Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Baada ya Anne Kilango Kufutwa Kazi Rais Magufuli Awashukia Mawaziri na Makatibu Wakuu..Adai Wakishindwa Waache Kazi

$
0
0
Dakika chache baada ya kutangaza kumuondoa Anne Kilango Malecela katika nafasi ya Ukuu wa Mkoa wa Shinyanga siku 22 tu baada ya kumuapisha, Rais John Magufuli ametoa onyo kwa Mawaziri na Makatibu wakuu aliowateua.

Akizungumza leo Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli ameeleza kuwa anafahamu wapo baadhi ya mawaziri na Makatibu wakuu ambao wamekuwa wakilalamika ‘chinichini’ kuhusu upatikanaji mdogo wa fedha zinazoelekezwa katika matumizi mengine, yaani OC (Other Charges).

Amemtaka Katibu Mkuu Kiongozi kuwaonya Makatibu Wakuu wanaoanza kulalamika na kudai waongezewe OC na kwamba kama kuna anayeona fedha zinazotengwa ni chache ajiondoe.

“Chief Secretary, huo ndio muelekeo kwa Makatibu Wakuu wengine, waache kudai OC… ninawasikia. Wapo wanaodai OC ni chache, wakiona ni chache waache kazi. Wenzao wabunge wanasema ni nyingi,” alisema.

Rais Magufuli amesema kuwa ametuma watu waweze kuwarekodi mawaziri ambao wanalalamika ‘chinichini’ kuhusu OC akieleza kuwa watu hao bado wanadhani wako kwenye mfumo uliopita.

“Kuna mpaka Mawaziri wengine naona wanalalamika, nawatafutatafuta… nimetuma watu wawarekodi kwa sababu mind set yao bado haijabadilika. Wanafikiri bado tuko kwenye treni hiyohiyo. They will go,” Rasi Magufuli alisema kwa msisitizo.

Awali, Rais Magufuli alitangaza kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela kutokana na kutoa taarifa kuwa hakuna mfanyakazi hewa kwenye Mkoa wake wakati timu ya Ikulu ilibainia uwepo wa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza ya ukaguzi.

Jerry Muro Afunguka Haya Kuhusu Rais John Pombe Magufuli Baada ya Kumfuta Kazi Anne Kilango

$
0
0

Msemaji wa Timu ya Yanga amefunguka kuhusu Rais Magufuli mara tu baada ya kutengua Ukuu wa Mkoa wa Anne Kilango huko Shinyanga....

Ameandika haya katika mtandao wake:

"Huyu ndie Rais ambae Mungu amemsisha katika taifa la Tanzania, Africa na Dunia na kupitia yeye Tanzania itapona, Africa itapona na Dunia itapona, tunakupenda rais wetu"

Wajapan Waikopesha Tanzania Mabilioni ya Fedha

$
0
0


Shirika la maendeleo la kimataifa la Japan (JICA) na Wizara ya Fedha na Mipango wametiliana saini mkataba wa mkopo kutoka Japan kwaajili ya mradi wa maendeleo wa kuimarisha mazingira ya biashara na uchumi nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar Mkurugenzi Mtendaji wa JICA Toshio Nagase amesema mradi huo unahusisha mfululizo wa mageuzi ya sera za maendeleo ambao utaweza kuondoa vikwazo katika mazingira muhimu ya biashara nchini hasa katika viwanda na sekta zinazotoa ajira.

Mradi huo utashughulikia maeneo makuu yenye vikwazo kwa kurahisisha usajili wa biashara na upatikanaji wa leseni, kuimarisha ufanisi na umahiri wa utawala wa forodha hasa katika bandari ya Dar es salaam , kuboresha ufanisi katika usimamizi wa kodi, kurahisisha mchakato ywa usajili wa ardhi, kuboresha upatikanaji wa fedha za mitaji na kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa za kilimo na mazao.

JICA imedhamiria kuunga mkono serikali mpya katika njia mbalimbali ili kuharakisha juhudi za serikali katika kuifanya Tanzania iwe nchi ya viwanda na ya uchumi wa kati kama ilivyoainishwa katika dira ya maendeleo ya 2025.

Mkopo huo una thamani ya fedha za kijapan billion 6 ambazo ni sawa na fedha za kitanzania shilingi bilioni 116 na mradi huo unafadhiliwa kwa pamoja na benki ya dunia.

Clouds FM Yaendeleza Nyakua Nyakua ya Watangazaji na Madj..Wamewachukua Hawa East Africa Radio

$
0
0

Ile Vuta N’kuvute ya vituo vya redio inaendelea na sasa East Africa Radio imekuwa mhanga mpya.

Dj wa kike, Sinyorita na mtangazaji wa The Cruise, Mami wanadaiwa kuondoka East Africa Radio kuanzia wiki hii baada ya kupata dau kubwa kutoka kwa guess what? Clouds FM.

Tetesi hizo zilianza kuvuma tangu wiki iliyopita lakini jana zimeonekana kupata ukweli baada ya wawili hao kutosikika kwenye kipindi cha The Cruise, kitu ambacho si cha kawaida.

Tetesi zinadai kuwa tangu Dj Fetty aache kazi Clouds FM, wamekuwa wakitafuta mtangazaji wa kike anayeweza kuchukua nafasi yake na Mami anaonesha kuwa na caliber hiyo.

Tayari wawili hao wamebadilisha profile zao za Instagram kwa kuondoa kipengele cha kuwa ni wafanyakazi wa East Africa Radio.

Undani Kifo cha Mwanamuziki Ndanda Kosovo Huu Hapa...

$
0
0


Habari zilizolifikia Wikienda mara tu baada ya kutokea kwa msiba huo asubuhi ya Jumamosi iliyopita zilieleza kuwa, Ndanda alisumbuliwa na tumbo ambapo alilazwa kwenye Hospitali ya Mwananyama na baadaye kuhamishiwa Muhimbili jijini Dar.
Akizungumza na Wikienda, mjomba wa Ndanda ambaye pia ni mwanamuziki, Cardinal Gento alisema kuwa, Ndanda alihamishiwa Muhimbili baada ya tatizo lake kushindikana Mwananyamala.

“Nilikesha naye hospitalini, ilipofika asubuhi nikaondoka kurudi nyumbani kwa ajili ya chakula, nikaacha anafanyiwa mpango wa damu maana alikuwa amepungukiwa, lakini muda mfupi baada ya kuondoka, nikapigiwa simu amefariki dunia,” alisema Gento wakiendelea na utaratibu wa msiba nyumbani kwa Ndanda, Madale, Dar.

Kabla ya kukutwa na umauti, historia ya ugonjwa wake inaonesha ilianza mwaka jana ambapo aliripotiwa na Magazeti ya Global kuwa alilazwa kwenye Hospitali ya PKA iliyoko Tegeta, Dar akisumbuliwa na tatizo la kupasuka kwa mmoja wa mishipa tumboni hivyo kutapika damu.

HISTORIA FUPI YA NDANDA KOSOVO
Ndanda aliwika na Bendi ya FM Academia International ambapo alitunga nyimbo za FM Academia baada ya kutoka jela akiwa na akina Nyoshi El-Sadaat, Maluu Stonch, Mulemule FBI, King Blaize, Patcho Mwamba, Gento na wengine kibao waliotamba na Wimbo wa Wajelajela.

Baadaye Ndanda alitoka FM Academia International akaanzisha Bendi ya Stono Musica akiita Wajelajela Original akiwa na Maluu, Chai Jaba, Patcho na wengine. Miongoni mwa nyimbo zake zilizotamba ni pamoja na Binadamu pamoja na rap zake za Kidedea na Kaokota Big G.

Baadaye Ndanda aliachana na Stono Musica akaelekea Marekani kwa shughuli za kimuziki ambazo zilikuwa na mafaniko makubwa. Aliporejea Bongo ndipo akaanzisha Kundi la Watoto wa Tembo kabla ya kuachana na bendi na vikundi na kuwa msanii anayejitegemea.

Chanzo:GPL

Juma Duni Haji Aikosoa CHADEMA Juu ya Muundo Wake

$
0
0

Aliyekuwa mgombea Mwenza wa Rais kwa tiketi ya Chadema, Juma Haji Duni ambaye wiki hii amerejea katika chama chake cha awali cha CUF amekosoa muundo wa uongozi wa chama hicho alichojiunga nacho mwaka jana ili kutimiza matakwa ya sheria na taratibu za uchaguzi mkuu.

Akiongea katika mahojiano maalum na kituo cha runinga cha Azam Two, Duni ameeleza kuwa muundo wa uongozi wa Chadema una urasimu mkubwa unaosababisha kila kiongozi katika ngazi fulani kujiona mkubwa na anayeweza kutoa maamuzi yake.

“Ule muundo wake wa kiutawala ni mkubwa mno, bureaucracy ni ndefu sana kiasi kwamba kila mmoja kule ni kambare ana sharubu. Kule kuna [ngazi]Taifa, kuna Kanda, kuna Mkoa, kuna Wilaya, kuna Jimbo. Sasa uamuzi unaweza ukatoka Taifa lakini mtu wa Jimbo akasema huo uamuzi mimi siukubali,” alisema Haji Duni.

Alisifafanua kuwa muundo huo mrefu wa uongozi unachelewesha na kukwamisha maamuzi yatokayo katika ngazi ya Juu.

Katika hatua nyingine, Mwanasiasa huyo alisisitiza kuwa kuna faida kubwa waliyoipata kutokana na kuunda Ukawa na kwamba ndio njia pekee ya kuiondoa CCM madarakani.

“Kitu kimoja ambacho nakiamini ni kwamba bila Ukawa hatuwezi kuiondoa CCM. Na matokeo ya mwaka huu yameonesha kwamba Chama cha CUF hakijawahi hata mara moja kwa miaka 20 iliyopita kupata viti vingi bara, kupata madiwani wengi Bara na kupata Halmashauri hadi Halmashauri ya Tanga ambayo tumenyang’anywa kwa nguvu,” alisema.

Alifafanua kuwa hali hiyo inaonesha dhahiri kuwa wapinzani wakishirikiana wanaweza kuiondoa CCM madarakani.

Jeshi la Tanzania JWTZ Walioko Kongo Watajwa Kuwa Kati ya Majeshi 35 Bora Duniani....

$
0
0

HONGERA JWTZ KWA KUTOA KIKOSI BORA NA MADHUBUTI CHA KIJESHI DUNIANI
Majarida mbalimbali duniani yamechapisha makala juu ya vikosi 35 bora zaidi vya jeshi duniani huku kikosi cha JWTZ Monusco kilichoko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kikiwemo. .
.
Mwandishi Micky Wren anataja vikosi hivyo kama ni bora zaidi duniani (World's most elite military teams) katika makala yake inauokwenda kwa jina la "35 Most Badass Fighting Units From Arround the world"

Katika makala hii ambayo inapatikana mtandaoni Micky Wren anasema vikosi hivyo vimefundishwa kwa viwango vya juu sana, vina zana bora za kijeshi na vimeandaliwa kwa hali ya juu kabisa kukabiliana na adui katika mazingira yoyote ikiwemo mapigano ya kijeshi, ugaidi na hata kuokoa mateka. Vikosi hivyo 35 duniani vinajumuisha mataifa makubwa duniani kama Marekani, Canada, Uingereza, Holland, Israel, Irish, Australia, Russia, Belgium, Norway, Ufaransa, Tanzania, Indonesia, Iraq n.k.
Vikosi hivyo ni hivi vifuatavyo:- 1. US Navy SEAL

2. British SAS

3. Huntsmen Corps : Danish Special Forces

4. French Special Forces

5. Shayetet 13 (Israeli Special Forces)

6. Irish army rangers

7. Australian SASR

8. MARSOC

9. Canadian counter terrorist group JTF2

10. Russian Special Forces: Spetsnaz

11. Dutch Special Forces

12. SBS

13. Delta Force

Delta-Force

14. Belgian Special Forces Group

15. Norwegion MJK

16. Canadian Joint Incident Response Unit (Nuclear, biological and chemical warfare defence)

17.Marinejegerkommandoen – Norwegian Navy Special Forces

18. French Commando Marine

19. Norwegian Armed Forces’ Special Command

20. New Zealand Special Forces

21. US Army Special Forces Sniper with Remington Modular Sniper Rifle

22. Polish GROM

23. U.S. Special Forces

24. Indonesian Special Forces Command

25. Romanian Special Forces

26. Serbian Gendarmerie

27. Tanzanian (JWTZ) Special Forces In Congo

28. German KSK (Army / Special Forces)

29. German Army Special Forces the KSK

30. ROC (Taiwan) Special Forces with bullet proof face masks

31. Austrian special forces: Jagdkommando

32. Kampfschwimmer (Combat Swimmers) from Germany’s elite SxEK-M special forces

33. Iraqi special forces

34. Korean Special Forces

Gardner G. Habash kaonyesha gari lake jipya siku sita baada ya mkataba mpya

$
0
0

Mtangazaji Gardner G.Habash amerejeaCloudsFM toka alipoacha kuifanyia kazi December 2010, sasa amerudi na kupewa mkataba mpya kuifanya show ileile ya JAHAZI kuanzia saa kumi mpaka moja jioni CloudsFM na ataanza kusikika kwa mara ya kwanza leo April 11 2016.

April 3 2016 ndio ilikua siku ya mkataba wake mpya wa kurejea CloudsFM na April 9 2016Gardner alifurahia gari lake jipya aina ya Discovery kama inavyoonekana kwenye hii video hapa chini.

Watumishi Walioiingizia serikali Hasara Kukiona Cha Moto....

$
0
0

Serikali imekemea na kuzitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha kwamba hazizalishi madeni yasiokuwa ya lazima na kama likitokea deni liwe deni la msingi ambalo lina umuhimu wa kuwepo kwa kujibu na kutatua hoja na shida za wananchi wake.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI George Simbachawene kwenye mkutano uliowakutanisha na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikalim za Mitaa LAAC kwenye majumuisho ya kamati hiyo ambayo ilikuwa ikihoji halmashauri 30 nchini.

Amewakanya wakurugenzi na maafisa fedha wa halmashauri nchini waache mara moja tabia ya kuandika madeni ya uongo ili wajipatie fedha kwa njia isiyo halali ambayo inawasababishia watanzania kukosa haki zao za msingi hasa zile za kuwasaida katika kupata huduma mbalimbali.

Amesema serikali imeanza kuhakiki madeni halali na kuanza kuyalipa na kwa yale ambayo sio halali kulipwa na serikali watawajibishwa watendaji husika hata kama kwa sasa hawapo kazini kwani serikali ina mkono mpana wa kuwachunguza wabadhirifu na kuwachukulia hatua mbalimbali kisheria.

Amesema kauli ya serikali kwa wakurugenzi ambao watahusishwa na ubadhirifu wa fedha na walioshindwa kujibu hoja za mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali ofisi yake itachukua hatua stahiki katika kuwawajibisha wakurugenzi hao waliohusika kwa namna moja ama nyingine.

Sheikh Afungwa Jela Miaka 30 kwa Kubaka Mwanafunzi wa Shule ya Msingi

$
0
0

Mahakama  ya Wilaya ya Kigoma imemhukumu Sheikh wa Msikiti wa Goma, Hassan Bamba (48), kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kukutwa na hatia ya kubaka.


Sheikh huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Kitongoni, mwenye umri wa miaka 14 na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.


Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu wa Mahakama hiyo, Frola Mtariania, baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.


Hakimu Frola, akitoa hukumu hiyo, alisema mahakama inatoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa viongozi wengine wenye tabia ya kikatili kama yake.


Alisema upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi watano, pamoja na kielelezo cha PF3, ambacho kilithibitisha kwamba Sheikh Bamba mshtakiwa alitenda kosa hilo.


Alipotakiwa kujitetea ili kupunguziwa adhabu, akiongozwa na wakili wa kujitegemea Method Kabuguzi, mshtakiwa aliangua kilio na kuiomba mahakama impunguzie adhabu kwa sababu ana familia inamtegemea.


Pia alidai ni kosa lake la kwanza tena shetani alimwingilia. Hakimu Frola alitupilia mbali utetezi huo na kusema: 

"Mshtakiwa ukiwa kiongozi wa dini, kitendo ulichokifanya si cha kijamii maana wewe ndiwe unayefundisha watu kuachana na maovu cha kushangaza unakuwa ndiye wa kwanza kuyatenda maovu.


"Sasa utakwenda gerezani miaka 30 ili ukajifunze tabia ya kuwa kiongozi bora wa dini, kwa sababu huku uraiani umeshindwa kuishi na jamii."


Awali, akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Anita Julius, alidai kuwa Januari Mosi, mwaka huu, saa 4 asubuhi eneo la Ujiji Kigoma, mshtakiwa huyo alibaka msichana huyo.


Ilidaikwa kuwa siku ya tukio mtoto aliyebakwa akiwa na pacha wake, ambao baba yao ni rafiki wa sheikh huyo, walikwenda kwa sheikh huyo kwa ajili ya kuombewa duwa na kufanyiwa dawa kwa ajili ya kufaulu mtihani wa kuingia darasa la saba.


Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, baada ya kufika, Bamba alimtuma mwenzake aende shuleni kuchukua mchanga na ndipo alipomfanyika kitendo hicho yule aliyebaki.


Mwenzake aliporejea, ilidaiwa kuwa alimkuta pacha wake analia na alipomuuliza alimjibu kuwa amebakwa na Bamba. 

Umati mkubwa wa wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji, wakiwamo waumini wa msikiti aliokuwa akiswalisha, ulikusanyika mahakamani na kushuhudia Sheikh huyo anapelekwa jela.

Ali Kiba Afunguka..Nammiss sana Dada yake na Diamond Queen Darleen

$
0
0

Msanii wa muziki Alikiba amefunguka kwa kusema kuwa kuna wakati huwa anamkumbuka sana msanii wa kike ambaye ni dada wa msanii Diamond Platnumz, Queen Darleen.

Ali Kiba na Darleen walikuwa washkaji zamani, ambapo Queen Darleen aliwahi mshirikisha Ali Kiba katika wimbo wake, ‘Wajua’ ambao ulifanya vizuri sana.

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Jumatatu hii, Ali Kiba alifunguka kwa kusema yeye mwenyewe anamkumbuka Queen Darleen sababu kuna vitu walikuwa wanaendana.

“Queen Darleen alikuwa mkongwe katika gemu na tulikuwa na ukaribu sana,” alisema Ali Kiba. “Kiukweli muda mwingi huwa nina ‘M-miss’ sababu mimi na yeye kuna vitu vingi tulikuwa tukiendana kama washikaji. Muda mwingine akili yangu na yake ni kama sawa vile”,

Kwa sasa wawili hao hawaelewani huku watu wakidai hali hiyo imesababishwa na ugomvi uliopo kati ya Diamond na Ali Kiba.

Hakimu Feki Akamatwa Mwanza..Akamatwa Huku Akiwa Ameshatoa Hukumu Ke

$
0
0

Mkazi  wa kijiji cha Kanyama Kata ya Bujora Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Erick Mkundi (23), ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kufanya kazi kama Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kongoro akiwa hana sifa hiyo.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuifanya kazi hiyo kuanzia Januari hadi Aprili 6, mwaka huu alipobainika baada ya kushindwa kujitambulisha kwa Hakimu Mfawidhi wa wilaya hiyo, Edmund Kente, kuwa ni hakimu na bila kuonyesha nyaraka zozote zinazomthibitisha kuwa  na taaluma hiyo, Aidha, ilidaiwa kuwa Mkundi alijikabidhi katika mahakama hiyo na kuanza kuendesha kesi na hadi anatiwa mbaroni, tayari alishatoa hukumu kwa washtakiwa wanne na wengine kadhaa kuwasotesha mahabusu.

Akizungumza jana, mmoja wa watumishi wa mahakama hiyo aliyeomba jina lake lisitajwe kwa madai kuwa si msemaji, alieleza kuwa walifanya kazi na Mkundi kwa miezi minne wakiamini kwamba ni mtumishi halali wa Idara ya Mahakama.

“Mkundi tuliamini ni hakimu halali, kwani alikuwa akiletwa na gari kama mheshimiwa fulani hivi, lakini baada ya kukamatwa Aprili 7, mwaka huu, ndipo tulipogundua ni mfanyakazi ‘hewa’, alisema mtoa taarifa huyo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Magu, Charles Mkapa, alisema Mkundi alikamatwa baada ya polisi kupewa taarifa zake za kufanya kazi bila kibali.

“Kweli tunamshikilia Mkundi tangu Aprili 7, mwaka huu, kwa tuhuma hizo, lakini taarifa kamili mnaweza kuzipata kwa Hakimu wa Wilaya ya Magu, kazi yetu ilikuwa kumtia mikononi mwa polisi,” alisema Kamanda Mkapa.

Awali, ilisemekana mtuhumiwa huyo aligundulika kuwa ‘feki’ baada ya kushindwa kulipa Sh. 40,000 yakiwa ni malipo ya gari alilokodi kwa ajili ya kutembelea kwenda na kurudi kazini pamoja na maeneo mbalimbali.

Habari zaidi zilidai kuwa mtuhumiwa Mkundi baada ya kushindwa kulipa gharama hizo, mmiliki wa gari alitoa taarifa kwa bosi wake wilayani na ndipo alipoanza kufuatiliwa, Aidha, Mkundi ilidaiwa alikuwa akipokea rushwa na zawadi mbalimbali kutoka kwa watu aliokuwa akiwahudumia kimahakama, zikiwamo mbuzi pamoja na fedha kwa lengo la kusimamia kwa ukaribu tuhuma zinazowakabili.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Francis Kabwe, alipoulizwa kuhusiana na tukio la ‘hakimu huyo feki’, alisema hajapata taarifa kamili, lakini atalizungumzia suala hilo leo.

Rais Magufuli " Watumishi Hewa Wamejaa Mpaka Ikulu"

$
0
0

Rais Magufuli asema watumishi hewa wamejaa mpaka Ikulu, Ofisi ya Waziri mkuu, Majeshini etc.Amuagiza Katibu mkuu kiongozi kuunda "task force" yenye ulinzi maalumu ku-deal na watumishi hewa.10% ya mishahara yote nchini hulipwa kwa watumishi hewa.Serikali yapoteza Tshs Billioni 54 kwa mwezi, sawa na zaidi ya Billioni 648 kwa mwaka kulipa mishahara ya watumishi hewa.

Obama: Tulikosea Sana Kuivamia Libya na Kumuondoa Muammar Gaddafi

$
0
0

Rais wa Marekani Barack Obama amekiri kwa mara ya kwanza kwamba serikali yake ilifeli katika kutatua mzozo wa Libya.


Amesema hilo huenda ndilo “kosa kubwa” zaidi alilolitenda wakati wa utawala wake.


Bw Obama amesema Marekani haikua na mpango mahususi wa jinsi taifa hilo litakavyotawaliwa baada ya kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar Gaddafi.


Alisema haya katika mahojiano na runinga ya Fox News kuangazia mafanikio na mapungufu ya utawala wake.


Hata hivyo ametetea hatua ya kuingilia kijeshi nchini Libya. Marekani na Muungano wa NATO zilitekeleza mashambulio ya anga kuwalinda raia baada ya kuzuka maasi dhidi ya Muammar Gaddafi mwaka 2011.


Lakini baada ya mauaji ya kiongozi huyo, Libya ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya makundi ya waasi huku makundi mawili yakiunda serikali na mabunge tofauti.

Katika hatua za kurejesha utulivu serikali ya muungano wa kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imewasili katika mji mkuu Tripoli ili kuanza mipango ya kuongoza nchi ya kurejesha hali ya kawaida.


Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika Novemba na Rais Obama atakabidhi madaraka kwa mrithi wake Januari mwakani baada ya kuongoza kwa mihula miwili.


Chanzo: BBC

WANASHERIA: Hivi ni Sahihi Rais Kudukua Mawasiliano ya Wateuliwa wake??

$
0
0
Mh rais amekiri kuwa ameagiza watu wake kurekodi (kwa lugha ya kitaalamu kudukua) maongezi ya mawaziri na makatibu wakuu ili apate ushaidi wa kuwafukuza.

Nimesoma katiba nzima sikuona sehemu iliyoandikwa eti kulalamika ni kosa la jinai au la kawaida. Sasa huu udukuzi anaoufanya Mh. rais hauvunji haki za binadamu??

Wanasheria nisaidieni,

Kwanini Wanawake Wengi Warembo Wanaishia Kuwa Michepuko?

$
0
0
Ni ukweli kwamba wako wanawake wengi sana ambao wanahesabu kuwa ni baraka na jambo la kumshukuru Mungu kwa kuwaumba wenye sura nzuri na wenye mvuto. Pamoja na ukweli huu, ni wazi na imethibitika kwamba wako wanawake ambao wanahesabu kuzaliwa warembo ni mojawapo ya laana au mkosi kwasababu ya zile hali ambazo wamezipitia hususani katika mahusiano yao ya kila siku na wanaume.

Mara kwa mara kumekuwepo na tabia ya wanaume kutamani sana kuwa kwenye mahusiano na wanawake warembo, na hupenda kuwatongoza hao mara kwa mara ingawa moyoni mwao wanawaangalia warembo hawa kama wasichana wa kula nao raha tu “good time girls” na wala sio wake wakuoa.

Utakubaliana na mimi labda umewahi kuona mwanaume anakuwa kwenye mahusiano na binti mzuri sana kisura na kiumbo tena wanakuwa kwenye mapenzi kwa muda mrefu tu huku huyu binti akijua mbeleni kuna ndoa, ghafla ukija kusikia huyu kaka anaona unapigwa mshangao kuona wala sio yule binti mrembo anayeolewa.

Hii imewaacha mabinti wa aina hii katika maumivu makali sana ya moyo, na wengine wamekata tama na kuamua kujirahisisha ili mraadi maisha yaende. Wengine wameamua kukaa wakitunzwa na waume za watu kwasababu wao wamejithibitishia kwamba kuolewa hakupo.Tafiti zinaonyesha kwamba ukiona mwanaume aliyeamua kukaa muda mrefu na mwanamke mrembo, mara ningi unakuta ni wale wanaume wenye tabia za kisanii “players” ambao hata wao huwatumia mabinti hawa na kuwatelekeza hapo baadae.

Inasemekana imani au mtazamo huu hauko tu kwa wanaume bali hata wanawake wale wenye uzuri au urembo wa kati au wasio warembo kabisa wanajua na kuamini hivyo na mara nyingine huwarushia vijembe wale wanawake warembo kuwa “utachezewa tu na utaachwa na wataolewa wengine”. Na pale inapotokea kwenye mahusiano binti wa kawaida akagundua mpenzi wake wa kiume ametembea au husiana kinyemela na binti mrembo zaidi kuliko yeye, utakuta wakikutana kwenye kupashana au hata kwenye ugomvi wa kuandikiana ujumbe wa maneo, huyu binti wa kawaida humwambia yule mrembo kwamba “we jifurahishe tu ila usiamini kwamba utaolewa, huyu mwenzako anakuchezea tu anajuwa nani wa kuoa”. Unadhani imani hii wameitoa wapi?

Wakati mfumo au mtazamo huu unapoenea au kujirudia zaidi, wanawake hawa warembo au wazuri wa sura na umbo huamini kwamba wanaume wote ndivyo walivyo, wanaamini kwamba wanaume wote huwasogelea ili kujifurahisha kimapenzi tu na baada ya hapo kuwakimbia. Wakati huu wa kusubiria kumpata mwanaume wa kuoa “Mr. Right” ukizidi wanawake hawa huchoka na kukata tama, na hivyo wao sasa huamua kukimbizana na kutafuta mwanaume wa kuwapenda na kutulizana nao.

Tabia hii ya kuwafukuzia wanaume kwa bahati mbaya kuwagharimu sana wanawake hawa kwasababu wanaume wengi wanamtazamo hasi kwa wanawake wa jinsi hii. Wanaume wengi wanaamini wao ndio wanatakiwa kuwa wa kwanza kumtongoza mwanamke na sio mwanamke kuwa wa kwanza kuwatongoza wao, na mbaya zaidi anapokuwa mwanamke mzuri ndio shida huongezeka, wengine wakianza kuambiana “huyu lazima atakuwa mgonjwa anataka kuambukiza wengine”. Hapa unaweza kuelewa ni kwa kiasi gani hali huwa ya kutatiza.

Kwa upande mwingine, wanawake hawa wanaoonekana wazuri wa umbo na sura, sio halisi kama wanavyoonekana. Kwa mbali ni kweli mwanaume yeyote atavutiwa nao lakini jinsi unavyowakaribia na kuwafahamu unagundua mengi yanayohuzunisha na kuogopesha kuishi nao. Unagundua kuwa uzuri mwingine umeongezewa kutoka madukani zaidi na sio ulio halisi. Mara nyingine uzuri huu na ile hali ya kuonekana ni wagharama sana huwaogopesha wanaume wasio na kipato kikubwa na kwahiyo wanaume hawa wakishapata kabahati ka kufaidi penzi mara moja au mbili wanakimbia tena kwa kasi wakihofia kukamuliwa kiuchumi, ingawa mara nyingine hofu yao hii huwa sio ya kweli. Inasemekana baadhi ya wanawake wa aina hii huwekeza zaidi kwenye kuonekana wazuri na walimbwende ili kuficha au kufunika baadhi ya mapungufu yao.

Wanaume wengi walioulizwa sababu za kuwatumia na kuwatelekeza wanawake wa jinsi hii walisema kuwa, kwa kutembea, kuonekana nao au kufanya nao mapenzi, wanaume hawa hujihisi sifa sana, hususani wanapoonekana na wanaume wenzao, yani ni kama vile timu ndogo iliyopata nafasi kucheza katika kombe la dunia. Unajua tena wanaume wanavyopenda kujionyesha wanapokuwa na wanawake wazuri mbele ya macho ya wanaume wenzao.

Wamesema kwamba wanapowaza kuishi na wanawake hawa kama mume na mke, huwa wanazidiwa na hofu ya kuelemewa au kujihisi kutokuwa salama “sense of insecurity”. Mioyoni mwao wanahisi kwamba kama wanaume wenye hela wamekuwa wanamfuatilia kwa kasi kubwa hivi mwanamke huyu, vipi nikishaoana naye?? Si ndiyo kila siku kusuguana na kukorofishana vishawishi vinapozidi? Je nitaweza kustahimili?

Wanaume wengine walioulizwa walijibu kwamba, wanawake wa jinsi hii ni wa gharama sana, sio rahisi kuwaweka mjini na kuhakikisha wanaishi maisha yao ya kawaida kama hauna fedha ya kutosha. Hata wale wanaume wachache waliokuwa na hao wanawake kwa muda wa maswali haya wameeleza jinsi wanavyohisi wanatumia fedha nyingi na yamkini zaidi ya wanavyojiweza.

Wanawake wa aina hii watahitaji mitoko ya nje ya mji, sehemu zilizojitenga, sehemu za faragha ambazo ni za bei ghali, wanataka zawadi za gharama, ukitaka kuwapa zawadi za kushtukiza “surprise” basi ujipange, sio vitu vya kitoto vitakavyomsisimua aweze kukwambia “waoooooow…this is wonderful” hapo lazima ujipinde mfukoni haswa.

Ukitaka kuwatoa nje kwa ajili ya chakula cha jioni basi lazima kwenda maeneo wanayoenda watu maarufu, mkitaka kwenda kupumzika kidogo nje ya nyumbani basi uwaambie wachague wao wapi pa kwenda, na hapo utakapotajiwa ni pa gharama kubwa sana, na imeelezwa kwamba pamoja na mambo yote haya ya gharama kubwa bado huko wapenzi hawa wanapoenda msichana huyu anaishia kuonekana ni mwanafunzi asiyejua tendo la ndoa kabisa tofauti na hali aliyoionyesha “poor perfomer”, wanaume wengine wanasema inaonekana kama kupoteza tu pesa, unaishia kutokufurahia penzi lenyewe.

Na wengine wameenda mbali zaidi kueleza kwamba hata unapotaka kuzaa na mwanamke wa jinsi hii basi yeye anataka mtoto mmoja au wawili tu akiogopa asije kuliharibu umbo lake, tofauti na kiu ya mwanaume ya kupata watoto zaidi ya wawili. Imeelezwa kuwa hata ujuzi wa kupika kwao ni shida maana kutwa kucha wako “bize” na sura zao, na hata ukikaa nao sio watu wakufurahisha zaidi ya kutumia tu hela zako “they are boring”.

Pamoja na uchunguzi huu na ukiangalia hali halisi ya maisha yetu ya kila siku tena katika jamii tofauti utagundua kwamba wanaume kiu yao sio kuoa wanawake wenye umaarufu, au wenye kujulikana sana, au walio warembo kupindukia, bali wanaume wanapotaka kutafuta mke wa kuoa wanaangalia tabia na haiba zilizojificha, wanauliza tabia ya huyo msichana, wanataka kujua anavyohusiana na watu, wataangalia nyendo zake kuanzia wakati anasoma.

Ni ngumu kuwakuta wamenaswa na aina ya wanawake ambao wanataka kuonekana wakati wote, wanataka wajulikane kuwa wao nao wapo kwenye makundi ya watu, la hasha. Kiu zao ni kuwa na mwanamke ambaye atakuwa mke anaye leta furaha nyumbani, anaye sikiliza, anaye weza kushauri na kushaurika, aliyeko tayari kufundishika sio kuwa mwalimu kwenye kila kitu, anayeweza kuandaa mapishi mazuri yatakayo wafurahisha watoto na mume wake, sio kila siku kuelekeza kipikwe nini wakati yeye analinda kucha zake zisiharibike.

Hivi umewahi kujiuliza kwanini watu wengi waliooa wakiwa na michepuko, hiyo michepuko ni mabinti warembo na walimbwende ila hawajaolewa, hivi hujajiuliza kwanini hawajaolewa? Na hata wengine wakiolewa hizo ndoa kila siku tia maji tia maji, wataachika leo na kuolewa kesho na kuachika kesho kutwa nakuolewa tena mtondogoo.

Unadhani hawa wanaume wanaoenda kwa hao wanawake ni kwamba hawajui wanachokitaka? utashangaa hata umpe mapenzi gani bado hawezi kukwambia atakuoa, ingawa yuko tayari akupangishie nyumba au hata akujengee lakini ulale huko mwenyewe, yeye anaenda kulala na mke wake. Ushauri wangu wa bure kwa wanawake wa jinsi hii; badilikeni tabia zenu, jitihada mnazotumia kwenye kucha na sura zenu ziwekeni kwenye kushuhulikia tabia na haiba zenu, la sivyo mtasubiri sana tu.

Dr. Chris Mauki

UDSM & University of Pretoria. SA

chrismauki57@gmail.com

Mishahara Hewa, ilikuwa ikiliwa na nani? Ni Vema Tukawajua na Wachukuliwe Hatua

$
0
0
Naomba mnisaidie kidogo,

Ni nani hasa aliyekuwa anakula hii mishahara hewa, ni wafanyakazi waliofukuzwa /kuachishwa kazi/kufariki nk na fedha kuendelea kuingia kwenye akaunti zao au viongozi ambao walikuwa wanajua fulani amefariki /amestaafu n.k na kujipakulia hiyo mishahara?

Je,mbinu gani ilikuwa inatumika?

Madudu Kibao Yabainika Katika Uhakiki wa Madeni ya Watumishi Wanayoidai Serikali

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Kassim Majaliwa amesema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) , amefanya uhakiki wa madeni yanayodaiwa serikali na watumishi na kubaini madudu kibao.

Amesema madai mengine yameonyesha mashaka ambapo amewataka wakurugenzi wa Halmashauri na Wakaguzi wakuu wa ndani kujiridhisha ukweli wa madai hayo kabla ya kuyafikisha serikalini kwa ajili ya malipo.

“Madai mengine yanatia mashaka, sisi hatuhitaji kuletewa madeni ya hovyo hovyo ni vema Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakaguzi wa ndani wakajiridhisha kabla kuyapeleka serikalini kwa ajili ya malipo.

"Madeni mengine ya ajabu, mfano unakuta mtumishi mmoja anaidai serikali sh. milioni 30,  jambo ambalo ni gumu hata kama alihamishwa haiwezekani kufikia kiwango hicho, pia kuna baadhi ya majina yamejirudia mara nne,” amesema.

Waziri Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa hospitali ya wilaya ya Ruangwa alipotembelea Hospitali hiyo wakati akiwa katika ziara ya kikazi iliyolenga kukabidhi msaada wa vifaa tiba alivyovitoa kwa ajili ya hospitali hiyo.

Amesema kuwa serikali italipa madeni yote inayodaiwa baada ya kumaliza kuyafanyia uhakiki, hivyo aliwaomba watumishi kuwa na subira wakati serikali ikiendelea zoezi la kuyahakiki ili kuweza kulipa deni sahihi inalodaiwa.

Awali akisoma taarifa ya Idara ya afya kwa Waziri Mkuu, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Dk. Japhet Simeo amesema idara ya afya inakabiliwa na madeni ya watumishi ambayo ni sh. milioni 109,662,483.

Amesema madeni hayo yametokana na likizo, matibabu, uhamisho wa ndani na nje ya wilaya, gharama za mizigo kwa watumishi waliostaafu, ambapo  halmashauri imejipangia utaratibu wa kulipa madeni hayo pindi inapotokea fedha kutoka serikali kuu.

Hata hivyo kasi ya mtiririko wa fedha ni ndogo ukilinganisha na mahitaji halisi ya maslahi ya watumishi ambapo Halmashauri inawapongeza na kuwapongeza watumishi wa Idara ya afya kwa kuendelea kuwa wavumilivu na kuwahudumia wananchi.

Dk. Simeo amesema halmashauri inawapongeza Rais Dk. John Magufuli na Waziri Mkuu, Majaliwa kwa juhudi kubwa wanazozifanya kuongeza mapato nchini, ambapo wana matumaini kuwa watumishi wataboreshewa maslahi na stahiki zao ili kuchochea motisha kiutendaji.

Katika hatua nyingine Dk. Simeo alizungumzia upatikanaji wa dawa, alisema ambao  umeongezeka kutoka asilimia 30 mwaka jana na kufikia asilimia 80 mwaka huu dawa muhimu katika vituo vyote vya kutolea huduma ambavyo viko 32.

Mwanamuziki Lady Jay Dee Akutana na Ray C Baada ya Miaka Sita...Afunguka Mazito

$
0
0
Mwanamuziki Mkongwe Lady Jay Dee Amefunguka haya kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kuonana na Mwanamuziki Ray C ambae yuko katika harakati za kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya........

From @jidejaydee - 
Thank you for visiting me doll( Ray C)
A message of Hope:
Kila Mtu Anapitia Magumu Katika Maisha
Kwa Njia Tofauti
Hakuna Jaribu Lisilo na Mlango wa Kutokea, Amini na Amua
Nakupa Moyo na Mungu Akusaidie
Kwa Yote Unayopitia
Akuondolee Akuepushie
Na Akupe Kufahamu na Kukiri Mabaya 🏼🏼🏼🏼🏼🏼
Watu Wanakupenda
Nakumbuka Tulivyo Anza
Kimtindo nai miss Competition
Pls Come Back
Naamini Bado Unayo Nafasi
Binti Amka Jikaze Anza Mwendo
Umrembo na Bado Wang'ara 🏻🏻🏻🏻🏻🏻🏻🏻🏻🏻
Ni baada ya miaka 6
Tangu kuonana mara ya Mwisho
Story nazo ni ndefu na nyingi

Ombi:
Tuheshimu na kuhurumia matatizo ya wengine, tafadhali msi comment vibaya wala kwa kejeli.
Lolote linaweza kumfika yoyote
SAA yoyote
Tuonyeshe Mapenzi


Akaunti za Instagram za Vanessa Mdee na Idris Sultan zawa ‘Verified’

$
0
0
Vanessa Mdee na Idris sultan wameongezeka kwenye orodha ya mastaa wachache Afrika ambao akaunti zao za  mtandao wa kijamii wa Instagram zimekuwa ‘Verified’
vee11

“We live in a world of blue ticks and purple hearts 💜 #Niroge” Vanessa Ameandika kwenye Instagram yake.
Akaunti zao zimekuwa verified na kuwekewa kitiki cha blue kuonesha kuwa ni akaunti halali.
iddy

“This is to all my beautiful fans...... #WataelewaTu#MeAmBiziii #HollywoodISeeYou#HuuMchezoHautakiHasira” Idris ameandika kwenye Instagram yake.
Vee na Idris wameungana na Flaviana Matata na Diamond Platnumz kwenye orodha ya mastaa wachache ambao akaunti zao za Instagram zimukuwa Verfied.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images