Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live

Kumbe LUGUMI Anasupply na Vifaa vya Polisi Kama Uniform, Boot na Tape za Polisi...Kweli Tanzania Ilikuwa Shamba la Bibi

0
0
Inasemekana Lugumi hakuwa ana tenda ya finger print peke yake kwa Jeshi la Polisi kumbe alikuwa ana supply na vifaa vya polisi kama uniform, boot na tape za polisi..

Wanasema kazi hiyo alikuwa akiifanya na mke wa aliyekuwa IGP Said Mwema, na huyo Lugumi Amemuoa Mtoto wa Said Mwema

Angalia huyo picha juu kwa makini uone hiyo tape ya Polisi yenye details za Lugumya.


Kusoma zaidi Ingia Hapa

Faiza Ally Afunguka Vilivyo Kuhusu Mbunge Sugu Kuoa Mwanamke Mwingine

0
0

Muigizaji wa Bongo movie na 'baby mama' wa Mbunge wa Mbeya Mjini maarufu kama Sugu afunguka Instagram kuhusu mapenzi yake kwa mzazi mwenzie na kutoa tambo za kutosha kuwa hata Sugu akioa nyumba na mali zote za mbunge huyo ni za mwanae Desderia Sasha na hivyo akikua atarudi kwa baba yake.


Faiza pia aliendelea na kumponda mtarajiwa wa Mbunge huyo kuwa ameshawahi kuolewa na kuachika hivyo hawana tofauti.


Sasa Faiza, wivu wa nini jamani?...wewe hutakagi kuwa 'judged' ila unavyomjudge mwenzio unajua kilichomfanya akatoka ndoani?

Hama Hama ya Watangazaji wa Radio za Bongo.. Maana Yake ni Nini!?

0
0
Watangazaji sasa wanabadilisha vituo kama team za soccer.

Gadner katoka Efm kaenda Clouds.

PJ na Hando wametoka Clouds wameenda Efm.

Jabir saleh na Bi Hindu wametoka Times fm wameenda Efm.

Dj Senyorita na Mami wametoka East Africa radio wameenda Clouds.

Kuna tetesi Clouds sasa wanamtaka Kitenge kwa pesa yoyote anayotaka, Kitenge akichukuliwa na Clouds Shafii amesema ataondoka na Efm wanataka kumchukua kwa pesa ndefu.

Ni mwendo wa kutangaziana dau.

Hapa haieleweki ni jeuri ya pesa?

Stunt za kuongeza kusikilizwa?

Tasnia chovu ya utangazaji inakua?

Nani anaefaidika na hii game?

Au umjini mjini?

Efm wanakwambia huu mchezo hauitaji hasira!

Tusubirie kuona mwisho wa huu mchezo au labda ndio mwanzo wa sinema.

Mjini kuzuri sana!

Chanzo: Hapa

Majambazi Watatu Wauawa na Jeshi la Polisi Kahama, Shinyanga

0
0
Jeshi la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga limefanikiwa kuuwa Majambazi watatu yaliokuwa yamevami duka la mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Emmanuel Mukumbo na kumuua kwa risasi ambapo majambazi hayo yalianza kujibizana risasi na Polisi baada ya raia wema kuijulisha polisi na kufika katika eneo la tukio.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kahama Bw.Vita Kawawa, amesema katika tukio hilo raia mwingine mmoja alipigwa risasi na majambazi hao na kupoteza maisha wakati akipelekwa hospitali huku akilipongeza jeshi la polisi kwa kazi nzuri waliyoifanya.

Akizungumza kwa njia ya simu kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Dismas Kisusi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la polisi punde wanapoona dalili zozote za kiuhalifu zinafanyika.

Katika tukio hilo jeshi polisi limefanikiwa kukamata bunduki mbili moja aina ya Short Gun na moja ya kivita aina ya Uzgun, bomu la kutupa kwa mkono, kisu cha kijeshi,risasi sitini,mkandawa kijeshi na magazine mbili za bunduki.

Breaking News: Mbunge Saed Kubenea Apatikana na Hatia Mahakani...Amehukumiwa Kifungo Hichi

0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtia hatiani Mbunge wa Jimbo la Ubungo Saed Kubenea kwa kosa la kutoa lugha chafu ya matusi kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mbunge huyo amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu nje kwa masharti ya kutorudia kosa la namna hiyo katika kipindi hicho na endapo atarudia kosa hilo basi atakuwa amevunja masharti ya kifungo hicho na kustahili kifungo cha gerezani.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema baada ya kupitia ushahidi na vielelezo vilivyotolewa mahakamani hapo mtuhumiwa amepatikana na hatia baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha bila chembe ya wasiwasi kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo.

Hukumu hiyo imefuatia ushahidi uliotolewa na mashahidi watatu kwa upande wa mashtaka wakiongozwa na Mheshimiwa Makonda huku upande wa utetezi ukiwa na mashahidi watatu akiwemo Kubenea mwenyewe.

Saed Kubenea alikuwa anakabiliwa na shtaka la kutoa lugha chafu kwa Makonda wakati wakiwa katika Kiwanda cha Ushonaji na Usafirishaji wa nguo cha Tooku Garments Co. Ltd kilichopo maeneo ya Mabibo External baada ya kutokea kutokuelewana baina ya viongozi hao walipokwenda kutatua mgogoro wa wafanyakazi wa kiwanda hicho na wamiliki.

Katika kesi hiyo, Kubenea anadaiwa kumtolea lugha chafu Makonda kuwa ‘wewe kibaka, mpumbavu, mjinga na cheo chenyewe cha kupewa tu’.

Upande wa mashtaka ulikiri kutokuwa na rekodi yoyote mbaya ya mtuhumiwa huyo na kwamba hili ni kosa lake la kwanza lakini wakaiomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine.

Awali, akijitetea baada ya kutiwa hatiani Kubenea alisema, hakwenda pale kwa nia mbaya ya kutukana bali alikwenda kutatua mgogoro uliokuwepo baina ya wafanyakazi na wamiliki wa kiwanda hicho na kwamba hakuwa na miadi yoyote na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ya kukutana pale.

Akijitetea zaidi Kubenea aliiomba mahakama impatie adhabu nafuu kwakuwa yeye ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo ameajiriwa kuwatumikia wananchi.

Mwanasiasa wa Upinzani Auawa Nairobi Kenya..

0
0
Mwanasiasa wa upinzani ameuawa kwa kupigwa risasi nje ya nyumba yake katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.

Stephene Mukabana ambaye ni kiongozi wa vijana wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM), aliuawa usiku wa jana wakati alienda kumsaidia mtu mmoja aliyekuwa akiporwa na kundi la watu sita kwa mujibu wa gazeti la Standard nchini humo.

Pia gazeti la Standard lilimnukuu gavana wa Nairobi Evans Kidero akisema kuwa kundi la wauaji limfuata na kumuua mwanasiasa huyo wa umri wa miaka 42.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yapongezwa Kwa Kuendesha Uchaguzi Mkuu wa 2015 Kwa Amani

0
0

Kamati ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala imeipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kufanikisha kuendesha Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015 vizuri na kuiacha nchi ikiwa na Amani, utulivu na Usalama.

Hayo yalisemwa jijini Dar ess Salaam jana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Najma Murtaza Giga walipokutana na Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere convention Center katika kikao mahsusi cha Kupitia Bajeti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Aidha, pongezi hizo kwa NEC zilitolewa na wajumbe wa pande zote mbili yaani wa Chama tawala na wale wa upinzani wa kamati hiyo kwa nyakati tofauti.

Baadhi ya wabunge hao ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mheshimiwa Najma Murtaza Giga(CCM), Twahir Awesu Mohammed (CUF) na Nassor Suleiman Omar (CUF).

Alisema ni jambo la heri sana pale ambapo taasisi ama mtu anafanya kazi ya kutukuka kupewa sifa yake na kupewa moyo ili aendelee  na moyo wa kufanya kazi kwa bidii na hatimaye kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi  si tu kwa manufaa ya taasisi yake bali hata kwa Taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhan aliiambia kamati hiyo kwamba haikuwa  kazi rahisi kuendesha na kusimamia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na Nchi ikaendelea kuwa na amani na utulivu kwani ushindani wa kisiasa ulikuwa mkubwa kiasi cha kutishia maisha ya watanzania.

“Tulijitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kufuata Sheria Kanuni na taratibu za kusimamia Uchaguzi pamoja na kwamba Bajeti ilikua haitoshi hasa wakati tunaanza zoezi la Uandikishaji wa Wapiga Kura kwa kutumia Teknolojia ya BVR ambapo tulilazimika kuandikisha wapiga Kura kwa kuhamahama” Alisema Kailima.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Uratibu na Bunge Jenista Mhagama aliwashukuru wabunge kwa niaba ya Serikali kwa jinsi walivyothamini na kutambua Kazi kubwa iliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kuahidi kufikisha Serikalini mawazo ya kuitafutia Tume fedha kwaajili ya Tume kuzipatia Asasi za Kiraia zinazotoa Elimu ya Mpiga Kura kwani lilijitokeza suala la Ukosefu wa Fedha za Kuendeshea Elimu hiyo.

Bajeti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 ni jumla ya Tsh 4,830,537.167/= ikiwa ni fedha za matumizi ya kawaida OC Miradi ya Maendeleo pamoja na Mishahara ya watumishi.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ulifanyika tarehe 25 Oktoba ambapo aliyekua Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mh.Dkt John Pombe Magufuli aliibuka Mshindi.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya April 14, Ikiwemo ya Lugumi Atoroka Nchini...

0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya April 14, Ikiwemo ya Lugumi Atoroka Nchini...

SOMA Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Katika Magazeti leo....

Walio ‘Benchi’ Kusubiri Rais Magufuli Awapangie Kazi Mpya Waongezeka

0
0
Uamuzi wa kutengua uteuzi wa makatibu wakuu, wakuu wa mikoa, wilaya na watumishi wengine waandamizi kwa maelezo kuwa watapangiwa kazi nyingine, inazidi kuongezeka baada ya Rais kumvua Anne Kilango ukuu wa mkoa na kuahidi kumpangia kazi nyingine.

Mpaka kufikia jana, makatibu wakuu sita na wakuu wa mikoa na wilaya kumi walikuwa wamevuliwa nyadhifa zao na kuelezwa na mamlaka zao za uteuzi kuwa watapangiwa kazi nyingine huku nafasi zao wakipewa watu wengine.

Utenguaji wa uteuzi wa makatibu wakuu sita na mkuu mmoja wa mkoa umefanywa na Rais John Magufuli tangu alipoingia madarakani Novemba 5, mwaka jana huku Jakaya Kikwete, aliyeongoza Serikali ya Awamu ya Nne, akitengua uteuzi wa wakuu tisa wa wilaya na mikoa ambao mpaka sasa hawajapangiwa kazi nyingine.

Kitendo cha kuwaweka pembeni wateule hao wa Rais kimezua maswali mengi, ikiwa ni pamoja na utaratibu wa ulipwaji wa stahiki mishahara na posho mbalimbali hasa kwa wale wanaokaa muda mrefu bila kupangiwa kazi nyingine.

Baadhi ya wachambuzi waliozungumzia suala hilo walisema licha ya mamlaka ya uteuzi ya watumishi hao kuwa chini ya rais, hoja ya kupangiwa majukumu mengine haraka kwa lengo la kuokoa fedha haikwepeki.

Kwa mujibu kwa kifungu cha 13 (6) cha Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2014, mtumishi wa umma wa ngazi ya uteuzi wa Rais, akivuliwa wadhifa, mshahara wake wa mwezi utabaki kama ulivyo isipokuwa posho aliyokuwa akipokea wakati wa uteuzi itapangwa kulingana na matoleo ya ofisi kuu ya Utumishi wa Umma.

Pia kifungu cha 20 (1) cha kanuni hizo kinasema: “Iwapo mtumishi wa ngazi ya uteuzi wa Rais, atakuwa hayupo katika nafasi yake ya utumishi, nafasi yake itashikiliwa na mtumishi mwenye wadhifa sawa na wake au anayemfuatia kwa idhini ya Katibu Mkuu au mkuu wa taasisi au Katibu Mkuu Kiongozi kulingana na wadhifa wa anayeondoka.”

Hata hivyo, makatibu wakuu walioondolewa nafasi zao zilijazwa na wengine walioteuliwa na Rais Magufuli, huku wakuu wa wilaya na mikoa pia nafasi zao zikijazwa na wengine na hivyo kuwafanya wote kuendelea kusubiri majukumu mengine.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Angela Kairuki, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, hakutaka kuzungumzia suala hilo.

“Mkuu wa utumishi wa umma ni Katibu Mkuu Kiongozi. Yeye ndiye atakuwa na nafasi nzuri ya kusema hilo, maana mimi nikisema nitakuwa kama naingilia.”

Jitihada za kumpata Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi hazikufanikiwa baada ya kutafutwa kwa wiki mbili mfululizo bila kupatikana.

Katibu mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi (Tucta), Nicolaus Mgaya alisema ni jambo linaloweza kuzua mjadala iwapo watumishi hao watakaa muda mrefu bila kupangiwa majukumu mengine.

“Kwanza wanalipwa fedha za umma bila kuwajibika popote. Ni vyema uteuzi wa mtu ukitenguliwa isichukue muda mrefu awe amepangiwa majukumu mengine,” alisema Mgaya.

“Inawezekana mtu akalipwa mpaka siku anastaafu akifikisha miaka 60. Na ikitokea hivyo na pia kama rais hajamstaafisha mtu huyo ana haki pia ya kulipwa na ataendelea kulipwa tu.”

Alisema litakuwa jambo jema kama uteuzi mpya utafanyika haraka iwezekanavyo ili kuondoa sintofahamu iliyopo sasa kwa kuwa jambo hilo lisipotazamwa kwa kina, nchi itajikuta inawalipa mishahara watumishi wanaosubiri kupangiwa kazi nyingine.

Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu Ruaha, Profesa Gaudence Mpangala aliungana na Mgaya na kufafanua kuwa jambo hilo si sawa na linahitaji kukumbushwa mara kwa mara.

Alisema ili kuondokana na suala hilo, inapaswa watendaji hao kupangiwa majukumu mengine muda mfupi baada ya kuwekwa kando.

“Ninachokiona ni kama kila Serikali kutaka kuwa na watu wapya. Rais Magufuli ameingia madarakani na inaonekana wazi kuwa anataka kufanya kazi na watu wapya. Tazama makatibu wakuu waliowateua hivi karibuni na hata kitendo cha kumuondoa Sefue,” alisema Mpangala.

Utenguaji wa uteuzi

Tangu aingie madarakani, Rais Magufuli amekuwa akisimamisha, kutengua uteuzi na kutimua watumishi kadhaa waandamizi na kati ya aliotengua uteuzi wao, alisema kuwa atawapangia kazi nyingine.

Desemba 30, mwaka jana Rais Magufuli alifanya uteuzi wa makatibu wakuu na naibu 50 wa wizara, huku akiwaacha baadhi yao ambao alisema watapangiwa kazi nyingine.

Walioachwa ni pamoja na Dk Donnan Mmbando (Afya), Balozi Liberata Mulamula (Mambo ya Nje), Omari Chambo (Nishati na Madini), Jumanne Sagini (Tamisemi) na Joyce Mapunjo (Afrika Mashariki).

Katika orodha hiyo, yupo Balozi Ombeni Sefue, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, ambaye alikuwa mteule wa kwanza wa Rais Magufuli kuondolewa Ikulu akimpisha Balozi John Kijazi.

Rais alisema atampangia kazi nyingine Balozi Sefue, lakini hadi sasa bado haijatangazwa kazi aliyopangiwa.

Wengine ambao uteuzi wao ulitenguliwa ni aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaban Mwinjaka kupisha uchunguzi baada ya kutajwa kuhusika katika matumizi mabaya ya Sh13 bilioni kwenye Shirika la Reli Tanzania (TRL).

Mwinjaka alikuwa kiongozi wa kwanza wa ngazi ya Katibu Mkuu kuondolewa na Rais Magufuli. Uteuzi wake ulitenguliwa wakati Dk Magufuli alipotimiza mwezi mmoja tangu awe Rais wa Awamu ya Tano.

Mbali na Rais Magufuli kuwaweka pembeni watumishi hao, Kikwete naye aliwaweka pembeni watumishi kadhaa kwa sababu tofauti.

Desemba 7, 2014 Kikwete aliteua wakuu wapya wa mikoa, akiwapandisha cheo wakuu wa wilaya na kuwaacha watatu akieleza kuwa watapangiwa kazi nyingine.

Walioachwa kwa ahadi ya kupangiwa kazi nyingine ni Dk Christine Ishengoma (Iringa) na Kanali Fabian Massawe (Kagera). Katika panga hilo pia alikuwepo Kanali Joseph Simbakalia aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mtwara, ambaye tayari ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzi ya Nje (EPZA).

Pia Februari 19, 2015 Kikwete alihitimisha uteuzi wa nafasi za kisiasa za mkupuo kwa kuwang’oa wakuu wa wilaya 19, kuteua wapya 27, kuhamisha 64 na 42 wakibaki kwenye vituo vyao.

Katika kundi la wakuu wa wilaya 19 waliong’olewa, uteuzi wa wakuu 12 ulitenguliwa na saba ilielezwa kuwa watasubiri majukumu mapya.

Wakuu saba wa wilaya waliobadilishiwa majukumu ni Brigedia Jenerali Cosmas Kayombo, aliyekuwa Simanjiro, Kanali Ngemela Lubinga (Mlele), Juma Madaha (Ludewa), Mercy Silla (Mkuranga), Ahmed Kipozi (Bagamoyo) na Elinas Pallangyo (Rombo).    


Rais Magufuli Apekua Mafaili ya CAG wa Jakaya Kikwete.....

0
0
Kilio cha muda mrefu cha wabunge na ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kimesikika.

Kilio hicho kilikuwa ni kufanyia kazi taarifa na mapendekezo mbalimbali dhidi ya ufisadi, usimamizi mbovu, ukiukwaji kanuni na malipo ya wafanyakazi hewa, lakini hakikuwa kikifanyiwa kazi hadi baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani.

Rais John Magufuli sasa ameanza kupekua mafaili aliyoyakuta mezani yanayofichua ufisadi na kupendekeza njia bora ya kudhibiti, akifanyia kazi kwa kutumbua majipu na kuweka kwenye mkakati mapendekezo hayo, hasa yaliyotolewa na CAG.

Uchunguzi wa Mwananchi umebaini hatua zilizochukuliwa na Serikali ya JPM ni matokeo ya kufanyia kazi mapendekezo yaliyomo katika ripoti za CAG za kuanzia mwaka 2009/ 2010 na 2013/ 2014 ambazo zilitolewa wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne.

Ripoti hizo zinapendekeza namna bora ya kuongeza vyanzo vya mapato pamoja, kudhibiti na kuratibu matumizi ya fedha, likiwamo suala la upunguzaji wa mishahara ambalo limeibua mjadala tangu Rais Magufuli alipolitamka wakati akiwa mapumzikoni Chato mkoani Geita.

Ripoti hizo zilikuwa zikifanyiwa kazi nusunusu au kwa shinikizo la Bunge la Jamhuri ya Muungano, kiasi cha CAG kuonekana kama anakata tamaa.

“Ninapenda kuifahamisha Serikali kwamba, mapendekezo ninayoyatoa mara kwa mara yana lengo la kuhakikisha kunakuwa na hatua madhubuti na umakini katika kuimarisha ukusanyaji na utumiaji wa mapato na rasilimali za Taifa,” anasema CAGk katika ripoti ya mwaka 2013/ 2014.
“Mapendekezo hayo pia yanalenga kuhakikisha matumizi ya fedha za umma yanaidhinishwa na wenye mamlaka na fedha zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Kwa hali hiyo, kwa kuzingatia sheria na kanuni katika kutumia rasilimali za Taifa; thamani ya fedha, tija na ufanisi vyaweza kufikiwa.
“Kwa misingi hiyo, ninaona ni vyema kuyarudia tena mapendekezo niliyoyatoa katika ripoti zilizopita ambayo hayajatekelezwa au yametekelezwa kwa kiwango kidogo na Serikali, Bunge, bodi za wakurugenzi na watendaji wakuu wa mashirika ya umma.”

Baadhi ya mapendekezo ya CAG ambayo hayakuwahi kufanyiwa kazi ni kuweka usawa katika marupurupu yatolewayo na mashirika na taasisi nyingine za umma, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kutumia mita za kupima mafuta zilizotelekezwa, kufuatilia misamaha ya kodi, pamoja na kuhimiza matumizi ya mashine za elektroniki.

Mapendekezo hayo na mengine mengi yamefanyiwa kazi kikamilifu na Serikali ya JPM katika kipindi kifupi na kufanikiwa kuokoa mabilioni ya fedha.

Ripoti ya mwaka 2009/ 2010 na hata ya mwaka 2013/ 2014, inaonyesha CAG alipendekeza uwepo usawa katika marupurupu yatolewayo na mashirika na taasisi nyingine za umma.

“Kuna umuhimu kwa Serikali kuhakikisha kuwa kuna uwiano katika marupurupu wanayopata menejimenti na bodi za wakurugenzi wa mashirika na taasisi nyinginezo za umma, kutokana na ukweli kwamba rasilimali wanazotumia (kama posho za vikao, ada za bodi za wakurugenzi) ni rasilimali za Umma. Hii itasaidia kuondoa tofauti zilizopo sasa, kuongeza ufanisi na uwajibikaji katika mashirika na taasisi nyingine za umma,” alisema.
Pendekezo hilo halikufanyiwa kazi, lakini hivi karibuni Rais Magufuli akiwa Chato, Geita alitangaza kurekebisha mishahara ya wafanyakazi, akisema atapunguza mishahara ya wakurugenzi wa taasisi za umma wanaolipwa hadi Sh40 milioni.
“Katika Serikali ninayoongoza, sitegemei kumlipa mtumishi zaidi ya Sh15 milioni. Tayari nimeunda tume kushughulikia hilo,” alisema Rais Magufuli ambaye amejikita katika kusimamia makusanyo ya mapato, huku akidhibiti matumizi na kupambana na wezi wa mali ya umma.
Katika ripoti ya mwaka 2012/2013, CAG alishauri mita za kupima mafuta zilizofungwa na TPA zianze kufanya kazi ili upimaji mafuta yanayoingia nchini ufanywe kwa usahihi.
“Mita hizo ziliwekwa tayari kwa matumizi kwenye bandari za Tanga na Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia kudhibiti mapato yanayopotea kutokana na kutokuwa na vifaa vizuri vya kupimia shehena za mafuta zinazoingia nchini… Hata hivyo, mita hizo zimetelekezwa kwa miaka kadhaa sasa,” anasema CAG.

CAG alisikitishwa na hali hiyo kwa sababu kutotumia vipimo hivyo sahihi na badala yake kupima kwa kutumia kijiti, kulisababisha upotevu wa mapato ya Serikali.

Lakini Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo alidai vifaa hivyo havikidhi viwango vinavyotakiwa.

“Baada ya matatizo hayo kushindikana, mamlaka ikaamua kuendelea kutumia njia zisizo za kielektroniki (fimbo ya kutumbukiza kwenye matangi ya mafuta) kwenye kupima shehena za mafuta yanayoingia nchini. Kitendo hicho kina athari kwa mapato ya Mamlaka ya Mapato Tanzania katika uhakiki wa usahihi wa kiasi cha kodi kinacholipwa kutokana na upimaji wa shehena hizo za mafuta bila ya kutumia vifaa stahiki na athari katika uendeshaji wa shughuli za TPA,” alisema.
Februari 11, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitembelea eneo la Kigamboni kukagua ujenzi wa mita hizo kwa ajili ya kupima mafuta yanayoingia ili kujua usahihi wa kiasi cha mafuta yaliyoingia.

Mapendekezo mengine yaliyowahi kutolewa na hayakufanyiwa kazi katika kipindi chote cha utawala wa Rais Kikwete ni kudhibiti misamaha ya kodi.
“Ninapendekeza Serikali iimarishe mfumo wa udhibiti na usimamizi wa misamaha ya kodi inayotolewa na menejimenti ya TRA (Mamlaka ya Kodi Tanzania) iimarishe mfumo wa ukaguzi na uchunguzi kupunguza migogoro kuhusiana na ulipaji wa kodi,” alisema.
“Pia, kuwe na kikao cha kimkakati kujadili maeneo maalumu na njia za kukuza ukusanyaji wa mapato pamoja na kushughulikia rufaa za kesi za kodi nchini. Mamlaka ya Mapato Tanzania kutoza wafanyabiashara wasiotumia mashine za kielektroniki. Serikali itoe miongozo kwa taasisi zake kuacha kufanya biashara na wazabuni wasiotoa risiti za kielektroniki.”

Katika kipindi chote cha kampeni za urais Magufuli aliahidi kufuta misamaha yote ya kodi isiyo na tija, na baada ya kuingia madarakani siyo tu alitimiza ahadi yake kwa Serikali yake ilianza kufuatilia wote waliotumia vibaya misamaha yakiwamo mashirika ya dini.

Kuhusu ukwepaji kodi Novemba 27 2015 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alifanya ziara ya kushtukiza TPA ambako ilibainika makontena 349 yamepotea, na siku tano baadaye yaani Desemba 3, 2015 Majaliwa alifanya ziara ya pili ambako alitaja makontena 2431 yaliyopitishwa bila kulipiwa kodi kati ya Machi na Septemba 2014. Serikali iliwataka wahusika wote kulipa kodi huku ikiwasimamisha au kuwafukuza wafanyakazi waliohusika.

Hata suala la kuwaondoa wafanyakazi hewa kutoka kwenye daftari la malipo ni ushauri wa CAG.
“Kuhusu usimamizi wa rasilimali watu na taarifa za mishahara, Serikali inashauriwa kuhakikisha kuwa kasoro hii haitokei na maafisa masuuli wote kuhakikisha mishahara iliyolipwa kwa wasio watumishi wa umma inarudishwa kutoka kwa watumishi hao na kuwasilishwa Hazina,” anasema.
Machi 2016 Rais Magufuli alipowateua wakuu wa mikoa na kuwaapisha aliwaagiza kufanya kazi ya kuwaondoa wafanyakazi hewa wote na kuonyesha hakuwa anatania, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela aliyedai hakukuwa na wafanyakazi hewa wakati wapo amefukuzwa kazi.

CAG alipendekeza pia maafisa waliostaafu katika balozi za Tanzania warudishwe nyumbani na nafasi zao kujazwa mara moja. Utekelezaji ulifanyika Januari na Machi wakati balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya, pamoja na watumishi wengine watano, waliporejeshwa nchini.

Wengine ni Balozi wa Tanzania aliyeko London, Uingereza, Peter Kallaghe, Balozi wa Tanzania nchini Italia, Dk James Msekela; na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan, Dk Batilda Buriani, baada ya mikataba yao kumalizika.

Wanasiasa walioongea na Mwananchi walipongeza hatua za Rais, lakini baadhi wakata kuwepo na mfumo wa kufanya uamuzi kama huo.

“Rais Magufuli anastahili pongezi kwa hatua alizozichukua kwa kuwa hazikufanywa na mtangulizi wake,” alisema mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini.
“Kuna vitu vingi vinavyoainishwa ndani ya ripoti za CAG na mojawapo ni Sheria ya Manunuzi ya Umma. Hii imeelezwa mara nyingi kuwa inachangia upotevu wa fedha za Serikali kwa kiasi kikubwa. Kinachotakiwa iondolewe au ifanyiwe marekebisho ili kukabiliana na watu wanaouza bidhaa au huduma zao kwa bei ya juu kuliko ya soko.”
Alisema nia nzuri ya Rais kukabiliana na rushwa pamoja na ufisadi itakuwa endelevu endapo kila mtu ataipa kipaumbele wakiwamo wasaidizi wake, lakini akaongeza kuwa jambo hilo linawezekana endapo kutakuwa na kanuni zinazombana kila mtumishi wa umma.

Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa alisema: “Kama ni ufuatiliaji ni jambo zuri, na mfano mzuri ni hili la watumishi hewa. Tunachotaka kukiona hivi sasa ni hao wanaofanya mpango wa malipo hayo kuchukuliwa hatua.”

Mchungaji Msigwa alisema wapinzani watapata nafasi ya kuzungumzia ufuatiliaji huo wa Rais Magufuli pale watakapoona kuwa wahusika wote wanachukuliwa hatua, akidai sasa kuna maneno mengi kuliko vitendo.

“Mbona hatujaona wakurugenzi wa halmashauri wakichukuliwa hatua maana wao wanajua siri ya mishahara hewa,” alisema.

Kwa upande wake, mbunge wa Gairo (CCM), Ahmed Shabiby alisema ofisi ya CAG ni chombo cha Serikali na kinafanya kazi kwa mujibu wa sheria hivyo ni lazima ripoti zake zitekelezwe kwa ajili ya maslahi ya nchi.
“Utekelezaji wa ripoti ya CAG unaipa nguvu ofisi yake lakini pia nashangaa kwa nini mapendekezo yake yalikuwa hayatekelezwi miaka ya nyuma?”
Mbunge wa Manyovu (CCM), Albert Obama alisema kila zama zina njia zake za kufuatilia masuala muhimu licha ya kasi ya ufuatiliaji ya Serikali iliyopita ilikuwa ndogo.
“Rais anataka kuleta nidhamu mpya ndani ya nchi kwa kupambana na masuala ya rushwa na ufisadi,” alisema Obama ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji (PIC).
“Nadhani huu ni wakati wa kumpa Rais ushirikiano ili kuweza kubainisha masuala mbalimbali. Hizi ni zama za wanyonge kunufaika na nchi yao.”     


Polisi watatu Wafikishwa Mahakamani Wakituhumiwa Kupokea Rushwa

0
0
Polisi watatu wa wilayani Urambo, Mkoa wa Tabora wamefikishwa mahakamani kwa mashitaka ya kuomba na kupokea rushwa.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Tabora, iliwafikisha askari hao jana katika Mahakama ya Wilaya ya Urambo huku mwingine akidaiwa kukimbia.

Askari hao waliofukuzwa kazi kabla ya kufikishwa mahakamani ni John Okinda, Kabila Pius na Patrick Robart.

Anayedaiwa kukimbia ni Elisha ambaye polisi inaendelea kumtafuta.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Urambo, Hassan Momba, Wakili wa Takukuru, Edsoni Mapalala alidai washitakiwa walitenda makosa hayo Machi 7 mwaka huu.

Mapalala alidai siku hiyo katika kijiji cha Mkirigi, Kata ya Ilege, Wilaya ya Kaliua, washitakiwa hao wakiwa waajiriwa wa jeshi la polisi, waliomba rushwa ya Sh milioni tatu kutoka kwa Dotto Gandulanye ili wasimchukulie hatua za kisheria baada ya kumkuta akiwa na bangi.

Baada ya Kutoka Tour Mwanamuziki Diamond Platnumz Apata Shavu Jingine la Nguvu....

0
0
Wanasema hela zinaenda kwa wale ambao tayari wanazo. Kwa Diamond kuamka na dili mpya kila kukicha kimekuwa ni kitu cha kawaida.

Na sasa staa huyo amesaini mkataba wa ubalozi wa tomato sauce tunayokutana nayo mara kibao kwenye vile vijiwe vya kulia viepe, Red Gold.

Amesaini mkataba huo jana kwenye ofisi zake za WCB. Huo ni mkataba wa tatu baada ya DSTV, Vodacom.

Nilimpeleka mama Ulaya kumtoa ushamba - Diamond

0
0
Amesema ameona kuwa mziki wa bongo fleva umekuwa mkubwa sana duniani kwani alijaza kumbi ambazo hata baadhi ya wanamuziki wa Marekani wakifika wanafanyia kule kwa sababu sio kila msanii wa marekani anaweza kujaza Arena hizo.

Msanii huyo amesema hii ni mara yake ya kwanza kusafiri na familia yake, kama mama yake hajawahi kwenda ulaya kabisa hivyo ameamua kumtoa ushamba.

"Miaka inaenda na tangia 'nimetoboa' sikuwahi kusafiri na mama yangu kwanza hakuwahi kwenda Europe au Ulaya alikuwa anaisikia tu kwenye bomba, inaweza kuwa kesho au kesho kutwa nikadondoka nikafa halafu mama yangu akabaki tena kuisikia nikaona ni bora kwenda kutoana ushamba kabisa"

Aidha msanii huyo amesema ataendelea na 'tour' yake ambapo atafanya 'show' 3 marekani, na pia 'show' nyingine zitafanyika India, Dar es Salaam , Mwanza, na Australia.

Diamond ameongeaza kuwa atakuwa na 'tour' rasmi kwa ajili ya Afrika na amesisitiza kuwa kuna nyimbo anasubiri zitoke maalum kwa ajili ya Afrika.

ACT-Wazalendo Waishambulia CHADEMA

0
0
CHAMA cha ACT-Wazalendo Wilaya ya Shinyanga Mjini kimetamba kuwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, ndicho kitakuwa mpinzani mkubwa wa CCM badala ya Chadema.

Katibu wa ACT-Wazalendo, Wilaya ya Shinyanga, Melkyoli Sebastian alisema hayo baada ya kumuingiza kwenye chama hicho, kada wa Chadema, Ibrahimu Mbogoma.

Mbogoma alikuwa mwenyekiti wa baraza la wazee kata ya Masekelo manispaa ya Shinyanga.

Sebastian alisema chama chao kimeanza kuaminiwa na wananchi kutokana na sera zake za kiujamaa ambazo zimelenga kumkomboa mwananchi wa hali ya chini bila ya kubagua dini, kabila wala rangi.

Alisema kutokana na sera hizo, ndiyo maana wanachama wa Chadema wameanza kujiunga na chama chao baada ya kusoma alama za nyakati.

“Kujiunga kwa kada huyo aliyekuwa Chadema ni salamu tosha kuwa Chadema inaelekea kufa kiupinzani, nina imani wapo wanachama wengi wa vyama vya upinzani watakuja kujiunga na ACT Wazalendo.

"Sisi tunawakaribisha waje kwa wingi ili tukijenge chama kuelekea Ikulu 2020,” alisema Sebastian.

Akieleza sababu za kuhama Chadema, Mbogoma, alisema ameamua hivyo kutokana na kuchoshwa na migogoro ndani ya Chadema pamoja na kuongozwa na viongozi wasiojua majukumu yao.

Mbogoma alisema tangu alipojiunga na Chadema mwaka 2010 hajaona mafanikio yoyote licha ya kushika nyadhifa mbalimbali. Alisema amekuwa akikumbana na migogoro ya mara kwa mara. Alisema anaamini ACT-Wazalendo ndicho kitaipindua CCM.

Katibu wa Chadema wilaya ya Shinyanga Mjini, George Kitalama alisema alikuwa hajapata taarifa rasmi za kiofisi za kuhama kwa mwanachama wake huyo.

Hata hivyo, alisema kila mtu ana haki ya kwenda kujiunga kwenye chama anachokitaka kwa mujibu wa Sheria za nchi.

Agizo la Paul Makonda Laanza Kutekelezwa..Ombaomba Waanza Kuondolewa Jijini Dar

0
0
Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda limeanza kufanyiwa kazi baada ya karandinga kuanza kuwasomba ombaomba waliojaa katika maeneo mengi jijini hapa.

Makonda alitangaza kuanza kuwaondoa ombaomba hao juzi, huku akipiga marufuku wananchi kuwapa pesa kwa kuwa ndicho chanzo cha kuwapo kwao jijini hapa.

Zoezi hilo la kuwaondoa watu hao lilianza juzi usiku katika maeneo ya Mnazi Mmoja, Samora na Kariakoo.

Jana maeneo mbalimbali ambayo aghalabu ombaomba hupenda kukaa  yalikuwa tupu.

Maeneo hayo ikiwamo barabara ya Morocco, Magomeni Usalama, Fire na Baridi hayakuwa na watu wa kundi hilo.

Mmoja wa ombaomba aliyekuwa na watoto wawili alipomuona mwandishi wa habari hizi katika maeneo ya Fire, alitimua mbio na kujificha pembeni mwa barabara, huku akisema: “Tumetoka Dodoma, hatutaki kurudi.”

Kadhalika, operesheni hiyo licha ya timuatimua kuwakumba ombaomba, wapigadebe nao wameunganishwa katika kundi hilo kwa kuanza kuondolewa kwenye vituo vya mabasi.

Baadhi ya wapigadebe hao wamedai ni vigumu kwa Makonda kuwaondoa kwa kuwa wanachofanya ni kwa manufaa ya maisha yao na hawana pa kwenda.

Agizo la kutaka ombaomba wakamatwe na kuondokana na vitendo hivyo liliwahi kutolewa pia na waliowahi kuwa wakuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuf Makamba, Abbas Kandoro na Said Mecky Sadiki.

Ripoti ya NSSF yatua kwa Rais John Pombe Magufuli...

0
0
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) inayohusu miradi inayosimamiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), imepelekwa kwa Rais Dk. John Magufuli kwa ajili ya kuipitia.

Awali ripoti hiyo ilitakiwa kuwasilishwa juzi kwenye Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge, baada ya wajumbe wa kamati hiyo kuiomba, lakini ilishindwa kuwasilishwa na viongozi wa NSSF kwa madai kuwa kuna tuhuma za ubadhirifu wa mamilioni ya fedha za miradi mbalimbali inayosimamiwa mfuko huo.

Akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo juzi, Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenister Mhagama, aliwaambia ripoti hiyo imetua mikononi mwa Rais Magufuli, hivyo hawawezi kuipata hadi aisome na kuiwasilisha bungeni.

“Kutokana na hali hii, kamati haiwezi kuipata ripoti hii hadi rais mwenyewe atakapoamua kuiwasilisha,” alisema.

Alisema kuna uwezekano mkubwa mjadala wa ripoti hiyo ukaendelea bungeni, baada ya Rais Magufuli kuipitia na kutoa maelekezo.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya kamati hiyo  jana vilisema  kuwa baada ya Waziri Jenister kutoa taarifa hiyo, wajumbe wa kamati walipinga na kuwataka watendaji wa NSSF waiwasilishe kwenye kamati hiyo kwa sababu wao ndio walioiomba ili waweze kuipitia na kuangalia utekelezaji wa majukumu ya mfuko huo.

Baada ya mvutano huo, Waziri Jenister alisisitiza taarifa alizonazo ripoti ipo kwa Rais, hivyo hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuipata hadi ipelekwe bungeni au atoe maelekezo mengine kwa kuwa yeye ndie mwenye kibali hicho kwa mujibu wa sheria.

Waziri Jenister alipotafutwa kuzungumzia suala hilo jana, alisema wizara yake haiwezi kulizungumzia kwa sababu liko mikononi mwa kamati.

Alisema kisheria ripoti ikifikishwa kwenye mikono ya rais, wizara haina mamlaka ya kujadili tena.

Wiki iliyopita, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohammed Mchengerwa, wakati akitoa majumuisho ya ziara walizofanya katika taasisi mbalimbali za Serikali na wizara, alisema walibaini kuwapo upungufu katika taarifa ya utekelezaji wa miradi mingi inayosimamiwa na NSSF.

Alisema kutokana na kasoro hizo, kamati iliona ni vema ikapata ripoti ya CAG ili ipitie na kujiridhisha kama miradi imetekelezwa au kuna harufu ya ufisadi.

“Kamati imebaini kuwepo nyumba nyingi zilizojengwa na NSSF ambazo hazikaliwi na watu, hali iliyotutia shaka. Inaonekana baadhi ya watu wamenufaika na miradi hii.

“Tunaamini miradi hii haijawanufaisha wanachama wake bali watu wachache, ndiyo maana tumeagiza ripoti ili tuipitie,” alisema Mchengerwa.

Alisema kutokana na hali hiyo, wameagiza kusimamishwa miradi mipya ya shirika hilo na kuiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Jamii (SSRA), kuhakikisha inasimamia ipasavyo mifuko pamoja na kuangalia miradi inayoanzishwa kama inawanufaisha wananchi na Serikali kwa ujumla.

Lugumi atoroka nchini......Adaiwa kupanda ndege usiku wa manane, haijulinani alikokwenda

0
0
Mfanyabiashara  anayemiliki Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd, Said Lugumi, ametoroka nchi.

Lugumi ambaye anatajwa kuwa na ukwasi wa kupindukia katika kipindi kifupi, aliingia mkataba tata na Jeshi la Polisi mwaka 2011, kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchi nzima kwa gharama ya Sh bilioni 37.

Taarifa za kutoroka nchi kwa mfanyabiashara huyo, zilielezwa na baadhi ya maofisa wa vyombo vya dola, ambapo inadaiwa kuwa aliondoka nchini Jumatatu wiki hii, siku ambayo Jeshi la Polisi lilitakiwa kuwasilisha mkataba huo Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kwa mujibu wa sheria.

Mfanyabiashara huyo ambaye amekuwa akitembea na msafara mkubwa wa magari ya kifahari, huku akilindwa na walinzi maalumu wa kukodi, ametoroka wakati vyombo vya dola vilikuwa vikimuwinda.

Utata wa Malipo
Pamoja na hali hiyo inaelezwa kuwa licha ya Lugumi kuingia mkataba na Jeshi la Polisi wa Sh bilioni 37, lakini bado alilipwa Sh bilioni 46 nje ya mkataba.

Katika mkataba huo, alilipwa kiasi Sh bilioni 34 ambazo ni sawa na asilimia 99 ya fedha za makubaliano ya mkataba, lakini hadi sasa mashine hizo zimefungwa katika vituo 14 pekee jijini Dar es Salaam ambavyo hata hivyo haijaainishwa maeneo vilipo.

Sakata hili lilibainika wiki iliyopita baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kukutana na maofisa wa jeshi hilo kupitia taarifa ya hesabu zao za mwaka 2013/14 zilizokaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Msafara wake Wapungua
Duru za ndani zinaeleza kuwa tangu Kamati ya Bunge ilipoibua sakata hilo na vyombo vya dola kuanza kuwahoji baadhi ya washirika wake katika biashara, msafara wa mfanyabishara huyo umepungua.

Chanzo kimoja kinasema kwa mara ya mwisho mfanyabiashara huyo alionekana eneo la Oysterbay jirani na Kanisa la St. Peter, huku akiwa na magari mawili badala ya saba hadi 10 kama ilivyokuwa awali.

Mtoa habari huyo alisema Lugumi aliopoonekana mwishoni mwa juma lililopita, alikuwa na magari mawili likiwamo Toyota GX V8 toleo la mwaka huu, ambalo lilikuwa limebeba walinzi wake, huku mwenyewe akiwa ndani ya gari la kifahari aina ya Escalade.

“Lugumi anaishi Mbweni na awali ilikuwa msafara wake ukipita magari husimamishwa ili kumpisha, na huwa na magari mengi kweli mithili ya kiongozi wa nchi, jamani kuna watu wamejua kuitafuna nchi hii, na sasa huenda unatimia usemi wa Rais Magufuli kuwa ni zamu yao kuishi kama mashetani na si kama malaika,” kilisema chanzo hicho.

Mkataba Wahamishwa
Sakata la mkataba huo wa Polisi na Lugumi limezidi kuchukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kunyang’nywa hoja hiyo na badala yake kuhamishiwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Hatua hiyo inatokana na utata uliogubika mkataba huo ambao unawahusisha vigogo kadhaa wa Jeshi la Polisi pamoja na baadhi ya watendaji wa Serikali ya Rais Dk. John Magufuli, huku ikidaiwa kuwa huenda ikawa njia ya ‘kulindwa’.

Kutokana na hali hiyo, hadi kufikia Jumatatu saa 10 jioni, Makamu Mwenyekiti wa PAC, Aeshi Hilaly, alisema kuwa kamati yao haijapokea taarifa yoyote kuhusu Kampuni ya Lugumi, ambapo kamati hiyo ililitaka Jeshi la Polisi kuwasilisha mkataba huo hadi kufikia leo.

Aeshi alisema wamemuomba Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah, ili aweze kuwaandikia Polisi barua kwa ajili ya kuwasilisha mkataba huo.

“Tumelazimika kumwandikia barua Katibu wa Bunge ili awaandikie barua polisi walete mkabata huo ndani ya siku tatu kutoka leo (juzi) kama walivyotakiwa na kamati yetu,” alisema Hilaly.

Kauli ya Bunge
Alipotafutwa Mkuu wa Idara ya Habari, Elimu na Mawasiliano, Ofisi ya Bunge, Owen Mwandumbya, alisema kama kuna hoja iliyoibuliwa na Kamati ya PAC kisha ikapelekwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, itakuwa ni kwa ajili ya kupata ufafanuzi kuhusu matumizi ya fedha.

“Kama suala hilo lipo Mambo ya Nje, itakuwa si kwa hoja iliyoibuliwa na PAC na hakuna suala linaloshughulikiwa kama limeanzia PAC.

“Na kama litakuwa limekwenda huko ni kwa ajili ya kupata uelewa kuhusu matumizi ya fedha, na unajua hivi sasa hizi  kamati zipo katika maandalizi ya bajeti. Ila hoja kuhamishiwa kamati nyingine hutokana na maelekezo ya Spika wa Bunge. Kwa hoja hii ya PAC bado suala hilo lipo chini yao,” alisema Mwandumbya.

Chanzo: Mtanzania

Kisa Mil.98 Wema Sepetu Ammwaga Idris Sultan..Sababu zingine zatajwa pia zipo Hapa

0
0
Habari ya mtoto mzuri Wema Sepetu ‘Madam’ kumwagana na mpenzi wake, Idris Sultan si ngeni masikioni mwa wapenda ubuyu, imetapakaa kwenye mitandao ya kijamii lakini Amani limenasa sababu kubwa inayodaiwa kusababisha penzi hilo kuvunjika, twende pamoja.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, wawili hao waliripotiwa kumwagana rasmi ambapo haikubainika mara moja sababu.

TUJIUNGE NA CHANZO
Iliposambaa habari hiyo, mapaparazi wetu waliingia kazini kuchimba zaidi ubuyu huo ambapo walifanikiwa kuzungumza na mmoja wa marafiki wa Wema ambaye alieleza siri ya wawili hao kumwagana.

“Kilichomfanya Wema amwagane na Idris si kingine ni shilingi milioni 98. Unajua Madam anadaiwa fedha hizo ili alikomboe lile gari lake (Range Rover Evoque) linaloshikiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Sasa akamuomba Idris amlipie, jamaa akazingua. Hapo ndipo penye sababu kubwa iliyomfanya Wema amaindi hadi wakamwagana na Idris,” alisema shosti huyo wa Wema.


IDRIS ADAIWA KUFULIA
Akaendelea: “Nasikia Idris kwa sasa amefulia. Zile shilingi milioni 500 alizoshinda kwenye Shindano la Big Brother (Hotshot 2014) zote zimeyeyuka. Ameshindwa kumhudumia Madam, Wema ameona isiwe tabu, bora amuweke pembeni aangalie ustaarabu mwingine.”

GARI LILIVYOKAMATWA
Mapema mwaka huu, Wema akiwa katika mizunguko yake maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar, alikamatwa na maafisa wa TRA waliokuwa wakifanya ukaguzi wa magari ambapo mrembo huyo alipotakiwa kuonesha vibali vya gari hilo ambalo awali alidai amejizawadia kwenye bethidei yake, hakuwa navyo na hata alipopewa muda wa wiki moja kuviwasilisha, hakuweza kufanya hivyo.
Baadaye, gari hilo lilishikiliwa na TRA ambapo walipoona Madam ameingia mitini, walianza kulinadi kwa shilingi milioni 98 hivyo mrembo huyo aliposikia, alimuomba Idris amlipie lakini jamaa inadaiwa alidunda.

SABABU NYINGINE
Chanzo kingine kilicho karibu na wawili hao kililieleza Amani kuwa mbali na shilingi milioni 98, sababu nyingine ambazo ni chanzo cha wawili hao kumwagana ni:

YA PILI
“Wema alikuwa hataki kufuatiliwafuatiliwa katika uhusiano wao. Kuna wakati Idris alizidisha kumfuatilia. Ilikuwa akimkosa kwake na kwenye simu, anamfuata kwa marafiki zake. Hata akijibiwa hayupo bado alikuwa anakwenda kwa rafiki husika kumtafuta.
“Kama mnakumbuka kuna kipindi alikuwa anakwenda kumfuata Wema hadi nyumbani kwa Aunt (Ezekiel). Sasa Madam ile kitu alikuwa hapendi.”

YA TATU
“Idris aligeuka kuwa tegemezi kwa muda mrefu. Wema mwanzoni hakushtukia, alitoa akiamini mapenzi ndivyo yalivyo lakini suala hilo lilipozidi nalo liligeuka kuwa kero. Wema anapenda akiwa na mtu kwenye uhusiano awe anamwagiwa mapesa kama vile ilivyokuwa kwa yule kigogo wake CK au Diamond.

YA NNE
“Sababu nyingine ni Idris kumzuia Wema kufanya matanuzi. Wema anataka akiwa nazo atumie sasa jamaa alipojifanya anajua kumpangia matumizi nalo lilikuwa tatizo. Madam unaanzaje kumbana kimatumizi kwa mfano?”

YA TANO
“Idris naye alimuona Wema kuhusu tukio lake la kupigana mabusu na yule mwanaume asiyeeleweka. Sasa kitendo hicho hakikumfurahisha Idris, akamchana ‘live’ Madam.”…

WEMA ANASEMAJE?
Alipotafutwa kuhusu sababu za yeye kummwaga Idris, Wema hakutaka kuingia moja kwa moja badala yake alifunguka kwa kifupi kuhusu sababu ya kupiga picha akiwa anambusu mwanaume huyo hivi karibuni.

“Ha! Ha! Haa! Davto tunazinguana tu na ni  mshikaji wangu kitambo… watu walikuwa kwenye pati and (na) tulikuwa tuna have fun (tunafurahia).”

IDRIS HUYU HAPA!
Jumatatu iliyopita, Amani lilimpigia simu Idris lakini hakupokea, alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kupitia Mtandao wa Instagram (Insta direct) kumuuliza juu ya yeye kumwagana na Wema pamoja na kufulia hadi kushindwa kumlipia Madam shilingi milioni 98, alicharuka na kuamua kujibu hadharani katika ukurasa wake wa Instagram.

“Nashangaa mwandishi kuniuliza kuwa nimefulia wakati sasa hivi mimi nipo vizuri kweli kweli. Nilifulia zamani na si sasa.”

“…mliokuja na skendo za Idris kuishiwa mbona mmechelewa sana? Mnazileta stori sasa hivi  wakati hela zimerudi… miezi minne nyuma zilipoisha mlikuwa wapi?”
Hata hivyo, taarifa za kufulia kwa Idris, zilitua kwenye dawati la gazeti hili siku nyingi nyuma lakini mwenyewe amekuwa akiwakwepa waandishi wetu, hivyo kufanya habari hiyo isiandikike kwa sababu za kitaaluma na kiweledi kwa kuwa haikuwa na mzani (balansi).

TUMEFIKAJE HAPA?
Idris alikipokea kijiti cha penzi la Wema mara baada ya kurejea Bongo akitokea Afrika Kusini akiwa amejishindia kitita cha shilingi milioni 500 kupitia Shindano la Big Brother.
Kabla ya hapo, mrembo huyo alikuwa akimilikiwa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye walimwagana na mshikaji huyo kuanza kutoka na Zarina Hassan ‘Zari’, mrembo kutoka Uganda.

Chanzo:Global Publishers

Ishu ya Kubwia Unga, JK Amuonya Mwanamiziki Ray C

0
0
Wakati msuguano mkubwa ukiwa umeibuka, Mbongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ akisukuma madongo kwa Magazeti Pendwa ya Global Publishers kwamba yanamtungia uongo kuhusu hali yake ya kurejea kubwia unga akisema hayuko hivyo kwa sasa, kuna taarifa kwamba, Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’ amemuonya kuhusu kutozingatia matumizi ya dawa za methadone.
Methadone ni dawa zinazotumiwa na waathirika wa matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’ ambapo Ray C anatumia kwenye Hospitali ya Mwananyamala, Dar baada ya kuathirika.

Kwa mujibu wa chanzo chetu makini hospitalini hapo, Ray C alipata onyo hilo baada ya Magazeti ya Global kuandika kwamba nyota huyo amerejea kwenye kubwia unga huku akiendelea na methadone, hali ‘inayomzimisha’ mara kwa mara.

“Jamani nataka kuwaambia, mnajua mlipoandika kwamba Ray C karejea kwenye unga wakati akiendelea kutumia methadone, JK alisoma, akamtumia ujumbe akimtaka ajiangalie kwenye kukazana kutumia dawa na kuachana moja kwa moja na matumizi ya unga.
“JK amemtaka aangalie mwenendo wake kwa sasa. Yaani bwana sijui vipi, JK anamtakia mema  lakini yeye hajijui tu.

“Lakini kubwa kuliko yote ni kwamba juzikati Ray C alikuja pale Hospitali ya Mwananyamala (jijini Dar), akawaangukia madaktari wake wanaomtibu akiwaomba msamaha kwamba amekuwa akiwapuuza katika ushauri lakini amegundua wao ndiyo msaada mkubwa kwake,” kilisema chanzo hicho.


Kitendo hicho kinatokana na madaktari hao siku za karibuni kumshindwa staa huyo katika kumpa mwongozo wa matumizi ya dawa hizo, hivyo kuamua kumrudisha nyumbani kwao, Bunju, Dar

Taarifa zaidi zinasema kuwa pia baada ya Magazeti ya Global kuandika habari ya anayemmaliza Ray C ni kijana Frank, ndugu zake wamemfuata na kumrudisha nyumbani kwao, Arusha.
“Unajua ndugu zake walikuwa wakimtafuta, alipotoka kwenye gazeti wakamwona, wakamfuata Mwananyamala kumchukua,” kilisema chanzo.

Utafiti uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa ile ‘posti’ ya Ray C aliyoitupia kwenye mtandao wake wa Instagram mara baada ya kuandikwa na Gazeti la Ijumaa Wikienda la Machi 28, mwaka huu, habari ikiwa na kichwa; RAY C ANASWA AMEZIMIKA, akitoa shutuma nzito kwamba picha zile si zake bali ziliungwaungwa, ameifuta!

Udadisi zaidi unasema kuwa kufutwa kwa posti hiyo kunatokana na Mbongo Fleva huyo kuguswa na dhamira yake huku pia michango ya wafuasi wake waliojitokeza kumwandikia ukweli kumwambia, picha zile ni yeye na hakuna aliyeziunga!

Ray C alipotafutwa juzi ili kujibu madai hayo alikosekana hewani licha ya kupigiwa simu mara kwa mara kwa siku nzima.

Chanzo:Global Publishers
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live




Latest Images