Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Jipu Ofisi ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Hili Hapa....

$
0
0
KAMATI ya Bunge ya Katiba na Sheria, imeagiza kufanyika uchunguzi haraka katika jengo la ofisi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ili kuweza kubaini ubadhirifu uliofanywa na wataalamu waliohusika katika mchakato wa ujenzi wa jengo hilo.

Akizungumza jana na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mohamed Mchengerwa ambaye pia ni Mbunge wa Rufiji alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya kamati hiyo kufanya ukaguzi katika jengo hilo na kubaini limejengwa chini ya kiwango.

“Tumetembelea jengo hilo na kujionea limetumia fedha nyingi lakini limejengwa chini ya kiwango kwani halina hata miaka tisa lakini lina ufa mkubwa ambao unahatarisha maisha ya wafanyakazi ndani ya jengo hilo,” alisema Mchengerwa.

Alisema jengo hilo limetumia zaidi ya Sh bilioni 8 katika ujenzi, lakini limejengwa chini ya kiwango.

Aliongeza kuwa kisheria fedha zilizopangwa kwa ajili ya mradi huo zilitakiwa zibaki asilimia 20 kwa ajili ya ukarabati lakini zimebaki Sh milioni 200 tu na hakuna maelezo ya kujitosheleza.

Mchengerwa alisema hali hiyo imesababisha kamati hiyo kuagiza uchunguzi ufanyike na wataalamu waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria kwa kufunguliwa kesi za jinai na madai.

Diamond Akitaka Kuandika Wimbo wa Kuumizwa Kimapenzi Humfikiria Msichana Huyu (Audio)

$
0
0
Diamond Platnumz ni bingwa wa kuandika nyimbo za kuachwa, kuumizwa na kutendwa kimapenzi.

Kamwambie, Mbagala, Mawazo, Ukimwona, Nataka Kulewa, Bado na zingine, zilihit kwasababu ziligusa maisha ya wanaume wengine wahanga wa malavidavi. Lakini staa huyo ambaye hivi karibuni alisema Zari ameutunza moyo wake kwenye friji kiasi cha masuala ya kuumizwa kuyasikia tu kwa wengine kwa sasa, humkumbuka msichana mmoja kila anapotaka kuandika nyimbo za aina hiyo.

Si Wema wale ex wake mwingine unayemfahamu, Harmonize amemtaja baada ya mimi kumuuliza tetesi kuwa mashairi ya bosi wake huyo kwenye Bado, yalimlenga ex wake, Wema Sepetu.


“Diamond hajaanza kuimba leo mambo ya kuachwa, aliimba Kamwambie, akaimba Mbagala,” Harmonize amesema kwenye Chill na Sky.
“Mimi naamini kabisa, hata mimi mwenyewe nilivyomuuliza ‘kwani ulimuimbia nani Kamwambie?’ akasema mimi nikitaka kuandika nyimbo yoyote ya mapenzi namkumbuka Sarah mwanamke ambaye nilimpenda sana.”

Sikiliza Chill na Sky na Harmonize hapo chini.

Bongo5.com

RAY C Afunguka Kuhusu Vita vya Madawa ya Kulevya..Adai Vijana Wengi Hawapo Tayari Kuingia Katika Vita Hiyo...

$
0
0
Kupitia Account yake ya Instgram Ray C aliandika haya na kuwataka vijana wa Tanzania kusimama mstari wa mbele kupiga vita matumizi ya dawa hizo kwani kuna watu wengi ambao hawapo tayari kuingia kwenye vita hiyo.

rayc1982 Ifike hatua vijana na watanzania mpende maendeleo na kuelimisha jamii vitu vyenye tija Kwa mstakabari wa taifa letu,wengine tumikuwa victim katika drugs and drug abuse ni matumaini yangu sasa watanzania wawe front line kusupport na kupiga vita madawa hayo. cha ajabu wengi wao hawako willing katika hilo Kwahiyo vijana wenzangu nawaasa kupiga vita madawa ya kulevya Tanzania yatamaliza kizazi bora cha watanzania ni wakati mwafaka kila mmoja wetu akachukua hatua kuanzia pale alipo,katika makazi yake,ama mashuleni,ama maofisini,ama mashambani,ama mahosipitalini..popote pale yatumikapo kupinga kwanguvu zote...nashangazwa unapo poteza muda wako kupost wasted things katika Social Media at kwamba Fulani kasema hivi kafanya vile! You do this for the benefit of whom!? Its shame...Tanzania bira madawa inawezekana chukua hatua na njoo upate tiba mwananyamala au mhimbili you wonna update.

Mahakama yakataa CD ya Askofu Gwajima kudaiwa kumtusi Askofu Pengo

$
0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetupilia mbali ombi la Jamhuri la kupokea CD pamoja na picha kama kielelezo katika kesi inayomkabili Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, akidaiwa kutoa lugha ya matusi dhidi ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama pengo.

Uamuzi huo ulisomwa jana mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi, Cyprian Mkeha, baada ya kupitia hoja za pande zote mbili.

Katika ombi lake, upande wa Jamhuri ulikuwa ukiitaka mahakama hiyo ipokee CD ya siku ya tukio hilo, huku upande wa utetezi ukipinga kupokelewa kwa CD hiyo.

Hakimu Mkeha alisema mahakama imetupilia mbali ombi la kupokea kielelezo hicho kwa kuwa upande wa Jamhuri umeshindwa kutimiza vigezo vya kisheria cha kuwasilisha vilelezo vya eletroniki mahakamani.

Awali, wakili wa utetezi, Peter Kibatala, alipinga kupokelewa kwa CD hiyo kwa madai kwamba shahidi aliyekuwa anawasilisha hakustahili kwani siye aliyeitengeneza CD hiyo.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro, akijibu hoja hiyo, alidai shahidi huyo ni mtaalam wa vielelezo vya elektoniki na picha na ndiye aliyeifanyia uchunguzi CD hiyo.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Mei 4 mwaka huu

NSSF yazidi Kuumbuka: Ufisadi wa Ujenzi wa Hoteli Mwanza, Jengo la Biashara Mzizima

$
0
0

Kwa kashfa hizi, watetezi wa Dr Dau washaumbuka, maana tuliambiwa hakuna mtu wa kuziba pengo lake, kumbe siri ni upigaji deal tuuu.

=> Ujenzi wa hoteli Mwanza, kampuni mbili zapewa mabilioni kwa kazi zile zile

=> Mkandarasi wa ujenzi wa jengo la Biashara la Mzizima azidishiwa malipo.

=> Ujenzi wa hoteli ya kitalii Mwanza, wakandarasi walizidishiwa zaidi ya Bilioni 16 sawa na asilimia 23 ya mradi wote bila sababu za msingi.

=> Kuhusu ujenzi wa jengo la biashara Mzizima Tower ni kwamba kampuni tatu ziliomba mradi huo ambazo ni Atlas, Ginde na Jandu ambayo ilishinda.

Wataki wa kuwasilisha maombi ya zabuni ya Jandu ilikuwa sh. 8,346,155,654 lakini kamati ya Tathmini iliketi na kupitia upya mkataba na kubaini makosa hivyo ilirekebisha zabuni hiyo isomeke 8,340,700,710.94 pamoja na ongezeko la Thamani (VAT). Jandu aliridhia marekebisho hayo.

Pamoja na marekebisho hayo, mkataba waliosainiana kati ya NSSF na Jandu ulikuwa wa kiwango kile kile kilichokosewa cha sh. 8,346,155,654 chenye ziada ya sh. 5,454,943.

Breaking News: Mtangazi Gadner G Habash Arudi Clouds FM Radio Kutoka EFM

$
0
0

Baada ya watangazaji Gerald Hando na Paul James kusemekana wameondoka Clouds FM radio, Clouds imeamua kumrudisha nguli wa utangazaji Gadner G Habash .
Diva loveness Amepost picha mtangazaji huyo akisign mkataba na kuandika haya :
So wanted to post him toka Jana .. welcome back Captain G Habash !... I am The Happiest Girl on earth, You Made Me ... 👻 S/O to My Big Boss .. ❤ You did it , ️. yaan Captainnnnn .. G. Habassshh!. Umeona Banah ..

Breaking News: Rais wa Zanzibar Dr Shein atangaza rasmi kufutika kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa

$
0
0

Akihutubia katika uzinduzi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein amesema kuwa kwenye uchaguzi wa Marudio uliofanyika Machi 20, hakuna chama kilichopata kura za rais kwa zaidi ya asilimia 10 isipokuwa CCM. Pia amesema kuwa hakuna chama kilichopata wabunge wengi isipokuwa CCM. 

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, hakuna chama kilichopewaa ridhaa ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa isipokuwa CCM. Kwamba, Makamu wa Pili amechaguliwa kwa mujibu wa sheria na hakuna nafasi Kikatiba ya kuteua Makamu wa Kwanza wa Rais ama Mawaziri kutoka Upinzani. Amesema hayo ni maamuzi ya wananchi na ni lazima yaheshimiwe. Wananchi Wamewakataa wapinzani na kuiamini CCM. Kwa hali hiyo ni kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa imekufa rasmi.

Mafuriko yafunga Barabara kuu Itokayo Dodoma Kwenda Morogoro kwa saa 10

$
0
0

Zaidi ya magari 1,500 jana, yalikwama katika eneo la Chalinze Nyama wilayani Chamwino mkoani Dodoma kwa zaidi ya saa 10, baada ya mafuriko kuziba barabara kuu itokayo Dodoma kwenda Morogoro.


Mafuriko hayo yalitokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa siku mbili mfululizo.


Akizungumza katika eneo la tukio, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema vyombo vya ulinzi na usalama vitakuwa katika eneo hilo ili kutoa ushauri kwa watumiaji wa barabara na kuwataka wananchi kufuata ushauri wa vyombo hivyo.


“Wakazi wanaoishi mabondeni wahame ili kuepusha athari zinazoweza kutokea kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha,”alisema.


Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Farida Mgomi alisema zaidi ya kaya 100 zimekosa mahali pa kuishi baada ya maji kujaa ndani ya nyumba zao.


“Kaya mbili zilichelewa kutoka kwenye nyumba wanazoishi ikabidi tutafute Kikosi cha Zimamoto ambacho kilifika na kuwaokoa,”alisema.


Mgomi alisema mafuriko katika sehemu hiyo yanatokana na daraja dogo lililopo ambalo linashindwa kuhimili wingi wa maji.


Kufuatia tukio hilo, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, viongozi wa halmashauri, tarafa na kata walitarajiwa kukutana jioni kwa ajili ya kuangalia jinsi ya kuwasaidia waliokumbwa na maafa.


“Tuone wadau wanatusaidiaje, tunapataje chakula lakini watu wa Msalaba Mwekundu wamefika na mablanketi na baadhi ya vifaa,” alisema.

Rais Magufuli Kuzuru Rwanda Kwa Mara ya Kwanza Tangu awe Rais.....Atazindua Daraja la Rusumo na Kufanya Mazungumzo na Rais Kagame Mjini Kigali

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli, kesho Jumatano, Aprili 06 mwaka huu anatarajia kufanya ziara wilayani Ngara mkoani Kagera, kwa ajili ya kuzindua daraja la Rusumo linalounganisha nchi ya Tanzania na Rwanda pamoja na jengo la Kituo cha  Pamoja cha Forodha - (OSBP).

Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habara, Mkuu wa wilaya ya Ngara Bi Honoratha Chitandaa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais Magufuli na kuongeza kuwa halmashauri ya wilaya hiyo imejipanga kuwasafirisha wananchi watakaokosa usafiri ili kufanikisha mapokezi.

Bi Chitanda amesema pia kamati ya ulinzi na usalama imejipanga kuhakikisha ziara ya Rais inakwenda vizuri bila kuingiliwa na dosari yoyote inayoweza kupelekea uvunjifu wa amani na kuwataka wananchi wote kutii sheria.

Katika ziara hiyo Rais magufuli anatarajia kukutana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame atakayeshirikiana naye katika Uzinduzi wa Daraja la Rusumo linalounganisha nchi mbili za Tanzania na Rwanda.

Baadaye, marais hao wataelekea Kigali-Rwanda  ambapo watafanya mazungumzo ya pamoja.

Rais Magufuli pia ataweka shada la maua katika makumbusho ya mauaji ya kimbari ya Rwanda 1994 mjini humo.

Mahakama ya ICC yafuta kesi dhidi ya makamu wa rais wa Kenya William Ruto na Mwandishi wa Habari

$
0
0
Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) iliyoko The Hague nchini Uholanzi imefuta kesi dhidi ya Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto na mwandishi wa habari Joshua Arap Sang waliokuwa wakituhumiwa kuhusika katika vurugu na mauaji ya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Majaji wa ICC wameeleza kuwa wameamua kuiondoa kesi hiyo baada ya kuwepo kwa mkanganyiko katika ushahidi uliofikishwa mahakamani. 

Baadhi ya mashahidi walianza kubadili ushahidi wao huku wengine wakijiondoa kwa madai kuwa walishinikizwa au kushawishiwa kutoa ushahidi huo.

Katika uamuzi wao, majaji hao wameeleza kuwa kuondolewa kwa kesi hiyo hakuwazuii wawili hao kushtakiwa tena kwenye mahakama hiyo au mahakama nyingine ya kimataifa na kitaifa.

Uamuzi huo wa ICC umepokelewa kwa hisia tofauti nchini humo. Wapo walioufurahia na kueleza kuwa kesi hiyo ilijaa mihemko ya kisiasa zaidi na kwamba kwa kuachiwa huru Ruto atakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuendelea kuwatumikia wananchi wake kwa umakini zaidi. 

Lakini wapo wanaolalamikia uamuzi huo wakiwaangazia hasa wahanga wa machafuko hayo yaliyopelekea mauaji ya zaidi ya watu 1000 na kuwakosesha makazi maelfu ya raia.

Waathirika wa tukio hilo wanaonekana kuwa katika hali ya sintofahamu zaidi kwani uamuzi wa mahakama hiyo haukufikia hatua ya kuweza kubainisha iwapo Ruto na Sang walikuwa na hatia.

Jumla ya Watumishi Hewa 7,795 Wabainika Katika Mamlaka za Mikoa Nchini......Wameisabishia Serikali Hasara ya Bilioni 7.5

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bibi Angela Kairuki amewapa wiki moja waajiri wa sekta za umma  nchini kukamilisha na kuwasilisha taarifa kuhusu watumishi hewa.

Bibi Kairuki ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokua akiongea na waandishi wa habari kuhusu taarifa za awali juu ya watumishi hewa zilizowasilishwa na Wakuu wa Mikoa nchini.

Amesema kuwa taarifa za  Machi 1 hadi April 4 mwaka huu zinaonyesha watumishi 4,317 waliondolewa katika Payroll ya Serikali ikiwa ni kasi ya kuondoa watumishi ambao utumishi wao umekoma kwa kipindi kifupi ambapo haijawahi kufikiwa kwa kipindi cha nyuma ikiwa ni mwitikio wa agizo la Rais Dkt Magufuli.

"Kutokana na Mfumo wa HCMIS ambao hufungwa kila tarehe 5 ya kila mwezi umewezesha Watumishi wa Serikali 1,284 kufutwa kwa Aprili 1 hadi 4 ikiwa imejumuishwa watumishi hewa, waliostaafu, walioacha kazi waliofukuzwa na waliofariki dunia"Amesema Angela.

 Angela amesema kuwa muda wa kufunga Payroll umeongezwa na utafungwa Aprili 12 ili kuhakiki watumishi wote wa serikali ambao hawastahili kuwepo kwenye Payroll"

Pia amesema kuwa baada ya tarehe hiyo Ofisi yake itafanya ukaguzi kwenye taasisi na mamlaka mbalimbali za Serikali ili kuhakikisha wale ambao hawawajibiki au kutimiza wajibu wao katika eneo la usimamizi wa rasilimali watu wanachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.

Mchina Anyongwa Ndani ya Gari Dar es Salaam..

$
0
0
Mfanyabiashara raia wa China aliyetambulika kwa jina la Luo Dongpeng (32), maiti yake imekutwa ndani ya gari lenye namba za usajili T145 DFY Machi 28, mwaka huu maeneo ya Kijitonyama, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar,Uwazi linakupasha.


Taarifa zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo wanaoishi  maeneo aliyokutwa Mchina huyo zinaeleza kuwa, gari la marehemu huyo walianza kuliona hapo tangu alfajiri ya siku hiyo lakini kadiri muda ulivyokuwa ukienda ndivyo walivyozidi kulitilia shaka maana hakukuwa na mtu aliyetoka ama kuingia.

Waliendelea kusema kwamba ilipofika saa 10.00 jioni walilazimika kulisogelea na kuchungulia ndani ndipo walipomuona mtu akiwa amelala kiti cha nyuma, walipomwamsha hakuamka wala kujigeuza ndipo waliwaarifu polisi wa Kituo cha Mabatini Kijitonyama.085A9757
Moja ya msumali uliokuwa umetegwa kwenye gari hilo.

Mashuhuda hao walidai kuwa huenda Mchini huyo aliuawa kisha kutelekezwa na gari lake maeneo hayo kwani alikuwa na michubuko mikononi na shingoni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Alphonce Fuime alipohojiwa na gazeti hili wiki iliyopita ofisini kwake alikiri kutokea kwa mauaji hayo.

“Huyu marehemu inaonekana alikuwa akitoka casino na uchunguzi wa awali unaonesha aliuawa sehemu nyingine na akutupwa hapo.Tunaendelea na uchunguzi kuwasaka watu aliokuwa nao casino kwa mara ya mwisho,” alisema Kamanda Fuime aliyefafanua kuwa mwili huo ulipelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Neema kwa wamiliki wa vyombo vya habari hasa magazeti

$
0
0
Ile sheria kandamizi inayolalamikiwa na wamiliki wa vyombo vya habari, inayompa mamalaka waziri wa habari, tamaduni na michezo ya kukifungia chombo chochote bila hata ya kwenda mahakamani, ipo mbioni kuondolewa.

Akiongea na waandishi wa habari mkoani kigoma waziri nape amesema serikali inataraji kuunda bodi ambayo itakuwa na uwezo wa kumhukumu mwandishi aliyekiuka taratibu za kiuandishi.....na hakutakuwa tena naaamuzi ya kuadhibu gazeti au chombo cha habari zima/kizima.

Source: Azam news

Je, Kuna umuhimu wa kuwa na mbio za mwenge kwa sasa?

$
0
0
Ndugu wadau,

Naomba kwa kina tujaribu kuliangalia suala la Mwenge kuendelea kuzunguuka nchi nzima huku zikitumika mamilioni ya fedha.

Je faida ya Mwenge kwa sasa ni nini? Vinginevyo ni vema fedha zinazotumika zikaelekezwa kwenye shughuli za kijamii kama kununua madawati madawa kujenga vyoo n.k.

Tanzia: Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Iringa, Sinkala, Apata Ajali na Kufariki

$
0
0
Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Iringa, Sinkala Mwenda amepata ajali jioni ya leo eneo la Tanangozi.

Amekimbizwa hospitali lakini kafariki dunia usiku huu.

Rais wa Zanzibar Afunguka.....Yanayosemwa Kuhusu Mimi Hayanikoseshi Usingizi

$
0
0
Rais wa Serikali ya Mapinduzi wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein amesema kuwa kwa mujibu wa Katiba hakuna chama kilichokidhi masharti ya kuunda serikali ya Umoja wa kitaifa hivyo serikali ya visiwa hivyo itakua ni ya chama cha Mapinduzi.

Akizungumza katika Uzinduzi wa Baraza la tisa la Wawakilishi la Zanzibar Rais Dkt. Shein amesema kwa mujibu wa Katiba aliamua kumteua balozi Seif Ali Idd kuwa makamu wa pili wa rais ili kuunda serikali visiwani humo kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo.

Dkt. Shein amewahakikishia wajumbe wa baraza la wawakilishi kuwa serikali atakayoiunda itasimamia misingi ya haki, uwajibikaji,haki, uwazi na usawa wa wananchi wote bila kujali itikadi zao.

Aidha Dkt. Shein amesema kuwa katika kipindi atakachokaa madarakani ataendelea kuulinda Muungano wa serikali mbili wa Tanganyika na Zanzibar uliasisiwa tangu mwaka 1964.
Dkt. Shein ameongeza kuwa atahikikisha serikali hizo mbili zinafanya kazi kwa umoja na ukaribu zaidi katika kupanga na kutekeleza mikakati ya kiuchumi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote.

Aidha amesema kuwa kwa kushirikiana na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema watadumisha Umoja na amani iliyopo visiwani humo huku akikisitiza kuwa maneno yanayotolewa na wapinzani hayamnyimi usingizi.

Sakata la Kijana Aliyefufuka Baada ya Kufa Lachukua Sura Mpya

$
0
0
Hatimaye Sakata la Uvumi na madai ya kijana,Nyabongo Manosa,ambaye inadaiwa alikufa kwa Malaria mwaka 2013 na kuzikwa na baadaye kudaiwa kuonekana hai katika kijiji cha Iroganzala,Wilayani Mbogwe Mkoani Geita mwaka 2015 limechukua sura mpya.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga Mponjoli Rotson,
Kwa Mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Rotson amesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya Polisi kwa kushirikiana na mamlaka zingine ikiwemo ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serkali kuazisha na uchunguzi wa kisayansi ili kubaini ukweli juu ya marehemu anaedaiwa kuzikwa na kufufuka.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga Mponjoli Rotson, amesema Uchunguzi huo unafanyika kupitia jalada la uchuguzi Namba MB/IR/867/2015 liliofunguliwa kuchunguza tuhuma za vitendo vya ushirikina ambapo Uchunguzi utahusisha pia Vinasaba vya DNA.

Aidha katika kesi hiyo Polisi inamtafuta Bw. Emanuel Mutabo[ 42]anayehusishwa na tukio hilo anatafutwa baada ya kutoweka kusikojulikana toka Septemba 14 mwaka 2015 toka nyumba yake iliyolindwa na Polisi kutovunjwa na wananchi.

Kamanda Rodson amesema Nyabongo Manosa [19]alionekana 14 Septemba 2015 katika hali inayohusishwa na mazingira ya kishirikina maarufu kama MSUKULE ikiwa na maana ya mtu anayedaiwa kufariki na kisha kufufuliwa kwa ajili yakutumikishwa katika kazi za shambani na nyumbani.

Kamanda Rotson amesema Baada ya tukio hilo mtu mmoja aliejulikana kwa jina la Manosa Benjamini, mkazi wa kijiji cha Shinyanga A katika kata ya Nyakafuru wilayani Mbogwe alijitokeza akiwa na mkewe na kudai kuwa marehemu aliedaiwa kufufuka alikuwa mtoto wao aliyefariki kwa Maralia june 7 na kuzikwa june 8, 2013 katika kijiji cha Mpunze wilayani Meatu.
Mkuu huyo wa polisi amesema kuwa Bw. Manosa Benjamin, alikabidhiwa kijana huyo kupitia Ofisi ya Ustawi wa jamii wilaya ya Mbogwe, ili kuishi naye wakati uchunguzi wa kina ukiendelea kwani hapakuwepo na uthibitisho wowote wa kisayansi uliofanyika hatua ambayo imeendelea kuibua Uvumi na hofu ndani ya jamii.

Kukamilika kwa uchunguzi huo unaotarajiwa kukamilika ndani ya wiki mbili kutoka sasa kutahitimisha hofu na Uvumi wa tukio hilo ambalo kila kunapokucha limekuwa likiibua hisia tofauti ndani ya jamii bila kupata majibu ya kiuhalisia.

Mwanamke Uliyeolewa Jua Kuitumia Smartphone yako Vizuri..Lasivyo Itakuponzam Uachike.....

$
0
0
Mwanamke aliyeolewa ni msaidizi wa mume wake, kuhakikisha amempikia mumewe,amemfulia, na mumewe akitoka kazini akili zake zote ziwe kwake, amuhudumie kwa kila kitu akisimama katika nafasi yake kama mwanamke aliyeolewa. Pia mwanamke aliyeolewa ni nguzo ya familia yampasa kuwa mtu anayemwomba Mungu kwa Imani yake kila wakati na pia kuwalea watoto vizuri na kuhakikisha usalama wao,

Siku hizi smartphone zinatuponzaa wanawake, kila saa tuko mitandaoni, mara kutafuta umbea, mara kuupload picha zisizo na mantiki et umepita kwa mangi umenunua kachips umepiga picha chaap umepost, mara kuandika status za vijembe watsapp, mara kutukana kwenye mitandao,
mwanamke umeolewa una account 20 insta,magroup yasiyo na maana ndo usiseme, mume karudi kazini wewe huna habari umetundika miguu uko busy na simu housegirl ndo amuhudumie mumeo chakula, we unafanya kuagiza tu nipe hichi mnawishe baba mikono kweli jamani?, smtms hadi unapika chakula kinaungua kisa ukobusy na simu.

Mara umepigiwa simu na mwanaume gani sijui anaongea upuuzi wewe ni kuchekacheka tu .Shost anakupigia simu nusu saa mnaongea tu upuuzi,hadi mwanaume anaboreka akikusubiria umalize kuongea aseme nawe jambo.

watoto wala huna habari nao hujui kwamba wamekula,hujui yupi ana homa, ni housegirl ndo anakuja kukuambia mama, Debora joto lake leo liko juu.mama mtu hujui kama joto la mtoto liko juu ila unajua picha ya mwisho leo wema sepetu kaweka insta kweli???? Halafu unajiita umeolewa wakati hujui majukumu yako kama mke??.

Aisee Wanawake mlioolewa badilikeni, simaanishi kwamba msitumie smartphone ila muwe na kiasi, hii ya mke wa mtu kiiila saa uko mitandaoni pasipo na sababu ya msingi acheni,waachieni single Girls.

Ndoto za Mourinho Kwenda Man U, Zaanza Kuyeyuka!

$
0
0
ALIYEKUWA kocha wa Chelsea kabla ya kutimuliwa, Jose Mourinho amekuwa akihusishwa kuhamia klabu ya Manchester United msimu ujao huku taarifa za wazi zikisema kuwa tayari ameshasaini mkataba wa awali wa kukinoa kikosi hicho cha Mashetani Wekundu.
Ripoti kutoka kwenye redio ya Cadena Cope ya nchini Hispania zinasema kuwa kandarasi ya Mreno huyo kuhamia Man U imeleta sintofahamu baada ya wamiliki wa klabu hiyo (Familia ya Glazer) kumgomea kujiunga na Man U.

Kocha huyo mahiri duniani mwenye umri wa miaka 52 amekuwa na matumaini makubwa ya kuinoa Man U msimu ujao ili kumrithi Louis van Gaal anayeonekana kushindwa kuimudu klabu hiyo na kufikia malengo yake.


Mourinho aliyewahi kuifundisha Real Madrid alitimuliwa Chelsea mwanzoni mwa msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza na nafasi yake kuchukuliwa na Guus Hiddink kwa muda kabla ya jana kumteua rasmi Antonio Conte kuwa kocha wao Mkuu.

Kwa upande wake Mwenyekiti Msaidizi wa Man United, Ed Woodward amesema, Van Gaal anamkataba wa miaka mitatu klabuni hapo, lakini wapo tayari kumpa muda wa miaka miwili tu kuendelea kuinoa klabu hiyo na endapo atashindwa kuisaidia kunyakuwa Kombe la Mabingwa (Champions League) basi atalazimika kuondoka klabuni hapo.
Japo ndani ya Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Manchester United kutofautiana mitazamo kuhusu nani ainoe klabu yao msimu ujao, Ed Woodward ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho iwapo ni Mourinho au Van Gaal kuinoa hiyo msimu ujao.

Rais Magufuli Kusafiri nje ya nchi Kwa Mara ya Kwanza leo, Anaondoka na Gari sio Ndege

$
0
0
Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli, April 5 2016 jina lake limerudi kwenye headlines kwa mara nyingine tena. Rais Magufuli amerudi kwenye headlines baada ya kukubali mwaliko wa Rais Paul Kagame wa Rwanda, hivyo atafanya ziara ya siku mbili Jumatano na Alhamisi.

Stori kutoka wizara ya mambo ya nje zinaeleza kuwa Rais Magufuli pamoja na Rais Kagame watafungua daraja la kimataifa la Rusumo linaounganisha mpaka wa Tanzania na Rwanda na kuzindua ushirikiano wa huduma za kituo cha pamoja.Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari na kusomwa katika television za Tanzania Rais Magufuli atasafiri kwa gari.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images