Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live

Julius Mtatiro Afunguka...Adai Staili Anayotumia Kufukuza Kazi Rais Magufuli ni ya Udikteta

$
0
0

Julias s. Mtatiro Ameandika haya katika kurasa wake ya Facebook kuhusu kutumbuliwa kwa Wilson Kabwe siku ya uzinduzi wa Daraja la Nyerere..


"Kuondolewa kwa Wilson Kabwe hakuwezi kupingwa na mtu. Lakini staili ya kufukuzana kazi kwa kudhalilishana inayofanywa na mtu mwenye mamlaka makubwa sana ambayo Mwalimu Nyerere aliwahi kuyalinganisha na "Udikteta", haikubaliki. Katika dunia ya utawala bora na utawala wa sheria, utu na heshima - inatosha sana RAIS akisema "nimelipokea", kisha nusu saa baadaye wananchi wakapokea taarifa ya ikulu ikieleza "fulani" amesimamishwa na uchunguzi unaendelea.

Viongozi wanapofanya mambo muhimu kwa kutumia njia zilizojaa hamasa, ushabiki na sifa halafu tukaendelea kuwapigia makofi, tunatengeneza tatizo kubwa na kuna siku tutalikuta milangoni mwetu.Mtatiro J"

Je kwa haya aliyo andika Julias Mtatiro je yanamashiko ???  toa maoni yako...

Bosi wa Bandari Aliyetumbuliwa Jipu Akutwa na Kesi ya Kujibu Kwa Matumizi Mabaya ya Madaraka

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Ephraim Mgawe, pamoja na aliyekuwa Naibu wake,  Hamad Koshuma, wanaokabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka wamepatikana na kesi ya kujibu.

Mgawe na mwenzake wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakidaiwa kutumia madaraka yao vibaya kwa kutoa zabuni kwa kampuni ya China, China Communication Construction Company Limited, kwa ajili ya ujenzi wa maghati katika Bandari ya Dar es Salaam.

Leo mahakama katika uamuzi wake baada ya kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka iliwaona kuwa wana kesi ya kujibu kwa mashtaka yanayaowakabili na hivyo kuwataka kupanda kizimbani kujitetea, Mei 16 mwaka huu.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mkazi Cyprian Mkeha anayesikiliza kesi hiyo alisema kwamba ameridhika kuwa upande wa mashtaka umeweza kujenga kesi dhidi ya washtakiwa hao na kuwa wana kesi ya kujibu.

“Baada ya kupitia ushahidi wa  uliowasilishwa na uapnde wa mashtaka pamoja na vielelezo nimeridhika kuwa washtakiwa wana kesi ya kujibu, hivyo wanatakiwa kutoa utetezi wao.”, alisema Hakimu Mkeha.

Baada uamuzi huo, Mgawe aliieleza Mahakama kuwa anatarajia kuita mashahidi tisa kumtetea mahakamani hapo, huku Koshuma akisema akisema kuwa yeye atajitetea mwenyewe na kwamba hatakuwa na shahidi mwingine.

Mgawe na  Koshuma wanadaiwa kula njama na kutoa zabuni tata kwa kampuni hiyo ya Kichina kwa ajili ya kujenga maghati namba  13 na 14 katika Bandari ya Dar es Salaam kwa gharama ya Dola 600 milion, kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma.

Wanadaiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa kusaini mkataba wa kibiashara na kampuni hiyo ya Kichina bila zabuni shindanishi kinyume cha sheria hiyo ya manunuzi ya umma.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka namna ambavyo zabuni hiyo ilivyotolewa kwa kampuni hiyo washtakiwa hao walikuwa na maksudi ya kujipatia manufaa kwa kampuni hiyo ya Kichina.

Upande wa mashtaka unaendelea kudai kuwa kitendo hicho cha washtakiwa walikiuka masharti ya kifungu cha 31 cha Sheria ya Manunuzi ya Umma, namba 21  ya mwaka  2004.

Wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo, upande wa mashtaka uliwaita mahakamani jumla ya mashahidi watano kujenga kesi yao, akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya  Sheria wa mamlaka hiyo, Kokutulage Kazaura.

Katika ushahidi wake Kazaura alidai kuwa mkataba baina ya kampuni hiyo na mamlaka hiyo December 5, 2011, na Mkurugenzi Mtendaji, Mgawe, ukishuhudiwa na naibu wake Koshuma.

Shahidi huyo aliendelea kuieleza mahakama kuwa walishindwa kufuata mchakato wa manunuzi kwa kuwa tayari TPA ilikuwa imeshaingia katika makubaliano na kampuni hiyo, na kwamba kwa hali hiyo hapakuwa na haja ya kutangaza zabuni.

Wakati huo huo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kutoa uamuzi wa uhalali wa shtaka la kutakatisha fedha linalomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA,

Harry Msamire Kitilya, na wenzake wawili.
Mbali na Kitilya washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni mshindi wa Mashindano ya Urembo (Miss Tanzania), mwaka 1996, Shose Mori Sinare na Sioi Graham Solomon.

Washtakiwa kupitia kwa mawakili wao walihoji uhalali wa shtaka hilo na kuiomba mahakama ilifute pamoja na mambo mengine wakida kuwa halijakidhi vigezo vya kisheria kuitwa shtaka la utakatishaji fedha.

Maombi yao hayo yalitarajiwa kutolewa uamuzi jana na Hakimu Mkazi Emilius Mchauru, anayesikiliza kesi hiyo, lakini uamuzi huo ulikwama na badala yake ulipigwa kalenda hadi April 27 mwaka huu.

Wabunge wa Upinzani Watoka nje ya Bunge....Watoa Sababu Mbili za Kufanya Hivyo

$
0
0

Wabunge wa Upinzani jana walitoka nje ya Bunge kwa madai kuwa Serikali ya Awamu ya Tano hadi sasa haina 'Mwongozo wa kuiongoza Serikali'. Madai mengine wanapinga ubadilishwaji wa matumizi ya fedha kwa kigezo cha kubana matumizi bila kushirikisha bunge

Je unamaoni gani?

Video: Wastara Juma Azungumzia Maisha yake ya Mapenzi, Biashara, Pamoja na Filamu

$
0
0
Msanii wa filamu na mfanyabiashara, Wastara Juma amefunguka na kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu maisha yake.

Akizungumza na Bongo5 Jumatano hii, Wastara amesema licha ya kufanya filamu na kumuingizia pesa, lakini maisha yake kwa sehemu kubwa wanategemea biashara.

“Mimi ni mfanyabiashara kitambo sana, nina miaka karibu 19 nafanya biashara na na bado zinaendelea vizuri,” alisema Wastara.

Pia Wastara amezungumzia maisha yake ya ndoa, kuhusu aliyekuwa mume wa Sadifa, baada ya kuachana watu wanamchuliaje iliwa ndoa hiyo idumu kwa miezi 3.

Mtoto Mtanzania wa Miaka 16 Alivyoongea Kwa Kujiamini Mbele ya Viongozi wa Dunia Umoja wa Mataifa

$
0
0
Mtoto Mtanzania mwenye umri wa miaka 16 Getrude Clement kutokea Mwanza amehutubia mbele ya viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa umoja wa mataifa akiwa mwenye kujiamini na kutoonekana kuwa na hofu japo anaongea kwenye jukwaa ambalo linatazamwa na viongozi mbalimbali.

Mataifa zaidi ya 150 yalitia saini makubaliano ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo Marekani ambapo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon ndio alimkaribisha Getrude kuongea kwa kusema ‘ni furaha yangu kumualika Getrude Clement ambaye pia ni mwakilishi wa vijana anayeishi Tanzania na anaziwakilisha sauti za vijana‘

Getrude alianza kwa kuwasalimia waalikwa huku ikiripotiwa Maraisi 60 walihudhuria na kisha akaeleza kuwawakilisha vijana na watoto ambapo alizungumzia mabadiliko ya tabia nchi, hatari yake na kwamba wamekua wakifikisha ujumbe kwa Wananchi juu ya mabadiliko hayo kama anavyoonekana kwenye hii video hapa chini.

 MTAZAME HAPA:

VIDEO: Baada ya Ukawa kususia Bunge, Waziri Nape Kawajibu Haya.....

$
0
0
Moja ya headline iliyochukua nafasi April 22 ni pamoja na hii ya Umoja wa vyama vya upinzani bungeni kutangaza kuwa havitashiriki kuchangia hoja mikutano yote inayoendelea hadi baadhi ya vipengele kama urushwaji wa matangazo ya moja kwa moja kutofanyika.

Baada ya hayo yote, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye anasema

‘Tunachotegemea wangewasilisha mpango mbadala kwa mwaka 2017/2017, badala yake mchana wakasema hawapo tayari, jioni wamekuja wanasema hatua zinazochukuliwa na Serikalini ni hatua zinzokiuka utaratibu‘ ;-Nape Nnauye

‘Tunachokiona hawa wenzetu pengine kasi ya hawamu ya tano inawashinda, sasa wanaamua kuweka vihoja n akushindwa kuweka mpango mbadala. Na kama hawana huo mpango mbadala basi si’mbaya waache mpango ulioletwa na Serikali upitishwe na utekelezwe‘ ;-Nape Nnauye

MTAZAME HAPA:

Mbowe Auchambua Utawala wa CCM Chini ya Magufuli: Umejaa Uvunjifu wa Katiba, Sheria

$
0
0
HOTUBA YA KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI (KUB) MHESHIMIWA FREEMAN AIKAELI MBOWE (MB) AKIWASILISHA BUNGENI MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KATIKA OFISI YA WAZIRI MKUU KWA MWAKA WA FEDHA 2016/17.

Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge,
Toleo la Januari, 2016
_________________________________


1. SHERIA YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA MAWAZIRI (MINISTERS – DISCHARGE OF MINISTERIAL FUNCTIONS – ACT, 1980.

Mheshimiwa Spika, kifungu cha 5(1) kinaweka masharti kwa Rais kutengeneza mwongozo wa muundo na utekelezaji wa majukumu ya Serikali yake.

Inasomeka ifuatavyo: Nanukuu “the President shall from time to time by notice published in the Gazette, specify the departments, business and other matters and responsibility for which he has retained for himself or he has assigned under his direction to any minister and may in that notice specify the effective date of the assumption of that responsibility…….” mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa Serikali inafanya kazi bila kuwa na mwongozo wa utendaji wake na kazi kwa wizara mbalimbali. Hii ina maana kwamba Serikali inafanya kazi kwa kauli za Rais na Mawaziri bila kufuata mwongozo wowote wenye msingi na uhalali wa kisheria.

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa mwongozo wa utendaji wa Serikali kwa kila Wizara (Instrument) unaotumika ni ule uliochapishwa kwenye gazeti la Serikali namba 494A la tarehe 17/12/2010. Kwa mujibu wa Instrument hiyo, majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni:
 Coordination of Government Business
 Leader of Government Business in the National Assembly
 Link between Political Parties and Government.
 National Festivals and Celebration of Management of Civic Contingencies (relief).
 Facilitation and Implementation of Plans for the Development of Dodoma as Capital of Tanzania.
 Coordination and Supervision of Transfer of the Government to Dodoma.
 Government Press Services.
 Investment, Economic Empowerment, Public-Private-Partnership (PPP), Poverty alleviation Policies and their Implementation.
 Facilitation of the Development of Informal Sector.
 Performance Improvement and Development of Human Resources under this Office
 Extra – Ministerial Department, Parastatal Organisations, Agencies, Programmes and Projects under this Office.

REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT:
 Decentralization by Devolution (D by D), Rural Development, Urban Development Policies and their Implementation.
 Regional Administration.
 Primary and Secondary Education Administration
 Dar Rapid Transit – DART.
 Performance Improvement and Development of Human Resources under this Office.
 Extra-Ministerial Departments, Parastatal Organisations, Agencies, Programmes and Projects under this Office.

Mheshimiwa Spika, kitendo cha Serikali hii kuendesha kazi zake kwa Mwongozo wa 2010 ina maanisha kwamba majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu bado ni yale yale yaliyochapishwa mwaka 2010, kwa sababu gazeti hilo la Serikali halijafutwa.

2. UVUNJWAJI WA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI KUHUSIANA NA BAJETI UNAOFANYWA NA SERIKALI

Mheshimiwa Spika, hili ni Bunge la Bajeti ambalo kwa mujibu wa ibara ya 63(3)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limepewa mamlaka ya kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaaka wa Bajeti kwa madhumuni ya kujadili na kuidhinisha Bajeti ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, Ikiwa fedha zilizoidhinishwa na Bunge hazikutosha kutekeleza majukumu ya Serikali , kifungu cha 41(1) cha Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015 kinaelekeza kwamba: “ Serikali itawasilisha Bungeni kwa idhini, bajeti ya nyongeza ya fedha zilizotumika ambazo zimezidi kiwango kilichoidhinishwa na Bunge au kwa madhumuni ya kugharamia mahitaji ambayo hayakupangwa”.

Mheshimiwa Spika utaratibu huu unatiliwa nguvu na Sheria ya Fedha za Umma wa mwaka 2001( Public Finacne Act, 2001)ambapo kifungu cha 18 (3) na (4) kinaitaka Serikali kuleta Bungeni bajeti ya nyongeza ( mini-budget) kwa ajili ya kupata idhini ya Bunge ikiwa fedha zilizoidhinishwa awali hazikutosha.

Mheshimiwa Spika, utaratibu huo wa kisheria umekuwa ukivunjwa na Serikali kwa kufanya matumizi ya fedha ambazo hazikuidhinishwa na Bunge jambo ambalo linaua dhana ya madaraka ya Bunge ya kuisimamia na kuishauri Serikali.

Mheshimiwa Spika, ili kuthibitisha jambo hilo, kwa mfano bajeti ya maendeleo iliyokuwa imeidhinishwa na Bunge kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2015/16 ilikuwa ni shilingi bilioni 883.8 ambapo kati ya fedha hizo, fedha za ndani zilikuwa ni shilingi bilioni 191.6

Mheshimiwa Spika, Jambo la kushangaza ni kwamba hadi kufikia mwezi Machi 2016 Wizara ilikuwa imeshapokea kutoka hazina shilingi bilioni 607.4 ikiwa ni fedha za ndani.

Mheshimiwa Spika, ukitazama takwimu hizo utaona kuwa kuna ongezeko la fedha zilizotolewa na hazina hadi kufikia mwezi Machi 2016 ukilinganisha na fedha zilizoidhinishwa na Bunge. Tangu kuidhinishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, hakuna bajeti ya nyongeza iliyoletwa Bungeni na Serikali kwa ajili ya kupata idhini kutokana na matakwa ya Sheria ya Bajeti ya 2015 au sheria ya Fedha ya 2015.

Mheshimiwa Spika, kitendo cha Serikali kuamua kufanya re-allocation ya bajeti bila kupata idhini ya Bunge ni dharau kwa bunge lakini mbaya zaidi ni uvunjaji wa Katiba na Sheria.

3. UHURU NA MADARAKA YA MHIMILI WA BUNGE

Mheshimiwa Spika, Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inalitaja Bunge kuwa ndicho chombo kikuu katika Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake. Katika hali isiyo ya kawaida, kifungu hiki cha Katiba kimevunjwa na badala yake Serikali imelipoka bunge madaraka yake na Bunge kwa maana ya uongozi wake wanaonekana kushiriki na kukubali kupokwa huku kwa madaraka na uhuru wake.

Mheshimiwa Spika, Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi, na wananchi wana haki ya kujua Bunge lao linavyofanya kazi ili wawe na uwezo wa kuwawajibisha wawakilishi wao iwapo hawafanyi kazi inavyostahili.

Katika hali isiyo ya kawaida, Serikali na uongozi wa Bunge, imewapoka wananchi haki yao ya kupata habari za Bunge kwa kuzuia mijadala Bungeni kurushwa moja kwa moja na televisheni ya Taifa na vyombo vingine vya habari vya kujitegemea.
Mheshimiwa Spika, Jambo hili pia ni uvunjwaji wa ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo inasema kwamba kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake; anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi; anao uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake na anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii.

Mheshimiwa Spika, katika Mazingira kama hayo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haiko tayari kuendelea kushiriki uvunjaji wa Katiba Sheria na haki za msingi za wananchi.

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani haitakuwa tayari kuwasilisha hotuba yake katika mazingira haya na inaushauri uongozi wa Bunge kupata ufumbuzi wa haraka wa kadhia hii ili kurejesha heshima ya Bunge na haki za msingi za wananchi. Hivyo basi Kambi bado inatafakari kwa kina na makini hatua za kufuata.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

Freeman Aikaeli Mbowe (Mb)

KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI NA
MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI
KATIKA OFISI YA WAZIRI MKUU
22 Aprili, 2016.

Serikali Yakiri Kudaiwa Sh67.3 bilioni na Walimu

$
0
0
Serikali imesema bado inadaiwa na walimu deni linalofikia Sh67.3 bilioni, ikiwamo mishahara.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jaffo alitoa kauli hiyo mjini Dodoma jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Aida Khenani bungeni.

Katika swali lake, mbunge huyo alitaka kujua Serikali imechukua hatua gani kumaliza madai ya walimu ya muda mrefu nchini.

Pia, alihoji kuhusu madai ya walimu waliosahihisha mitihani ya kidato cha nne mwaka jana ambao hawajalipwa hadi sasa.

Naibu Waziri huyo alisema Serikali imeendelea kulipa madeni ya walimu kupitia mamlaka zake kila yanapojitokeza.

“Mfano, Oktoba 2015, Serikali ililipa Sh20.1 bilioni na Februari mwaka huu imelipa Sh1.17 bilioni za madeni ya walimu nchi nzima,” alisema Jaffo.

Alitoa mchanganuo kuwa kati ya kiasi kinachodaiwa, alisema Sh17.5 bilioni ni madeni yasiyo ya mishahara wakati madeni ya mishahara yanafikia Sh49.8 bilioni ambayo kwa pamoja yanafanyiwa uhakiki.

Kuhusu malipo ya walimu waliofanya kazi ya kusahihisha mitihani alisema baadhi ya mikoa haijapeleka madai yao hadi sasa licha ya kuwa mwisho wa kupelekwa ilikuwa ni Aprili 15.

Alisema mikoa tisa tu ndiyo ilipeleka na kuitaja kuwa ni Mbeya, Mara, Tanga, Arusha, Kigoma, Lindi, Mtwara, Kilimanjaro na Iringa.

Alisema madeni hayo ya mikoa hiyo yanahakikiwa ili walimu walipwe.

PAUL Makonda Amtumbua Asha Baraka....Kisa Hichi Hapa

$
0
0
Ile amri ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya kutaka kumbi zote za starehe kufungwa inapofika saa sita za usiku, imemwangukia Mkurugenzi wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka baada ya juzikati polisi walioambatana na maafisa wa serikali kuvamia onesho la bendi yake.

Sakata hilo lilitokea mishale ya saa nane za usiku, kwenye Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini hapa ambapo bendi hiyo ilikuwa ikiendelea kupiga shoo na kutoa tuzo kwa wadau wake lakini ghafla wakaingia askari kadhaa wakiwa na silaha sambamba na maafisa hao na kuamuru muziki uzimwe.

“Unaambiwa ulikuwa ni mtiti wa nguvu, Asha Baraka akawa hataki muziki uzimwe kwa sababu mashabiki waliolipa viingilio wasingemuelewa, wangeweza hata kuharibu vyombo vyake vya muziki,” alisema shuhuda mmoja wa tukio hilo na kuongeza:

“Maofisa hao walimwambia Asha Baraka kuwa walikuwa wakitekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar, Makonda la kumbi zote za burudani kufungwa saa sita kamili vinginevyo kuwe na kibali maalum. Walivutana kwa muda mrefu sana.”

Hata hivyo, baada ya majadiliano yaliyochukua muda mrefu, maafisa hao na polisi waliondoka na kuacha burudani ikiendelea lakini walimuonya Asha Baraka kwamba akirudia kuvunja sheria ‘atakiona’.

Akizungumza na mwandishi wetu kuhusu tukio hilo, Asha Baraka alisema: “Ni kweli kibali changu hapa kinaonesha inatakiwa tufunge saa sita lakini wakati mwingine mashabiki wanakuwa wagumu kuelewa, wanaweza kusababisha vurugu,” alisema.

Mbowe Ataja Sababu 3 Zilizomfanya Awaongoze Wabunge wa UKAWA Kususa na Kutoka Nje Ya Ukumbi wa Bunge

$
0
0
Kambi ya Upinzani bungeni jana imesusia kuwasilisha na kujadili hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, huku kiongozi wake, Freeman Mbowe akitoka nje ya ukumbi huo, akitaja kasoro tatu zilizosababisha wachukue uamuzi huo.

Staili ya kususia kujadili hotuba hiyo ya bajeti ni mpya kwa kambi hiyo ya upinzani baada ya kutumia njia ya kutoka nje ya ukumbi wakati wa vikao vya Bunge la Katiba na baadaye kutumia njia ya kupiga kelele kukwamisha shughuli za chombo hicho wakati wa Bunge la Kumi.

Jana, Mbowe aliwaambia waandishi nje ya ukumbi kuwa kasoro zilizofanya wachukue uamuzi huo ni kukiuka masuala ya kisheria katika utekelezaji wa bajeti, kutotangaza kwenye Gazeti la Serikali mabadiliko ya wizara na kutorushwa kwa vipindi vya Bunge kwenye televisheni.

Mbowe, ambaye alikuwa akitarajiwa kusoma bajeti ya upinzani kuhusu Ofisi ya Waziri Mkuu, aliibuka na hoja hizo tatu kabla ya kuamua kutoka nje.

“Bajeti inakuwapo kwa sababu ni hitaji la kisheria. Inapokuwa Serikali inataka kupitisha bajeti, lakini haiheshimu bajeti hakuna sababu ya wabunge kukaa hapa kujadiliana, kutoa povu, kupitisha vifungu vya Katiba, halafu yenyewe haitekelezi wajibu wake kisheria,” alisema Mbowe nje ya ukumbi wa Bunge.

Alisema Serikali imekuwa ikikiuka sheria ya utekelezaji wa majukumu ya mawaziri inayomtaka Rais kutengeneza mwongozo wa muundo wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali yake, ikiwa ni pamoja na kutangaza katika gazeti la Serikali mabadiliko ya wizara zake.

Alisema “Tulichelewa kuunda (Baraza Kivuli la Mawaziri) kwa sababu tulikosa instrument (nyaraka rasmi). Tukalazimika kuunda hivyohivyo. Sasa tumefika kwenye (Bunge bado Serikali haijaundwa officially (rasmi), kisheria. Haijawa gazetted (haijatangazwa kwenye Gazeti la Serikali),” alisema Mbowe.

“Mpaka leo Serikali hii inafanya kazi kwa kutumia instrument iliyosainiwa na Rais (wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya) Kikwete mwezi wa 12 mwaka 2010.

“Na wizara kuu kwa mujibu wa instrument ya mwaka 2010 ilikuwa ni Wizara ya Waziri Mkuu Tamisemi. Na Tamisemi ilikuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Kwa hiyo baada ya uchaguzi wa 2010, Tamisemi imerudishwa Ofisi ya Rais, haiku tena Ofisi ya Waziri Mkuu. Lakini haijawa gazetted.”

Alitaja hoja nyingine kuwa ni uvunjwaji wa Katiba na sheria za nchi kuhusiana na bajeti unaofanywa na Serikali pamoja na kuminya uhuru na madaraka ya mhimili wa Bunge kwa kuzuia matangazo ya wasusia Bunge kurushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni.

“Hatutashiriki mjadala tunaendelea kutafakari hatua nyingine za kuchukua kama Serikali na Bunge hawatatafuta ufumbuzi wa masuala hayo matatu,” alisema Mbowe.

Mbowe aliingia ukumbini saa 9:56 alasiri akiongozana na mbunge wa Momba, David Silinde na alikwenda kusalimiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju na Waziri wa Kilimo, Mwigulu Nchemba.

Mara baada ya kupewa nafasi na Mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge, Mbowe alieleza sheria ya utekelezaji wa majukumu ya mawaziri ambapo alidai kifungu cha 5(1) kinaweka masharti kwa Rais kutengeneza mwongozo wa muundo na utekelezaji wa majukumu yake.

Alisema mpaka sasa Serikali inafanya kazi bila kuwa na mwongozo wa utendaji kwa wizara mbalimbali hivyo kazi nyingi za Serikali zinafanywa kwa kauli ya Rais.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo mpaka sasa mwongozo wa utendaji wa Serikali kwa kila wizara unaotumika ni uliochapishwa kwenye Gazeti la Serikali Namba 494 A la Desemba 17, 2010 ambao pia umetoa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kiongozi huyo alinukuu baadhi ya majukumu katika mwongozo huo kuwa ni kuratibu shughuli za Serikali, kiongozi wa Serikali ndani ya Bunge, kiungo kati ya Bunge na Serikali, shughuli za kisiasa na serikali na kuratibu sherehe na misaada mbalimbali.

“Kazi nyingine ni kusaidia urahisishaji wa mipango ya serikali katika kuhamishia makao makuu Dodoma, uwekezaji, uchumi, sekta binafsi na kusaidia maendeleo katika sekta za ndani,” alisema Mbowe.

Alisema Rais John Magufuli alifanya mabadiliko ya kuziunganisha wizara bila kubadili muongozo wa kisheria.

“Kitendo cha Serikali hii kuendesha kazi zake kwa mwongozo wa 2010 kina maana kwamba majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu bado ni yale yale ya mwaka 2010 kwa sababu gazeti hilo halijafutwa,” alisema.

Alifafanua kuwa jambo hilo ni uvunjwaji wa Katiba na sheria za nchi kuhusu bajeti unaofanywa na serikali na kwa mujibu wa Ibara ya 63 (3) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bunge limepewa mamlaka ya kujadili utekelezaji wa kila wizara na kuidhinisha bajeti ya Serikali.

Mbowe alisema ikiwa fedha zilizoidhinishwa na bunge hazikutosha kutekeleza majukumu, kifungu cha 41 (1) cha Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015 kinaelekeza kuwa serikali itawasilisha bungeni maombi ya idhini, bajeti ya nyongeza ya fedha zilizotumika ambazo zimezidi kiwango.

Alituhumu kuwa kumekuwa na uvunjwaji wa kifungu hicho na kutolea mfano bajeti ya Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano ya mwaka wa 2015/16 ilikuwa Sh 883.8 bilioni ambazo kati ya hizo, fedha za ndani zilikuwa Sh191.6 bilioni.

 “Jambo la kushangaza ni kwamba hadi kufikia mwezi Machi 2016 Wizara ilikuwa imeshapokea kutoka hazina Sh607.4 bilioni ikiwa ni fedha za ndani, kitendo kinachoonyesha kuwa na ongezeko kubwa la fedha za ndani,” alisema.

Alitaja kuwa tangu kuidhinishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, hakuna bajeti ya nyongeza iliyopelekwa bungeni na Serikali kwa ajili ya kupata idhini kutokana na matakwa ya Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015 au sheria ya fedha ya 2015.

 “Kitendo cha Serikali kuamua kuhamisha kiasi cha fedha ya bajeti bila ya kupata idhini ya Bunge ni dharau kwa bunge lakini mbaya zaidi ni uvunjwaji wa Katiba na sheria.” alisema.

 Nje ya ukumbi wa Bunge alisema:”Ukiwauliza wanapata wapi hizi fedha, wanasema ni maelekezo ya Rais kwamba fedha ziondolewe kwenye fungu hili, zipelekwe wizara hii.”

Vipindi vya Bunge
 Kadhalika, Mbowe alisema uamuzi wa Serikali kuminya uhuru na madaraka ya Bunge umewapora wananchi haki yao ya kupata habari kwa kuzuia mijadala bungeni kurushwa moja kwa moja na vyombo vya habari.

Alisema jambo hilo ni uvunjwaji wa Ibara ya 18 ya Katiba inayotoa uhuru kwa kila mtu kutoa maoni na kueleza fikra zake, kutafuta, kupokea na kutoa habari.

“Bunge ndipo mahali ambapo wananchi wanahoji na kuiwajibisha Serikali na wanajadili hoja za maendeleo kupitia wabunge wao waliowachagua, hivyo huwafuatilia kupitia kwenye luninga zao pia ubadhirifu wa miradi mingi uibuliwa huko,” alisema.

Alisema wapinzani wataendelea kutafakari kwa kina na makini hatua za kufuata na kisha akawasilisha.

“Kwa mazingira kama hayo, kambi rasmi ya upinzani bungeni haiko tayari kuendelea kushiriki katika uvunjaji Katiba, sheria na haki za msingi za wananchi,” alisema.

“Kambi rasmi haitakuwa tayari kuwasilisha hotuba yake katika mazingira haya na inaushauri uongozi wa Bunge kutafuta ufumbuzi wa haraka wa kadhia hii ili kurejesha heshima ya Bunge na haki za msingi.”

Baadaye, Chenge aliipinga kauli ya Mbowe kuwa Katiba imevunjwa na kusema alitumia maneno mazito na badala yake alimtaka atumie maneno kuwa Katiba ilitaka kuvunjwa.

Chenge aliitaka kambi ya upinzani kufuata taratibu kama wanaona kuwa wameonewa, badala ya kutumia maneno hayo na pia akata watafakari kama wangependa kuendelea na mjadala.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge wa upinzani walionyesha kususia kwani hata walipoitwa na mwenyekiti hawakuchangia licha ya kuwapo ndani ya ukumbi wa Bunge.

Kauli ya Mbowe kwa wanahabari
Akizungumza na wanahabari Mbowe alisema uamuzi huo haujakiuka sheria kwa sababu Bunge liko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na kwamba hawawezi kwenda mahakamani ili kupata tafsiri kuhusu suala hilo kwa sababu shughuli za Bunge zinatatuliwa na Bunge lenyewe si mahakama.

“Rais kama kiongozi wa nchi ana mamlaka ya kulisemea hili, atueleze kama ni yeye ndiye aliyeruhusu Bunge lisirushwe moja kwa moja. Awali walisema TBC hawatarusha ila kwa sasa vyombo vyote vimezuiwa,” alisema.

“Hivi sasa luninga zilizopo ndani ya Bunge zilizokuwa zikionyesha matangazo  nazo hazionyeshi kinachoendelea. Sasa watumishi wa Bunge watafuatilia nini?” alihoji Mbowe.

Kauli ya AG
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alisema: “Nitashukuru kama mtavuta subira majibu ya Serikali yatatolewa wakati wa kufanya majumuisho.”

Sheikh Mkuu Akerwa Tabia za Akina Wema Sepetu

$
0
0
Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salim amesema anakerwa na mastaa wanaodaiwa kuwa na tabia chafu zenye viashiria vya usagaji.

Shehe huyo aliyasema hayo hivi karibuni baada ya kutafutwa na gazeti hili kufuatia kusambaa kwa picha mitandaoni zinazomuonesha mwigizaji Wema Sepetu ‘Madam’ akiwa kwenye pozi la kimahaba na mwanamuziki Diana Exavery ‘Malaika’.


“Vitendo hivyo vinavyoashiria tabia za usagaji ni machukizo kwa Mwenyezi Mungu, pia ni laana na havikubaliki kabisa katika imani yeyote, anayefanya vitendo hivyo anatakiwa kuachana navyo maana havimpendezi Mungu.

“Wasanii wote, wanapaswa kutambua kuwa wao ni kioo cha jamii na watu wanahitaji kujifunza mambo mengi mazuri kutoka kwao na si kuwapotosha,” alisema Shehe Alhadi.


Ikumbukwe kuwa hii si mara ya kwanza kwa Wema Sepetu kujianika akiwa kwenye mapozi ya kimahaba na wanawake wenzake, alishawahi pia kuonekana katika pozi tata na mwigizaji Aunt Ezekiel.

Ombaomba Dar es Salaam Wacheza Mchezo wa Kuviziana na Askari

$
0
0
Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutangaza operesheni ya kuwaondoa ombaomba katikati ya jiji, ombaomba hao wameendelea kuviziana na askari mgambo huku wakidai wanaangalia upepo unavyokwenda.

Kazi ya kuwakamata ombaomba hao inafanywa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Isaya Mngurumi alisema kazi hiyo inaendelea huku baadhi yao wakiwa wamefikishwa mahakamani. “Kazi hii ni endelevu, ombaomba walikuwa kero katikati ya jiji letu, hivyo tutahakikisha wote wanakamatwa,” alisema Mngurumi.

Gazeti hili lilitembelea maeneo ya katikati ya jiji ikiwamo barabara ya Bibi Titi na kushuhudia ombaomba hao wakiomba fedha kwa wapita njia na kwenye magari.

Mmoja wa ombaomba hao, Abdallah Isaya alisema wanalazimika kuomba kutokana na ulemavu walio nao.

Alisema wanaomba kwa kuvizia kwa kuhofia kukamatwa na mgambo na pale wanapotokea hupanda baiskeli zao na kuondoka. Baadhi ya ombaomba walisema wanaishi maisha magumu na kulazimika kuomba fedha kwenye magari yanayosiamama pembezoni mwa barabara. “Juzi wenzetu walikamatwa na mgambo sisi tulikimbia na kwenda kujificha,” alisema mmoja wao.

Kamanda wa Polisi Ilala, Lucas Mkondya alisema operesheni ya kuwakamata inafanywa na jiji kama wakishindwa jeshi hilo litawasaidia.

UVCCM Yataka Majipu Ndani ya Chama Yaanze Kujitumbua ......Ni wale Waliokisaliti Chama katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka Jana

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Shaka Hamduni Shaka amewataka wanachama wanaojitambua kuwa ni majipu kwa kukisaliti chama kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka jana, waanze kujitumbua kabla hawajatumbuliwa.

Shaka alitoa rai hiyo jana katika mji wa Orkesumet na Kata ya Ngorika Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wakati wa ziara yake ya kuhamasisha vijana kujiunga na chama hicho, kufungua matawi mapya, kumsimika kamanda wa Kata ya Naisinyai na kukagua uhai wa chama.

Alisema lazima wajenge chama chenye heshima na nidhamu kuliko kuwa na wanachama wasaliti ambao hawana msimamo.

Shaka alisema wanachama wa aina hiyo nyakati za asubuhi wanakuwa sehemu moja na ikifika jioni wanakwenda kwingine.

“Ni heri wabakie wanachama wawili waadilifu kuliko wengi ambao hawana msimamo, kufanya kosa siyo kosa, bali kosa kurudia kosa, tunajua uchaguzi ukirudiwa tena hapa Simanjiro CCM itafanikiwa kushinda,” alisema Shaka.

Alisema kukata tamaa ni mwiko ukiwa CCM, kwa kuwa miaka mitano siyo mingi, hivyo wanatarajia kurudisha kata sita na Jimbo la Simanjiro linaloshikiliwa na Chadema.

Alisema hilo litafanikiwa kutokana na uongozi bora wa Rais John Mafuguli.

“Tumesikia wapo waliotusaliti wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, tutawachukulia hatua, ila hivi sasa kutokana na juhudi za Rais Magufuli hata upinzani watatupigia kura za ndiyo,” alisema.

Mwenyekiti wa UVCCM, Wilayani Simanjiro, Kiria Laizer alisema vijana ndiyo nguvu ya chama, hivyo kupitia jumuiya hiyo wamejipanga kukipigania na kukitetea.

“Vijana ndiyo nguzo ya chama, tumejipanga vizuri kuhakikisha kupitia CCM, wananchi wa eneo hili wanaendelea kukiamini na kukithamini, hivyo tutasonga mbele,” alisema.

Juma Abdul Jaffar Mnyamani Awa Lulu Yanga...Wamsainisha Mkataba Mpya Fasta

$
0
0
BEKI hodari wa kulia wa kimataifa wa Tanzania, Juma Abdul Jaffar Mnyamani amesaini Mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga SC ya Dar es Salaam hadi mwaka 2018.

Habari kutoka ndani ya Yanga zinasema kwamba Abdul alisaini Mkataba huo kabla ya timu hiyo kwenda Misri kucheza na Ahly.

Na hakuna kingine kilichoisukuma Yanga kumsainisha Mkataba mpya beki wake huyo zaidi ya kiwango chake kizuri kwa sasa akionekana kabisa kuwa miongoni mwa wachezaji muhimu kikosini.

Na kwa kusaini Mkataba huo, Juma ataingia kwenye orodha ya wachezaji walioitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu.

Juma aliyezaliwa Novemba 10, mwaka 1992
Mwananyamala, Dar es Salaam, alijiunga na Yanga mwaka 2012 akitokea Mtibwa Sugar kwa Mkataba wa miaka miwili, ambao ulipoisha akaongezwa mwingine wa miaka miwili.

Na wakati Mkataba wake wa sasa unaelekea kumalizika mwishoni mwa msimu, inaelezwa tayari Juma Abdul amesaini Mkataba mwingine mpya wa miaka miwili utakaomfanya afikishe miaka sita Jangwani.

Uganda Yatangaza Rasmi Kutumia Bandari ya Tanga nchini Tanzania kusafirishia Mafuta Ghafi Yake.

$
0
0
Hatimaye Serikali ya Jamhuri ya Uganda imetangaza rasmi uamuzi wake wa kutumia Bandari ya Tanga nchini Tanzania kusafirishia mafuta ghafi yake.

Uamuzi huo umetangazwa na Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Ushoroba wa Kaskazini uliomalizika Jijini Kampala Uganda.

Ujumbe wa Tanzania ulio kamilisha mazungumzo hayo na hatimaye kushuhudia utangazwaji wa hatua hiyo uliongozwa na Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa

Jopo la wataalamu kutoka Tanzania lililoongozwa na Mhe. Prof. Sospeter Muhongo bado wako jijini Kampala kukamilisha mpango huo wa Bomba la Mafuta Ghafi ambapo pia nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati zinatarajia kunufaika.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Dar es Salaam
23 Aprili, 2015

Wema Sepetu Akiwa Kwenye Ubora Wake

$
0
0
Wema Sepetu Akiwa Kwenye Ubora Wake..

Maneja wa Diamond Sallam Ataja Anapokosea Alikiba, Adai Akitaka Amsimamie yupo Tayari

$
0
0
Meneja wa Diamond, Sallam Sharaff yupo tayari kumsimamia Alikiba iwapo akitaka iwe hivyo.

Akiongea kwenye mahojiano na gazeti la Champion, Sallam alisema: Sina tatizo kabisa, akitaka tufanye kazi nitamweleza mahitaji yangu akikubali tutafanya kazi. Nilishawahi kukutana na Kiba, Nairobi, alinifuata akaomba tupige picha, sikuwa na kinyongo, tukapiga ikawa safi japokuwa ile picha aliitumia kunitukanisha baadaye.

Akifafanua kuhusu hilo, Sallam alisema: Hakuiweka yeye katika mtandao, aliitoa kwa mashabiki wake ambao wakasema nimeenda Nairobi kumfuata Ne-Yo halafu nikafukuzwa, wakasema mimi ndiyo niliomba kupiga picha na Kiba, ikawa gumzo sehemu nyingi. Ukweli nilikuwa na Ne-Yo na Diamond ambaye alikwenda pale kurekodi, yeye Kiba alikuwa Coke Studio.

Anasema Kiba alimuomba radhi na kudai kuwa aliwatumia wapost lakini wakaweka maneno yao.

Kuhusu anavyomchukulia Kiba kimuziki, Sallam alisema:

Siwezi kusema anakosea wapi, maana kila msanii ana njia zake. Wimbo wake wa Mwana ni mkali na ulifanya vizuri yawezekana anakosea kwenye ‘market’. Kuna vitu lazima ulazimishe, hata Diamond yupo juu lakini hawezi kutoa kitu halafu akatulia tu akaacha watu wapende wenyewe. Kila mtu ana staili yake yawezekana yeye hataki kwenda kwenye staili kama hiyo, ndiyo maana kuna muda huwa nasema huwezi kumfananisha Diamond na Ali kwa sababu wanaimba muziki wa tofauti. Wote ni Bongo Fleva lakini staili zao ni tofauti, kwa mtu anayefuatilia muziki anaweza kugundua hilo.

Kuhusu bifu ya Diamond na Kiba, Sallam alisema:

Hakuna bifu kabisa, mimi nafahamu hilo. Wameshakutana na kusalimiana na hakuna chochote. Nasema kabisa wanapiga stori na wanaongea ‘fresh’ kabisa. Kinachotokea ni kwamba watu wanawauliza kama wana bifu kwa hiyo wenyewe wanasema hawana bifu basi, lakini kwa kuwa hakuna maelezo mengi watu wanachukulia hivyo.

Kuhusu madai kuwa uongozi wa Diamond unafanya fitna ya kuzuia video za Kiba zisipigwe katika vituo vikubwa vya nje kama MTV na Trace, Sallam alisema:

Siyo kweli. Kiba na ana nguvu kubwa MTV na Trace kuliko Diamond kwa ajili ya Seven (ni mmoja wa wasimamizi wa Ali Kiba). Seven alikuwa mfanyakazi wa MTV, anawajua watu wote wa MTV, hata yule bosi wa Trace wa sasa alikuwa chini ya Seven, ndiyo maana hata video yake ya Chekecha Cheketua ilichezwa wiki nzima mfululizo ikiwa ni ‘Exclusive’.

Wenzetu katika vituo wanaangalia vigezo vyao. Nikupe siri kuwa wakati naanza kazi na Diamond, alikuwa anabaniwa kweli zisipigwe kabisa hata Channel O.

Aliendelea: Siwezi kutaja jina lakini nyimbo zilikuwa zinapelekwa DStv hapo lakini anaambiwa hazina viwango, zinarudi. Aliyekuwa anafanya hivi ni Mtanzania na ni mhusika mkubwa wa muziki wa Tanzania. Nilimfuata nikamchana ‘live’ baadaye tukaamua kazi zetu kuzipitishia Nigeria kisha tukarudi hapa na kila kitu kikawa rahisi. Niwashauri watu kuwa wafanye kazi na watangaze kazi zao dunia ya sasa hakuna kitu kinachoenda chenyewe tu.

Matokeo ya Mechi Kati ya Chelsea na Bournemouth Haya Hapa...

$
0
0
Kiungo wa Chelsea, Willian akimvisha kanzu kipa wa Bournemouth, Boruc kumalizia pasi ya Fabregas kuifungia Chelsea katika ushindi wa 4-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Vitality. Mabao ya Chelsea yamefungwa na Pedro, Hazard mawili na Willian, huku la wenyeji likifungwa na Elphick Uwanja wa

Sakata la Lugumi na Jeshi la Polisi Lachukua Sura Mpya...Kamati Yaundwa Kuchunguza Kwa Kina Utata wa Mkataba Huo....

$
0
0
Kamati ya kudumu ya Bunge inayoshughulikia Hesabu za Serikali (PAC) imeunda kamati ndogo ya watu tisa itakayochunguza kwa kina mkataba uliozua utata wa Sh37bilioni ulioingiwa baina ya Jeshi la Polisi na Lugumi Enterprises.

Pande hizo mbili, Jeshi la Polisi na Lugumi Enterprises, ziliingia mkataba huo kwa ajili ya kufunga vifaa 108 vya kuhifadhia alama za vidole katika vituo vya polisi.

Akizungumza na wanahabari leo mjini Dodoma, makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Aeshi Hilary amesema kamati hiyo itafanya kazi kwa siku 30, kuanzia Jumatatu ijayo.

Wajumbe tisa wa kamati hiyo ndogo ni; Japhet Hasunga (Vwawa-CCM), wengine wa CCM ni Livingstone Lusinde (Mtera), Stanslaus Mabula (Nyamagana), Haji Mponda (Malinyi) na Hafidh Ali Tahir (Dimani).

Wabunge wa upinzani waliopo katika kamati hiyo ni Nahenjwa Kaboyoka (Same Mashariki-Chadema), Musa Mbaruk (Tanga Mjini-CUF), Tuza Malapo (Viti Maalum-Chadema) na Khadija Nassor Ali (Viti Maalum-CUF).

Hii Hapa Ndiyo Maana ya Wimbo wa Lady Jaydee ‘Ndindindi’

$
0
0


Lady Jaydee ametoa maana ya wimbo wake ‘Ndindindi’ ambalo lilikuwa ni fumbo lililokuwa linawapa majibu mengi yasiyokuwa na uhakika mashabiki wake.

Wimbo wa ‘Ndindindi’ unazidi kufanya kwenye medi mbalimbali na kumrudisha vizuri Jide aka Binti Komando kwenye muziki wa Bongo Fleva baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila ya kuachia wimbo wowote.

Akiongea kwenye kipindi cha FNL, kinachoruka kupitia EATV, Lady Jaydee alisema, “The Ndi mimi ni kitu tori wewe si kitu” lakini pia aliongezea “ili kuleta fleva ya muziki ndiyo nikaiita Ndindindi. Mimi ni kitu na wewe si chochote.”
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live




Latest Images