Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104427 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli amteua Humphrey Polepole kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Hamphrey Polepole kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mkoani Mara.

Bw. Hamphrey Polepole anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Musoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (Mstaafu) Zelothe Steven ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

Uteuzi wa Bw. Hamphrey Polepole umeanza leo tarehe 18 Aprili, 2016

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
18 Aprili, 2016

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya April 19, Ikiwemo ya Lugumi Giza Nene Bungeni

0
0
SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya April 19

Jengo la Machinga Complex Lina Deni la Bilioni 36, Paul Makonda Abaini Madudu zaidi....Ni Miongoni Mwa Miradi Yenye Ufisadi Mkubwa

0
0
Mkuu  wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza kufanyika kwa uchunguzi jengo la Machinga Complex kubaini uhalali wa mkataba uliowezesha ujenzi wa jengo hilo, ikiwa ni pamoja na gharama halisi za ujenzi.

Alisema hayo kutokana na jengo hilo kuwa na deni la zaidi ya Sh bilioni 36, kiasi ambacho ni mara tatu ya thamani halisi ya jengo hilo na kuleta shaka ya ufisadi ndani yake. Jengo hilo lina thamani ya Sh bilioni 12.

Alisema kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa itaanza kufanya uchambuzi wa mkataba ili kupata uhalali wa gharama na kujua kiwango kinachostahili kulipwa na wafanyabiashara hao.

“Katika miradi mingi duniani huu ni wa aina yake, mradi ambao kabla haujaanza unaweka jiwe la msingi unaanza kudaiwa benki, mpaka unakuja kumaliza deni lako ni kubwa linakaribia robo mbili au tatu ya mkopo wenyewe, kabla hata hujaanza kupangisha hata mtu.

“Kwa takwimu zinaonesha tumekopeshwa na jengo limejengwa Sh bilioni 12.7, lakini mpaka dakika hii mnadaiwa Sh bilioni 36 na nyinyi ndio mnatakiwa kuzilipa, sasa kwa maelezo hayo ndio mnapata picha kwa nini tumeamua kujipa muda,” alisema Makonda.

Alisema katika maelezo ya awali yanaonesha kuwa jengo hilo lina mkanganyiko mkubwa na inawezekana kuwa ni miongoni mwa miradi iliyofanyiwa ufisadi mkubwa.

Hivi karibuni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simbachawene aliifuta bodi inayosimamia jengo hilo na kumsimamisha kazi meneja anayesimamia jengo hilo na kumtaka kwenda katika ofisi za jiji kwa ajili ya kumpangia kazi nyingine.

Katika hatua nyingine, Simbachawene alilikabidhi jengo hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuwaingiza wafanyabiashara bila masharti huku ukiangaliwa utaratibu mpya kwa wafanyabiashara hao.

Mkuu wa Idara ya Utumishi Jijini Mwanza Kikaangoni Kwa Mikopo ya Watumishi Hewa

0
0
 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amemueleza Mkuu wa Idara ya Utumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Sigrifid Kaunala kuwa ni miongoni mwa watumishi watakaochunguzwa kutokana na kugundulika kuwepo kwa baadhi ya watumishi hewa waliopata mamilioni ya fedha kama mikopo kutoka taasisi za fedha.

Mongella alitoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Jiji hilo ambao pamoja na mambo mengine alitumia nafasi hiyo kuzungumzia suala la watumishi hewa.

Alisema baada ya uchunguzi wa uhakiki wa awamu ya pili wa watumishi hewa uliofanywa na Serikali mkoani humo umebaini kuwepo kwa watumishi watano (majina yao yanahifadhiwa) waliojipatia mikopo ya mamilioni ya fedha kutoka taasisi za fedha hali inayoonesha baadhi ya mikopo hiyo isingetolewa bila ya kibali cha waajiri wao.

“Mkuu wa utumishi nasikia hata wewe unahusika kwenye sakata hili la watumishi hewa, haiwezekani mambo haya yatokee na wewe usijue na wewe ni miongoni mwa watu tunaowachunguza,” alisema Mongella.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mkoa ya kuhakiki watumishi hewa, Waryoba Sanya alisema kazi ya kuhakiki watumishi walioko kazini lilianza jana kwa kuanza na uhakiki wa watumishi wote wa Ofisi Kuu ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza walioko kazini na kuwa lilikuwa linaendelea vizuri.

Wagombea Urais 11 CCM Wapewa Kazi Serikalini

0
0
Rais John Magufuli amemteua Mathias Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.

Huu ni mwendelezo wa kuwakumbuka kwa kuwapangia majukumu ya kitaifa baadhi ya makada wa CCM waliopambana naye katika mbio za kuwania nafasi ya urais kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Kabla ya kupangiwa kituo hicho cha kazi, Chikawe aliteuliwa kuwa balozi Februari 15, mwaka huu sambamba na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi wa Taifa (NSSF), Dk Ramadhani Dau na Dk Asha-Rose Migiro.

Chikawe, ambaye ameanza kutekeleza majukumu yale tangu Aprili 13, alikuwa miongoni mwa makada 38 wa CCM waliochukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM.

Makada waliokumbukwa

Makada wengine waliokumbukwa katika Serikali ya Magufuli ni Profesa Sospeter Muhongo, Dk Harrison Mwakyembe, January Makamba, Mwigulu Nchemba, Dk Khamis Kigwangalla, Balozi Augustino Mahiga na Dk Asha-Rose Migiro.

Ukimuondoa Dk Migiro anayesubiri kupangiwa kituo cha kazi baada ya awali kuteuliwa kuwa balozi, waliobaki kwa sasa wanamsaidia Rais baada ya kuwateua kuwa mawaziri.

Baada ya kuapishwa, Rais Magufuli, alimteua Dk Mahiga kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kitaifa.

Dk Mwakyembe, aliteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Akamteua Makamba kuwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

Wengine ni Luhaga Mpina aliyemteua kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Dk Khamis Kigwangwalla (Naibu Waziri Afya, Maendeleo, Jinsia, Wazee na Watoto), Mwigulu Nchemba (Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi). Rais Magufuli alimteua pia Profesa Muhongo kuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Makada visiwani

Kwa upande wa visiwani Zanzibar, makada waliopambana na Magufuli kupitia CCM na wameteuliwa na Rais Ali Mohamed Shein kushika nafasi za uongozi kwenye Serikali yake ni Balozi Amina Salum Ali na Balozi Ali Karume, ambao wote waligombea nafasi za urais wa Tanzania.

Akitoa maoni yake kuhusu uteuzi wa Magufuli, mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Kessy alisema: “Kugombea nafasi kama hiyo siyo kuwa maadui, mbona hata Rais mstaafu Kikwete (Jakaya) aliwahi kufanya hivyo,”alisema.

Mwingine aliyeunga mkono hatua ya Rais ni mwanasheria maarufu nchini, Profesa Abdallah Safari aliyesema Rais ana haki ya kumteua mtu yeyote anayemuona anaweza kumsaidia katika uongozi.  

Chanzo:Mwananchi

Utata Wazuka Kuhusu Mtu Aliyepoteza Maisha Kwenye Ajali ya Tundaman

0
0
Utata umeibuka kuhusu mtu aliyefariki kwenye ajali ya gari aliyokuwa amepanda Tundaman kutokea Njombe kuja Dar es Salaam, Jumapili hii.

Kwenye ajali hiyo, alifariki dereva aliyekuwa akiendesha aliyejulikana kwa jina la Man Katuzo. Hata hivyo imebainika kuwa, Katuzo hakuwa tu dereva, bali ndiye alikuwa bosi wa Tunda kwenye show hiyo na ndiye aliyekuwa akigharamika kwa kila kitu. Taarifa hiyo imebainika kupitia segment ya ‘Simu ya Mwisho’ inayoendeshwa na rapper Baghdad kupitia kipindi cha Papaso cha TBC FM.

Hii ni taarifa ambayo Baghdad ametutumia baada ya kuongea na ndugu wa marehemu:

Baghdad alizungumza na kaka wa marehemu ambaye ndiye msemaji wa familia juu ya kifo cha mdogo wake ambapo alithibitisha taaarifa ya kifo cha mtu mmoja ambaye hamkumtaja jina ambaye alikuwa ameketi siti ya mbele na kusema kweli Tundaman alikuwepo kwenye gari iliyopata ajali lakini hakuumia.

Aidha kaka yake aliendelea kusema ya kuwa amesikitishwa na kitendo cha wakati wa tukio Tunda aliingia kwenye gari aina ya Noah iliyokuwa kwenye msafara mmoja na gari ya marehemu na kuendelea na safari na walipofika Mikumi askari walisimamisha gari na kuikagua na kukuta bag la marehemu lenye camera 2 aina ya 5d mac 3 na lenzi tatu ambazo zililiripotiwa kupotea kwenye ajali hiyo

Kaka wa marehemu amesema Tunda hakupaswa kutokuja kumzika marehemu Man Katuzo na hajui sababu ingawa alijaribu kumpigia sana simu yake na hakupokea na kuomba kuliweka sawa kwa jamii ya kuwa simu ya marehemu kwa mara ya mwisho alipewa aishike mpaka sasa haionekani, na kama kuna lolote ambalo ni haki ya marehemu kuna yoyote alihusika kulichukua wameamua kumuachia Mungu na kusahihisha usemi wa Tundaman kuwa aliyekufa alikuwa ni dereva wake,hapana bali ndiye bosi wake ambaye alimgharamia kila kitu toka Dar kwenda kwenye show na kurejea. Marehemu Man Katuzo ameacha mke bila mtoto na amezikwa jana tar 19/4/2016 kijijini kwao Kilosa mjini Morogoro.

Kwa upande wake Tundaman alipost video inayomuonesha Katuzo enzi za uhai siku chache kabla ya mauti na kuandika: Dah nikiangalia hii video nazidi kuumia ila sisi tulikupenda ila mungu alikupenda zaidi maneno ulioniambia kuhusu familia i promise sitoyapuuza..mungu ailaze roho ya marehem musa katuzo mahali pema peponi..aamen.”

Katuzo aliyekuwa akiishi nchini Afrika Kusini, alikuwa aachie wimbo wake uitwao ‘Nguzo Saba za Sanaa’ aliomshirikisha Tundaman.

Chini ni baadhi ya picha za marehemu na mke wake:

Chanzo:Bongo5

Kigamboni Bridge: Tanzania Has Just Built East Africa’s Longest Suspension Bridge

0
0
Tanzanian President John Magufuli will tomorrow officially open the most magnificent bridge in the region.

Dubbed ‘Kigamboni Bridge’, it will connect Dar es Salaam’s central business district to Kigamboni ward across the Kurasini creek. Construction started in 2012, and the project has cost more than KSh13 billion.

The 680 metre long cable-stayed bridge is the first of its kind in East Africa. However, it is still not the longest bridge in Tanzania. That fete goes to ‘Mkapa Bridge’, which is almost a kilometre long.

Unity Bridge that connects Mozambique and Tanzania is the second longest at 720 metres, while the new Kigamboni Bridge completes the top 3.

Here in Kenya, Kilifi Bridge is listed as the longest bridge with a total length of 420 metres. Nyali Bridge is only 391 metres long. Kenya has at least one suspension bridge, but none long enough to break any records.

For instance, this Masalani Bridge across River Tana is barely 100 metres. 



Tanzania’s Kigamboni Bridge is East Africa’s first suspension bridge worth its salt and one of 3 in Sub-Saharan Africa (minus South Africa).

It is owned by Tanzanian government and NSSF – 40% and 60% respectively. It is replacing the MV Magogoni ferry.

Kigamboni Bridge is a toll bridge, meaning vehicles will be charged to pass through.

Here are some photos:








Hofu Yatandaa Shkuba Kinara wa Madawa ya Kulevya Kutoroka Gerezani

0
0
Kufuatia kuendelea kushikiliwa kwa kigogo anayedaiwa kujishughulisha na biashara ya madawa ya kulevya ‘unga’, Ali Khatib Haji ‘Shkuba’ (pichani) katika Gereza Kuu la Mkoa wa Lindi, hofu imezidi kutanda kwa madai kwamba, mfanyabiashara huyo yupo kwenye maandalizi ya kutoroka gerezani hapo, Uwazi limechimba kwa kina.

BOMBA LA MAJI LATAJWA
Habari zilizolifikia gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita na kutiliwa nguvu na hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea gereza hilo, zilieleza kwamba, kuna ‘mchongo’ unaofanywa na vigogo kadhaa wa unga kwa lengo la kumtorosha Shkuba, wakitumia kivuli cha mradi wa kuingiza bomba la maji gerezani hapo ambapo pengine hata wenye mradi huo hawajui lolote.
“Kuna bomba linachimbwa kuingia gerezani, wenyewe wanasema ni mradi wa kulipatia gereza hilo maji lakini kuna tetesi kwamba huenda bomba hilo ndiyo njia ya kutaka kumtolea Shkuba gerezani lakini wenye mradi hawana habari.

NJAMA ZAFANANISHWA
“Si unajua hata El Chapo (kigogo maarufu wa unga nchini Mexico), alitoroshwa kupitia bomba la chooni? Hakuna aliyejua kumbe wenzake ambao ni Mafia walikuwa wakilipigia hesabu bomba lile la chooni kuja kushtuka, El Chapo ameshatoka,” kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa jina.
Baada ya kupata taarifa hiyo, Uwazi lilianza kufuatilia kwa kina ili kujua kuhusu mradi huo lakini wakati uchunguzi ukiendelea, Waziri Mkuu Majaliwa naye alichezwa na machale na kuuzungumzia mradi huo.

Akiwa ziarani mkoani Lindi hivi karibuni, Waziri Majaliwa alimtahadharisha Mkuu wa Gereza la Lindi, Tusikile Mwaisabila kuwa makini na zabuni wanazotoa gerezani hapo, ikiwemo ya uwekwaji wa mabomba ya maji kwani inaweza kutumika kuwatorosha vigogo wa unga, akasisitiza kwamba ulinzi uimarishwe ili kuhakikisha hakuna kigogo wa unga atakayetoroka.

MSIKIE WAZIRI MKUU
“…hata hili bomba la maji linalopeleka maji gerezani lisije likawa ni njia, simamieni sana hili,” alisema waziri Majaliwa akimaanisha kuimarisha ulinzi katika gereza hilo kwa hofu kwamba watuhumiwa wa unga wasije wakatumia nafasi hiyo kutoroka.


WAZIRI KITWANGA
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Uwazi lilimtafuta Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga ili kumuuliza kuhusu kudaiwa kwamba mradi huo unaweza kutumika kutaka kumtorosha Shkuba ambapo alipopatikana kwa njia ya simu asubuhi na kusomewa maelezo hayo mwanzo hadi mwisho, alimsukumia mzigo Kamishna Jenerali wa Magereza Tanzania, John Minja kwamba ndiye anayetakiwa kujibu kuhusu mradi huo na hali ya ulinzi gerezani hapo kufuatia uwepo wa watuhumiwa wa madawa ya kulevya.

“Sasa hilo tafadhali sana muulize Kamishna wa Jeshi la Magereza Tanzania, atakwambia nini kinaendelea,” alisema Waziri Kitwanga.

MSEMAJI WA MEGEREZA
Jitihada za kumpata Kamishna Minja ziligonga mwamba kutokana na simu yake kutopatikana hewani kila alipopigiwa lakini badala yake, alipatikana Msemaji wa Jeshi la Magereza Tanzania, Deodatus Kazinja ambaye kimsingi ndiye mwenye kujua mambo ya magereza yote nchini.

Katika mahojiano na Uwazi, Kazinja alikiri kuwepo kwa mradi huo lakini akaeleza kwamba wanafuatilia kwa kina kujua ni nani aliyepewa zabuni ya kuingiza mabomba ya maji gerezani hapo na lini na kuangalia kama kuna uhusiano wowote kati ya mzabuni huyo na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya walioko gerezani humo.

“Nitafuatilia, nipe muda nijue mradi ulianza lini na nani mwenye zabuni hiyo na uhusiano wake na madai hayo,” alisema Kazinja.

KAMISHNA MINJA KUWASILI
Habari za uhakika kutoka gerezani hapo zinaeleza kwamba siku yoyote kuanzia Jumapili iliyopita,  Kamishna Minja angewasili kwenye gereza hilo ambapo pamoja na mambo mengine atafuatilia hali ya usalama wa gereza hilo pamoja na watuhumiwa wa unga waliopo mahabusu.

KIKAO KIZITO CHA GEREZA
Pia, taarifa zilizotufikia wakati tunakwenda mitamboni zinasema kuwa, jana Jumatatu, baadhi ya vigogo wa gereza hilo walitarajia kukaa kikao kizito cha dharura kuangalia mustakabali mzima wa ulinzi gerezani hapo pamoja na madai kwamba, mradi huo wa kuingiza maji unaweza kutumika kutaka kumtorosha Shkuba na wenzake.

KAULI ILIYOWAHI KUTOKA
Wiki chache zilizopita, Kamishna Minja alipokutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya jijini Dar alikaririwa akisema:

“Jeshi la Magereza limekuwa na changamoto ya uhaba wa fedha za kufanya ukarabati na upanuzi wa magereza za zamani ili yawe na miundombinu inayoendana na ongezeko la wafungwa na mahabusu.
“Mfano mzuri unapokuwa na mtu kama Shkuba ambaye ni hatari hata kwa nchi kama Marekani, imetulazimu kuongeza ulinzi katika Gereza la Lindi ambalo yupo mahabusu mpaka sasa.”
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umedhihirisha kwamba, tangu kauli hiyo ya waziri mkuu, ulinzi kwenye gereza hilo umeimarishwa maradufu ambapo askari wengi wameonekana wakirandaranda gerezani hapo kwa saa ishirini na nne kuhakikisha hakuna ‘figisufigisu’ yoyote inayoweza kutokea na kusababisha Shkuba na wenzake kutoroshwa.

Shkuba alinaswa saa sita usiku wa Februari 23, 2014 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar akijiandaa kwenda nchini Afrika Kusini na kuhusishwa na unga aina ya heroin kiasi cha kilo 211 yenye thamani ya shilingi bilioni 9.4 uliokamatwa Januari, mwaka huo mkoani Lindi.

Baada ya kukamatwa, alisafirishwa usiku huohuo kwenda Lindi chini ya ulinzi mkali wa polisi ambapo Februari 27, mwaka huo aliunganishwa na watuhumiwa wengine na kufikishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kusini.

Watuhumiwa hao wengine ni pamoja na binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, Maureen Liyumba.

ULINZI KEKO, SEGEREA
Mbali na Gereza la Lindi, ulinzi umeimarishwa pia katika Magereza ya Keko na Segerea jijini Dar es Salaam ambako vigogo wengine wa unga wanashikiliwa.

Taarifa zilizopatikana kutoka vyanzo vyetu makini kutoka katika Gereza la Keko zinaeleza kuwa, ulinzi ulianza kuimarishwa tangu mwaka jana baada ya magaidi kutishia kuvamia maeneo yote ya magereza yanayohifadhi wenzao wakiwemo wale waliohusika kupiga Kituo cha Polisi Stakishari, Dar.

Mkuu wa Gereza la Keko, Kibwana Sinashida alipohojiwa kuhusu hali ya usalama gerezani hapo, alisema imeimarishwa na hawana hofu katika hilo.
Kwa upande wa Gereza la Segerea, chanzo kilisema kuwa umeimarishwa kwani hata zana na vitendea kazi vya kisasa vipo vya kutosha.

Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Katika Magazeti leo

VIDEO:Rais Magufuli Amuapisha Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe Mathias Chikawe Ikulu Jijini Dar es Salaam

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli amemuapisha Balozi wa Tanzania nchini Japani asubuhi hii  Mhe.Mathias Chikawe Ikulu jijini Dar es Salaam.

Waziri Nape aufuta mchakato wa Vazi la Taifa. Ashauri kila kabila litumie vazi lake

0
0
Mhe. Nape Nnauye ametoa tamko la kuufuta mchakato wa kutafuta vazi la Taifa na kuagiza kila kabila litumie vazi lake.

Uamuzi huu alioutoa akiwa ziarani Singida, anasema umetokana na ugumu wa kupata vazi hilo, kukosa mifano ya nchi iliyofanikiwa kupata vazi kupitia mchakato kama wetu na zaidi ni enforcement ya uvaaji.

Akachekesha kwa kuhoji, "Kama uvaaji wake utakuwa ni kwa amri kama magwanda ha jeshi au ni hiari?"

Hivyo, kwa kauli yake huo mchakato umefikia ukomo wake.

Tundaman Adaiwa Kudanganya Kuwa Alikuwepo Kwenye Gari Lililopata Ajali na Kumuua Rafiki yake....

0
0
Najaribu kufikiria nje ya box Kama ni kweli huu uongo wa ajali ya Tundaman kwa faida ya nani?
Kwenye mitandao kunaenea habari kuwa Mwimbaji Tunda Man hakuwa kwenye gari lililopata ajali juzi wakati wakutoka kwenye show ambapo ajali hiyo ilipoteza maisha ya rafiki wa karibu wa Tundaman.....Inasemekana Tunda Man alikuwa kwenye gari ya Noah ambayo ilikuwa imeongozana na Gari iliyopata ajali lakini baada ya ajali Tunda akajifanya na yeye alikuwepo ndani ya gari hiyo...

Soma hapa kinachoendelea mitandaoni:

Breaking News: Rais Magufuli Amsimamisha Kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe

0
0
Rais Magufuli amemsimamisha kazi mchana huu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Wilson Kabwe kutokana na ufisadi wa kutisha katika utekelezwaji wa mikataba mitatu, inayohusu maeneo ya ukusanyaji mapato ya Stendi Kuu ya Mabasi Yaendayo Mikoani ya Ubungo na kodi ya uegeshaji magari katikati ya mji  na  kuisababishia  serikali  hasara  ya  bilioni 3.

Rais Magufuli amechukua uamuzi huo mchana huu wakati wa uzinduzi wa daraja la Kigamboni, ambapo kabla ya Rais kuhutubia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Paul Makonda alitoa Hotuba fupi ya maswala kadhaa ya Mkoa wa Dar es Salaam  ikiwemo  ripoti ya tume aliyounda  kuchunguza utekelezwaji wa mikataba hiyo.

Akieleza zaidi, Makonda  amesema, Kamati aliyounda  ilibaini kuwa pale ubungo kunatumika sheria ndogo mbili za ukusanyaji mapato moja ya mwaka 2004 na nyingine ya mwaka 2009  ambazo zote zilisainiwa na Wilson Kabwe.

Amesema  kuwa Sheria  ya Mwaka 2004 ya ukusanyaji mapato, inaonesha kuwa kila basi  linaloingia Ubungo linatakiwa kutozwa Sh 4,000, hivyo makusanyo halisi kwa mwezi ni Sh milioni 42 kutokana na mabasi 350 yanayoegeshwa kituoni hapo   na   Sheria  ya Mwaka 2009 ya ukusanyaji mapato, inaonesha kuwa kila basi  linaloingia Ubungo linatakiwa kutozwa Sh 8,000, hivyo makusanyo halisi kwa mwezi ni Sh milioni 82  kwa mwezi

Makonda amesema kwamba, Kabwe alisaini mikataba miwili, wa 2004 na wa mwaka 2009  ambapo ule wa mwaka 2004  ulipelekwa jiji  na  ule wa 2009 ukapelekwa kwa mzabuni, hivyo jiji wanajua kuwa basi linatozwa sh. 4000 kwa  siku wakati mzabuni  anatozwa  8000 kwa siku

Kutokana  na  maelezo hayo, Mheshimiwa Rais ametangaza kumsimamisha kazi bwana Kabwe ambaye  ni  Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam  na ameagiza vyombo vya dola vianze uchunguzi mara moja ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa

Kamanda Kova Aibuka Sakata la Ufisadi wa Lugumi

0
0
Kamanda Mstaafu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (pichani) ameibuka kufuatia ‘kubumburuka’ kwa sakata linalomhusu mfanyabiashara Said Lugumi, anayemiliki kampuni ya Lugumi Enterprises inayodaiwa kuingia mkataba tata na Jeshi la Polisi Tanzania.
Mkataba kati ya Lugumi Enterprises na jeshi hilo ulisainiwa mwaka 2011, ulihusu kufungwa kwa vifaa vya kuchukulia alama za vidole katika vituo 108 nchi nzima kwa gharama ya shilingi bilioni 37. Lakini hadi sasa, vifaa hivyo vimefungwa katika vituo 14, vyote vikidaiwa kuwa ni vya Dar es Salaam lakini bila kujulikana sehemu.

Kova, ndiye aliyekuwa Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam wakati vifaa hivyo vikifungwa katika vituo 11 vya Polisi huku ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi ikiwa chini ya Said Mwema. Kampuni hiyo inadaiwa kulipwa karibu asilimia 99 ya fedha zote za makubaliano.

Akizungumza kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki iliyopita, Kova ambaye alidai yupo kijijini kwao akijishughulisha na kilimo, alisema hajui lolote kuhusu Lugumi, kwa sababu kule aliko hakuna magazeti wala vyombo vingine vya habari zaidi ya mitandao.

“Mimi nilikuwa nashughulika na wahalifu na Lugumi hakuwa mhalifu, siwezi kumzungumzia lolote kwa sababu mimi nimeshastaafu. Huku nilipo sipati taarifa zozote za kiofisi, nimekuwa kama samaki nje ya maji, sina nguvu zozote,” alisema kamanda huyo.

Aliongeza: “Lakini Lugumi namfahamu ila si kwa hilo sakata la vifaa vya kuchukulia alama za vidole ndugu yangu.”

Sakata la Kampuni ya Lugumi Enterprises liliibuliwa kwa mara ya kwanza na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) chini ya Makamu Mwenyekiti, Aeshi Hilary, April 6, mwaka huu, baada ya kubaini utata wa utekelezaji wake na kuagiza kupelekwa kwao ili kujua masharti yaliyomo.
GPL

VIDEO:Rais Magufuli Azindua Rasmi Daraja la Kigamboni

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe huku viongozi wengine wakiushikilia kuashiria uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipata picha ya kumbukumbu viongozi wengine baada ya  uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. John Magufuli amekataa daraja la Kigamboni  lisiitwe ‘Daraja la Magufuli’ na badala yake ameshauri lipewe jina la muasisi wa Taifa hili, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Akiongea wakati wa kuzindua daraja hilo leo, Rais Magufuli amesema kuwa awali aliletewa mapendekezo  na waziri mwenye dhamana akimtaka aridhie daraja hilo lipewe jina lake, lakini kwakuwa wazo la ujenzi huo lilianza tangu wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere, alikataa na  kushauri jina  la Nyerere litumike .

“Nilikataa lisiitwe kwa jina langu kwa sababu wazo  la ujenzi wa daraja hili lilianza  mwaka 1979 wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.

“Wazo hilo halikufanikiwa kutokana na ukosefu wa pesa wakati huo. Mwalimu Nyerere ni kiongozi aliyejenga  misingi imara katika taifa letu.

“Alikuwa ni kiongozi asiyebagua mtu kwa misingi ya dini, chama au kabila. Alifanikiwa kutuunganisha watanzania wote bila kujali itikadi zetu.

“Leo hii, daraja hili limekamilika, ni daraja ambalo halitambagua mtu kwa sababu wa CCM watapita hapa, wa Chadema watapita hapa na bahati nzuri mstahiki Meya wa jiji hili  ambaye ni Chadema naye yuko hapa na amepita katika daraja hili.

“Ndugu zangu sistahili sifa zozote, najua nimefanikisha ujenzi huu  nikiwa waziri wa ujenzi, lakini wakati huo nilikuwa natimiza wajibu wangu kama mtumishi wa umma, hivyo nashauri hili daraja liitwe daraja la Nyerere ili tuweze kumuenzi  mwasisi wa taifa hili” alisema  Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanalitunza daraja hilo katika kujenga uchumi wa taifa.

TAZAMA VIDEO YA HUTOBA YAKE:


Harmonize 'Sijamtukana DJ K Flip' , Hiki Ndicho Kilichotokea Hadi Kuzima Mziki Katikati ya Show

0
0
Msanii wa lebel ya WCB 'Harmonize' amefunguka kuhusu tuhuma za kumtukana Dj K Flip kwenye show mjini Mwanza.

Harmonize alisema
“Kwanza nategemea sana maDJ kwenye kazi yangu na siwezi fanya kitendo kama hicho, nilikuwa nafanya show na nikawaambia watu kuhusu ujio wa Diamond Mwanza hivi karibuni na kuwataka waimbe na mimi akapela, nikamwambia DJ azime mziki sababu utazingua, DJ hakunielewa akakasirika na kushuka chini, ila nilimfuata na kuongea naye na show ikaendelea”.

Aidha Harmonize amemalizia kwa kusema kuwa kwa sasa matatizo yake DJ K Flip wameyamaliza na wapo poa.

Idadi ya Watumishi Hewa Waliomfukuzisha Kazi Anne Kilango Shinyanga Yafika 226

0
0
Idadi ya wafanyakazi hewa katika mkoa wa Shinyanga ambao awali ulidaiwa kutokuwa na wafanyakazi hao kabisa, imeongezeka na kufikia 226.

Hayo yamebainishwa leo na Rais John Magufuli katika uzinduzi wa Daraja la Kigamboni, ambapo alisisitiza kuwa serikali yake haitawafumbia macho viongozi ambao kwa namna moja au nyingine wataruhusu mianya ya ubadhirifu wa fedha katika maeneo yao.

”Mkoa wa Shinyanga kwa taarifa nilizonazo hadi sasa wameshapatikana wafanyakazi hewa 226 kutoka ‘zero’ hivyo ni lazima tuwajibike kwa watanzania wanyonge,” amesema Rais Magufuli.

Wakati wa kuwasilisha ripoti ya Mikoa Serikalini aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela alisema mkoa wake hauna mtumishi hewa hata mmoja jambo lililopelekea Rais Magufuli kuunda tume iliyobaini watumishi  hewa  45 katika awamu ya kwanza.

Baada ya kubainika uwepo wa watumishi hao, Raisi alitangaza kutengua uteuzi wa Mkuu huyo wa Mkoa kwa kutokuwa makini na taarifa anazopewa na wasaidizi wake.

Sikumjua Nay wa Mitego ni mtu wa Aina Gani ila Baada ya Kutoka Naye Kimapenzi Nikajua - Shamsa Ford

0
0
Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford amefunguka na kusema kuwa moja ya sababu yeye kuachana na mpenzi wake Nay wa Mitego ni kutokana na ukweli kwamba yeye hakutambua toka mwanzo kuwa msanii huyo ni mtu wa namna gani.

Akizungumza kwenye kipindi cha Enews Shamsa Ford anasema wakati anaanza kutoka na Nay wa Mitego hakutambua ni mtu wa namna gani ndiyo maana aliweza kuanza naye mahusiano lakini kadili siku zilivyokuwa sikienda akagundua kuwa wana tofauti kubwa kwani tabia zao zilikuwa zikipishana sana.

Shamsa Ford alizidi kueleza kuwa awali alikuwa anaficha kama wanatoka kimapenzi na msanii huyo kutokana na ukweli kwamba kila mmoja alikuwa hana uhakika na mwenzake ndiyo maana walikuwa wanaitana "Cousin" ili hali wao ndiyo walikuwa wanajua ukweli kwamba ni wapenzi.

Mbali na hilo Shamsa Ford alisema baadaye aligundua kuwa akiwa ni mshikaji tu na Nay wa Mitego wanakuwa wanaelewana zaidi kuliko kuwa wapenzi ndiyo maana walifikia hatua kuachana na kuwa washikaji. Kwa sasa anasema amepata mpenzi mwingine ambaye ana sifa zaidi na wanapendana sana.

Mi Mzungu, Namchukulia Ney Kama Mwehu -Gigy Money

0
0
Mrembo anayefanya poa kwenye video za wasanii wa Bongo kama video model Gigy Money, amempa za uso msanii Ney wa Mitego na kumuita mpumbavu asiyejitambua ni nani, baada ya kumtapeli pesa yake.


Gigy Money ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa kama msanii hawezi kuwaimba wenzako vibaya, huku ukiacha yale mabaya yako.
“Ni upumbavu wake tu mi nilishamuonaga mwehu, kwa sababu kwa mtu ambaye anajua muziki huwezi ukaanza kuimba maisha ya wenzake wakati ya kwako yanakushinda”, alisema Gigy Money.
Pia Gigy Money amesema pamoja na kumtapeli pesa hiyo ambayo alitakiwa kulipwa baada ya kuonekana kwenye video yake ya shika adabu yako, ameamua kumpotezea kwani hana shida ndogo ndogo, na pia ameamua kuwa na tabia ya kizungu, kutojali vitu ambavyo huenda vikaleta ugomvi kati yao.
“Mi simaindi kwenye kuwekwa kwenye scene yeyote ya video as longer as nalipwa, lakini baadae tena anakuja kuniletea mambo ya kunipa hela ndogo, from laki tano to elfu 20 imagine, mi nimechukulia uzungu ningekuwa mswahili ningemdai dai, ningempigia simu, mi naendelea na maisha yangu ye atajua na maisha yake, sijawahi kumdai na wala simdai sina njaa hiyo ya hivyoo, naweza kuwa na laki tano ndani ya siku mbili au moja so what is laki tano, nigombane na watu tuwekeane mabeef kisa laki tano?”, alisema Gigy Money.

Chanzo:EATV

Mwanamuziki Baraka da Prince Ashutumiwa Kuazima Magari Nakutamba Nayo Mtaani..Mwenyewe Asema Haya

0
0
eNewz imenasa udaku kutoka mitaani kuwa msanii wa Bongo Fleva Baraka da Prince anaongoza kwa kuazima magari ya watu na kuvimba nayo mitaani

Akipiga stori na eNewz Baraka amekanusha kashfa hizo na kusema kuwa wanaosema anagongea magari ni machizi tu.
Zaidi Baraka ameongeza kuwa yeye anamiliki magari zaidi ya moja na hajawahi kuendesha gari ya mtu.

Pia Baraka hakuficha kuwa kwa sasa amekwisha mtambulisha msanii mwenzake Naj kwa wazazi wake kuwa ndiye mchumba wake, na amemvisha pete ya ahadi kuwa atakuwa naye milele daima.
Alipoulizwa kuwa pete hiyo inamaanisha ana nia ya kumuoa Naj, Baraka alisema “Kwa hilo Mungu ndiye anayejua”.
Viewing all 104427 articles
Browse latest View live




Latest Images