Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104702 articles
Browse latest View live

Haya Hapa Matokeo ya Mechi ya Azam FC na Esperance ya Tunisia

$
0
0
TIMU ya Azam FC leo imeibuka kidedea kwa kuifunga Esperance ya Tunisia mabao 2-1 kwenye mchezo wa raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar.

Mabao ya Azam yamewekwa kimiani na Farid Mussa katika dakika ya 68 na Ramadhan Singano ‘Messi’ aliyefunga bao la pili dakika ya 69 ya mchezo.
Bao la Esperance limefungwa na Haithem Jouini dakika ya 33.

MAKONDA: Marufuku kwa wanaotoa Pesa kwa Omba omba kando ya barabara

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dsm Paul Makonda amepiga marufuku wananchi wanaotoa Pesa kwa Omba omba kando ya barabara kwa kuwa wanachangia uwapo wa watu hao huku baadhi ya watu wakiwatumia watoto hao kujipatia kipato kinyume cha sheria.

Akizungumza jijini dsm Bw.Makonda amesema kumekuwa na Ongezeko kubwa la watoto katika barabara kadhaa za jiji la dsm wakijihusisha na Kuomba pesa huku wanaowatuma wakiwa wamekaa pembeni jambo ambalo ni kinyume na sheria lakini pia linahatarisha Usalama wa watoto hao.

Aidha amesema mkakati uliokuwapo kwa kushirikiana na Ustawi wa jamii, Tamisemi pamoja na manispaa kuhakikisha kuwa watoto hao wanakusanywa na kuwekwa katika vituo maalum huku wanaohusika na kuwatumia kufanya kazi hiyo wakichukuliwa hatua.

Mtu Aliyeambukiza Ukimwi Watu 200 Afungwa Miaka 25 Jela....

$
0
0
Daktari aliyewaambukiza wagonjwa 200 virusi vya ukimwi nchini Cambodia amehukumiwa jela.Daktari huyo bandia alipatikana na hatia ya kuwaambukiza takriban watu 200 virusi vya ugonjwa wa Ukimwi amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kwa makosa yake.

Baadhi ya wahasiriwa wa makosa hayo wamekwisha fariki dunia, Yem Chrin alikuwa akitumia sindano zilizokuwa zimekwisha tumika kuwatibu wenyeji wa kijiji cha Roka bila ya kujua alickuwa akisambaza Virusi vya Ukimwi.Awali Chrin alikuwa ameshtakiwa kwa mauaji lakini upande wa mashtaka ukabadilisha shtaka na kuwa kuua bila ya kukusudia.

Kesi hiyo imefichua uhaba wa madaktari na ugumu ulioko kwa raia kupata huduma za afya katika maeneo mengi ya vijijini nchini Cambodia.

Utafiti umebaini kuwa zahanati nyingi katika maeneo ya vijijini huendeshwa na madakatari bandia ambao hawajahitimu kuwatibu wagonjwa.

Al-Shabaab Attack Kenyan Police Station

$
0
0

About 100 Al-Shabaab militants on Sunday morning attacked Diff Police Station in Wajir County, injuring three officers.

The heavily armed attackers are said to have stormed the police post at 3am, where they shot indiscriminately at 18 police officers who were at the station.

A heavy gunfire exchange ensued for two hours as the officers engaged the somali-based militants who later escaped taking with them a police land cruiser and mortar.

"The terrorists took the camp Landcruiser that we believe was used to ferry the many casualties they suffered, As they fled, the terrorists set ablaze shops at Diff market one belonging to the local chief," police noted in a statement.

Police affirmed that security personnel drawn from the Kenya Defence Force (KDF) and National Police Service (NPS) were in hot pursuit of the gunmen to interdict them and recover the stolen vehicle.

This is the latest attack from the militia group. In January, seven police officers were killed and a few others injured when a vehicle they were traveling in drove over an explosive device planted along the Hindi-Kiunga road in Lamu by Al-Shabaab militants.

Five days after that incident, gunmen who were heavily armed raided a village at Kaisari in Pandanguo, Lamu County killing several people.


KQ to Transfer Pilots to Ethiopian Airline

$
0
0

Troubled national carrier Kenya Airways is planning to offload some of its pilots to Ethiopian Airlines as part of austerity measures to see the airline return to profitability.

It is reported that 21 captains and 18 First Officers have received letters to the effect that they are being redeployed to the Ethiopian national carrier.

However, the news has not gone down well with the targeted officers, who have been given upto Tuesday April 12, to acknowledge their redeployment.

The Nation reports that Kenya Airline Pilots Association (Kalpa) subsequently set a meeting to deliberate on the next move for its members and is likely to move to court challenging the move.

The targeted pilots are among personnel of a fleet of Boeing 777 planes that have remained grounded for close to half a year now.

A letter sent to the pilots by Acting Head of Employee Relationship Murage Latiffa Cherono read in part: “As you are aware, the company has in the past few years experienced great business challenges that have led to poor financial results. As such, there has been a decline in the expected pace of growth of the network and subsequent reduction in fleet size including the B777 fleet, which you operate. This development led to most of the B777 pilots being underutilized in flying duties over the last several months and has therefore necessitated the company, as part of Operation Pride turnaround programme, to look for alternative deployment opportunities for you.”

Those who apply for the lateral transfer will work for Ethiopian Airlines for three years. They will however, have an option to rejoin Kenya Airways if the ongoing turnaround strategy is successful.

The carrier has been flying in turbulent skies struggling to remain afloat after registering huge losses in two consecutive years.

KQ had earlier announced plans to retrench some 600 of its staff to reduce its employee headcount in a bid to improve profitability.

Read also: Qatar Airways Poaches 20 Best KQ Engineers

The carrier is also reported to have sold off its morning landing slot at London’s Heathrow airport for an estimated Sh7.5 Billion to Oman Air. Oman Air have also accepted a deal with KQ to lease two of it's Boeing 787-8s . There are also plans to reduce the fleet from the current 52 planes to 36.

Read also: Kenya Airways Decides to Sell Planes

Group Managing Director Mbuvi Ngunze has reassured the public that the financial troubles the carrier is facing will be addressed soon.

Jinsi Ya Kutambua Simu Feki

$
0
0
1. Kabla hujanunua simu mpya hakikisha unaandika namba hii *#06#, kwenye simu hiyo au ambayo tayari umenunua.
2. Ukishaandika itaonyesha namba ya pekee (serial number) au IMEI (International Mobile Equipment Identity) ambayo ni lazima ziwe tarakimu 15 au zaidi na ni lazima ianze na 35.
3. Angalia kwa makini kama namba unazoziona zinafanana moja kwa moja na namba zilizoandikwa katika simu yako kwenye sehemu ambayo betri inakaa. Namba hizi zinapaswa kufanana kwa simu ambayo ni halisi. Kama hazifananani simu hiyo ni feki.
4. Tuma namba ya pekee (IMEI) kwenda namba 15090 na utapokea ujumbe mfupi unaoelezea kama simu yako ni orijino au feki.


KUJUA UBORA WA SIMU
1. Katika namba hizo namba ya sasa (7) na ya nane (8) ndizo zinazohakikisha ubora wa simu yako.
2. Kama namba ya saba na ya nane ni 00 ina maana kuwa simu yako imetengenezwa kwa ubora wa juu kabisa katika viwanda vya kuaminika.
3. Kama namba ya saba na ya nane ni 01 au 10 ina maana simu yako imetengenezwa Finland na ina ubora wa juu pia.
4. Kama namba ya saba na ya nane ni 13 ina maana simu yako imeunganishwa katika nchi za Azerbaijan na ni hatari kwa matumizi ya afya yako.
5. Kama namba ya saba na ya nane ni 02 au 20 ina maana simu yako imeunganishwa katika nchi ya Emirates na ina kiwango cha chini, lakini siyo feki.
6. Kana namba ya saba na ya nane ni kati ya 03 au 30 au 04 au 40 ina maana simu yako imentengenezwa China, lakini ina ubora mzuri ila haijafikia zile zenye 00, 01 au 10.
7. Kama namba yako ya saba na ya nane ni 05 au 50 ina maana simu yako imetengenezwa labda Brazil au USA ama Finland.
8. Kama namba ya saba na ya nane ni 06 au 60, simu yako imetengenezwa Hong Kong, China au Mexico.
9. Kama namba ya saba na ya nane ni 08 au 80, simu yako imetengenezwa Ujerumani na ina ubora wa kawaida.

Diamond Amaliza ziara ya Ulaya, Adai Reality TV Show yake itaweka Wazi Mambo Mazito

$
0
0
Diamond Platnumz amemaliza ziara yake ya Ulaya aliyoipa jina, From Tandale to The World Tour iliyompeleka kwenye nchi takriban nane.

Show yake ya mwisho ilifanyika Jumamosi hii jijini Copenhagen, Denmark ambayo video zake inaonesha ilikuwa na mafanikio makubwa.

Mchumba wake Zari aliyemsindikiza kwenye nchi zote alizopita, ameshukuru kwa kuandika: Allow me to thank everyone that helped us while out there in Europe. For showing us around and hosting us. Mostly thank you for allowing my hubby entertain you. Stay blessed.

Tayari Zari amerejea Afrika Kusini kuungana na familia yake.



Katika hatua nyingine Diamond amedai kuwa reality TV show yake ijayo itaweka wazi mambo mengi mazito.

“Can you try to guess the name of our Reality Show?) (Muda si Mwingi Kipindi cha Maisha yangu ya kila siku, Familia na Team yangu nzima itaanza kuwa kwa Tv yako pendwa, ” ameandika Instagram.

“Nakuahidi sio tu eti Kireality show … ni Reality show Bora ambayo naamini utaipenda kunzia kwenye Quality, Mikasa na matukio yote nnayopitia mimi, Familia na Team yangu kila siku….Mengi yanaonekana, Unayoyasikia, Unayasoma ila kwenye Hiki kipindi ndio itakuwa Thibitisho la kila uvumi uusikiao….Sjui Kipini puani, Mara jicho, Mara sjui @officialshetta , Mara DNA, Mara @romyjons kutoinekana tena kwenye Tour Ghafla….Niamini mimi yote utaona na kuyapata kwa uwazi kabisa, Kaa na Mimi…….! We unavyohisi reality Show yetu itakuwa inaitwaje…..?” ameongeza.

Manny Pacquiao Astaafu Ndondi Baada ya Kumdunda Timothy Bradley

$
0
0
Bondia wa Ufilipino, Manny Pacquiao amethibitisha kustaafu masumbwi baada ya kumdunda Timothy Bradley kwenye pambano lao la Jumamosi hii.

Pacquiao alishinda kwa pointi licha ya kumwangusha Bladley mara mbili.


Hilo limekuwa pambano lake la kwanza baada ya kushindwa na Floyd Mayweather Jnr May mwaka jana.


“As of now I am retired,’ alisema Pacquiao. “I am going to go home and think about it but I want to be with my family. I want to serve the people.”


Pacquiao anastaafu akiwa ameingiza dola milioni 500 kutokana na ndondi pamoja na endorsements katika kipindi cha miongoni miwili ya career yake.


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya April 11, Ikiwemo ya Seif Kudai Dr Shein Atasalimu Amri

$
0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya April 11, Ikiwemo ya Seif Kudai Dr Shein Atasalimu Amri

Ole Sendeka Aunguruma Babati......Asema Wanaopingana na Sera ya Rais Magufuli Ya "Kupasua Majipu" Wanapoteza Muda wao

$
0
0
Msemaji Mkuu wa CCM ambaye pia ni Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Kata ya Bashneti, wilayani Babati mkoani Manyara alisema, Chama Cha Mapinduzi kinamuunga mkono na kumtetea kwa nguvu zake zote Rais Dk. John Magufuli katika jitihada zake za kuliinua taifa la Tanzania.

Alisema, CCM itafanya hivyo kwa sababu kazi anayoifanya ya kupambana na wazembe na wezi wa mapato kwenye vyanzo vya uchumi wa taifa inatokana na maelekezo ya ilani ya CCM.

Sendeka alisema, CCM inawataka wale wote wanaojaribu kupotosha jitihada zinazofanywa na Rais za ‘kupasua majipu’ wakidai kuwa ni kuwaonea wanaochukuliwa hatia, kuacha mara moja, kwa sababu kinachofanyika ni sahihi na  kipo kwa mujibu wa sheria.

Alisema, upasuaji majipu huo unaofanaywa na Rais Magufuli hauchagui chama bali yeyote anayebainika kuwa ni jipu hata akiwa mwana CCM haachwi.

Kwa upande wake, Mjumbe wa NEC, Kilumbe Ng’enda, aliwataka Watazania kutambua kuwa Uchaguzi umeshamalizika kwa hivyo asitokee yeyote kuanza kuweweseka, kwa kutoa maneno ya kejeli kuhusu utendaji kazi wa Rais Dk. Magufuli kwa sababu baada ya uchaguzi kumalizika sasa kiichobaki ni kuchapa kazi.

Alisema, hakuna sababu za mwanasiasa yeyote kuanza mambo ya fitina za kisiasa wakati huu kwa kuwa kufanya hivyo ni kujisumbua

KITUMBUA Kimeingia Mchanga...Ikulu Yafuta Safari ya Wakuu wa Wilaya 10 Kwenda China China

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi John Kijazi

Ikulu imefuta safari ya wakuu wa wilaya 10 na wakurugenzi idadi kama hiyo waliotakiwa kwenda China kwa mafunzo ya uchumi wa kimaeneo kuanzia jana, na kuna uwezekano mkubwa ikatangaza uteuzi mpya leo.

Wakuu hao wa wilaya na wakurugenzi wao  walikuwa waondoke jana kwa ufadhili wa Serikali ya Watu wa China, lakini habari zinaarifu kuwa Ikulu iliamua kutotoa kibali, hali inayozidisha ubashiri kuwa uamuzi huo umetokana na kukamilika kwa uteuzi wa wakuu wapya.

Safari hiyo ilishakamilika kwa kiwango kikubwa baada ya kupata visa na wengi wao kuwasili jijini Dar es Salaam tayari kwa safari hiyo, lakini wakalazimika kurejea kwenye vituo vyao baada ya kukosa kibali cha Ikulu ambacho hutolewa na Katibu Mkuu Kiongozi.

Mara tu baada ya kuapishwa Novemba 5 mwaka jana, Rais John Magufuli alitangaza kudhibiti safari za nje za watumishi na viongozi wa umma kwa kuagiza kuwa Ikulu ndiyo itakayotoa kibali baada ya kujiridhisha na umuhimu wa safari hizo kwa Taifa.

Tangu atoe agizo hilo, ni mawaziri wawili tu ambao wameruhusiwa kwenda Vietnam kwenda kujifunza kilimo na viwanda. Mawaziri hao ni Mwigulu Nchemba (Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi) na Charles Mwijage (Viwanda na Biashara).

Naibu Waziri wa Fedha, Dk Ashatu Kijaji alikwenda nchini Ethiopia kuhudhuria mkutano wa mawaziri wa fedha, wakati kwa nyakati tofauti Makamu wa Rais Samia Suluhu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa walikwenda Afrika Kusini na Botswana.

Mpaka sasa, Rais Magufuli amefanya safari moja tu ya nje alipokwenda Rwanda kwenye maadhimisho ya mauaji ya kimbari.

Lakini safari ya wakuu hao wa wilaya ilikuwa ifadhiliwe na China, kwa mujibu wa habari hizo na hivyo isingeisababishia Serikali kutumia vibaya fedha za walipa kodi.

Uamuzi huo unaonekana kuzingatia zaidi uteuzi wa wakuu wapya ambao taarifa zinasema unaweza kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa, wakati wa wakurugenzi wa wilaya unatazamiwa kutangazwa baadaye wiki hii au wiki ijayo.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene alikiri kuwapo kwa safari hiyo, lakini akasema hajui kama imeidhinishwa na Ikulu kwa kuwa si muhusika.

“Katika hatua za awali nilisaini safari hiyo kuwaruhusu waende China, lakini sijui kama wamenyimwa kibali kwa sababu hilo si suala la ofisi yangu,” alisema Waziri Simbachawene.

Kama ni kweli, alifafanua Simbachawene, inaweza kuwa ni kutokana na umuhimu wao wa kuwatumikia wananchi kwenye maeneo wanayotoka. “Hawawezi kuondoka na kuziacha wilaya zao ilhali wao ndiyo waangalizi,” alisema Simbachawene.

Akiwa Chato mkoani Geita, Rais aliwataka wakuu wa wilaya kuchapa kazi badala ya kuwa na woga wa kutoteuliwa akisema uchapaji kazi ndio utawafanya waendelee kuwapo kwenye nafasi zao.

Rais pia amekuwa akitoa maelezo kadhaa yanayoonyesha atafanya uteuzi kwa kutumia vigezo hivyo, hasa suala la elimu ambayo inakabiwa na tatizo kubwa la uhaba wa madawati na vyumba na majengo, kipindupindu, njaa, migogoro ya ardhi na watumishi hewa.

SAKATA la Ukwepaji wa Kodi..Mgodi wa Acacia kuilipa Serikali Dola mil.20

$
0
0
KAMPUNI ya Acacia Mining PLC imesema itailipa serikali kodi ya dola za Kimarekani milioni 20 mwaka huu baada ya kusainiwa mkataba wa maridhiano kati yake na Mamlaka ya Mapato (TRA) mwezi uliopita jijini Dar es Salaam.

Makubaliano hayo baina ya Acacia na TRA ni kilele cha mchakato uliofanywa kwa lengo la kuendeleza dhamira ya utendaji ya kampuni hiyo nchini Tanzania na kuongeza ushirikiano na wadau mbalimbali wa kampuni hiyo.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Bradley Gordon, alitoa taarifa hiyo kwenye mawasiliano na wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Alisema kutokana na makadirio, kampuni hiyo italipa kodi ya ushirika ya miaka mitatu, endapo kampuni hiyo mwaka huu itaingiza mapato yanayofikia kiasi cha dola za Marekani milioni 80.

Alisema mkataba kati ya Acacia na TRA umetiwa saini na umetambuliwa na pande zote mbili kwamba hakuna kodi yoyote ya mapato yatokanayo na faida ambayo Acacia inastahili kulipa, haitalipwa.

Gordon alisema Acacia Mining ambayo iliingia nchini katika sekta ya madini ikijulikana kama Barrick na baadaye kama African Barrick Gold miaka 15 iliyopita, imekuwa ikitengeneza faida lakini haijarejesha mtaji iliowekeza wa dola za Kimarekani bilioni 3.8.

Hivi karibuni, Baraza la Rufaa za Kodi (TRAT), liliamua katika rufaa iliyokatwa na Acacia kwamba kampuni hiyo ilijenga mazingira ya kukwepa kodi ya dola za Marekani 41,250,426 (Sh bilioni 89) kwa kipindi cha miaka minne mfululizo.

Katika hukumu hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa TRAT, Jaji Dk Fauz Twaib, ilielezwa kuwa fedha hizo zilizopaswa kulipwa na ABG kwa TRA kama kodi ya zuio katika kipindi hicho, lakini ikakata rufaa kupinga kodi hiyo na baraza hilo kuipa haki TRA.

Hata hivyo, Acacia imepinga uamuzi huo katika Mahakama ya Rufaa. Akizungumzia historia ya mgodi huo, Gordon alisema wakati Barrick ilipoingia Tanzania miaka zaidi ya 15 iliyopita, kulikuwa na shughuli za kiwango kidogo za migodi nchini.

Gordon alisema tangu wakati huo, Barrick, African Barrick Gold na kisha Acacia Mining zimewekeza kiasi cha dola bilioni 3.8 katika ujenzi na uendelezaji wa migodi mitatu iliyopo hadi sasa.

Alisema Tanzania sasa ni mzalishaji mkuu wa nne wa dhahabu duniani, na kwamba kampuni yao ndiyo wazalishaji wakubwa nchini jambo alilosema hawana budi kujivunia.

Akizungumza madai kwamba wanatoa taarifa za uongo za kupata hasara ili kukwepa kulipa kodi nchini , alisema akaunti zao pamoja na zile za migodi mingine duniani hufanyiwa uhakiki makini.

“Kwa Tanzania peke yake, kuna mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Shirika la Uhakiki wa Migodi, Mahakama ya Udhibiti na Mamlaka ya Mapato Tanzania –taasisi zote hizi zinapembua hesabu zetu.

"Kwa kuwa tuna Soko la Hisa la London lenye umahiri mkubwa nalo pia linafanya kazi makini kuhakiki shughuli zetu,” alisema.

Alisisitiza kuwa hawajakwepa kulipa kodi bali katika biashara, panahitajika kwanza kuondoa gharama zote katika mapato kabla ya kutangaza kwamba wamepata faida.

Alisema katika miaka sita iliyopita pekee, tumelipa zaidi ya dola za Kimarekani milioni 750 kama kodi na mrabaha nchini Tanzania, karibu mara mbili ya kiasi ambacho wanahisa wamepokea kama mgao.

Gordon alisema wamewekeza dola za Kimarekani milioni 65 kwenye miradi ya maendeleo ya jamii . Alisema hivi sasa wanatoa ajira zaidi ya 45,000 nchini.

Wabunge Wahoji Uhalali wa Kisheria wa Rais Magufuli kuhamisha fedha za Muungano na Kuzipeleka Kwenye Ujenzi wa Barabara Mwanza

$
0
0
Baadhi ya Wabunge wamehoji uhalali wa kisheria wa Rais John Magufuli kuhamisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe ya Muungano na kuzipeleka kwenye ujenzi wa barabara katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Wabunge hao walihoji hilo wakati wa semina iliyofanyika jana katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam , iliyoendeshwa na Dk Haji Semboja kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Harold Sungusia wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali alihoji juu ya mamlaka ya Rais katika kutumia fedha ambazo zilishapangiwa bajeti na Bunge na kuzipeleka kwenye maeneo mengine.

Alihoji pia juu ya nidhamu ya Serikali katika usimamizi wa Bajeti iliyopitishwa na Bunge. Mbunge huyo alisema dhana ya mgawanyo wa madaraka haipo kwa sababu Serikali ina nguvu kuliko Bunge na Mahakama hivi sasa.

Alisisitiza kuwa nguvu hiyo ndiyo inayomfanya Rais afanye kitu chochote anachotaka.

Mbunge wa Viti Maalumu, Lucia Mlowe alisema moja ya majukumu ya Bunge ni kuisimamia Serikali, lakini anashangaa kuona yenyewe ikilisimamia Bunge katika mambo mbalimbali.

Alisema hata suala la Rais kuhamisha fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe ya Muungano, ni kuingilia madaraka ya Bunge, kwa sababu fedha hizo tayari zilikuwa zimeidhinishwa kwa ajili ya matumizi hayo.

“Naomba kupata ufafanuzi kutoka kwa wataalamu hapa, Rais ana mamlaka gani ya kuhamisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya jambo fulani? Pia, ni namna gani wabunge tunaweza kuisimamia Serikali kama hamna uwiano kati ya mihimili hii mitatu,” alihoji mbunge huyo.

Akijibu hoja hizo, Dk Semboja alisema Sheria ya Bajeti ya 2015, inampa mamlaka Rais kupeleka fedha katika eneo analoona inafaa.

Alisema sheria hiyo inatoa sharti moja, kwamba Rais kupitia Waziri wa Fedha, atatoa taarifa bungeni juu ya matumizi ya fedha hizo.

Dk Semboja alisema mamlaka hayo yanatambuliwa pia katika Ibara ya 137 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, hivyo Rais hajakosea kuhamisha fedha hizo kwenda kujenga barabara isipokuwa taarifa ya matumizi itolewe bungeni hata kama matumizi yanaonekana.

“Bunge lazima lifahamishwe kuhusu matumizi ya fedha hizo.Kama ni udhaifu wa kipengele hiki, basi unaanzia kwenye Katiba,” alisema Dk Semboja.

Pia, Sungusia alisema, “Fedha ambazo Rais hawezi kuziingilia ni zile zilizo kwenye consolidated fund (mfuko hodhi), nje ya hapo anaweza kufanya lolote,” alisema mwanasheria huyo.

Zamaradi Mtetema Amwagia Sifa Hizi Mwigizaji Riyama Ally

$
0
0
Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa instagram, muuandaaji wa filamu na matantazaji wa kipindi cha Take One  cha maswala ya filamu , Zamaradi Mtetema  amemwagia sifa muigizaji wa kike, Riyama Ally kuwa ni moja ya waigizaji wa kike wenye uwezo na nguvu sokoni.

“Anafahamika zaidi kwa uigizaji wake… MUIGIZAJI wa kike mwenye uwezo wa kusimama kwenye Cover PEKE YAKE bila nguvu ya muigizaji wa kiume na bado filamu IKAUZA… sio kitu rahisi!!! Anafahamika kwa jina la Riyama Ally”,  Zamaradi aliandika hayo mara baada ya kuweka picha hiyo hapo juu ya Riyama.

Riyama naye kupitia ukurasa wake alimshuruku Zamaradi kwa maneno haya;  “Asante sana my dear umekua mstari wa mbele kuni support ktk kazi yangu tangu mwanzo na mpaka sasa bado hujanikatia tamaa ukiamni kabisa ipo siku unacho kiona kwangu na waTanzania watakiona kwa vitendo asante”, liyama alieza hayo kwenye ukurasawake instagram.

MTANGAZAJI Gardner G Habash Kuanza Kusikika Leo Clouds FM

$
0
0
Msimu Mpya Clouds FM
Mwezi huu umekuwa wa mapambano makubwa kati ya vituo vya redio viwili jijini Dar es Salaam, Clouds FM na EFM.

EFM walibomoa kipindi cha Power Breakfast kwa kuwachukua Gerald Hando, Paul James na mtayarishaji wa kipindi hicho, Abel Onesmo huku Clouds FM wakikibomoa kipindi cha Ubaoni cha EFM kwa kumchukua mtangazaji wake wa zamani, Gardener G Habash.

Gardener aka Captain anaanza kazi rasmi Jumatatu hii kwenye msimu mpya wa kituo hicho kwa kuendelea kukiendesha kipindi chake cha zamani, Jahazi.

Mtangazaji huyo anadaiwa kupewa mshahara mnono unaoweza kumfanya kuwa mtangazaji anayelipwa fedha nyingi zaidi kuliko wote Tanzania. Kwanza miongoni mwa vitu alivyopewa ili kurejea tena CMG ni gari aina ya Land Rover Discovery na mashavu mengine mengi.

Kwa upande wa EFM kuna kila dalili kuwa kipindi chao cha asubuhi kitapata nguvu mpya kuanzia wiki hii. Haijulikani ni watu wapi Clouds FM wamewachukua kuziba pengo lililoachwa kwenye Power Breakfast.

CHADEMA Mrudisheni Dr.Slaa Kundini Mtengamae..Hakuna wa Kuvaa Viatu Vyake..

$
0
0
Tuseme tu ukweli,Dr Slaa alikuwa nguzo kubwa ndani ya CHADEMA na UKAWA,tunamhitaji huyu mzee wa kukusanya nyaraka na kutoa matamko yenye facts tupu.

Inaonekana wazi sasa hata CHADEMA hawajui wanasimama kwenye nini hasa!either kupinga ufisadi?hell no hawana huo ubavu kama mwanzo!Je kukosoa serikali ya Magufuli?pamoja na kukosoa tunakosoa hata utumbuaji majipu ambayo yalikomaa.


2020 kuna sera gani UKAWA CHADEMA watatumia?kama ni mabadiliko je kwa Magufuli hamna?utumbuaji majipu TRA,bandari,ndege 3 zinakuja,kiasi flani bila unafki Rais Magufuli anajitahidi ingawa kukosolewa ni kawaida.

Tumlaumu Magufuli kwa kukaa pembeni suala LA uchaguzi Zanzibar,na tuilaumu tume ya uchaguzi kwa kasoro za uchaguzi.

Ni mabadiliko gani UKAWA/CHADEMA tunahitaji hasa kwa sasa?Kujipanga kunahitajika sana!


Bado CHADEMA tunamhitaji Dr.Slaa,mtu ambaye anajua anachokisema,anajua anachokisimamia,chadema haitakiwi kutoa matamko ambayo hata wao wenyewe wanajifunga kwa kauli zao awali.

Ili UKAWA ipate miguu ya kusimama,kukosoa serikali,kufichua maovu ,kutoa tamko zenye kutikisa nchi na zenye facts ili Magufuli atumbue majipu vizuri bado inamhitaji Dr.Slaa.

Mheshimiwa Edward Lowasa hana credibility ya kutoa tamko,Mbowe bila Dr Slaa hana pia,misingi ya CHADEMA ilikuwa kwenye Dr Slaa 30%.

Tunamhitaji Dr.Slaa kuwa ndani ya CHADEMA ili akiongea kuwe na kipya maana akiwa pamoja na Mbowe ,Mnyika,Lissu,Msigwa n.k,wakipaza sauti kwa pamoja wanasikika na watanzania tunawaelewa.

Ili upinzani ukue Tanzania UKAWA NA CHADEMA tunamhitaji Dr Slaa,pia Dr.Slaa hawezi kusimama mwenyewe bila CHADEMA,hakuna chama aliyoijenga kama CHADEMA,nje na hapo hawezi kuaminika.

Viongozi wa UKAWA na CHADEMA washauriane wawe timu moja na Dr Slaa,wanamhitaji.

NAFUNGUA MJADALA.


Viol wa JF.

Breaking News:Rais Dkt. Magufuli Amfukuza Kazi Mkuu Wa Mkoa Wa Shinyanga, Mama Anne Kilango Malecela

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga  mama Anna kilango Malecelakuanzia leo.


Utenguzi huo umetokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Anna kilango Malecela kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa jambo ambalo lilisababisha Ikulu kufanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili ya uchunguzi bado inaendelea.


Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya kubana matumizi kwa ajili ya kununulia madawati, Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa  sana na hali hiyo.


Amesema idadi ya wafanyakazi hewa mkoani Shinyanga huenda ikaongezeka zaidi kwani wilaya mbili za mkoa huo bado zinaendelea kuhakikiwa.


Rais pia ametengua uteuzi wa  Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Abdul R. Dachikwa kumshauri vibaya Mkuu wa Mkoa.

 

Mama Anna Kilango Malecela, ambaye katika awamu ya nne alikuwa Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi na Mbunge wa Same Mashairiki, anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kwanza kuachishwa kazi akiwa amedumu katika nafasi hiyo kwa mwezi mmoja tu..

Mtoto Wa Gadner G Habash Ni Tishio Kwa Urembo (Picha)

$
0
0


Mtoto wa kike  wa mtangazaji  Gardner G Habash anayeitwa Karen ni moto wa kuotea mbali kwa urembo na mwonekano alionao.Ni mwanafunzi wa chuo kikuu jijini Mbeya.

Maneno ya Le Mutuz baada ya Mama yake ‘Anne Kilango Malecela’ kuondolewa kwenye ukuu wa mkoa

$
0
0

Jina lake la kuzaliwa ni William Malecela na jina lake maarufu la mitandaoni ni Le Mutuz ambaye ni mmiliki wa williammalecela.com na jana April 11 2016 aliamua kuwajibu wanaomuandama kutokana na uteuzi wa ukuu wa mkoa wa Shinyanga chini ya Anne Kilango Malecela ambaye ni mama yake  kutenguliwa.


Le Mutuz Aliandika: "Guys naomba kusema hivi nimepigania Rais Magufuli kuwa Rais na ninamuunga mkono kwa juhudi zake za kusafisha uozo hata kama unamuhusu Mama yangu mzazi kwa sababu hata mimi wafanyakazi wa Kampuni yangu wasipofuata masharti yangu kama muajiri ni lazima niwaondoe sasa Nina wafanyakazi 4 ambao ili kuwa nao nilipitia kama watu 100


"Now nimesikia kwamba Mama yangu hakufuata masharti ya muajiri wake so amefukuzwa kazi kwangu sina pingamizi wala ishu na Rais kwa sababu Sheria ni msumeno inatakiwa kukata kote….now naona maneno mengi sana ambayo hayana UKWELI wala Msingi ndani yake


"Nimekaa Majuu Miaka 30 nimerudi Bongo nimesota nimeanzisha Kampuni yangu ya BLOGU YA WANANCHI MEDIA COMPANY LTD na sasa hivi nipo njiani kuhamia kwenye RADIO na TV now katika Maisha yangu sijawahi kuishi kwa kumtegemea mtu ila ninaishi kwa kumtegemea MUNGU‘


"Nilikuwa nafagia Majuu na pia nahangaika Baharini wakati Baba yangu Makamu wa Rais na Waziri Mkuu Leo eti Maisha yangu yataharibika kwa sababu Mama yangu sio RC? hahahaha imenichekesha sana hizi CHUKI guys zitawaua bure mnazitoa wapi? ….I mean Jana nimerudi Nairobi na sasa najitayarisha kwenda South Africa weekend hii na nikirudi ni safari ya Dubai eti Mama yangu kuwa RC wa Wiki Mbili Shinyanga kunahusika na Maisha yangu hapa Mjini Downtown na hizi Safari zangu za kikazi?


"Hahahahahaha imenichekesha sana guys nimeshasema Mara nyingi kwamba ninajua sana kwamba uhusiano wa Public na Watu Maarufu huwa ni feki ila sikutegemea kwamba watu wanaweza kuwa na CHUKI za mpaka kulazimisha kwamba eti u RC wa Mama yangu kwa Wiki Mbili tu unahusika na Maisha yangu hapa Downtown kwamba Nina Ofisi


"Apartment na Kampuni kwa sababu Mama yangu alikuwa RC wa Shinyanga kwa Wiki Mbili tu na sasa Maisha yangu yataisha HAHAHAHAHAH jamani this is the best joke of my life….otherwise guys nimewasikieni ila ninasimama na Rais Magufuli na I feel sorry for my Mum ila ni Kawaida in life na Sheria ni msumeno ….otherwise Lov U guys HAHAHAHAHa and I am Super Humbled U know"– le Mutuz Nation

Kigogo wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) ‘Ajimilikisha’ kiwanja cha shirika.....Naibu Waziri Ampa Siku 7 za Kujieleza

$
0
0

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura, ametoa siku saba kwa Meneja Rasilimali Watu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Neema Mrindoko kujieleza sababu za kuandika jina lake katika kiwanja cha shirika kilichopo Kisarawe mkoani Pwani.


Wambura alitoa agizo hilo juzi alipotembelea kiwanja hicho kilichopo eneo la Kimani ambacho mpaka sasa hakijakamilisha usajili wake na kupewa hati wakati kilinunuliwa na shirika hilo mwaka 2012. 


Kiwanja hicho kimejengwa nyumba za watumishi ambao wangekuwa wakifanya kazi katika kituo cha Kisarawe lakini hazijakamilika.


“Natoa siku saba, mtu huyu awe amenipa maelezo ya kutosha kwa nini hati hiyo imesainiwa na mtu mmoja ambaye ni yeye na ameandika jina lake badala ya jina la Shirika, ina maana alikuwa hajui? Hii ni makusudi,” alisema Wambura.


Wambura alisema mtu huyo amefanya makusudi kwa nafasi yake kushindwa kutambua kukaa miaka yote hiyo bila kupewa hati na kutelekezwa bila kuendelezwa ni ufisadi ambao hauwezi kuvumiliwa.


Awali Wambura alipokuwa akipokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo, Mwanamvua Mrindoko, alisema kiwanja hicho chenye meta za mraba 9,567 kilipimwa na kusajiliwa kwa namba 68,480 mwaka huo huo shirika liliomba kuandaliwa hati.


Mrindoko alisema utaratibu wa ukamilishaji hati ulifanyika na walilipia na kujaza fomu ya maombi ya hati. Ilielezwa kwamba, baada ya TBC kuisaini na kuirudisha Wizara ya Ardhi ilionekana kuwa na upungufu ikarudishwa.


Alitaja upungufu huo kuwa ni hakukuwa na nakala halisi ya kuanzishwa shirika na pia fomu hiyo ilisainiwa na mtu mmoja badala ya wahusika wawili wa TBC na hivyo kukwamisha mchakato wa kupata hati.


Naibu Waziri huyo alipomhoji Ofisa miradi wa wizara hiyo, Macksselin Chota ambaye alikuwepo kwenye ziara, alisema maelezo hayo ni sahihi na kwamba upungufu wanaufanyia kazi. Chota alisema viwanja vingi vya TBC havijapata hati.


Kati ya viwanja 55, viwanja 19 pekee ndivyo vyenye hati. Alisema pia viwanja vingi viko katika migogoro mbalimbali kama vile uvamizi na pia uporaji. Naibu Waziri Wambura aliagiza ndani ya siku hizo saba hati ya kiwanja hicho cha Kisarawe iwe imepatikana.


Alitaka shirika pia lieleze ni namna gani watafanya kuendeleza majengo ambayo yameanza kujengwa hapo. 


“Hii inatia mashaka kabisa, mnachelewesha kupata hati na baadaye viwanja vinainigia kwenye migogoro, unafanya hivyo ili baadaye nyie wenyewe mzunguke, tutashindwaje kuamini hivyo?”Alihoji Naibu Wazi
Viewing all 104702 articles
Browse latest View live




Latest Images