Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Malinzi Hana Nafasi ya Kulikwepa hili la Upangaji Matokeo, Lazima Ajiuzulu – Mchambuzi

$
0
0
Sauti za viongozi wawili wa juu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zimesikika wakijadili namna ambavyo wanaweza kuisaidia timu moja kupata ushindi.

Viongozi hao, wanaeleza wanavyotaka kitita cha fedha, Sh milioni 10, walipwe viongozi wengine, Sh milioni 10, nyingine kwa ajili ya moja ya kamati za TFF na baada ya hapo Sh milioni 5, ambayo atapewa ofisa mwingine wa shirikisho hilo ili aende kuzungumza na wakubwa wa Idara ya Uhamiaji ambako inatakiwa kumkandamiza mchezaji wa timu fulani ili nyingine ipate ushindi.

Siku moja tu baada ya sauti hizo kusikika, Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Martin Chacha akatangaza kuachia ngazi, huku akisema ni kutokana na kubanwa na matatizo ya kifamilia.

Gazeti hili likafanya mahojiano na Juma Matandika, kutaka kujua vipi alishiriki kwenye kikao hicho, akasisitiza anaamini sauti zao zimeigizwa kwa kuwa na watu wengi wana uwezo wa kuigiza huku akimtaka mwandishi kama naye anataka sauti yake iigizwe, basi aende ili ampeleke.

Tuliacha hilo, tuamini kabisa Rais wa TFF, Jamal Malinzi, hawezi kuhusika na kitu kama hiki na waliokwenda kutenda jambo hilo walifanya bila ya kumueleza kwamba wana ujanja wanaofanya. Lakini najiuliza, yeye atalikwepa vipi?

Wote tunajua suala hili linahusiana na rushwa, adui wa haki, adui wa mpira wa Tanzania na adui wa nchi yetu, lakini naona kuna ujanja unafanyika kuona hili linaonekana limetengenezwa.

Najua lazima Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) haitaliacha lipite hivihivi na hasa ukizingatia serikali ya sasa ni ile inayotaka mambo yaende kwa haki na uamuzi wake ni haraka, si kama ilivyokuwa katika awamu nyingine zilizopita za uongozi.

Nimeanza kuona harufu ya njama zinazoanza kutengenezwa kutaka kulifanya jambo hili lionekane ni bahati mbaya au halikuwahi kabisa kutokea.

Kuna mipango inatengenezwa ili ionekane kwamba waliosikika sauti zao zimetengenezwa na kuna lengo la kuwadhalilisha. Lakini naona hata TFF yenyewe inataka kuingia mkenge kutaka kuanza kuzuia vyombo vya habari kuliripoti jambo hili, niwahakikishie mtafeli.

Huenda ni njia ya kutaka kutulazimisha kwa ulaini kuamini maelezo ya Matandika? Kwamba sauti zao zimetengenezwa? Jamani, uoneeni huruma mpira wa Tanzania nanyi muwe na aibu kiungwana!

Niliona taarifa yao waliyoitoa TFF siku moja baada ya sakata hilo, wakisisitiza kwamba wanaonya viongozi wa juu wa shirikisho hilo kuhusishwa na sakata hilo.

Kwangu ninaona ni kuingilia uhuru wa vyombo vya habari, kwangu naona ni kulazimisha kuwafumba midomo waandishi wa habari kwa lengo la kufunika maovu kwa nguvu, jambo ambalo haliwezi kuvumilika wala halitakuwa na nafasi kwangu.

Sauti zinazosikika, zinajulikana ni za kina nani. Wanaozungumza ndiyo viongozi wa ngazi za juu. Sasa unashindwa vipi kuwahusisha na viongozi wa ngazi za juu?

Viongozi wa ngazi za juu wanakwenda vipi katika hili na wengineo wametajwa ndani yake. Hata kama waliotaja ingekuwa hatuwajui, basi isingekuwa rahisi kuruka maneno waliyosema hasa yale waliotaja viongozi wa juu wa TFF.

Ninachomshauri Rais wa TFF, Jamal Malinzi ni kujiandaa. Kuwa tayari, kukaa mguu sawa kama itathibitika wahusika walichofanya kupitia vyombo vya dola, basi yeye ajivue madaraka kwa kuwa atakuwa amechafuliwa na aliowaamini.

Tulilalama kuhusu tuhuma za rushwa kwenye soka, sasa tuhuma ziko ndani ya shirikisho, waliopewa dhamana ya kuuendesha mpira, nini maana yao wao kuwepo? Kwani waliojiuzulu wote ni wale waliopatikana na hatia tu, kuhofiwa ni kuondolewa kwenye uadilifu tena kwa njia kama hiyo ya sauti.

Hii ndiyo kashfa kubwa zaidi kutokea katika shirikisho hilo tokea kuanzishwa kwake. Nakumbuka kiongozi wa Chama cha Soka Tanzania (Fat), alifungwa jela. Lakini TFF haikuwa imewahi kuchafuka kwa kiwango hiki.

Tena inachafuka kipindi ikiwa imetoka kutoa adhabu kupitia moja ya kamati zake ambayo iliwafungia wachezaji, waamuzi na viongozi kwa madai ya kupanga matokeo. Haki iko wapi sasa?

Badala ya kupambana kuizima, kwa kutaka kuwaziba watu midomo kwa nguvu. Huu ni wakati wenu wa kutafakari na kutengeneza mwisho wa kuongoza kwa matamanio ya maendeleo ya nafsi zenu na kuwaacha wenye nafasi ya kuongoza kwa lengo la kuleta maendeleo kwenye mpira wa Tanzania. Leo nimeanza, kesho nitarudi tena, nina mengi ya kusema.

Imeandikwa na Saleh Ally

Source: salehjembe.blogspot

Jeshi La Polisi Kanda Maalum Ya Dar Es Salaam Limefanikiwa Kuwakamata Watu 63 Wanaodhaniwa Kuwa Majambazi

$
0
0
Jeshi  la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata watu 63 wanaodhaniwa kuwa  majambazi wa kutumia silaha katika operesheni endelevu ya kuwasaka majambazi wanaofanya matukio mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Kamishna wa Polisi kanda maalumu Simon Sirro aamesema, miongoni mwa majambazi waliokamatwa ni Ibrahim Juma(31) mkazi wa Kiwalani Kigilagila, Samweli Mbonea (40) Fundi gereji Mkazi wa Kiwalani pamoja na Anthony Kanywenywe (60) Mwindaji na mkazi wa Kiwalani.

Amesema majambazi hao walikutwa na taa kubwa nne za magari, pawa windo moja na nati za magari na watuhumiwa sita  kati ya waliokamatwa wamekiri kushiriki katika matukio ya unyanganyi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali likiwemo la Riki Hill Hotel katikati ya jiji na Lake oil Buguruni.

Katika tukio jingine  kikosi maalumu cha kupambana na majambazi kimefanikiwa kukamata silaha sita  aina ya SMG  moja ,Short gun pump action tatu na Rifle mbili katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.

Amesema silaha aina ya SMG iliyokatwa kitako ilipatikana baada ya askari kuwafyatulia risasi majambazi hao waliokuwa eneo la vingunguti ndipo walipoitupa silaha hiyo ikiwa kwenye mfuko mweusi wa plastiki na wao kukimbia katika bonde la Mto Msimbazi.

“Tunaendelea kuwatafuta watuhumiwa hao na upelelezi unaendelea ili kubaini mmiliki halali wa silaha hiyo. Hatupotayari kuendelea kuona maovu yakiendelea kufanyika, jeshi lipo imara na tutapambana nao,” alisema Sirro.

Ameongeza kuwa jeshi hilo pia lilifanikiwa kukamata silaha Rifle mbili katika eneo la Masaki ambazo zilikuwa zimefichwa na kufunikwa kwa taulo zikiwa na maandishi ya Collessium Fitness Club  moja ikiwa na namba A 6777013 iliyosajiliwa nchini kwa namba TZCAR 58596, na nyingine ikiwa na namba L 691848176 iliyosajiliwa kwa namba TZCAR 75062.

Wakati huo huo Jeshi la Polisi Kanda maalum Dar es salaam limefanikiwa kukamata jumla ya risasi 15 za silaha ndogo aina ya bastola zikiwa kwenye magazine.

Risasi hizo alikutwa nazo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mamboleo Willium (41) Mfanyabiashara mkazi wa Mikocheni.

Katika mahojiano mtuhumiwa huyo alikiri kuwa na risasi hizo kinyume na sheria na kushindwa kueleza mahali alipozipata, mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa  na uchunguzi unaendelea kufanyika

Singida Washukuru kuwa wa Kwanza Mgawo wa Milioni 50/- za Magufuli

$
0
0
Mbunge  wa Viti Maalumu, Aysharose Matembe (CCM), amesema vijana na wanawake mkoani Singida, wameishukuru Serikali kwa kuchagua mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa 10 ya kwanza itakayonufaika na mgawo wa Sh milioni 50 kila kijiji na kila mtaa.

Matembe amesema wako tayari kuzitumia kwa uangalifu fedha hizo kwa kuhakikisha wanaunda vikundi vyenye malengo madhubuti ya kujenga ili wajikwamue kiuchumi.

Mbunge huyo jana alisema Singida ni miongoni mwa mikoa yenye rasilimali nyingi, ikiwemo ardhi yenye rutuba ambayo kwa kiasi kikubwa wananchi wanaitumia kujishughulisha na kilimo cha mazao mbalimbali yanayochangia kukua kwa pato la Taifa.

Alisema amezungumza na wananchi hao ambapo walikiri fedha hizo kuwa na mchango chanya kwa maendeleo ya mkoa na kaya zao, hivyo kila mtendaji atakayehusika kwa namna moja au nyingine na fedha hizo, anapaswa kuwa mwadilifu ili ziwafikie walengwa kwa wakati.

“Kutolewa kwa hizi fedha ni kama kupatikana kwa maji jangwani kwa vijana na wanawake wa Singida, kwa nyakati tofauti nimezungumza nao na wananipa salamu kuishukuru Serikali kwa kuwatambua na kuieleza kwamba wamejipanga kunufaika nazo.

CAG Aikana Ripoti Feki ya NSSF Asema Ripoti itatolewa na Bunge April 25

$
0
0
OFISI ya Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imekana taarifa inayosambazwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya jamii kuonyesha kuna ufisadi mkubwa kwenye miradi mbalimbali ya Shirika la Taifa la Hifadhi za Jamii (NSSF).

Taarifa ya kuaminika iliyopatikana ndani ya ofisi hiyo na mmoja wa viongozi wa ofisi hiyo, wameeleza kuwa taarifa kamili kuhusiana na NSSF itatolewa na bunge April 25, mwaka huu na wanashangazwa na mambo yanayoenezwa kwenye vyombo vya habari.

Kiongozi huyo mwandamizi huku akikataa kutajwa jina lake alisema hata magazeti hayo yanayoandika uvumi huo, hakuna hata moja linaloeleza kwa ufasaha kuhusiana na ripoti ya CAG.
Ilisema watanzania wanapaswa kutulia na kusubiri taarifa rasmi itakayopelekwa bungeni, kwa kuwa imeeleza kila kitu na sio hicho ambacho kinaonekana kama kinakolezwa na watu wenye maslahi nayo.
"Hata sisi tunashangazwa kumekuwa na msukumo mkubwa na hatujui dhamira yake ni nini, ila tunachoamini tusubiri tu taarifa rasmi ya ripoti itakayopelekwa bungeni,''alisema mtoa taarifa wetu.
Akizungumza na Wabunge wajumbe wa Kamati za Bunge za usimamizi wa fedha, LAAC na PAC, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Mussa Assad kwenye semina ya mafunzo aliwaeleza wabunge kuwa Ripoti ya CAG anayo yeye na Rais Magufuli tu na anashangazwa na wanaosambaza kinachoitwa taarifa ya CAG wanapata wapi nguvu ya kufanya hivyo.

Profesa Assad alikuwa anajibu maswali ya wabunge ambapo mmoja wa Wabunge kutoka Kambi ya Upinzani alitaka maelezo ya CAG kuhusu kinachoitwa ufisadi katika NSSF.

“taratibu za ukaguzi zinajulikana. Baada ya mkaguzi kuandaa taarifa ya awali hutoa kwa mkaguliwa kujibu hoja za ukaguzi. Kisha Mkaguzi huweza kuziondoa hoja zenye majibu aliyoridhika nayo na baada ya hapo huitwa kikao kinachoitwa ‘exit meeting’ na kukubaliana masuala ya ukaguzi”, alifafanua.

Profesa Assad kwa wabunge wajumbe wa PAC,LAAC na Kamati ya Bajeti. Aliwaeleza wabunge kuwa inawezekana kinachosambazwa ni taarifa ya awali kwa malengo mahususi ambayo yeye kama CAG hawezi kuyajua na kuwataka wabunge wasubiri taarifa yake rasmi itakayowasilishwa Bungeni kabla ya tarehe 25 Aprili 2016.

Kumekuwepo na taarifa mbalimbali, ambazo nyingi zinaonekana zinamtuhumu aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau aliyeliendesha shirika hilo kwa mafanikio makubwa kuhusishwa na vitendo vya ufisadi wa miradi mbalimbali.

Baadhi ya wachunguzi wa mambo wanasema nguvu inayosukumwa kuichafua NSSF ina lengo la kufifisha nyota ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo kabla ya uzinduzi wa daraja la Kigamboni mnamo tarehe 16 Aprili 2016.

Wachina Kizimbani Kwa Kukwepa Kulipa Kodi

$
0
0
Raia wawili wa China, Ma Jun na Huifang Ma leo wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashtaka mawili likiwamo la kushindwa kutumia  Mashine ya Kodi za Kielektroniki (EFDs) katika biashara zao.

Jun na Ma, ambao wote ni  wafanyabiashara na wakazi wa Mtaa wa Narung’ombe eneo la Kariakoo wanakabiliwa na kushindwa kutumia mashine za EFDs pamoja na kushindwa kujisajili katika kodi ya ongezeko la Thamani(Vat) wakati wakijua kufanya hivyo kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Hata hivyo, mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Jun hakuwepo mahakamani hapo kwa madai kuwa yupo nje ya nchi na upande wa mashtaka umeiomba Mahakama kutoa hati kwa ajili ya kumkamata mshtakiwa huyo.

Akisoma hati ya mashtaka, mbele ya Hakimu Mkazi Mwanadamizi Mfawidhi wa mahakama hiyo Said Mkasiwa, Wakili kutoka Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Cherubin Chuwa alidai kuwa washtakiwa kwa pamoja walitenda  makossa hayo Machi 23,mwaka huu.

Chuwa alidai siku hiyo ya tukio, washtakiwa hao ambao wanamiliki Kampuni ya HM Textile  Co Ltd  Iliyopo  block 54 katika kiwanja namba 6 kilichopo mtaa wa Agrey  eneo la Kariakoo, walishindwa kutumia  mashine za EFDs kwa ajili ya kutoa risiti kwa wateja wao ambao walikuwa wanafanya manunuzi mbalimbali katika duka hilo ambalo linauza mapazia na nguo mbalimbali, huku wakijua kuwa ni kosa kisheria.

Mwandesha Mashtaka huyo aliendelea kudai kuwa, katika shitaka la pili ambalo pia linawakabili washtakiwa wote, inadaiwa kuwa muda na siku hiyo  hiyo katika duka hilo, washtakiwa walishindwa kujisajili katika kodi ya ongezeko la Thamani(Vat) wakati wakijua kufanya hivyo kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Chuwa alidai washtakiwa hao walishindwa kujisajili katika Kodi ya Ongezeko la Thamani(Vat) ambayo ni kinyume cha sheria , na kwamba mashtaka hayo yamefunguliwa kupitia sheria za TRA.

Hata hivyo mshtakiwa wa  pili, Huifang  alikiri shtaka la kwanza huku shtaka la pili akikana kuhusika.

Kutokana na hatua hiyo wakili Chuwa alisema dhamana ya mshtakiwa huyo iko wazi ambayo ni kuwa na wadhamini wawili kila kutoka taasisi inayotambuliwa kisheria watasaini bondi ya Sh 3milioni na kuwasilisha mahakamani hati yake ya kusafiria.

Mshtakiwa huyo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi April 21, mwaka huu.

Waziri Muhongo Apiga Marufuku Wafanyakazi wa Wizara yake Kupewa Bonus

$
0
0
Waziri wa Nishati amekataa wafanyakazi wa wizara yake kupewa bonus akitolea mfano TANESCO hutoa bonus ya kati ya sh milioni 1 hadi milion 50 kwa mtu mmoja. Sasa kama gharama za nguzo moja ni sh laki 3 hivo hela hizo zitatumika kwenye nguzo nyingi sana.

Chanzo: TBC

Mbwana Samatta Afanya Mambo Tena Genk Usiku wa Jana....Tazama Hapa Video ya Goli Alilofunga

Mrema wa TLP Amuomba Rais Magufuli Atimize Ahadi yake ya Kumpa KAZI Kama Alivyokuwa Amemwahidi Wakati wa Kampeni

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) taifa, Augustine Mrema amemuunga mkono Rais John Mgufuli kwa kasi yake ya kupambana na ufisadi na kumuomba ampe kazi ili amsaidie kutekeleza jukumu hilo.

Mrema alimuomba Rais Magufuli atambue uzoefu wake kwa kukumbuka jinsi alivyopambana na mafisadi wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu.

Huku akieleza CV yake hiyo, Mrema alimkumbusha Rais kuhusu ahadi aliyompa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana, ya kumpa kazi katika Serikali ya Awamu ya Tano ikiwa atashinda na kuwa Rais.

Akizungumza na waandishi wa habari kijijini kwake Kiraracha mkoani Kilimanjaro, Mrema alisema kuwa anasikitishwa na ukimya wa Rais Magufuli kwa sababu aliamini kuwa angetekeleza ahadi hiyo ya kumpa kazi muda mfupi baada ya kutangaza Baraza la Mawaziri, jambo ambalo hadi sasa hajalifanya.

Alisema, alikutana na Rais Magufuli mwaka jana katika kampeni jimboni Vunjo kwenye eneo la Njia Panda lililopo ndani ya mji mdogo wa Himo na kuambatana naye kwenye mkutano wa hadhara, ambapo alimwombea kura kwa wafuasi wake na kuahidiwa ajira.

“Katika kampeni, Dk Magufuli alifika kwenye mkutano wangu nikamwombea kura kwa kuwaambia watu wangu wamchague kwa kuwa ni mchapakazi na mwadilifu. Aliahidi kunipatia kazi katika Serikali na sasa namkumbusha na kumuuliza mbona yupo kimya?” Mrema alieleza na kuhoji.

Alipoulizwa ni kazi gani inayomfaa katika Serikali ya Magufuli, alisema yeye alishawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu hivyo yuko tayari kufanya kazi yoyote itakayomfaa ila alitamani zaidi kupangwa sehemu nyeti ili amsaidie kutumbua majipu.

Mrema alimpongeza Rais Magufuli kwa jitihada binafsi za kutumbua majipu anazozifanya na alijigamba kuwa yeye ndio mwenye uzoefu wa kupambana na mafisadi kutokana na rekodi yake nzuri ya kipindi cha Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.

Katika hatua nyingine, Mrema alikanusha taarifa ya kuhongwa fedha ili kufuta kesi ya kupinga matokeo aliyoifungua dhidi ya Mbunge wa jimbo hilo, James Mbatia.

Alisema, taarifa hizo ni za kupuuzwa kwa sababu zinalenga kumpaka matope kwa wananchi wake wa Vunjo.

Mrema alieleza kuwa walifikia maridhiano ya pamoja kuhusu kuondoa kesi hiyo mahakamani na kwamba, hilo lilifanywa kwa kuzingatia maslahi ya wananchi.

Pamoja na hayo, alikiri kumlipa Mbatia Sh mil 40 ikiwa ni sehemu ya kupunguza gharama alizotumia katika kesi hiyo, ikiwemo malipo ya mawakili wake.


Download Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

$
0
0

Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 

Au Bonyeza hii picha hapa chini

Tendo la Ndoa Hudumu Kwa Muda Gani? Wanasayansi Wana Jibu Hili

$
0
0
Ni muda gani tendo la ndoa (ama nalisema kiheshima sana?) Au niseme ni muda gani watu wanaofanya mapenzi hutumia kumaliza?

Na sasa wanasayansi wamekuja na jibu halisi kuwa kitendo cha ngono hudumu kwa dakika 5.4. Wanasayansi hawa wanazungumzia ule muda ambao mwanaume na mwanamke huwa tendoni na kufikia kileleni, bila kuweka muda wanaotumia kushikana, kubusiana au kuchezeana.

Wanasayansi hao walifanya utafiti kwa couple 500 na kuwaweka stop watch pale tu kitendo kinapoanza hadi pale mwanaume anapoutua mzigo. Utafiti huo ulibaini kuwa kitendo hicho hudumu popote kuanzia sekunde 33 na 44 huku muda wa wastani ukiwa dakika 5.4.

KR Mullah Ajibu Tuhuma Na Sir Nature Kuhusu TID na Matumizi ya Madawa ya Kulevya

$
0
0
Mwanamuziki KR Mullah amefunguka baada ya msanii mwenzake wa kundi la Wanaume Halisi Juma Nature, kusema kitendo cha KR kujiunga na Radar Entertainment, huenda kitamuharibu asipokuwa makini.

KR Mullah, amemtaka Juma Nature amuache kwa sasa afanye kazi, kwani kwa sasa anataka kubadilisha ladha ya muziki wake na huenda hajapendezwa na yeye kuingia Radar Entertainment na kuachana na Wanaume Halisi.
“Nilikuwepo ndani ya kundi la wanaume halisi, sasa labda anavyoona mimi nipo huku anaona kazi zake tena zitakuwa zinalegalega, pengine labda hakupendezewa mimi kwenda kufanya kazi na yule mtu na kwamba yeye alitegemea mi nifanye kazi naye,” alisema

Sambamba na hilo KR, amemuongelea TID ambaye Juma Nature alimtahadharisha kuwa makini nao wasije wakamuingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kuwa  hajawahi kumuona kutumia vitu hivyo.

“Kusema kweli zamani nilikuwa nasikia sikia hizi taarifa, lakini yeye mwenyewe alitangaza kuacha muda mrefu, lakini kwa sasa tangu nimeanza kukaa naye sijawahi kumuona akiitumia au akifanya hayo mambo, muda mwingi tunapiga stori za kikazi zaidi” alisema KR Mullah

Ukweli Kuhusu Kipini Cha Diamond Huu Hapa...Maneja wake Afunguka Ukweli....

$
0
0
Kwa masaa kadhaa picha ya Diamond Plutnumz akiwa na kipini puani, imekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii na kuwaacha mashabiki wake njia panda.

Mashabiki wengi walionekana kumkosoa kwa uamuzi wake wa kubandika kipini puani huku wengine wakionekana kuwa waelewa wa kile alichokifanya.

Swali ambalo linazunguka kwenye vichwa vya mashabiki na wapenzi wengi wa muziki je, ni kweli Chibu katoga pua yake?

Meneja wake Sallam, aliamua kutegua kitendawili hicho na kaamua kuandika kwenye mtandao wa kijamii, akisema msanii wake huyo aliamua tu kuwashtua watu si kweli kwamba ametoboa pua.
“Usiamini kila unachoona kwenye picha au unachoambiwa, mlikuwa mmelala sana amewaamsha kidogo,” aliandika Sallam

Ridhiwani Kikwete Akana Taarifa Kuwa Yeye ni Mmoja wa Wamiliki wa Kampuni ya Lugumi...Inayotuhumiwa Kwa Ufisadi Mkubwa Jeshi la Polisi

$
0
0
MBUNGE wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amekanusha taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari kuwa yeye ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Lugumi, inayodaiwa kupewa zabuni ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole kwenye vituo vya Polisi.

Ridhiwani ametajwa katika habari hizo kuwa ni mmiliki wa kampuni ya Lugumi pamoja na wamiliki wengine ambao ni Said Lugumi na aliyekuwa mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema.

Akizungumza na gazeti hili, Ridhiwani ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete alisema yeye hahusiki na kampuni yoyote ya Lugumi ingawa wana urafiki wa kawaida na mmiliki wa kampuni hiyo.

“Kwanza kabisa mimi si mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo, hilo ni jambo la msingi kabisa watu waelewe na sijawahi kufanya biashara yoyote na Lugumi. Said Lugumi ambaye ni mmiliki wa kampuni hiyo tunafahamiana naye na ni rafiki yangu,” alisema Ridhiwani.

Ridhiwani alisisitiza kuwa hana uhusiano wa kibiashara na mtu huyo na kwamba hafahamu ni kwa nini amehusishwa na kampuni ya Lugumi.

“Hapa ni watu tu wanaamua kuingiza tu maneno yao, haya maghorofa ninayotajwa kumiliki Dar es Salaam hata sijawahi kutembelea ujenzi wake, wameamua kuniingiza, Lugumi nafahamiana naye binafsi tu lakini wananiingiza,” alisema Ridhiwani.

Alisema jambo hilo bado liko ndani ya Kamati ya Bunge na baadae ameliona kwenye magazeti ya juzi kuwa Jeshi la Polisi litatoa taarifa yao, hivyo asingependa kulizungumzia kwa undani. Hivi karibuni Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilitoa siku saba kwa Jeshi la Polisi nchini kupeleka mkataba walioingia baina yao na Kampuni ya Lugumi.

Kamati hiyo ilipokutana na Jeshi hilo kupitia taarifa ya hesabu zao za mwaka 2013/14 zilizokaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Aeshi Hilaly alisema jeshi hilo

mwaka 2011 liliingia mkataba na kampuni hiyo kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya Polisi vya wilaya nchi nzima ambavyo viko 108.

Alisema mkataba huo ulikuwa wa Sh bilioni 37 pamoja na kodi na kwamba hadi sasa kampuni hiyo imeshapewa asilimia 99 ya fedha zote ili hali vituo vilivyofungwa mashine hizo ni 14 tu, kati ya vituo vyote 108.

Ridhiwani alisema angependa jamii ifahamu kuwa hana uhusiano na kampuni hiyo kwa kuwa hafahamu kabisa hata malipo yaliyofanywa kati ya Serikali na kampuni ya Lugumi anasikia tu kama ambavyo watu wengine wamesikia.

Chanzo: Habarileo

Lowassa Afunguka na Kumkosoa Rais Magufuli Tena

$
0
0

Hali ya siasa nchini ni ya hamasa, lakini isiyokuwa na misingi endelevu.
Kwa kuwa Rais amekuwa akigawa fedha wakati chombo cha kufanya hivyo kipo ambacho ni bunge.
Pia nasononeshwa ninapoona watu wanaachishwa kazi na mashirika mbalimbali kwasababu ya hali ngumu ya uendeshaji wa mashirika hayo.

Bandari sasa hivi nasikia uingizaji mizigo umeshuka kwa asilimia 50, kampuni nyingi za mizigo zimefunga shughuli zake na pale palikua na vijana wetu wengi wameajiriwa,sasa hivi wako mtaani hakuna mbadala wa ajira, hii inasababisha hali ya maisha ya wananchi yanakua magumu.

Kuhusu swala la MCC ni pigo kwa mustakabali wa uchumi, kutaka nchi ya viwanda kunahitaji uwekezaji mkubwa,katika hili fedha tutatoa wapi kama sio wafadhili wa ndani na nje kufanikisha?
Hawa wafadhili sio watu wa kuwabeza kwakuwa tunafanya nao miradi mingi ya kimaendeleo na wanavyotoka hivi itaturudisha nyuma, Tunahitaji kujitegemea, ndiyo, ila kwa mipango huku tunatafuta mbadala wa kila msaada.

Hapa kinachotakiwa ni kufanya mabadiliko katika mfumo na kuufanya kuwa endelevu.

Maalim Seif Sharrif Hamad Kutoa Mwelekeo Wake Kisiasa Kesho

$
0
0

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad kesho ataelezea mwelekeo wake kisiasa, ikiwamo kufafanua kiundani uamuzi wa chama hicho kususia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu.


Mgombea huyo wa urais Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana ataeleza mambo hayo ikiwa imepita takribani wiki moja tangu Baraza Kuu la chama hicho kutoa msimamo wake wa kutomtambua Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein pamoja na wawakilishi na madiwani.


CUF kilisusia kushiriki uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu baada ya Oktoba 28 mwaka jana, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya urais, uwakilishi na udiwani, akisema kulikuwapo na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi.


Habari kutoka ndani ya chama hicho zinaarifu kuwa mkutano wa kiongozi huyo utakuwa wa kwanza kwake, tangu kumalizika kwa uchaguzi wa marudio na ataeleza mambo muhimu yatakayotoa picha halisi ya mwelekeo wake na CUF.


“Katika mkutano uliopita tamko lilikuwa la Baraza Kuu ila keshokutwa (kesho) Maalim Seif atazungumza kama Katibu Mkuu na aliyekuwa mgombea urais. Kuna masuala mengi atayaeleza kwa kina, hasa hili la uamuzi wa CUF kususia uchaguzi,”zilieleza taarifa hizo.


“Atazungumzia kwa kina uchaguzi ulivyokuwa na kujibu maswali ya watu wa kada mbalimbali waliokuwa wakihoji nini hatima ya CUF, baada ya kususia uchaguzi na hivyo kupoteza nafasi za uwakilishi.”

Mwigizaji Shamsa Ford Amsweka Baba wa Mtoto Wake Lupango...Kisa Hichi Hapa

$
0
0

STAA wa filamu Bongo, Shamsa Ford juzikati amemsweka lupango mzazi mwenziye Dick Matoke, katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa kile kinachodaiwa kuwa mzazi mwenzake huyo kuwa na tabia ya kumtukana mara kwa mara akishirikiana na mpenzi wake wa sasa ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja.

Kwa mujibu wa chanzo makini, Dick na mwanamke wake wa sasa wamekuwa wakimtumia meseji za matusi Shamsa kitendo ambacho mwigizaji huyo alikuwa akikivumilia lakini katikati ya wiki hii, uvumilivu ukamshinda, akaamua kwenda kumshtaki.

“Yaani hakuna kitu ambacho Shamsa alikuwa hakipendi kama kutumiwa meseji na mzazi mwenzake huyo na mwanamke wake zikimtusi kwa maana alivumilia mpaka akachoka, akaona bora aende polisi kumshtaki,” kilisema chanzo.



Shamsa Ford enzi akiwa na mzazi mwe


Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, baada ya kwenda polisi na kufungua mashtaka yaliyosomeka; OB/RB/6522/2016, usiku wa Aprili 6, mwaka huu, polisi walikwenda nyumbani kwa Dick maeneo ya Mikocheni jijini Dar ambapo walifanikiwa kumkuta, wakampeleka kituoni Oysterbay.

“Polisi wanaendelea kumtafuta na mpenzi wa Dick aliyekuwa akishirikiana naye kumtukana Shamsa ili naye waweze kumhoji kisha hatua nyingine za kisheria zichukue mkondo wake,” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa Shamsa kuhusiana na sakata hilo, alikiri kutokea lakini akaomba muda ili alizungumze vizuri kwa kile alichosema yuko  bize na shughuli zake za filamu.

“Mh! Umeipata hiyo na wewe?  Nani aliyekuambia? Any way ni kweli imetokea lakini nitakuelezea vizuri nikitulia, niko bize kidogo na kazi,” alisema Shamsa.

Breaking News: Dkt. Shein Atangaza Baraza Lake la Mawaziri

$
0
0

RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dkt. Ali Mohamed Shein leo Jumamosi, April 9, 2016 ametangaza Baraza la Mawaziri litakalosimamia kazi za serikali kwa kipindi cha uongozi wake wake kwa mujibu wa sheria.

Dkt. Shein amesema amepunguza ukubwa wa baraza hilo kutoka wizara 16 hadi kuwa wizara 13 zenye Mawaziri ni 13 na Manaibu waziri 7, ambapo wizara tatu amezivunja na kuzigawa ndani ya hizo wizara 13 za sasa.

Ameongeza kuwa, mawaziri aliowatangaza leo atawaapisha kesho Jumapili asubuhi katika Viwanja vya Ikulu visiwani Zanzibar.

Baraza la Mawaziri Zanzibar hao ni;

1). Ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi – Issa Haji Ussi Gavu.

2). Katiba na Sheria Utumishi wa Umma – Haroun Ali Sleiman.

3). Tawala za Mikoa na Idara maalum – Haji Omari Kheir.

4). Makamo wa 2 wa Rais – Mohd Aboud.

5). Waziri wa Fedha na Mipango – Dk. Khalid Salum Mohd.
6). Afya – Mahmoud Thabit Kombo.

7). Wizara ya Elimu – Riziki Pembe Juma.

8). Viwanda na Masoko – Amina Salum Ali.

9). Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi – Ali Karume.

10). Habari Utalii Utamaduni na Michezo – Rashid Ali Juma.

11). Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi – Hamad Rashid Mohd.

12). Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto – Mauldine Castiko.

13). Maji Ardhi Nishati na Mazingira – Salama Aboud Talib.

Tunda: Kupiga Picha Nusu utupu ni Hobi Yangu

$
0
0

MUUZA nyago Bongo, Tunda Sebastian amesema miongoni vya vitu ambavyo anajiona yuko huru kuvifanya ni kupiga picha za kihasara kwani anachukulia kama hobi yake.

Tunda alifunguka hayo baada ya kuulizwa sababu za yeye kupenda kupiga picha hizo ambapo alisema, yeye haoni tatizo katika hilo kwani hata wazazi wake walikuwa wakimpigia kelele lakini sasa wametulia.

“Huwezi kumjaji mtu kwa picha, sioni tatizo kwani hata ‘home’ wanajua kuwa hiyo ni hobi yangu,” alisema Tunda huku wengi wakimponda kwa tabia hiyo chafu inayokwenda kinyume na maadili ya Kitanzania

Idriss Afunguka...Niliumia Kumuona Wema Sepetu Akimbusu Mwanaume Mwingine

$
0
0
Idris Sultan aliumia kumuona mpenzi wake Wema Sepetu akimbusu mwanaume mwingine.

Idris na mtangazaji wa The Trend, Larry Madowo

Akiongea kwenye kipindi cha The Trend cha NTV ya Kenya, Idris alisema ‘hicho ni kitu kibaya zaidi kuwahi 

YAMETIMIA..Radio EFM Yawachukua Watangazaji Gerald Hando na PJ...Imewatambulisha leo Rasmi

$
0
0
(PJ) pamoja na Abel Onesmo Jumamosi hii wametambulishwa rasmi EFM.
Watangazaji wa zamani wa kipindi cha Power Breakfast cha Clouds Fm, Gerald Hando, Paul James

Mkurungenzi wa EFM Radio, Francis Siza ‘DJ Majay’ (kushoto) Paul James (PJ) pamoja na Gerald Hando

Utambulisho huo umefanyika katika sherehe za shindalo la Shika Ndinga 2016 zilizofanyika Mbagala Zakhiem jiji Dar.

Kupitia ukurasa wa EFM, wameandika:
Utambulisho wa wanafamilia wapya wa @efm_93.7@geraldhando @pjpauljames @abelonesmo #TUNALISONGESHA#huumchezohauhitajihasira
Tazama picha za utambulisho huo.

Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images