Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

MSAFARA WA MWENYEKITI UVCCM WAWEKEWA MAGOGO

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) taifa, Sadifa Juma Khamis (MB)Polisi mkoani Pwani inachunguza kundi la watu linalodaiwa kuweka magogo barabarani kuzuia msafara wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) taifa, Sadifa Juma Khamis (MB) katika eneo la Tondoroni, wilayani Kisarawe, mkoani humo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Ulrich Matei, alisema atazungumzia suala hilo baada ya  kupata  taarifa kamili.
Kwa mujibu  wa watu walioshuhudia tukio hilo, kundi hilo liliweka magogo hayo jana usiku katika barabara ya kati ya eneo la Mpuyani katika njia panda ya barabara iendayo vijijini kuingia barabara kuu ya Morogoro.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema katika nyakati tofauti kundi hilo lilianza kuzuia msafara huo kwa kutaka kushinikiza dai la mgogoro wa mipaka kati ya eneo la Jeshi la Wananchi wa Ulinzi Tanzania (JWTZ) na makazi ya watu katika eneo la Tondoroni, wilayani humo.
Watu hao ambao idadi yao haikuweza kufahamika walidaiwa kutishia kuchoma moto magari ya msafara huo wa mwenyekiti wakati alipotaka kushuka na kuzungumza nao na kuamua kujisalimisha kwa kuingia ndani ya gari  na kurudi Kisarawe.
Mwenyekiti  huyo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Donge, Tanzania Visiwani mapema akiwahutubia  wananchi wa Kisarawe aliwataka kudumisha amani kwa  kukiweka Chama Cha Mapinduzi madarakani. “Amani ikivurugika hakuna atakayekuwa salama, hata askari  nao  hawatokuwa salama”.
Akiongea na viongozi wa CCM na UVCCM  katika jengo la ofisi za CCM wilaya, aliwataka wanachama hao kuvunja makundi ya kampeni kwa kuwa hayana tija kwa sasa, isipokuwa wakati wa kampeni za uchaguzi.
Alisema kuwa Muungano wa Tanzania ni muhimu hivyo changamoto zilizomo ndani yake zitafutiwe muafaka kwa njia ya amani.
Alisema kuna  baadhi ya watu wakorofi ambao wanadai muungano uvunjwe hasa kutoka Pemba wakidai kuwa kisiwa hicho ni chao wakati  visiwa hivyo vya Pemba na Zanzibar havina wenyewe na watu walioko huko wametokana  na  biashara ya utumwa na wengi wao walitoka upande wa Tanzania Bara wa makabila mbalimbali.
Wakati huo huo, mwenyekiti huyo alimsimika mwandishi wa siku nyingi, Abubakar Mlawa kuwa kamanda wa UVCCM wilayani humo na wengine 15  wakiwamo madiwani  kuwa makamanda wa UVCCM wa kata zao.
 

CHANZO: NIPASHE

IGP SAIDI MWEMA ATANGAZA MABADILIKO KATIKA JESHI LA POLISI TANZANIA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema   amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera pamoja na baadhi ya Wakuu wa Upelelezi wa mikoa na  wakuu wa Polisi wa Wilaya katika baadhi ya mikoa hapa Nchini.
Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Philipo Kalangi amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam, kuwa Mkuu  wa kikosi cha kusimamia usalama wa Mazingira na nafasi yake  inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi  (SACP) George Mayunga ambaye alikuwa Mkuu wa kikosi cha  kusimamia mazingira Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.
 Aidha, baadhi ya Wakuu wa Upelelezi wa  mikoa (RCO) na wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) waliobadilishwa ni pamoja na 
aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa  makosa ya jinai mkoa wa Tabora ACP Edward Bukombe amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam, Mkuu wa Upelelezi wa mkoa wa Geita (RCO) ACP Francis Kibona  amehamishiwa mkoa wa Njombe kuwa mkuu wa Upelelezi mkoa na  nafasi yake inachukuliwa na SSP Simon Pasua kutoka  Makao makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.
Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ya Wanging’ombe SSP. Francis Maro amehamishiwa Mkoa wa Katavi kuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa na aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Katavi ACP. Emmanuel Nley amehamishiwa kikosi cha Polisi wanamaji Dar es Salaam. Mkuu wa Upelelezi mkoa wa  Rukwa SSP. Peter Ngussa amehamishiwa Makao makuu ya Upelelezi Dar es Salaam, nafasi yake inachukuliwa na SSP  Alan Bukumbi aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Njombe.
Aliyekuwa Mkuu wa Polisi wilaya ya kati( OCD) Mrakibu wa  Polisi (SP) Salum Ndalama anaenda kuwa kaimu mkuu wa upelelezi mkoa wa Tabora na aliyekuwa mkuu wa Polisi wa  wilaya ya Tunduru (OCD) SP. Amadeus Tesha anakwenda kuwa Mkuu wa upelelezi kikosi cha Polisi reli.
Uhamisho huo ni wa kawaida katika kuboresha utendaji kwa  mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
Imetolewa na:Advera Senso-SSPMsemaji wa Jeshi la Polisi.

ANGALIA PICHA YA MSHINDI WA BONGO STAR SEARCH ALIYE PATIKANA USIKU WA KUAMKIA LEO

$
0
0

Zawadi kwa mshindi wa mwaka huu ni Milion hamsini[50]ambayo kakabidhiwa jukwaani.


Kinyanganyiro cha kumtafuta Super Star wa Bongo kupitia Epiq Bongo Star Search 2013 kimekamilika alfajiri hii kwenye ukumbi wa Escape 1.

Mashindano haya ambayo kidogo yalichelewa kuanza yalipambwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Barnaba,Makomando,Young Killer,water chilambo,Shaa,Kimbunga na Snura.

Katika mashindano haya ambayo yalikua na jumla ya washiriki watano ambao ni Amina Chibaba,Elizabeth Mwakijambile,Emmanuel Msuya,Maina Thadei na Melisa John,ambao walipita kwa round tatu kisha majaji kuwapunguza watatu na kisha kubakia Emanuel Msuya na Elizabeth Mwakijambile katika Round ya 4 na ya mwisho.
Katika round ya mwisho,Emmanuel Msuya ameibuka kidedea na kuwa Mshindi wa Epiq Bongo Star Search 2013,akiwa ni mshiriki anaetokea Jijini Mwanza na kumpokea taji water chilambo ambae alikua mshindi wa mwaka jana.
CREDIT: millardayo.com

KAMPUNI 100 BORA TANZANIA ZATAJWA

$
0
0
Dar es Salaam. Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda amesema kuwa, Serikali itaendelea kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya biashara ili wawekezaji wa nje na ndani waweze kutekeleza majukumu yao bila kikwazo.
Dk Kigoda aliyasema hayo juzi usiku alipokuwa kwenye hafla ya kuzitambua Kampuni 100 Bora zinazokua kwa kasi nchini (Top 100 Mid–Sized Companies), ambapo Kampuni ya Kipipa Millers Limited ya jijini Mwanza ilishika nafasi ya kwanza.
Kampuni hizo zilitambuliwa na kupewa tuzo kutokana na shindano linaloendeshwa na Kampuni ya Mwananchi Communications (MCL) na KPMG Tanzania na kudhaminiwa na Benki ya NBC pamoja na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
Dk Kigoda alisema shindano hilo linaimarika kila mwaka na lina nafasi kubwa ya kuimarisha uchumi kwa Kampuni za Afrika Mashariki.
Alisema ili kampuni hizo ziweze kufikia mafanikio, Serikali itajitahidi kuweka mazingira yatakayoziwezesha kufanya shughuli zake vizuri na kufanya uzalishaji kwa gharama nafuu.
Alizitaka kampuni zilizofanikiwa kuingia kwenye kundi la kampuni 100 bora, kujitambua kuwa sasa wao ni washindi na hivyo wajitahidi kufanya shughuli zao kitaalamu zaidi.
“Kwa kiwango hiki mlichofikia sasa ni washindi, mfanye kazi zenu kitaalamu zaidi,”  alisema Dk Kigoda.
Alisema kwa sasa Tanzania imeshuka kwenye nchi zenye viwango vizuri vya kufanya biashara duniani, hali inayofanya baadhi ya wawekezaji kukimbia.
Alieleza suala hilo linaipa Serikali changamoto ya kutengeneza mazingira bora na rafiki ili kuvutia wawekezaji kufanya shughuli zao kwa faida.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Zuhura Muro alisema kwa kushirikiana na KPMG, wanaendesha shindano hilo kwa sababu wanaelewa kuwa hiyo ni njia muhimu ya kuhamasisha kampuni kufanya vizuri.
Alisema kuwa, kampuni hizo ni muhimu kwa uchumi wa nchi na ustawi wake kwani kodi wanazolipa ndizo zinazotumika kwa maendeleo ya nchi.
“Sasa ni wakati wetu wa kuinuka, lakini hatuwezi kuinuka bila kuwa na watu muhimu kama ninyi (kampuni 100 bora) kwani ndiyo mnaotengeneza ajira, nyie ni watu muhimu sana kwa uchumi wa nchi hii,” alisema Muro.
Huu ni mwaka wa tatu wa shindano hilo, mwaka 2011 Kampuni ya BQ Contractors ya Dar es Salaam ilishika nafasi ya kwanza, huku mwaka 2012 Kampuni ya Helvetic Solar Contractors ya jijini Arusha ikichukua nafasi hiyo.
Mara baada ya kutangaza kuwa mshindi jana,  Mkurugenzi Mkuu wa Kipipa Millers Limited, Oliver Matemu alisema hakutarajia kushika nafasi hiyo.
“Nilipokuwa hapo ndani nilikuwa nasikia tu wakitangaza, walipofika nafasi ya 50 bila kusikia tukiitwa nilijua kuwa sisi tumerukwa,” alisema Matemu.
Matemu alisema kuwa, kampuni yake inajishughulisha na usagaji wa nafaka na kuzisambaza pamoja na kusambaza bidhaa za Kiwanda cha Bia cha Tanzania (TBL).
“Kilichotufanya tukaibuka washindi ni namna ambavyo tunajitahidi kuandaa hesabu zetu,” alisema Matemu.
Alisema kuwa, alianza shughuli hiyo kwa kununua unga kwenye mashine za watu na kuusambaza wakati huo akiwa na mtaji wa kati ya Sh1.5 milioni.
“Kwa sasa kwa mwaka nafanya biashara ya kama Sh5 bilioni,” alisema.
Kampuni nyingine zilizoingia kwenye 10 bora ni Otonde Group of Companies Tanzania Limited, iliyoshika nafasi ya pili, SEEDCO Tanzania Limited ya tatu, Kays Logistics Company Limited ya nne, Sihebs Technologies Company Limited  ya tano na Techno Brain Tanzania Limited ya sita. 
Kampuni nyingine ni Anjari Soda Factory Limited nafasi ya saba, NPK Technologies Limited nane, Palray limited ya tisa na Fomcom International Limited  nafasi ya 10.
CHANZO: MWANANCHI

ZITTO: URAIS, MABILIONI YA USWISI VINANIMALIZA

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesema tuhuma alizosomewa na uongozi wa Chadema katika kikao cha Kamati Kuu sizo zilizoelezwa na chama hicho mbele ya waandishi wa habari na viongozi wa chama hicho.
Aidha, amesema kuwa vita aliyopo siyo kati ya Chadema na Zitto, bali ni vita ya watu wengi, akitaja magenge ya watu wanaotaka urais 2015 na walioficha fedha nje ya nchi walioungana wakiona tatizo lao ni yeye hivyo kutaka kumwondoa bungeni.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili kwa njia ya simu, Zitto alisema kuwa hadi sasa bado hajapokea tuhuma 11 anazokabiliwa nazo, hivyo hajui makosa hayo na bado anasubiri akabidhiwe kwa maandishi.
Ana ugomvi gani na viongozi wenzake?
Alipotakiwa kueleza iwapo ana ugomvi na watu ndani ya Chadema, Zitto alisema kuwa huenda mambo hayo yanatokea kwa sababu mahasimu wake wa kisiasa wa ndani na nje wameamua kuungana na kupambana naye ili kumdhoofisha kisiasa kwa masilahi yao.

MWIGIZAJI WA FAST & FURIOUS AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI

$
0
0

Marekani. Mwigizaji wa Fast & Furious, Paul Walker amefariki dunia hivi punde nchini Marekani baada ya dereva aliyekuwa akiendesha gari hiyo kukosa ‘control’ na kugonga moja ya nguzo za taa za barabarani.

Nyota huyo wa kuigiza mwenye umri wa miaka 40 alikuwa abiria kwenye gari ya kisasa na ajali hiyo ilitokea katika eneo la Santa Clarita.

Idara ya usalama ya nchini humo imedhibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kubainisha kwamba watu wawili wamefariki dunia kwenye ajali hiyo.

Wawakilishi wa mwingizaji huyo wamethibitisha kwamba Paul Walker ni mmoja wa watu wawili waliofariki mchana wa LEO nchini Marekani.




“Ni kweli, tunapenda kuthibitisha kwamba mwigizaji Paul Walker  amefariki dunia leo katika ajali mbaya ya gari wakati alipokuwa akienda kuudhuria kuchangia mfuko wa  Reach Out Worldwide.



“Alikuwa abiria kwenye gari ya rafiki yake na wote wamepoteza maisha leo,” taarifa hizi zimesomeka kwenye akaunti maalum ya facebook ya muigizaji huyo.

DIAMOND AULA ZIARA YA KOMBE LA DUNIA TANZANIA (PHOTOS)

$
0
0


Nchi yangu Tanzania imepata bahati  nyingine tena ya kutembelewa na ,kombe la dunia atakalo pewa mbabe wa kabumbu Duniani ,ni kombe linaloheshimika  sana duniani kote..Hafla ya kulipokea
imefanyika usiku  huu ndani ya viwanja vya hotel ya Serena jijini Dar ,na Diamond kama balozi wa Coca cola alikuwepo na alipangwa kama mmoja ya wasanii wa Kitanzania aliyetumbuiza
angalia picha zaid hapa........


Home sweet home,akijiandaa.........

My personal security officer,call him Mwarabu akiwa satandby kabisa akinisubili...

 Baada ya kuwasili hotelini@Serena hotel,kulikwa
 na ulinzi wa hali ya juu sanaa.........
                                      Akikwea ngazi kuelekea kwenye vyumba 

                                      

                                                              Backstage with my boys.............
                                                             Kazi ikaanza kihivii.............!!!!




                                                           Kwani nani amenunaa........!!!!!!!!!!!
                                                                   Mwali mwenyewe...!!!


                                                   Hapa sasa.ngololo ngololo..!!!!!!!!!
                                         Aha aaha aaha aipooh..aah aipooh............!!!!!!!!!
                                                        Amemaliza

BAADA YA ZITTO KUVULIWA UONGOZI KUNDI LA WATU LASAMBAZWA MIKOANI KUMCHAFU

$
0
0
Kundi la watu lasambazwa mikoani kumshughulikia 
*Mwenyewe akiri kupata taarifa, Chadema yasema ni ratiba ya kawaida
BAADA ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumvua madaraka aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe, chama hicho sasa kimechukua hatua ya kusambaza kundi la watu katika mikoa mbalimbali nchini kwa kazi maalumu ya kushughulika na upepo uliosababishwa na hatua hiyo.

Habari ambazo zimelifikia Rai Jumapili zinaeleza kuwa kundi hilo limepewa maelekezo mahususi kutoka makao makuu ya Chadema kwa ajili ya kwenda kuwashawishi wafuasi na wanachama wake waamini kwamba kijana huyo ni msaliti.

Kwa mujibu wa habari hizo, kundi hilo la watu karibu 15 litazunguka mikoani kupeleka kile inachokiita elimu kuhusu kuvuliwa uongozi kwa Zitto pamoja na Mwanazuoni kutoka katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Kitila Mkumbo litalenga kuwafikia wafuasi wa chama hicho hususani vijana kupitia mabaraza yao ya chama ambao kwao Zitto amekuwa akionekana kama nembo ya mtu anayepigania mabadiliko. 

Source: Mtanzania

PICHA ZA GARI AINA YA RANGE ROVER AMBALO NI REFU KULIKO YOTE AFRICA MASHARIKI

$
0
0

5921_643916678955211_694058705_n-4570-600-600-80Mara nyingi tumezoea kuziona Limousine ndefu kwenye harusi tofautitofauti lakini Range hii ambayo ipo Kenya inaweza kuwa ndio ndefu zaidi kuliko Range zote ambazo zipo Afrika Mashariki ambapo unaweza kutazama picha zake za ndani na nje hapa.
58873_618020604878152_762034716_n-4569-600-600-80
64755_590187184328161_235651424_n-4568-600-600-80
226879_590182380995308_543629288_n-4565-600-600-80 (1)
226879_590182380995308_543629288_n-4565-600-600-80
383670_557935277553352_1184415968_n-4571-600-600-80
529115_615751478438398_1881184687_n-4566-600-600-80
545705_590182444328635_1651343247_n-4564-600-600-80

Use Facebook to Comment on this Post

MTANZANIA WA KWANZA NDANI YA JARIDA LA PLAYBOY MAREKANI

$
0
0
Pichani juu ni Mtanzania wa kwanza kuwepo katika ukurasa wa mbele wa Jarida maarufu la Playboy la nchini Marekani ambapo amelipwa kitita kikubwa mno. Jarida hilo limewatoa mastaa kibao wakiwemo Madonna, Kim Kardashian, Naomi Campbell, Garcelle, Vanessa Williams na wengineo.
GPL

MAJANGA:KATIBU WA WILAYA YA CHUNYA CHADEMA AJIUNGA CCM

$
0
0
1
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmani Kinana akipiga makofi wakati Braison Mwasimba aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA wilaya ya Chunya aliporejesha kadi yake ya chama hicho na kujiunga na chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Lupa.
3
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmani Kinana akipiga makofi wakati Braison Mwasimba aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA wilaya ya Chunya alikionyesha kadi yake ya chama cha Mapinduzi CCM baada ya kukabidhiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Lupa.
5
Mbunge wa jimbo la Songwe na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mh Philip Mulugo akimvisha shati la CCM Bw. Braison Mwasimba aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA wilaya ya Chunya aliporejesha kadi yake ya chama hicho na kujiunga na chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa hadhara kata ya Lupa.
 6
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akimuangalia Bw. Braison Mwasimba aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA wilaya ya Chunya wakati akihutubia aliporejesha kadi yake ya chama hicho na kujiunga na chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa hadhara kata ya Lupa.
GPL

P-UNIT WACHUKUA TUZO MBILI ZA CHANNEL O KWA WIMBO WAO ULIO WAHI KUPIGWA MARUFUKU KUONESHWA KWENYE BAADHI YA TV KENYA

$
0
0
It was a great night in Soweto as Channel O awarded Africa’s best music videos. Kenya’s P-Unit who had been nominated twice were the only double category winners at the event. Here is the full list of winners and nominees. Winners are marked in bold.

MOST GIFTED KWAITO VIDEO
L’VOVO DERRANGO FT PROFESSOR – Palesa
PROFESSOR FT OSIKIDO & CHARACTER – Finger Prints [Winner]
EES – Woza December
KABELO – Impilo
DJ TIRA FT BIG NUZ & JOOCY – Summer Time
MOST GIFTED AFRICAN (EAST) VIDEO
AY/MARCO CHALI – Party Zone
P-UNIT FT COLLO: You Guy (Dat Dendai) [Winner]
RADIO & WEASEL – Can’t Let You Go
SAUTI SOL – Money Lover
NAVIO – Kata
MOST GIFTED AFRICAN (WEST) VIDEO
D’PRINCE – Goody Bag
ICE PRINCE – Aboki
R2BEES – Life (WALAAHI)
DBLACK FT JOEY B – Vera
CHIDINMA FT ILLBLISS & SUSPECT – Emi Ni Baller
P-SQUARE – Alingo [Winner]
MOST GIFTED RAGGA/DANCEHALL VIDEO
BUFFALO SOULJAH – Basawine
KAAKIE – Too Much
JESSE JAGZ – Murder Dem
P-UNIT FT COLLO – You Guy (Dat Dendai) [Winner]
RADIO AND WEASEL – Can’t Let You Go
MOST GIFTED R&B VIDEO
BANKY W – Yes/No [Winner]
ANSELMO RALPH – Curticao
DANNY K – Brown Eyes
CHASE – Lonely
VICTORIA KIMANI/M.I – Oya
MOST GIFTED HIP HOP VIDEO
AKA – Jealousy [Winner]
JAYSO & SARKODIE – Pizza & Burger
REASON – Do It Like I Can
IFANI FT BLAKSUGA – Chocolate Vanilla
EL/M.aNIFEST – Hallelujah
MOST GIFTED AFRICAN (SOUTH) VIDEO
DAMA DO BLING – My Eish
OSKIDO – Tsa Mandebele [Winner]
BLACK COFFEE FT ZAKES – Take it All Off
PAUL G FT FABULOUS – Get Control
DJ DIMPLEZ ft L-TIDO & ANATii – We Ain’t Leaving
KHULI CHANA – Hazzadazmove
MOST GIFTED DANCE VIDEO
KCEE – Limpopo
MAFIKIZOLO – Khona [Winner]
FUSE ODG FT WYCLEF JEAN – Antenna (Remix)
DJ MALVADO FT PETTY – Jamaica
DJ GANYANI FT FB – Xigubu
MOST GIFTED AFRO POP VIDEO
THE SOIL FT ZAKWE – Linkomo [Winner]
SAUTI SOL – Money Lover
2FACE IDIBIA – Ihe Ne Me
THE MUFFINZ – Umsebenzi Wendoda
DAVIDO – Gobe
MOST GIFTED DUO/GROUP/FEATURING VIDEO
TEAR GAS – Wake Up
XTATIC/AKA & PRIDDY UGLY -Hit Em Up
MI CASA – Can’t Get Enough
EME – Baddest Boy
NAETO C FT D’BANJ – Tony Montana (Bad Pass) Remix
ZONEFAM – Contolola [Winner]
MOST GIFTED NEWCOMER VIDEO
MONEOA – Is’bhanxa
LOLA RAE – Watch My Ting Go
KHAYA MTHETHWA – Move [Winner]
VICTORIA KIMANI – Mtoto
BURNA BOY – Tonight
MOST GIFTED FEMALE VIDEO
ZONKE – Feelings [Winner]
LIZHA JAMES FT ANSELMO RALPH – Vais Rochar
STL – Stella Stella Stella
TIWA SAVAGE ft DON JAZZY – Without My Heart
TOYA DELAZY – Heart
MOST GIFTED MALE VIDEO
DONALD – Over The Moon
Zeus FT AKA & TUMI – #DatsWasup [Winner]
WIZKID – Azonto
AY/MARCO CHALI – Party Zone
IYANYA – Flavour
MOST GIFTED VIDEO OF THE YEAR
XTATIC/AKA & PRIDDY UGLY – Hit Em Up
ZEUS FT AKA & TUMI – #DatsWasup
WIZKID – Azonto [Winner]
STL – Stella Stella Stella
AKA – Jealousy
REASON – Do It Like I Can
MAFIKIZOLO – Khona
FUSE ODG FT WYCLEF JEAN – Antenna
ICE PRINCE – Aboki
R2BEES – Life (Walaahi)
P-SQUARE – Alingo
PAUL G FT FABULOUS – Get Control

 Congratulations to P-Unit and all the other Kenyans who had been nominated. Thank you for rising the Kenyan flag up high!

TANZANIA YAIBUKA MSHINDI LEO DHIDI YA SOMALIA KOMBE LA CHALLENGE

$
0
0
Baada ya timu ya soka ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Ethiopia katika mechi ya michuano ya Kombe la Chalenji iliyochezwa kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi.



Timu ya soka ya Tanzania bara,Kilimanjaro Stars leo imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Somalia.

Bao pekee la Haroun Chanongo dakika ya 57 limetosha kuipa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Somalia mchana wa leo katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.

Hivi sasa Kilimanjaro ina pointi nne baada ya kufungana bao 1-1 na Zambia kwenye mechi iliyopita na ushindi wa 1-0 dhidi ya Somaria wakati Somalia haina pointi baada ya kupoteza mechi zake zote dhidi ya Burundi na Kilimanjaro stars.

KAULI YA BEN POL BAADA YA MSHINDI WA BSS WA MWAKA JANA NA MWAKA HUU KUIMBA WIMBO WAKE NA KUIBUKA WASHINDI

$
0
0
Mwaka jana katika mahindano ya BSS mshindi Walter Chilambo alitumia wimbo wa nikikupata wa Ben Pol na kuibuka mshindi katika shindano hilo.. Mwaka huu tena mshiliki aliyeshinda kinyang'anyilo hicho (Emmanuel Msuya) Alitumia tena wimbo wa Ben Pol  na ukampa alama za juu na kufanya ashinde. Kutokana na hatua hiyo soma alichokiandika Ben Pol na jinsi anavyojisikia kwa sasa.

BIKIRA KWA WASICHANA YAGEUKA KITU ADIMU HUKO ZANZIBAR

$
0
0
DAKTARI mwenye dhamana ya kituo cha Mkono kwa Mkono ambacho kinachunguza wanawake waliodhalilishwa ikiwemo kubakwa, Dk Marijani Msafiri amesema asilimia 80 ya watoto wa kike wanaoletwa kituoni hapo na wazazi wao , wanafikishwa kuchunguzwa masuala ya ubikira.

Dk Msafiri alisema hayo akizungumza na waandishi wa habari waliotaka kupata maelezo zaidi kuhusu matumizi ya kituo hicho ambacho kimewekwa kwa ajili ya kutoa huduma za haraka kwa wanawake wanaopata matatizo ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo kubakwa au kulawitiwa.

Alisema kituo hicho kinatumika vibaya kinyume na malengo yake ambapo wazazi wanawalazimisha watoto wa kike kuchunguzwa bikira yao baada ya kuwatilia shaka kwamba wanayo mahusiano ya kimapenzi na wanaume.

“Kituo hiki Mkono kwa Mkono malengo yake ni kutoa huduma za dharura kwa wanawake wanaokabiliwa na matukio ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo kubakwa.....sasa wazazi wanawaleta watoto wao hapa baada ya kuwatilia shaka kwamba wanamahusiano ya kimapenzi na wanaume kwa ajili ya kuchunguzwa kujua ubikira wao,” alisema.

Alisema huo ni aina mpya ya udhalilishaji wa kijinsia kwa sababu wanawake wengi wanapinga kuchunguzwa ubikra huo ambapo kazi hiyo inafanyika kwa nguvu kwa maelekezo ya wazazi tu.
Aidha alisema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa madaktari wa kufanya vipimo na kuchunguza matukio ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo kubakwa au kuchunguza ubikra ambapo kazi hizo hufanywa na madaktari wanaume.

Kituo cha Mkono kwa Mkono kilifunguliwa miaka miwili iliyopita ambapo lengo lake kubwa ni kurahisisha kupatikana kwa huduma zote katika kituo kimoja za matukio ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo matukio ya ubakaji.

Kituo hicho kinachotoa huduma zake katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja mjini hapa kinatoa huduma zake kwa ushirikiano mkubwa wa mashirika ya kimataifa yanayoshughulikia afya na maendeleo ya mtoto na mwanamke ikiwemo UNFPA na UNICEF.

KWA WADADA:DALILI ZA MWANAUME ANAYEKUPENDA KWA DHATI

$
0
0
ANAVYOKUTAZAMA
Mwanasaikolojia Zick Rubin kutoka Chuo cha Havard nchini Marekani aliwahi kusema kwamba watu wanaopendana hutumia asilimia 75 kutazamana kuliko wasiopendana, ambao kiwango chao ni asilimia 30-50. 

Hii ina maana kwamba mwanaume anapotumia muda wake mwingi kumtazama msichana na kugeuka taratibu kuangalia vitu vingine kama mtu asiyependa kuacha kumwangalia, ujue anampenda.

MIPANGO 
Mwanaume anayekupenda atakushirikisha kwenye mipango yake hasa ya muda mrefu. Mfano akitaka kununua kiwanja, kujenga nyumba atakuambia na pengine kutaka mchango wako wa hali na mali katika kulifanikisha hilo. Ukiona mwanaume anakuficha mambo yake, tambua kuwa huyo ana walakini kwenye penzi la dhati na la muda mrefu.

ATAONESHA HUZUNI
Katika maisha ya mapenzi kuna wakati wa kuhuzunika. Mwanaume mwenye upendo wa dhati atashirikiana nawe wakati wa huzuni na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa unapata furaha. 





ATAKUAMINI
Dalili nyingine ya kupendwa na mwanaume ni kuaminiwa kwenye maisha kwa ujumla. Yaani mwanaume anayekupenda hatakuficha kitu, mfano pesa zake, atakupa uhuru kwenye simu yake na kukuamini katika usimamizi wa miradi yake.

ATAKUPA NAFASI
Ninapozungumzia nafasi nina maana atakukaribisha kwake bila hofu na kukupa nafasi ya kuingia na kutoka bila mipaka, atakupa nafasi ya kuweka vitu vyako kwenye kabati na kuruhusu nguo, picha na vitu vyako kuonekana wakati wote chumbani kwake.

UTAKUWA MWANAFAMILIA
Mwanaume aliyefikia chaguo la mwisho kwa mwanamke humshirikisha mpenzi wake kwenye masuala yake ya kifamilia, mfano atamwalika kwenye vikao vya harusi, kipaimara, atatoa nafasi ya kuambatana naye kuona wagonjwa, kusalimia ndugu na atakuwa huru kukutambulisha kwao.

ATAZUNGUMZA NAWE KUHUSU WATOTO
Kwa kuwa wanaume wengi hufikiria kuwa na familia, mwanaume anayekupenda atazungumza nawe mipango ya kupata watoto kwa kuwa atakuwa amekuchagua wewe kuwa mama wa wanaye na atapenda mazungumzo hayo.

ATAKUSAIDIA
Kwa kuwa kukwama ni sehemu ya maisha yetu, mwanaume anayekupenda atakuwa tayari kukusaidia unapokwama. Kila mara atahakikisha kuwa unakuwa na mafanikio na yeye atakuwa tayari kukupunguzia usumbufu wa maisha, kwa kukufuata kazini, kukusaidia baadhi ya mambo na hata ya nyumbani.

ATAJITOLEA
Ninaposema kujitolea ninamaanisha atakuwa tayari kufanya mambo yako na kuyaweka yake nyuma. Kwa mfano akiwa anapenda mpira na siku hiyo kuna mechi, lakini muda huo ukamwambia akufuate kwa mjomba wako atakuwa tayari kuacha furaha yake na kukujali wewe. Huyu ni mwanaume anayekupenda kwa dhati.

ATAAMBATANA NAWE
Wapenzi wengi wasiokuwa na mapenzi ya dhati huona aibu kuambatana na wapenzi wao kwenye mikusanyiko ya watu, lakini mwanaume anayekupenda atafurahia kutoka moyoni kuongozana nawe kwenye halaiki ya watu na kufurahia uwepo wako bila kuona aibu.

KAMA UMEIPENDA MADA NA KUKUSAIDIA, TUPIA BASI LIKE NIKUPAKULIE NYINGINE!!!!

ETI BOY FRIEND WANGU ANAFIKIRI MIMI BADO NI BIKIRA

$
0
0
Admin
Mimi ni Msichana wa Miaka 21 , Nasoma chuo kimoja hapa dar ..nimetokea mkoa niko mwaka wa Pili sasa , huko nilipotokea nina Boyfriend ambae nimekuwa nae kwa muda mrefu toka secondary ila swala mapenzi hatujawahi fanya kwa vile kabla ya kuja chuo nilikuwa Bikira ..Baada ya kuja chuo naweza sema nimekutana na vijana wajanja na nadiriki kusema sina tena Bikira washaitoa ...Sasa nashindwa ni namna gani nimwambie boy wangu huyo wa mkoa ..Likizo nilienda nikamtega tufanye ili nijidai yeye ndio kaitoa lakini aliniambia tutafanya mapenzi siku ya ndoa ...Naombeni ushauri mie nataka nimwambie kwamba sina tena na tuwe tunafanya mapenzi ..Nitaanzia wapi ?

MANGE KIMAMBI "DO YOU THINK ZITTO NA WENZIE WATAUNDA CHAMA CHAO AU WATAKUJA CCM?"

$
0
0


"So what do you think?

Zitto na wenzie wataunda chama chao au wataingia kile chama kizuuuuuuuuuuuuuuriiiiiiiiiiii

kinachoitwa CCM?

Im guessing anakuja CCM ,,,,

With Zitto ndani ya nyumba, CCM itazidi pata nguvu, come 2015 ushindi utakuwa wa kishindoooo,,,,



WELCOME TO CCM KAKA ZITTO.....

By the way sijaelewa hili sakata la kwamba mtu mwingine keshapewa nafasi yake huko CHADEMA

Although yeye Zitto mwenyewe bado hajapewa barua ya kuenguliwa.........

mnaojua siasa kiundani tuchambulieni hili....." Mange 
Chanzo:Mange Blog

SUMAYE ALITAKA BUNGE KUFUTA TAKRIMA SEREKALINI...WENGI WANATUMIA KAMA KICHAKA CHA KUFICHA MAOVU YAO

$
0
0

  Alishauri Bunge kuibadili sheria `aliyoiasisi`
  Asema inatumika kama kichaka cha rushwa
  Asisitiza ilitungwa kwa wema, sasa inakiukwa
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye
Msemo wa sheria ni msumeno, umedhihirika sasa kwa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, ambaye anataka sheria iliyohalalisha matumizi ya takrima kwenye uchaguzi ifutwe.
 Sheria hiyo iliyopitishwa miaka ya 2000, ilitungwa na Bunge lililoongozwa na Spika Pius Msekwa, wakati Sumaye akiwa Waziri Mkuu na Kiongozi wa shughuli za serikali bungeni.
Aliyasema hayo wakati wa hafla ya kuzindua album ya waimbaji wa kwaya zilizo chini ya Umoja wa Vijana wa Kipentekoste katika vyuo vikuu (UPSF) vilivyopo mjini Morogoro jana, ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Kwa mujibu wa hotuba yake iliyopatikana kwa njia ya mtandao, Sumaye alisema kumekuwapo matumizi mabaya ya takrima hasa wakati wa uchaguzi, akisema inachochea rushwa. “Leo sote tu mashuhuda wa neno takrima kutumika kama kichaka cha kujifichia wala rushwa,” alisema.
Aliongeza, “sheria zote hutungwa kwa malengo mazuri, lakini katika matumizi yake likijitokeza tatizo ambalo halikutegemewa, basi sheria hiyo hufanyiwa marekebisho au kufutwa kabisa.” 
Sumaye alisema, “ni vizuri Bunge letu tukufu sasa likaifanyia sheria hiyo marekebisho kwa kuliondoa kabisa neno takrima au kuipa tafsiri na ufafanuzi ulio wazi zaidi, ili wala rushwa wasiitumie takrima kama kichaka cha kujifichia.”
AKEMEA MAUAJI YA OPERESHENI
Sumaye, amekemea mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola, dhidi ya raia wasiokuwa na hatia ikiwamo kupitia operesheni zinazolenga kudhibiti uhalifu nchini.
Sumaye alisema, upungufu wa maadili mema ni tatizo kubwa katika jamii hivyo ipo haja ya kuweka misingi imara ya kuondokana na tatizo hilo.
Leo kuna mauaji ya kutisha yanayotokea bila sababu zinazotosheleza, kama vile watu kujitoa mhanga na kuua watu wengi wasio na hatia,” alisema.
Alitoa mfano akisema, “hapa kwetu tumeshuhudia watu wakiteketeza familia nzima kwa sababu tu kakosana na mpenzi wake, vyombo vya serikali kufanya mauaji wakati wanafanya operesheni mbali mbali jambo ambalo wanajua ni makosa.
MISINGI YA HAKI
Sumaye alisema wapo Watanzania wengi wanaoshindwa kupata haki zao mpaka `kutoa chochote’, wakiwamo madereva barabarani wanaopata shida kupita bila kuwahonga baadhi ya askari wa usalama barabarani.
Na haya yapo katika sehemu na sekta nyingi nchini. Ninapozungumza haya sijawahi kusema hata siku moja kuwa rushwa hii imeanza sasa na huko nyuma haikuwepo. La hasha! Rushwa imekuwepo hata kabla ya uhuru na imeendelea kuwapo hadi leo,” alisema.
Aliongeza, “hata  Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alikiri kuwa hata wakati wa utawala wake rushwa ilikuwepo ila walikuwa hawana utani katika kukabiliana nayo.
Alisema ipo haja kukubali kuwa rushwa ni tatizo linaloongezeka kwa kasi, linaumiza uchumi wa nchi, wananchi na kuvunja heshima na hadhi ya taifa kwa jumuiya za kimataifa.
AOMBA RADHI
Hata hivyo, Sumaye aliomba radhi kwa kauli aliyonukuliwa Novemba 24, mwaka huu mjini Moshi, akisema Tanzania inaongoza kwa rushwa katika Afrika Mashariki.
Hapo niliteleza ulimi naomba radhi kama kuna waliokwazwa na hilo. Nilichotaka kusema ni kuwa “rushwa ni tatizo linaloongoza Tanzania katika kuathiri maisha ya watu wengi,” alisema.
 AWAASA VIJANA
Aliwaasa vijana kujiandalia maisha yatakayowawezesha kuchagia mabadiliko chanya katika kuwapo utawala bora na kupiga vita maovu, kuimarisha uchumi.
Aliyataja mabadiliko mengine kuwa ni katika kupiga vita umasikini, kustawisha ulinzi na amani.
Sumaye alisema, “kwa maoni yangu wasomi wetu hamjachukua nafasi yenu katika nchi na labda hata katika jamii. Kuna mambo mengi makubwa yanayotokea katika nchi lakini wasomi mnakaa kimya halafu yakisha haribika tunatafuta wa kuwanyooshea vidole,” alisema.
Aliongeza, “tuna maprofesa waliobobea wa fani mbali mbali, madaktari wahadhiri na wanachuo wanaoweza kutufanyia uchambuzi na utafiti ili kuwa na mchango chanya katika jambo lolote. Nafasi hii haijatumika ipasavyo na wakati mwingine hata nahisi imetumika vibaya.”
Alisema wanataaluma hao hawapaswi kuwaachia wanasiasa kila kitu pasipo kukosoa na kuonya, badala yake kuwa mithili ya watazamaji na baadaye walalamikaji.
AIPONGEZA UPSF
Alisema UPSF ina umuhimu kwa jamii kwa sababu, pamoja na mambo mengine, inawajenga vijana kiroho ili wawe watu wenye hofu ya Mungu.
Awali Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi wenye imani wa makanisa ya Pentekoste Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), Vicent Komba, alisema umoja huo haufungamani na upande wala taasisi ya dini yoyote bali upo kwa ajili ya kubadilisha watu kwa njia ya maombi na elimu kuweza kumrudia Mungu.
Alitaja baadhi ya mambo ambayo umoja huo umekuwa ukipambana nayo kuwa ni kuwabadilisha watu wanaojihusisha na madawa ya kulevya, pombe, ukimwi na masuala ya kifisadi ambayo yamekuwa ni tatizo kubwa hapa nchini na kusababisha madhara kwa kundi kubwa la vijana.
Alisema kuwa hali hiyo pia imekuwa ikisababisha taifa kukosa viongozi bora na wasio kuwa na maadili katika kuwatendea watu haki hivyo kupitia umoja huo watahakikisha wanarudisha uhusiano chanya baina ya viongozi na wananchi ili kuleta amani.
Walimhakikishia Sumaye kuwa watakuwa naye bega kwa bega kwa kumfanyia maombi ili kila kukicha wale wanaokusudia kumfanyia mabaya wasifanikiwe na yale anayokusudia kuyafanya katika siku zake za usoni yafanikiwe baada ya kuona mambo mazuri aliyofanya wakati wa uongozi wake alipokuwa madarakani.

KHADIJA KOPA AVAMIWA..APONZWA NA MWANAUME TATA

$
0
0
Stori:  Hamida Hassan na Gladness Mallya
MASKINI! Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki na Kati, Khadija Omary Kopa amevamiwa na vijana wahuni wakitaka kumfanyia fujo kwa madai ya kukatiza mitaani akiwa ameongozana na ‘mwaume tata’.
Baadhi ya vijana wakiwa wamelizingira gari alilokuwemo Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa na mwanaume aliyedaiwa kuwa tata.
Tukio hilo lilijiri maeneo ya Kariakoo, Dar wiki iliyopita ambapo vijana hao walianza kwa kuzomea wakitaka kumshika mwanaume huyo waliyedai alikuwa amevaa nguo za jinsia ya kike.
Alichokifanya Khadija ni kuingia kwenye gari na kumwambia dereva aondoke haraka kukwepa kufanyiwa vurugu huku mwanaume huyo naye akiungana na malkia huyo kuondoka eneo hilo.
Vijana wakimzingira Khadija Kopa aliyekuwa ameambatana na 'mwanaume tata'.
Wakizungumza na gazeti hili, vijana hao walidai kuwa Khadija alijiabisha kwa kuongozana na mwanaume huyo.
Khadija aliliambia gazeti hili kuwa alishangazwa na tukio hilo lililomkuta na kusema kuwa mwanaume aliyeongozana naye ni mwimbaji mwenzake ambaye pia ni shemeji yake.
Alifunguka: “Hivi kuwa mwimba taarabu wa kiume ndiyo ushoga jamani? Au kuvaa kaptura ya kitenge ni tatizo? Mbona alikuwa amevaa mavazi mazuri tu ya kiume?”
...Vijana wakizidi kulizingira gari alilokuwemo Khadija Kopa.
Khadija alisema kuwa amewazoea mashabiki wake wa Kariakoo kwani huwa wakiwaona mastaa huwa na tabia hiyo na ndiyo maana walianza uzushi huku wakisema kuwa waimba taarabu wote ni wanawake, kitu ambacho si kweli.
“Sikuona sababu ya kuchukua hatua, nilikuwa najaribu kuwaelewesha lakini hawakunielewa, wakazidi kuzomea na kutuzingira ndiyo maana tuliamua kuondoka,” alisema Khadija.
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live




Latest Images