Lakini tatizo la hawa yote ni watu wa karibu, ndio maana mimi nimeshawaambia kwa mdomo wangu, hili jambo nataka liishe, sitaki kusema naomba liishe kwa sababu nilishawaomba sana, na ninachoona ustaa ndio unawasumbua wanashindwa kujua mimi ni staa zaidi yao,” aliongeza Mzee Yussuf.

Mwanzo wa mwaka huu, Mzee Yussuf alidai wake zake Leila Rashid na Chiku awamekatazwa kutumia mtandao wa Instagram kwa madai mtandao huo unakuza ugomvi wao.

Augustino Mrema: Nimekubaliana na Mbatia yaishe Nimefuta Kesi Kuendelea na Kazi zingine

$
0
0
Aliyekuwa Mbunge wa Vunjo Augustino Mrema amesema wamekubaliana na Mbunge wa sasa James Mbatia kwamba kesi ambayo alikuwa ameifungua Mrema iishe kwa maslahi mapana ya wananchi wa jimbo la Vunjo.

'Mrema ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na EATV kuhusiana na taarifa kwamba ameshindwa kesi ya uchaguzi wa jimbo la Vunjo aliyoifungua Mahakama Kuu Moshi''-Amesema Mrema
''Taarifa kwamba nimeshindwa kesi sii za kweli ambacho tumekifanya ni maelewano ya mimi na Mbatia kwamba kesi hii tunapoteza muda bure ambao kila mtu angefanya shughuli nyingine''-Amesisitiza Mrema.

Mrema na Mbatia wamefikia uamuzi huo baada ya kesi hiyo kuanza hivi karibuni ambapo Mrema alikuwa anapinga ushindi wa James Mbatia kwamba Mbatia alitumia njia zisizo halali katika kuupata Ubunge wa Jimbo la Vunjo.

''Tumeenda mahakamani na kila kitu kimekuwa ''settled'' baada ya kuiandikia mahakama ''statement'' ya kuwa tumeridhia kwa pamoja kuisitisha kesi ambayo ilikuwa mbele yangu kwa ajili ya kufanya kazi nyingine kwa maslahi ya wananchi na Jaji ameridhia''- Amesema Mrema.

Aidha katika matokeo ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 Mbatia alishinda Ubunge katika jimbo hilo kwa jumla ya kura 60,187 aliyemfuata ni Innocent Shirima aliyepata kura 16,617 na Mrema alipata kura 6,416.

Kazi ya TRA kukusanya kodi inaendelea…. Pesa walizokusanya kwa March 2016 zimetangazwa

$
0
0
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli ilianza kwa ajenda kubwa ya kupunguza matumizi ya serikali na kuongeza ukusanyaji wa mapato ambapo iliipangia Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ kufikia kiwango cha TRILIONI 12.363 kwenye makusanyo yake kwa mwaka 2015/2016.

April 04 2016 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’, Alphayo Kidata ametoa ripoti inayoonyesha kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha March 2016 kwa kukusanya TRILIONI 1.316 ambayo ni sawa na 101.0% ya lengo la kukusanya shilingi TRILIONI 1.302.

Jionee makusanyo kuanzia December 2015 mpaka kufikia March 2016 kwenye hii orodha hapa chini…….

                                      Lengo              

                                   (Trilioni)         Makusanyo halisi

December  2015        1,346,690.4          1,403,189.8

January     2016        1,059,863.9          1,079,993.2

February    2016       1,028,379.4           1,040,620.8

March         2016       1,302,482.3           1,316,072.4

Jumla ya makusanyo hadi sasa kuanzia mwezi July 2015 ni TRILIONI 9.88 ambayo ni 99% ya lengo la makusanyo ya TRILIONI 9.98 ya miezi tisa kwa mwaka wa fedha 2015/2016

Huyu Ndio Kocha Mpya wa Chelsea Atakayejiunga na Timu Mwisho wa Msimu 2015/2016

$
0
0
Baada ya klabu ya Chelsea ya Uingereza kumfukuza aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho  miezi kadhaa iliyopita na nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa muda Guus Hiddink, April 4 uongozi wa Chelsea umetangaza kocha wa kudumu atakayejiunga na klabu hiyo mwishoni mwa msimu.

Chelsea imetangaza kuingia mkataba wa miaka mitatu na kocha wa timu ya taifa ya Italia Antonio Conte, Chelsea imempa mkataba Conte ambaye atajiunga na timu hiyo baada ya michuano ya Euro 2016 kumalizika akiwa anaiongoza timu ya taifa ya Italia katika michuano hiyo.


Klabu ya Chelsea na soka la Uingereza kwa ujumla unaangaliwa sana popote uendapo, mashabiki wa soka Uingereza wanamapenzi na soka kweli, natumaini nitafurahia mafanikio hapa kama ilivyokuwa Italia”  Antonio Conte

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Antonio Conte aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Italia kuanzia mwaka 1994 hadi mwaka 2000, lakini amewahi kuvifundisha vilabu vya Juventus ya Italia kuanzia mwaka 2011-2014, Siena na timu ya taifa ya Italia kuanzia mwaka 2014 hadi 2016. Conte kwa sasa ana umri wa miaka 46.

Dayna Nyange Adai Anapenda Kuvaa Nguo za Kuacha Kiuno Chake Wazi

$
0
0

Msanii wa kike, Dayna Nyange amedai anapenda kuvaa nguo ambazo zinaacha wazi sehemu ya kiuno chake.
Dayna

Akizungumza katika kipindi cha Hatua Tatu cha Times Fm, Dayna amewataka watu kuacha tabia ya kuingilia maisha ya watu wengine.

“Unajua usipende kumjaji mtu kwa mavazi, mimi si mvaaji wa vikaptula au vinguo vifupi napenda tu kuvaa nguo inayoniacha ‘kakiuno’ tu kidogo wazi, kwa sababu napenda” alisema Dayna.

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na video yake ya wimbo ‘Angejua’.

Fally Ipupa Amshirikisha Diamond Platnumz kwenye Wimbo Wake Mpya

$
0
0
Nguli wa muziki wa Africa kutoka DRC Congo mwenye makazi yake jijini Paris Ufaransa amefanya collabo na mkali wa Africa Mashariki Diamond Platnumz, kazi hiyo imefanyika jijini Paris wakati Diamond akiwa kwenye mapumziko mafupi na familia yake.

Diamond Ameandika hivi:

I wish you guys can get jus a second to hear what we did with my brother @fallyipupa01 Last night in Paris!!!
(Natamani walau mngepata japo sekunde moja tu ya Kuskia tulichokifanya jana katika Ngoma Mpya alonishirikisha @fallyipupa01 ..... Mwenyewe anasema kabla ya Kushoot Video lazma tuiingilie Chimbo kama Wiki nzima Hivi na Madancers wetu wote, Full Dance na Mapande ya ajabu

Mbunge Sadifa Alalamika, Asema Wastara Alimloga

$
0
0
Aliyekuwa mume wa nyota wa Filamu za Bongo, Wastara Juma ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Donge (CCM), Zanzibar, Sadifa Juma ameibua jambo zito miongoni mwa jamii akidai kuwa, mtalaka wake, Wastara Juma amekuwa akimroga.

Madai hayo aliyatoa Alhamisi iliyopita baada ya gazeti hili kumuuliza habari zilizoenea kwamba, amemuangukia Wastara akitaka warudiane kwani yaliyopita si ndwele.
Sadifa alisema kuwa, aligundua hilo la kurogwa baada ya Wastara kuondoka nyumbani kwake na kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa, amepewa talaka mbili.

Akizungumza kwa dakika 25, Sadifa alikwenda mbele zaidi kwa kusema: “Ukimwangalia Wastara harakaharaka unaweza kusema ni mwema sana lakini hana wema wowote. Hivi Wastara ni wa kuniroga mimi kweli?”
Alipoulizwa kuwa amepata wapi hizo habari za kulogwa Muheshimiwa akasema:

“Niliambiwa na watu wawili, mmoja dereva wangu, mwingine ni kijana wangu. Tena hao wameniambia juzi tu baada ya mambo kuharibika. Wakasema kuna siku walikwenda na Wastara kwa huyo mganga. Wastara alikuwa na ndugu yake mmoja.
Walipofika, vijana wangu hawakuingia. Kwa hiyo hawakujua walifuata nini! Mara ya pili akawaambia kuwa, wamekwenda pale kuchukua dawa eti ili isaidie ndoa yetu iwe na amani na mimi niache macho juujuu. Akapewa kombe kama unalijua kombe, aitie kwenye maji anipe ninywe."
“Sasa wale vijana wangu wakamshauri Wastara kwamba, kama maji hayo ya kombe atanipa yeye ninywe nikigundua itakuwa balaa, wakamwambia awape wao ndiyo wanipe mimi ninywe ili nikijua wataniambia ni dawa ya kukinga mwili. Lakini wao hawakunipa na wanayo mpaka leo (juzi, Alhamisi)!”

Akizungumzia suala la kupigia magoti Wastarra ili warudiane Sadifa alisema,
“Kwanza hizo habari si za kweli. Mimi wale mashemeji zangu waliniomba gari wamfuate ndugu yao. Nilitoa kwa ubinadamu tu, nikawawekea na mafuta.” na akadai kuwa mtu anayejitambulisha kuwa babu yake Wastarra sio babu yake ni bwana ake.

“Yule si babu yake Wastara. Yule ni bwana’ake kama hamjui. Mimi juzi tu ndiyo baadhi ya ndugu zake wameniambia ukweli kwamba yule babu, si babu yao bali alikuwa rafiki mkubwa wa marehemu Sajuki (Juma Kilowoko, aliyekuwa mume wa Wastara).”

“Sasa wewe jiulize, mkeo mnagombana, anakwenda kwa rafiki wa marehemu mume wake. Kwa nini asiende kwao? Kule anakaa kufanya nini? Yule Babu ndiye amenirithi mimi kwa Wastara.”

“Kuna wakati fulani Wastara aliumwa, dokta akamwambia atulie kwa muda asitembeetembee. Kesho yake akaniambia anakwenda Morogoro kwa huyo babu yake. Nilimkatalia, akalazimisha, akaenda. Sasa mke anawezaje kwenda mahali bila ridhaa ya mumewe?

“Alipokuwa kule, nikawa nampigia simu hapokei kwa muda wa siku tatu. Siku moja nyumbani alikuja kijana wake anayemfanyia biashara, nikamwambia Wastara yupo Morogoro, akampigia simu mbele yangu, akapokea, wakaongea. Walipomaliza, mimi nikampigia, hakupokea!”

SIKU YA WASTARA KUONDOKA NYUMBANI
“Mimi sikuwahi kutoa talaka kama Wastara anavyoeneza hizi habari. Siku hiyo anaondoka nyumbani mimi nilikwenda kwenye kamati za bunge, wakati naingia akanipigia simu na kusema anataka tuongee.

“Nilimwambia tutaongea baadaye yeye akataka muda uleule, nikakataa. Akasema anachotaka yeye nimpe shilingi milioni kumi afanye biashara. Nikamwambia sina, ndiyo akaondoka. Sasa jamani, mkeo kama anataka pesa ukamwambia huna ndiyo aondoke nyumbani? Mimi naona alifuata pesa tu

Picha zinatisha: Kweli michepuko sio dili, awamwagia Tindikali kisa wivu wa Mapenzi

$
0
0
Kwa mujibu wa taarifa nlioipata toka.kwa grup la wasapu inasema
Mdada ambae ni mpendwa aliomba ruhusa kwa mumewe anaenda kwa maombi /mkutano wa injili Mbeya jamaa akamkubalia kumbe moyoni anamsaree.. mke alipotoka kupanda daladala mume nae akapanda la kwake walipofika stand mdada akapanda gari ya kyela na mumewe nae akamfata (bila mke kujua).

Mwanamke akafika guest na mchepuko ulikua ushafika na mume bae akafikia guest hiyo hyo bila bibie kujua,sasa baadae usiku mme akaenda kugonga rum ya bibie na mchepuko bila kujua wakafungua mlango .
Mme alikua na tindikali iliomixiwa kwa "uweledi" wa hali ya juu, akawamwagia na mwishowe akajimwagia.

Hizo picha ndo matokeo ya tindikali.

PNC: Wananiroga Ndio Maana Sifanyi Vizuri Tena Kwenye Music

$
0
0
Msanii PNC ametoa sababu ya yeye kutofanya vizuri sasa hivi kwenye kona ya muziki, huku akihusisha imani za kishirikina, ambazo hivi karibuni baadhi ya wasanii wamekiri kuwepo kwa mambo hayo.

PNC ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa pamoja na kuwa ameshawahi kufanya kazi zingine tofauti na muziki, ana imani anafanyiwa figisu figisu za kishirikina.

“Wananiroga kweli kweli, mi nimetoka maisha ya local kabisa, mimi nimeshawahi kuwa hata mchunga ng'ombe mchunga mbuzi, nishakuwa muwindaji, maisha yetu yale ni ya dhiki, kwa hiyo yani asije mtu akafikiria labda tunamuona anahangaika hangaika, anakomaa kutoa nyimbo kwa sababu labda anataka tu ajitutumue kufanya kitu kimsaidie katika maisha”, alisema PNC.

Pia msanii huyo ambaye kwa sasa ana wimbo mpya unaoitwa 'ekotite' amesema hata akiendelea kutoa muziki na kutofanya vizuri, hatoacha kwa sababu ki kitu ambacho anakipenda.

“Na hata nikifeli muziki niko tayari kufanya kitu chochote, nafanya muziki kwa sababu naupenda”, alisema PNC

HAPA Nimekuwekea Habari za Kutoka Katika Magazeti ya Siku ya Leo Jumanne Tarehe 5 April...Ikiwemo ya NSSF Kuliwa Kweupe...

$
0
0

HAPA Nimekuwekea Magazeti ya Siku ya Leo Jumanne Tarehe 5 April...

Wabunge Washtushwa TCRA kutumia Bilioni 18 kwa Semina na Warsha

$
0
0
Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji (PIC) imeshtushwa baada ya kubaini Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitumia Sh18 bilioni mwaka 2013/2014 kwa ajili ya mafunzo, semina na warsha.

Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Lolesia Bukwimba alisema matumizi ya fedha hizo ni makubwa ikilinganishwa na kazi iliyofanywa na mamlaka hiyo kwa mwaka huo wa fedha.


Alisema wakati mapato ya TCRA kwa mwaka huo yalikuwa Sh79 bilioni, gharama za uendeshaji zilikuwa Sh76 bilioni.



“Hii ina maana fedha zilizopelekwa Hazina zilikuwa kidogo. Kama mamlaka ingepunguza matumizi, Serikali ingepata mapato ya kutosha,” alisema.

Bukwimba alisema hilo ni tatizo na kamati hiyo itatoa maagizo kwa mamlaka hiyo Jumamosi ijayo itakapoitembelea.



“Kuna mambo mengi ya kitaalamu ambayo tunahitaji kuona shughuli zake zinazofanywa na mamlaka, tutatoa maagizo siku ambayo tutaitembelea,” alisema Bukwimba.

Hata hivyo, mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Profesa Haji Semboja aliitetea mamlaka hiyo akisema kiasi hicho kilichotumika kwa ajili ya semina, mafunzo na warsha kinatokana na unyeti wa taasisi hiyo.



“Taasisi inasimamia kampuni zinazotoa huduma za teknolojia za kisasa ambayo ni ngeni hapa kwetu, hivyo wafanyakazi wetu wanatakiwa kuwa na ufahamu zaidi ya hao watoa huduma,” alisema Profesa Semboji.

Semboja, ambaye ni mchumi, alisema: “Pamoja na mambo mengine, wafanyakazi wetu wanasimamia kampuni za mitandao ya simu, matoleo ya simu yanatoka mara kwa mara, wanatakiwa kufahamu teknolojia wanayoisimamia. Hapa ni lazima waende darasani.”


Alisema wafanyakazi hao wakiachwa bila kupata mafunzo ya mara kwa mara watajikuta baada ya kipindi kifupi wanapitwa na teknolojia zinazozidi kuibuka kila wakati.


Kwa upande wake, Sabrina Sungura ambaye ni mjumbe na mbunge wa Viti Maalumu, aliitaka mamlaka hiyo kufanya marekebisho ya minara ya simu mkoani Kigoma.



“Hii ni hatari kwa usalama,” alisema.

TAHADHARI: Mboga za Majani Wanazokula Wakazi wa Dar es Salaam ni Sumu Tupu

$
0
0
Nimeileta hii mada huku kwa makusudi kwakuwa inahusika na mapishi lakini vile vile na afya zetu kwakuwa mapishi na afya haviachani

Sehemu kubwa ya mboga za Darisalama zinatoka mabonde ya Mto Msimbazi, Mandela road bonde lililoko kituo cha garage, Jangwani, Kigogo sambusa na maeneo ya Tandale na kwingineko
maji yanayopita kwenye mabonde haya ni machafu, yenye kemikali toka viwandani, yenye vinyesi toka vyooni nk ndio hayo hayo yanayonyweshea mbogamboga hizi tangu kuchipua hadi kukomaa.

Kwa vyovyote vile, maji haya yakipimwa ni wazi yatakutwa na kiwango kikubwa cha sumu mbalimbali zinazosababisha magonjwa kansa na ngozi.

Uchafu tunaoutupa kwenye mito ipitayo kwenye haya mabonde kama betri za simu na magari material za friji mbovu, computer mbovu nk nk vyote hivi vimebeba kemikali zenye sumu kali.

Tusipochukua tahadhari tutaishia kuongeza vyumba pale Ocean road kwenye ile hospital ya kansa

By Mshana JR/Jamii Forums

Wanajeshi wa Tanzania Waingia katika Kashfa ya ngono DRC ya Kuwaingilia Watoto Wadogo

$
0
0
Wanajeshi Congo
Ujumbe wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (Monusco) umeanzisha uchunguzi dhidi ya wanajeshi wa Tanzania wanaodaiwa kuhusika na vitendo vya udhalilishaji kingono.

Wanajeshi hao wanaodaiwa kufanya vitendo hivyo vya kingono dhidi ya raia ni wale wanaohudumu chini ya kikosi cha jeshi kilichopo Kijiji cha Mvivi karibu na mji wa Beni ulioko jimbo la mashariki mwa DRC la Kivu ya Kaskazini.

Monosco imesema imetuma mara moja timu ya uchunguzi katika eneo hilo kubaini ukweli wa kashfa hiyo inayowakabili Watanzania hao.


Monusco ilisema hatua za kinidhamu zitachukuliwa iwapo itathibitishwa kuwa wanajeshi hao walihusika katika unyanyasaji wa kingono ikiwamo dhidi ya watoto.


Shutuma hizo zinakuja baada ya wanajeshi wa Ufaransa na wa kutoka nchi nyingine kutuhumiwa kuhusika katika udhalilishaji wa kingono katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.


Umoja wa Mataifa (UN) umesema umesikitishwa na vitendo vya baadhi ya wanajeshi kufanya unyama kwa wananchi wa nchi hizo.


UN walisema kinachosikitisha zaidi wanaofanyiwa vitendo hivyo ni watoto wadogo.


Matukio ya Ushirikina..Walimu Walazwa UCHI na Kuchapwa Viboko

$
0
0
Ofisi ya Elimu wilayani Kisarawe, Mkoa wa Pwani imelazimika kuwapa likizo walimu saba wa Shule ya Msingi Mingwata ili kuwajenga kisaikolojia baada ya kukithiri kwa matukio ya kishirikina yanayowakumba katika shule hiyo.

Walimu hao wanakumbana na matukio ya ajabu ikiwamo kujikuta uchi, kupigwa fimbo na mtu asiyeonekana na kulazwa nje ya nyumba zao.

Mmoja wa walimu walioathirika na matukio hayo, Emmanuel Shaaban alisema yeye na familia yake hawana raha kutokana na matukio hayo kwa kuwa usiku huvuliwa nguo na kujikuta wamelazwa sehemu nyingine, huku wakiwa wamechanjwa kwa wembe mwili mzima.

“Tarehe 26 mwezi wa pili, siku ya Alhamisi sitaisahau kabisa. Ndiyo siku ambayo nilikatwa viwembe mwili mzima na hali yangu ilikuwa mbaya, niliishiwa nguvu na mwili ukawa na ganzi na nilipokwenda hospitali niliambiwa sina ugonjwa,” alisema Shaaban.

Alisema alipotoka hospitali alikwenda kijijini kwao mkoani Mwanza na huko aliendelea kuwa na hali mbaya kutokana na kuzimia mara kwa mara kwa sababu ya maumivu ya kichwa hadi alipotibiwa kienyeji.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Mikidadi Mbelwa alisema awali alikuwa akiona vituko usiku na mchana, lakini alivumilia huku akitunza siri bila kuwaeleza wenzake ili asiwakatishe tamaa.

Mbelwa alisema baadhi ya matukio aliyokutana nayo ni kuvuliwa nguo usiku, kulazwa eneo jingine, kuchapwa viboko, kumwagiwa damu kwenye korido ya nyumba, kuchanjwa kwa wembe, kuzungukwa na nyoka mwilini, kuona mtu na kisha anapotea na kutupwa kwenye mashimo.

Mzazi wa watoto wanaosoma katika shule hiyo, Asha Kondo alikiri kuwapo kwa matukio ya watoto kuugua na kuanguka hadi uongozi wa kijiji ulipopeleka mganga wa kienyeji kutoa kinachodaiwa ni uchawi.

Mratibu wa Elimu wa Kata ya Marui, Damaru Charles alisema amekuwa akipokea malalamiko hayo na kuyawasilisha ngazi za juu.

Ofisa Elimu Msingi wilayani hapa, Aurelia Rwenza alisema tatizo hilo linawapa shida walimu na kurudisha nyuma maendeleo ya elimu katika sehemu hiyo.

“Kwa kweli walimu wameathirika, hivi sasa tunatakiwa kuwajenga kisaikolojia,” alisema.

Maalim Seif Amfungia Milango Dk. Shein Asema Hayuko Tayari Kukutana Naye Kwa Ajili ya Muafaka....

$
0
0

Maalim Seif Sharif Hamad
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema hayuko tayari tena kukutana na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kwa ajili ya mazungumzo ya kutafuta mwafaka.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini Unguja, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kutangazwa kwa maazimio 13 ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho, kilichokutana kuanzia Aprili 2, mwaka huu.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua kama atakwenda Ikulu pindi akiitwa na Dk. Shein kwa ajili ya mazungumzo ya kutafuta mwafaka, Maalim Seif aliweka wazi kwamba hana haja ya kufanya hivyo kwani tangu awali kiongozi huyo hakuwa na nia njema na suala la Zanzibar.
“Siko tayari kukutana na Shein, kama nani na nazungumza nini nikikutana na Dk. Shein Ikulu? Labda kama nitakutana naye kwa njia nyingine sawa za kibinaadamu, lakini hatuko tayari tena kuzungumza na Shein,” alisisitiza Maalim Seif.
Alisema haoni uwezekano wa Serikali ya Dk. Shein kuendelea kuwapo madarakani hadi ifikapo 2020 na hilo linatokana na msukumo wa nchi wafadhili kusita kutoa misaada katika baadhi ya miradi waliyoahidi kwa Tanzania.
“Uwezekano wa Serikali hii kuendelea hadi 2020 siuoni kutokana na presha hii  ya jumuiya za Kimataifa,” alisema Maalim Seif.

Kesi Imemgeukia Lyatonga Mrema, Anatakiwa Kulipa MILIONI 40 Kabla ya Tarehe 5 June

$
0
0
Kesi ya Lyatonga Mrema kupinga ushindi wa Ubunge wa James Mbatia jimbo la Vunjo ilikua Mahakamani tena April 4 2016 ambapo jipya lililotangazwa ni kwamba Mahakama kuu kanda ya Moshi imeridhia makubaliano yaliyofikiwa kati ya Mbunge wa Vunjo James Mbatia na Agustino Mrema kwa shauri hilo kuisha na kwamba Mbatia ndiye Mbunge halali wa Vunjo na Mrema atatakiwa kulipa sehemu ya gharama za mawakili wa Mbatia shilingi Milioni 40.

Majambazi Sugu Yakuiba Magari Aina ya Noah Yadakwa DAR...Kama Ulishawahi Ibiwa Gari Soma Hapa

$
0
0
Wezi wa Magari wamedakwa waligeuza nyumba yao maeneo ya Boko/Bunju Yard ya Magari ya Wizi , Kama kuna ndugu jamaa au Rafiki aliibiwa Noah mpe Taarifa afike Oysterbay police ‪#‎UlinziShirikishi‬..

Viewing all 104774 articles
Browse latest View live




Latest Images