Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104423 articles
Browse latest View live

"KAMA MIMI SIO CLASS YA HUDDAH MONROE IWEJE ALINIVULIA NGUO?" MUSTAPHA CO

0
0
Speaking on Tuva’s show, Mambo Mseto, Mustapha started by saying that Huddah is lying and that they were in love until most recently when a photo of Mustapha snuggling a ‘fan’ surfaced online.

“Huo ni uongo. Kama mtu hayuko class yako mnapigaje ukiwa sindiria? Mbona hakupiga na watu wengine?”

On allegations that Huddah cautioned Ogopa’s management against releasing a song in which Mustapha featured her, the ‘Lenga Stress’ contends that in the first place Huddah cannot sing!

“Huddah ajui kuimba, Huddah ajui ku-rap,” reveals Mustapha adding, “Huddah ana hasira nyingi sana. Hakueza kungoja sauti yake itengenezwe kulingana na beat.”

“Hizo vitu zote tulikua tumefanya. Tuli-date. But kulikua na kitu kama hio,” adding, “Na kama anataka kurudiana na Prezzo, labda Prezzo amembembeleza kuwa wanaweza rudiana, amwambie tu Prezzo ukweli kile kili-happen na Prezzo atamsamehea na watarudiana tu fresh.”

LULU: OLE WAKE MTU AMFUATE BWANA’NGU

0
0

YELEUUWI! Msanii asiyeishiwa matukio Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ amewatemea cheche wanaomnyemelea mpenzi wake aliyemtaja kwa jina moja la Amani, akiwataka waache mara moja kwani akiwagundua atawatembezea kichapo.

Akipiga stori na mwanahabari wetu, Aunty Lulu aliweka ‘pleini’ kuwa ameshatonywa baadhi ya majina ya wanawake japokuwa hana uhakika kama ni kweli wanamnyemelea mumewe mtarajiwa ambapo akithibitisha kitachofuata ni mkong’oto kwani timbwili analiweza.

“Nampenda sana Amani, anachonipa hakuna anayeweza kunipatia, nimetulia, ameshanitambulisha kwa wazazi wake, ole wake nimnase mtu, atanieleza,” alisema Lulu.
GPL

MUME ATELEKEZA FAMILIA NA KWENDA KUISHI GESTI NA KIMADA..AFUMWA LIVE

0
0
Stori: Issa Mnally na Richard Bukos

HII ni ni fedheha! Mzee Mbonde, mkazi wa Kimara jijini Dar, anadaiwa kutelekeza familia na kwenda kuishi na mwanamke mwingine gesti kisha kufumwa laivu na mkewe, Herieth Mngodo.

Tukio hilo lililokusanya kadamnasi ya mjini, lilijiri wikiendi iliyopita katika gesti iitwayo New Samri, Manzese jijini Dar ikiwa ni sehemu ya kazi nyingine nzuri ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers.

SARAKASI ZA NDOA

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Mzee Mbonde ambaye aliwahi kuwa Diwani wa Kata ya Sinza- C, Dar, alidaiwa kuitelekeza familia yake (mke na watoto watatu) na kuishi na mwanamke mwingine katika gesti hiyo tangu mwishoni mwa mwaka jana.

Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa, Mzee Mbonde alioana na mkewe huyo mwaka 1984, bomani na ilikuwa ni ndoa ya mke mmoja.
Kilidai, mwishoni mwa mwaka jana mzee huyo alianza, ‘kuchepuka kutoka njia kuu’ na kuanzisha uhusiano na mwanamke wa nje kisha kwenda kujichimbia naye kwenye gesti hiyo.

UMBEYA WAMFIKIA MKEWE

“Mjini watu watakunyima ugali siyo maneno, kuna watu walimtonya mama Herieth kuwa mumewe anaishi katika gesti hiyo ndipo alipovaa kininja na kwenda kufanya utafiti, akabaini kuwa ni kweli na kuwajuza OFM,” kilisema chanzo hicho.

OFM MZIGONI

Kikosi kazi cha OFM, baada ya kumegewa mchapo huo, kilitinga katika gesti hiyo na kupanga chumba ambacho kilikuwa kinatazamana na chumba cha diwani huyo mstaafu kwa siku tatu kuchunguza kama kweli kigogo huyo anaishi na mwanamke mwingine, ‘results’ zikaonesha ni kweli. 

MUVI LILIVYOANZA

Baada ya OFM kumpa majibu mke huyo wa diwani mstaafu, alikusanya nguo zote za mumewe akaambatana na mwanaye wa kike kwenda kwenye gesti hiyo kumkabidhi.

“Sitaki ugomvi na mume wangu, kaamua kunitelekeza na familia, dawa yake ni kumpelekea hizi nguo zake ili aendelee kuishi na huyo mwanamke wake hukohuko,” alisema mama huyo.

FUMANIZI KABANG!

Huku makamanda wa OFM wakifuatilia kwa karibu na kunasa picha hatua kwa hatua, walimshuhudia mama huyo akizama na Bajaj katika gesti hiyo, akagonga katika chumba cha mzee huyo, alipofungua tu, alimnyunyizia mumewe pilipili machoni na kuanza kumtupia nguo zake.

Timbwili zito liliibuka, mke alianza kumzaba makofi mumewe, ndani ya muda mfupi watu kibao wakajaa nje na ndani ya gesti hiyo kumshuhudia mzee huyo akiangua kilio, hali iliyowashtua wateja wengine waliopanga katika gesti hiyo.

MFUMANIWAJI ATOKA NDUKI

Wakati timbwili likiendelea, mwanamke aliyefumaniwa alifanikiwa kupata mwanya na kutokomea kusikojulikana hivyo msala ukabaki kwa diwani huyo mstaafu.

Mke huyo, baada ya kutekeleza matakwa yake (fumanizi), naye aliondoka eneo hilo na mwanaye kuelekea nyumbani kwao na kumuacha mumewe akiwa hoi kwa maumivu ya pilipili machoni kwani yalishaanza kuvimba.
GPL

SUMAYE AKATA RUFAA KWA KUZUIWA KUFANYA KAMPENI ZA URAIS

0
0
Dodoma. Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye amekata rufaa Kamati Kuu ya CCM kupinga adhabu ya onyo kali aliyopewa na chama kutokana na madai ya kuanza kampeni za urais mapema kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.

Akizungumza na gazeti hili mjini Dodoma jana, Sumaye alisema kwa ufupi hakuridhishwa na adhabu hiyo na kuthibitisha hilo, tayari amekata rufaa.

Hata hivyo, alisema hadi jana hakuwa amepata mrejesho wowote kwa sababu kanuni hazielezi ni muda gani anatakiwa kuwa amepewa taarifa kuhusu rufaa hiyo.

Sumaye na wanachama wenzake, Edward Lowassa, Bernard Membe, Stephen Wassira, William Ngeleja na January Makamba walitiwa hatiani kwa kuanza kampeni mapema, hivyo kupewa onyo linalokwenda sambamba na kutowania nafasi yoyote ndani ya chama kwa miezi 12.

“Siwezi kuwazungumzia wenzangu, nazungumza kwa upande wangu, sikuridhishwa na adhabu hii na nimeshakata rufaa ingawa sijapata majibu yoyote, naendelea kusubiri,” alieleza Sumaye.

Waziri Sumaye alikataa kuzungumzia hali ya utekelezaji wa adhabu hiyo, akisema anachosubiri ni mwitiko wa rufaa yake aliyoiwasilisha Kamati Kuu ya CCM, mwanzoni mwa mwezi huu. “Sina kumbukumbu nzuri ilikuwa tarehe ngapi, lakini ni mwezi huu wa tatu.”

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa juu ya rufaa hiyo alisema hana taarifa zaidi ya habari hizo kuzisikia kutoka kwa mwandishi.

Hata alipotakiwa kueleza nani anatakiwa kuwa na taarifa hizo, alisema: “Mimi ndiye msemaji wa chama, hakuna wa kuzungumzia suala hili zaidi yangu. Kwanza inatakiwa ijulikane, rufaa hiyo imepelekwa ngazi gani ya uongozi kwa sababu kila ngazi ina muda tofauti wa kufanya vikao vyake vya uamuzi.”

Nnauye baada ya kuelezwa kuwa rufaa ya Sumaye imewasilishwa Kamati Kuu ya CCM, alisisitiza kuwa hana taarifa nayo na kwamba haiwezekani rufaa ipelekwe kwenye kikao kilichotoa adhabu husika.

Hata hivyo, Sumaye alisisitiza kuwa rufaa yake ameiwasilisha Kamati Kuu kwa mujibu wa kanuni zinazohusika.

MAPOLISI WAIPEKUA NYUMBA YA RUBANI WA NDEGE YA MALAYSIA ILIYOPOTEA

0
0
Kuala Lumper. Polisi nchini Malaysia wamevamia nyumba aliyokuwa akiishi rubani wa ndege iliyopotea na kuendesha msako mkali, ikiwamo kukusanya nyaraka muhimu ambazo zinazamiwa kuwa zitasaidia kufichua ukweli kuhusu tukio la kupotea kwa ndege hiyo.

Ripoti zilisema kuwa upekuzi huo, ambao pia umefanyika katika nyumba aliyokuwa akiishi rubani msaidizi, umefanyika baada ya kuibuka kwa taarifa zinazodai kuwa rubani huyo, Zaharie Ahmad Shah alikuwa na mrengo wa siasa kali.

Shah alikuwa ni shabiki na mfuasi wa wazi wa mwanasiasa wa upinzani, Anwar Ibrahim ambaye sasa yupo gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kujihusisha na vitendo vya fedheha.

Inaaminika kuwa rubani huyo alikuwapo mahakamani wakati mwanasiasa huyo alipopandishwa kizimbani mwezi Machi mwaka huu na pengine hakufurahishwa na hukumu hiyo.

Kwa sasa polisi wanashikilia nyaraka kadhaa, ikiwamo kompyuta ambayo inadhaniwa kuwa na taarifa muhimu zilizohifadhiwa na rubani huyo.

Polisi hao wameenda mbali zaidi kwa kuanzisha uchunguzi wa kimazingira ambao utasaidia kupata historia binafsi kuhusu maisha ya rubani huyo aliyetajwa kuwa na uzoefu mkubwa wa urushaji wa ndege.

Wataalamu wa saikolojia na wale wanaohusika na usalama wa anga wameitwa kuongeza nguvu ili kusaidia kuchambua taarifa zinazoendelea kukusanywa kuhusu mwenendo wa rubani Shah ambaye nyumba yake bado inaendelea kulindwa.

Kitendo cha polisi kuifanyia upekuzi nyumba ya rubani huyo pamoja na kukusanya taarifa zake binafsi kimeelezwa kwamba ni jitihada za Serikali kutaka kujiridhisha hasa kutokana na mazingira yanayohusisha upotevu wa ndege hiyo.

Wachunguzi hao wanataka kujua kama kumekuwa na tukio lolote la matatizo ya kiakili na kumewahi kujitokeza kwa changamoto za kifamilia kwa marubani hao au kwa yeyote aliyekuwamo kwenye ndege hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka Kuala Lumpur na kuelekea Beijing.

Pamoja na kwamba marubani wa ndege hiyo ya Malaysia walikuwa na rekodi nzuri, kuna wasiwasi pengine walikutwa na tukio lililosababisha kujiingiza kwenye hali ambayo ingepoteza umakini wa kuongoza ndege.

Uchunguzi pia unawalenga abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo iliyokuwa na umri wa miaka 11 na kwamba hatua hiyo inaweza kusaidia upatikanaji ukweli halisi juu ya tukio hilo.

Serikali yaomba msaada

JERRY TEGETE"YANGA HAUNA CHAKO RUDI SHULE AMA UHAME TEAM"

0
0
BABA mzazi wa straika wa Yanga Jerry Tegete, John Tegete amemtaka mwanae achague mawili ifikapo mwisho wa msimu huu iwapo ataendelea kusugua benchi kwenye kikosi hicho.
Kocha huyo wa zamani wa Toto African ya Mwanza alisema kuwa mbali na ukocha yeye pia ni mzazi hivyo lazima afuatilie maendeleo ya mwanae.; “Naona mwanangu hana bahati na Yanga, licha ya kucheza michezo minne na kufunga mabao matano. Naamini bado anaweza kucheza na kupachika mabao, lakini kama hana nafasi basi nampa hadi mwisho wa msimu aweze kuamua kati ya kusoma au kucheza soka nje ya Yanga,” alisema.
Kama ni kurudi shule basi Jerry ni kati ya wachezaji watakaokuwa na elimu zaidi kwenye soka la Tanzania kwani tayari ni mhitimu wa kidato cha nne. Lakini amefunikwa kielimu na  Reliants Lusajo mwenye Digrii ya ugavi, Salum Telela anayesoma Digrii ya Biashara na Issa Ngao naye anayesomea biashara.
SOURCE: MWANASPOTI

"SIWEZI KUINGIA MAPENZINI NA MSANII WA BONGO MOVIES..WENGI WAPO KIMASLAHI"MBOTO

0
0
Muigizaji wa filamu za Kiswahili, Haji Salum aka Mboto amesema kuwa hawezi kuanzisha uhusiano wa mapenzi na wasanii wa Bongo Movie kwa kuwa anaogopa kuchafuliwa jina na kuumizwa kimapenzi.

Mboto alifunguka kupitia mahojiano maalum na Zourha Malisa, ambapo amedai kuwa wasanii wengi wa kike wa filamu za kitanzania (Bongo Movies) hawana mapenzi ya kweli na kwamba wengi wanaangalia maslahi zaidi.

Hata hivyo, alieleza kuwa hatamani kuwa na uhusiano na baadhi ya wasanii hao, bali inamlazimu kuzuia hisia zake ili kuepuka mambo mbalimbali yatakayoyumbisha maisha yake.

"Unajua mimi pia nina tamani na pengine wao wananitamani ila najizuia na wala sitaki kuruhusu majaribu kwani najua ninachokifanya huku kwenye tasnia yetu tunakijua hivyo ni lazima ujiepushe na mambo mengine." Alisema Mboto.

Ameeleza kuwa kuna waigizaji wengi wa kike ambao ni rafiki zake wa karibu na wanashirikiana vizuri kwenye kazi.

DIRECTOR NICK DIZZO AACHANA NA E-MEDIA SASA AMEANZISHA KAMPUNI YAKE MWENYEWE INAITWA FOCUS FILMS

0
0
Kama umeshaiona video mpya ya rapper anaeiwakilisha Mbeya City, Izzo Bizness ‘Tummoghele’ iliyotoka rasmi Ijumaa iliyopita, utagundua kuwa video hiyo imefanywa na director yule yule aliyefanya video zake zilizopita aitwaye Nick Dizzo lakini safari hii sio kupitia kampuni ya E-Media

Nick Dizzo ameiambia Bongo5 exclusively kuwa kwa sasa ana kampuni yake mpya iitwayo ‘Focus Films’ ambayo imechukua nafasi ya E-Media aliyokuwa akishirikiana na Sama Jahn.

“E-Media pia ilikuwa company yangu, ila kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu kwa sasa natumia company yangu mpya ya Focus Films, ina team mpya ambayo iko focused zaidi kwenye kazi”.

Dizzo ambaye pia alidirect video ya Quick Rocka ‘My Baby’, amesema kampuni ya E-media haitakuwepo tena, pia kuanzia sasa atakuwa akisimama mwenyewe kama director tofauti na mwanzo kila video ilikua inasomeka majina mawili likiwemo la Sama Jahn.

“one of the changes pia ni hivyo, nitakuwa niko peke yangu kama director”.Alisema Dizzo

Baadhi ya video zingine zilizotayarishwa na Nick Dizzo chini ya E-Media ni pamoja na ‘Love Me’ ya Izzo B, ‘Nafanya’ ya Cyril ft. Jux, ‘Going Crazy’ ya Hemed PHD na ‘Lovely’ ya Gelly wa Rhymes.

Tummoghele ya Izzo B na Nishike mkono ya D-Knob ndio za kwanza kufanywa na Nick Dizzo kupitia Focus Films.

M-RAP "SIUTAMBUI WIMBO WANGU ULIACHIWA NA B-HITS LEO, B-HITS NILISHA GIVE UP"

0
0
Rapper M-Rap amesema hautambui wimbo ulioachiwa leo na B’Hits kwakuwa anaamini umeachiwa ili kumharibia mipango yake.

Rapper huyo aliyejitoa/ondolewa kwenye label hiyo wiki iliyopita aliachia wimbo mpya uitwao ‘Usiende Mbali’ aliomshirikisha Jux na kutayarishwa na AM Records na Jumatatu hii B’Hits wameachia wimbo wake mwingine mpya uitwao ‘Nishike’. “Mimi hii nyimbo sina taarifa nayo sasa sielewi sababu mimi nilishasema nimemaliza nao na nyimbo tayari nilishafanya sehemu nyingi kwahiyo hii siitambui,” M-Rap ameiambia Bongo5.

“Sawa ni yangu lakini hapo mwanzo walikataa kunipa mimi hiyo nyimbo sababu ni nyimbo ambayo mimi nilikuwa naiulizia itoke, kwahiyo mimi nilishaamua kugive up nikasema naendelea na mambo yangu mengine ilimradi tu nifanya kitu kingine kizuri,” ameongeza.

M-Rap amesema hatofanya chochote kuhusu wimbo huo kwakuwa hautambui.
 Bongo5

WATAKAOHUDHURIA HARUSI YA KIM NA KANYE HAWATARUHUSIWA KUINGIA NA SIMU, JAY Z NA BEYONCE TU RUKSA

0
0
Bonge la harusi inayosubiriwa kwa Hamu kati ya Kanye West na Mchumba wake wa Muda Mrefu Kim Kardashian itakayofanyika Mwezi wa Tano Imeanza kuwa Gumzo Baada ya Taarifa kuzagaa kuwa waalikwa hawataruhusiwa kuingia na Simu za mkononi wala kamera ya aina yoyote , kuepusha watu kupiga picha ama video na kuzipeleka mtandaoni kama ilivyokuwa Engagment party yao ambapo mtu mmoja alichukua video na kuipost Youtube bila ruhusa yao...Taarifa mpya zimekuja na kusema kuwa Jay z na Beyonce pekee ndio watakao ruhusiwa kuingia na Simu zao za Mkononi...
By John K

HENRY KILEWO" WANAKALENGA TUNAJUA MAAMUZI YALIYOFANYIKA SIYO YENU BALI TUME YA UCHAGUZI NA POLISI"

0
0
Henry Kilewo Ameandika yafuatayo katika Ukurasa Wake wa Facebook kuhusu Uchaguzi wa Jana katika Jimbo la Kalenga Ambapo CCM waliibuka Washindi:

"Mapambano yanaendelea,hatujafa moyo, hatujahuzunika na wala hatutarudi nyuma, safari ndiyo inaanza kuwa na chachu ya mafanikio huku tukiendelea kuwa imara na kuimarika zaidi... wanakalenga tutaendelea kuongea na nyie na tunajua maamuzi yaliyofanyika yalikuwa siyo yenu bali Tume ya Taifa ya uchaguzi iliamua kuucheza mchezo mchafu pamoja na jeshi la polisi.

Hatujashindwa na kamwe hatutashindwa wala kukubali kushindwa pasipo na mazigira huru"

PICHA ZA DIAMOND, JOHARI, RAY NA UWOYA ZATUMIKA KUPAMBA RESTAURANT CHINA

0
0
Picha za mastaa wa filamu na muziki nchini Tanzania zimetumika kama mapambo katika restaurant moja nchini China. Kwa mujibu wa blog ya Swahiliworldplanet restaurant hiyo inaitwa Medina na haijajulikana kama inamilikiwa na mtanzania au lah, huku picha za Irene Uwoya, Diamond Platinumz, Johari na Vicent Kigosi "Ray" zikitumika kupamba kuta za restaurant hiyo. Angalia picha hizo hapo juu.

Picha hii ya Johari na Ray inasemekana ilipigwa miaka kadhaa nyuma wakati wakiigiza filamu ya Revenge na ipo katika Restaurant ya Medina nchini China.

MOYES AONDOKE MAN UNITED - NA HIZI SABABU KWANINI HAFAI KUENDELEA KUIFUNDISHA KLABU HIYO

0
0
Manchester United lazima imtimue David Moyes mwishoni mwa msimu huu. David Moyes hana uwezo wa kuiongoza Manchester United kuendeleza mazuri ya aliyemrithi na kuipeleka timu kwenye kilele cha mafanikio, jambo ambalo ndilo linalotegemewa katika klabu ya ukubwa wa United. Badala ya kuendelea uongozi mbovu wa Moyes, klabu inabidi ubora na uimara wa timu kupitia kocha na benchi la ufundi ambalo huko nyuma tayari wameshaongoza timu kwa mafanikio. United ina ufuasi mkuwa wa mamilioni ya mashabiki duniani kote na kutokana na hili United inastahili kupata uongozi bora zaidi kuliko huu wa Moyes. 

Sababu kwanini Moyes aondoke Manchester United: 

Kukosa uzoefu wa kushinda - Moyes hajawahi kushinda kombe katika career yake ya ukocha - ukiondoa kombe la nguo la hisani, ambalo alikuta timu yake imeshafikishwa kwenye mchezo huo tena dhidi ya timu ya ligi ya daraja ya kwanza ya Wigan. 

Ukosefu wa uwezo wa kufundisha wachezaji wakubwa - Ukweli wa kwamba hajawahi kuwa na bahati ya kuwa na kikosi chenye wachezaji wakubwa unamaanisha kwamba hajui namna nzuri ya kudili na aina ya wachezaji wa aina hiyo, kuwafurahisha na kuwapa motisha au kujua namna ya kupata kiwango kilicho bora kutoka kwao. Ni vigumu kutegemea wachezaji walioshinda kila kitu na matajiri kumheshimu kocha ambaye hajawahi kushinda kitu chochote. 

  Ukosefu wa uzoefu wa kudili na mategemeo makubwa - Baada ya kuwa Everton kwa miaka 11, mahala ambapo alikuwa akifaulu kumaliza ligi katikati mwa msimamo akiwa na bajeti ndogo ya usajili, Moyes hana uzoefu wa kudili na presha ya mategemeo makubwa ambayo huja pamoja na kazi yake ndani ya United - na hilo tayari limeshaonekana.  

Mbinu zilizopitwa na wakati - Ukosefu wake wa mbinu bora mwanzoni na kati kati ya mchezo zimeigharimu sana timu msimu huu. Baada ya mechi ya Fulham Rene Maulesteen alisema ilikuwa kazi rahisi sana kucheza na United yenye mbinu zilezile zilikosa mabadiliko, pia beki wa kati wa Fulham Dan Burn alizidharau mbinu za Moyes kwamba zilikuwa rahisi sana kuzuia. Akiichezesha timu kwa mfumo wa kizamani 4-4-2 - timu haionyeshi kuwa na maendeleo bora katika kipindi cha miezi tisa ya utawala wake, lakini pamoja na haya yote bado haonekani kulitambua tatizo hili la mfumo na kulitafutia ufumbuzi. 

Wasaidizi wabovu - Makocha wasaidizi wa United chini ya Sir Alex walikuwa Meulensteen, Mike Phelan na Eric Steele. Wote kwa pamoja walikuwa na uzoefu wa ukocha wa level ya juu kwa miaka 25 na walikuwa walikuwa wanajua namna ya kuwaandaa vijana kushinda mechi na kushinda makombe. Uamuzi wa Moyes kuwaondoa hawa wasaidizi umezidi kuwa mbovu baada ya kuwaleta wabadala wao: Phil Neville (hakuwa mchezaji wa daraja la juu, hana uzoefu mzuri wa ukocha zaidi ya kuhusika na timu ya  England U21, ambayo ilikuwa ikifanya vibaya), Steve Round (alikuwa mmoja ya makocha walioishusha timu mpaka daraja la kwanza kutoka EPL, hana uzoefu wa kufundisha timu kubwa), Ryan Giggs (mchezaji wa daraja la juu - lakini ni kocha ambaye hana uzoefu), na Moyes mwenyewe (mbinu zake hasi - anaendekeza zaidi mazoezi magumu badala ya mazoezi ya kiufundi). Je watu hawa wana uwezo na wanafaa kuliongoza benchi la ufundi na kupata kilicho bora kutoka kwa wachezaji wa hadhi ya juu, na kwa mtazamo wa sasa inaonekana jibu ni hapana, wameishindwa kazi hiyo. 

Namna mbovu ya kudili na vyombo vya habari - Namna Moyes anavyodili na vyombo vya habari tangu sio sawa kabisa tangu alivyofika Old Trafford. Hana approach nzuri - Amekuwa akisisitiza kwenye jibu moja kwamba timu ina "bahati mbaya" na kurudia rudia msemo wake wa "Nadhani tumecheza vizuri" (Timu iwe imefungwa, imeshinda, au suluhu) - hii kauli inaonyesha ambition. Manchester United inabidi isiwe na mtazamo wa kukubali suluhu au vipigo kwa namna Moyes anavyochukulia. Inabidi tutegemee ujuzu, mbinu, na nguvu katika kutafuta ushindi kuliko kutegemea bahati kama Moyes anavyosema. 

Usajili - Jaribio la kusajili wachezaji wakubwa dirisha kubwa la usajili lilopita lilionyesha kufeli. Baada ya hapo akamleta Marouane Fellaini (kwa £27.5m, £4m zaidi ya fedha ambayo angeweza kumsajili kabla) kuja kucheza kama kiungo mkabaji. Moyes alifanya kazi na Fellaini kwa miaka kadhaa Everton na kwa maana hiyo alikuwa akijua kabisa uwezo wa kucheza kwenye hiyo nafasi na aliamini angeweza kucheza. Hata hivyo, ameonekana hayupo ccomfortable kuicheza nafasi hiyo kwa kuangalia kiwango chake mpaka sasa - hivyo haukuwa usajili mzuri kwa United.  Usajili Juan Mata umekuwa wa kuvutia, lakini ukweli unabaki kwamba Wayne Rooney anacheza kama namba 10, nafasi ambayo Mata huicheza kwa ubora, hivyo matokeo yake Mhispania huyo huchezeshwa pembeni. Mata anakosa mbio na nguvu ya kucheza kama winga asilia, hivyo Moyes anavyoendelea na mfumo wa 4-4-2 sioni mabadiliko chanya ya kupata kilicho bora kutoka Juan Mata. Akiwa tayari kashatumia kiasi cha £65.5m huku kukiwa hakuna mabadiliko yoyte yanayoonekana katika kiwango cha timu, United haipaswi kumuamini Moyes na fedha zao katika dirisha la usajili lijalo pia kutegemea yeye na wasaidizi wake kupata kilicho bora kutoka wachezaji waliopo na watakaosajiliwa.  
Moyes amekuwa akivunja rekodi nzuri kwa matokeo mabaya kila kukicha. Ile hali ya timu kuiogopa Man United iliyojengwa kwa miaka mingi iliyopita imeondoka ndani ya miezi michache. Akiwa na rekodi mbovu kuliko zote dhidi ya timu za Top 6 kama kocha wa Everton, ilikuwa wazi kwamba Moyes hana uwezo wa kuiongoza United. Hali inaonekana itaendelea kuwa hivyo wakati wote Moyes atakapoendelea kuwa kocha - uongozi wake ndani ya United dhidi ya timu za Top 6 msimu huu ameambulia pointi sita tu - akiambulia sare 3 na ushindi mmoja tu. Mechi dhidi ya timu kubwa kwenye ligi ni muhimu sana - kwa pointi pia kisaikolojia. Huku United wakishindwa kuzifunga timu hizi, inaonekana wazi ni vigumu kwa United kupata mafanikio chini ya Moyes. 
-shaffihdauda

RAGE ANA POINTI, SIMBA KWELI MAMBUMBUMBU.

0
0
Ninaposikia kauli za viongozi wa vilabu vyetu hapa Tanzania, huwa najiuliza maswali mengi sana. Weekend hii umefanyika mkutano wa wanachama wa Simba Sports club katika bwalo la polisi pale Oyster Bay. Katika mkutano huo, mwenyekiti wa sasa wa klabu hiyo alitoa kauli zenye utata kidogo, miongoni mwa kauli zake ilikua hivi, “Simba oyeee…. Mimi sitagombea tena katika uchaguzi ujao, sina njaa, mimi sio masikini…. Hata mkinizomea nasemaje, sina njaa wala si masikini, msiwe kama mambumbumbu”.


Kauli hizi za mwenyekiti wa klabu hii ya simba, zimeibua hoja kadhaa kichwani mwangu ambazo nazitafakari katika makala hii.

Simba Sports Club, timu iliyoanzishwa miaka ya 1930, na kuwa na wapenzi na wanachama wanaokadiriwa kufikia milioni tano (5) kwa ujumla, hadi leo inafanyia mikutano yake kwenye bwalo la polisi.


Simba Sc, miongoni mwa timu zenye umri mkubwa hapa Tanzania, (inakadiriwa kuwa na zaidi ya miaka 75), ina jengo kariakoo ambalo hata kupata eneo la kuegesha gari ni taabu.

Hadi leo, timu hii iliyowahi kufika makundi ya ligi ya mabingwa Afrika mwaka 2003, haina mkataba na kampuni yoyote ya utengenezaji wa vifaa vya michezo, kama Adidas au Nike wala kampuni yoyote kubwa, bali inategemea vifaa vya mchezo kutoka kwa wadhamini wa ligi.


Hadi leo, pesa za usajili wa wachezaji zinatoka mifukoni mwa watu wachache, na hata mauzo ya wachezaji hao hurudi kwenye akaunti zao binafsi za benki, na hakuna mwanachama mwenye uhalali wa kuhoji matumizi ya fedha hizo. 
i ni baadhi ya hoja nilizonazo kichwani mwangu, ambazo zinaashiria ukweli wa kauli ya mwenyekiti wa Simba, kwamba wanachama wake ni mambumbumbu. Sina maana ya kumtukana wala kumkejeli mtu, ila nia yangu ni kuwafumbua macho wanachama wa Simba, ili kama ni kufanya mabadiliko, basi wakati ndio huu wa kuondokana na kauli za kudhalilishwa kutoka kwa viongozi wao.


Hivi Simba Sc, ni kampuni, ama taasisi, ama biashara ya watu binafsi? Kwa utaratibu uliopo kwasasa, inaashiria kwamba Simba Sc ni taasisi Fulani, inayopata udhamini kutoka kwa wadhamini wa ligi na wadhamini wa timu, ambapo ndani yake inafanyika biashara ya WATU Fulani wachache. 

Mfano mzuri ni pale mwenyekiti wa club hii alipoamua kufanya usajili wa mchezaji mmoja kutoka Zanzibar, na usajili ule ulifanyikia sebuleni kwa mwenyekiti huyu, kwa kumkabidhi kitita cha fedha, wakapiga picha, zikaenea mitandaoni. Endapo mchezaji huyu akiuzwa kwenda timu nyingine kwa kitita kirefu zaidi, ni mwanachama gani mwenye uhalali wa kuhoji matumizi ya pesa za mauzo yake? Maana hakuna mwanachama anayejua pesa za manunuzi yake zilitoka wapi, ndio maana nimesema kwamba ni biashara ya watu binafsi.


Kama Simba Sc ingekua ni kampuni, leo hii mambo yangekua tofauti. Timu ingeweza kujitegemea kiuchumi, ingekua na waajiriwa wa kudumu ambao wangeifanya timu hii kuwa biashara ya kudumu kwa faida ya wanachama na wapenzi wote kwa ujumla na si kwa watu wachache peke yake. Makampuni mbali mbali yangeweza kuwekeza kwenye timu hii kwasababu imani ya matumizi ya pesa ingekuwepo.
 Eliya Rioba.

MKE WA SUGU KUNANI..APEWA MAKAVU LIVE LIVE INSTAGRAM

0
0

Nimekutana na hii Hapa Embu jisomee Mwenyewe..maana mweeeee


NI WAKATI SASA WA MBOWE KUACHIA NGAZI CHADEMA

0
0

Kutokana na trend ya maendeleo ya chama ya siku za hivi karibuni, kuanzia kwenye uchaguzi wa madiwani, nashawishika kwamba huu ni wakati mzuri sasa wa Mbowe kuondoka. Ni dhahiri kwamba Mbowe ameshindwa kukiongoza chama au anazeeka kama mwenzake Lipumba kiasi cha kukifanya chama kianze kupoteza mwelekeo na watu wengi kuanza kurudisha imani kwa CCM. Sikutegemea kabisa kwamba Kalenga tungeshindwa vibaya kiasi hiki, despite resources tulizotumia kwenye kampeni. Na kwa matokeo haya ya Kalenga, ni dhahiri kule Chalinze hata kura 5000 hatutafikisha. 

Hata NCCR na CUF walianza kuporomoka polepole hivi hivi na mwisho wa siku wakapotea kabisa. Naanza kuona dalili za CHADEMA kupoteza mwelekeo siku za hivi karibuni. Chini ya utawala wa Mbowe naona hatuwezi kuwa na jipya kwa sasa kama chama. Amefanya kazi kubwa na nzuri sana ya kukiwezesha CHADEMA kukuwa na kufikia kuwa chama kikuu cha upinzani, lakini kwa sasa mbinu zake zimeexpire! Matumizi makubwa ya fedha za chama yasiyokuwa na matunda mazuri kwa kweli yafikie mwisho. 

Tunataka kuona returns za kile tunachospend. Naamini Mbowe atajitathimini na kuamua kwa nia njema kabisa kutogombea katika kinyang'anyiro cha mwenyekiti wa chama kwenye uchaguzi wa chama ujao.

By Lokolo From JF

WOLPER: LAZIMA NIOLEWE NJE YA NCHI

0
0
Na Hamida Hassan

STAA wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper ameibuka na kudai kuwa, atafanya kila njia ili aolewe na mwanaume wa nje ya nchi na siyo Wabongo ambao hawathamini mastaa.

Akizungumza na Uwazi, Wolper alisema, amefikia uamuzi huo kwa sababu ana uchungu moyoni unaotokana na dhana waliyonayo wanaume wa Kitanzania juu yao, wakiamini kuwa ni wahuni tu hivyo kuwashusha thamani.

“Unajua Mtanzania anamchukulia staa kama chombo cha starehe tu na hawezi kumuoa kamwe na hata akimuoa basi hatamthamini kama wanavyothaminiwa wasanii wa huko nje.

“Kule bwana (hajataja nchi) mtu akimuoa staa, anampa kipaumbele. Anaweza hata kutumia fedha kuhakikisha anakuwa na staa na maisha ya mke wake yanakuwa yenye amani lakini hapa kwetu tunadharaulika sana ndiyo maana nimefikia uamuzi huu,” alisema Wolper na kuongeza:

“Unajua Watanzania wanaamini staa kuandikwa magazetini ni uhuni lakini wanasahau kuwa maisha yake na magazeti ni kitu cha kawaida kwa sababu ya kujulikana. Mimi sina haja ya kueleza sana lakini naapa kabisa, mimi siwezi kuolewa na Mbongo.”
GPL

TUNDU LISSU:SITTA ANANITONESHA VIDONDA

0
0
Mjumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, Tundu Lissu amesema ktendo cha Mwenyekiti wa Bunge la Katiba kubadilisha kanuni kwa kutoa muda zaidi wa kuwasilishwa kwa rasimu ya katiba, kinamkera.

Lissu alisema kitendo kama hicho ndicho kilichomfanya yeye na mjumbe mwenzake, Ismail Jussa kutaka kujiuzulu mara mbili kutokana na kupingana na wajumbe wenzao.

Akizungumza na gazeti hili jana mjini hapa, Lissu alisema walitaka kujiuzulu kutokana na kuchoshwa na wajumbe kufikia makubaliano ndani ya vikao, lakini wakitoka nje wanarudi na mabadiliko.

“Tulikuwa hatusongi mbele tunafanya uamuzi na kufikia makubalino, lakini wenzetu baadaye wanaenda kujadiliana upya na kuja na mapendekezo tofauti na kuturudisha nyuma,” alisema Lissu.

“Baada ya majadiliano yao, mimi na Jussa tuliomba tujiondoe lakini walituomba tusijiuzulu kwa masharti kuwa tunachokubaliana  hawataweza kubadilisha.”

Alisema kile ambacho kimeanza kutokea sasa ni kitendo cha Mwenyekiti Sitta kubadilisha kanuni ya 47 (a) ya Bunge hilo juu ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kupewa muda unaofaa kuwasilisha rasimu katika Bunge Maalumu la Katiba.

Lissu,  ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), alisema pia hata kubadilisha kanuni kwa kupokea kwanza taarifa ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na baadaye ndipo Rais Jakaya Kikwete azungumze ni jambo wanalolipinga.

BABU SEYA, PAPII FURAHA UPYA! WAKILI ANASA USHAHIDI WA KUWATOA GEREZANI

0
0
Na Elvan Stambuli na Haruni Sanchawa

MWANAMUZIKI mkongwe nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ anayetumikia kifungo cha maisha jela na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kwa kuwanajisi watoto tisa, wana furaha upya baada ya mwanga wa kuweza kurudi uraiani kuchomoza tena, wakili wao, Mabere Nyaucho Marando amezungumza na Uwazi.

KASORO HUKUMU YA MWANZO Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam, Marando alisema kwamba katika kesi ya Babu Seya na mwanaye iliyosikilizwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar aligundua kuna vielelezo muhimu ambavyo havikuambatanishwa hivyo kuwa vigumu kwake kuviingiza na kuvitetea katika ngazi ya mahakama ya rufaa iliyoshindilia adhabu dhidi ya wawili hao.

Marando alisema mwanga mwingine wa kupitiwa upya wa mashitaka yao umekuja baada ya kuwepo kwa kesi mpya inayofanana na ya akina Babu Seya kwa asilimia mia moja. Alisema kesi hiyo ipo kwenye hatua ya mwisho ambapo ushindi wake utamfanya apate nguvu ya kurudi mahakamani kuwatetea wafungwa hao waliohukumiwa mwaka 2004.

DIRA KWENYE KESI HIYO “Kuna kesi mahakama kuu kanda moja nchini inayotetewa na wakili maarufu (jina tunalo). Hii kesi inafanana sana na ya akina Babu Seya. Uzuri wake ina dalili zote za washtakiwa kuibuka na ushindi wa kishindo. MAHOJIANO Mazungumzo kati ya Marando na Uwazi yalikuwa hivi:

Uwazi: Lakini mheshimiwa kesi ya Babu Seya si ilifika katika rufaa mara tatu na wakashindwa na ulisema hakuna namna tena, sasa itakuwaje kurejeshwa tena huko? Marando: Ni kweli, lakini ni jambo linalowezekana.

Nimesema kama hiyo kesi ninayoitaja watashinda na wanaweza kushinda, basi mimi nitaenda kwa Nguza na kumwambia wazo langu, akikubali nitaiandikia barua mahakama ya rufaa kuomba kupitiwa tena kwa yale mashitaka, nitajenga hoja.

Uwazi: Hiyo kesi unayoingoja hukumu yake inahusu nini? Marando: Inahusu kubaka na kulawiti, ni kama hii ya Babu Seya na wanawe. Hakuna tofauti. Sasa washitakiwa wale wakishinda ndipo hoja inapokuja, kwa nini vipengele vilevile viwatie hatiani akina Babu Seya wengine viwaweke huru, ndivyo inavyokuwa katika kesi. Uwazi: Ukiwaandikia mahakama ya rufaa wakakubali, majaji walewale watasikiliza ombi lako?

Marando: Hilo ni la mahakama lakini idadi inaweza kuongezwa na kufikia majaji sita au saba.Uwazi: Una hakika utashinda na kukubaliwa? Marando: Kama nilivyokueleza, ikipita ile kesi halafu mahakama ya rufaa wakakubali kupitia tena jalada, nina uhakika wa kushinda.

ANALIPWA NA NANI? Wakili huyo maarufu alisema yeye aliwatetea wanamuziki hao bure kwenye kesi yao ikiwa katika ngazi ya mahakama ya rufaa baada ya kusoma jalada lenye kurasa 1,362 ambapo aligundua kuwa kuna nyaraka kadhaa ambazo hazikuambatanishwa katika Mahakama ya Kisutu ambazo zingeweza kuwaokoa na kifungo wateja wake.

“Unajua kesi inapokuwa mahakama ya rufaa, majaji wanachofanya ni kupitia jalada si kusikiliza, hivyo haiwezekani kuambatanisha vielelezo vipya,” alisema Marando ambaye anajipambanua kuwa awali alishinda nusu kwa kuwatoa nje watoto wa Babu Seya, Mbangu na Francis Nguza ambao nao walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa moja na wafungwa hao.

HUKO NYUMA Juni 25, 2004 Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam, Addy Lyamuya aliwatia hatiani kwa ubakaji na ulawiti Babu Seya na wanawe Papii Kocha, Mbangu na Francis. Januari 27, 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu hiyo.

Wakili Marando akapeleka suala hilo Mahakama ya Rufaa Tanzania ambako Mbangu na Francis waliachiwa huru na yeye kutangaza kwamba ameshinda nusu. Babu Seya na wanawe walidaiwa kutenda makosa 10 ya kubaka na kulawiti watoto hao kati ya Aprili na Oktoba 2003 katika maeneo ya Sinza ya Kwaremmy, Dar es Salaam.
GPL

IF ALL GOES WELL LUPITA MIGHT BE IN "STAR WARS MOVIE"

0
0
With the movie – 12 Years A Slave - that won her an Oscar out of the way and another one in theatres – Non Stop - Kenyan Hollywood actress, Lupita Nyong’o has got to keep her feet moving. Only this time her next move will be under the microscope.

Anyway, Lupita reportedly met with J.J. Abrams about unspecified role a few weeks ago, just before the Academy Awards, about starring in the next installment of the Star Wars franchise, reports the Hollywood Reporter.

It’s still not clear what role Nyong’o might be up for as the Star Wars director has remained tight-lipped. There are reportedly two characters in their 20s as well as a descendant of Obi-Wan Kenobi - which has been described as a non-Caucasian role - she could play.

Lupita’s stardom has closely been building throughout the awards season and in the last few weeks she found herself in the mix for the high-profile role of “Tiger Lily” in Warner Bros.’s Pan. She is also in the running for a role in The Whole Truth, a courtroom drama starring Daniel Craig.

Star Wars: Episode VII opens on Dec. 18, 2015.
Viewing all 104423 articles
Browse latest View live




Latest Images