Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Serikali yakamata Mzigo wa Maana wa Tanzanite Ukitoroshwa nje

$
0
0
Serikali imefanikiwa kuyakamatwa madini ya Tanzanite yenye thamani ya Sh2.5  bilioni yaliyokuwa njiani kusafirishwa nje ya nchi bila kulipiwa vibali kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka jana.

Hayo yameelezwa leo jijini hapa na Kaimu Kamishna wa madini nchini, Mhandisi Ally Namaje wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya tatu ya kimataifa ya madini ya Vito yanayofanyika jijini hapa.

Mhandisi Namaje amesema madini hayo yaliyokuwa na uzito wa Kilo  mbili ni sehemu tu ya madini yanayoendelea kutoroshwa na watanzania wasiokuwa wazalendo na nchi yao lakini hata hivyo Serikali inaendelea kuziba mianya yote ya utoroshwaji wa madini hayo nje ya nchi.

"Sheria inasema baada ya madini hayo kukamatwa tunayataifisha na kuyauza kwa mnada, kwa hiyo katika maonyesho haya tutayauza katika mnada wa hadhara ili kila mtu mwenye uwezo aweze kununua," amesema Namaje.

Amesema pia katika kipindi hicho wizara yake imefanikiwa kukamata madini ya Dhahabu yakiwa njiani kutoroshewa nje ya nchi ambayo na yalikuwa njiani kuuzwa kwenye mnada wa hadhara katika maonyesho hayo.

Akizungumzia faida za maonyesho hayo Namaje amesema katika maonyesho ya mwaka jana Serikali ilifanikiwa kupata mapato ya Sh301 milioni  kutokana na mrahaba uliotokana na mauzo ya Tanzanite iliyofikia Sh7.2 bilioni.

Amesema katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015 Tanzania imeweza kupata kodi ya tozo kupitia madini ya Tanzanite inayofikia dola za kimarekani  Sh5.4 milioni ikiwa ni wastani wa dola moja milioni kwa mwaka na kwamba fedha hizo zimetokana na uwekezaji wa kampuni ya Tanzanite One.

Maonyesho hayo yalifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu kwa niaba ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk Merdad Kalemani ambaye aliwataka wafanyabiashara wa madini kufuata sheria za nchi ili kuepuka kufilisiwa endapo watakamatwa wakitorosha madini nje ya nchi.

Chanzo:Mwananchi

Utafiti: Wadada Wengi Wako Radhi Kutafutiwa Wenzi wa Kimapenzi na Marafiki zao

$
0
0
Kwa takwimu nilizozikusanya inaonekana wadada wengi wako radhi kutafutiwa wapenzi na marafiki zao wa karibu au na marafiki zao wa kiume ambao wanaonekana kuwa ni mfano wa kuigwa kwenye jamii. Idadi kubwa ya wadada wa aina hii ni wale walioumizwa hasa kwa kutokuwa na wapenzi waaminifu au ambao wako dedicated.

Nimejaribu mara kadhaa kuwaambia wadada mbali mbali kuwa wako tayari niwatafuite mahali pa 'kujiweka'? Wengi wao wameonesha utayari wa hali ya juu na wengine wamekuwa hata wakinipigia kufuatilia wajue nimefikia wapi.

Hii inanidhirishia kuwa hata wazazi wetu kutafutiwa wenzi ilikuwa ni jambo ambalo 'walilifurahia' tofauti na picha ambayo tunaipata sasa hivi kuwa walinyimwa haki yao ya kujitafutia wenzi wa maisha.

Hata mimi sasa tu vitoto vyetu na vitoto vya ndugu zangu ambavyo hata miaka minne havijafikisha, lakini nimeshaanza kuona watoto wa marafiki na jama wengine kama potentially wana ndoa wa uzao wetu. Mara nyingi nawataniaga rafiki zangu kuwa binti yako ataolewa kwetu and they seems to be fine with that...

Video ya NdiNdiNdi Imemrudisha Mwanamuziki Jide kwa Director Campos wa South Africa

$
0
0
Baada ya miaka 10 ya kufanyakazi na muongozaji wa video Justin Campos, Komando Jide au Lady Jaydee amerudi tena kwake kufanyanaye kazi, kutengeneza video ya wimbo wake wa #NdiNdiNdi

Taarifa hiyo ya kufanyakazi na Justin Campos ameitoa Lady Jaydee mwenyewe kwenye ukurasa wake wa Instagram, baada ya kupost video ikimuonyesha Justin Campos akisema ni heshima kwake kufanyakazi na Jaydee ingawa si mara ya kwanza.

“Nilikutana na Justin Campos kwa mara ya kwanza 2006 wakati tunafanya video ya 'Njalo' nilioshirikiana na kundi la Afrika Kusini linalojulikana kama 'Mina Nawe', Justin ndio alikuwa Director wa video hiyo baada ya miaka 10 tumefanyanae kazi tena 2016,” aliandika Jaydee.

Pia Lady Jaydee ameanza kupost picha za video hiyo huku akiandika “#NdiNdiNdi loading Kikomandooooooo #NguvuYaUmma #WananchiWameipokea #NdiNdiNdiMusicVideo”

Mwanamuziki Diamond Platnumz Atangaza Nafasi za Kazi....

$
0
0
Katika hali ya kuendelea kusaidia vijana wenzetu ambao bado wapo mtaani... Ndugu zangu kuna nafasi za kazi hapa @wcb_wasafi ...tunauhitaji wa:
1. Videographer mweye uwezo wa kushoot na kuedit...
2. Kijana Mwenye taaluma nzuri ya IT/ Socila Media Adminstrator Mwenye uwezo wa kuandika na Kuzungumza kingereza fasaha....
3. Secretary wa kike, Mwenye uwezo wa Kuandika Kiswahili na kingereza fasaha.... sio vingereza vya "baby i love you" au "Chilling home" mara "Less wig on fleek" sjui hapana, Fasaha.... wasiliana nasi kwa namba zetu +255757339215 au fika katika ofisi zetu zilizopo Sinza

Waarabu Waitupa nje AZAM Kombe la Shirikisho Barani Afrika...Waichapa Kipigo Kitakatifu

$
0
0
Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika Azan FC wametupwa nje ya michuano ya hiyo baada ya kuchapwa kwa magoli 3-0 na Esperance ya Tunisia kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wa Tunis, Tunisia.

Azam walikomaa kipindi cha kwanza na kufanikiwa kwenda mapumziko wakiwa hawajaruhusu goli hata moja licha ya mashambulizi makali ya mara kwa mara kufanywa kwenye goli lao lakini golikipa Aishi Manula alikuwa imara kuondosha hatari zote na kuiweka Azam salama.

Dakika ya 49 kipindi cha pili Esperance walipata bao la kuongoza lililopachikwa kambani na Saad Bguir kisha Jouini akaiandika bao la pili na Ben Yousef akaihakikishia timu yake kusonga mbele baada ya kufunga bao la ushindi dakika tisa kabla ya mchezo kumalizika.

Benchi la ufundi la Azam chini ya Stewart Hall lilifanya mabadiliko kujaribu kubadili matokeo kwa kuwapumzisha Farid Musa, Salum Abubakar ‘Sure Boy’na Wazir Salum huku nafasi zao zikichukuliwa na Hamisi Mcha, Himid Mao na Didier Kavumbagu lakini bado mabadiliko hayo hayakumlipa kocha huyo raia wa England.

Esperance imeitupa Azam nje ya mashindano kwa jumla ya magoli 4-2 baada ya kucheza mechi mbili. Mchezo wa kwanza Azam ikiwa nyumbani ilishinda kwa magoli 2-1 lakini leo imejikuta ikikubali kuchapwa magoli 3-0 ndani ya dakika 32 na kuyaaga mashindano rasmi.

Ni Kweli Kanye West Alilazimishwa Kupiga Picha na Diamond?

$
0
0
Ni takribani mwezi mmoja sasa tangu Diamond na Kanye West walipokutana kwenye uwanja wa ndege, Los Angeles nchini Marekani na kupiga picha ya pamoja.


Hivi karibuni maneno yameanza kuzuka tena mitaani kuhusu picha hiyo waliyopiga Diamond na Yeezy. Watu wanazungumza kwanini alinuna kwenye ile picha?

Akiongea kwenye stori tatu ya Planet Bongo, inayoruka kupitia EA Radio, Diamond amesema, “Nafikiria ni attitude ya Kanye ndivyo alivyo.”

“Ananuna hata akipiga picha na mkewe na mkwe wake, nafikiria nilipata bahati kwenye ile picha yangu kidogo alifurahi. Kuhusu collabo chochote kinaweza kutokea tumuombe Mungu. Naposema nataka muziki wetu upenye Marekani ni kujaribu kwenda kupambana na wale manguli wao ili tuone itakuwaje,” aliongeza.


Kama ni Kweli, Ulichofanya Tundaman Kudanganya Kuwa Ulikuwepo Kwenye Ajali Iliyoua Rafiki Yako ,Umekosea Sana

$
0
0
Gari hiyo ilihusisha gari ndogo aina ya Toyota Aurion iliyokuwa ikiendeshwa na Musa ‘Man Katuzo’ Katunzi aliyefariki kwenye ajali hiyo.

Taarifa za awali zilidai kuwa Tundaman alikuwa mmoja wa abiria waliokuwemo kwenye gari hiyo. Lakini sasa imekuja kubainika kuwa, Tundaman hakuwemo kwenye gari hilo, bali alikuwa kwenye gari aina ya Noah.

Tetesi hizo zilikuwa kubwa zaidi kutokana na jinsi gari ilivyoharibika baada ya ajali hiyo huku Tundaman akidaiwa kutopata jeraha lolote ukilinganisha ma majerehi wengine watatu.

Tundaman anasisitiza kuwa alikuwemo kwenye gari hilo kwa kudai kuwa walikuwemo abiria watano. Utata kuhusu kutokuwemo kwa Tundaman kwenye gari hiyo ulianza kusambaa Jumanne hii kwenye mitandao ya kijamii.

Mimi niliiona kupitia HR wa kituo cha redio cha Ebony FM, Luther Akyoo aliyeandika kwenye Facebook: “TUKATAE TAIFA KUJENGWA KWA UONGO UONGO. Tundaman hakuwemo katika ajali hii mbaya, kinachoendelea naweza kuita ni ule ujanja ujanja wa kutafuta “Kiki” kupitia njia ambazo sio sahihi,” aliandika.

“Tundaman alikuwepo katika Noah, na yeye ni mmoja wa watu waliofika katika eneo la ajali hii na kumkuta Dereva na mmiliki wa gari akiwa ameishatutoka. Narudia, TUNDAMAN HAKUWEPO KATIKA GARI HII, watengeneza story yake watengeneze vyema na upya. Sidhani kama ni sahihi kwa upotoshaji huu kuendelea, tusikubali kuwa sehemu ya jamii ya watu kupokea habari zisizokua na uchunguzi wa kina,” alisisitiza.

“Ukweli ni huo, huyu alipata ajali alikuwepo kwenye shoo yake, baadaye aliondoka mapema, Tundaman hata ofisi za radio ebony FM alifika na gari aina ya NOAH, sio hii inayosambazwa mitandaoni. Hii ilipata ajali na mtu mwingine, Tundaman alifika kwenye eneo la TUKIO kama SHUHUDA mwingine,” aliongeza.

Niliamua kufuatilia kwa ukaribu zaidi habari hiyo kwa kuongea na Dj wa Ebony FM aliyekuwa host wa show zao na aliyedai kuwa ni kweli Tundaman hakuwepo kwenye gari iliyopata ajali. Anadai kuwa Tunda alikuwa kwenye Noah pamoja na wasanii wa Khanga Moko, Dj Kman na dereva.

Kujiridhisha nilizungumza na Dj Kman aliyekuwa akizunguka na Tundaman ambaye hata hivyo alisisitiza kuwa Tundaman alikuwemo kwenye gari iliyopata ajali.

Kipindi cha XXL cha Clouds FM nacho kiliamua kufanya uchunguzi wake na awali kiliongea na Tundaman aliyeendelea kusisitiza kuwa alikuwemo kwenye gari hilo.

Kipindi hicho kilizungumza na Kaimu Kamanda Mkuu wa polisi Iringa, John Kauga. Kamanda Kauga amedai kuwa gari iliyopata ajali ilikuwa na abiria wanne ambapo mmoja alifariki. Pia aliwataja majeruhi waliokuwemo kwenye gari hilo na jina la Tundaman halikutajwa.

Kwa maelezo hayo kila mmoja anaweza kujiridhisha kuwa Tundaman hakuwemo kwenye gari hilo jambo linalowashangaza wengi na kuwafanya waulize nini hasa sababu ya Tundaman kusema uongo katika suala kubwa kama hili.

Mimi na wewe hatukuwepo kwenye tukio hili na hatuna mamlaka ya kuhukumu, lakini kwa maelezo hayo yanayozipa ukweli tetesi hizo, Tundaman amenishangaza sana. Kuna mambo mengi mno ya kutafutia umaarufu lakini sio kwa hili.

Inashangaza pale mtu anapokuwa na amani tu kupokea pole pomoni kwa kitu ambacho hakuhusika nacho. Ajali hii imepoteza maisha ya kijana aliyekuwa na mke na familia yake iliyokuwa ikimtegemea – huwezi kuweka mzaha. Si ustaarabu kulaghai katika suala serious kama hili.

HATIMAYE Mkataba Tata wa Lugumi na Jeshi la Polisi Watua Bunge...Waanza Kujadiliwa

$
0
0
Hatimaye taarifa ya utekelezaji wa mkataba tata wa Kampuni ya Lugumi Enterprises, iliyoshinda zabuni mwaka 2011 ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya Polisi vya wilaya nchi nzima kwa gharama ya Sh bilioni 37, umetua ndani ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na kuanza kujadiliwa.

Akizungumza jana bungeni, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Aeshi Hilaly alisema taarifa ya utekelezaji wa mkataba huo, ilifikishwa bungeni juzi na jana asubuhi wamepewa na wakaanza kuujadili papo hapo.

“Wametuletea taarifa ya utekelezaji wa mkataba huo leo asubuhi (jana), ila taarifa hiyo ilifika bungeni jana (juzi), na sisi kamati tumekaa asubuhi kuijadili kama tulivyokubaliana wakati wa vikao vya kamati mjini Dar es Salaam na tutatoa taarifa ya maamuzi ya kamati,” alisema Aeshi ambaye ni Mbunge wa Sumbawanga Mjini.

Akizungumza baada ya kuahirisha kikao cha kamati hiyo jana jioni, Aeshi alisema hawajafikia maamuzi na kwamba leo wataendelea kujadili taarifa hiyo na mchana watatoa maazimio ya kamati.

“Tumeahirisha kikao hadi kesho (leo) na bado tunapitia taarifa hiyo na kama kamati itaona haja ya kuwaita tena jeshi hilo kutoa maelezo, tutajua baada ya kufikia maamuzi,” alisema Aeshi na kuongeza kuwa kwa sasa wanachambua taarifa hiyo na iwapo wataona kuna haja pia ya kuutaka mkataba huo watatoa maelekezo.

Awali, Aprili 5, mwaka huu mjini Dar es Salaam, kamati hiyo ilitoa siku saba kuanzia siku hiyo kwa Jeshi la Polisi nchini, kupeleka mkataba walioingia baina yao na Kampuni ya Lugumi iliyopewa zabuni ya kufunga mashine 108 katika vituo tajwa nchini, ila hadi sasa ni vituo 14 tu ndivyo vilivyofungwa mashine hizo.

Hatua hiyo ilikuja baada ya kamati hiyo kukutana na jeshi hilo kupitia taarifa ya hesabu za jeshi hilo za mwaka 2013/14 zilizokaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kubainika kuwa na ukiukwaji wa utekelezaji wa mkataba huo.

Ukiukwaji wa utekelezaji wa mkataba huo mwingine ni pamoja na kampuni hiyo kulipwa asilimia 99 ya fedha zote za mkataba huo wenye thamani ya Sh bilioni 37, huku kazi iliyofanywa ni chini ya robo.

“Ukiangalia kazi iliyofanywa tangu mwaka 2011 hadi leo ni kidogo na pesa hawa kampuni wameshachukua asilimia 99, sasa tumewaagiza watuletee huo mkataba ndani ya wiki moja walioingia na kampuni hiyo ili tuupitie,” alisema Aeshi wakati wa vikao vya Dar es Salaam.

Hata hivyo, baada ya maagizo hayo, taarifa hiyo ya utekelezaji haikuwasilishwa kwenye kamati hiyo ndani ya muda uliokubaliwa na Aeshi alisema siku zote wamekuwa wakitoa maagizo kwa mdomo na taasisi nyingi zimekuwa zikitekeleza.

Aliongeza ila hilo la mkataba wa Lugumi lilikuwa tabu kutekelezwa hadi kamati hiyo, ilipochukua hatua za kukumbushia kwa kuandika maelezo.

Hata hivyo, baada ya taarifa za mkataba huo,zilisambaa habari kwenye vyombo vya habari kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo ni Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (CCM), Said Lugumi na vigogo wengine.

Kutokana na sakata hilo, mbunge huyo alikanusha kuhusika kwake na kusema ni kweli kwamba ana urafiki wa kawaida na Said Lugumi na kusisitiza kwamba hahusiki kwa njia yoyote na kampuni hiyo.

“Kwanza kabisa mimi si mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo, hilo ni jambo la msingi kabisa watu waelewe na sijawahi kufanya biashara yoyote na Lugumi. Said Lugumi ambaye ni mmiliki wa kampuni hiyo tunafahamiana naye na ni rafiki yangu,” alisema Ridhiwani.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya April 20, Ikiwemo ya Magufuli Kufyatua Mtego wa Paul Makonda

$
0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya April 20

HATIMAYE Waziri Charles Kitwanga Afunguka na Kuikana Kampuni ya LUGUMI...Asema Haya

$
0
0
Wakati sakata la Kampuni ya Lugumi kudaiwa kushindwa kutekeleza mradi wa utambuzi wa vidole kwenye vituo vya polisi likianza kudaliwa  na  Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema hana uhusiano wowote na kampuni hiyo kama watu wanavyodai.

Kitwanga ambaye alihusishwa na Lugumi kupitia kampuni ya Infosys iliyodaiwa kwamba kiongozi huyo ni mmoja wa wanahisa wakati akiwa mfanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ameeleza kuwa hahusiki na wala halijui suala la Lugumi.

Infosys ambayo imekanusha kuhusika katika sakata hilo imedaiwa kuwa iliisaidia kampuni ya Lugumi kupata vifaa kutoka kampuni ya Dell ya Marekani ili viweze kufungwa kwenye vituo vya polisi.

Jana Kitwanga alisema anashangazwa jinsi anavyohusishwa kwa maelezo kuwa wakati tukio hilo likitokea mwaka 2011, yeye hakuwa waziri wa wizara hiyo.

“Inanishangaza sana sihusiki na wala silijui hili suala la Lugumi. Wakati linatokea sikuwa waziri wa wizara hii ndiyo maana huwa sipendi na wala sitaki kuzungumza chochote kuhusu Lugumi,” alisema.

Kitwanga alifafanua kuwa baadhi ya mambo yameanza kubainika baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, licha ya kutotaka kuweka wazi kama suala la Lugumi ni miongoni mwa mambo hayo.

Kampuni ya Lugumi ilibainika kutotimiza matakwa ya mkataba wake baada ya kufunga mashine 14 tu kati  ya 108 zilizotakiwa kufungwa, licha ya kulipwa zaidi ya asilimia 90 ya fedha kwa mujibu wa mkataba.

Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) ya mwaka 2013/14 ndiyo iliyofichua udhaifu huo.

Utekelezwaji wa mkataba huyo uliwasilishwa jana kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na mwenyekiti wake Aeshi Hilaly alisema wameanza kuupitia na watakapokamilisha wataweka kila kitu wazi.

Kwa upande wake Ndugai alipotakiwa kuzungumzia suala hilo alisema,  “Mimi sijapata taarifa zozote za Lugumi. Jambo hilo bado lipo katika kamati ya bunge.”

Diamond Platnumz Anunua Nyumba Mpya Dar es Salaam Maeneo ya Sala Sala...Bei Aliyonunulia Ipo Hapa

$
0
0
Diamond platnumz ameendelea kuonyesha yeye ni msanii wa kuigwa baada ya leo hii kununua nyumba mpya iliyopo dar es salaam maeneo ya salasala mwanzo
Nyumba hiyo imemgharimu diamond zaidi milion 100 za kitanzania.
Wasanii wengine wanapwa kuekeza kwenye ardhi ili kesho yake wasikose pakujificha.
Hongera sana kijana diamond una umri mdogo lakini unajitambua 

TAZAMA VIDEO Jinsi Wenje Alivyolipuaga Ufisadi wa Wilson Kabwe Mwanza...Lakini Hakuna Hatua iliyochukuliwa...Leo Kailiza Dar Pia

$
0
0
Mkurugenzi  wa Jiji la Dar es Salaam aliyesimamishwa kazi Jana, Wilson Kabwe kumbe alishawahi kutuhumiwa na Ufisadi mwingine alioufanya Jijini Mwanza, Tuhuma hizo zilitolewa na Wenje aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana kipindi cha awamu ya nne...

Tazama Video hii Jinsi Wenje alivyolipua Ufisadi wa Wilson Kabwe Mwanza:

HABARI MBAYA:Gari Latumbukia Baharini Wakati likisubiri Kivuko cha Kigamboni leo Asubuhi..Lilikuwa na Watu Wawili Ndani

$
0
0
 Habari mbaya imetufikia kuwa leo asubuhi eneo kivukoni Kigamboni kuna gari ambalo lilikuwa linasuburia kivuko ili kuvuka limeingia baharini huku likiwa na watu wawili ndani yake mpaka sasa inasemekana amepatikana mtu mmoja ambaye wakati gari linaelekea baharini aliruka , mtu wa pili ni mwanamke ambaye hajapatikana mpaka sasa na gari pia alijapatikana utafutaji bado unaendelea....


Hii Hapa Ndio Hali ya Msanii CHID BENZ Baada ya Kukaa Sober House Kwa Mwezi Mmoja...

$
0
0
Toka msanii Chid Benzi akubali msaada wa kumsaidia kuachana na madawa ya kulevya na kupelekwa Sober House Bagamoyo afya yake kwa sasa inaendelea vizuri sana na mwili wake umeanza kunawiri tofauti na alivyokuwa mwanzo kabla hajapelekwa...

Ikumbukwe kuwa Meneja wa Diamond na Tip Top Babu Tale ndio aliyeamua kumsaidia baada ya Chid kuonekana kwenye TV akiwa katika hali iliyowatisha watu wengi na kuhoji amekubwa na nini kwani mwili wake ulionekana kudhoofu sana na kukonda kupita kiasa..

Tazama Video Hapa Akiwa Sober House baada ya Mwezi mmoja:



Kabwe Asema Uchunguzi Ufanyike ili Kubaini Ukweli, ni Baada ya Kutumbuliwa

$
0
0
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amesema uchunguzi wa tuhuma zilizomfanya Rais John Magufuli kumsimamisha kazi jana utabainisha ukweli wa tukio hilo.
kabwe

Alisema hayo mara baada ya Dk Magufuli kutangaza kumsimamisha kazi wakati wa uzinduzi wa Daraja la NSSF Kigamboni ambalo sasa litaitwa Daraja la Nyerere baada ya kumwita Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kueleza tuhuma dhidi ya mkurugenzi.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi Jumanne hii, Kabwe alisema hakuwa na taarifa za kusimamishwa kwake na kama imetokea hivyo ni sawa kwa kuwa Magufuli ni mkubwa wake.

“Nimekwambia sina la kukwambia kwa sasa lakini nimesema tu sina shida na hilo, uchunguzi ufanyike nina uhakika ukweli utajulikana tu. Lakini kama ukijulikana na ikibainika nimeonewa je, kuna fidia yoyote nitalipwa?,” alisema Kabwe.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Jumanne hii alimlaumu mkurugenzi huyo kwa mambo kadhaa ya kiutendaji ikiwemo kuongeza mkataba wa maegesho ya magari kwenye jiji na ulanguzi wa kodi za mapango kwenye stendi ya mabasi ya Ubungo

Kampuni ya Lugumi Yajitokeza na Kusema Mkurugenzi wake Hajatoroka nchi.....Bofya Hapa Kuisoma Taarifa Yao

$
0
0
Lugumi  Enterprises ni kampuni iliyoandikishwa na kufanya kazi hapa Tanzania na imekuwa ikifanya kazi mbalimbali ikiwemo ununuzi na ufungaji mashine za utambuzi wa alama za vidole yaani Automated FingerPrint Information System (AFIS)

Hivi karibuni kumekuwa na habari zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kwa namna ambayo inapotosha ukweli kuhusu kampuni yetu iliyotekeleza mradi huu muhimu kwa nchi yetu na, mradi wa AFIS.

Aidha taarifa hizo katika mitandao na magazeti mbalimbali imekuwa ikitoa habari zisizo na ukweli wowote kuhusu mtendaji mkuu Bwana Said H. Lugumi.

Ukweli ni kwamba mnamo mwaka 2011 Jeshi la Polisi liliingia mkataba na kampuni ya Lugumi Enterprises Limited wa kufunga mitambo ya utambuzi kwa kutumia alama za vidole (AFIS) katika vituo vya Polisi kwa mujibu wa matakwa ya Jeshi. Vituo vilikuwa nchi nzima Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za kampuni yetu, ukweli ni kwamba mkataba huu umetekelezwa nasi kwa kushirikiana na wabia wetu katika kuhakikisha mkataba huo unatekelezwa ipasavyo.

Kwa mujibu wa mkataba, kama kuna mgogoro katika utekelezaji,upande usioridhika na utekelezaji wake, utatangaza mgogoro kwa mwanasheria mkuu.

Si jeshi la polisi kwa upande mmoja wala sisi kwa upande mwingine aliyetangaza mgogoro wowote dhidi ya mwingine,kwa mujibu ya matakwa ya mkataba.
 
Kwa mantiki hiyo basi, mambo yaliyo mengi yalitajwa katika vyombo vya habari si ya kweli na ni upotoshaji mkubwa na ni muhimu kuyapuuza, na kuendelea na shughuli za kawaida za ujenzi wa taifa.

Ni katika muktadha huo huo tunapenda kuujulisha umma kwamba tuhuma nyingi za uzushi zimetungwa kumwelekea Mtendaji Mkuu Bwana Said H. Lugumi ikiwemo kuzushiwa kutoroka na kukamatwa nje ya nchi na kadhalika.

Taarifa hizo ni uzushi mtupu, ni za kupuuza, Mkurugenzi wetu yuko nchini na anaendelea na shughuli zake za kawaida.

Imetulazimu kuandika na kueleza haya maana tumeona  vyombo vya habari vimezidi kuandika na kupotosha umma kuhusu jambo hili.


Katibu Mkuu mpya CHADEMA yuko Wapi? Ni Kweli Kiatu Kinampwaya Kama Walivyotabiri Wengi?

$
0
0
Kutokana na kazi ya katibu mkuu wa chama na ukimya uliopo wa katibu mkuu huyu ni vema tukafahamu yupo kweli?

Inawezekana ni mazoea tuliojengewa na katibu mkuu aliejiondoa CDM Dr Slaa ambaye alikuwa ni mtu wakimkakati zaidi,katibu mkuu wa sasa anaonekana kama kiatu kinampwaya.

Maswali haya ni muhimu kwani kama kalala huenda yakamuamsha kutoka usingizini.

Una Maoni Gani?

HATIMAYE Barakah Da Prince Amvisha Naj ‘Pete ya Uchumba'

$
0
0
Barakah Da Prince ambaye kwa sasa amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii wa kike, Naj, amedai kupiga hatua zaidi kuelekea kwenye uchumba.

Wamefunguka exclusively kwa Bongo5 kuhusu uhusiano wao:

“Yeah ni kweli mimi na Naj tuna uhusino na hadi kwetu nimeshamtambulisha na yeye kwao najulikana na pia nimemvisha pia pete, sio ya uchumba ila ni Promise Ring,” amesema Barakah.

“Ndio hivyo yaani kuna kazi pia ambazo tumefanya ila hazitatoka sasa hivi hadi kwanza kila mtu atoe single yake halafu ndio itakuja hiyo ngoma ya pamoja mimi na Naj,” ameongeza.

Kwa upande wake Naj amesema:

Ni kweli Barakah amenivisha pete kama alivyosema. Kwangu ni furaha sana maana nimeshakuwa na mahusiano yaliyopita lakini sikuwahi kufanya kitu kama hiki. Naona kabisa kuwa mahusino haya ni ya ukweli na naona kuna malengo kabisa, nafurahia kwakweli.”

“Bado hatujaanza kuishi wote ila muda mwingi tupo pamoja, nafurahia mahusiano yangu ya sasa. Ni kweli tumefanya ngoma ya pamoja lakini haitatoka sasa hivi mimi natakiwa niachie ngoma yangu na pia nishoot video, halafu pia nitarudi Uingereza mara moja, kuna vitu vyangu kule then nitarudi tena Bongo.”

Chanzo:Bongo5

Video: Makonda Atangaza VITA ya Wafanyakazi Hewa jijini Dar es Salaam

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa kazi ya kutafuta watumishi hewa katika manispaa za jiji la Dar es Salaam bado linaendelea baada kubaini njia chafu wanazotumia watumishi hewa hao.

Akizungumza leo na waandishi habari ,Makonda amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam ni kioo kwa nchi hivyo jitihada zinaendelea ya kutafuta na kazi hiyo itafanywa sekta kwa sekta.

Amesema kuwa Wakuu wa Wilaya katika jiji la Dar es Salaam hakuna kufanya kazi yeyote mpaka wamelize kutafuta watumishi hewa kwa kutumia malipo ya watumishi kutoka taasisi za fedha (Pay Row).

Makonda amesema idadi ya watumishi hewa 71 aliowasilisha kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –Tamisemi, Georgre Simbachawene  ni ndogo katika  jiji la Dar es Salaam hivyo kazi lazima iwe endelevu.

Amesema kuwa watumishi Hewa hawawezi wakawa wanalipwa mshahara huku wanaofanya kazi kwa moyo mmoja wanajisikia  vibaya hivyo ni lazima watafutwe na wachukuliwe hatua na vyombo vya dola.

Mkuu Mkoa amesema kuwa kati ya watumishi hewa 71 ni watumishi 34 hewa wamefunguliwa mashitaka katika mahakama mbalimbali kutokana kuchukua fedha wasioifanyia kazi.

Nafasi za Kazi zilizo Tangazwa Katika Magazeti ya Leo Tarehe 20 April 2016

Viewing all 104689 articles
Browse latest View live




Latest Images