Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104766 articles
Browse latest View live

Nimechanganyikiwa Nimegundua Mke wangu na Dada wa Kazi Wanasagana

$
0
0
Yamenikuta Mie mwenzenu hata sijui nifanye nini ila kwa kifupi ni kuwa nimepata ushahidi bila chenga kuwa mke wangu na mfanyakazi wa ndani ama House Girl Wanasagana, Bado sijamwambia mke wangu kwamba najua kwa sababu hata sijui nianzie wapi ..ila ni kwamba juzi asubuhi nilipomaliza kujiandaa kwenda kazini nikatoka ndani ila nilisahau simu hivyo nikarudi kuichukua cha kushangaza nilimkuta mke wangu hayupo chumbani kwetu kwani nilimuacha amelala basi sikujali sana nikajua yupo chooni ila wakati nataka kutoka ndani nikawa nasikia makalele ya mihemeko ya mapenzi kwa mbali hapo ndipo nilipostuka na kunyemelea chumba cha house girl wetu na ambapo sauti zilikuwa zinatokea,

Nilichosikia hata sina hamu ila nikelele za ku do kabisa wakihamasishana wakijua wapo wenyewe ndani ya nyumba…kiufupi kilinishuka nikashindwa nifanye nini …

Baada ya muda nilitoka nikaenda zangu kazini bila kufanya chochote huku nafikiria ni kitu gani nakosea mpaka mke wangu haridhiki na dozi yangu?? Isitoshe asubuhi hiyo hiyo nimetoka kumpa kimoja cha haja ….Embu nishaurini nifanye nini Jamani ??

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya April 17, Ikiwemo ya Lugumi ni Tishio

$
0
0


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya April 17

Rais Magufuli Awataka Mawaziri Wajiandae Kwa Machungu.....Kama Ambavyo Wananchi Walivyovumilia Tangu Uhuru.

$
0
0
Viongozi  serikalini wakiwemo mawaziri na makatibu wakuu, wameombwa na Rais John Magufuli, kuvumilia machungu wakati wa uongozi wake, kama ambavyo wananchi walivyovumilia tangu Uhuru.

Amesema hayo jana wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya kwanza ya juu (flyover) nchini Tanzania, inayojengwa katika makutano ya Barabara ya Mandela na Barabara ya Nyerere, eneo la Tazara, kwa ufadhili wa Serikali ya Japan.

Machungu hayo kwa mujibu wa Rais Magufuli, yataanza kuonekana wakati wa utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya kwanza kwa Awamu ya Tano, ambayo fedha za maendeleo zimeongezeka kutoka asilimia 27 za bajeti iliyopita, hadi kufikia asilimia 40.

Machungu yenyewe
Ili kufanikisha dhamira hiyo ya Serikali, Rais Magufuli alisema katika bajeti hiyo inayotarajiwa kupelekwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, litakaloanza vikao vyake Dodoma wiki ijayo, machungu hayo yataanza kuonekana kwani fedha za chai, semina na safari, zimekatwa na kujaziwa katika fedha za maendeleo.

Kutokana na makato hayo, Dk Magufuli amesema kutakuwa na machungu hasa kwa watendaji wa Serikali na kuwaomba mawaziri na makatibu wakuu ambao alisema walikuwa wakifaidi matunda ya Uhuru, wavumilie machungu hayo kwani wananchi wa maisha ya chini wamevumilia machungu kwa muda mrefu.

“Wananchi wamechoka kutuona sisi viongozi tunafaidi matunda ya Uhuru wa nchi tangu Uhuru na wao wakiwa wasindikizaji halafu wao tunawaomba kura na wakishatupigia tunawasahau,” alisema na kuongeza kuwa anataka wananchi watoke kwenye machungu na sasa wawe ‘watamu’ kwa maendeleo.

Magufuli alisema lazima viongozi wabadilike na kurudi kwa wananchi wa maisha ya chini na hiyo itakuwa sadaka kwa kuwapa madaraka kwani wananchi wanyonge wameteseka siku nyingi.

Wasiovumilia
Alisema waliokuwa wamezoea chai, safari na posho za ovyo kama wanaona au wanafikiri hawawezi kufanya kazi bila hizo chai, waache kazi mara moja kwani sasa fedha zinazokusanywa za walipa kodi wanyonge, zitaenda kutatua matatizo yao ya hospitali, barabara na kununua ndege za Serikali.

Pia alionya kuwa katika uongozi wake hakuna mtu atakayekwenda kinyume na utaratibu na kisha ‘akachomoka salama’ na kama kuna anayeona hawezi ajiondoe mwenyewe kwani Watanzania wanaendelea kumuombea.

Dk Magufuli alisema wananchi wote bila kujali vyama vya siasa, wanalilia maendeleo na maendeleo hayana chama, kwani wananchi wamechoka ‘machama chama’, wanataka kwenda mbele, hivyo hakuna sababu ya kubaki nyuma na kubishana kwa mambo ya chama chama, wakati uchaguzi umepita na aliyeshinda ni yeye ambaye ni CCM.

Machungu ya zamani
Ingawa Rais Magufuli alisema machungu hayo yataanza kuonekana katika Bajeti inayotarajiwa kuanza kujadiliwa na Bunge litakaloanza vikao wiki ijayo, lakini watendaji wa Serikali walianza kuona machungu ya msimamo wake tangu alipoingia madarakani Novemba mwaka jana.

Itakumbukwa kuwa Novemba 7, mwaka jana akiwa Ikulu, Dar es Salaam, katika mkutano wake wa kwanza na watumishi wa ngazi za juu wa Serikali, hasa makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu na watendaji wengine wakuu wa Serikali, Rais Magufuli alitangaza kufuta safari zote za nje ya nchi hadi hapo atakapolitolea suala hilo uamuzi mwingine.

Mpaka sasa Rais Magufuli amehakikisha shughuli zote zinazotakiwa kufanywa nje ya nchi zinafanywa na kusimamiwa na mabalozi wa Tanzania wanaowakilisha nchi, ambapo watumishi watasafiri nje iwapo kutatokea jambo la dharura na pamoja na udharura wake, lazima kibali kitolewe na yeye, Katibu Mkuu Kiongozi au Makamu wa Rais.

Katika kile kinachoonekana kuwa hatanii, Rais Magufuli aliagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi waandamizi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ambao walikaidi agizo lake la kuwataka watumishi wa umma kutosafiri nje ya nchi.

Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri kwenda nje ya nchi, licha ya kutokuwa na kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi.

Aidha ndani ya siku zake 100 za kwanza tangu alipoingia madarakani, tayari Serikali yake ilikuwa imeshawafukuza kazi vigogo zaidi ya 70 kwa tuhuma mbalimbali ikiwamo za ufisadi.

Novemba 9, mwaka jana, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue, alitangaza kuwa Rais Magufuli aliamua kufuta shamrashamra za Sikukuu ya Uhuru ambapo fedha zilizookolewa aliagiza zipelekwe katika mradi wa kupanua kipande cha barabara kutoka Morocco mpaka Mwenge katika wilaya ya Kinondoni.

Hatua hiyo ilitanguliwa na kupunguza fedha za sherehe ya kupongezana ya wabunge, ambazo alizielekeza kwenda kununua vitanda, magodoro na mashuka kwa ajili ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Hivi karibuni alipokuwa akiapisha wakuu wa mikoa, aliwataka kwenda kuwasaka watumishi hewa na kutangaza idadi yao, ambapo aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela, aliposema hajakuta watumishi hewa wakati wapo, Dk Magufuli hakusita kumuondoa mwanzoni mwa wiki hii, ingawa hakuwa amemaliza hata mwezi tangu aripoti kazini.

Imebainika Baadhi ya Omba Omba Jijini Dar Wanajihusisha na Uuzaji wa Madawa ya Kulevya-Paul Makonda

$
0
0
Mkuu  wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kwa mujibu wa utafiti alioufanya, ombaomba walioko jijini Dar es Salaam baadhi yao wanajihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya.

Akihojiwa katika mahojiano ya moja kwa moja na kituo kimoja cha redio, Makonda alisema wapo watu ambao wanatumia mwanya huo kusambaza dawa za kulevya.

“Wapo wanaotumia fursa hii kusambaza dawa za kulevya kwa sababu anavyopita huwezi kumhisi kwa namna anavyoonekana, lakini watu hawa ni miongoni mwa mawakala wa kusambaza dawa za kulevya,” alisema Makonda.

Makonda aliwataka wakazi wa jiji hilo kushirikiana naye katika kuwaondoa ombaomba hao ambao wengi wanatoka nje ya Da es Salaam na kwamba hakuna tija kuendelea kuwaacha.

“Watanzania tuna upendo sana lakini tunahitaji kutafakari kama kweli watu walioko barabarani wakiomba kama kweli wanahitaji msaada huo au la,” alisema Makonda.

Alisema kwa kuendelea kuwaacha ombaomba hao pia kutasababisha vijana ambao sasa wanaomba barabarani kuwa watu hatari katika maisha yao ya baadaye kwani wakikosa pesa wataingia katika shughuli za uporaji ili wapate fedha.

“Itafika kipindi ataanza kuangalia kile alichokuwa anakikusanya wakati akiomba na kile anachokipata akifanya kazi, ataona akifanya kazi hapati kiasi kikubwa, ataamua kuwa mporaji,” alisema Makonda.

Makonda alisema kwa mujibu wa utafiti alioufanya, asilimia 80 ya ombaomba wanatoka nje ya Dar es Salaam na kesho operesheni ya kuwaondoa watu hao itaanza rasmi huku wale ambao hawana ulemavu wowote wakikamatwa kwa makosa ya uzururaji.

Nyota ya Mbwana Samatta Yazidi Kung'aaa Ligi ya Nchini Ubelgiji..Aifungia Timu yake Bao na Kuibuka Washindi...

$
0
0
Timu anayochezea Mtanzania, Mbwana Samatta ya Genk imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Zulte-Waregem katika ligi ya nchini Ubelgiji.

Katika mchezo huo, Mbwana Samatta aliweza kupachika bao kupitia dakika ya 8 ya mchezo huo ya kipindi cha kwanza. Mbali na Mbwana Samatta pia mchezo wa timu hiyo ya Genk Marvin Baudry alifanikiwa kupachika bao la pili dakika ya 15 na kufanya matokeo kuwa 2-1.

Hata hivyo wapinzani hao wa akina Mbwana Samatta walifanikiwa kupata bao la kufutia machozi katika dakikaya 45, kwa njia ya penati iliyofungwa na Mbaye Leye.

Mrembo Aamua Kujioa Mwenyewe Baada ya Kukosa Mchumba Huku Umri Unaenda...Picha

$
0
0
Yasmin Eleby hakupata mchumba wa kumuoa mtu ambaye alitaka awe mume wake atakapofikisha miaka 40--kwa hivyo akafanya kitendo ambacho kimewashangaza wengi, aliamua kujioa mwenyewe.

Kwa mujibu wa mtandao wa MySanAntonio.com,Eleby aliahidi kwamba ikiwa hatapata mchumba wakati atakapokuwa ametimiza miaka 40, basi atafanya harusi ya mtu mmoja yaani atajioa ili kusherehekea miaka yake 40.

Duru zinasema kuwa mwanamke Eleby alifanya harusi yake mwenyewe katika makavazi ya Houston akiambatana na jamaa na familia yake na wageni wengine waalikwa.

Kwa sherehe hii, dadake Eleby ndiye aliendesha sherehe hio, kwani ni kinyume na sheria kwa mtu kujioa mwenyewe. Harusi ya kawaida ni kati ya watu wawili.

Katika picha za kanisani sherehe ilionekana kuwa ya kawaida bila ya mchumba.

Kulingana na John Guess Jr afisaa mkuu wa makavazi hayo, sherehe hiyo ilionekana kuwa bila tashwishi na kuonekana kama jambo la kawaida kwani makavazi hayo huwakumbatia watu wa jinsia mbali mbali kuendesha harusi zao hapo.

Aliposikia kwamba Eleby, ambaye anaishi na kufanya kazi ugenini alikuwa anapanga kujioa mwenyewe, aliharakisha kwenda katika eneo hilo kujionea mwenyewe.

"Eleby alipofikisha umri wa miaka 40 bila ya kupata mpenzi na mtu mwenye nia ya kumuoa, aliamua angejioa mwenyewe,''alisema Guess Jr ambaye anasema harusi hiyo imewashangaza wengi na kuwa gumzo katika mitandao ya kijamii.

Anasema anakubaliana na Eleby na mtazamo wake wa mapenzi kwamba mtu anaweza kujipenda na kujioa kwa kukosa wa kumuoa kwani cha muhimu ni mtu kujipenda kwanza kabla ya kupendwa.

"watu wengu huolewa bila ya kutafakari mara mbili kuhusu yule anayemuoa, '' Guess Jr alisema.

Anadhani kwamba pindi watu watakapomuona Eleby anavyojishughulikia mwenyewe, huenda akapata ushindani.


"ni mrembo, anafanya kazi kwa bidii na anasifika duniani na pia anaona uamuzi wake umewapa gumzo watu wengi.

Ofisi ya Bunge Yalivaa Gazeti la Nipashe....Yalitaka Liombe Radhi

$
0
0
Ofisi ya Bunge imebaini upotoshwaji mkubwa Katika habari iliyochapishwa na Gazeti la Nipashe toleo la Aprili 16, 2016 yenye kichwa cha habari kisemacho “ Bunge sasa laufyata mkataba wa Lugumi”.

Habari hiyo imeandikwa kufuatia ufafanuzi uliotolewa na Bunge jana kuhusu maagizo yaliyotolewa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) dhidi ya utekelezaji wa mkataba wa Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd  kuhusu mradi wa utambuzi wa alama za vidole (AFIS) (Automated Fingerprint Identification System.)

Ndani ya habari hiyo pia, Gazeti hilo limeeleza kuwa kamati ya PAC iliwahi kuliandikia Jeshi la Polisi kulitaka liwasilishe mkataba huo mbele ya Kamati, jambo ambalo si kweli bali ni upotoshwaji wa makusudi wenye lengo la kujenga hisia mbaya kuhusu mwenendo wa shughuli za Bunge mbele ya Umma.

Ukweli ni kwamba PAC haijawahi kuliandikia jeshi la Polisi kama inavyodaiwa na Gazeti hilo. Nukuu ya  maelezo ya PAC katika Hansard kwa Afisa Masuhuli kuhusu jambo hilo inasema kama ifuatavyo:

“Kamati inamuagiza Afisa Masuhuli kuwasilisha maelezo ya kina kuhusu utekelezaji wa Mkataba baina ya Jeshi la Polisi na  Kampuni ya Lugumi Enterprises  kuhusu mradi wa AFIS. Maelezo hayo yawasilishwe kwa Ofisi ya  Katibu wa Bunge kabla ya Jumatatu tarehe 11 Aprili, 2016”.

Katika agizo hilo PAC haikuwa imeandika kwa maandishi kuhusu agizo lake hilo hadi tarehe 12 Aprili, 2016 ilipo mweleza Katibu wa Bunge aweze kuwasilisha agizo hilo kwa maandishi ili liweze kupata Kinga chini ya Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge ambapo barua iliandikwa na kuwasilishwa kwa Afisa Masuhuli ili kupatiwa maelezo hayo kabla ya tarehe 18 Aprili, 2016.

Aidha, Mwandishi pia amelituhumu Bunge kuwa lina nia ya kuficha ukweli kuhusu jambo hili kwa kusema   taarifa ya ufafanuzi iliyotolewa na Bunge ni “kama kufunika kombe mwanaharamu apite kwa kujaribu kupotosha maagizo ya yaliyotolewa na kamati ya PAC ambayo inataka kuuona mkataba huo”

Ni vyema ikafahamika kuwa si jambo jema kwa mwandishi au chombo chochote cha habari kulituhumu Bunge linapotekeleza majukumu yake kwa kuwa Bunge linafanya kazi zake kwa kwa kuzingatia kanuni zake za Kudumu ikiwa ni pamoja na Sheria.

Ofisi ya Bunge inalisihi Gazeti la Nipashe kuomba radhi kutokana na taarifa yake hiyo iliyojaa upotoshwaji mkubwa kwa uzito ule ule au kurekebisha taarifa yake kulingana na ukweli ulivyo haraka iwezekanavyo.

Imetolewa na;
Ofisi ya Bunge,
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
S.L.P 9133,
DAR ES SALAAM.
16 Aprili, 216.

SAKATA LA LUGUMI : Rais alishawahi kusema ukitajwa kwa rushwa unaondoka hapo hapo hakuna kuunda tume

$
0
0
Wakati wa hotuba yake Mh Rais aliwahi kusema kua mtimishi wa umma akitajwa kwa ufisadi tayari ana doa atawajibishwa hapo hapo hakuna mambo kuunda tume.Sasa waziri kitwanga anatajwa sana kua na maslahi kwenye hili sakata, sasa kinachosubiriwa ni nini?


Uchunguzi Mara nyingi ni kujiridhisha na uhusika wa mtu katika sakata flani ili kukwepa mishale ya kisheria maana kumshutumu mtu bila ushahidi mwisho wa Siku ataidai haki yake Mahakamani.Kuunda tume ni kuujua ukweli wa jambo na ikithibitika ni kweli basi mtu achukuliwe hatua za kisheri bila kumuonea haya mtu.

Waziri kitwanga akae pembeni kupisha uchunguzi maana kampuni zake zimetajwa na kuunganishwa na mnufaika mkuu kampuni ya LUGUMI.Ni swali la kijiuliza ni kwanini mtu anakua waziri katika wizara ambayo tayari anafanya biashara nayo? hivi hakuna mgongano wa kimaslahi hapa? Sheria ya maadili ya utumishi wa umma inasemaje? Kiukweli Kitwanga mpaka sasa kwa maoni yangu hatakiwi kua waziri wa mambo ya ndani,kama sivyo basi ni bora kumhamisha wizara.Kampuni zake kuhusishwa kufanya biashara ndani ya wizara hiyo tayari ni tatizo kwake.

Chanzo:Jamii Forums

Nafasi za Kazi Mohammed Enterprises Tanzania limited (METL)...Soma Hapa

Malori ya Kubeba Mizigo Kuondolewa Dar....Trilioni 1 Yatengwa Kwa Kazi Hiyo

$
0
0
Malori  ya kubeba mizigo, ambayo yamekuwa yakichangia msongamano wa magari kwa kiasi kikubwa jijini Dar es Salaam, yanatarajiwa kuondolewa mara tu reli ya kisasa ‘Standard Gauge’, iliyotengewa Sh trilioni moja katika Bajeti ya Serikali, itakapofika Ruvu mkoani Pwani.

Rais John Magufuli amesema hayo jana wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya kwanza ya juu (Flyover) nchini Tanzania, inayojengwa katika makutano ya Barabara ya Mandela na Barabara ya Nyerere eneo la Tazara, kwa ufadhili wa Serikali ya Japan.

Barabara hiyo ya juu kwa mujibu wa taarifa za Wakala wa Barabara (Tanroads), ikikamilika inatarajiwa kupunguza muda wa magari kukatiza katika makutano hayo kwa asilimia 80, kutoka wastani wa dakika 45 hadi dakika 10 tu kwa wanaotoka upande mmoja kwenda mwingine.

Akifafanua zaidi kuhusu reli, Rais Magufuli alisema fedha hizo zimetengwa katika bajeti itakayopelekwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza vikao vyake wiki ijayo, ili ujenzi uanze kwa fedha za ndani wakati wafadhili wa kusaidia kuendeleza wakitafutwa na wakipatikana, wakute reli hiyo imeanza kujengwa.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli, reli hiyo itakapofika Ruvu, kutajengwa bandari kavu kubwa ambayo ikikamilika, mizigo yote inayoshuka Bandari ya Dar es Salaam, itasafirishwa kwa reli mpaka katika bandari hiyo na malori yanayochukua na kupeleka mizigo katika bandari hiyo, yataishia katika bandari hiyo kavu.

Ili kuepuka wizi wa mizigo, Rais Magufuli alisema kutafungwa kamera katika njia yote ya reli mpaka Ruvu, ili kontena linaloshushwa katika Bandari ya Dar es Salaam, lifuatiliwe mpaka katika bandari hiyo.

Mbali na reli hiyo ambayo ikikamilika kwa mujibu wa taarifa za Mamlaka ya Bandari (TPA), itapunguza gharama za usafirishaji wa mizigo kwa asilimia 30 na kuongeza kivutio cha bandari hiyo duniani, Rais Magufuli alisema Mfuko wa Barabara utatoa fedha za kujenga barabara za pete, zitakazoongeza kasi ya kupunguza msongamano kama si kuumaliza.

Alionya kuwa fedha za Mfuko wa Barabara si za kulipana posho, bali kutengeneza barabara hizo za pete katika halmashauri na kuagiza makandarasi wanaotoa asilimia 10 kwa ajili ya rushwa, wasipewe zabuni bali watafute makandarasi wazuri.

Alisema kilometa 27 za barabara hizo za pete, zimeanza kujengwa na kwa kuwa wabunge wa Dar es Salaam waliopita walisema sana, waliongezewa kilometa nyingine 86 za barabara hizo za pete, zitakazojengwa kwa lami kwa fedha za mfuko huo.

Malori kutaifishwa
Pia Rais Magufuli ameagiza halmashauri za Dar es Salaam kuweka sheria itakayokataza kupitisha magari yenye tani zaidi ya 56 katika barabara hizo, yakiwemo malori ili barabara hizo zilizokusudiwa kutumika na magari madogo, zisiharibiwe na magari yenye uzito mkubwa.

“Hakuna kupitisha magari yenye tani zaidi ya 56 na mtu akipitisha kamateni gari na ikiwezekana litaifishwe kabisa ili ajifunze kutopita katika barabara hizo na kuziharibu,“ alisisitiza.

Akizungumzia miradi hiyo ya kupunguza msongamano ikiwemo barabara za juu ikiwemo ya Ubungo, Rais Magufuli alisema zitapunguza hasara iliyokuwa ikitokea kwani katika utafiti wa mwaka 2013, ulionesha kuwa Jiji la Dar es Salaam pekee lilipoteza Sh bilioni 411.3 katika msongamano wa magari.

Mbali na hasara hiyo iliyooneshwa katika utafiti, Rais Magufuli alisema inawezekana kabisa msongamano wa magari Dar es Salaam umesababisha baadhi ya watu kufa kwa kuchelewa kufikishwa hospitalini na baadhi ya ndoa kuvunjika kutokana na kuchelewa kufika nyumbani na kushindwa kujieleza.

Rais alisema msongamano ni tatizo na kama siyo kumaliza basi lazima lipunguzwe kabisa kwa kuwa Dar es Salama ndiyo kioo cha Tanzania, ambapo mizigo inayotoka na kwenda nchi zisizo na bandari inapita hapo.

Alisema barabara ya juu ya Tazara, itatengeneza ajira nyingi na asilimia kubwa ya wanufaika watakuwa Watanzania tena wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, akawaomba vijana watakaopata ajira kwenye mradi huo, kufanya kazi kwa uaminifu wasiibe mafuta, vifaa na wasigome ili umalizike mapema.

Jealous Wife Sets Husband's Property On Fire For Attending Girlfriend's Funeral

$
0
0
A jealous wife in a marital battle with her husband has set the man's house on fire after learning that he attended his girlfriend's funeral.

The woman from Cowdray Park suburb in Bulawayo of Zimbabwe has appeared in court charged with assaulting her ex-husband and setting his property on fire for attending his alleged girlfriend's funeral.

According to The Chronicle, Fortunate Ndlovu, 33, said Benjamin Mukumbira, 45, of the same suburb deserved what he got.

"I do admit that I tore his blankets and poured paraffin on his bed and set them on fire after I found out that he had attended his girlfriend's funeral after I had just recently lost my twins and he had refused to take responsibility for them," said Ndlovu. "I also assaulted him with fists and slammed him against the wall and burnt his clothes for leaving me while I was pregnant."

Ndlovu appeared before Western Commonage magistrate Themba Chimiso facing physical abuse and malicious damage to property charges.

She however pleaded guilty and was remanded in custody to April 27. Prosecuting, Mufaro Mageza told the court that on April 6 at around 10AM, the complainant left his house to attend a funeral at Luveve cemetery.

"At around 12 noon he received a call from his neighbours who said that the accused person was damaging his property. "He immediately left the burial grounds to his house. When he arrived he discovered that the accused person had broken down the door and burnt his bed, clothes and radio," said Mageza.

The prosecutor said when Mukumbira confronted Ndlovu she pushed him against the wall and assaulted him with fists.

"The value of the damaged property is $400 and nothing was recovered," said Mageza.

DARAJA la Kigamboni Laanza Kutumika Kwa Mbwembwe...Wengine Wafanya Kama Sehemu ya Kivutio

$
0
0
Baada ya Serikali kuruhusu matumizi ya daraja jipya la Kigamboni kwa watembea kwa miguu na magari kwa majaribio, hatua hiyo imepeleka neema kwa wakazi wa mji huo, huku ikipunguza idadi ya vyombo vya moto katika vivuko.

Jana asubuhi, mwandishi wetu alishuhudia magari yakipita katika daraja hilo, kama ilivyo katika barabara zilizozoeleka za Mandela na Morogoro, huku baadhi ya madereva wakiendesha na kujipiga picha kwa simu za mkononi.

Watembea kwa miguu nao hawakuwa nyuma na idadi yao ilizidi kuongezeka mchana baada ya mvua zilizokuwa zikinyesha kuisha na sehemu kubwa walionekana kama watalii waliokuwa wakipiga picha na kuzunguzunguka katika eneo hilo.

“Sasa hivi mtu anakuwa na chaguo apite wapi anapoona atafanikisha safari yake kulingana na mahitaji,” alisema mmoja wa madereva waliotumia daraja hilo, Emmanuel Nzera.

Alisema kufunguliwa kwa daraja hilo ni neema kwa kuwa litaondoa usumbufu wa foleni katika vivuko upande wa Kigamboni na Feri na kwamba, kinachosubiriwa sasa ni gharama ya kulipia itajwe.

Mkazi wa Kigamboni, Ashura Ally alisema matumizi ya daraja hilo yatarahisisha usafiri kwa kuruhusu daladala kupita, jambo ambalo litawapunguzia gharama za bodaboda.

“Sasa kutakuwapo na wingi wa watu, hivyo na magari yatakuwa na safari za huku ambazo zitatusaidia kufika Feri na mjini kwa urahisi,” alisema.

Awali, mitumbwi ambayo ilikuwa ikitumika kuvusha abiria kabla kutoka Kigamboni kwenda Kurasini ilionekana ikiwa imeegeshwa kwenye ufukwe chini ya daraja hilo.

Hata wakati magari mengi na watu wakikimbilia katika daraja hilo la kisasa, hali ilikuwa tofauti katika eneo la Kivukoni kulikoshuhudiwa magari machache yakiingia kwenye vivuko vya Mv Kigamboni na Mv Magogoni.

Idadi kubwa ya watu iliyozoeleka kuwapo katika eneo la kusubiria vivuko mwishoni mwa wiki ilionekana kupungua na hakukuwa na pilika za abiria kuwahi kuingia kwenye vivuko.

Mmoja wa madereva waliokuwapo Kivukoni, Mussa Nzilo alisema ataendelea kutumia vivuko kwa kuwa kuna watu wanakaa maeneo ya karibu na Feri, hivyo kutumia daraja itakuwa safari ndefu kwao.

“Mimi nakaa hapo Feri kwenye kota za Bandari nikisema nipite kule Kurasini nitapoteza muda, ikizingatiwa kwamba huku hakuna foleni kama unavyoona sehemu kubwa ya watu wamekimbilia darajani,” alisema Nzilo.

Pamoja na watu wengi kuhamasika kutumia daraja hilo, kulikuwa na mkanganyiko wa baadhi ya watumiaji kushindwa kufahamu njia sahihi wanazotakiwa kupita.

Wafanyabiashara katika eneo hilo walisema huenda daraja likawa neema kwao kutokana na kuongezeka kwa watu, hivyo mzunguko wa fedha unaweza ukaongezeka.

“Japokuwa sijaona kituo, lakini hata kitendo cha watembea kwa miguu kupita hapa kwa wingi inaashiria baada ya kuzinduliwa rasmi pengine idadi ya watu itaongezeka na kusababisha kupanuka kwa biashara,” alisema Neema Nditi.

Daraja hilo linatarajiwa kuzinduliwa rasmi Jumanne ijayo na Rais John Magufuli.

Wakenya Wameanza Tena...Waitangaza Daraja Jipya la Kigamboni Kuwa lao

$
0
0
Safari wamehamia kwenye daraja la kigamboni.yani wameona haitoshi kwa mlima kilimanjaro,olduvai gorge,diamond platnumz....

Soma hii Hapa Chini:


Mwanamuziki Tunda Man Apata Ajali Mbaya ya Gari Akiwa na Wenzake Watano..Taarifa za Kifo na Majerui ipo Hapa

$
0
0
Kama ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii utakua umekutana na taarifa inayomhusisha Tunda Man kupata ajali  akiwa Mkoani iringa Asubuhi ya April 17 millardayo.com imempata Tunda Man mwenyewe na amekubali kutuelezea.


Maelezo ya mwanzo ya Tunda Man amesema
‘Tulikua tunatoka Njombe baada ya kumaliza show yetu na tukasema bora tusilale tuwahi kufika Dar,tumetoka Njombe saa 10 alfajiri mimi nikawa nasikia usingizi nikamwambia mwanangu hebu tuendeshe kidogo,kufika kijiji cha Idetelo kilomita kama 20 au 30 kabla ya kufika Mafinga tukiwa tumelala tukashtuka Gari inaingia porini tukasikia mshindo mkubwa gari imepiga puuuh Dereva hapo hapo akawa amefariki‘

Tunda Man anamalizia kwa kusema
‘Tulikua watu watano kwenye gari aliyekaa mbele na Dereva amevunjika mkono na nyama zimechanika,kuna mtu aliyekua nyuma mapafu yamepasuka,Mimi nipo poa,kwa sasa hivi tuko Mafinga hapa Hospitali ya Wilaya tunaangalia taratibu za kuchukua mwili tuupeleke Kilosa kwa ndugu zake,marehemu aliyefariki anaitwa Mussa lakini watu wengi wanamjua kwa jina la Man katuzo.

Mange 'Sidhani Kama Kuna Rais Aliechambwa na Kutukanwa Matusi ya Nguoni Kama JK..Tanzania itamkumbuka For Freedom of Speech'

$
0
0
Insta Blogger Maarufu Mange Kimambi ameendelea kuliongelea suala la freedom of speech kupitia mitandao..Amemzungumzia Rais Mstaafu Jakaya kama ifuatavyo..
Mangekimambi_ Na yooote aliyofanya JK one thing Tanzania itamkumbuka JK for ni Freedom of speech! Sidhani Kama kuna Raisi alichambwa na kutukanwa matusi ya nguoni Kama JK, Yani ilikuwa kama tunaishi Marekani au nchi za Ulaya kumbe TZ. Sometimes mpaka freedom ilipitiliza Ila jamaaa alikuwa Kama haoni anavyochambwa na kipindi Cha 10 years sikuona mtu kashikwa kwa kumchamba JK.. JK mpaka aliwekwa zeutamu na kina Mange Kimambi ?? Ila Yule zeutamu jamani alijua kutikisa nchi aiseee!!🏽🏽. Yani ilibidi media iingilie kati kuwasema usalama why wanaruhusu Raisi anadhalilishwa vile ndo usalama kumfatilia mwenye blog, Ila JK wala hakuwa na time yeye alikuwa zake anganiiiiiiiii. .
.JK alituacha tuchongeeeee mpaka makoo yakauke yeye yuko zake vacation anakula bata maulaya hukooo .. Ila JK kibokooooooo. Ila nimeamini Kweli you can't have everything, Jk alitupa freedom of speech mpaka ikapitiliza ila Aliimaliza Nchi, Magufuli is repairing the country Ila katunyima freedom of speech .... Mtihani Kweli Kweli!
Nyie ambao hamjaelewa somo la leo soon mtaelewa tu, trust me. Ngoja Jamii forums wafungiwe na blog zoote ambazo ziko against the government then mtaelewa. Wameanza taratibu kihivyo yani! No live Bunge, mseme Rais unawekwa ndani soon mtaelewa tu! .
Eti Mange analalamika issue ya freedom of speech sababu ni mtukanaji, chief mimi watanifanya nini kwani?Hata nirudi Tanzania leo legally hawana cha kunifanya zaidi ya kunisumbua , labda waning'oe meno kama Dr. Ulimboka Ila kisheria hakuna kesiiii..... All I need is good lawyer like Kibatala and I will be out the same day. Tena this time najisalimisha mwenyewe saa mbili asubuhi ili wasipate mwanya wa kunilaza ndani wajifanye muda uliisha na nilikuwa sijatoa maelezo. Kama nimefanya kosa nimelifanya nikiwa nje ya Tanzania.. Serikali ya Tanzania haiwezi kunishtaki Kwa makosa niliyofanya nikiwa Marekani. So mnaodhani nafight hii law for me you are wrong hii law Mimi haini affect hata robo,So napoongea najua nachoongelea na najua nafight kitu gani. Hao kina Hoyce Temu walionifungulia kesi wanajisumbuaaaaaaaaa. Yani hakuna wakunishtaki Tanzania as long as nilivyokupa ukweli wako sikuwa kwenye ardhi ya Tanzania. Sorry bitches'Mange
Source:Mangekimambi_

Hizi Hapa Sababu Timu ya Toto Africa Kukaza na Kuinyima Point 3 Timu ya Simu Jana

$
0
0
Kocha wa Toto Africans John Tegete amesema timu yake inacheza soka linaloshabihiana na la Simba kwa kiasi kikubwa lakini wachezaji wake wananguvu na ndiyo siri ya kuichapa Simba katika mchezo wao wa Jumapili.

Simba imekubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Toto na kuziachia pointi tatu muhimu ambazo kama wangezipata zingewapandisha kileleni mwa ligi na kuipiku Yanga kwa ponti moja mbele.

“Mfumo wanaoutumia Simba ndiyo tunaoutumia sisi kucheza, wao wanapenda kuchezea mpira na sisi tunapenda kuchezea mpira lakini sisi tunawazidi ujanja kwasababu sisi tunafanya mazoezi ya nguvu kwasababu wachezaji wetu wananguvu za kutosha. Wachezaji wa Simba hawana nguvu ndiyo maana tunawafunga”, anasema John Tegete ambaye ni baba mzazi wa mshambuliaji wa Mwadui FC Jerry Tegete.

“Wachezaji wangu wamefanya kazi niliyowatuma mchezo huu ulikuwa kama fainali kwetu kwasababu tulikuwa tunajua tunacheza na timu yenye jina kubwa, siyo timu timu kubwa kwasababu timu zote zipo sawa zote zipo kwenye Premier League”.

“Mchezo wetu dhidi ya Simba ndiyo ulikuwa unaamua kama tunabaki kwenye ligi au tunashuka daraja, lakini tumedhihirisha kwamba bado upo kwenye ligi na ndiyo maana wachezaji wangu wanafurahi”.

Simba wameambulia pointi moja msimu huu kutoka kwa Toto kufuatia kutoka sare ya kufungana bao 1-1 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza ulichezwa jijini Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba kabla ya kupoteza mchezo wa marudiano kwenye uwanja wa taifa na kuichangia pointi nne timu hiyo kutoka mwan

Diamond ni Msanii Pekee wa Afrika Mashariki Aliyetakwa Kuwania Tuzo za African Culture Image 2016

$
0
0
Msimu wa tuzo umeanza na mwaka huu kuna tuzo mpya imeanzishwa na taasisi ijulikanayo kama African Culture Initiatives.

Imeanzisha tuzo ziitwazo African Culture Image (ACI) Awards ambazo ni kwaajili ya kuwatuza waafrika popote walipo duniani.

Diamond ni msanii pekee kutoka Afrika Mashariki aliyetajwa kuwania tuzo hizo zilizotawaliwa na Wanaijeria. Ametajwa kuwania kipengele cha Male Artist of the Year akichuana na wasanii kama Wizkid, Davido, KCEE, Patoranking, Olamide na wengine.

Tuzo hizo zitatolewa katikati ya mwaka huu huko Atlanta Georgia, Marekani. Bofya hapa kuanzia kumpigia kura Diamond.

Unamkumbuka Mwimbaji MAD ICE wa Baby Gal? Tazama Hapa Video ya Wimbo Wake Mpya Hapa

$
0
0
Ni miongoni mwa waimbaji waishio nje ya Tanzania na bado wana mashabiki wengi kwenye nchi ya Tanzania… Mad Ice anayo video nyingine mpya ya kutuonyesha… ukishamaliza kuitazama sio mbaya ukimuachia na comment akipita ajue mashabiki wake wameipokeaje.

Miswada Tata Kutua Bungeni .....Serikali Kubanwa kwa Maswali 553 Huku 88 Yakiwa ya Papo Kwa Papo

$
0
0
Serikali inatarajiwa kuwasilisha miswada mbalimbali ya sheria katika Mkutano wa Bunge la Bajeti utakaloanza kesho mjini Dodoma ili ijadiliwe na kupitishwa na wabunge.

Miswada mingi ya sheria imekuwa ikilalamikiwa na wadau, hata Rais John Magufuli wakati akizindua Bunge la 11 mwaka jana, alilalamikia Sheria ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2011.

Alisema kuwa sheria hiyo inatoa mianya kwa watumishi kuiba fedha za umma.

Katika mkutano huo, Bunge linatarajia kujadili na kupitisha miswada miwili ambayo ni wa Sheria ya Matumizi wa mwaka 2016 na Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2016.

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bunge, Owen Mwandumbya jana alisema Serikali itawasilisha pia bungeni miswada mingine ya sheria ijadiliwe na kupitishwa baada ya kupitisha bajeti kukamilika.

Hata hivyo, alisema Bunge bado halijapokea miswada itakayowasilishwa na Serikali zaidi ya hiyo miwili, lakini kuanzia Juni 24 hadi 30 zimetengwa kwa ajili ya kujadili miswada mingineyo.

Mwandumbya alisema pamoja na shughuli hizo, jumla ya maswali 465 yataulizwa na kujibiwa na Serikali bungeni na kila Alhamisi yataulizwa Maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu na anatarajia kujibu jumla ya maswali 88.

“Baada ya wabunge kujadili miswada itakayowasilishwa na Serikali, hoja ya kuahirisha Bunge itatolewa Julai Mosi. Hapo Bunge litakuwa limemaliza kazi yake ya kujadili bajeti za wizara zote katika mkutano huu,” alisema Mwandumbya.

Mkuu wa Wilaya Amzuia Waziri Nchemba Kwenda Kijijini Kusikiliza Kero za Wananchi

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara, juzi alimzuia Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba kwenda kijiji cha Mikomario wilayani Bunda kutatua mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na mwekezaji kwa madai ya wasiwasi wa usalama kuwa mdogo.

Baada ya jitihada zake za kumzuia kugonga mwamba, Nyamubi ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Bunda aliamua kujitenga na ziara hiyo kwani licha ya kufika eneo la mkutano, hakujihusisha na lolote kwa kuamua kukaa pembeni.

“Mheshimiwa waziri nakushauri usiende Kijiji cha Mikomario kwa muda huu ambao unakaribia usiku kwa sababu usalama utakuwa ni mdogo kutokana na ukorofi wa wananchi wa eneo lile,” alishauri Nyamubi wakati akizungumza na Nchemba ofisini kwake.

Hata hivyo, waziri Nchemba alisisitiza kuwa lazima aende kuzungumza na wananchi hata kama atalazimika kuhutubia kwa kutumia taa za gari kwa sababu aliwaahidi kuwa angefika na kuzungumza nao na walikuwa wakimsubiri tangu mchana.

 “Mheshimiwa kaimu mkuu wa mkoa, bado sijashawishika kutotimiza ahadi ya kwenda kuzungumza na wananchi wale, wamenisubiri tangu asubuhi na nimepata taarifa wako uwanjani hadi jioni hii wakinusubiri. Kutokwenda ni kutowatendea haki,” alisisitiza Nchemba.

Baada ya msimamo huo, ndipo Nyamubi alipotangaza kujitoa kwa lolote ambalo lingetokea, licha ya kuwamo kwenye msafara wa viongozi uliofika kijijini hapo saa 12.40 jioni, hakukaa meza kuu wala kujishughulisha na lolote hadi mkutano ulipomalizika kwa amani saa 1.10 usiku.

Akizungumza na wakazi wa kijiji hicho ambacho kimekuwa na mgogoro wa ardhi kwa miaka 30 sasa bila ufumbuzi, Waziri Nchemba aliahidi kuutafutia ufumbuzi, lakini akawasihi kuwa na subira kwa sababu lazima awasiliane na wizara nyingine zinazoguswa nao.

“Suala hili ni la kisheria, hivyo linatakiwa kutatuliwa kisheria badala ya mapigano, nipeni fursa ili wizara yangu iwasiliane na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Tamisemi ili kwa pamoja tuutafutia ufumbuzi.

“Wenye mamlaka ya kupanga na hata kubadili matumizi ya ardhi ya kijiji ni ninyi wananchi kupitia mikutano na Serikali yenu ya kijiji, viongozi na wataalamu kazi yetu ni kutoa ushauri kuhakikisha uamuzi wenu unakuwa halali,” alisema.

Wakiwa na mabango yenye ujumbe, wakazi hao walimpongeza waziri kwa kutimiza ahadi ya kuzungumza nao ili kutafutia ufumbuzi mgogoro huo unaohusu hekta 2, 500 zinazodaiwa kutolewa kwa mwekezaji bila ridhaa ya Serikali ya Kijiji.
Viewing all 104766 articles
Browse latest View live




Latest Images