Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104706 articles
Browse latest View live

Mhandisi Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam na Wasaidizi Wake Watumbuliwa Majipu

$
0
0
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akizungumza na wanahabari kuhusu kumvua madaraka Mhandisi wa Manispaa hiyo,Japhery Bwigane na wasaidizi wake wawili kwa tuhuma za kusimamia ujenzi wa barabara za manispaa hiyo kwa kujengwa chini ya kiwango.

MANISPAA ya Ilala jijini Dar es Salaam imemvua madaraka Mkuu wa Idara ya ujenzi, Mhandisi Japhery Bwigane na wasaidizi wake wawili kwa tuhuma za kusimamia ujenzi wa barabara za manispaa hiyo kwa kujengwa chini ya kiwango.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam wakati akitoa taarifa hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko aliwataja maofisa wengine wa idara hiyo waliosimamishwa kuwa ni Siajari Mahili na Daniel Kirigiti ambao wamehamishwa idara hiyo ili kupisha uchunguzi unaoendelea.

Kuyeko alisema kikao cha Baraza la Madiwani kimefikia uamuzi huo baada ya manispaa kujiridhisha kuwa maofisa hao wamechangia kwa kiasi kikubwa ujenzi wa barabara mbovu ndani ya manispaa hiyo.

Alisema baada ya kuingia madarakani kwa miezi mitatu walijaribu kutafuta kero ndani ya manispaa ya Ilala ambapo walibaini idara ya ujenzi ina malalamiko mengi kutoka kwa madiwani wa kata mbalimbali kwa sababu ya kusimamia ujenzi wa barabara chini ya kiwango na hakuna hatua stahiki zilizochukuliwa na maofisa hao.

Alisema madiwani hao walimlalamikia Mhandisi Bwigane kuwa amekuwa akikaidi wito wao wa kujadili ujenzi wa barabara mbovu pindi zinapobainika jambo ambalo limesababisha manispaa hiyo kuwa na barabara nyingi mbovu.

Jitihada za gazeti hili za kumtafuta Mhandisi Bwigane ili kuzungumzia kusimamishwa kwake kazi hazikuzaa matunda baada ya kupigiwa simu yake na wakati wote kuwa imefungwa.

Diamond Platnumz, Mrisho Mpoto Walivyotajwa Bungeni Leo

$
0
0
Kikao cha tatu cha mkutano wa tatu wa Bunge la 11 kimeendelea tena Dodoma leo April 21 2016 , shughuli nzima iliyoanza asubuhi ni maswali na majibu kwa Waziri Mkuu, Pia baadhi ya Wizara zilihusishwa katika maswali hayo, ambapo Mawaziri na Manaibu Waziri wa Wizara hizo walilazimika kuyatolea majibu.

Baadhi ya Wizara hizo ni pamoja na Wizara ya Habari,  Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambapo swali lililoulizwa na Mbunge wa Kasuru Mjini Daniel Nsanzugwanko ilikuwa ‘Je, Serikali haioni umuhimu wa kuwekeza kwakiwango kikubwa katika Mkoa wa Kigoma kwa kujenga jumba la sanaa ili vijana wawe na sehemu nzuri ya kujiendeleza kisanaa?’

Swali la pili likawa ‘Kama Serikali inakubaliana na hoja hiyo, kituo hicho kitaanza kujengwa lini?’

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akajibu ‘Wizara yangu inatambua mchango mkubwa wa wasanii wenye asili ya mkoa wa Kigoma kama vile Diamond, Alikiba, Banana, Mrisho Mpoto na wengine‘

‘Wizara yangu inaendelea kuhimiza Halmashauri na Manispaa zote nchini kutenga maeneo ya kujenga vivutio vya sanaa. Kuhusu mkoa wa Kigoma, tunashauri Serikali ya mkoa kwa kushirikiana na Halmashauri zote kutekeleza ujenzi wa jumba la sanaa ‘ ;-Anastazia Wambura

VIDEO: Gari lililozama Baharini Kivukoni Dar es salam April 20 2016

$
0
0
April 20 2016 gari aina ya Toyota Hiace lililokuwa ndani ya Pantoni kuelekea Kigamboni Dar es salaam liliserereka na kuzama baharini ambapo inasadikiwa lilikuwa na watu wawili, uokoaji ulifanyika ambapo asubuhi jeshi la zimamoto na uokoaji lilifanikiwa kuupata mwili mmoja na mchana mwili wa pili wa Nice Karago ukapatikana...

Source:AyoTV

Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-WAZALENDO, Samson Mwigamba Atangaza Kujiuzulu Leo

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT - Wazalendo, Samson Mwigamba amejiuzulu nafasi yake ili apate nafasi ya kwenda masomoni Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya.

Kwa mujibu wa ACT-Wazalendo, kamati ya uongozi imekubali maombi ya Mwigamba na kumruhusu kwenda masomoni na kuwa mchakato wa kujaza nafasi hiyo utaanza mara moja.

Naye Mwigamba ameushukuru uongozi wa chama chake kwa ushirikiano waliompatia tangu chama hicho kinaanzishwa. Amesisitiza kwamba bado ni mwanachama na ataendelea kutoa ushirikiano hata akiwa nje ya nchi.

Mwanasiasa huyo anakwenda kusoma shahada ya uzamili katika masuala ya utawala na usimamizi wa biashara (MBA) na baada ya masomo hayo ataendelea na shahada ya uzamivu (PhD).\

Nafasi za Kazi Tembelea www.ajirayako.com

WOSIA wa Liyumba kabla ya Kifo Chake

$
0
0
Wosia huo wa Liyumba, ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu Tanzania (BoT), ulifanya waombolezaji waliofika kuuaga mwili wake, kutopewa fursa ya kuona sura yake kwa mara ya mwisho kabla ya maziko.

Ndugu huyo alitangaza utaratibu huo jana baada ya ndugu, jamaa na marafiki kufika nyumbani kwa marehemu kutoa heshima za mwisho.

Baada ya mwili kuwasili na taratibu nyingine kufanyika, Merito alisimama na kutangaza kuwa kaka yake aliacha wosia kwamba wakati wa kuagwa, ndugu pekee ndiyo wamtazame uso wake.

“Alisema watu wengine watakaoshiriki msiba wake, wapite kwenye jeneza lake likiwa limefunikwa,” alifafanua.

Baada ya utaratibu huo kutangazwa, waliofika kuaga walipita mbele ya jeneza hilo likiwa limefungwa na kutoa heshima zao za mwisho.

Aidha, alisema kutokana na taratibu za kimila, mwili huo ambao jana ulitangazwa utazikwa leo mkoani Morogoro, utaratibu umebadilika na kwamba atazikwa kesho.

“Mila zinasema mwili wa marehemu baada ya kuwasili Morogoro, unatakiwa kulala kwenye nyumba yake hadi siku inayofuata ndipo utaratibu mwingine wa maziko ufanyike. Kwa hiyo atazikwa Ijumaa (kesho),” alisema.

Miongoni mwa walioshiriki kwenye msiba huo ni pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa BoT.

Liyumba ameacha watoto saba, mkewe alifariki dunia miaka 10 iliyopita.

Enzi za uhai wake, alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2009 kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi na kuisababaishia serikali hasara ya Sh. bilioni 221.

Hata hivyo, alishinda kesi hiyo baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha tuhuma hizo.

Upendo Peneza (CHADEMA) Amlipua Rais Magufuli, Amtaka Alipe Kodi Kutoka Kwenye Mshahara wake

$
0
0
Katika mjadala wa leo bungeni, mbunge wa CHADEMA viti maalum kutoka mkoa wa Geita, Upendo Peneza amlipua Rais Magufuli ya kwamba anapaswa kuonyesha mfano katika kulipa kodi kutoka kwenye mshahara wake ambao kwa sasa haukatwi kodi..

Hali hiyo ilizua taharuki ambapo waziri wa ofisi ya Rais, TAMISEMI Simbachawene aliinuka na kuomba kutoa taarifa. Katika kutoa kwake taarifa waziri alisema mshahara wa Rais haujadiliwi popote pale, ikiwa ni sharti ndani ya katiba ibara ya 43.

Mbunge Peneza katika kukataa taarifa hiyo alisema hoja yake ya msingi ni kutaka Rais aonyeshe kuongoza kwa mfano kwa kulipa kodi kama anavyosisitiza wananchi na wafanyabiashara kulipa kodi.

Hizi Hapa Picha za Mrembo Anayedaiwa Kutoka Kimapenzi na Diamond Platnumz...Timu Zari Waendelea Kumuandama

$
0
0
Mashabiki wa Zari the Bosslady wanamshambulia Lynn, mrembo aliyetumika kwenye video ya ‘Kwetu’ ya msanii wa WCB, Raymond kwasababu wamesikia tetesi kuwa amechepuka na Diamond Platnumz.

Tetesi hizi ni kubwa kiasi ambacho watu walio karibu na mastaa hao wamedai kuwa zimeitikisa ikulu ya Chibu. Wanadai kuwa Zari amekerwa na tetesi hizo na kwamba uhusiano wao umepata dosari.

Wiki hii tetesi hizo zimevuma zaidi kiasi ambacho mashabiki wa Zari wamekuwa wakimmiminia matusi Lynn kwenye akaunti yake ya Instagram.

Inafurahisha kwasababu Lynn haoneshi kutikiswa na matusi hayo huku pia akipewa support kubwa kutoka kwa mashabiki ambao hawampendi Zari. Of Course Team Wema yote inaonesha kuwa nyuma yake!

Cha kuvutia zaidi ni kuwa Lynn ni msichana mdogo na mrembo sana kiasi ambacho wasiompenda Zari wanasema anafaa zaidi kuwa kifaa cha Bin Mondi. Kwa wengi hizi bado ni tetesi tu lakini kama ukiangalia post za nyuma za Lynn, utagundua kuwa alikuwa shabiki mkubwa wa Daimond kwakuwa amekuwa akiweka picha zake [Diamond] mara kwa mara.


Toa Maoni yako:

Siwezi Kumuomba Msamaha Chidi Benz Kwa Kauli Yangu ‘Acha Afe’ – Dudu Baya

$
0
0
Msanii mkongwe wa muziki, Dudu Baya, amesema hawezi muomba msamaha Chidi Benz kutokana na kauli yake ‘acha afe’ ambayo aliitoa baada ya rapa huyo kuzidiwa na matumizi ya Madawa ya kulevya na kuomba msaada.
Dudu Baya

Akizungumza na Bongo5 Jumatano hii, Dudu Baya amesema aliitoa kauli hiyo baada ya kuona rapa huyo hakuwa tayari kusaidiwa na watu ambao walijitokeza kumsaidia.

“Siwezi kumuomba msamaha Chidi Benz kwa kauli yangu ya acha afe,” alisema Dudu Baya “Nachoweza kufanya ni kumpa pole kwa matatizo yaliyompata, na ninamwombea dua Mungu ampe nguvu mpya, akili mpya, mwanga mpya. Bongofleva inamwitaji, jamii imemmis, familia yake inamwitaji na inamtegemea. My best rapper, my friend Chidi Benz hakuna wa kukuokoa, jiokoe,”

Chizi Benz kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kukubali kupelekwa Bagamoyo Sober House kumsaidiwa kuondokana na matatizo yanayomkabili.

CHADEMA Mkoa wa Dar es salaam watoa tamko, wailaumu Televisheni ya Taifa kwa ubaguzi

$
0
0
Viongozi wa greater Dar Es Salaam wakati wa kikao na waandishi wa habari mapema hii leo wakitoa maazimio yao dhidi ya ubaguzi unaofanywa na kituo cha television ya TBC dhidi ya upinzani.

Makamu mwenyekiti Mwakyembe ametoa onyo kali na la mwisho kwa TBC maana ni chombo cha umma kinachoendeshwa kwa kodi za watanzania hivyo kiache kuendeshwa kwa minajali ya CCM tu.

Pia katika kikao hicho viongozi wa Dar es salaam kuu wameongelea zoezi linaloendelea chini ya serikali ya rais Magufuli la utumbuaji majipu na kubainisha ni kiini macho kwa watanzania.

Akifafanua zaidi katibu Ndugu Kileo amesema anachofanya magufuli kwanza ni ukiukwaji wa sheria za nchi za ajira kazini ya mwaka 2004 lakini pia ni kinyume cha uongozi wa kidemokrasia ambapo kila mtu anahaki ya kusikilizwa na si maamuzi ya upande mmoja tu.

Zaidi Mh. Kileo amesema kinachofanyika ni kiini macho kwa sababu CCM inataka kujisafisha na uchafu huo wa jiji uliotendwa na Meya aliyepita ambaye ni mwanachama wa CCM Mh Masaburi, maana ki uhalisia mkurugenzi hapitishi mkataba bila kuwepo saini ya Meya na kamati ya mahesabu kuidhinisha.

Hivyo basi wao wanamtaka Mh Magufuli kudeal na watendaji wazembe ila kwa kufuata utaratibu wa kisheria na si mabavu.

Akihitimisha kikao hicho Mh Kileo amesema wao kama kamati kuu ya Dar es salaam kuu pia wanasikitishwa na ubaguzi unaofanywa na serikali dhidi ya mameya wanaotokana na UKAWA kwa kile kilichotokea juzi kwenye uzinduzi wa daraja la Kigamboni na hata ile kauli aliyotoa Mh rais wakati wa uzinduzi wa mradi wa kinyerezi 2.

Nafasi za Ajira Bonyeza www.ajirayako.com

Video: Rais Magufuli Awajibu Haki za Binadamu, Asema Nao Wanaweza Kuwa Majipu Kwa Kutetea Maovu....

$
0
0
Katika hali inayoonyesha kuwa na majibizano kati ya Rais Magufuli na Kituo Cha Haki za Binadamu LHRC kinachoongozwa na Dr. Hellen Kijo Bisimba, leo Rais Magufuli hadharani kasema wanaosema amekiuka haki za binadamu kumsimamisha ndugu Kabwe hadharani walitakiwa pia waseme vivyo hivyo kipindi anamuapisha hadharani kwa kuwa ni mteule wake, Amesema hao Waliotumbuliwa wamewaibia Watanzania hadharani hivyo inabidi watumbuliwe hadharani nao wapate maumivu kama waliyoyapata Watanzania...Hivyo, ni vyema wakaiacha serikali ikafanya kazi yake, na ikiwezekana itabidi awachunguze hao LHRC credibility yao kama wanatetea mambo maovu inawezekana nao ni majipu..

Mtazame Hapa Alivyokuwa anamwaga cheche:

Watu Wanne Watiwa Mbaroni Sengerema Kwa Kunywa Pombe Mchana

$
0
0
Wilaya ya Sengerema imeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais baada ya kukamata watu wanane waliokutwa wakinywa pombe saa za kazi.

Amri ya kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa watu hao ilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya Zainabu Terack baada ya kukuta baa zimefunguliwa asubuhi zikiwa na wateja waliokuwa wakipata kinywaji kabla ya saa 9:30 alasiri, muda ambao ofisi za Serikali hufungwa.

Rais John Magufuli alitoa agizo hilo la kupiga marufuku unywaji pombe na uchezaji pool nyakati za kazi wakati alipokuwa akiwaapisha wakuu wa mikoa mwezi uliopita. Alitaka vijana ambao watakaidi maelezo ya kuambiwa, nguvu itumike kuwalazimisha kufanya kazi.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya, aliyeongoza oparesheni ya dakika 45 ya kusaka wanaokunywa pombe na kucheza pool muda wa kazi, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa makosa ya uzembe na kukiuka amri halali ya serikali.

Wakijitetea baada ya kutiwa mbaroni, baadhi ya waliokamatwa walidai kuwa walienda baa kujiliwaza wakati wa msiba wa ndugu yao waliyemtaja kwa jina la Petro Shoyo, na kumwomba mkuu wa wilaya kuwasamehe kwa sababu ni kosa lao la kwanza.

Lakini mkuu huyo wa wilaya alisisitiza wapelekwe mahakamani.

Gari Aina ya Toyota Hiace Lililozama Majini Kivuko cha Kigamboni na Kuua Watu Wawili Lapatikana

$
0
0
Lile Gari Aina ya Toyota Hiace lililozama kwenye bahari kivukoni Kigamboni na kuuwa watu wawili limepatikana na kutolewa majini na wana maji baada ya Jumatano ya April 20 2016 kuzama  ikiwa na watu wa wawili ambao wote walipatikana wakiwa wameshafariki...

Picha likiwa linatolewa majini hii hapa:
Hatimaye kikosi cha ukoaji cha baharini kimefanikiwa kuitoa gari aina ya Hiace ambayo jana ilizama katika bahari ya hindi eneo la Kivukoni na kuua watu wawili.

Aina Kumi za Wanawake Ambao Wanaume Wengi Wanavutiwa Kuwa Nao Kimapenzi

$
0
0
1. The childish woman

There are some men that like childish women. They may appreciate the fact that this type of women is cheerful, playful and represents sunshine in their dull or stressful life. However, try not to exaggerate. Sometimes they need you to act responsible and wise.

2. The mysterious lady

I think all men like a bit of mystery in a woman. They don’t mind the large doses of mystery either! All men try to get behind “the mask” of a woman, to discover her secrets. Thus, you should always keep a bit of mystery in your life, to spice up your relationship.

3. The s3x addict

Tell me a man who would not be interested in such a woman…It’s their basic instincts working. This doesn’t guarantee, however, that he will marry such a woman, or that he would like a serious relationship with her! Do try to act like one from time to time, and only when you are alone, this will certainly “inspire” him…

4. The Vi.rginal

Many men feel attracted to the purity of a woman. Especially these days, when finding a woman of this type is kind of difficult, don’t be ashamed if you are one. What’s more, acting shy or seeming not to have a lot of se.xual knowledge will make many men go crazy about you. Most of them enjoy acting as teachers, so you might want to allow them too, there’s nothing to lose…

5. The action woman

Yeah, they like the Lara Croft type, you know it already. But there’s no need for you to go so far. Something as simple as a bike ride, for example, is a good way to win his admiration. If you like climbing, if you know how to ride a horse, if you save your cat from trees on a regular basis, or if you are the sportive type, then you might want to show off. Men find action women really sexy.

6. The spoiled type

They like women that look spoiled, or like to spoil themselves, but do not exaggerate, because being spoiled has 2 faces: while spoiling yourself in bed at night or with a new bag and a massage is great, spending all your money, or worse HIS money, on shoes is not attractive anymore.

7. The confident lady
There’s nothing sexier in a man’s eyes than a woman who is sure of her qualities, likes her own body, knows what she wants and has an accomplished career to boost her confidence. However, do ask for his help from time to time; showing him that you sometimes need him does wonders for his self respect and will make him feel comfortable when in need to ask for your help.

8. The motherly sweetheart
Men like women to act motherly; it is because most of them are “big babies” and they are used to be taken care of – their mothers did that for a long while, in most cases. Moreover, they will typically look for women that resemble their own mothers. It is also true the other way around, so don’t blame them for it.

9. The diva

Though they find divas sexy, they will rarely have the courage to approach them. So, if you are the diva type, you might want to give him a sign that you are interested in him. Otherwise, you might find yourself desired by many but alone…

10. The unconventional woman

Same as with the childish type, men like women who make them smile. Eccentric women will be noticed by everybody. Not all men think that unconventional is sexy, but some really do. So, o need for you to change, unconventional is sexy and fun!

Jinsi ya Kupunguza Uzito wa Mwili/Unene Kwa Kutumia Saladi

$
0
0
Ulaji saladi ya spinachi, matunda ya apple na parachichi unaweza kumsaidia mtu kuwa na uzito unaotakiwa kiafya.

Kabla mtu hajaanza kula mlo wake wa asubuhi, mchana au usiku anashauriwa aanze na mboga za majani za spinachi au aina nyingine.  Ulaji wa aina hii unamwezesha mtu kula kidogo vyakula vyenye wanga, sukari au mafuta ambavyo vinasababisha kuongezeka uzito na unene.

Saladi ya mboga za majani hujaza tumbo na kumfanya mtu ajihisi ameshiba na hivyo kuzuia tabia ya kutamani kula hasa vyakula vya wanga au sukari.  Mboga za majani za spinachi pia, zina kirutubisho kinachoitwa thylakoids, ambacho kinachochea mwili kuzalisha homoni inayopunguza hamu ya mtu kutaka kula hasa vyakula vyenye sukari.

Kuhusu matunda ya apple, kwa siku mtu akila tunda moja ni jambo zuri.  Matunda ya apple yana maji na nyuzi lishe ambazo zinalifanya tumbo kujisikia limeshiba.  Matunda ya epo pia yana kirutubisho cha pectin, ambacho kinakifanya chakula kilichomo tumboni kusagwa kwa muda mrefu na kumfanya mtu kujisikia ameshiba.

Mtu akila tunda zima la epo (siyo juisi), kabla ya mlo atajisikia hali ya kushiba na hivyo atakula kidogo chakula cha wanga au sukari.
Kwa upande wa matunda ya parachichi, kula nusu ya tunda hilo kwa siku kunaupa mwili mafuta bora kiafya na nyuzi lishe ambazo zinamfanya mtu ajisikie ameshiba muda mwingi na kutokutamani chakula mara kwa mara.


Anachopaswa kufahamu mtu ni kwamba kula vyakula vya wanga, sukari au mafuta kwa wingi ndipo mwili unaongezeka uzito na unene kupita kiasi.

Diwani na Mwenyekiti Chadema Nusura Watwangane laivu Bila Gloves

$
0
0
Diwani wa Kata ya Isyesye, Ibrahimu Mwampwani (Chadema) na Mwenyekiti wa Mtaa wa Manga Veta, Godlove Haule (Chadema) nusura watwangane makonde mbele ya wananchi baada ya kutuhumiana kula rushwa kutoka kwa mwenye jengo la ghorofa linalodaiwa kujengwa juu ya mkondo wa maji na kusababisha mafuriko jijini Mbeya.

Sakata hilo lilitokea baada ya viongozi hao kukutana mbele ya jengo hilo wa kiwa na baadhi ya watendaji wa halmashauri na wananchi wakijadiliana jinsi yakukabiliana natatizo la mafuriko yanayotokea mara kwa mara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha .

Akizungumziatukiohilo, John Steven mkazi wa Isyesye alisema kuwa walifika katika eneo hilo kwalengo la kupata suluhisho la mafuriko na ubovu wa miundombinu ya barabara kwani limekuwa nitatizo kubwa katika eneo hilo ambapo asilimia kubwa ya wananchi wanaokaa eneo hilo wameyafungia ndani magari yao kutokana na kushindwa kupita.

 “Hawa ni viongozi wetu na ndiyo wanashughulikia suala hili lakini cha kushangaza inaonyesha baadhi yao wanamaslahi binafsi hadi wanafikia hatua kama hii yakurushiana maneno na kutaka kupigana wakati tunaoumia ni sisi wananchi wa kawaida kutokana na mafuriko,” alisema

Haule alipoulizwa kuhusu tukio hilo alisema kuwa ni kweli walitaka kurushiana makonde kutoka na na baadhi ya viongozi wa kisiasa wamekuwa wakifanya kazi kwa maslahi yao kwani tatizo la jengo hilo la ghorofani la muda mrefu lakini hakuna hatua inayochukuliwa.

Kwa upande wake Mwampwani alipoulizwa kuhusiana natukio hilo alisema kuwa ni kweli hali hiyo ilikuwepo ni baada ya kuambiwa na mwenyekiti huyo kuwa inawezekana atakuwa amechukua rushwa kwa mmilikiwa jengo hilo.



Tarehe ya Kikomo cha Daladala Zinazofanya Safari zake Katikati ya Jiji Dar es Salaam Yatajwa..Watakiwa Kubadilisha Ruti Kupisha Dart

$
0
0
Daladala zinazofanya safari zake katikati ya jiji zimetakiwa  kuondoka   ifikapo Mei
Hayo yameelezwa leo na Msemaji wa Mradi wa Mabasi  yaendayo kasi (Dart),  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Mkoa wa Dar  es Salaam (Darcoboa), Sabri Mabrouk. Amelisema tayari wamiliki wote wa mabasi walishalipwa fidia ya kubadili njia.

“Wamiliki wote wa mabasi wameshalipwa fedha zao tangu Desemba mwaka jana, hakuna anayedai na tumewapa siku saba kuondoka barabara kabla ya Mei 10,” amesema Mabrouk.

Mradi wa Dart unatarajia kuanza rasmi Mei 10, mwaka huu na tayari mabasi hayo yameshaanza kufanya majaribio katika njia mbali mbali katikati ya jiji huku changamoto kubwa ikidaiwa na waendesha pikipiki, raia na daladala kupita kwenye njia hiyo ya mradi na kusababisha msongamano wa magari kitendo ambacho kinalazimu mabasi hayo nayo kujikuta yakikaa foleni.


Sugu Asema Tanzania iliingia Kwenye Soko la Albamu za Muziki Kabla ya Muda Wake

$
0
0
Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop na mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema wasanii wa Tanzania waliingia mapema kwenye soko la albamu kabla ya muda wake.
Sugu

Rapa huyo ambaye aliachia wimbo ‘Freedom’ ambao unafanya vizuri kwa sasa, ameiambia Bongo5 kuwa wakati ndio umesabisha soko la albamu kupotea.

“Sisi Tanzania nafikiri tuliwahi kuingia kwenye biashara ya albamu, wenzetu Jamaica wasanii wakubwa kwao, yaani nyumbani kwao Jamaica hawauzi hata nakala elfu 10000, labda wawe International ndio wanaweza kuuza zaidi kazi. Lakini kule kwao ndani waliwekeza kwenye show zaidi na matamasha. Sisi tulianza na albamu bila kuboresha matamasha, na watu wakatuacha huko huko tunagombana na Waindi, na huku show kwa sababu hatukutolea macho wakawa wanatulipa pesa ndogo, kwa sababu tulikuwa hatujui show zina pesa nyingi. Kwa hiyo kilichotokea ni kama mabadiliko, tulianza na ambako pengine hatukutakiwa tuanze, na sasa hivi nyakati imeturudisha pahala ambapo tunatakiwa kuwepo,” alisema Sugu.

Pia alisema kwa sasa mataifa makubwa ya ulaya ambayo yameendelea kiteknolojia wameanzisha mifumo mipya ya kuuza albamu ambayo inawapa pesa nyingi.

Chanzo:Bongo5

Madhehebu ya Kiislam Yafunguka Kuunga Mkono Kasi ya Rais Magufuli na Utumbuaji Majipu Uchungu...

$
0
0
KASI  ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli inazidi kushika moto baada ya Kiongozi Mkuu wa Chuo cha Kiislam (Hawza) Imam Swadiq ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa Waislam wa Madhehebu ya Shia Ithnasheria, Tanzania,  Shekh Hemed Jalala amewataka Watanzania na waumini wa madhehebu yote nchini kumuunga mkono kwa kasi yake.

Shehe Jalala akizungumza leo na wanahabari katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mmoja wa  wanafunzi wa Mtume Mohamed (S.A.W),  Imam Ali (A.S), amesema alikuwa kiongozi jasiri, mpenda haki,  aliyepinga rushwa, muwajibikaji na mpinga ufisadi, kama ilivyo kwa sasa kwa Rais Magufuli ambaye ameonesha nia ya dhati ya kuifanya Tanzania kuwa mpya kwa kupinga ufisadi, rushwa  na mambo mengine ambayo yanawaumiza Watanzania wa hali ya chini.
“Tunaadhimisha zaidi ya miaka  1430 ya kuzaliwa kwake

Imam Ali kwa kuwa alikuwa mwanafunzi bora wa kuigwa kwa kile alichokipigania ndicho kinachoonekana kwa Rais Magufuli, viongozi wa dini tuwaongoze waumini wetu katika kumuombea na kukemea pale tunapoona si sahihi, ila mpaka hapa tulipo ameonesha dira ya Tanzania mpya,” alisema Shehe Jalala.

Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Katika Magazeti

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya April 22, Ikiwemo Rais Magufuli Kujibu Mapigo

$
0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya April 22, Ikiwemo Rais Magufuli Kujibu Mapigo
Viewing all 104706 articles
Browse latest View live




Latest Images