Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Shamsa Ford: Simtaki Nay wa Mitego!

$
0
0
Staa wa filamu Tanzania Shamsa Ford amesafisha hewa baada ya kuwepo kwa uvumi wa yeye na Nay wa Mitego kutamaniana kurudisha penzi lao.

Shamsa alifunguka yote hayo baada ya vyombo kadhaa vya habari na mitandao tofauti tofuti ya kijamii kuripoti kuwa Nay katika moja ya mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni alisema kuwa anatamani kurudiana na Shamsa Ford, kisha baadae ikadaiwa kuwa Shamsa naye amesema yuko tayari kurudiana na Nay, Shamsa alikanusha vikali uvumi huu.

akizungumza na eNewz Shamsa alisema kuwa “Mimi siwezi kurudiana na Nay na kwasasa nina mpenzi wangu ninayempenda, kwahiyo Nay aendelee tu na maisha yake asitake kuniharibia mahusiano yangu, lakini kwa kuendelea kunisifu kwa mazuri hata baada ya kuachana, ninamshukuru na ninafurahi kwa hilo, lakini si zaidi ya hapo”.

eatv.tv

Hemed PHD: Sitaacha Kujipodoa kwa Hofu ya Watu

$
0
0
MWIGIZAJI wa filamu na msanii wa Bongo Fleva, Hemed Suleiman ‘Hemedy PhD’, amesema kwamba hataacha kutumia vipodozi kwa kuwa humuweka nadhifu na humwongezea mvuto wa mwili wake.

Hemed anayetamba na wimbo wake wa ‘Imebaki stori’, alisema vipodozi anavyotumia zaidi ni poda, lipshine na pafyum na hataacha kujiremba.

“Sitaacha kujiremba kwa sababu kujiremba siyo kwa wasichana tu hata wanaume tunatakiwa tujipake vipodozi, kama poda na lipshine zinasaidia kuongeza mvuto na mwonekano nadhifu zaidi, mimi ni staa natakiwa niishi kistaa hivyo vipodozi ni kitu cha kawaida.

“Mara nyingi vipodozi navitumia nikiwa katika kazi zangu ili nionekane tofauti nyumbani na kazini hivyo nasisitiza kwamba siwezi kuacha kupaka vipodozi kwa kuogopa maneno ya watu,” alimaliza Hemed.

Mtanzania

Idris Sultan aungana na Feza Kessy kama watangazaji wapya wa Choice FM

$
0
0
Idris Sultan ameungana na Feza Kessy kama watangazaji wapya wa Choice FM.

Wawili hao watakuwa wakitangaza kipindi cha Hard Drive kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa tatu.

“Wataelewa tuu @choicefmtz natanguliza shukrani kwa Mungu kisha tukutane saa 12 asubuhi mpaka saa 3 asubuhi. Ntawaamsha,” ameandika Idris.

Feza na Idris wamechukuliwa katika usajili mpya wa Clouds Media Group katika vituo vyake vya redio ambapo Clouds FM jana waliwatangaza rasmi Dj Sinyorita na Mami waliokuwa East Africa Radio kama wafanyakazi wao wapya.

Shilole Alazwa Hospitali Baada ya Kuzidiwa Usiku wa Jana

$
0
0
Staa wa Bongo Movies na Bongo Fleva,  Shilole amelazwa hospitali baada ya kuzidiwa usiku wa jana.

Akiongea na Bongo5, Babalevo ambaye yupo katika hospitali aliyolazwa muimbaji huyo iliyopo Kinondoni, amedai kuwa usiku wa jana alichemka kiasi cha kukosa nguvu na kulazimika kupelekwa hospitali.

Aliwekewa drip kushusha homa hiyo na madaktari wamemshauri apate muda wa kupumzika zaidi. Babalevo amesema Shilole ambaye siku za hivi karibuni amekuwa akifanya mazoezi makali ya mwili anaendelea vizuri.

Tunakuombea upone haraka Shishi.

Chanzo:BONGO5

Daraja la Kigamboni Kuanza Kutumika Kesho

$
0
0
Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake kesho watapata fursa ya kulitumia kwa mara ya kwanza Daraja la Kigamboni litakalofunguliwa rasmi na Rais John Magufuli, Jumanne wiki ijayo.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Joseph Nyamhanga ilieleza jana kuwa pia, Rais Magufuli kesho atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya juu (Flyover) katika makutano ya Tazara jijini hapa.

Akizungumzia ujenzi wa daraja la Kigamboni, Meneja mradi wa Kampuni ya China Railway Construction Engineering Group wanaotekeleza mradi huo kwa ushirikiano na Kampuni ya China Railway Major Bridge Group, Zhang Bangxu, alisema kesho watawaruhusu wakazi wa jiji na magari kupita bila kutozwa fedha katika daraja hilo ambalo ujenzi wake umegharimu Dola 135 milioni za Marekani (takribani Sh283.5 bilioni).    

Jiji la Dar es Salaam Kufumuliwa na Kupangwa Upya...

$
0
0
Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema kuwa jiji la Dar es Salaam litafumuliwa na kisha kupangwa upya, baada ya Ramani ya Mipango Mji (Master Plan) mpya kukamilika.

Akizungumza na Wadau wa Sekta ya Uendelezaji Ujenzi jijini Dar es Salaam leo, Waziri Lukuvi amesema ameagiza mpango huo utakamilika kabla ya Julai ili mpango wa upangaji upya jiji hilo uanze.

Pia Waziri Lukuvi amesema kuwa nyumba zianazojengwa kwa sasa na kampuni na mashirika ya Umma, likiwemo Shirika la Nyumba la Taifa sio za bei nafuu kulingan na hali halisi ya kipato cha Watanzania wengi, na badala yake ameagiza NHC liwakusanye wabunifu wa nyumba za bei nafuu watoe muundo ili Watanzani ndio waamue aina ya nyumba za bei nafuu.


CHADEMA Wapata Pigo...Mwenyekiti wa zamani CHADEMA Mwanza, Adrian Tizeba ahamia CCM

$
0
0
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha Demokrsaia  na Maendeleo Chedema mkoa wa Mwanza Andrian Tizeba, leo amejiunga rasmi na CCM wilayani  Sengerema tawi la Lugata.

Tizeba ambaye alitangaza kujivua uanachama wa chadema Machi 29 mwaka huu baada ya kusimamishwa uongozi kwa muda wa mwaka mmoja, na kutangaza kuachana na siasa, amekabidhiwa kadi hiyo  na katibu wa tawi hilo Alfred Mwambala.

Akizungumza kwa njia ya simu, Tizeba amesema uamuzi wake si wa kulazimishwa na mtu bali, ameona ni vema arudi kwenye chama chake cha awali.

Tizeba ambaye ni kaka wa mbunge wa jimbo la Buchosa, Charles Tizeba amesema, nia na dhumuni la kujiunga na chama hicho ni kutokana na utendaji wa Rais John Magufuli anaoufanya.

Mganga wa Zahanati Kigoma Atiwa Mbaroni kwa Tuhuma za Kumbaka Mgonjwa

$
0
0
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linamshikilia Mganga wa Zahanati ya kijiji cha Kidahwe wilayani Kigoma kwa tuhuma za kumbaka mgonjwa aliyekuwa akimtibu katika zahanati ya kijiji hicho.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ferdinand Mtui amemtaja mganga huyo kuwa ni Ibrahim Bundala (29)na kwamba anatuhumiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 14 aliyefika katika zahanati hiyo kwa ajili ya kupata matibabu.

Amesema mtuhumiwa huyo ambaye atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika alitenda kosa hilo baada ya binti huyo kuingia katika chumba cha daktari kwa ajili ya kumueleza ugonjwa anaoumwa.

Katika tukio jingine wahamiaji 55 toka Burundi wamekamatwa katika maeneo mbalimbali baada ya kuingia nchini kinyume cha sheria na wamekabidhiwa idara ya uhamiaji kwa ajili ya taratibu nyingine ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani.

Download Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

$
0
0

Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 

Au Bonyeza hii picha hapa chini

Nimetumia Dawa za Kukuza Kuku wa Kisasa Kukuza Makalio Yangu

$
0
0
"I had always wanted to have a bigger butt since high school i felt my figure one shape wasn't sexy enough and made me unattractive to men, i never got to be hit on by men as much which as a lady got me worried and concerned. When i joined campus all my friends were getting hooked up but me, a friend advised me to buy the booty pads which i bought at 3k in town, surprisingly i started getting advances but my fear of going to bed and the man discovering the secret kept me away from sleeping with them,i felt lonely inside i couldn't get to enjoy"

She continued, "in a secret Facebook group which im a member, a lady suggested the chicken feeds trick which would fatten and give you a big ass in few months, i contacted and she organized it for me,i finally found the solution to my problem. I started using them around may last year and by August the magic was showing i had added weight and my butt was getting bigger day by day. By December last year they got extremely big beyond my preference so i stopped usage. I was okay and so i thought"

As you are about to discover the problems were yet to start and the big butt didn't only bring relief to her but also grief, "it was too big that made me so uncomfortable, the toilet seat at home was never enough which inconvenienced me, people around started giving me raised eyebrows looks. Now i joined the gym to reduce it, i walk to town daily from Kinondoni to shake off this baggage but nothing seems to work. Now last three weeks i have noticed puss swellings in my butt and are very smelly when burst. It has got me worried, i researched and read about consequences of butt enhancers and im now sleeping and walking with fears of a cancer infection, I’m only 22 and yet to finish campus and already cancer could be in the equation and it is all my fault and naivety i hate my life" confessed Catharine* amidst tears while talking to NE.

She has what is known in the streets language as 'figure number nane' big butt but she now has to live with even bigger problems.

Infosys IPS (T) LTD wakanusha kuhusika na LUGUMI katika kashfa ya ubadhirifu

$
0
0
Kampuni ya INFOSYS IPS (T) LTD imekanusha taarifa zinazoenezwa katika mitandao ya kijamii kwamba kampuni hiyo inahusika na inashirikirikiana na Lugumi Enterprises katika kashfa ya ubadhirifu.

Katika habari zilizosambaaa inasemekana kwamba kampuni ya Infosys ilipokea mabilioni ya shilingi kutoka katika kampuni ya Lugumi, jambo ambalo wao wanadai si la kweli na ni la kupuuzwa na umma.

'Hatujawahi kufanya biashara na kampuni ya Lugumi Enterprises' Amesisitiza Bwana Sweki Donald, Naibu Meneja Mkuu Infosys IPS (T) LTD.

Goat Gives Birth To Half-Human Half-Goat Creature

$
0
0
We are truly living in the final moments of the end times! All indications show that a very sharp bad guy has been having sexual relations with the female goat. Investigation into the matter has started.

Sudan Kusini yajiunga rasmi na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Rais Magufuli ashuhudia utiaji wa saini

$
0
0
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ametia saini mkataba wa nchi yake kujiunga rasmi kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Rais Kiir ametia saini mkataba huo jijini Dar es Salaam mbele ya mwenyeji wake, Rais wa Tanzania John Magufuli, ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa jumuiya hiyo.

Viongozi wa nchi za jumuiya hiyo waliidhinisha kukubaliwa kwa Sudan Kusini kujiunga na jumuiya hiyo kwenye mkutano mkuu uliofanyika mjini Arusha mwezi uliopita.

Sudan Kusini itakuwa nchi ya sita kujiunga na jumuiya hiyo iliyoanza kwa nchi tatu Tanzania, Kenya na Uganda. Rwanda na Burundi zilijiunga na jumuiya hiyo baadaye.

Baada ya kujiunga rasmi leo, Sudan Kusini inatarajiwa kufungua mipaka yake kwa ajili ya biashara. Tayari kampuni na asasi nyingi za kifedha kutoka Kenya zimefungua biashara nchini Sudan Kusini.

Wengi wanatarajia hatua ya leo itafungua fursa zaidi za kibiashara kati ya Sudan Kusini na nchi wanachama wa jumuiya.

Wadadisi wengine wanaamini kuwa baadhi ya miradi ambayo Sudan Kusini ingetaka kujumuishwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ni miundo msingi ikiwemo reli na mabomba ya mafuta.

Mapenzi yamekua Rahisi Sana Ndo Maana Ndoa Hamna Siku Hizi

$
0
0
Eeh ndo hivyo, akina dada wengi wanajirahihisha sana wala hawaoni aibu kuzungusha kwa vijana wa mtaani na maofisini.Zamani nasikia msichana unaweza ukafukuzia miaka mi 2 na kuendelea nowdays ukitoka nae tu appointment chupa ya pili ikikolea kichwani akili yote inakimbilia chini kazi kwako tu kuangusha kwa ubua

Kingine material things, watu wengi wako kimaslahi ndo maana anaweza easily aka confuse mapenzi na pesa hii ni kutokana na economic liberalisation sijui? Utaona mdada ana mpenzi wake atakuambia i love my guy blah blah nyingi lakini sasa kama huyo Guy hawezi kumnunulia Iphone 7 wala hawezi ku offord outing za zanzibar weekend, we muambie tu twende Zanzibar this week lazima lovely Guy atoswe na lazima ujilie tu huko.

Mapenzi yakishakua tu biashara basi tambua kuwa soko lake litatawaliwa na demand and supply kwa kuwa kuna wadada wengi mjini supply ni kubwa lakini wanalazimika kushusha bei, utu tena katika mapenzi taratibu unapotea hapa ni chapa tu ilale. Kwanini wanaume waweke ndani wakati kinapatikana tu kirahisi? Na hata hiki kilichokua ndani kutokana na ushindani wa soko kinaweza kikachukuliwa?

Bibi Kizee wa Miaka 84 Abakwa na Kijana wa Miaka 32......

$
0
0
Pichani ni Bibi kizee mwenye umri wa miaka 84 na mkazi wa Kijiji cha Chungu, tarafa ya Ihanja, wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida akiwa amebebwa na mmoja wa ndugu zake wakati akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya mjini Singida kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili kijana mmoja mwenye umri wa miaka 32 (jina lake halikupatikana) anayetuhumiwa kumbaka bibi kizee huyo kwa mara ya tatu sasa ndipo walipofanikiwa kumkamata.

Set foot in Tanzania and I’ll lock you in Prison, Magufuli warns Hon Duale From Kenya

$
0
0
By Gregory Mponda

Tanzanian ‘Bulldozer’ President Dr. John Pombe Joseph Magufuli has vowed to send to prison Kenyan majority leader in Parliament Aden if he dares set foot on Tanzanian soil.

Magufuli’s curfew comes days after he ordered the detainment of Kenyan Cabinet Secretary Alfred Keter for possession of fake travel documents.

Following the Magufuli fiat on Keter, hon. Duale took it to the media to do what he does best, undermining and disrespecting the Tanzanians authorities.

Speaking today morning from State House Tanzania, President Magufuli reportedly ordered the police to arrest Duale if he dares step in Tanzanian soil.

Here is what Magufuli had to say:

“Kuna punguani mwingine huko Kenya anaitwa Duale anazungumza kama kasuku akitukana watu wa Tanzania. Huyu mtu anafikiria huo upuuzi wake anaweza akatuletea sisi watu wa Jamhuri ya Muungano wa Watu wa Tanzania? Mkatazeni kabisa na mtu amuelezee kwamba hapa ni Tanzania wala si Kenya. Kelele zake zisizokua na msingi wacha azipige huko Kenya akitukana Mheshimiwa Raila. Hapa tutamfunga kabisa na nataka kumwagiza waziri wa usalama amkamate mnafiki Yule punde tu atakapokanyaga ardhi ya watanzania”

(There is this other crazy one from Kenya called Duale. This one talks like a parrot while insulting Tanzanians. If this fool thinks he can insult Tanzanians and get away with it, someone should tell him we are Tanzanians. Let him make his noise in Kenya as he insults Prime Minister Raila. Here, we shall send him to prison forever. I also want to direct the Minister for security to capture the hypocrite if he sets foot in Tanzanian soil)

Chanzo: Politics.co.ke

TIBA MBADALA: Kunywa Maji ya Moto ni Tiba ya Magonjwa Mengi....

$
0
0
Kuna tiba nyingi za kitabibu, zilizogawanyikaa katika makundi mbalimbali. Kuna zile za hospitali ambazo ni lazima zinunuliwe, lakini kuna tiba ambazo kwa ushauri wa daktari hata wewe unaweza kuziandaa bila kutumia gharama kubwa.

Moja ya tiba hizo ni kunywa maji ya moto. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya maji moto yanatibu magonjwa mengi ikiwemo: Figo, kutoa sumu mwilini, kuyeyusha mafuta tumboni, kurahisisha mzunguko wa damu, kuondoa sumu kwenye ubongo na kusafisha haja ndogo.

Kunywa maji ya moto kila unapotaka kwenda kufanya kazi ya nguvu au mazoezi iwe kama kinga na inashauriwa kila siku anywe glasi nane ili kutoa taka na kila kisichotakiwa kubaki mwilini, kupitia jasho.

 Wadau wa afya wanasema kuwa  ni vyema pia kunywa maji ya moto yenye ndimu au limao kabla ya kifungua kinywa ili kurahisisha mfumo wa mwili kwa siku nzima.

Pazi Mwinyimvua,  Mtaalamu wa Chakula na Lishe kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anasema kuwa maji yanarahisisha uyeyushaji wa chakula na mafuta mwilini, hivyo kutokana na umuhimu huo ni vyema kunywa maji  ya moto yatakayofanya kazi haraka na kwa ufanisi mkubwa bila kuchosha figo.

Anaitaja faida nyingine ya kunywa maji ya moto kuwa ni kutoa sumu zilizopo kwenye mishipa ya fahamu na kuisaidia figo kufanya kazi kikamilifu, tofauti na maji baridi ambayo yanagandisha na kuilazimisha figo kuyeyusha kwanza na kisha kuchuja

Anashauri umuhimu wa kunywa maji moto kabla ya kufanya mazoezi kuwa ni kujiandaa kwa ajili ya kuchuja jasho ambalo litatoa sumu, hivyo yakiwa ya moto yakifika yanaanza kufanya kazi moja kwa moja, kuliko yakiwa ya baridi yanaweza kusumbua kwa kuwa ni lazima yapate joto la mwili kwanza kabla ya kuanza kufanya kazi.

“Ukiachilia kusubiri yachemke pia ni kumuepusha mtumiaji na hatari ya kuumwa tumbo kutokana na kunywa maji ya baridi bila kuweka kitu tumboni na kwenda kufanya mazoezi kitu kinachoweza kuzidisha maumivu au maji kucheza wakati wa kukimbia kama mazoezi ya kukimbia. Lakini yakiwa ya moto ni kama umekunywa chai au kula chakula cha kawaida” anasema Mwinyimvua.

Mwinyimvua anaongeza kuwa maji ya moto ni mazuri hata kwa kupata choo, kwa vile kinarahisisha uyeyushaji na uchambuaji wa kinachotakiwa na kisichotakiwa, wanaokunywa ya baridi wana uwezekanao mkubwa wa kupata haja kubwa kwa shida.

Vilevile Mwinyimvua anashauri kuwa ni vyema kunywa maji moto yaliyochemshwa na kuyaacha yapoe na kuwa vuguvugu na kuongeza limao na asali  mbali na kuongeza  ladha, asali na limao vina faida kiafya.

Gayl Canfield , RD, Mkurugenzi wa Lishe kutoka katika Kituo cha Biashara cha Pritikin Longevity kwenye Mji wa  Miami , Florida nchini Marekani, anasema kuwa kunywa maji ya uvuguvugu au ya moto ni vyema kwa kuwa hufanya kazi moja kwa moja kutokana na hali ya tumbo kuwa na joto muda wote.

Canfield anasisitiza, “Maji ni muhimu kwa mwili wako,  yakiwa ya   moto ni bora zaidi, kwa kuwa yanatoa rangi ya njano ya mkojo na kuufanya uwe msafi na wenye rangi angavu”.

Anasema  maji ya moto yanaweza kukusaidia kupoteza uzito au kudumisha uzito ulionao sasa.

 “Maji ya moto yanaweza  kuongeza joto la mwili na hivyo kuongeza kiwango  ufanyaji kazi wa mwili kidogo, “ anasema Dk Michael Wald , Mkurugenzi wa Huduma za lishe katika kituo cha Integrated kilichopo  New York, Marekani.

Anasema  ili mwili ufanye kazi ipasavyo husaidia utumbo na figo kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Kunywa maji ya moto pia husaidia kupunguza uzito wa mwili na  kuwa na  nuru na siyo kusinyaa. Vilevile huchangamsha utendaji kazi wa ubongo.

Dk  Michael Wald anaitaja faida  nyingine ya kunywa maji ya moto kuwa ni kujenga mazoea ya kuchemsha maji hivyo kupunguza idadi ya maambukizi yanayotokana na kunywa maji bila kuchemsha.

“Maji baridi hugandisha mafuta ndani ya miili yetu, ikiwa ni pamoja na mishipa ya damu,hali hii ikiendelea inaweza kusababisha  shinikizo la damu kutokana na ukosefu wa mzunguko wa damu pamoja na magonjwa mengine mengi.  Kama haikufanyiwa kazi  inaweza hata kusababisha saratani ” anasema Dr Michael Wald .

Mganga Mkuu Hospitali ya Amana, Dk. Meshack Shimwela, anasema kuwa kunywa maji ni muhimu yawe  baridi au ya moto na hakuna sababu za kitaalamu zinazohusisha na dawa au kutibu kitu chochote.

Anasema, watu wa tiba mbadala ndiyo wamelikuza hilo lakini kitaalamu halipo na kunywa maji ni muhimu kwa kila mtu bila kujali ni ya moto au baridi, hayo mengine ni maneno tu.

“Watu wanashauriwa kunywa maji ya moto kwa wale wasiopenda kunywa maji, kwa kuwa yakiwa ya uvuguvugu inakuwa nafuu kwao kunywa na wengine huambiwa waweke ndimu au limao siyo kama dawa bali kuyapa ladha ili waweze kunywa” anasema Shimwela.

Anaendelea kufafanua kuwa kama kuna wanaodharau kunywa maji wakiona ni kitu kidogo wanakosea sana kwa kuwa maji ni msaada hata unapopata tatizo la kiafya.

Anasema kuwa hata katika usagaji wa chakula maji husaidia, hivyo kama mhusika amekunywa maji atarahisisha kitendo hicho.

Dk Raymond Mwenesano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, anasema kuwa kunywa maji ni muhimu kwa kila mwanadamu ili kurahisisha utendaji wa mwili ikiwamo mzunguko wa damu bila kujali ni moto au baridi.

Dk Mwenesano anazitaja faida za kunywa maji moto kuwa ni : Kuboresha uyeyushwaji wa chakula. Maji ya vuguvugu yakiwekwa limao, yanasaidia usafishaji wa tumbo, kuondoa sumu mwilini kupitia jasho, kusafisha pua na koo, kuboresha mzunguko wa damu , husaidia upatikanaji wa haja kubwa, kuongeza kinga mwilini endapo asali na limao vitaongezwa.

MPYA Kuhusu Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (Dart)...Tarehe ya Kuanza Kazi Yatajwa Rasmi...

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene amesema mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (Dart), unatarajia kuanza rasmi Mei 10, mwaka huu.

Akizungumza kwenye majumuisho ya ziara ya Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Simbachawene alisema baada ya kukutana na wadau wa mradi huo, wamewahakikishia kuwa utaanza rasmi mwezi ujao bila kukosa.

“Tumeambiwa mradi huu una mikataba mingi na kuwa bado kuna mjadala mkubwa wa mikataba. Hatuwezi kulazimisha maana unaweza kujikuta ukitengeneza mikataba mibaya, hivyo tunaendelea na mijadala ya mikataba,” alisema.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza alisema wameutembelea mradi huo zaidi ya mara nne na kugundua tatizo linaloukwamisha kuwa ni fedha na kuitaka Serikali kutoa fedha ili uanze.

Aliesema lengo la kuanzishwa kwa mradi huo ni kupunguza kero ya usafiri kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wanaokabiliwa na tatizo la usafiri na foleni za barabarani, hivyo kutumia muda mrefu barabarani.

Rweikiza alisema kukamilika kwa mradi huo na kuanza kufanya kazi kutapunguza kero na kuokoa muda mwingi uliokuwa ukitumia bila uzalishaji.

Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) yakana Ulinzi wa Makapuni Binafsi Kwenye Sehemu Nyeti

$
0
0
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imesema kuwa makampuni binafsi ya ulinzi yanayofanya kazi bandarini hayahusiki na ulinzi wa sehemu nyeti za za Mamlaka hiyo.

Akitoa ufafanuzi huo jana jijini Dar es salaam, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Bi. Janeth Ruzangi alikiri kuwepo kwa makampuni yanayofanya kazi ya ulinzi bandarini na akafafanua kuwa hayahusiki kwa namna yoyote ile kulinda sehemu za ndani za ofisi zilizoko bandarini.

“Ninapenda kuwafahamisha wananchi kuwa Bandari inalindwa na walinzi wa aina tatu ; Jeshi la polisi, Polisi wasaidizi walioajiriwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (Auxilliary Police) pamoja na walinzi wa Makampuni binafsi”

Aliongeza kuwa makampuni hayo yanalinda maeneo ya nje ya bandari yakiwemo maegesho ya magari ya watumishi wa mamlaka kama ilivyo kwenye ofisi nyingine.

Aidha,alifafanua kuwa Polisi wa bandari walioajiriwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania wako kwa mujibu wa sheria zilizotungwa na Bunge na wamepata baadhi ya mafunzo ya kipolisi.

Ikumbukwe kuwa agizo la kuwandoa walinzi wa makampuni binafsi kwenye maeneo nyeti ya bandari lilitolewa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mwezi Februari mwaka huu alipofanya ziara ya kushtukiza bandarini hapo.

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha Limemkamata Kijana Aliyemwita Rais Magufuli Bwege Kupitia Facebook....

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, limemkamata Isaack Habakuk Emily, kwa kosa la kumtukana Rais John Magufuli kuwa ni 'Bwege' na kwamba hawezi kufananishwa na Nyerere na kusambaza ujumbe huo kwenye mitandao ya kijamii.
Nini maoni yako?
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images